Nini Maana Ya ‘Itikaaf?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
Maana ya Mu’takif: Mwenye kuingia katika niyyah ya I’tikaaf.
1. Nini Maana Ya ‘Itikaaf?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
Ni kujiweka faragha kwa ajili ya ‘ibaadah na kujipwekesha kwa Allaah kwayo. Na hii ndio kujipwekesha ki-shariy’ah. Na wengineo wakasema kuhusu maana ya I’tikaaf ni kukata mahusiano na kila kiumbe kwa yale yanayohusiana na kuwahudumia viumbe.
[Majmu’w Al-Fataawaa (15/438)]
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
I’tikaaf ni mtu kujilazimisha kubakia Msikitini kwa ajili ya utiifu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), ili ajitenge na watu na ashughulike katika utiifu kwa Allaah na ajiweke faragha nayo.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/155)]
Nini Hukmu Ya I’tikaaf?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
2. Nini Hukmu Ya I’tikaaf?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
I’tikaaf ni Sunnah kwa wanaume na wanawake.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (15/442)]
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
Ni Sunnah ya kutafuta Laylatul-Qadr.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/156)]
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
I’tikaaf katika Ramadhwaan ni Sunnah aliyoifanya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika uhai wake, kisha wake zake wakafanya I’tikaaf baada yake. Na Ahlul-‘Ilm (Wanachuoni) kwa ijmaa’ wakasema kuwa ni Sunnah.
[Majmuw’ Al-Fataawa (20/158)]
Je, I’tikaaf Inafaa Ki-Shariy’ah Miezi Mingineyo Isiyokuwa Ramadhwaan?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
3. Je, I’tikaaf Inafaa Ki-shariy’ah Miezi Mingineyo Isiyokuwa Ramadhwaan?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
Inafaa ki-shariy’ah Ramadhwaan na miezi mingineyo na ikiwa pamoja na Swiyaam ni bora zaidi.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (15/438)]
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
Inapasa ki-shariy’ah iwe katika Ramadhwaan pekee, lakini ikiwa mtu atafanya I’tikaaf ghairi ya Ramadhwaan itakuwa inafaa.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/159-160)]
Kufanya I´itikaaf Haishurutishwi Kuwa Na Swawm
Shaykh ´Abdul-Muhsin Al-‘Abbaad (Hafidhwahu Allaah)
SWALI:
Je, ni sharti mtu ili afanye I´tikaaf awe ana Swawm?
JIBU:
Hapakudhihiri kitu kwangu kuwa ni sharti hilo (la mtu awe katika Swawm) kutokana na kufanya kwake (Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) I´tikaaf siku kumi za Shawwaal, haikuthibiti kuwa alifunga. Hakuna kinachoonesha kuwa alifunga.
[Bawaabah Al-Haramayn Ash-Shariyfayn] [9]
Je, Ili I’tikaaf Iwe Sahihi Inalazimika Mtu Awe Katika Swawm?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
06. Je, Ili I’tikaaf Iwe Sahihi Inalazimika Mtu Awe Katika Swawm?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
Sahihi ni kwamba haina ulazima mtu awe katika Swawm.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (15/441)]
Je, I’tikaaf Inajuzu Wakati Wowote Ule Nje Ya Masiku Kumi Ya Mwisho Ya Ramadhwaan?
Al-Lajnah Ad-Daaimah
07-Je, I’tikaaf Inajuzu Wakati Wowote Ule Nje Ya Masiku Kumi Ya Mwisho Ya Ramadhwaan?
Jibu: Naam, I’tikaaf inajuzu wakati wowote ule lakini iliyo bora kabisa ni ya katika masiku kumi ya Ramadhwaan.
[Al-Lajnah Ad-Daaimah (10/410)]
Je, I’tikaaf Mwanamke Ni Sawa Na Ya Mwanaume?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
08-Je, I’tikaaf Ya Mwanamke Ni Sawa Na Ya Mwanaume?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
I’tikaaf ya mwanamke ki-shariy’ah ni sawasawa na ya mwanaume lakini tu iambatane na sharti kwamba haitomsababisha ufisadi au fitnah. Pindi itakaposababisha kuwa ni ufisadi au fitnah basi hapo hapaswi kufanya I’tikaaf. Au kama I’tikaaf itamsababisha asiwe na (majukumu na) watoto wake nyumbani mwake au asitimize haki za mumewe basi hapaswi kufanya I’tikaaf.
