Bid’ah Inayotendeka Katika Ziara Ya Kaburi La
Nabiy Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam
Shaykh Swaalih Al-Fawzaan
SWALI:
Je, bid’ah gani zinazotendeka na baadhi ya watu katika Kaburi la Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)?
JIBU:
Bid’ah mbali mbali zinatendeka mara kwa mara katika kaburi la Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), mfano; mtu kuingia Msikitini akitoa salaam kwake na kukaa karibu na kaburi. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( لا تجعلوا قبري عيدًا))
((Msifanye kaburi langu ni sehemu ya kurudiwa rudiwa [kuendewa kila mara])) [Musnad Ahmad, Muswannaf 'Abdir-Razzaaq]
Bid’ah nyingine ni kuamini kwamba du'aa hapo hutaqabaliwa na watu huomba kwa sauti na kumuomba yeye Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuamini kuwa du'aa yake itakubaliwa. Hii ni shirk kubwa kabisa.
Inapasa kuzingatia yaliyo katika Shariy’ah kama kumtolea salaam Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
Akiwa anataka mtu kuomba du'aa aombe sehemu yoyote katika Msikiti. Na kuomba baada ya Swalaah ni bora zaidi
[Al Bid’ah wal- Muhdathaat Wa Maa Laa Aswla Lahu – uk. 240 Majallah ad-Da’wah , uk. 1612 uk 37]
Hujaji Kubakia Majumbani Wiki Wanaporudi Kwao Bila Kwenda Swalaah Ya Jamaa
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Baadhi ya Hujaji wanaporudi kwao kutoka ardhi tukufu (Makkah) hubakia majumbani mwao muda wa wiki hawatoki nje, hata inapombidi atoke, wala hawaendi Msikitini kuswali, wanabaki kupokea watu ili wawaombee du'aa. Je hivi ni Sunnah?
JIBU:
Haikuthibitika katika Sunnah, bali ni bid’ah na ni makosa kwa yeyote anayeamini kuwa ni Sunnah.
Kubakia majumbani na kukosa kuhudhuria Swalaah ya Jamaa Misikitini hairuhusiwi isipokuwa kwa sababu zilizokubalika katika katika Shariy’ah. Kwa hiyo kuacha kuhudhuria Swalaah ya Jamaa ni dhambi.
Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Al-Bid'ah wal-Muhdathaat Wa Maa Laa Aswala Lahu – Uk. 406]
Kubusu Ar-Ruknul-Yamaaniy
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Je inaruhusiwa kubusu Ar-Ruknul-Yamaaniy (pembe ya Yemen iliyoko katika Ka'bah)
JIBU:
Kubusu Ar-Ruknul-Yamaaniy (Pembe ya Yemen) haikuthibitika kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
Kitendo chochote ambacho hakikupatikana dalili kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) huwa ni bid’ah na hakimkaribishi mtu kwa Allaah.
Hivyo hakuna shariy’ah ya kubusu Ar-Ruknul-Yamaaniy. Hadiyth iliyotaja hivyo imechambuliwa kuwa ni Hadiyth dhaifu, hivyo haiwezi kuhesabiwa kama ni dalili.
[Al-Bid’ah wal-Muhdathaat wa maa laa aswla lahu – Uk. 388, Fiqh al-'Ibaadaat – Uk. 348]
Mihraab Na Minbar Ya Masjid An-Nabawiy
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Nini hukmu ya kugusa mihraab na minbar ya Masjidun-Nabawiy? (Msikiti wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
JIBU:
Kugusa mihraab, minbar na kuta za Masjidun-Nabawiy yote hayo ni bid’ah.
[Al-Bid'ah wal-Muhdathaat Wa Maa Laa Aswla Lahu – Uk. 403]
Kuingia Masjidul-Haraam Katika Mlango Mahsusi Na Du'aa Anapoona Ka'bah
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Makosa gani yanatendwa na Mahujaji wanapoingia Al-Masjidul-Haraam?
