Kutumia Dawa Kuzia Hedhi Katika Ramadhwaan Apate Kufunga Mwezi Mzima
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Nini hukmu ya mwanamke kutumia dawa za uzazi ili kuzuia kufika kwa damu ya hedhi apate kumaliza swiyaam mwezi mzima? Tufaidisheni, Allaah Akufaidisheni nanyi.
JIBU:
Hakuna ubaya kufanya hivyo kwamba atumie vidonge vya kuzuia hedhi ili aweze kuswali na watu na afunge nao kwa sharti kwamba kufanya hivyo kuna usalama kwake na havitomdhuru. Na pia baada ya kupata ushauri wa daktari ili asije kujidhuru nafsi yake, na pia apate ruhusa kutoka kwa mumewe ili asimuasi mumewe.
Itakapokuwa baada ya kushauriana na kutahadhari upande wa salama kutokana na madhara, basi hakuna ubaya.
Na hali hiyo hiyo iwe katika masiku ya Hajj.
Baaraka Allaahu Fiykum
[Al-Mawqi’ Ar-Rasmiy – Imaam Ibn Baaz] [5]
Alipe Siku Ambayo Amepata Maumivu Ya Hedhi Kabla Ya Jua Kuzama?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Je, Swawm ya mwanamke ni Sahihi, au ni waajib kwake kulipa siku hiyo, ikiwa anadhani (anahisi) atapata hedhi au yuko na maumivu ya hedhi lakini bila ya yeye kupata chochote kabla ya jua kuzama?
JIBU:
Ikiwa mwanamke aliye msafi anahisi kwamba damu iko njiani au ana maumivu ya hedhi wakati yeye ni mwenye Swawm bila ya yeye kutokwa na kitu kabla ya jua kuzama, Swawm yake ni sahihi. Hana haja ya kulipa siku hiyo ikiwa kama ni Swawm ya waajib, na hatokosa ujira wake ikiwa ni Swawm ya Sunnah.
[Imaam Ibn 'Uthaymiyn - Su-alaat ‘an Ahkaamil-Haydhw uk. 11]
Aliyepatwa Na Damu Ya Hedhi Baada Ya Kutiya Niyyah Ya Swawm
Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)
SWALI:
Nini hukmu ya mwanamke imemjia damu baada ya kutia niyyah ya swiyaam?
JIBU:
Ikiwa amefunga kisha ikamtokea damu ya mwezi, basi swawm yake imeharibika na inambidi afungue na ale masiku ya hedhi. Itakapokatika damu pindi imemalizika hedhi yake, basi arudie kufunga mwezi uliobakia kisha alipe masiku aliyokuwa hakufunga ambayo ni ya siku za hedhi yake.
[Al-Muntaqaa Min Fataawaa Al-Fawzaaan (7/51]
Imemjia Hedhi Dakika Chache Kabla Ya Magharibi Nini Hukmu Ya Swawm Yake?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Hukmu ya mwanamke aliyefunga amepata hedhi dakika chache tu kabla ya kuzama jua (Magharibi).
JIBU:
Ikiwa hedhi imeanza wakati mwanamke amefunga hata ikiwa ni dakika moja basi Swawm yake haifai na itambidi ailipe siku ile. Haruhusiwi kufunga wakati yuko kwenye hedhi, na akifunga basi Swawm yake haifai.
[Imaam Ibn 'Uthaymiyn - Majaalis Shahr Ramadhwaan, Ukurasa 39]
Mwanamke Mwenye Hedhi Aliyetwaharika Baada Tu Ya Alfajiri
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Je, mwanamke ambaye anayetwaharika baada tu ya alfajiri atafunga siku inayobaki, au ni juu Yake kulipa siku hiyo?
JIBU:
Ikiwa mwanamke atatwaharika baada tu ya Alfajiri, Wanachuoni wana kauli mbili kuhusiana na Swawm yake:
Rai ya kwanza: Anapaswa kufunga siku iliyobaki bila ya kupewa thawabu ya siku hiyo. Kisha baadaye ni waajib kwake kulipa siku hiyo. Hii ni kauli maarufu katika madhehebu ya Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah).
Rai ya pili: Hana haja ya kufunga siku iliyobaki. Swawm yake ni batili (ikiwa atafunga) siku hiyo kwa kuwa alianza siku hali ya kuwa ni mwenye hedhi na si kama mwenye Swawm. Kwa hiyo hali kama hii Swawm yake si sahihi, hakuna faida yoyote ya yeye kufunga.