[Nuwr ‘Alaa Ad-Darb]
Sehemu Gani Inapaswa Kutekelezwa I’itikaaf?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
09-. Sehemu Gani Inapaswa Kutekelezwa I’itikaaf?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
Sehemu inayopaswa kutekelezwa I’tikaaf ni Misikitini ambayo inasimamishwa Swalaah za Jamaa’ah.
[Majmu’w Al-Fataawaa (15/42)]
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
Katika kila Msikiti, ikiwa ni Misikiti inayoswaliwa Ijumaa au katika Misikiti isiyoswaliwa humo. Lakini iliyo bora ni iwe katika Misikiti inayoswalishwa humo (Jamaa’ah).
[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/155)]
Je, I’tikaaf Inajuzu Katika Masjid Al-Haraam (Makkah) Kwa Ajili Ya Wanawake Na Wanaume?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
10-Je, I’tikaaf Inajuzu Katika Masjid Al-Haraam (Makkah) Kwa Ajili Ya Wanawake Na Wanaume?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
Hakuna makatazo kutekelezwa I’tikaaf katika Masjid Al-Haraam na Masjid An-Nabawiy Ash-Shariyf, ikiwa ni wanaume au wanawake na ikiwa haiwaletei madhara wanaoswali wala haimuudhi yeyote basi hakuna ubaya hivyo.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (15/440)]
Je, I’tikaaf Inasihi Katika Misikiti Mingineyo Isiyokuwa Ile Mitatu?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
11-Je, I’tikaaf Inasihi Katika Misikiti Mingineyo Isiyokuwa Ile Mitatu? (Masjid Al-Haraam (Makkah), Masjid An-Nabawiy (Madiynah), Masjid Al-Aqswaa (Palestina).
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
a. I’tikaaf inasihi katika Misikiti mingineyo isiyokuwa katika mitatu isipokuwa ikiwa mtu ametoa nadhiri kutekeleza I’tikaaf katika Misikiti mitatu basi hapo inamlazimu atekeleze I’tikaaf humo ili atimize nadhiri yake.
b. Isipokuwa ikiwa haiswaliwi Swalaah ya jamaa’ah humo basi I’tikaaf haisihi kutekelezwa humo.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (15/444)]
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
Inajuzu I’tikaaf katika Misikiti mingineyo isiyokuwa ile mitatu na ikiwa Hadiyth hii ni swahiyh “Isifanywe I’tikaaf isipokuwa Misikiti mitatu”, basi iliyokusudiwa ni kwamba I’tikaaf humo ni yenye ukamilifu na bora zaidi.
[Majmuw’ Al-Fataawa 20/160)]
Mwanamke Atekeleze Wapi I’tikaaf Akipenda Kufanya Hivyo?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
12-Mwanamke Atekeleze Wapi I’tikaaf Akipenda Kufanya Hivyo?
Mwanamke akitaka kutekeleza I’tikaaf, basi iwe katika Msikiti ambao hauna tahadharisho la ki-shariy’ah lakini ikiwa kuna tahadharisho la ki-shariy’ah basi asifanye I’tikaaf humo.
[Majmuw’ Al-Faataawaa (20/163)]
Vyumba Vya Matumizi Vya Masjid Vinafaa Kutumika Kwa I'tikaaf?
Al-Lajnah Ad-Daaimah
13-Chumba Cha Mlinzi Na Chumba Cha Wasimamizi Wa Zakaah Katika Masjid; Je, Vinafaa Kutumika Kwa Ajili Ya I’tikaaf?
a. Vyumba vilivyomo ndani ya Msikiti pamoja na milango yake yote hukmu zake ni za Msikiti.
b. Lakini ikiwa ni nje ya Msikiti, basi si katika Msikiti ijapokuwa ikiwa milango yake imo ndani ya Msikiti.