JIBU:
Miongoni mwa makosa yanayotendwa na Mahujaji wanapoingia Masjidul-Haraam ni yafuatayo:
Kwanza:
Baadhi ya watu wanaofanya Hajj au 'Umrah wanadhania kuwa ni muhimu kuingia Masjidul-Haraam katika mlango mahsusi. Mfano wengine wanadhani kwamba kwa ajili ya 'Umrah shariy’ah inampasa mtu aingie katika Baab Al-Umrah (mlango wa 'Umrah). Wengine wanadhani kuwa ni muhimu kuingilia katika Baabus-Salaam (Mlango wa Amani) na kwamba kuingilia milango mingine ni dhambi au jambo lisilopendeza. Hakuna dalili yoyote inayotaja hivi, kwa hiyo anaweza mtu kuingilia mlango wowote uliokuwa karibu naye. Kinachompasa ni kufuata Sunnah kwa kuingia Msikitini kwa kutanguliza mguu wa kulia na kusema:
أَعُوذُ بِاللَّهِ الْعَظِيمِ, وَبِوَجْهِهِ الْكَرِيمِ, وَسُلْطَانِهِ الْقَدِيمِ, مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ. بِسْـمِ الله، وَالصَّلاةُ وَالسَّلامُ عَلى رَسولِ الله، اللّهُـمَّ افْتَـحْ لي أَبْوابَ رَحْمَتـِك
Najikinga na Allaah Aliye Mtukufu, na kwa Wajihi Wake Karimu, na kwa utawala Wake wa kale, kutokana na shaytwaan aliyeepushwa na Rehma za Allaah
Kwa jina la Allaa na Swalaah na Salaam zimfikie Rasuli wa Allaah. Ee Allaah nifungulie milango ya Rehma Yako
Pili:
Baadhi ya watu wanazusha du'aa wanapoingia Masjidul-Haraam na wakati wa kuliona Ka'bah. Du'aa hizo ni za bid’ah kwa sababu hazikutajwa na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Hivyo ikiwa vitendo vyote vya ‘ibaadah ikiwa ni kauli au matendo havikupatikana dalili kutoka katika Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba zake huwa ni vya bid’ah na kuvitenda ni kutenda dhambi ambayo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameonya sana.
[Al-Bid’ah wal-Muhdathaat wa maa laa aswla lahu – Uk. 384, Fiqh al-'Ibaadaat – Uk. 344]
Kuomba Du'aa Ndefu Anapoanza Twawaaf Katika Mstari Wa Hajar Al-Aswad
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Baadhi ya Hujaji wanapofikia mstari ambao ni alama ya kuanzia twawaaf (iliyoko sambamba na Hajar al-Aswad), husimama kwa muda mrefu kuomba du'aa wakiwazuia wenzao wasiendelee kufanya twawaaf zao. Nini hukmu ya kufanya hivyo?
JIBU:
Haifai kusimama muda mrefu katika mstari huo na kuomba du'aa. Inavyopasa ni kuelekea Hajar al-Aswad na kuliashiria kwa mkono wa kulia na kusema: “Allaahu Akbar”, kisha aanze kufanya twawaaf.
Wengine pia husimama na kutia niyyah kwa kutamka kwa sauti kusema "Natia niyyah kufanya twawaaf (mizunguko) saba za 'Umrah kwa ajili ya Allaah." Kutamka niyyah katika vitendo vya ‘ibaadah ni bid’ah kwani haikuthibitika kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wala Maswahaba. Hivyo niyyah huwekwa moyoni na Allaah Anajua niyyah za waja Wake. (Na hivi ndivyo ilivyokuja katika mafunzo ya Sunnah).
[Daliyl al-Akhtwaa Yaqa'a fiyhaa al-Haaj wal-Mu’tamir wat-Tahdhiyr minhaa – Uk. 42].
Kuomba Du'aa Ndefu Nyuma Ya Maqaam Ibraahiym
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Nini hukmu ya kusoma du'aa ndefu nyuma ya Maqaam Ibraahiym?
JIBU:
Miongoni mwa bid’ah zinazofanywa na baadhi ya Hujaji wanaposimama nyuma ya Maqaam Ibraahiym ni kwamba wanasoma du'aa ndefu wanayoiita du'aal-Maqaam (du’aa ya kisimamo).
Hakuna dalili hiyo katika Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Hii ni bid’ah iliyokatazwa na kila bid’ah humpotosha Muislamu.
