كِتَابُ اَلصَّلَاةِ
Kitabu Cha Swalaah
Abu Maalik Kamaal Bin As-Sayyid Saalim
Imetarjumiwa na 'Abdullaah Mu'aawiyah (Abu Baasim)
Imepitiwa Na 'Abu 'Abdillaah
Alhidaaya.com
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
000-Swalaah
Alhidaaya.com [3]
· Taarifu Yake:
[Mawaahibul Jaliyl (1/277), Al-Majmu’u (3/3) na Kash-Shaaful Qina’a (1/221)]
"Swalaah" kilugha ina maana ya du’aa. Na Swalaah ya kisharia imeitwa hivyo kwa vile inakusanya du’aa. Hivi ndivyo walivyosema mabingwa wengi wa lugha na wahakiki wengineo.
Allaah Mtukufu Anasema:
((وصل عليهم))
Yaani waombee
Na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( إذا دعي أحدكم فليجب، فإن كان صائما فليصل...))
((Anapoalikwa mmoja wenu basi aitikie, na kama amefunga basi amwombee du’aa mwalikaji chakula)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim. Itakuja kuelezewa mbeleni].
Ama kiistilahi, Swalaah ni kumfanyia ‘ibaadah Allaah Mtukufu kwa maneno na vitendo maalumu, vikifunguliwa kwa takbiyrah na kuhitimishwa kwa tasliym, pamoja na niya, kwa masharti mahsusi.
· Cheo Chake Katika Dini
1- Swalaah ndio faradhi iliyosisitiziwa na iliyo bora zaidi baada ya shahada mbili na ni moja kati ya nguzo za Kiislamu.
Imepokelewa na Ibn 'Umar kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Uislamu umejengewa juu ya (nguzo) tano: Kushuhudia kwamba hapana mungu mwingine isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Rasuli wa Allaah, kusimamisha Swalaah, kutoa Zakaat, kufunga Ramadhwaan na kuhiji)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (8) na Muslim (16)].
2- Allaah Ametoa onyo kali kwa mwenye kuacha Swalaah kufikia mpaka Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kumnasibisha mtu huyo na ukafiri, akasema:
((Hakika baina ya mtu na shirki na ukafiri ni kuacha Swalaah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (987), Abu Daawuud (1658), An-Nasaaiy (1/231) na wengineo].
Na anasema tena:
((Ahadi iliyopo baina yetu na wao ni Swalaah, mwenye kuiacha basi amekufuru)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (2621), An Nasaaiy (1/231) na Ibn Maajah. Angalia Sanad Zake katika kitabu cha Ta-’adhwiymu Qadri As-Swalaat (uk. 894) nilichokifanyia uhakiki]
‘Abdullah bin Shuqayq ambaye ni Taabi’iy amesema: “Maswahaba wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) walikuwa hawaoni amali ambayo kuiacha kwake ni ukafiri isipokuwa Swalaah”.[Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (2622), na Ibn Naswr katika kitabu cha Ta’adhiymu Qadri As-Swalaat (uk. 948) nilichokifanyia uhakiki]
3- Swalaah ndio nguzo ya dini, na dini haisimami ila kwa nguzo hii. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:
((Kichwa cha mambo yote ni Uislamu, nguzo yake ni Swalaah, na kilele chake cha juu kabisa ni kufanya jihadi katika Njia ya Allaah)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (2616), na Ibn Maajah (3973)].
4- Ni kitu cha kwanza atakachohisabiwa mja. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:
((La kwanza atakalohisabiwa mja Siku ya Qiyaamah ni Swalaah. Ikiwa imefaa, basi amefaulu na kufuzu. Na ikiwa imeharibika, basi amepita utupu na amekula hasara)).
5- Swalaah ilikuwa ndio kitulizo cha jicho kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika maisha yake. Anasema Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Kitulizo cha jicho langu kiko ndani ya Swalaah)).
6- Swalaah ilikuwa ndio wasiya wa mwisho aliousia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) umati wake wakati wa kufariki kwake. Alisema:
((Chungeni Swalaah, na watumwa wenu)).
7- Ni ‘ibaadah pekee isiyombanduka aliyebaleghe. Humganda maisha yake yote na wala hasameheki nayo vyovyote hali iwavyo.
8- Swalaah ina sifa za kipekee kulinganisha na ‘ibaadah nyinginezo. Kati ya sifa hizo:
(a) Allaah Mtukufu Aliifaradhisha Yeye Mwenyewe kwa kuzungumza moja kwa moja na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) usiku wa Mi-’iraaj.
(b) Ni faradhi iliyotajwa zaidi katika Qur-aan Tukufu.
(c) Ni ‘ibaadah ya kwanza Aliyoifaradhisha Allaah Mtukufu kwa Waja Wake.
(d) Imefaradhishwa mara tano mchana na usiku kinyume na ‘ibaadah na nguzo nyinginezo.
· Vigawanyo Vya Swalaah
Swalaah ina vigawanyo viwili. Kuna Swalaah za faradhi na Swalaah za Sunnah
1- Swalaah za Faradhi
Ni zile ambazo mwenye kuziacha kwa kusudi, huwa amemwasi Allaah Mtukufu, nazo ziko aina mbili:
(a) Fardhu ‘Ayn
Hizi ni zile ambazo ni lazima kwa kila aliyebaleghe na mwenye akili, mwanamke au mwanamume, aliye huru na mtumwa. Hizi ni kama Swalaah tano.
(b) Fardhu Kifaayah
Hizi ni zile ambazo baadhi ya watu wakiziswali, basi huwatosheleza wengineo. Ni kama Swalaah ya maiti.
2- Swalaah za Sunnah
Ni zile ambazo mwenye kuacha kuziswali kwa kusudi, hamuasi Allaah Mtukufu. Ni kama Sunnah zilizozoeleka na nyinginezo zitakazoelezewa katika milango ijayo. Lakini pamoja na hivyo, imesuniwa kuziswali Swalaah za Sunnah, kwani kuziacha ni makruhu.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
001-Kwanza: Swalaah Tano
Alhidaaya.com [3]
Mwenye kuacha kuswali ana hali mbili: Ima aache akikataa kwamba si fardhi na si wajibu, au aache kwa uzembe na uvivu tu lakini anakubali kwamba ni wajibu kwake kuswali.
[1] Anayeacha kwa kupinga:
[Al-Majmu’u (3/16), kwa mabadilisho madogo. Angalia vitabu rejea vilivyoashiriwa katika suala linalofuatia]
Mwenye kuacha Swalaah akikataa kwamba si lazima, au akakataa ulazima wake lakini akawa anaonekana akiswali, basi huyo ni kafiri murtadi kwa Ijma’a ya Waislamu.
Kiongozi atamtaka atubie. Kama atatubia ataachwa, na kama atakataa basi atamwua kwa kuwa ni murtadi, na atafanyiwa hukmu zote za wenye kuritadi. Haya atafanyiwa yule aliyeishi na kukulia katika jamii ya Kiislamu. Lakini ikiwa bado ni mgeni na Uislamu, au aliishi maeneo ya mbali na Waislamu ikawezekana kwamba hakuweza kujua wajibu wa Swalaah, basi huyo hatokufurishwa kwa kukataa, bali tutamweleza wajibu wa Swalaah. Ikiwa atakataa baada ya kuelezwa, basi anakuwa ni murtadi.
[2] Anayeacha kwa uvivu na kuzembea tu lakini hakatai kuwa ni wajibu:
Waislamu wote wanakubaliana kwamba kuacha Swalaah ya fardhi kwa makusudi (bila ya udhuru wowote wa kisharia), ni moja kati ya makosa mazito na madhambi makubwa, na kwamba kosa hilo mbele ya Allaah ni kubwa kuliko madhambi ya kuua mtu, kupora mali, kuzini, kuiba na kunywa tembo, na kwamba kosa hilo hupelekea kwenye adhabu ya Allaah, hasira Zake na hizaya Yake duniani na aakhirah. [As-Swalaat wa Hukmu Taarikihaa cha Ibn Al-Qayyim (uk. 60). Nyongeza kati ya mabano nimeiweka mimi na umuhimu wake haufichiki]
Halafu 'ulamaa wamekhitalifiana kuhusu hukmu yake juu ya kauli mbili:
Ya kwanza: Mtu huyu ni fasiki, mwasi na mtendaji kosa kubwa kabisa lakini si kafiri. Haya wameyasema Maulamaa wengi, nayo ni rai yenye nguvu ya Ath-Thawriy, Abu Haniyfah na Masahibu zake, Maalik, Ash-Shaafi’iy na Ahmad katika moja ya riwaya mbili. [Haashiyat Ibn ‘Aabidiyna (1/235), Al-Fataawaa Al-Hin-diyyah (1/50), Haashiyat Ad-Dusuwqiy (1/189), Mawaahibul Jaliyl (1/420), Mughnil Muhtaaj (1/327) na Al-Majmu’u (3/16 na zinazofuatia). Angalia I’ilaamu Al-Ummat cha Sheikh ‘Atwaa bin ‘Abdillatwiyf (Allaah Amhifadhi)]
Ya pili: Ni kafiri mwenye kutoka nje ya Uislamu. Ni rai yenye nguvu ya Sa’iyd bin Jubayr, Ash-Sha’abiy, An-Nakh’iy, Al-Awzaa’iy, Ibn Al-Mubaarak, Is-Haaq, na kauli mbili sahihi toka kwa Ahmad na moja kati ya ijtihadi za Mafuqahaa wa Kishaafi’iy. Kauli hii imesimuliwa na Ibn Hazm toka kwa ‘Umar bin Al-Khattwaab, Mu’aadh bin Jabal, ‘Abdul Rahmaan bin ‘Awf, Abu Hurayrah na Maswahaba wengineo. [Muqaddimaat Ibn Rushdi (1/64), Al-Muqni-’i (1/307), Al-Inswaaf (1/402), Majmu’u Al-Fataawaa (22/48), As-Swalaat cha Ibn Al-Qayyim na Hukmu Taarikis Swalaat cha Sheikh Mamdouh Jaabir (Allaah Amhifadhi)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
002-Baadhi Ya Dalili Za Makundi Mawili
Alhidaaya.com [3]
[1] WENYE KUSEMA SI KAFIRI
Wanasema kwamba hukmu ya Uislamu imeshathibiti kwake baada ya kuingia, nasi hatuwezi kumtoa kwenye Uislamu ila kwa uthibitisho. Kisha wakatoa dalili zifuatazo kuthibitisha kwamba mtu huyo hatoki kwenye Uislamu:
(a) Dalili zinazoonyesha kwamba Allaah Mtukufu Anayasamehe madhambi yote isipokuwa shirki tu. Ni kama:
1- Neno Lake Ta’alaa:
(( إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدِ افْتَرَىٰ إِثْمًا عَظِيمًا))
((Hakika Allaah Haghufurii kushirikishwa; lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae. Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amezua dhambi kuu)). [An Nisaa: (4:48)].
Wanasema kwamba kwa mujibu wa Aayah hii, mwenye kuacha Swalaah si kafiri, kwa kuwa anaingia ndani ya wigo wa Utashi wa Allaah (wa kusamehewa).
Wenye kusema ni kafiri wamejibu:
“Aayah hii haikanushi ukafiri wa mwenye kuacha Swalaah, kwa kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Hakika baina ya mtu na shirki na ukafiri ni kuacha Swalaah)). [Hadiyth Swahiyh: Imeelezewa nyuma kidogo].
Hivyo basi, mwenye kuacha Swalaah anaingia kwenye ujumuishi wa Aayah wenye kuashiria kwamba hilo (la kuacha Swalaah) ni katika mambo ambayo Allaah Hayasamehi, kwa kuwa mtu huyo ni mushrik kwa mujibu wa Hadiyth hii. Na lau tutachukulia kwamba mtu huyu ni kafiri na si mushrik na kwamba Aayah inaeleza kuwa kuna msamaha kwa makosa yaliyo chini ya shirki, basi hakuna ndani ya Aayah hii linaloonyesha kwamba Allaah Hasamehi ukafiri ambao hautokani na shirki, bali makusudio hapa ni kuwa Allaah Anasamehe yaliyo chini ya shirki. Ama yasiyo shirki katika mambo ya kikafiri (kama kumkadhibisha Allaah na Rasuli Wake au kuwatusi), hakuna katika Aayah linalogusia kwamba yanasamehewa, bali hilo linapingana na Qur-aan na Hadiyth zilizo wazi. Hivyo basi, kwa makadirio yote mawili, hakuna mashiko ya kuitumia Aayah katika kutolea hoja.” [Kitabu cha Dhwawaabit At-Takfiyr In-da Ahlis Sunnati wal Jama’a cha Al-Qarniy (uk. 158) kwa mabadilisho madogo]
(b) Dalili zinazoonyesha kwamba mwenye kusema (Laa ilaah illa Allaah) ataingia peponi bila sharti la kuwepo Swalaah. Kati ya hizo ni:
2- Hadiyth ya Mu’aadh bin Jabal kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Hakuna mja yeyote anayeshuhudia kwamba hapana mola isipokuwa Allaah, na kwamba Muhammad ni Rasuli wa Allaah isipokuwa Allaah Humharamishia moto)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (128) na Muslim (32) na tamko ni lake. Kwa Al-Bukhaariy kuna: “..akisadikisha toka moyoni mwake”].
3- Hadiyth ya ‘Ubaadah bin Swaamit kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Mwenye kushuhudia ya kwamba hapana mola isipokuwa Allaah Mmoja Asiye na mshirika, na kwamba Muhammad ni Mja Wake na Rasuli Wake, na kwamba ‘Iysaa ni Mja wa Allaah na Rasuli Wake, na kwamba Neno Lake Alilitia kwa Maryam na roho itokayo Kwake, na kwamba Pepo ni kweli na Moto ni kweli, Allaah Atamwingiza Peponi kwa amali yoyote atakayokuwa nayo)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (3435) na Muslim (28)].
4- Hadiyth ya Mu’aadh bin Jabal kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Mtu ambaye maneno yake ya mwisho yatakuwa: Laa ilaaha illa Allaah, ataingia Peponi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (3116)].
5- Hadiyth ya ‘Utbaan bin Maalik kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Hakika Allaah Amemharamishia Moto mwenye kusema: “Laa ilaaha illa Allaah” akitaka kwa hilo Uso wa Allaah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (425) na Muslim (33)].
Wanasema kwamba katika Hadiyth hizi hakuna sharti ya kuwepo Swalaah ili aokoke na Moto na aingie Peponi.
Wenye kusema ni kafiri wamejibu:
“Hadiyth hizi na zinginezo mfano wake zina vigawanyo viwili: Ima ni jumuishi zenye kuainishwa na Hadiyth zenye kuthibitisha ukafiri wa asiyeswali, au zisizo ainishi zenye kuainishwa na Hadiyth zinazoonyesha kwamba haiwezekani kwa mwenye kusema maneno hayo asiswali kama inavyobainika katika neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((..akitaka kwa hilo Uso wa Allaah)) au ((akisadikisha toka moyoni mwake)) na mfano wa hivyo. Hadiyth kama hizi zina ainisha kuwa kutamka shahada kwa niya safi na moyo kusadikisha kikweli, humzuia mtu asiache Swalaah, kwa kuwa utakasifu wake wa niya na ukweli wa moyo wake, vitamfanya aswali tu. [Kitabu cha “Hukmu Taarikis Swalaat” cha Al’Allaamah bin ‘Uthaymiyn Rahimahul Laahu]
(c) Allaah Mtukufu Atamtoa motoni mtu ambaye hakufanya kheri yoyote katu.
[Kitabu cha “Hukmu Taarikis Swalaat” cha Al’Allaamah Al-Albaaniy Rahimahul Laahu (uk. 36)]
6- Katika Hadiyth ya Abu Sa’iyd kuhusiana na uombezi, baada ya kuelezea uombezi wa Waumini kwa nduguzo ili watolewe Motoni, Hadiyth inaendelea ikisema: ((…Watasema: Ee Rabb wetu! Hakika tumewatoa wale Uliotuamuru, na katika waliobakia hakuna hata mmoja mwenye kheri!! Kisha Allaah Atasema: Malaika wamefanya uombezi, Manabii wamefanya uombezi, na Waumini wamefanya uombezi, na Amebakia Mrehemevu zaidi kuliko wote wenye huruma. Atakamata kamato la Moto lenye watu ambao hawakumfanyia Allaah jema lolote katu, wameungua mpaka wamekuwa makaa, kisha watapelekwa kwenye maji yaitwayo (Uzima) wamiminiwe. Wataota kama inavyoota punje katika taka za maji..)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (6560) na Muslim (183)].
Wenye kusema ni kafiri wamejibu:
“Swalaah haiingii katika ujumuishi wa neno lake Rasuli Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam: “Hawakufanya kheri yoyote katu”. Vipi iwezekane asiyeswali aingie katika kundi la hawa huku akiwa ameangamia pamoja na wenye kuangamia!!:
((يَوْمَ يُكْشَفُ عَن سَاقٍ وَيُدْعَوْنَ إِلَى السُّجُودِ فَلَا يَسْتَطِيعُونَ ● خَاشِعَةً أَبْصَارُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۖ وَقَدْ كَانُوا يُدْعَوْنَ إِلَى السُّجُودِ وَهُمْ سَالِمُونَ))
((Siku utakapofunuliwa Muundi na wataitwa kusujudu lakini hawatoweza ● Macho yao yatainama chini, udhalilifu utawafunika. Na hali walikuwa wakiitwa wasujudu (kuswali duniani) walipokuwa wazima wa afya)). [Al Qalam (68: 42 na 43)]
Kisha Hadiyth Swahiyh zinatutaarifu kwamba kila atakayetolewa motoni katika wale wenye Iymaan ya Tawhiyd, atajulikana kutokana na athari ya sijdah. Katika Hadiyth Marfu’u ya Abu Hurayrah, Rasuli anasema: ((Mpaka Allaah Atakapomaliza kuhukmu baina ya Waja Wake, na Akataka kumtoa kwa Rahma Zake yule Atakayemtaka katika wale waliokuwa wakishuhudia kwamba hapana mola isipokuwa Allaah, Atawaamuru Malaika wawatoe, nao watawatambua kwa alama zao za sijdah. Allaah Ameuharamishia Moto kuila athari ya sijdah ya mwanadamu. Malaika watawatoa wakiwa wamevimba, na hapo hapo watamiminiwa maji yajulikanayo kama “Maji ya uzima”. Atabakia mtu mwenye kuuelekea Moto kwa uso wake, kisha uso wake utageuzwa kuepushwa na Moto)). Anasema Abu Hurayrah: “Na huyo ndiye mtu wa mwisho kuingia Peponi”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (6573-7337) na Muslim (182)].
Wanasema: “Hadiyth inaonyesha wazi kabisa kwamba wale ambao Allaah Mtukufu Atawatoa Motoni kwa Rahma Zake, Malaika watawatambua kwa athari zao za sijdah, na hao bila shaka ni wenye kuswali. Ama neno la Waumini (katika Hadiyth ya Abu Sa’iyd): “Na katika waliobakia, hakuna hata mmoja mwenye kheri!!”, hii ni kwa mazingatio ya kuwa wanalijua hilo kwa dalili kwamba Allaah Amewaambia (kama ilivyo katika Hadiyth ya Abu Sa’iyd): “Basi watoeni wale mnaowajua kati yao”. Na kama si hivyo, basi ndani ya Moto wapo wenye kuswali katika umma huu na umma zilizotangulia ambao hakuna awajuao isipokuwa Allaah, na hao Atawatoa kwa Rahma Yake. Ama wasioswali, hao hawatoki humo”. [Ni sehemu ya utangulizi wa Sheikh Muhammad ‘Abdul Maqsoud (Allaah Ampe afya njema) aliouandika kwenye Tasnifu ya Mamdouh (uk. 38 na zinazofuatia) kwa mabadilisho madogo]
(d) Hadiyth zinazofahamika kwamba kutoswali hakumtoi mtu katika Uislamu. Kati yake ni:
7- Hadiyth ya ‘Ubaadah bin Swaamit aliyesema: “Nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
(( Allaah Amezifaradhisha Swalaah tano kwa Waja Wake. Atakayekutana Naye na Swalaah hizo akiwa hajapoteza chochote, atakutana Naye nailhali Yeye Anayo ahadi kwake ya kumwingiza kwayo Peponi. Na atakayekutana Naye na Swalaah hizo akiwa amepunguza chochote kwa kuzembea haki zake, atakutana Naye Akiwa Hana ahadi kwake. Akitaka Atamwadhibu, na Akitaka Atamsamehe)). [Hadiyth Dhwa’iyf: Angalia Kitabu cha “Ta’adhiymu Qadris Swalaat” (1029) nilichokifanyia uhakiki. Nimezihakiki kwa kina Sanad Zake, nikapata yakini kwamba ni Dhwa’iyf. Al-Albaaniy (Rahimahul Laahu) anasema ni Swahiyh]
Wanasema: “Hadiyth hii inaonyesha kwamba mwenye kuacha baadhi ya Swalaah si kafiri kwa kuwa anaingia ndani ya wigo wa Mapendeleo ya Allaah”.
Wenye kusema ni kafiri wamejibu:
“Haijuzu kuichukulia Hadiyth hii kwa kuacha baadhi ya Swalaah, kwani Hadiyth imethibitisha mtu kuziswali Swalaah tano pamoja na kuzembea baadhi ya mawajibiko yake pale anaposema Rasuli: ((Na atakayekutana Naye na Swalaah hizo akiwa amepunguza chochote kwa kuzembea haki zake…)).
8- Hadiyth ya Abu Hurayrah aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((La kwanza watakalohisabiwa watu katika amali zao ni Swalaah. Mola wetu Atawaambia Malaika (Naye Anajua zaidi): Mwangalieni Mja Wangu kama ameitimiza au kaipunguza. Ikiwa imetimia ataandikiwa imetimia, na kama imepungua chochote Atasema: Angalieni kama Mja Wangu ana Sunnah zozote. Kama anazo Atasema: Mkamilishieni Mja Wangu faradhi zake kwa Sunnah zake, kisha zitachukuliwa amali zake zikiwa hivyo)). [Hadiyth Dhwa’iyf Marfu’u: Ina Sanad nilizozihakiki kwa kina katika Kitabu cha “Ta’adhiymu Qadris Swalaat (182) nilichokifanyia uhakiki. Tamiym Ad-Daariy anasema ni Swahiyh Mawquwf]
Wanasema: “Upungufu katika faradhi utakamilishwa na Sunnah, na upungufu huu unakusanya upungufu katika Swalaah yenyewe ya faradhi na unakusanya upungufu katika idadi ya faradhi”.
Wenye kusema ni kafiri wamejibu:
“Hadiyth haifai kuwa Marfu’u. Ina Sanad Dhwa’iyf na zilizo dhahiri zaidi: ((Ikiwa imefaa, basi amefaulu na kufuzu. Na ikiwa imeharibika, basi amepita utupu na amekula hasara)). Neno lake: ((Imefaa)), lina maana Swalaah iliyokamilika nguzo zake sawasawa, na hivyo haiswihi kulichukulia neno lake: ((..na kama imepungua chochote)) juu ya kuacha nguzo na masharti. Hivyo ni lazima kuuchukulia upungufu kama ni kuacha yaliyo chini ya hayo.” Kwa hoja hii, Hadiyth haifai kutolewa ushahidi.
9-Hadiyth Marfu’u ya ‘Aaishah isemayo: ((Madaftari mbele ya Allaah ni matatu: Daftari ambalo Allaah Hajali kwalo chochote, daftari ambalo Allaah Hatoacha kitu humo, na daftari ambalo Allaah Hatosamehe kitu. Ama daftari ambalo Allaah Hatosamehe kitu ni shirki. Ama daftari ambalo Allaah Hajali kitu ni kujidhulumu mja mwenyewe kwa yaliyo baina yake na Rabb wake kwa kuacha siku moja ya funga, au Swalaah aliyoiacha, kwani Allaah Ta’alaa Huyasamehe na kuyaachilia kama Atataka)). [Hadiyth Dhwa’iyf Marfu’u: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (6/240). Angalia Kitabu cha “Dhaiyful Jaami’i (3022). Iko Hadiyth nyingine kama hii ambayo Swalaah haikutajwa, Al-Albaaniy kasema ni Hasan]
Wenye kusema ni kafiri wamejib
“Kwa kuongezwa neno: ((kwa kuacha siku moja ya funga, au Swalaah aliyoiacha)), Hadiyth inakuwa ni Dhwa’iyf!!
10- Hadiyth ya Nasr bin ‘Aasim Al Laythiy aliyoipokea toka kwa mtu miongoni mwao kwamba mtu huyo alimjia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasilimu lakini kwa sharti kwamba aruhusiwe kuswali Swalaah mbili tu, na Rasuli akamkubalia. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (5/363)].
Wamesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimkubalia mtu huyo kusilimu huku akijua kwamba hatoswali isipokuwa Swalaah mbili tu kati ya tano!!”
Wenye kusema ni kafiri wamejibu:
“Hadiyth haielezi kwamba Swalaah wakati huo zilikuwa ni tano!!”
Inavyoonekana ni kuwa hili lilikuwa wakati Swalaah za faradhi zilikuwa ni mbili tu kabla ya kuwa ni tano. Au inaweza kuwa ni katika mlango wa kumkubalia mtu kusilimu pamoja na kuvunja mwiko. Na hili ni mahsusi kwa Rasuli peke yake, mwingine haruhusiwi kulifanya baada yake.
(d) Wamechukulia kuwa ni ukafiri mdogo uliotajwa kwenye Hadiyth zenye kueleza kwa bayana ukafiri wa asiyeswali
11- Wamesema: “Katika Hadiyth nyingi, tumeuchukulia ukafiri uliotajwa kuwa si ukafiri unaomtoa mtu katika Uislamu kama Hadiyth zisemazo:
((KumtukanaMuislamu ni ufasiki na kumuua ni ukafiri)).
((Mambo mawili waliyonayo watu ni ukafiri kwao: Kutusi nasaba za watu, na kumlilia maiti kwa mayowe))…pamoja na Hadiyth zote zenye kusema: ((Si katika sisi mwenye kufanya kadha…)).
Na hapa ni hivyo hivyo”.
Wenye kusema ni kafiri wamejibu:
“Haya hayaswihi kwa mambo haya yafuatayo: [Kitabu cha “Hukmu Taarikis Swalaat” cha Ibn ‘Uthaymiyn (uk. 14- pamoja na Tasnifu ya Sheikh Mamdouh) kwa mabadilisho madogo]
Kwanza: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameifanya Swalaah kuwa ni mpaka unaotenganisha kati ya ukafiri na Iymaan, na kati ya Waumini na makafiri. Mpaka hukipambanua kilichomo ndani yake na hukitenga na kingine. Na hapa, viwili vilivyomo ndani ya mpaka havifanani na wala haviingiliani.
Pili: Swalaah ni nguzo kati ya nguzo za Kiislamu, na kumwelezea asiyeswali kama ni kafiri kunahukumia kumtoa nje ya Uislamu. Sababu ni kuwa yeye amevunja nguzo kinyume na kumwita kafiri mtu aliyefanya kitendo kati ya vitendo vya kikafiri.
Tatu: Kuna Hadiyth nyinginezo zinazotutaarifu kwamba asiyeswali ni kafiri ukafiri unaomtoa nje ya Uislamu. Hivyo ni lazima kuuchukulia ukafiri huo kama ulivyo ili uendane sambamba na Hadiyth.
Nne: Ukafiri uliotajwa katika Hadiyth walizozitolea hoja hapa umekuja ukiwa bila ya alif na laam “Nakirah”, au kwa tamko la kitenzi. Na hii inaonyesha kuwa ni sehemu ya ukafiri, au ni ukafiri katika kitendo hiki. Ukafiri huu haumtoi mtu katika Uislamu. Ama kuhusu kuacha Swalaah, Rasuli ameutaja ukafiri kwa alif na laam kuonyesha kwamba anakusudia ukafiri wa kweli”.
(e) 12 Wameubebesha ukafiri wa asiyeswali uliotajwa kwenye Hadiyth kwa yule aliyeacha Swalaah kwa kupinga na kukataa
Wenye kusema ni kafiri wamejibu:
“Ubebeshaji huu una mawili ya kutahadhariwa: La kwanza ni kutengua wasifu alioutoa Rasuli na kuuwekea hukmu. Wasifu huu ni ukafiri na sio kupinga au kukataa. La pili ni kuuchukulia wasifu ambao Rasuli hakuufanya ni kiini au kitovu cha hukmu. Kwani kupinga na kukataa ulazima wa Swalaah tano, kunawajibisha ukafiri kwa yule ambaye haijashindikana kwake kulijua hilo sawasawa akiswali au asiswali. Hivyo basi, inabainika kwamba kuzibebesha Hadiyth kuwa zinamkufurisha mwenye kuacha Swalaah kwa kupinga ulazima wake tu, si sahihi. [Tasnifu ya Ibn ‘Uthaymiyn (uk. 12)]
(g)- 13 Wamesema: “Sisi hatujawahi kusikia katika enzi yoyote kwamba asiyeswali hakuoshwa, au kuswaliwa, au kuzikwa kwenye makaburi ya Waislamu, au kunyimwa mirathi, au kuachanishwa mke na mume kwa sababu ya kuacha Swalaah. Na kama angelikuwa ni kafiri, basi angefanyiwa hukmu hizi. [Al-Mughniy (2/446). Ametilia nguvu kutokufurishwa asiyeswali].
[1] WENYE KUSEMA NI KAFIRI
Hawa wametoa hoja kwa dalili zifuatazo:
(a) Hadiyth bayana zenye kumkufurisha asiyeswali. Kati ya Hadiyth hizo ni:
1- Hadiyth ya Jaabir kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Hakika kati ya mtu na kati ya shirki na ukafiri, ni kuacha Swalaah)). [Hadiyth Swahiyh: Imeshaelezwa nyuma]
2- Hadiyth ya Buraydah bin Al-Haswiyb aliyesema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
((Ahadi iliyopo kati yetu na wao ni Swalaah, mwenye kuiacha basi amekufuru)). [Hadiyth Swahiyh: Imeshaelezwa nyuma].
Wenye kusema si kafiri wamejibu:
“Tumeshasema kuwa anayekusudiwa ni yule aliyeupinga na kuukataa ufaradhi wa Swalaah, au ukafiri unaokusudiwa hapa ni ule usiomtoa mtu katika Uislamu.”
3- Yaliyopokelewa Marfu’u toka kwa Anas:
((Mwenye kuacha Swalaah kwa kukusudia, basi amekufuru waziwazi)). [Hadiyth Dhwa’iy: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Twabaraaniy katika Kitabu cha “Al-Awsatw”. Angalia Kitabu cha “Dhwa’iyful Jaami’i” (5530).
Wenye kusema si kafiri wamejibu:
“Hadiyth ni Dhwa’iyf, haifai kwa dalili. Na kama ni Swahiyh, tungeijibu kama tulivyoijibu Hadiyth iliyotangulia”.
4- Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba amesema:
((Vishikio vya Uislamu na amri za dini ni tatu, na juu yake ndiyo misingi ya Uislamu. Mwenye kuacha moja kati ya hayo, basi huyo ni kafiri ambaye damu yake ni halali: Kushuhudia kwamba hapana mungu isipokuwa Allaah, Swalaah za faradhi, na kufunga Ramadhwaan)). [Hadiyth Dhwa’iy: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Ya’alaa. Angalia Kitabu cha “Adh-Dhwa’iyfah” (94)]
Wenye kusema si kafiri wamejibu:
“Hadiyth ni Dhwa’iyf Marfu’u, haifai kutolewa dalili. Na kama itakuwa Swahiyh, ukafiri utakaochukuliwa ni ule usiomtoa mtu kwenye Uislamu. Ama neno lake “Damu yake ni halali”, kuuawa kwake kutachukuliwa kwamba ni adhabu ya kisharia “hadd” na si kwamba ni kafiri”.
(b) Aayah na Hadiyth zinazofahamisha kwamba asiyeswali ni kafiri. Kati ya hizo ni:
5- Neno Lake Ta’aalaa:
((فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَإِخْوَانُكُمْ فِي الدِّينِ ۗ وَنُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ))
((Wakitubu, na wakasimamisha Swalaah, na wakatoa Zakaat; basi ni ndugu zenu katika Dini. Na Tunafasili waziwazi Aayaat kwa watu wanaojua)). [At Tawbah (09: (11)]
Wamesema: “Ili upatikane udugu kati yetu na washirikina, ni lazima watubie shirki yao, wasimamishe Swalaah na watoe Zakaat. Na kama litakosekana mojawapo ya haya, basi udugu utakuwa haupo. Na udugu hauondoki kwa ufasiki au ukafiri mdogo usiomtoa mtu katika Uislamu, bali kwa kutoka nje ya Uislamu”.
Wenye kusema si kafiri wamejibu:
“Kwamba dalili walizozitoa katika kuthibitisha kwamba asiyeswali si kafiri zinatangulizwa juu ya Aayah. Aayah inabebeshwa juu ya ukamilifu wa udugu na si juu ya asili ya udugu. Kama tulivyomtoa mzuiaji wa Zakaat toka kwenye ukafiri kwa Hadiyth: ((Kisha ataiona njia yake; ima kuelekea Peponi au kuelekea Motoni)). [Hadiyth Swahiyh: Itakuja kamili mwanzoni mwa mlango wa Zakaat]. Na hii ni baada ya kutaja adhabu ya asiyetoa Zakaat.
6- Kauli Yake Ta’alaa:
((فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ أَضَاعُوا الصَّلَاةَ وَاتَّبَعُوا الشَّهَوَاتِ ۖ فَسَوْفَ يَلْقَوْنَ غَيًّا ● إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ وَلَا يُظْلَمُونَ شَيْئًا))
((Wakafuata baada yao waovu, walipoteza Swalaah na wakafuata matamanio; basi watakutana na adhabu motoni ● Isipokuwa yule aliyetubu na akaamini na akatenda mema; basi hao wataingia Jannah na wala hawatadhulumiwa chochote)). [ Maryam 19 (59 na 60) ]
Wamesema: “Neno Lake: ((Ila aliyetubia na akaamini)) ni dalili kwamba wakati wao walipoipoteza Swalaah na kufuata matamanio, hawakuwa ni Waumini”.
Wenye kusema si kafiri wamejibu:
“Makusudio ya Neno Lake Ta’alaa ((na akaamini)), ni ima alidumu katika iymaan yake, au aliingia katika iymaan kamili kwa kujikita katika Swalaah”.
7- Neno Lake Ta’alaa kuwazungumzia watu wa motoni:
((مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَر ● قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ ● وَلَمْ نَكُ نُطْعِمُ الْمِسْكِينَ ● وَكُنَّا نَخُوضُ مَعَ الْخَائِضِين ● وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوْمِ الدِّينِ ● حَتَّىٰ أَتَانَا الْيَقِينُ ))
(((Watawauliza): “Nini kilichokuingizeni motoni?”● Watasema: “Hatukuwa miongoni mwa wanaoswali ● “Na wala hatukuwa tunalisha masikini ●“Na tulikuwa tunatumbukia kwenye upuuzi pamoja na wanaotumbukia upuuzini ● “Na tulikuwa tunaikadhibisha Siku ya malipo ● “Mpaka ikatufikia yakini (mauti))). [ Al Muddath-thir 74 (42-47) ]
Wamesema: “Ima kiwe kila kitendo katika vitendo hivi ndicho kilichowaingiza motoni na kuwafanya kuwa katika wahalifu, na ashirio liko wazi, au viwe ni vitendo vyote kiujumla, na hili bila shaka ni kwa ajili ya kuushadidia ukafiri wao na adhabu yao. Na kama si hivyo, basi kila kitendo kati ya hivyo kinahitajia adhabu, kwa kuwa haijuzu kujumuishwa kwenye adhabu kisicho na athari kwenye kile chenye adhabu yake peke”.
Wenye kusema si kafiri wamejibu:
“Aayah imeeleza kwamba wao wameingia Motoni na haikutaja muda wa kukaa wao humo au kama watakaa milele, hivyo basi haiwi ni hoja. Lakini hoja inabakia katika kumfanya asiyeswali kuwa katika wahalifu, na wahalifu katika Kitabu cha Allaah ni makafiri. Nasi tunauchukulia uhalifu huu kuwa ni ule usiomtoa mtu katika Uislamu!! Kinachotatiza uchukuliaji huu ni kwamba Allaah Ta’alaa Amewafanya Waumini kuwa mkabala na wahalifu:
((أَفَنَجْعَلُ الْمُسْلِمِينَ كَالْمُجْرِمِينَ))
(( Je, Tuwafanye Waislamu (watiifu) sawa kama wahalifu?)) [Al Qalam (68:35) ]
Hivyo maana haifai kuwa: ((Je, Tuwafanye Waislamu kama Waislamu?)), na hili liko wazi.
8- Neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Mwenye kuswali Swalaah yetu, akaelekea Qibla chetu na akala kichinjwa chetu, basi huyo ni Muislamu. Ni haki yake haki zetu, na ni juu yake yaliyo juu yetu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (391), At-Tirmidhiy (2608), na An-Nasaaiy (3966) kwa mfano wake].
9- Hadiyth ya Mihjan bin Al-Adra’i Al-Aslami ya kwamba alikuwa katika kikao na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam, halafu adhana ikaadhiniwa, Rasuli akanyanyuka kisha akarejea huku Mihjan akiwa amekaa vile vile. Rasuli akamuuliza: ((Kitu gani kinakuzuilia usiswali? Kwani wewe siMuislamu?)) Akajibu: “Hapana, lakini niliswali kwa watu wangu”. Rasuli Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam akamwambia: ((Ukija, swali pamoja na watu hata kama ulikwishaswali)). [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (857), Ahmad (15800), na Al-Bayhaqiy (2/300). Ndani yake kuna Busra bin Mihjan ambaye hajulikani kwa kauli yenye nguvu].
10- Hadiyth ya Mu’aadh Marfu’u: ((Mwenye kuacha Swalaah ya faradhi kwa kusudi, basi Dhima ya Allaah iko mbali naye)). [Hadiyth Dhwa’iyf: Angalia Kitabu cha “Ta’adhiymu Qadris Swalaat” (921) nlichokifanyia uhakiki, chapa ya Al-‘Ilm]
Wamesema: “Lau kama angelikuwa anabakia kwenye Uislamu, basi angelikuwa na dhima ya Uislamu”.
Wenye kusema si kafiri wamezijibu Hadiyth hizi na zingine zenye maana hizi wakisema:
“Baada ya kuthibiti yanayofahamisha kwamba hatoki kwenye Uislamu, zitakuwa zinabebeshwa maana ya ukamilifu wa Uislamu na sio asili yake, kwa kukusanya kati ya dalili”.
(c) Hadiyth zinazotutaarifu kwamba damu ya asiyeswali ni halali. Kati ya hizo ni:
11- Hadiyth ya Abu Sa’iyd kuhusiana na kisa cha mtu aliyemwambia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Mche Allaah”. Kisa kinasema: “Khalid bin Al-Waliyd akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Je, niikate shingo yake?” Rasuli akasema: ((Hapana, pengine anaswali)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (4351) na Muslim (1064)].
Wamesema: “Rasuli ameifanya Swalaah kuwa ni kizuizi cha kuuawa mtu huyo wakati Maswahaba walipoazimia kumuua walipoona uwezekano wa kuwa kwake ni kafiri”.
Wenye kusema si kafiri wamejibu:
“Inawezekana kuhalalika kumuua asiyeswali kuwa ni adhabu tu ya kisharia “hadd” na si kwa ajili ya ukafiri!!”
Wamejibiwa: “Wanaouliwa kwa adhabu ya kisharia “hadd” kwa Hadiyth ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni: ((Mzinifu aliyeoa, nafsi kwa nafsi, na mwenye kuiacha dini yake, mwenye kufarikiana na jamaa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (6878) na Muslim (1676)].
Mwenye kuacha Swalaah si mzinifu, wala muuaji, bali anabakia kuwa ni mwenye kuiacha dini yake. Na kwa hili, si kila aliyesema kwamba asiyeswali hakufuru kasema kwamba anauliwa kama itakavyokuja kubainishwa.
(d) Hadiyth zinazotutaarifu kwamba ni marufuku kuwapiga pande viongozi na kuwasusia isipokuwa kama hawakusimamisha Swalaah. Kati yake ni:
12- Hadiyth ya Ummu Salamah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mtaletewa viongozi, kisha mtajua (mabaya yao) na mtakemea. Mwenye kuchukia basi ameokoka, na mwenye kukemea basi amesalimika, lakini mwenye kuridhia na kuwafuata (kaangamia) )). Wakasema: "Je, tuwapige vita?" Akasema: ((Hapana, madhali wanaswali)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (1854), At-Tirmidhiy (2266) na Abu Daawuud (4760)].
Imethibiti kwamba haijuzu kuwapiga vita viongozi ila tu kama watakufuru ukafiri dhahiri shahiri kama katika Hadiyth ya 'Ubaadah inayoelezea kumpa kwao Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) bay-'i. Hadiyth inasema: (( Na wala tusizozanie madaraka na watu wake, isipokuwa mkiona ukafiri dhahiri kwao wenye dalili toka kwa Allaah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (7055) na Muslim (1709)].
Hivyo basi, imejulikana kwamba kuacha Swalaah ni ukafiri mkubwa wa dhahiri shahiri.
(e) Ukafiri wa asiyeswali ni kauli ya Jamhuri ya Swahaba bali watu wengi wameelezea Ijma’a yao juu ya kauli hiyo
13- ‘Abdullaah bin Shuqayq amesema: "Maswahaba wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) walikuwa hawaoni kitu chochote kuacha kwake katika amali ni ukafiri isipokuwa Swalaah". [Isnadi yake ni Swahiyh. Imeshaelezewa nyuma].
'Umar bin Al-Khattwaab amesema: "Naam, mwenye kuacha Swalaah hana fungu la Uislamu ". [Isnadi yake ni Swahiyh. Angalia Kitabu cha "Ta'adhiymu Qadris Swalaat" (923-931) nilichokifanyia uhakiki].
Ibn Mas-’oud amesema: "Asiyeswali hana dini". [Sanad yake ina ulaini. Angalia Kitabu cha "Ta'adhiymu Qadris Swalaat" (935-937) nilichokifanyia uhakiki].
Abud Dardaai amesema: "Hana Iymaan asiyeswali". [Sanad yake ni Hasan. Angalia Kitabu cha "Ta'adhiymu Qadris Swalaat" (945) nilichokifanyia uhakiki].
Wenye kusema si kafiri wamejibu:
"Kauli ya Jamhuri ya Maswahaba si hoja madhali Ijma’a yao haijafungika pamoja, na Ijma’a haidhaminiki. Kwa kuwa Ibn Hazm amenukuu kauli hii toka kwa 'Umar bin Al-Khattwaab, Mu'aadh, ‘Abdur Rahmaan bin 'Awf, Abu Hurayrah na wengineo na akasema baada ya hapo: "Sisi kutomjua Swahaba yeyote katika hawa aliyepingana na hili hakuonyeshi kwamba hakuna wengine waliopingana nalo!!"
Kundi lenye nguvu zaidi
“Baada ya kutaja sehemu ya dalili za pande zote mbili pamoja na malumbano yao, bila shaka mwenye kuyatizama hayo, ataona kwamba kwa mujibu wa dalili zilizotolewa na kila kundi katika suala hili, inakuwa si wepesi kukata ni nani aliye sawa na ni nani aliyekosa. Aidha, kutilia kwangu nguvu kundi fulani, hakuizidishii kauli yoyote nguvu, lakini lenye nguvu kwa mujibu wa mwono wangu kwa upande wa usuwl ni kusema: "Asiyeswali ni kafiri, na hasa hasa kama atatubishwa na kiongozi. Kwa kuwa mtu anayeikiri Swalaah moyoni mwake, na anaitakidi kwamba ni wajibu, hawezi kuendelea kushikilia msimamo wa kukataa kuswali mpaka auawe. Haiingii akilini aitwe mbele ya hadhira huku akiuona upanga unang'aa juu ya kichwa chake, akifungwa kamba na akitiwa kitambaa machoni, halafu aambiwe: Swali, la sivyo tutakuua, kisha aseme: Niueni! Mimi sitoswali kamwe, kisha mtu huyo awe baada ya yote hayo niMuislamu!!". [Angalia Kitabu cha "Majmu'u Al-Fataawaa (22/48, 49) na "As-Swalaat" cha Ibn Al-Qayyim (uk.41)]
· Tanbihi
Makusudio ya “Taariku Swalaah” anayehukumiwa kuwa ni kafiri, ni yule asiye swali kamwe na anaendelea kung'ang'ania msimamo wake wa kuacha Swalaah na kudai kwamba anaamini kwamba ni wajibu. Ama watu wengi ambao mara wanaswali mara wanaacha, hawa ni wale wasioihifadhi, na hawa wako ndani ya wigo wa makamio, lakini hawahukumiwi kama ni makafiri. [Angalia Kitabu cha "Majmu'u Al-Fataawaa (22/ 49)]
Kiini cha ukufurishaji katika kuacha Swalaah si tu kuacha, bali kiini chake ni kuiacha kabisa nzima nzima na kuigomea katu katu, au kuiacha kwa picha yake nzima kiasi cha kustahiki asiyeswali kuambiwa kwamba ameipoteza na kuipa mgongo. Kiini hiki ndicho kile kinachofahamika katika Neno Lake Ta’alaa:.
((فَلَا صَدَّقَ وَلَا صَلَّىٰ • وَلَـٰكِن كَذَّبَ وَتَوَلَّى))
((Kwani hakusadiki (Qur-aan na Rasuli) na wala hakuswali •Lakini alikadhibisha na akakengeuka)). [Al Qiyaamah (31 na 32) ] … Hivyo ukengeukaji umefanywa kuwa ndio kitovu cha ukafiri. Ni maarufu kwamba si kila anayeacha Swalaah au baadhi ya Swalaah anakuwa ni mwenye kuipa mgongo Swalaah moja kwa moja. Allaah Ndie Mjuzi Zaidi. [Kitabu cha "Dhwawaabitut Takfiyr” cha Al-Qarniy (uk. 159-161) kwa mabadilisho madogo].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
003-Hukmu Za Kidunia Kwa Asiyeswali
Alhidaaya.com [3]
Tuliyoyaeleza ni hukmu za aakhirah kwa asiyeswali. Ama kwa hapa duniani, hukmu zake ni hizi zifuatazo:
[1] Kwa wenye kusema ni fasiki na si kafiri
Kwa mujibu wa hawa, asiyeswali ni fasiki muasi, naye ni sawa na Waislamu wengine wafanyaji maasi; ni haki yake haki zao, na ni juu yake yaliyo juu yao. Lakini wamekhitalifiana kwa kauli mbili kuhusu nini kiongozi amfanye:
(a)
Atauawa kama adhabu ya kisharia “haddi”.
Maalik na Ash-Shaafi’iy wanasema kwamba atatakwa aswali endapo kama wakati utakuwa mfinyu, na ataonywa kwamba atauawa kama ataichelewesha Swalaah wakati wake ukapita. Na kama ataichelewesha mpaka wakati wake ukatoka, italazimu auawe, na hauawi mpaka atubishwe wakati huo huo. Na kama atashikilia msimamo wake, basi atauawa kama ni adhabu ya kisharia. Wengine wamesema kwamba atapewa muda wa siku tatu.
Baadhi ya Mahanbali wanaosema si kafiri, wanaona kwamba ataitwa aambiwe: “Swali, na kama huswali tutakuua”. Akiswali ataachiliwa, na kama akikataa ni lazima auawe. Na hauawi ila baada ya kuhabisiwa siku tatu ambapo kila wakati wa Swalaah ataitwa ili aswali. Akiswali ataachwa, na kama hakuswali atauawa kama adhabu ya kisharia. Halafu wamekhitalifiana namna ya kumuua. Jamhuri yao wamesema kwamba atapigwa upanga wa shingo.
Na wote hawa wamekubaliana kwamba baada ya kuuawa ataoshwa, ataswaliwa, atazikwa katika makaburi ya Waislamu na atarithiwa.
(b)
Hatouawa bali atafanyiwa izara na atawekwa kifungoni mpaka afe au atubie
Ni rai yenye nguvu ya Az-Zuhriy, Ibn Al-Musayyib, ‘Umar bin ‘Abdul Aziyz, Abu Haniyfah, Daawuud Adh-Dhwaahiriy, Al-Muzniy na Ibn Hazm. Hawa wametoa dalili ya Hadiyth isemayo:
((Si halali damu ya Muislamu anayeshuhudia kwamba hapana mungu isipokuwa Allaah na kwamba mimi ni Rasuli wa Allaah isipokuwa kwa moja ya matatu….)) Hadiyth hii tushaieleza nyuma na Hadiyth zenye maana hii kama ((Nimeamriwa niwapige vita watu mpaka waseme “Laailaaha illa Allaah”, wakisema hilo watazihifadhi damu zao na mali zao kutokana nami ila kwa haki zake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (25) na Muslim (22)].
[2] Kwa wenye kusema ni kafiri
Atafanyiwa hukmu zote za kafiri murtadi. Kati ya hizo ni: [Tasnifu ya Ibn ‘Uthaymiyn (uk. 20-24) pamoja na Tasnifu ya Sheikh Mamdouh]
1- Uwalii (usimamizi) wake utapomoka, hawezi tena kuwa walii kwa jambo lililoshurutishwa awe walii kama kumwozesha binti yake au kuwasimamia watoto wake wadogo na mfano wa hivyo.
2- Harithi wala harithiwi kwa kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Muislamu hamrithi kafiri, wala kafiri hamrithi Muislamu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (4283) na Muslim (1614)].
3- Ni marufuku kuingia Makkah.
4- Alichochinja hakifai kuliwa kinyume naMuislamu na Ahlul Kitaab.
5- Akifa haswaliwi wala haombewi du’aa baada ya kufa.
6- Haruhusiwi kuoa mwanamke wa Kiislamu kwa kuwa yeye ni kafiri kama ilivyo marufuku kwa mwanamume wa Kiislamu kumwoa mwanamke wa kikafiri. Na kwa mujibu wa maimamu wanne, ndoa huvunjika endapo kama mume au mke ataritadi.
Kiongozi atamtaka asiyeswali aswali, na kama hatoswali atauawa. Kama atatubia na kuswali basi ataachiwa. Na kama hatofanya hivyo, basi atamuua kwa hukmu ya kuritadi. Na hili si kwa mtu yeyote, bali ni kwa kiongozi tu. Hili ni muhimu watu walijue!!
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
004-Swalaah Ni Wajibu Kwa Nani?
Alhidaaya.com [3]
Swalaah ni wajibu kwa mwenye akili, aliyebaleghe mwanamume au mwanamke, au muungwana na mtumwa.
1- Ama akili, hii ni sharti ya wajibu wa Swalaah kwa mtu. Swalaah si wajibu kwa mwendawazimu kwa Ijma’a kutokana na kauli yake Rasuli Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam: ((Kalamu imenyanyuliwa kwa watatu: Aliyelala mpaka aamke, mtoto mpaka abaleghe, na mwendawazimu mpaka akili iwe timamu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (4398), An-Nasaaiy (6/156), Ibn Maajah (2041) na wengineo].
Maulamaa wamekhitalifiana kuhusiana na mtu ambaye akili yake imepotea kwa sababu ya ugonjwa, au kwa kupotewa na fahamu au kwa kutumia dawa halali. Kiilivyo ni kwamba aliyepotewa na fahamu na mfano wake, anakuwa hana akili na hatambui lolote. Hukmu kwa huyu inakuwa haipo na wakati wote huo halazimikiwi na Swalaah. Na kama atazindukana akawa na akili katika wakati ambao anaweza kuswali baada ya kujitwaharisha, basi itambidi aswali.
Ama mtu aliyelewa, au aliyelala au aliyesahau mpaka Swalaah ikampita, hawa (hasa) itawabidi walipe Swalaah zilizowapita kutokana na Neno Lake Ta’alaa:
((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنتُمْ سُكَارَىٰ حَتَّىٰ تَعْلَمُوا مَا تَقُولُونَ وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغْتَسِلُوا ۚ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَفُوًّا غَفُورًا))
((Enyi walioamini! Msikaribie Swalaah na hali mmelewa mpaka mjue mnayoyasema, na wala mkiwa mna janaba isipokuwa mmo safarini mpaka muoge josho. Na mkiwa wagonjwa au safarini au mmoja wenu ametoka msalani au mmewagusa wanawake kisha hamkupata maji, basi mtayammam (ikusudieni) ardhi safi ya mchanga, pakeni nyuso zenu na mikono yenu. Hakika Allaah daima ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kughufuria)). [ An Nisaa (4:43)]
Allaah Mtukufu Hakumruhusu mlevi kuswali mpaka akili yake iwe sawa na akijue anachokisema. Na neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Akisahau mmoja wenu Swalaah, au akalala ikampita, basi aiswali anapoikumbuka)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (684)].
Haya ndiyo waliyoyasema Maalik na Ash-Shaafi’iy [isipokuwa wao wametofautisha kati ya ulevi wa kukusudia na wa kutokukusudia]. Na haya haya ndiyo aliyoyasema Ibn Hazm na kukhitariwa na Al-‘Allaamah Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahul Laah) ya kwamba ikiwa akili itamwondoka kwa kujipiga ganzi au kunywa dawa ya kulewesha kwa hiari yake mwenyewe, basi ni lazima alipe, na kama si kwa khiyari yake, basi si lazima alipe. [Haashiyatud Dusuwqiy (1/184), Mughnil Muhtaaj (1/131), Al-Muhallaa (2/233-234) na Al-Mumti’i (2/18)]
2- Ama kubaleghe, hii ni sharti ya wajibu wa Swalaah bila upinzani. Swalaah si wajibu kwa mtoto mpaka abaleghe kutokana na dalili yenye kuonyesha kwamba kalamu ya makalifisho haifanyi kazi kwa mtoto kama ilivyotangulia katika Hadiyth.
·
Kumfundisha Kijana Mdogo Swalaah Na Kumwamuru
Kijana mdogo hata kama si wajibu kwake kuswali, lakini hata hivyo ni lazima baba yake amwamuru kuswali anapofikia umri wa miaka saba, na ampige kumtia adabu kama ataacha anapofikia miaka kumi ili aizoee kutokana na neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Mwamrisheni kijana mdogo kuswali akiwa na miaka saba, na mpigeni akiiacha akiwa na miaka kumi)). [Swahiyh kwa nyingine: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (494) na At-Tirmidhiy (407) toka kwa Sibrah bin Ma’abad. Ina Hadiyth mwenza iliyopokelewa na ‘Abdullaah ‘Umar]
Hii ndio rai yenye nguvu ya Jamhuri ya Maulamaa; Hanafi, Ash- Sha’afi’i na Hanbali. Ama Maalik, yeye ameichukulia amri hii katika Hadiyth kama jambo zuri tu la Sunnah. [Haashiyat Ibn ‘Aabidiyn (1/234), Ad-Dusuuqiy (1/186), Mughnil Muhtaaj (1/131) na Kash-Shaaful Qinaa (1/225).
Na hili ikiwa litaswihi kwao katika kauli yake Rasuli ((Waamrisheni)), basi halitosihi katika kauli yake ((na wapigeni)), kwa kuwa kupiga ni kumtia mtu adabu, nalo haliendani na jambo lililosuniwa. Inavyoonekana ni kuwa imewachanganya amri ya kumwamuru aswali na kumpiga naye bado hajakalifishwa!!
Jawabu: Hilo litakuwa wajibu endapo kama kungelikuwepo usawa, na hapa hauko. Mzazi yuko upande wa wajibu kwa kuwa ni mukallaf, na mtoto wa chini ya miaka kumi hayuko upande huu. Kutokuwepo ulazima kwa mtoto hakumaanishi kwamba mzazi pia hana ulazima, bali ni lazima ampige, lakini mtoto naye hapati dhambi kwa kuacha Swalaah. [Naylul Awtwaar (1/369-370) kwa mabadilisho madogo. Tizama As Saylul Jarraar (1/156)]
·
Tanbihi
Baadhi ya Mafuqahaa wameufanya Uislamu kuwa ni sharti ya kumwajibikia mtu Swalaah. Wanasema: “Si wajibu kwa kafiri wa asili, na kafiri huyu anaposilimu, haamuriwi kuzilipa Swalaah. Na kutowajibishiwa kwa kafiri kunakwenda kinyume na yale yaliyoswihi katika usuul ya kwamba makafiri wanaamuriwa kufuata Uislamu. Hivyo basi ni wajibu kwao, na wao wataadhibiwa huko aakhirah kwa kuiacha.” [As Saylul Jarraar (1/155)]
Ash-Shaafi’iy na Hanbal wameeleza kwamba Swalaah haimlazimu kafiri wa asili ulazima wa kutakwa aswali hapa duniani kwa kuwa Swalaah kwake haiswihi, lakini ataadhibiwa aakhirah kwa kuiacha mbali na adhabu ya ukafiri wake, kwa kuwa lau angesilimu, basi angeweza kuswali. [Mughnil Muhtaaj (1/130) na Kash-Shaaful Qinaa (1/222)]
Na juu ya msingi wa haya, khilafu na wao inakuwa ni ya kilafudhi kwa maana kwamba Swalaah ni lazima kwa kafiri ingawa haiswihi, na hivyo basi Uislamu unakuwa ni sharti ya kuswihi Swalaah na si sharti ya wajibu wa Swalaah. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
Ninasema: “Kwa mujibu wa Aayah, kafiri anaposilimu haamuriwi kuzilipa Swalaah. Na kwa kuwa yeye haamini kwamba ni wajibu, na akafanya kusudi kutoswali na Swalaah zikapita bila ya udhuru, basi hawezi kuzilipa kama utakavyokuja uhakiki wa hilo.”
·
Idadi ya faradhi
Swalaah zilizofaradhishwa mchana na usiku ni tano. Nazo ni Adhuhuri, alasiri, Magharibi, ‘Ishaa na Alfajiri. [Hii ni kwa mujibu wa maneno ya Jamhuri ya Maulamaa. Abu Haniyfah na Maulamaa wa Kihanafi wamesema: “Witr ni wajibu pamoja na Swalaah Tano”. Ufafanuzi wake utakuja].
Ufaradhi wa Swalaah hizi umethibiti kwenye Qur-aan, Sunnah na Ijma’a, nao unajulikana na wote, na anayeupinga ni kafiri. [Al-Badaai-’i (1/91), Al-Fawaakihu Ad-Dawaaniy (1/192), Mughnil Muhtaaj (1/121), na Al-Mughniy (1/370)]
1- Imepokelewa toka kwa Abu Raziyn amesema: “Naafi’i bin Al-Azraq alijibishana na Ibn ‘Abbaas akamuuliza: Je, unazipata Swalaah tano katika Qur-aan?”. Ibn ‘Abbaas akajibu ndio, kisha akamsomea (( فسبحان الله حين تمسون )): Magharibi na ‘Ishaa‘, ((وحين تصبحون)) Alfajiri, ((وعشياً )) Alasiri, ((وحين تُظهرون )), Adhuhuri. [Isnadi yake ni Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Twabariy kwenye “At-Tafsiyr” (20/21), na Ibn Al-Mundhir kwenye “Al-Awsatw” (2/322), na Al-Bayhaqiy kwenye “Al-Kubraa” (1/359) na At-Twabaraaniy kwenye “Al-Kabiyr” (10/304)].
2- Imepokelewa toka kwa Twalha bin ‘Ubaydullaah akisema: “Bedui alikuja kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Nieleze, ni Swalaah zipi ambazo Allaah Amenifaradhia?” Akasema: ((Ni Swalaah Tano mchana na usiku)). Akauliza: “Je, kuna zingine?”. Akasema: ((Hapana, ila za kujitolea za Sunnah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (46) na Muslim (11)].
3- Imepokelewa na Anas bin Maalik akisema: “Swalaah hamsini zilifaradhishwa kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) usiku wa Israa, kisha zikapunguzwa mpaka zikabakia tano, kisha pakanadiwa: “Ee Muhammad! Hakika neno halibadilishwi Kwangu, na wewe utapata hamsini kwa hizi tano”. [Hadiyth Swahiyh: Al-Bukhaariy kaifanyia “ikhraaj” mfano wake (349) na Muslim (162) kwa urefu]
·
Idadi ya rakaa
Ibn Al-Mundhir amesema kwenye Al-Awsatw (2/318):
“Maulamaa wote wanasema kwamba Swalaah ya Adhuhuri ni rakaa nne. Kisomo kwenye Swalaah hii ni cha sauti ya chini, na hukaliwa vikao viwili vya tashahhudi, na kila kimoja kinakuja baada ya rakaa mbili. Idadi ya rakaa za Alasiri ni nne kama Swalaah ya Adhuhuri na kisomo chake ni kwa sauti ya chini, na hukaliwa vikao viwili vya tashahhudi, na kila kimoja kinakuja baada ya rakaa mbili. Idadi ya rakaa za Swalaah ya Magharibi ni tatu. Katika rakaa mbili za mwanzo, kisomo ni kwa sauti ya juu na katika rakaa ya tatu, kinakuwa kwa sauti ya chini. Katika rakaa mbili za mwanzo kuna kikao cha tashahhudi, na katika rakaa ya mwisho pia kuna kikao. Idadi ya rakaa za Swalaah ya isha ni nne. Katika rakaa mbili za mwanzo, kisomo ni kwa sauti ya juu na katika rakaa mbili nyingine, kinakuwa kwa sauti ya chini. Hukaliwa vikao viwili vya tashahhudi, kila kikao katika kila rakaa mbili. Idadi ya rakaa za Swalaah ya Alfajiri ni rakaa mbili. Kisomo ni cha sauti ya juu katika rakaa zote mbili na hukaliwa kikao kimoja tu cha tashahhudi.
Hii ni faradhi kwa mkazi. Ama msafiri, faradhi yake ni rakaa mbili isipokuwa Swalaah ya Magharibi. Ufaradhi wa Swalaah hii kwa msafiri ni sawa na ufaradhi wa mkazi”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
005-Nyakati Za Swalaah
Alhidaaya.com [3]
Waislamu wanakubaliana kwamba Swalaah tano zina nyakati zake ambazo ni lazima ziswaliwe katika nyakati hizo. Asili ya hili ni Kauli Yake Ta’alaa:
((فَإِذَا قَضَيْتُمُ الصَّلَاةَ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِكُمْ ۚ فَإِذَا اطْمَأْنَنتُمْ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ ۚ إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتً))
((Mtakapomaliza Swalaah, mdhukuruni Allaah msimamapo, na mkaapo na mnapolala ubavuni mwenu Mtakapopata utulivu, simamisheni Swalaah (kama desturi), hakika Swalaah kwa Waumini ni fardhi iliyowekwa nyakati maalumu)). [ An Nisaa (4:103) ]
Na ufuatao ni uainisho wa mipaka ya nyakati hizi na ubainisho wa alama zake:
[1] Swalaah Ya Adhuhuri
Adhuhuri ni pale jua linapopindukia upande wa Magharibi toka katikati ya mbingu. Swalaah hii inakuwa ni wajibu wakati wa Adhuhuri unapoingia, nayo huitwa pia vile vile “Al-Uwlaa” kwa kuwa ndiyo Swalaah ya kwanza kabisa ambayo Jibriyl alimswalisha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
[Al-Miswbaahul Muniyr, Al-Majmu’u (3/24) na Al-Mughniy (1/372)]
Huitwa pia “Al-Hajiyrah” kutokana na yaliyopokelewa toka kwa Abu Barzah aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiiswali Al-Hajiyrah wanayoiita Al-Uwlaa wakati jua linapopinduka”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (541)].
Mwanzo wake:
Ni pale jua linapopindukia upande wa Magharibi toka katikati ya mbingu. Maulamaa wote wamekubaliana hilo kutokana na kuthibiti habari toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ya kwamba aliswali Adhuhuri wakati jua lilipopinduka kama ilivyo katika Hadiyth ya Barzah iliyotangulia.
Imepokelewa toka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amri ya kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:
((Wakati wa Adhuhuri ni pale jua linapopinduka na kivuli cha mtu kikawa sawa na kimo chake madhali Alasiri haijaingia. Na wakati wa Alasiri ni kabla ya jua kuwa la kinjano. Na wakati wa Swalaah ya Magharibi ni kabla ya kupotea wekundu, na wakati wa Swalaah ya isha ni mpaka nusu ya usiku. Na wakati wa Swalaah ya Alfajiri, ni kuanzia Alfajiri inapotokea madhali jua halijachomoza, na jua linapochomoza basi usiswali, kwani huchomoza kati ya pembe mbili za shaytwaan)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (612)].
Mwisho wake:
Maulamaa wametofautiana kuhusiana na wakati huu. Kauli sahihi zaidi ni ile isemayo kuwa mwisho wake ni pale urefu wa kivuli cha kitu unapokuwa mfano wa kimo chake bila kuhesabu urefu wake wakati jua linapopinduka. [Kila kitu kinakuwa na kivuli kabla ya Adhuhuri, kisha kivuli hiki hupungua, halafu huanza tena kuongezeka. Na hiki ndicho kivuli cha kupinduka jua na ndio mwanzo wa wakati wa Adhuhuri. Kivuli kikizidi na kupindukia kipimo hiki na kuwa sawa na urefu wa kitu, unakuwa ndio mwisho wa wakati wa Adhuhuri].
Wakati huu unakuwa ndio wakati wa kuingia Alasiri. Hii ndiyo rai yenye nguvu zaidi ya Jamhuri ya Maulamaa. Abu Haniyfah amekwenda kinyume na rai hii. Anasema kuwa mwisho wa Adhuhuri ni pale kivuli cha kitu kinapokuwa mara mbili yake bila kuhesabia urefu wa kivuli wakati jua linapopinduka. [Mawaahibul Jaliyl (1/382), Mughnil Muhtaaj (1/121), Al-Mughniy (1/371), Al-Awsatw (2/327), Badaai’u Asw-Swanaai’i (1/123) na Al-Aswl (1/144)]
Jamhuri ya Maulamaa wametoa dalili kwa haya yafuatayo:
1- Hadiyth ya Ibn ‘Umar iliyotangulia isemayo: “Wakati wa Adhuhuri ni pale jua linapopinduka na kikawa kivuli cha kila mtu kama kimo chake madhali Alasiri haijaingia”.
2- Hadiyth ya Jaabir bin ‘Abdillaah Al-Answaariy isemayo: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka akaswali Adhuhuri wakati jua lilipopinduka, na kivuli kikawa kiasi cha kamba ya kiatu. Halafu aliswali Alasiri wakati kivuli kilipokuwa kiasi cha kamba ya kiatu na kivuli cha mtu. Kisha aliswali Magharibi wakati jua lilipokuchwa. Halafu aliswali ishaa pale wekundu ulipotoweka, kisha akaswali Alfajiri wakati ilipochomoza Alfajiri. Na siku iliyofuatia, aliswali Adhuhuri wakati kivuli kilipokuwa sawa na kimo cha mtu, kisha aliswali Alasiri wakati kivuli cha mtu kilipokuwa mara mbili yake kiasi cha mwendo wa kutoka Al-‘Unuk hadi Dhul Hulayfah kwa mtu aliyepanda mnyama. Halafu aliswali Magharibi wakati jua lilipozama, kisha aliswali ishaa mpaka theluthi ya usiku au nusu ya usiku (shaka ya msimuliaji), halafu aliswali Alfajiri kukipambazuka”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (1/261). Angalia “Al-Irwaa” (1/270)].
Hadiyth hii inachukulika kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimaliza Adhuhuri wakati kivuli cha kila kitu kilipokuwa sawa nacho. Na katika siku ya kwanza, aliianza Alasiri wakati kivuli cha kila kitu kilipokuwa sawa nacho. Na hapa hakuna maingiliano kati ya nyakati mbili. [Naylul Awtwaar (1/374)]
Na hatuwezi kusema kwamba kivuli cha kitu kinapokuwa mfano wake ndio kwamba wakati wa Alasiri umeingia na wakati wa Adhuhuri haujatoka, bali kunabakia baada ya hapo muda wa kiasi cha rakaa nne kinachofaa kuswaliwa Adhuhuri na Alasiri kama walivyosema baadhi yao. [An-Nawawiy ameinasibisha kauli hii kwa Maalik kwenye Sharhu Muslim. Pia ameisimulia toka kwa Maalik katika Bidaayatul Mujtahid (1/125) ambapo pia Ibn Al-Mundhir (2/327) kainasibisha kwake kwamba amesema: “Wakati wa Adhuhuri unatoka” !!]
Tuliyoyaeleza yanatiliwa nguvu na Hadiyth ya Abu Qataadah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika kupoteza wakati ni kwa yule ambaye hakuiswali Swalaah mpaka ukaingia wakati wa Swalaah nyingine)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (595) na Muslim (681) katika Hadiyth ndefu.
·
Faida:
- Wakati wa Adhuhuri unaweza kujulikana kwa njia ya kuhesabu masaa. Ni kuhesabiwa wakati wa baina ya jua linapochomoza mpaka pale linapokuchwa, na wakati wa Adhuhuri utakuwa katikati ya masaa hayo kamili.
- Imesuniwa kuharakisha kuswali Adhuhuri mwanzoni mwa wakati wake kutokana na Hadiyth ya Jaabir bin Samurah aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali Adhuhuri linapopinduka jua kuelekea Magharibi”. Pia Hadiyth ya Abu Barzah iliyotangulia nyuma kidogo.
- Imesuniwa kuichelewesha joto linaposhitadi kutokana na Hadiyth ya Anas aliyesema: “Baridi ilipokuwa inashitadi, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiwahisha Swalaah, na joto linaposhitadi huikawiza”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (618), Abu Daawuud (403) na Ibn Maajah (673)].
Na Hadiyth ya Abu Dharri aliposema: “Tulikuwa safarini pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Mwadhini akataka kuadhini akamwambia: ((Subiri papoe)). Kisha akataka kuadhini akamwambia: ((Subiri papoe)) mara mbili hivi au tatu mpaka tukaona kivuli cha vilima. Halafu akasema: ((Ukali wa joto unatokana na mwako na pumuo la Jahannam, na joto linaposhitadi basi kawisheni Swalaah papoe)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (906), na mfano wake iko kwa Al-Bukhaariy (534) na Muslim (615) toka kwa Jaabir].
Mpaka wa kukawisha Swalaah hadi joto lipungue unatofautiana kwa mujibu wa hali. Cha kuangaliwa ni muda usiachiwe mpaka mwisho wa wakati.
[2] Swalaah Ya Alasiri
Alasiri ni saa za mwisho wa mchana jua linapokuwa jekundu na huitwa “Al-‘Ashiy”. Swalaah ya Alasiri huitwa “Swalaah ya Kati” na inakuwa ni wajibu wakati wake unapoingia.
Mwanzo wake:
Ni pale kivuli cha kitu kinapokuwa mfano wake kwa mujibu wa kauli ya Jamhuri kinyume na rai mashuhuri ya Abu Haniyfah. Yeye ameufanya mwanzo wake ni pale kivuli cha kitu kinapokuwa mara mbili yake!! Hadiyth zilizotangulia kuhusiana na wakati wa Adhuhuri, zinaipa nguvu kauli ya Jamhuri. [Jawaahirul Ikliyl (1/32), Mughnil Muhtaaj (1/121), Al-Mughniy (1/375) na Fat-hul Qadiyr (1/195)]
Mwisho wake:
Udhahiri wa Hadiyth umegongana kuhusiana na mwisho huo. Mgongano huo unaonekana katika:
- Hadiyth ya Jaabir wakati Jibriyl alipomswalisha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Ni kwamba, katika siku ya kwanza, aliswali Alasiri wakati kivuli cha kitu kilipokuwa mfano wake. Na katika siku ya pili, aliswali Alasiri wakati kivuli cha kitu kilipokuwa mara mbili yake. Kisha akasema: “Wakati ni kati ya nyakati hizi mbili”. [Hadiyth Swahiyh: Imeshaelezwa nyuma]
Na haya ndiyo aliyoyasema Ash-Shaafi’iy [lakini hili ni katika wakati wa khiyari] na Maalik katika moja ya riwaya mbili. [Bidaayatul Mujtahid (1/126) na Al-Umm (1/73)]
- Hadiyth Marfu’u ya ‘Abdullaah bin ‘Amri isemayo: ((Wakati wa Alasiri ni kabla ya jua kuwa la kinjano)). [Hadiyth Swahiyh: Imeelezwa nyuma kidogo] Kayasema haya Maalik, Abu Thawr na riwaya toka kwa Maalik. [Bidaayatul Mujtahid (1/126), Al-Mughniy (1/376) na Al-Awsatw (2/331). Kuna kauli sita zilizosimuliwa katika mas’ala haya]
Pia Hadiyth mwenza ya Abu Musa kuhusiana na kisa cha mtu aliyeuliza kuhusu nyakati za Swalaah akituambia: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali Alasiri siku ya kwanza jua likiwa limenyanyuka, na katika siku ya pili mwisho wa Alasiri. Akaondoka baada ya Swalaah huku muulizaji akisema: “Jua limekuwa jekundu”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (614), Abu Daawuud (395) na An-Nasaaiy (1/260)].
- Hadiyth ya Abu Hurayrah ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Mwenye kuipata rakaa ya Alasiri kabla ya jua kuchwa, basi kaipata Alasiri)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (579) na Muslim (163/608)].
Is-Haaq na Ahlu Adh-Dwaahir wakasema: “Mwisho wa wakati wake ni kabla ya kuchwa jua kwa rakaa moja”. [Bidaayatul Mujtahid (1/126), Al-Awsatw (2/332) na Al-Muhalla]
Ninasema: “Kile ambacho dalili za Hadiyth hizi zote na zinginezo zinakutania, ni kuchukuliwa Hadiyth ya Jibriyl kwamba inabainisha wakati wa khiyari, Hadiyth ya Ibn ‘Umar inabainisha wakati wa kujuzu, na Hadiyth ya Abu Hurayrah inabainisha wakati wa udhuru na dharura. Tunasema: Mwisho wa wakati wa khiyari ni kivuli cha kitu kuwa mara mbili yake na huendelea mpaka jua linapokuwa njano, na hukirihishwa kuchelewesha kupindukia muda huo bila ya udhuru kutokana na Hadiyth ya Anas aliyesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Hiyo ni Swalaah ya mnafiki. Hukaa akilichunga jua mpaka linapokuwa kati ya pembe mbili za shaytwan, ndipo hapo husimama akiidonoa nne, na hamdhukuru Allaah isipokuwa kidogo tu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (622), Abu Daawuud (409), At-Tirmidhiy (160) na An-Nasaaiy (1/254)].
Na kama kuna udhuru au dharura, itajuzu kuiswali bila ukaraha kabla jua kuchwa kwa kiasi cha rakaa moja. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
Imesuniwa Kuharakisha Alasiri
1- Kwa Hadiyth ya Anas isemayo: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali Alasiri jua likiwa angavu limenyanyuka. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (550) na Muslim (621)]
Mtu akaenda hadi Al-’Awaaly akarudi na jua bado limenyanyuka”. Al-‘Awaaly ni umbali wa maili nne toka Madiynah.
2- Imepokelewa toka kwa Raafi’i bin Khudayj akisema: “Tulikuwa tukiswali Alasiri pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kisha tukachinja ngamia, tukamgawa mafungu kumi. Halafu tukapika na tukaila nyama yake kabla jua halijakuchwa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (2485) na Muslim (625)].
Pia inasisitiziwa kuiharakisha katika siku yenye mawingu kwa kuwa ni aghalabu watu kutatizikiwa na wakati. Muda ukivutwa, basi wakati unaweza kuponyoka, au jua likawa njano kabla ya Swalaah. Imepokelewa toka kwa Abul Mulayhi akisema: “Tulikuwa pamoja na Buraydah vitani katika siku iliyofunga mawingu akasema: Iwahisheni Swalaah ya Alasiri, kwani Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwenye kuacha Swalaah ya Alasiri, basi amali zake zimepomoka)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (553), An-Nasaaiy (1/83) na Ahmad (5/349)].
Hamasisho La Kuilinda Swalaah Ya Alasiri Na Matahadharisho Ya Kuiacha Katika Qur-aan na Hadiyth.
1- Allaah Anasema:
((حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ))
((Shikamaneni na Swalaah na khaswa Swalaah ya katikati (Alasiri), na simameni mbele ya Allaah katika hali ya utiifu)). [ Al-Baqarah (2:238)]
“Swalat Al-Wustwaa” ni Swalaah ya Alasiri kwa mujibu wa kauli sahihi kutokana na neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliposhughulishwa na makundi: ((Wametushughulisha tukaghafilika na “Swalat Al-Wustwaa: Swalaah ya Alasiri)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (2931) na Muslim (627) na tamko ni lake].
2- Imepokelewa na Abu Buswrah Al-Ghaffaariy (Radhwiya Allaahu Anhu) akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alituswalisha Alasiri huko Al-Makhmasw. Akasema: ((Hakika Swalaah hii ilifaradhishwa kwa waliopita kabla yenu wakaipoteza. Mwenye kuihifadhi, basi atakuwa na malipo mara mbili, na hakuna Swalaah baada yake mpaka nyota ichomoze)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (830)].
3- Imepokelewa toka kwa ‘Ammaarah bin Ru’uyah (Radhwiya Allaahu Anhu) akisema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Hatoingia motoni yeyote aliyeswali kabla ya kuchomoza jua na kuchwa)). Yaani Alfajiri na Alasiri. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (634)].
4- Hadiyth Marfu’u ya Buraydah tuliyoieleza nyuma isemayo: ((Mwenye kuacha Swalaah ya Alasiri, basi amali yake imepomoka)).
Ibn Al-Qayyim amesema: [As-Swalaatu wa Hukmu Taarikihi uk. 43-44]
“Kinachoonekana katika Hadiyth – na Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi muradi wa Rasuli Wake - ni kuwa kuacha ni kwa aina mbili: Ima kuacha kabisa Swalaah, na hili hupomosha amali yote, au kuacha baadhi ya siku, na hili hupomosha amali ya siku hizo tu. Kuporomoka kiujumla ni kwa kuacha kabisa, na kuporomoka kisehemu ni kwa kuacha siku fulani. Ikiwa pataulizwa: Vipi amali zitapomoka bila mtu kuritadi? Itajibiwa kuwa Qur-aan, Sunnah na nukuu toka kwa Maswahaba zinaonyesha kwamba mabaya hupomosha mema kama ambavyo mema huondosha mabaya. Allaah Amesema:
(( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُبْطِلُوا صَدَقَاتِكُم بِالْمَنِّ وَالْأَذَىٰ كَالَّذِي يُنفِقُ مَالَهُ رِئَاءَ النَّاسِ وَلَا يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ صَفْوَانٍ عَلَيْهِ تُرَابٌ فَأَصَابَهُ وَابِلٌ فَتَرَكَهُ صَلْدًا ۖ لَّا يَقْدِرُونَ عَلَىٰ شَيْءٍ مِّمَّا كَسَبُوا ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ ))
((Enyi walioamini! Msibatilishe swadaqah zenu kwa masimbulizi na udhia kama yule ambaye anatoa mali yake kwa kujionyesha kwa watu wala hamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Basi mfano wake ni kama jabali juu yake pana udongo, kisha likapigwa na mvua kubwa ikaliacha tupu. Hawana uwezo juu ya lolote katika waliyoyachuma. Na Allaah Haongoi watu makafiri)). [Al-Baqarah (2:264)]
Na Anasema:
((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَرْفَعُوا أَصْوَاتَكُمْ فَوْقَ صَوْتِ النَّبِيِّ وَلَا تَجْهَرُوا لَهُ بِالْقَوْلِ كَجَهْرِ بَعْضِكُمْ لِبَعْضٍ أَن تَحْبَطَأَعْمَالُكُمْ وَأَنتُمْ لَا تَشْعُرُونَ))
((Enyi walioamini! Msipandishe sauti zenu juu ya sauti ya Nabiy, na wala msiseme naye kwa sauti ya juu, kama mnavyosemezana wenyewe kwa wenyewe kwa sauti za juu; zisije zikaporomoka ‘amali zenu nanyi hamhisi)). [Al-Hujuraat (49:2)]
Ninasema: “Hili ni kwa yule aliyeitelekeza kabisa na kupuuzilia mbali fadhila ya wakati wake naye ana uwezo wa kuiswali. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi”.
5- Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu Anhumaa) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Anayepitwa na Swalaah ya Alasiri, ni kama aliyepokonywa ahli wake na mali yake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (552) na Muslim (626/200)].Yaani ni kama vile amebakia pweke bila mali wala ahli. Na hii ni taswira ya kupomoka amali kwa sababu ya kuiacha kwa namna tuliyoielezea. [As-Swalaat cha Ibn Al-Qayyim (44)]
Au inaweza kusemwa: Mtu atahadhari isimpite kama anavyotahadhari kupotea ahli zake na mali yake.
[3] Swalaah Ya Magharibi
Neno “Al-Maghrib” lina maana ya wakati jua linapokuchwa, au sehemu linapokuchwia, au Swalaah inayoswaliwa wakati huu. [Al-Miswbaahul Muniyr na Kash-Shaaful Qinaa (1/253)]
Al-Maghrib huitwa pia vile vile Al-’Ishaa, lakini hili ni makruhu kutokana na kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama ilivyo katika Swahiyh Mbili:
((Angalieni Mabedui wasiwazidini nguvu juu ya jina la Swalaah yenu ya Magharibi)). Mabedui huiita ‘Ishaa.
Mwanzo wake:
Ni pale jua linapokuchwa, likapotea na machweo yakakamilika kwa mujibu wa Ijma’a ya Maulamaa. Hili huonekana wazi kwenye majangwa, na hujulikana kwenye miji kwa kutoweka mwangaza juu ya vilele vya milima, na giza kuanza kutanda toka mashariki na kuchomoza nyota. [Al-Badaai’u (1/123), Al-Mughniy (1/381), na Naylul Awtwaar (2/5,6)]
Mwisho wake:
Maulamaa wamehitalifiana juu ya kauli mbili:
Ya kwanza: Magharibi ina wakati mmoja tu baada ya kuchwa jua kwa kiasi cha mtu kutawadha, kujisitiri, kuadhini na kuqimu. Hii ni rai ya Maalik, Al-Awzaa’iy na Ash-Shaafi’iy. [Bidaayatul Mujtahid (10/126), Al-Majmu’u (3/28) na Al-Awsatw (2/335)]
Hoja yao ni Hadiyth iliyotangulia ya Jibriyl kumswalisha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambapo katika siku ya kwanza na ya pili, aliswali Magharibi wakati mmoja pale jua lilipokuchwa. Pia yaliyosimuliwa na Suwayd bin Ghafalah anayesema kwamba amemsikia ‘Umar bin Al-Khattwaab akisema: “Swalini Swalaah hii nailhali njia zina mwanga, yaani Magharibi”. [Isnadi yake ni Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdul Razzaaq (2092) na Ibn Abu Shaybah (1/329)]
Ya pili: Mwisho wake ni kutoweka wekundu. Ni kauli ya Ath-Thawriy, Ahmad, Is-Haaq, Abu Thawr, Abu Haniyfah na Mafuqahaa wa Kihanafi, na baadhi ya Mafuqahaa wa Kishaafii. An-Nawawiy kaikubali na Ibn Al-Mundhir kaikhitari. [Bidaayatul Mujtahid (1/127), Al-Majmu’u (3/28) na Al-Awsatw (2/337)]
Ni kauli sahihi, na dalili juu ya usahihi wake ni:
1- Hadiyth Marfu’u ya Ibn ‘Amri: ((Na wakati wa Swalaah ya Magharibi ni kabla ya kupotea wekundu)).
2- Hadiyth ya Abu Muusa kuhusu mtu aliyeuliza nyakati za Swalaah isemayo: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali Magharibi siku ya kwanza wakati jua lilipokuchwa, na siku ya pili mwishoni mwa Magharibi mpaka wekundu ulikuwa unakurubia kuondoka”. Tushaitaja nyuma kama ilivyo Hadiyth ya Buraydah. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (613), At-Tirmidhiy (152), na An-Nasaaiy (1/337)].
3-Hadiyth ya Zayd bin Thaabit kwamba alimwambia Marwaan: “Vipi wewe unasoma katika Swalaah ya Magharibi Suwrah ndogo za Aayah fupi fupi?! Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisoma Suwrah ndefu zaidi ya Suwrah mbili ndefu”. Yaani Al-A’araaf. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (764), An Nasaaiy (2/170) na Ahmad (5/188)].
Na kisomo cha Swalaah ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kilikuwa bayana, herufi kwa herufi na tartiyl pamoja na utulivu katika rukuu na sijdah. Na hii inaonyesha kwamba wakati wa Magharibi unaendelea mpaka wekundu unapopotea.
4- Hadiyth ya Anas (Radhwiya Allaahu Anhu) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Chajio kikitengwa, basi anzeni kula kabla ya Swalaah ya Magharibi, na wala msiharakishe Swalaah mkaacha mlo wenu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (672) na Muslim (557)].
Na katika tamshi la Hadiyth ya ‘Aaishah: ((Swalaah ikiqimiwa na chajio kikatengwa, basi anzeni kwanza kula)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (671)].
Hadiyth iko wazi kwamba inajuzu kuichelewesha Swalaah ya Magharibi mpaka baada ya kula baada ya kuingia wakati wake.
5- Hadiyth ya Mu’aadh isemayo kwamba alikuwa akiswali pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Magharibi, kisha hurejea kwa watu wake akawaswalisha. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (711) na Muslim (465)].
Imesuniwa Kuiharakisha
1- Imepokelewa toka kwa Raafi’i bin Khudayj akisema: “Tulikuwa tunaswali Magharibi pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na mmoja wetu anapoondoka, anaweza kuona sehemu ya kuangukia mshale wake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (559) na Muslim (637)].
2- Imepokelewa toka kwa ‘Uqbah bin ‘Aamir (Radhwiya Allaahu Anhu) akisema kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Umma wangu hautaacha kuwa juu ya kheri – au juu ya Uislamu- madhali hawakuichelewesha Magharibi mpaka nyota zikaingiliana)). [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (414) na Ahmad (4/147)]
[4] Swalaah Ya ‘Ishaa
‘Ishaa ni pale giza linapoingia kuanzia Magharibi hadi linaposhitadi “atamah”. Swalaah ya ‘Isha imeitwa hivi kwa vile huswaliwa katika wakati huu. Pia huitwa “‘Ishaa ya mwisho” kama alivyosema Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Mwanamke yeyote aliyejifukiza manukato, basi asitoke kuswali nasi ‘Ishaa ya mwisho)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (444), Abu Daawuud (4175) na An-Nasaaiy (5128)].
Huitwa pia vile vile “Atamah” kama anavyosema Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Lau wangelijua yaliyomo katika ‘Atamah na Alfajiri, basi wangeziendea hata kwa kutambaa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (615,721) na Muslim (437)].
Lakini kuitwa kwa jina hilo kumeelezewa kuwa ni makruhu katika Hadiyth ya Ibn ‘Umar anayesema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
((Angalieni sana mabedui wasije kuwazidieni nguvu katika jina la Swalaah yenu. Jueni kwamba inaitwa ‘Ishaa, nao huichelewesha mpaka giza linaposhitadi ili kukama ngamia)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (228), An-Nasaaiy (1/270) na Ibn Maajah (705)].
Kuiita ‘Ishaa “atamah” ni kinyume cha ubora kwa mujibu wa Hadiyth hii kama wanavyoona hivi akina Maalik na Ash-Shaafi’iy na kukhitariwa na Ibn Al-Mundhir. Ibn Hajar katilia nguvu.
Mwanzo wake:
Maulamaa wote (isipokuwa wachache mno) wanasema kwamba mwanzo wa wakati wa ‘Ishaa ni pale unapopotea wekundu. Lakini wamehitilafiana kuhusu maana ya neno “Ash-Shafaq”. [Angalia Al-Awsatw (2/339-342) na Al-Majmu’u (3/44-45)]
Jamhuri wanasema maana yake ni wekundu, lakini Abu Haniyfah na Al-Awzaa’iy wanasema ni weupe baada ya wekundu.
Ninasema: “Maana ya kwanza ndio sawa, kwa kuwa lililothibiti ni kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali wakati wekundu ulipotoweka. Mtaalamu wa taaluma ya mapambazuko na machweo anajua kwamba weupe haupotei isipokuwa katika theluthi ya kwanza ya usiku. [Ukweli huu umenukuliwa katika Naylul Awtwaar (2/16) toka kwa Ibn Sayyidi An Naas katika Sharh At-Tirmidhiy. Kisha ninamwona Ibn Rushd katika Bidaayatul Mujtahid (1/127) akiukadhibisha]
Na imethibiti katika Hadiyth ya ‘Aaishah kwamba wao walikuwa wakiswali baina ya pale wekundu unapopotea mpaka theluthi ya kwanza ya usiku.” [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (569) na Muslim (218)]
Mwisho wake:
Maulamaa wamehitilafiana kuhusu hili katika kauli tatu mashuhuri:
Ya kwanza: Ni mpaka mwisho wa usiku. Ni kauli ya Ash-Shaafi’iy katika madhehebu mapya [isipokuwa hili kwake ni wakati wa khiyari. Na kwenye Al-Ummu ameeleza kwamba theluthi inapopita, basi Swalaah nayo imepita]. Pia wamelisema hili Abu Haniyfah na Maalik. [Al-Awsatw (2/343), Al-Ummu (1/74), Bidaayatul Mujtahid (1/128) na Al-Majmu’u ( 3/42)]
Dalili yao ni Hadiyth ya Jibriyl kumswalisha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Inasema kwamba katika siku ya pili, aliiswali na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika theluthi ya usiku.