[Al-Lajnah Ad-Daaimah (10/412)]
Zipi Nguzo Za I’tikaaf Na Sharti Zake? Na Je, Inasihi Bila Ya Swawm?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
14-Zipi Nguzo Za I’tikaaf Na Sharti Zake? Na Je, Inasihi Bila Ya Swawm?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
a. Nguzo ya I’tikaaf ni kulazimika (kufanyika I’tikaaf) katika Msikiti kwa ajili ya utiifu kwa Allaah (‘Azza wa Jalla) katika kumwabudu Yeye, na kujikurubisha Kwake na kujipwekesha katika kumwabudu.
b. Ama sharti zake, basi ni kama zilivyo sharti za ‘ibaadah zote miongoni mwazo ni: Uislamu, akili, na inasihi kwa asiyebaleghe, na inasihi kwa mwanaume na mwanamke.
c. Na inasihi bila ya Swawm, na inasihi katika Misikiti yote.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/162)]
Je, I’tikaaf Ina Wakati Maalumu Katika Kuingia Na Kutoka Kwake Na Je, Inajzu Kuikata?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
15. Je, I’tikaaf Ina Wakati Maalumu Katika Kuingia Na Kutoka Kwake Na Je, Inajzu Kuikata?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
a. Kauli ya sahihi kabisa ya Ahlul-‘Ilm ni kwamba haina wakati maalumu.
b. Na Sunnah ni mtu aingie akiwa Mu’takif pindi anapotia niyyah kwa ajili ya I’tikaaf na atoke baada ya kumaliza muda wake alionuiya.
c. Na anaweza kuikata ikiwa atahitaji kufanya hivyo kwa sababu I’tikaaf ni Sunnah haipasi kujiwajibisha nayo ikiwa ni mwenye udhuru.
d. Na I’tikaaf inapendekezeka katika makumi ya mwisho ya Ramadhwaan na ni mustahabu kwa mwenye kuingia I’tikaaf aingie akiwe Mu’takif baada ya Swalaah ya Alfajiri kuanzia siku ya ishirini na moja, kama alivyofanya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na atoke inapomalizika masiku kumi (ya mwisho).
[Majmu’w Al-Fataawaa (15/442)]
I’tikaaf Inaanza Lini?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
16. I’tikaaf Inaanza Lini?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
‘Ulamaa wote wamekubaliana kwamba I’tikaaf inaanza usiku wa (kuamkia tarehe) ishirini na moja, na si Alfajiri ya ishirini na moja.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/160)]
Lini Anapaswa Mu’takif Kutoka Katika I’tikaaf Yake?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
17. Lini Anapaswa Mu’takif Kutoka Katika I’tikaaf Yake?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
Anatoka Mu’takif kutoka katika I’tikaaf yake inapomalizika Ramadhwaan, na Ramadhwaan humalizika kwa kuzama jua usiku wa ‘Iyd.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/170)]
Kutiya Niyyah I’tikaaf Makumi Ya Mwisho Ramadhwaan Kisha Kutoka Usiku Wa Mwisho
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
18. Aliyetia Niyyah Kuingia I’tikaaf Makumi Ya Mwisho Katika Ramadhwaan Kisha Akataka Kutoka Usiku Wa Mwisho; Je, Kuna Makosa Juu Yake?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
Ikiwa hakuwekea nadhiri na kukata kwake ni katika siku ya mwisho au kabla yake, basi hakuna dhambi juu yake. Lakini linalopendekezeka zaidi ni akamilishe ili apate kutekeleza Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwani yeye hakuwa akitoka kwenye I’tikaaf yake mpaka iingie mwezi wa Shawwaal.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/184)]
Nini Kimpasacho Mu’takif Katika Kutekeleza I’tikaaf Yake?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
19. Nini Kimpasacho Mu’takif Katika Kutekeleza I’tikaaf Yake?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
Ni juu ya Mu’takif atimize I’tikaaf yake na ajishughulishe na dhikru-Allaah na ‘ibaadah wala asitoke isipokuwa kwa haja anayohitaji mwana Aadam kama kwenda msalani kukojoa na kadhaalika, au akihitaji chakula ikiwa hakupata uwezekano wa mwenye kumtayarishia chakula basi atoke kwa ajili ya haja yake hiyo wala haijuzu kwa mwanamke amwendee mumewe hali ya kuwa yeye mke yuko kwenye I’tikaaf.