Baadhi ya watu hukusanyika katika vikundi wanasoma vijitabu vya du'aa kwa sauti, akiwa mmojawao anaongoza na nyuma yake wanaitikia kwa mkarara na kusema 'Aamiyn'. Yote hayo ni bid’ah na husababisha madhara ya tashwishi kwa Hujaji wanaoswali Maqaam Ibraahiym, nalo ni jambo ovu.
[Al-Bid'u wal-Muhadathaat wa maa laa aswala lahu – Uk. 399; Fiqh al-'Ibadaat – Uk 356]
Kuosha Vijiwe Kwa Ajili Ya Jamaraat
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Nini hukmu ya kuosha mawe kwa ajili ya Jamaarat? (Sehemu za kurusha vijiwe)
JIBU:
Yasioshwe, kwani kufanya hivyo kwa niyyah ya ‘ibaadah kwa ajili ya Allaah, huwa ni bid’ah kwa sababu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakufanya hivyo.
[Al-Bid'ah wal-Muhdathaat wa maa laa aswla lahu – Uk. 404]
Kusoma Du’aa Zisizothibiti Na Kwa Mkusanyiko Wa Watu Katika Twawaaf
Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)
SWALI:
Makosa gani yanayotendekea katika twawaaf?
JIBU:
Hujaji wanasoma du'aa mahsusi wanapofanya twawaaf. Na wengi wao wanakuwa katika vikundi, kisha mmoja wao anayewaongoza husoma hizo du'aa na wengine wanakariri kwa mkarara mmoja. Haya ni makosa katika vipengele viwili;
Kwanza:
Hivyo ni kufuata du'aa ambazo hazimo katika mafunzo ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika twawaaf.
Pili:
Kuomba du'aa katika kikundi kwa mkarara ni bid’ah (uzushi). Juu ya hivyo ni kusababisha tashwishi kwa Hujaji wengine wanaofanya twawaaf. Shariy’ah inampasa kila mmoja asome du'aa yake bila ya kupandisha sauti.
[Al-Bid’ah wal-Muhdathaat wa maa laa aswla lahu – Uk. 398. Al-Fataawa Fadhwiylatush-Shaykh Swaalih Ibn Fawzaan al-Fawzaan – Mjalada 2, Uk. 30]
Kutamka Talbiyah Pamoja Kwa Kukariri
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Nini hukmu ya kutamka talbiyah katika kikundi kwa mkarara?
JIBU:
Baadhi ya Hujaji wanatamka talbiyah pamoja kwa mkarara, aidha mmoja wao akiwa mbele yao, au katikati au nyuma yao akitamka na wengine wakikariri. Hii haikuthibitika kutoka kwa Swahaba yeyote, bali Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) alisema:
"Tulikuwa na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika ‘Hijjatul-Widaa’ (Hajj Ya Kuaga) na miongoni mwetu kuna waliokuwa wakisema: “Allaahu Akbar” na wengine wakisema: “Laa Ilaah Illa Allaah” na wengine wakitamka talbiyah."
Hivyo ndivyo inavyopasa kuwa kila mmoja atamke talbiyah pekee na sio kwa pamoja.
[Al-Bid’ah wa-Muhdathaat wa maa laa aswla lahu – Uk 394 Fiqh al-Ibadaat Uk 343]
Kuwaombea Du'aa Wazazi Katika Swalaah Na Kupeleka Thawabu
Za Kusoma Qur-aan Au Twawaaf Kwa Ajili Yao
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Inasemekana kuwa kuwaombea du'aa wazazi katika Swalaah za fardhi hairuhusiwi wala kuwasomea Khitmah kutegemea thawabu ziwafikie au kuwafanyia twawaaf.