Ya pili: Ni mwisho wa nusu ya usiku. Waliosema hivi ni Ath-Thawriy, Ibn Al-Mubaarak, Is-Haaq, Abu Thawr, Aswhaab Ar Ra-ay na Ash-Shaafi’iy katika madhehebu yake ya zamani. [Isipokuwa Aswhaab Ar Ra-ay wanasema kwamba inatosheleza baada yake pamoja na ukaraha. Ama Ash-Shaafi’iy, yeye anaona kwamba ni wakati wa khiyari, na Swalaah haimpiti mtu mpaka Alfajiri]. Pia Ibn Hazm kasema hivi.
Dalili yao ni Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Amri iliyotajwa mara nyingi isemayo: “Wakati wa ‘Ishaa ni mpaka nusu ya kati ya usiku”, pamoja na Hadiyth ya Anas isemayo: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliikawiza Swalaah ya ‘Ishaa mpaka nusu ya usiku”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (572)].
Aidha, ‘Umar bin Al-Khattwaab alimwandikia Abu Musa Al-Ash’ariy akimwambia: “Na uswali ‘Ishaa katika wakati wa baina yako na kati ya theluthi ya usiku, na kama utaichelewesha, basi hadi nusu ya usiku, na wala usiwe katika wenye kughafilika”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Maalik, At-Twahaawiy na Ibn Hazm kwa Sanad Swahiyh kama ilivyo kwenye Tamaam Al-Minnah (uk. 142)].
Ya tatu: Mwisho wake ni kuchomoza Alfajiri ya kweli (walau bila ya dharura). Waliosema hivi ni ‘Atwaa, Twaawus, ‘Ikrimah na Daawuud Adh-Dwaahiriy. Nayo imesimuliwa toka kwa Ibn ‘Abbaas na Abu Hurayrah. Ibn Al-Mundhir ameikhitari. [Al-Awsatw (2/346) na Bidaayatul Mujtahid (1/128)]
Dalili yao ni:
1- Hadiyth Marfu’u ya Qataadah: ((Hakika kupoteza wakati ni kwa yule ambaye hakuiswali Swalaah mpaka ukaingia wakati wa Swalaah nyingine)). [Hadiyth Swahiyh: Imeshatajwa nyuma].
2- Kauli ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Lau kama si kuuchelea umma wangu uzito, ningeliichelewesha ‘Ishaa mpaka nusu ya usiku)). [Hadiyth Swahiyh: Itakuja muda si mrefu].
Wanasema: “Hii ni dalili ya kwamba hakuna ubaya kwa aliyeichelewesha hadi nusu ya usiku. Na kama Rasuli angeliichelewesha kisha akatoka kwenda kuwaswalisha baada ya nusu ya usiku, basi Swalaah ingelikuwa ni baada ya sehemu ya nusu ya usiku. Na ikiwa ni hivyo, basi inathibiti kwamba wakati wake ni mpaka Alfajiri inapotoka”. [Al-Awsatw cha Ibn Al-Mundhir (2/346)]
3- Hadiyth ya ‘Aaishah: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alichelewa usiku ule mpaka sehemu kubwa ya usiku ikapita na watu Msikitini wakalala. Halafu alitoka akaswali, kisha akasema: ((Hakika huu ndio wakati wake lau kama si kuuchelea umma wangu uzito)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (219) na An-Nasaaiy (1/267)].
Hadiyth Yenye Uzito Zaidi
Hadiyth yenye nguvu zaidi kati ya Hadiyth zilizotangulia ambayo ina ainisha mwisho wa Swalaah ya ‘Ishaa, ni Hadiyth ya ‘Abdullah bin ‘Amri isemayo: ”Wakati wa ‘Ishaa ni mpaka nusu ya kati ya usiku”. Ash-Shawkaaniy kaipa uzito lakini kaufanya mwisho wa wakati wa khiyari. Ama wakati wa kujuzu, huu unaendelea mpaka Alfajiri kwa kuitegemea Hadiyth iliyotangulia ya Qataadah isemayo: “Kiilivyo ni kuwa wakati wa kila Swalaah huendelea mpaka unapoingia wakati wa Swalaah nyingine isipokuwa Swalaah ya Alfajiri, Swalaah hii ina hali pekee toka kwenye ujumuishi huu kwa Ijma’a”.
Ninasema: [Nimefaidika hapa kwa maneno ya Al-‘Allaamah Al-Albaaniy kwenye Tamaam Al-Minnah (uk. 141). Maana yake imenukuliwa toka kwa Ibn Hazm (3/178)]
“Ama kutolea dalili kwa Hadiyth ya Qataadah ya kwamba wakati wa ‘Ishaa unaendelea mpaka kuchomoza Alfajiri, hapa pana neno. Kwa kuwa Hadiyth haibainishi nyakati za Swalaah, na wala haikuja kwa ajili ya hilo, bali imekuja kwa ajili ya kubainisha madhambi ya mwenye kuichelewesha Swalaah kwa makusudi mpaka wakati wake ukatoka, sawasawa ikiwa inafuatiliwa na Swalaah nyingine kama Alasiri pamoja na Magharibi, au haifuatiwi kama Alfajiri na Adhuhuri. Linaloonyesha hilo ni kuwa Hadiyth imekuja kwa ajili ya Swalaah ya Alfajiri wakati ilipompita Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na Maswahaba wake wakiwa wamelala safarini. Maswahaba wakahisi vibaya mno kutokea hilo kwao, na hapo Rasuli akaisema Hadiyth hiyo. Na lau kama makusudio ni hayo waliyoyasema ya kuwa wakati wa kila Swalaah unaendelea mpaka unapoingia wakati wa Swalaah nyingine, basi maneno yangelibainisha wazi kwamba wakati wa Alfajiri unaendelea mpaka wakati wa Adhuhuri, lakini wao hawasemi hivyo. Na kwa ajili hiyo, wamelazimika kuivua Swalaah ya Alfajiri na kuiweka kando. Na uvuaji huu juu ya tuliyoyabainisha kutokana na sababu ya Hadiyth, unakuja kuibatilisha, kwa kuwa Hadiyth imekuja kuhusiana na Swalaah ya Alfajiri tu. Basi vipi iwezekane kuivua Swalaah hii?! Kiukweli ni kuwa Hadiyth haikuja kwa ajili ya kuainisha, bali kwa ajili ya kukataza kuitoa Swalaah nje ya wakati wake kiujumla”.
Ninasema tena: “Ama Hadiyth ya ‘Aaishah isemayo: “Mpaka sehemu kubwa ya usiku ikapita”, makusudio yake hapa si sehemu kubwa sana. Ni lazima tuifanye taawili hii kutokana na neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Hakika huu ndio wakati wake)). Na haijuzu makusudio ya kauli hii yawe ni baada ya nusu ya usiku, kwa kuwa hakuna Mwanachuoni yeyote aliyesema kwamba ni bora kuichelewesha hadi baada ya nusu ya usiku. [Sharhu Muslim cha An-Nawawiy]
[Na haibakii kwa wanaosema kwamba wakati wa ‘Ishaa unaendelea mpaka Alfajiri (sawasawa kwa khiyari au kwa lazima) isipokuwa Hadiyth ya Anas asemaye: “ Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliichelewesha Swalaah ya ‘Ishaa mpaka nusu ya usiku, kisha akaiswali..” [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (572)]
Ikiwa itaswihi kuchukulia kwamba alimaliza kuiswali nusu ya usiku, basi neno lake “kisha akaiswali” linakuwa ni la wapokezi wao wenyewe, na kama si hivyo, neno linakuwa ni neno lao. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
Imesuniwa Kuichelewesha ‘Ishaa
Kuna Hadiyth nyingi Swahiyh zilizozungumzia kuhusu kuichelewesha ‘Ishaa. Hili ndilo linalofuatwa na Maulamaa wengi katika Maswahaba na Taabi’iyna. [Tabyinul Haqiyqah cha Az-Zayla’iy]
Kati ya Hadiyth hizo ni kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Lau kama si kuuchelea umma wangu uzito, ningeliwaamuru waicheleweshe ‘Ishaa mpaka theluthi ya usiku au nusu yake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (167), Ibn Maajah (691) na Ahmad (2/245)]
Hikma yake ni kuwa wakati huu una faida zaidi kwa kuwa akili ya mtu haishughulishwi na mambo yenye kumsahaulisha kumdhukuru Allaah Ta’alaa, na pia hukata gumzo la usiku. Lakini hata hivyo, kuichelewesha huenda kukapelekea kuipunguza jamaa na kuwakimbiza watu. Na kwa ajili hiyo, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaichelewesha wakati, na wakati mwingine anaiharakisha, yaani akiwaona watu wamekusanyika huikarakisha, na akiwaona wamekawia huichelewesha. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (560) na Muslim (233) toka Hadiyth ya Jaabir].
Ni Karaha Kulala Kabla Yake Na Kupiga Gumzo Baada Yake
Ni kwa Hadiyth ya Abu Barzah isemayo kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akichukia kulala kabla ya ‘Ishaa, na kuzungumza baada yake. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (568) na Muslim (237)].
Sababu ya ukaraha wa kulala kabla ya Swalaah ya ‘Ishaa ni kuchelea kupitiwa na usingizi wakati wake ukatoka, au likawafungulia watu mlango wakashindwa kuiswali kwa jamaa. [Tabyinul Haqaaiq (1/84), Al-Fawaaqihu Ad Dawaaniy (1/197) na Naylul Awtwaar (2/18)]
Ama ukaraha wa kuzungumza baada yake, ni kuwa hilo linaweza kuwafanya watu wakeshe halafu wakapitwa na Alfajiri, au ili wasije kuzungumza maneno yasiyo na faida ambayo si vizuri mtu kuyamalizia kwayo siku yake, au kwa kuwa mtu anaweza kupitwa na ‘ibaadah za usiku. Swalaah inatakikana iwe ndiyo amali bora anayoimalizia kwayo mtu amali zake, na usingizi ni nduguye mauti, na mtu huenda akafia usingizini. [As-Saabiq, Al-Majmu’u (3/42) na Mughnil Muhtaaj]
Lakini hii ikiwa mazungumzo yenyewe hayana umuhimu. Ikiwa yana umuhimu wa kidini kwa wote au kwa mtu binafsi, au yana faida kwa mtu au maslaha kwa Waislamu, basi hakuna ubaya. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikesha pamoja na Abu Bakr na ‘Umar kwa ajili ya jambo kati ya mambo ya Waislamu. [Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (169) na Ahmad (1/26). Ina mkatiko, na pia Hadiyth wenza].
Na katika Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas ni kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alizungumza na mkewe Maymounah saa moja, kisha akalala. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (190)].
[5] Swalaah Ya Alfajiri
Asili ya Alfajiri ni “Ash-Shafaq” yenye maana ya mwanga wa asubuhi. Alfajiri mwishoni mwa usiku, ni kama “Ash-Shafaq” mwanzoni mwake.
Alfajiri ziko za aina mbili: [Al-Badaai-’i (1/122), Mughnil Muhtaaj (1/124), Al-Fawaakih (1/192) na Kash-Shaaful Qinaa (1/255)]
Alfajiri ya kwanza (ya bandia), nao ni weupe wa kimstatili unaoonekana kutoka sehemu ya mbingu, kisha hutoweka na kufuatiliwa na kiza. Weupe huu unajulikana kwa Waarabu kama “Mkia wa mbwa mwitu”.
Alfajiri ya pili (ya kweli), nao ni weupe kinza wenye kusambaa upeoni, na nuru yake huzidi kuongezeka mpaka jua linapochomoza. Katika Hadiyth Rasuli anasema:
((Angalieni isiwazuieni daku yenu adhana ya Bilaal wala Alfajiri ya kimstatili, lakini Alfajiri yenye kusambaa upeoni)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (1094), At-Tirmidhiy (706) na tamko ni lake, Abu Daawuud (2346), An-Nasaaiy (2171) na wengineo].
Alfajiri hii ya pili ndiyo inayofungamana na hukmu zote, si ya kwanza ya bandia. Na Alfajiri huitwa Swalaah ya Alfajiri kwa kuwa huswaliwa katika wakati huu, na pia huitwa “Swalaatus Subh” na Swalaatul Ghadaat”.
Mwanzo wake: Maulamaa wote wanakubaliana kwamba mwanzo wa wakati wa Alfajiri ni kuchomoza Alfajiri ya kweli.
Mwisho wake: Na wote wanakubaliana kwamba mwisho wake ni kuchomoza jua.
Imesuniwa Kuiharakisha:
Jamhuri ya Maulamaa akiwemo Maalik, Ash-Shaafi’iy, Ahmad, Is-Haaq, na Abu Thawr, wanaona kwamba kuiswali Alfajiri wakati giza bado liko ni bora zaidi kuliko kuiswali jua likianza kuwa la kinjano. [Al-Mudawwanah (1/56), Al-Awsatw (2/377), Mughnil Muhtaaj (1/125), Al-Mughniy (1/394) na Sharhus Sunnah cha Al Baghawiy (1/197)]
Hili limesimuliwa toka kwa Makhalifa wanne pamoja na Ibn Mas-’oud. Hoja yao ni:
(a) Kwamba habari zinaeleza kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali Alfajiri giza likiwa bado lingaliko. Kati ya hizo ni:
1- Hadiyth ya ‘Aaishah anayesema: “Wanawake Waumini walikuwa wakihudhuria pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Swalaah ya Alfajiri wakijifunika mitandio (murutw) yao, kisha hurejea majumbani mwao wanapomaliza Swalaah. Hakuna anayewatambua kutokana na kiza kilichochanganyika na mwanga”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (578) na Muslim (230)]
2- Hadiyth ya Abu Barazah Al-Aslamiy asemaye: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaswali Alfajiri, kisha huondoka, na mtu kati yetu hamjui aliyekaa naye, na alikuwa akisoma Aayah sitini hadi mia”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (541) na Muslim (1097)].
3- Hadiyth ya Anas toka kwa Zayd bin Thaabit asemaye: “Tulikula daku pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kisha tukaenda kuswali. Nikauliza: “Kulikuwa na muda gani kati ya daku na Swalaah?” Akasema: “Kiasi cha Aayah 50”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (576) na Muslim (47)].
Muda wa kati ya kumaliza daku na kuingia kwenye Swalaah ambayo ni kiasi cha Aayah khamsini, ni kiasi cha wudhuu. Na hili linatuhisisha kwamba aliiswali mwanzoni mwa wakati wa Alfajiri.
4- Hadiyth ya Abu Mas-’oud Al-Answaariy asemaye: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali Alfajiri mara moja giza likiwa limechanganyika na mwanga, kisha akaswali mara nyingine jua likiwa njano. Kisha baada ya hapo, Swalaah yake ilikuwa ni wakati giza likiwa limechanganyika na mwanga mpaka alipofariki. Hakuswali tena jua likiwa njano”. [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (394). Asili yake ni kwenye Swahiyh Mbili bila neno “Kisha baada ya hapo, Swalaah yake ilikuwa…”.]
(b) Kwamba kuiswali mapema kunaingia ndani ya wigo wa ujumuishi wa Hadiyth zenye kupendezeshea kuharakia kuiswali Swalaah mwanzoni mwa wakati wake. Baadhi yake zitakuja karibuni.
(c) Kuiharakia ni kitendo cha Makhalifa Waongofu (Radhwiya Allaahu Anhum). [Angalia athar zilizopokelewa toka kwao katika Al-Awsatw cha Ibn Al-Mundhir (2/374 na yanayofuatia). Kuswali jua likiwa njano kumesimuliwa pia toka kwa ‘Aliy na ‘Uthmaan]
(d) Kwamba baadhi ya Maulamaa kama Ash-Shaafi’iy na Ahmad wanaichukulia maana ya jua kuwa njano juu ya uhakika wa kuchomoza Alfajiri na kuthibiti kwake. Na kwa vile unjano wa jua unabeba maana mbili, Hadiyth zilizothibiti toka kwa Rasuli ambazo hazibebi isipokuwa maana moja tu, zinakuwa ni bora zaidi.
Ath-Thawriy, Abu Haniyfah na Mafuqahaa wa Kihanafi, wanaona kwamba kuswali jua likiwa linjano ni bora zaidi. [Tabyinul Haqaaiq cha Az Zayla’iy (1/82), Sharhu Ma’anil Aathaar (1/184) na Al-Awsatw (2/377)]
Wametoa hoja kwa haya yafuatayo:
1- Hadiyth ya Raafi’i bin Khudayj isemayo: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Swalini Alfajiri jua likiwa njano, kwani hilo lina thawabu kubwa zaidi)). [Hadiyth Swahiyh Lighayrih: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (424), At-Tirmidhiy (154), An-Nasaaiy (1/272) na Ibn Maajah (672)].
Ibn Hibaan ameijibu hoja hii akisema: “Makusudio ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa neno lake: “Jua likiwa njano” ni katika masiku ya mbalamwezi ambapo weupe wa kuchomoza Alfajiri haubainiki, ili mtu asiswali Swalaah ya Alfajiri mpaka baada ya kupata uhakika wa kuchomoza Alfajiri kwa unjano wa jua. Kwani ikiwa Swalaah itaswaliwa kama tulivyoelezea, inakuwa na malipo makubwa zaidi kuliko kuswaliwa bila ya uhakika wa kuchomoza Alfajiri”. [Swahiyh Ibn Hibaan (4/359-Al-Ihsaan)]
2- Hadiyth ya Ibn Mas-’oud kuhusiana na Swalaah ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) huko Muzdalifah isemayo: “Na aliswali Alfajiri siku hiyo kabla ya wakati wake [giza likiwa limechanganyika na mwanga]..”. Wanasema: “Wamezingatia kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali Alfajiri giza likiwa limechanganyika na mwanga kabla ya wakati wake ambao Ibn Mas-’oud anaujua, hivyo wakati wake aliouzoea ni jua linapokuwa njano”.
Ninasema: “Hili haliko wazi kwa upande wa dalili, kwani kuswali kwake Rasuli Alfajiri giza likiwa limechanganyika na mwanga kabla ya muda wake uliozoeleka, hakupingani na kuwa lililozoeleka pia ni kuswali giza likiwa limechanganyika na mwanga”.
Atw-Twahaawiy (Rahimahul Laahu) ambaye ni Mhanafi, amejaribu kuoanisha kati ya dalili za kuswali giza likiwa limechanganyika na mwanga, na kati ya kuswali jua likiwa la njano. Anasema kuwa mtu anaingia kwenye Swalaah mapema, kisha hurefusha kisomo mpaka akaimaliza jua likiwa limeshakuwa njano. [Sharhu Ma’anil Aathaar (1/184)]
Ninasema: “Huu ni mwoanisho mzuri. Lakini unatilia nguvu mwelekeo wa Jamhuri ya Maulamaa wa kufadhilisha kuiharakia Swalaah wakati giza likiwa bado limechanganyika na mwanga, kwa kuwa mzozano ni kuhusu wakati wa kuingia kwenye Swalaah, na si wakati wa kuimaliza. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
006-Masuala Yanayohusiana Na Nyakati Za Swalaah
Alhidaaya.com [3]
[1] Wakati Ni Faradhi Muhimu Sana Kati Ya Faradhi Za Swalaah
- Kuiswali Swalaah katika wakati wake ni faradhi. Wakati ni faradhi muhimu zaidi kati ya faradhi za Swalaah. Allaah Ta’alaa Anasema:
((فَإِذَا قَضَيْتُمُ الصَّلَاةَ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِكُمْ ۚ فَإِذَا اطْمَأْنَنتُمْ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ ۚ إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا ))
((Mtakapomaliza Swalaah, mdhukuruni Allaah msimamapo, na mkaapo na mnapolala ubavuni mwenu Mtakapopata utulivu, simamisheni Swalaah (kama desturi), hakika Swalaah kwa Waumini ni fardhi iliyowekwa nyakati maalumu)).
[An-Nisaa (4:103)]
Na kwa ajili hii, haijuzu kuichelewesha Swalaah mpaka wakati wake ukapita hata kama mtu ana janaba, au hadathi, au najsi nguoni, au hata kama hana cha kujisitiria uchi, au kwa dharura nyingineyo. Mtu (kulingana na rai sahihi) ataswali wakati huo kwa mujibu wa hali ilivyo. [Ibn Taymiyah kalikhitari hili katika Al-Fataawaa (22/30) na akalinasibisha kwa Jamhuri ya Maulamaa. Angalia Al-Furu’u (1/293), Al-Ummu (1/79) na Al-Majmu’u (1/182)]
- Allaah Ta’alaa Amewasifu wenye kuzihifadhi nyakati za Swalaah Akisema:
((الَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ دَائِمُون))
((Ambao wenye kudumisha Swalaah zao)). [Al-Ma’aarij (70:23)]
((وَالَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُون))
(( Na ambao kwenye Swalaah zao ni wenye kuhifadhi)). [Al-Ma’aarij (70:23)]
Ibn Mas-’oud kasema: “Hilo ni katika nyakati zake”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Al-Mundhir katika Al-Awsatw (2/386) na At-Twabaraaniy kama ilivyo katika Al-Majma’a (7/129)].
Allaah Ta’alaa Amekufanya kuiswali Swalaah katika wakati wake ni katika amali bora zaidi na zinazopendeza zaidi Kwake. Imepokelewa na Ibn Mas-’oud (Radhwiya Allaahu Anhu) akisema: “Nilimuuliza Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): Ni amali ipi inayopendeza zaidi kwa Allaah? (Katika riwaya nyingine: Iliyo bora zaidi) Akasema: ((Ni Swalaah katika wakati wake)). Nikauliza: Kisha ipi? Akasema: ((Kuwatendea wema wazazi wawili)). Nikauliza: Kisha ipi? Akasema: ((Ni Jihaad katika Njia ya Allaah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (527) na Muslim (85)].
- Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametahadharisha kuwatii viongozi katika suala la kuichelewesha Swalaah (ukapita wakati wake wa khiyari). Imepokelewa na Abu Dharri akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia: ((Utafanya nini ikiwa viongozi wako wanaichelewesha Swalaah na wakati wake?)) Nikamwambia: Unaniamuru nini? Akasema: ((Iswali Swalaah katika wakati wake, na kama utaipata pamoja nao basi swali nao, nayo kwako itakuwa Sunnah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (648) na At-Tirmidhiy (176). Angalia Taadhiymu Qadri As-Swalaat (1007) nilichokifanyia uhakiki].
- Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu Anhu amebainisha kwamba kuichelewesha Swalaah ukapita wakati wake wa khiyari (bila ya udhuru) kunakwenda kinyume na Hidaayah ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kunaipoteza Swalaah. Imepokelewa toka kwa Az-Zuhriy akisema: “Niliingia kwa Anas bin Maalik huko Damascus nikamkuta analia. Nikamuuliza: “Nini kinachokuliza?” Akasema: “Sikijui kitu katika nilivyovipata (katika enzi ya Rasuli) isipokuwa Swalaah hii, na Swalaah hii hakika imepotezwa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (530)].
Ninasema: “Ni stahikivu mno kwa mtu mwenye kujithamini, awe anachunga nyakati za Swalaah kwa kuziswali mwanzo wa nyakati zake (isipokuwa Swalaah ya “Ishaa kama hakuna uzito) kwa kutekeleza Kauli Yake Ta’alaa:
(( وَلِكُلٍّ وِجْهَةٌ هُوَ مُوَلِّيهَا ۖ فَاسْتَبِقُوا الْخَيْرَاتِ ۚ أَيْنَ مَا تَكُونُوا يَأْتِ بِكُمُ اللَّـهُ جَمِيعًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ))
(( Na kila mmoja ana upande wa kuuelekea. Basi shindaneni kwenye mambo ya khayr. Popote mtakapokuwa Allaah Atakuleteni nyote pamoja (Qiyaamah). Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Muweza)). [Al-Baqarah (2:148)]
((أُولَـٰئِكَ يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَهُمْ لَهَا سَابِقُونَ))
(( Hao wanakimbilia katika mambo ya kheri; na wao ndio wenye kuyatanguliza)). [Al-Muuminuwn (23:61)]
Na kwa ajili pia ya kuifuata Sunnah ya Rasuli wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Wallaahu Al-Musta’anu”.
[2] Ni Kwa Nguzo Gani Mtu Huipata Swalaah Katika Wakati Wake?
Maulamaa wana kauli mbili kuhusiana na suala hili:
Ya kwanza:
Huipata kwa takbiyr ya kuhirimia. Hii ni rai yenye nguvu ya Abu Haniyfah, Ash-Shaafi’iy na Ahmad. [Al-Majmu’u (3/49), Al-Awsatw (2/348), na Al-Ikliyl (1/304)]
Hoja yao ni:
1- Kuipata sehemu ya Swalaah (nayo ni takbiyr ya kuhirimia) ni kama kuipata yote kwa kuwa Swalaah haigawanyiki. [Al-Mubdi’i (1/353). Lakini kwa mujibu wa Abu Haniyfah, Swalaah yake inabatilika kama jua litachomoza hata kama imebakia rakaa moja katika Swalaah ya Alfajiri!! Na hii ni kinyume na dalili]
2- Hadiyth ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu Anha) isemayo: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwenye kuipata sijdah katika Alasiri kabla jua halijazama, au Alfajiri kabla jua halijachomoza, basi ameipata Swalaah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (609) na Ahmad (6/78)].
Wamesema: “Sijdah ni sehemu ya Swalaah, nayo ni sawa kabisa na takbiyr ya kuhirimia”.
Ya pili:
Huipata kwa kuipata rakaa kamili iliyo ndani ya wakati. Ni rai ya Maalik na riwaya toka kwa Ahmad. Sheikh wa Uislamu ameikhitari, nayo ndiyo yenye nguvu zaidi kutokana na haya yafuatayo: [Mawaahibul Jaliyl (1/408), Ad-Dusuwqiy (1/182) na Al-Inswaaf (1/439)]
1- Hadiyth ya Abu Hurayrah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwenye kuipata rakaa katika Swalaah, basi ameipata Swalaah nzima)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (580) na Muslim (607)]
Na neno: “Mwenye kuipata” ni sentensi sharti, na maana yake ni kuwa mwenye kupata chini ya rakaa basi hakuipata, kwani kuipata kunafungamana na rakaa kamili, na kutofungamanisha na rakaa kamili, ni sawa na kutengua yaliyosemwa na Rasuli. Na kufungamanisha na takbiyr ni sawa na kufuata lile ambalo Rasuli amelitengua.
2- Ama Hadiyth isemayo: ((Mwenye kuipata sijdah..)), makusudio yake ni rakaa kamili. Ni katika mlango wa kuita sehemu ya kitu kwa kukikusudia chenyewe kizima. Ndio maana wakati mwingine anasema: ((Mwenye kuipata rakaa)), na wakati mwingine ((Mwenye kuipata sijdah..)), na haya yote yanaonyesha kwamba makusudio ni mamoja, nayo ni rakaa kamili. Ibn ‘Umar amesema: “Nilihifadhi toka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) sijdah mbili kabla ya Adhuhuri na sijdah mbili baada yake”, yaani rakaa mbili. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
·
Mwenye Kupata Sehemu Ya Wakati Kisha Akapata Udhuru
Udhuru ukitokea ghafla baada ya wakati kuingia kama wendawazimu, kupotewa fahamu, hedhi, nifasi na kadhalika, basi hapa kutakuwa na hali mbili:
1- Wakati wa Swalaah uwe umepita kwa kitambo cha kuweza kuswali chini ya rakaa moja kamili ya faradhi. Hapa haitomlazimu kuilipa baada ya kuondoka udhuru.[Al-Majmu’u (3/71)]
2- Wakati wa Swalaah uwe umepita kwa kitambo cha kuweza kuswali rakaa kamili. Kuna kauli mbili kuhusiana na ulazima wa kuilipa zilizoelezewa katika mlango wa hedhi. [Angalia yaliyotangulia. (1/209)]
Sheikh wa Uislamu anaona kwamba haimlazimu kulipa, kwa kuwa udhuru umemtokea katika wakati ambapo anaruhusiwa kuichelewesha Swalaah naye si mwenye kukiuka mipaka, na kwa kuwa pia haikuripotiwa na yeyote kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwamuru mwanamke yeyote kuilipa Swalaah baada ya kupata hedhi katika wakati wake, na hili linatokea sana. Hii ndiyo hoja yenye nguvu ingawa kuilipa ni akiba zaidi. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
[3] Nyudhuru Za Kuichelewesha Swalaah Na Wakati Wake
1,2- Ni kulala na kusahau:
Mtu aliyelala au aliyesahau mpaka wakati wa Swalaah ukapita, basi huyo anasameheka. Atalazimika kuiswali Swalaah hiyo iliyompita anapoamka au anapokumbuka kutokana na Hadiyth ya Anas bin Maalik kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwenye kuisahau Swalaah, basi aiswali anapokumbuka, hakuna kifutio chake isipokuwa hilo)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (597) na Muslim (314-316)].
Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa safarini pamoja na Maswahaba wake walilala na hakikuwaamsha isipokuwa joto la jua baada ya kuchomoza. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawaambia: ((Hakuna taksiri katika kulala, bali taksiri ni kwa yule ambaye hakuiswali Swalaah mpaka ukaingia wakati wa Swalaah nyingine. Mwenye kufanya hilo, basi aiswali anapozindukana, na inapokuja kesho aiswali katika wakati wake)). [Hadiyth Swahiyh: Imeelezwa nyuma kidogo].
Kuiswali Swalaah wakati mtu anapoamka au anapoikumbuka, kiuhakika si kama anailipa bali anaiswali kawaida kwa kuwa huo ndio wakati alionao na hakuna wakati mwingine zaidi. [Angalia: As-Saylul Jarraar (1/188)]
·
Tanbihi:
Kauli za Maulamaa zimegongana kuhusiana na maana ya neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((na inapokuja kesho aiswali katika wakati wake)) katika Hadiyth ya Abu Qataadah iliyotangulia. Lililo sahihi zaidi ambalo wahakiki wamelikubali ni yale aliyoyaeleza An Nawawiy akisema kwamba maana yake ni kuwa Swalaah ikimpita mtu akailipa, basi wakati wake haubadiliki; utageuka kuwa mustakbali lakini unabakia kama ulivyo. Na inapokuja kesho yake, ataiswali Swalaah ya kesho katika wakati wake uliozoeleka, na hii haimaanishi kwamba anailipa Swalaah iliyompita mara mbili, yaani mara moja hapo hapo na mara nyingine kesho yake. [Sharhu Muslim cha An Nawawiy (2/988)]
3- Kulazimishwa:
Mwenye kulazimishwa asiswali kabisa, au hata kuswali kwa kuashiria, au akalazimishwa kutenda yaliyo kinyume na Swalaah, basi huyo anasameheka. [Al-Majmu’u (3/67), Haashiyat Ad-Dusuwqiy (1/200) na Al-Ashbaahu wa An-Nadhwaair (208)]
(Atazilipa udhuru unapoondoka). Na ikiwa ataweza kuashiria kwa kichwa, basi itampasa aswali kwa wakati na hatokuja kulipa kwa mujibu wa kauli sahihi. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
4- Kukusanya Swalaah mbili kwa anayeruhusiwa kukusanya:
Mwenye kukusanya Swalaah mbili kwa jam’u ya kuchelewesha, anakuwa anaiswali Swalaah ya kwanza katika wakati wa Swalaah ya pili. Naye kiuhalisia haambiwi kwamba ameichelewesha wakati wake ukapita, isipokuwa kidhahiri inaonekana hivyo. Katika hali hii ya kukusanya, wakati wa Swalaah zote mbili unakuwa ni mmoja. Vipengele vya hukmu za kukusanya kati ya Swalaah mbili vitakuja kuelezewa mbeleni InshaAllaah.
5- Kizaazaa cha vita:
Ikiwa hofu imetanda kiasi cha mtu kutoweza kuswali kwa njia yoyote ile hata kwa moyo wake, basi habebeshwi kosa endapo kama wakati wa Swalaah utamtoka (kwa mujibu wa moja ya kauli mbili za Maulamaa). Kwa kuwa ikiwa ataswali wakati huo, hatoweza kukijua anachokisoma au anachokifanya na hususan wakati vita vinapoumana. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliichelewesha Swalaah ya Alasiri katika vita vya Khandaq mpaka jua likazama. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (598) na Muslim (631). Angalia Ash-Sharhul Mumti’i (2/23) na Naylul Awtwaar (2/36)].
Imepokelewa toka kwa Anas akisema: “Vita vilipamba moto Alfajiri ya kukombolewa Tustar. Hawakuswali isipokuwa baada ya jua kuchomoza”. [Ibn Hazm ameiweka katika Al Muhallaa (2/244) na kaitilia nguvu kwa riwaya ya Mak-huol toka kwa Anas. Amesema: “Mak-houl hakumwahi Anas”. Ninasema: “Abu Haatim Ar Raaziy kama ilivyo katika Al-Maraasiyl (1/121) na At-Tirmidhiy kama ilivyo kwenye At-Tahdhiyb (1/290), amethibitisha kwa mwanawe kwamba Mak-houl ameisikia toka kwa Anas. Na kama katika Isnadi hakuna isipokuwa huyu, basi ni Swahiyh. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi”]
[4] Anayepata Sifa Ya Kuwajibikiwa Na Swalaah Kabla Ya Wakati Wake Haujatoka
Mtoto anapobaleghe, au akili ikamrejea mwendawazimu, au fahamu zikamrejea aliyepotewa nazo, au mwenye hedhi au nifasi akatwaharika kabla ya kutoka wakati wa Swalaah kwa kiasi ya rakaa moja au zaidi, basi itawalazimu kuiswali. Lakini je, itawalazimu kuziswali Swalaah za kabla ya Swalaah hiyo zinazojumuishwa kwake? Swali hili litakuwa wazi kwa mfano ufuatao: Ikiwa mwanamke mwenye hedhi atatwaharika kabla ya kuchwa jua, au kabla ya kuchomoza Alfajiri, basi Maulamaa wana kauli tatu kuhusiana na hali hii:
Ya kwanza: Akitwaharika kabla ya kuchwa jua, ni lazima aswali Adhuhuri na Alasiri, na kama akitwaharika kabla ya Alfajiri, ni lazima aswali Magharibi na ‘Ishaa. Haya yamehadithiwa toka kwa ‘Abdul Rahman bin ‘Awf, Ibn ‘Abbaas na Abu Hurayrah. Ni rai yenye nguvu ya Twaawus, An-Nakh’iy, Mujaahid, Rabiy’ah, Maalik, Al-Layth, Ash-Shaafi’iy, Ahmad, Abu Ath-Thawr na Is-Haaq. Hawa wote ni Jamhuri ya Maulamaa. [Ikhtilaaful ‘Ulamaa (uk. 380), Al-Awsatw (2/243), Masaail Ahmad cha Ibn Haaniy (1/131) na Bidaayatul Mujtahid (1/133)]
Na hoja yao ni:
1- Yaliyosimuliwa toka kwa ‘Abdul Rahmaan bin ‘Awf akisema: “Mwenye hedhi akitwaharika kabla jua halijazama, ataswali Adhuhuri na Alasiri, na akitwaharika kabla ya kuchomoza Alfajiri, ataswali Magharibi na ‘Ishaa”. [Isnadi yake ni Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abu Shaybah, (2/336), na kutoka kwake Ibn Al-Mundhir (2/243) na ‘Abdul Razzaaq (1285)]
2- Yaliyosimuliwa toka kwa Ibn ‘Abbaas akisema: “ Akitwaharika kabla ya Magharibi, ataswali Adhuhuri na Alasiri, na akitwaharika kabla ya Alfajiri, ataswali Magharibi na ‘Ishaa. [Isnadi yake ni Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ad-daaramiy (889), Ibn Abu Shaybah (2/337) na Ibn Al-Mundhir (2/244)]
Imenukuliwa mfano wake toka kwa Abu Hurayrah.
3- Adhuhuri na Alasiri, au Magharibi na ‘Ishaa, hukusanywa katika hali ya dharura katika wakati wa moja ya Swalaah mbili. Ikiwa atatwaharika mwishoni mwa mchana, basi wakati wa Adhuhuri unakuwa bado uko na hivyo ataiswali kabla ya Alasiri. Na kama akitwaharika mwishoni mwa usiku, basi wakati wa Magharibi unakuwa bado uko katika hali ya dharura na hivyo ataiswali kabla ya ‘Ishaa. [Majmu’u Al-Fataawaa. Angalia pia Sharhul ‘Umdah cha Ibn Taymiyah (Mjalada wa Pili)]
Ya pili: Akitwaharika katika wakati wa Alasiri, ni lazima aswali Alasiri lakini si lazima aswali Adhuhuri. Hii ni rai yenye nguvu ya Al-Hasan, Qataadah, Ath-Thawriy na Abu Haniyfah. [Ikhtilaaf Al-Ulamaa (uk. 380), Al-Awsatw (2/245) na Al-Aswl (1/330)]
Hoja yao ni:
1- Kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Mwenye kuipata rakaa ya Swalaah, basi ameipata Swalaah nzima)). Wanasema: “Alif na Laam” katika “As-Swalaah الصلاة “ ni ya “Al-‘Ahdi”, kwa maana kuwa ameipata Swalaah ambayo ameipata rakaa ndani ya wakati wake. Ama Swalaah ya kabla yake, yeye anakuwa hakupata chochote katika wakati wake, na wakati huo unakuwa umeshapita, naye hakuwa mwenye sifa ya ulazima. Sasa vipi itakuwa lazima kwake?! [Ash-Sharhul Mumti’i (2/130)]
2- Hatukhitalifiani kuwa mwenye kuacha Swalaah mbili mpaka jua likakurubia kuzama kwa rakaa moja, kisha akaingia kuswali kwa kuzikusanya, akaswali rakaa moja kabla jua halijazama na rakaa saba baada ya kuzama, kwamba huyo anakuwa amemwasi Allaah na anashutumiwa. Ikiwa amekusudia katika hali ya kutokuwa na udhuru, basi haijuzu kufanywa hukmu ya wakati ambao pameruhusiwa kukusanya kati ya Swalaah mbili kuwa hukmu ya wakati ambao pamekatazwa kukusanya kati ya Swalaah hizo. [Al-Awsatw cha Ibn Al-Mundhir (2/245)]
3- Tunakubaliana kwamba lau kama ameipata rakaa moja katika Swalaah ya Adhuhuri, kisha kikatokea kizuizi cha kisharia, ni kuwa atalazimika kulipa Adhuhuri tu pamoja na kwamba wakati wa Adhuhuri ni wakati wa Adhuhuri na Alasiri katika hali ya udhuru na kukusanya. Hivyo, tofauti iko wapi katika masuala mawili? Ikiwa watasema: “Tofauti yetu ni kwa mujibu wa athari toka kwa Maswahaba”, basi wataambiwa kwamba ikiwa athari zao ni Swahiyh, basi zitachukuliwa juu ya uakiba na uhadhari basi kwa ajili ya kuchelea uwezekano wa kuwa kizuizi kimeondoka kabla ya kumalizika wakati wa Swalaah ya kwanza, na hususan hedhi, kwani mwenye hedhi anaweza asitambue kutwaharika kwake ila baada ya kupita muda. [Ash-Sharhul Mumti’i cha Ibn ‘Uthaymiyn (2/130) kwa mabadilisho madogo]
Ya tatu: Mwanamke akitwaharika kabla ya jua kuchwa kwa kitambo cha kuweza kuswali Swalaah mbili, basi ataswali Adhuhuri na Alasiri. Na kama wakati hautoshi isipokuwa kwa Swalaah moja tu, atalazimika kuswali Alasiri peke yake. Na hii ni kauli ya Maalik na Al-Awzaa’iy. [Al-Awsatw (2/246) na Bidaayatul Mujtahid (1/133)]
Lenye Nguvu
Ninaloliona mimi ni kuwa kauli ya pili ndio yenye nguvu zaidi. Ama ya kwanza ni ya hadhari na akiba, na ya tatu ni makimbilio ya mwisho kama wakati ni mfinyu. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
[5] Ikiwa Mtu Hakuswali Mpaka Wakati Wa Swalaah Ukatoka Bila Ya Udhuru
Mafuqahaa wana kauli mbili kuhusiana na hukmu ya kuilipa Swalaah hii:
Ya kwanza: Ni lazima ailipe. Ni kauli ya Jamhuri ya Maulamaa wakiwemo Maimamu wanne na wengineo mpaka An-Nawawiy amethubutu kudai kuwa ni Ijma’a ya Maulamaa wote. [Al-‘Inaayah (1/485-pamoja na Fat-hul Qadiyr), Ad-Dusuwqiy (1/264), Al-Majmu’u (3/71), Al-Insaaf (1/342) na Al-Mumti’i (2/133)] Dalili yao ni haya yafuatayo:
1- Hadiyth zinazogusia wajibu wa kulipa Swalaah kwa mwenye kusahau. Wanasema kwamba kutokana na yanayofahamika kwenye Hadiyth hizo, wajibu wa kulipa kwa mwenye kufanya kusudi unakuwa na uzito zaidi.
Hili linajibiwa: “Mwenye kusema kuwa aliyefanya kusudi halipi, hakusema kuwa hali yake ni nafuu zaidi kuliko aliyesahau, bali kinachozuilia wajibu wa kulipa kwa mwenye kufanya kusudi ni kuwa dhambi hazimwondokei, hivyo kulipa hakuna faida. Hivyo basi, kusema kuwa ni wajibu kulipa bila kuwepo kinachothibitisha ni upuuzi kinyume na aliyesahau au aliyelala. Hawa Rasuli amewaamuru kulipa na akaeleza wazi kwamba kulipa ni kafara kwao, na hakuna jingine zaidi ya hilo. [Naylul Awtwaar (2/32)]
Kisha kipimo cha kitu hufanywa kwa kinachofanana nacho na si kwa kile kilicho kinyume nacho, na hili halina mjadala. Kinyume cha kusudi ni sahau, na kinyume cha maasia ni utiifu, basi vipi vitakuwa katika kipimo kimoja?!” [Al-Muhallaa (2/237). Kuna utafiti murua kabisa uliofanywa kwa ajili ya kuwajibu wenye kusema kuwa ni wajibu kulipa]
2- Neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusiana na kulipa kwa mwenye kulala na mwenye kusahau: ((Hakuna kafara yake isipokuwa hilo)). Wanasema: “Hadiyth inaonyesha kwamba anayekusudiwa ni mwenye kufanya kusudi, kwa kuwa aliyelala na aliyesahau, hao hawana dhambi, hivyo makusudio ya mwenye kusahau ni mwenye kuacha”.
Hili linajibiwa: “Kwamba maneno haya yanamaanisha kuwa si lazima kulipa kwa aliyelala au aliyesahau kwa kutokuwepo dhambi walilolifanya kafara kuwa mwega wake wakati ambapo Hadiyth Swahiyh zinaeleza wazi kwamba hilo ni wajibu kwa wawili hao!! Isitoshe, kafara inaweza kuwa kwa kosa kama inavyokuwa kwa kusudi, na hili li wazi”.
3- Ulinganisho wa aliyefungua kwa makusudi katika mwezi wa Ramadhwaan kuwa ni lazima alipe sawa na yule aliyemwingilia mkewe mchana wa Ramadhwaan.
Hili linajibiwa: “Hadiyth inayothibitisha wajibu wa kulipa kwa mwenye kuingilia mchana wa Ramadhwaan ni dhwa’iyf. Al-Bukhaariy na Muslim wameifanyia Hadiyth hiyo “ikhraaj” bila ya nyongeza isemayo: “Na funga siku badala ya ile uliyojamii”, na nyongeza ni dhwa’iyf, haitegemewi”. [Angalia Majmu’u Al-Fataawaa (22/40), Nasbu Ar-Raayah (2/453) na At-Talkhiysw (2/219)]
4- Wanaweza kusaidiwa posho ya dalili ambayo wao hawakuitoa kwa Hadiyth isemayo: ((Basi deni la Allaah lina haki zaidi ya kulipwa)), tukisema kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameziita ‘Ibaadah (Hijjah na Swaum) ni deni. [Hadiyth Swahiyh: Itakuja katika mlango wake, Insha-Allaah]
Hili linajibiwa: “Kutokana na hili, ni lazima wajuzishe kuswali kabla ya kuingia wakati wa Swalaah!! Kwani deni linaweza kulipwa kabla muda wake haujafika. Ufafanuzi zaidi utakuja katika dalili la kundi jingine.
Ya pili: Hapaswi kuilipa, bali hata Swalaah hiyo haiswihi. Yamesemwa haya na ‘Umar bin Al-Khattwaab na mwanawe ‘Abdullaah, Sa’ad bin Abu Waqqaas, Ibn Mas-’oud [Ibn Hazm amesema: “Hatumjui Swahaba aliyekhilafiana na hilo], Al-Qaasim bin Muhammad, Budayl Al-‘Uqayliy, Muhammad bin Siyriyn, Mutwarrif bin ‘Abdullah, ‘Umar bin ‘Abdul ‘Aziyz, kundi la Maulamaa wa Kishafii, Al-Jawzjaaniy, Abu Muhammad Al-Barbahaariy, Ibn Battwah, Daawuud Adh-Dhwaahiriy na Ibn Hazm. Ni chaguo la Sheikh wa Uislamu Ibn Taymiyah, Al-‘Allaamah Al-Albaaniy na Ibn ‘Uthaymiyn. [Al- Muhallaa (2/235- na zinazofuatia), Majmu’u Al-Fataawaa (22/40) Fat-hul Baariy cha Ibn Rajab kama ilivyo katika Al-Inswaaf (1/443), Al-Mumti’i (2/133) na Naylul Awtwaar (2/31-32)]
Hii ndio kauli yenye nguvu zaidi. Na dalili ya hili ni:
1- Kauli Yake Ta’alaa:
((فَإِذَا قَضَيْتُمُ الصَّلَاةَ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِكُمْ ۚ فَإِذَا اطْمَأْنَنتُمْ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ ۚ إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا ))
(( Mtakapomaliza Swalaah, mdhukuruni Allaah msimamapo, na mkaapo na mnapolala ubavuni mwenu Mtakapopata utulivu, simamisheni Swalaah (kama desturi), hakika Swalaah kwa Waumini ni fardhi iliyowekwa nyakati maalumu)). [An-Nisaa (4:103)].
Swalaah ni ‘ibaadah yenye pande mbili zenye mipaka. Ina mwanzo wake na mwisho wake. Hivyo basi, haijuzu kuiswali kabla ya wakati wake au baada ya wakati wake, hakuna kitenganishi kati ya pande hizi ila kwa Aayah au Hadiyth yenye amri mpya kama ilivyo kwa mwenye kulala na mwenye kusahau na wengineo wenye nyudhuru. Ni kama vile vile ilivyo katika Hijjah, na kufunga Ramadhwaan.
Aidha, inajulikana kwamba ikiwa mtu ataswali kabla ya wakati kwa kusudi, basi Swalaah yake ni batili kwa makubaliano ya Maulamaa wote, na hali inakuwa hivyo hivyo kama ataiswali baada ya wakati wake.
2- Kauli Yake Ta’alaa:
((فَوَيْلٌ لِّلْمُصَلِّين •الَّذِينَ هُمْ عَن صَلَاتِهِمْ سَاهُونَ))
(( Basi Ole kwa wanaoswali ... • Ambao wanapuuza Swalaah zao)). [Al-Maa’uwn (107:4-5)]
3- Kauli Yake Ta’alaa:
((فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ أَضَاعُوا الصَّلَاةَ وَاتَّبَعُوا الشَّهَوَاتِ ۖ فَسَوْفَ يَلْقَوْنَ غَيًّا))
(( Wakafuata baada yao waovu, walipoteza Swalaah na wakafuata matamanio; basi watakutana na adhabu motoni)). [ Maryam (19:59)]
Lau kama mwenye kuacha Swalaah kwa makusudi anaweza kuipata baada ya kutoka wakati wake, basi asingeliingia katika makamio wala asingelikutana na adhabu. Kama ambavyo hakuna makamio wala adhabu kwa yule mwenye kuichelewesha hadi mwisho wa wakati wake, akaiswali na kuipata.
4- Hadiyth isemayo: ((Mwenye kuisahau Swalaah, basi aiswali anapoikumbuka)), [Hadiyth Swahiyh: Imeelezwa nyuma kidogo], nayo ni dalili ya kwamba mwenye kufanya kusudi, basi hailipi Swalaah, kwani neno (Mwenye kusahau) ni sharti, na kukosekana sharti kunahitajia kukosekana chenye kushurutiwa. Hivyo basi, ambaye hakusahau, haswali.
5- Kulipa ni lazimisho la kisharia, na sharia haijuzu ila kutoka kwa Allaah kupitia ulimi wa Rasuli Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na haipasi kulipa isipokuwa kwa amri mpya (kwa lililo sahihi katika usuul), na hakuna dalili kuhusiana na amri ya kulipa. Na lau kama kulipa kungelikuwa ni wajibu kwa mwenye kufanya kusudi ya kuacha Swalaah mpaka wakati wake ukatoka, Allaah Mtukufu Asingelighafilisha hilo wala Rasuli Wake, Wasingelisahau hilo wala Wasingelifanya kusudi ya kututaabisha kwa kuacha kulibainisha.
((وَمَا نَتَنَزَّلُ إِلَّا بِأَمْرِ رَبِّكَ ۖ لَهُ مَا بَيْنَ أَيْدِينَا وَمَا خَلْفَنَا وَمَا بَيْنَ ذَٰلِكَ ۚ وَمَا كَانَ رَبُّكَ نَسِيًّا))
(( Na (sisi Malaika) hatuteremki ila kwa amri ya Rabb wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Ni Yake Yeye yaliyoko mbele yetu, na yaliyoko nyuma yetu, na yaliyoko baina ya hayo. Na Rabb wako si Mwenye kusahau kamwe)). [Maryam (19:64)].
6- Hadiyth: ((Anayepitwa na Swalaah ya Alasiri, ni kama aliyepokonywa ahli wake na mali yake)). [Hadiyth Swahiyh: Imeelezwa nyuma kidogo]
Ni sawa na kusema kuwa kilichopita haiwezekani kukirejesha tena. Na ikiwa kitapatikana au ikawezekana kukipata, basi kisingelipita kama ambavyo Swalaah yenye kusahauliwa, haipiti kamwe. Na lau ingeliwezekana kuilipa iliyoachwa makusudi, tungelisema kwamba imempita kwa uongo na kwa batili!!
7- Mwenye kuwajibisha kuilipa kwa aliyeiacha makusudi ataulizwa: “Swalaah hii unayomwamrisha aiswali, je ni ile ambayo Allaah Amemwamrisha, au ni Swalaah nyingine?” Akisema: “Ni hiyo hiyo”, tutamwambia: “Basi mwenye kufanya kusudi ya kuiacha si mwasi, kwa kuwa amefanya lile Alilomwamrisha Allaah Ta’alaa, na hakuna madhambi kwa mujibu wa kauli yako!! Na hakuna lawama kwa mwenye kufanya kusudi ya kuacha Swalaah mpaka wakati wake ukatoka!!” Na hili hakunaMuislamu anayelisema. Na kama atasema: “Siyo ile ambayo Allaah Ameiamuru”, basi tutamwambia: “Umesema kweli”. Na hili ni jibu tosha kwa kuwa wao wamekiri kwamba wamemwamuru kile ambacho Allaah Hakukiamuru. [Angalia Al-Muhallaa (2/235-na zinazofuatia) na Al-Ihkaam cha Ibn Hazm (1/301)]
Ninasema: “Kauli hii ndiyo yenye nguvu zaidi. Wenye kwenda kinyume nayo, hawana kifaacho kutegemewa kama dalili. Na Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
·
Mwenye Kuipoteza Swalaah Miaka Mingi Ya Umri Wake
Kwa kusema kwamba mwenye kuacha Swalaah kwa kusudi bila ya udhuru mpaka wakati wake ukatoka si wajibu kwake kuilipa wala hilo haliswihi, tunajengea juu ya kauli hiyo kwamba mwenye kuacha Swalaah kwa miaka mingi ya umri wake, kisha akatubia kwa Allaah na akalingamana sawa katika dini yake, basi huyo hatozilipa Swalaah zote zilizompita sawasawa tukimhukumia kwamba ni kafiri wakati alipokuwa haswali au la. Lakini hii ni kinyume na Jamhuri ya Maulamaa wanaosema kwamba ni lazima azilipe Swalaah zote zilizompita!! [Ibnu ‘Aabidiyn (2/62) Ad-Dusuwqiy (1/264) na Mughnil Muhtaaj (1/308)]
·
Na Vipi Kuhusu Mwenye Kuiacha Kwa Makusudi?
Hukmu ya kutoilipa Swalaah kwa mwenye kuiacha mpaka muda wake ukatoka bila ya udhuru, haimaanishi kuwa anahafifishiwa mambo, bali mambo yalivyo ni kuwa hilo ni adhabu na ghadhabu kutokana na kitendo chake hicho. Dhambi halimwondokei hata kama ataiswali Swalaah hiyo mara elfu moja baada ya wakati wake isipokuwa kama atatubia kwa Allaah na kuomba maghfirah. Hili ndilo linalompasa; kuomba tawbah na maghfirah, kukithirisha kheri na kuswali Swalaah za Sunnah kutokana na neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): (( Jambo la kwanza atakalofanyiwa hisabu mtu Siku ya Qiyaamah katika amali zake ni Swalaah. Kama ni sahihi, basi amefaulu na kufanikiwa, na kama ni mbovu, basi amepita utupu na amekula hasara. Na kama kimepungua chochote katika faradhi yake, Mola (Tabaaraka wa Ta’alaa) Atasema: Angalieni! Je, Mja Wangu anazo Swalaah za Sunnah zikamilishie kilichopungua katika faradhi zake? Kisha amali zake zilizobakia huchukuliwa juu ya hilo)). [Haya yashazungumziwa. Angalia Al-Muhallaa (2/235), Al-Fataawaa (22/40-41) na Tuhfat Al-Ahwadhy (2/463)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
007-Kulipa Swalaah Zilizopita
Swalaah iliyopita, ni Swalaah ambayo wakati wake maalum umetoka. Tumefanya uhakiki na kubaini kwamba Swalaah hazilipwi isipokuwa zile ambazo wakati wake ulitoka kwa udhuru kinyume na Jamhuri ya Maulamaa wanaosema kwamba ‘ibaadah zenye mpaka maalumu wa wakati, hupita kwa kupita wakati wake uliowekwa bila kuifanya, na ‘ibaadah hizo humganda mtu mpaka zitakapolipwa bila kutofautisha kati ya mwenye udhuru na asiye na udhuru.
·
Je, Ni Lazima Kuilipa Haraka Swalaah Iliyopita?
Mtu ambaye Swalaah imempita bila ya udhuru wa kisharia, ni lazima ailipe haraka kutokana na neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusiana na aliyelala na mwenye kusahau: ((Aiswali anapoikumbuka, hakuna kafara yake isipokuwa hilo)). Hili ni agizo, nalo ni la wajibu wa hapo kwa papo. Makusudio ya hapo kwa papo ni uharaka wa kawaida usio wa kuvuta sana. Hii ni kauli ya wafuasi wa Maalik na Hanbali. [Ash-Sharhu As-Swaghiyr (1/3665) na Kash-Shaaful Qina’a (1/260)]
Wafuasi wa Hanafi na Shaafi’i wanaona kwamba ni vizuri kufanya haraka, na inajuzu pia kuchelewesha kidogo katika kulipa. [Haashiyatu Ibn ‘Aabidiyn (2/74) na Al-Majmu’u (3/69)]
Wanatoa dalili ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na Maswahaba wake walipoamka usingizini baada ya jua kuchomoza, hawakuswali ila baada ya kuhamia mahala pengine!
Wanajibiwa: “Kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alilitolea sababu hilo kwa kusema: ((Kila mtu akamate kichwa cha mnyama wake, kwani hapa ni mashukio ambayo shaytwaan alitujia)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (680) na An Nasaaiy (1/80) toka kwa Abu Hurayrah].
Kizuizi cha kuswali ni kuwa mahala hapo shaytwaan alikuwepo, kwa hivyo basi, Hadiyth haionyeshi kutoa ruhusa ya kuvuta vuta wakati katika kulipa. Na juu ya msingi wa hili, ikiwa mtu ataamka baada ya jua kuchomoza, haitojuzu kwake arudi tena kulala mpaka aswali kwanza, kwani huo ndio wakati wake. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
·
Mpangilio Wa Kuzilipa Swalaah Zilizopita
Imepokelewa toka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah kwamba ‘Umar bin Al-Khattwaab alikuja siku ya Khandaq baada ya kuchwa jua. Akaanza kuwashutumu makafiri wa Kikureshi na kusema: “Ewe Rasuli wa Allaah! Sikukurubia kuswali Alasiri mpaka jua likawa limekurubia kuzama”. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: ((Wal-Lahi sikuiswali)). Akatawadha, nasi tukatawadha, akaswali Alasiri baada ya kuchwa jua, kisha akaswali Magharibi”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (598) na Muslim (209)].
Imepokelewa na Abu Sa’iyd akisema: “Tulizuilika tusiweze kuswali Siku ya Khandaq mpaka ilipoingia sehemu ya usiku baada ya Magharibi, Allaah Alitutosha. Na hiyo ni Kauli Yake Ta’alaa:
((وَرَدَّ اللَّـهُ الَّذِينَ كَفَرُوا بِغَيْظِهِمْ لَمْ يَنَالُوا خَيْرًا ۚ وَكَفَى اللَّـهُ الْمُؤْمِنِينَ الْقِتَالَ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ قَوِيًّا عَزِيزًا ))
Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwita Bilaal, akaqimu Adhuhuri akaiswali, tena aliiswali kwa utuvu na umakini kama anavyokuwa akiiswali katika wakati wake. Kisha akamwamuru aqimu Alasiri akaiswali, tena aliiswali kwa utuvu na umakini kama anavyokuwa akiiswali katika wakati wake. Kisha akamwamuru aqimu Magharibi akaiswali hivyo hivyo. Na hili lilikuwa kabla Allaah Ta’alaa Hajateremsha hukmu ya Swalaah ya vita: فإن خفتم فرجالا أو ركبانا “. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (1/297), Ahmad (3/25), Ibn Khuzaymah (996) na Abu Ya’alaa (1296)].
Katika Hadiyth hizi mbili, tunaona kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alizilipa Swalaah zilizompita kimpangilio. Na hapa ndipo Jamhuri ya Maulamaa ikasema kwamba ni lazima kuzipangilia Swalaah zilizompita mtu ingawa wamekhitalifiana kati yao kuhusiana na chambuzi zake. [Al-Badaai-’i (1/131), Sharhu As-Swaghiyr (1/367), Al-Mughniy (1/607) na Naylul Awtwaar (2/36)]
Wametolea dalili kwa kitendo cha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na kwamba wakati wa Swalaah ya kulipwa ni mfinyu zaidi kuliko wakati wa Swalaah iliyopo, na kwa hivyo ni wajibu kuitanguliza ile iliyofinyika.
Ash-Shaafi’iy anasema: [Rawdhwat At-Twaalibiyna (1/269)]
“ Ni Sunnah kufanya hivyo na si lazima, kwa kuwa kitendo alichokifanya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) peke yake bila na wengine, hakionyeshi kwamba ni lazima”.
·
Vinavyoondosha Mpangilio
1- Ufinyu wa wakati wa Swalaah iliyopo
[Al-Binaayah (2/628), Al-Mughniy (1/610), Al-Inswaaf (1/444), Al-Kharshiy (1/301) na Al-Awsatw (2/415)]
Ufinyu hupomosha mpangilio, kwa kuwa ufaradhi wa wakati uliopo ni muhimu zaidi kuliko ufaradhi wa kupangilia. Mtu ataswali Swalaah iliyopo kisha atailipa iliyompita. Na hii ni kauli ya Abu Haniyfah na riwaya toka kwa Ahmad pamoja na Ibn Al-Musayyib, Al-Hasan, Al-Awzaaiy, Ath-Thawriy na Is-Haaq. Ama Ash-Shaafi’iy, yeye anasema kuwa hakuna kabisa wajibu wa kupangilia kama ilivyotangulia.
Ama wafuasi wa Maalik (na riwaya toka kwa Ahmad, ‘Atwaa na Al-Layth), hawa wanasema kwamba mtu atafanya mpangilio hata kama wakati wa Swalaah iliyopo utatoka!!
Ninasema: “Kauli ya kwanza ina mwelekeo zaidi na hasa hasa pakizingatiwa kuwa suala la wajibu wa kupangilia lina mvutano.”
2- Kupitwa na Jamaa
Mtu ambaye kwa mfano amepitwa na Adhuhuri, halafu akachelea kwamba kama atailipa ataikosa jamaa ya Alasiri, basi hapo mpangilio utaondoka na ataswali Alasiri kwa jamaa, halafu atailipa Adhuhuri baada yake. Hii ni riwaya toka kwa Ahmad na ni chaguo la Sheikh wa Uislamu. [Al-Inswaaf (1/444-445)]
Aidha, anaweza kujiunga nao katika Jamaa ya Alasiri kwa niya ya Adhuhuri – kwa mujibu wa fatwa inayojuzisha kutofautiana niya ya maamuma na ya imamu, na hili litakuja kuelezewa – kisha aswali Alasiri. La kwanza linaweza kuwa na nguvu zaidi, na Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
3- Kupitwa na Swalaah ambayo hawezi kuilipa peke yake kama Swalaah ya Ijumaa.
Kama atakumbuka kwamba ana Swalaah iliyompita baada ya kuqimiwa Swalaah ya Ijumaa, basi atatanguliza kwanza Ijumaa kwa kuwa hatoweza kuilipa na wakati wake humalizika kwa kumalizika Swalaah. Hii ni riwaya toka kwa Ahmad. [As-Saabiq (1/444) na Al-Mumti’i (2/141)]
4- Kusahau.
Kama ataswali Swalaah zilizompita bila mpangilio kwa kusahau, basi hapana kitu kutokana na ujumuishi wa Kauli Yake Ta’alaa:
((لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ ۗ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِ ۖ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا ۚ أَنتَ مَوْلَانَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ))
(( Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake. Itapata (thawabu) iliyoyachuma, na ni dhidi yake (kwa maovu) iliyojichumia. “Rabb wetu Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Rabb wetu, Usitubebeshe mzigo kama Ulivyoubebesha juu ya wale waliokuwa kabla yetu. Rabb wetu, Usitutwike tusiyoyaweza, na Tusamehe, na Tughufurie na Turehemu, Wewe ni Mola Mlinzi wetu, basi Tunusuru dhidi ya watu makafiri)). [Al-Baqarah (2:286)]
Katika Hadiyth, Allaah Ta’alaa Alisema: “Naam”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (125)]
Na katika riwaya nyingine: “Nishafanya”. Na pia kutokana na Hadiyth isemayo:
((Hakika Allaah Ameusamehe umati wangu walilolikosea, walilolisahau na walilolazimishwa)). [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Maajah (2045) na wengineo. Angalia Al-Irwaa (82)].
Hili ndilo lililopo katika madhehebu ya Hanafi na Hanbali kinyume na Maalik na riwaya toka kwa Ahmad. [Al-Binaayah (2/629), Al-Mughniy (1/609), Al-Kharshiy (1/301)]
5- Kutokujua
Asiyejua wajibu wa kupangilia akaswali bila mpangilio, basi hakuna kitu juu yake, kwa kuwa kutokujua ni ndugu ya kusahau katika Kitabu cha Allaah na Sunnah ya Rasuli Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na hii ni riwaya toka kwa Ahmad na chaguo la Sheikh wa Uislamu, na Mahanafi pia. [Al-Inswaaf (1/445) na Al-Binaayah (2/629)]
·
Kuilipa Swalaah Iliyopita Kwa Umbo Lake Lilivyo
Wafuasi wa Hanafi na Maalik (na kauli toka kwa Ash-Shaafi’iy), Abu Thawr na Ibn Al-Mundhir wanaona kwamba umbo la Swalaah yenye kulipwa linafungamanishwa na wakati wake ule ule wa asili ili ulipaji huo uendane na utendaji wake. [Majma’a Al-Anhur (1/164), Ash-Sharhu As-Swaghiyr (1/365), Rawdhwat At-Twaalibiyna (1/269) na Ikhtilaaf Al-‘Ulamaa (uk wa 60)]
Aliyesahau Swalaah ya ‘Ishaa (ambayo husomwa kwa sauti) kisha akaikumbuka mchana, basi ataisoma kwa sauti kama ilivyo, na hivyo hivyo kwa Swalaah zinazosomwa kimya kimya. Wanatolea dalili kwa Hadiyth ya Abu Sa’iyd iliyotangulia kuhusiana na kisa cha Khandaq anaposema: “Akaqimu Adhuhuri akaiswali, tena aliiswali kwa utuvu na umakini kama alivyokuwa akiiswali katika wakati wake”. Hadiyth. Na hii ilikuwa ni baada ya Magharibi.
Ama Mahanbali na Mashaafi’i, wanaona kwamba umbo hufungamanishwa na wakati ule wa kuilipa!!
Na ikiwa mtu alisahau kuswali akiwa mjini kwake kisha akakumbuka akiwa safarini, basi ataiswali kamili kama ilivyo bila kuipunguza juu ya rai ya kundi la kwanza. Ash-Shaafi’iy na Ahmad wamekubaliana nao juu ya hili lakini wamekataa kinyume cha hivyo wakisema: “Akiisahau Swalaah ya safari kisha akaikumbuka mjini kwake baada ya kurudi, basi ataiswali kamili. [Al-Ummu (1/161), Al-Majmu’u (4/249), Al-Mughniy (1/570) na Ikhtilaaful ‘Ulamaa (uk. 60)]
·
Kuzilipa Sunnah Za Rawaatib
Inaruhusiwa kuzilipa Sunnah za rawaatib kama zimempita mtu kwa mujibu wa kauli sahihi ya Maulamaa. Limesimuliwa hili toka kwa Ibn ‘Umar, na ni kauli yenye nguvu ya Al-Awzaa’iy, Ash-Shaafi’iy, Ahmad, Is-Haaq, Muhammad bin Al-Hasan, Al-Mazniy na wengineo. [Rawdhwat At-Twaalibiyna (1/337), Al-Inswaaf (2/178). Angalia kauli nyinginezo kwenye Kitabu cha Naylul Awtwaar]
Hili litakuja kuelezewa kichambuzi katika mlango wa “Swalaah za Sunnah” Insha-Allaah.
·
Adhana Na Iqaamah, Na Kuswali Kwa Jamaa Katika Swalaah Ya Kulipa
Aliyepitwa na Swalaah na akataka kuilipa, anaruhusiwa kuadhini na kuqimu. Pia waliopitwa na jamaa, wanaruhusiwa kuilipa kwa Jamaa. Na hii ni kutokana na Hadiyth ya Abu Qataadah kuhusiana na kisa cha kulala Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na Maswahaba wake wakapitwa na Swalaah ya Alfajiri mpaka jua likachomoza. Katika Hadiyth hiyo, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia Bilaal: ((Simama uwaadhinie watu Swalaah)). Jua lilipochomoza na pakapambauka sawasawa, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaswalisha. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (595), Abu Daawuud (439) na An-Nasaaiy (2/105)]
Na katika tamshi la Hadiyth ya Ibn Mas-’oud: “Akamwamuru Bilaal akaadhini, kisha akaqimu na Rasuli akatuswalisha”. [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (1/450) na Ibn Hibaan (1580)].
Na hii ndiyo kauli yenye nguvu ya Jamhuri ya Maulamaa.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
008-Nyakati Zisizoruhusiwa Kuswali
Alhidaaya.com [3]
1,2- Baada ya Swalaah ya Alfajiri mpaka kupanda jua kiasi cha mkuki, na baada ya Swalaah ya Alasiri mpaka kuchwa jua
Imethibiti kupigwa marufuku kuswali Swalaah za Sunnah katika nyakati hizi mbili, na asili katika hili ni:
(a) Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas akisema: “Walinieleza watu wasio na chembe ya shaka kuhusu ukweli na uaminifu wao – na pia kwa ‘Umar (Radhwiya Allaahu Anhu) - kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kuswali baada ya Alfajiri mpaka jua lichomoze, na baada ya Swalaah ya Alasiri mpaka jua lichwe. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (581) na Muslim (826)].
(b) Hadiyth ya Abu Sa’iyd aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (( Hapana Swalaah baada ya Alfajiri mpaka jua lipande, na hapana Swalaah baada ya Alasiri mpaka jua lichwe)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (586) na Muslim (827)].
3- Wakati jua linapopinduka Adhuhuri
Ni kwa Hadiyth ya ‘Uqbah bin ‘Aamir (Radhwiya Allaahu Anhu) aliposema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitukataza kuswali au kuwazika maiti zetu katika nyakati tatu: Jua linapochomoza angavu mpaka lipande, jua linapokuwa katikati ya mbingu Adhuhuri mpaka lipinduke, na wakati jua linapokurubia kuchwa mpaka lichwe kabisa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (831)].
·
Sababu Ya Katazo
Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amebainisha sababu ya kukataza kuswali katika nyakati hizi alipomwambia ‘Amri bin ‘Absah: ((Swali Swalaah ya Alfajiri, kisha acha kuswali hadi jua lichomoze na mpaka linyanyuke, kwani jua huchomoza wakati linapochomoza kati ya pembe mbili za shaytwaan, na wakati huo makafiri hulisujudia. Halafu swali, kwani Swalaah huhudhuriwa na hushuhudiliwa mpaka kivuli kinapokuwa kando ya mkuki. Kisha acha kuswali, kwani wakati huo Jahannamu hukolezwa. Na kivuli kinapokuja, basi swali, kwani Swalaah huhudhuriwa na hushuhudiliwa mpaka utakaposwali Alasiri. Kisha acha kuswali mpaka jua lizame, kwani jua huzama kati ya pembe mbili za shaytwaan, na wakati huo makafiri hulisujudia)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (832)].
·
Yasiyokuwemo Kwenye Katazo
1- Adhuhuri ya Siku ya Ijumaa
Wakati huu imesuniwa kuswali Sunnah yoyote kabla ya Swalaah ya Ijumaa mpaka khatibu apande mimbari. Anapopanda mimbari, basi hapo hairuhusiwi tena kuswali Sunnah. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Haogi mtu Siku ya Ijumaa, akajitwaharisha upeo wa kujitwaharisha, akajipaka mafuta au akajitia mafuta mazuri ya nyumba yake, kisha akatoka (mapema) asije kufarakanisha kati ya wawili, halafu akaswali kilichosuniwa kwake, kisha akanyamaza wakati khatibu anapozungumza, isipokuwa husamehewa yaliyo kati yake na ijumaa nyingine)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (883)].
Na kwa haya, Ash-Shaafi’iy (Rahimahul Laahu) anasema akitolea dalili kwa Hadiyth hii na Hadiyth ya Abu Hurayrah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kuswali nusu ya mchana mpaka jua lipinduke isipokuwa Siku ya Ijumaa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (595), Abu Daawuud (439) na An-Nasaaiy (2/105)]
Ni Dhwa’iyf, na yaliyotajwa yanatosheleza, walil-Laahi Al-Hamdu.
Maulamaa wana kauli nyingine mbili:
Ya kwanza: Ni kuwa si karaha kuswali nusu ya mchana Swalaah yoyote sawasawa ikiwa ni Siku ya Ijumaa au siku nyingine. Hii ni kauli ya Maalik, na hoja yake ni kitendo cha watu wa Madiynah, lakini hoja yake hii inapingwa na Hadiyth zilizotangulia.
Ya pili: Ni karaha kuswali nusu ya mchana Swalaah yoyote sawasawa ikiwa ni Siku ya Ijumaa au siku nyingine. Ni kauli ya Abu Haniyfah na mashuhuri katika madhehebu ya Ahmad.
Madhehebu ya Ash-Shaafi’iy ndiyo yenye nguvu zaidi, nayo ni chaguo la Sheikh wa Uislamu. [Zaadul Ma’aad cha Ibn Al-Qayyim (1/378) chapa ya Ar-Risaalah]
2- Rakaa mbili za twawaaf katika Baytul Haraam
Haizuiliwi kuswali rakaa mbili za twawaaf katika nyakati za marufuku tulizozitaja kutokana na dalili zifuatazo:
(a) Hadiyth ya Jubayr bin Mutw’am (Radhwiya Alaahu Anhu) asemaye kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Enyi ukoo wa ‘Abdi Manaaf! Msimzuie yeyote aliyetufu Nyumba hii na akaswali saa yoyote aitakayo usiku au mchana)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (869), An-Nasaaiy (1/284) na Ibn Maajah (1254)].
(b) Ibn ‘Abbaas, Al-Hasan, Al-Husayn na baadhi ya Masalaf walilifanya hilo.
(c) Rakaa mbili za twawaaf zinaifuata twawaaf, na ikiwa chenye kufuatwa kinaruhusiwa, basi chenye kukifuata huruhusiwa pia.
Hii ndiyo kauli ya Ash-Shaafi’iy na Ahmad, nayo imesimuliwa toka kwa Ibn ‘Umar, Ibn Az-Zubayr, ’Atwaa, Twaawus na Abu Thawr. [Al-Ummu (1/150), Al-Majmu’u (4/72) na Al-Mughniy (2/81)]
3- Kulipa Swalaah za qadhwaa katika nyakati za marufuku
Maulamaa wamekhitalifiana kuhusu hukmu ya kulipa Swalaah iliyompita mtu katika nyakati za marufuku katika kauli mbili:
Ya kwanza: Haijuzu katika nyakati za marufuku. Ni kauli ya Abu Haniyfah na Asw-Haab Ar-Raay. [Al-Mabsuwtw (1/150)]
Hoja yao ni:
1- Kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipolala ikampita Swalaah ya Alfajiri mpaka jua likachomoza, aliikawiza mpaka jua likawa angavu. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (344) na Muslim (682) toka kwa ‘Imraan bin Haswiyn].
2- Hiyo ni Swalaah, hivyo haijuzu katika nyakati hizi kama Sunnah.
3- Yaliyosimuliwa toka kwa Abu Bakrah (Radhwiya Allaahu Anhu) kwamba yeye alilala huko Daaliyah, akaamka wakati jua linakuchwa, kisha akasubiri mpaka jua likazama, halafu akaswali. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abu Shaybah (2/66) na ‘Abdul Razzaaq (2250)]
4- Yaliyosimuliwa toka kwa Ka’ab bin ‘Ajrah kwamba mwanaye alilala mpaka ilipotoka mboni ya jua, akamkalisha, na jua lilipopanda alimwambia: “Swali sasa”. [Isnadi yake ni Dhwa’iyf: At-Tirmidhiy kaitaja ikiwa Mu’allaq (1/158) na Ibn Abu Shaybah kaifanya Mawswuul (2/66)]
Ya pili: Inajuzu kuzilipa qadhwaa katika nyakati za marufuku na nyakati nyinginezo. Ni kauli ya Maalik, Ash-Shaafi’iy, Ahmad na Jamhuri ya Maswahaba na Taabi’iyna. [Al-Mudawwanah (1/130), Al-Umm (1/148), Al-Mughniy (2/80) na Al-Awsatw (2/411)]
Hoja yao ni:
1- Kauli ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Aliyelala Swalaah ikampita au akaisahau, basi aiswali anapoikumbuka, hakuna kafara yake isipokuwa hilo)). [Hadiyth Swahiyh: Imeshatajwa mara nyingi].
2- Hadiyth Marfu’u ya Abu Qataadah: ((Bali taksiri ni kwa yule ambaye hakuiswali Swalaah mpaka ukaingia wakati wa Swalaah nyingine. Mwenye kufanya hilo, basi aiswali anapozindukana)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (311) na wengineo, nayo ishaelezwa nyuma].
Katika Hadiyth hizi mbili, kuna agizo la kuswali wakati mtu anapokumbuka au anapoamka bila ya kuzivua nyakati za marufuku.
Ninasema: “Hili ndilo lenye nguvu zaidi. Ama Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuichelewesha Swalaah mpaka jua likawa angavu, ni kuwa kilichowaamsha hasa ni joto la jua. Na tushaeleza kwamba Rasuli alibainisha sababu ya kuwa mahala hapo walipolala, shaytwaan aliwahudhuria. Hivyo kizuizi cha kuswali kilikuwa ni mahala na si wakati. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
4- Kuzilipa Sunnah za rawaatib katika nyakati za marufuku
Inajuzu kuzilipa Sunnah za rawaatib ijapokuwa katika nyakati za marufuku kutokana na dalili zifuatazo:
(a) Hadiyth ya Ummu Salamah ya kwamba alimwona Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiswali rakaa mbili baada ya Alasiri. Akamuuliza sababu ya kufanya hivyo naye akajibu: ((Ee Binti Abu Umayyah! Umeuliza kuhusu rakaa mbili baada ya Alasiri. Hakika walinijia watu kutoka ukoo wa ‘Abdul Qays wakanishughulisha mpaka zikanipita rakaa mbili za baada ya Adhuhuri, nazo ndizo hizi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1233) na Muslim (297)].
(b) Yaliyosimuliwa toka kwa Qays bin ‘Amri akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliniona nikiswali rakaa mbili za Alfajiri baada ya Swalaah ya Alfajiri akaniuliza: ((Rakaa hizi mbili ni za nini ee Qays?)) Nikasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Sikuwa nimeswali rakaa mbili za Alfajiri, naye akanyamaza”. [Hadiyth Hasan kwa Sanad zake: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1267), At-Tirmidhiy (422) na Ahmad (5/447). Ni Hadiyth Mursal, nayo ina Sanad nyingine kwa Ibn Al-Mundhir katika Al-Awsatw (2/391), Al-Haakim (1/273), na Al-Bayhaqiy (2/483). Na kwa ujumuisho wa yote, ni Hadiyth Hasan]
Na katika riwaya nyingine: “Rasuli hakumkatalia hilo”.
(c) Kutokana na ujumuishi wa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Mwenye kuisahau Swalaah, basi aiswali anapoikumbuka)). Hii ni kauli ya Maalik na Ash-Shaafi’iy. [Bidaayatul Mujtahid (1/137) na Al-Ummu (1/149)]
5- Swalaah ya maiti baada ya Alfajiri na Alasiri
Maulamaa wote wamekubaliana kwamba inajuzu kumswalia maiti baada ya Swalaah ya Alfajiri na Alasiri. [Ibn Qudaamah ameinukuu katika Al-Mughniy (2/82)]
Kisha wakakhitalifiana kuhusiana na kuiswali Swalaah hii katika nyakati zilizotajwa katika Hadiyth ya ‘Uqbah bin ‘Aamir ambazo ni wakati jua linapochomoza mpaka lipande, wakati linapolingamana sawa Adhuhuri mpaka lipinduke, na wakati linapokurubia kuchwa mpaka lichwe. Wamekhitalifiana kuhusu nyakati hizi tatu katika kauli mbili:
Ya kwanza: Haijuzu kuswalia maiti katika nyakati hizi tatu. Ni kauli ya Abu Haniyfah, Maalik, Ahmad na Maulamaa wengi. [Al-Mudawwanah (1/190), Al-Mabsuutw (1/152), Al-Mughniy (2/82) na Maalim As-Sunan (1/313)].
Na hii ni kwa Hadiyth ya ‘Uqbah bin ‘Aamir isemayo: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitukataza kuswali katika nyakati tatu na kuwazika maiti wetu katika nyakati hizo…akazitaja”. [Hadiyth Swahiyh: Imeelezwa karibuni hivi].
Ya pili: Inajuzu kuswalia maiti katika nyakati zote zilizokatazwa. Ni kauli ya Ash-Shaafi’iy na riwaya toka kwa Ahmad. [Al-Ummu (1/150) na Al-Majmu’u (4/68)] Hoja ya Ash-Shaafi’iy ni kuwa Swalaah hii ina sababu, na hivyo inatolewa nje ya wigo wa umarufuku.
Ninasema: “Linaloonekana ni kuwa Swalaah hii haijuzu katika nyakati hizi tatu kwa ajili ya Hadiyth, kwa kuwa ndani ya Hadiyth, pamoja na kukatazwa Swalaah, pamekatazwa pia kuzika maiti katika nyakati hizo. Hivyo inazuilika kuivua Swalaah na katazo. Isitoshe, nyakati hizi tatu ni fupi na hakuna kinachochelewa ikiwa patasubiriwa mpaka zimalizike. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.”
6- Swalaah zenye sababu
Ni kama Swalaah ya maamkizi ya Msikiti, Sunnah ya wudhuu, Swalaah ya Kupatwa Jua na mfano wake. Kisha Maulamaa wamekhitalifiana kuhusu suala hili juu ya kauli mbili:
Ya kwanza: Haijuzu kuziswali katika nyakati zilizokatazwa. Ni madhehebu ya Abu Haniyfah na mashuhuri katika madhehebu ya Ahmad. [Al-Mabsuutw (1/152), Sharhu Fat-hul Qadiyr (1/204) na Al-Mughniy (2/90)]
Ya pili: Inajuzu. Ni kauli ya Ash-Shaafi’iy, na riwaya ya pili toka kwa Ahmad. Hoja yao ni:
1- Imethibiti kuwa inajuzu kuswali rakaa mbili za twawaaf wakati wowote. Hili lishaelezwa nyuma.
2- Imethibiti kuwa inajuzu kuswali baada ya kutawadha wakati wowote ule kama ilivyo katika Hadiyth ya Bilaal wakati Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomwambia: ((Nielezee amali yenye matarajio zaidi uliyoifanya katika Uislamu)). Bilaal akasema: “Sikufanya amali yoyote yenye matarajio makubwa kwangu zaidi ya kuwa sikupata kujitwaharisha wakati wowote wa usiku au mchana, ila huswali kwa twahara hiyo kile nilichoandikiwa kukiswali”. [Hadiyth Swahiyh: Imeelezwa katika mlango wa wudhuu].
3- Neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusiana na kupatwa jua: ((Mnapoliona limepatwa, basi kimbilieni kwenda kuswali. [Hadiyth Swahiyh: Itakuja katika mlango wa Swalaah ya kupatwa jua na mwezi].
4- Ni kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Anapoingia mmoja wenu Msikitini, asiketi mpaka aswali rakaa mbili. [Hadiyth Swahiyh: Itakuja katika mlango wa Swalaah za Sunnah].
5- Imethibiti kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali Sunnah ya Adhuhuri baada ya Alasiri kama tulivyoeleza kabla.
6- Ijma’a ya Maulamaa wanaosema kwamba inajuzu kumswalia maiti baada ya Alfajiri na Alasiri.
Wanasema: “Swalaah zote hizi ni Swalaah zenye sababu na imejuzu kuziswali wakati wowote, nazo haziko ndani ya wigo wa katazo”.
Ninasema: “Madhehebu haya yanatolewa dalili vile vile na haya yafuatayo:
7- Hadiyth ya Abu Dharr wakati Rasuli Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam alipomwambia: ((Ee Abu Dharr! Utafanyaje ikiwa viongozi wako wanaiua Swalaah (au alisema) wanaichelewesha Swalaah na wakati wake?)) Nikamjibu: “Unaniamuru nini?” Akasema: ((Swali Swalaah katika wakati wake, na ikiwa utaiwahi pamoja nao basi swali, kwani hiyo itakuwa ni ziada kwako)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (648) na Abu Daawuud (431). Angalia Taadhiymu Qadris Swalaat (1008) nilichokifanyia uhakiki].
Na katika Hadiyth Mawquuf ya Ibn Mas-’oud: (( Watakuja viongozi watakaoitendea Swalaah ubaya, wataisonga mpaka mwisho wa mchana)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (534) na wengineo. Angalia Qadrus Swalaat (1015) nilichokifanyia uhakiki].
Na ametaja mfano wa Hadiyth ya Abu Dharr, akajuzisha Swalaah ya Sunnah katika wakati wa karaha kwa sababu iliyotajwa.
8- Hadiyth ya Yaziyd bin Al-Aswad aliyesema: “Nilikuwa pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hijjah yake. Nikaswali pamoja naye Swalaah ya Alfajiri katika Msikiti wa Al-Khayf. Alipomaliza Swalaah yake na kuondoka, mara walikuja watu wawili katika watu waliochelewa ambao hawakuwahi kuswali pamoja naye. Akasema: ((Nitawafuatia)). Wakaletwa huku vifua vyao vikitetema. Akawauliza: ((Kitu gani kimewazuia msiswali nasi?)) Wakasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Hakika sisi tulikuwa tumeswali safarini. Akawaambia: ((Msifanye! Mkiswali safarini, kisha mkaja Msikiti wa Jamaa, basi swalini pamoja nao, kwani hiyo ni ziada kwenu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (219), An-Nasaaiy (2/112) na wengineo].
Al-Khattwaabiy kasema: “Katika neno lake: ((kwani hiyo ni ziada kwenu)), ni dalili kwamba Swalaah ya Sunnah inajuzu baada ya Alfajiri kabla ya kuchomoza jua ikiwa Swalaah ina sababu”. [Maalimus Sunan (1/165)]
Ninasema: “Juu ya msingi wa tuliyoyazungumzia, katazo la kuswali katika nyakati zilizotajwa katika Hadiyth, linahusiana hasa na Sunnah zisizo na sababu yoyote, na kwa mtu aliyekusudia kwa ari kuziswali katika nyakati hizo. Hili linatiliwa nguvu na Hadiyth ya Ibn ‘Umar kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anasema: ((Asipanie mmoja wenu akaswali wakati wa kuchomoza jua wala wakati wa kuchwa kwake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (585) na Muslim (828)].
·
Faida
Nyakati zilizokatazwa kuswali tulizozielezea, ni zile ambazo katazo linafungamana na nyakati za asili. Kuna nyakati nyinginezo ambazo Swalaah imekatazwa kutokana na kufungamana kwake na jambo ambalo liko nje ya asili ya wakati. Litakuja kuelezewa kichambuzi katika sehemu zake katika mlango wa Swalaah za Sunnah Insha-Allaah.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
009-Adhana Na Iqaamah
Alhidaaya.com [3]
Taarifu:
[Al-Lisaan, Al-Miswbaahul Muniyr, Sharhu Muntahaa Al-Iraadaat (1/122) na Al-Mumti’i (35-36)]
Maana ya adhana kilugha ni kutangaza. Allaah Anasema:
((وَأَذِّن فِي النَّاسِ بِالْحَجِّ))
((Na tangaza kwa watu Hajj)) [Al-Hajji (27:22)]
Ama kisharia, ni kutaabudia kwa Allaah Mtukufu kwa kutangazia kuingia wakati wa Swalaah kwa utajo maalumu.
Iqaamah kilugha, ni kisoukomo cha kitenzi ((أقام)) kutokana na sentensi ya أقام الشيء , anapokinyoosha mtu kitu kikanyooka. Pia neno hili lina maana nyinginezo kama kutulia, kudhihirisha na kuita. Ama kishariah, ni kutaabudia kwa Allaah kwa ajili ya kusimama na kuswali kwa utajo maalumu.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
010- Kwanza: Adhana
Alhidaaya.com [3]
Fadhila Za Adhana:
1- Imepokelewa na Abuu Hurayrah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Swalaah inapoadhiniwa, shaytwaan hukimbia na kupiga mashuzi ya sauti ili asiisikie adhana, na adhana inapomalizika hurudi tena. Inapoqimiwa Swalaah hukimbia, na inapomalizika huja tena akaingia kati ya mtu na nafsi yake akimwambia: “Kumbuka kadha, kumbuka kadha”, na huendelea kumsonga mtu hivyo mpaka anakuwa hajui ni rakaa ngapi kaswali)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (608) na Muslim (389)].
2- Abuu Sa’iyd Al-Khudriy alimwambia Ibn Abiy Swa’aswa’a: “Nakuona unapenda kondoo na nyika. Basi unapoadhini ukiwa na kondoo wako au nyikani, nyanyua sauti yako ya adhana kwani:
((Hausikii upeo wa mwisho wa sauti ya mwadhini jini, au mwanadamu au kitu chochote ila watamshuhudilia Siku ya Qiyaamah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (609) na An-Nasaaiy (2/12)].
Abuu Sa’iyd akasema: “Nimeyasikia toka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
3- Abuu Hurayrah anasema kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:
(( Lau kama watu wangelijua fadhila zilizopo kwenye adhana na safu ya kwanza, kisha wasipate njia ya kuzipata ila kwa kupiga kura, basi wangelipiga kura. Na lau wangelijua fadhila za kuwahi mapema (Msikitini), basi wangelishindania. Na lau wangelijua fadhila za ‘Ishaa na Alfajiri, basi wangeliziendea hata kwa kutambaa)).[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (615) na Muslim (437].
4- Mu’aawiyah bin Abiy Sufyaan (Radhwiya Allaahu Anhu) anasema: Rasuli wa Allaah Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam anasema:
((Waadhini ndio watu wenye shingo ndefu zaidi Siku ya Qiyaamah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (387), Ibn Maajah (725) na Ahmad (4/95)].