Na kadhaalika Mu’takif haimpasi kumwendea mkewe, na lilo bora kwake ni kwamba asizungumze na watu lakini akiwa ametembelewa na baadhi ya ndugu zake au mwanamke ametembelewa na baadhi ya mahaarim wake akazungumza nao (wanaume) au akazungumza na wanawake wenzake, basi hakuna neno.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (15/440)]
Yepi Yanayopendekezeka Kwa I’tikaaf?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
20. Yepi Yanayopendekezeka Kwa I’tikaaf?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
Yanayopendekeza kwake ni mtu kujishughulisha na utiifu kwa Allaah (‘Azza wa Jalla) katika kusoma Qur-aan, na dhikru-Allaah, na Swalaah na kadhaalika, na wala asipoteze muda wake katika yasiyokuwa na faida humo.’
[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/175)]
Nini Hukmu Ya Mu’takif Kutoka Katika I’tikaaf?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
21. Nini Hukmu Ya Mu’takif Kutoka Katika I’tikaaf?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
Ama kutoka kwake kutoka Masjid, ‘Ulamaa wameigawa katika sehemu tatu:
[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/157)]
Inajuzu Kwa Mu’takif Aende Nyumbani Kwake Kwa Ajili Ya Kula Chakula Na Kuoga?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
22. Je Inajuzu Kwa Mu’takif Aende Nyumbani Kwake Kwa Ajili Ya Kula Chakula Na Kuoga?
Imaam Ibn ‘Uthaymin (Rahimahu Allaah) amesema:
[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/178)]
Inajuzu Kwa Mu’takif Apige Simu Kukidhi Haja Za Baadhi Ya Waislamu?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
23. Je, Inajuzu Kwa Mu’takif Apige Simu Kukidhi Haja Za Baadhi Ya Waislamu?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
a. Inajuzu kwa Mu’takif kutumia simu kwa ajili ya kuwakidhia haja za Waislamu ikiwa simu iko katika Msikiti ambao anatekeleza I’tikaaf, kwa sababu hatoki nje ya Msikiti.
b. Ama ikiwa nje ya Msikiti basi asitoke kwa ajili ya jambo hilo. Na kuwakidhia haja Waislamu ikiwa mtu huyo ndiye mwenye jukumu nao basi asikae I’tikaaf kwa sababu kuwakidhia haja Waislamu kuna umuhimu zaidi kuliko kutekeleza I’tikaaf.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/180)]
Inajuzu Kwa Mu’takif Amtembelee Mgonjwa? Au Inamuajibikia Kufanya Da’wah?
Al-Lajnah Ad-Daaimah
24. Je, Inajuzu Kwa Mu’takif Amtembelee Mgonjwa? Au Inamuajibikia Kufanya Da’wah?
Sunnah ni kwamba asitembelee mgonjwa wakati akiwa katika I’tikaaf, wala haiwajibiki da’wah wala kuwakidhia haja ahli zake wala kuhudhuruia janaazah, wala asitoke nje ya Msikiti kwa ajili ya kwenda kazini kwake.
[Al-Lajnah Ad-Daaimah (10/410)]
Hukmu Ya Mu’takif Kutoka Kwa Ajili Ya Kwenda Kutekeleza ‘Umrah?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
25. Nini Hukmu Ya Mu’takif Kutoka Kwa Ajili Ya Kwenda Kutekeleza ‘Umrah?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
[Majmuw’ Al-Fataawaa (15/446)]
Mu’takif Anayekuwa Katika Al-Haram Apande Sakafu Za Juu Kwa Ajili Ya Kusikiliza Duruws?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
26. Je, Inajuzu Kwa Mu’takif Anayekuwa Katika Al-Haram (Makkah) Apande Sakafu Za Juu Kwa Ajili Ya Kusikiliza Duruws?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
Kupanda sakafu za juu ya Msikiti hiyo haidhuru kwani kutoka katika mlango wa Msikiti wa chini kupanda juu kwenye sakafu si chochote bali ni hatua chache, na pia anakusudia kurudi (chini) Msikitini pia. Basi hakuna ubaya katika hili.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/181)]
Lipi Bora Kwa Mwenye Majukumu; Atekeleze I’tikaaf Au Atimize Majukumu Yake?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
27. Lipi Bora Kwa Mwenye Majukumu; Atekeleze I’tikaaf Au Atimize Majukumu Yake?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/178)]
Inajuzu Kwa Mu’takif Abadilishe Sehemu Kuhamahama Ndani Ya Msikiti?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
28. Je, Inajuzu Kwa Mu’takif Abadilishe Sehemu Kuhamahama Ndani Ya Msikiti?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
Inajuzu kwa Mu’takif kbadilisha sehemu katika Msikiti katika pande zozote zile.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/177)]
Mu’takif Katika Masjid Al-Haraam Afanye Twawaaf Kuzunguka Al-Ka’bah?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
29. Je, Inajuzu Kwa Mu’takif Katika Masjid Al-Haraam (Makkah) Afanye Twawaaf Kuzunguka Al-Ka’bah?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
Ikiwa yuko Masjid Al-Haraam afanye Twawaaf, kwa sababu I’tikaaf haimaanishi kwamba mtu agande sehemu moja asibadilishe sehemu, bali maana ya I’tikaaf ni kujiambatanisha na Masjid.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/180)]
Wanawake Kwenda Msikitini Kuswali Taraawiyh Na I´tikaaf
Shaykh ´Abdul-´Aziyz Aali Ash-Shaykh (Hafidhwahu-Allaah)
SWALI:
Je, inajuzu kwa mwanamke ambaye hajaolewa kwenda Msikitini wakati wa futari, kisha abakie Msikitini mpaka ifike wakati wa Taraawiyh? Na je inajuzu kwake kufanya I’tikaaf siku 10 za mwisho Msikitini?
