Sababu Za Kuteremshwa
(Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Suwrah Al-Anfaal
Imekusanywa na: Alhidaaya.com [2]
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com [4]
Al-Anfaal: 1
01- Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu ngawira. Sema: Ngawira ni ya Allaah na Rasuli.
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَنفَالِ ۖ قُلِ الْأَنفَالُ لِلَّـهِ وَالرَّسُولِ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَصْلِحُوا ذَاتَ بَيْنِكُمْ ۖ وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿١﴾
Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu ngawira. Sema: Ngawira ni ya Allaah na Rasuli. Basi mcheni Allaah na suluhisheni yaliyo baina yenu. Na mtiini Allaah na Rasuli Wake mkiwa ni Waumini. [Al-Anfaal: 1]
Sababun-Nuzuwl:
Aayah hii imeteremka kama alivyohadithia Musw’ab bin Sa’d (رضي الله عنه) kutoka kwa baba yake kwamba: “Aayah nne za Qur-aan zimeteremshwa kuhusu mimi. Niliukuta upanga (katika ngawira za vita). Ukaletwa kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Baba yangu akasema: Ee Rasuli wa Allaah, nipatie mimi. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Uweke hapa! Kisha (baba yangu) akasimama na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: “Uweke ulipoukuta.” Kisha akasimama akasema: Ee Rasuli wa Allaah, nipatie mimi. Akamwambia: “Uweke!” Akasimama akasema tena: Ee Rasuli wa Allaah nipatie. Je, nitafanywa kama ambaye hana sehemu (ya ngawira)? Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: “Uweke ulipoukuta.” Hapo ikataremshwa:
يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَنفَالِ ۖ قُلِ الْأَنفَالُ لِلَّـهِ وَالرَّسُولِ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَصْلِحُوا ذَاتَ بَيْنِكُمْ ۖ وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿١﴾
Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu ngawira. Sema: Ngawira ni ya Allaah na Rasuli.
[Muslim Kitaab Al-Jihaad was-Siyar, Baab Al-Anfaal]
Pia Musw-‘ab bin Sa’d amehadithia kutoka kwa baba yake (Sa’d bin Abiy Waqqaasw): “Nilikuja kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) siku ya Badr nikiwa na upanga nikasema: Ee Rasuli wa Allaah, hakika Allaah Amenipa shifaa ya kifua changu kutokana na adui leo, basi nipe upanga.” Akasema: “Upanga si wangu wala si wako.” Nikaondoka huku nikisema: “Leo atapewa huo (upanga) mtu ambaye hakutiwa mtihanini kama mimi.” Mara akaja mjumbe akaniambia: “Itikia.” Nikadhani kwamba imeteremshwa Wahy kuhusu mimi kutokana na kauli yangu. Nikaenda kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ulinitaka nikupe upanga huu lakini huu haukuwa wangu wala wako. Lakini sasa Allaah Amenipa mimi kwa hiyo sasa ni wako.” Kisha akasoma:
يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَنفَالِ ۖ قُلِ الْأَنفَالُ لِلَّـهِ وَالرَّسُولِ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَصْلِحُوا ذَاتَ بَيْنِكُمْ ۖ وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿١﴾
Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu ngawira. Sema: Ngawira ni ya Allaah na Rasuli.
[Abuu Daawuwd, Kitaab Al-Jihaad]
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com [4]
Al-Anfaal: 9
09-Na pale mlipomuomba uokovu Rabb wenu Naye Akakuitikieni kuwa: Hakika Mimi Nitakusaidieni kwa Malaika elfu wafuatanao mfululizo
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
إِذْ تَسْتَغِيثُونَ رَبَّكُمْ فَاسْتَجَابَ لَكُمْ أَنِّي مُمِدُّكُم بِأَلْفٍ مِّنَ الْمَلَائِكَةِ مُرْدِفِينَ﴿٩﴾
Na pale mlipomuomba uokovu Rabb wenu Naye Akakuitikieni kuwa: Hakika Mimi Nitakusaidieni kwa Malaika elfu wafuatanao mfululizo. [Al-Anfaal: 9]
Sababun-Nuzuwl:
Amesimulia ‘Umar bin Al-Khatwwaab (رضي الله عنه) Ilipokuwa siku ya vita vya Badr, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwatazama washirikina wakiwa ni elfu moja na Swahaba zake ni mia tatu na kumi na tisa. Basi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alielekea Qiblah akanyoosha mikono yake akiomba kwa Rabb wake: “Ee Allaah, Nitimizie Yale Uliyoniahidi. Ee Allaah, Nipe yale Uliyoniahidi. Ee Allaah, kikundi hiki kidogo cha Waislamu kikiangamia, hutoabudiwa tena katika ardhi.” Akaendelea kuomba kwa Rabb wake akinyoosha mikono yake huku ameelekea Qiblah mpaka ridaa (vazi la juu ya nguo kama kanzu au joho) lake likamuanguka kutoka mabegani mwake. Abuu Bakr akamjia akaliokota ridaa lake na akamwekea mabegani. Kisha akamgeukia nyuma akasema: Ee Nabiy wa Allaah, Du’aa yako hii kwa Rabb wako itakutosheleza kwani Atakutimizia yale Aliyokuahidi. Hapo Allaah (عز وجل) Akateremsha:
إِذْ تَسْتَغِيثُونَ رَبَّكُمْ فَاسْتَجَابَ لَكُمْ أَنِّي مُمِدُّكُم بِأَلْفٍ مِّنَ الْمَلَائِكَةِ مُرْدِفِينَ﴿٩﴾
Na pale mlipomuomba uokovu Rabb wenu Naye Akakuitikieni kuwa: Hakika Mimi Nitakusaidieni kwa Malaika elfu wafuatanao mfululizo. [Al-Anfaal: 9]
Basi Allaah Akamsaidia kwa kumteremshia Malaika.
