Hadiyth Al-Qudsiy
Hadiyth Ya 42
Watu Wa Jannah Watapata Ridhaa Ya Allaah
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ اللَّهَ تَبَارَكَ وَتَعَالَى يَقُولُ لِأَهْلِ الْجَنَّةِ: يَا أَهْلَ الْجَنَّةِ! فَيَقُولُونَ لَبَّيْكَ رَبَّنَا وَسَعْدَيْكَ، فَيَقُولُ: هَلْ رَضِيتُمْ؟ فَيَقُولُونَ وَمَا لَنَا لَا نَرْضَى وَقَدْ أَعْطَيْتَنَا مَا لَمْ تُعْطِ أَحَدًا مِنْ خَلْقِكَ، فَيَقُولُ: أَنَا أُعْطِيكُمْ أَفْضَلَ مِنْ ذَلِكَ، قَالُوا: يَا رَبِّ وَأَيُّ شَيْءٍ أَفْضَلُ مِنْ ذَلِكَ؟ فَيَقُولُ: أُحِلُّ عَلَيْكُمْ رِضْوَانِي فَلَا أَسْخَطُ عَلَيْكُمْ بَعْدَهُ أَبَدًا)) البخاري، مسلم و الترمذي
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Tabaaraka wa Ta’aalaa Atawaambia watu wa Jannah: Enyi watu wa Jannah! Watasema: Labeka Rabb wetu tuko chini ya amri Yako na kheri zote zimo katika Mikono Yako. Kisha Atasema: Je, mmeridhika? Watasema: Vipi tusiridhike na hali Umetupa ambayo Hukumpa yeyote mwengine katika viumbe Vyako? Kisha Atasema: Nitakupeni kilichobora kuliko hayo. Watasema: Ee Rabb, ni kipi kilicho bora kuliko haya? Atasema: Nitafanya ridhaa (mapenzi) Yangu iwateremkie na baada ya hapo Sitoghadhibika nanyi tena abadan)) [Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhy]
Links
[1] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F2697&title=42-Hadiyth%20Al-Qudsiy%3A%20Watu%20Wa%20Jannah%20Watapata%20Ridhaa%20Ya%20Allaah