JIBU:
Lililo asili na bora zaidi ni kuwa Swalaah ya mwanamke aswali nyumbani. Lakini kwenda (mwanamke) Msikitini, kama haitosababisha fitnah inajuzu.
Anasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
"Ikiwa mmoja wenu mke wake atamuomba ruhusa ya kwenda, asimkatalie".
Na anasema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa):
"Alikuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiswali Swalaatul-Fajr, wakihudhuria naye Swalaah waumini wanawake, wakirudi (majumbani kwao) hakuna aliyekuwa akiwajua kutokana na giza".
Kwa hiyo wanaweza kwenda kuswali Msikitini ikiwa kama haitosababisha fitnah, na wajisitiri vizuri, na wasichanganyike na wanaume.
Hali kadhalika wanaweza kwenda kufanya I’tikaaf Msikitini kama hakutokuwa fitnah.
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/261
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8390&title=Fataawaa%3A%20%27Itikaaf%20%28Kubakia%20Msikitini%20Kufanya%20%27Ibaadah%29
[4] http://www.alhidaaya.com
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8575&title=01-%20Imaam%20Ibn%20Baaz%20na%20Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%20%3A%20Nini%20Maana%20Ya%20%E2%80%98Itikaaf%3F
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8576&title=02-%20Imaam%20Ibn%20Baaz%20na%20Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%20%3A%20Nini%20Hukmu%20Ya%20I%E2%80%99tikaaf%3F
[7] http://www.alhidaaya.com/
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8577&title=03-%20Imaam%20Ibn%20Baaz%20na%20Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%20%3A%20Je%2C%20I%E2%80%99tikaaf%20Inafaa%20Ki-Shariy%E2%80%99ah%20Miezi%20Mingineyo%20Isiyokuwa%20Ramadhwaan
[9] http://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarallsubjects&schid=
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8393&title=05-Shaykh%20%C2%B4Abdul-Muhsin%20Al-%E2%80%98Abbaad%3A%20Kufanya%20I%C2%B4itikaaf%20Haishurutishwi%20Kuwa%20Na%20Swawm
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8578&title=06-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20Je%2C%20Ili%20I%E2%80%99tikaaf%20Iwe%20Sahihi%20Inalazimika%20Mtu%20Awe%20Katika%20Swawm%3F
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8579&title=07-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Je%2C%20I%E2%80%99tikaaf%20Inajuzu%20Wakati%20Wowote%20Ule%20Nje%20Ya%20Masiku%20Kumi%20Ya%20Mwisho%20Ya%20Ramadhwaan%3F
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8580&title=08-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Je%2C%20I%E2%80%99tikaaf%20Ya%20Mwanamke%20Ni%20Sawa%20Na%20Ya%20Mwanaume%3F%20
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8581&title=09-Imaam%20Ibn%20Baaz%20na%20Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Sehemu%20Gani%20Inapaswa%20Kutekelezwa%20I%E2%80%99itikaaf%3F
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8582&title=10-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20Je%2C%20I%E2%80%99tikaaf%20Inajuzu%20Katika%20Masjid%20Al-Haraam%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Wanawake%20Na%20Wanaume%3F
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8583&title=11-Imaam%20Ibn%20Baaz%20na%20Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%20%3A%20Je%2C%20I%E2%80%99tikaaf%20Inasihi%20Katika%20Misikiti%20Mingineyo%20Isiyokuwa%20Ile%20Mitatu%3F%20%20
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8584&title=12-Imaam%20Ibn%20Baaz%20%3A%20Mwanamke%20Atekeleze%20Wapi%20I%E2%80%99tikaaf%20Akipenda%20Kufanya%20Hivyo%3F
[18] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8585&title=13-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Vyumba%20Vya%20Matumizi%20Vya%20Masjid%20Vinafaa%20Kutumika%20Kwa%20I%27tikaaf%3F