Wakati huo hauna faida kwake. Kaamrishwa kujiepusha na kufunga katika siku za mwanzo ya siku hiyo. Kwa kuwa amekatazwa kufunga wakati huo (wa hedhi). Msingi wa Shariy’ah kuhusiana na Swawm kama tujuavyo sote ni kuacha chakula na kunywa kuanzia Alfajiri mpaka jioni tukiwa na niyyah ya kumuabudu Allaah kwa hilo.
Tunaamini kuwa mtazamo huu ni wenye nguvu zaidi kuliko mtazamo unaosema afunge siku nzima iliyobaki. Hata hivyo maoni zote mbili ni waajib kwake kulipa siku hiyo.
[Imaam Ibn ‘Uthyamiyn - Sualaat ‘An Ahkaamil-Haydhw, uk. 9-10]
Imemjia Hedhi Dakika Tano Kabla Ya Magharibi
Akidhi Swalaah Ya Magharibi Baada Ya Kutoharika?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Nimefunga siku moja katika Ramadhwaan na haikubaki kitu siku hiyo isipokuwa dakika tano tu kufikia wakati wa kufuturu ikanijia hedhi ya mwezi. Je, ninawajibika kuswali Swalaah ya Magharibi kama kukidhi baada ya kutwaharika au la?
JIBU:
Ikiwa hedhi imemjia kabla ya Magharibi kuingia basi haimuwajibikii kuswali Swalaah ya Magharibi wala Swalaah nyinginezo.
Na Swawm pia siku hiyo haitosihi, siku ambao imemjia hedhi kabla ya kuzama jua kwani swawm imebatilika na imemuwajibikia kulipa siku hiyo, ikiwa anajua kuwa imemjia hedhi kabla ya Magharibi kuingia.
[Al-Mawqi’ Ar-Rasmiy - Imaam Ibn Baaz] [11]
Amemaliza Damu Ya Uzazi Kabla Ya Ramadhwaan Kisha Akaanza Swiyaam
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Mke wangu alizaa mtoto kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhwaan baada ya siku saba alisafika (damu ya uzazi ikaisha) kabla ya kuingia Ramadhwaan. (Kisha akafunga Ramadhwaan) Je, funga yake imefaa au anatakiwa alipe siku hizo ingawa alifunga wakati alikuwa yuko katika twahaarah (ya damu ya uzazi) Tafadhali tujulisheni. Allaah Akulipeni mema.
JIBU:
Ikiwa hali ni kama ilivyoelezwa, basi swawm ya mke wako katika mwezi wa Ramadhwaan wakati yuko katika hali ya twahaarah (kukauka damu ya uzazi) inafaa na haimpasi kulipa siku hizo.
Na kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ndio yako mafanikio yote na Swalah na Salaam zimfikie Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaaba zake.
[Halmashauri Ya Kudumu Ya Utafiti wa Kiislamu na Fataawaa inayoongozwa na:
Kiongozi Mkuu: Shaykh 'Abdul-'Aziyz 'Abdillaah Ibn Baaz.
Msaidizi Kiongozi Mkuu: Shaykh 'Abdur-Razzaaq 'Afiyfiy
Mwanachama: Shaykh 'Abdullah Ibn Ghudayyaan
Fataawa Ramadhwaan, Mjalada 2, Ukurasa 590, Fatwa Nambari 575. Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah Lil-buhuwth Al-'Ilmiyyah Wal-Iftaa , Fatwa Nambari 10138
Nyongeza:
Hii ina maana kwamba si lazima mwanamke aliyezaa akamilishe siku 'arubaini ndio aweze kufunga au kuswali. Madamu kamaliza kutoka damu ya uzazi na ametwaharika, basi siku yoyote ile atakayotwaharika, inampasa afanye ghuslu (josho) kisha atimize ‘ibaadah zake kama kawaida.
Imemjia Hedhi Muda Mdogo Tu Kabla Ya Adhaan Ya Magharibi
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Ikiwa amefunga kisha wakati wa Magharibi kabla ya muda mdogo tu na kabla ya Adhaan imemjia hedhi je swawm yake itakuwa imeharibika?
JIBU:
Ikiwa hedhi imemjia kabla ya Magharibi swawm yake itakuwa imebatilika na itampasa ailipe, ama ikiwa baada ya Magharibi basi swawm yake ni sahihi wala hahitaji kuilipa.
Wa bi-LLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyinaa Muhammad wa ‘alaa Aalihi wa Swahbihi wa sallam
[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah 10/155]
Imemjia Hedhi Baada Ya Magharibi Kabla Ya ‘Ishaa Swawm Yake Sahihi?
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Inapokuwa mwezi wa Ramadhwaan baada ya kufuturu na baada ya Swalaah ya ‘Ishaa imemjia hedhi; je, alipe siku hiyo au swawm yake sahihi?