5- ‘Uqbah bin ‘Aamir anasema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:
((Mola wenu Anapendezwa sana na mchunga kondoo aliyeko juu kileleni mlimani; anaadhini kwa ajili ya Swalaah, kisha anaswali. Hapo Allaah ‘Azza wa Jalla Husema: Mtazameni Mja Wangu huyu! Anaadhini na kuisimamisha Swalaah, ananiogopa Mimi. Hakika Mimi Nimemghufiria Mja Wangu na Nimemwingiza peponi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (1203), An Nasaaiy (2/20) na Ahmad (4/158)].
6- Abuu Hurayrah anasema kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:
((Imamu ni mdhamini, na mwadhini ameaminiwa, Allaah Awaongoe maimamu, na Awaghufirie waadhini)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa“ikhraaj” na Abuu Daawuud (517), At-Tirmidhiy (207) na Ahmad (2/284-419). Angalia Al-Irwaa (1/231)].
7- Kuadhini kuna ubora zaidi kuliko uimamu. Ni kwa Hadiyth zilizotangulia kuhusu fadhila za adhana, na kwa kuwa imamu ni mdhamini, na mwadhini ni mwaminiwa. Kuaminiwa na watu kuna uzito zaidi kuliko udhamini, na maghfirah iko juu kuliko hidaayah. Lakini pamoja na hivyo, Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakufanya kazi ya kuadhini wala Makhalifa Waongofu, kwa vile uimamu ni jukumu lao la wajibu na ni kazi adhimu. Haikuwezekana kuzifanya kazi zote mbili kutokana na ufinyu wa wakati na kushughulishwa na mengineyo muhimu zaidi kama kuendesha mambo ya Waislamu. Uimamu ukawa na fadhila zaidi kwao kuliko adhana kutokana na umahususi wa hali yao ingawa adhana kwa watu wengine ina ubora zaidi.
Haya ndio madhehebu ya Ash Shaafi’iy na riwaya mbili sahihi zaidi toka kwa Ahmad. Masahibu zake wengi wamelikhitari hili pamoja na Maalik. Pia Shaykh wa Uislamu Ibn Taymiyya ameliunga mkono. [Al-Mughniy (1/402), Al-Majmu’u (3/74), Mawaahibul Jaliyl (1/422) na Al-Ikhtiyaaraat (uk 36)]
·
Mwanzo Wa Kupitishwa Adhana Kisharia
Adhana ilipitishwa kisharia mwaka wa kwanza wa Hijrah huko Madiynah kwa mujibu wa Hadiyth Swahiyh zilizokuja kuhusiana na hilo. Kati ya hizo ni Hadiyth ya Ibn ‘Umar aliyesema:
“Waislamu walipokuja Madiynah, walikuwa wakikusanyika na kusubiri Swalaah bila kuwepo adhana. Siku moja wakalizungumzia hilo. Baadhi wakasema: “Tupigeni kengele kama wanavyofanya Manaswara”. Wengine wakasema: “Tupulizeni tarumbeta kama ya Mayahudi”. ‘Umar akawaambia: “Kwa nini msimpeleke mtu akaadhini?” Hapo hapo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:
((Ee Bilaal! Simama uadhini)) [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (604) na Muslim (377)].
·
Hukmu Ya Adhana
Umma wa Kiislamu, umeafikiana wote kwamba adhana imepitishwa kisharia na imekuwa ikifanywa tokea enzi ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mpaka hivi leo bila mvutano wowote.
Maulamaa wametofautiana kuhusiana na hukmu yake kama ni wajibu au ni Sunnah iliyokokotezwa?
La sahihi lisilo na shaka yoyote katika mfano wa ‘ibaadah hizi tukufu ni kuwa adhana ni faradhi ya kutoshelezana. Si wajibu kwa wakazi wa mji au kijiji kufanya adhana na iqaamah. Hili linatolewa dalili kwa haya yafuatayo:
1- Adhana ni moja kati ya alama tukufu na mashuhuri kabisa za utambulisho wa Uislamu na dini. Na tokea Allaah (Subhaanahu wa Taalaa) kuiweka kisharia, adhana iliendelea kupigwa nyakati zote na katika hali zote mpaka alipokufa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Hatujasikia kabisa kwamba iliwahi kuachwa au kutolewa ruksa ya kuiacha.
2- Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameifanya kuwa ni nembo ya Uislamu, dalili ya mtu kushikamana nao na kuingia ndani yake. Imepokelewa na Anas akisema:
“Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapotuongoza kuwashambulia watu vitani, alikuwa hatuamuru kushambulia mpaka iingie asubuhi, halafu husikilizia. Akisikia wanaadhini, basi huwaacha, na kama hakusikia, huwashambulia”.[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (610) na Muslim (382)].
3- Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameamuru adhana iadhiniwe. Imepokelewa na Maalik bin Al-Huwayrath (Radhwiya Allaahu Anhu) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia yeye na wenzake:
((Wakti wa Swalaah unapoingia, aadhini mmoja wenu na mkubwa wenu awe imamu wenu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (631) na Muslim (674)].
4- Imepokelewa na Anas bin Maalik akisema: “Bilaal aliamuriwa aifanye adhana shufwa, na iqaamah witri”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (605) na Muslim (378).
5- Katika Hadiyth ya ‘Abdullah bin Zayd kuhusu njozi yake ya adhana, Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema:
((Hakika hiyo ni njozi ya kweli, In Shaa Allaah)), [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (499), At-Tirmidhiy (189), Ibn Maajah (706) na wengineo]….kisha akaamuru iadhiniwe.
6- Ni neno lake Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kumwambia ‘Uthmaan ibn Abil ‘Aasiy:
((Mweke mwadhini asiyechukua malipo kwa kazi hiyo)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (531), An-Nasaaiy (672), At-Tirmidhiy (209) na Ibn Maajah (714)]
7- Imepokelewa na Abud Dardaai akisema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
((Hakuna katika watatu ambao adhana haiadhiniwi wala Swalaah haiqimiwi baina yao, ila shaytwaan huwatalawa)). [Isnadi yake ni laini: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (547), An-Nasaaiy (847) na Ahmad (6/446), na ziada ni yake].
Hadiyth hii inaonyesha wajibu wa adhana, kwa kuwa kuliacha lile ambalo ni aina ya kutawaliwa na shaytwaan, ni lazima kuliepuka.
Maalik na Ahmad wanasema kwamba adhana ni lazima na hususan katika Misikiti mikubwa inayoswaliwa jamaa. Hili kwa Mashaaf’iy lina walakini. ‘Atwaa, Mujaahid, Al-Awzaaiy, Daawuud na Ibn Hazm wamesema hivyo hivyo. Ibn Al-Mundhir na Sheikh wa Uislam Ibn Taymiyyah wamelikhitari hilo. [Al-Inswaaf (1/407), Mawaahibul Jaliyl (1/422), Rawdhwat At-Twaalibiyn (1/195), Al-Awsatw (3/24), Majmu’u Al-Fataawaa (22/64) na As Saylul Jarraar (1/196)]
Lakini Abuu Haniyfah na Ash-Shaafi’iy, wao wanasema kwamba adhana ni Sunnah iliyokokotezwa!!
Ninasema: “Hapana shaka kwamba kauli ya kwanza kuwa ni wajibu, ndiyo yenye nguvu zaidi. Kisha Mahanafi wanaosema kwamba ni Sunnah, wameeleza kwamba Sunnah hii ni kama wajibu katika kupata madhambi, kana kwamba khilafu yao ni ya kilafudhi. [Ibn ‘Aabidiyn (1/384) na Fat-hul Qadiyr (1/240)]
Na Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi”.
·
Faida
1- Adhana kwa wasafiri:
Wasafiri ni lazima waadhini wakitaka kuswali kama ilivyo kwa wakazi. Hii ni kutokana na ujumuishi wa dalili, Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuendelea kulifanya hilo akiwa mjini au safarini, na kumwamrisha Maalik ibn Al-Huwayrath na wenzake kuadhini walipokuwa safarini kurudi kwa jamaa zao. Na hili ndilo la sawa kinyume na madhehebu ya Hanbali na Jamhuri.
2- Swalaah ya kulipwa iadhiniwe:
Ni lazima kuadhini kwa Swalaah zote tano za faradhi, sawasawa ikiwa zinaswaliwa katika wakati wake au zinalipwa qadhwa. Katika milango iliyopita, tuliisoma Hadiyth iliyozungumzia kuhusu kupitiwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba zake na usingizi, ikawapita Swalatul Fajr mpaka jua likachomoza wakati walipokuwa safarini. Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwamuru Bilaal aadhini na aqimu.
Jingine linaloonyesha hilo ni ujumuishi wa kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa Maalik ibn Al-Huwayrath alipomwambia:
((Wakati wa Swalaah unapoingia, aadhini mmoja wenu..))
Lakini, lau kama watu watalala (katika mji fulani ugenini), na usingizi ukawachukua mpaka wakati wa Swalaah ukatoka, huku adhana ikiwa iliadhiniwa katika mji huo, basi si lazima kuadhini, kwani adhana hiyo itatosheleza, na faradhi ya adhana itawaondokea. [Mengi zaidi ya faida yako kwenye Ash-Sharh Al-Mumti’i (2/41). Angalia yaliyozungumzwa nyuma katika mlango wa kulipa Swalaah zilizopita]
3- Hukmu ya kuadhini wanawake na kuqimu:
[Al-Mughniy (1/422), Al-Majmu’u (3/98), Al-Badaai-’i (1/135), Minahul Jaliyl (1/120), Al-Awsatw (3/53), na Jaami’u Ahkaamin Nisaa cha Sheikh wetu (1/299)]
- Si lazima kwa wanawake kuadhini wala kuqimu kwa rai ya Jamhuri ya Salaf na Khalaf kati ya Maimamu wanne na Adh-Dhwaahiriyya. Imeripotiwa Marfu’u toka kwa Asmaa: “Wanawake hawana adhana, wala iqaamah wala Ijumaa”. [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bayhaqiy (1/408)]
Hadiyth hii ni Dhwa’iyf, haifai. Lakini pamoja na hivyo, haikuja amri yoyote kwa wanawake ya kuadhini au kuqimu.
- Haijuzu (bali haitoshelezi) adhana ya mwanamke kwa wanaume kwa mujibu wa rai ya Jamhuri kinyume na Hanafiy, kwa kuwa adhana ni tangazo na ilivyo kisharia, ni kunyanyua sauti, na mwanamke haijuzu kunyanyua sauti yake kisharia. Haikusikiwa kamwe katika masiku ya Rasuli, wala Maswahaba zake, wala waliokuja baada yao kwamba mwanamke aliadhini adhana ya kisharia ya kutangazia kuingia wakati na kuwaita watu kwenda kuswali.
- Maulamaa wametofautiana kuhusiana na adhana na iqaamah kwa wanawake ikiwa wako peke yao mbali na wanaume. Yaliyosemwa ni:
Yote mawili ni karaha, yote mawili yanafaa, yote mawili ni mustahabu, imesuniwa iqaamah bila adhana.
Linaloonekana kuwa ni la nguvu ni kuwa kama wanawake wako peke yao mbali na wanaume, kuadhini na kuqimu itakuwa ni vizuri zaidi kwao, kwa kuwa mawili hayo ni kumdhukuru Allaah Mtukufu, na hakuna lolote lililopokelewa kuzuia hilo. Ibn ‘Umar aliulizwa: “Je, wanawake waadhini?” Alighadhibika na kujibu: “Nikataze kudhukuriwa Allaah?!!” [Isnadi yake ni Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (1/223)].
Imepokelewa toka kwa Mu’utamir bin Sulaymaan toka kwa baba yake akisema: “Tulikuwa tukimuuliza Anas: “Je, ni lazima kuadhini na kuqimu kwa wanawake?” Akajibu: “Hapana, lakini kama watafanya, basi hilo ni dhikri” [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (1/223)].
Na hii ni kauli ya Ash-Shaafi’iy na riwaya toka kwa Ahmad, na Ibn Hazm ana msimamo huu huu. [Al-Ummu (1/84), Al-Mughniy (1/422) na Al-Muhallaa (3/129)]
Ash-Shaafi’iy amesema: “Mwanamke hanyanyui sauti yake, ataadhini kwa sauti ya kujisikia mwenyewe au ya kusikiwa na wenzake, na hivyo hivyo atakapoqimu”.
4- Adhana ya mwenye kuswali peke yake ikiwa watu washaswali jamaa Msikitini:
Mtu mwenye kuswali peke yake katika mji ambao adhana ilikwisha adhiniwa, anaweza kutosheka na adhana hiyo iliyoadhiniwa. Lakini ikiwa ataadhini na kuqimu, itakuwa ni vizuri zaidi kwa ajili ya kuipata fadhila ya adhana. Na hii ni kutokana na Hadiyth ya Abuu Sa’iyd na ‘Uqbah bin ‘Aamir iliyotangulia katika mlango wa fadhila za adhana.
Aidha, kama jamaa imempita akaingia katika Msikiti ambao watu wake washaswali, ikiwa atatosheka na adhana yao, basi itamtosheleza. Lakini ni bora kwake kuadhini na kuqimu kama alivyofanya Anas ibn Maalik. Imepokelewa na Abuu ‘Uthmaan akisema: “ Alitujia Anas ibn Maalik katika Msikiti wa Bani Tha’alabah akauliza: “Je, mshaswali?” (ilikuwa swala ya Alfajiri). Tukamjibu ndio. Akamwambia mtu aadhini. Akaadhini na kuqimu, kisha wakaswali jamaa”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (1/221)].
Hivi ndivyo walivyosema Ash-Shaafi’iy na Ahmad. Lakini Maalik na Al-Awzaa’iy wanasema kuwa ataqimu tu bila kuadhini. Naye Abuu Haniyfah na wenzake wanasema kuwa haadhini wala haqimu. [Al-Ummu (1/84), Al-Mughniy (1/418), Al-Mudawwanah (1/61) na Al-Awsatw (3/60-62)]
5- Adhana ya Swalaah mbili za kukusanywa:
Zikikusanywa Swalaah mbili katika wakati wa mojawapo kama kukusanya Alasiri na Adhuhuri katika wakati wa Adhuhuri ‘Arafah, au kukusanya Magharibi na ‘Ishaa Muzdalifah, itatosheleza adhana moja tu, lakini kila Swalaah itaqimiwa kwa iqaama yake kama alivyofanya Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Haya ndiyo waliyoyasema Jamhuri kinyume na mashuhuri kwa Maalik anayesema kwamba kila Swalaah itaadhiniwa kivyake!! [Al-Badaai-’i (1/152), Al-Majmu’u (3/83), Mawaahibul Jaliyl (1/468), na Al-Mumti’i (2/41)]Yatafafanuliwa zaidi katika mlango wa Hajji.
6- Swalaah zinazoadhiniwa kisharia:
Maulamaa wamekubaliana kwamba adhana kisharia, ni kwa Swalaah tano tu za faradhi. Swalaah nyinginezo kama ya Maiti, Witri, ‘Iyd Mbili na kadhalika hazina adhana. Kwani lengo la adhana, ni kutangazia kuingia wakati wa Swalaah, na Swalaah tano za faradhi zimepangiwa nyakati zake maalumu. Ama Swalaah za Sunnah, hizo ziko chini ya Swalaah za faradhi, na adhana ya asili ya Swalaah ya faradhi, hujumuisha na Swalaah husika za Sunnah. Ama Swalaah ya maiti, Swalaah hii si Swalaah kiuhakika, kwani haina kisomo, wala rukuu wala sujudi.
Na kati ya yaliyokuja kuhusiana na hili, ni Hadiyth ya Jaabir bin Samrah asemaye: “Niliswali pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ‘Iyd, si mara moja wala mbili bila ya adhana wala iqaamah”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (887), Abuu Daawuud (1148) na At-Tirmidhiy (532).
·
Vipi Hutangaziwa Swalaah Zisizo Na Adhana?
Ash-Shaafi’iy anaona kwamba kila Swalaah isiyo na adhana, hunadiwa kwa neno: " الصلاة جامعة ". Mahanbali wamekubaliana naye lakini katika Swalaah za ‘Iyd, Kupatwa Jua na Kuomba Mvua tu. Ama Mahanafi na Maalik wamekubaliana naye katika Swalaah ya Kupatwa Jua basi. [Ibn ‘Aabidiyn (1/565), Al-Majmu’u (3/77), Al-Mawaahib (1/435) na Kash-Shaaf Al-Qinaa (1/211)]
Ninasema: “La sawa ni kuegemezwa na kudhibitiwa hili kwa Aayah au Hadiyth. Swalaah iliyothibitishwa kwa Aayah au Hadiyth hunadiwa kwa kusema: " الصلاة جامعة ", basi ni Sunnah kufanya, na kama hakuna, basi isifanywe. Maelezo yake kiuchambuzi yatakuja katika milango husika InshaAllaah.
·
Masharti Ya Adhana
1- Ni kuingia wakati wa Swalaah (isipokuwa Swalaah ya Alfajiri)
Sharti ya adhana ni kuingia wakati wa Swalaah ya Fardhi. Haitofaa kuadhini kabla ya wakati kuingia (isipokuwa kwa Swalaah ya Alfajiri kwa ufafanuzi utakaokuja baadaye). Wakati unapoingia, imesuniwa kuadhini mwanzo wake ili watu wajue na waanze kujiandaa kwa ajili ya Swalaah. Imepokelewa na Jaabir bin Samrah akisema:
“Bilaal alikuwa akiadhini jua linapopinduka, haachi kitu katika matamshi yake. Kisha haqimu mpaka Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amtokee. Anapotoka, huqimu anapomwona”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (606), Abuu Daawuud (537) na At-Tirmidhiy (202) na Ahmad (5/91).
Ama Alfajiri, Maalik, Ash-Shaafi’iy, Al-Awzaa’iy, Ahmad, Is-haaq, Abuu Thawr, Abuu Yuusuf na Ibn Hazm, hawa wanasema kwamba adhana ya Alfajiri kisharia, inaweza kuadhiniwa kabla ya wakati (kabla ya kuchomoza Alfajiri ya kweli). [Al-Mudawwanah (1/60), Al-Ummu (1/83), Masaail Ahmad cha ‘Abdullaah (58), Al- Majmu’u (3/88), Al-Awsatw (3/29) na Al-Muhallaa (3/160)] Ni kwa Hadiyth ya Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu Anhumaa) anayesema kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Bilaal huadhini usiku, basi kuleni na kunyweni mpaka Ibn Ummi Maktoum aadhini)).
Anasema: “Alikuwa ni kipofu, haadhini mpaka aambiwe: Alfajiri imeingia, Alfajiri imeingia. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (617), na ziada ni yake, na Muslim (1092)].
Adhana ya kwanza inakuwa kwa ajili ya kumwamsha aliyelala ili aanze kujitayarisha kwa Swalaah, na ili kumpunguza kasi mwenye kuswali tahajudi apate kupumzika na kupata kuswali Swalaah ya Alfajiri kwa uchangamfu, au apate kula daku kama ana niya ya kufunga. Ni kama ilivyo katika Hadiyth ya Ibn Mas-’oud kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:
(( Isimzuie mmoja wenu adhana ya Bilaal kula daku, kwani yeye anaadhini usiku ili kumtua mwenye kuswali kati yenu, na kumwamsha aliyelala kati yenu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (621) na Muslim (1093)].
Jamhuri imestahabu adhana ya pili unapoingia wakati. Wanaona kwamba inajuzu kutosheka nayo kwa kunadi “Swalaah”!! La sahihi ni lile alilolifuata Ibn Al-Mundhir na Ibn Hazm wanaosema kwamba ni lazima adhana ya pili iliyo katika wakati, kwa kuwa ndio asili. Kwani Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Wakati wa Swalaah unapoingia, aadhini mmoja wenu)), na hii ni kwa Swalaah zote; haitolewi Swalaah yoyote kando, wala halipingwi na Hadiyth: ((Bilaal huadhini usiku)), kwa kuwa adhana hii si kwa ajili ya Swalaah ya Alfajiri kama ilivyotangulia.
Lakini Ath-Thawriy na Abuu Haniyfah [Al-Muhallaa (3/163), Al-Majmu’u (3/88), Al-Awsatw (3/30) na Al-Mabsuutw (1/134)]….wanaona kwamba Alfajiri haiadhiniwi mpaka baada ya kutoka Alfajiri ya kweli kupimia na Swalaah zinginezo, na kwa yaliyosimuliwa toka kwa Shaddaad mwachwa huru wa ‘Ayyaadh bin ‘Aamir kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia Bilaal:
((Usiadhini mpaka uione Alfajiri)). [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (534). Al-Bayhaqiy ameikosoa kwamba ina mkatiko. Ibn Al-Qattaan amesema: “Shaddaad hajulikani”. Angalia Nasb Ar-Raayah (1/283)].
Hadiyth hii haifai.
Na kwa yanayosimuliwa toka kwa Ibn ‘Umar kwamba Bilaal aliadhini kabla ya kuchomoza Alfajiri, Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwamuru arejee anadi: “Jueni kwamba mja alilala”. [Al-Muhallaa (3/163), Al-Majmu’u (3/88), Al-Awsatw (3/30) na Al-Mabsuutw (1/134)]
Hii pia imekosolewa na Maulamaa wa Hadiyth, haifai kwa hoja.
Ama kipimo chao, hicho kiko mkabala na Hadiyth zilizotangulia katika kuithibitisha adhana kabla ya Alfajiri, nazo zinaonyesha kuwa Bilaal alidumu na hilo. Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimkubalia hilo na wala hakumkataza, ikathibiti kujuzu kwake bali kuwa mustahabu. Ama Hadiyth walizozitolea hoja, zote zina kasoro na hazifai kwa hoja, mbali na kujibiwa na Hadiyth Swahiyh zilizothibiti.
2- Niya ya adhana:
Ili adhana iswihi, ni lazima pawepo niya kama zilivyo ‘ibaadah nyinginezo kwa kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
((Hakika amali ni kwa niya)). [Hadiyth Swahiyh: Tumeitaja sehemu nyingi].
Ikiwa mtu ameanza kumdhukuru Allaah kwa takbiyr, kisha baada ya takbiyr akaona aunganishe adhana, basi itabidi aanze tena mwanzo wala asijengee juu ya aliyoyasema. Haya ni madhehebu ya Maalik na Hanbali. [Mawaahibul Jaliyl (1/424) na Muntahaa Al-Iraadaat (1/129)]
3- Iwe kwa Lugha ya Kiarabu
[Ibn ‘’Aabidiyn (1/256), Kash-Shaaf Al-Qinaa (1/215) na Al-Majmu’u (3/129)]
Ni lazima matamshi ya adhana yawe kwa Lugha ya Kiarabu. Haifai kwa lugha nyingine yoyote hata kama itajulikana kwamba ni adhana. Haya ni madhehebu ya Hanafi na Hanbali. Shaafi’i wanaona hivyo hivyo isipokuwa wanasema kwamba ikiwa hakuna anayejua Kiarabu, basi itawatosheleza kwa lugha nyingine.
4- Kutokuwepo makosa yanayogeuza maana
[Ibn ‘’Aabidiyn (1/259), Muntahaa Al-Iraadaat (1/130), Al-Mawaahib (1/438) na Al-Majmu’u (3/425)]
Ni kama kuvuta “Hamzah ya (Akbar) au “Baa” yake na mengineyo yenye kugeuza maana. Pia kuvuta zaidi ya mpaka unaotakiwa. Ikiwa maana itakuwa haifahamiki, basi adhana ni batili, na kama ina makosa, inakuwa ni makruhu kwa Jamhuri kinyume na Mahanafi.
5- Matamshi yake yawe katika mpangilio
[Al-Badaai-’i (1/149), Mughniy Al-Muhtaaj (1/137), Al-Iraadaat (1/128) na Al-Mawaahib (1/425)]
Mwadhini ni lazima ayalete matamko ya adhana kwa mfumo na utaratibu uliokuja katika Sunnah (utakaokuja kuelezwa baadaye kidogo) bila kutanguliza au kuakhirisha neno juu ya jingine au sentensi juu ya nyingine. Ikiwa mwadhini atafanya hivyo, basi ni lazima aanze tena upya (kwa mujibu wa Jamhuri kinyume na Hanafiy) kwa kuwa kuacha mpangilio, hupindisha ujulisho uliokusudiwa. Haifai kupangua mtiririko huu kwa kuwa adhana ni dhikri inayotambulika hivyo. Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(Mwenye kufanya tendo lolote ambalo si amri yetu, basi hurejeshewa mwenyewe)). [Hadiyth Swahiyh: Al Bukhaariy kwenye I’itiswaam ameifanya “Mu’allaq”, Muslim (1718) na wengineo ameifanya “Mawswuul”].
6- Kuandamisha kati ya matamko ya adhana
[Rejea zilizotangulia]
Ni kufuatanisha kati ya matamko bila kuyakata kwa neno au tendo. Ikiwa mwadhini atakata kidogo kwa chafya wakati wa adhana, basi ataendelea pale alipokomea kwa mujibu wa rai ya Jamhuri. Na kama mkato utakuwa mrefu kati ya matamko kwa maneno mengi, au kupotewa na fahamu na mfano wake, basi adhana itabatilika, na ni lazima aanze tena mwanzo. Haifai kuendeleza pale alipokomea, bali lazima aanze tena upya.
7- Waisikie walio mbali
[Rejea zilizotangulia]
Hii ni ima kwa kupaza sauti au kutumia kipaza sauti ili makusudio ya adhana yapatikane. Na kama anajiadhinia mwenyewe, basi si lazima anyanyue sauti isipokuwa kwa kiasi cha kujisikia yeye mwenyewe au aliye pamoja naye. Imetangulia katika Hadiyth ya Abuu Sa’iyd:
((Nyanyua sauti yako ya adhana, kwani hausikii upeo wa mwisho wa sauti ya mwadhini jini, au mwanadamu au kitu chochote ila watamshuhudilia Siku ya Qiyaamah)). [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa kwenye mlango wa (Fadhila za adhana)].
Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia ‘Abdullaah bin Zayd:
((Mfundishe Bilaal adhana, kwani yeye ana sauti kali nzuri na pumzi ndefu kuliko wewe)). [Hadiyth Hasan: Imetajwa katika (Hukmu za adhana)].
Haya ni madhehebu ya Shaafi’i na Hanbali, na kauli kwa Mahanafi. Ni Sunnah kwa Maalik, na jambo muhimu kwa Mahanafi.
·
Je, Inatosheleza Kurusha Adhana Kupitia Redio?
[Ash-Sharhul Mumt’i (2/61-62) kwa maana yake]
Kurusha adhana kwa njia ya redio au tapurikoda si sahihi, kwa kuwa adhana ni ‘ibaadah ambayo kama tulivyotangulia kusema ni bora kuliko hata uimamu. Na kama ambavyo haisihi watu kufuata Swalaah ya kurekodiwa, hali ni hivyo hivyo kwa upande wa adhana. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.
·
Je, Inafaa Kuzungumza Wakati Wa Adhana Na Iqaamah?
Maulamaa wamekhitilafiana kuhusiana na hukmu ya kuzungumza mwadhini wakati anaadhini katika kauli zifuatazo:
[Al-Awsatw (3/43), Masaail Ahmad cha Abuu Daawuud (27), Al-Mudawwanah (1/59) na Al-Ummu (1/85)]
Ya kwanza: Inajuzu kuzungumza wakati wa adhana kwa hali yoyote
Hili wamelisema Al-Hasan, ‘Atwaa, Qataadah, na Ahmad (isipokuwa yeye amekataza kwenye iqaamah). Nayo imesimuliwa toka kwa Sulaymaan bin Sward ambaye ni Swahaba na ‘Urwa bin Zubayr. Hoja zao ni hizi zifuatazo:
1- Ibn ‘Abbaas alimwamuru mwadhini wake siku ya ijumaa mvua ilipokuwa kali wakati alipofikia:"حي على الصلاة" , aseme: "الصلاة في الرحال". Akaulizwa: “Nini hili?” Akasema: “Amelifanya aliye bora zaidi kuliko mimi”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (616) na Muslim (699) kwa mfanowe].
2- Imepokelewa toka kwa Muusa bin ‘Abdullaah bin Zayd kwamba Sulaymaan bin Sward alikuwa akiadhini kambini, huku akimwagiza mtumishi wake kitu naye anaendelea na adhana. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy ikiwa “Mu’allaq” (2/116), Ibn Abuu Shaybah kaifanya “Mawswuul” (1/212), Ibn Al-Mundhir (3/44) na Abuu Na’iym Sheikh wa Al-Bukhaariy kwa Sanad Swahiyh kama ilivyo kwenye Al-Fat-h (2/116)]
Ya pili: Ni karaha kuzungumza wakati wa adhana na iqaamah
An-Nakh’iy, Ibn Siyriyn, Al-Awzaa’iy, Maalik, Ath-Thawriy, Ash-Shaafi’iy na Abuu Haniyfah wamesema hili.
Kauli ya tatu: Haitakikani kwa mwadhini kuzungumza wakati wa adhana isipokuwa maneno yanayohusiana na Swalaah kama kusema: "صلوا في رحالكم" . Hii ni kauli ya Is-Haaq ambayo Ibn Al-Mundhir kaikubali.
Kauli ya nne: Kama atazungumza katikati ya iqaamah, basi atairudia.
Hii ni kauli ya Az-Zuhriy.
·
Sifa Za Mwenye Kuadhini
Imesuniwa mwadhini awe na sifa zifuatazo:
1- Afanye kwa ajili ya Allaah tu
Asichukue malipo yoyote kwa kuadhini na kuqimu, kwa kuwa haijuzu kudai malipo kwa kazi ya twa’a. Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia ‘Uthmaan bin Abiyl ‘Aasw:
((Mweke mwadhini asiyechukua malipo kwa adhana yake)). [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa katika “Hukmu za adhana”].
Kama hakupatikana wa kujitolea, basi Imamu atampangia mshahara atakayeadhini toka Baytul Maal, kwa kuwa Waislamu wanamhitajia.
2- Awe mwadilifu na mwaminifu
Hii ni kwa vile “mwadhini ni mwaminiwa”[Hadiyth Swahiyh: Imetajwa katika “Fadhila za adhana”], yaani ni mtu anayeaminika kwa kuchunga nyakati za Swalaah. Ni lazima pia ayachunge macho yake yasiangalie aibu na nyuchi za watu. Adhana ya mtu fasiki inasihi pamoja na umakuruhu kama wanavyosema Jamhuri. Sheikh wa Uislamu anaona kwamba adhana ya fasiki anayejulikana haijuzu kwa kuwa anakwenda kinyume na amri ya Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Ama kwa Mahanbali, hili lina khilafu. [Ibn ‘Aabidiyn (1/263), Al-Mawaahib (1/436), Mughniy Al-Muhtaaj (1/138), Al-Mughniy (1/413) na Al-Ikhtiyaaraat (37)]
3- Awe na sauti nzuri
[Ibn ‘Aabidiyn (1/259), Al-Mawaahib (1/437), Mughniy Al-Muhtaaj (1/138), Al-Mughniy (1/413) na Muntahaa Al-Iraadaat (1/125)]
Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipomwambia ‘Abdullah bin Zayd:
((Nenda na Bilaal umfundishe uliyoyaona, kwani yeye ana sauti kali nzuri na pumzi ndefu kuliko wewe)).[Hadiyth Hasan: Imetajwa mara kadhaa, na itakuja tena kwenye “Sifa ya adhana”].
Na ili kulifanikisha hili, ni vizuri kutumia vyombo vya kisasa vya sauti ili kuichekecha sauti na kuifikisha. Na hii ni pamoja na ukaraha wa kuvuta sana na kughani kwa madoido.
4- Ajue wakati
Ili aweze kuadhini mwanzoni mwa wakati na kuepusha matatizo, inajuzu kuadhini kwa asiyeweza kujua wakati yeye mwenyewe kama kipofu ikiwa atakuwa na mtu wa kumweleza wakati. Ibn Ummi Maktoum aliyekuwa kipofu, alikuwa haadhini mpaka aambiwe: “Alfajiri imeingia, Alfajiri imeingia”. [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa karibuni.]
·
Sifa Ya Adhana
Matamko ya adhana yamekuja kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa miundo mitatu:
Wa kwanza:
Ni sentensi 15; Takbiyr mara nne, na matamshi yaliyobakia mara mbili isipokuwa tamko la mwisho la Tawhiyd ambalo ni mara moja tu. Namna hii imethibiti katika Hadiyth ya ‘Abdullah bin Zayd (Radhwiya Allaahu Anhu) aliposema:
“Rasuli wa Allaah Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam alipoamuru kengele ipigwe ili watu wakusanyike kuswali, alinizungukia mtu nikiwa usingizini akiwa amebeba kengele mkononi. Nikamuuliza: Ee ‘Abdullah: Unauza kengele? Akasema: Nawe utaifanyia nini? Nikamwambia: Tutawaitia watu Swalaah. Akaniambia: Kwa nini nisikuonyeshe kilicho bora zaidi kuliko kengele? Nikamwambia sawa. Akasema: Utasema:
" الله أكبر الله أكبر الله أكبر الله أكبر، أشهد أن لا إله إلا الله أشهد أن لا إله إلا الله، أشهد أن محمدا رسول الله أشهد أن محمدا رسول الله، حي على الصلاة حي على الصلاة، حي على الفلاح حي على الفلاح، الله أكبر الله أكبر، لا إله إلا الله"
Halafu akarudi nyuma mbali kidogo akaniambia: Kisha utasema utakapoqimu Swalaah:
" الله أكبر الله أكبر، أشهد أن لا إله إلا الله، أشهد أن محمدا رسول الله، حي على الصلاة، حي على الفلاح، قد قامت الصلاة قد قامت الصلاة، الله أكبر الله أكبر، لا إله إلا الله"
Kulipopambauka, nilimwendea Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nikamweleza niliyoyaona usingizini. Akaniambia: Hakika hiyo ni njozi ya kweli In ShaaAllaah. Basi nenda na Bilaal umfundishe uliyoyaona ili ayatolee adhana, kwani yeye ana sauti kali nzuri na pumzi ndefu kuliko wewe. Nikaenda pamoja na Bilaal, nikaanza kumfundisha na yeye anaadhini. ‘Umar ibn Al-Khattwaab (Radhiya Allaahu Anhu) akalisikia hilo akiwa nyumbani kwake, akatoka mbio akikokota nguo yake akisema: Naapa kwa Yule Ambaye Amekutuma wewe kwa haki ee Rasuli wa Allaah! Hakika mimi nimeoteshwa kama hayo hayo aliyooteshwa. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: " Falil-Laah Al-Hamdu". [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (499), At-Tirmidhiy (189) na Ibn Maajah. Angalia Al-Irwaa (2/264)].
Abuu Haniyfah na Ahmad kwa ilivyo mashuhuri kwake wanautumia muundo huu.
Wa pili:
Ni sentensi 19 kama uliotangulia pamoja na kuongeza “Tarji’i” katika shahada mbili. “Tarji’i” maana yake ni mwadhini kupunguza sauti yake kwenye shahada mbili kiasi cha kusikia waliopo karibu naye, kisha ainyanyue tena kwa shahada zingine mbili.
Muundo huu umethibiti katika Hadiyth ya Abuu Mahdhuurah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimfundisha adhana:
(( الله أكبر الله أكبر الله أكبر الله أكبر، أشهد أن لا إله إلا الله أشهد أن لا إله إلا الله، أشهد أن محمدا رسول الله أشهد أن محمدا رسول الله ))
Kisha akasema:”Rudia tena kwa sauti ya chini”. Halafu akasema: “Sema:
((أشهد أن لا إله إلا الله أشهد أن لا إله إلا الله، أشهد أن محمدا رسول الله أشهد أن محمدا رسول الله، حي على الصلاة حي على الصلاة، حي على الفلاح حي على الفلاح، الله أكبر الله أكبر، لا إله إلا الله)) الحديث
Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (500-503), At-Tirmidhiy (192), An-Nasaaiy (2/3) na Ibn Maajah (709).
Na katika riwaya nyingine toka kwake kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimfundisha adhana maneno 19 na iqaamah maneno 17.
Muundo huu anautumia Ash Shaafi’iy. [Al-Ummu (1/85)]
Wa tatu:
Sentensi 17 kama uliotangulia lakini kwa kufanya takbiyr mara mbili mwanzoni, si mara nne. Na hii ni riwaya nyingine ya Hadiyth ya Abuu Mahdhuurah iliyotangulia kwamba Rasuli wa Allaah alimfundisha adhana hii:
((الله أكبر الله أكبر، أشهد أن لا إله إلا الله أشهد أن لا إله إلا الله، أشهد أن محمدا رسول الله أشهد أن محمدا رسول الله))
Kisha hurejea akisema:
((أشهد أن لا إله إلا الله أشهد أن لا إله إلا الله، أشهد أن محمدا رسول الله أشهد أن محمدا رسول الله، حي على الصلاة حي على الصلاة، حي على الفلاح حي على الفلاح، الله أكبر الله أكبر، لا إله إلا الله ))
[Imekosolewa kwa tamko hili. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (379) na wengineo]
Riwaya hii imekosolewa, haifai. La sahihi ni kufanya takbiyr mara nne kama ilivyotangulia.
Muundo huu anautumia Maalik na masahibu wawili wa Abuu Haniyfah. [Al-Mudawwanah (1/57) na Al-Badaai-’i (1/147)]
Baadhi ya Maulamaa wametilia nguvu kufanya takbiyr mara nne (muundo wa pili) katika Hadiyth ya Abuu Mahdhuurah wakisema kwamba hiyo ni ziada inayokubalika kwa kuwa haiendi kinyume, matoleo yake ni sahihi na inawafikiana na riwaya ya: “Alimfundisha adhana maneno 19”.
Kisha wakaitilia nguvu kuliko namna ya kwanza (isiyo na takbiyr nne) wakisema kwamba Hadiyth ya Abuu Mahdhuurah ni ya mwaka wa nane wa Hijrah baada ya Hunayn, na Hadiyth ya Ibn Zayd ilikuwa ni mwanzo wa suala la adhana, na kwamba watu wa Makkah na Madiynah wanafanya takbiyr nne. [Al-Muhallaa (3/203-206), Al-Awsatw (3/16), Naylul Awtwaar (2/45) na Zaaadul Ma’ad (2/389)]
Wengine wanasema kwamba miundo yote hii inafaa na mtu anaweza kuchagua muundo wowote. Waliosema hili ni Ahmad (ingawa yeye kapendelea zaidi muundo wa kwanza), Is-Haaq na Ibn Taymiyah. [Masaail Ahmad cha Abuu Daawuud (27), Al-Mughniy (1/404), Majmu’u Al-Fataawaa (22/336-337) na Al-Mumti’i (2/51)]
Msimamo huu unaweza kuwa bora zaidi kuliko kuchagua muundo fulani na kuufanya kuwa ndio sahihi zaidi, kwa kuwa qaida inasema: “‘ibaadah zilizokuja katika njia tofauti, ni bora kuzifanya katika njia hizo”. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
·
“Tathwiyb” Katika Adhana Ya Alfajiri
“Tathwiyb”, ni mwadhini kusema: "الصلاة خير من النوم" mara mbili baada ya “Hay-‘alatayn” katika adhana ya Alfajiri.
”Hay-‘alatayn” ni: حي على الصلاة، حي على الفلاح .
Kufanya hivi ni Sunnah kwa Jamhuri. [Mawaahibul Jaliyl (1/431), Al-Majmuu (3/92), Al-Mughniy (1/407) na Subulus Salaam (1/250)]
Na hii ni kwa Hadiyth ya Abuu Mahdhuurah iliyotangulia ambapo alisema: “Ikiwa ni Swalaah ya Alfajiri utasema:
((الصلاة خير من النوم، الصلاة خير من النوم، الله أكبر ألله أكبر، لا إله إلا الله))
Na katika tamko jingine: “Mwanzoni mwa Alfajiri”. [Hasan kwa Sanad zake: lmefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (501), An-Nasaaiy (2/7-8), na Ahmad (3/408). Al-Albaaniy kaipitisha kuwa Swahiyh kwa yenyewe katika “takhriyj” ya Al-Mishkaat (645). Inapata hadhi ya kuwa Hasan kwa Sanad tofauti. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi]
“Tathwiyb” katika adhana ya Alfajiri imekuja katika Hadiyth ya Bilaal, Sa’ad Al-Qardh, Abuu Hurayrah, Ibn ‘Umar, Nu’aym An-Nahaam, ‘Aaishah, na Abuu Mahdhuurah. Sanad zake zina walakin, na bora zaidi zake ni tatu za mwisho ambazo zote zinathibitisha uhalali wa “tathwiyb” katika adhana ya Alfajiri.
“Tathwiyb” ni kwenye adhana ya kwanza tu na si ya pili
Hadiyth tulizoziashiria hivi punde, kuna zilizotaja “tathwiyb” bila kuainisha kama inafanywa kwenye adhana ya kwanza au ya pili, na kuna nyingine zinazoeleza kwamba ni katika adhana ya kwanza. Hakuna hata Hadiyth moja iliyoeleza kwamba inafanywa kwenye adhana ya pili. Hii inaonyesha kwamba “tathwiyb” kisharia inakuwa katika adhana ya kwanza kwa ajili ya kumwamsha aliyelala kama ilivyotangulia. Ama adhana ya pili, hii ni kwa ajili ya kutangazia kuingia wakati na kuwaita watu kwenda kuswali.
Inajulikana kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na waadhini wawili. Wa kwanza ni Bilaal ambaye alikuwa akiadhini na “tathwiyb”, na wa pili ni Ibn Ummu Maktoum. Adhana ya Bilaal ilikuwa ya kwanza, na haikuwahi kuelezewa kwamba Ibn Ummu Maktoum alikuwa akifanya “tathwiyb” kwenye adhana yake. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi. [Angalia Tasnifu: ((تحفة الحبيب ...بحكم الأذانين للفجر والتثويب)) ya Sheikh wetu Majdiy bin ‘Arfaan Allaah Amtukuze]
·
Faida
Baadhi ya Mahanafiy na Mashaafi wamejuzisha kufanya “tathwiyb” katika adhana ya ‘Ishaa. Wanasema kwamba sababu ni kuwa huo ni wakati wa mdororo na kusinzia sinzia kama Alfajiri!! Na baadhi ya Mashaafi wamejuzisha “tathwiyb” nyakati zote!! Hii ni bid-’a yenye kukhalifu Sunnah. ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu Anhu) aliipinga. Alipoingia Msikitini kuswali, alimsikia mtu anafanya “tathwiyb” kwenye adhana ya Adhuhuri, akatoka nje. Akaulizwa: “Wapi?” Akasema: “Bid-’a imenitoa”. [Al-Albaaniy anasema ni Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (538), na Al-Bayhaqiy (1/424). Angalia Al-Irwaa (236)]
·
Yaliyosuniwa Kwa Mwadhini
1- Awe na twahara
Ni kutokana na ujumuishi wa dalili juu ya kusuniwa kumdhukuru Allaah mtu akiwa twahara. Na haya yametangulia katika mlango wa wudhuu. Imepokelewa Hadiyth:
((Haadhini isipokuwa mwenye wudhuu)), lakini si Swahiyh.
Ikiwa ataadhini bila wudhuu, adhana itaswihi kwa mujibu wa Mafuqahaa wote. Vile vile, hata akiwa na janaba, adhana itaswihi kwa vile hakuna dalili yoyote ya kuzuia hili, na mwenye janaba si najsi. Ahmad na Is-Haaq wamezuia kuadhini na janaba. [Al-Awsatw (3/28)]
2- Aadhini kwa kusimama
Wanachuoni hawakukhitalifiana, bali wote wamekubaliana kwamba ni Sunnah mwadhini aadhini kwa kusimama isipokuwa tu kama mgonjwa. Kama ni mgonjwa, basi ataadhini kwa kukaa.
Maalik, Al-Awzaa’iy na Abuu Haniyfah na wenzake, wamesema kuwa ni makruhu kusimama kwa kuketi katika hali yoyote. [Al-Awsatw (3/46)]
Imetangulia katika Hadiyth ya Ibn ‘Umar kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema:
((Simama ee Bilaal unadie Swalaah)). [Hadiyth Swahiyh: “Takhriyj” yake ishatangulia].
Na katika Hadiyth ya ‘Abdullah bin Zayd:
“Niliona usingizini kama vile mtu amesimama, akaadhini mbili mbili, akaqimu mbili mbili”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (1/203) na Ahmad (5/232)].
3- Aelekee Qiblah
Maulamaa wote wanakubaliana kwamba ni Sunnah mwadhini aelekee Qiblah anapoadhini. [Al-Awsatw (3/28)]
Zimesimuliwa Hadiyth tofauti kuhusiana na hili zikiwa na mengi tofauti. Katika baadhi ya riwaya, kuna Hadiyth ya Ibn Zayd kwamba Malaika aliyemwona akiadhini, alikuwa ameelekea Qiblah. [Angalia Irwaaul Ghaliyl (1/250)]
4- Aingize vidole vyake kwenye masikio mawili
Ni kwa Hadiyth ya Abuu Juhayfah aliyesema: “Nilimwona Bilaal akiadhini na kuduru, anafuatisha kinywa chake hapa na hapa, na vidole vyake viwili ndani ya masikio yake”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (1/203) na Ahmad (5/232)].
5- Azikusanye kwa pamoja kila takbiyr mbili
Ni kwa Hadiyth ya ‘Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu Anhu) aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Anaposema mwadhini: Allaahu Akbar Allaahu Akbar, akasema mmoja wenu: Allaahu Akbar Allaahu Akbar, kisha akasema: Ash-hadu an laa ilaaha illal Laah, akasema: Ash-hadu an laa ilaaha illal Laah,……)). [Hadiyth Swahiyh: Itakuja kamili karibuni].
Hadiyth hii inaashiria wazi kwamba mwadhini hukusanya kati ya kila takbiyr mbili, na mwenye kumsikia humjibisha hivyo hivyo. [Sharhu Muslim cha An-Nawawiy (3/79)]
Si kama wanavyofanya baadhi ya waadhini ambao hutenga kila takbiyr moja kwa pumzi nne!!
6- Ageuze kichwa chake kulia wakati anaposema:"حي على الصلاة" , na kushoto wakati anaposema:"حي على الفلاح"
Ni kwa Hadiyth ya Abuu Juhayfah aliyemwona Bilaal akiadhini. Anasema: “Nikawa nafuatilia kinywa chake hapa na hapa kwa adhana”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (634) na Muslim (503)].
Hivyo ni Sunnah ageuze kichwa tu na kiwiliwili kibaki kimeelekea Qiblah. Hivi ndivyo walivyosema Jamhuri kinyume na Maalik aliyelikataa!! Ahmad na Is-Haaq wamelihusisha hilo kwa mwenye kuadhini kwenye mnara tu ili watu wamsikie, na si vinginevyo. [Al-Awsatw (3/26,27)]
7- Afanye “tathwiyb” katika adhana ya kwanza ya Alfajiri
Hili tushalizungumza.
·
Yaliyosuniwa Kwa Mwenye Kusikia Adhana
1- Kuitikia kwa sauti ya chini kila sentensi ya mwadhini
Imepokelewa toka kwa Abuu Sa’iyd kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Mkisikia adhana, semeni mfano wa anayoyasema mwadhini)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (611) na Muslim (383)].
Anaposema mwadhini: " حي على الصلاة "، " حي على الفلاح ", aseme:
" لا حول ولا قوة إلا بالله " Ni kwa Hadiyth ya ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu Anhu) aliyesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Anaposema mwadhini: Allaahu Akbaru Allaahu Akbar, akasema mmoja wenu: Allaahu Akbar Allaahu Akbar, kisha akasema: Ash-hadu an laailaaha illa Laah, akasema: Ash-hadu an laailaaha illa Laah, kisha akasema: Ash-hadu anna Muhammadan Rasuulul Laah, akasema: Ash-hadu anna Muhammadan Rasuulul Laah, kisha akasema: Hayya alas Swalaah, akasema: Laa hawla walaa quwwata illaa bil Laah, kisha akasema: Hayya alal falaah, akasema: Laa hawla walaa quwwata illaa bil Laah, kisha akasema: Allaahu Akbar Allaahu Akbar, akasema: Allaahu Akbar Allaahu Akbar, kisha akasema: Laailaaha illa Laah, kutoka moyoni mwake, ataingia peponi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (385) na Abuu Daawuud (523)].
Jamhuri wamezihusisha “hay-ala” mbili na Hadiyth hii kutokana na ujumuishi wa Hadiyth ya Abuu Sa’iyd iliyotangulia. Na kwa vile “hay-ala” mbili ni kitenzi agizi (njoo kwenye Swalaah, njoo kwenye mafanikio), kumjibu mwadhini itakuwa ni upuuzi.
·
Mwadhini Anaposema: " الصلاة خير من النوم ", Atajibiwa Nini?
Mwenye kumsikia atamjibu kwa kusema: " الصلاة خير من النوم ", juu ya ujumuishi wa Hadiyth ya Abuu Sa’iyd iliyotangulia. Ama baadhi yao kujibu kwa kusema: " صدقت وبررت ", hakuna Hadiyth yoyote Swahiyh iliyothibitisha hilo, hivyo haijuzu kuitaabudia. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
·
Faida
Inatosha kumjibu mwadhini kwenye shahada mbili kwa kusema: "وأنا" au " وأنا أشهد " na mfano wa hilo kwa Hadiyth ya Sahl bin Hunayf kwamba alimsikia Mu’aawiyah bin Abiy Sufyaan (Radhwiya Allaahu Anhu) akiwa ameketi juu ya mimbari. Mwadhini aliadhini, akasema: Allaahu Akbar Allaahu Akbar, Mu’aawiyah akasema: Allaahu Akbar Allaahu Akbar, akasema: Ash-hadu an laailaaha illa Laah, Mu’aawiyah akasema: Na mimi, akasema: Ash-hadu anna Muhammadan Rasuulul Laah, Mu’aawiyah akasema: Na mimi. Adhana ilipomalizika akasema: “Enyi watu! Hakika mimi nimemsikia Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya mimbari hii (wakati alipoadhini mwadhini) akiyasema mliyoyasikia nikiyasema”.[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (914), An-Nasaaiy (2/24) na Ahmad (4/95)].
2- Kumswalia Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumwombea “Al Wasiylah” baada ya kumalizika adhana
Imepokelewa na ‘Abdullaah bin ‘Amri kwamba alimsikia Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
((Mkimsikia mwadhini, basi semeni mfano wa anayoyasema, kisha niswalieni, kwani mwenye kuniswalia mara moja, Allaah Humswalia mara kumi. Kisha niombeeni kwa Allaah Wasylah, kwani Wasylah ni daraja peponi, haitakikani isipokuwa kwa mja kati ya Waja wa Allaah, nami nataraji niwe mimi. Basi mwenye kuniombea Wasylah, atastahiki kupata shufaa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (384), Abuu Daawuud (523), At-Tirmidhiy (3694) na An-Nasaaiy (4/95)].
Jaabir anasema: “Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Mwenye kusema wakati anaposikia adhana: Ewe Mola wa wito huu uliotimu, na Swalaah ya kudumu! Mpe Muhammad Wasylah na daraja ya juu zaidi, na Mfufue Umpe maqaam ya kuhimidiwa Uliyomwahidi, basi atastahiki kuipata shufaa yangu Siku ya Qiyaamah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (614), Abuu Daawuud (529), At-Tirmidhiy (211) na An-Nasaaiy (2/27)].
3- Kushuhudia tawhiyd, risala, na kumridhia Allaah, Rasuli Wake na Dini Yake
Imepokelewa na Sa’ad bin Abiy Waqqaas kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Mwenye kusema wakati anapomsikia mwadhini: Na mimi ninashuhudia kwamba hapana mola mwingine isipokuwa Allaah, Mmoja Asiye na mshirika, na nashuhudia kwamba Muhammad ni Mja Wake na Rasuli Wake, nimemridhia Allaah Mola, na Uislamu Dini, na Muhammad Swalla Allaahu 'alayhi wasallam Rasuli, Hughufiriwa madhambi yake yaliyotangulia)).[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (386), Abuu Daawuud (525), At-Tirmidhiy (210) na An-Nasaaiy (2/26)].
4- Kuomba du’aa kati ya adhana na iqaamah
Kwa kuwa du’aa wakati huu hujibiwa. Anas anasema kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Du’aa hairejeshwi kati ya adhana na iqaamah {basi ombeni})). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (521), At-Tirmidhiy (212), Ibn Khuzaymah (425) na Ahmad (3/155)].
Imepokelewa na ‘Abdullah bin ‘Amri kwamba mtu mmoja alisema: “Ee Rasuli wa Allaah! Waadhini wanatuzidi sana sisi”. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia:
((Sema kama wanavyosema, ukimaliza, omba utajibiwa)). [Haina ubaya: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (524), Ahmad (2/172) na Ibn Hibaan (1695)].
·
Kutoka Msikitini Baada Ya Adhana
Imepokelewa toka kwa Abu Ash-Sha’asha’a akisema: ”Tulikuwa tumeketi Msikitini pamoja na Abuu Hurayrah, na mwadhini akaadhini. Na hapo hapo, akasimama mtu mmoja akatoka Msikitini. Abuu Hurayrah akawa anamtizama mpaka akatoka nje, kisha akasema: “Ama huyu, hakika amemwasi Abal Qaasim Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (655), Abuu Daawuud (536), An-Nasaaiy (2/29) na At-Tirmidhiy (131)].
An-Nawawiy kasema: “Kutoka Msikitini baada ya adhana ni karaha mpaka aswali Swalaah ya faradhi ila kwa udhuru”. [Sharhu Muslim (5/157). Angalia Sunan At-Tirmidhiy (1/398) – Shaakir]
Ninasema: “Asitoke mtu ila kwa dharura kama kutawadha, au kuoga na kadhalika. Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka baada ya kuqimiwa Swalaah na safu kunyoroshwa, akaoga kisha akarudi tena. Maelezo zaidi yatakuja katika mlango wa “Iqaamah”.
Al Haafidh katika Al Fat-h (2/143) anasema: “Mwenye hadathi, mwenye kutokwa na damu, aliyebanwa na haja na mfano wao, ni kundi moja na mwenye janaba. Pia, yule ambaye ni imamu katika Msikiti mwingine na mfano wake”.
·
Baadhi Ya Makosa Na Bid-’a Zinazohusiana Na Adhana
Adhana ni ‘ibaadah, na asili yake ni kuifanya kwa mujibu wa yaliyomo ndani ya wigo wa Sunnah basi. Yasiingizwe humo isipokuwa Aliyoyapanga Allaah na Rasuli Wake. Katika jamii zetu, kuna mambo mengi yenye kwenda kinyume pamoja na makosa mengi katika suala zima la adhana. Mfano wa hayo kwa ufupi ni:
(a)
Baadhi ya makosa ya waadhini
1- Kuvuta sana na kughani kwa madoido.
2- Kuongeza tamko la “Sayyidinaa” kwenye tamko la shahaadah.
3-Kuleta tasbihi, tawashihi na mfano wake kabla ya adhana.
4- Kumswalia Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa sauti kubwa baada ya adhana.
5- Kutowajibika na Sunnah za adhana tulizozitaja nyuma.
6- Kuacha adhana ya kwanza Alfajiri, na kuacha kufanya “tathwiyb” humo.
(b)
Baadhi ya makosa ya wenye kuisikia adhana
1- Kutowajibika na Sunnah tulizozitaja nyuma.
2- Kusema: (( الله أعظم والعزة لله )) wakati wa kusikia takbiyr.
3- Kuapa kwa haki ya adhana.
4- Kuzidisha: (( والدرجة العالية الرفيعة )) na (( إنك لا تخلف الميعاد )) katika du’aa ya baada ya adhana.
5- Kusema: (( لا إله إلا الله )) mwadhini anaposema takbiyr ya mwisho. Kwa kufanya hivi, wanakuwa wamemtangulia mwadhini.
(c)
Baadhi ya makosa wakati wa kuqimiwa Swalaah
1-Kutomjibu mwenye kuqimu
2- Kusema: (( أقامها الله وأدامها )) wakati mwenye kuqimu anaposema: (( قد قامت الصلاة ))
3- Kusema baada ya iqaamah: (( اللهم أحسن وقوفنا بين يديك ))
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
011-Pili: Iqaamah
Alhidaaya.com [3]
· Taarifu Yake:
Tumeshasema nyuma kwamba iqaamah maana yake ni kujulisha watu wasimame kuswali kwa matamshi yaliyopokelewa na kwa sifa mahsusi.
· Sifa Za Iqaamah
Sifa za iqaamah kama ilivyothibiti toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni namna mbili:
Ya kwanza: Ni sentensi 11
(( الله أكبر الله أكبر، أشهد أن لا إله إلا الله، أشهد أن محمدا رسول الله، حي على الصلاة، حي على الفلاح، قد قامت الصلاة، قد قامت الصلاة، الله أكبر الله أكبر، لا إله إلا الله ))
Aina hii ndiyo iliyokuja katika Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Zayd tuliyoielezea katika adhana. Hadiyth hii inaongezewa uzito na yaliyothibiti toka kwa Anas aliyesema:
“Bilaal aliamuriwa afanye shufwa katika adhana, na witri katika iqaamah”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (605) na Muslim (378)].
Na kwa vile Bilaal alikuwa akiadhini kwa namna alivyofundishwa na ‘Abdullah bin Zayd, Jamhuri ya Maulamaa wa salaf na khalaf wamekwenda juu ya msingi huo huo.
Ya pili: Ni sentensi 17
(( الله أكبر (X4)، أشهد أن لا إله إلا الله(X2) ، أشهد أن محمدا رسول الله (X2) ، حي على الصلاة (X2) ، حي على الفلاح (X2) ، قد قامت الصلاة (X2) ، الله أكبر الله أكبر، لا إله إلا الله ))
Namna hii imethibiti katika Hadiyth ya Abuu Mahdhuurah iliyoelezewa kwenye adhana.
Mwenye kuamua kujiwajibishia Hadiyth ya Ibn Zayd katika adhana, ni lazima katika iqaamah atumie namna ya kwanza, na mwenye kujiwajibishia Hadiyth ya Abuu Hudhayfah, ni lazima atumie namna ya pili. Ama mwenye kuchagua yoyote, basi atafanya hivyo hivyo kwenye iqaamah, nalo ndilo bora zaidi, na Allaaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
· Je, Ni Lazima Aqimu Aliyeadhini?
Ni bora aliyeadhini aqimu, kwa kuwa Bilaal (Radhwiya Allaahu Anhu), alikuwa ndiye mwenye kuadhini na kuqimu kama itakavyokuja. Msimamo huu ndio walionao Maulamaa wengi. Lakini kama ataadhini mtu, akaqimu mwingine, basi itajuzu.
Ama Hadiyth Marfu’u ya Zayd Asw-Swadaaiy: “Anaqimu Akhu Asw-Swadaaiy, kwani mwenye kuadhini, ndiye mwenye kuqimu”. [Hadiyth hii si Swahiyh, ni Dhwa’iyf Angalia Adh-Dhwa’iyfah (35) na Al-Irwaa (237)]
Pia Hadiyth ya ‘Abdullah bin Zayd kwamba yeye aliqimu baada ya Bilaal kuadhini ni Dhwa’iyf. [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (499) na Ahmad (4/43)]
· Je, Mtu Atamjibisha Mwenye Kuqimu?
Kisharia, mwenye kusikia iqaamah, anatakikana aseme kama anavyosema mwenye kuqimu kutokana na ujumuishi wa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
((Mkisikia wito, basi semeni kama anavyosema mwadhini)). [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa karibuni].
Iqaamah ni wito na adhana pia. Ni kama alivyosema Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
((Kati ya kila adhana mbili ni Swalaah)). [Hadiyth Swahiyh: Itakuja kwenye mlango wa Swalaah za Sunnah].
Yaani adhana na iqaamah.
Imesemwa: Hakuna kujibisha ila katika adhana.
Ninasema: “La kwanza ndilo lenye nguvu zaidi, na suala lina wasaa”.
· Mwenye Kuqimu Akisema: “Qad Qaamatis Swalaah, Qad Qaamatis Swalaah”, Nini Mtu Atajibu?
Sunnah, ajibu kama alivyosikia “Qad Qaamatis Swalaah, Qad Qaamatis Swalaah” kutokana na ujumuishi wa Hadiyth iliyotangulia. Ama yanayosimuliwa kwamba mtu aseme: Aqaamahal Laahu wa Adaamahaa”, hayo hayapo. [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (528). Angalia Al-Irwaa (241)]
· Ni Upi Wakti Wa Kuqimu Swalaah?
1- Kiasili, inatakiwa asiqimu mpaka amwone imamu. Imepokelewa toka kwa Jaabir bin Samrah (Radhwiya Allaahu Anhu) akisema: “Bilaal alikuwa anaadhini jua linapopinduka, haqimu Swalaah mpaka Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) atoke. Anapotoka huqimu Swalaah anapomwona”.[Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (606). Ishatajwa].
2- Wakati mwingine inafaa kuqimu kabla imamu hajatoka kama atamwona kwa mbali, au akajua kwamba karibu atatoka. Ni kama ilivyo katika Hadiyth ya Abuu Hurayrah inayosema: “Swalaah ilikuwa ikiqimiwa kwa Rasuli wa Allaah Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam, na watu huanza kujipanga safu kabla Rasuli Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam hajasimama mahala pake”.[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (605)].
· Ni Wakti Gani Watu Husimama Kwa Swalaah?
1- Kama imamu hayuko nao Msikitini, ni Sunnah kwao wasisimame mpaka wamwone, sawasawa ikiwa mwadhini ameqimu au hajaqimu. Na hii ni kauli ya Jamhuri kutokana na Hadiyth ya Abuu Qataadah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Ikiqimiwa Swalaah, msisimame mpaka mnione)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (637) na Muslim (604)].
2- Kama imamu yuko nao Msikitini, Ash-Shaafi’iy na wengineo wengi, wanaona kwamba watu wasisimame mpaka iqaamah imalizike. Maalik anasema wasimame anapoanza kuqimu. Ahmad anasema wasimame wakati mwenye kuqimu anaposema: “Qad qaamatis Swalaah”. Na Abuu Haniyfah anasema wasimame anaposema: “Hayya alas Swalaah”. [Sharhu Muslim cha An-Nawawy (3/840)]
Ninasema: “Ninaloliona mimi ni kuwa watu wasimame wanapomwona imamu ashasimama, kwa kuwa kusimama imamu mahala pake ni sawa na kutoka kwa wenye kuswali. Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Msisimame mpaka mnione)). Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.”
· Tanbihi
Baadhi ya Mashekhe wetu wa enzi ya leo, wanasema kwamba si sharia kuqimu Swalaah kwa kutumia kipaza sauti ili walioko nje ya Msikiti waisikie!! Kauli hii imenasibishwa kwa Al-‘Allaamah Al-Albaaniy (Rahimahul Laah).
Ninasema: “Huenda kiegemeo cha kauli hii ni kuwa makusudio ya iqaamah ni kujulisha kuingia kwenye Swalaah na kuihirimia, na si kujulisha kuingia wakati wa Swalaah ili kujitayarisha nayo na kuiitia kama ilivyo kwenye adhana. Pamoja na hivyo, hakuna kinachozuia kuwasikilizisha iqaamah waliopo nje ya Msikiti. Imethibiti kwamba Ibn ‘Umar alisikia iqaamah akiwa Baqiy’i, akaharakia kuwahi Msikitini”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ash-Shaafi’iy kama ilivyo kwenye Musnadi wake (183)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
012-Masharti Ya Kuswihi Swalaah
Alhidaaya.com [3]
Sharti ni kile ambacho kukosekana kwake hulazimisha kukosekana chenye kushurutiwa, na kuwepo kwake hakulazimishi kuwepo chenye kushurutiwa au kutokuwepo. Ni kama twahara kwa mfano, kukosekana kwake, hufanya kuswihi kwa Swalaah kukosekane, na kuwepo kwake, hakulazimishi kuwepo kwa Swalaah.
Yafuatayo ni baadhi ya masharti ambayo Swalaah haiswihi bila kuwepo pamoja na uwezo:
1- Kujua kuingia wakati wa Swalaah
Allaah Mtukufu Anasema:
((إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا))
(( Hakika Swalaah kwa Waumini ni fardhi iliyowekewa nyakati maalumu)). [An Nisaa (4:103)].
Hadiyth za Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) zimesha ainisha nyakati za Swalaah zote kama ilivyotangulia, na Swalaah ni ‘ibaadah yenye nyakati zilizowekwa ndani ya mpaka wa mabano mawili, haiswihi kuifanya kabla ya wakati wake, wala haiswihi kuifanya baada ya wakati wake, isipokuwa kwa udhuru kwa mujibu wa kauli yenye nguvu ya Ijma’a kama tulivyotangulia kuelezea nyuma.
Mafuqahaa wamekubaliana kwamba inatosha kujua kuingia kwa wakati kwa kutopea dhana. [Ibn ‘Aabidiyn (1/247), Ad-Dusuwqiy (1/181), Mughniy Al-Muhtaaj (1/184) na Kash-Shaaf Al Qinaa (1/257)]
2- Kutwaharika na hadathi mbili pamoja na uwezo wa kujitwaharisha
Hii ni sharti ya kuswihi kwa Swalaah kwa dalili zifuatazo:
- Neno Lake Ta’alaa:
((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ ۚ وَإِن كُنتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا ۚ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم مِّنْهُ ۚ مَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيَجْعَلَ عَلَيْكُم مِّنْ حَرَجٍ وَلَـٰكِن يُرِيدُ لِيُطَهِّرَكُمْ وَلِيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ))
(( Enyi walioamini! Mnaposimama kwa ajili ya Swalaah; osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye visugudi, na panguseni (kwa kupaka maji) vichwa vyenu na (osheni) miguu yenu hadi vifundoni. Na mkiwa na janaba basi jitwaharisheni. Na mkiwa wagonjwa au mko safarini au mmoja wenu akitoka msalani, au mmewagusa wanawake, kisha hamkupata maji; basi tayammamuni (ikusudieni) ardhi kwa juu panguseni kwayo nyuso zenu na mikono yenu. Allaah Hataki kukufanyieni magumu, lakini Anataka kukutwaharisheni na Akutimizieni neema Yake juu yenu ili mpate kushukuru)). [Al-Maaidah (5:6)]
- Neno Lake Ta’alaa:
((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنتُمْ سُكَارَىٰ حَتَّىٰ تَعْلَمُوا مَا تَقُولُونَ وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغْتَسِلُوا ۚ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَفُوًّا غَفُورًا ﴿٤٣﴾
(( Enyi walioamini! Msikaribie Swalaah na hali mmelewa mpaka mjue mnayoyasema, na wala mkiwa mna janaba isipokuwa mmo safarini mpaka muoge josho. Na mkiwa wagonjwa au safarini au mmoja wenu ametoka msalani au mmewagusa wanawake kisha hamkupata maji, basi mtayammam (ikusudieni) ardhi safi ya mchanga, pakeni nyuso zenu na mikono yenu. Hakika Allaah daima ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kughufuria)). [An-Nisaa (4:43)]
- Hadiyth ya Abuu Hurayrah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( Allaah Haikubali Swalaah ya mmoja wenu anapopatwa na hadathi mpaka atawadhe)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (135) na Muslim (225)].
- Hadiyth ya Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu Anhumaa) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Allaah Haikubali Swalaah yoyote bila ya twahara)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (224), At-Tirmidhiy (1), An-Nasaaiy (139), Abuu Daawuud (59) na Ibn Maajah (273)].
Hadiyth hizi mbili ziko wazi kwa upande wa shuruti, na Swalaah haiswihi ila kwa kupatikana twahara kutokana na hadathi isipokuwa kwa wale wenye nyudhuru za kisharia kama mwenye kichocho, mwenye tatizo la kuponyokwa upepo na mwanamke mwenye damu ya istihadhwa. Hawa wataswali hata kama watapatwa na hadathi ndani ya Swalaah. Pia aliyekosa maji au mchanga kama mfungwa na mfanowe, huyu ataswali kwa mujibu wa mazingira yalivyo.
· Je, Ni Sharti Kutwaharika Na Najsi Katika Mwili, Nguo Na Mahala Pa Kuswalia?
Kwa upande wa mwili, ni lazima utwaharishwe na najsi kwa dalili zifuatazo:
1- Neno Lake Ta’alaa:
((وَثِيَابَكَ فَطَهِّر))
((Na nguo zako toharisha)). [Al-Muddath-thir (74 :4)]
Ikiwa kuzitwaharisha nguo ni wajibu, basi kuutwaharisha mwili inakuwa ni wajibu zaidi.
2- Hadiyth za kustanji kwa maji na mawe zilizoelezewa kwenye mlango wa twahara, zinatuarifu juu ya ulazima wa kuutwaharisha mwili kutokana na najsi.
3- Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameamuru kuiosha dhakari inapoingia madhii.
4- Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameamuru kujikinga na mkojo, na akaelezea kuhusu watu wawili waliokuwa wakiadhibiwa ndani ya makaburi yao. Mmoja wao alikuwa hajikingi na mkojo.
Dalili zote hizi tumezielezea katika mlango wa twahara.
Ama nguo, ni lazima kuzitwaharisha na kuziweka mbali na najsi kwa dalili zifuatazo:
1- Neno Lake Allaah Mtukufu:
((وَثِيَابَكَ فَطَهِّر))
((Na nguo zako toharisha)) [Al-Muddath-thir (74 :4)]
2- Neno lake Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusiana na nguo inayopatwa na damu ya hedhi:
((Ataipikicha, kisha ataikwangua kwa ncha ya vidole na maji, halafu ataisuuza, na kisha atasali nayo)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (227) na Muslim (291)]
3- Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alivivua viatu vyake akiwa ndani ya Swalaah baada ya Jibriyl kumjuvya kwamba vina najsi. [Hadiyth Swahiyh: Imeelezewa katika mlango wa kuzitwaharisha najsi].
Hili linatutaarifu juu ya wajibu wa kujivua na najsi ya kilichovaliwa wakati wa Swalaah.
Ama mahala pa kuswalia, ni lazima kupatwaharisha mahala hapo kwa dalili zifuatazo:
1- Neno Lake Ta’alaa:
((وَإِذْ جَعَلْنَا الْبَيْتَ مَثَابَةً لِّلنَّاسِ وَأَمْنًا وَاتَّخِذُوا مِن مَّقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى ۖ وَعَهِدْنَا إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ أَن طَهِّرَا بَيْتِيَ لِلطَّائِفِينَ وَالْعَاكِفِينَ وَالرُّكَّعِ السُّجُودِ))
((Na Tulipoifanya Nyumba (Al-Ka’bah) kuwa ni mahali pa kurejewa na watu na pa amani, na fanyeni mahali pa kusimama Ibraahiym kuwa ni pahala pa kuswalia. Na Tulichukua ahadi kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl kwamba: “Itakaseni Nyumba Yangu kwa wanaotufu na wanaokaa i’tikaaf, na wanaorukuu na kusujudu.”)). [Al-Baqarah (2:125)]
2- Kuamuru Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) imiminwe ndoo ya maji kwenye mkojo wa bedui Msikitini. [Hadiyth Swahiyh: Imeelezewa katika mlango wa twahara].
Ninasema: “Maulamaa wana kauli mbili kuhusiana na matni zilizotangulia:
Ya kwanza: Dalili zilizotangulia zinatutaarifu kwamba ni wajibu kujiepusha na najsi kwenye mwili, nguo na mahala pa kuswalia, na kwamba mtu akiswali mbele ya najsi, au akaibeba, au akakabiliana nayo, basi atapata dhambi lakini Swalaah yake itakuwa ni sahihi. Kwa kuwa matni hizi hazina kinachotutaarifu kukanushika kiini cha dhati ya Swalaah yenyewe, au kuswihi kwake kinyume na kujitwaharisha na hadathi. La wajibu halilazimiki kuwa sharti. [Angalia As-Sayl Al-Jarraar cha Ash-Shawkaaniy (1/157-158)]
Ya pili: Matni zote za Aayah na Hadiyth zinaamuru kujiepusha na najsi, na kuamuru kitu ni kukataza kinyume chake. Na ukatazaji kitu ndani ya ‘ibaadah kunahukumia uharibifu wa kitu hicho, na kwa hilo inatolewa dalili juu ya usharuti. Huu ndio msimamo wa Jamhuri ya Maulamaa. [Al-Badaai-’i (1/114), Haashiyatud Dusuwqiy (1/200), Mughnil Muhtaaj (1/188) na Kash-Shaaful Qinaa (1/288)]
Kinachotubainikia hapa ni kuwa kauli ya kwanza ndiyo yenye nguvu zaidi. Naam! Inajuzu kutolea dalili juu ya usharuti wa katazo linaloonyesha juu ya uharibifu wenye maana sawa na ubatili. Lakini hii ikiwa katazo la kitu hicho ni kwa dhati yake yenyewe au sehemu yake, si kwa lililo nje ya wigo wake. Na katazo hapa kama inavyoonekana wazi, liko nje ya Swalaah yenyewe. Allaah Ndiye Mjuzi zaidi”.
·
Mwenye Kuswali Akiwa Na Najsi, Naye Hakujua Ila Baada Ya Kumaliza, Je, Atairudia Swalaah?
[Mahala pa mas-ala haya panahusiana na kauli ya Jamhuri yenye kushurutisha kutwaharika na najsi ndani ya Swalaah. Ama kwa kauli tuliyoipa nguvu ya uwajibu (bila ushuruti), hapana kitu juu yake kama ilivyo wazi]
Maulamaa wamekhitalifiana katika suala hili kwa kauli tatu:
Ya kwanza: Swalaah yake ni baatwil. Atalazimika kuswali tena kama atajua kuwa alikuwa na najsi kabla ya wakati wa Swalaah kutoka. Lakini ikiwa amejua baada ya kutoka wakati, hatolipa.
Hii ni kauli ya Rabiy-’a, Maalik na Al-Hasan. [Al-Mudawwanah (1/21,22) na Al-Awsatw (2/164)]
Ya pili: Swalaah yake ni baatwil, na atalazimika kuilipa tena hata baada ya wakati. Hii ni kauli ya Ash-Shaafi’iy na riwaya ya Ahmad. [Al-Ummu (155), Al-Mughniy (2/65) na Al-Awsatw (2/164)]
Wanasema kwamba kwa kuwa amekosa sharti kati ya shuruti za kuswihi Swalaah, basi Swalaah yake ni baatwil na ni lazima aiswali tena.
Ya tatu: Swalaah yake ni Swahiyh, na halazimiki kuiswali tena. Wamelisema hili Ibn ‘Umar, ‘Atwaa, Ibn Al-Musayyib, Mujaahid, Abuu Thawr, Is-Haaq, Ash-Sha’abiy, An-Nakh’iy na Al-Awzaa’iy. Ni riwaya ya Ahmad, na Ibn Al-Mundhir kaikubali. [Al-Awsatw (2/163), Al-Mughniy (2/65) na Al-Majmu’u (3/163)]
Dalili yao ni:
1- Kwamba alikuwa hajui kama ana najsi, na Allaah Anatuambia:
((وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ آمِنُوا كَمَا آمَنَ النَّاسُ قَالُوا أَنُؤْمِنُ كَمَا آمَنَ السُّفَهَاءُ ۗ أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ السُّفَهَاءُ وَلَـٰكِن لَّا يَعْلَمُونَ))
((Na wanapoambiwa: “Aminini kama walivyoamini watu.” Husema: “Je, tuamini kama walivyoamini wapumbavu.” Tanabahi! Hakika wao ndio wapumbavu lakini hawajui)). [Al-Baqarah (2:13)]
Na katika Hadiyth Swahiyh, ni kuwa Allaah Mtukufu Anasema: ((Hakika Nimeshafanya)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (125)].
2- Hadiyth ya Abuu Sa’iyd kuhusiana na kisa cha Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuvua viatu wakati Jibriyl alipomjulisha kwamba vina najsi. Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwa akijua kwamba viatu vina najsi, na Swalaah yake aliikamilisha. Na lau kama Swalaah ingelikuwa baatwil, basi angeiswali tena upya.
Ninasema: “Tukisema kwamba ni sharti kujiepusha na najsi, basi itatulazimu tuseme kwamba Swalaah ni baatwil, na kama si hivyo, italazimu kwa yule aliyekumbuka kwamba aliswali bila ya wudhuu, asiirejeshe tena Swalaah yake!! Wao hili hawalisemi. Huku ni kuvunja qaida ambazo kati yake ni kuwa shuruti na nguzo hazipomoki kwa kusahau.
Ama Hadiyth ya Rasuli kuvua viatu vyake, hiyo ni dalili kwetu kwamba si sharti kujiepusha na najsi ndani ya Swalaah. Dalili hii inaipa nguvu kauli yetu ya uwajibu pasina usharuti. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.”
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
013-Mahala Palipokatazwa Kuswalia
Alhidaaya.com [3]
Kiasili, ardhi yote ni sehemu ya kuswalia, na Swalaah inajuzu pahala pake popote kutokana na kauli ya Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
((Nimefadhilishwa juu ya Manabii kwa mambo sita…Nimefanyiwa ardhi twahara na mahala pa kuswalia..)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (523), na mahala pa ushahidi kwenye Al-Bukhaariy (335), na Muslim (520) toka kwa Jaabir].
Lakini hutolewa ndani ya wigo wa ujumuishi huu, mahala ambapo imethibiti kwa Hadiyth kwamba ni marufuku kuswalia. Kati ya mahala hapo ni:
1- Kwenye mapumzikio ya ngamia na kwenye zizi lao
Ni sehemu ambapo ngamia husimama wakati wanapofika sehemu ya kunywa maji, au sehemu wanakojihifadhi na kulala. Jaabir bin Samrah anasema kwamba mtu mmoja alimuuliza Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Je, naweza kuswali kwenye zizi la mbuzi na kondoo?” Akamjibu: “Ndio”. Akamuuliza: “Je, naweza kuswali kwenye zizi au sehemu ya mapumzikio ya ngamia?” Akamjibu: “Hapana”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (360)]. Sababu ya karibu zaidi inayoweza kusemwa kuhusu katazo hilo, ni pale Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliposema:
(( Msiswali kwenye zizi au mapumzikio ya ngamia, kwani ni sehemu ya mashaytwaan)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (493), Ibn Maajah (769), na Ahmad (5/55)].
Uwezekano hauko mbali wa mashaytwaan kuandamana na ngamia, na kuwa maeneo yake ya kupumzikia na kulala ni hifadhi ya mashaytwaan. Na kwa ajili hiyo, imekatazwa kuswalia hapo. Ni kama alivyokataa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuswali mahala ambapo Swalaah ya Alfajiri iliwapita. Ameeleza sababu ya hilo katika neno lake:
(( Mahala hapo shaytwaan alitujia )). [Hadiyth Swahiyh: Imekuja katika mlango wa “Nyakati za Swalah”]
2- Makaburini
Imepokelewa toka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriy akisema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Ardhi yote ni sehemu ya kuswalia, isipokuwa makaburi na bafu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (492), At-Tirmidhiy (236), na Ibn Maajah (745). Kuna mvutano kuhusu kama ni ‘Mawswuul” au “Mursal”. La sawa ni “Mawswuul”. Angalia Al-Irwaa (1/320)].
Imepokelewa toka kwa Abuu Murthad kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( Msikae juu ya makaburi, na wala msiswali kuyaelekea )). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (972)].
Na Bi ‘Aaishah anasema kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Allaah Amewalaani Mayahudi na Manaswara, waliyafanya makaburi ya Manabii wao Misikiti)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (435) na Muslim (529)].
Kana kwamba sababu ya kukataza kuswali kwenye makaburi ni kuzuia njia ya kuyaabudu makaburi au kujishabihisha na makafiri.
Makaburi yote ni hali moja hapa, yawe ya Waislamu au ya makafiri. Na ikiwa yatafukuliwa na maiti zikatolewa, basi Swalaah itajuzu hapo.
Kumswalia maiti baada ya kuzikwa kwa yule ambaye hakuwahi kumswalia, hutolewa ndani ya wigo wa katazo. Na hii ni kwa Hadiyth ya Ibn 'Abbaas aliyesema kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali mbele ya kaburi baada ya maiti kuzikwa, na akampigia takbiyr mara nne. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (954)].
Aidha, imepokelewa toka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu Anhu) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimuulizia mtu aliyekuwa anasafisha Msikiti. Wakamjibu: "Amefariki ee Rasuli wa Allaah!" Akasema: "Kwa nini msinijulishe?" Wakajibu: " Yeye alikuwa hivi na hivi" (yaani wakamdunisha). Akawaambia: "Nionyesheni lilipo kaburi lake". Rasuli akaenda kwenye kaburi lake, akamswalia. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1337) na Muslim (956)].
Hadiyth hii inatuarifu kuhusu uhalali wa kumswalia maiti kwenye kaburi, na Jamhuri wamejuzisha hili. Lakini Maalik na Abuu Haniyfah wamelikataa hili. Mengi zaidi yatakuja katika mlango wa "Janaaiz".
3- Bafu:
Ni mahala pa kuogea (na si pa kukidhia haja) kama wanavyopaita watu. Haijuzu kuswali hapo kutokana na Hadiyth ya Abuu Sa'iyd iliyotangulia: ((Ardhi yote ni sehemu ya kuswalia isipokuwa makaburi na bafu)).
Ama mahala pa kukidhi haja kama chooni au msalani, haijuzu kuswali hapo pia kutokana na unajsi wa mahala na kuwa ni makazi ya mashaytwaan. Zayd bin Arqam anasema kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Hakika sehemu hizi za kufanyia haja, ni makazi yaliyokaliwa, basi anapoingia mmoja wenu msalani aseme: Ninajilinda kwa Allaah na majini wa kiume na majini wa kike)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (6) na Ibn Maajah (296)].
·
Je, Inajuzu Kuswali Juu Ya Shimo La Majitaka?
Kiusahihi, sehemu ya juu ya shimo la majitaka haihusiani na shimo lenyewe, na wala sehemu hiyo haiitwi choo. Hivyo inajuzu kuswali juu yake madhali hapo juu hapana najsi. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
·
Nini Hukmu Ya Kuswalia Nguo Ya Wizi Au Iliyoharamishwa, Au Ardhi Ya Kupora?
Maulamaa wana kauli mbili kuhusiana na suala hili na mengineyo yanayofanana:
Ya kwanza:
Swalaah haiswihi. Kauli hii ni mashuhuri katika madhehebu ya Ahmad na Ibn Hazm. Sheikh wa Uislamu ameikubali kauli hii. [Al-Inswaaf (1/194), Al-Muhallaa (4/33) na Majmu’u Al-Fataawaa (21/89)]
Hoja yao ni:
1- Yaliyopokelewa toka kwa Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu Anhumaa) ikiwa Marfu’u:
((Mwenye kununua nguo kwa dirham kumi, na katika hizo kuna dirham moja ya haramu, basi Swalaah yake haitokubaliwa madhali dirham hiyo ipo)). [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (2/98) kwa Sanad Dhwa’iyf].
2- Nguo inafungamana na nguzo na masharti ya ‘ibaadah, hivyo huiathiri kinyume na kama iko nje yake. Ni kama mtu aliyetawadha kwa chombo cha dhahabu, hiki hakiathiri, kwani kiko nje ya Swalaah.
Ya pili:
Swalaah inaswihi, lakini atapata dhambi kwa kuivaa. Haya ni madhehebu ya Abuu Haniyfah, Maalik na Ash-Shaafi’iy. [Al-Majmu’u (3/180), Al-Mabsuutw (1/206) na Naylul Awtwaar (2/92)]
Nayo ndiyo yenye nguvu kwa kuwa hakuna Hadiyth yoyote inayokataza kuswalia kwenye ardhi ya kupora, au nguo ya wizi, au iliyoharamishwa, bali imekuja Hadiyth yenye kukataza kitendo cha uporaji au kuzungumzia vivazi kiujumla. Hivyo Swalaah inaswihi lakini madhambi ya uporaji yapo, na hili huitwa “Kanuni ya uchangukaji”. [Angalia Qawaa’id Ibn Rajab (uk 11 na 12)] Ama Hadiyth waliyoitolea dalili, Hadiyth hii haifai, juu ya kwamba kukubaliwa huko hakulazimu kukanusha usahihi wake.
Ninasema: “Huenda tuliyoyatilia nguvu, yanathibitishwa zaidi na Hadiyth ya ‘Uqbah bin ‘Aamir aliyesema: “Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alizawadiwa joho la hariri akalivaa, kisha akaswali nalo. Halafu alinyanyuka, akalivua kwa kishindo mno kana kwamba amelichukia. Kisha akasema: “Hili halitakikani kwa wachaMungu”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (375) na Muslim 2075)]
Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa amelivaa kabla ya kuharamishwa, kisha Jibriyl akamjulisha kuwa ni haramu kuvaa hariri (kama ilivyo kwenye riwaya ya Muslim toka kwa Jaabir) ndani ya Swalaah na nje ya Swalaah. Lakini pamoja na hivyo, Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuirudia tena Swalaah.
1-
Kusitiri uchi pamoja na uwezo wa kufanya hivyo
Maulamaa wamekubaliana (isipokuwa wachache mno) kwamba kusitiri uchi ni sharti ya kuswihi Swalaah kwa atakayeweza kufanya hivyo kwa dalili zifuatazo:
1- Kauli Yake Ta’alaa:
يَا بَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ
Enyi wana wa Aadam! Chukueni mapambo yenu (ya mavazi ya sitara na twahara) katika kila mahala pa ‘Ibaadah. Na kuleni na kunyweni na wala msifanye israfu. Hakika Yeye (Allaah) Hapendi wanaofanya israfu. [Al-A’araaf ( 7:31)]
Kwa maana kwamba zisitirini nyuchi zenu mnapotaka kuswali, kwani wao walikuwa wakiitufu Ka’abah wakiwa uchi, ndipo ikashuka Aayah hii (kama ilivyoelezwa kwenye Swahiyh Muslim).
2- Hadiyth ya Salamah bin Al-Akwa’a aliyesema: “Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Sisi tunakuwa mawindoni. Je, anaweza mtu kuswali na nguo moja? Akajibu: “Ndio, ajifunge nayo chini, na kama hakuweza, basi aifunge kwa mwiba”. [Isnadi yake ni teketeke. Al-Bukhaariy ameifanya ‘Mu’allaq” kwa muundo wa kutothibiti kuwepo (1/553) na akasema kuwa Isnadi yake ichunguzwe. Ninasema: “Hivyo ndivyo ilivyo kutokana na kasoro aliyoieleza Al-Haafidh kwenye Al-Fat-h (1/555). Kisha Hadiyth hii imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (632), na An-Nasaaiy (2/70). Mzingo wake uko kwa mpokezi asiye makini. Al’Allaamah Al-Albaaniy kwenye Al-Mishkaat (760) na kabla yake An-Nawawiy kwenye Al-Majmu’u (3/164), wanaona kwamba ni Hadiyth Hasan!!”]
3- Hadiyth ya ‘Aaishah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Allaah Haikubali Swalaah ya msichana aliyebaleghe ila kwa khimar)). [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (641), At-Tirmidhiy (377) na wengineo. Baadhi ya Maulamaa wameitia walakini. Katika Al-Irwaa (1/215), Al-Albaaniy ameipasisha kuwa ni Hasan].
4- Hadiyth ya Jaabir akisimulia kuswali kwake pembezoni mwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ikihusiana na nguo. Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia:
((Kama ni pana, jizungushie, na kama inabana, jifunge nayo chini)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (361) na Muslim (3010].
Haitotosheleza chini ya izari (sitara ya chini ya mwili). Hivyo inaonyesha ulazima wa kusitiri mwili katika Swalaah. Wajibu huu ni katazo la kinyume chake, na kinyume hiki ni uharibifu. Hivyo kujisitiri kunabeba usharuti kwa Jamhuri.
5- Ibn ‘Abdul Barri amehadithia kwamba Maulamaa wote kwa ijmai wamekubaliana kwamba Swalaah inakuwa baatwil kwa mwenye kuswali uchi naye ana uwezo wa kujisitiri. Pia Sheikh wa Uislamu amenukuu hivyo. Lakini baadhi ya wafuasi wa Maalik wamenukuu kwamba Swalaah haibatiliki kwa kutositiri uchi. Naye Ash-Shawkaaniy, juu ya msingi wa qaida yake iliyotangulia katika kushurutisha utwahara wa nguo, mwili na mahala, anasema kwamba ni wajibu. [At-Tamhiyd, Majmu’u Al-Fataawaa (22/117), Al-Fat-h (1/555), Bidaayatul Mujtahid (1/156) na As-Saylul Jarraar (1/158)]
Linaloonekana kwangu ni kuwa suala hapa linatofautiana kwa mwenye kuliangalia kwa mtizamo wa kina.
