Israfu Ya Chakula Wakati Wa Futari
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Je, mtu hupata thawabu ndogo (ya Swawm) ikiwa atakithirisha kukata Swawm (Futari) kwa masahani ya vyakula mbali mbali?
JIBU:
Hapana, hupati thawabu ndogo ya Swawm. Mtu kufanya kitendo cha haraam baada ya kumaliza Swawm, (kitendo kile) hakiathiri thawabu (za Swawm). Bali inaingia katika neno Lake Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ ﴿٣١﴾
“Na kuleni na kunyweni; na wala msifanye israfu. Hakika Yeye (Allaah) Hapendi wanaofanya israfu. [Al-A’raaf 7: 31]
Huku kufanya israfu ndiyo haraam. Na iktisadi ni nusu ya maisha. Ikiwa bila kukusudia kutabaki chakula, ni afadhali kitolewe swadaqah.
[Fiqhu Al-'Ibaadah, uk. 252]
Kupiga Punyeto Mchana Wa Mwezi Wa Ramadhwaan
Shaykh 'Abdul-'Aziyz Aal Ash-Shaykh (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Muuliza kutoka Canada anauliza, nimetoa Manii (punyeto) mchana wa Ramadhwaan hali ya kuwa nimefunga. Nifanye nini?
JIBU:
(Alichofanya ni haraam) na ni juu yake alipe siku hio. Kwa kuwa kutoa manii kwa makusudi haijuzu. Allaah Anasema: "Mwenye kufunga anatakiwa kuacha chakula chake, kinywaji chake na matamanio yake kwa ajili Yangu".
Kusafiri Kwa Niyyah Ya Kukwepa Kufunga Swawm Ramadhwaan
Imaam Ibn ‘Uthyamiyn (Rahimahu-Allaah)
Tuchukulie mtu anasema:
"Kama inajuzu mtu kusafiri katika Ramadhwaan na inajuzu kutofunga kwa msafiri, ina maana kwamba mnajuzisha kuepuka waajib wa kufunga."
Kama niyyah (lengo) la safari ni kwa ajili ya kuepuka Swiyaam, hivyo safari imekatazwa. Safari haijuzu kwa kuwa mtu amenuia kuepuka kitu ambacho ni waajib kwake. Hali kadhalika haijuzu kukata Swawm katika hali kama hii.
[Imaam Ibn 'Uthaymiyn Fat-h Dhil-Jalaal Wal-Ikraam (7/257)]
Anayempikia Chakula Mume Wake Asiefunga Katika Ramadhwaan
Imaam Bin Baaz (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Mume wangu hataki kufunga zaidi ya miaka ishirini. Kipindi chote hicho nilikuwa nikimpikia chakula wakati mimi mwenyewe nimefunga. Je ninapata madhambi?
JIBU:
Ndiyo, ni dhambi. Lazima utubu kwa Allaah kwa kitendo hicho. Wakati wewe unampikia chakula mchana wa Ramadhwaan, unamsaidia kumuasi Allaah (’Azza wa Jall). Allaah (Jalla wa 'Alaa) Anasema:
وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ ۚ
Na shirikianeni katika wema na taqwa, na wala msishirikiane katika dhambi na uadui. [Al-Maaidah : 2]
Kumpikia chakula au kumtengea chakula na kumpa mchana wa Ramadhwaan au kumpa sigara au pombe n.k. ni dhambi, na ni maovu juu ya maovu. Hupaswi kabisa kumsaidia kutofunga sawa ikiwa ni (kwa kumpa) chakula, kinywaji, sigara au pombe. Yote haya ni madhambi juu ya madhambi, Tunamuomba Allaah Al-‘Aafiyah. Bali ni juu yako kumnasihi na kukataa kumtii na kumwambia huwezi kumsadia kwa hilo, na arudie kubeba madhambi mwenyewe.
[Mawqi' Ar-Rasmiy li-Imaam bin Baaz] [8]
Hukmu Ya Anayefunga Na Kuswali Ramadhwaan Pekee
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Unasemaje kwa yule mtu ambaye anaswali na kufunga wakati wa Ramadhwaan tu? Wakati Ramadhwaan inakwisha, anaacha kuswali na kufunga?
JIBU:
Kilicho dhahiri kwangu kutokana na dalili, ni kwamba mtu kama huyo anachukuliwa kama ni kafiri kama haswali kabisa. Ama kuhusu yule ambaye anaswali wakati fulani na wakati mwingine haswali, sidhani kuwa dalili yaonesha kuwa mtu huyo ni kafiri (moja kwa moja).
Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Ahadi baina yetu sisi na wao (makafiri) ni Swalaah. Yule atakayeiacha huyo amekufuru.”
Na pia:
"Baina ya mshirikina na shirki ni mtu kuacha Swalaah.”
Ndiyo maana nina mashaka ya iymaan ya mtu ikiwa anaswali na kufunga wakati wa Ramadhwaan pekee. Kama kweli ni Muumini wa kweli, anapaswa kuswali wakati wote ikiwa ni Ramadhwaan na baada ya Ramadhwaan.
Kumjua Rabb wake wakati wa Ramadhwaan pekee, ninaingiwa na shaka kutokana na iymaan yake. Hata hivyo sisemi kuwa ni kafiri moja kwa moja, badala yake ninamdhania vizuri na kumuachia suala lake kwa Allaah (‘Azza wa Jalla).
[Fiqhul-'Ibaadat, uk. 248, Madaar Al-Watwan, 1424]
Anayeacha Swiyaam Ramadhwaan Juu Ya Kuwa Hapingi Kuwajibika Kwake
Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu-Allaah)
SWALI:
Mwenye kuacha Swiyaam ya Ramadhwaan lakini hapingi kuwajibika kwake je anakufuru kwa hilo?
JIBU:
Ndio. Vipi ataacha Swiyaam na wakati huo hapingi? Vipi ataacha Swawm ya Ramadhwaan naye hana udhuru unaomruhusu ki-Shariy’ah ikiwa kweli hapingi? Ameacha kwa kuwa anaona si waajib:
[Fataawa Ramadhwaan Shaykh Fawzaan]
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/261
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8406&title=Fataawaa%3A%20Maasi%20Katika%20Ramadhwaan
[4] http://www.alhidaaya.com/
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8408&title=01-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Israfu%20Ya%20Chakula%20Wakati%20Wa%20Futari
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8410&title=03-Shaykh%20%27Abdul-%27Aziyz%20Aal%20Ash-Shaykh%3A%20Kupiga%20Punyeto%20Mchana%20Wa%20Mwezi%20Wa%20Ramadhwaan%20
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8411&title=04-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthyamiyn%3A%20Kusafiri%20Kwa%20Niyyah%20Ya%20Kukwepa%20Kufunga%20Swawm%20Ramadhwaan
[8] https://binbaz.org.sa/noor/9859
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8412&title=05-Imaam%20Bin%20Baaz%3A%20Anayempikia%20Chakula%20Mume%20Wake%20Asiefunga%20Katika%20Ramadhwaan%20
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8413&title=06-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Hukmu%20Ya%20Anayefunga%20Na%20Kuswali%20Ramadhwaan%20%20Pekee
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8499&title=07-Shaykh%20Swaalih%20Al-Fawzaan%3A%20Anayeacha%20Swiyaam%20Ramadhwaan%20Juu%20Ya%20Kuwa%20Hapingi%20Kuwajibika%20Kwake