JIBU:
Swawm ya ambaye imemjia hedhi baada ya Magharibi na kabla ya Swalaah ya ‘Ishaa ni sahihi swawm yake aliyofunga siku hiyo wala haimwajibikii kuilipa.
Wa bi-LLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyinaa Muhammad wa ‘alaa Aalihi wa Swahbihi wa sallam
[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah (14043)]
Ametumia Vidonge Vya Kuzuia Mimba Je Alipe Masiku Ya Hedhi Japokuwa Hakuona Damu?
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Mke wangu ametumia vidonge vya kuzuia mimba, na katika Ramadhwaan ya mwaka huu, ameendeleza kula dawa mpaka mwisho wa mwezi akisema kusudio lake akamilishe Swiyaam ili asifungulie. Je anapaswa kulipa masiku ya hedhi japokuwa hakuona damu isipokuwa siku ya nne katika masiku ya ‘Iyd, basi je, inamlazimu afunge masiku hayo ambayo hakuwa akila?
JIBU:
Ikiwa hali na kama ilivyotajwa kwamba haikumtremkia mkewe damu ya hedhi katika mchana wa Ramadhwaan kwa sababu ya kutumia vidonge vya kuzuia mimba basi haiwajibiki kwake kulipa masiku hayo.
Wa bi-LLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyinaa Muhammad wa ‘alaa Aalihi wa Swahbihi wa sallam
[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah (16264)]
Hakulipa Swawm Alipokuwa Katika Hedhi Miaka Yote Iliyopita Ya Ramadhwaan
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Bibi mtu mzima mwenye umri wa miaka 60 alikuwa hajui hukumu ya kulipa Swawm alizokuwa hafungi wakati alipokuwa katika hedhi miaka mingi. Miaka yote iliyompita hakulipa siku zake za Swawm za Ramadhwaan akifikiri kwamba kulikuwa hakuna haja ya kuzilipa. Hivi ni kutokana na alivyosikia kutoka kwa watu.
JIBU:
Inampasa aombe maghfirah na tawbah kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa kutokuuliza wenye elimu.
Kisha alipe siku zote alizokuwa hakufunga na alipe kafara kwa kulisha maskini mmoja nusu pishi (vibaba viwili ambavyo ni sawa na 1.5kg) ya shayiri au tende au mchele au chakula chochote kinachotumika (sana) katika nchi anayoishi. Hivyo ni kama anao uwezo, na ikiwa hana uwezo wa kulisha maskini basi inamtosha kulipa tu siku alizokuwa hakufunga.
Wa biLLaahi at-tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Al-Lajnah Ad-Daaimah - Halmashauri ya kudumu ya Utafiti Wa Kiislaam Inayoongozwa:
Kiongozi Mkuu: Shaykh 'Abdul 'Aziyz ibn 'Abdillaah ibn Baaz
Msaidizi Kiongozi Mkuu: Shaykh ‘Abdullaah ibn Ghudayyaan
Mwanachama: Shaykh 'Abdullaah Ibn Ghudayyan
Mwanachama: Shaykh ‘Abdullah ibn ‘Awd
Fataawa Ramadhwaan - Mjalada 2, Ukurasa 583, Fatwa Namba 567]
Fataawa al-Lajnah ad-Daaimah lil-Buhuuth al-'Ilmiyyah wal-Iftaa. - Fatwa Namba 1790]
Hakuweza Kulipa Swawm Kwa Sababu Miaka Michache Alikuwa Anazaa Siku Za Ramadhwaan
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Nini hukmu kuhusu mwanamke aliyekuwa akizaa siku za Ramadhwaan (kwa kutokea hivyo) muda wa miaka michache na hakuweza kulipa Swawm ya siku alizokuwa hakufunga?
JIBU:
Inawajibika kwa mwanamke aliyejifungua katika mwezi wa Ramadhwaan kulipa siku alizokuwa hakuweza kufunga siku za mbele.
Na ikiwa hakulipa siku hizo bila sababu inayokubalika katika Shariy’ah ya Kiislamu hadi imeingia Ramadhwaan nyingine, basi inampasa alishe maskini kwa idadi ya siku alizokuwa hakufunga na pia afunge Swaum za siku hizo.
Lakini kama kuchelewa kulipa kulikuwa kwa sababu inayokubaliwa katika Shariy’ah ya Kiislamu basi inamtosha kuzilipa tu siku hizo.
Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Fataawa Ramadhwaan - Mjalada 2, Ukurasa 588, Fatwa Namba 573;
Fataawa Al-Lajnah Ad-Daaimah lil-Buhuwth Al-'Ilmiyyah wal-Iftaa. - Fatwa Namba 9861]
Mwenye Mimba Na Mnyonyeshaji Walipe Swawm Au Walishe Masikini?