6- Kuusitiri uchi wakati mtu anaposimama mbele ya Allaah Mtukufu, kunaingia katika mlango wa kumtukuza. [Al-Badaai-’i (1/116), Ad-Dusuwqiy (1/211), Mughnil Muhtaaj (1/184) na Kash-Shaaful Qinaa (1/263)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
014-Sehemu Ya Mwili Inayopasa Kusitiriwa
Alhidaaya.com [3]
Ijulikane mwanzo kabisa kwamba uhakiki (nao ni muhtasari wa yaliyohakikiwa na Sheikh wa Uislamu Ibn Taymiyah Rahimahul Laahu katika Al-Fataawaa (22/113-120)) unasema: “Hakuna mafungamano ya kimahusiano kati ya uchi nyeti na uchi wa Swalaah, bali istilahi ya “kusitiri uchi” wanayoizingatia Mafuqahaa kwamba ni sharti ya kuswihi Swalaah, si katika matamshi ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Hakuna katika Quraan wala Hadiyth linaloeleza kwamba sehemu anayoisitiri mwenye kuswali ni uchi, bali Allaah Mtukufu Anasema:
((يَا بَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ))
Enyi wana wa Aadam! Chukueni mapambo yenu (ya mavazi ya sitara na twahara) katika kila mahala pa ‘Ibaadah. Na kuleni na kunyweni na wala msifanye israfu. Hakika Yeye (Allaah) Hapendi wanaofanya israfu. [Al-A’araaf (7 :31)]
Uchi wa kuangaliwa, ni uchi wa kutamanika kimwili. Ama kujisitiri kwenye Swalaah, hiyo ni kwa Haki ya Allaah Mtukufu. Haifai kwa yeyote kuzunguka Al-Ka’abah au kuswali akiwa uchi hata kama yuko peke yake. Hivyo imejulikana kwamba kujisitiri kwenye Swalaah si kwa ajili ya kujisitiri na watu. Hivyo basi, hii ni aina, na hii ni aina nyingine.
Na wakati huo, wakati wa Swalaah, mwenye kuswali anaweza kusitiri sehemu inayojuzu kuiacha wazi wakati usio wa Swalaah, na wakati wa Swalaah anaweza kuiacha wazi sehemu anayoisitiri watu wasimwone. Kwa mfano, Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza mtu kuswali na nguo moja bila kuwa na chochote juu ya mabega yake. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Al-Bukhaariy (359) na Muslim (516)].
Na hii ni kwa upande wa haki ya Swalaah, lakini inajuzu kwa wanaume kuyawacha wazi mabega nje ya Swalaah. Kadhalika, mwanamke katika Swalaah hujitanda ushungi, lakini hajitandi kwa mumewe wala kwa maharimu zake.
Na kinyume cha hivyo kwa uso, mikono miwili na miguu miwili, hairuhusiwi kuvionyesha kwa ajanibu kwa mujibu wa kauli mbili zilizo Swahiyh. Ama kuvisitiri viungo hivi wakati wa Swalaah, si wajibu kwa itifaki ya Waislamu, bali inajuzu kwake kuonyesha uso wake na viganja vyake katika Swalaah kwa rai ya Jamhuri. Pia, miguu miwili kwa mujibu wa rai ya Abuu Haniyfah, na rai hii ndiyo yenye nguvu zaidi. Tukilijua hili, tunasema:
·
Kinachopasa Akisitiri Mwanamume Katika Swalaah
- Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kutufu Al Ka’abah uchi. [Hadiyth Swahiyh: Itakuja katika mlango wa Hajji].
Hivyo basi kujisitiri kwenye Swalaah ni bora zaidi.
- Na amesema kuhusu nguo moja: ((Kama ni pana, jizungushie, na kama inabana, jifunge nayo chini)). [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa katika mlango tulionao].
Hivyo basi, haitoshelezi sitara isiyoweza kusitiri sehemu ya chini ya mwili.
- Na amesema Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Sehemu iliyo kati ya kitovu na magoti ni uchi)). [Al-Albaaniy ameipa daraja ya Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (495, 496). Angalia Al-Irwaa (1/226)].
Na imepokelewa na Buraydah akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza mwanamume kuswali na nguo ya kujitanda bila kujifunga nayo, na amekataza mwanamume kuswali na sirwali bila kuwa na nguo ya kufunika juu” [Al-Albaaniy ameipa daraja ya Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (636). Angalia Swahiyh Abuu Daawuud (636)].
Hii inaonyesha kuwa ni lazima kuisitiri sehemu ya juu ya mwili wakati wa Swalaah.
-Rasuli amekataza mtu kuswali na nguo moja bila kuwa na chochote juu ya mabega yake. [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa katika mlango tulionao].
Hadiyth hii inaonyesha kwamba mwanamume anaamuriwa asitiri uchi katika Swalaah yake kama paja na viungo vinginevyo hata juu ya kuwepo kauli isemayo kwamba paja si uchi, bali uchi ni utupu wa mbele na nyuma tu. (Hili limetiliwa nguvu kama itakavyokuja kuelezwa baadaye katika mlango wake hata kama ataswali peke yake nyumbani kwake bila kuwepo amwonaye, itamlazimu hilo).
Ama yule mwenye kujengea kwamba uchi ni tupu mbili, [ juu ya moja ya riwaya mbili toka kwa Ahmad na Ibn Hazm ] na kwamba inajuzu kuswali mapaja wazi, basi huyo amekosa, na wala hilo Ahmad (Rahimahul Laahu) hakulisema. Vipi Ahmad aamuru kusitiri mabega mawili, halafu aruhusu kuwacha wazi mapaja mawili?!
Kikhulaswa, tunasema kwamba mwanamume katika Swalaah ameamuriwa asitiri mwili wake kuanzia mabega mawili hadi magoti yake mawili. Na kama hana nguo ya kumtosha, hapo atajifunga nayo chini na sehemu ya juu ya mwili ataiacha wazi kama ilivyotangulia katika Hadiyth ya Jaabir.
·
Faida
Ni lazima kusitiri sehemu zinazopasa kusitiriwa katika Swalaah kwa nguo isiyoonyesha rangi ya ngozi ya mwili kama ni nyeupe, au nyekundu au nyeusi. Ama ikiwa nguo ni nzito lakini inabana na kuonyesha muundo wa kiungo bila rangi yake, basi ni karaha kuswali nayo, lakini Swalaah inakuwa ni sahihi. [Sheikh Wahiyd Hafidhahul Laah ametupatia faida kwa haya katika kitabu cha Al-Ikliyl (1/311)]
·
Kinachopasa kusitiriwa na mwanamke katika Swalaah
[Nimenukulu toka kitabu changu cha Fiqhus Sunnat Lin-Nisaa (kurasa 81,82 na 83)]
1- Mwanamke akiswali mbele ya watu wasio maharimu wake (ajanibu), ni lazima asitiri mwili wake wote isipokuwa uso na viganja viwili kwa mujibu wa rai ya Jamhuri. [Kuna makhitalifiano baina ya Maulamaa kuhusiana na suala la kufunua uso na viganja viwili. Litaelezewa kwa uchambuzi katika mlango wake]
2- Ikionekana sehemu yoyote inayolazimu kusitiriwa mbele ya wanaume wasio maharimu, basi atapata madhambi lakini Swalaah yake haibatiliki kwa mujibu wa kauli sahihi ya Maulamaa, kwa kuwa hakuna dalili yoyote ya kubatilika Swalaah yake kwa hilo.
3- Kama anaswali peke yake au mbele ya mumewe au maharimu zake, basi inajuzu kufunua uso wake na viganja vyake. Hii ndio kauli ya Maulamaa wengi.
Ama kwa upande wa nywele za mwanamke, imekuja Hadiyth isemayo:
((Allaah Haikubali Swalaah ya mwanamke aliyebaleghe ila kwa khimari)). [Imefanyiwa "ikhraaj" na Abuu Daawuud (641), At-Tirmidhiy (377) na wengineo. Maulamaa zaidi ya mmoja wameikosoa. Angalia Jaami'i Ahkaamun Nisaa (1/310)].
Hadiyth hii ingawa ni Dhwaíyf, lakini At-Tirmidhiy alisema baada yake: "Wanavyoitumia Maulamaa ni kuwa ikiwa mwanamke anaswali na huku sehemu ya nywele zake inaonekana, basi Swalaah yake haijuzu. Na hii ni kauli ya Ash-Shaafi'iy aliyesema: "Haijuzu Swalaah ya mwanamke ikiwa sehemu ya mwili wake iko wazi".
Na kwa mujibu wa rai ya Maulamaa wengi wakiwemo Abuu Haniyfah na Ahmad, Swalaah ya mwanamke inakuwa ni Swahiyh na wala hairejeshi ikiwa sehemu ndogo ya nywele zake na mwili wake itaonekana. Lakini kama ni sehemu kubwa, basi ataswali tena katika wakati wake kwa mujibu wa rai ya Maulamaa wote, Maimamu wanne na wengineo. [Majmu'u Al-Fataawaa cha Ibn Taymiyah (22/123). Angalia Al-Mughniy cha Ibnu Qudaamah (1/601)]
·
Mguu Wa Mwanamke Katika Swalaah
Imepokelewa Hadiyth ya Ummu Salamah kwamba alimuuliza Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Je, mwanamke anaweza kuswalia diraa na khimar bila nguo ya chini?” Akamjibu: ((Ikiwa diraa ni pana inafunika mgongo wa miguu yake)). Hadiyth hii ni Dhwaíyf. [Imefanyiwa "ikhraaj" na Abuu Daawuud (640) na Al-Bayhaqiy (2/232) kwa Sanad Dhwaíyf ikiwa mawquuf na Marfu’u].
Ash-Shaafi'iy katika Al-Ummu (1/77) anasema: "Mwili wote wa mwanamke ni uchi (yaani katika Swalaah) isipokuwa uso wake, viganja vyake na miguu yake”. Na At-Tirmidhiy amenukulu kauli yake: "Imesemwa kwamba ikiwa mgongo wa miguu yake uko wazi, basi Swalaah yake inajuzu". Na haya ni madhehebu ya Abuu Haniyfah kama alivyonukulu Ibn Taymiyyah katika Al-Fataawaa (22/123).
Maalik na Ahmad, wao wanaona kwamba mwili wote wa mwanamke ni uchi, na Ahmad amevuka zaidi ya hapo kwa kusema: "Mwanamke aswali na kisionekane chochote cha mwili wake hata ukucha".
Ninasema: "Ninaloliona lina nguvu ni kuwa inajuzu kuswali hata kama mgongo wa mguu wake utakuwa wazi lakini si mbele ya wasio maharimu zake ingawa kusitiri miguu yake itakuwa ni akiba zaidi. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi."
4- Ni mustahabu mwanamke aswali kwa kuvaa nguo inayositiri mwili, na bora zaidi ni ile yenye kumsitiri zaidi. Na kwa ajili hiyo, Ash-Shaafi’iy amesema: “Wote wamekubaliana juu ya diraa na khimar , na yenye kuzidi ni bora na sitara zaidi. [Diraa inafanana na kanzu, lakini yenyewe ni ndefu hadi kufunika miguu miwili. Khimaar hufunika kichwa na shingo. Ama jilbabu, hii hutandiwa juu ya diraa. Imepokelewa kwa njia Swahiyh toka kwa ‘Umar, Ibn ‘Umar, Ibn Siyriyn na wengineo kwamba wamesema: “Mwanamke huswali kwa nguo tatu: Diraa, khimaar na jilbabu”]
Na kwa vile ikiwa amejitanda jilbabu, ataitanua wakati wa kurukuu na kusujudu ili nguo yake isionyeshe makalio yake na sehemu nyingine za mwili”. [Al-Mughniy (1/602), Al-Muhadh-Dhab (3/172) na Jaami’u Ahkaamin Nisaa (1/335)]
5- Ama ikiwa mwanamke ni kijakazi, hukumu yake ni kama ya mwanamke muungwana isipokuwa inajuzu aswali bila kufunika nywele zake kwa makubaliano ya Maulamaa wote isipokuwa Al-Hasan na ‘Atwaa.
6- Binti mdogo ambaye bado hajabaleghe, si lazima afunike nywele zake wakati wa Swalaah. ‘Abdur Raaziq katika Al-Muswannaf (3/113) kwa Sanad Swahiyh toka kwa Jariyj anasema: “Nilimwambia ‘Atwaa: Vipi kuhusu msichana ambaye hajavunja ungo anaposwali?” Akasema: “Inamtosha izari yake”.
·
Faida Mbalimbali
(a)
Mwenye Kufunukwa Uchi Wakati Wa Swalaah Bila Kukusudia, Je Swalaah Itabatilika?
Jamhuri ya Maulamaa wanasema kwamba mtu ambaye sehemu ya uchi wake itafunuka wakati wa Swalaah hata bila kukusudia, basi Swalaah yake itabatwilika kama hakuifunika hapo hapo. Mahanafi wameweka mpaka wa robo kiungo, kiasi cha kutekeleza nguzo!! [Ibn ‘Aabidiyn (1/273), Al-Mawaahib (1/498) na Al-Majmu’u (3/166)]
Mahanbali nao wanaona kwamba Swalaah haibatiliki kwa kufunuka uchi kwa kitambo kidogo kama vile upepo kupeperusha nguo uchi ukaonekana, au pia kama uchi wake utaonekana kidogo hata kwa muda mrefu. [Kash-Shaaf Al-Qinaa (1/269)]
Na hii ni kwa Hadiyth ya ‘Amri bin Salamah anayesema: “ Baba yangu aliondoka na ujumbe wa watu wake kuelekea kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), naye Rasuli akawafundisha namna ya kuswali. Akawaambia: Imamu wenu atakuwa yule mwenye kujua zaidi kusoma, nami nilikuwa ndiye mwenye kujua zaidi kusoma wakati nilipokuwa nikihifadhi, nao wakanitanguliza kuwa imamu. Nilikuwa nikiwaswalisha nikiwa nimevaa burdah yangu ndogo ya njano, nikisujudu, inanivuka. Mwanamke mmoja akasema: “Tusitirieni uchi wa msomaji wenu”. Wakaninunulia kanzu ya Kiomani, nami sikufurahishwa na kitu chochote baada ya kusilimu kwangu kama nilivyofurahishwa na kanzu hii.” [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (4302) na Abuu Daawuud (585), na tamko ni lake].
Haikusikika kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), alilipinga hilo au Swahaba yeyote.
Ninasema: “Hili ndilo Swahiyh. Lakini ni lazima aufunike uchi wake kama ataweza ikiwa amejua kwamba umefunuka”.
(b)
Swalaah Ya Asiyeweza Kujisitiri Uchi
[Ibn ‘Aabidiyn (1/275), Ad-Dusuwqiy (1/216), Al-Majmu’u (3/142, 182) na Kash-Shaaf Al-Qina’a (1/270)]
Maulamaa wote wamekubaliana kwamba Swalaah haipomoki kwa mtu asiyepata kitu cha kujisitiri nacho, lakini wamekhitalifiana namna ya kuswali kwake. Jamhuri wanasema kwamba ikiwa hakupata isipokuwa nguo yenye najsi, au nguo ya hariri (kwa mwanamume), basi ni lazima avae. Na kama hakupata chochote, basi ataswali uchi kwa Neno Lake Allaah Mtukufu:
(( فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ وَاسْمَعُوا وَأَطِيعُوا وَأَنفِقُوا خَيْرًا لِّأَنفُسِكُمْ ۗ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ))
(( Basi mcheni Allaah muwezavyo, na sikilizeni; na tiini na toeni (kwa ajili ya Allaah) ni kheri kwa ajili ya nafsi zenu. Na yeyote anayeepushwa na ubakhili na tamaa ya uchu wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu)). [At-Taghaabun (64:16)].
Kisha Mahanafi na Mahanbali wakasema kuwa atachaguzwa kati ya kuswali kwa kukaa au kusimama, na wamependezesha aashirie wakati wa kurukuu na kusujudu, kwani ni sitara zaidi. Lakini Maalik na Mashafii wanasema kwamba ni lazima aswali kwa kusimama, na haijuzu kuswali kwa kukaa.
Na je atailipa Swalaah kama atapata cha kujisitiria? La sawa na sahihi ni kuwa hatoilipa Swalaah kama walivyosema Mashafii na Mahanbali. Na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi.
(c)
Kujipamba Na Kujiweka Maridadi Kwa Swalaah
Inajuzu kuswali kwa nguo moja kama ilivyotangulia. Lakini inapendeza mtu kuswalia na zaidi ya nguo moja, kujipamba na kujiweka maridadi kiasi awezavyo kutokana na Neno Lake Ta’alaa:
(( خذوا زينتكم عند كل مسجد))
Yaani kwa kila Swalaah. Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Anaposwali mmoja wenu, basi avae nguo zake mbili, kwani Allaah Anastahiki zaidi kupambiwa )). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bayhaqiy (2/236). Angalia Al-Majmu’u (2/54)].
1-
Kuelekea Qiblah na kuwa na uwezo wa kufanya hivyo
Ni sharti ya kuswihi Swalaah kwa Ijma’a ya Maulamaa. [Maraatibul Ijma’a cha Ibn Hazm (uk 26)]
Ni kwa dalili hizi zifuatazo:
1- Neno Lake Ta’alaa:
(( فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِۚ وَحَيْثُ مَا كُنتُمْ فَوَلُّوا وُجُوهَكُمْ شَطْرَهُ ))
((Basi elekeza uso wako upande wa Al-Masjidil-Haraam. Na popote mtakapokuwepo (mkataka kuswali), basi elekezeni nyuso zenu upande wake)). [Al-Baqarah (2:144)]
2- Hadiyth ya Ibn ‘Umar: “Watu wakiwa Qubaa katika Swalaah ya Alfajiri, aliwajia mtu akawaambia: Hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameteremshiwa usiku Quraan akaamuriwa aelekee Al-Ka’abah, basi nanyi elekeeni. Walikuwa wameelekeza nyuso zao Sham, wakageuka kuelekea Al-Ka’abah”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (4491), Muslim (526) na An-Nasaaiy (2/61)].
3- Hadiyth mashuhuri ya aliyeswali vibaya iliyopokelewa na Abuu Hurayrah kwamba mtu mmoja aliingia Msikitini na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekaa pembeni mwa Msikiti. Aliswali kisha alikwenda kwa Rasuli kumsalimia. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: ((Waalaykas Salaam. Rudi ukaswali, kwani hukuswali)). Kisha mara ya pili au iliyofuatia, mtu yule akasema: “Nifundishe ee Rasuli wa Allaah”. Akamwambia:
((Ukisimama kuswali, tawadha wudhuu kikamilifu, halafu elekea Qiblah upige takbiyr. Kisha soma chepesi ulichonacho katika Quraan, halafu rukuu mpaka utulie katika rukuu, kisha nyanyuka mpaka usimame wima sawasawa, halafu sujudu mpaka utulie katika sijdah, kisha nyanyuka mpaka utulie katika kikao, halafu sujudu mpaka utulie katika sijdah, kisha nyanyuka mpaka utulie katika kikao, halafu fanya hivyo katika Swalaah yako yote)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (6251) na Muslim (397)].
·
Kuelekea Kuko Namna Mbili:
Mwenye kuswali ima awe anaiona Al Ka’abah au haioni. Anayeiona, ni lazima aielekee Al Ka’abah yenyewe kwa mwili wake wote. Akiwa ndani ya Al Haram na anaiona Al Ka’abah, haitomtosheleza kuelekea sehemu ya Msikiti bila ya Al-Ka’abah.
Ama kwa asiyeiona, huyu ni lazima aelekee upande wake iliko na si yenyewe hasa, kwa kuwa huo ndio upeo wa mwisho anaouweza. Na Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Msikielekee Qiblah au kukipa mgongo kwa haja ndogo au haja kubwa, lakini elekeeni mashariki au Magharibi)). [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa katika mlango wa Twahara].
Hadiyth hii inaonyesha kwamba sehemu iliyopo kati ya mashariki na Magharibi, inazingatiwa kuwa ni Qiblah kwa watu wa Madiynah. Ama kwa watu wa Misri, mwelekeo wa Qiblah kwao ni kati ya mashariki na kusini.
Qiblah kinaweza kujulikana kwa mihrabu zilizoko ndani ya Misikiti ya Waislamu, au kwa kutumia dira na vinginevyo.
·
Ni Wakati Gani Kuelekea Qiblah Husameheka?
Umejua kwamba kuelekea Qiblah ni sharti ya kuswihi Swalaah. Lakini kuna hali zisizo za kawaida ambazo Swalaah itajuzu bila ya kuelekea Qiblah. Hali hizo ni:
1-
Asiyeweza kuelekea Qiblah:
Ni kama mgonjwa asiyeweza kujigeuza na hana wa kumgeuzia Qiblah. Huyu atasamehewa kwa Neno Lake (Subhaanahu wa Ta’alaa): ((Mcheni Allaah muwezavyo)), na Neno Lake: ((Allaah Hamkalifishi mtu isipokuwa kwa uwezo wake)).
2-
Asiyejua Qiblah kilipo, akajitahidi kukisia lakini akaswali na kuelekea kwingine.
Asiyejua Qiblah kilipo, ni lazima amuulize mtu aonyeshwe, na kama hakumpata, atajitahidi kukiainisha kilipo. Ikiwa atajitahidi, akaswali, kisha akalibaini kosa lake wakati anaendelea kuswali, ni lazima azunguke kukielekea huku Swalaah ikiendelea kama ilivyo katika Hadiyth ya ‘Ibn ‘Umar tuliyoitaja hivi karibuni ambayo sehemu yake inasema: “Wakageuka kuelekea Al-Ka’abah”. Na ikiwa kosa atalijua baada ya kumaliza Swalaah, basi Swalaah yake ni Swahiyh na wala hatoiswali tena kwa kauli yenye nguvu. Hii ni kwa Hadiyh ya ‘Aamir bin Rabiy’a (Radhwiya Allaahu Anhu) aliyesema: “Tulikuwa pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) safarini katika usiku wa giza. Hatukujua Qiblah kilipo, na kila mmoja wetu aliswali kuelekea upande wake. Tulipopambaukiwa, tulimweleza Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Na hapo ikashuka:
(( وَلِلَّـهِ الْمَشْرِقُ وَالْمَغْرِبُ ۚ فَأَيْنَمَا تُوَلُّوا فَثَمَّ وَجْهُ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ وَاسِعٌ عَلِيمٌ))
((Na Mashariki na Magharibi ni ya Allaah; basi popote mnapogeuka kuna Wajihi wa Allaah. Hakika Allaah ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote)) [Al-Baqarah (2:115)].
Haya ni madhehebu ya Ath-Thawriy, Ibn Mubaarak, Ahmad na Is-Haaq.
3- Wakati inaposhitadi hofu ya kushambuliwa na adui au jinginelo:
Allaah Anasema:
((حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ • فَإِنْ خِفْتُمْ فَرِجَالًا أَوْ رُكْبَانًا ۖ فَإِذَا أَمِنتُمْ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَمَا عَلَّمَكُم مَّا لَمْ تَكُونُوا تَعْلَمُونَ ))
(( Shikamaneni na Swalaah na khaswa Swalaah ya katikati (Alasiri), na simameni mbele ya Allaah katika hali ya utiifu • Mkikhofu (swalini) huku mnatembea au mmepanda kipando. Mtakapokuwa katika amani mdhukuruni Allaah kama Alivyokufunzeni yale mliyokuwa hamuyajui )). [Al-Baqarah (2:238 na 239)].
Na katika Hadiyth ya Ibn 'Umar kuhusiana na Swalaah ya hofu: "Na ikiwa hofu ni kubwa kuliko hivyo, waliswali wakienda kwa miguu au wamepanda, wakiwa wameelekea Qiblah au hawakuelekea". [Hadiyth Swahiyhi: Imefanyiwa "ikhraaj" na Al-Bukhaariy (4535) na Maalik (396)].
Na Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Wanapopambana, basi ni takbiyr na kuashiria kwa kichwa)). [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bayhaqiy (3/255)].
4- Katika Swalaah ya Sunnah kwa mpandaji anapokuwa safarini
Inajuzu kwa msafiri aswali Swalaah ya Sunnah akiwa juu ya mnyama wake (au kwenye gari, ndege, au meli), na si lazima aelekee Qiblah kama itakuwa ni uzito kwake. Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar kwamba yeye alikuwa akiswali juu ya mnyama wake usiku akiwa safarini, hajali popote pale atakapoelekea. Na amesema: “Rasuli wa Allaah Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam alikuwa anaswali juu ya mnyama wake kuelekea upande wowote ule, na huswali juu yake witri, lakini alikuwa haswali juu yake Swalaah ya faradhi”. [Hadiyth Swahiyhi: Imefanyiwa "ikhraaj" na Al-Bukhaariy (1098) na Muslim (700)]
Na imepokelewa toka kwa ‘Aamir bin Rabiy’a akisema: “Nilimwona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiswali juu ya mnyama wake; anaashiria kwa kichwa chake upande wowote anapoelekea, na hakuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) analifanya hilo katika Swalaah ya faradhi”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1098)].
Na imepokelewa na Jaabir (Radhwiya Allaahu Anhu) akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali juu ya mnyama wake popote pale anapoelekea, na anapotaka kuswali Swalaah ya faradhi, huteremka akaelekea Qiblah”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Al-Bukhaariy (400)].
Lakini; ikiwa ataweza kuanza Swalaah yake kwa kuelekea Qiblah, kisha akaelekea na mnyama wake kule anakokwenda, basi ni bora. Na hii ni kwa yale yanayohadithiwa kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapotaka kuswali Swalaah ya Sunnah juu ya mnyama wake, anaelekea naye Qiblah akapiga takbiyr, kisha huswali kuelekea kule msafara unakoelekea” [Al-Albaaniy kaipa daraja ya Hasan. Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (1225) na wengineo. Angalia Swifatu Swalaatin Nabiyyi ukurasa wa 75].
Mas-ala: Ikiwa msafiri amepanda gari ambalo yeye si dereva baada ya Swalaah ya Adhuhuri, na akajua kwamba hatoswali ila baada ya Magharibi, je anaweza kuswali Swalaah ya Alasiri ndani ya gari? Au ataiswali pamoja na Magharibi?
Linaloonekana kuwa na nguvu hapa ni kuwa ni lazima aswali Alasiri katika wakati wake ndani ya gari hata kwa kukaa na hata bila kuelekea Qiblah, kwa kuwa wakati ni muhimu zaidi kwa Swalaah za faradhi kama ilivyoelezewa nyuma, na hupewa kipaumbele zaidi kuliko sharti ya kuelekea Qibla. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
015-Niya
Alhidaaya.com [3]
Niya maana yake ni kuazimia kufanya ‘ibaadah kwa ajili ya kujikurubisha kwa Allaah Mtukufu. Swalaah haiswihi bila ya niya kwa hali yoyote, na niya haipomoki kwa hali yoyote ila kwa mtu kuondokewa na akili. Katika hali hiyo, taklifu nayo hupomoka, kwani akili ndiyo kitovu cha taklifu.
Ijma’a imefungika kuizingatia niya kuwa ni sharti ya kuswihi Swalaah. [Ad-Dusuwqiy (1/233), Mughnil Muhtaaj (1/148), Bidaayatul Mujtahid (1/167) na Kash-Shaaful Qinaa (1/313)]
Na asili ya hilo, ni Kauli Yake Allaah Mtukufu:
((وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ))
((Na hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Allaah wenye kumtakasia Dini, wenye kujiengua na upotofu kuelemea Dini ya haki na wasimamishe Swalaah na watoe Zakaat; na hiyo ndiyo Dini iliyosimama imara)). [Al-Bayyinah (98:5)]
Na neno lake Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
(( Hakika amali ni kwa niya, na hakika kila mtu ni kwa lile alilolinuwia)). [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa mara nyingi, nayo imepasishwa na Al-Bukhaariy na Muslim]
·
Yasiyokuwa Na Mabishano:
1- Niya mahala pake ni moyoni na si kwa ulimi katika ‘ibaadah zote ikiwemo Swalaah.
2- Akitamka kwa ulimi kwa kusahau kinyume na yale aliyoyanuwia moyoni, yanayozingatiwa ni ya moyoni. Ni kama aliyekusudia moyoni kuswali Adhuhuri lakini ulimi ukateleza akataja Alasiri kwa kusahau.
3- Akitamka kwa ulimi bila kuweka niya moyoni, basi haitotosheleza.
4- Kutamka niya kwa sauti katika Swalaah ni katika bid-’a mbaya, na si katika bid-’a njema. Na haya yamekubaliwa na Waislamu wote. Hakuna yeyote aliyesema kwamba kuitamka niya kwa sauti ni Sunnah au bid-’a njema, na anayesema hivyo, basi amekhalifu Sunnah ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), Ijma’a ya Maimamu wanne na wengineo. Mwenye kusema hivi atatubishwa, na kama atatubu basi, kama atakataa ataadhibiwa adhabu stahiki. [Majmu’ul Fataawaa (22/233)]
Mbali na hilo kuwa bid-’a, pia huwakera wenye kuswali.
·
Kuitamka Niya Hata Kwa Siri Ni Bid-’a
Sheikh wa Uislamu anasema: [Majmu’ul Fataawaa (22/237-238)]
“Hajanukuu Muislamu yeyote si kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), wala kutoka kwa Swahaba yeyote kwamba Rasuli alitamka tamko la niya kabla ya kupiga takbiyr, si kwa siri wala kwa sauti, wala kwamba aliamuru hilo. Ni maarufu kwamba hima na shime za kunukuu hilo zipo tele lau kama hilo lingekuwepo, na juu ya uasili wa tawaatur kidesturi na kisharia, haiwezekani kufichwa unukuu wa hilo. Na kwa vile hakuna yeyote aliyenukuu, imejulikana kwa hakika isiyo na shaka kwamba hilo halikuweko. Kuzidisha hili na mfano wake katika sifa ya Swalaah, kunaingia ndani ya wigo wa mazidisho mengineyo yaliyozushwa kwenye ‘ibaadah nyinginezo kama mwenye kuzidisha adhana na iqaamah katika Swalaah ya ‘Iyd mbili, au mwenye kuswali rakaa mbili katika Jabal Marwa wakati wa kusai na mengineyo mfano wa hayo”.
Kisha niya ni nyepesi zaidi kuliko kuitamka. Mwenye kutawadha, kisha akatoka kuelekea Msikitini huku akiwa analijua lengo lake la kufanya hivyo, basi huyo kaipata niya. Na kwa ajili hiyo, Sheikh wa Uislamu anasema: “Niya hufuata lijulikanalo. Mwenye kujua analotaka kulifanya, basi ashalinuwi kwa kuwa haiwezekani kutenda bila niya”. [Al-Ikhtibaaraat ukurasa wa 49]
·
Kuainisha Swalaah
Katika niya, ni lazima mtu aiainishe Swalaah anayoiswali; kama ni ya Sunnah au ya Faradhi, Adhuhuri au Alasiri. Na makusudio ni kuhudhurisha haya katika moyo.
·
Mahala Pa Niya
1- Hakuna mvutano wowote kati ya Maulamaa kwamba niya ikikutana na takbiyr (takbiyr ikaja baada yake moja kwa moja) basi itatosheleza, bali hili ndilo asili na bora zaidi.
2- Hakuna mvutano wowote kati yao kwamba niya baada ya takbiyr haitoshelezi.
3- Akinuwia Swalaah, kisha akashughulishwa, halafu akaja kuswali, Swalaah yake itaswihi kwa kuwa niya yake inaambatana na hukmu madhali hakukusudia kuivunja Swalaah. [Al-Inswaaf (1/23), na Al-Mubdi’u (1/417). Ibn ‘Uthaymiyn ameliunga mkono katika Al-Mumti’i (2/291)]
Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
·
Kugeuza Na Kubadili Niya Wakati Wa Swalaah
[Al-Mumti’i (2/294-301) na Al-Ikliyl (1/348-355) cha Sheikh Wahiyd Baaliy Allaah Amhifadhi]
Kuna picha mbalimbali za kuhama kutoka niya moja kwenda nyingine katika Swalaah. Kati yake:
1- Kutoka Swalaah ya faradhi kwenda Swalaah yoyote ya Sunnah
Kwa mfano, haijuzu kwa mwenye kuswali Adhuhuri peke yake, kisha akaona watu wanaswali Jamaa, aigeuze Faradhi yake kuwa Sunnah, kisha aswali pamoja nao Jamaa.
2- Kutoka faradhi kwenda faradhi nyingine
Haijuzu, na faradhi zote mbili hubatilika. Faradhi ya kwanza kwa vile ameikata, na ya pili kwa kutoitilia niya kabla ya kuianza. Picha ya hii ni kama mtu aliyeanza kuswali Alasiri, kisha akakumbuka kwamba hakuswali Adhuhuri, hapo haitojuzu aigeuze kuwa Adhuhuri.
3- Kutoka Sunnah kwenda faradhi
Haijuzu vile vile kutokana na sababu iliyotangulia.
4- Kutoka Sunnah maalumu kwenda Sunnah yoyote
Haijuzu, kwa kuwa Sunnah maalumu inakusanya niya ya Sunnah yoyote. Mfano wake ni mtu aliyenuwia kuswali rakaa nne za Sunnah ya Adhuhuri, kisha akaona jamaa, halafu akaigeuza Sunnah hiyo rakaa mbili ili aiwahi jamaa.
5- Kutoka Sunnah maalumu kwenda Sunnah maalumu
Haijuzu, ni kama aliyenuwia Sunnah ya maamkizi ya Msikiti, kisha katikati yake akaigeuza Sunnah ya Alfajiri. Ya kwanza itabatilika kwa kuikata, na ya pili kwa kutoitilia niya mwanzoni.
6- Kutoka Sunnah yoyote kwenda Sunnah maalumu
Haijuzu kwa yaliyotangulia.
7- Kutoka niya ya imamu kuwa maamuma
Hii inajuzu kutokana na Hadiyth ya ‘Aaishah kuhusiana na kisa cha Abu Bakri kuwaswalisha watu. Anasema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipoingia Msikitini, Abu Bakri alisikia mchakato wake na kuanza kurudi nyuma. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwashiria abaki alipo. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaja mpaka akakaa kushotoni mwa Abu Bakri. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akawa anawaswalisha watu kwa kukaa na Abu Bakri amesimama. Abu Bakri anafuata Swalaah ya Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), na watu wanaifuata Swalaah ya Abu Bakr”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (664) na Muslim (418].
8- Maamuma kutoka imamu kwenda imamu mwingine
Inajuzu, kutokana na Hadiyth ya ‘Aaishah iliyotangulia. Watu walikuwa wakimfuata Abu Bakri, kisha wakamfuata Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Na pia kisa cha kuuawa ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu Anhu) ambapo alimtanguliza ‘Abdul Rahmaan bin ‘Awf akakamilisha Swalaah. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (664) na Muslim (418)].
9- Kutoka maamuma kuwa imamu
Inajuzu. Ni kama imamu kutokewa na udhuru katika Swalaah, na maamuma mmoja akakamata nafasi yake kutokana na Hadiyth ya ‘Umar iliyotangulia.
10- Kutoka anayeswali peke yake na kuwa imamu
Inajuzu. Ni kama mtu kuwa anaswali peke yake akaja mtu mwingine akamfuata. Hapo ataikamilisha Swalaah akiwa imamu kutokana na Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas aliyesema: “Nililala kwa khalati yangu. Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasimama usiku kuswali, nami nikasimama kuswali pamoja naye. Nilisimama kushotoni mwake, akanikamata kichwa changu na kunisimamisha kuliani mwake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (699) na Muslim (763)].
Katika hili hakuna tofauti kati ya Swalaah ya Sunnah au faradhi juu ya kauli Swahiyh.
11- Kutoka imamu na kuswali peke yake
Haijuzu ila kwa udhuru. Ni kama maamuma kupatikana na udhuru akamwacha imamu peke yake. Wakati huo itajuzu na Swalaah yake ni Swahiyh.
12- Kutoka maamuma na kuswali peke yake
Imesemwa: Inajuzu kutokana na udhuru wa kisharia kama imamu kurefusha Swalaah zaidi ya inavyotakikana kiSunnah, au maamuma kupata maumivu ya ghafla na mfano wake katika yanayomlazimisha kuswali peke yake, kufupisha na kuondoka. Waliosema hivi wametolea dalili kisa cha mtu aliyeswali nyuma ya Mu’aadh bin Jabal ambaye alirefusha kisomo. Mtu yule akatoka kwenye Swalaah, akaswali peke yake. Kisha akaenda kumlalamikia Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), naye hakumwamuru aswali tena. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (699) na Muslim (763)].
Imesemwa pia: Hapaswi kuswali peke yake, bali anatakikana aivunje Swalaah kama atatokewa na dharura yoyote, kisha aswali peke yake. Waliosema hivi wamejibu kwamba Hadiyth ya Mu’aadh inaonyesha kwamba mtu yule alitoka kwenye Swalaah, kisha akaswali peke yake kama ilivyo kwenye riwaya ya Muslim (465) isemayo: “Mtu akatoka kando, akatoa taslimu, kisha akaswali peke yake”.
Ninasema: [Sheikh Ibn ‘Uthaymiyn ameliwafiki hili kinyume na alilowafiki Sheikh Wahiyd]
“Rai ya kwanza ina nguvu zaidi hata kwa riwaya ya mwisho. Kitendo cha mtu yule hakionyeshi kwamba kuswali peke hakujuzu. Kisha ninalolipa nguvu mimi ni kuwa uimamu na umaamuma ni sifa ya ziada juu ya asili ya Swalaah. Niya ya wawili hawa, haina athari katika kuswihi kwa Swalaah ingawa inaweza kuathiri katika kuzipata thawabu za jamaa kama zinavyoonyesha juu ya hili Hadiyth kadhaa zilizotangulia kuhusiana na niya ya imamu na maamuma. Allaah Mtukufu Ndiye Ajuaye Zaidi”.
·
Kutofautiana Niya Ya Imamu Na Maamuma
[Angalia Al-Manhiyyaat Ash-Shar-’iyyah Fiy Swifatis Swalaat cha Al Kamaaliy ukurasa wa 14 na zinazofuatia]
Hakuna mahitalifiano katika usharia wa maamuma kumfuata imamu na kuafikiana niya yao sawasawa ikiwa Swalaah ya faradhi au ya Sunnah. Kisha Maulamaa wametofautiana endapo kama niya ya imamu na maamuma itatofautiana. Lililo sahihi ni kuwa hakuna sharti ya kuwafikiana niya ya maamuma na niya ya imamu. Haya ni madhehebu ya Ash-Shaafi’iy na Ibn Hazm. [Mughnil Muhtaaj (1/502), Al-Muhallaa (4/223) na Bidaayatul Mujtahid (1/167)] Na dalili ya hili ni kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
(( Hakika amali ni kwa niya, na hakika kila mtu ni kwa lile alilolinuwia)).
Ibn Hazm amesema: “Rasuli (Alayhis Salaam) ameeleza wazi hapa kwamba kila mmoja ni kwa lile alilolinuwia, na kwa hiyo, imekuwa sahihi kiyakini kwamba imamu ana niya yake na maamuma ana niya yake, na niya ya mmoja haifungamani na niya ya mwingine”.
Ama Hadiyth isemayo:
(( Hakika amefanywa imamu ili afuatwe, nanyi msikhitilafiane naye)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (689) na Muslim (411)].
Makusudio yake ni kuwa msikhitilafiane naye katika vitendo vya kidhahiri kwa dalili ya kauli yake katika Hadiyth hii hii:
(( Anaporukuu nanyi rukuuni, anaponyanyuka nanyi nyanyukeni, anaposujudu nanyi sujuduni, na anaposwali kwa kukaa, nanyi nyote swalini kwa kukaa)). Hadiyth hapa haifungamani na kutofautiana niya, na linaloonyesha hilo ni makubaliano ya Maulamaa wote kwamba mwenye kuswali Sunnah anaweza kumfuata mwenye kuswali faradhi pamoja na kuwa niya zao ni tofauti (kama itakavyokuja baadaye). Pia dalili nyinginezo zitakazokuja katika picha za kutofautiana niya mbili. Nazo ni:
1- Mwenye kuswali Sunnah kumfuata mwenye kuswali faradhi
Inajuzu kwa Maulamaa wote wakiwemo Maimamu wanne na wengineo kutokana na dalili zifuatazo:
(a) Hadiyth ya Abuu Dharri aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliniuliza: (( Utafanyaje ikiwa viongozi wako wanaichelewesha Swalaah na wakati wake, au wanaiua Swalaah na wakati wake?)) Nikamjibu: “Unaniamuru nini?” Akasema: ((Swali Swalaah katika wakati wake, na ikiwa utaiwahi pamoja nao basi swali, kwani hiyo itakuwa ni ziada kwako)). [Hadiyth Swahiyh: Imeelezwa katika mlango wa Nyakati zilizokatazwa kuswali].
(b) Hadiyth ya Yaziyd bin Al-Aswad aliyesema: “Nilikuwa pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hijjah yake. Nikaswali pamoja naye Swalaah ya Alfajiri katika Msikiti wa Al-Khayf. Alipomaliza Swalaah yake na kuondoka, mara walikuja watu wawili katika watu waliochelewa ambao hawakuwahi kuswali pamoja naye. Akasema: ((Nitawafuatia)). Wakaletwa huku vifua vyao vikitetema. Akawauliza: ((Kitu gani kimewazuia msiswali nasi?)) Wakasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Sisi tulikuwa tumeswali safarini. Akawaambia: ((Msifanye! Mkiswali safarini, kisha mkaja Msikiti wa jamaa, basi swalini pamoja nao, kwani hiyo inakuwa ni ziada kwenu)). [Hadiyth Swahiyh: Imeelezwa katika mlango wa Nyakati zilizokatazwa].
2- Mwenye kuswali faradhi kumfuata mwenye kuswali Sunnah: Inajuzu kwa dalili zifuatazo:
(a) Hadiyth ya Jaabir bin ‘Abdillaah isemayo: “Mu’aadh bin Jabal alikuwa akiswali na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ‘Ishaa ya mwisho, kisha hurejea kwa watu wake na kuswali nao tena Swalaah hiyo”.[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (711) na Muslim (465) na tamko ni lake].
Wengine wameongeza: “Hiyo kwake ni Sunnah na kwao ni faradhi”. [Isnadi yake ni Dhwa’iyf. Imefanyiwa “ikhraaj” na Ash-Shaafi’iy katika Al-Umm (1/173, Atw-Twahaawiy (1/409) na Ad-Daara Qutwniy (1/274). Kuna “’an-‘ana” (fulani toka kwa fulani) ya Ibn Jariyj, naye ni mdanganyifu. Al-Haafidh kaipa daraja ya kuwa ni Swahiyh katika Al-Fat-h]
Al-Haafidh amesema: “Kwa Hadiyth hii, pametolewa dalili juu ya kuswihi mwenye kuswali faradhi kumfuata mwenye kuswali Sunnah, kwa msingi kwamba Mu’aadh alikuwa akinuwia faradhi kwa Swalaah ya kwanza, na Sunnah kwa Swalaah ya pili. Kisha ziada iliyoashiriwa, imetolewa dalili kadhalika”.
Ninasema: “Aliyoyaeleza Al-Haafidh yanaonyesha kwamba mimi nimepata katika riwaya ya Hadiyth nyingine – katika kisa cha mtu aliyemshitaki Mu’aadh – neno lake: “..na kwamba Mu’aadh aliswali pamoja nawe ‘Ishaa, kisha akaja akaanza kwa Suwrat Al-Baqarah…..Hadiyth. [Hadiyth Swahiyh: Imeelezewa hivi karibuni]”. Ndani ya riwaya hii, kuna ishara kwamba Swalaah aliyoiswali Mu’aadh pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ilikuwa faradhi ya ‘Ishaa.”
(b) Hadiyth ya Abu Bakrah aliyesema: “Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali Swalaah ya Adhuhuri ya vita. Baadhi yao walipanga safu nyuma yake na wengine mkabala na adui. Aliswali nao rakaa mbili, akatoa tasliym, kisha wakaondoka wale walioswali naye, wakasimama sehemu ya wenzao. Halafu wakaja wale (waliokuwa mkabala na adui) wakapanga swafu nyuma yake. Akaswali nao rakaa mbili, kisha akatoa tasliym. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akawa ameswali rakaa nne, na Maswahaba wake rakaa mbili mbili”. [Wapokezi wake wanaaminika: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (1248). Al-Hasan kuisikia toka kwa Abu Bakrah kuna mvutano pamoja na kwamba Al-Bukhaariy amemfanyia “ikhraaj” Hadiyth nyingi, naye hatosheki kwa uwezekano wa kuwepo maonano tu!! Angalia Jaami’u At-Tahswiyl (1/163)]
Ash-Shaafi’iy anasema katika Al-Ummu (1/173): “Ya mwisho katika mbili hizi ni Sunnah kwa Rasuli, na kwa wengineo ni faradhi”.
Na kwa picha hii yote, inajuzu kwa mtu aliyeikuta Jamaa ya watu wanaoswali tarawehe (ikiwa hakuwahi kuswali ‘Ishaa) kujumuika nao kwa niya ya ‘Ishaa. Imamu akitoa tasliym baada ya rakaa mbili, yeye atakamilisha peke yake, au atasimama kwa rakaa mbili zilizosalia. Imamu anaposimama kwa rakaa mbili nyinginezo, atamfuata, kisha atatoa tasliym pamoja naye. La kwanza ni bora zaidi. Na Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
3- Mwenye kuswali faradhi kumfuata mwenye kuswali faradhi nyingine:
Hii ina hali tatu:
(a) Kulingana idadi ya rakaa za faradhi mbili. Ni kama kuswali qadhwa ya Adhuhuri nyuma ya anayeswali Alasiri au ‘Ishaa. Hii inajuzu kutokana na ujumuishi wa yaliyotangulia.
(b) Idadi ya rakaa za maamuma za faradhi kuzidi rakaa za imamu. Ni kama anayeswali Adhuhuri nyuma ya anayeswali Alfajiri au Magharibi. Hii inajuzu kutokana na yaliyopita ya kutolazimu kuwa sawa niya mbili, na kwa kipimo cha Swalaah ya aliyetanguliwa kwa rakaa, au mkazi kumfuata msafiri anayepunguza.
(c) Idadi ya rakaa za maamuma kuwa kidogo zaidi ya rakaa za imamu. Hii haijuzu. Ni kama anayeswali Alfajiri nyuma ya anayeswali Adhuhuri, au Magharibi nyuma ya ‘Ishaa. Sababu ya kutojuzu ni kuwa ni lazima maamuma akhilafiane na imamu wake katika vitendo vya dhahiri; ima kwa kufarikiana naye ili yeye atoe tasliym, au amsubiri aje atoe tasliym pamoja naye, au asimame naye kuthibitisha umaamuma wake na idadi ya rakaa za Swalaah yake zizidi kimakusudi, na hili litaitengua Swalaah yake.
Lakini je, maamuma anaweza kungoja mpaka imamu akabakisha idadi ya rakaa zilizo sawa na Swalaah yake, kisha akajiunga naye na kutoa tasliym kwa pamoja? Suala hili ni la kutafitiwa na kupekuliwa. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
4- Mwenye kuswali kamili kumfuata mwenye kupunguza:
Hii inajuzu. Mwenye kuswali kamili ni lazima amalizie rakaa zilizobakia baada ya imamu wake kutoa tasliym. Hakuna mvutano wowote kati ya Maulamaa katika hili.
Imehadithiwa toka kwa ‘Imraan bin Haswiyn (Radhwiya Allaahu Anhu) akisema: “Nilishiriki vita pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), na nilikuwa pamoja naye katika ukombozi wa Makkah. Alikaa Makkah masiku 18 haswali isipokuwa rakaa mbili. Alikuwa akisema: “Enyi wenyeji wa mji! Swalini rakaa nne, kwani sisi ni wasafiri”. [Hadiyth Dhwaíyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (1229)].
Pamoja na udhwa’íyf wake lakini kiuhalisia inatumika, kwani mkazi ni lazima aswali nne, na haijuzu aache rakaa yoyote.
·
Faida
Haishurutishwi kutia niya ya kupunguza kwa anayetaka kupunguza Swalaah. [Majmu’u Al-Fataawaa (24/21, 104/105)]
Ndivyo walivyosema Masalaf wote. Hakuna yeyote aliyenukulu toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba aliwaamuru Maswahaba wake; si kwa niya ya kupunguza wala niya ya kukusanya, na wala Makhalifa wake hawakuwa wakimwamuru kufanya hivyo aliyekuwa akiwafuata. Hii ni pamoja na kwamba waamuriwa au wengi wao, hawajui alifanyalo imamu. Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipotoka kwa Hijjah yake, aliswali pamoja nao Adhuhuri mjini Madiynah rakaa nne, na akaswali nao Dhul Hulayfah rakaa mbili nyuma yake ukiwa umma wa watu usiohesabika. [Hadiyth Swahiyh: Itakuja katika mlango wa Hajji]
Wote hao walitoka kuhiji pamoja naye, na wengi wao walikuwa hawajui Swalaah ya safari; ima kwa ugeni wao katika Uislamu, au kuwa hawakuwahi kusafiri hususan akina mama.
Linaloonyesha kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali kwa kupunguza na Maswahaba wake na wala hawajulishi kabla ya kuingia kwenye Swalaah kwamba yeye anapunguza, ni Hadiyth ya Dhul Yadayn isemayo kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitoa tasliym baada ya rakaa mbili katika Swalaah ya Adhuhuri au Alasiri kwa kusahau, naye Dhul Yadayn akamuuliza: “Je, umepunguza Swalaah au umesahau?” Akajibu: “Sikusahau wala haikupunguzwa”. Akasema: “Naam, umesahau”. [Hadiyth Swahiyh: Itakuja katika mlango wa Sijdah ya kusahau]. Rasuli hakumwambia: “Lau kama ningelipunguza, ningekujulisheni ili mtie niya ya kupunguza”.
Ninasema: “Faida ya hili ni kuwa msafiri anaposwali nyuma ya imamu katika mji fulani na akamwona amepunguza Swalaah, basi atatoa tasliym pamoja naye, na wala haishurutishwi kuwa alinuwia kupunguza kabla ya Swalaah”.
5- Mwenye kupunguza kumfuata mwenye kuswali kamili:
Hii inajuzu, lakini maamuma atalazimika wakati huo aswali rakaa nne hata kama alimfuata imamu kwa kitambo kifupi. Na hii ni kwa dalili zifuatazo:
- Imepokelewa toka kwa Muusa bin Salamah akisema: “Tulikuwa pamoja na Ibn ‘Abbaas Makkah. Nikamwambia: Sisi tukiwa nanyi, tunaswali rakaa nne, na tunaporejea kwenye msafara wetu, tunaswali rakaa mbili”. Akasema: “Hiyo ni Sunna ya Abul Qaasim Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (1/216), Ibn Khuzaymah (952) na Al-Bayhaqiy (3/153). Angalia Al-Irwaa (3/21)].
- Imepokelewa kwamba Ibn ‘Umar alipokuwa akiswali na imamu, huswali rakaa nne, na anaposwali peke yake, huswali rakaa mbili. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim].
- Imepokelewa toka kwa Abu Mujlaz akisema: “Nilimwambia Ibn ‘Umar: Msafiri huzipata rakaa mbili za wenyeji. Je, zitamtosha rakaa mbili, au aswali pamoja nao? Alicheka akasema: Ataswali pamoja nao”.[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bayhaqiy (3/157). Angalia Al-Irwaa (3/22)].
Haijuzu kumfuata anayeswali Swalaah ambayo vitendo vyake ni tofauti na Swalaah yake. Ni kama anayeswali Adhuhuri kumfuata anayeswali Swalaah ya maiti, au Swalaah ya Kupatwa Jua na kadhalika. Hili litapelekea kwenda kinyume na vitendo vya dhahiri vya imamu, na hii haifai.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
016-Nguzo Za Swalaah
Alhidaaya.com [3]
Nguzo za Swalaah ni maneno na vitendo vinavyounda uhakika na uhalisia wa Swalaah. Ikiwa nguzo moja kati ya nguzo hizi itawachwa, basi Swalaah haiswihi, haizingatiwi kisharia, na haiungwi kwa sijdah ya sahau.
Kuacha Nguzo Katika Swalaah
[Ibn ‘Aabidiyn (1/297, 318), Ad-Dusuwqiy (1/239, 279) na Kash-Shaaful Qinaa (1/385, 402)]
Mwenye kuacha nguzo katika Swalaah, haachi kuwa ima:
(a) Ameiacha makusudi: Mwenye kuacha nguzo yoyote ya Swalaah kwa kusudi, Swalaah yake itabatilika na haitoswihi kwa Ijma’a ya Maulamaa.
(b) Au ameiacha kwa kusahau au kwa kutojua: Ikiwa ataweza kuitadaraki na kuitenda, itakuwa ni wajibu, na kama hatoweza kuitadaraki, basi Swalaah yake itaharibika kwa mujibu wa kauli ya Mahanafi. Ama kwa upande wa Jamhuri ya Maulamaa, itafutwa tu rakaa ambayo aliacha nguzo, isipokuwa tu kama aliacha takbiyr ya kuhirimia Swalaah, hapo itabidi aanze Swalaah upya kwa kuwa hajaingia aslani katika Swalaah.
Nguzo za Swalaah Ni:
1- Kusimama katika Swalaah ya faradhi kwa mwenye kuweza
Dalili ya hili ni:
(a) Neno Lake Allaah Mtukufu:
((حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ))
((Shikamaneni na Swalaah na khaswa Swalaah ya katikati (Alasiri), na simameni mbele ya Allaah katika hali ya utiifu.)) [Al-Baqarah (2:238)]
(b) Neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kumwambia ‘Imraan bin Haswiyn:
(( Swali kwa kusimama, ukishindwa swali kwa kukaa, ukishindwa swali kwa ubavu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1117), Abuu Daawuud (939), na At-Tirmidhiy (369)].
(c) Maulamaa wote kwa Ijma’a, wamekubaliana kwamba kusimama ni nguzo katika Swalaah ya faradhi kwa atakayeweza. Pia wamekubaliana kwamba nguzo hii haimhusu mgonjwa kama hawezi kusimama, huyu ataswali kwa kukaa. Pia nguzo hii haimuhusu anayeweza kusimama, ikiwa kusimama huko kunamwia uzito na mashaka makubwa, au anahofia kuzidi maradhi yake, au kukawia kupona.
Imepokelewa na Anas akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alianguka toka juu ya farasi akachubuka ubavu wake wa kulia. Tukaenda kumzuru na wakati wa Swalaah ukafika. Alituswalisha kwa kukaa, nasi tukaswali nyuma yake kwa kukaa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (378) na Muslim (411) na tamko ni lake].
Ibn Qudaamah amesema: “Inavyoonekana ni kuwa hakuwa ameshindwa kabisa kusimama, lakini kwa vile ilikuwa ni uzito na tabu, kisimamo kilipomoka kwake na kwa wengine”. [Al-Mughniy (2/571)]
·
Faida
(a) Swalaah ya Sunnah inajuzu juu ya kipando katika safari yoyote; ndefu au fupi, lakini haifai mjini. Yameelezwa haya katika masharti ya kuelekea Qiblah.
(b) Inajuzu kuswali Swalaah ya Sunnah kwa kukaa (hata bila ya udhuru) lakini thawabu za anayesimama ni kubwa zaidi. Thawabu za anayekaa ni nusu ya thawabu za anayesimama.
Imepokelewa toka kwa ‘Imraan bin Haswiyn (Radhwiya Allaahu Anhu) akisema: “Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu Swalaah ya anayeswali kwa kukaa akasema:
((Akiswali kwa kusimama, basi ni bora zaidi, na mwenye kuswali kwa kukaa, atapata nusu ya thawabu za mwenye kusimama, na mwenye kuswali kwa kulala, atapata nusu ya thawabu za mwenye kukaa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1115), At-Tirmidhiy (371), An-Nasaaiy (3/223) na Ibn Maajah (1231)].
Al-Khattwaabiy amesema: “Makusudio hapa ni mtu anayechukulika kuwa mgonjwa anayeweza kujihemeza akasimama kwa tabu, yakafanywa malipo ya mwenye kukaa nusu ya malipo ya mwenye kusimama kwa ajili ya kumtia utashi wa kusimama ingawa anaruhusika kukaa”.
Al-Haafidh amesema: “ Ni makisio mazuri”. [Fat-hul Baariy (2/585) chapa ya Al-Ma’arifah]
Ninasema: “Nguvu ya makisio haya ipo katika kauli yake Rasuli ((na mwenye kuswali kwa kulala, atapata nusu ya thawabu za mwenye kukaa)), kwa maana kwamba Swalaah ya mwenye kuswali kwa kulala kwa ubavu bila ya udhuru haifai kwa mujibu wa kauli ya Jamhuri hata kama ni Swalaah ya Sunnah, kwa kuwa haijulikani kabisa kwamba kuna yeyote katika Uislamu aliyeswali kwa kulala ubavu akiwa mzima. Na kama hili lingelikuwepo, basi Waislamu wangelilifanya katika enzi ya Nabii wao (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) au baada yake, na angelifanya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ijapokuwa mara moja ili kubainisha kujuzu kwake. [Majmu’u Fataawaa Ibn Taymiyah (23/235)]
Anas amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwatokea watu wakiwa wanaswali kwa kukaa (kwa sababu ya ugonjwa) akasema: ((Hakika Swalaah ya mwenye kukaa, ni nusu ya thawabu ya mwenye kusimama)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Maajah (1229) na Ahmad (3/214), na ziada ni yake. Angalia kitabu cha Swifatu Swalaahatin Nabiy ukurasa wa 78].
Ninasema: “Hivi ndivyo Al-Khattwaabiy alivyoichukulia Hadiyth ya ‘Imraan kuwa inahusiana na Swalaah ya faradhi na Al-Haafidh akaliridhia hilo. Lakini wengi wameichukulia kuwa inahusiana na Swalaah ya Sunnah sawasawa kwa mwenye udhuru na asiye na udhuru, kwa kuwa inaonyesha kwamba kusimama katika Swalaah ya Sunnah siyo nguzo bali ni mustahabu. Hili linaongezewa nguvu na kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali Swalaah ya Sunnah safarini juu ya mnyama wake lakini si Swalaah ya faradhi. Ama Hadiyth ya Anas, hakuna pingamizi ndani yake, kwa kuwa inaonyesha kwamba inaruhusika kiujumla kuswali kwa kukaa katika Swalaah ya Sunnah. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
Ujumuishi huu unatiliwa nguvu na yale yaliyothibiti kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali Swalaah za Sunnah kwa kukaa kama Hadiyth ya ‘Aaishah isemayo kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipowanda na kupata mwili, alikuwa akiswali Swalaah zake nyingi kwa kukaa. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (732)].
Aidha, yaliyothibiti kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akianza Swalaah ya usiku kwa kusimama, kisha hukaa. Hili litazungumziwa karibuni”.
·
Faida mbili
Ya kwanza: Thawabu za Swalaah ya mwenye kukaa kwa udhuru hazipungui. Sababu ni kuwa yeye kwa kawaida huswali kwa kusimama, na maradhi au mfano wake ndio yaliyomzuilia, hivyo malipo yake ni kamili kutokana na neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama ilivyo katika Al-Bukhaariy (2996):
((Anayegonjeka au akasafiri, huandikiwa aliyokuwa akiyafanya katika hali ya uzima na ukazi)).
Ya pili: Kati ya umahususi maalumu wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni kuwa yeye hapunguziwi thawabu hata kama ataswali Swalaah ya Sunnah kwa kukaa bila udhuru. [Sharhu Muslim cha An-Nawawiy na Fat-hul Qadiyr (1/460)]
Hii ni kwa Hadiyth ya ‘Abdullah bin ‘Amri aliyesema: “Nilihadithiwa kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Swalaah ya mtu aliyekaa ni nusu ya Swalaah)). Nikamwendea, nikamkuta anaswali kwa kukaa, nikauweka mkono wangu juu ya kichwa chake akaniambia: ((Una nini ee ‘Abdullah bin ‘Amri?)). Nikamwambia: “Nimehadithiwa ee Rasuli wa Allaah kwamba umesema: Swalaah ya mtu aliyekaa ni nusu ya Swalaah, nawe unaswali kwa kukaa!! Akasema: (( Naam, lakini mimi si kama yeyote kati yenu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (735), An-Nasaaiy (1659), na Abuu Daawuud (950)].
(c) Mtu anaweza kufungua kisomo katika Swalaah ya Sunnah kwa kukaa, kisha akasimama kwa mujibu wa makubaliano ya Maulamaa. Na hii ni kutokana na Hadiyth ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu Anha) aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaswali kwa kukaa. Anasoma naye amekaa, na Suwrah anayoisoma inapobakia kiasi cha aya 30 au 40, husimama akasoma kwa kusimama, kisha hurukuu na kusujudu, halafu hufanya hivyo hivyo katika rakaa ya pili”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1119) na Muslim (731)].
(d) Mtu anaweza kufungua kisomo katika Swalaah ya Sunnah kwa kusimama, kisha akakaa kutokana na Hadiyth iliyotangulia.
(e) Mwenye kuswali kwa kukaa, ni bora akae katika umbo la mkao wa tashah-hud. Atakaa mkao wa “iftiraash” katika hali ya kusimama na kurukuu, kwa kuwa Hadiyth za ‘Imraan na ‘Aaishah zilizotangulia hazikuainisha kikao, na makusudio ya moja kwa moja tunayoyafahamu ya kikao ni kile kilichozoeleka katika Swalaah. Hata hivyo, kikao cha “tarabbu’i” kinajuzu na hasahasa kwa ajili ya udhuru, kwani hili limeripotiwa kufanywa na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). [Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (3/224), Ibn Khuzaymah (2/236) na Al-Bayhaqiy (2/305). Angalia kitabu cha Swifatu Swalaatin Nabiy ukurasa wa 80]
Na pia baadhi ya Maswahaba wake. [Imehadithiwa toka kwa Ibn ‘Umar katika Muswannaf Ibn Abiy Shaybah (2/220)]
Ama kunyoosha miguu miwili wakati wa kuswali kwa kukaa, hili halifai isipokuwa kwa udhuru.
(f) Swalaah ya mwenye kuswali kwa ubavu inajuzu kwa udhuru sawasawa katika Swalaah ya faradhi au ya Sunnah ikiwa hawezi kukaa. Ama katika Swalaah ya Sunnah kama hakuna udhuru, Jamhuri wanaona kwamba haifai kisharia kwa kuwa haikunukuliwa kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wala kwa Swahaba yake yeyote kwamba alifanya hivyo angalau kwa mara moja.
Ninasema: “Lau kama mtu atashikamana na dhahiri ya Hadiyth ya ‘Imraan iliyotangulia: ((Na mwenye kuswali kwa kulala, atapata nusu ya thawabu za aliyekaa)), je, atakuwa na haki? Jibu sahihi ni kuwa ana haki. Na haya ni madhehebu ya Ibn Hazm katika Al-Muhallaa (3/56) ambayo yameungwa mkono na Ibn ‘Uthaymiyn katika Al-Mumti’i (4/113).”
(g) Mwenye kuswali kwa kulala kwa ubavu, imesuniwa alalie ubavu wake wa kulia akielekeza uso wake Qiblah, kwa kuwa imesuniwa kufanya hivyo wakati mtu anapotaka kulala, na kwa Hadiyth ya ‘Aaishah asemaye: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akipendezwa kuanza kwa kulia katika kuvaa viatu, kutembea, kujitwaharisha na katika mambo yake yote”. [Hadiyth Swahiyh: “Takhriyj” yake imetangulia mara nyingi].
Na kama hawezi kulala kwa ubavu ila kwa namna maalumu, basi itabidi hivyo hivyo. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
·
Kusimama Katika Swalaah Ya Faradhi Kwenye Ndege Na Meli
Mwenye kuabiri ndege au meli, ni lazima asimame wakati wa kuswali Swalaah ya faradhi kama ataweza. Na kama atahofia kuanguka, kughariki na mfano wake, basi atahesabiwa kuwa hawezi. Hapo ataswali kwa kukaa na ataashiria kwa kichwa katika rukuu na sujudi. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa kuhusu kuswali katika meli akajibu:
((Swali humo kwa kusimama ila tu kama utahofia kughariki)). [Al-Albaaniy ameipasisha kuwa Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bazzaaz (68) na wengineo. Angalia Swifatu Swalaahatin Nabiy ukurasa 79].
·
Kuegemea Kitu Wakati Wa Kusimama
Mwenye kuswali kwa kuegemea ukuta, bakora na mfano wake kwa sababu ya udhuru, hili Maulamaa wamekubaliana kwamba linajuzu kwa kuwa imebidi lifanyike. Allaah Amesema:
((فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ وَاسْمَعُوا وَأَطِيعُوا وَأَنفِقُوا خَيْرًا لِّأَنفُسِكُمْ ۗ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ))
((Basi mcheni Allaah muwezavyo, na sikilizeni; na tiini na toeni (kwa ajili ya Allaah) ni kheri kwa ajili ya nafsi zenu. Na yeyote anayeepushwa na ubakhili na tamaa ya uchu wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu)). [At-Taghaabun (64:16)]
Imepokelewa toka kwa Ummu Qays binti Muhswin kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipozeeka na kupata mwili, aliweka nguzo katika sehemu yake ya kuswalia ili kuiegemea)). [Al-Albaaniy kaiipasisha kuwa Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (948), Al-Bayhaqiy (2/288) na Al-Haakim (1/264). Angalia Asw-Swahiyhah (319)].
·
Mtu akiswali nyuma ya imamu aliyekaa kwa udhuru, naye ataswali kwa kukaa juu ya kauli sahihi kama itakavyokuja kuelezewa katika mlango wa Swalaah ya jamaa.
2- Takbiyr ya kuhirimia
Hii ni nguzo kati ya nguzo za Swalaah kwa makubaliano ya Maulamaa wote kutokana na dalili zifuatazo:
1- Neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Ufunguo wa Swalaah ni twahara, mlango wake ni takbiyr, na kutoka kwake ni tasliym)). [Al-Albaaniy kaipasisha kuwa Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (61) na At-Tirmidhiy (3). Ameipasisha kuwa Swahiyh katika Al-Irwaa (301)].
2- Neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa aliyeswali kwa kukosea:
((Ukisimama kuswali, basi piga takbiyr)). [Hadiyth Swahiyh. Imetajwa kikamilifu pamoja na “takhriyj” yake]
3- Katika tamshi la Hadiyth ya aliyeswali kwa kukosea:
((Hakika haitimu Swalaah ya yeyote katika watu mpaka atawadhe, na atawadhe kama inavyotakikana, kisha aseme: Allaahu Akbar)). [Al-Albaaniy kaipasisha kuwa Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Twabaraaniy (5/38). Angalia Swifatus Swalaahat (uk.86)].
Imepokelewa na ‘Aaishah akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifungua Swalaah kwa takbiyr”.[Hadiyth Swahiyhy. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (498)].
“Na takbiyr hapa, ni ile ijulikanayo na wote ambayo umma kupitia kizazi hadi kizazi, umeinukuu moja kwa moja toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye yeye alikuwa akiitamka katika kila Swalaah (Allaahu Akbar), na hakusema neno jingine zaidi ya hilo hata mara moja”. [Tahdhiyb As-Sunan cha Ibn Al-Qayyim (1/49)]
Haitojuzu kuingia kwenye Swalaah bila ya kusema (Allaahu Akbar). Hii ndiyo kauli ya nguvu ya Ath-Thawriy, Maalik, Ahmad na Ash-Shaafi’iy [isipokuwa yeye amejuzisha kusema: Allaahu Al-Akbar]. Na hili limeripotiwa toka kwa Ibn Mas-’oud.
Lakini Abuu Haniyfah amekwenda kinyume na hao akisema: “Swalaah inafungika kwa kila Jina la Allaah Mtukufu lenye utukuzo kama: Allaahu Al-Adhwiym, au Al-Kabiyr, Au Al-Jaliyl, au Subhaana Allaah, au Al-Hamdulil Laah na kadhalika.” Anasema: “Wote wamesema hivi, kama ilivyo katika khutba ambayo hakuna tamko moja lililoainishwa”!!
Hakuna shaka kwamba kipimo hiki hakifai, kwa kuwa amekifanya kwenda kinyume na Hadiyth. Kauli ya Jamhuri ndiyo sahihi. [Ibn ‘Aabidiyn (1/442), Al-Mudawwanah (1/62), Al-Ummu (1/100), Al-Majmu’u (3/233) na Al-Mughniy (1/333)]
·
Takbiyr Haijuzu Ila Kwa Kiarabu Kwa Mwenye Kuweza
Takbiyr haiswihi kwa lugha nyingine isiyo Kiarabu kwa mwenye kuweza kuitamka kwa kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akipiga takbiyr kwa Lugha ya Kiarabu, na wala hakutumia lugha nyingine kamwe. Naye ndiye mwenye kusema: ((Swalini kama mnavyoniona nikiswali)). [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (631) na Ahmad toka katika Hadiyth ya Maalik bin Al-Huwayrath].
Kwa asiyeweza kuitamka takbiyr kwa Kiarabu, itabidi ajifundishe, lakini kama atahofia kupitwa na wakati wa Swalaah kabla hajajifundisha, au hakuweza kabisa kuitamka kwa Kiarabu, basi hapo ataisema kwa lugha yake. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
3- Kusoma Al-Faatihah katika kila rakaa
Kusoma Al-Faatihah ni nguzo katika kila rakaa ya kila Swalaah ya Sunnah au ya faradhi, ya kusoma kwa sauti au kwa sauti ya chini. Hii ni kauli ya Ath-Thawriy, Maalik, Ash-Shaafi’iy na Ahmad. Nalo limehadithiwa toka kwa ‘Umar bin Al-Khattwaab na ‘Uthmaan bin Abul ‘Aasw. [Al-Mudawwanah (1/66), Al-Ummu (1/93), Al-Majmu’u (3/285), Al-Mughniy (1/343) na Al-Awsatw (3/101)]
Dalili ya hili ni:
1- Hadiyth ya ‘Ubaadah bin Swaamit kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Hakuna Swalaah kwa asiyesoma Faatihahtul Kitaab )). [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (756), Muslim (394) na wengineo].
2- Hadiyth ya Abuu Hurayrah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Mwenye kuswali Swalaah yoyote bila kusoma Faatihahtul Kitaab, basi Swalaah hiyo ni pungufu, ni pungufu, ni pungufu, haikutimu)). [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (41), Abuu Daawuud (821), An-Nasaaiy (2/135), At-Tirmidhiy (312) na Ibn Maajah (838)].
Swalaah pungufu haiwezi kuitwa kuwa ni Swalaah. Linaloonyesha kwamba upungufu unaokusudiwa hapa ni ule unaoifanya Swalaah isikamilike, ni ukamilisho wa Hadiyth hii kwa Muslim usemao kuwa Abu As- Saaib alisema: “Nilimwambia Abuu Hurayrah: “Wakati mwingine mimi ninakuwa nyuma ya imamu. Abuu Hurayrah akanibonyeza mkono akaniambia: Isome mwenyewe”.
3- Riwaya ya Rifa’a bin Raafi’i katika Hadiyth ya aliyeswali kimakosa, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia:
((..kisha soma Ummul Qur-aan, halafu soma Suwrah uitakayo..kisha fanya hivyo hivyo kila rakaa)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (18225). Na neno lake (Soma Ummul Kitaab) si la kawaida, Is-Haaq bin ‘Abdullah kalitumia yeye peke yake. Sheikh wetu Abuu ‘Umayr Allaah Amhifadhi amelihariri katika Shifaaul ‘Ayyi (1/192)]
Abuu Haniyfah kwa mujibu wa riwaya toka kwa Ahmad, anasema kwamba si lazima kusoma Suwrat Al-Faatihah, na kwamba inatosha kusoma Aayah yoyote ya Qur-aan. Hoja ya kauli hii ni dalili zifuatazo:
1- Neno Lake Ta’alaa:
((فَاقْرَءُوا مَا تَيَسَّرَ مِنَ الْقُرْآنِ ۚ ))
((Basi someni kile kilicho chepesi katika Qur-aan)). [Al-Muzzammil (73:20)]
Amejibiwa kwamba makusudio ya Aayah Tukufu ni Al-Faatihah pamoja na Suwrah nyepesi. Pia kuna uwezekano kwamba iliteremka kabla ya kuteremshwa Suwrat Al-Faatihah.
2- Katika Hadiyth ya Abuu Hurayrah kuhusiana na kisa cha aliyeswali kwa kukosea, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia mtu yule:
((Soma kilicho chepesi kwako katika Qur-aan)). [Hadiyth Swahiyh: Imekariri mara nyingi nyuma].
Anajibiwa kwamba neno lake (kilicho chepesi) ambacho hakikuainishwa ni kipi hasa, kimebainishwa kuwa ni Al-Faatihah katika riwaya isemayo: ((Soma Ummul Qur-aan)) kama itakuwa sahihi!! Kwa kuwa Al-Faatihah, ilikuwa ndiyo Suwrah nyepesi ya kuhifadhiwa na Waislamu. Imesemwa pia kwamba makusudio ya (kilicho chepesi), ni Suwrah nyingine zaidi ya Al-Faatihah kwa kuunganisha dalili tofauti.
3- Lau kama Suwrat Al-Faatihah ingelikuwa ni nguzo, basi ingelazimu kujifunza, na wala Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) asingeliruhusu kisomwe kingine mbadala kama ilivyo katika tamko la Hadiyth ya aliyeswali kwa kukosea lisemalo: ((Ikiwa umehifadhi chochote katika Qur-aan (soma), na kama huna basi mhimidi Allaah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (856)].
Anajibiwa kwamba hili alilipitisha wakati mtu anapokuwa hajahifadhi chochote katika Qur-aan. Pia linaweza kufungamanishwa na kutoweza mtu kujifundisha Qur-aan kama ilivyo katika Hadiyth ya Ibn Abiy Awfaa kwamba mtu mmoja alisema: “Ee Rasuli wa Allaah! Mimi siwezi kujifunza chochote katika Qur-aan, basi nifundishe kitakachonitosheleza katika Swalaah yangu”. Akamwambia: ((Sema: Subhaanal Laah, walhamdulil Laah, walaailaaha illal Laahu, wal Laahu Akbar, walaahawla walaaquwwata illaa bil Laahi)). [Al-Albaaniy kaipa daraja ya Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (832) na wengineo. Angalia Al-Irwaa (303)].
Ninasema: “Hapana shaka yoyote kwamba kauli ya Jamhuri ndiyo yenye nguvu zaidi, nayo ndiyo inayopasa kufuatwa. Swalaah ambayo haikusomwa ndani yake Suwrat Al-Faatihah haiswihi kwa mwenye kuweza kuihifadhi kutokana na Hadiyth ya ‘ibaadah iliyotangulia ambayo haitiwi doa na lolote katika hayo yaliyotangulia. Kwa kuwa Hadiyth hii (kwa makadirio ya chini kabisa) ina hukmu ya ziada mbali ya ile iliyoko kwenye Aayah pamoja na Hadiyth ya aliyeswali kwa kukosea. Hivyo basi, ni lazima kuitumia.”
Kisha ikiwa mwonekano wa Hadiyth hizi utajumlishwa na Hadiyth ya Abuu Qataadah isemayo: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisoma Faatihahtul Kitaab katika kila rakaa”[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (759) kwa maana yake], ongezea na kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa aliyeswali vibaya: ((Kisha fanya hivyo katika Swalaah yako yote)), yaani katika kila rakaa, basi hayo yote yanaonesha kwamba kusoma Al-Faatihah katika kila rakaa ni nguzo bila kuwepo tofauti kati ya imamu na maamuma, au kati ya imamu kusoma kwa sauti ya chini au ya juu kwa mujibu wa maelezo yatakayokuja baadaye.
·
Kusoma Basmalah (Bismil Laahi Ar Rahmaan Ar Rahiym) Mwanzoni Mwa Al-Faatihah
Maulamaa wamekhitalifiana kuhusiana na hukmu ya kusoma basmalah mwanzoni mwa Suwrat Al-Faatihah kwa mujibu wa mahitilafiano yao kuhusu mas-ala ya: Je, “basmalah” ni Aayah katika Suwrat Al-Faatihah au si Aayah?
Lililo sahihi ni kuwa basmalah ni Aayah katika Qur-aan kabla ya kila Suwrah kwa kuwa imethibitishwa katika Msahafu ingawa (kwa mujibu wa kauli yenye nguvu) si Aayah katika Suwrat Al-Faatihah. Hivyo ni lazima kuisoma kabla ya Al-Faatihahh kwa mujibu wa msimamo wa Jamhuri ya Maulamaa. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
·
Asiyeweza Kuihifadhi Al-Faatihahh
Al-Khattwaabiy amesema: [Maalimus Sunan]
“Kiasili ni kuwa Swalaah haikamiliki ila kwa kusoma Suwrat Al-Faatihahh, na ni mantiki kwamba kuisoma Suwrat Al-Faatihahh ni kwa mwenye kuimudu, na si kwa asiyeimudu. Na ikiwa mwenye kuswali haimudu lakini anaweza kusoma Aayah zingine za Qur-aan, basi itamlazimu asome kiasi cha Aayah saba za Qur-aan, kwa kuwa dhikri bora zaidi baada ya Al-Faatihahh ni Aayah mfanowe katika Qur-aan. Na kama mtu hana uwezo wa kujifunza chochote katika Qur-aan kutokana na ulemavu wa kimaumbile, au udhaifu wa hifdhi, au matatizo ya ulimi wake, au kilema, basi dhikri bora kwake baada ya Qur-aan itakuwa ni tasbiyh, tahmiyd, tahliyl n.k kama alivyofundisha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)”.
Ninasema: “Ni neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa asiyeweza kuhifadhi Al-Faatihahh:
((Sema: Subhaanal Laahi, walhamdulil Laahi, walaailaaha illa Laahu, wal Laahu Akbar, walaa hawla walaa quwwata illaa bil Laah)). [Imetangulia karibuni].
4, 5- Kurukuu, na kutulizana katika rukuu
Kurukuu ni nguzo katika kila rakaa ya Swalaah kwa Ijma’a ya Maulamaa. [Maraatibul Ijma’a cha Ibn Hazm ukurasa wa 26]
Dalili zao ni:
1- Neno Lake Ta’alaa:
((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ارْكَعُوا وَاسْجُدُوا وَاعْبُدُوا رَبَّكُمْ وَافْعَلُوا الْخَيْرَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ))
(( Enyi walioamini! Rukuuni, na sujuduni na mwabuduni Rabb wenu, na fanyeni ya kheri ili mpata kufaulu)). [Al-Hajji (22:77)]
2- Neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa aliyeswali kwa kukosea: ((Kisha rukuu mpaka utulie hali umerukuu)). [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa mara nyingi nyuma].
3- Kudumu Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuifanya rukuu katika kila Swalaah pamoja na kauli yake: ((Swalini kama mnavyoniona nikiswali)). [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa hivi karibuni].
Uchache wa kutosheleza rukuu ni kuinama mtu kiasi cha mikono yake kukamata magoti.
Ama kutulizana, ni kwa neno lake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Kisha rukuu mpaka utulie hali umerukuu)).
Na kwa neno lake:
((Haikamiliki Swalaah yoyote ambayo mtu hanyooshi uti wake wa mgongo katika rukuu na sujudi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (2/183), At-Tirmidhiy (264), Abuu Daawuud (840) na Ibn Maajah (870)]
Kutulizana ni nguzo katika rukuu (na sujudi) kwa mujibu wa Jamhuri ya Maulamaa kinyume na Abuu Haniyfah. [Al-Mabsuutw (1/21), Al-Mudawwanah (1/71), Al-Majmu’u (3/407) na Al-Mughniy (1/360)]
Nako hutimu kwa kutulia na kunyamaa viungo vya mtu kama alivyomweleza Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mtu aliyeswali kwa kukosea:
((Haitimu Swalaah ya mmoja wenu mpaka atawadhe wudhuu kamili, kisha arukuu na aweke mikono yake juu ya magoti yake mpaka viungo vyake vitulie na vinyamae)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (859), An Nasaaiy (2/20), At-Tirmidhiy (302) na Ibn Maajah (460)].
Imesemwa: Ni kwa kadiri ya dhikri ya wajibu katika rukuu.
6, 7- Kuitadili (Kusimama sawa) baada ya rukuu na kutulizana
Ni kwa neno lake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa aliyeswali kwa kukosea:
((Kisha nyanyuka mpaka utulizane ukiwa umenyanyuka)).
Na katika Hadiyth ya Abuu Humayd (katika Sifa ya Swalaah ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)): ” Na anaponyanyua kichwa chake, hulingamana sawa mpaka irudi kila pingili ya uti wa mgongo (vertebra) mahala pake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (828)].
Na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Swalini kama mnavyoniona nikiswali)).
Kunyanyuka toka kwenye rukuu kunaingia katika nguzo ya kuitadili kwa kuwa kunalazimiana nako.
8, 9- Kusuduju na kutulia katika sajdah
Kusujudu mara mbili katika kila rakaa, ni nguzo katika nguzo za Swalaah kwa Ijma’a ya Maulamaa. Na dalili yake ni:
1- Neno Lake Ta’alaa:
((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ارْكَعُوا وَاسْجُدُوا وَاعْبُدُوا رَبَّكُمْ وَافْعَلُوا الْخَيْرَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ))
((Enyi walioamini! Rukuuni, na sujuduni na mwabuduni Rabb wenu, na fanyeni ya kheri ili mpata kufaulu.)) [Al-Hajj (22:77)]
2- Neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa aliyeswali kwa kukosea:
((Kisha sujudu mpaka utulie ukiwa umesujudu)).
3- Neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Haikamiliki Swalaah yoyote ambayo mtu hanyooshi uti wake wa mgongo katika rukuu na sujudi)). [Hadiyth Swahiyh: Imetangulia hivi karibuni].
4- Neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
(( Hana Swalaah mtu ambaye pua yake haigusi sehemu ya ardhi kama kinavyogusa kipaji chake)). [Al-Albaaniy kaipasisha kuwa Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Ad-Daara Qutwniy (1/348). Angalia Sifa ya Swalaahah ukurasa 142].
5- Neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Timizeni rukuu na sujudi. Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu iko Mkononi Mwake, hakika mimi nawaoneni nyuma yangu mnaporukuu na kusujudu)). [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (418) na Muslim (424) kutoka kwenye Hadiyth ya Abuu Hurayrah].
Ni lazima sijdah iwe juu ya viungo saba: Viganja viwili, magoti mawili, nyanyo mbili na kipaji cha uso pamoja na pua kutokana na Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu Anhumaa) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Tumeamrishwa tusujudu juu ya viungo saba: Kipaji – akaashiria kwa mkono wake kwenye pua – mikono miwili (na katika tamko jingine: viganja viwili), magoti mawili, ncha za miguu miwili, na wala tusiikusanye nguo sehemu moja au nywele)). [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (812) na Muslim (490)].
10, 11- Kikao kati ya sijdah mbili na kutulizana
Ni nguzo kati ya nguzo za Swalaah kutokana na neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa aliyeswali kwa kukosea:
((Kisha sujudu mpaka utulie ukiwa umesujudu, kisha nyanyuka mpaka utulie ukiwa umekaa, kisha sujudu mpaka utulie ukiwa umesujudu)).
Imepokelewa na ‘Aaishah amesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa hasujudu mara ya pili anaponyanyua kichwa chake toka kwenye sajdah mpaka alingamane akiwa amekaa”. [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (498) na Ibn Maajah (893)].
Ash-Shaafi’iy na Ahmad wamesema kuwa hii ni nguzo, na Maalik hakusema lolote. Ama Abuu Haniyfah, kwake inatosha kunyanyua kichwa kama ncha ya upanga!! [Al-Ummu (1/100), Al-Majmu’u (3/412), Al-Mughniy (1/375), Al-Mudawwanah (1/70) na Ibn ‘Aabidiyn (1/474)]
12, 13- Tashah-hudi ya mwisho na kikao chake
Ni nguzo kati ya nguzo za Swalaah. Swalaah hubatilika kwa kuiacha kwa kukusudia au kwa kusahau kutokana na dalili zifuatazo:
1- Hadiyth ya Ibn Mas-’oud (Radhwiya Allaahu Anhu) aliyesema: “Kabla ya kufaradhishwa kwetu tashah-hudi, tulikuwa tukisema: Assalaamu ‘alal Laahi kabla ‘ibaadihi, assalaam ‘alaa Jibriyl, assalaam ‘alaa Miykaaiyl. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatuambia:
((Msiseme: Assalaamu ‘alal Laahi, lakini semeni: At-Tahiyyaatu lil Laahi…mpaka mwisho wake)). [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” kwa tamko la: ( قبل أن يفرض علينا ) na An-Nasaaiy (3/40) na Al-Bayhaqiy (2/138). Angalia Al-Irwaa (309) na asili yake ni katika Swahiyh Mbili].
Hii ni dalili kwamba tashah-hudi ilifaradhishwa baada ya kuwa si faradhi.
2- Hadiyth ya Ibn Mas-’oud kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Anapokaa mmoja wenu katika Swalaah basi aseme: At-Tahiyyaatu lil Laahi…..)). [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (831) na Muslim (402)].
3- Kudumu Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuifanya.
Hii ndiyo kauli ya Ash-Shaafi’iy na Ahmad. Maalik anasema kwamba tashah-hudi ni Sunnah na wala si nguzo isipokuwa sehemu inapofanyika tasliym!! Ama Abuu Haniyfah, yeye anaona kwamba kukaa kiasi cha tashah-hudi ndiyo nguzo, ama tashah-hudi yenyewe si lazima!! [Al-Ummu (1/102), Al-Mughniy (1/387), Mawaahibul Jaliyl (2/525), Al-Mabsuutw (1/29)]
Wanaosema kwamba tashah-hudi si lazima hawakuleta dalili yoyote isipokuwa wanasema kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakumfundisha Swahaba aliyeswali kwa kukosea. Naam! Hii itafaa kuwa ni hoja na dalili itakapothibiti kwamba Hadiyth ya aliyeswali kwa kukosea ilikuja baada ya kuwajibishwa tashah-hudi. Lakini ikiwa Hadiyth hiyo ilikuja kabla ya kuwajibishwa, basi hakuna pingamizi ya kuja upya wajibu katika mawajibiko ambayo hayakuwemo kabla, kwa kuwa kuyabana mawajibiko yaliyoko kwenye Hadiyth hiyo tu na kuzifumbia macho dalili nyinginezo zilizokuja baada yake zenye kupasisha ulazima wa tashah-hudi, ni kuziba mlango wa sharia na kuyapa mgongo mawajibiko yote mapya yaliyokuja kuhusiana na Swalaah. Na kama historia ya suala haijulikani, basi kusema kuwa ni wajibu ni bora zaidi kwa kuwa yako yenye kuthibitisha wajibu huo. Isitoshe, hakuna chochote cha uhakika chenye kuondosha wajibu huo. Hivyo ni lazima kwa mwenye dalili za wajibu huo, kushikamana na dalili hizo. [As- Saylul Jarraar (1/219) na Naylul Awtwaar (2/309). Chapa ya Al-Hadiyth]
·
Muundo Wa Tamko La Tashah-hudi
Imepokelewa toka kwa Ibn Mas-’oud (Radhwiya Allaahu Anhu) akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alinifundisha tashah-hudi viganja vyangu vikiwa kati ya viganja vyake kama anavyonifundisha Suwrah ya Qur-aan:
(( التحيات لله والصلوات لله والطيبات، السلام عليك أيها النبي ورحمة الله وبركاته، السلام علينا وعلى عباد الله الصالحين، أشهد أن لا إله إلا الله وأشهد أن محمدا عبده ورسوله))
((At-Tahiyyaatu lil-Laahi, was- Swalaawaatu lil-Laahi, wat-Twayyibaatu, As- Salaamu ‘alayka ayyuhan-Nabiyyu warahmatul-Laahi wabarakaatuh, as- Salaamu ‘alaynaa wa’ala ‘ibaadil- Laahis- swaalihiyna. Ash-hadu an laailaaha illal-Laahu wa ash-hadu anna Muhammadan ‘Abduhu wa Rasuwluhu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (6265) na Muslim (402)].
Huu ndio muundo sahihi zaidi wa tamko la tashah-hudi. Haya ndiyo waliyoyasema Abuu Haniyfah na masahibu zake, Ath-Thawriy, Ahmad, Is-Haaq, Abuu Thawr na Jamhuri ya Maulamaa. [Al- Awsatw cha Ibn Al-Mundhir (3/207) na Al-Muhallaa (3/207)]
Lakini hata hivyo, Maulamaa wamekubaliana kwamba miundo yote ya matamshi ya tashah-hudi iliyothibiti toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inafaa. Baadhi yake itakuja mbeleni.
·
Faida
Katika baadhi ya Sanad za Hadiyth hii ya Ibn Mas-’oud, yamekuja baadhi ya yanayolazimia mapishano katika neno lake (As Salaamu ‘Alayka) kati ya wakati wa uhai wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa tamshi la nafsi ya pili (msemeshwa), na kati ya baada ya kufariki kwake kwa tamshi la nafsi ya tatu (mzungumzwa): (As-Salaam ‘alan- Nabiyyi). Katika tamko lililopo kwa Al-Bukhaariy (6265) baada ya kuleta tashah-hudi, Ibn Mas-’oud alisema: “Na yeye akiwa hai nasi, na baada ya kufariki tulisema: As-Salaam, yaani juu ya Rasuli”.