Abuu Zumayl amesema kwamba Hadiyth imesimuliwa kwake na Ibn ‘Abbaas ambaye amesema: “Siku hiyo, pindi Muislamu alipokuwa anamfukuza kafiri aliyekuwa anamwendea mbele yake, alisikia mpigo wa mjeledi na sauti ya mpandaji farasi akisema: “Tangulia ee Zumayl! Basi alimtazama kafiri ambaye hapo alianguka chini akiwa amelala chali. Alipomtazama aliona pua yake ina kovu na uso umechanwa kama kwamba umepigwa na mjeledi na uso umegeuka rangi ya kijani kutokana na sumu. Answaariy mmoja alikuja akamhadithia hayo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Umesema kweli, huo ni msaada kutoka mbingu ya tatu.” Basi siku hiyo Waislamu waliwaua watu sabini na wakawateka sabini. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia Abuu Bakr na ‘Umar (رضي الله عنهما): “Nini ushauri wenu kuhusu mateka hawa?” Abuu Bakr akasema: “Hao ni watoto wa ‘ammi zetu na jamaa zetu. Naona kuwa uwaache baada ya kuwatoza fidia ili tupate nguvu dhidi ya makafiri, na ‘asaa Allaah Awahidi katika Uislamu.” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Je, ee ‘Umar unaonaje wewe?” Akasema: “Hapana! Wa-Allaahi ee Rasuli wa Allaah, mimi sioni anavyoona Abuu Bakr, lakini ninaloona ni kuwa utukabidhi tuwakate vichwa vyao! Basi mkabidhi ‘Aqiyl kwa ‘Aliy ili amkate kichwa chake. Na nikabidhi mimi ‘fulani’ (jamaa wa ‘Umar) ili nimkate mimi kichwa chake, kwani hao ni viongozi wa makafiri na ndio mashujaa wao. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaunga mkono aliyoyasema Abuu Bakr lakini hakuunga mkono niliyoyasema mimi. Siku ya pili, nilipomwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) nimekuta yeye na Abuu Bakr wamekaa kitako huku wanalia. Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah, nijulishe kinachokuliza wewe na Swahibu yako ili nami nilie pamoja nanyi au angalau nijilize kwa kuwaonea huruma. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Nalia kutokana na yaliyomtokea Swahibu wako kuchukua fidia (kwa mateka). Nimeonyeshwa adhabu yao iliyokaribia chini ya mti huu (akaashiria mti ulio karibu naye). Kisha Allaah (عز وجل) Akateremsha:
مَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَكُونَ لَهُ أَسْرَىٰ حَتَّىٰ يُثْخِنَ فِي الْأَرْضِ ۚ تُرِيدُونَ عَرَضَ الدُّنْيَا وَاللَّـهُ يُرِيدُ الْآخِرَةَ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴿٦٧
Haikumpasa Nabiy yeyote awe ana mateka mpaka apigane vikali mno kuwaua na kuwajeruhi (maadui wa Allaah) nchini. Mnataka vitu vya dunia, na hali Allaah Anataka (mpate vya) Aakhirah. Na Allaah Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
لَّوْلَا كِتَابٌ مِّنَ اللَّـهِ سَبَقَ لَمَسَّكُمْ فِيمَا أَخَذْتُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴿٦٨﴾
Lau kama si hukumu iliyotangulia kutoka kwa Allaah bila shaka ingekupateni kwa yale mliyoyachukua adhabu kuu.
فَكُلُوا مِمَّا غَنِمْتُمْ حَلَالًا طَيِّبًا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٦٩﴾
Basi kuleni katika ghanima mlizozipata, ni halali na ni vizuri, na mcheni Allaah. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu. [Al-Anfaal: 67-69]
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com [4]
Al-Anfaal: 16
16-Na yeyote atakayewageuzia mgongo wake siku hiyo - isipokuwa ...
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا لَقِيتُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا زَحْفًا فَلَا تُوَلُّوهُمُ الْأَدْبَارَ﴿١٥﴾
Enyi walioamini! Mtapokutana na wale waliokufuru vitani, basi msiwageuzie migongo (kukimbia).