JIBU:
Hakuna ubaya kuomba du'aa katika Swalaah aidha kwa ajili ya nafsi yake mtu, au kuwaombea wazazi (au wengineo) bali hii inapasa. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mja huwa karibu kabisa na Rabb wake akiwa katika sujuud, hivyo ongezeni kufanya du'aa [humo])) [Muslim]
Pia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ama Rukuu ni kumtukuza Allaah, na ama sujuud ni kujitahidi kufanya du'aa kwani ni karibu zaidi na kukubaliwa)) [Muslim]
Na katika Swahiyhayn za Imaam al-Bukhaariy na Imaam Muslim kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimfundisha tashahhud akasema: ((…na chagua du'aa ambayo unaipenda na uombe [humo]))
Riwaayah nyengine: ((…na chagua unachotamani))
Inavyokusudiwa hapa ni kuwa kabla ya tasliym (kutoa salaam), kwa hiyo akiomba du'aa katika sujuud au mwisho wa Swalaah kwa ajili ya nafsi yake, wazazi wake au Waislamu, hakuna ubaya kwani ni kama ilivyotajwa kwa ujumla katika Hadiyth hizi na nyinginezo.
Ama kusoma khitmah na kutegemea thawabu, au kuwafanyia twawaaf wazazi, au Waislamu wengineo, hii ni mas-ala yenye ikhtilaaf baina ya ‘Ulaama. Lililokuwa ni bora ni kuacha kwani hakuna dalili inayotaja kuruhusiwa kwake. Vitendo vya ibaada vimebainishwa wazi kwa kuthibiti daima kwa hiyo kusitendewe vitendo vingine ila vikiwa vimetajwa katika Shariy’ah ya Dini kwani Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
( من أحدث في أمرنا هذا ما ليس منه فهو رد) متفق عليه.
((Atakayezusha katika mambo yasiyokuwa yetu (Ya Dini yetu) kitarudishwa)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Katika Riwaayah nyengine:
(( من عمل عملاً ليس عليه أمرنا فهو رد)) البخاري
((Atakayetenda kitendo kisichokuwa chetu (katika Dini yetu) basi kitarudishwa)) [Al-Bukhaariy]
Wa Billaahi Tawfiyq
[Al-Bid’ah wal-Muhdathaat wa Maa Laa aswla lahu – Uk.382]
[Majalah al-Buhuuth al-Islaamiyyah - Mjalada 46, Uk. 198]
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/265
[2] http://www.alhidaaya.com
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9202&title=Fataawaa%3A%20Bid%27ah%20Katika%20%27Umrah%20Na%20Hajj
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9203&title=01-Shaykh%20Swaalih%20Al-Fawzaan%3A%20Bid%E2%80%99ah%20%20Inayotendeka%20Katika%20Ziara%20Ya%20Kaburi%20La%20Nabiy%20%20Swalla%20Allaahu%20%27Alayhi%20Wa%20Aalihi%20Wa%20Sallam%20
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9204&title=02-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Hujaji%20Kubakia%20Majumbani%20Wiki%20Wanaporudi%20Kwao%20Bila%20Kwenda%20Swalaah%20Ya%20Jamaa
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9205&title=03-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Kubusu%20Ar-Ruknul-Yamaaniy%20%20
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9206&title=04-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Kugusa%20Mihraab%20Na%20Minbar%20Ya%20Masjid%20An-Nabawiy
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9207&title=05-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Kuingia%20Masjidul-Haraam%20Katika%20Mlango%20Mahsusi%20Na%20Du%27aa%20Anapoona%20Ka%27bah
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9208&title=06-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Kuomba%20Du%27aa%20Ndefu%20Anapoanza%20Twawaaf%20Katika%20Mstari%20Wa%20Hajar%20Al-Aswad
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9209&title=07-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Kuomba%20Du%27aa%20Ndefu%20Nyuma%20Ya%20Maqaam%20Ibraahiym
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9210&title=08-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Kuosha%20Vijiwe%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Jamaraat%20%20
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9211&title=09-Shaykh%20Swaalih%20Al-Fawzaan%3A%20Kusoma%20Du%E2%80%99aa%20Zisizothibiti%20Na%20Kwa%20Mkusanyiko%20Wa%20Watu%20Katika%20Twawaaf
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9212&title=10-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Kutamka%20Talbiyah%20Pamoja%20Kwa%20Kukariri
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9213&title=11-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20Kuwaombea%20Du%27aa%20Wazazi%20Katika%20Swalaah%20Na%20Kupeleka%20Thawabu%20Za%20Kusoma%20Qur-aan%20Au%20Twawaaf%20Kwa%20Ajili%20Yao