Al-Haafidh ameitilia nguvu katika Al-Fat-h (2/366) akisema: “Imesihi bila shaka yoyote, nami nimempata mtu makini aliyeifuatilia. ‘Abdur Raaziq amesema: “Ibn Jariyj ametueleza, amenieleza ‘Atwaa kwamba wakati Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa hai, Maswahaba walikuwa wakisema: As-Salaamu ‘alayka ayyuhan Nabiyyu, na baada ya kufariki walisema: As-Salaam ‘alan Nabiyyi”. Na hii ni Isnadi Swahiyh.
Al-‘Allaamah Al-Albaaniy Rahimahul Laahu amesema: “Ni lazima hilo liwe ni kwa matni thabiti toka kwake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hili linatiliwa nguvu na kwamba ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu Anhaa) alikuwa akiwafundisha tashah-hudi katika Swalaah”. [Swifatu Swalaatin Nabiy ukurasa wa 161]
14- TASLIYM (KUTOA SALAAM)
Jamhuri ya Maulamaa wote isipokuwa Abuu Haniyfah wanasema kwamba tasliym ni nguzo ya Swalaah kwa dalili zifuatazo:
1- Neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):)
((na kutoka kwake ni tasliym)). [Al-Albaaniy kaipa daraja ya Hadiyth Swahiyh. Imeshatajwa nyuma].
2- ‘Aaishah amesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akimaliza Swalaah kwa tasliym”. [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (498) na Abuu Daawuud (783)].
3- Kudumu Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuifanya.
Imesemwa kwamba dalili hizi hazifikii ngazi ya kuipa tasliym hukumu ya kuwa ni nguzo, kwa kuwa tasliym haikutajwa katika Hadiyth ya aliyeswali kwa kukosea mpaka ijulikane kwamba Hadiyth ya ((kutoka kwake ni tasliym)) ilikuja baadaye nyuma. Hivi ndivyo alivyosema Ash-Shawkaaniy. [Naylul Awtwaar (2/352)]
Ninasema: “Hapa amekwenda kinyume na yale aliyokuwa ameyakubali (katika yale niliyoyanukuu kutoka kwake yakieleza kuwa tashah-hudi ni wajibu) ya kwamba kama historia haijulikani, basi kusema ni wajibu kutakuwa na nguvu zaidi kutokana na Hadiyth yenye kuashiria ulazima. Linaloweza kuzozaniwa ni kuwa je Hadiyth ya ((mlango wake ni takbiyr, na kutoka kwake ni tasliym)) ni Swahiyh au la? Anayeona kuwa ni Swahiyh, basi itamlazimu kuizingatia tasliym kuwa ni nguzo.
Jingine linaloonyesha kwamba tasliym ni nguzo ni dalili hizi zingine zifuatazo:
4- Hadiyth ya Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( Anapofanya shaka mmoja wenu katika Swalaah yake akawa hajui ameswali rakaa ngapi, je ni tatu au nne, basi aiweke kando shaka yake, kisha ajengee juu ya lile aliloliyakinisha, halafu asujudu sijdah mbili kabla ya kutoa tasliym)). [Hadiyth Swahiyh. Itakuja katika mlango wa sijdah ya kusahau].
5- Hadiyth ya Ibn Mas-’oud (kuhusiana na sijdah ya kusahau) : ”…basi alipanie lile analoliona kwamba ni sawa, kisha atoe tasliym, halafu asujudu sijdah mbili za kusahau”. [Hadiyth Swahiyh. Itakuja katika mlango wa sijdah ya kusahau]
Katika Hadiyth hizi mbili, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameamuru kutoa tasliym katika kila Swalaah hata ile ambayo mtu amesahau kitu ndani yake. Na amri hii pamoja na dalili nyingine zilizotangulia, zinajulisha kwamba tasliym ni faradhi. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
Ama kwa upande wa Abuu Haniyfah, yeye anasema kwamba tasliym mbili ni jambo la khiyari na wala si katika faradhi za Swalaah, bali ikiwa mtu atakaa kiasi cha tashah-hudi, basi Swalaah yake inakuwa imetimu. Kauli yake hii imetolewa dalili kwa riwaya ya Hadiyth ya Ibn Mas-’oud alipofundishwa tashah-hudi na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kuambiwa:
((Ukisema hivi, basi Swalaah yako imemalizika, ukitaka kusimama simama, na ukitaka kukaa kaa)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Hazm katika Al-Muhalla (3/279) na Al-Bayhaqiy katika Al-Khilaafiyyaat kama ilivyo katika An-Nayl (2/251)].
·
Je, Inatosheleza Tasliym Moja, Au Lazima Tasliym Mbili?
Ash-Shaafi’iy, Maalik na Jamhuri ya Maulamaa wanasema kwamba tasliym ya kwanza ndio nguzo, ama ya pili ni Sunnah. Ibn Al-Mundhir kasema: “Maulamaa wote mashuhuri wamejuzisha Swalaah ya tasliym moja ingawa linalopendeza zaidi ni kufanya tasliym mbili”.
An-Nawawiy kasema: “Maulamaa wakubwa weledi wamekubaliana kwamba haipasi isipokuwa tasliym moja tu!!”
Ninasema: “Ahmad bin Hanbali (katika riwaya iliyopokelewa toka kwake) amekwenda kinyume nao kwa kusema kwamba tasliym mbili ni lazima, na haya ndio madhehebu ya Hanbali. Hivi ndivyo pia walivyosema akina Ibn Hazm, Ahlu Dh-Dwaahir, baadhi ya wafuasi wa Maalik na Al-Hasan bin Swaaleh. Dalili zao ni hizi zifuatazo:
1- Kudumu Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kufanya tasliym mbili pamoja na Hadiyth yake isemayo: ((Swalini kama mnavyoniona nikiswali)), na hakuna Hadiyth yoyote Swahiyh waliyoipokea kwamba Rasuli alifanya tasliym moja.
2- Neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa Maswahaba wake alipowaona wanaashiria kwa mikono yao wakati wa kutoa tasliym:
(( Inamtosha mmoja wenu kuweka mkono wake juu ya paja lake na kumtolea salamu nduguye aliye kuumeni kwake na kushotoni kwake)). [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (431)].
Wamesema: “Kisichotosha, hakitoshelezi”.
Jamhuri ya Maulamaa wametoa dalili zifuatazo za kujuzisha kwao tasliym moja:
1- Hadiyth isemayo: ((..na kutoka kwake ni tasliym)). Ni kwamba tamko hili si ainishi na linaweza kumaanisha tasliym moja tu.
2- Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Ubayya Awfaa aliyesema: “Nilimuuliza ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu Anhaa) kuhusiana na Swalaah anayoswali Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) usiku. Kati ya aliyoyasema: “Hakai mpaka anapofika rakaa ya nane, na hapo hukaa kwa ajili ya tashah-hudi, kisha husimama bila kutoa tasliym, na huswali rakaa moja. Halafu hukaa, akasoma tashah-hudi na kuomba du’aa, kisha hutoa tasliym moja akisema: As-Salaam ‘Alaykum kwa sauti ya juu ya kutufanya tuamke”. [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim].
Na katika tamko la Muslim (746): “..kisha hutoa tasliym tunayoisikia”. Inawezekana hapa ikawa moja au mbili, isipokuwa tasliym moja imethibiti toka kwa Maswahaba wengi akiwemo Anas na Ibn ‘Umar.
·
Faida Mbili
Ya kwanza: Uchache wa tamko linalotosha katika tasliym ni kusema “As-Salaamu ‘Alaykum” kwa mujibu wa kauli sahihi zaidi, lakini ukamilifu na ubora zaidi ni kusema “As-Salaamu ‘Alaykum wa Rahmatul Laahi” kulia na kushoto.
Ya pili: Je, kuna nyongeza ya neno “Wa Barakaatuhu” katika tasliym? [Huu ni muhtasari wa utafiti murua uliofanywa na ndugu yetu Ibrahiym Sheikh – Allaah Amlipe jaza yake – ukiwa na anwani isemayo: “Matamko ya Tasliym katika Swalaah”. Utafiti huu ulitolewa utangulizi na Sheikh wetu Mustwafa Al-‘Adawiy (Allaah Ainyanyue hadhi yake)]
La sahihi lililothibiti toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika tasliym ni kusema “As-Salaamu ‘Alaykum wa Rahmatul Laahi” kulia na kushoto. Hili limepokelewa toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa Sanad Swahiyh katika Hadiyth ya Jaabir bin Samrah, Ibn ‘Umar na Ibn Mas-’oud.
Ama nyongeza ya “Wa Barakaatuhu”, hii haikuja ikiwa marfu’u kwa isnadi isothabiti isipokuwa kupitia kwa Muusa bin Qays toka kwa Salamah bin Kuhayl toka kwa ‘Al-Qamah toka kwa Waail bin Hajar. Ad-daaraqutwniy ameikosoa riwaya hii, na baadhi ya Maulamaa wamezungumzia shaka yao kuhusiana na ‘Al-Qamah kuisikia toka kwa baba yake. Haikuja ikiwa Mawquwf kwa Isnadi Swahiyh isipokuwa toka kwa Al-Aswad bin Yaziyd.
Ili kuiweka ziada hii katika hali ya usahihi na kutanua wigo wa ijtihada na uhakiki zaidi, tunasema kuwa kwa yule anayeona kuwa riwaya ni Swahiyh, basi atachukulia kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiisema mara chache sana katika tasliym ya kwanza. [Kafanya hivi Al’Allaamah Al-Albaaniy – Allaah Aitakase roho yake – katika kitabu cha Swifatus Swalaat]
Ama yule anayeichukulia kwamba ni Dhwa’iyf, basi aiache lakini asimshambulie mwenye kukhalifiana naye ambaye anaisema kwa nadra. Ama kudumu nayo kama wanavyofanya baadhi ya wanaodai kuwa ni wana Sunnah, huko ni kwenda kinyume kabisa na Sunnah.
Ijulikane kwamba wanachoona Jamhuri ya Maulamaa ni kufupisha na kusema: “As-Salaamu ‘Alaykum wa Rahmatul Laahi, As-Salaamu ‘Alaykum wa Rahmatul Laahi”.
15- Kufuatisha kimpangilio nguzo baada ya nyingine
Hii ni kutokana na yaliyothibiti kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), alikuwa akiswali kwa kuzifuatisha nguzo hizi kuongezea na neno lake: ((Swalini kama mnavyoniona nikiswali)). Aidha, alimfundisha aliyeswali kwa kukosea aswali kimpangilio kwa kusema: ((kisha..kisha)).
Na kwa vile Swalaah ni ‘ibaadah inayobatilika kwa hadathi, mpangilio umekuwa ni nguzo ndani yake kama ‘ibaadah nyinginezo. [Ad-Dusuwqiy (1/241), Mughnil Muhtaaj (1/158), Kash-Shaaful Qinaa (1/389) na Al-Mumti’i (3/426)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
017-Waajibati Za Swalaah
Alhidaaya.com [3]
Waajibati ni yale ambayo ni lazima kuyafanya au kuyasema katika Swalaah. Mambo haya yanapomoka kwa kusahau lakini huungwa kwa sijdah ya kusahau, na mwenye kuacha kwa kusudi, Swalaah yake itabatilika ikiwa anajua kwamba aliloliacha ni wajibu.
Tafsiri hii ni kwa Mahanafi na Mahanbali isipokuwa Mahanafi hawaoni kwamba mwenye kuwacha la wajibu kwa makusudi Swalaah yake inabatilika, bali atapata madhambi na anakuwa fasiki anayestahiki adhabu!!
Ama Maalik na Ash-Shaafi’iy, wao hawana isipokuwa nguzo na Sunnah kimjumuisho.
Wajibati katika Swalaah ni:
1- Du’aa ya ufunguzi wa Swalaah
Kwa mujibu wa kauli yenye nguvu, du’aa hii ni wajibu sawasawa ikiwa Swalaah ni ya faradhi au ni ya Sunnah. Ni lazima Swalaah ianzwe kwa du’aa hii baada ya takbiyr na kabla ya kusoma Al-Faatihahh kutokana na neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hadiyth ya Rifa’a bin Raafi’i kwa aliyeswali kwa kukosea:
((Hakika haitimu Swalaah ya yeyote katika watu mpaka atawadhe..kisha apige takbiyr, amhimidi Allaah Mtukufu na amsifu, asome kilicho chepesi katika Qur-aan. Na anapofanya hivi, basi Swalaah yake imetimia)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (859), An-Nasaaiy (2/20), At-Tirmidhiy (302) na Ibn Maajah (460)].
Neno lake ((Amhimidi Allaah Mtukufu na amsifu)) linaonyesha kwamba ni du’aa ya ufunguzi. Asw-Swan-’aaniy amesema: “Huchukuliwa kutokana na kauli hii kwamba ni wajibu kufanya himdi yoyote na sifa yoyote baada ya takbiyr ya kuhirimia Swalaah”. [Subulus Salaam (1/312)]
Ninasema: “Hakuna kinachozuia kusema kuwa ni wajibu, kwa kuwa Hadiyth ni Swahiyh, na hakuna makhitilafiano yoyote yaliyotokea kwa Ijma’a. Kusema kuwa ni wajibu ni kwa riwaya toka kwa Ahmad iliyokubaliwa na Ibn Battwah. [Al-Furu’u (1/413) na Al-Inswaaf (2/120)]
Na Ibn Rushdi katika Bidaayatul Mujtahid (1/172) ametoa kauli inayosema kwamba du’aa ya ufunguzi ni wajibu katika Swalaah akinukuu toka kwa Ash-Shaafi’iy na Abuu Haniyfah!! Nami sikupata linalotilia nguvu maneno haya kutoka kwa wawili hawa isipokuwa yaliyoandikwa kwenye Ad-Durru Al-Mukhtaar (1/476) yanayozingatia kwamba (kumsifu Allaah) ni katika mambo ya lazima katika Swalaah.
Na asili katika du’aa hii ya ufunguzi ni kufanywa kwa sauti ya chini, kwa kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuisoma kwa sauti ya juu na hata Maulamaa wote pia. Lakini katika baadhi ya nyakati, inafaa kwa Imamu kunyanyua sauti ili awafundishe watu. [Imetajwa mfanowe katika Al-Mughniy (2/145) toka kwa Ahmad]
Ni kama alivyofanya ‘Umar bin Al-Khattwaab aliposema: ((Subhaanakal Laahumma wa bihamdika))”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (399) ikiwa ni Munqatwi-’i. Ad-daaraqutwniy (1/199) na Al-Bayhaqiy (2/34) wameifanya ni Mawswuwl na wametilia nguvu kuwa ni Mawquwf. Naye ‘Abdur Raaziq (2555-2557) na Ibn Shaybah (1/230) wameifanyia “ikhraaj” kwa njia ya kuwa Mawswuwl na Munqatwi-’i. Angalia Al-Majmu’u (3/277) na Al-Irwaa (340)]
·
Du’aa Ya Ufunguzi Haisomwi Mahala Pawili
1- Katika Swalaah ya Maiti:
Du’aa hii haisomwi katika Swalaah hii kwa kuwa ni Swalaah ya muundo wa uhafifu na ufupi. Imepokelewa toka kwa Twalha bin ‘Ubaydul Laah bin ‘Awf aliyesema: “Niliswali nyuma ya ‘Abbaas katika Swalaah ya maiti. Alisoma Suwrat Al-Faatihahh akasema: Ili wajue kwamba ni Sunnah”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1335), Abuu Daawuud (3182), At-Tirmidhiy (1032), Ibn Maajah (2490), na An-Nasaaiy. Riwaya nyingine ni yake].
Na katika riwaya nyingine: “Akasoma Suwrat Al-Faatihah na Suwrah kwa sauti ili tupate kumsikia”.
Hapa kuna ishara ya kuwa du’aa ya ufunguzi haisomwi katika Swalaah ya maiti kwa kuwa hakuisoma ili awajulishe kama alivyodhihirisha kisomo cha Suwrat Al-Faatihah.
Imesemwa: “Bali inasomwa katika Swalaah hiyo kama Swalaah nyinginezo lakini kauli ya kwanza ndiyo iliyo karibu zaidi. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.”
2- Aliyetanguliwa kama atamkuta imamu hayuko katika kisimamo
Huyu hataisoma du’aa hii kwa kuwa mahala pake pashapita.
·
Muundo Wa Matamko Ya Du’aa Ya Ufunguzi
Kuna matamko mbalimbali sahihi ya du’aa hii yaliyopokelewa toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kati ya matamko hayo ni:
1- Hadiyth ya Abuu Hurayrah asemaye: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapoifungua Swalaah yake, hunyamaza kidogo hivi kabla ya kusoma. Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Naapa kwa baba yangu na mama yangu! Nakuona ukinyamaza kati ya takbiyr na kisomo, nini unasoma? Akasema: ((Ninasema:
اللهم باعد بيني وبين خطاياي كما باعدت بين المشرق والمغرب، اللهم نقني من خطاياي كما ينقى الثوب الأبيض من الدنس، اللهم اغسلني من خطاياي بالثلج والماء والبرد.
Al-Laahumma Baa’id bayniy wabayna khatwaayaaya kamaa Baa’adta baynal mashriqi wal maghribi. Al-Laahumma Naqqiniy min khatwaayaaya kama yunaqqa ath-thawbul abyadhu minad danasi. Al-Laahumma Ghsilniy min khatwaayaayi bith-thalji wal maai wal baradi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (744) na Muslim (598)].
2- Hadiyth ya Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu Anhu) aliyesema: “Tulikuwa tunaswali pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na mtu mmoja katika kundi akasema: ((Allaahu Akbaru Kabiyraa, wal-Hamdulil-Laahi Kathiyraa, wa Subhaanal-Laahi bukratan wa aswiylaa”. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Nimestaajabishwa nayo, milango ya mbingu imefunguliwa kwayo)).
Ibn ‘Umar akasema: “Sikuacha tokea nilipomsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiyasema hayo.”[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (601), At-Tirmidhiy (3592) na An-Nasaaiy (2/125)].
3- Hadiyth ya ‘Aaishah, Abuu Sa’iyd na wengineo kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisema wakati akifungua Swalaah:
(( سبحانك اللهم وبحمدك، وتبارك اسمك، وتعالى جدك، ولا إله غيرك))
((Subhaanakal Laahumma wa Bihamdika, wa Tabaaraka Smuka, Wa Ta’alaa Jadduka, wa Laailaaha ghayruka)). [Hadiyth Hasan kwa Sanad zake: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (776), At-Tirmidhiy (234), An-Nasaaiy (2/132), Ibn Maajah (806) na wengineo. Angalia Al Irwaa (341)].
Tumeshasema kwamba ‘Umar alikuwa akifungulia kwayo Swalaah.
4- Hadiyth ya ‘Aliyyi (Radhwiya Allaahu Anhu): “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaposimama kwa ajili ya Swalaah husema:
وجهت وجهي للذي فطر السموات والأرض حنيفا وما أنا من المشركين، إن صلاتي ونسكي ومحياي ومماتي لله رب العالمين، لا شريك له وبذلك أمرت وأنا أول المسلمين، اللهم أنت الملك، لا إله إلا أنت، أنت ربي وأنا عبدك، ظلمت نفسي واعترفت بذنبي فاغفر لي ذنوبي جميعا، إنه لا يغفر الذنوب إلا أنت، واهدني لأحسن الأخلاق لا يهدي لأحسنها إلا أنت، واصرف عني سيئها لا يصرف عني سيئها إلا أنت، لبيك وسعديك، والخير كله بيديك، والشر ليس إليك، أنا بك وإليك، تباركت وتعاليت، أستغفرك وأتوب إليك
Wajjahtu wajhiy lil Ladhiy Fatwaras Samaawaati wal Ardhwa haniyfan wamaa ana minal mushrikiyna, inna Swalaahaty wa nusukiy wamhyaaya wa mamaaty lil-Laahi Rabbil ‘aalamiyna, laa shariyka lahu, wabidhaalika umirtu wa ana awwalul Muslimiyna. Allaahumma Antal Maliku, laailaaha illaa Anta, Anta Rabbiy wa ana ‘Abduka, dhwalamtu nafsiy wa’ataraftu bidhanbiy jamiy’an, innahuu laa yaghfiru dh-dhunuuba illaa Anta, wahdiniy liahsanil akhlaaq laa yahdiy liahsanihaa illaa Anta, wa swrif ‘anniy sayyiahaa laa yaswrifu ‘anniy sayyiahaa illaa Anta. Labbayka wa sa’addayka, wal khayru kulluhuu biyadika, wash-sharru laysa ilayka, ana bika wa ilayka, Tabaarakta wa Ta’aalayta, astaghfiruka wa atuwbu ilayka)).
Tamko la: “Wa ana awwalul Muslimiyna” limethibiti, na hakuna tatizo lolote kumfuata Rasuli katika kulisoma. Inakuwa ni katika mlango wa kumfuata na si katika mlango wa mtu kujieleza kuwa yeye niMuislamu wa mwanzo.
Inasemwa kuwa alikuwa akilisema tamko hili katika Swalaah za faradhi na Sunnah. [Hadiyth Swahiyh:Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (771), Abuu Daawuud (760), At-Tirmidhiy (342) na An-Nasaaiy (2/130)].
Katika ambayo Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifungulia Swalaah za usiku ni yale yaliyokuja katika:
5- Hadiyth ya ‘Aaishah akisema: “Alikuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akifungua Swalaah yake ya usiku kwa kusema:
(( اللهم رب جبريل وميكائيل وإسرافيل، فاطر السموات والأرض، عالم الغيب والشهادة، أنت تحكم بين عبادك فيما كانوا فيه يختلفون، اهدني لما اختلف فيه من الحق بإذنك، إنك تهدي من نشاء إلى صراط مستقيم))
Allaahumma Rabba Jibriyl wa Miikaaiyl wa Israafiyl, Faatwiras Samaawaati wal ardhwi, ‘Aaalimal ghayb wash Shahaada, Anta Tahkumu bayna ‘ibaadika fiymaa kaanuw fiyhi yakhtalifuuna, Ihdiniy limakhtulifa fiyhi minal hakki biidhnika, innaka Tahdiy man Tashaau ilaa swiraatin mustaqiym)). [Hadiyth Swahiyh:Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (770)].
Ninasema: “Kuna du’aa nyingine sahihi za kufungulia Swalaah mbali ya hizi toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na anayetaka aziangalie kwenye vitabu husika”. [Angalia Swifatu Swalaatin Nabiy cha Al-Albaaniy (ukurasa wa 91-95) chapa ya Al-Ma’arif]
Katika matamko yaliyotangulia, kila kundi katika Maulamaa limechagua tamko lake mahsusi. [Al-Awsatw cha Ibn Al-Mundhir (3/86), Al-Ummu (1/106) na Masaail Ahmad cha Abuu Daawuud (30)]
Ath-Thwariy, Ahmad, Is-Haaq na Abuu Haniyfah na wenzake wamechagua yaliyopokelewa toka kwa ‘Umar [na ‘Aaishah na Abuu Sa’iyd].
Ash-Shaafi’iy amechukua Hadiyth ya ‘Aliyy. Abu Thawr anasema: “Yoyote atakayoisema itamtosheleza”, na Ibn Al-Mundhir ameichagua.
Ninasema: “Imesuniwa kusoma du’aa hii au ile ambayo ni nyepesi kwa mtu katika du’aa hizi”.
Ama Maalik (Allaah Amrehemu), alikuwa haoni kwamba du’aa hii ipo, au “isti’aadhah”, au “basmalah”!! [Al-Awsatw (3/86) na Al-Mudawwanah (1/62)] Na Hadiyth hizi na zinginezo ni hoja dhidi yake. Na Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
2- Kusema “Isti’aadhah” (A’uwdhu bil Laahi minash-shaytwaanir rajiym) kabla ya kusoma
Ni wajibu kwa kauli yenye nguvu kutokana na Kauli Yake Ta’alaa:
((فَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ))
((Unapotaka kusoma Qur-aan basi (kwanza) omba kinga kwa Allaah dhidi ya shaytwaan aliyetokomezwa mbali na kulaaniwa)). [An-Nahl (16:98)]
Katika Aayah hii, kuna amri ya kufanya isti’aadhah wakati mtu anapotaka kusoma Qur-aan, na uhakika wa amri hii ni wajibu kwa kuwa isti’aadhah inaondosha shari ya shaytwaan. Na lile ambalo wajibu hautimu ila kwalo, basi linakuwa wajibu.
Kati ya waliosema kuwa hili ni wajibu ni pamoja na ‘Atwaa, Ath-Thawriy, Al-Awzaa’iy, Daawuud na Ibn Hazm, nayo ni riwaya toka kwa Ahmad. [Al-Muhallaa (3/247), Al-Majmu’u (3/281), Al-Furu’u (1/413) na Al-Inswaaf (2/120)]
Jamhuri ya Maulamaa wanasema kwamba isti’aadhah ni Sunnah, na Maalik ameizuia!! [Ibn ‘Aabidiyn (1/328), Al-Dusuwqiy (1/251), Mughnil Muhtaaj (1/156) na Kash-Shaaf Al-Qina’a (1/335)]
· Miundo Ya Matamko Ya Isti’aadhah
Mwanzoni mwa kusoma Suwrah, isti’aadhah inaweza kusomwa kwa matamko yafuatayo:
- أعوذ با لله من الشيطان الرجيم
A’uwdhubil Laahi minash-shaytwaanir rajiym.
- أعوذ بالله السميع العليم من الشيطان الرجيم
A’uwdhubil Laahi As-Samiy’il ‘Aliym minash-shaytwaanir rajiym.
- أعوذ بالله السميع العليم من الشيطان الرجيم من همزه ونفخه ونفثه
A’uwdhubil Laahi As-Samiy’il ‘Aliym minash-shaytwaanir rajiym min hamzihi wa nafkhihi wa nafthih.
Ibn Qudaamah katika Al-Mughniy (2/146) anasema: “Huu wote ni wasaa, vyovyote atakavyoisema isti’aadhah, basi ni vyema”.
· Kuisoma Kimya Kimya
Asili ya isti’aadhah ni kuisoma kimya kimya, kwani haikunukuliwa toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba aliisoma kwa sauti wala kwa Makhalifa wake waongofu kuwa wao walidumu kuisoma kwa sauti. Lakini imamu katika baadhi ya nyakati, anaweza kuisoma kwa sauti ili awafundishe watu kwa mfano uliotangulia kutoka kwa Ibn ‘Abbaas.
· Je, Atairejea Kila Rakaa?
Maulamaa wengi wamesema kwamba inamtosheleza mtu kuisoma katika rakaa ya kwanza tu. Ash-Shaafi’iy anaona ni vizuri isomwe katika kila rakaa, na Ibn Siyriyn amesema kuwa ni lazima. [Al-Awsatw (3/89). Ibn Hazm katika Al-Muhallaa (3/254) anasema kuwa ni lazima kusoma “isti’aadhah” katika kila rakaa ya kwanza]
Ninasema: ”Uzingatio wa kusema ni wajibu ni kuwa Aayah inalazimia kukariri isti’aadhah wakati wa kuikariri Aayah. Na inapotokea mtengano kati ya visomo viwili kwa rukuu, sujudi na mfano wake, hapo inabidi kusoma isti’aadhah. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
3- Kuitikia “Aamiyn” baada ya Al-Faatihah
Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Imamu anaposema aamiyn, nanyi pia semeni aamiyn, kwani yeyote ambaye aamiyn yake inakutana na ya Malaika, hughufiriwa madhambi yake yaliyotangulia)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (780) na Muslim (410) kutoka kwa Hadiyth ya Abuu Hurayrah].
Jamhuri ya Maulamaa wameichukulia amri hii kama ni amri ya Sunnah, nami sikupata njia yoyote ya kuitoa amri hii nje ya uwajibu!!
Ibn Hazm amesema: “Ni wajibu kwa maamuma. Ama mwenye kuswali peke yake, au imamu, hao kwao ni Sunnah kutokana na Hadiyth iliyotangulia. [Ibn ‘Aabidiyn (1/320), Ad-Dusuwqiy (1/248), Mughnil Muhtaaj (1/160) Kash-Shaaful Qina’a (1/339), Al-Muhallaa (3/262) na Naylul Awtwaar (2/258)]
Imethibiti kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapomaliza kusoma Al-Faatihah husema “Aamiyn” kwa sauti na huivuta sauti yake. [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy katika Juz-ul Qiraa-at na Abuu Daawuud (932). Al-Albaaniy kasema kuwa ni Hadiyth Swahiyh katika Swifatus Swalaahat ukurasa wa 101].
Lililo sahihi ni kuwa kusema aamiyn ni lazima kwa imamu, maamuma, na mwenye kuswali peke yake katika hali yoyote, kwa sauti katika Swalaah ya kusoma kwa sauti, na kimya kimya katika Swalaah ya kusoma kimya kimya. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
4, 5, 6- Takbiyr za kuhama (toka nguzo kwenda nguzo), kusema “Sami’al Laahu liman hamidah”, na kusema “Rabbanaa lakal hamdu”.
Ni kwa dalili zifuatazo:
1- Neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Anapopiga takbiyr na nyinyi pigeni takbiyr, na anaposema: Sami’al Laahu liman hamida”, nanyi semeni: “Al-Laahumma Rabbanaa lakal Hamdu”)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (722) na Muslim (409)].
2- Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alidumu kufanya hivyo. Abuu Hurayrah amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapotaka kuswali, hupiga takbiyr wakati anaposimama, kisha hupiga takbiyr wakati anaporukuu, halafu husema: ”Sami’al Laahu liman hamidah” wakati anapounyanyua mgongo wake toka kwenye rukuu, kisha husema huku amesimama: “Rabbanaa lakal Hamdu”. Kisha hupiga takbiyr wakati anapopomoka (kwenda sijdah), halafu hupiga takbiyr wakati anapokinyanyua kichwa chake, kisha hupiga takbiyr wakati anaposujudu, halafu hupiga takbiyr wakati anapokinyanyua kichwa chake, kisha hufanya hivyo hivyo katika Swalaah yake yote mpaka anapoimaliza. Na hupiga takbiyr wakati anaponyanyuka baada ya kikao cha rakaa mbili”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (289) na Muslim (392)]
Mfano wa haya, yako katika Hadiyth ya Abuu Hamiyd As-Saa’idiy.
Na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Swalini kama mnavyoniona nikiswali)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (631)].
3- Amri ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa aliyeswali kwa kukosea katika Hadiyth ya Rifa’a bin Raafi’i:
((Hakika haitimu Swalaah ya yeyote katika watu mpaka atawadhe, na atawadhe kama inavyotakikana, kisha aseme: Allaahu Akbar na amhimidi Allaah ‘Azza wa Jalla na amsifu, kisha asome akitakacho katika Qur-aan, halafu aseme: Allaahu Akbar, kisha arukuu mpaka viungo vyake vitulie, halafu aseme: “Sami’al Laahu liman Hamidah” mpaka alingamane wima sawasawa, kisha aseme: “Allaahu Akbar”, kisha asujudu mpaka viungo vyake vitulie, halafu aseme: “Allaahu Akbar”, na anyanyue kichwa chake mpaka alingamane hali amekaa, kisha aseme: “Allaahu Akbar”, kisha asujudu mpaka viungo vyake vitulie. Halafu anyanyue kichwa chake apige takbiyr. Anapofanya hivi, basi Swalaah yake imetimu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (859), An-Nasaaiy (2/2), At-Tirmidhiy (302) na Ibn Maajah (460)].
4- Ni ujulisho wa kuhama toka nguzo hadi nyingine, na kipengee kwenda kingine. [Ash-Sharhul Mumti’i (3/432)]
Na mambo haya matatu ni wajibu katika Swalaah kwa mtu anayeswali peke yake, imamu na maamuma kwa kauli sahihi. Ni madhehebu ya Hanbali, na ni Sunnah kwa upande wa Jamhuri. [Ibn ‘Aabidiyn (1/334), Ad-Dusuwqiy (1/243), Mughnil Muhtaaj (1/165) na Kash-Shaaful Qinaa (1/348)]
· Faida
Imepokewa kwa njia sahihi toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) matamko manne katika tahmiyd baada ya kusema “Sami’al Laahu liman Hamida”, nayo ni:
1- ((ربنا لك الحمد))
Rabbanaa walakal Hamdu
[Al-Bukhaariy (689) na Muslim (392)]
2- ((اللهم ربنا ولك الحمد))
Allaahumma Rabbanaa walakal Hamdu
[Al-Bukhaariy (795), At-Tirmidhiy (3432), An-Nasaaiy (1060) na Abuu Daawuud (770)]
3- ((ربنا لك الحمد))
Rabbanaa lakal Hamdu
[Al-Bukhaariy (722) na Muslim (409)]
4- ((اللهم ربنا لك الحمد))
Allaahumma Rabbanaa lakal Hamdu
[Al-Bukhaariy (792) na Muslim (404)]
7- Tasbiyh katika rukuu na sujudi
Ni kusema “Subhaana Rabbiyal ‘Adhwiym” katika rukuu, na “Subhaana Rabbiyal A’alaa” katika sijdah. Ahmad bin Hanbal, Is-Haaq, Daawuud na Ibn Hazm wanasema kwamba ni lazima katika Swalaah. [Al-Inswaaf (2/115) na Al-Muhallaa (3/260)]
Dalili zao ni:
1- Hadiyth ya ‘Uqbah bin ‘Aamir aliyesema: “Wakati iliposhuka Aayah:
(( فسبح باسم ربك العظيم ))
..Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alituambia: ((Ifanyeni katika rukuu zenu)), na iliposhuka Aayah:
(( سبح اسم ربك الأعلى))
..alituambia: ((Ifanyeni katika sujudi zenu)). [Isnadi yake ni Laini: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (869), Ibn Maajah (887) na Ahmad (16773)]
Maulamaa wamesema kwamba amri hii ni ya wajibu kwa vile Amri za Allaah na Rasuli Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) zimekusanyika, na pia kutokana na kitendo chake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Ninasema: “Hadiyth ni laini katika Sanad yake isipokuwa inaafikiana na haya yafuatayo yanayoitilia nguvu:
2- Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Jueni na tambueni! Hakika mimi nimekatazwa kusoma Qur-aani katika rukuu na sijdah. Ama katika rukuu, basi mtukuzeni humo Mola ‘Azza wa Jalla. Ama sujudi, basi jitahidini kuomba du’aa humo, kwani ni stahikivu kwenu kujibiwa humo du’aa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (479) na Abuu Daawuud (876)].
3- Hadiyth ya Hudhayfah aliyesema: “Niliswali na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na katika rukuu alikuwa anasema: “Subhaana Rabbiyal ‘Adhwiym”, na katika sujudi: “Subhaana Rabbiyal A’alaa”. [Hadiyth Hasan Lighayrih: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (262), Abuu Daawuud (871), An-Nasaaiy (3/226) na Ibn Maajah (888)].
Jamhuri ya Maulamaa wanasema kwamba tasbiyh katika rukuu na sujudi ni Sunnah na si wajibu kwa kigezo kwamba Rasuli hakumwamuru kufanya hivyo aliyeswali kwa kukosea. [Ibn ‘Aabidiyn (1/474), Mawaahibul Jaliyl (1/525), Al-Ummu (1/101), na Al-Majmu’u (3/410)]
Hili litapata uimara kwa yule anayeoina Hadiyth ya ‘Uqbah bin ‘Aamir kama ni Dhwa’iyf na pia haoni Hadiyth nyingine yenye kuisapoti Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas. Ama yule ambaye anaona kwamba Hadiyth ya ‘Uqbah iko sawasawa, basi itamlazimu kusema kuwa hilo ni wajibu.
8, 9- Tashah-hud ya kati na kikao chake
Ni kwa amri yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa aliyeswali kwa kukosea katika Hadiyth ya Rifa’a – kwa kusema:
(( Unapokaa katikati ya Swalaah, basi tulizana ulitandike paja lako la kushoto, kisha fanya tashah-hudi)). [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (860) na Al-Bayhaqiy (2/133). Angalia Al-Irwaa (337)].
Na kwa dalili nyinginezo zilizotangulia zinazoonyesha kwamba tashah-hudi ya mwisho ni nguzo, tashah-hudi hii ya kati kati hatusemi kwamba ni nguzo kwa kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipoisahau, hakurudi tena kuifanya, bali aliiunga kwa sujudi ya kusahau. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1230) na Muslim (570) kutokana na Hadiyth ya ‘Abdullah bin Buhaynah]. Na lau kama ingelikuwa ni nguzo, basi isingeliungwa. [Ash-Sharh Al-Mumti’i (3/441)]
Ahmad, Is-Haaq, Al-Layth, Abuu Thawr, Daawuud na Ibn Hazm wanasema kuwa tashah-hudi ya katikati ni wajibu. Lakini Jamhuri ya Maulamaa wanasema kwamba ni Sunnah. [Al-Muhallaa (3/268) na Al-Majmu’u (3/430)]
Kwa kuwa lau kama ingelikuwa ni wajibu, basi isingelipomoka kwa kuisahau kama nguzo za Swalaah!!
Inajibiwa kwamba hili linakuwa ni dalili lau kama sujudi ya kusahau inahusishwa kwa kuacha lisilo la wajibu, na hilo haliruhusiwi. [As-Saylul Jarraar (1/229)]
Bali sujudi ya kusahau haifanywi ila kwa kuacha la wajibu kwa kuwa asili ni kuzuia ziada katika Swalaah, na sujudi ya kusahau kabla ya tasliym ni ziada katika Swalaah, na kuzuia huku hakukiukwi ila kwa kufanya la wajibu. Na itakapokuwa sujudi ya kusahau ni wajibu kwa kuacha kwake, hilo litaonyesha kwamba ni wajibu, na kama si hivyo, basi kuwepo kwake na kutokuwepo kungelikuwa ni sawa)). [As-Sharhul Mumti’i (3/443-444)]
· Kusoma Tashah-hudi Kimya Kimya
Maulamaa wote kwa sauti moja wanasema kwamba tashah-hudi mbili husomwa kimya kimya na ni karaha kusoma kwa sauti. Ni kwa vile haikunukuliwa toka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba alisoma kwa sauti, na watu tokea enzi ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mpaka hivi leo wamerithiana kusoma kimya kimya, na kurithiana ni kama tawaaturi. [Al-Mabsuutw (1/32). Angalia Al-Awsatw (3/207) na Al-Majmuu (3/444)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
018-Sunnah Za Swalaah
Alhidaaya.com [3]
Sunnah za Swalaah ni maneno au matendo ambayo yamesuniwa kuyafanya ndani ya Swalaah. Mwenye kuyafanya hupata thawabu, na Swalaah haibatiliki kwa kuyaacha hata kwa kusudi, na kwa kuyaacha pia hakuna sujudi ya kusahau.
Ijulikane kwamba katika mlango huu kuna mambo ambayo Maulamaa wote kwa pamoja wamekubaliana nayo, na kuna mambo mengine ambayo Maulamaa wamekhitalifiana. Kwa hiyo, imekuwa ni vizuri zaidi niyathibitishe yale tu ambayo dalili zake ni sahihi bila ya kujisokomeza kwenye yale waliyokhitalifiana kwa ajili ya kuchelea urefushaji mada, kwani makusudio hasa ni kuujua mwongozo wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika Swalaah yake ili tuweze kumfuata. Na baada ya kuujua mwongozo huu, hakuna madhara kumkhalifu mwenye kwenda kinyume vyovyote awavyo.
Sunnah hizi zimegawanyika katika Sunnah za kimaneno na Sunnah za kivitendo.
Sunnah Za Kimaneno
1- Kusoma baada ya Al-Faatihah
Imesuniwa kusoma Suwrah katika rakaa mbili za mwanzo baada ya Al-Faatihah kwa makubaliano ya Ijma’a ya Maulamaa. Aidha, imesuniwa vile vile, kusoma Suwrah wakati mwingine katika rakaa za tatu na nne.
Imepokelewa toka kwa Abuu Qataadah akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisoma katika rakaa mbili za mwanzo za Adhuhuri na Alasiri Al-Faatihah pamoja na Suwrah na wakati mwingine anatusikilizisha Aayah, na katika rakaa mbili za mwisho husoma Al-Faatihah tu”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (421), na mfanowe, na katika Al-Bukhaariy (759)].
Ama kusoma Suwrah katika rakaa ya tatu na ya nne, hii ni kwa Hadiyth ya Abuu Sa’iyd Al-Khudriy akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisoma katika Swalaah ya Adhuhuri kwenye rakaa mbili za mwanzo kiasi cha aya 30 katika kila rakaa, na katika mbili za mwisho kiasi cha aya 15”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (452)].
Kutokana na Hadiyth hii, tunapata faida nyingine kuwa imesuniwa Suwrah zinazosomwa katika rakaa mbili za mwanzo ziwe ndefu zaidi kuliko katika rakaa mbili za mwisho.
Mambo mengine yaliyosuniwa hapa ni pamoja na:
- Kuisoma Qur-aan kwa tartiyl na kuitadaburi kwa mujibu wa Ijma’a ya Maulamaa. Ni makruhu kuisoma haraka haraka kutokana na Neno Lake Ta’alaa:
((أَوْ زِدْ عَلَيْهِ وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلًا))
((Au izidishe, na soma Qur-aan kwa kisomo cha utaratibu upasao, kuitamka vizuri na kutaamali)). [Al-Muzzammil (73:4)]
- Kumwomba Allaah Mtukufu na kujilinda Kwake zinaposomwa Aayah za rehma au adhabu.
Imepokelewa toka kwa Hudhayfah akisema: “Niliswali pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) usiku mmoja akaanza na Al-Baqarah. Alikuwa akisoma kwa tartiyl na utuvu. Akiipita Aayah yenye tasbiyh husabbih, akiipita yenye du’aa huomba, akiipita ya kujilinda hujilinda, kisha hurukuu”. Imesimuliwa na Muslim.
- Aseme ndani ya Swalaah “Subhaanal Laah” anaposoma Neno Lake Ta’alaa:
((سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى ))
((Sabbih Jina la Rabb wako Mwenye ‘Uluwa Ametukuka kabisa kuliko vyote)). [Al-A’alaa (87:1)]
Na anaposoma:
((أَلَيْسَ ذَٰلِكَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يُحْيِيَ الْمَوْتَىٰ))
((Je hivyo sivyo (Allaah Anayeumba) kuwa ni Muweza wa kuhuisha wafu?)) [Al-Qiyaamah (75:40)]
..aseme “Subhaanaka fabalaa”. Dalili thabiti ya mawili haya ipo.
- Anaposoma:
((أَلَيْسَ اللَّـهُ بِأَحْكَمِ الْحَاكِمِينَ))
(( Je, kwani Allaah Si Mwadilifu zaidi wa wanaohukumu kuliko mahakimu wote?)) [At-Tiyn (95:8)]
..hairuhusiwi kusema: “Balaa, wa ana ‘alaa dhaalika minash shaahidiyn”, au kusema: “Aaman-naa bil Laahi” mtu anaposoma:
((فَبِأَيِّ حَدِيثٍ بَعْدَهُ يُؤْمِنُونَ))
(( Basi kauli gani baada ya hii (Qur-aan) wataiamini?)) [Al-Mursalaat (77:50)]
Au kusema: “Ista-‘antu bil Laahi” imamu anaposoma:
((إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ))
((Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada)). [Al-Faatihahh (1:5)]
Haya yote hayana Hadiyth yoyote inayoyathibitisha.
2- Kufanya adhkaari zifuatazo katika rukuu:
1-
(( اللهم لك ركعت، ولك أسلمت وبك آمنت، خشع لك سمعي وبصري ومخي وعظمي وعصبي ))
(( Allaahumma laka raka’atu, wa laka aslamtu wa bika aamantu, khasha’a laka sam’iy wa baswariy wa mukh-khiy wa ‘adhwmiy wa ‘aswabiy)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (771), At-Tirmidhiy (4317), Abuu Daawuud (760) na An-Nasaaiy (2/130)].
2-
(( سبحانك اللهم ربنا وبحمدك اللهم اغفر لي ))
(( Subhaanakal Laahumma Rabbanaa wa bihamdika, Allaahumma Ghfir liy)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (2/247) na Muslim (484) na wengineo].
3-
(( سبوح قدوس رب الملائكة والروح ))
((Subbuwhun Qudduwsun Rabbul Malaaikati war Ruwh)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (487) na Abuu Daawuud (872)].
4-
(( سبحان ذي الجبروت والملكوت والكبرياء والعظمة ))
((Subhaana Dhil Jabaruuti wal Malakuuti wal Kibriyaa wal Adhwamah)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (873) na An-Nasaaiy (2/191) kwa Sanad Swahiyh].
3- Kufanya dhikri baada ya kusimama kutoka kwenye rukuu na baada ya kusema “Rabbanaa Lakal Hamdu”. Adhkaar hizo ni:
1-
(( اللهم ربنا لك الحمد ملء السموات وملء الأرض وملء ما بينهما وملء ما شئت من شيئ بعد، أهل الثناء والمجد، أحق ما قال العبد وكلنا لك عبد، اللهم لا مانع لما أعطيت، ولا معطي لما منعت، ولا ينفع ذا الجد منك الجد))
((Al- Laahumma Rabbanaa Lakal Hamdu mil-as Samaawaati wa mil-al Ardhi wa mil-a maa baynahumaa wa mil-a maa shiita min shay-in baadu. Ahluth-Thanaai wal Majdi, ahaqqu maa qaalal ‘Abdu wa kul- lunaa Laka ‘Abdun. Allaahumma laa maani’a limaa A’atwayta, walaa mu’utwiya limaa Mana’ata, walaa yanfa’u dhal jaddi minkal Jaddu)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (477), Abuu Daawuud (747) na An-Nasaaiy (2/198)].
2-
(( ربنا ولك الحمد حمدا كثيرا طيبا مباركا فيه ))
((Rabbanaa wa Lakal hamdu hamdan kathiyran twayyiban mubaarakan fiyh)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (2/237), Abuu Daawuud (770), An-Nasaaiy (2/196) na At-Tirmidhiy (404)].
4- Kufanya dhikri katika sujudi. Adhkaar hizo ni:
1-
(( اللهم لك سجدت وبك آمنت، ولك أسلمت، سجد وجهي للذي خلقه وصوره، وشق سمعه وبصره، تبارك الله أحسن الخالقين))
((Al-Laahumma Laka sajadtu wa bika aamantu, wa Laka aslamtu, sajada wajhiy lil Ladhiy Khalaqahu wa Swaw-warahu, wa Shaqqa sam’ahu wa baswarahu. Tabaaraka Allaahu Ahsanul khaaliqiyna)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (771). Imeshatangulia].
2-
(( سبحانك اللهم ربنا وبحمدك اللهم اغفرلي ))
((Subhaanaka Al-Laahumma Rabbanaa wa bihamdika Allaahumma Ghfir liy )).
3-
(( سبوح قدوس رب الملائكة والروح ))
(( Subbuwhun Qudduwsun Rabbul Malaaikati war Ruwh)).
4-
(( سبحان ذي الجبروت والملكوت والكبرياء والعظمة ))
((Subhaana Dhil Jabaruuti wal Malakuuti wal Kibriyaa wal Adhwamah)). [Zote tatu zimetajwa hivi karibuni katika adhkaar za rukuu].
5- Kukithirisha kuomba du’aa katika sujudi kutokana na neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Ama sujudi, basi jitahidini kuomba du’aa humo, kwani ni stahikivu kwenu kujibiwa humo du’aa)). [Imetajwa hivi karibuni]
Na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisema wakati anaposujudu:
(( اللهم اغفر لي ذنبي كله، دقه وجله وأوله وآخره وعلانيته وسره))
((Allaahumma Ghfir liy dhanbiy kullahu, diqqahu wa jullahu, wa aw-walahu wa aakhirahu, wa ‘alaaniyyatahu wa sirrahu)) [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (483)].
5- Kuomba du’aa kati ya sijdah mbili. Du’aa hizo ni kama:
1-
((اللهم اغفر لي وارحمني واجبرني واهدني وارزقني))
((Allaahumma Ghfir liy Warhamniy Wajburniy Wahdiniy Warzuqniy)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (850) na At-Tirmidhiy (284). Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh].
2-
(( رب اغفرلي ..رب اغفر لي ))
(( Rabbi Ghfir liy..Rabbi Ghfir liy )). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (874) na An-Nasaaiy (3/226). Angalia Al-Irwaa (335)].
6- Kumswalia Rasuli baada ya tashah-hudi ya kwanza na ya mwisho
Imepokewa toka kwa ‘Aaishah akisema: “Tulikuwa tukimtayarishia Rasuli wa Allaah mswaki wake na maji yake ya kutawadhia. Halafu Allaah Humwamsha katika wakati Alioutaka usiku. Hupiga mswaki na kutawadha, kisha huswali rakaa tisa; hakai kati ya rakaa hizo isipokuwa katika rakaa ya nane. Na hapo humwomba Mola wake na humswalia Rasuli Wake, kisha hunyanyuka na wala hatoi tasliym. Kisha huswali rakaa ya tisa, akakaa, halafu humhimidi Mola wake, humswalia Nabii Wake, kisha hutoa tasliym”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (746)].
Tamko bora zaidi la kumswalia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni:
(( اللهم صل على محمد وعلى آل محمد كما صليت على آل إبراهيم إنك حميد مجيد، اللهم بارك على محمد وعلى آل محمد كما باركت على إبراهيم إنك حميد مجيد))
((Allaahumma Swalli ‘alaa Muhammadin wa’alaa aali Muhammadin kama Swallayta ‘alaa aali Ibraahiyma innaka Hamiydun Majiydun. Allaahumma Baariyk ‘alaa Muhammadin wa’alaa aali Muhammadin kamaa Baarakta ‘alaa Ibraahiyma innaka Hamiydun Majiydun)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (6357), Muslim (406) na wengineo].
7- Du’aa baada ya tashah-hudi ya kwanza na ya pili
Du’aa baada ya tashah-hudi ya kwanza imekuja kutokana na neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Mnapokaa katika kila rakaa mbili semeni: At-Tahiyyaatu lil-Laahi, was- Swalawaatu wat-Twayyibaatu, As- Salaamu ‘alayka ayyuhan-Nabiyyu warahmatul-Laahi wabarakaatuhu, as- Salaamu ‘alaynaa wa’alaa ‘ibaadil-Laahis-Swaalihiyna. Ash-hadu an laailaaha illal-Laahu wa ash-hadu anna Muhammadan ‘Abduhu wa Rasuwluhu. Kisha achague mmoja wenu du’aa inayompendeza, halafu amwombe Mola wake ‘Azza wa Jalla)). [“Takhriyj” yake ishatangulia].
Ama baada ya tashah-hudi ya pili ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Anapomaliza mmoja wenu tashah-hudi ya mwisho, basi ajilinde kwa Allaah na mambo manne: Adhabu ya Jahannam na adhabu ya kaburi, fitna ya uhai, fitna ya mauti, na shari ya Masihi Dajjaal)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (3/192), Muslim (588) na wengineo].
Na katika riwaya: ((na madhambi na madeni)).
Kuna du’aa nyinginezo Swahiyh kati ya tashah-hudi na tasliym. Kati ya du’aa hizo ni:
1-
(( اللهم إني ظلمت نفسي ظلما كثيرا، ولا يغفر الذنوب إلا أنت، فاغفر لي مغفرة من عندك، وارحمني إنك أنت الغفور الرحيم)).
(( Allaahumma inniy dhwalamtu nafsiy dhulman kathiyran, walaa yaghfiru dh-dhunuwba illaa Anta, Faghfir liy maghfiratan min ‘in-dika, warhamniy Innaka Anta Al-Ghafuwru Ar Rahiymu)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (6357), Muslim (406)].
2-
(( اللهم اغفر لي ما قدمت وما أخرت، وما أسررت وما أعلنت، وما أسرفت، وما أنت أعلم به مني، أنت المقدم، وأنت المؤخر لا إله إلا أنت ))
((Allaahumma Ghfir liy maa qaddamtu wamaa akh-khartu, wamaa asrartu wamaa a’alantu, wamaa asraftu, wamaa Anta A’alamu bihii minniy, Anta Al-Muqaddimu, wa Anta Al-Muakh-khiru laa ilaaha illaa Anta)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (771), Abuu Daawuud (760), At-Tirmidhiy (3417) na An-Nasaaiy (2/130)].
8- Tasliym ya pili
Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitoa tasliym mbili. Imepokelewa na ‘Aamir bin Sa’ad toka kwa baba yake akisema: “Nilikuwa nikimwona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akitoa tasliym kuliani kwake na kushotoni kwake mpaka ninaona weupe wa shavu lake”. [Imepokewa na Muslim (1/582)].
Tasliym ya kwanza ni nguzo lakini ya pili ni Sunnah. Imethibiti kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitosheka na ya kwanza basi. Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitoa tasliym moja mkabala wa uso wake akimili kidogo upande wa kulia)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (295) kwa Sanad Swahiyh].
9- Kuleta nyiradi na kuomba du’aa baada ya Swalaah
Ama nyiradi, kuna Hadiyth kadhaa Swahiyh zilizothibitisha hilo. Kati ya hizo ni:
1- ((Mwenye kufanya tasbiyh baada ya kila Swalaah mara 33, akamhimidi Allaah mara 33, na akapiga takbiyr mara 33, basi hizo ni mara 99, na akasema katika kutimiza 100: Laa ilaaha illa Allaahu Wahdahuu laa shariyka Lahuu, Lahul Mulku, Walahul Hamdu, wa Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr, basi husamehewa makosa yake hata kama yako mithili ya povu la bahari)). [Imepokewa na Muslim (597)].
2-
(( لا إله إلا الله وحده لا شريك له، له الملك وله الحمد وهو على كل شيئ قدير، لا حول ولا قوة إلا بالله، لا إله إلا الله، ولا نعبد إلا إياه، له النعمة والفضل، وله الثناء الحسن، لا إله إلا الله مخلصين له الدين ولو كره الكافرون))
((Laailaaha illa Allaahu Wahdahuu laa shariyka Lahuu, Lahul Mulku Walahul Hamdu Wahuwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyrun. Laa hawla walaa quwwata illaa bil Laahi, laa ilaah illa Allaahu, walaa na’abudu illaa Iyyaahu, Lahun ni’imata wal fadhwli, walahuth-thanaaul hasan. Laa ilaaha illa Allaahu mukhliswiyna Lahud Diyna walaw karihal kaafiruwna)). [Imepokewa na Muslim (594)].
3-
(( لا إله إلا الله، وحده لا شريك له، له الملك وله الحمد، وهو على كل شيء قدير، اللهم لا مانع لما أعطيت ولا معطي اما منعت، ولا ينفع ذا الجد منك الجد))
((Laailaaha illa Allaahu Wahdahuu laa shariyka Lahuu, Lahul Mulku Walahul Hamdu Wahuwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyrun. Allaahumma laa maani’a limaa A’atwayta, walaa mu’utwiya lima Mana’ata, walaa yanfa’u dhal jaddi mikal jaddu)). [Imepokewa na Al-Bukhaariy (844) na Muslim (471)].
4- Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapomaliza Swalaah yake husema: “Astaghfiru” mara tatu, kisha husema:
(( اللهم أنت السلام ومنك السلام، تباركت يا ذا الجلال والإكرام ))
((Allaahumma Anta As-Salaam waminka as-salaam, Tabaarakta yaa Dhal Jalaal wal Ikraam)). [Imepokewa na Muslim (591)].
5- Imepokelewa toka kwa ‘Uqbah bin ‘Aamir akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliniamuru nisome “Mu’awwadhaati” baada ya kila Swalaah”. [Imepokewa na Abuu Daawuud (1523), At-Tirmidhiy (2903) na An Nasaaiy kwa Sanad Swahiyh].
6- ((Mwenye kusoma aayatil Kursiy baada ya kila Swalaah ya faradhi, hayatazuia kati yake na kuingia peponi isipokuwa mauti)). [Imepokewa na Ibn As-Sunniy kwa Sanad Swahiyh]
Ama du’aa za kuomba baada ya Swalaah, du’aa hizo zimethibiti kwa njia sahihi toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa matamko mbalimbali. Kati yake ni:
1-
((اللهم أعني على ذكرك وشكرك وحسن عبادتك))
((Allaahumma A’inniy ‘alaa dhikrika wa shukrika wa husni ‘ibaadatika)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (1508) na An-Nasaaiy (3/53) kwa Sanad Swahiyh].
2-
((اللهم إني أعوذ بك من الجبن، وأعوذ بك أن أرد إلى أرذل العمر، وأعوذ بك من فتنة الدنيا، وأعوذ بك من عذاب القبر))
(( Allaahumma inniy auwdhu bika minal jubni, wa auwdhu bika an uradda ilaa ardhalil ‘umuri, wa auwdhu bika min fitnatid dunyaa, wa auwdhu bika min ‘adhaabil qabri)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (2822), At-Tirmidhiy (3562) na An-Nasaaiy (8/266)].
3-
(( رب قني عذابك يوم تبعث عبادك ))
((Rabbi Qiniy ‘adhaabaka yawma Tab’athu ibaadaka)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (709)].
4-
(( اللهم اغفر لي ما قدمت وما أخرت وما أسررت وما أعلنت وما أسرفت وما أنت أعلم به مني، أنت المقدم وأنت المؤخر، لا إله إلا أنت ))
(( Allaahumma Ghfir liy maa qaddamtu wamaa akh-khartu, wamaa asrartu, wamaa a’alantu, wamaa asraftu, wamaa Anta A’alamu bihii minniy, Antal Muqaddimu wa Antal Muakh-khiru, laailaah illaa Anta)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (771). Ishatajwa].
5-
((اللهم إني أسألك علما نافعا، ورزقا طيبا، وعملا متقبلا))
(( Al Laahumma inniy as-aluka ‘ilman naafi’an, wa rizqan twayyiban, wa ‘amalan mutaqqabalan )). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (771). Ishatajwa].
6-
(( اللهم إني أعوذ بك من الكفر والفقر وعذاب القبر))
((Allaahumma inniy a’uwdhubika minal kufri wal faqri wa ‘adhaabil qabri)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (8262) na Ibn As-Sunniy (111) kwa Sanad Hasan].
· Faida
Du’aa baada ya Swalaah inajibiwa Insha Allaah. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa: “Ni du’aa gani inajibiwa zaidi? Akajibu: ((Ni ile ya usiku wa manane, na baada ya Swalaah za faradhi)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (3499) na Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh].
· Sunnah Za Kivitendo
1- Kuweka kizuizi katika Swalaah
Imesuniwa kuweka mbele kizuizi kitakachozuia mtu kupita mbele yake na kuzuia macho yake yasitembee huku na kule kutokana na neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
(( إذا صلى أحدكم فليصل إلى سترة، وليدن منها، لا يقطع الشيطان عليه صلاته))
((Anaposwali mmoja wenu, basi aswali kikiweko kizuizi mbele yake na akikurubie ili shaytwaan asimkatizie Swalaah yake)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (681), An-Nasaaiy (2/62), na Al-Haakim (1/251). Tamko ni lake, nayo ni Swahiyh].
Kizuizi hiki kinaweza kuwa ni ukuta, nguzo, fimbo iliyokitwa na kadhalika. Uchache wa hilo ni kipande kidogo cha mbao anachokiegemea msafiri kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Anapoweka mmoja wenu mbele yake mfano wa kiegemeo cha msafiri, basi aswali na wala asishughulishwe na anayepita nyuma yake)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (499), At-Tirmidhiy (334) na Abuu Daawuud (671)].
Mtu akiweka kizuizi wakati anaswali, basi asimruhusu yeyote kupita mbele yake kutokana na neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Anaposwali mmoja wenu, basi asimruhusu kabisa mtu kupita mbele yake na amzuie kwa nguvu zake zote. Na kama atakataa basi apigane naye, kwani huyo ni shaytwaan)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (487) na Muslim (505) na wengineo].
Na hii ingawa baadhi ya Maulamaa wamelipinga hili kwa dalili sahihi lakini haziko wazi, au kwa dalili wazi lakini si sahihi. Wanasema kwamba hakuna kitu chochote chenye kuweza kuikata Swalaah, kwani makusudio ya kuikata katika Hadiyth, ni kuikata khushuu na si kubatilika Swalaah kwa mtu kupita tu mbele yake. [Zaadul Ma’ad (1/306) na Jaami’u Ahkaamin Nisaa (1/424)]
· Faida mbalimbali
[Jaami’u Ahkaamin Nisaa (1/414)]
1- Kupita msichana mdogo ambaye hakubaleghe mbele ya mwenye kuswali, hakuikati Swalaah kwa kuwa haitwi mwanamke. Qataadah anasema: “Mwanamke haikati Swalaah ya mwanamke”. Na aliulizwa: “Je, msichana ambaye hajabaleghe anaikata Swalaah?” Akajibu: “Hapana”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdur Razzaaq katika Al-Muswannaf (2/28) kwa Sanad Swahiyh iliyoegemezwa kwa Qataadah].
2- Mwanamke akipita kulia au kushotoni mwa mwanamume anayeswali, basi haikati Swalaah yake.
3- Mwanamke akisimama pembeni mwa mwanamume Swalaah yake haibatiliki. Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali usiku nami niko pembeni mwake nikiwa na hedhi na nimejifunika nguo, sehemu ya nguo iko pembezoni mwake”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (499)].
4- Ikiwa panaswaliwa jamaa, basi hakuna ubaya kupita kati ya safu, kwa kuwa kizuizi cha imamu ndio kizuizi cha maamuma. Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Abbaas akisema: “Nilikuja nikiwa nimepanda punda jike, na wakati huo nilikuwa nimekwisha baleghe. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiwaswalisha watu Mina. Nikapita mbele ya safu, nikateremka, kisha nikamwacha punda akajilie. Niliingia katika safu na hakuna yeyote aliyelipinga hilo”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (493), Muslim (504) na wengineo].
2- Kunyanyua mikono miwili wakati wa takbiyr ya kuhirimia, kurukuu, na kunyanyuka toka rukuuu. Pia wakati wa kunyanyuka toka tashah-hudi ya kwanza na katika kila kinyanyuko na kiinamo.
Imepokelewa na Naafi’i kwamba Ibn ‘Umar alikuwa anapoingia katika Swalaah hupiga takbiyr akanyanyua mikono yake miwili, anaporukuu hunyanyua mikono yake miwili, na anaposema “Sami’a Allaahu liman hamidah” na anaposimama toka rakaa mbili, hunyanyua mikono yake miwili”. Hilo limerufaishwa kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (739), Abuu Daawuud (727) na Hadiyth mwenza iko kwa Muslim (390)].
Ninasema: “Hizi ndizo sehemu nne ambazo ukokotezo wa kunyanyua mikono miwili uko lakini wakati mwingine imesuniwa kunyanyua mikono miwili katika kila kinyanyuko na kiinamo kutokana na Hadiyth ya Maalik bin Al-Huwayrath kwamba alimwona Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akinyanyua mikono yake katika Swalaah yake anaporukuu, anaponyanyua kichwa chake toka kwenye rukuu, anaposujudu na anaponyanyua kichwa chake toka kwenye sujudi mpaka mikono inakuwa usambamba wa ndwele za masikio yake.”[Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (2/206) na Ahmad (493). Ni Hadiyth Swahiyh].
· Mahala Pa Kunyanyua Mikono Na Namna Yake
Imethibiti toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba alikuwa wakati mwingine ananyanyua mikono yake pamoja na takbiyr, wakati mwingine baada yake, na wakati mwingine kabla yake. Imesuniwa ainyanyue mikono miwili vidole vikiwa vimenyooshwa, na aiweke mikono yake mkabala wa mabega yake kama ilivyo katika Hadiyth ya Abuu Qataadah [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy na wengineo]., au aiweke mkabala wa masikio yake mawili kama ilivyo katika Hadiyth ya Waail bin Hajar iliyotangulia.
3- Kuweka mkono wa kulia juu ya wa kushoto juu ya kifua
Imepokelewa toka kwa Shal bin Sa’ad akisema: “Watu walikuwa wakiamuriwa kwamba mwanamume aweke mkono wake wa kulia juu ya mkono wake wa kushoto katika Swalaah yake. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (740) na Maalik katika Al-Muwattwai (376)].
Imepokelewa toka kwa Waail bin Hajar akisema: “Niliswali pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), akaweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wake wa kushoto juu ya kifua chake”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Khuzaymah (479). Al-Albaaniy kasema ni Hadiyh Swahiyh katika Al-Irwaa (352)].
4- Kuangalia mahali pa kusujudia
Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipoingia Al-Ka’abah macho yake hayakuacha kuangalia mahala anaposujudia mpaka alipotoka humo”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Haakim (1/479) na Al-Albaaniy kasema kuwa ni Hadiyth Swahiyh].
5- Kunyooka mgongo sawasawa katika rukuu bila kukinyanyua kichwa au kukiinamisha, kuyakamata magoti mawili kwa viganja na kuvitawanya vidole vyake, na kuviweka mbali viungabega na mbavu.
Ni kwa Hadiyth ya Abuu Humayda katika sifa ya Swalaah ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliposema: “Anaporukuu, huyakamata vizuri magoti yake, kisha huupindisha mgongo wake ukanyooka sawasawa bila kibyongo”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (828) na Abuu Daawuud (717)].
Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaporukuu, hakinyanyui kichwa chake (kikawa juu kuliko mgongo) wala hakiteremshi, lakini inakuwa kati na kati”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (498) na Abuu Daawuud (768)].
Na katika Hadiyth ya Abuu Humayd: “Kisha alirukuu, akaweka mikono yake juu ya magoti yake kana kwamba ameyakamata, na akaipindisha mikono yake ikawa mbali na mbavu zake”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (720) na At-Tirmidhiy (259), nayo ni Swahiyh].
Imepokelewa na Waail bin Hajar akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anavitandaza vidole vyake anaporukuu”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Khuzaymah (594) na Al-Albaaniy kasema ni Hadiyth Swahiyh].
6- Kutanguliza mikono miwili kabla ya magoti wakati wa kwenda kusujudu
Ni kwa Hadiyth ya Abuu Hurayrah aliposema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( إذا سجد أحدكم فلا يبرك كما يبرك البعير، وليضع يديه قبل ركبتيه))
(( Anaposujudu mmoja wenu asipige magoti kama anavyopiga magoti ngamia bali atangulize mikono yake kabla ya magoti yake)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud, An-Nasaaiy na Ahmad kwa Sanad Swahiyh].
7- Kuambatisha paji la uso, pua na mikono miwili ardhini, kuiweka mikono miwili kando isigusane na mbavu, kuweka viganja viwili mkabala wa mabega mawili au masikio mawili, kunyanyua vifundo vya mikono miwili, kuikita miguu miwili barabara na kuvilingamanisha vifundo vyake, na kuvielekeza Qiblah vidole vya viganja na miguu.
Katika Hadiyth ya Abuu Humayda ameeleza: “Anaposujudu, huweka mikono yake miwili bila kutandaza vidole wala kuvibana, na huvielekeza Qiblah viungo vya mikono yake na miguu yake”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy na Abuu Daawuud].
Na imepokelewa toka kwa ‘Abdullaah bin Buhaynah akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaposwali, hutanua kati ya mikono yake mpaka ukaonekana weupe wa kwapa zake”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (807), Muslim (495) na wengineo].
Na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:
((Unaposujudu, viweke viganja vyako na unyanyue vifundo vya mikono yako)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (494)].
Na katika Hadiyth ya Abuu Humayda anasema: “Alikuwa anaposujudu, huambatisha pua yake na kipaji chake ardhini, huiweka mikono yake mbali na mbavu zake, na huweka viganja vyake mkabala wa mabega yake”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Khuzaymah na At-Tirmidhiy].
Na katika Hadiyth ya ‘Aaishah anasema: “Nikamkuta amesujudu akiwa amevilingamanisha vifundo vya miguu yake na kuvielekeza vidole vyake Qiblah”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Khuzaymah (654) na Al-Bayhaqiy (2/116). Al-Albaaniy kasema ni Hadiyth Swahiyh].
· Faida
Baadhi ya Maulamaa wanaona kwamba mwanamke hutofautiana na mwanamume katika vipengee vya kurukuu na kusujudu. Wanasema kwamba mwanamke hukusanya viungo vyake kwa pamoja badala ya kuviweka mbalimbali na huyashikanisha mapaja yake na sehemu nyinginezo, kwani hilo ndio sitara zaidi kwake. [Angalia Sunan Al-Bayhaqiy (2/222), Al-Mughniy (1/562) na Subulus Salaam (1/308). Ibn Hazm katika Al-Muhallaa (4/124) ameijibu hoja hii bila kupambanua kati ya mwanamke na mwanamume katika vipengee vya Swalaah]
Hakuna dalili yoyote yenye Sanad Swahiyh iliyokuja toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inayoelezea utofauti wowote wa vitendo vya mwanamume na mwanamke katika Swalaah. Aidha, hakuna chochote swahiyh thabiti kilichopatikana toka kwa Maswahaba wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) chenye kuthibitisha hilo.
Hivyo basi, mwenye kushikamana na uasili, akavifanya sawa vipengee vyote vya Swalaah kati ya mwanamke na mwanamume kutokana na ujumuishi wa kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Swalini kama mnavyoniona nikiswali)), basi rai yake huyo ndiyo iliyo sawa zaidi na yenye nguvu zaidi na hasahasa ikiwa mwanamke anaswali peke yake. Ama yule anayeona kinyume na hivyo na kwamba mwanamke anaamuriwa ajisitiri kiasi inavyowezekana, basi huyo ana mwelekeo wake. Mwelekeo huu wanao idadi kubwa ya Watangu wema. Allaahu Ndiye Mjuzi Zaidi. [Jaami’u Ahkaamin Nisaa cha Sheikh wetu (1/378) kwa mabadilisho madogo]
8- Kuulaza mguu wa kushoto na kuusimika wa kulia katika kikao cha kati ya sijdah mbili
Imepokelewa na ‘Aaishah akisema: “Alikuwa akiulaza mguu wake wa kushoto na kuusimika mguu wake wa kulia”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (498) na Abuu Daawuud (768)].
Inajuzu wakati mwingine aisimike miguu yake miwili na avikalie visigino vyake kati ya sijdah mbili. Kikao hiki huitwa “Al-Iq’aau”. Hii ni kwa Hadiyth ya Twaawus aliyesema: “Tulimuuliza Ibn ‘Abbaas kuhusiana na kuisimika miguu na kuvikalia visigino viwili, akasema kuwa hiyo ni Sunnah. Tukamwambia: “Tunaona kuwa hilo ni ukavu kwa mwanamume”. Ibn ‘Abbaas akasema: “Bali hiyo ni Sunnah ya Nabii wako (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)”.
Imepokelewa na Abu Zubeyr akisema kwamba alimwona ‘Abdullah bin ‘Umar wakati ananyanyua kichwa chake toka katika sijdah ya kwanza, akikaa juu ya ncha za vidole vyake, kisha akasema: “Hii ni katika Sunnah”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (536), Abuu Daawuud (830) na At-Tirmidhiy (282)].
9- Kukirefusha kikao kati ya sijdah mbili
Hii ilikuwa ni maongozi ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Imepokelewa toka kwa Anas akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikaa kati ya sijdah mbili mpaka tunadhania pengine amepitikiwa”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (473)].
Sunnah hii watu wengi wameiacha baada ya kumalizika enzi ya Maswahaba. Na kwa ajili hiyo, Thaabit amesema: “Anas alikuwa akifanya jambo ambalo siwaoni mkilifanya; anakaa kati ya sijdah mbili mpaka tunasema: Pengine amesahau au amepitikiwa”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (536)].
10- Kikao baada ya sijdah kabla ya kusimama kwenda rakaa ya pili au ya nne
Imesuniwa baada ya kumaliza sijdah ya pili katika rakaa za kwanza na tatu, kukaa kikao chepesi kabla ya kusimama kwenda rakaa ya pili na ya nne. Ni kwa Hadiyth ya Maalik bin Al-Huwayrith kwamba alimwona Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiswali, anapokuwa katika rakaa ya Witr ya Swalaah yake, hanyanyuki mpaka alingamane akiwa amekaa”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (823) Muslim (829)].
11- Kuegemeza mikono chini wakati wa kunyanyuka kwenda rakaa nyingine
Ni kwa neno la Maalik bin Al-Huwayrith: “Je, nikuzungumzieni kuhusu sifa ya Swalaah ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)? Ni kuwa anaponyanyua kichwa chake toka sijdah ya pili, hukaa akaegemeza mikono yake chini, kisha husimama”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (824)].
12- Kukaa kikao cha “iftiraash” katika tashah-hud ya kwanza, na kikao cha “tawar-ruk” katika tashah-hud ya mwisho.
“Iftiraash” ni kuusimamisha mguu wa kulia na kuulaza wa kushoto na kuukalia. Ama “tawar-ruki” ni kuunyanyua mguu wa kulia na kuutanguliza wa kushoto na kulilaza tako lake chini.
Katika Hadiyth ya Abuu Humayda: “Anapokaa katika rakaa mbili, hukalia mguu wake wa kushoto na kuunyoosha wa kulia, na anapokaa katika rakaa ya mwisho, huutanguliza mguu wake wa kushoto akausimamisha mwingine, kisha hukalia juu ya tako lake”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1/201), Abuu Daawuud (194) na At-Tirmidhiy (2/105)].
· Faida
Ikiwa Swalaah ni ya rakaa mbili tu kwa maana kuwa ina tashah-hudi moja tu, basi imesuniwa kukaa kikao cha iftiraash. Ni kwa Hadiyth ya ‘Aaishah katika sifa ya Swalaah ya Rasuli isemayo: “Alikuwa akisema katika kila rakaa mbili “at-tahiyyaat”, na alikuwa akiulaza mguu wake wa kushoto na kuunyanyua mguu wake wa kulia..”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (1/357)].
13- Kuashiria kwa kidole cha shahada katika tashah-hudi toka mwanzoni hadi mwishoni mwa du’aa na kutuliza jicho kwenye kidole
Ni kwa Hadiyth ya Ibn ‘Umar isemayo: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapokaa katika Swalaah, huweka mikono yake miwili juu ya magoti yake, hukinyanyua kidole chake cha kulia kinachofuatia dole gumba [na huyakita macho yake juu yake], na huuweka mkono wake wa kushoto juu ya goti lake la kushoto akivitandaza vidole vyake”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (580)]
· Faida
Haijuzu kuashiria kwa kidole kingine kisicho cha shahada cha mkono wa kulia. Imepokelewa toka kwa Sa’ad bin Abiy Waqqaas akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alinipitia nami nanyoosha vidole vyangu viwili. Akaniambia: “Kimoja, kimoja basi”, akaashiria kidole cha shahada”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (2/80) na An-Nasaaiy (3/83)].
Na kama kidole cha shahada cha mkono wa kulia kimekatwa, basi kwa kauli yenye nguvu ni kuwa uashirio hupomoka, na hairuhusiki kuashiria kwa kidole kingine. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
019-Mambo Yaliyoruhusiwa Ndani Ya Swalaah
Alhidaaya.com [3]
Vitendo Vilivyoruhusiwa
1- Kumbeba mtoto
Imepokelewa na Abuu Qataadah akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaswali huku amembeba Umaamah binti Zaynab binti wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Anaposujudu, humweka chini, anaponyanyuka humbeba”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (516), Muslim (543) na wengineo].
2- Kutembea hatua chache kwa dharura
Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaswali nyumbani na mlango kaufunga kwa ndani. Nilipokuja niligonga, naye akatembea akaja kuufungua, kisha akarejea na kuendelea na Swalaah yake, na mlango ulikuwa mwelekeo wa Qiblah”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (598), Abuu Daawuud (910) na An-Nasaaiy (3/11). Al-Albaaniy kaipa daraja ya Hasan].
3- Kutaharaki kwa ajili ya kumwokoa mtoto au kumzuia mtu asiporomoke shimoni au asipatwe na adha
Imepokelewa toka kwa Al-Azraq bin Qays akisema: “Tulikuwa Al-Ahwaaz tukipigana na Makhawaarij. Nilipokuwa ukingoni mwa mto, mara nikamwona mtu anaswali [Ni Abuu Barzah Al-Aslamiy] akiwa ameshikilia ugwe mkononi. Mnyama wake akaanza kufanya matata naye akaanza kumfuata. Na mimi nimepigana pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) vita kati ya sita, au saba, au nane na nikashuhudia namna alivyokuwa akifanya wepesi. “ [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1211)].
Al-Haafidh katika Al-Fat-h (3/82) anasema: “Konteksi ya kisa hiki inaonyesha kwamba Abuu Barzah hakuikata Swalaah yake, nayo inatiliwa nguvu na riwaya ya ‘Amri bin Marzouk isemayo: “Akamkamata kisha akarejea kinyume nyume. Ikiwa aliikata Swalaah yake, asingelijali kurudi kukipa mgongo Qiblah. Na katika kurejea kwake kinyume nyume kunaonyesha kwamba kwenda katika makusudio yake hakukuwa kwa hatua nyingi”.
·
Faida
Inaingia katika hili kwamba inajuzu kwako ikiwa unaswali na simu ikalia kwa mfano, uifungue ili mpigaji ajue kwamba uko kwenye Swalaah.
4- Kumzuia mtu asipite mbele yake katika Swalaah yake
Tumeielezea Hadiyth ya Abuu Sa’iyd kuhusiana na amri ya kupambana na anayepita mbele ya mwenye kuswali.
5- Kuua nyoka, nge au chochote chenye madhara
Imepokelewa na Abuu Hurayrah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliamuru kuwaua nge na nyoka wakati wa Swalaah. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (921), An-Nasaaiy (1202), At-Tirmidhiy (390) na Ibn Maajah (1245) na tamshi ni lake, nayo ni Hadiyth Swahiyh].
6- Kumbonyeza aliyelala kwa haja
‘Aaishah anasema: “Nilikuwa nikiinyoosha miguu yangu katika Qiblah cha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakati anaswali. Anaposujudu hunibonyeza (nikaikunja), na anaposimama nainyoosha”.
7- Kuvua viatu na mfano wake kwa haja
Imepokelewa toka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy akisema: “Wakati Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa anaswali na Maswahaba zake, alivivua viatu vyake akaviweka kushotoni mwake. Maswahaba walipoona hivyo, nao pia walivivua viatu vyao.” [“Takhriyj” yake ishaelezewa].
8- Kutema mate nguoni au kwenye leso
Imepokelewa toka kwa Jaabir toka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
(( إن أحدكم إذا قام يصلي فإن الله تبارك وتعالى قبل وجهه، فلا يبصقن قبل وجهه ولا عن يمينه، وليبصق عن يساره تحت رجله اليسرى فإن عجلت به بادرة فليقل بثوبه هكذا))
((Hakika mmoja wenu anaposimama kuswali, basi Allaah (Tabaaraka wa Ta’alaa Huukabili) uso wake. Basi atahadhari asije kutema mate mbele yake au kuliani kwake, bali ateme kushotoni mwake chini ya mguu wake wa kushoto. Na ikiwa mate yatamzidi nguvu, basi afanye hivi kwa nguo yake)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (3008) na Abuu Daawuud (477)]. Kisha akaikunjia kunjia nguo yake.
9- Kuiweka sawa nguo au kujikuna
Imepokelewa na Jariyj Adh-Dhwaby akisema: “Aliyyi alikuwa anaposimama kuswali, huweka mkono wake wa kulia juu ya kifundo cha mkono wake wa kushoto. Huendelea kufanya hivyo mpaka anaporukuu isipokuwa kama ataiweka sawa nguo yake au kujikuna”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abuu Shaybah (1/391) na Al-Bukhaariy (2/58) akiielezea kwa tamko la mkato].
Ibn ‘Abbaas anasema: “Mtu anaweza kukitumia kiungo chake chochote cha mwili atakavyo katika Swalaah yake”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (2/58) akiielezea kwa tamko la mkato].
10- Kusema “Subhaanal Laah” kwa wanaume na kupiga kikofi kwa mwanamke ikiwa patatokea jambo
Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
(( من نابه شيء في صلاته فليسبح، فإنه إذا سبح التفت إليه، وإنما التصفيح للنساء))
((Anayetokewa na jambo katika Swalaah yake, basi aseme “Subhaanal Laah”, kwani anaposema hivyo hutanabaikiwa, lakini wanawake hupiga kikofi)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1201) na Muslim (421) na tamko ni lake. Maneno التصفيح na التصفيق yana maana moja, nayo ni kupiga tumbo la kiganja kwa tumbo la kiganja kingine].
·
Faida
“Nimejua kwamba mwanamke kisharia hasemi Subhaanal Laahi anapotokewa na jambo katika Swalaah, lakini ikiwa jambo lililomtokea ni la dharura, inajuzu aseme Subhaanal Laah kama hakuna wanaume. Imepokelewa na Asmaa binti Abiy Bakr akisema: “ Nilimwendea ‘Aaishah wakati jua lilipokuwa limepatwa, nikawakuta watu wamesimama wakiswali, naye pia amesimama anaswali. Nikauliza: “Watu wana nini?” Akaashiria kwa mkono wake mbinguni akisema: Subhaanal Laah”. Imepasishwa na Maimamu wawili.
11- Kugeuka kulia au kushoto kwa ajili ya haja
Imepokelewa na Jaabir akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitujulisha kuwa hajisikii vizuri, tukaswali nyuma yake akiwa yeye amekaa huku Abuu Bakri akitusikilizisha takbiyr yake. Akatugeukia akatuona tumesimama. Akatuashiria tukae, nasi tukakaa, tukaswali pamoja naye huku tumekaa”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (413), An-Nasaaiy (3/9) na Abuu Daawuud (588)].
Na katika Hadiyth ya Sahl bin Sa’ad: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuja watu wakiwa katika Swalaah, akapenya mpaka akasimama katika safu, watu wakapiga vikofi. Abuu Bakri alikuwa hageuki katika Swalaah, na watu walipozidi kupiga vikofi, aligeuka akamwona Rasuli wa Allaah..” [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (684), Muslim (421) na wengineo].
12- Kuashiria kwa kichwa au mkono kwa ajili ya haja
Jaabir anasema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alinituma huku yeye akielekea kwenda kwa Bani Al-Mustwalaq. Nikamjia na yeye anaswali juu ya ngamia wake. Nikamsemesha na yeye akaashiria kwa mkono wake hivi. Kisha nikamsemesha akaashiria kwa mkono wake hivi huku mimi namsikia akisoma na kuashiria kwa kichwa chake. Alipomaliza aliniuliza: “Umefanya nini kwa jambo nililokutuma? Sikuweza kukujibu kwa kuwa nilikuwa ninaswali”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (540) na Abuu Daawuud (926)].
Na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimjibu kwa ishara kijakazi ambaye Ummu Salamah alikuwa amemtuma kwake ili amuulize kuhusu rakaa mbili alizoziona akiziswali. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (4370) na Muslim (834)].
13- Kujibu salamu kwa ishara kwa aliyekusalimia
Mtu akikusalimia ukiwa unaswali, inajulikana kuwa haijuzu kumjibu kwa maneno, lakini inajuzu kumjibu kwa ishara ya mkono. Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka kuelekea Qubaa ili akaswali huko. Ma-Answaar wakamjia, wakamsalimia na yeye yuko ndani ya Swalaah. Nikamwambia Bilaal: Ulimwonaje Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwajibu wakati walipokuwa wakimsalimia? Akasema: Hivi; akakunjua kiganja chake [Akaelekeza tumbo lake chini na mgongo wake juu]”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (915) kwa Sanad Swahiyh].
14- Kunyanyua kichwa katika sujudi ili kujua mambo yakoje ikiwa imamu atarefusha sijda
Ukiwa ndani ya sijdah katika Swalaah ya jamaa, imamu akarefusha sijdah, au ukawa hujaisikia takbiyr, au mfano wa hilo, inajuzu unyanyue kichwa ili kupeleleza jambo. Imepokelewa toka kwa ‘Abdullaah bin Shaddaad toka kwa baba yake akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitutokea katika moja ya Swalaah mbili za ‘Ishaa akiwa amembeba ima Al-Hasan au Al-Husayn. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatangulia akamweka, kisha akapiga takbiyr ya Swalaah. Na katikati ya Swalaah alisujudu na sijdah ikawa ndefu. Nikanyanyua kichwa, mara nikamwona mtoto yuko juu ya mgongo wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) naye yuko ndani ya sijdah, nami nikarudi tena kwenye sijdah yangu. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomaliza Swalaah yake watu walisema: “Ee Rasuli wa Allaah! Umesujudu sijdah ndefu ndani ya Swalaah yako mpaka tukadhani kwamba kuna jambo limetokea, au pengine unateremshiwa wahyi”. Akasema: ((Hayo yote hayajatokea, lakini mwanangu alinipanda mgongoni, nikachukia kumharakisha mpaka ashuke)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (2/230 kwa Sanad Hasan].
15- Kuangalia kwenye Msahafu na kusoma kutoka humo katika Swalaah ya Sunnah kwa haja
Hakuna ubaya kusoma kutoka kwenye Msahafu katika Swalaah ya usiku kwa mfano ikiwa mtu anataka kurefusha kisomo na yeye hakuhifadhi Qur-aan. Imepokelewa toka kwa Al-Qaasim akisema kwamba ‘Aaishah alikuwa akisoma kwenye Msahafu katika Swalaah zake mwezi wa Ramadhwaan. [Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdur Raaziq (2/240) na Ibn Abuu Daawuud katika Al-Maswaahif (192)].
Al-Qaasim amesema: “Mtumwa alikuwa akimswalisha ‘Aaishah kwa kusoma toka kwenye Msahafu”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy ikiwa Mu’allaq katika Kitabu cha Adhana mlango wa “Mtumwa kuwa imamu”. Ibn Abuu Shaybah amesema ni Mawsuul (2/338) na Ibn Abuu Daawuud katika Al-Maswaahif ukurasa wa 192]
Haijuzu kufanya hivi katika Swalaah ya faradhi, au katika Swalaah ya Sunnah kama haihitajiki.
(A)
Maneno Yenye Kuruhusiwa Na Mfano Wake
1- Kumtatua imamu
Ikiwa imamu atatazikiwa katika kisomo, inajuzu kwa aliye nyuma yake kumtatua, kwa kuwa ikiwa hatamtatua, matokeo yake yatakuwa ni kubadili Maneno ya Allaah. Imepokelewa toka kwa ‘Abdullah bin ‘Umar kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali Swalaah fulani, akasoma, akatatizikiwa. Alipomaliza alimuuliza Ubayya: “Je, umeswali nasi?” Akajibu: “Ndio”. Akamuuliza: “Basi kipi kimekuzuia?” [Imefanyiwa “ikhraaj”na Abuu Daawuud (894) na Ibn Hibaan (1/316-Ihsaan) kwa Sanad Swahiyh].
·
Faida
1- Inatakikana imamu asitatuliwe kwanza madhali atakuwa akikariri kariri Aayah ili kujikumbusha. Kumsubiria itakuwa ni bora zaidi.
2- Imamu hatatuliwi kama atanyamaza bila kubabaika katika kisomo chake isipokuwa tu kama mnyamao wake utakuwa mrefu. Kunyamaa kwa imamu kunawezekana kuwa anayataamuli anayoyasoma.
3- Imamu akikosea kosa lisilo haribu maana katika kisomo chake, basi hatatuliwi.
Imepokelewa toka kwa Ubayya bin Ka’ab kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( Mimi nimesomeshwa Qur-aan…kwa visomo (lugha) saba, hakuna humo isipokuwa yaliyo wazi yenye kutosheleza. Ukisema: Ghafuuran Rahiyman, au ukasema: ‘Aliyman Hakiyman, basi Allaah ni hivyo madhali hukubadili aayah ya adhabu kwa rehma, au aayah ya rehma kwa adhabu)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (20646) kwa Sanad Swahiyh].
2- Kuirudia rudia Aayah moja katika Swalaah ya Sunnah
Imepokelewa toka kwa Abuu Dharri kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliisoma Aayah hii akairudia rudia mpaka asubuhi:
((إِن تُعَذِّبْهُمْ فَإِنَّهُمْ عِبَادُكَ ۖ وَإِن تَغْفِرْ لَهُمْ فَإِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ))
((“Ukiwaadhibu, basi bila shaka hao ni waja Wako; na Ukiwaghufuria basi hakika Wewe Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.”)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (1010), Ahmad (20831) na Al-Haakim. Katika Sanad yake kuna ulaini].
Na Masrowq anasema: “Tamiym Ad-Daariyy aliirudia rudia Aayah hii:
((أَمْ حَسِبَ الَّذِينَ اجْتَرَحُوا السَّيِّئَاتِ أَن نَّجْعَلَهُمْ كَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَوَاءً مَّحْيَاهُمْ وَمَمَاتُهُمْ ۚ سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ))
((Je, wanadhania wale waliochuma maovu kwamba Tutawafanya sawa na wale walioamini na wakatenda mema, sawasawa uhai wao na kufa kwao? Uovu ulioje wanayouhukumu))
[Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abuu Shaybah katika Al-Muswannaf (2/477)].
Imepokelewa toka kwa Sa’iyd bin ‘Ubayd akisema: “Nilimwona Sa’iyd bin Jubayr akiwaswalisha watu mwezi wa Ramadhwaan huku akiikariri Aayah hii:
((أَوَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ كَانُوا مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَانُوا هُمْ أَشَدَّ مِنْهُمْ قُوَّةً وَآثَارًا فِي الْأَرْضِ فَأَخَذَهُمُ اللَّـهُ بِذُنُوبِهِمْ وَمَا كَانَ لَهُم مِّنَ اللَّـهِ مِن وَاقٍ))
Pamoja na:
((يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ الْكَرِيمِ • الَّذِي خَلَقَكَ فَسَوَّاكَ فَعَدَلَكَ))
Akiikariri mara mbili au tatu. [Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdul Razzaaq katika Al-Muswannaf (2/492)].