[19] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8586&title=14-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%20%3A%20Zipi%20Nguzo%20Za%20I%E2%80%99tikaaf%20Na%20Sharti%20Zake%3F%20Na%20Je%2C%20Inasihi%20Bila%20Ya%20Swawm%3F
[20] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8587&title=15-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20I%E2%80%99tikaaf%20Ina%20Wakati%20Maalumu%20Katika%20Kuingia%20Na%20Kutoka%20Kwake%20Na%20Je%2C%20Inajzu%20Kuikata%3F
[21] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8588&title=16-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20I%E2%80%99tikaaf%20Inaanza%20Lini%3F
[22] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8589&title=17-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Lini%20Anapaswa%20Mu%E2%80%99takif%20Kutoka%20Katika%20I%E2%80%99tikaaf%20Yake%3F
[23] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8590&title=18-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Kutiya%20Niyyah%20I%E2%80%99tikaaf%20Makumi%20Ya%20Mwisho%20Ramadhwaan%20Kisha%20Kutoka%20Usiku%20Wa%20Mwisho
[24] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8591&title=19-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20Nini%20Kimpasacho%20Mu%E2%80%99takif%20Katika%20Kutekeleza%20I%E2%80%99tikaaf%20Yake%3F
[25] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8592&title=20-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Yepi%20Yanayopendekezeka%20Kwa%20I%E2%80%99tikaaf%3F
[26] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8593&title=21-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Nini%20Hukmu%20Ya%20Mu%E2%80%99takif%20Kutoka%20Katika%20I%E2%80%99tikaaf%3F%20
[27] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8594&title=22-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20%20Inajuzu%20Kwa%20Mu%E2%80%99takif%20Aende%20Nyumbani%20Kwake%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Kula%20Chakula%20Na%20Kuoga%3F
[28] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8595&title=23-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Inajuzu%20Kwa%20Mu%E2%80%99takif%20Apige%20Simu%20Kukidhi%20Haja%20Za%20Baadhi%20Ya%20Waislamu%3F
[29] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8596&title=24-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Inajuzu%20Kwa%20Mu%E2%80%99takif%20Amtembelee%20Mgonjwa%3F%20Au%20Inamuajibikia%20Kufanya%20Da%E2%80%99wah%3F
[30] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8597&title=25-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20Hukmu%20Ya%20Mu%E2%80%99takif%20Kutoka%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Kwenda%20Kutekeleza%20%E2%80%98Umrah
[31] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8598&title=26-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%20%3A%20Mu%E2%80%99takif%20Katika%20Al-Haram%20Apande%20Sakafu%20Za%20Juu%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Kusikiliza%20Duruws%3F
[32] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8599&title=27-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%20%3A%20Lipi%20Bora%20Kwa%20Mwenye%20Majukumu%3B%20Atekeleze%20I%E2%80%99tikaaf%20Au%20Atimize%20Majukumu%20Yake%3F%20
[33] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8600&title=28-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%20%3A%20Inajuzu%20Kwa%20Mu%E2%80%99takif%20Abadilishe%20Sehemu%20Kuhamahama%20Ndani%20Ya%20Msikiti%3F%20
[34] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8601&title=29-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%20%3A%20Mu%E2%80%99takif%20Katika%20Masjid%20Al-Haraam%20Afanye%20Twawaaf%20Kuzunguka%20Al-Ka%E2%80%99bah%3F
[35] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8394&title=31-Shaykh%20%C2%B4Abdul-%C2%B4Aziyz%20Aali%20Ash-Shaykh%3A%20Wanawake%20Kwenda%20Masjid%20Kuswali%20Taraawiyh%20Na%20I%C2%B4tikaaf