وَمَن يُوَلِّهِمْ يَوْمَئِذٍ دُبُرَهُ إِلَّا مُتَحَرِّفًا لِّقِتَالٍ أَوْ مُتَحَيِّزًا إِلَىٰ فِئَةٍ فَقَدْ بَاءَ بِغَضَبٍ مِّنَ اللَّـهِ وَمَأْوَاهُ جَهَنَّمُ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ﴿١٦﴾
Na yeyote atakayewageuzia mgongo wake siku hiyo - isipokuwa akigeuka kama mbinu ya kupigana au kujiunga na kikosi kingine - basi amestahiki Ghadhabu ya Allaah, na makazi yake ni Jahannam, na ni pabaya palioje mahali pa kuishia. [Al-Anfaal: 15-16]
Sababun-Nuzuwl:
Aayah hii imeteremshwa siku ya vita vya Badr. [Sunan Abiy Daawuwd – Kitaab Al-Jihaad – Hadiyth ya Abuu Sa’iyd na ameisahihisha Al-Albaaniy]
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com [4]
Al-Anfaal: 17
17- Hamkuwaua nyinyi, lakini Allaah Ndiye Aliyewaua. Na wala hukurusha...
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
فَلَمْ تَقْتُلُوهُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ قَتَلَهُمْ ۚ وَمَا رَمَيْتَ إِذْ رَمَيْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ رَمَىٰ ۚ وَلِيُبْلِيَ الْمُؤْمِنِينَ مِنْهُ بَلَاءً حَسَنًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿١٧﴾
Hamkuwaua nyinyi, lakini Allaah Ndiye Aliyewaua. Na wala hukurusha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم mchanga) pale uliporusha lakini Allaah Ndiye Aliyerusha, na ili Awajaribu Waumini jaribio zuri kutoka Kwake. Hakika Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote. [Al-Anfaal: 17]
Sababun-Nuzuwl:
Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
وَمَا رَمَيْتَ إِذْ رَمَيْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ رَمَىٰ ۚ
Na wala hukurusha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم mchanga) pale uliporusha lakini Allaah Ndiye Aliyerusha.
Amehadithia Hakiym bin Hizaam kwamba Imeteremshwa siku ya Badr pindi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipoamrishwa, akateka changarawe za mawe mkononi, akatukabili nazo na kuturushia akisema: “Nyuso zinyauke!” Tukashindwa. Allaah (عز وجل) Akateremsha:
وَمَا رَمَيْتَ إِذْ رَمَيْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ رَمَىٰ ۚ
Na wala hukurusha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم mchanga) pale uliporusha lakini Allaah Ndiye Aliyerusha. [Atw-Twabaraaniy]
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com [4]
Al-Anfaal: 19
019- Mkitafuta hukmu (enyi makafiri), basi imeshakujieni hukmu.
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
إِن تَسْتَفْتِحُوا فَقَدْ جَاءَكُمُ الْفَتْحُ ۖ وَإِن تَنتَهُوا فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَإِن تَعُودُوا نَعُدْ وَلَن تُغْنِيَ عَنكُمْ فِئَتُكُمْ شَيْئًا وَلَوْ كَثُرَتْ وَأَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُؤْمِنِينَ﴿١٩﴾
Mkitafuta hukmu (enyi makafiri), basi imeshakujieni hukmu. Na mkikoma (ukhalifu) basi hivyo ni kheri kwenu. Na mkirudia (kuhujumu) Nasi Tutarudia, na wala kundi lenu halitokufaeni kitu chochote japo likikithiri. Na Hakika Allaah Yu Pamoja na Waumini. [Al-Anfaal: 19]
Sababun-Nuzuwl:
Amesimulia ‘Abdullaah bin Tha’labah bin Swughayr (رضي الله عنه) kwamba aliyeomba hukmu siku ya Badr alikuwa ni Abuu Jahl. Alisema pale majeshi mawili yalipokutana: “Ee Allaah, muangamize miongoni mwetu yeyote yule anayekata undugu na akaleta ambayo hatukupatapo kuyajua.” Hiyo ndiyo hukmu aliyoiomba na Allaah Akateremsha:
إِن تَسْتَفْتِحُوا فَقَدْ جَاءَكُمُ الْفَتْحُ ۖ
Mkitafuta hukmu (enyi makafiri), basi imeshakujieni hukmu. [Ibn Jariyr (9/208), Musnad (5/431), Al-Haakim amesema Hadiyth Swahiyh]
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com [4]
Al-Anfaal: 32-34
033-Na Allaah Hakuwa wa kuwaadhibu na hali wewe uko nao
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَإِذْ قَالُوا اللَّـهُمَّ إِن كَانَ هَـٰذَا هُوَ الْحَقَّ مِنْ عِندِكَ فَأَمْطِرْ عَلَيْنَا حِجَارَةً مِّنَ السَّمَاءِ أَوِ ائْتِنَا بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٣٢﴾
Na pindi waliposema: Ee Allaah! Kama haya ni haki kutoka Kwako, basi Tunyeshee mvua ya mawe kutoka mbinguni au Tuletee adhabu iumizayo.
وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُعَذِّبَهُمْ وَأَنتَ فِيهِمْ ۚ وَمَا كَانَ اللَّـهُ مُعَذِّبَهُمْ وَهُمْ يَسْتَغْفِرُونَ﴿٣٣﴾
Na Allaah Hakuwa wa kuwaadhibu na hali wewe (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uko nao. Na Allaah Hakuwa wa kuwaadhibu hali wao wanaomba Maghfirah.
وَمَا لَهُمْ أَلَّا يُعَذِّبَهُمُ اللَّـهُ وَهُمْ يَصُدُّونَ عَنِ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَمَا كَانُوا أَوْلِيَاءَهُ ۚ إِنْ أَوْلِيَاؤُهُ إِلَّا الْمُتَّقُونَ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿٣٤﴾
Na wana nini hata Allaah Asiwaadhibu na hali wao wanazuia (watu) na Al-Masjidil-Haraam, na hawakuwa walinzi wake (Msikiti huo). Hawakuwa walinzi wake isipokuwa wenye taqwa, lakini wengi wao hawajui. [Al-Anfaal: 32-34]
Sababun-Nuzuwl:
Aayah hii na iliyotangulia ni kama alivyohadithia Anas bin Maalik (رضي الله عنه) kwamba Abuu Jahl alisema:
اللَّـهُمَّ إِن كَانَ هَـٰذَا هُوَ الْحَقَّ مِنْ عِندِكَ فَأَمْطِرْ عَلَيْنَا حِجَارَةً مِّنَ السَّمَاءِ أَوِ ائْتِنَا بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٣٢﴾
Ee Allaah! Kama haya ni haki kutoka Kwako, basi Tunyeshee mvua ya mawe kutoka mbinguni au Tuletee adhabu iumizayo. [Al-Anfaal: 32]
Allaah Akateremsha:
وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُعَذِّبَهُمْ وَأَنتَ فِيهِمْ ۚ وَمَا كَانَ اللَّـهُ مُعَذِّبَهُمْ وَهُمْ يَسْتَغْفِرُونَ﴿٣٣﴾
Na Allaah Hakuwa wa kuwaadhibu na hali wewe (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uko nao. Na Allaah Hakuwa wa kuwaadhibu hali wao wanaomba Maghfirah. [Al-Anfaal: 33] [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com [4]
Al-Anfaal: 65-66
066- Sasa Allaah Amekukhafifishieni na Amejua kwamba kuna udhaifu kwenu
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ حَرِّضِ الْمُؤْمِنِينَ عَلَى الْقِتَالِ ۚ إِن يَكُن مِّنكُمْ عِشْرُونَ صَابِرُونَ يَغْلِبُوا مِائَتَيْنِ ۚ وَإِن يَكُن مِّنكُم مِّائَةٌ يَغْلِبُوا أَلْفًا مِّنَ الَّذِينَ كَفَرُوا بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَفْقَهُونَ﴿٦٥﴾
Ee Nabiy! Shajiisha Waumini kupigana vita. Wakiweko miongoni mwenu (Waumini) wahimilivu ishirini basi watawashinda (makafiri) mia mbili. Na wakiweko miongoni mwenu mia watawashinda elfu katika wale waliokufuru, kwa kuwa wao ni watu wasiofahamu.
الْآنَ خَفَّفَ اللَّـهُ عَنكُمْ وَعَلِمَ أَنَّ فِيكُمْ ضَعْفًا ۚ فَإِن يَكُن مِّنكُم مِّائَةٌ صَابِرَةٌ يَغْلِبُوا مِائَتَيْنِ ۚ وَإِن يَكُن مِّنكُمْ أَلْفٌ يَغْلِبُوا أَلْفَيْنِ بِإِذْنِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ مَعَ الصَّابِرِينَ﴿٦٦﴾
Sasa Allaah Amekukhafifishieni na Amejua kwamba kuna udhaifu kwenu. Hivyo basi wakiweko miongoni mwenu (Waumini) wahimilivu mia watawashinda (makafiri) mia mbili. Na wakiweko miongoni mwenu (Waumini) elfu, wawatashinda (makafiri) elfu mbili kwa Idhini ya Allaah. Na Allaah Yu pamoja na wenye kusubiri. [Al-Anfaal: 65-66]
Sababun-Nuzuwl:
Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنه) kwamba ilipoteremka:
إِن يَكُن مِّنكُمْ عِشْرُونَ صَابِرُونَ يَغْلِبُوا مِائَتَيْنِ ۚ
Wakiweko miongoni mwenu (Waumini) wahimilivu ishirini basi watawashinda (makafiri) mia mbili. [Al-Anfaal:65] ikawa jambo gumu kwa Waislamu kwamba mtu mmoja hapaswi kukimbia (vita) mbele ya (makafiri) kumi. Basi ikaja takhfifu pindi (Allaah) Aliposema:
الْآنَ خَفَّفَ اللَّـهُ عَنكُمْ وَعَلِمَ أَنَّ فِيكُمْ ضَعْفًا ۚ فَإِن يَكُن مِّنكُم مِّائَةٌ صَابِرَةٌ يَغْلِبُوا مِائَتَيْنِ
Sasa Allaah Amekukhafifishieni na Amejua kwamba kuna udhaifu kwenu. Hivyo basi wakiweko miongoni mwenu (Waumini) wahimilivu mia watawashinda (makafiri) mia mbili.