Ninasema: “Hili halikunukuliwa kwa upande wa Swalaah ya faradhi, hivyo kuliacha ni bora zaidi. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
3- Kulia na kutoa mlio wa hisia ya uchungu, huzuni na kadhalika
Kulia katika Swalaah ikiwa ni kwa kumkhofu Allaah, kukumbuka Pepo au Moto na mfano wake, kunakuwa ni jambo zuri analolipwa mtu thawabu. Jambo hili halibatwilishi Swalaah kama wanavyodhani baadhi ya watu. Aidha, ikiwa kulia ni kwa ajili ya maumivu, au msiba nawe ukashindwa kujizuia, basi hakuna ubaya.
Zifuatazo ni baadhi ya dalili zinazothibitisha hili:
1- Allaah Mtukufu Amewasifu wenye kulia Aliposema:
((أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ مِن ذُرِّيَّةِ آدَمَ وَمِمَّنْ حَمَلْنَا مَعَ نُوحٍ وَمِن ذُرِّيَّةِ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْرَائِيلَ وَمِمَّنْ هَدَيْنَا وَاجْتَبَيْنَا ۚ إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُ الرَّحْمَـٰنِ خَرُّوا سُجَّدًا وَبُكِيًّا))
(( Hao ndio ambao Allaah Amewaneemesha miongoni mwa Manabii katika kizazi cha Aadam, na miongoni mwa Tuliowabeba pamoja na Nuwh (katika jahazi), na katika kizazi cha Ibraahiym na Israaiyl na miongoni mwa Tuliowaongoa na Tukawateua. Wanaposomewa Aayaat za Ar-Rahmaan huporomoka kifudifudi wakisujudu na kulia)).
Na Neno Lake Ta’alaa:
(( وَيَخِرُّونَ لِلْأَذْقَانِ يَبْكُونَ وَيَزِيدُهُمْ خُشُوعًا ))
(( Na wanaporomoka kifudifudi huku wanalia na inawazidishia unyenyekevu )).
Aayah hizi mbili zinamjumuisha aliye ndani ya Swalaah na aliye nje ya Swalaah.
2- Imepokelewa toka kwa ‘Abdullaah bin Ash-Shukhayr akisema: ”Nilimjia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa anaswali, na kifuani mwake kuna mvumo kama mvumo wa maji yachemkayo chomboni”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (1214), Abuu Daawuud (1/328) na Ahmad (4/25), na Sanad yake ni Swahiyh].
3- Imepokelewa toka kwa ‘Aliyyi akisema: “Hakuna aliyekuwa amepanda farasi Siku ya Badr isipokuwa Al-Miqdaad. Ungelituona, ungekuta sote tumelala isipokuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) chini ya mti akiswali na akilia mpaka pakapambauka”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (1026) na Ibn Khuzaymah (2/53), na Sanad yake ni Swahiyh].
4- Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar akisema: “Rasuli wa Allaah alipozidiwa na maumivu, aliulizwa nani aswalishe. Akasema: ((Mwamuruni Abu Bakri awaswalishe watu)). ‘Aaishah akamwambia: “ Abu Bakri ana moyo laini, anaposoma hawezi kujizuia kulia. Akasema: ((Mwamuruni aswalishe)). Akamkariria tena na Rasuli akasema:(( Mwamuruni aswalishe, hakika nyinyi ni (kama) wanawake wa Yusuf)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (682)].
5- ‘Abdullaah bin Shaddaad amesema: “Nilisikia mtetemo wa ‘Umar nami niko safu ya mwisho akisoma:
(( قَالَ إِنَّمَا أَشْكُو بَثِّي وَحُزْنِي إِلَى اللَّـهِ وَأَعْلَمُ مِنَ اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ))
((Akasema: “Hakika mimi nashitakia dhiki ya majonzi yangu na huzuni zangu kwa Allaah. Na najua kutoka kwa Allaah yale msiyoyajua.”)) [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy katika mlango wa adhana. Angalia Fat-hul Baariy (2/206). Ibn Taymiyah katika Al-Fataawaa (22/623) ameeleza kwamba athar hii imehifadhiwa toka kwa ‘Umar].
·
Faida
Sauti ya kuugulika kama “aah” au ya maumivu kama “ooh”, hazibatwilishi Swalaah, lakini ni karaha kuzifanya bila haja.
3- Kupuliza kwa haja fulani
Imepokelewa toka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar akisema: “Jua lilipatwa wakati wa enzi ya Rasuli wa Allaah. Katika sijdah yake ya mwisho alipuliza: “Uf uf”, kisha akasema: ((Mola wangu! Je, Hukuniahidi kwamba Hutowaadhibu mimi nikiwa pamoja nao? Je, Hukuniahidi kwamba Hutowaadhibu nailhali wanaomba maghfirah?)) [Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (1194), An-Nasaaiy (3/137) na Ahmad (2/159), na wapokezi wake ni watu wa kuaminika. Al-Bukhaariy (2/62) ameileta kwa tamko la kutothibiti usahihi wake kutokana na hitilafu katika riwaya ya ‘Atwaa bin As-Saaib ambaye alikuwa amekoroga. Lakini Hammaad bin Salamah alikuwa ameisikia kutoka kwa ‘Atwaa kabla ya kukoroga katika kauli ya Ibn Ma’iyn na Abuu Daawuud]
Imepokelewa na Ayman bin Naayil akisema: “Nilimwambia Qudaamah bin ‘Abdullaah bin ‘Ammaar Al-Kullaabiy ambaye alikuwa swahibu wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa ninakerwa na manyoya ya njiwa kwenye Al-Masjidul Haraam tunaposujudu akasema: “Pulizeni”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bayhaqiy (2/253), na Al-Haafidh katika Al-Fat-h kaipasisha kuwa Hadiyth Swahiyh (3/85)].
4- Kujikohoza kwa ajili ya haja
Hakuna ubaya kufanya katika Swalaah. Hii ni kwa vile Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kuzungumza ndani ya Swalaah aliposema: ((Haifai ndani yake maneno ya watu)), na kujikohoza au kutoa mgumio wa ishara haviitwi kuwa ni maneno, kwani vyenyewe pamoja na matamshi mengine havileti maana ya kufahamika, na wala mtendaji wake haambiwi kazungumza, bali makusudio yake yanafahamika kutokana na dalili, hivyo ni kama ishara tu. [Majmu’u Al-Fataawaa cha Ibn Taymiyah (22/617)]
5- Maneno machache kwa ajili ya maslaha ya Swalaah
Maneno kwa ajili ya maslaha ya Swalaah hayaibatilishi ikiwa yatasemwa na imamu au maamuma lakini yasiwe mengi bali ya ufahamisho tu.
Linalothibitisha haya ni Hadiyth mashuhuri ya Dhul Yadayn kuhusiana na kisa cha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwaswalisha watu Alasiri akisema: “Akatoa tasliym baada ya rakaa mbili. Akasimama Dhul Yadayn akauliza: Je, umepunguza Swalaah ee Rasuli wa Allaah au umesahau?” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Hakuna lolote katika hayo mawili)). Akasema: “Ilikuwa ni sehemu ya hayo ee Rasuli wa Allaah”. Rasuli wa Allaah akawaelekea watu akawauliza: “Je, Dhul Yadayn anasema kweli?” Wakajibu: “Ndio ee Rasuli wa Allaah”. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akakamilisha rakaa mbili zilizobakia, kisha akasujudu sijdah mbili akiwa amekaa baada ya kutoa tasliym. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (714), Muslim (573) na wengineo].
Mwelekeo wa kutoa dalili hii ni kuwa imamu na maamuma wamezungumza kwa ajili ya maslaha ya Swalaah kabla hawajaimaliza. Hivyo imekuwa ni katika hukumu ya Swalaah.
6- Kusema “Al-Hamdu” kwa anayepiga chafya
Inajuzu kwa anayepiga chafya kwenye Swalaah amhimidi Allaah kwa yeye mwenyewe lakini aliye pembeni mwake hamjibishi kwa “Yarhamukal Laahu”. Hii ni kutokana na Hadiyth ya Rifa’ah bin Maalik aliyesema: “Niliswali nyuma ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) nikapiga chafya na kusema: “Alhamdu Lillaahi hamdan kathiyran twayyiban mubaarakan ‘alayhi kamaa Yuhibbu Rabbunaa wa Yardhwaa”. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomaliza Swalaah aliuliza: ((Nani aliyezungumza ndani ya Swalaah?)). Rifa’ah akajibu: “Ni mimi ee Rasuli wa Allaah”. Rasuli akasema: ((Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu iko Mkononi Mwake, hakika Malaika thelathini na ushee walishindana nani kati yao apande nalo)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (404) na An-Nasaaiy (2/245). Al-Bukhaariy pia kaifanyia “ikhraaj” lakini hakumtaja Al-‘At Twaas].
Ash-Shawkaaniy anasema: “Inaonyesha tena ruhusa ya kumhimidi Allaah ndani ya Swalaah kwa aliyepiga chafya. Na hili linatiliwa nguvu na ujumuishi wa Hadiyth zinazogusia uhalali wake, kwani hazikupambanua kati ya Swalaah na kwingineko”.
Ninasema: “Linalotilia nguvu hili vile vile ni yale yaliyokuja katika Hadiyth ya Mu’aawiyah bin Al-Hakam aliyesema: “Nilipokuwa naswali pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), mtu mmoja alipiga chafya akasema: “Al-Hamdu lil Laah”, nami nikamwambia: “Yarhamukal Laahu”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (537) na Abuu Daawuud (930)].
Tunafahamu hapa kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kumwambia aliyepiga chafya “Yarhamukal Laahu”, lakini hakumkataza mpigaji kusema “Al-Hamdu lil Laah”, hivyo basi, inaonyesha kujuzu kwake. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
7- Kumhimidi Allaah kwa jambo la furaha
Hadiyth ya Sahl bin Sa’ad kuhusiana na kisa cha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwenda kwa Bani ‘Amri bin ‘Awf ili kusuluhisha kati yao inasema kwamba Abuu Bakri aliwaswalisha. Na Rasuli alipokuja wao wakiwa bado ndani ya Swalaah, Abu Bakri alitaka kurejea nyuma. Rasuli wa Allaah akamwashiria abaki kama alivyo. Abu Bakri akanyanyua mikono yake, na akamhimidi Allaah ‘Azza wa Jalla kutokana na amri hiyo ya Rasuli wa Allaah. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (684) na Muslim (431)].
8- Kumsemesha anayeswali na kumuuliza jambo
Tumeeleza nyuma kisa cha Jaabir wakati Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomtuma kwa Bani Al-Muswtwalaq kuwa alipokuja kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimkuta ndani ya Swalaah na akamsemesha. Rasuli hakumjibu bali alimwashiria kwa mkono wake. [Muslim (540)].
Pia imeelezwa nyuma Hadiyth ya Asmaa aliyesema: “Nilimjia ‘Aaishah wakati jua lilipopatwa, kutahamaki nikawaona watu wamesimama wanaswali, naye pia kasimama anaswali. Nikamuuliza: “Watu wana nini?” Akaniashiria mbinguni kwa mkono wake”. [Al-Bukhaariy (1220) na Muslim (545)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
020-Yaliyokatazwa Ndani Ya Swalaah
Alhidaaya.com [3]
Ni mambo ambayo Hadiyth zimeyakataza au kuyafanya makruhu ndani ya Swalaah. Lakini mambo haya hayabatilishi Swalaah, bali hupunguza thawabu za mwenye kuswali. Mambo hayo ni:
1- Kukamata kiuno
Hili halijuzu kutokana na Hadiyth ya Abu Hurayrah aliposema kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kukamata kiuno ndani ya Swalaah. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1220) na Muslim (545)].
Na imepokelewa toka kwa ‘Aaishah kwamba alikuwa akichukizwa na mwenye kuswali anayeweka mkono wake kwenye kiuno chake akisema: “Mayahudi hufanya hivyo”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (3458)].
Aidha, imepokelewa toka kwa Ziyaad bin Swubayh akisema: “Niliswali pembezoni mwa Ibn ‘Umar nikaweka mikono yangu juu ya kiuno changu. Alipomaliza kuswali alisema: “ Huu ni msalaba katika Swalaah. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikataza”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (903), An-Nasaaiy (2/127) na Ahmad (2/30) kwa Sanad ambayo haina tatizo].
As-Sandiy anasema: “ Umbo la msalaba katika Swalaah ni kuweka mikono yake kwenye nyonga zake na wakati anaposimama huviweka kando viunga bega vyake.
2- Kunyanyua macho mbinguni
Hili halijuzu kutokana na kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliposema:
(( لينتهن أقوام عن رفع أبصارهم عند الدعاء في الصلاة إلى السماء أو لتخطفن أبصارهم))
(( Hakika watakoma watu kunyanyua macho yao mbinguni wakati wanapoomba du’aa katika Swalaah au macho yao yatanyakuliwa)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (429) na An-Nasaaiy (3/39)]..
3- Kuangalia kishughulishacho
Ni kwa Hadiyth ya ‘Aaishah asemaye kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali na guo lenye mistari stari akasema: ((Mistari stari ya hili imenishughulisha. Lichukueni kwa Abu Jahm, mniletee guo zito)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (752) na Muslim (556)].
4- Kugeuka bila haja
Tumeshaeleza nyuma kwamba inajuzu kugeuka ndani ya Swalaah kwa haja. Lakini kama hakuna haja ya kufanya hivyo, basi haijuzu. Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah akisema: “Nilimuuliza Rasuli wa Allaah kuhusiana na kugeuka ndani ya Swalaah akasema:
(( هو اختلاس يختلسه الشيطان من صلاة العبد))
((Huo ni mnyakuo anaounyakua shaytwaan katika Swalaah ya mja)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (752) na Muslim (556)].
5- Kushikamanisha vidole vya mikono
Ni karaha mtu kuingiza vidole vya mkono mmoja kwenye vidole vya mkono mwingine kwa Hadiyth ya Abuu Hurayrah aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( إذا توضأ أحدكم في بيته ثم أتى المسجد كان في صلاة حتى يرجع، فلا يقل هكذا، وشبك بين أصابعه))
((Anapotawadha mmoja wenu nyumbani kwake kisha akaenda Msikitini, anazingatiwa yuko ndani ya Swalaah mpaka arejee. Basi asifanye hivi. Akavishikamanisha vidole vyake)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Haakim (1/206). Ipo katika Swahiyhul Jaami’i (445) na kuna Hadiyth nyingine kama hii katika Musnadi ya Ahmad (3/42) toka kwa Abuu Sa’iyd].
Imepokelewa toka kwa Ismaa’iyl bin Umaymah akisema: “ Nilimuuliza Naafi’i kuhusu mtu anayeswali huku ameshikamanisha vidole akasema: Ibn ‘Umar amesema: Hiyo ni Swalaah ya walioghadhibikiwa”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (2/261), na Al-Albaaniy katika Al-Irwaa (2/103) kasema ni Hadiyth Swahiyh].
6- Kuminya vidole vitoe sauti
Kufanya hivi hata kama ni kudogo ni karaha, kwa kuwa humpumbaza mtu mbali na Swalaah, na kama kutakuwa ni kwingi, basi ni haramu, kwa kuwa itakuwa ni kuichezea Swalaah.
Shu’ubah mwachwa huru wa Ibn ‘Abbaas amesema: “Niliswali pembezoni mwa Ibn ‘Abbaas nikavivunja vidole vyangu. Nilipomaliza Swalaah aliniambia: “Mwanaharamu we! Unavunja vidole vyako nawe uko ndani ya Swalaah?!” [Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Shaybah (2/334), na katika Al-Irwaa (2/99) imepewa daraja ya Hasan]
7- Kujizungushia nguo na kuiacha mikono ndani ukarukuu na kusujudu ikiwa ndani
Ni kwa Hadiyth ya Abuu Hurayrah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kufanya “As-Sadl” ndani ya Swalaah. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (629) na At-Tirmidhiy (376) kwa Sanad Swahiyh].
“As-Sadl” ni kujizungushia nguo na kuiingiza mikono ndani, na wakati wa kurukuu na kusujudu inabakia humo humo.
8- Kwenda miayo
Haijuzu kuivuta sana, bali ni wajibu kuizuia kwa kuweka mkono kwenye kinywa kwa Hadiyth ya Abuu Hurayrah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( التثاؤب ]في الصلاة[ من الشيطان فإذا تثاءب أحدكم فليكظم ما استطاع))
((Kwenda miayo [ndani ya Swalaah] kunatokana na shaytwaan. Anapokwenda mmoja wenu miayo, basi ajizuie awezavyo)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (3289), Muslim (2994) na At-Tirmidhiy (368), na ziada ni yake].
Hakuna uhalali wa kusema “A’uwdhu bil Laahi” kwa kuwa hakuna dalili inayothibitisha hilo. Ni ada iliyoenea kwa watu wengi bila kuwa na dalili yoyote.
9- Kutema mate upande wa Qiblah au upande wa kulia
Ni kwa Hadiyth ya Jaabir aliyesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( إن أحدكم إذا قام يصلي فإن الله تبارك وتعالى قبل وجهه، فلا يبصقن قبل وجهه ولا عن يمينه، وليبصق عن يساره تحت رجله اليسرى فإن عجلت به بادرة فليقل بثوبه هكذا))
((Hakika mmoja wenu anaposimama kuswali, basi Allaah Tabaaraka wa Ta’alaa Huukabili uso wake. Basi atahadhari asije kutema mate mbele yake au kuliani kwake, bali ateme kushotoni mwake chini ya mguu wake wa kushoto. Na ikiwa mate yatamzidi nguvu, basi afanye hivi kwa nguo yake)). Kisha akaikunjilia nguo yake sehemu juu ya sehemu. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (3008). Ishatajwa nyuma].
10- Kufumba macho
Ikiwa mtu atafanya hivyo kwa ajili ya kujikurubisha kwa Allaah, basi ni haramu, kwani kunaingia katika mlango wa bid-’a, na kama si kwa lengo hilo, basi ni makruhu kwa kuwa anakwenda kinyume na Sunnah.
Ibn Al-Qayyim anasema: [Zaadul Ma’ad (1/294)]
“Haikuwa ni katika maongozi ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kufumba macho ndani ya Swalaah. Linaloonyesha kwamba hakuwa akifumba ni kunyoosha kwake mkono ndani ya Swalaah ya Kupatwa Jua ili akikamate kishada alipoiona Pepo. Pia kuuona Moto, mwanamke aliyeingia humo kwa kumtesa paka, pamoja na mdokozi aliyekuwa akiwaibia mahujaji kwa kutumia bakora yake. Aidha, kusukumana na mnyama aliyetaka kupita mbele yake wakati anaswali…[ametaja Hadiyth nyingi, kisha akasema:] Hadiyth hizi na nyinginezo, zote kwa pamoja zinatupa faida kwamba Rasuli hakuwa akifumba macho yake ndani ya Swalaah”.
11- Kunyoosha viungo
Ni karaha kujinyoosha isipokuwa kama ni kidogo kwa haja. Hii ni kwa vile kitendo hicho hakiendani na khushuu katika Swalaah. Ibn Abuu Shaybah (1/349) amepokea toka kwa Sa’iyd bin Jubayr akisema: “Kujinyoosha hupunguza (thawabu za) Swalaah”.
12- Kushikamanisha viganja katika rukuu
Hii ni kwa kuweka tumbo la kiganja kwenye tumbo la kiganja kingine, kisha kuviweka viganja viwili kati ya magoti mawili na mapaja mawili. Hili mwanzoni lilikuwa likiruhusiwa, kisha likakatazwa.
Imepokelewa toka kwa Musw-‘ab bin Sa’ad akisema: “Niliswali pembezoni mwa baba yangu, kisha nikaweka mikono yangu kati ya magoti yangu. Baba yangu akanambia: “Kamata magoti yako kwa viganja vyako”, nami nikafanya vile vile kama mwanzo. Akanipiga mikono yangu miwili na kuniambia: Sisi tumekatazwa hivi, na tumeamuriwa tuyakamate magoti kwa viganja”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (790) na Muslim (535), na tamko ni lake].
13- Kusoma Qur-aan wakati wa kurukuu na kusujudu
Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
(( ألا وإني نهيت أن أقرأ القرآن راكعا أو ساجدا))
((Tambueni kwamba mimi nimekatazwa kusoma Qur-aan nikiwa nimerukuu au nimesujudu)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (479) na ishaelezwa nyuma].
14- Kutandaza mikono miwili wakati wa kusujudu
Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliposema:
(( اعتدلوا في السجود، ولا يبسط أحدكم ذراعيه انبساط الكلب))
((Lingamaneni katika sijdah, na mmoja wenu asitandaze mikono yake kama anavyoitandaza mbwa)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (823), Muslim (493) na wengineo].
Haifai kutandaza mikono miwili juu ya ardhi, bali vifundo viwili hunyanyuliwa kama tulivyoeleza nyuma.
15- Kuikusanya na kuifumbata nguo wakati wa kusujudu au kunyanyua mikono ya nguo
Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Abbaas akisema: “ Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameamuriwa asujudu juu ya viungo saba, na amekatazwa asibane au kuikusanya nguo au nywele”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (809) na Muslim (490), na tamko ni lake].
16- “Al-Iq’aa”, nako ni kuambatisha matako chini, kuinyanyua miundi miwili na kuiweka mikono chini.
Mkao huu haufai katika Swalaah kwa Hadiyth ya ‘Aaishah kuhusiana na sifa ya Swalaah ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambapo anasema: “Alikuwa akikataza mkao wa shaytwaan”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (498)].
Mkao huu ndio huo tulioutaja wa “al-iqaa”.
Na katika Hadiyth ya Abuu Hurayrah anasema: “..na ametukataza tusidokoe mdokoo wa jogoo, na kukaa kikao cha mbwa”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (2/265) kwa Sanad Dhwa’iyf].
·
Faida
“Al-Iq’aa” kwa maana hii haijuzu kwa dalili zilizotangulia. Lakini ninatanabahisha hapa kwamba neno hili lina maana nyingine ambayo ni kusimamisha miguu miwili, na kuweka matako mawili juu ya visigino wakati wa kikao kati ya sijdah mbili. Kikao hiki kinaruhusika kisharia.
17- Kuweka mkono chini wakati wa kikao ila kwa udhuru
Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza mtu anapokaa katika Swalaah kutegemea mkono wake wa kushoto”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (1/260), Ahmad (2/116), Al-Haakim (1/230) na Al-Bayhaqiy (2/136)].
Na katika riwaya nyingine Ibn ‘Umar amesema: “Usikae hivi, kwani wanaoadhibiwa ndivyo wanavyokaa”.
18- Mgonjwa kusujudu juu ya kitu kilichonyanyuka
Ikiwa mgonjwa ataweza kusujudu chini, basi itakuwa ni wajibu kwake, lakini kama hawezi, ataashiria kwa kichwa. Si lazima aweke mto au mfano wake ili asujudie juu yake.
Hii ni kwa Hadiyth ya Ibn ‘Umar aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimzuru mgonjwa katika mmoja wa Maswahaba wake, nami nilikuwa naye. Akaingia kwa mgonjwa akamkuta anaswali juu ya ujiti, na mgonjwa akaweka kipaji chake juu ya ujiti. Rasuli akamwashiria, kisha akaondosha ujiti. Mgonjwa akachukua mto na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia:
((Achana nao, kama utaweza kusujudu juu ya ardhi (ni bora), na kama huwezi, basi ashiria. Inama zaidi kwenye sijdah yako kuliko unavyoinama katika rukuu)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Twabaraaniy katika Al-Kabiyr (12/270). Ina Hadiyth mwenza ya Jaabir kwa Al-Bazzaar (1/275) katika kitabu cha Kashful Astaar, na Al-Bayhaqiy (2/306). Al-Albaaniy kasema ni Hadiyth Swahiyh katika Asw-Swahiyha (323)]
19- Kupangusa vijiwe sehemu ya kusujudia na kucheza cheza
Inafaa ikiwa ni kwa haja ya dharura sana lakini mara moja tu. Kuacha itakuwa ni bora zaidi ikiwa kuwepo kwa vijiwe hivyo hakumwathiri mtu kufanya khushuu. Ni kwa Hadiyth ya Mu’ayqiyb kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia mtu mmoja aliyekuwa anauweka sawa mchanga pale anaposujudu:
((Ikiwa ni mwenye kufanya, basi ni mara moja tu)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1207) na Muslim (546)].
Na katika riwaya nyingine: ((Usipanguse ukiwa katika Swalaah, na kama itabidi ufanye, basi sawazisha vijiwe mara moja tu)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (1/249). An-Nawawy amesem kwamba Isnadi yake iko juu ya sharti ya Al-Bukhaariy na Muslim].
·
Faida
Ikiwa mchanga au vijiwe vitakamata kipaji kutokana na kusujudu juu ya ardhi, basi ni karaha kuviondosha kwa kuwa ni kitendo kinachomshughulisha mtu mbali na Swalaah yake, na hususan kama kitendo kitakariri.
Imepokelewa toka kwa Abuu Sa’iyd akisema: “Nilimwona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisujudu kwenye maji na udongo mpaka nikaona alama ya udongo katika kipaji chake”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (669) na Muslim (1167)].
Ibn Mas-’oud anasema: “Manne si katika mambo ya staha. Akataja kati yake: Mtu kupangusa vumbi la usoni wakati yuko ndani ya Swalaah”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bayhaqiy (2/285). Al-Albaaniy katika Al-Irwaa (1/97) kasema kuwa ni Hadiyth Swahiyh].
Lakini ikiwa vumbi hilo linamkera na kumsumbua mwenye kuswali, basi atalifuta na kuliondosha. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
20-Kutanguliza magoti mawili kabla ya mikono miwili chini wakati wa kwenda kusujudu
Imepokelewa na Abuu Hurayra akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( إذا سجد أحدكم فلا يبرك كما يبرك البعير وليضع يديه قبل ركبتيه))
((Anaposujudu mmoja wenu, basi asitangulize magoti kama anavyofanya ngamia, bali aweke mikono yake kabla ya magoti yake)). [Takhriyj yake imeelezwa nyuma].
21- Kuashiria kwa mikono miwili pambizo mbili wakati wa kutoa tasliym
Desturi hii ambayo imekatazwa katika Swalaah, imeenea kwa watu wengi wa kawaida wake kwa waume.
Imepokelewa toka kwa Jaabir bin Samrah akisema: “Tulikuwa tunaposwali pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), tunasema: As-Salaam ‘alaykum wa rahmatul Laahi, As-Salaam ‘alaykum wa rahmatul Laahi; akaashiria pambizo mbili kwa mkono wake. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatuambia:
(( علام تومئون بأيديكم كأذناب خيل شمس؟ إنما يكفي أحدكم أن يضع يده على فخذه ثم يسلم على أخيه، من على يمينه وشماله))
((Mnaashiria kitu gani kwa mikono yenu kama mikia ya farasi waliotibuka? Hakika inamtosha mmoja wenu kuweka mkono wake juu ya paja lake, kisha atoe tasliym kwa nduguye aliyeko kuliani na aliyeko kushotoni)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (431), An-nasaaiy (1185) na Abuu Daawuud (998)].
22- Kumtangulia imamu
Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
(( أما يخشى أحدكم إذا رفع رأسه قبل الإمام أن يجعل الله رأسه رأس الحمار، أو يجعل الله صورته صورة حمار))
((Je, haogopi mmoja wenu Allaah kukigeuza kichwa chake kichwa cha punda kama atakinyanyua kabla ya imamu, au Allaah kuifanya sura yake kuwa sura ya punda?)) [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (691), Muslim (427) na wengineo].
23- Baada ya kutengwa chakula au kubanwa na haja ndogo au kubwa
Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah akisema: “Nimemsikia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
(( لا صلاة بحضرة الطعام ولا وهو يدافعه الأخبثان))
((Hapana Swalaah chakula kikiwa tayari, wala kwa aliyebanwa na haja ndogo au haja kubwa)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (560) na Abuu Daawuud (89)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
021-Yenye Kubatwilisha Swalaah
Alhidaaya.com [3]
1- Kuwa na uhakika wa kupata hadathi yenye kubatilisha wudhuu
Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alilalamikiwa kuhusiana na mtu ambaye anaona kana kwamba kimemtoka kitu ndani ya Swalaah yake akasema:
((Asiondoke mpaka asikie sauti, au anuse harufu)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (137) na Muslim (361)].
2- Kuacha sharti kati ya masharti ya Swalaah au nguzo kati ya nguzo zake bila ya udhuru
Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa mtu aliyeswali vibaya wakati alipomwona kwamba hatulii katika Swalaah yake na kumwambia:
((Rejea uswali tena, kwani hukuswali)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (793) na Muslim (397)].
Nyuma tumekwisha zitaja shuruti na nguzo za Swalaah, unaweza kuzirejea.
3- Kula au kunywa kwa makusudi
Ibn Al-Mundhir amesema: “Maulamaa wote wamewafikiana kwamba mwenye kula au kunywa katika Swalaah ya faradhi kwa makusudi, basi lazima aswali tena”.
Jamhuri ya Maulamaa wanasema pia kuwa hata Swalaah ya Sunnah inabatilika, kwani linalobatilisha faradhi, hubatilisha vile vile Sunnah.
4- Kuzungumza makusudi kwa jambo lisilohusiana na maslaha ya Swalaah
Imepoekelewa toka kwa Zayd bin Arqam akisema: “Tulikuwa tukizungumza katika Swalaah; mmoja wetu anamzungumzisha swahibu yake pembeni ndani ya Swalaah mpaka ikateremka:
((حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ))
..na hapo tukaamuriwa kunyamaza [tukakatazwa kuzungumza]. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1200) na Muslim (539) na ziada ni yake].
·
Faida
Mwenye kuzungumza ndani ya Swalaah kwa kusahau au kutojua hukmu, Swalaah yake haibatiliki. Mu’aawiyah bin Al-Hakam amehadithia kwamba aliswali pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na mtu mmoja alipiga chafya, akamhimidi Allaah, naye akamwambia: “Yarhamukal Laahu”. Watu wakaanza kumwangalia akawaambia: “Ebo!! Mna nini!! Mbona mnanitizama hivyo?!”
Hadiyth hii inatuonyesha kwamba alizungumza lakini Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuibatilisha Swalaah yake wala hakumwamuru kuirejesha kwa kuwa alikuwa hajui hukmu, bali alimwambia:
((Hakika Swalaah hii haifai ndani yake chochote katika maneno ya watu, bali ni tasbiyh, takbiyr na kusoma Qur-aan)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (537). Tumeshaieleza nyuma].
5- Kicheko cha sauti
Kicheko hiki hubatilisha Swalaah kwa Ijma’a ya Maulamaa kama alivyonukulu Ibn Al-Mundhir. Kicheko ni kibaya kuliko maneno kwa sababu huandamana na dharau na kuichezea Swalaah. Kuna athari nyingi toka kwa Maswahaba (Allaah Awaridhie) zinazoonyesha kwamba Swalaah hubatilika kwa kucheka. [Imepokelewa toka kwa Jaabir na Abuu Muusa kama ilivyo kwa Ibn Abuu Shaybah katika Al-Muswannaf (1/387)].
·
Faida
Kutabasamu hakubatilishi Swalaah, lakini kunakuwa makruhu kama kutakuwa bila ya udhuru. Imepokelewa toka kwa Jaabir akisema: “Kutabasamu hakuivunji Swalaah, lakini mkoromo huivunja”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abu Shaybah (1/387) na ‘Abdul Razzaaq kwa Sanad Hasan].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
022-Qunuwt Katika Swalaah Za Faradhi
Alhidaaya.com [3]
Kwanza: Qunuwt katika Swalaah ya Alfajiri
[Haya yamenukuliwa toka kwenye tasnifu murua kabisa ya ndugu yetu katika iymaan Magdiy bin ‘Abdul Haadiy yenye anwani isemayo: “ Isfaar As-Subhi Fiy Qunuwtis Subhi”. Imefanyiwa utangulizi na kupitiwa na Sheikh wetu Mustwafa Al-‘Adawiy (Allaah Ainyanyue hadhi yake)]
Maulamaa wamekhitalifiana kuhusiana na uhalali wa qunuwt katika Swalaah ya Alfajiri na muundo wake. Wamekhitalifiana juu ya kauli nne:
Kauli ya kwanza:
Ni Sunnah endelevu iliyokokotezwa, imesuniwa kudumu nayo
Ni madhehebu ya Maalik na Ash-Shaafi’iy. [Al-Mudawwanah (1/100), Al-Istidhkaar (6/201), Al-Ummu (8/814), Al-Majmu’u (3/494) na Al-Adhkaar cha An-Nawawiy (69)]
Hoja ya kauli hii ni haya yafuatayo:
1- Hadiyth ya Al-Barraa bin ‘Aazib aliyesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisoma qunuwt Alfajiri [na Magharibi]. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (678), At-Tirmidhiy (401), Abuu Daawuud (1441) na An-Nasaaiy (2/202). ‘Amri bin Murrah amekhitalifiwa katika tamko la (Magharibi)].
2- Hadiyth ya Anas ya kuwa aliulizwa: “Je, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alifanya qunuwt Alfajiri?” Akajibu: “Ndio”. Akaulizwa: “Je, alifanya kabla ya kurukuu?” Akajibu: “Baada ya kurukuu kwa kidogo”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraj” na Al-Bukhaariy (1001) na Muslim (677)].
3- Hadiyth ya Abuu Hurayrah aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anasema wakati anapomaliza kusoma katika Swalaah ya Alfajiri, kisha akapiga takbiyr na kunyanyua kichwa chake: ((Sami’al Laahu liman hamidah, Rabbanaa wa Lakal hamdu)). Kisha anasema na yeye amesimama:
(( اللهم أنج الوليد بن الوليد، وسلمة بن هشام وعياش بن أبي ربيعة، والمستضعفين من المؤمنين، اللهم اشدد وطأتك على مضر، واجعلها عليهم كسني يوسف، اللهم ألعن لحيان ورعلا وذكوان، وعصية عصت الله ورسوله))
((Allaahumma Anji Al-Waliyda bna Al-Waliyd, wa Salamata ibna Hishaam, wa ‘Ayyaasha ibna Abiy Rabiy’ah, wal Mustadhw’afiyna minal Muuminiyna. Allaahumma Shdud watw-ataka ‘alaa Mudhwirr Waj-’alhaa ‘alayhim kasiniyyi Yuusuf. Allaahumma Al-’an Lahyaana wa Ra’alan wa Dhakawaana, wa ‘Uswayyatan ‘aswatil Laaha wa Rasuulahu)). Kisha ikatufikia habari kwamba ameacha du’aa hiyo wakati ilipoteremka: [Msemaji ni Az Zuhriy kama alivyomwashiria Al-Haafidh katika Al-Fat-h (8/75)]
(( لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ ))
[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (804) na Muslim (678) na tamko ni lake].
4- Na du’aa kama hiyo hiyo kama ilivyopokelewa toka kwa Ibn ‘Umar ya kuwa alimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anaponyanyua kichwa chake toka kwenye rukuu ya rakaa ya mwisho ya Swalaah ya Alfajiri akisema:
((Ee Mola! Mlaani fulani na fulani na fulani)) baada ya kusema: ((Sami’al Laahu liman hamidah, Rabbanaa wa Lakal hamdu)). Na hapo Allaah Akateremsha:
(( لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ ))
[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (4559)].
Wamesema: “Mwelekeo wa Maalik na Ash-Shaafi’iy kutoa dalili hizi ni kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifanya qunuwt baada ya kusimama toka kwenye rukuu katika Swalaah ya Alfajiri, na hii inaonyesha kwamba alikuwa akiomba kila siku. Ama kuacha kuomba du’aa baada ya kuteremka Aayah, basi hilo haliharibu kitu kwa mambo mawili: Moja ya mawili hayo ni kuwa kauli hii ni taarifa toka kauli ya Az-Zuhriy kama ilivyo katika riwaya ya Abuu Hurayrah, nayo imekatika, haifai. [Fat-hul Baariy (8/75) na Ma’arifatus Sunan wal Aathaar cha Al-Bayhaqiy (2/74)]
Na kama tutajaalia kwamba ni sahihi, basi makusudio yanayoweza kukubalika ni kuwa aliacha kulaani tu na si kuomba du’aa kabisa”. [Angalia: Al-Ummu (8/815), Ibn Khuzaymah (1/316), Ma’alimus Sunan (1/250), Al-Majmu’u (3/505) na Twarhut Tathriyb (2/289). Angalia Isfaarus Swubh ukurasa 52]
5- Ni yale yaliyoripotiwa toka kwa Anas kwamba amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuacha kuomba qunuwt katika Swalaah ya Alfajiri mpaka alipofariki”. Kauli hii ni munkari na haifai. [Hadiyth Munkar: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (3/162), Ad-daaraqutwniy (2/39), Al-Bayhaqiy (2/201) na Ibnul Jawziy katika Al’Ilal Al-Mutanaahiyah (1/441)].
Kauli ya pili:
Qunuwt katika Swalaah ya Alfajiri na nyinginezo imenasikhiwa na ni bid-’a
Ni madhehebu ya Abuu Haniyfah. [Al-Mabsuwtw (1/165) na Fat-hul Qadiyr (1/431)] Dalili za kauli hii ni haya yafuatayo:
1- Ni Hadiyth ya Abuu Maalik Al-Ashja’iy aliyemuuliza baba yake: “Wewe umeswali nyuma ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Abu Bakr, ‘Umar, ‘Uthmaan, na ‘Aliyy bin Abiy Twaalib hapa Kufa kiasi cha miaka hamsini, je walikuwa wakifanya qunuwt?” Akasema: “Ndio, ee mwanangu”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (402), Ibn Maajah (1241), na Ahmad (3/472). Al-‘Uqayliy ameitia doa katika Adh-Dhu’afaa (2/119)].
Hoja hii inapingwa kwa kusema kwamba hakuna lolote linaloonyesha kuwa baba wa Abuu Maalik –Twaariq bin Ashyam (Allaah Amridhie) – alisuhubiana na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Aidha, upo uwezekano mkubwa kuwa hakuwa akijua kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifanya qunuwt. Isitoshe, hata Maswahaba wakubwa waliokuwa wakiandamana sana na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) walikuwa hawajui mambo kadhaa aliyokuwa akiyafanya. [Angalia mifano ya hili katika MaFaatihahu Lilfiqhi Fid Diyn cha Sheikh wetu (Allaah Amhifadhi) ukurasa wa 82]
Ninasema: “Kisha qunuwt imethibiti toka kwa Makhalifa wanne vile vile!!”
2- Ni yale yaliyoripotiwa toka kwa Ummi Salamah aliyesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza qunuwt katika Swalaah ya Alfajiri”. [Isnadi yake mbovu: Imefanyiwa “ikhraj” na Ad- Daaraqutwniy (2/38)].
3- Ni yale yaliyoripotiwa toka kwa Ibn Mas-’oud aliyesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakufanya qunuwt isipokuwa mwezi mmoja tu, hakufanya kabla yake wala baada yake”. [Isnadi yake mbovu: Imefanyiwa “ikhraj” na Atw-Twahaawiy katika Sharhul Ma’aniy (1/245) na Al-Bayhaqiy (2/213)].
4- Na mfano wake toka kwa Ibn ‘Umar aliyesema: “Ni bid-’a, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakufanya qunuwt ila mwezi mmoja tu, kisha akaiacha”. [Isnadi yake ni dhwa’iyf: Imefanyiwa”ikhraaj” na Al-Bayhaqiy (2/213)].
Riwaya hizi tatu ni dhwa’iyf, hazifai kutolewa dalili lakini imethibiti toka kwa Ibn ‘Umar kwamba alisema: “Sikushuhudia yeyote akiifanya!!” [Isnadi yake ni Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdul Razzaaq (4954)].
Imepokelewa kwamba Ibn Mas-’oud alikuwa hafanyi qunuwt katika Swalaah ya Alfajiri. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdul Razzaaq (4949)].
5- Kuacha qunuwt katika Hadiyth ya Ibn ‘Umar na Abu Hurayrah iliyotangulia katika dalili za kundi la kwanza, inaonyesha naskh, na hilo limeshajibiwa katika njia mbili.
6- Wamesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alifanya qunuwt katika Swalaah za Magharibi na Alfajiri, kisha ikaondoshwa qunuwt ya Magharibi, na pia ya Alfajiri!!
Linajibiwa hili kwamba naskhi haiingii kwa hili wala lile.
Kauli ya tatu:
Qunuwt haisomwi ila wakati wa misukosuko tu
Ni kauli ya Ahmad na baadhi ya Mahanafi waliofuatia. [Al-Mughniy (2/587) na Fat-hul Qadiyr cha Ibnul Hammaam (1/434)]
Dalili yao ni Hadiyth ya Anas Allaah Amridhie anayesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa hafanyi qunuwt isipokuwa pale anapowaombea watu mema au anapowaombea watu mabaya”. [Isnadi yake Laini: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abu Khuzaymah (620). Inaonekana kwamba ni muhtasari toka katika Hadiyth ya Anas iliyotangulia katika kuelezea qunuwt yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa ‘aalihi wa sallam) na kuwaombea du’aa mbaya makabila. Hadiyth hii imefunga mpaka wa kuwa qunuwt haifanyiki ila katika kuwaombea tu watu du’aa mbaya. Ninakhofia mzigo katika hili akaubeba Muhammad bin Muhammad bin Marzouq, kwani Ibn ‘Uday amezikanusha Hadiyth zake mbili ambazo yeye peke yake kazipokea toka kwa ‘Abdullah bin Answaar, na yeye hapa, anasimulia toka kwake!!]
Kauli ya nne:
Inajuzu kuifanya au kuiacha
Ni kauli ya Ath-Thawriy, Ibn Jariyj Atw-Twabariy, Ibn Hazm na Ibnul Qayyim. [Tahdhiybul Aathaar (1/337), Al-Muhallaa (4/143) na Zaadul Ma’ad (1/274)]
Wamesema: “Imethibiti kutokana na mjumuiko wa riwaya kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiifanya qunuwt wakati, na kuiacha wakati mwingine kwa ajili ya kuufundisha umma wake kwamba wana khiyari ya ima kuifanya au kuiacha.
Ibn Al-Qayyim anasema: “Maulamaa wa Hadiyth wako kati na kati; kati ya hawa na hawa [yaani: wale walioizuia kabisa] na kati ya wale wanaosema kwamba ni Sunnah wakati wa misukosuko na mengineyo. Maulamaa hawa hawana tatizo na makundi yote mawili, kwani wanaifanya qunuwt pale alipoifanya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na wanaiacha pale alipoiacha. Wao humfuata katika kutenda kwake na kuacha kwake wakisema: “Kufanya kwake ni Sunnah na kuacha kwake ni Sunnah”. Pamoja na hivi, hawamkatalii mwenye kuifanya daima, wala hawachukulii kuifanya kama ni makruhu, wala hawachukulii kama ni bid-’a, na wala hawamzingatii mfanyaji wake kama anakwenda kinyume na Sunnah. Aidha, hawamkatalii mwenye kukataa kufanywa wakati wa kuzuka misukosuko, wala hawaoni kwamba kuiacha ni bid-’a wala mwenye kuiacha kama anakwenda kinyume na Sunnah, bali mwenye kuifanya katenda wema, na mwenye kuiacha katenda wema pia”.
Lenye nguvu
Hakuna shaka yoyote kwamba kufanya qunuwt daima katika Swalaah ya Alfajiri, haikuwa katika mwenendo wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Pia hakuna shaka yoyote kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliifanya. Hivyo basi, suala linabakia ndani ya mzunguko wa kati ya kuwa kwake ni Sunnah wakati wa kutokea misukosuko tu, au kuwa ifanywe baadhi ya nyakati na iachwe wakati mwingine ingawa ninaloliona mimi kupitia Hadiyth zilizothibiti katika suala hili ni kuwa lililo karibu zaidi ni kuwa qunuwt haifanywi ila wakati wa misukosuko tu. Na hii si kwa Hadiyth iliyotolewa dalili na Maulamaa wa kauli ya tatu, bali ni kwa Hadiyth zinazohusiana na du’aa alizoziomba Rasuli katika qunuwt ya Alfajiri. Du’aa zote hizi ni za ima kuwaapizia watu mabaya au kuwaombea mema. Kadhalika, kuna yale yaliyothibiti toka kwa ‘Umar bin Al-Khattwaab yasemayo:
((..وانصرهم على عدوك وعدوهم، اللهم العن كفرة أهل الكتاب... اللهم خالف بين كلمتهم، وزلزل أقدامهم، وأنزل بهم بأسك الذي لا ترده عن القوم المجرمين..))
((..wan Swurhum ‘alaa ‘aduwwika wa aduwwihim. Allaahumal ‘An kafarata Ahlil Kitaab..Allaahumma Khaalif bayna kalimatihim, wa Zalzil aqdaamahum, wa Anzil bihim baasakal ladhiy laa Tarudduhuu ‘anil qawmil mujirimiyna)). [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdul Razzaaq (4969)].
Nami nasisitiza hapa kwamba ikiwa mtu atachukua msimamo huu, basi haijuzu kwake kumzingatia anayekwenda kinyume nao kama ni mtu wa bid-’a au mtu asiyefaa kuwa imamu. Anayefanya hivi atakuwa haijui Dini ya Allaah (Subhaanah) ambayo sisi tunajitakasa nayo kuelekea Kwake. Imamu Ahmad alipoulizwa kuhusu watu wanaosoma qunuwt mjini Basrah kama inafaa kuwafuata au la alijibu: “Waislamu walikuwa wakimfuata anayesoma qunuwt, na wanamfuata asiyesoma qunuwt pia”. [Ibn Al-Qayyim kainukuu kutoka kwake katika kitabu cha As-Swalaahat wa Hukmu Taarikihaa uk. 120]
·
Qunuwt Alfajiri inakuwa ni baada ya kurukuu
Lililothibiti katika Hadiyth zilizotangulia za Anas, Ibn ‘Umar na Abu Hurayrah ni kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisoma qunuwt baada ya kuitadili toka kwenye rukuu. Haya ndiyo waliyoyasema akina Ash-Shaafi’iy, Ahmad, na Is-Haaq, nayo ni riwaya toka kwa Maalik.
Maalik kwa ilivyo tangaa kwake ni kuwa mahala pa qunuwt ni kabla ya kurukuu. Na hili limethibiti kwa baadhi ya Maswahaba kama vile ‘Umar, ‘Aliyyi na Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu Anhum). Suala uwanja wake ni mpana, lakini la kwanza la kuisoma baada ya kuitadili, ni bora zaidi kama tunavyoona.
Pili: Qunuwt katika Swalaah tano
Qunuwt inaruhusiwa katika Swalaah zote tano za faradhi endapo kama patazuka kwa Waislamu janga au misukosuko. Ni kutokana na Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), alifanya qunuwt mwezi mzima mfululizo katika Swalaah za Adhuhuri, Alasiri, Magharibi, ‘ishaa na Alfajiri baada ya kusema: “Sami’al Laahu liman hamidah” katika rakaa ya mwisho akiwaombea walio hai katika ukoo wa Baniy Sulaym dhidi ya Ra’al, Dhakawaan na ‘Uswayyah, na walio nyuma yake wakiitikia “aamiyn”. [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (1/301), Ibn Al-Jaarowd (197), Ibn Khuzaymah (618), Al-Haakim (1/225) na Al-Bayhaqiy (2/200). Ina Hadiyth mwenza toka kwa Abuu Hurayrah].
·
Faida Kadhaa Kuhusiana Na Qunuwt
1- Imamu hunyanyua sauti wakati wa kuomba du’aa kwa kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifanya hivyo. Na kwa kufanya hivyo, Anas, Abuu Hurayrah na Ibn ‘Abbaas waliweza kuinukuu du’aa yake katika qunuwt.
2- Watu wanaomfuata imamu huitikia “aamiyn”. Ni kutokana na yaliyomo ndani ya Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas iliyotangulia yasemayo: “Na huitikia aamiyn walioko nyuma yake”. Ibn Qudaamah amesema: “Hatujasikia makhitilafiano yoyote hapa”.
Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Uthmaan akisema: “Niliswali nyuma ya ‘Umar bin Al-Khattwaab, akasoma aayah 200 za Al-Baqarah, akasoma qunuwt baada ya rukuu, akanyanyua mikono yake mpaka nikaona weupe wa kwapa zake, na akanyanyua sauti yake kwa du’aa mpaka wakasikia walio nyuma ya ukuta. [Angalia Isfaarus Swubh ukurasa wa 66-69 na rejea zinazofuatia]
3- Je, mikono hunyanyuliwa katika qunuwt? [Isnadi yake ni Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bayhaqiy katika Ma’arifatus Sunan (2/83)]
Jamhuri ya Maulamaa akiwemo Abuu Haniyfah, Ahmad na Is-Haaq wote wananyanyua mikono katika qunuwt. Ibn Al-Mundhir ameliripoti hili toka kwa ‘Umar - nayo ni sahihi toka kwake kama ilivyotangulia – pamoja na Ibn Mas-’oud na wengineo. Mwelekeo huu unaungwa mkono na Hadiyth ya Anas isemayo kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) – katika Swalaah ya Alfajiri – alinyanyua mikono yake akawaombea…Hadiyth”. [Al-Awsatw (5/212), Al-Mughniy (2/584) na Al-Majmu’u (3/499)]
Maalik amesema: “Mikono hainyanyuliwi, na la kwanza ni sahihi zaidi. Allaah Ndiye Mjuzi zaidi”.
Masuala mengineyo yanayohusiana na qunuwt yatakuja kuelezewa kwenye mlango wa Witr InshaAllaah.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
023-Swalaah Za Sunnah (Tatwawwu’’u)
Alhidaaya.com [3]
Taarifu yake:
Asili ya neno “tatwawwu’u” ni kufanya amali ya kumtii Allaah (twa’a), kisha likawa kiistilahi kwa maana ya kufanya amali ya kumtii Allaah isiyo ya wajibu. Swalaah za Sunnah ni zile za nyongeza juu ya Swalaah za faradhi kutokana na neno la Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakati alipoulizwa kuhusu Uislamu na kusema:
((Ni Swalaah tano mchana na usiku)). Muulizaji akasema tena: Je, kuna jingine zaidi? Akasema: ((Hapana, ila kama utaswali za Sunnah)). [Hadiyth Swahiyh: Takhriyj yake ishatangulia].
Umuhimu Wa Swalaah Za Sunnah
1- Swalaah ndio amali bora zaidi
Swalaah ndio ‘ibaadah bora zaidi ya kimwili, na ndio jambo bora zaidi ambalo mtu hujikurubisha nalo kwa Allaah Mtukufu. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( استقيموا، ولن تحصوا، واعلموا أن خير أعمالكم الصلاة))
((Lingamaneni sawa, lakini hamtoweza (kwa nguvu zenu na juhudi zenu) na jueni kwamba amali yenu bora zaidi ni Swalaah)).[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Maajah (277) na wengineo. Ina Sanad ambazo zote ni Swahiyh. Angalia Ta’adhiymu Qadris Swalaat (170- kwa uhakiki tulioufanya sisi)]
2- Hunyanyua hadhi ya mtu peponi kwa kuzikithirisha
Imepokelewa toka kwa Rabiy’a bin Maalik Al-Aslamiy akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia: ((Omba)). Nikasema: “Nakuomba nisuhubiane nawe Peponi. Akasema: ((Kuna jingine zaidi?)). Nikasema: “Ni hilo tu”. Akasema: ((Basi jisaidie mwenyewe kwa kukithirisha sujudi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (489), An-Nasaaiy (2/227), Abuu Daawuud (1320) na Ahmad (4/59)].
Na Thawbaan alimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu amali itakayomwingiza Peponi. Rasuli akamwambia:
(( عليك بكثرة السجود فإنك لا تسجد لله سجدة إلا رفعك الله بها درجة وحط عنك بها خطيئة ))
((Jilazimishe kusujudu kwa wingi, kwani hakika wewe husujudu sijda yoyote kwa ajili ya Allaah isipokuwa Allaah Hukunyanyua daraja moja na Hukupomoshea kwayo kosa moja)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (488). Angalia Ta’adhiymu Qadris Swalaahat nilichokifanyia uhakiki (300).]
3- Huunga mapungufu ya Swalaah za faradhi
Imepokelewa toka kwa ‘Ammaar bin Yaasir akisema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
(( إن الرجل لينصرف ]من صلاته[ وما كتب له إلا عشرها تسعها ثمنها سبعها سدسها خمسها ربعها ثلثها نصفها))
((Hakika mtu huondoka [toka kwenye Swalaah yake], na huwa hakuandikiwa isipokuwa moja ya kumi yake, moja ya tisa yake, moja ya nane yake, moja ya saba yake, sudusi yake, khumsi yake, robo yake, theluthi yake, nusu yake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (796) na Ahmad (4/321). Angalia Qadrus Swalaahat nilichokifanyia uhakiki (156)].
Swalaah za Sunnah zimewekwa kwa ajili ya kuyaunga na kuyakamilisha mapungufu yanayoweza kuwa yamefanyika ndani ya Swalaah ya faradhi. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:
(( Jambo la kwanza watakalofanyiwa hisabu watu Siku ya Qiyaamah katika amali zao ni Swalaah. Mola wetu Atawaambia Malaika – Naye Anajua kila kitu - : Angalieni katika Swalaah ya mja Wangu; je ameiswali kamili au ameiswali pungufu? Ikiwa kamili, ataandikiwa Swalaah kamili, na kama ameiswali pungufu Atawaambia: “Angalieni, je mja Wangu ana Swalaah za Sunnah? Ikiwa anazo Swalaah za Sunnah Atasema: Mkamilishieni Mja Wangu faradhi zake kwa Sunnah zake, kisha amali zake huchukuliwa juu ya hilo)). [Hadiyth Swahiyh katika jumla: Angalia Ta’adhiymu Qadris Swalaahat nilichokifanyia uhakiki (180)].
Vigawanyo Vya Swalaah Za Sunnah
1- Sunnah “Mutwlaq”
Hizi ni zile zisizo na sababu, zisizo na hesabu au idadi maalumu ya rakaa zake. Mwenye kuswali anaweza kunuwia idadi ya rakaa au kutonuwia, bali atanuwia tu Swalaah. Na ikiwa ataingia kuswali Sunnah bila kunuwia idadi maalumu, basi anaweza kutoa tasliym katika rakaa ya kwanza, au akaongeza akatoa katika rakaa ya pili, au ya tatu, au ya kumi au zaidi. Na kama ataswali rakaa ambazo hajui idadi yake kisha akatoa tasliym, basi itakuwa sahihi. [Al-Majmu’u cha An-Nawawiy (3/541)]
Imepokelewa toka kwa Abuu Hurayrah kuwa aliswali rakaa nyingi sana. Baada ya kutoa tasliym, Al-Ahnaf bin Qays alimuuliza: “Je, umemalizia kwa shufwa au Witr?” Akajibu: “Kama sijui, basi Allaah Anajua. Hakika mimi nimemsikia Kipenzi changu Abal Qaasim akisema:
(( ما من عبد يسجد لله سجدة إلا رفعه الله بها درجة وحط عنه بها خطيئة ))
((Hakuna mja yeyote anayemsujudia Allaah sijdah moja, isipokuwa Allaah Humnyanyulia kwayo daraja, na Humpomoshea kwayo kosa moja)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (5/164), ‘Abdul Razzaaq (3561, 4847), Al-Bazzaar (9/345) na Al-Bayhaqiy (2/489)]
Wakati Gani Atafanya Tashah-hudi?
Kama ataswali Sunnah ya rakaa moja, ni lazima afanye tashah-hudi mwisho wake, na kama ataswali zaidi ya rakaa moja, basi atatosheka na tashah-hudi moja tu mwishoni mwa Swalaah yake. Tashah-hudi hii ni nguzo ambayo ni lazima aifanye. Pia anaweza kufanya tashah-hudi baada ya kila rakaa mbili kama ilivyo katika Swalaah za faradhi za rakaa nne. Na kama idadi ya rakaa ni Witr, basi ni lazima afanye tashah-hudi katika rakaa ya mwisho vile vile ikiwa Swalaah yake ni ya rakaa nne. Na ikiwa ni ya rakaa sita, au kumi au zaidi ya hizo, sawasawa ikiwa ni shufwa au Witr, basi hapo kuna njia nne: [Al-Majmu’u (3/542-543)]
1- Inajuzu kufanya tashah-hudi katika kila rakaa mbili hata kama tashah-hudi zitakithirika, lakini tashah-hudi katika rakaa ya mwisho ni lazima. Pia anaweza kutosheka na tashah-hudi moja tu ya mwisho, au akafanya tashah-hudi baada ya kila rakaa nne, au tatu, au sita na kadhalika. Lakini pamoja na hivi, haijuzu kufanya tashah-hudi katika kila rakaa moja, kwani hiyo itakuwa ni kuzua picha ambayo haijawahi kufanyika katika Swalaah.
2- Haijuzu zaidi ya tashah-hudi mbili katika Swalaah moja, au kuwepo kati ya tashah-hudi mbili zaidi ya rakaa mbili ikiwa idadi ya rakaa ni shufwa, na ikiwa ni Witr, haijuzu kati yao zaidi ya rakaa moja. An-Nawawiy kasema: “Hii ina nguvu, na ndio mwelekeo wa Sunnah”. Dalili ya njia hii itakuja kuelezewa katika mlango wa “Qiyaamul Layl”.
3- Asikae ila katika rakaa ya mwisho. An-Nawawiy kasema: “Ni makosa”. Nami nasema: “Bali imethibiti Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kufanya hilo. Tutakuja kufafanua hilo katika mlango wa Swalaah ya Witr”.
4- Inajuzu kufanya tashah-hudi katika kila rakaa mbili na katika kila rakaa moja. An-Nawawiy kasema: “Hili ni dhwa’iyf, au batili”.
Ni Bora Kuswali Rakaa Mbili Mbili
Hakuna makhitilafiano yoyote kwamba lililo bora ni kutoa tasliym baada ya kila rakaa mbili katika Sunnah za usiku na mchana. Imeripotiwa toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
(( صلاة الليل ] والنهار[ مثنى مثنى))
((Swalaah ya usiku [na mchana] ni rakaa mbili mbili)). [Ni Hadiyth Shaadh kwa nyongeza hii: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (1295), At-Tirmidhiy (594), An-Nasaaiy (3/227) na Ibn Maajah (1322). Angalia Fataawaa Ibn Taymiyah (21/289). Imekosolewa na Ahmad, An-Nasaaiy, At-Tirmidhiy, Ad-daaraqutwniy, Ibn ‘Abdul Barri na Ibn Hajar]
Hadiyth hii si Swahiyh. Iliyo Swahiyh ni kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
(( صلاة الليل مثنى مثنى، فإذا خشيت الصبح فأوتر بواحدة))
((Swalaah ya usiku ni rakaa mbili mbili. Ukichelea Alfajiri, basi swali Witr kwa rakaa moja)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (990) na Muslim (749) toka Hadiyth ya Ibn ‘Umar]
Haya niliyoyaeleza ya kujuzu kukusanya rakaa nyingi za Swalaah za Sunnah “mutwlaq” kwa tasliym moja, na kwamba lililo bora katika Sunnah za usiku na mchana ni kutoa tasliym baada ya kila rakaa mbili, yote haya ni matamshi ya akina Maalik, Ash-Shaafi’iy, Ahmad, Daawuud na Ibn Al-Mundhir. Pia yameripotiwa toka kwa Al-Hasan, na Sa’iyd bin Jubayr.
Abu Haniyfah amesema: “Tasliym ni baada ya rakaa mbili au nne katika Swalaah ya mchana, na isizidi zaidi ya hapo, na Swalaah ya usiku ni rakaa mbili, au nne, au sita, au nane kwa tasliym moja, wala zisizidi rakaa nane”.
2- Sunnah “Muqayyad”
Hizi ni zile ambazo Hadiyth zimethibitisha uwepo wake. Sunnah hizi ni za aina mbili:
(a) Sunnah “Rawaatib”
Hizi ni zile zinazofungamana na Swalaah tano za faradhi. Kati ya Sunnah hizi, kuna zile zinazoswaliwa kabla ya Swalaah za faradhi, nazo hujulikana kama “As-Sunnat Al-Qabliyyah”, na kuna zingine zinazoswaliwa baada ya Swalaah za faradhi, nazo huitwa “As-Sunnat Al-Ba’adiyyah”. Kuna maana murua kabisa na mwafaka ya kuwepo Sunnah hizi za kabla na baada ya Swalaah za faradhi. Ama za kabla, ni kuwa nafsi kutokana na kushughulishwa na mihangaiko ya kidunia, inakuwa iko mbali na khushui na uwepo wake ambao ndio roho ya ‘ibaadah. Swalaah hizi zinaposwaliwa kabla ya faradhi, basi nafsi ya mtu inapata utulivu ndani ya Swalaah anayoiswali. Ama zile za baada, ni kuwa kama tulivyosema kwamba Swalaah za Sunnah hujazilia mapungufu yaliyotokea kwenye Swalaah za faradhi, basi faradhi inaposwaliwa, imekuwa ni mwafaka kuswaliwa Sunnah baada yake ili ijazilie pengo lolote lililotokea.
· Rawaatib: Kuna zilizokokotezwa, na zisizokokotezwa
Sunnah hizi zinazofungamana na faradhi, kuna kati yake ambazo zimekokotezwa, nazo ni zile ambazo Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akidumu nazo bila kuziacha, nazo ziko kumi.
Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu Anhumaa) akisema: “Nimehifadhi toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) rakaa kumi: Rakaa mbili kabla ya Adhuhuri na rakaa mbili baada yake, rakaa mbili baada ya Magharibi, rakaa mbili baada ya ‘ishaa, na rakaa mbili kabla ya Alfajiri”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1180) na Muslim (729)].
Haya kayasema Ash-Shaafi’iy na Hanbali. [Al-Majmu’u (3/501) na Kash-Shaaf Al-Qina’a (1/422)]
Kwa Mahanafi [Ibn ‘Aabidiyn (1/441)], “Rawaatib” zilizokokotezwa ni kumi na mbili: Ni hizo kumi zilizotangulia lakini kabla ya Adhuhuri ni rakaa nne kutokana na Hadiyth ya ‘Aaishah asemaye: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa haachi rakaa nne kabla ya Adhuhuri”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1182)].
Imepokelewa toka kwa Ummu Habiybah (Allaah Amridhie) akisema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
((Mwenye kuswali rakaa kumi na mbili mchana na usiku, atajengewa kwa rakaa hizo nyumba peponi)). Ummu Habiybah anasema: “Sikuziacha kamwe tokea nilipomsikia Rasuli wa Allaah akisema hivyo”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (728), At-Tirmidhiy (415), na ziada ni yake, Abuu Daawuud (1250), na Ibn Maajah (1141). Ina mwenza wake kutoka Hadiyth ya ‘Aaishah iliyoko kwa At-Tirmidhiy (414), An-Nasaaiy (3/260) na Ibn Maajah (1140)].
At-Tirmidhiy kaongeza: “Nne kabla ya Adhuhuri na mbili baada yake, rakaa mbili baada ya Magharibi, rakaa mbili baada ya ishaa, na rakaa mbili kabla ya Alfajiri”.
Ama Maalik, wao hawana idadi maalumu ya rakaa za rawaatib. Inatosha kwao kuipata Sunnah kwa kuswali rakaa mbili wakati wote.
Ama rawaatib ambazo hazikukokotezwa, hizi ni zile ambazo zimesuniwa kuziswali kiujumla bila kutiliwa mkazo.
Sunnah Ya Alfajiri
· Kusisitizwa Kwake
Rakaa mbili kabla ya Alfajiri, ni katika Sunnah za rawaatib iliyohimiziwa sana. Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah (Allaah Amridhie) akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwa ameshikamana zaidi na chochote katika Swalaah za Sunnah kama alivyokuwa ameshikamana na rakaa mbili za Alfajiri”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1094) na Muslim (1191)].
Na katika tamko jingine: “Hakuwa akiziacha kamwe”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1159)].
Na katika Hadiyth nyingine iliyosimuliwa na bibi huyu huyu, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Rakaa mbili za Alfajiri, ni bora kuliko dunia na vilivyomo ndani yake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (725) na At-Tirmidhiy (416)].
Ibn Al-Qayyim anasema katika Az-Zaad (1/315): “ Na kwa ajili hiyo Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuziacha pamoja na Sunnah ya Witr sawasawa akiwa safarini au akiwa nyumbani. Akiwa safarini, alikuwa haziachi kabisa kulinganisha na Sunnah nyinginezo zote. Na haikunukuliwa kutoka kwake kuwa yeye (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali Sunnah nyingine zaidi ya hizo mbili akiwa safarini”.
· Kuzifupisha
Imesuniwa kuzifupisha rakaa hizi mbili za Alfajiri ili zisije kugongana na la wajibu. Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar akisema: “Hafswah alinieleza kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaswali rakaa mbili fupi kabla ya kuqimiwa Swalaah wakati mwadhini anapokaa kwa ajili ya Alfajiri, na Alfajiri ikadhihiri”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (583)].
Na imepokelewa toka kwa ‘Aaishah akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali rakaa mbili fupi kati ya adhana na iqaamah katika Swalaah ya Alfajiri”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (584)].
Pia anasema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akizifupisha rakaa mbili za kabla ya Swalaah ya Alfajiri mpaka nikawa najiuliza: “Je, kasoma Al-Faatihahh?” [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1095) na Muslim (1189)].
Ama Suwrah zinazosomwa baada ya Al-Faatihah katika rakaa hizi mbili ni kuwa imethibiti toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa alikuwa akisoma Aayah zifuatazo katika rakaa mbili za Sunnah ya Alfajiri:
1- Imepokelewa toka kwa Abuu Hurayrah akisema kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisoma katika rakaa mbili za Sunnah ya Alfajiri: (( قل يا أيها الكافرون )) na (( قل هو الله أحد )). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (726)].
2- Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Abbaas akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anasoma katika rakaa mbili za Alfajiri:
((قُولُوا آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ
وَمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَمَا أُوتِيَ النَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ))
na
((قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّـهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا
وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ))
[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (727) na An-Nasaaiy (2/155)].
Husoma baada ya Al-Faatihah katika rakaa ya kwanza aya ya (136) ya Suwrat Al-Baqarah, na baada yake katika rakaa ya pili aya ya 64 ya Suwrat Aal-‘Imraan”.
3- Alikuwa anaweza pia kubadili Aayah ya Aal-‘Imraan katika rakaa ya pili kwa Neno Lake Ta’alaa:
((فَلَمَّا أَحَسَّ عِيسَىٰ مِنْهُمُ الْكُفْرَ قَالَ مَنْ أَنصَارِي إِلَى اللَّـهِ ۖ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ نَحْنُ أَنصَارُ اللَّـهِ
آمَنَّا بِاللَّـهِ وَاشْهَدْ بِأَنَّا مُسْلِمُونَ))
mpaka mwisho wa Aayah kama ilivyo katika Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (727) na Abu Daawuud (1259)].
Ninasema: “Lililo bora ni kufanya uanuwai katika haya yote kwa ajili ya kuipata Sunnah kama ilivyo katika ‘ibaadah nyinginezo zinazofanyika kwa njia zaidi ya moja ambazo usahihi wake umethibiti”.
· Kulala Kwa Ubavu Wa Kulia Baada Ya Kuziswali
Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah akisema: “ Baada ya mwadhini kumaliza adhana ya Alfajiri, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anasimama, akaswali rakaa mbili fupi kabla ya Swalaah ya Alfajiri baada ya Alfajiri kudhihiri, kisha hulala kwa ubavu wake wa kulia mpaka aje mwadhini aqimu Swalaah”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (590)].
Maulamaa wamekhitalifiana kuhusu hukmu ya kulala ubavu baada ya rakaa mbili za Sunnah ya Alfajiri juu ya kauli zifuatazo: [Naylul Awtwaar (3/28-32), Al-Muhallaa (3/196) na Al-Majmu’u (3/523-524)]
1- Ni Sunnah bila mpaka
Ni madhehebu ya Ash-Shaafi’iy. Wamelisema hili pia akina Abuu Musa Al-Ash-‘Ariy, Raafi’i ibn Khudayj, Anas bin Maalik na Abuu Hurayrah. Pia Ibn Syriyn na Mafuqahaa saba.
2- Ni wajibu
Ni kauli ya Abu Muhammad bin Hazm. La kushangaza zaidi ni kuwa yeye amekufanya kulala huku ni sharti ya kuswihi Swalaah ya Alfajiri!! Sheikh wa Uislamu amesema: “Hili ndilo alilopwekeka nalo mbali na umma wote”.
Ninasema: “Kigezo chake ni Hadiyth ya Abu Hurayrah aliyesema: “ Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( إذا صلى أحدكم الركعتين قبل صلاة الصبح، فليضطجع على جنبه الأيمن ))
((Anaposwali mmoja wenu rakaa mbili kabla ya Swalaah ya Alfajiri, basi alale kwa ubavu wake wa kulia)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (1261), At-Tirmidhiy (420), Ahmad (2/415) na wengineo. Ibn Taymiyah amesema: “Hii ni batili, si sahihi, bali sahihi ni kufanya, na si amri ya kulala. Amri ya kufanya kabaki nayo ‘Abdul Waahid bin Ziyaad peke yake]
Anajibiwa kwamba Hadiyth hii imetiwa walakini. Na kama tutaichukulia kuwa ni Swahiyh, basi amri ya kufanya itageuzwa kuwa ni mustahabu kwa Hadiyth ya ‘Aaishah asemaye: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali rakaa mbili. Nikiwa macho hunisemesha, na kama siko macho, hulala kwa ubavu”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1092) na Muslim (1227)].
Inaonyesha kwamba hakuwa akilala ikiwa ‘Aaishah yu macho, hivyo imekuwa ni alama ya kuigeuza amri kuwa ni Sunnah.
3- Ni makruhu
Ni kauli ya mjumuiko wa Masalaf akiwemo Ibn Mas-’oud, Ibn Al-Musayyib na An-Nakh’iy. Al-Qaadhwiy ‘Ayyaadh ameisimulia toka kwa Jamhuri ya Maulamaa. Hoja yao ni kuwa haikujulikana toka kwa yeyote kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alilifanya hilo Msikitini, kwani lau angelifanya, basi nukuu yake ingelielezewa kizazi baada ya kingine!!
4- Ni kinyume cha ubora
Hili limesimuliwa toka kwa Al-Hasan Al-Baswriy.
5- Imesuniwa kwa anayeswali usiku ili apumzike.
Ni chaguo la Ibn Al’Arabiy na Sheikh wa Uislamu Ibn Taymiyah.
6- Kulala kwa ubavu si kwamba ndiko hasa kulikokusudiwa, bali ni kwa ajili ya kutenganisha kati ya Sunnah na faradhi.
Hili limesimuliwa toka kwa Ash-Shaafi’iy, nalo limepingwa, kwa kuwa kutenganisha kunaweza kuwa kwa kitu kingine badala ya kulala.
Ninasema: “Lenye nguvu ni kuwa kulala kwa ubavu baada ya rakaa mbili mbili za Sunnah ya Alfajiri, kumesuniwa kwa masharti mawili:
La kwanza: Kuwe ni nyumbani na si Msikitini, kwa kuwa haikunukuliwa kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alilifanya hilo msikitini.
La pili: Awe mtu anaweza kufanya hivyo na kwenda kuswali Alfajiri bila ya kupitiwa tena na usingizi Swalaah ikampita. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
· Ulipaji Wake
Mwenye kupitwa na rakaa mbili za Sunnah ya Alfajiri kwa udhuru, anaruhusiwa kuzilipa wakati wowote udhuru wake unapoondoka kutokana na dalili zifuatazo:
1- Hadiyth ya Abu Hurayrah aliyesema: “Tulilala pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na hatukuweza kuamka mpaka jua likachomoza. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatuambia: ((Kila mmoja akamate ugwe wa mnyama wake tuondoke, kwani shaytwaan ametujia katika mashukio haya)). Tukafanya, kisha akaagiza maji akatawadha, halafu akasujudu sijdah mbili. Kisha ikaqimiwa Swalaah, akaswali Swalaah ya Alfajiri”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (1098) na wengineo].
Kuna Hadiyth kama hii ya ‘Imraan bin Haswiyn ambayo tumeitaja nyuma.
2- Hadiyth ya Qays bin ‘Amri aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwona mtu mmoja akiswali rakaa mbili baada ya Swalaah ya Alfajiri. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: ((Swalaah ya Alfajiri ni rakaa mbili)), na mtu yule akamwambia: “Mimi sikuwa nimeziswali rakaa mbili za kabla yake, nikaziswali sasa”. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akanyamaza”. [Hadiyth Hasan Litwuruqihi: Imeshatajwa katika mlango wa “Nyakati zilizoharamishwa kuswali”].
Yaliyotangulia hayapingani na Hadiyth ya Abu Hurayrah aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Ambaye hakuziswali rakaa mbili za Alfajiri, basi aziswali baada ya kuchomoza jua)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (423), Ibn Khuzaymah (1117), Al-Haakim (1/274), Ibn Hibaan (2472) na wengineo].
Hadiyth hii haielezi wazi kwamba mwenye kuziacha haziswali isipokuwa baada ya kuchomoza jua – kama walivyosema Jamhuri ya Maulamaa – kwani hakuna hapo isipokuwa amri tu kwa yule ambaye hakuziswali kabisa ya kwamba aziswali baada ya jua kuchomoza. Na hakuna shaka yoyote kwamba rakaa mbili hizi zikiachwa kuswaliwa katika wakati wake, huswaliwa katika wakati wa kulipa, na katika Hadiyth hakuna kinachozuia kuswaliwa baada ya Swalaah ya Alfajiri. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
Je, Baada Ya Kuingia Alfajiri, Kuna Sunnah Zingine Zaidi Ya Rakaa Mbili Za Alfajiri?
[Al-Awsatw cha Ibn Al-Mundhir (2/399-400)]
Maulamaa wamekhitalifiana kuhusiana na Sunnah zinginezo zaidi ya rakaa mbili za kabla ya Alfajiri kwa kauli mbili:
Ya kwanza:
Ni karaha kuswali Sunnah nyinginezo zaidi ya rakaa mbili za Alfajiri
Ni kauli ya Masalaf wengi akiwemo Al-Hasan Al-Baswriy, An-Nakh’iy, Sa’iyd bin Al-Musayyib, na Abuu Haniyfah na Masahibu zake. Kauli hii imesimuliwa toka kwa ‘Abdillaah bin ‘Amri na Ibn ‘Umar lakini kuna maneno kuhusiana na Isnadi zao.
Imepokelewa toka kwa Yasaar mtumishi wa Ibn ‘Umar akisema: “Ibn ‘Umar aliniona nikiswali baada ya kuchomoza Alfajiri akaniambia: “Ee Yasaar! Hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitutokea nasi tunaswali Swalaah hii akatuambia:
(( ليبلغ شاهدكم غائبكم، لا تصلوا بعد الفجر إلا سجدتين))
((Aliyekuwepo wenu amfikishie asiyekuwepo wenu. Msiswali baada ya Alfajiri isipokuwa rakaa mbili)). [Al-Albaaniy kasema ni Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1264) na At-Tirmidhiy. Angalia “Swahiyhul Jaami’i (5353)].
Ya pili: Si vibaya kuswali Sunnah nyinginezo baada ya Alfajiri kuchomoza
Limesimuliwa hili na Ibn Al-Mundhir toka kwa Al-Hasan Al-Baswriy vile vile aliyesema: “Maalik alikuwa anaona kwamba atafanya hivyo yule ambaye alipitwa na Sunnah ya usiku, nalo limehadithiwa toka kwa Bilaal”.
Ninasema: “Kauli ya kwanza ndiyo yenye nguvu zaidi, nayo inatiliwa nguvu na Hadiyth ya Ibn ‘Umar aliyoipokea toka kwa Hafswah akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa haswali isipokuwa rakaa mbili tu za Alfajiri wakati Alfajiri inapochomoza”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1173), Muslim (723) na wengineo].
Hadiyth hii inaitilia nguvu Hadiyth ya Ibn ‘Umar iliyotangulia – ingawa marejeo yake si kwa Hadiyth ya Hafswah -!! Huvuliwa katika hili kuilipa Swalaah iliyopita na Swalaah yenye sababu kama tulivyoeleza katika mlango wa nyakati zilizokatazwa kuswali. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
Zindushi mbili:
1- Si makruhu kuzungumza baada ya rakaa mbili za Alfajiri
Baadhi ya Maswahaba wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na wengineo wamekwenda kinyume na hili kwa kusema kwamba ni makruhu kuzungumza baada ya kuchomoza Alfajiri mpaka aswali mtu Alfajiri isipokuwa kama ni dhikri au lisilo na budi. Hawa hawana dalili yoyote kuhusu madai haya, bali Hadiyth ya ‘Aaishah iliyotangulia ni dalili inayowapinga pale anaposema: “Nikiwa macho hunisemesha, na kama siko macho, hulala kwa ubavu”.
2- Hakuna du’aa yoyote iliyothibiti toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kumaliza rakaa mbili
Kuna Hadiyth mbili dhwa’iyf mno kuhusiana na hili ambazo hazifai kama ushahidi hata kwa wale wenye kutetea utumiaji wa Hadiyth Dhwa’iyf katika utendaji wa amali bora kutokana na nguvu ya udhwa’iyf wake. [Al’Allaamah Al-Albaaniy (Rahimahul Llaahu) kalitanabahisha hili katika Tamaamul Minnah (ukurasa wa 238-239)]
Sunnah Ya Adhuhuri
Sunnah hii imekuja kwa njia tatu:
Ya kwanza:
Rakaa mbili kabla ya Adhuhuri na rakaa mbili baada yake. Ni kama ilivyo katika Hadiyth ya Ibn ‘Umar aliposema: “Nimehifadhi toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) rakaa kumi: Rakaa mbili kabla ya Adhuhuri na rakaa mbili baada yake, rakaa mbili baada ya Magharibi, rakaa mbili baada ya ‘ishaa nyumbani kwake, na rakaa mbili kabla ya Alfajiri”. [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa karibuni].
Ya pili:
Rakaa nne kabla yake na mbili baada yake
Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa haziachi rakaa nne kabla ya Adhuhuri”. [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa karibuni].
Imepokelewa pia toka kwa ‘Abdullaah bin Shaqiyq akisema: “Nilimuuliza ‘Aaishah kuhusiana na Swalaah ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), naye akasema: “Alikuwa anaswali rakaa nne kabla ya Adhuhuri, na mbili baada yake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (730) na Ahmad (6/30)].
Hadiyth kama hii ya Ummu Habiybah tumeitaja nyuma.
Ya tatu:
Rakaa nne kabla yake na rakaa nne baada yake
Ni kwa Hadiyth ya Ummu Habiybah aliyesema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
(( من صلى أربع ركعات قبل الظهر، وأربعا بعدها حرمه الله على النار))
((Mwenye kuswali rakaa nne kabla ya Adhuhuri, na rakaa nne baada yake, Allaah Atamharamishia moto)). [Hadiyth Swahiyh bituruqihi: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1269), At-Tirmidhiy (428), An-Nasaaiy (3/265), Ibn Maajah (1160), Ahmad (6/326) na Al-Haakim (1/312). Ina njia kadhaa zinazoipa zote uSwahiyh].
· Faida
Lililo bora ni kuswali nne kwa rakaa mbili mbili. Ama Hadiyth ya Abu Ayyuub (Allaah Amridhie) ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( أربع قبل الظهر لا يسلم فيهن، تفتح لهن أبواب السماء))
((Rakaa nne kabla ya Adhuhuri bila tasliym, hufunguliwa kwazo milango ya mbingu)), ni dhwa’iyf haifai. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1270), Ahmad (5/416), ‘Abdu bin Hamiyd (226), At-Twayaalsiy]
· Kuilipa Sunnah Ya Adhuhuri
Kuilipa ya Qabliyyah:
Mwenye kupitwa na Sunnah ya kabla ya Adhuhuri kwa udhuru, basi atailipa baada yake. Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu Anha) akisema kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa kama hakuswali rakaa nne kabla ya Adhuhuri, huziswali baada yake. [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (426)].
Kuilipa ya Ba’adiyyah:
Aidha, mwenye kuondokewa na udhuru wake, atailipa Sunnah ya ba’adiyyah ya Adhuhuri hata kama baada ya Swalaah ya Alasiri. Ni kwa Hadiyth ya Ummu Salamah kwamba alimwona Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiswali rakaa mbili baada ya Alasiri – na hili amelikataza – naye akamuuliza kwa nini anaswali wakati huo? Rasuli akamjibu: ((Ee binti Abuu Umayyah! Unauliza kuhusu rakaa mbili baada ya Alasiri? Hakika walinijia watu kutoka Bani ‘Abdul Qays, wakanishughulisha zikanipita rakaa mbili za baada ya Adhuhuri, nazo ndizo hizo nimeziswali)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1233), Muslim (834) na Ahmad (6/310)].
Sunnah Ya Alasiri
Alasiri haina Sunnah raatib iliyokokotezwa, lakini hata hivyo imesuniwa mtu aswali kabla yake rakaa mbili kutokana na ujumuishi wa kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
(( بين كل أذانين الصلاة))
((Kati ya kila adhana na iqaamah, kuna Swalaah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (624) na Muslim (838)].
Na pia imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((رحم الله امرأ صلى قبل العصر أربعا))
((Allaah Amrehemu mtu aliyeswali kabla ya Alasiri rakaa nne)). [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1271), At-Tirmidhiy (430) na Ahmad (2/117). Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh, lakini kinyume chake ndio kauli ya nguvu. Angalia Al-Miyzaan (6/332) na Al-Kaamil (6/243)].
Hadiyth hii kwa anayeiona ni Swahiyh, inaonyesha kuwa yajuzu kuswali rakaa nne kabla ya Alasiri.
· Tanbihi
Imethibiti kwamba ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu Anha) amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuziacha kamwe rakaa mbili sawasawa akiwa peke yake au akiwa na watu: Rakaa mbili kabla ya Alfajiri, na rakaa mbili baada ya Alasiri”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (592)].
Pia amesema tena: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuacha katu rakaa mbili akiwa nyumbani kwangu”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (591)].
Kuendelea na kudumu huko kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuswali baada ya Alasiri, ni katika mambo mahsusi yanayomhusu yeye peke yake. Hivi ndivyo walivyosema Maulamaa wengi. [Angalia Fat-hul Baariy (2/77)]
Ninasema: “Hili linaweza kutiliwa nguvu na kauli ya ‘Aaishah isemayo: “Aliloondoka nalo, ni kuwa hakuziacha kabisa rakaa mbili mpaka alipokutana na Allaah [yaani rakaa mbili baada ya Alasiri]. Na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiziswali, na hakuwa akiziswali Msikitini kwa kuchelea kuutia uzito umma wake. Alikuwa akipenda kuwafanyia wepesi”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (590)].
Sunnah Ya Magharibi
Kabla yake:
Imesuniwa - kwa anayetaka - kuswali rakaa mbili kabla ya Swalaah ya Magharibi kutokana na dalili zifuatazo:
1- Hadiyth ya ‘Abdullah bin Mughfal Al-Mazniy (Radhwiya Allaahu Anhu) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Swalini kabla ya Magharibi, swalini kabla ya Magharibi, kisha akasema mara ya tatu: Kwa anayetaka)) kuchelea watu kuifanya ni Sunnah raatibah. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1129) na Abu Daawuud (1281)].
2- Hadiyth ya Anas bin Maalik aliyesema: “Mwadhini alikuwa anapoadhini, watu katika Maswahaba wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) husimama na kuziwahi nguzo (za Msikiti) kuswali mpaka anapowatokea Rasuli wa Allaah wakiwa hivyo hivyo. Wanaswali rakaa mbili kabla ya Magharibi, na hakukuwa na chochote kati ya adhana na iqaamah” [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa ikhraaj na Al-Bukhaariy (624) na Muslim (837 na wengineo]
Walikuwa wakiharakia kwenye nguzo ili ziwe ni kama sutrah kwa watu wanaopita mbele yao.
Na hii inaonyesha kwamba imesuniwa kuzifupisha kama katika rakaa mbili za Alfajiri. Na Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
3- Hadiyth ya ‘Abdallah bin Mughfal kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Kati ya kila adhana na iqaamah, kuna Swalaah – mara tatu – kwa anayetaka)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (624), na Muslim (838)].
4- Hadiyth ya ‘Abdallah bin Az-Zubayr akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
(( ما من صلاة مفروضة إلا وبين يديها ركعتان))
((Hakuna Swalaah yoyote ya faradhi isipokuwa kabla yake kuna rakaa mbili)). [Hadiyth Swahiyh Bimaa Qablahu: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Hibaan (2455) na Ad-daaraqutwniy (1/267), na Hadiyth iliyo kabla yake inaitolea ushahidi].
Baada yake:
Kuswali rakaa mbili baada ya Swalaah ya Magharibi kunatiliwa nguvu kama ilivyotangulia katika Hadiyth za Ibn ‘Umar, ‘Aaishah na Ummu Habiybah. Imesuniwa kuziswali rakaa mbili baada ya Magharibi nyumbani kutokana na Hadiyth ya Ibn ‘Umar aliyesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa haswali rakaa mbili baada ya Magharibi, na rakaa mbili baada ya Ijumaa isipokuwa nyumbani kwake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (432), At-Twayaalsiy (1836), na At-Twahaawiy (1/336)].
Imepokelewa toka kwa Mahmoud bin Lubayd akisema: “Rasuli wa Allaah aliwaendea Bani ‘Abdul Ash-Hal, akawaswalisha Magharibi, na alipotoa tasliym alisema: ((Swalini rakaa hizi mbili majumbani mwenu)). [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (5/428) na Ibn Maajah (1165)].
Ama kisomo katika rakaa hizi mbili, imesuniwa kusoma
(( قل يا أيها الكافرون)) na (( قل هو الله أحد))
baada ya Suwrat Al-Faatihah kutokana na Hadiyth ya Ibn Mas-’oud aliyesema: “Sidhibiti kwa idadi nilivyomsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisoma katika rakaa mbili baada ya Magharibi, na rakaa mbili kabla ya Alfajiri
(( قل يا أيها الكافرون)) na (( قل هو الله أحد))
[Hadiyth Hasan kwa nyinginezo mfano wake: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (431) na Ibn Maajah (1166) kwa Sanad Dhwaíyf. Ina Hadiyth mwenza iliyopokelewa na Ibn ‘Umar kwa An-Nasaaiy (992), Ibn Maajah (833) na Ahmad (4533) kwa Sanad ambayo haina tatizo]
Sunnah Ya ‘Íshaa
Kabla yake
Imesuniwa - kwa anayetaka - kuswali rakaa mbili kabla ya ‘Ishaa kutokana na ujumuishi wa kusuniwa kuswali kabla ya Swalaah ya faradhi kama ilivyotangulia.
Baada yake
Kuswali rakaa mbili baada ya Swalaah ya ‘Ishaa kunatiliwa nguvu katika Hadiyth za Ibn ‘Umar, ‘Aaishah na Ummu Habiybah kama ilivyotangulia.
(b) Sunnah zisizo rawaatib
Hizi ni zile ambazo hazihusiani au kufungamana na Swalaah za faradhi, nazo ni:
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
024-Swalaah Ya Witr
Alhidaaya.com [3]
· Taarifu Yake:
Witr kilugha ina maana ya idadi pweke kama moja, tatu na tano. Ni kama neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anaposema:
((Hakika Allaah ni Witr, Anapenda Witr)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (6410) na Muslim kutoka kwa Hadiyth ya Abu Hurayrah].
Na neno lake: ((Mwenye kustanji, afanye kwa Witr)). [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa katika Mlango wa Twahara]
Ama kiistilahi, Swalaah ya Witr, ni Swalaah inayoswaliwa kati ya Swalaah ya ‘Ishaa na kuchomoza Alfajiri, na huhitimishiwa Swalaah ya usiku. Imeitwa hivyo kwa kuwa inaswaliwa kwa idadi ya Witr kama rakaa moja, au tatu, au zaidi, na haiwi kwa idadi shufwa.
Baadhi ya Maulamaa wanasema kwamba Swalaah hii ni sehemu ya Swalaatul Qiyaam na Tahajjudi, na wengine wanasema si Tahajjudi. [Al-Majmu’u cha An-Nawawiy (4/480)]
·
Hukmu Yake:
Maulamaa wana kauli mbili kuhusiana na hukmu yake:
Ya kwanza:
Ni wajibu kwa madhehebu ya Abu Haniyfah. [Al-Hidaaya Ma’a Fat-hil Qadiyr (1/300), Al-Majmu’u (3/514) na Naylul Awtwaar (3/38)]
Nao ni msimamo wake peke yake mpaka Ibn Al-Mundhir akasema: “Simjui yeyote aliyekubaliana na Abu Haniyfah katika hili”. Hoja zake ni:
1- Hadiyth Marfu’u ya Abu Hurayrah:
((من لم يوتر فليس منا))
((Asiyeswali Witr, si katika sisi)). [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (2/443). Kuna Hadiyth kama hii ya Buraydah ambayo ni Dhwa’iyf pia. Angalia Al-Irwaa (417)].
