Dawa Ya Mswaki Inabatilisha Swawm?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Je, dawa ya mswaki inabatilisha Swawm?
JIBU:
Dawa ya mswaki haibatilishi Swawm ikiwa atasafisha meno yake kisha ateme bila ya kuimeza. Ikiwa atameza kwa kukusudia, Swawm yake imebatilika.
[Mawqi’ Ar-Rasmiy – Imaam Ibn Baaz] [5]
Alisukutua Maji Baridi Akiwa Katika Swawm Kutokana Na Mdomo Kuwa Mkavu Mno
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Nilikuwa mja mzito na hali ya hewa ilikuwa ni joto mno mdomo wangu ukawa umekauka, basi nikafanya madhwmadhwah (kusukutua) kwa maji ya baridi ili kuurutubisha mdomo wangu, lakini nilijitahadharisha kutokumeza maji. Je, nimefanya dhambi na je, nilipe kafara kwa hilo?
JIBU:
Kutokana na ulivyosema, hakuna dhambi juu yako na huwajibiki kulipa siku hiyo uliyofanya madhwmadhwah kwa maji kwa sababu haibatilishi swawm ya mtu.
Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Fataawa Al-Lajnah Ad-Daaimah Lil Buhuwth Al-‘Ilmiyyah Wal Iftaa (20344)]
Kujipaka Au Kunusa Mafuta Mazuri Akiwa Katika Swawm
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Nini hukumu ya mtu aliyefunga na kutumia mafuta mazuri siku za Ramadhaan?
JIBU:
Hakuna ubaya kutumia na kunusa mafuta mazuri siku za Ramadhwaan isipokuwa kufukiza bukhuwr (udi) usikaribie hadi ukavuta pumzi za moshi na ukaingia tumboni.
[Imaam Muhammad bin Swaalih Ibn ‘Uthyamiyn - Fiqhul ‘Ibaadaat Uk. No. 217 Maktabatul-Iymaan]
Aliyesilimu Katika Ramadhwaan Anawajibika Swiyaam?
Imaam Ibn Qudaamah Al-Maddisiyy
Al-Khiraqiy kasema:
"Ikiwa Kafiri atasilimu wakati wa Ramadhwaan, anatakiwa kufunga mwezi (masiku) yaliyobakia.
Ama kuhusu siku za mwezi huo zilizompita kabla hajakuwa Muislamu, sio waajib kwake kulipa siku hizo. Kauli hii ni ya Ash-Sha'biy, Qataadah, Maalik, Al-Awza'iy, Ash-Shaafi'iy, Abu Thawr na Hanafiyyah.
'Atwaa kasema analazimika kulipa siku hizo.
Kutoka kwa al-Hassan [Al-Baswriy] kumepokelewa kauli zote mbili.
Ama kuhusu sisi – Hanaabilah – hatuoni kama ni waajib kwake kulipa siku hizo ambazo zilipita hali ya kuwa alikuwa kafiri. Hali kadhalika si waajib kwake kulipa Ramadhwaan iliyopita.
[Al-Mughniy (4/414-415)]
Akijitoa Manii Swawm Inabatilika Na Je, Anawajibika Kafara?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Je, kutoa manii kunabatilisha Swawm? Na je, anapaswa kulipa kafara?
JIBU:
Mtu akitoa manii Swawm yake inabatilika, inabatilika na mtu analazimika kulipa siku hiyo na kufanya tawbah [kwa kuwa ni haramu].
Kulipa kafara ni pindi mtu anapofanya jimai wakati wa Swawm.
[Imaam Muhammad Swaalih Ibn 'Uthaymiyn - Fataawa Arkaanil-Islaam, uk. 478]
Akimeza Maji Bila Kukusudia Kutokana Na Kusukutua Swawm Yake Inabatilika?
Imaam Ibn ‘Uthyamiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Je, Swawm ya mfungaji inabatilika ikiwa atasukutua kinywa au pua na kwa bahati mbaya akameza maji?
JIBU:
Aliyekuwa katika swawm akaukutua kinywa au pua na maji yakamuingia, Swawm yake haibatiliki, kwa kuwa hakukusudia hilo. Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:
وَلَـٰكِن مَّا تَعَمَّدَتْ قُلُوبُكُمْ ۚ
lakini isipokuwa katika yale yaliyoyakusudia nyoyo zenu [Al-Ahzaab 33;5]
[Imaam Muhammad Swaalih Ibn 'Uthaymiyn - Fiqhul-'Ibaadat, uk. 253]
Kipulizio Cha Kusaidia Upungufu Wa Pumzi Hakibatilishi Swawm
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Nini hukmu ya kutumia kipulizio kwa ajili ya kusaidia matatizo ya upungufu wa pumzi?
JIBU:
Kipulizio ni mvuke na haufikii tumboni. Kwa hiyo tunasema kwamba hakuna ubaya kutumia mtu anapokuwa katika swawm na haitabatilisha swawm yako kwa sababu kama tulivyosema hakuna kitu kitakachoingia tumboni. Kwa vile ni kitu kinachovutwa na kutoka mvuke kisha unapotea, basi hakuna kinachofika tumboni kwa hiyo inarushusiwa kutumia wakati una swawm na swawm haibatiliki kwayo.
[Imaam Ibn ‘Uthaymiyn Fataawaa Arkanul-Islaam Darus-salaam Mjalada 2 Uk. 658]
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/261
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8444&title=Fataawaa%3A%20%20Yanayobatilisha%20Na%20Yasiyobatilisha%20Swawm
[4] http://www.alhidaaya.com
[5] https://binbaz.org.sa/noor/9809
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8445&title=01-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20Dawa%20Ya%20Mswaki%20Inabatilisha%20Swawm%3F
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8447&title=03-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Alisukutua%20Maji%20Baridi%20Akiwa%20Katika%20Swawm%20Kutokana%20Na%20Mdomo%20Kuwa%20Mkavu%20Mno%20
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8448&title=04-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Kujipaka%20Au%20Kunusa%20Mafuta%20Mazuri%20Akiwa%20Katika%20Swawm
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8449&title=05-Imaam%20Ibn%20Qudaamah%20Al-Maddisiyy%3A%20Aliyesilimu%20Katika%20Ramadhwaan%20Anawajibika%20Swiyaam%3F
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8450&title=06-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Akijitoa%20Manii%20Swawm%20Inabatilika%20Na%20Je%2C%20Anawajibika%20Kafara%3F
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8451&title=07-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthyamiyn%3A%20Akimeza%20Maji%20Bila%20Kukusudia%20Kutokana%20Na%20Kusukutua%20Swawm%20Yake%20Inabatilika%3F
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8534&title=08-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Kipulizio%20Cha%20Kusaidia%20Upungufu%20Wa%20Pumzi%20Hakibatilishi%20Swawm