Basi Allaah Alipowafanyia takhfifu kwa kuwapunguzia idadi (ya maadui ambao kila mmoja wao atapambana nao), kukapungua kuhimili kwao kadiri ya walivyofanyiwa takhfifu (ya idadi ya maadui watakaopigana nao). [Al-Bukhaariy na wengineo]
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com [4]
Al-Anfaal: 67- 69
067-Haikumpasa Nabiy yeyote awe ana mateka mpaka apigane vikali mno
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
مَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَكُونَ لَهُ أَسْرَىٰ حَتَّىٰ يُثْخِنَ فِي الْأَرْضِ ۚ تُرِيدُونَ عَرَضَ الدُّنْيَا وَاللَّـهُ يُرِيدُ الْآخِرَةَ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴿٦٧﴾
Haikumpasa Nabiy yeyote awe ana mateka mpaka apigane vikali mno kuwaua na kuwajeruhi (maadui wa Allaah) nchini. Mnataka vitu vya dunia, na hali Allaah Anataka (mpate vya) Aakhirah. Na Allaah Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
لَّوْلَا كِتَابٌ مِّنَ اللَّـهِ سَبَقَ لَمَسَّكُمْ فِيمَا أَخَذْتُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴿٦٨﴾
Lau kama si hukumu iliyotangulia kutoka kwa Allaah, bila shaka ingekupateni kwa yale mliyoyachukua adhabu kuu.
فَكُلُوا مِمَّا غَنِمْتُمْ حَلَالًا طَيِّبًا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٦٩﴾
Basi kuleni katika ghanima mlizozipata, ni halali na ni vizuri, na mcheni Allaah. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu. [Al-Anfaal: 67-69]
Sababun-Nuzuwl:
Amesimulia ‘Abdullaah bin ‘Umar (رضي الله عنهما) : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimtaka ushauri Abuu Bakr (رضي الله عنه) kuhusu mateka akamwambia: “Ni watu wako na jamaa zako waachilie.” Alipomtaka ushauri ‘Umar (رضي الله عنه) alisema: “Waue.” Basi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akatoza fidia. Allaah (عز وجل) Akateremsha:
مَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَكُونَ لَهُ أَسْرَىٰ حَتَّىٰ يُثْخِنَ فِي الْأَرْضِ ۚ تُرِيدُونَ عَرَضَ الدُّنْيَا وَاللَّـهُ يُرِيدُ الْآخِرَةَ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴿٦٧﴾
Haikumpasa Nabiy yeyote awe ana mateka mpaka apigane vikali mno kuwaua na kuwajeruhi (maadui wa Allaah) nchini. Mnataka vitu vya dunia, na hali Allaah Anataka (mpate vya) Aakhirah. Na Allaah Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
لَّوْلَا كِتَابٌ مِّنَ اللَّـهِ سَبَقَ لَمَسَّكُمْ فِيمَا أَخَذْتُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴿٦٨﴾
Lau kama si hukumu iliyotangulia kutoka kwa Allaah, bila shaka ingekupateni kwa yale mliyoyachukua adhabu kuu.
فَكُلُوا مِمَّا غَنِمْتُمْ حَلَالًا طَيِّبًا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٦٩﴾
Basi kuleni katika ghanima mlizozipata, ni halali na ni vizuri, na mcheni Allaah. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu. [Al-Anfaal: 67-69] [Al-Haakim (2/239)]
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com [4]
Al-Anfaal: 68
068- Lau kama si hukumu iliyotangulia kutoka kwa Allaah, bila shaka ingekupateni..
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
لَّوْلَا كِتَابٌ مِّنَ اللَّـهِ سَبَقَ لَمَسَّكُمْ فِيمَا أَخَذْتُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴿٦٨﴾
Lau kama si hukumu iliyotangulia kutoka kwa Allaah, bila shaka ingekupateni kwa yale mliyoyachukua adhabu kuu. [Al-Anfaal: 68]
Sababun-Nuzuwl:
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) : Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ghanima hazipasi kuchukuliwa na yeyote yule wa vichwa vyeusi (vichwa vyeusi imekusudiwa ni wana wa Aadam kwa vile wengi ya watu vichwa vyao ni vyeusi kutokana na nywele nyeusi), bali moto kutoka mbinguni utateremka kuzila ghanima.” Sulaymaan Al-A’mash akasema: Hakuna asemaye haya sasa isipokuwa Abuu Hurayrah. Basi siku ya Badr pindi ghanima za vita zilipoletwa, zilifanywa halali kwao. Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:
لَّوْلَا كِتَابٌ مِّنَ اللَّـهِ سَبَقَ لَمَسَّكُمْ فِيمَا أَخَذْتُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴿٦٨﴾
Lau kama si hukumu iliyotangulia kutoka kwa Allaah, bila shaka ingekupateni kwa yale mliyoyachukua adhabu kuu. [Al-Anfaal: 68] [At-Tirmidhiy (Abuu ‘Iysaa) amesema: Hii Hadiyth Hasan Swahiyh Ghariyb katika Hadiyth ya Al-A’mash]
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com [4]
Al-Anfaal: 75
075- Na wale walioamini baada (ya hijra) na wakahajiri na wakafanya Jihaad pamoja nanyi, basi hao..