2- Hadiyth Marfu’u ya Abu Ayyuub:
((الوتر حق، فمن أحب أن يوتر بخمس فليفعل، ومن أحب أن يوتر بثلاث فليفعل، ومن أحب أن يوتر بواحدة فليفعل))
((Witr ni haki. Mwenye kupenda kuswali Witr rakaa tano afanye, mwenye kupenda kuswali Witr rakaa tatu afanye, na mwenye kupenda kuswali Witr rakaa moja afanye)). [Hadiyth Swahiyh Mawquuf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1422), An-Nasaaiy (8/238) na Ahmad (5/418). Maimamu wameibadili kuwa Swahiyh badala ya Mawquwf].
3- Hadiyth Marfu’u ya Abu Baswrah:
(( إن الله زادكم صلاة، وهي صلاة الوتر، فصلوها فيما بين العشاء إلى الفجر))
((Hakika Allaah Amewaongezeeni Swalaah, nayo ni Swalaah ya Witr, basi iswalini kati ya ‘Ishaa mpaka Alfajiri)). [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (6/397) na At-Twahaawiy (1/250). Angalia njia zake kwenye Al-Irwaa (423)].
4- Hadiyth Marfu’u ya Ibn ‘Umar:
(( اجعلوا آخر صلاتكم بالليل وترا))
((Ifanyeni Swalaah yenu ya mwisho ya usiku Witr)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (998) na Muslim (751)].
5- Hadiyth Marfu’u ya Abu Sa’iyd:
(( أوتروا قبل أن تصبحوا))
((Swalini Witr kabla hamjapambaukiwa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (754), At-Tirmidhiy (468), An-Nasaaiy (1/247) na Ibn Maajah (1189)]
6- Hadiyth ya ‘Aaishah: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali usiku. Na anapotaka kuswali Witr huniambia: ((Simama uswali Witr ee ‘Aaishah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (512) na Al-Bukhaariy kwa namba hii hii (512)]
Kauli ya pili:
Ni Sunnah iliyokokotezwa. Ni kauli ya Jamhuri ya Maulamaa kati ya Maswahaba, Taabi’iyna, waliowafuatia na maswahibu wa Abu Haniyfah.
Wamezijibu dalili zilizotangulia za Abu Haniyfah kwamba Hadiyth zake nyingi ni Dhwaíyf na hazina mashiko. Ama zilizothibiti kuwa Swahiyh na ambazo amri zake zinaonyesha kuwa ni wajibu, basi amri hizo zinageuzwa kuwa ni Sunnah kutokana na Hadiyth zifuatazo:
1- Hadiyth ya Twalha bin ‘Ubaydullaah kuhusu mtu aliyemuuliza Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), naye Rasuli akamwambia: ((Swalaah tano mchana na usiku)). Akamuuliza: “Je, kuna jingine zaidi ya hilo linalonipasa?” Akamwambia: ((Hapana, isipokuwa kama utaswali Sunnah)). Mtu yule akasema: “Wal Laahi! Sitozidisha zaidi ya haya wala sitopunguza”. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Amefaulu kama atakuwa mkweli)). [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa mara nyingi].
Katika Hadiyth hii moja tu, kuna dalili kadhaa kwamba Witr si wajibu, zitaamuli vizuri.
2- Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomtuma Mu’aadh kwenda Yemen alimwambia: ((Wewe unawaendea watu katika Ahlul Kitaab, basi la kwanza utakalowalingania liwe ni kumwabudu Allaah. Wakimjua Allaah, basi wajulishe kwamba Allaah Amewafaradhia Swalaah tano mchana na usiku, na wanapolifanya..)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1395) na Muslim (19)].
Hadiyth hii ndiyo yenye nguvu zaidi kutolewa dalili, kwa kuwa kutumwa Mu’aadh kwenda Yemen, kulikuwa kabla ya kufariki Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa siku chache. Na lau kama Witr ingelikuwa ni wajibu, au jambo ambalo Allaah Amewaongezea watu katika Swalaah zao, basi Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) angelimwamrisha Mu’aadh awajulishe kwamba Allaah Amewafaradhishia Swalaah sita na si tano.
3- Hadiyth ya Abu Hurayrah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( الصلوات الخمس، والجمعة إلى الجمعة، كفارات لما بينهن ما لم تغش الكبائر))
((Swalaah tano, na Ijumaa hadi Ijumaa, ni kafara ya yaliyoko kati yake madhali hayakufanywa madhambi makubwa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (233), At-Tirmidhiy (214) na Ibn Maajah (1086)],
Hapa hakuitaja Witr katika Swalaah zilizotajwa ambazo ni wajibu.
4- Hadiyth ya Ibn ‘Umar kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali Witr juu ya mnyama. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (999), Muslim (700) na wengineo].
Na lau kama Witr ingelikuwa ni wajibu, basi isingelijuzu kuiswali juu ya mnyama kama ilivyotangulia.
5- Hadiyth ya Ibn Muhayriyz toka kwa Al-Mukhaddajiy aliyesema: “Mtu mmoja alimuuliza Abu Muhammad (ambaye ni katika Ma-Answaar) kuhusu Witr akasema: “Witr ni wajibu kama wajibu wa Swalaah”. Akamwendea ‘Ibaadah bin Swaamit akamwelezea hilo, naye akasema: “Ameongopa Abu Muhammad, nimemsikia Rasuli wa Allaah akisema: ((Swalaah tano Allaah Amezifaradhisha kwa Waja Wake)). [Ni Dhwa’iyf kwa kauli yenye nguvu. Imeshafanyiwa “ikhraaj” katika mlango wa Hukmu ya mwenye kuacha Qur-aan. Angalia takhriyj yake kiuchambuzi katika kitabu cha Ta’adhiym Qadrus Swalaahat kwa takhriyj yangu].
6- Hadiyth ya Jaabir aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alituswalisha katika mwezi wa Ramadhwaan rakaa nane, na akaswali Witr. Ulipokuja usiku wa pili, tulikusanyika Msikitini tukitaraji kwamba atatoka ili atuswalishe. Tukakaa humo mpaka asubuhi ikaingia tukasema: Ee Rasuli wa Allaah! Tulitaraji utatoka utuswalishe. Akasema: ((Nilichukia – au nilihofia – Witr ifaradhishwe kwenu)). [Ni Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Khuzaymah (1070), Abu Ya’alaa (1802) na Ibn Hibaan (2409)].
· Faida
Sheikh wa Uislamu Ibn Taymiyah (Rahimahul Laahu) amekhitari kwamba Witr ni wajibu kwa mtu ambaye ni mazoea yake kuswali usiku. [Al-Ikhtiyaarat uk. 64]
Ninasema: “Huenda kigezo chake ni kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Ifanyeni Swalaah yenu ya mwisho ya usiku Witr)).
· Wakati Wa Witr
Maulamaa wote wamekubaliana kwamba muda wa kati ya Swalaah ya ‘Ishaa mpaka kuchomoza Alfajiri ni wakati wa Swalaah ya Witr. Kisha wakakhitalifiana kuhusu kujuzu kuswaliwa kwake baada ya Swalaah ya Alfajiri kwa kauli tano. Zilizo mashuhuri zaidi ni kauli mbili: [Al-Awsatw, At-Tamhiyd (2/349 – Fat-hul Maalik), Bidaayatul Mujtahid (1/294) na Al-Majmu’u (3/518)]
Ya kwanza:
Haijuzu baada ya kuchomoza Alfajiri. Hii ni kauli ya Abu Yusuf, Muhammad bin Al-Hasan, Maswahibu wawili wa Abu Haniyfah, Sufyaan Ath-Thawriy, Is-Haaq, ‘Atwaa, An-Nakh’iy na Sa’iyd bin Jubayr. Kauli hii pia imehadithiwa toka kwa Ibn ‘Umar, na hoja yao ni:
1- Hadiyth ya Khaarijah bin Hudhaafah – iliyotangulia karibuni – isemayo: ((Basi iswalini muda wa kati ya ‘Ishaa mpaka kuchomoza Alfajiri)). [Al-Albaaniy kasema ni Hadiyth Swahiyh. Tumeshaitaja na angalia Al-Irwaa (423)].
2-Hadiyth Marfu’u ya Abu Sa’iyd isemayo: ((Swalini Witr kabla hamjapambaukiwa)). [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa hivi karibuni.]
Na katika tamshi lake: ((Mwenye kuingiliwa na Alfajiri na hakuwahi kuswali Witr, basi hana Witr tena)). [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Khuzaymah (1092), Ibn Hibaan (2409), Al-Haakim (1/301) na Al-Bayhaqiy (2/478)].
3- Hadiyth ya Ibn ‘Umar kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Harakisheni kuswali Witr kabla ya Alfajiri)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (750), Abu Daawuud (1436), At-Tirmidhiy (467) na Ahmad (2/37)].
4- Hadiyth ya Ibn ‘Umar kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Swalaah ya usiku ni rakaa mbili mbili. Akichelea mtu kuingia Alfajiri, ataswali rakaa moja iwe ni Witr kwa zile alizoziswali)). [Hadiyth Swahiyh: Imetangulia hivi karibuni].
5- Imepokelewa na Ibn ‘Umar akisema: “Alfajiri ikiingia, basi Swalaah ya usiku na Witr zinakuwa hazipo tena, kwani Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema: ((Swalini Witr kabla ya Alfajiri)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (469), Ibn Khuzaymah (2/148), Al-Haakim (1/302) na Al-Bayhaqiy (2/478)].
Ya pili:
Inajuzu baada ya kuchomoza Alfajiri madhali mtu bado hajaswali Alfajiri. Ni kauli ya Maalik, Ash-Shaafi’iy, Ahmad na Abu Thawr. Wametoa dalili kwa athar zilizopokelewa toka kwa Maswahaba kwamba walikuwa wakiswali Witr baada ya Alfajiri wakiwemo akina Ibn Mas-’oud, Ibn ‘Abbaas, ‘Ubaadah bin As-Swaamit, Abud Dardaa, Hudhayfah na ‘Aaishah. Na haikuhadhithiwa kinyume na hivyo kutoka kwa Maswahaba wengine zaidi yao.
· Lenye nguvu
Kauli ya kwanza inaonyesha kuwa ni madhubuti zaidi kutokana na uimara wa dalili zake. Ama athar toka kwa Maswahaba, inavyoonyesha kama anavyosema Ibn Rushd ni kuwa athar hizi haziendani kinyume na athar zilizotangulia, bali kujuzisha kwao hilo ni katika mlango wa kulipa, na si mlango wa kutekeleza. Lakini kauli yao itakuwa ni kinyume cha athar lau kama watazifanya Swalaah zao baada ya Alfajiri kuwa ndio wakati wake wa kuziswali. Liangalie hilo kwa makini. Kisha inatakikana itaamuliwe sifa ya Sunnah yao katika hilo vipi walitenda!!.
· Wakati Wake Mwafaka Zaidi
Tumeshasema kwamba inajuzu kuswali Witr kuanzia baada ya Swalaah ya ‘Ishaa mpaka kuchomoza Alfajiri, lakini wakati bora zaidi ni katika theluthi ya mwisho ya usiku.
Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameswali Witr katika kila sehemu ya usiku; kuanzia mwanzo wake, katikati yake na mwisho wake, akamalizia Witr yake mwisho wa usiku”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (996) na Muslim (745).].
Na imesuniwa – kwa makubaliano ya wote – mtu aifanye Witr kuwa ndiyo Sunnah yake ya mwisho anayoiswali usiku kutokana na Hadiyth ya Ibn ‘Umar kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ifanyeni Swalaah yenu ya mwisho ya usiku Witr)). [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa nyuma kidogo].
Lakini hii ni pale mtu atakapokuwa na uhakika wa kuweza kuamka mwisho wa usiku. Kama ni hivyo, imesuniwa aicheleweshe Witr yake mpaka mwisho wa usiku. Na kama atachelea kwamba hatoweza kuamka kwa ajili ya Witr mwisho wa usiku, basi imesuniwa hapo aswali Witr kabla hajalala. Na hii ni kwa Hadiyth ya Jaabir bin ‘Abdullaah (Radhwiya Allaahu Anhu) aliyesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Mwenye kuchelea kati yenu kwamba hatoweza kuamka mwisho wa usiku, basi aswali Witr mwanzoni mwake kisha alale. Na mwenye matumaini kati yenu ya kuamka mwishoni mwa usiku, basi aswali Witr mwishoni mwake, kwani Swalaah ya mwishoni mwa usiku huhudhuriwa, na hilo ni bora zaidi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (755), At-Tirmidhiy (455) na Ibn Maajah (1187)].
Imepokelewa toka kwa Abu Qataadah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuuliza Abuu Bakr: ((Wakati gani unaswali Witr?)) Akajibu: “Ninaswali Witr kisha nalala”. Kisha alimuuliza ‘Umar: ((Wakati gani unaswali Witr?)). Akajibu: “Ninalala kisha naswali Witr”. Kisha akamwambia Abu Bakr: ((Umefanya kwa umadhubuti, au kwa kujiamini)) na ‘Umar akamwambia: ((Umefanya kwa nguvu ya kujiamini)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1421), Ibn Maajah (1202) na Ibn Khuzaymah (1084)].
· Je, Inajuzu Kuswali Sunnah Nyingine Baada Ya Kuswali Witr? Je, Witr Inaweza Kuswaliwa Zaidi Ya Mara Moja?
Mwenye kuswali Witr, kisha baada ya hapo akapata utashi wa kuswali Sunnah nyingine, basi Maulamaa wana kauli mbili juu ya suala hili: [Fat-hul Qadiyr (1/312), Az-Zarqaaniy (1/285), Al-Majmu’u (3/521), Kash-Shaaf Al-Qinaa (1/427) na Bidaayatul Mujtahid (1/297)]
Ya kwanza:
Inajuzu, na mtu ana khiyari ya kuswali Sunnah azitakazo, lakini asiswali tena Witr. Ni msimamo wa Maulamaa wengi wakiwemo Hanafiy, Maalik, Hanbali na mashuhuri kwa Ash-Shaafi’iy. Pia ni kauli ya akina An-Nakh’iy, Al-Awzaa’iy na ‘Alqamah. Nayo imehadithiwa toka kwa Abu Bakr, Sa’ad, ‘Ammaar, Ibn ‘Abbaas na ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu Anhaa).
Dalili ya kujuzisha hili ni haya yafuatayo:
1- Hadiyth ya ‘Aaishah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitoa tasliym kwa sauti ya wao kusikia, kisha huswali rakaa mbili baada ya kutoa tasliym akiwa amekaa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (749)].
2- Hadiyth ya Ummu Salamah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali rakaa mbili baada ya Witr akiwa amekaa. [Isnadi yake ni laini: At-Tirmidhiy (471) na Ibn Maajah (1195). Ipo Hadiyth mwenza katika As-Swahiyh].
3- Hadiyth iliyotangulia ya Jaabir kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: ((Mwenye kuchelea kati yenu kwamba hatoweza kuamka mwisho wa usiku, basi aswali Witr mwanzoni mwake kisha alale )). [Hadiyth Swahiyh: Tumeieleza karibuni]
Inafahamika kutokana na Hadiyth hii kwamba anapoamka – akiwa ashaswali Witr kabla ya kulala – basi anaweza kuswali.
Ama zuio la kuswali Witr zaidi ya mara moja, ni kutokana na Hadiyth ya Twaliq bin ‘Aliyy kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna Witr mbili usiku mmoja)). [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (468), Abu Daawuud (1439), An-Nasaaiy (3/229) na wengineo].
Ya pili:
Haijuzu kuswali Sunnah nyingine baada ya Witr ila kama ataitengua Witr yake, aswali tena, kisha amalizie kwa Witr. Maana ya kuitengua ni kuianza Sunnah yake kwa rakaa moja azifanye mbili kujumlisha na ile moja ya Witr yake, kisha aswali idadi ya shufwa kiasi apendacho, kisha amalizie kwa Witr. Na hii ndiyo kauli ya mwisho ya Ash-Shaafi’iy, nayo imehadithiwa toka kwa ‘Uthmaan, ‘Aliyy, Usaamah, Ibn ‘Umar, Ibn Mas-’oud na Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu Anhum). Hoja yao ni neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Ifanyeni Swalaah yenu ya mwisho ya usiku Witr)). [Hadiyth Swahiyh: Tumeieleza karibuni].
Kauli Yenye Nguvu:
Ni ya kwanza kutokana na kuthibiti kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali Sunnah baada ya kuswali Witr. Kitendo hicho kimetutaarifu kwamba inajuzu kufanya hivyo. Kuitengua Witr kwa picha tuliyoielezea hakuna nguvu kwa sababu mbili:
1- Witr iliyoswaliwa mwanzo inahesabiwa kuwa ishakuwa sahihi, hivyo hakuna maana kuitengua baada ya kuiswali, na haiwezekani ikageuka kuwa ni Sunnah nyingine kwa kuzifanya rakaa shufwa.
2- Sunnah ya rakaa moja haijulikani katika sharia, na Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
· Idadi Ya Rakaa Za Witr Na Namna Yake
Inajuzu kuiswali Witr rakaa moja, au tatu, au tano, au saba, au tisa.
1- Kwa rakaa moja:
Inajuzu kwa mujibu wa kauli ya Jamhuri ya Maulamaa kwa kuwa rakaa moja inatosheleza makusudio, na kwa kauli ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Swalaah ya usiku ni rakaa mbili mbili. Akichelea mtu kuingia Alfajiri, ataswali rakaa moja iwe ni Witr kwa zile alizoziswali)). [Hadiyth Swahiyh: Tumeieleza karibuni].
Na kwa Hadiyth ya Ibn ‘Umar kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Witr ni rakaa moja ya mwishoni mwa usiku)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (752) na wengineo].
Na ‘Aaishah anasema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaswali usiku rakaa kumi na moja, huifanya moja kati yake Witr”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (736), Abu Daawuud (1335), At-Tirmidhiy (440) An-Nasaaiy (3/234) na Ahmad (6/35)].
Ama Abu Haniyfah, yeye anasema kuwa Witr haiwi ila kwa rakaa tatu kutokana na Hadiyth isemayo:
(( المغرب وتر النهار))
((Maghrib ni Witr ya mchana)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (2/30,41), Ibn Abu Shaybah (2/81) na ‘Abdul Raaziq (4675) kutoka kwa Hadiyth Marfu’u ya Ibn ‘Umar. Maalik ameifanyia “ikhraaj” ikiwa Marfu’u (276). Hakuna madhara kuifanya Mawquwf, kwani Maalik huzifanya Hadiyh Marfu’u kuwa Mawquwf. Hadiyth hii ina wenza wake toka kwa ‘Aaishah na Ibn Mas-’oud]
Na kwa kuwa Maghrib – yenye rakaa tatu - imefananishwa na Witr ya Swalaah ya usiku, ni lazima Witr ya usiku iwe rakaa tatu!!
Ninasema: “Swalaah ya Magharibi - yenye rakaa tatu – kuwa Witr, hakuzuii nyinginezo kuwa Witr pia. Na kama Magharibi ni Witr ya mchana, basi dalili zilizotangulia zinatuarifu kwamba rakaa moja ni Witr ya usiku, na hili liko bayana.
2- Kwa rakaa tatu:
Nayo inajuzu kwa njia mbili, na zote zinafaa kisharia. Njia hizo ni:
Ya kwanza:
Aswali rakaa mbili kisha atoe tasliym, halafu aswali rakaa ya tatu peke yake.
Imepokelewa kwamba Ibn ‘Umar alikuwa akitoa tasliym kati ya rakaa mbili na Witr mpaka aagize baadhi ya mahitaji yake. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (991) toka kwa Maalik (1/125)].
Imepokelewa toka kwake kwa njia Marfu’u akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitenganisha shaf-’i na Witr kwa tasliym anayoisema kwa sauti tukaisikia”. [Swahiyh Bituruqihi: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (2/76), At-Twahaawiy (1/278) na Ibn Hibaan (2433-2435). Al-Haafidh ameitia nguvu katika Al-Fat-h (2/482)].
Linatolewa ushahidi hili na Hadiyth ya ‘Aaishah isemayo: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anasoma katika rakaa mbili ambazo baada yake huswali rakaa moja (Sabbihisma Rabbika Al-A’alaa) na (Qul yaa ayyuhal kaafiruwna), na katika rakaa ya Witr anasoma (Qul Huwa Allaah) na (Qul a’uwdhu birabbil Falaq) na (Qul a’uwdhu birabbin Naas). [Dhwa’iyf kwa nyongeza hii: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Twahaawiy (1/285), Al-Haakim (1/305), Ad-daaraqutwniy (2/35) na Ibn Hibaan (3432). Hadiyth hii imekuwa Swahiyh bila kutaja “Mu’awwadhatayn” toka Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas na Ubayya bin Ka’ab kama itakavyokuja. Angalia At-Talkhiysw (533)]
Katika Swahiyh Ibn Hibaan kuna mlango maalumu usemao: (Kutaja habari zinazoonyesha kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitenganisha tasliym kati ya rakaa mbili na rakaa ya tatu).
Ya pili:
Aswali rakaa tatu kwa tashah-hudi moja
Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwa katika Ramadhwaan au mwezi mwingineo wowote akizidisha zaidi ya rakaa 11. Anaswali nne, basi usiulize uzuri wake na urefu wake, kisha anaswali nne, basi usiulize uzuri wake na urefu wake, kisha anaswali tatu….”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1147), Muslim (738) na wengineo].
Pia ‘Aaishah amesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali Witr rakaa tatu, hakai isipokuwa katika rakaa ya mwisho”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Maalik (466), An-Nasaaiy (3/234), At-Twahaawiy (1/280), Al-Haakim (1/304) na Al-Bayhaqiy (3/31)].
· Tanbihi
Hairuhusiwi kuswali rakaa tatu kwa tashah-hudi mbili na tasliym moja kama ilivyo katika Swalaah ya Magharibi. Ni kwa Hadiyth ya Abu Hurayrah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Msiswali Witr ya rakaa tatu, bali swalini Witr ya rakaa tano au saba, wala msiifananishe na Swalaah ya Magharibi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Haakim (1/304), Al-Bayhaqiy (3/31), Ibn Hibaan (2429), na Ad-daaraqutwniy (2/24). Al-Haafidh katika At-Talkhiys anasema kuwa watu wa Isnadi yake wote wanaaminika. Hakuna dhara kwa waliosema kuwa ni Mawquwf].
· Sura Zinazosomwa Katika Rakaa Tatu
Anaposwali mtu rakaa tatu, basi imesuniwa ayasome yaliyomo katika Hadiyth hizi mbili:
- Ya Ibn ‘Abbaas asemaye: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema alikuwa akisoma katika Witr (Sabbihisma Rabbika Al-A’alaa) na (Qul yaa ayyuhal kaafiruwn) na (Qul Huwa Allaahu Ahad) katika rakaa rakaa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (461) na An-Nasaaiy (3/236)]. Yaani katika kila rakaa Suwrah moja kati ya hizo tatu.
- Ya Ubayya bin Ka’ab aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisoma katika Witr (Sabbihisma Rabbika Al-A’alaa) na (Qul yaa ayyuhal kaafiruwn) na (Qul Huwa Allaahu Ahad), na anapotoa tasliym husema: (Subhaana Al-Maliki Al Qudduws) mara tatu. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1423), An-Nasaaiy (3/244) na Ibn Maajah (1171). Kuna makhitilafiano ndani yake yasiyo na madhara yoyote kwa Tawfiyq ya Allaah].
Mahanbali wamezishikilia Hadiyth hizi mbili. Maalik na Ash-Shaafi’iy wanaona ni mustahabu aongeze mtu “Mu’awwadhatayn” katika rakaa ya tatu kwa mujibu wa Hadiyth ya ‘Aaishah iliyotangulia, lakini isiwe ni ada yake. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
3- Kwa rakaa tano:
Inajuzu, na imesuniwa kama ataswali, asikae kwa tashah-hudi ila katika rakaa ya tano. Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah aliyesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali usiku rakaa 13, kati ya hizo akiswali Witr tano, na hakai isipokuwa katika rakaa ya mwisho”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (737), Abu Daawuud (1324) na At-Tirmidhiy (457)].
4- Kwa rakaa saba au tisa:
Inajuzu. Ikiwa ataswali kwa idadi hizi, imesuniwa aandamishe rakaa na asikae kwa tashah-hudi isipokuwa katika rakaa ya kabla ya mwisho – na asitoe tasliym – halafu asimame kwa rakaa ya mwisho, akae tashah-hudi halafu atoe tasliym.
Bi ‘Aaishah akiizungumzia namna ya Swalaah ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema: “Tulikuwa tukimtayarishia Rasuli mswaki wake, kisha Allaah Humwamsha wakati wowote Apendapo kumwamsha usiku. Huamka akapiga mswaki na kutawadha, kisha huswali rakaa tisa, na hakai katika rakaa hizo isipokuwa katika rakaa ya nane. Hapo humdhukuru Allaah, akamhimidi na kumwomba. Halafu hunyanyuka bila ya kutoa tasliym kwa rakaa ya tisa. Kisha hukaa akamdhukuru Allaah, akamhimidi na kumwomba. Halafu hutoa tasliym ya sisi kuisikia. Kisha huswali rakaa mbili baada ya kutoa tasliym nailhali amekaa. Hizo ndizo rakaa kumi na moja ee mwanangu. Na Rasuli wa Allaah alipowanda na kupata mwili, alikuwa akiswali Witr rakaa saba, na akafanya katika rakaa mbili kama alivyokuwa akifanya mwanzo, na hizo ni tisa ee mwanangu”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (746), Abu Daawuud (1328) na An-Nasaaiy (3/199)].
· Je, Ni Sharti Swalaah Ya Witr Itanguliwe Na Swalaah Ya (Shaf-’i)?
Kwa maana kwamba, je mtu anaweza kuswali rakaa moja au tatu za Witr na zaidi ya hapo bila kuswali kabla yake chochote? Maalik na Ash-Shaafi’iy – wanaona kwamba Witr kwa rakaa moja haiwi ila baada ya kutanguliwa na shaf-’i. [Al-Muntaqaa cha Al Baajiy (1/223) na vitabu rejea husika]
Wanasema kwamba asili ya hilo ni ni Hadiyh isemayo: ((Swalaah ya usiku ni rakaa mbili mbili. Akichelea mtu kuingia Alfajiri, ataswali rakaa moja iwe ni Witr kwa zile alizoziswali)).
Lakini Mashafii na Mahanbali wanaona kwamba inajuzu kuswali Witr kwa rakaa moja tu ingawa hilo litakuwa ni kinyume cha ubora, na uchache wa ukamilifu ni rakaa tatu. [Haashiyat Al-Qalyouniy (1/212), Kash-Shaaf Al-Qinaa (1/416) na Al-Mughniy (2/150)]
Ninasema: “Huenda dalili za kujuzisha ni hizi zifuatazo: [Bidaayatul Mujtahid cha Ibn Rushd (1/293) chapa ya Al-Kutub Al-‘Ilmiyyah]
1- Hadiyth ya ‘Aaishah asemaye: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaswali nami nimelala na kumkinga juu ya tandiko lake, na anapotaka kuswali Witr, huniamsha nami nikaswali Witr”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (512) na Muslim (512)].
Hadiyth hii inaonyesha kwamba Bi ‘Aaishah alikuwa akiswali Witr bila ya kutanguliza Shaf-’i.
2- Hadiyth ya ‘Aaishah tuliyoitaja karibuni kuhusiana na kuswali kwake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Witr rakaa saba na tisa, kisha kuswali kwake rakaa mbili akiwa amekaa. Tunafahamu katika Hadiyth hiyo kwamba Witr ni yenye kuitangulia Shaf-’i, na pia tunapata humo hoja kwamba si sharti Witr itanguliwe na Shaf-’i. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
· Qunuwt Katika Witr
Qunuwt ina maana mbalimbali. Kati ya maana hizo ni kusimama, kunyamaza, kutoacha ‘ibaadah, du’aa, tasbiyh na khushui. Ama kiistilahi, ni jina la du’aa katika Swalaah katika mahala mahsusi na katika kisimamo. [Al-Futuwhaat Ar Rabbaaniya ‘Alal Adhkaar An Nawawiyyah (2/286) na Baswaair Dhawiyt Tamyiyz (4/298)]
Qunuwt katika Swalaah ya Witr inaruhusika kisharia kwa mujibu wa Jamhuri ya Maulamaa kinyume na Maalik. [Ni mashuhuri kwamba yeye anasema ni karaha kufanya qunuwt katika Witr. Riwaya iliyopokelewa toka kwake inasema kwamba Qunuwt hufanywa katika nusu ya mwisho ya Ramadhwaan (Al-Kaafiy) cha Ibn ‘Abdul Barri (uk.74), Al-Qawaaniyn (uk.66), Al-Mughniy (2/580) na Al-Majmu’u (4/24)]
Lakini wamekhitalifiana kama qunuwt hiyo ni wajibu au Sunnah. [Abu Haniyfah anasema kwamba ni wajibu kinyume na Maswahibu wawili na Jamhuri. Al-Badaai-’i (1/273) na Al-Bahr Ar Raaiq (2/43)]
Au kama inakuwa katika Swalaah zote za Sunnah au katika Ramadhwaan tu. [Kwa Mahanafi ni mwaka wote, na kwa Mashaafi’i ni nusu ya mwisho ya Ramadhwaan hasa, nao wanaona kuwa inakuwa vyema kuifanya katika mwezi wote wa Ramadhwaan. Ama kwa Mahanbali, ni katika mwaka wote. Al-Badaai-’i (1/273), Al-Majmu’u (4/15), Al-Mughniy (2/58) na Al-Muhallaa (4/145)]
Au kama inakuwa kabla ya kurukuu au baada yake. [Kwa Mahanafi, ni kabla ya kurukuu, na kwa Mashaafi’i na Mahanbali ni baada ya kunyanyuka toka kwenye rukuu [Vitabu rejea vilivyotangulia]
Au ni yepi yaliyosuniwa aombe kwayo katika qunuwt hiyo. [Kwa Mahanafi na Mashaafi’i: Du’aa ni kwa (Allaahumma Ihdinaa fiyman Hadayta….), na kwa Mahanbali ni (Allaahumma innaa nasta’iynuka wa nastahdiyka…)]
Lililo sahihi ni haya yafuatayo:
1- Qunuwt imesuniwa baadhi ya nyakati katika wakati wowote wa mwaka
Asili ya hili ni Hadiyth ya Al-Hasan bin ‘Aliyy (Radhwiya Allaahu Anhu) aliposema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alinifundisha maneno ya mimi kuyasema katika Witr:
((Allaahumma Ihdiniy fiyman Hadayta, wa ‘Aafiniy fiyman ‘Aafayta, wa Tawallaniy fiyman Tawallayta, wa Baariyk liy fiymaa A’atwayta, wa Qiniy sharra maa Qadhwayta, fainnaka Taqdhwiy walaa yuqdhwaa ‘alayka, wa innahuu laa yadhillu man Waalayta, Tabaarakta Rabbanaa wa Ta’alayta)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1425), At-Tirmidhiy (464), An-Nasaaiy (3/248) na Ibn Maajah (1178). Angalia Al-Irwaa (429)].
Na imepokelewa toka kwa “Ubayya bin Ka’ab akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali Witr na kusoma Qunuwt kabla ya rukuu”. [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1425), At-Tirmidhiy (464), An-Nasaaiy (3/248) na Ibn Maajah (1178). Angalia Al-Irwaa (426)].
Nasi tumesema: “Qunuwt imesuniwa katika Witr “baadhi ya nyakati”, kwa kuwa Maswahaba waliohadithia kuhusu Witr, hawakuelezea kusomwa qunuwt ndani yake. Na lau kama Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) angelikuwa anaifanya siku zote, basi wote wangelinukuu hilo kutoka kwake. Tunakubali kwamba ‘Ubayya bin Ka’ab peke yake amehadithia kuhusu hilo likifanywa na Rasuli, na hii inaonyesha kwamba Rasuli alikuwa akilifanya baadhi ya nyakati, na kwamba hilo si wajibu. Na hii ndio kauli ya Jamhuri ya Maulamaa kinyume na Abu Haniyfah”. [Al-Albaaniy amebainisha na kufafanua mfano wa haya katika Swifatus Swalaat (uk. 179)]
2- Qunuwt katika Witr ni bora zaidi ifanywe kabla ya kurukuu na baada ya kisomo
Ni kwa Hadiyth iliyotangulia ya Ubayya bin Ka’ab isemayo: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali Witr na kusoma Qunuwt kabla ya rukuu”.
Imepokelewa toka kwa ‘Aaswim akisema: “Nilimuuliza Anas bin Maalik kuhusu qunuwt akasema: “Qunuwt ilikuwepo”. Nikamwambia: “Je, ni kabla ya kurukuu au baada ya kurukuu?”. Akasema: “Ni kabla”. Nikamwambia: “Fulani kanieleza kwamba wewe umesema ni baada ya kurukuu”. Akasema: “Ni mwongo. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiifanya baada ya rukuu mwezi mzima. Alikuwa amepeleka watu 70 wanaosemekana kuwa ni wasomaji wakubwa mahiri kwa washirikina. Washirikna hawa walikuwa na mkataba na Rasuli wa Allaah, na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawasomea qunuwt ya kuwaombea laana mwezi mzima”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1002) na Muslim (677)].
Al-Haafidh katika Al-Fat-h (2/569) amesema: “Mjumuiko wa yaliyokuja toka kwa Anas kuhusiana na hayo ni kuwa qunuwt ni kwa ajili ya haja [yaani kwa janga] baada ya rukuu, na hilo halina mvutano wowote. Ama ikiwa si kwa haja, basi lililo sahihi ni kuwa hufanywa kabla ya kurukuu. Maswahaba walitofautiana katika utendaji wa hilo, na kiilivyo hayo ni makhitilafiano yanayoruhusika”.
Imepokelewa toka kwa ‘Abdur Rahmaan bin Al-Aswad toka kwa baba yake akisema: “ ‘Abdullaah – yaani Ibn Mas-’oud – alikuwa hafanyi qunuwt kwa lolote katika Swalaah, isipokuwa katika Witr kabla ya rakaa”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Twabaraaniy katika Al-Kabiyr (9/238). Angalia Al-Irwaa (2/166)].
3- Yaliyosuniwa kuombwa ndani ya qunuwt
Katika qunuwt ya Witr, imesuniwa kuomba kwa yale ambayo Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimfundisha Al-Hasan bin ‘Aliy: ((Allaahumma Ihdiniy fiyman Hadayta…)) mpaka mwisho kama ilivyotangulia.
Inajuzu kumswalia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika qunuwt kwa kuthibiti hilo toka kwa Maswahaba. Limethibiti hilo wakati Ubayya bin Ka’ab alipowaswalisha watu katika Qiyaam ya Ramadhwaan, na pia wakati Abu Haliymah Mu’aadh Al-Answariy alipowaswalisha watu, naye ni mmoja wa wale ambao ‘Umar aliwateua kuswalisha Tarawehe. [Swifatu Swalaatin Nabiyy (uk.180)]
4- Si katika Sunnah kurefusha du’aa ya qunuwt
Yaliyothibiti toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika kumfundisha Al-Hasan du’aa ya qunuwt katika Witr, ni kuwa du’aa yenyewe ni nyepesi na haina urefu.
5- Je, inajuzu kughani kwa du’aa ya qunuwt?
Haijanukuliwa toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wala toka kwa Swahaba yake yoyote – kwa ninavyojua – kwamba alighani kwa du’aa, si katika qunuwt wala katika du’aa nyingine yoyote, nami nachelea kuwa ni uzushi hili wanaloliona Maimamu wengi kuwa ni jambo zuri hivi leo!!
Ibn Al-Hammaam amesema: “Sioni kuiachilia na kuvuta tuni katika du’aa – kama wanavyofanya baadhi ya wasomaji hivi leo – kunafanywa na yule aliyefahamu maana hasa ya du’aa na kuomba. Hilo si jinginelo bali ni aina ya mchezo. Tukichukulia uhalisia wa mambo kwa mtu mwenye ombi lake kwa Mfalme, ikiwa atawasilisha ombi lake kwa kuvuta tuni, kunyanyua sauti, kushusha, kukurubisha na kukariri kariri kama wimbo, basi hilo litazingatiwa moja kwa moja kama ni masikhara na mchezo. Manzili ya kuomba, inahitaji unyenyekevu na si kughani.” [Fat-hul Qadiyr (1/370, 371)]
6-Imesuniwa kunyanyua mikono miwili katika qunuwt
Imepokelewa toka kwa Anas kuhusiana na kisa cha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwaapiza waliowaua wasomaji wake akisema: “Hakika nilimwona Rasuli wa Allaah kila anaposwali Alfajiri, hunyanyua mikono yake miwili akiwaapizia”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (3/137) na Al-Bayhaqiy (2/211)].
Pia imepokelewa toka kwa Abu Raafi’i akisema: “Niliswali nyuma ya ‘Umar bin Al-Khattwaab, akasoma qunuwt baada ya kurukuu, akanyanyua mikono yake na akasoma du’aa kwa sauti”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (3/137) na Al-Bayhaqiy (2/211)].
Abu Hurayrah alikuwa akinyanyua mikono yake katika qunuwt ya mwezi wa Ramadhwaan. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Nasr katika Kitabu cha Qiyaamul Layl ukurasa wa 138]
7- Hakuna usharia wa kupangusa uso au kifua kwa mikono miwili baada ya qunuwt
Hii ni kwa vile hakuna dalili yoyote inayothibitisha hilo. Al-Bayhaqiy anasema katika Sunanih (2/212): “Ama kupangusa mikono miwili usoni wakati wa kumaliza du’aa, sikulihifadhi hili kutoka kwa yeyote katika Masalaf katika du’aa ya qunuwt”.
Ninasema: “Si sahihi vile vile Hadiyth inayozungumzia kupangusa uso baada ya du’aa nje ya Swalaah. Sheikh wa Uislamu (22/519) anasema: “Ama kupangusa kwake uso wake kwa mikono yake, hilo halikufanywa na Rasuli. Kuna Hadiyth moja au Hadiyth mbili zinazogusia hilo lakini hazifai kama dalili. Allaahu Ndiye Mjuzi Zaidi”.
· Kufanya Tasbiyh Na Kuomba Du’aa Baada Ya Witr
Imesuniwa baada ya kutoa tasliym ya Witr, kufanya tasbiyh kutokana na Hadiyth ya Ubayya bin Ka’ab aliyesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisoma katika Witr (Sabbihisma Rabbika Al-A’alaa) na (Qul yaa ayyuhal kaafiruwn) na (Qul Huwa Allaahu Ahad). Anapotoa tasliym husema: (Subhaana Al-Malik Al-Qudduuws) mara tatu. [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa karibuni].
Imepokelewa pia toka kwa ‘Aliy kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisema mwishoni mwa Witr yake:
(( اللهم إني أعوذ برضاك من سخطك، وبمعافاتك من عقوبتك وأعوذ بك منك، لا أحصي ثناء عليك، أنت كما أثنيت على نفسك))
((Allaahumma inniy a’uwdhubika min sakhatwika, wa bimu’aafaatika min ‘uquwbatika wa a’uwdhubika minka, laa uhswiy thanaan ‘alayka, Anta kamaa Athnayta ‘alaa Nafsika)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (1427), At-Tirmidhiy (3566), An-Nasaaiy (1/252) na Ibn Maajah (1179)].
· Kuilipa Witr
Mtu akilala akapitwa na Witr au akasahau kuswali, basi ataiswali anapoamka au anapoikumbuka wakati wowote ule. Hii ni kwa Hadiyth ya Abu Sa’iyd Al-Khudriyy aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Aliyelala akapitwa na Witr au akaisahau, basi aiswali anapopambazukiwa au anapokumbuka)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (465), Abu Daawuud (1431), Ibn Maajah (1188) na Ahmad. Angalia Al-Irwaa (2/153)].
Na kutokana na ujumuishi wa kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Mwenye kulala akapitwa na Swalaah, au akaisahau, basi aiswali anapokumbuka)).
Ujumuishi huu unakusanya Swalaah zote za faradhi na Sunnah. Kwa Swalaah za faradhi ni amri ya faradhi, na kwa Swalaah za Sunnah ni amri ya Sunnah. Aidha, atailipa Witr kama ilimpita kutokana na sababu yoyote kama ugonjwa na mfano wake.
Ninasema: “Anayefanya makusudi kuiwacha Witr bila ya udhuru wowote mpaka ikaingia Alfajiri, basi haruhusiwi kuilipa kwa mujibu wa uhakiki tulioufanya katika mlango wa kulipa qadhwaa. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
· Ni Rakaa Ngapi Za Kulipiwa Witr?
Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu Anha) akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapolala usiku au akaugua, huswali rakaa 12 mchana..”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (746) na wengineo].
Na imejulikana kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali usiku rakaa 11, na ikajulikana kwamba kulipa kwake Witr mchana ilikuwa ni kwa shaf-’i. Kwa hiyo, mwenye mazoea ya kuswali Witr rakaa moja, atalipa mchana kwa kuswali rakaa mbili, na mwenye mazoea ya kuswali rakaa tatu, atazilipa nne na kadhalika.
Imesuniwa mtu afanye haraka kuilipa kabla ya Adhuhuri ili aandikiwe thawabu za Swalaah ya Usiku. Imepokelewa toka kwa ‘Umar bin Al-Khattwaab akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( من نام عن حزبه أو عن شيئ منه، فقرأه بين صلاة الفجر وصلاة الظهر، كتب له كأنما قرأه من الليل))
(( Mwenye kulala asifanye uradi wake, au sehemu ya uradi huo, halafu akaja kuusoma kati ya Swalaah ya Alfajiri na Swalaah ya Adhuhuri, huandikiwa kama aliyeusoma usiku)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (747), At-Tirmidhiy (578), Abu Daawuud (1299), An-Nasaaiy (3/259) na Ibn Maajah (1343)].
Hadiyth hii inatuhimizia kuwahi haraka, na pia inaonyesha uweze
kano wa kwamba ubora wa kutenda jambo pamoja na kuzidishiwa maradufu, kunafungamana na ule wakati wake uliopangwa. [Haashiyat As-Suyuutwiy ‘Ala An-Nasaaiy (3/259)]
· Rakaa Baada Ya Witr
‘Aaishah akizungumzia kuhusu namna Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alivyokuwa akiswali usiku anasema: “Alikuwa anaswali rakaa 13; huswali rakaa nane, na Witr rakaa moja. Anapotoa tasliym, hupiga takbiyr akaswali rakaa mbili akiwa amekaa, na huswali rakaa mbili kati ya adhana ya Alfajiri na iqaamah”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1159), Muslim (738) na wengineo].
Maulamaa wana miono mitatu kuhusiana na rakaa hizi mbili baada ya Witr:
1- Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameziswali ili kubainisha kwamba inajuzu, naye hakudumu nazo, bali aliziswali mara moja au mara chache sana, na kwamba neno la ‘Aaishah “Alikuwa anaswali”, hakulazimishi kuwa alidumu au alikariri mpaka ije dalili inayothibitisha hivyo. [Sharhu Muslim ya An-Nawawiy (6/21) chapa ya Ihyaau At-Turaath Al-‘Arabiy]
2- Rakaa hizi mbili zinapita mapitio ya Sunnah na makamilisho ya Witr, kwani Witr ni ‘ibaadah kando, nazo zinakuwa ni kama rakaa mbili baada ya Magharibi, na hiyo ndiyo Witr ya mchana. Na rakaa mbili baada yake ni ukamilisho wake, pia na rakaa mbili baada ya Witr ya usiku. [Zaadul Ma’adiy ya Ibn Al-Qayyim (1/318, 319)]
3- Rakaa hizi mbili ni mahsusi kwake Rasuli basi. Hivyo Hadiyth haiwi mahsusi kwa amri ya kuifanya Swalaah ya mwisho ya usiku Witr!! [Naylul Awtwaar (3/48) chapa ya Al-Hadiyth]
Ninasema: “Kauli mbili za mwanzo, kila moja ina uzito wa nguvu, ama ya tatu, hii ni lazima iangaliwe. Umahususi hauthibiti ila kwa dalili, na asili ya vitendo vyake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni kufuatwa na kuigwa nasi. Ikiwa itasemwa: “ Kitendo chake Rasuli hakulifanyi agizo lake la kuifanya Swalaah ya mwisho ya usiku kuwa Witr kuwa ni agizo mahsusi”, basi sisi tunasema: “Ni kweli, lakini agizo hilo linageuzwa kuwa Sunnah kutokana na kauli yake iliyotangulia isemayo: ((Mwenye kuchelea kati yenu kutoweza kuamka mwishoni mwa usiku, basi aswali Witr mwanzoni mwake halafu alale..)). [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa karibuni].
Na kwa kumkubalia kwake Abu Bakr aswali Witr kabla ya kulala. [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa karibuni].
Kwa mujibu wa Hadiyth hizi mbili, ni halali kuswali kwa aliyeamka baada ya kuwa aliswali Witr kabla ya kulala. Kisha nililidadisi agizo la Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) la kuswali rakaa mbili baada ya Witr katika Hadiyth Marfu’u ya Thawbaan isemayo:
(( إن هذا السفر جهد وثقل، فإن أوتر أحدكم فليركع ركعتين، فإن استيقظ وإلا كانتا له ))
((Hakika safari ni tabu na uzito, ikiwa mmoja wenu ataswali Witr, basi aswali rakaa mbili. Na ikiwa ataamka (itakuwa vyema), na kama hakuweza basi zitamtosheleza)). [Albaaniy kasema ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ad-daaramiy (1594) na kwake limetumika neno "السهر" badala ya "السفر" , Ibn Khuzaymah (1106) na Ad-daaraqutwniy (2/36). Angalia Asw-Swahiyhah (1993)] ….nikakuta agizo limekutana na kitendo, na usharia ukathibiti. Hivyo agizo la kuifanya Witr mwisho wa usiku, ni agizo la kupendelewa hivyo. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
· Suwrah Zinazosomwa Katika Rakaa Mbili Baada Ya Witr
Imepokelewa toka kwa Abu Umaamah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali rakaa mbili baada ya Witr akiwa ameketi akisoma ndani ya rakaa hizo: (Idhaa zulzilatil ardhu) na (Qul yaa ayyuhal kaafiruwn). [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (5/260), At-Twahaawiy (1/280-341), At-Twabaraaniy katika Al-Kabiyr (8/277) na Al-Bayhaqiy (3/33). Ina Hadiyth mwenza ya Anas].
· Imesuniwa Kulala Baada Ya Rakaa Mbili
Imesuniwa kulala baada ya rakaa mbili za baada ya Witr – au baada ya Swalaah ya Usiku – mpaka iadhiniwe Alfajiri. Ibn ‘Abbaas katika Hadiyth yake ambapo anaelezea namna Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alivyoswali usiku wakati yeye alipolala kwa khalati yake Maymuwnah anasema: “Kisha akasimama kuswali, nami nikasimama nikafanya kama alivyofanya, halafu nikaondoka na kwenda kusimama kandoni mwake. Naye akauweka mkono wake wa kulia juu ya kichwa changu na akalikamata sikio langu la kulia na kulisokota. Halafu akaswali rakaa mbili, kisha rakaa mbili, kisha rakaa mbili, kisha rakaa mbili, kisha rakaa mbili, kisha rakaa mbili, halafu akaswali Witr. Baadaye alilala mpaka alipojiwa na mwadhini, akasimama, akaswali rakaa mbili nyepesi, kisha akatoka, akaswali Alfajiri”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj“ na Al-Bukhaariy (1146) na Muslim (739)]
Na katika riwaya ya Ibn Khuzaymah anasema: “Akaswali Witr tisa au saba, kisha akaswali rakaa mbili, halafu akaulaza ubavu wake mpaka nikasikia mkoromo wake, kisha Swalaah ikaqimiwa, akaondoka, akaenda kuswali”. Rakaa hizi mbili, inawezekana ni zile alizokuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiziswali baada ya Witr, na pia inawezekana zikawa ni rakaa mbili za Alfajiri. [Swahiyh ya Ibn Khuzaymah (2/157-158)].
Ninasema: “Uwezekano wa kwanza unatiliwa nguvu na Hadiyth ya Al-Aswad aliposema: “Nilimuuliza ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu Anha): Ni vipi Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anaswali Swalaah ya usiku? Akasema: Alikuwa akilala mwanzo wake, anasimama mwishoni mwake akaswali, kisha hurejea kwenye tandiko lake. Na mwadhini anapoadhini hutoka haraka. Na kama ana kitu hivi huoga, na kama hana, hutawadha akatoka”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1146) na Muslim (739)].
Na hili halipingi uhalali wa kulala baada ya rakaa mbili za Sunnah ya Alfajiri, bali inavyoonyesha ni kuwa mara alikuwa akilala kati ya Swalaah ya usiku na Swalaah ya Alfajiri, na mara nyingine baada ya rakaa mbili za Sunnah ya Alfajiri, na huenda alikuwa akilala katika mwahala kote kuwili. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
025-Qiyaamul Layl
Alhidaaya.com [3]
Qiyaamul layl huitwa Tahajjud. Jamhuri ya Maulamaa wanaielezea kama ni Swalaah ya Sunnah inayoswaliwa usiku baada ya kulala katika usiku wowote katika mwaka. [Mughnil Muhtaaj (1/228)]
· Fadhila Za Qiyaamul Layl Na Kuraghibishwa Kwake
Swalaah ya Sunnah usiku wa manane kwenye kiza totoro, ina fadhila kubwa sana na thawabu adhimu zisizohesabika ambazo hakuna mtu yeyote awezaye kuzielezea. Ni nembo ya watu wema na ni sifa muhimu mahsusi ya Muttaqiyn.
Kutokana na fadhila yake kubwa, Allaah Mtukufu Alimwagiza Rasuli Wake Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aikabili na avaane na sharafu hii adhimu na fadhila hii kubwa ili aweze kuipata “Al-Maqaamu Al-Mahmoud” Akamwambia:
((وَمِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَّكَ عَسَىٰ أَن يَبْعَثَكَ رَبُّكَ مَقَامًا مَّحْمُودًا ))
((Na katika usiku, amka uswali (tahajjud) kuisoma (Qur-aan); ni ziada ya Sunnah kwako Asaa Rabb wako Akakuinua cheo kinachosifika)). [Al-Israa (17:79)]
Kuna Aayah na Hadiyth nyingi sana zinazoelezea fadhila za Qiyaamul Layl na kuraghibishia. Tutazitaja baadhi yake ili mwenye utashi na maisha hayo ya baraka aingiwe na hamu ya kujisikia na kujiridhisha nafsi yake, na akajiwekea azma ya kulitenda hilo angalau kwa kiasi kidogo.
1- Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema:
((لَيْسُوا سَوَاءً ۗ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَائِمَةٌ يَتْلُونَ آيَاتِ اللَّـهِ آنَاءَ اللَّيْلِ وَهُمْ يَسْجُدُونَ ))
((Hawako sawa sawa; miongoni mwa Ahlil-Kitaabi wako watu wenye kusimama (kwa utiifu) wanasoma Aayaat za Allaah nyakati za usiku na wao wanasujudu (katika Swalaah)). [Aal-‘Imraan (3:113)]
2 -Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema:
((وَعِبَادُ الرَّحْمَـٰنِ الَّذِينَ يَمْشُونَ عَلَى الْأَرْضِ هَوْنًا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ الْجَاهِلُونَ قَالُوا سَلَامًا ● وَالَّذِينَ يَبِيتُونَ لِرَبِّهِمْ سُجَّدًا وَقِيَامًا))
(( Na Waja wa Ar-Rahmaan ni wale wanaotembea katika ardhi kwa unyenyekevu na upole, na majahili wanapowasemesha, wao husema: Salaam! ● Na wale wanaokesha usiku kwa ajili ya Rabb wao wakisujudu na kusimama)). [Al-Furqaan (25 :63 na 64)]
3- Anasema Subhaanah:
((يَا أَيُّهَا الْمُزَّمِّلُ ● قُمِ اللَّيْلَ إِلَّا قَلِيلًا ● نِّصْفَهُ أَوِ انقُصْ مِنْهُ قَلِيلًا ● أَوْ زِدْ عَلَيْهِ وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلًا))
((Ee uliyejifunika ● Simama (kuswali) usiku kucha isipokuwa kidogo tu ● Nusu yake, au ipunguze kidogo ● Au izidishe, na soma Qur-aan kwa kisomo cha utaratibu upasao, kuitamka vizuri na kutaamali)). [Al-Muzzammil ( 73: 1-4)]
4- Anasema Subhaanah:
((وَاذْكُرِ اسْمَ رَبِّكَ بُكْرَةً وَأَصِيلًا ● وَمِنَ اللَّيْلِ فَاسْجُدْ لَهُ وَسَبِّحْهُ لَيْلًا طَوِيلًا))
((Na lidhukuru Jina la Rabb wako asubuhi na jioni ● Na katika usiku msujudie na uswali kwa ajili Yake usiku mrefu)). [Al-Insaan (76: 25 na 26)]
5- Anasema Subhaanah:
((أَمَّنْ هُوَ قَانِتٌ آنَاءَ اللَّيْلِ سَاجِدًا وَقَائِمًا يَحْذَرُ الْآخِرَةَ وَيَرْجُو رَحْمَةَ رَبِّهِ ۗ قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ۗإِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الْأَلْبَابِ))
(( Je, yule aliye mtiifu nyakati za usiku akisujudu, au akisimama (kuswali), anatahadhari na aakhirah na anataraji rahmah ya Rabb wake (ni sawa na aliyekinyume chake?). Sema: “Je, wanalingana sawa wale wanaouja na wale wasiojua?” Hakika wanakumbuka wenye akili tu)). [Az-Zumar (28 :9)]
6-Anasema Subhaanah:
(( إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ ● آخِذِينَ مَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَٰلِكَ مُحْسِنِين ● كَانُوا قَلِيلًا مِّنَ اللَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ ● وَبِالْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ))
((Hakika wenye taqwa watakuwa katika Jannaat na chemchemu ● Wakichukua yale Atakayowapa Rabb wao. Hakika wao walikuwa kabla ya hapo ni wahisani ● Walikuwa kidogo tu katika usiku wakilala kwa raha ● Na kabla ya Alfajiri wakiomba maghfirah)). [Adh-dhaariyaat ( 51:15-18)]
7- Anasema Subhaanah:
((إِنَّمَا يُؤْمِنُ بِآيَاتِنَا الَّذِينَ إِذَا ذُكِّرُوا بِهَا خَرُّوا سُجَّدًا وَسَبَّحُوا بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ ● تَتَجَافَىٰ جُنُوبُهُمْ عَنِ الْمَضَاجِعِ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ خَوْفًا وَطَمَعًا وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ● فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَّا أُخْفِيَ لَهُم مِّن قُرَّةِ أَعْيُنٍ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ))
(( Hakika wanaamini Aayaat Zetu wale wanapokumbushwa nazo huporomoka kusujudu, na wakasabbih kwa Himidi za Rabb wao, nao hawatakabari ● Mbavu zao zinatengana na vitanda, wanamuomba Rabb wao kwa khofu na matumaini, na katika yale Tuliyowaruzuku wanatoa ● Basi nafsi yoyote haijuiyaliyofichiwa katika yanayoburudisha macho. Ni jazaa kwa yale waliyokuwa wakiyatenda)). [As-Sajdah (32 :15-17)]
8- Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah akisema: “Rasuli wa Allaah aliulizwa: “Ni Swalaah ipi bora zaidi baada ya Swalaah za faradhi?” Akasema: ((Ni Swalaah usiku wa manane)). Akaulizwa: “Ni swawm ipi bora zaidi baada ya Ramadhwaan?” Akasema: ((Ni Mwezi wa Allaah wa Muharram)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (1163), At-Tirmidhiy (438), Abu Daawuud (2429), An-Nasaaiy (3/207) na Ibn Maajah (1742)].
9- Imepokelewa na ‘Abdullaah bin Salaamah (Radhwiya Allaahu Anhu) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( أيها الناس، أفشوا السلام وأطعموا الطعام، وصلوا الأرحام، وصلوا بالليل والناس نيام، تدخلوا الجنة بسلام))
((Enyi watu! Enezeni amani, lisheni watu chakula, ungeni ukoo, swalini usiku watu wakiwa wamelala, mtaingia Peponi kwa amani)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (1855), Ibn Maajah (1334) na Ahmad (7591). Angalia Asw-Swahiyhah (569)].
10- Abuu Maalik Al Asha-’ariy amepokea toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
(( إن في الجنة غرفا يرى ظاهرها من باطنها، وباطنها من ظاهرها، أعدها الله لمن أطعم الطعام وأفشى السلام وصلى بالليل والناس نيام))
((Peponi kuna vyumba; nje yake huonekana toka ndani yake, na ndani yake huonekana toka nje yake. Allaah Amevitayarisha kwa ajili ya mwenye kulisha chakula, akaeneza amani, akaswali usiku na watu wamelala)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Hibaan (509) na wengineo. Angalia Swahiyhut Targhiyb (614) na Swahiyhul Jaami’i (2123)].
11- Imepokelewa toka kwa ‘Amri bin ‘Absah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( أقرب ما يكون الرب من العبد في جوف الليل الآخر، فإن استطعت أن تكون ممن يذكر الله في تلك الساعة فكن))
((Wakati ambao Mola Huwa karibu zaidi na Mja Wake, ni mwisho wa usiku wa manane. Ikiwa wewe utaweza kuwa ni katika wanaomdhukuru Allaah katika saa hizo, basi fanya)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (3579) na An-Nasaaiy (572). Angalia Swahiyhut Targhiyb (624) na Swahiyhul Jaami’i (1184)].
12- Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu Anhu) anasema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( رحم الله رجلا قام من الليل فصلى، وأيقظ امرأته ] فصلت [ فإن أبت نضح في وجهها الماء، ورحم الله امرأة قامت من الليل فصلت، وأيقظت زوجها ] فصلى [ فإن أبى نضحت في وجهه الماء))
((Allaah Amrehemu mtu aliyesimama usiku akaswali, na akamwamsha mkewe [akaswali]. Na kama atakataa, atamnyunyizia usoni maji. Na Allaah Amrehemu mwanamke aliyesimama usiku akaswali, na akamwamsha mumewe [akaswali]. Na kama atakataa, atamnyunyizia usoni maji)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud ( 1308), An-Nasaaiy (3/205), Ibn Maajah (1336) na Ahmad (2/250). Iko katika Swahiyhul Jaami’i (3488).]
Na katika tamshi jingine:
(( إذا قاما وصليا ركعتين كتبا من الذاكرين الله كثيرا والذاكرات))
((Wakisimama wakaswali rakaa mbili, wataandikwa ni katika wanaume wenye kumdhukuru Allaah kwa wingi na wanawake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1309), An-Nasaaiy katika Al-Kubraa (1310) na Ibn Maajah (1335). Iko katika Swahiyhul Jaami’i (330)].
13- Imepokelewa toka kwa Abu Dharri toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
(( ثلاثة يحبهم الله...- فذكر منهم -.. ورجل سافر مع القوم فارتحلوا حتى إذا كان من آخر الليل وقع عليهم الكرى فنزلوا، فضربوا برؤوسهم، ثم قام فتطهر، وصلى رغبة لله عز وجل، ورغبة لله عز وجل، ورغبة فيما عنده))
((Watu watatu Allaah Anawapenda – kati ya aliowataja -..ni mtu aliyesafiri na watu, wakaenda mpaka ilipofika mwisho wa usiku, wakapatwa na usingizi wakapumzika na wakalala. Kisha mtu huyo akasimama, akatawadha, kisha akaswali kwa ajili ya raghba kwa Allaah ‘Azza wa Jalla, na kwa ajili ya hamu ya kuyapata yaliyoko Kwake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (5/176), At-Twayalsiy (468), At-Twabaraaniy katika Al-Kabiyr (2/1637) na Al-Bayhaqiy (9/160)].
14- Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
(( عليكم بقيام الليل، فإنه دأب الصالحين قبلكم، وقربة إلى الله، ومنهاة عن الإثم، وتكفير للسيئات))
((Jilazimisheni kusimama usiku, kwani huo ndio mwenendo wa watu wema kabla yenu, ni kujikurubisha kwa Allaah, ni katazo la madhambi na kifutio cha mabaya)). [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh. Angalia Al-Irwaa (452) na Swahiyhul Jaami’i (3958)].
15- Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar kwamba aliona njozi akamhadithia Hafswah, naye Hafswah akamhadithia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Rasuli akasema:
(( نعم الرجل عبد الله، لو كان يصلي من الليل))
((Mbora wa watu ni ‘Abdullaah, laiti angelikuwa anaswali usiku)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1122) na Muslim (2479)].
Na katika tamko jingine:
(( إن عبد الله رجل صالح، لو كان يكثر الصلاة من الليل))
((Hakika ‘Abdullaah ni mtu mwema, laiti angelikuwa anakithirisha kuswali usiku)).
Saalim anasema: “ ‘Abdullaah tokea baada ya hapo, alikuwa halali usiku isipokuwa kidogo”.
Al-Qurtubiy amesema: “Hakuwa akiswali usiku, na kutokana na hilo, ‘Abdullaah alipata zindusho kwamba kusimama usiku ni katika amali za kujikinga nazo na moto na kuukurubia. Na kwa ajili hiyo, hakuacha tena kuswali usiku baada ya hapo”.
16- Imepokelewa toka kwa Ummu Salamah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliamka usiku mmoja (kwa mshtuko) akasema:
((سبحان الله، ماذا أنزل الليلة من الفتن، ماذا أنزل من الخزائن، من يوقظ صواحب الحجرات، يا رب كاسية في الدنيا عارية يوم القيامة))
((Subhaanal Laah! Ni wingi ulioje wa fitna zilizoteremshwa usiku huu! Ni wingi ulioje wa hazina za rahmah zilizofunguliwa! Nani atawaamsha walioko vyumbani? Ee (mwenye kusikia)! Huenda anayevaa duniani, asivae kitu Siku ya Qiyaamah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1126) na At-Tirmidhiy (2196)].
Hadiyth hii inatupa funzo kwamba mtu anatakiwa amwamshe mkewe usiku kwa ajili ya ‘ibaadah na hususan wakati wa kuteremka tukio fulani. Yamesemwa haya katika Al-Fat-h.
Ninasema: “Hii ni sehemu tu ya Aayah na Hadiyth kochokocho zinazogusia kuhusu fadhila za kusimama usiku na kuraghibisha hilo. Nyinginezo zitakuja Insha Allaah katika sehemu iliyobakia ya mlango wa “Qiyaamul Layl”, nazo huenda zikapata moyo mkweli ukanufaika, nami nikapata –Bi Idhnil Laahi – thawabu za kuongozea kwenye kheri”. [Kati ya mambo muhimu yanayomsaidia mtu kusimama usiku, ni kusoma wasifu wa watu wema kuhusiana na suala hili. Kati ya yaliyo kusanya zaidi na yenye utamu zaidi katika niliyoyasoma kuhusiana na hili, ni yale yaliyoko katika kitabu cha “Ruhbaanul Layl” cha Sheikh Al-Habiyb Al-Hammaam mwandishi asiyeweka kalamu chini. Basi jitahidi ukipate]
· Wakati Wa Qiyaamul Layl
Swalaah ya usiku inajuzu kuiswali mwanzoni mwa usiku, katikati yake na mwishoni mwake. Yote hayo aliyafanya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Imepokelewa toka kwa Anas akisema: “Hatukutaka kumwona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) usiku akiswali ila tulimwona, na hatukutaka kumwona amelala ila tulimwona”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1090), An-Nasaaiy (1627) na tamko ni lake, na At-Tirmidhiy (769)].
Al-Haafidh amesema katika Al-Fat-h (3/23): “Kwa maana kwamba kuswali kwake na kulala kwake kulikuwa kukitofautiana usiku, na hakuwa akipanga wakati maalumu, bali ilikuwa kwa mujibu wa itakavyowepesika kwake”.
· Wakati Wake Ulio Bora Zaidi
Imesuniwa kuswali Qiyaamul Layl katika theluthi ya mwisho ya usiku kwa ajili ya kuvipata Vipawa Adhimu vya Allaah katika masaa hayo ambapo hawaamki kwa ajili ya kumwabudu Allaah ila watu kidogo mno. Watu hawa ndio wanaopata kujibiwa du’aa zao, wanaokubaliwa toba zao, wanaopata maghfirah na kusitiriwa na kasoro zao.
Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( ينزل الله إلى السماء الدنيا كل ليلة حين يبقى ثلث الليل فيقول: أنا الملك، من الذي يدعوني فأستجيب له، من الذي يسألني فأعطيه، من الذي يستغفرني فأغفر له)) وفي لفظ لمسلم (758) (( حتى ينفجر الفجر))
((Allaah Huteremka katika mbingu ya dunia kila usiku wakati inapobakia theluthi ya usiku Akasema: Mimi Ndiye Mfalme. Nani aniombaye Nikamjibu? Nani anitakaye haja Nikampa? Nani aniombaye maghfirah Nikamghufiria?)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1145) na Muslim (758) na tamko ni lake].
Na katika tamko la Muslim: ((Mpaka Alfajiri ipambazuke)).
Imepokelewa na ‘Amri bin ‘Absah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( أقرب ما يكون الرب من العبد في جوف الليل الآخر، فإن استطعت أن تكون ممن يذكر الله في تلك الساعة فكن))
((Wakati ambao Mola Huwa karibu zaidi na Mja Wake, ni mwisho wa usiku wa manane. Ikiwa wewe utaweza kuwa ni katika wanaomdhukuru Allaah katika saa hizo, basi fanya)). [Hadiyth Swahiyh. Imetajwa hivi karibuni].
Imepokelewa toka kwa ‘Abdullah bin ‘Amri kwamba Rasuli wa Allaah amesema:
(( إن أحب الصيام إلى الله صيام داود، وأحب الصلاة إلى الله عز وجل صلاة داود، كان ينام نصف الليل، ويقوم ثلثه، وينام سدسه، وكان يصوم يوما ويفطر يوما ))
((Hakika Swiyaam inayopendeza zaidi kwa Allaah ni Swiyaam ya Daawuud, na Swalaah inayopendeza zaidi kwa Allaah ‘Azza wa Jalla ni Swalaah ya Daawuud. Alikuwa akilala nusu ya usiku, akisimama katika theluthi yake na akilala katika sudusi yake. Na alikuwa akifunga siku moja na kula siku moja)). [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1131) na Muslim (1159)].
Na hivi ndivyo Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alivyokuwa akifanya. ‘Aaishah akiielezea Swalaah ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema: “Alikuwa akilala mwanzo wake, anasimama mwishoni mwake akaswali, kisha hurejea kwenye tandiko lake. Na mwadhini anapoadhini hutoka haraka. Na kama ana kitu hivi huoga, na kama hana, hutawadha akatoka”. [Hadiyth Swahiyh. Imetajwa hivi karibuni].
Imepokelewa toka kwa Ummu Salamah Hadiyth kama hii.
Na katika Hadiyth ya Humayd bin ‘Abdul Rahmaan kuhusiana na Swahaba Mmoja wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliyesuhubiana naye katika safari anatuambia: “Kisha akasimama akaswali mpaka nikasema: Hakika ameswali kiasi cha alivyolala, kisha akalala mpaka nikasema: Hakika amelala kiasi cha alivyoswali. Halafu akaamka, akafanya kama alivyofanya mwanzoni, na akasoma mfano wa alivyosoma. Halafu Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akafanya mara tatu kabla ya Alfajiri”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (1626). Ina Hadiyth mwenza iliyopokelewa toka kwa Ummu Salamah].
Imepokelewa toka kwa Masrouq kwamba alimuuliza ‘Aaishah: “Ni wakati gani Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaswali?” Akasema: “Alikuwa anapomsikia jogoo, hunyanyuka akaswali”.
Ni kawaida ya jogoo kuwika usiku wa manane au katika theluthi ya usiku.
· Adabu Za Qiyaamul Layl
Mtu ambaye Allaah Amekikunjua kifua chake na akataka kuswali Qiyaamul Layl, basi imesuniwa azichunge adabu zifuatazo:
1- Ajiandae kwa kufanya mambo yatakayomsaidia kuamka. Kati ya mambo hayo ni:
(a) Kulala mchana qayluulah kama itakuwa wepesi kwake.
(b) Kutokukesha katika yasiyokuwa na maslaha ya kisharia. Tumeshazungumzia kuhusu ukaraha wa kupiga gumzo baada ya ‘Ishaa isipokuwa katika maslaha ya kisharia.
(c) “Ni bora kwa aliyezidiwa na uvivu na kupondokea ureda na kujisikia, asikisheheneshi sana kitanda, kwani hilo huleta usingizi mwingi, mghafiliko na kuachana na majukumu ya mambo ya kheri”. [Faydhul-Qadiyr (5/180)]
Ninasema: “Tandiko la Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) lilikuwa kavu. Imepokelewa toka kwa ‘Umar akisema: “Niliingia kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), nikamkuta amelala juu ya mkeka nami nikakaa. Akaiteremsha izari yake, nayo ni moja tu, hana nyingine. Nikatahamaki kuona alama za mkeka kwenye ubavu wake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (2468) na Muslim (1479) na tamko ni lake].
Na ‘Aaishah anasema: “Mto wake aliokuwa akilalia usiku, ulikuwa ni wa ngozi uliojazwa ufumwele”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (4146) na At-Tirmidhiy. Iko katika Swahiyhul Jaami’i (4714)].
2- Wakati anapolala, anuwie kwamba ataamka
Imepokelewa toka kwa Abu Ad-Dardaai kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( من أتى إلى فراشه وهو ينوي أن يقوم فيصلي من الليل، فغلبته عينه حتى يصبح كتب له ما نوى، وكان نومه صدقة عليه من ربه))
((Mwenye kwenda kulala nailhali ananuwia kwamba aamke usiku kisha usingizi ukamzidia mpaka akapambaukiwa, basi ataandikiwa alilolinuwia, na usingizi wake unakuwa ni swadaqah kwake toka kwa Mola wake)). [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (1784), Ibn Maajah (1344) na Al-Bayhaqiy (3/15)].
3- Alale na wudhuu wake
Tumeeleza katika mlango wa wudhuu kwamba huu ulikuwa ni mwenendo wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
4- Alale kwa ubavu wake wa kuume
Imepokelewa toka kwa Hafswah akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapolala, huweka mkono wake wa kulia juu ya shavu lake la kulia”. [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh: Angalia katika Swahiyhul Jaami’i (4523)].
Kulala kwa ubavu wa kulia ndiyo fitwrah kama itakavyokuja katika Hadiyth ya Al-Barraa bin ‘Aazib.
· Faida
Kuna siri nyeti kuhusiana na kulala Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ubavu wake wa kulia. Siri yenyewe ni kuwa damu nzito imening’inia upande wa kushoto. Na mtu anapolalia ubavu wake wa kushoto usingizi huwa mzito, kwa vile anakuwa yuko katika hali ya ushwari na utulivu, na hapo usingizi humzidia. Ama akilalia ubavu wake wa kulia, hapo hawi katika hali ya ushwari na utulivu, na usingizi haumchukui mzima mzima kwa vile moyo hauwi mtuvu na haupondokei kwenye utulivu. Na kwa ajili hiyo, madaktari wanawashauri watu kulalia ubavu wa kushoto ili kupata mapumziko kamili na usingizi mzuri. Lakini Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anapendelea kulalia ubavu wa kulia ili mtu asilale usingizi mzito akashindwa kuamka kuswali Qiyaamul Layl. Kulalia ubavu wa kulia kuna manufaa zaidi kwa moyo, na kwa ubavu wa kushoto kuna manufaa zaidi kwa mwili. Na Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”. [Zaadul Ma’ad cha Ibn Al-Qayyim (1/321/322)]
5- Akichelea kutoweza kuamka, basi aswali Witr kabla ya kulala
Ikiwa ataamka, ataswali kiasi atakacho lakini bila ya kuikariri Witr. Haya yashaelezwa katika mlango wa Witr.
6- Amdhukuru Allaah wakati anapolala
Kuna adhkaar nyingi zilizopokelewa kwa njia Swahiyh kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kati ya adhkaar hizo ni:
(a) Hadiyth ya ‘Aaishah asemaye: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapokwenda kulala kila usiku, huvikusanya viganja vyake, kisha huvipulizia akivisomea: (Qul Huwa Allaahu Ahad), (Qul A’uwdhu bi Rabbil Falaq) na (Qul A’uwdhu bi Rabbi An Naas), halafu hujipangusa kwavyo mwili pale vinapoweza kufika katika viungo vyake. Huanza kupangusa kichwa chake na uso wake, kisha sehemu ya mbele ya mwili wake. Hufanya hivi mara tatu”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (5018) na Muslim (2192)].
(b) Imepokelewa na Abu Hurayrah kwamba shaytwaan alimwambia wakati alipotaka kumpeleka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Niache nikufundishe maneno ambayo Allaah Atakufaa nayo: Ukienda kulala, basi soma Aayatul Kursiy (Allaahu Laailaaha illaa Huwa Al-Hayyu Al-Qayyuwm….) mpaka mwisho, utaendelea kupata mlinzi toka kwa Allaah, na shaytwaan hatokukurubia mpaka upambazukiwe”. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Amekwambia kweli lakini ni mwongo mno, na huyo ni shaytwaan)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy ikiwa Mu’allaq (3275) na An-Nasaaiy katika “Mlango wa Amali za Mchana na Usiku” (959)].
(c) Imepokelewa toka kwa Abu Mas-’oud Al-Answaariy toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
((Mwenye kuzisoma Aayah mbili za mwisho za Suwrat Al-Baqarah zitamtosheleza)).
[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (4008) na Muslim (808)].
Kwa maana kwamba zitamlinda na shari na adha. Imesemwa pia kwa maana ya kuwa zitamtosheleza na kusimama usiku kuswali.
(d) Imepokelewa toka kwa Nawfal Al-Ashja’iy akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia: ((Soma: (Qul yaa ayyuhal kaafiruwn)) halafu lala ukiifanya Suwrah ya mwisho kuisoma, kwani ni utakaso na shirk)). [Al-Albaaniy kasema ni Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (5055), At-Tirmidhiy (3401) na Ahmad (5/456). Angalia Swahiyh At-Targhiyb (604) na Swahiyhul Jaami’i (1161)].
(e) Imepokelewa toka kwa Hudhayfah akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapotaka kulala husema: ((Bismika Al-Laahumma amuwtu wa ahyaa)), na anapoamka usingizini husema: ((Alhamdu lil Laahi Al Ladhiy Ahyaanaa ba’ada maa Amaatanaa wa ilahyi an nushuwr)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (6312), Abu Daawuud (5049) na At-Tirmidhiy (3413)].
(f) Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( إذا قام أحدكم عن فراشه ثم رجع إليه فلينفضه بصنفة إزاره ثلاث مرات، فإنه لا يدري ما خلفه عليه بعده، وإذا اضطجع فليقل: "باسمك ربي وضعت جنبي، وبك أرفعه، فإن أمسكت نفسي فارحمها، وإن أرسلتها فاحفظها بما تحفظ به عبادك الصالحين))
((Anaponyanyuka mmoja wenu toka kitandani mwake, kisha akarejea tena, basi akikung’ute kwa ncha ya nguo yake mara tatu, kwani hajui alivyoviacha humo. Na anapolala aseme: “Kwa Jina Lako ee Mola wangu! Nimeuweka ubavu wangu, na kwa Msaada Wako naunyanyua, ikiwa Utaikamata nafsi yangu basi Irehemu, na ikiwa Utaiachia basi Ihifadhi kwa yale Unayowahifadhia Waja Wako wema”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (6320) na Muslim (2714)].
(g) Imepokelewa toka kwa ‘Aliy bin Abiy Twaalib kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia yeye pamoja na Faatwimah wakati walipomuulizia kuhusu mtumishi:
(( ألا أدلكما على ما هو خير لكما من خادم: إذا آويتما إلى فراشكما فسبحا ثلاثا وثلاثين، واحمدا ثلاثا وثلاثين، وكبرا ثلاثا وثلاثين، فإنه خير لكما من خادم ))
((Je, niwaambieni lililo bora zaidi kwenu kuliko mtumishi? Mkienda kulala, basi semeni “Subhaana Allaah” mara 33, “Al Hamdu lil Laah” mara 33, na “Allaahu Akbar” mara 33. Hivyo ni bora zaidi kwenu kuliko mtumishi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (3705) na Muslim (2727)].
(h) Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar kwamba alimwamuru mtu mmoja aliyelalia kitanda chake aseme: ((Ee Mola wangu! Wewe Umeiumba nafsi yangu na Wewe Ndiye Unayeilinda, mauti yake na uhai wake ni Kwako. Ukiipa uhai basi Ihifadhi, na Ukiifisha basi Ighufirie. Ee Mola wangu! Mimi nakuomba afya kamili)).
Ibn ‘Umar akasema: “Nimeyasikia haya toka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (2712), An Nasaaiy katika “Al-Yawm wa Al-Laylah” (796) na Ahmad (2/79)].
Imesuniwa amalizie adhkaar zilizotangulia ambazo zitakuwa nyepesi kwake kwa yaliyomo ndani ya Hadiyth hii ifuatayo:
(i) Imepokelewa toka kwa Al-Barraa bin ‘Aazib akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( إذا أتيت مضجعك، فتوضأ وضوءك للصلاة ثم اضطجع على شقك الأيمن، وقل: اللهم أسلمت وجهي إليك، وفوضت أمري إليك، وألجأت ظهري إليك، رغبة ورهبة إليك، لا ملجأ ولا منجا منك إلا إليك، آمنت بكتابك الذي أنزلت، وبنبيك الذي أرسلت، فإن مت مت على الفطرة، فاجعلهن آخر ما تقول))
((Ukienda kulala, basi tawadha wudhuu wa Swalaah, kisha lalia ubavu wako wa kulia halafu sema: Ee Mola wangu! Nimeusalimisha uso wangu Kwako, nimetegemeza jambo langu Kwako, nimeuelekeza mgongo wangu Kwako. Nina raghba na hofu kuelekea Kwako, na hakuna makimbilio wala maokozi kutokana na Wewe ila Kwako. Nimekiamini Kitabu Chako Ulichokiteremsha, na Nabiy Wako Uliyemtuma. Ikiwa utakufa, basi utakufa katika fitwrah, basi yafanye kuwa ndiyo maneno yako ya mwisho)).
Nikasema kujikumbusha: “Na kwa Rasuli Wako Uliyemtuma”, akaniambia: ((Hapana, na kwa Nabiy Wako Uliyemtuma)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (247) na Muslim (2710)].
7- Apanguse uso kuondosha usingizi kama ataamka, amdhukuru Allaah na atawadhe
(a) Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah akisema kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( يعقد الشيطان على قافية رأس أحدكم إذا هو نام ثلاث عقد، يضرب على كل عقدة مكانها: عليك ليل طويل فارقد، فإن استيقظ وذكر الله تعالى انحلت عقدة، فإن توضأ انحلت عقدة، فإن صلى انحلت عقده كلها فأصبح نشيطا طيب النفس، وإلا أصبح خبيث النفس كسلان))
((Anapolala mmoja wenu, shaytwaan hufunga kisogoni mwake vifundo vitatu. Hukikita kila kifundo mahala pake (akimwambia): Umebakiwa na usiku mrefu, basi lala. Anapoamka akamtaja Allaah, kifundo kimoja hufunguka. Anapotawadha hufunguka kingine, na anaposwali cha tatu hufunguka. Hapo huwa mchangamfu na mwenye nafsi nzuri, na kama si hivyo, huwa na nafsi mbaya na mvivu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1142) na Muslim (776)].
(b) Imepokelewa toka kwa ‘Ubaadah bin Swaamit toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
(( من تعار من الليل فقال: لا إله إلا الله وحده لا شريك له، له الملك وله الحمد، وهو على كل شيء قدير، الحمد لله، وسبحان الله، ولا إله إلا الله، والله أكبر، ولا حول ولا قوة إلا بالله، ثم قال: اللهم اغفرلي، أو دعا، استجيب له، فإن توضأ وصلى قبلت صلاته))
((Mwenye kuamka usiku akasema: Laa ilaaha illa Allaahu wahdahuu laa shariyka lahu, lahul Mulku walahul Hamdu, wa Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr. Al-Hamdu lil Laah, wa Subhaana Allaah, wa laa ilaaha illa Allaahu, wa Allaahu Akbar, wa laa hawla walaa quwwata illaa bil Laah. Kisha akasema: Allaahumma Ighfir liy, au akaomba, du’aa yake hujibiwa. Na kama atatawadha akaswali, Swalaah yake hukubaliwa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1154), At-Tirmidhiy (3414), Abu Daawuud (5060) na Ahmad (5/313)].
(c) Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Abbaas akisema: “Nililala kwa khalati yangu Maymuunah mke wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Mimi nililalia mto kwa upana, na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na mkewe wakalalia kwa urefu. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akalala, na ilipoingia katikati ya usiku – au kabla yake kwa kidogo au baada yake kwa kidogo – aliamka, akakaa akiupangusa uso wake kwa mkono wake kutoa usingizi. Kisha akazisoma Aayah kumi za mwisho za Suwrat Aal-‘Imraan. Halafu akaenda kwenye kiriba cha ngozi, akatawadhia maji yake wudhuu kamili uliotimia, kisha akasimama kuswali…..” [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (183) na Muslim (763)]
Aayah zinazokusudiwa hapa ni:
((إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ....))
..mpaka mwisho wa Suwrat Aal-‘Imraan.
8- Apige mswaki
Imepokelewa toka kwa Hudhayfah akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapoamka usiku (katika riwaya nyingine: kwa ajili ya tahajjud), alikuwa akisafisha kinywa chake kwa mswaki”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (246) na Muslim (255)].
Na imepokelewa toka kwa Ibn ‘Abbaas kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Alikuwa akiswali usiku rakaa mbili mbili, kisha huondoka akaenda kupiga mswaki”. [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Maajah (228) na Ahmad (1784), nayo iko katika Swahiyhul Jaami’i (4837)].
Yaani hupiga mswaki kila baada ya rakaa mbili.
Mswaki unaweza kupigwa baada ya kuamka au baada ya kutawadha, na kila moja lina sababu yake.
9- Afungue Swalaah yake kwa kuswali rakaa mbili fupi
Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaposimama usiku kuswali, hufungua Swalaah yake kwa rakaa mbili khafifu”. [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (767) na Ahmad (22890)].
Imepokelewa na Abu Hurayrah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Anaposwali mmoja wenu usiku, basi afungue Swalaah yake kwa rakaa mbili khafifu)). [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (768), Abu Daawuud (1323) na At-Tirmidhiy katika Ash-Shamaail (265)].
Sababu ya rakaa mbili hizi ni kuuchangamsha mwili kwa ajili ya rakaa zinazofuatia. Hivi ndivyo bora zaidi, na kama hawezi, basi hapana ubaya kufungua kwa rakaa mbili ndefu, kwani Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwahi kufanya hivyo wakati fulani kama inavyothibitisha Hadiyth ya Hudhayfah asemaye: “Niliswali na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) usiku mmoja, akafungua kwa Al-Baqarah nikadhani atarukuu katika Aayah 100 za mwanzo, naye akapitiliza. Nikadhani ataimaliza Suwrah yote katika rakaa moja, naye akapitiliza. Nikadhani atarukuu kabla hajaimaliza, kisha akaianza An-Nisaa akaisoma, kisha akaingia Aal-‘Imraan, akaisoma, naye akaisoma kwa utuvu na kwa kituo”. [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (772), An Nasaaiy (1664) na Abu Daawuud (874)].
10- Aifungue Swalaah yake ya usiku kwa moja ya du’aa zifuatazo baada ya takbiyr:
(a) Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Abbaas akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaposimama usiku kuswali tahajjud husema:
(( اللهم لك الحمد أنت قيم السموات والأرض ومن فيهن، ولك الحمد أنت نور السموات والأرض ومن فيهن، ولك الحمد أنت ملك السموات والأرض ومن فيهن، ولك الحمد، أنت الحق ووعدك الحق، ولقاؤك حق، وقولك حق، والجنة حق، والنار حق، والنبيون حق، ومحمد حق، والساعة حق، اللهم لك أسلمت، وبك آمنت، وعليك توكلت، وإليك أنبت، وبك خاصمت، وإليك حاكمت، فاغفر لي ما قدمت وما أخرت، وما أسررت وما أعلنت، ] وما أنت أعلم به مني [ أنت المقدم، وأنت المؤخر، لا إله إلا أنت، ولا إله غيرك، ولا حول ولا قوة إلا بالله))
Allaahumma lakal hamdu Anta Qayyimus Samaawaati wal Ardhi waman fiyhinna, wa lakal hamdu Anta Nuurus Samaawaati wal Ardhi waman fiyhinna, wa lakal hamdu Anta Malikus Samaawaati wal Ardhi waman fiyhinna, wa lakal hamdu, Anta Al-Haqqu wa wa’adukal haqqu, wa liqaauka haqqun, wa qawluka haqqun, wal Jannatu haqqun, wan Naaru haqqun, wan Nabiyyuwna haqqun, wa Muhammadun haqqun, was Sa’atu haqqun. Allaahumma laka aslamtu, wa bika aamantu, wa ‘alayka tawakkaltu, wa ilayka anabtu, wa bika khaaswamtu, wa ilayka haakamtu, Faghfirliy maa qaddamtu wamaa akh-khartu, wa maa asrartu wa maa a’alantu, [wamaa Anta A’alamu bihii minniy] Anta Al-Muqaddimu, wa Anta Al-Muakh-khiru, laa ilaaha illaa Anta, walaa ilaaha ghayruka, walaa hawla walaa quwwata illaa bil Laahi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1069) na Muslim (769)].
(b) Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiifungua Swalaah yake anaposwali usiku kwa kusema:
(( اللهم رب جبريل وميكائيل وإسرافيل فاطر السموات والأرض، عالم الغيب والشهادة، أنت تحكم بين عبادك فيما كانوا فيه يختلفون، اهدني لما اختلف فيه من الحق بإذنك، إنك تهدي من تشاء إلى صراط مستقيم ))
Allaahumma Rabba Jibryla wa Miykaaiyla wa Israafiyla Faatwiras Samaawaati wal Ardhi, ‘Aalimal ghaybi wash shahaadati, Anta Tahkumu bayna ‘ibaadika fiymaa kaanuw fiyhi yakhtalifuwna, Ihidiniy limakhtulifa fiyhi minal haqqi bi idhnika. Innaka Tahdiy ilaa swiraatwin mustaqiymin)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (770)].
(c) Imepokelewa na Hudhayfah kwamba yeye alimwona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiswali usiku na alikuwa anasema:
(( الله أكبر (ثلاثا) ذو الملكوت والجبروت والكبرياء والعظمة))
(( Allaahu Akbar (mara tatu), Dhul Malakuwti wal Jabaruwti wal Kibriyaai wal ‘Adhwamati)). [Albaaniy kasema ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud ( 873) na An-Nasaaiy (1069). Angalia Al-Mishkaat (1200)].
Ninasema: “Ana khiyari ya kuomba du’aa yoyote aitakayo kati ya du’aa nyingine za kufungulia Swalaah tulizozitaja katika mlango wa “Mawajibiko ya Swalaah”.
11- Arefushe kisimamo awezavyo bila ya kujitia uzito
Imepokelewa toka kwa Jaabir kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( أفضل الصلاة طول القنوت))
((Swalaah bora zaidi ni yenye kisimamo kirefu zaidi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (756) na wengineo].
An Nawawiy kasema: “Makusudio ya “qunuwt” hapa ni kisimamo kwa makubaliano ya Maulamaa kwa mujibu wa ninavyojua. Ash-Shaafi’iy ana dalili pamoja na yule anayesema kama yeye. Anasema: “Kurefusha kisimamo ni bora zaidi kuliko kukithirisha rukuu na sijdah”.
Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akirefusha kisimamo. Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisimama usiku mpaka miguu yake ikavimba…”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (3748) na Muslim (2820)].
Tushaeleza nyuma katika Hadiyth ya Hudhayfah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisoma Al-Baqarah, An-Nisaai na Aal-‘Imraan katika rakaa moja.
Aidha, imepokelewa na Ibn Mas-’oud akisema: “Niliswali pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), akarefusha mpaka nikadhamiria kufanya jambo baya”. Akaulizwa: “Ulidhamiria nini?” Akajibu: “Niliazimia kukaa nimwache”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1135) na Muslim (773)].
Al-Haafidh katika Al Fat-h (3/19) anasema: “Katika Hadiyth, kuna dalili kwamba kurefusha Swalaah za usiku, ni chaguo lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na Ibn Mas-’oud alikuwa imara mwenye kuhifadhi kumfuata Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Naye hakuazimia kukaa ila baada ya kisimamo kupindukia zaidi ya alivyozoea”.