Shaykh Swaalih Al-Luhaydaan
SWALI:
Mwanamke anauliza pamoja na dada yake. Yeye ni mja mzito na dada yake ananyonyesha. Wanauliza kama wanaingia katika hukmu ya mgonjwa au inatosha kwao kulisha maskini kwa kila siku moja bila ya kulipa siku hizo?
JIBU:
Mwenye mimba na mwenye kunyonyesha, wakikhofia madhara kwenye afya zao, hukmu yao itakuwa kama ya mgonjwa itabidi wale na wasifunge.
Ama ikiwa atakuwa na khofu kwa ajili ya mtoto aliye tumboni au kijusu, basi ni juu yao kulipa siku hizo na walipe pia kafara. Na Kafara ni kulisha masikini mmoja kwa kila siku.
Na kuna ikhtilaaf katika masuala ya (kulisha) chakula. Kuna wanaosema akila sawa akiwa na khofu mwenyewe au na kwa mtoto wake watakula na hawatolisha masikini, ama kuhusiana na kulipa siku zile ni jambo la waajib.
(Hatomlisha masikini) ikiwa yeye binafsi hakuweza kufunga siku miongoni mwa siku (kwa sababu za ki Shariy’ah) hapo ndipo ataingia kwenye hukmu ya mgonjwa.
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/261
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8433&title=Fataawaa%3A%20Kulipa%20Swawm%20Na%20Kafara%3A%20Hedhi%2C%20Mja%20Mzito%2C%20Kunyonyesha%2C%20Nifaas
[4] http://www.alhidaaya.com
[5] http://www.binbaz.org.sa/noor/9833
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8435&title=01-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20Kutumia%20Dawa%20Kuzia%20Hedhi%20Katika%20Ramadhwaan%20Apate%20Kufunga%20Mwezi%20Mzima
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8436&title=02-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Alipe%20Siku%20Ambayo%20Amepata%20Maumivu%20Ya%20Hedhi%20Kabla%20Ya%20Jua%20Kuzama%3F
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8440&title=03-Shaykh%20Swaalih%20Al-Fawzaan%3A%20Aliyepatwa%20Na%20Damu%20Ya%20Hedhi%20Baada%20Ya%20Kutiya%20Niyyah%20Ya%20Swawm
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8437&title=04-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Imemjia%20Hedhi%20Dakika%20Chache%20Kabla%20Ya%20Magharibi%20Nini%20Hukmu%20Ya%20Swawm%20Yake%3F
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8439&title=05-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Aliyetwaharika%20Na%20Hedhi%20Baada%20Tu%20Ya%20Alfajiri%20Vipi%20Swawm%20Yake%3F
[11] http://www.binbaz.org.sa/noor/4580
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8438&title=06-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20Imemjia%20Hedhi%20Dakika%20Tano%20Kabla%20Ya%20Magharibi%20Akidhi%20Swalaah%20Ya%20Magharibi%3F%20%20%20%20%20%20%20%20%20%20%20%20%20%20%20%20%20%20%20%20%20%20
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8434&title=07-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Amemaliza%20Damu%20Ya%20Uzazi%20Kabla%20Ya%20Ramadhwaan%20Kisha%20Akaanza%20Swiyaam%20%20
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8441&title=08-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Imemjia%20Hedhi%20Muda%20Mdogo%20Tu%20Kabla%20Ya%20Adhaan%20Ya%20Magharibi
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8442&title=09-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Imemjia%20Hedhi%20Baada%20Ya%20Magharibi%20Kabla%20Ya%20%E2%80%98Ishaa%20Swawm%20Yake%20Sahihi%3F
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8443&title=10-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Ametumia%20Vidonge%20Vya%20Kuzuia%20Mimba%20Je%2C%20Alipe%20Masiku%20Ya%20Hedhi%20Japokuwa%20Hakuona%20Damu%3F%20%20
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8495&title=11-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Hakulipa%20Swawm%20Alipokuwa%20Katika%20Hedhi%20Miaka%20Yote%20Iliyopita%20Ya%20Ramadhwaan
[18] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8497&title=12-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Hakuweza%20Kulipa%20Swawm%20Kwa%20Sababu%20Miaka%20Michache%20Alikuwa%20Anazaa%20Siku%20Za%20Ramadhwaan
[19] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8498&title=13-Shaykh%20Swaalih%20Al-Luhaydaan%3A%20Mwenye%20Mimba%20Na%20Mnyonyeshaji%20Walipe%20Swawm%20Au%20Walishe%20Masikini%3F