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَالَّذِينَ آمَنُوا مِن بَعْدُ وَهَاجَرُوا وَجَاهَدُوا مَعَكُمْ فَأُولَـٰئِكَ مِنكُمْ ۚ وَأُولُو الْأَرْحَامِ بَعْضُهُمْ أَوْلَىٰ بِبَعْضٍ فِي كِتَابِ اللَّـهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ﴿٧٥﴾
Na wale walioamini baada (ya hijra) na wakahajiri na wakafanya Jihaad pamoja nanyi, basi hao ni miongoni mwenu. Na ndugu wa uhusiano wa damu wanastahikiana wenyewe kwa wenyewe (kwa kurithiana), katika Shariy’ah ya Allaah. Hakika Allaah Ni Mjuzi wa kila kitu. [Al-Anfaal: 75]
Sababun-Nuzuwl:
Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaunga undugu Swahaba wakawa wanarithiana mpaka ilipoteremka:
وَأُولُو الْأَرْحَامِ بَعْضُهُمْ أَوْلَىٰ بِبَعْضٍ
Na ndugu wa uhusiano wa damu wanastahikiana wenyewe kwa wenyewe (kwa kurithiana).
Wakaacha kurithiana wakawa wanarithiana kwa uhusiano wa damu. [Atw-Twabaraaniy, na amesema Al-Haythamiy katika Majma’u Az-Zawaaid (7/28) Watu wake ni Swahiyh. Na imepokelewa na Ibn Abiy Haatim (4/25) Hadiyth ya Az-Zubayr bin Al-‘Awwaam (4/24) na imepokelewa na Ibn Jariyr (10/58)]
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/238
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9034&title=008-Asbaabun-Nuzuwl%3A%20Al-Anfaal
[4] http://alhidaaya.com
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9035&title=001-Asbaabun-Nuzuwl%3A%20Al-Anfaal%20Aayah%20001%3A%20%D9%8A%D9%8E%D8%B3%D9%92%D8%A3%D9%8E%D9%84%D9%8F%D9%88%D9%86%D9%8E%D9%83%D9%8E%20%D8%B9%D9%8E%D9%86%D9%90%20%D8%A7%D9%84%D9%92%D8%A3%D9%8E%D9%86%D9%81%D9%8E%D8%A7%D9%84%D9%90%20%DB%96%20%D9%82%D9%8F%D9%84%D9%90%20%D8%A7%D9%84%D9%92%D8%A3%D9%8E%D9%86%D9%81%D9%8E%D8%A7%D9%84%D9%8F%20%D9%84%D9%90%D9%84%D9%91%D9%8E%D9%80%D9%87%D9%90%20%D9%88%D9%8E%D8%A7%D9%84%D8%B1%D9%91%D9%8E%D8%B3%D9%8F%D9%88%D9%84%D9%90%20
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9036&title=009-Asbaabun-Nuzuwl%3A%20Al-Anfaal%20Aayah%20009%3A%20%20%D8%A5%D9%90%D8%B0%D9%92%20%D8%AA%D9%8E%D8%B3%D9%92%D8%AA%D9%8E%D8%BA%D9%90%D9%8A%D8%AB%D9%8F%D9%88%D9%86%D9%8E%20%D8%B1%D9%8E%D8%A8%D9%91%D9%8E%D9%83%D9%8F%D9%85%D9%92%20%D9%81%D9%8E%D8%A7%D8%B3%D9%92%D8%AA%D9%8E%D8%AC%D9%8E%D8%A7%D8%A8%D9%8E%20%D9%84%D9%8E%D9%83%D9%8F%D9%85%D9%92%20%D8%A3%D9%8E%D9%86%D9%90%D9%91%D9%8A%20%D9%85%D9%8F%D9%85%D9%90%D8%AF%D9%91%D9%8F%D9%83%D9%8F%D9%85%20%D8%A8%D9%90%D8%A3%D9%8E%D9%84%D9%92%D9%81%D9%8D%20%D9%85%D9%90%D9%91%D9%86%D9%8E%20%D8%A7%D9%84%D9%92%D9%85%D9%8E%D9%84%D9%8E%D8%A7%D8%A6%D9%90%D9%83%D9%8E%D8%A9%D9%90%20%D9%85%D9%8F%D8%B1%D9%92%D8%AF%D9%90%D9%81%D9%90%D9%8A%D9%86%D9%8E
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9037&title=016-Asbaabun-Nuzuwl%3A%20Al-Anfaal%20Aayah%20016%3A%20%20%D9%88%D9%8E%D9%85%D9%8E%D9%86%20%D9%8A%D9%8F%D9%88%D9%8E%D9%84%D9%90%D9%91%D9%87%D9%90%D9%85%D9%92%20%D9%8A%D9%8E%D9%88%D9%92%D9%85%D9%8E%D8%A6%D9%90%D8%B0%D9%8D%20%D8%AF%D9%8F%D8%A8%D9%8F%D8%B1%D9%8E%D9%87%D9%8F%20%D8%A5%D9%90%D9%84%D9%91%D9%8E%D8%A7%20%D9%85%D9%8F%D8%AA%D9%8E%D8%AD%D9%8E%D8%B1%D9%90%D9%91%D9%81%D9%8B%D8%A7%20%D9%84%D9%90%D9%91%D9%82%D9%90%D8%AA%D9%8E%D8%A7%D9%84%D9%8D%20%D8%A3%D9%8E%D9%88%D9%92%20%D9%85%D9%8F%D8%AA%D9%8E%D8%AD%D9%8E%D9%8A%D9%90%D9%91%D8%B2%D9%8B%D8%A7%20%D8%A5%D9%90%D9%84%D9%8E%D9%89%D9%B0%20%D9%81%D9%90%D8%A6%D9%8E%D8%A9%D9%8D%20%20
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9038&title=017-Asbaabun-Nuzuwl%3A%20Al-Anfaal%20Aayah%20017%3A%20%D9%81%D9%8E%D9%84%D9%8E%D9%85%D9%92%20%D8%AA%D9%8E%D9%82%D9%92%D8%AA%D9%8F%D9%84%D9%8F%D9%88%D9%87%D9%8F%D9%85%D9%92%20%D9%88%D9%8E%D9%84%D9%8E%D9%80%D9%B0%D9%83%D9%90%D9%86%D9%91%D9%8E%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%91%D9%8E%D9%80%D9%87%D9%8E%20%D9%82%D9%8E%D8%AA%D9%8E%D9%84%D9%8E%D9%87%D9%8F%D9%85%D9%92%20%DB%9A%20%D9%88%D9%8E%D9%85%D9%8E%D8%A7%20%D8%B1%D9%8E%D9%85%D9%8E%D9%8A%D9%92%D8%AA%D9%8E%20%D8%A5%D9%90%D8%B0%D9%92%20%D8%B1%D9%8E%D9%85%D9%8E%D9%8A%D9%92%D8%AA%D9%8E%20%D9%88%D9%8E%D9%84%D9%8E%D9%80%D9%B0%D9%83%D9%90%D9%86%D9%91%D9%8E%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%91%D9%8E%D9%80%D9%87%D9%8E%20%D8%B1%D9%8E%D9%85%D9%8E%D9%89%D9%B0%20
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9039&title=019-Asbaabun-Nuzuwl%3A%20Al-Anfaal%20Aayah%20019%3A%20%D8%A5%D9%90%D9%86%20%D8%AA%D9%8E%D8%B3%D9%92%D8%AA%D9%8E%D9%81%D9%92%D8%AA%D9%90%D8%AD%D9%8F%D9%88%D8%A7%20%D9%81%D9%8E%D9%82%D9%8E%D8%AF%D9%92%20%D8%AC%D9%8E%D8%A7%D8%A1%D9%8E%D9%83%D9%8F%D9%85%D9%8F%20%D8%A7%D9%84%D9%92%D9%81%D9%8E%D8%AA%D9%92%D8%AD%D9%8F%20%DB%96%20%D9%88%D9%8E%D8%A5%D9%90%D9%86%20%D8%AA%D9%8E%D9%86%D8%AA%D9%8E%D9%87%D9%8F%D9%88%D8%A7%20%D9%81%D9%8E%D9%87%D9%8F%D9%88%D9%8E%20%D8%AE%D9%8E%D9%8A%D9%92%D8%B1%D9%8C%20%D9%84%D9%91%D9%8E%D9%83%D9%8F%D9%85%D9%92%20%DB%96%20%D9%88%D9%8E%D8%A5%D9%90%D9%86%20%D8%AA%D9%8E%D8%B9%D9%8F%D9%88%D8%AF%D9%8F%D9%88%D8%A7%20%D9%86%D9%8E%D8%B9%D9%8F%D8%AF%D9%92%20
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9040&title=033-Asbaabun-Nuzuwl%3A%20Al-Anfaal%20Aayah%20033%3A%20%D9%88%D9%8E%D9%85%D9%8E%D8%A7%20%D9%83%D9%8E%D8%A7%D9%86%D9%8E%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%91%D9%8E%D9%80%D9%87%D9%8F%20%D9%84%D9%90%D9%8A%D9%8F%D8%B9%D9%8E%D8%B0%D9%90%D9%91%D8%A8%D9%8E%D9%87%D9%8F%D9%85%D9%92%20%D9%88%D9%8E%D8%A3%D9%8E%D9%86%D8%AA%D9%8E%20%D9%81%D9%90%D9%8A%D9%87%D9%90%D9%85%D9%92%20%DB%9A%20%D9%88%D9%8E%D9%85%D9%8E%D8%A7%20%D9%83%D9%8E%D8%A7%D9%86%D9%8E%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%91%D9%8E%D9%80%D9%87%D9%8F%20%D9%85%D9%8F%D8%B9%D9%8E%D8%B0%D9%90%D9%91%D8%A8%D9%8E%D9%87%D9%8F%D9%85%D9%92%20%D9%88%D9%8E%D9%87%D9%8F%D9%85%D9%92%20%D9%8A%D9%8E%D8%B3%D9%92%D8%AA%D9%8E%D8%BA%D9%92%D9%81%D9%90%D8%B1%D9%8F%D9%88%D9%86%D9%8E
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9041&title=066-Asbaabun-Nuzuwl%3A%20Al-Anfaal%20Aayah%20066%3A%20%20%D8%A7%D9%84%D9%92%D8%A2%D9%86%D9%8E%20%D8%AE%D9%8E%D9%81%D9%91%D9%8E%D9%81%D9%8E%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%91%D9%8E%D9%80%D9%87%D9%8F%20%D8%B9%D9%8E%D9%86%D9%83%D9%8F%D9%85%D9%92%20%D9%88%D9%8E%D8%B9%D9%8E%D9%84%D9%90%D9%85%D9%8E%20%D8%A3%D9%8E%D9%86%D9%91%D9%8E%20%D9%81%D9%90%D9%8A%D9%83%D9%8F%D9%85%D9%92%20%D8%B6%D9%8E%D8%B9%D9%92%D9%81%D9%8B%D8%A7%20
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9042&title=067-Asbaabun-Nuzuwl%3A%20Al-Anfaal%20Aayah%20067%3A%20%D9%85%D9%8E%D8%A7%20%D9%83%D9%8E%D8%A7%D9%86%D9%8E%20%D9%84%D9%90%D9%86%D9%8E%D8%A8%D9%90%D9%8A%D9%8D%D9%91%20%D8%A3%D9%8E%D9%86%20%D9%8A%D9%8E%D9%83%D9%8F%D9%88%D9%86%D9%8E%20%D9%84%D9%8E%D9%87%D9%8F%20%D8%A3%D9%8E%D8%B3%D9%92%D8%B1%D9%8E%D9%89%D9%B0%20%D8%AD%D9%8E%D8%AA%D9%91%D9%8E%D9%89%D9%B0%20%D9%8A%D9%8F%D8%AB%D9%92%D8%AE%D9%90%D9%86%D9%8E%20%D9%81%D9%90%D9%8A%20%D8%A7%D9%84%D9%92%D8%A3%D9%8E%D8%B1%D9%92%D8%B6%D9%90
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9043&title=068-Asbaabun-Nuzuwl%3A%20Al-Anfaal%20Aayah%20068%3A%20%20%D9%84%D9%91%D9%8E%D9%88%D9%92%D9%84%D9%8E%D8%A7%20%D9%83%D9%90%D8%AA%D9%8E%D8%A7%D8%A8%D9%8C%20%D9%85%D9%90%D9%91%D9%86%D9%8E%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%91%D9%8E%D9%80%D9%87%D9%90%20%D8%B3%D9%8E%D8%A8%D9%8E%D9%82%D9%8E%20%D9%84%D9%8E%D9%85%D9%8E%D8%B3%D9%91%D9%8E%D9%83%D9%8F%D9%85%D9%92%20%D9%81%D9%90%D9%8A%D9%85%D9%8E%D8%A7%20%D8%A3%D9%8E%D8%AE%D9%8E%D8%B0%D9%92%D8%AA%D9%8F%D9%85%D9%92%20%D8%B9%D9%8E%D8%B0%D9%8E%D8%A7%D8%A8%D9%8C%20%D8%B9%D9%8E%D8%B8%D9%90%D9%8A%D9%85%D9%8C
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9044&title=075-Asbaabun-Nuzuwl%3A%20Al-Anfaal%20Aayah%20075%3A%20%20%D9%88%D9%8E%D8%A7%D9%84%D9%91%D9%8E%D8%B0%D9%90%D9%8A%D9%86%D9%8E%20%D8%A2%D9%85%D9%8E%D9%86%D9%8F%D9%88%D8%A7%20%D9%85%D9%90%D9%86%20%D8%A8%D9%8E%D8%B9%D9%92%D8%AF%D9%8F%20%D9%88%D9%8E%D9%87%D9%8E%D8%A7%D8%AC%D9%8E%D8%B1%D9%8F%D9%88%D8%A7%20%D9%88%D9%8E%D8%AC%D9%8E%D8%A7%D9%87%D9%8E%D8%AF%D9%8F%D9%88%D8%A7%20%D9%85%D9%8E%D8%B9%D9%8E%D9%83%D9%8F%D9%85%D9%92%20%D9%81%D9%8E%D8%A3%D9%8F%D9%88%D9%84%D9%8E%D9%80%D9%B0%D8%A6%D9%90%D9%83%D9%8E%20%D9%85%D9%90%D9%86%D9%83%D9%8F%D9%85%D9%92