· Faida
Kurefusha hakuhusiani na kisomo tu, bali kumesuniwa vile vile katika rukuu, sijdah, kikao, dhikr, du’aa na katika vipengele vyote vya Swalaah. Katika Hadiyth ya Hudhayfah inayoelezea kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisoma Al-Baqarah, An-Nisaai na Aal-‘Imraan katika rakaa moja, Hadiyth inaendelea ikisema: “Kisha alirukuu akawa anasema: “Subhaana Rabbiya Al-‘Adhiymi”, na rukuu yake ilikuwa takriban sawa na kisimamo chake, kisha akasema: “Sami’a Allaahu liman Hamidah”, kisha akasimama sana takriban sawa na alivyorukuu, kisha akasujudu akasema: “Subhaana Rabbiyal A’alaa”, na sijdah yake ilikuwa kiasi cha kisimamo chake”. [“Takhriyj” yake ishaelezwa].
Na katika Hadiyth ya ‘Aaishah: “Anabakia katika sijdah yake kiasi cha mtu kusoma Aayah hamsini kabla hajanyanyua kichwa chake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1336), Ibn Maajah (1358) na Ahmad (6/83)].
Ninasema: “Kurefusha huku kisomo na nguzo nyinginezo, si sharti katika Swalaah ya usiku, bali kufanya hivyo ni bora na ukamilifu zaidi kwa mwenye kuweza. Katika baadhi ya nyakati, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisoma katika kila rakaa kiasi cha Aayah 50 au zaidi.. [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (994)]…na alikuwa akisema:
(( من صلى ليلة بمائة آية لم يكتب من الغافلين ))
((Mwenye kuswali usiku kwa Aayah mia moja, hatoandikwa kati ya watu wenye kughafilika)). [Albaaniy kasema ni Hadiyth Swahiyh. Angalia Asw-Swahiyhay (643) na Swahiyhut Targhiyb (636)].
12- Anaweza kuswali kwa kusimama au kukaa. Zimekuja kwa njia sahihi aina tatu za namna alivyokuwa akiswali Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) usiku:
Ya kwanza: Alikuwa akiswali kwa kusimama kama ilivyobainika katika Hadiyth zilizotangulia.
Ya pili: Alikuwa akiswali kwa kukaa, na anarukuu kwa kukaa. Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakufa mpaka zikawa Swalaah zake nyingi ni kwa kukaa”. [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraj” na Muslim (735) na An-Nasaaiy (1656)].
Na katika riwaya nyingine, ni kuwa alifanya hivi aliponenepa na kupata mwili.
Pia ‘Aaishah amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaswali usiku mrefu kwa kusimama, na usiku mrefu kwa kukaa. Anaposwali kwa kusimama, hurukuu akiwa amesimama, na anaposwali kwa kukaa, hurukuu akiwa amekaa”. [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraj” na Muslim (730), Abu Daawuud (955) na An-Nasaaiy (3/219)].
Ya tatu: Alikuwa akisoma huku amekaa, na inapobakia kidogo katika kisomo chake, husimama akarukuu akiwa amesimama. Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaswali kwa kukaa, na husoma huku amekaa. Na inapobakia kiasi cha Aayah thelathini au arobaini, husimama akasoma huku amesimama, kisha hurukuu, halafu husujudu, kisha hufanya katika rakaa ya pili hivyo hivyo”. [Hadiyth Swahiyhy: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1118) na Muslim (731) na tamko ni lake].
13- Anapohisi uvivu, au kuchoka, au kulemewa na usingizi, basi alale na anapochangamka aswali.
Imepokelewa na Anas akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia Msikitini akakuta kamba imefungwa kati ya nguzo mbili akauliza: ((Nini hii?)) Wakajibu: “Ni ya Zaynab anaposwali. Anapohisi uvivu au kuchoka, huikamata”. Akasema: ((Ifungueni, aswali mmoja wenu anapokuwa mchangamfu, akihisi uvivu au kuchoka, basi alale)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1150) na Muslim (784)].
Imepokelewa na ‘Aaishah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( إذا نعس أحدكم في الصلاة، فليرقد حتى يذهب عنه النوم، فإن أحدكم إذا صلى وهو ناعس، لعله يذهب يستغفر فيسب نفسه))
((Akisinzia mmoja wenu wakati anaswali, basi alale mpaka usingize umwishe, kwani anaposwali mmoja wenu huku anasinzia, anaweza akaona kwamba anastaghfir kumbe anajitusi mwenyewe)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (212) na Muslim (786)].
Pia Abu Hurayrah anasema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( إذا قام أحدكم من الليل، فاستعجم القرآن على لسانه، فلم يدر ما يقول: فليضطجع))
((Anaposwali mmoja wenu usiku, Qur-aan ikakanganyika ulimini mwake asiweze kukijua anachokisoma, basi alale)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhaaj” na Muslim (787), Abu Daawuud (1311) na Ibn Maajah (1372)].
14- Airattil Qur-aan na aipambe sauti yake
Allaah Anasema:
((أَوْ زِدْ عَلَيْهِ وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلًا))
((Au izidishe, na soma Qur-aan kwa kisomo cha utaratibu upasao, kuitamka vizuri na kutaamali)) [Al-Muzzammil (73:4)].
Imepokelewa toka kwa Hafswah akisema: “Rasuli wa Allaah alikuwa akisoma Suwrah akiirattil mpaka inakuwa ndefu kuliko iliyo ndefu yake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (733), Maalik (311) na An-Nasaaiy (1658)].
Naye Ya’alaa bin Mamlak alimuuliza Ummu Salamah namna kisomo cha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kinavyokuwa na anavyoswali. Ummu Salamah akakielezea kisomo chake akawa anakisifu kiuchambuzi herufi kwa herufi. [Al-Albaaniy kasema ni Hadiyth Swahiyh: Angalia Al-Mishkaat (1210) na Swifatus Swalaat (uk 124)].
Anakusudia uratili bora na kisomo murua.
Qataadah anasema: Nilimuuliza Anas: Ni vipi Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anasoma?” Akasema: “Kisomo chake kilikuwa ni kuvuta”. Kisha akasoma: Bismil Laahi Ar Rahmaan Ar Rahiym: Anavuta Bismil Laahi, anavuta Ar Rahmaan, na anavuta Ar Rahiym”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (5046), An-Nasaaiy (1014) Abu Daawuud (1465) kwa muhtasari, Ibn Maajah (1353) na Ahmad (11835)].
Makusudio ni kuwa alikuwa akivuta herufi za “madda” na “al liyn” katika matamshi yake kwa kipimo kinachojulikana.
Ummu Salamah anasema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikikata kisomo chake Aayah kwa Aayah: ((Al Hamdu lil Laahi Rabbil ‘Aalamiyna) kisha anasimama, (Ar Rahmaan Ar Rahiym) kisha anasimama”. [Al-Albaaniy kasema ni Hadiyth Swahiyh: Angalia Swahiyhul Jaami’i (4876)].
Imesuniwa aghani akisoma Qur-aan kutokana na Hadiyth ya Abu Hurayrah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Si katika sisi asiyeghani akisoma Qur-aan)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (7527). Kana kwamba iliyo Swahiyh toka kwa Abu Hurayrah, ni Hadiyth inayofuatia. Lakini pamoja na hivyo, wameifanyia “ikhraaj” kwa tamko hili akina Abu Daawuud (1469), Ahmad (1396) na wengineo toka kwa Sa’iyd na wengineo kwa tamko lake]
Na pia kutoka kwa Abu Hurayrah amesema kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( ما أذن الله لشيء ما أذن لنبي حسن الصوت يتغنى بالقرآن يجهر به))
((Allaah Hakusikiliza kitu kama Anavyomsikiliza Nabii mwenye sauti nzuri, anayeghani vizuri kwa kuisoma Qur-aan kwa sauti)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (5023) na Muslim (792)].
Maana ya kughani ni kuirembesha sauti kwa kuinyanyua na kwa kiimbo kwa picha ya kuhuzunika, kwa namna itakayozilainisha nyoyo na kububujisha machozi lakini kwa sharti ya kutopetuka wigo uliowekwa na mabingwa wa taaluma ya visomo. Ama kuvuta sana kisomo na kuingiza madoido ya kuchupa hadi kuyatoa maneno nje ya mahala pake, hilo ni makruhu kwa mujibu wa Jamhuri ya Maulamaa. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
· Je, Kisomo Ni Kwa Sauti Au Kwa Sauti Ya Chini?
Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisoma kwa sauti ya chini katika Swalaah za usiku baadhi ya nyakati, na wakati mwingine akisoma kwa kunyanyua sauti. Imepokelewa toka kwa ‘Abdullaah bin Abiy Qays akisema: “Nilimuuliza ‘Aaishah: Je, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisoma kwa kunyanyua sauti katika Swalaah yake au akisoma kwa sauti ya chini? Akajibu: Alikuwa akisoma kwa kunyanyua sauti, na alikuwa akisoma kwa sauti ya chini. Nikasema: Allaahu Akbar, namshukuru Allaah Aliyefanya wasaa katika jambo hili”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (307), An-Nasaaiy (1199), Abu Daawuud (1437) na Ahmad (6/73)].
Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Abbaas akisema: “Kisomo cha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kilikuwa kinaweza kusikika na aliyeko chumbani, naye akiwa nyumbani”. [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1327), At-Tirmidhiy katika Ash-Shamaail (275-muhtasar) na Ahmad (1/271)].
Yaani Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifanya wastani kati ya kunyanyua na kuteremsha sauti.
Ninasema: “Hili ndilo linalopendeza. Imepokelewa toka kwa Abu Qataadah akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka usiku na mara akamkuta Abu Bakri anaswali kwa sauti ya chini. Akapita kwa ‘Umar akamkuta anaswali kwa sauti ya juu. Na wawili hao walipokutana kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Rasuli alisema: ((Ee Abu Bakr! Nimekupitia nawe unaswali kwa sauti ya chini)). Akasema: “Nimemsikilizisha niliyemnong’oneza ee Mjumbe wa Allaah! Akamwambia ‘Umar: ((Nimekupitia nawe unaswali kwa sauti ya juu)). Akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Ninamzindusha aliyelala usingizi wa mang’amung’amu, na ninamfukuza shaytwaan”. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Ee Abu Bakr! Nyanyua sauti yako kidogo)). Na akamwambia ‘Umar: ((Punguza kidogo sauti yako)). [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1329) na At-Tirmidhiy (447)].
Hivi ndivyo ulivyokuwa usikilizaji wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wa Qur-aan kwa sauti za Ma’ashaairah, na Abu Muusa wakati alipokuwa akisoma usiku akamwambia: ((Ee Abu Muusa! Laiti ungeniona nami nakusikiliza kisomo chako jana. Hakika umepewa sauti nzuri ajabu kama sauti ya ukoo wa Daawuud)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (1322)].
An Nawawiy amesema: “Zimekuja Hadiyth kuhusiana na fadhila za kusoma kwa sauti, na athar kuhusiana na fadhila za kusoma kwa sauti ya chini. Maulamaa wamesema: Kuoanisha kati ya mawili haya ni kuwa kusoma kwa sauti ya chini kunakuwa mbali zaidi na riyaa, nako kunakuwa ni bora zaidi kwa anayechelea hilo. Na kama mtu hachelei hilo, basi kusoma kwa sauti ni bora lakini kwa sharti kwamba asisababishe kero kwa mwingine mwenye kuswali, au aliyelala au mwingineyo”.
15- Atadaburi Aayaat, ajilinde, asabbih katika kisomo, na alie katika Swalaah
(a) Imekuja katika Hadiyth ya Hudhayfah aliposwali pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “..anasoma kwa utuvu na kwa kituo, akiipita Aayah yenye tasbiyh husabbih, akiipitia yenye maombi huomba, akiipita ya kujilinda, hujilinda….”. [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (1010) na Ibn Maajah (1350). Angalia Swifatus Swalaahat uk. 121].
“Inatakikana kwa Waumini wote wawe hivyo, bali wawe zaidi kuliko yeye. Ikiwa Allaah Amemghufiria madhambi yake yaliyopita na yajayo, basi wao wamo hatarini”. [Faydhul Qadiyr cha Al-Minaawiy (5/160) chapa ya Al-Maktabat At-Tijaariyyah]
(b) Imepokelewa toka kwa Abu Dharri akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikesha akiikariri Aayah moja mpaka Alfajiri. Aayah yenyewe ni:
(( إِن تُعَذِّبْهُمْ فَإِنَّهُمْ عِبَادُكَ ۖ وَإِن تَغْفِرْ لَهُمْ فَإِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ))
(c) Imepokelewa toka kwa ‘Abdullaah bin Ash-Shukhayr akisema: ”Nilimjia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa anaswali, na kifuani mwake kuna mvumo kama mvumo wa maji yachemkayo chomboni [kwa sababu ya kulia]”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (904), An-Nasaaiy (1214) na Ahmad (15722)].
(d) Tulielezea nyuma kauli ya ‘Aaishah – wakati Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomwamuru Abu Bakr awaswalishe watu – isemayo: “Abu Bakr ana moyo laini, na anaposimama mahala pako, watu hawamsikii….” [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (664) na Muslim (418)].
Yaani kwa sababu ya kulia. Na katika riwaya nyingine: “Hakika Abu Bakri ana moyo laini, anaposoma hawezi kujizuia kulia..”.
(e) ‘Abdullaah bin Shaddaad amesema: “Niliusikia mkwamo wa kilio kwa ‘Umar nami niko swafu ya mwisho akisoma:
(( قَالَ إِنَّمَا أَشْكُو بَثِّي وَحُزْنِي إِلَى اللَّـهِ وَأَعْلَمُ مِنَ اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ))
[Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy ikiwa Mu’allaq, na Sai’yd bin Mansour ameifanya Mawsuwl (1138), Ibn Abu Shaybah (5/405), ‘Abdur Raaziq (2/114) na Al-Bayhaqiy katika Ash-Sha’ab (2/364). Sheikh wa Uislamu (22/623) amesema: “Athar hii imehifadhiwa toka kwa ‘Umar”]
16- Akithirishe du’aa – saa za mwisho wa usiku – ndani ya Swalaah na nje ya Swalaah
Kutokana na kama tulivyoeleza kwamba katika nyakati hizi Mola (Tabaaraka wa Ta’alaa) Huteremka katika wingu wa dunia kwa ajili ya kumjibu mwombaji du’aa na kumpa mtaka haja, haja yake.
Imepokelewa toka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( إن في الليل لساعة، لا يوافقها رجل مسلم يسأل الله خيرا من أمر الدنيا والآخرة إلا أعطاه إياه وذلك كل ليلة ))
((Hakika katika usiku kuna saa, haisadifu saa hiyo Muislamu akimwomba Allaah kheri yoyote katika mambo ya dunia au aakhirah isipokuwa Humpa, na hiyo ni kila usiku)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (757)].
Tushazitaja nyuma du’aa za Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakati anapoianza Swalaah yake ya usiku.
Imesuniwa akithirishe zaidi du’aa katika sijdah, kwani hapo ndipo penye uhakika zaidi wa kujibiwa. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( أقرب ما يكون العبد من ربه وهو ساجد، فأكثروا فيه من الدعاء ))
((Wakati ambao mja huwa karibu zaidi na Mola wake, ni pale anapokuwa amesujudu, basi kithirisheni hapo du’aa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (482), An-Nasaaiy (1137) na Abu Daawuud (875)].
Na anasema tena:
(( أما السجود، فأكثروا من الدعاء فيه، فقمن أن يستجاب لكم))
((Ama sijdah, basi kithirisheni kuomba du’aa hapo, kwani ni stahikivu kwenu kujibiwa humo du’aa )). [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa katika mlango wa “Mawajibiko ya Swalaah”].
Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah akisema: “Nilimkosa Rasuli wa Allaah ((Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)) usiku kitandani. Nikapapasa kumtafuta na mkono wangu ukagusa tumbo la nyayo zake mbili zikiwa zimesimamishwa na yeye yuko katika sijdah. Alikuwa akisema:
((اللهم أعوذ برضاك من سخطك، وبمعافاتك من عقوبتك، وأعوذ بك منك، لا أحصي ثناء عليك، أنت كما أثنيت على نفسك))
((Allaahumma a’uwdhu bika biridhwaaka min sakhatwika, wa bimu’aafaatika min ‘uquwbatika, wa a’uwdhu bika minka, laa uhswiy thanaan ‘alayka, Anta kamaa Athnayta ‘alaa nafsika)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (486) na wengineo].
17- Imesuniwa kumwamsha mke kuswali usiku
Hili limezungumziwa katika mlango wa “Fadhila za kuswali usiku”.
18- Alale baada ya kuswali na kabla ya Alfajiri
Ili iwe ni kama kitenganishi kati ya Swalaah ya Sunnah na Swalaah ya faradhi. Kulala huku huleta uchangamfu wa kuiswali Swalaah ya Alfajiri, kwa kuwa ikiwa mtu ataunganisha Swalaah ya usiku na Swalaah ya Alfajiri, hatokuwa na dhamana ya kupata uchangamfu na khushuu wakati wa kuswali kutokana na tabu na mchoko. Dalili za kupendezeshwa hili zimeelezwa katika mlango wa “Witr”.
19- Ni karaha kuacha kuswali usiku kwa mtu aliyezoea
Imepokelewa toka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amri akisema: “ Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia: ((Ee ‘Abdullaah! Usiwe kama fulani. Alikuwa akiswali usiku akaacha kuswali usiku)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1152) na Muslim (1159)].
· Qiyaamul Layl Wakati Wa Misukosuko
Majanga yanaposhitadi, mambo yakashindikana, hapo inakuwa hakuna tena njia isipokuwa kugonga mlango wa Mfalme Mwenye Kumiliki hatamu ya kila kitu, kusimama mbele yYake na kumwomba kwa unyenyekevu ndani ya giza totoro.
Imepokelewa toka kwa ‘Aliyy (Radhwiya Allaahu Anhu) akisema: “Hakuna aliyekuwa amepanda farasi Siku ya Badr isipokuwa Al-Miqdaad. Ungeshangaa ungetuona, hakuna yeyote katika sisi isipokuwa alilala ila Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) chini ya mti akiswali na akilia mpaka pakapambauka”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (973). Angalia Swahiyhut Targhyb (546)].
Imepokelewa toka kwa ‘Amri bin Shu’ayb toka kwa baba yake toka kwa babu yake akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika mwaka wa Vita vya Taabuk, alisimama usiku akaswali. Maswahaba wakakusanyika nyuma yake wakimchunga mpaka akamaliza kuswali na kujumuika nao”. [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (6771)].
· Idadi Ya Rakaa Za Qiyaamul Layl
1- Idadi inayopendeza
Imesuniwa idadi ya rakaa za Qiyaamul Layl isizidi rakaa 11 au 13. Idadi hii ndio aliyojichagulia mwenyewe Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
(a) Imepokelewa toka kwa Masrouq akisema: “Nilimuuliza ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu Anha) kuhusiana na Swalaah ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) usiku. Akasema: Ni saba, tisa na kumi na moja pasina rakaa mbili za Alfajiri”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1139)].
(b) Ibn Salamah bin ‘Abdur Rahmaan naye alimuuliza, ‘Aaishah akasema: “Hakuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akizidisha zaidi ya rakaa kumi na moja, si katika Ramadhwaan au katika miezi mingineyo. Huswali nne, usiulize vipi uzuri wake na vipi urefu wake, kisha huswali nne, usiulize vipi uzuri wake na vipi urefu wake, kisha huswali tatu”. [Hadiyth Swahiyh: Imeelezwa karibuni].
(c) Ibn ‘Abbaas amesema: “Swalaah ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ilikuwa ni rakaa 13, yaani usiku”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1138) na Muslim (764)].
(d) Imepokelewa toka kwa Zayd bin Khaalid Al-Juhaniy akisema: “Hakika niliifuatilia kwa macho Swalaah ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), akaswali rakaa mbili khafifu, kisha akaswali rakaa mbili ndefu ndefu ndefu, halafu akaswali rakaa mbili si ndefu kama za kabla yake. Kisha akaswali rakaa mbili si ndefu kama za kabla yake, halafu akaswali rakaa mbili si ndefu kama za kabla yake, kisha akaswali rakaa mbili si ndefu kama za kabla yake, halafu akaswali Witr. Na hizo ni rakaa kumi na tatu”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (765)].
Baadhi ya Maulamaa wanasema kwamba Swalaah ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ilikuwa ni rakaa kumi na moja. Ama rakaa mbili za mwisho, baadhi wamesema ni rakaa mbili za Alfajiri, na wengine wamesema ni rakaa mbili za Sunnah ya ‘Ishaa. Hili likipita katika baadhi ya riwaya, basi halipiti kwenye riwaya nyinginezo. Na wengine wamesema ni rakaa mbili ambazo Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifungulia kwazo Swalaah yake. Huenda kauli hii ikawa na mwelekeo bora zaidi. [Ni kauli aliyoichagua Al-Haafidh katika Al Fat-h (3/21)]
2- Je, inajuzu kuongeza zaidi ya idadi hii?
Suala hili limezusha mvutano kati ya wanafunzi ambao bado hawajakomaa kielimu na ndugu zetu wenye pupa ya kuifuata Sunnah ya Rasuli. Wanasema kwamba haijuzu kuzidisha zaidi ya rakaa kumi na moja wakimfuata mmoja kati ya Maulamaa Wakubwa wa enzi yetu ya leo. Huenda ‘Aalim huyu kwa kufanya hivi, amepata thawabu moja.
Lakini Jamhuri ya Salaf na Khalaf wanasema kwamba inajuzu kuzidisha zaidi ya idadi hii wakisisitiza kwamba kufanya hivyo ni Sunnah. Na kwa ajili hiyo, Al-Qaadhwiy ‘Ayyaadh anasema: “Hakuna mvutano wa kusema kwamba kuna mpaka maalumu wa kutozidishwa au kutopunguzwa katika hilo, na kwamba Swalaah ya usiku ni katika ‘ibaadah ambazo kila rakaa zinavyoongezeka, na ndivyo thawabu nazo zinavyoongezeka. Lakini mabishano yapo katika kitendo chake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na hilo alilojichagulia yeye mwenyewe. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
Ibn ‘Abdul Barri amesema katika At-Tamhiyd: “Hakuna kabisa mahitalifiano kati ya Waislamu kwamba Swalaah ya usiku haina mpaka maalumu, na kwamba Swalaah hiyo ni ya Sunnah, na ni kitendo cha kheri na amali njema. Mwenye kutaka atakalilisha na mwenye kutaka atakithirisha”.
Ninasema: “Yenye kuonyesha usahihi wa msimamo huu ni haya yafuatayo: [Sheikh wetu Mustwafa Al-‘Adawiy – Allaah Ainyanyue daraja yake – ana tasnifu murua inayozungumzia kuhusu “Idadi ya rakaa za Swalaah ya Usiku”. Katika tasnifu hii, amelimaliza na kulifungia kazi suala hili, nami nimefaidika sana nayo]
1- Neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Swalaah ya usiku ni rakaa mbili mbili, ukichelea Alfajiri, basi swali Witr rakaa moja)). [Hadiyth Swahiyh:”Takhriyj” yake ishaelezwa nyuma].
2- Neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Jisaidie mwenyewe kwa kukithirisha sijdah)). [Hadiyth Swahiyh:”Takhriyj” yake ishaelezwa nyuma].
3- Neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Hakika wewe hutosujudu sijdah moja kwa ajili ya Allaah, isipokuwa Allaah Atakunyanyulia kwayo daraja moja na kukupomoshea kwayo kosa moja)). [Hadiyth Swahiyh:”Takhriyj” yake ishaelezwa nyuma].
4- Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kujichagulia mwenyewe idadi hii, hakumaanishi kuwa idadi iwe ni hiyo hiyo tu kutokana na haya yafuatayo:
(a) Kitendo chake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakihusishi kauli yake kama inavyoelezwa katika taaluma ya Uswuul.
(b) Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakukataza kuzidisha zaidi ya rakaa kumi na moja, bali ametuainishia Swalaah ambayo Allaah Anaipenda zaidi, nayo ni Swalaah ya Daawuud Alayhis Salaam katika theluthi ya usiku.
Na kwa ajili hiyo, Sheikh wa Uislamu (22/272-273) amesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuweka idadi maalum ya rakaa katika Qiyaam Ramadhwaan, na yeye hakuwa akizidisha zaidi ya rakaa kumi na tatu katika Ramadhwaan na katika miezi mingineyo yote, lakini alikuwa akirefusha sana rakaa. Na mwenye kudhani kwamba Qiyaam Ramadhwaan ina idadi maalumu iliyowekwa na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) isiyozidishwa wala kupunguzwa, basi amekosea.
(c) Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakumwamuru anayeswali usiku kuswali kwa idadi hii. Na lau kama tutajaalia kwamba aliamuru – na hili hakuna aliyelisema – basi haifai vile vile ahusishe ujumuishi wa dalili zilizotangulia kutokana na yaliyobainishwa katika taaluma ya Uswuul ya kuwa cha jumla hakiainishwi na moja ya vipengele vyake isipokuwa wakati wa kukinzana.
5- Mwenye kutaka kwenda sawia na Sunnah ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), basi ni lazima aende nayo sambamba kihesabu, kisifa, kiidadi na kinamna. Na nyuma tumeelezea namna Rasuli alivyokuwa akirefusha Swalaah ya usiku akiswali idadi hii ya rakaa. Mtu akiziangalia Aayah zilizogusia nyuma kuhusu fadhila za Qiyaamul layl, atakuta kwamba mhimili wake ni muda wa kisimamo. Basi ikiwa mtu anayetaka kwenda sawia na Sunnah ya Rasuli hawezi urefushaji huo – na hususan ikiwa anawaswalisha watu - je tutamzuia kuongeza idadi ya rakaa ili iwe nafuu kwake na kwa wanaomfuata, na chachu kwake ya kuweza kusimama theluthi ya usiku?!! Na je aliyeswali rakaa kumi na moja kwa muda wa saa moja ni bora kuliko aliyeswali rakaa ishirini au zaidi au chini ya hapo kwa muda wa saa nne?!!
Naam, hakuna mabishano ya kwamba lau kama atakwenda sawia na Sunnah katika idadi na wakati basi hilo ni bora, na kama hawezi basi ataswali kwa mujibu wa itakavyokuwa wepesi kwake.
6- Imethibiti kwamba ‘Umar bin Al-Khattwaab aliwakusanya watu katika Qiyaam Ramadhwaan (Tarawehe). Watu hawa waliswalishwa na Ubayya bin Ka’ab na Tamiym Ad Daariy kwa rakaa ishirini na moja. Walikuwa wakisoma Suwrah ndefu na kuondoka wakati Alfajiri inapokurubia. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdur Razzaaq (7730) na Ibn Al-Ja’ad (2926), na kupitia kwake Al-Bayhaqiy (2/496). Wao wanasema ni rakaa ishirini]
Imethibiti vile vile kwamba aliwakusanya kuswali rakaa kumi na moja kama itakavyokuja kuelezwa katika mlango wa Tarawehe.
· Kulipa Qiyaamul Layl
Imesuniwa kuilipa Qiyaamul Layl mchana kabla ya Adhuhuri kwa aliyezoea ikiwa itampita kwa sababu ya usingizi au ugonjwa. Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali mchana rakaa kumi na mbili ikiwa atapitwa na Swalaah ya usiku kwa sababu ya maumivu au jinginelo. [Hadiyth Swahiyh: Imeelezwa katika mlango wa “Kulipa Witr”].
Imepokelewa toka kwa ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu Anhu) akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( من نام عن حزبه أو عن شيئ منه، فقرأه بين صلاة الفجر وصلاة الظهر، كتب له كأنما قرأه من الليل))
((Mwenye kulala asifanye uradi wake, au sehemu ya uradi huo, halafu akaja kuusoma kati ya Swalaah ya Alfajiri na Swalaah ya Adhuhuri, huandikiwa kama aliyeusoma usiku)). [Hadiyth Swahiyh: Imeelezwa katika mlango wa “Kulipa Witr”].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
026-Qiyaam Ramadhwaan (Tarawehe)
Alhidaaya.com [3]
· Fadhila Yake Na Kuruhusika Kwake
Swalaah ya Tarawehe ni Sunnah iliyokokotezwa kwa wanaume na wanawake katika mwezi wa Ramadhwaan, nayo ni moja kati ya alama mashuhuri za dini. [Raddul Mukhtaar (1/472), Haashiyatul ‘Adawiy (1/352) na Al-Majmu’u (4/31)] Na Swalaah hii ndiyo inayokusudiwa na neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
(( من قام إيمانا واحتسابا غفر له ما تقدم من ذنبه))
((Mwenye kusimama hali ya kuwa na iymaan na kutafuta thawabu, husamehewa madhambi yake yaliyopita)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (2009) na Muslim (759)].
Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliiswali pamoja na Maswahaba wake katika baadhi ya masiku lakini hakuendelea nayo kwa ajili ya kuchelea isije ikafaradhishwa kwao ikawashinda. Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah akisema: “ Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali Msikitini na watu wakaswali pamoja naye. Kisha akaswali usiku uliofuatia na watu wakakithiri zaidi. Halafu wakakusanyika usiku wa tatu lakini yeye hakutoka kuswali nao. Kulipopambazuka alisema: “Nimeona mlilolifanya, na hakuna lililonizuilia kutoka kuwajieni isipokuwa nimechelea Swalaah hii kufaradhishwa kwenu”. Na hii ni katika Ramadhwaan [Rasuli wa Allaah akafariki na hali ikabaki hivyo]” [Hadiyth Swahiyh:Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1129) na Muslim (761)].
· Jamaa Katika Tarawehe
Tumeeleza katika Hadiyth ya ‘Aaishah iliyopita kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali Tarawehe pamoja na Maswahaba wake katika baadhi ya masiku. Na imepokelewa toka kwa Abu Dharri akisema: “Tulifunga Ramadhwaan pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na yeye hakuswali nasi kwa chochote katika mwezi. Zilipobakia siku saba, aliswali nasi mpaka ikamalizika theluthi ya usiku, kisha katika usiku wa nne, hakuswali nasi. Na usiku uliofuatia, aliswali nasi mpaka ikamalizika takriban nusu ya usiku. Tukasema: Ee Rasuli wa Allaah! Kwa nini Usituswalishe usiku wetu huu uliobakia ukatupatisha thawabu zaidi? Akasema:
(( إن الرجل إذا قام مع الامام حتى ينصرف حسبت له بقية ليلته ))
((Hakika mtu atakaposimama pamoja na imamu mpaka akamaliza, basi huhisabiwa usiku uliobakia)).
Kisha usiku wa sita hakutuswalisha, lakini usiku wa saba alituswalisha. Halafu alikwenda kwa mkewe na watu wakakusanyika. Akatuswalisha mpaka tukaogopa kukosa daku”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1375), At-Tirmidhiy (806), An-Nasaaiy (3/202) na Ibn Maajah (1327)].
Mambo yaliendelea hivyo mpaka ilipokuja enzi ya ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu Anhu). Akawakusanya watu katika Tarawehe ili waswalishwe na imamu mmoja. Katika Hadiyth ya ‘Urwah bin Az Zubayr toka kwa ‘Aaishah anasema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alifariki na mambo yako hivyo, na yaliendelea hivyo hivyo katika Ukhalifa wa Abu Bakr mpaka mwanzoni mwa Ukhalifa wa ‘Umar. ‘Umar akawakusanya watu pamoja waswalishwe na Ubayya bin Ka’ab, naye akawaswalisha katika Ramadhwaan. Huo ukawa ndio mkusanyiko wa kwanza wa watu wakiswalishwa na imamu mmoja katika Ramadhwaan”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (924), An-Nasaaiy (4/155) na wengineo].
Imepokelewa toka kwa ‘Abdul Rahmaan bin ‘Abdul Qaadir akisema: “Tulitoka pamoja na ‘Umar bin Al-Khattwaab katika mwezi wa Ramadhwaan kwenda Msikitini. Tukawakuta watu makundi makundi wametawanyika; huyu anaswali peke yake, na mwingine anaswali na kundi la watu linamfuata. ‘Umar akasema: Mimi naona hawa wangelikusanywa waswalishwe na imamu mmoja ingelikuwa bora zaidi. Akapitisha shauri, akawakusanya pamoja waswalishwe na Ubayya bin Ka’ab. Usiku mwingine nilitoka naye tukawakuta watu wanaswalishwa na imamu mmoja. ‘Umar akasema: “Bid-’a njema kabisa hii, na ile wanayoiacha watu wakalala ni bora zaidi kuliko ile wanayoiswali –yaani mwisho wa usiku-, na watu walikuwa wakiswali mwanzoni mwa usiku”. [Hadiyth Swahiyh:Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (2010) na Maalik (252) na tamko ni lake].
Kisha Swalaah iliendelea kuswaliwa katika hali hii mpaka hivi leo. Na kwa ajili hiyo, Maulamaa wamekubaliana kwamba inaruhusika Tarawehe kuswaliwa kwa Jamaa.
· Idadi Ya Rakaa Za Tarawehe
Tumeshaeleza kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa hazidishi zaidi ya rakaa kumi na moja au kumi na tatu wakati anaposwali Qiyaamul Layl nyumbani kwake, si katika Ramadhwaan au katika miezi mingine.
“Ama masiku aliyoswali Tarawehe pamoja na Maswahaba wake, idadi ya rakaa haikutajwa, na hakuna Hadiyth Swahiyha inayoainisha idadi ya rakaa hizo”. [Al-Maswaabiyh Fiy Swalaat At Taraawiyh (uk 14-15) cha As-Suyuutwiy]
Na kwa ajili hiyo, Maulamaa wametofautiana kwa kauli nyingi katika kuainisha idadi ya rakaa za Tarawehe. Kati ya kauli hizo ni:
1- Rakaa kumi na moja
(a) Kwa kuwa ndiyo idadi aliyojichagulia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mwenyewe.
(b) As-Saaib bin Yaziyd anasema: “ ’Umar bin Al-Khattwaab alimwamuru Ubayya bin Ka’ab na Tamiym Ad Daariy wawaswalishe watu rakaa kumi na moja. Imamu alikuwa akisoma Suwrah inayozidi Aayah mia moja mpaka tukawa tunaegemea fimbo kutokana na urefu wa kisimamo, na tulikuwa hatuondoki isipokuwa mwanzoni mwa Alfajiri”. [Isnadi yake ni Swahiyh :Imefanyiwa “ikhraaj” na Maalik katika Al-Muwattwaa (1/115)].
2- Rakaa ishirini kutoa Witr
Hii ni kauli ya Maulamaa wengi kama Ath-Thawriy, Ibn Al-Mubaarak, Ash-Shaafi’iy na Abu Haniyfah na masahibu zake. Na hili limehadithiwa toka kwa ‘Umar, Aliyy na Maswahaba wengineo. [Sharhus Sunnat (4/120), Al-Badaai-’i (1/288), Al-Mughniy (1/208) na Al-Majmu’u (4/32-33)]
Dalili yao ni:
Yaliyokuja toka kwa As-Saaib bin Yaziyd (vile vile) akisema: “’Umar aliwakusanya watu waswalishwe na Ubayya bin Ka’ab na Tamiym Ad-Daariy kwa rakaa ishirini na moja, wanasoma Suwrah zenye Aayah zaidi ya mia moja, na wanaondoka mwanzoni mwa Alfajiri”. [Sijui kama athar hii na iliyo kabla yake moja inamtia walakini mwenzake, au zinabeba uwezekano wa kuwa ni matukio mawili tofauti]
Al-Kaasaaniy kasema: “ ’Umar aliwakusanya Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika mwezi wa Ramadhwaan chini ya uimamu wa Ka’ab, naye akawaswalisha rakaa 20. Hakuna yeyote aliyempinga, na kwa hivyo inakuwa ni Ijma’a ya wote juu ya hilo.”
3- Rakaa thelathini na tisa pamoja na Witr
Ni kauli ya Maalik aliyesema: [Al-Mudawwanah (1/193), na Sharhu Az-Zarqaaniy (1/284)]
“Hilo kwetu ni jambo la tangu zamani”. Hoja yake ni yale yaliyopokelewa toka kwa Daawuud bin Qays anayesema: “Niliwakuta watu wakati wa enzi ya ‘Umar bin ‘Abdul ‘Azizy na Abaan bin ‘Uthmaan wanaswali rakaa thelathini na sita, na wanaswali Witr rakaa tatu.” [Hadiyth Swahiyh:Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abu Shaybah (2/393) na Ibn Nasr katika Qiyaam Ramadhwaan (uk. 60)].
4- Rakaa arobaini na Witr rakaa saba
Al-Hasan bin ‘Abdullah amesema: “‘Abdul Rahmaan bin Al-Aswad alikuwa anatuswalisha katika mwezi wa Ramadhwaan rakaa arobaini na Witr rakaa saba”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abu Shaybah (2/393)].
Pia inaelezewa kwamba Ahmad bin Hanbali alikuwa akiswali katika mwezi wa Ramadhwaan rakaa zisizo na hesabu. [Kash-Shaaful Qinaa (1/425) na Matwaalibu Ulin Nuhaa (1/563)]
Ninasema: “Uhakikisho ni yale aliyoyasema Sheikh wa Uislamu Ibn Taymiyah (22/272/273):
“Na haya yote ni wasaa na ukunjufu. Idadi yoyote itakayoswaliwa kati ya hizi, inakuwa ni vizuri. Wingi wa idadi ya rakaa hutofautiana kwa mujibu wa hali ya waswaliji. Ikiwa wanaweza kuhimili kisimamo kirefu, basi kuswali rakaa kumi na rakaa tatu za baada yake kama alivyokuwa akiswali Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mwenyewe katika Ramadhwaan na katika miezi mingineyo itakuwa ni bora. Na kama hawakiwezi kisimamo kirefu, basi kuswali rakaa ishirini ni bora zaidi, nazo ndizo zinazoswaliwa na Waislamu wengi, kwani idadi hii ni kati na kati baina ya kumi na arobaini. Na ikiwa ataswali rakaa arobaini na zaidi, basi itajuzu, na hakuna lolote lililo makruhu katika hilo. Maimamu wengi wamelielezea hili kama Ahmad na wengineo. Na mwenye kudhani kwamba Tarawehe ina idadi maalumu ya rakaa iliyowekwa na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) isiyozidi wala kupungua, basi amekosea”.
Ninasema: “Hivi ndivyo Fiqh inavyotakikana iwe. Yako wapi haya kwa baadhi ya ndugu zetu wanaoiwacha jamaa ya Tarawehe katika “Al-Haram” na kwenda zao baada ya kuswali rakaa kumi?!! Allaah Atusamehe sote”.
· Mapumziko Baada Ya Kila Rakaa Nne
Mafuqahaa wamekubaliana kwamba inaruhusiwa kupumzika baada ya kila rakaa nne, kwani jambo hili limerithiwa toka kwa watangu wema. Wao walikuwa wakirefusha kisimamo katika Tarawehe na wanapumzika baada ya kila rakaa nne. [Fardul Mukhtaar (1/474), Haashiyatul ‘Adawiy (2/321) na Matwaalibu Ulin Nuhaa (1564)]
Ninasema: “Huenda asili ya hili ni kauli ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu Anha) tuliyoitaja mara kadhaa inayoelezea namna Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alivyokuwa akiswali: “Anaswali nne, basi usiulize uzuri wake na urefu wake, kisha anaswali nne, basi usiulize uzuri wake na urefu wake”. Kauli hii inatuarifu kuwepo mapumziko baina ya kila rakaa nne. Katika mapumziko haya, hakuna dhikri maalumu wala dhikri nyingine za aina zozote kama wanavyofanya baadhi ya wasiojua.”
· Je, Qur-aan Hukhitimishwa Katika Tarawehe?
Hakuna Sunnah yoyote iliyopokelewa toka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba ameainisha mpaka wa kisomo katika Tarawehe, bali kisomo hutofautiana kwa mujibu wa hali ilivyo. Imamu atasoma kiasi cha kutowakimbiza watu wakaikacha jamaa. Na lau kama watu wataridhika wenyewe kurefushwa kisomo, basi ni bora kutokana na athar zilizotangulia.
Hanafiy na Hanbali wanapendelea Qur-aan Tukufu ikhitimishwe katika mwezi mzima ili watu waisikilize Qur-aan yote katika Swalaah hiyo. [Fat-hul Qadiyr (1/335), Al-Badai’i (1/289) na Al-Mughniy (2/169)]
· Kuswali Na Imamu Hadi Mwisho
Anayeswali nyuma ya imamu, anatakikana asimwache njiani bali akamilishe naye mpaka mwisho. Katika Hadiyth ya Abu Dharri, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:
((Mwenye kuswali na imamu mpaka akamaliza, huandikiwa thawabu za Qiyaamul Layl)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abu Shaybah].
Ikiwa imamu ataswali Witr mwishoni mwa Swalaah, ataswali naye hata kama niya yake ni kuja kuswali Qiyaamul Layl, hili haliharibu kitu kama tulivyotangulia kusema. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
027-Swalaat Adh-dhuhaa
Alhidaaya.com [3]
Wakati wa Dhuhaa kwa mujibu wa Mafuqahaa, ni baina ya kunyanyuka jua na kupinduka. [Haashiyat Ibn ‘Aabidiyn (2/23) chapa ya Fikr]
Kuna Hadiyth nyingi zinazozungumzia fadhila za Swalaah hii. Hadiyth hizo ni:
1- Hadiyth ya Abu Dharri (Radhwiya Allaahu Anhu) asemaye: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( يصبح على كل سلامى من أحدكم صدقة، فكل تسبيحة صدقة، وكل تحميدة صدقة، وكل تهليلة صدقة، وأمر بالمعروف صدقة، ونهي عن المنكر صدقة، ويجزئ من ذلك ركعتان يركعهما من الضحى ))
((Kila kiungo cha mmoja wenu kinakuwa ni swadaqah. Kila tasbiyha moja ni swadaqah, kila tahmiydah moja ni swadaqah, kila tahliylah moja ni swadaqah, kuamrisha mema ni swadaqah, na kukataza munkari ni swadaqah. Rakaa mbili za Dhuhaa anazoziswali, zinamtosheleza na hayo yote)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (720), Abu Daawuud (1285), na Ahmad (5/167)].
2- Al Buraydah (Radhwiya Allaahu Anhu) anasema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( في الانسان ستون وثلاثمائة مفصل، عليه أن يتصدق عن كل مفصل منها صدقة ))
((Kila mwanadamu ana viungo 360, ni juu yake akifanyie swadaqah kila kiungo katika hivyo)). Wakasema: “Nani atayaweza hayo ee Rasuli wa Allaah?”. Akasema:
(( النخامة في المسجد يدفنها، أو الشيئ ينحيه عن الطريق، فإن لم يقدر فركعتا الضحى تجزئ عنه ))
((Alifukie kohozi lililoko ndani ya Msikiti, au aondoshe kitu njiani, na kama hawezi, basi rakaa mbili za Dhuhaa zitamtosheleza)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (2/524) na Ahmad (5/354)].
“ Hadiyth hizi mbili zinaonyesha juu ya fadhila kubwa ya Swalaah ya Dhuhaa, hadhi yake adhimu na uthibitisho wa uhalali wake, na kwamba rakaa zake mbili zinatosheleza swadaqah ya viungo 360. Jambo lenye mambo haya, linastahiki kuendelea na kudumu nalo mtu daima…”. [Naylul Awtwaar (3/78) chapa ya Al-Hadiyth]
3- Imepokelewa toka kwa Zayd bin Arqam akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwatokea watu wa Qubaa wakiwa wanaswali Dhuhaa akawaambia:
(( صلاة الأوابين حين ترمض الفصال))
(( Swalaah ya watiifu warejelefu ni pale jua linaposhitadi na kuwataabisha ngamia wachanga)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (748) na Ahmad (4/366)].
4- Imepokelewa toka kwa Jubayr bin Nafiyr toka kwa Abud Dardaai na Abu Dharr toka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba Allaah ‘Azza wa Jalla Anasema:
(( ابن آدم، اركع لي ركعات من أول النهار، أكفك آخره))
((Ee mwanadamu! Rukuu kwa ajili Yangu rakaa kadhaa mwanzoni mwa mchana, Nitakutosheleza mwishoni mwake )). [Swahiyh Bituruqihi (kwa Sanad tofauti): Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (475). Ina Hadiyth mwenza ya Nu’aym bin Hammaar iliyoko kwa Abu Daawuud (1289). Angalia Al-Irwaa (465)].
5- Imepokelewa na ´’Abdullaah bin ‘Amri akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alituma kikosi cha vita, wakapata ngawira na wakarejea haraka. Watu wakazungumza kuhusu kushinda kwao vita haraka, wingi wa ngawira walizozipata na kurejea kwao haraka. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:
(( ألا أدلكم على أقرب منهم مغزى وأكثر غنيمة وأوشك رجعة؟ من توضأ ثم غدا إلى المسجد لسبحة الضحى فهو أقرب منهم مغزى وأكثر غنيمة وأوشك رجعة ))
(( Je, nikuonyesheni lililo karibu zaidi kuliko vita vyao, lililo jingi zaidi kuliko ngawira zao na lililo haraka zaidi kuliko walivyorejea? Mwenye kutawadha, kisha akaenda Msikitini kwa ajili ya Sunnah ya Dhuhaa, basi yuko karibu zaidi kuliko vita walivyoshinda, ana ngawira nyingi zaidi kuliko walizopata na urejeaji wa haraka zaidi kuliko wao)). [Al-Albaaniy kasema ni Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (2/175). Angalia Swahiyhut Targhiyb (663-664)].
· Hukmu Ya Swalaat Adh-Dhuhaa
Maulamaa wamekhitalifiana kuhusu hukmu ya Swalaah ya Dhuhaa kwa kauli sita. [Zaadul Ma’ad (1/341-360), Badai’ul Fawaaid, na Fat-hul Baariy (3/66)] Zilizo karibu zaidi ni tatu:
Ya kwanza:
Ni Sunnah na inapendeza kuendelea kuiswali bila kuacha. Hii ni kauli ya Jamhuri kinyume na Hanbali. [’Umdatul Qaarii (7/240), Mawaahibul Jaliyl (2/67) Rawdhwat At Twaalibiyna (1/337) na Al-Mughniy (2/132)]
Dalili yao ni:
1- Ujumuishi wa Hadiyth zilizotangulia zinazozungumzia fadhila ya Swalaah ya Dhuhaa na hususan Hadiyth isemayo:
((Kila kiungo cha mmoja wenu kinakuwa ni swadaqah..)).
2- Hadiyth ya Abu Hurayrah isemayo: “Kipenzi changu ameniusia mambo matatu: Kufunga siku tatu kila mwezi, rakaa mbili za Dhuhaa, na kuswali Witr kabla sijalala”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1178) na Muslim (721)]. Abud Dardaai na Abu Dharri wana Hadiyth kama hii.
3- Hadiyth ya Ma’adha Al-‘Adawiyya aliyesema: “Nilimwambia ‘Aaishah: Je, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali Dhuhaa?” Akasema: “Naam, nne na anaongeza idadi aitakayo”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1178) na Muslim (721)].
Ash-Shawkaaniy amesema katika An Nayl (3/76): “Haifichiki kwamba Hadiyth zenye kuithibitisha Dhuhaa, zimefikia upeo wa baadhi yake kutoishilia kwenye kusuniwa tu”.
Al Haafidh amesema katika Al Fat-h (3/66): “Al-Haakim amekusanya Hadiyth zilizokuja kuhusiana na Swalaat adh-dhuhaa katika mlango mmoja, na idadi ya wapokezi wa Hadiyth walioithibitisha imefikia kiasi cha Maswahaba ishirini”.
4- Ama kudumu bila kuiacha ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
(( أحب العمل إلى الله تعالى ما دام عليه صاحبه وإن قل ))
(( Amali inayopendeza zaidi kwa Allaah ni ile ambayo mtendaji wake hudumu nayo hata kama ni ndogo)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (43) na Muslim (782) na tamko ni lake].
Ya pili:
Imesuniwa kuiswali wakati fulani na kuiacha wakati mwingine bila kudumu. Ni madhehebu ya Hanbali. [Al-Furu’u cha Ibn Muflih (1/567)]
Na dalili yao ni:
1- Hadiyth ya Abu Sa’iyd aliyesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaswali Dhuhaa mpaka tunasema hatoiacha, na huiacha mpaka tunasema hatoiswali tena”. [Hadiyth Dhwaíyf. Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (477) na Ahmad (3/21-36). Angalia Al-Irwaa (460)].
2- Katika Hadiyth ya Anas kuhusiana na kisa cha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuswali Dhuhaa katika nyumba ya ‘Utbaan bin Maalik, na Fulaan Ibn Al-Jaaroud akamwambia Anas: “Je, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali Dhuhaa? ”Akasema: “Sikumwona akiswali isipokuwa siku hiyo”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (670).
3- Hadiyth ya ‘Aaishah aliyesema: “Sikumwona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiswali Sunnah ya Dhuhaa, na mimi ninaiswali [ingawa yeye anaacha amali ambayo yeye ni wajibu kwake aifanye kwa kuchelea watu kuifanya ikaja kufaradhishwa kwao]”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1177/1128) na Muslim (718)].
Ya tatu:
Haiswaliwi ila kwa sababu fulani
Ni kama kupitwa na Qiyaamul Layl na mfano wake. Na hili ndilo alilolikhitari Ibn Al-Qayyim baada ya kuzichambua kauli kuhusiana na suala. [Zaadul Ma’ad (1/341-360) na Badaai’ul Fawaaid]
Hoja ya wenye kusema hivi ni kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuiswali isipokuwa kwa sababu fulani. Wamekubaliana kwamba iliswaliwa wakati wa dhuhaa kutokana na sababu mbalimbali:
1- Hadiyth ya Ummu Haani isemayo: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia nyumbani kwake Siku ya Ukombozi wa Makkah, akaoga na akaswali rakaa nane [Sunnah ya Dhuhaa]. Sikuiona Swalaah yoyote nyepesi kuliko hiyo isipokuwa yeye hutimiza rukuu na sijdah”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1176), Muslim (719) na Abu Daawuud (1290)].
Ilikuwa ni kwa sababu ya Ukombozi. Wamesema: “Na Sunnah ya Ukombozi, ni kuswali rakaa nane”. At-Twabariy amelinukulu kutokana na alivyofanya Khaalid bin Al-Waliyd alipoikomboa Al-Hiyrah.
2- Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliposwali nyumbani kwa Utbaan bin Maalik alipomwomba aswali hapo katika sehemu ambayo yeye huswalia. Ikawa imewafikiana na wakati wa Dhuhaa. Msimulizi amekifupisha kisa kwa kusema: “Aliswali Dhuhaa katika nyumba yake”. [Hadiyth Swahiyh: “Takhriyj” yake tumeielezea karibuni].
3- ‘Abdullaah bin Shuqayq alimuuliza ‘Aaishah: “Je, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali Dhuhaa?” Akasema: “Hapana, isipokuwa anaporudi toka safarini”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (717). Zimepokelewa toka kwa ‘Aaishah riwaya tofauti. Hapa ‘Aaishah ameifungamanisha Swalaah ya Dhuhaa ya Rasuli Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam na safari. Na katika Hadiyth ya Muslim, ‘Aaishah amekanusha kabisa kumwona Rasuli akiswali, na katika riwaya nyingine amethibitisha hilo bila mpaka. Kundi la Maulamaa akiwemo ‘Abdul Barri wanayatilia nguvu yaliyopo katika Swahiyh Mbili pamoja na yale ambayo Muslim amebaki nayo peke yake. Wengine wameunganisha kati ya riwaya zote hizi. Angalia Fat-hul Baariy (3/67)]
Hii ni kwa vile Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikataza kuingia usiku nyumbani toka safarini. Akawa anaingia mwanzoni mwa mchana, anaanza kwenda Msikitini na kuswali wakati wa Dhuhaa.
Wamesema: “Ama Hadiyth zinazoraghibisha na kubembelezea, hazionyeshi kwamba Swalaah hii ni ya kila siku kwa kila mtu. Na kwa ajili hiyo, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kalihusisha hilo kwa Abu Dharri na Abu Hurayrah basi, na wala hakuwausia Maswahaba wakubwa!!
Ibn Al-Qayyim amesema: “Kwa kuzitaamuli Hadiyth Marfu’u na athar za Maswahaba peke yake, hatuoni kingine zaidi ya kauli hii”.
Sheikh wa Uislamu anaona kwamba mtu ambaye ni ada yake kuswali usiku, haisuniwi kwake kuswali Dhuhaa. Ama yule ambaye si ada yake, basi imesuniwa kwake aswali Dhuhaa kila siku katika hali zote. [Al-Ikhtiyaaraat (uk. 64) na Al-Furu’u (1/567)]
Ninasema: “Ni wazi kabisa kwamba kauli ya kwanza ndiyo sahihi zaidi kutokana na ujumuishi wa uraghibisho kwa Swalaah ya Dhuhaa, na kuwa kwake inamtosheleza mtu kwa swadaqah ya viungo vyake 360. Ama pingamizi ya baadhi ya Maswahaba kama vile Ibn Mas-’oud, Ibn ‘Umar na wengineo, pingamizi hii haidhuru kitu, kwani wengineo wamethibitisha ruksa na uhalali wa Swalaah hii. Kila mmoja wao amesimulia aliyoyaona, na aliyejua ni hujja kwa ambaye hakujua.
Aidha, yaliyoelezewa kuhusiana na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na baadhi ya Maswahaba wake kuiacha baadhi ya nyakati, hakukanushi uhalali wake, kama ambavyo kuendelea nayo Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) si sharti ya ruksa hii, bali ni ruksa ya kuraghibisha kuiswali Swalaah hii kwa mujibu ya yaliyozungumzwa kuhusiana na fadhila zake. Na kwa ajili hiyo, ‘Aaishah amesema: “Sikumwona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiswali Sunnah ya Dhuhaa, na mimi ninaiswali [ingawa yeye anaacha amali ambayo yeye ni wajibu kwake aifanye kwa kuchelea watu kuifanya ikaja kufaradhishwa kwao]”. [Hadiyth Swahiyh: “Takhriyj” yake tumeielezea karibuni].
· Wakati Wa Swalaah Ya Dhuhaa
Wakati wake unaanza tokea baada ya jua kunyanyuka na kumalizika wakati uliokirihishwa hadi kabla kidogo ya kupinduka jua madhali haujaingia wakati uliokatazwa kwa mujibu wa Jamhuri ya Maulamaa. [Mawaahibul Jaliyl (2/68), Kash-Shaaful Qinaa (1/442), Rawdhwat At-Twaalibiyna (1/332) na Asnal Matwaalib (1/203)]
Ninasema: “Kwa maelezo haya, wakati wake huanza baada ya takriban robo saa tokea kuchomoza jua”.
Wakati wake bora zaidi ni kucheleweshwa mpaka pale joto linaposhitadi kutokana na Hadiyth ya Zayd bin Arqam kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema:
(( صلاة الأوابين حين ترمض الفصال))
((Swalaah ya watiifu warejelefu ni pale jua linaposhitadi na kuwataabisha ngamia wachanga)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (748) na Ahmad (4/366)].
Maana yake ni pale mchanga unapokuwa moto na kuzichoma kwato za ngamia wadogo, na hii inakuwa muda mfupi kabla ya jua kupinduka.
· Idadi Ya Rakaa Zake
Hakuna makhitilafiano yoyote ya kuwa uchache wa Swalaah ya Dhuhaa ni rakaa mbili kati ya waliosema kuwa ni Sunnah kutokana na Hadiyth tuliyoielezea isemayo: ((Rakaa mbili za Dhuhaa anazoziswali, zinamtosheleza na hayo yote)), na Hadiyth ya Abu Hurayrah isemayo: “Kipenzi changu ameniusia mambo matatu…na rakaa mbili za Dhuhaa”. [Al-Fataawaa Al-Hin-diyyah (1/112), Ad-Dusuwqiy (1/313), Rawdhwat At-Twaalibiyna (1/332) na Al-Inswaaf (2/190)]
Hakuna makhitilafiano yoyote ya kuwa uchache wa Swalaah ya Dhuhaa ni rakaa mbili kati ya waliosema kuwa ni Sunnah. Kisha wakakhitalifiana kuhusu wingi wa rakaa zake kwa kauli tatu:
Ya kwanza:
Wingi wake ni rakaa nane. Ni madhehebu ya Maalik, Shaafi’i na Hanbali. [Ad-Dusuwqiy (1/313), Al-Majmu’u (4/36), Ar-Rawdhwah (1/332), Al-Inswaaf (2/190) na Al-Mughniy (2/131)]
Ni kutokana na Hadiyth ya Ummi Haani kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia nyumbani kwake Siku ya Ufunguzi wa Makkah, akaswali rakaa nane. [Hadiyth Swahiyh: Imeelezwa karibuni].
Ya pili:
Wingi wake ni rakaa kumi na mbili. Ni madhehebu ya Hanafi kutokana na Hadiyth Marfu’u ya Anas: “Mwenye kuswali Dhuhaa rakaa kumi na mbili, Allaah Atamjengea kasri peponi”. [Hadiyth hii ni Dhwa’iyf].
Ya tatu:
Hakuna mpaka wa wingi wake. Hili limesimuliwa na baadhi ya Masalaf, nalo ndilo lenye uzito zaidi kwa sababu mbili:
1- Hadiyth ya Muaadhat isemayo: Nilimwambia ‘Aaishah: “ Je, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali Dhuhaa? Akasema: “Naam, rakaa nne, na huzidisha idadi atakayo”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (719)].
2- Kuishilia kwenye rakaa nane tu katika Hadiyth ya Ummu Haani kunajibiwa kwa mambo mawili:
La kwanza ni kwamba kuna Maulamaa waliosema kwamba hiyo ilikuwa ni Swalaah ya Ukombozi wa Makkah na si Swalaah ya Dhuhaa. La pili ni kuwa kuishilia kwenye rakaa nane, hakumaanishi kwamba hakuna ruksa ya kuongeza zaidi ya hapo, kwa kuwa suala hili linamhusu kila mtu binafsi. [Ash-Sharhul Mumti’i (4/120)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
028-Swalaat Al-Istikhaarah
Alhidaaya.com [3]
Mwenye kutaka kufanya jambo la halali, kisha akawa na shakashaka kama litakuwa na kheri ndani yake au litakuwa sawa, basi imesuniwa kwake aswali rakaa mbili zisizo za faradhi - rakaa zozote mbili hata kama ni katika Sunnah za rawaatib – kisha aombe baada ya kuziswali kwa du’aa iliyokuja katika Hadiyth ifuatayo:
Imepokelewa toka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anatufundisha istikhaarah katika mambo yote. Aidha, anatufundisha Suwrah ya Qur-aan anasema:
((Akiazimia mmoja wenu kufanya jambo, basi aswali rakaa mbili zisizo za faradhi, kisha aseme: Allaahumma inniy astakhiyruka bi’ilmika, wa astaqdiruka biqudratika, wa as-aluka min fadwlikal Adhwiym, fainnaka Taqdiru walaa aqdiru, wa Ta’alamu walaa a’alamu, wa Anta ‘Allaamul Ghuyuub. Allaahumma in Kunta Ta’alamu anna haadhaal amra (atalitaja) khayrun liy fiy diyniy wa ma’aashiy wa ‘aaqibati amriy (au atasema: ‘aajilihi wa aajilihi) Faqdirhu liy wa Yassirhu liy, thumma Baariyki liy fiyhi. Wain Kunta Ta’alamu anna haadhal amra sharrun liy fiy diyniy wa ma’aashiy wa ‘aaqibati amriy (au atasema: ‘aajilihi wa aajilihi) Faswrifhu ‘anniy Waswrifniy ‘anhu, Waqdir liy al khayra haythu kaana, thumma Irdhwiniy bihi”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (719)].
Zifuatazo ni tanbihi ambazo inabidi zizingatiwe:
1-Istikhaarah hufanywa wakati mtu anapoazimia kufanya jambo la halali, na haifanywi katika mambo ya halali ila kwa ajili ya kuchagua la kheri zaidi kati yake. Pia haifanywi katika mambo ya wajibu au ya haramu.
2- “Baada ya kuiswali, inatakikana mtu alifanye lile ambalo anakuta kifua chake kimefunguka kwalo, asiutegemee ukunjufu aliokuwa ameulemea kabla ya kuswali, bali aliache chaguo lake moja kwa moja. Na kama si hivyo, basi atakuwa hamfanyii istikhaarah Allaah bali hawaa ya nafsi yake, na anaweza asiwe mkweli katika kuiomba kwake kheri na kujivua na ujuzi na uwezo na kuuthibitisha kwa Allaah Mtukufu. Akiwa mkweli katika hilo, atajivua uwezo, nguvu na chaguo lake mwenyewe.” [Yamenukuliwa haya kutoka Naylul Awtwaar (3/90) toka kwa An Nawawiy]
3- Si lazima aliyefanya istikhaarah aone njozi usingizini kama wanavyoitakidi watu wengi, bali inakuwa ni kwa lile ambalo kifua chake mtu kitalikunjukia, au jambo hilo litarahisishwa kwake kwa mujibu wa Alivyolikadiria Allaah.
4- Chaguo la Allaah linaweza kuja kinyume na mtu anavyotaka au kwa lile ambalo analiona kama ni shari. Hapa ni lazima asalimishe jambo lake kwa Allaah.
(( كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ وَهُوَ كُرْهٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَن تُحِبُّوا شَيْئًا وَهُوَ شَرٌّ لَّكُمْۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ))
((Mmeandikiwa shariy’ah kupigana vita nako kunachukiza mno kwenu. Na asaa mkachukia jambo na hali lenyewe ni khayr kwenu. Na asaa mkapenda jambo na hali lenyewe ni la shari kwenu. Na Allaah Anajua na nyinyi hamjui)). [Al-Baqarah (2:216)]
5- Istikhaarah ni du’aa, hakuna ubaya kuikariri.
· Tanbihi
Kuna Hadiyth isemayo:
(( إذا هممت بأمر فاستخر ربك فيه سبع مرات))
((Ukiazimia jambo, basi mfanyie istikhaarah Mola wako mara saba)). Hadiyth hii ni batili na haifai.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
029-Swalaat At-Tasbiyh
Alhidaaya.com [3]
Swalaah ya Tasbiyh ni aina ya Swalaah za Sunnah ambayo huswaliwa kwa picha maalumu itakayokuja kufafanuliwa. Imeitwa “Swalaah ya Tasbiyh” kwa vile ina tasbiyh nyingi ndani yake zinazofikia sabini na tano katika kila rakaa moja.
· Hukmu Yake
Maulamaa wametofautiana kuhusu hukumu yake kutokana na kukhitilafiana kwao juu ya uthibiti wa Hadiyth iliyoizungumzia Swalaah hii. Hadiyth hii ni ya Ibn Abbaas anayesema kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia ‘Abbaas bin ‘Abdil Muttalib:
((Ee ‘Abbaas! Ee ami yangu kipenzi! Je, nikupe? Je, nikutunuku? Je, nikukurubishie? Je, nikufanyie? Mambo kumi ukiyafanya, Allaah Atakughufiria madhambi yako; ya mwanzo yake na ya mwisho yake, ya zamani yake na ya sasa yake, ya kukosea yake na ya kukusudia yake, madogo yake na makubwa yake, na ya siri yake na ya wazi yake. Mambo kumi ni wewe uswali rakaa nne, utasoma katika kila rakaa Al-Faatihah pamoja na sura yoyote. Ukimaliza kusoma katika rakaa ya kwanza, utasema ukiwa bado umesimama: “Subhaana Allaah wal Hamduli Laahi wa laailaaha illa Allaahu Allaahu Akbar” mara kumi na tano. Kisha utarukuu na utasema hivyo hivyo mara kumi ukiwa umerukuu. Kisha utanyanyua kichwa chako toka kwenye rukuu na utayasema hayo hayo mara kumi. Halafu utakwenda kusujudu na utayasema hayo hayo mara kumi ukiwa ndani ya sijdah. Kisha nyanyua kichwa chako toka kwenye sijdah, na utayasema mara kumi, kisha sujudu tena na useme mara kumi, halafu nyanyua kichwa chako uyaseme mara kumi. Na hizo ni mara sabini na tano katika kila rakaa. Utafanya hivi katika rakaa nne. Ukiweza kuiswali kila siku mara moja, basi swali. Kama huwezi, basi mara moja kila ijumaa, na kama hukuweza, basi kila mwezi mara moja. Kama hukuweza, basi mara moja kila mwaka, na kama hukuweza, basi mara moja katika umri wako)). [Hadiyth Dhwa’iyf: Kuna mvutano katika kuifanya kuwa Hadiyth Hasan. Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1297), Ibn Maajah (1387), Al-Haakim (1/318-319), Al-Bayhaqiy (3/51), At-Twabaraaniy (11/161), Abu Na’iym katika Al-Hilyah (1/2-25-26) na wengineo kupitia njia mbalimbali toka kwa Ibn ‘Abbaas, na njia zote ni Dhwa’iyf. Ina Hadiyth wenza lakini zote hazifai kuitilia nguvu. Na kwa ajili hiyo, Al-Haafidh amesema katika At-Talkhiys (2/7): “Kiukweli ni kuwa Sanad zake zote ni Dhwa’iyf ingawa Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas inakurubia sharti ya kuwa ni Hasan isipokuwa ni “Shaadh” kutokana na upekee wake usio wa kawaida, kutokuwa na muundo wa kukinaisha akili na kutofautiana kabisa na miundo ya Swalaah nyinginezo”. Ninasema: “Maulamaa wengi wamesema kuwa Hadiyth hii ni Dhwa’iyf kama Al Imaam Ahmad (ambaye inasemekana alijirudi na kusema si Dhwa’iyf), At-Tirmidhiy na Ibn Al-‘Arabiy. Ibn Al-Jawziy ameiweka kwenye kitabu chake cha Al-Mawdhuwaat, na Maulamaa waliobobea hifdh ya Hadiyth wamemjibu kwa hilo. Sheikh wa Uislamu amesema ni Dhwa’iyf, na Ibn Khuzaymah na Adh-Dhahabiy hawako huku wala kule]
Maulamaa wamekhitalifiana kuhusiana na hukmu yake katika kauli tatu:
Ya kwanza:
Ni Sunnah. Limesemwa hili na baadhi ya Maulamaa akiwemo Ibn Mubaarak na baadhi ya Mashaafi’i. [Al-Majmu’u (3/647) na Nihaayatul Muhtaaj (2/119)]
Hawa wamesema kwamba Hadiyth hiyo ni Swahiyh na wao wanaikubali.
Ya pili:
Haina ubaya (inajuzu). Hili wamelisema baadhi ya Mahanbali. [Al-Mughniy (2/132)]
Wamesema: “Ikiwa hakuna Hadiyth iliyothibiti kuhusiana na Swalaah hii, basi Swalaah hii ni katika amali bora, na Hadiyth Dhwa’iyf inatosha kuipitisha!!
Na kwa ajili hiyo, Ibn Qudaamah amesema katika Al-Mughniy (2/132): “Ikiwa mtu ataiswali basi hakuna ubaya, kwani Sunnah na ‘ibaadah za fadhila si lazima zithibitishwe na Hadiyth Swahiyh!!
Ya tatu:
Swalaah hii haipo. Ni kauli ya Al-Imaam Ahmad. Amesema: “Linanishangaza jambo”. Akaulizwa: “Kwa nini?” Akasema: “Hakuna chochote Swahiyh kilichoizungumzia”, akaikung’uta mikono kuonyesha anakataa. [Al-Mughniy cha Ibn Qudaamah (2/132)]
An Nawawiy amesema: “Jambo la kusema kwamba Swalaah hii ni Sunnah ni lazima liangaliwe, kwa kuwa Hadiyth yake ni Dhwa’iyf, nayo imebadili mfumo wa Swalaah ujulikanao. Inatakikana lisifanywe jambo bila Hadiyth, na Hadiyth ya Swalaah hii si thabiti. [Al-Majmu’u (3/548)]
Ninasema: “Kauli hii ya mwisho ndiyo yenye uzito zaidi kwa kuwa Hadiyth haijathibiti mbali na utaratibu wa Swalaah hiyo kukhalifiana na Swalaah nyinginezo. Lakini ikiwa mtu ana sifa za kufanya ijtihadi, na akakuta kwamba Hadiyth ni Swahiyh kwa mujibu wa ijtihaad yake, basi imesuniwa kwake kuiswali. Ama kauli ya pili yenye kujuzisha pamoja na udhwa’iyf wa Hadiyth, nayo pia ni kauli dhwa’iyf kutokana na mambo mawili:
1- La sawa ni kuwa Hadiyth Dhwa’iyf haifanyiwi kazi kabisa, si katika amali bora wala katika amali nyinginezo zozote. Huu ndio msimamo wa Maulamaa wahakiki wakiongozwa na Al-Bukhaariy, Muslim, Yahya bin Ma’iyn, Ibn Hazm na wengineo. [Angalia Tamaam Al-Minnah (uk. 34) na utangulizi wa Swahiyhut Targhyb (1/16-36)]
2- Wanaosema kwamba Hadiyth Dhwa’iyf inaweza kutumiwa katika amali bora wameweka masharti kadhaa. Kati ya masharti hayo ni kuwa amali hiyo iwepo kisharia. Na Swalaah hii kwa muundo huu, haipo kisharia isipokuwa kwa Hadiyth hii, nasi hatuwezi kuiswali kama ni amali bora inayotambulika kisharia.
· Tanbihi
Kwa wanaosema kwamba Swalaah hii inajuzu, tunawaambia kwamba kuipangia Swalaah hii tarehe 27 ya Mwezi wa Ramadhwaan na watu kukusanyika Msikitini ili kuiswali, ni bid-’a isiyo na asili yoyote. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
030-Swalaah Ya Tahiyyatul Masjid
Alhidaaya.com [3]
Imesuniwa kwa anayeingia Msikitini asikae ila baada ya kuswali rakaa mbili kutokana na dalili zifuatazo:
1- Hadiyth ya Abu Qataadah anayesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( إذا دخل أحدكم المسجد فلا يجلس حتى يصلي ركعتين))
((Anapoingia mmoja wenu Msikitini, asikae mpaka aswali rakaa mbili)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (444) na Muslim (714)].
2- Jaabir bin ‘Abdullaah anasema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwamuru Sulayka Al-Ghatwafaaniy aswali rakaa mbili wakati alipokuja siku ya ijumaa na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anakhutubu, akakaa kabla ya kuswali rakaa mbili”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (930) na Muslim (875)].
3- Hadiyth ya Jaabir asemaye: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwamuru aswali rakaa mbili wakati alipoingia Msikitini kwa ajili ya fedha ya ngamia wake ambaye Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimnunua”.
Amri katika Hadiyth hizi zinaonyesha kwamba ni za wajibu, na makatazo yanaonyesha uharamu wa kuziacha rakaa mbili. Lakini Jamhuri ya Maulamaa akiwemo Ibn Hazm, wanaona kwamba uwajibu huu unapinduliwa kupelekwa katika uSunnah kwa dalili mbalimbali. Kati ya dalili hizo ni Hadiyth isemayo: ((Ni Swalaah tano mchana na usiku)). Muulizaji akasema tena: “Je, kuna jingine zaidi?” Akasema: ((Hapana, ila kama utaswali za Sunnah)). [Hadiyth Swahiyh: Tushaielezea mara nyingi].
Ash-Shawkaaniy Rahimahul Laahu ameijibu akisema kwamba neno lake Rasuli ((Ila kama utaswali za Sunnah)) linakanusha kimsingi wajibu lakini si wajibu unaotokana na sababu ambazo mkalifishwaji anachagua mwenyewe kuufanya kama kuingia Msikitini kwa mfano. Hapa mwenye kuingia, amejiwajibishia mwenyewe Swalaah kwa kuingia, kana kwamba yeye amejiwajibishia mwenyewe, na hivyo basi haisihi kuingiza cha kugeuza ujiwajibishaji huu kwa mfanowe. [Naylul Awtwaar (3/84) chapa ya Al-Hadiyth. Faida ya maneno haya iko ndani ya Hadiyth lakini Al-Haafidh hakuitohoa humo!]
Ninasema: “ Hadiyth ya Abu Waaqid Al-Layth inaweza kutilia nguvu ya kwamba amri hizi ni Sunnah. Hadiyth inasema kwamba wakati Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa amekaa Msikitini pamoja na watu, waliingia watu watatu. Wawili wakaelekea kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na mmoja akaondoka. Hao wawili wakasimama mkabala wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Mmoja wao akaiona nafasi kwenye halaqa akakaa, na yule mwingine akakaa nyuma yao. Ama yule wa tatu, huyo aligeuza njia na kwenda zake. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomaliza darsa alisema:
((Je, niwaelezeni habari ya watu watatu? Ama mmoja wao, huyu alikimbilia kwa Allaah na Allaah Akampa hifadhi. Ama mwingine, huyu aliona haya na Allaah Akamwonea haya. Ama wa tatu, huyo aligeuza mgongo na Allaah Akamwachilia mbali)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (930)].
Ninasema: “Walikaa na Rasuli hakuwaamuru kuswali rakaa mbili. Allaah Ndiye Mjuzi zaidi”.
· Faida
Tumetangulia kusema katika mlango wa “Nyakati zilizoharamishwa kuswali” kwamba Tahiyyatul Masjid ni katika Swalaah zenye sababu zinazoswaliwa wakati wowote hata katika nyakati za karaha kwa mujibu wa kauli zenye nguvu. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
· Swalaah Baada Ya Kutawadha
Imesuniwa kwa aliyetawadha aswali rakaa mbili au zaidi wakati wowote hata katika nyakati zilizokirihishwa kutokana na Hadiyth ya Abu Hurayrah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia Bilaal wakati wa Swalaah ya Alfajiri:
((Ee Bilaal! Nielezee amali yenye matarajio zaidi uliyoifanya katika Uislamu, kwani mimi nimesikia mtaharuki wa viatu vyako mbele yangu huko peponi)).
Bilaal akasema: “Sikufanya amali yoyote yenye matarajio makubwa kwangu zaidi ya kuwa sikupata kujitwaharisha wakati wowote wa usiku au mchana, ila huswali kwa twahara hiyo kile nilichoandikiwa kukiswali”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1149) na Muslim (910)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
031-Swalaah Ya Tawbah
Alhidaaya.com [3]
Mwenye kuteleza akatenda dhambi, ni lazima aharakie kutubia na kurejea kwa Allaah Mtukufu, kwani Allaah ni Mwenye Kughufiria madhambi na Mwenye Kukubali toba.
Swalaah kwa ajili ya toba ya madhambi imesuniwa katika madhehebu yote manne. [Ibn ‘Aabidiyn (1/462), Ad-Dusuwqiy (1/314), Asnal Matwaalib na Kash-Shaaful Qinaa (1/443)]
Na hii ni kutokana na Hadiyth ya Abu Bakri (Radhwiya Allaahu Anhu) aliyesema: “Nimemsikia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
(( Hakuna mtu yeyote anayetenda dhambi, kisha akasimama, akatawadha na kuswali, halafu akaomba maghfirah kwa Allaah isipokuwa Allaah Humghufiria)). [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (406), Abu Daawuud (1521) na Ibn Maajah (1395). Katika Sanad yake yuko Asmaa bin Al Hakam. Al-Haafidh kasema: “Ni mkweli asiye na shaka”. Ninasema: “Bali hajulikani”] Kisha akasoma Aayah hii:
(( وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّـهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّـهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَىٰ مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ ))
Sanad ya Hadiyth hii ni Dhwa’iyf, lakini Aayah inatilia nguvu maana yake. Baadhi ya Maulamaa wameipasisha kuwa ni Hadiyth Swahiyh.
· Kuswali Rakaa Mbili Baada Ya Kutufu Al-Ka’abah
Jamhuri ya Maulamaa wanasema kwamba imesuniwa kuswali rakaa mbili nyuma ya Maqaamu Ibraahiym baada ya Kutufu. Katika rakaa hizo mbili, atasoma baada ya Al-Faatihahh (Qul yaa ayyuhal kaafiruwna) na (Qul Huwa Allaahu Ahad). Na hii ni kutokana na kitendo chake Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hijjah yake kama ilivyo katika Hadiyth ndefu ya Jaabir itakayoelezewa kikamilifu katika mlango wa Hijjah. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (1218). Itaelezewa kikamilifu katika mlango wa Hijjah]
Abu Haniyfah anasema kwamba rakaa hizo mbili ni wajibu.
Rakaa hizi mbili huswaliwa wakati wowote hata katika wakati usioruhusiwa kuswali kutokana na Hadiyth ya Jubayr bin Mutwim kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Enyi ukoo wa ‘Abdi Manaaf! Msimzuie yeyote aliyetufu Nyumba hii na akaswali wakati wowote aupendao mchana au usiku)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (869), An-Nasaaiy (5/223) na Ibn Maajah (1254)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
032-Swalaah Ya Kupatwa Jua (Kusuwf)
Alhidaaya.com [3]
· Taarifu Yake
“Kusuwf” ni kupotea mwanga wa jua au mwezi au sehemu ya mwanga na kubadilika kuwa weusi, na “Khusuwf” ni kisawe chake. Wataalamu wengine wanasema kwamba “Kusuwf” ni kupatwa jua na “Khusuwf” ni kupatwa mwezi, na tafsiri hii ndiyo mashuhuri zaidi katika lugha. [Lisaan Al-‘Arab, Kash-Shaaf Al-Qinaa (2/60) na Asnaa Al-Matwaalib (1/385)]
Swalaah ya “Kusuwf” ni Swalaah inayoswaliwa kwa mtindo maalumu wakati jua au mwezi ukipatwa wote au sehemu. [Mawaahibul Jaliyl (2/199), Nihaayatul Muhtaaj (2/394) na Kash-Shaaful Qinaa (2/60)]
· Hukmu Ya Swalaah Ya Kupatwa Jua
Jamhuri ya Maulamaa wanasema kwamba Swalaah ya Kupatwa Jua ni Sunnah iliyokokotezwa. Lakini Abu ‘Awwaanah ameeleza kwamba ni wajibu kwa mujibu wa riwaya iliyopokelewa toka kwa Abu Haniyfah wakati ambapo Maalik ameichukulia kama ni Swalaah ya Ijumaa. Kauli hii ya kusema ni wajibu iliyopewa uzito na Ash-Shawkaaniy, Swiddiyq Khaan na kisha Al-Albaaniy, ina mwelekeo wa nguvu kutokana na kuthibiti maagizo ya kuiswali. [Fat-hul Baariy (2/612), As Saylul Jarraar (1/323), Ar-Rawdhwat An Nadiyyah (uk 156) na Tamaam Al-Minnah (uk.261)]
Ama hukmu ya Swalaah ya Kupatwa Mwezi, Maulamaa wamekhitalifiana juu ya kauli mbili:
Ya kwanza:
Ni Sunnah iliyokokotezwa na huswaliwa jamaa kama Swalaah ya Kupatwa Jua. Hii ni kauli ya Ash-Shaafi’iy, Ahmad, Daawuud, Ibn Hazm, ‘Atwaa, Al-Hasan, An-Nakh’iy na Is-Haaq. Kauli hii imehadithiwa toka kwa Ibn ‘Abbaas. [Al-Ummu (1/214), Al-Mughniy (2/420), Al-Inswaaf (2/442), Bidaayatul Mujtahid (1/160) na Al-Muhalla (5/95)]
Na hoja yao ni haya yafuatayo:
1- Hadiyth ya Al-Mughiyrah ya kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( Hakika jua na mwezi ni alama mbili kati ya Alama za Allaah. Havipatwi kwa kufa mtu wala kwa kuzaliwa, na mnapoona vimepatwa, basi mwombeni Allaah na mswali mpaka mwanga urudi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1060) na Muslim (904)].
Kuna Hadiyth kama hii ya ‘Aaishah, Ibn ‘Umar, Ibn ‘Abaas na Abu Bakrah.
2- Yaliyosimuliwa ya kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali Swalaah ya Kupatwa Mwezi. [Angalia (Fat-h) (3/638)]
3- Yaliyosimuliwa toka kwa Ibn ‘Abbaas kwamba aliswali na wakazi wa Basrah Swalaah ya Kupatwa Mwezi rakaa mbili kisha akawaambia: “Nimeswali hivi kwa kuwa nimemwona Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiswali”. [Isnadi yake ni Dhwa’iyf: “Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bayhaqiy (3/342). Pia Ash-Shaafi’iy kaifanyia “ikhraaj” mfano wake katika musnadi wake (484), na Al-Bayhaqiy kanukuu toka kwake (3/342) lakini Sanad yake haifai].
Ya pili:
Haiswaliwi kwa jamaa, nayo ni Sunnah kama Sunnah zinginezo bila kuzidisha katika rukuu. Ni kauli ya Abu Haniyfah na Maalik. [Ibn ‘Aabidiyn (2/183), Al-Badaai-’i (1/282), Mawaahibul Jaliyl (2/201), Bidaayatul Mujtahid (1/312), na Ad-Dusuwqiy (1/402)]
Wamesema: “Ni kutokana na uzito wakati wa usiku kinyume na mchana, na kutotaarifiwa toka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba aliiswali kwa Jamaa pamoja na kwamba kupatwa mwezi kulikuwa zaidi kuliko kupatwa jua!!
Ninasema: “Kauli ya kwanza ina nguvu zaidi kwa kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameagiza kuziswali Swalaah hizo mbili bila ya kufarakanisha”.
· Wakati Wake
Ni kuanzia pale jua linapoanza kupatwa mpaka linapoachiliwa kutokana na kauli yake Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Mnapoona vimepatwa, basi mwombeni Allaah na swalini mpaka mwanga urudi)). [Hadiyth Swahiyh: Tushaitaja].
Kuachiliwa kumefanywa kuwa ndiyo lengo la Swalaah kwa ajili ya kumtaradhi Allaah Airejeshe neema ya mwanga. Na linapoachiliwa, basi lengo la Swalaah linakuwa lishapatikana. [Vitabu rejea vilivyotangulia]
· Kupita Kwake
Swalaah ya Kupatwa Jua inapita kwa moja ya mawili:
1- Kurejea mwanga kamili. Ikiwa mwanga utarejea kidogo, basi inajuzu kuswali kwa sehemu iliyobakia ya giza kana kwamba hiyo ndiyo bado inayopatwa.
2- Ni kuchwa jua likiwa bado limepatwa.
Na Swalaah ya Kupatwa Mwezi hupita kwa moja ya mawili:
1- Kurejea nuru kamili.
2- Kuchomoza jua au kutoweka mwezi ukiwa bado umepatwa. Na ikiwa mawingu yatazuia na mtu akashakia kama umeachiwa au la, basi ataswali kwa kuwa asili ni kubakia kusuwf. [Al-Mughniy (2/427), Rawdhwat At-Twaalibiyna (2/87) na Al-Mawaahib (2/203)]
· Faida
Swalaah ya Kupatwa Jua huswaliwa wakati wowote hata katika nyakati zilizopigwa marufuku kuswali. Hii ni kauli ya Ash-Shaafi’iy.
· Yaliyosuniwa Kwa Mwenye Kushuhudia Kusuwf
1- Akithirishe dhikri, kuomba maghfirah, kupiga takbiyr, kutoa swadaqah na amali nyingine njema.
‘Aaishah anasema kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema: ((Mtakapoona hilo, basi mwombeni Allaah, pigeni takbiyr, swalini na toeni swadaqah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1044) na Muslim ( 901)].
Na Asmaa anasema: “Hakika Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliniamuru nimwache huru mtumwa jua lilipopatwa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1056) na Muslim (903)].
2- Aende kuswali kwa Jamaa Msikitini
Hadiyth ya ‘Aaishah inaeleza: “Kisha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipanda asubuhi kipando (mnyama), jua likapatwa, akarejea dhuhaa. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akapita baina ya vyumba, kisha akasimama na kuswali”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1056) na Muslim ( 903)].
‘Aaishah anasema tena kwenye tamshi lililopokelewa na Muslim: “Nikatoka na wanawake katikati ya vyumba. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaja akiwa ameshuka toka juu ya kipando chake mpaka akafika sehemu yake aliyokuwa anaswalia”.
Al-Haafidh anasema kwenye Al Fat-h (3/633): “Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa ndani ya kipando hicho kutokana na kifo cha mwanawe Ibraahiym. Aliporejea, alikwenda Msikitini na hakuswali nje uwanjani. Na Sunnah katika Swalaah ya Kupatwa Jua ni kuswaliwa Msikitini, na lau si hivyo, kuswalia kwake jangwani kungelikuwa ni bora zaidi kwa kuwa ni wepesi kuona jua likiachiliwa. Allaah Ndiye Mjuzi zaidi”.
3- Wanawake watoke kwenda kuswali
Ni kutokana na Hadiyth ya Asmaa binti Abiy Bakri aliyesema: “Nilimwendea ‘Aaishah mke wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) jua lilipopatwa. Nikawakuta watu wamesimama wanaswali, naye pia kasimama anaswali”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1053) na Muslim ( 905)].
Tumeshalieleza tamko la ‘Aaishah aliposema: “Nikatoka pamoja na wanawake katikati ya vyumba Msikitini.”
Mwanamke mwenye kuchelea fitna husameheka kwenda Msikitini, na badala yake ataswalia nyumbani peke yake.
4- Ainadie Swalaah kwa kusema “As-Swalaatu Jaami’ah” bila adhana wala iqaamah
Imepokelewa toka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amri (Radhwiya Allaahu Anhu) akisema:”Jua lilipopatwa wakati wa enzi ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) palinadiwa: "As-Swalaatu Jaami’ah”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1045)].
Swalaah hii haina adhana wala iqaamah kwa makubaliano ya Maulamaa wote.
5- Khutbah baada ya Swalaah
Katika Swalaah hii, imesuniwa kutolewa khutbah kama khutbah ya Swalaah ya ‘Iyd kutokana na Hadiyth ya ‘Aaishah aliyesema kwamba baada ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kumaliza Swalaah, alisimama na kuwakhutubia watu. Alimhimidi Allaah na kumsifu, kisha akasema: ((Hakika jua na mwezi ni alama mbili kati ya Alama za Allaah ‘Azza wa Jalla. Havipatwi kwa kufa mtu wala kwa kuzaliwa, na mnapoona vimepatwa, basi mwombeni Allaah, tamkeni takbiyr, swalini na toeni swadaqah)). [Hadiyth Swahiyh: Tumeitaja nyuma kidogo].
Hii ni kauli ya Ash-Shaafi’iy, Is-Haaq na Maulamaa wengi wa Hadiyth. [Al-Majmu’u (5/52), Asnaa Al-Matwaalib (1/286), Fat-hul Baariy (2/620) na Bidaayatul Mujtahid (1/311)]
Abu Haniyfah, Maalik na Ahmad wamesema kwamba Swalaah ya Kusuwf haina khutbah!! [Al-Badaai-’i (1/282), Mawaahibul Jaliyl (2/202), Al-Mughniy (2/425) na rejea zilizotangulia]
Wengine wamesema kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakukusudia khasa khutbah kwa vipengele vyake katika Swalaah hiyo, bali alikuwa anataka kuwabainishia watu jibu kwa wale wenye kuitakidi kwamba kupatwa jua kunatokana na kifo cha baadhi ya watu.
Haya yanajibiwa na yaliyomo kwenye Hadiyth Swahiyh zinazoelezea kwa uwazi kuhusu khutbah, masharti yake, himdi, kumsifu Allaah, mawaidha na mengineyo yanayobainishwa humo. Khutbah haihusiani na kuwajulisha tu watu sababu ya kusuwf, bali asili ya mambo ni kumfuata Nabiy, na mambo yanayomuhusu yeye pekee pasina wengine hayathibiti ila kwa dalili. [Fat-hul Baariy cha Ibn Hajar (2/620) chapa ya As-Salafiyyah]
· Namna Ya Kuswali Kusuwf
Swalaah ya Kusuwf ni rakaa mbili tu, hakuna mabishano kati ya Maulamaa kuhusu hili. Walilobishania ni utendaji wake kwa kauli tofauti. Zilizo mashuhuri zaidi ni mbili:
Ya kwanza:
Ni rakaa mbili. Kila rakaa ina visimamo viwili, visomo viwili, rukuu mbili na sijdah mbili. Wanaosema haya ni Maalik, Ash-Shaafi’iy na Ahmad. [Ad-Dusuwqiy (1/405), Al-Ummu (1/215), Kash-Shaaful Qinaa (2/62) na Al-Mughniy (2/422)]
Dalili zao ni:
1- Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas aliyesema: “Jua lilipatwa wakati wa enzi ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Nabiy akaswali pamoja na watu. Akasimama kisimamo kirefu cha kiasi cha kusoma Suwrat Al-Baqarah. Kisha alirukuu rukuu ndefu, halafu akasimama kisimamo kirefu chini kidogo ya kisimamo cha kwanza. Kisha alirukuu rukuu ndefu chini kidogo ya rukuu ya kwanza”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1046) na Muslim (901)].
2- Hadiyth ya ‘Aaishah isemayo kwamba Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali siku jua lilipopatwa. Alisimama akapiga takbiyr, akasoma kisomo kirefu, kisha alirukuu rukuu ndefu. Halafu alinyanyua kichwa chake akasema: Sami’a Allaahu liman hamidah, na akasimama tena kama alivyokuwa. Kisha alisoma kisomo kirefu chini ya kisomo cha mwanzo, halafu alirukuu rukuu ndefu chini ya rukuu ya kwanza, kisha akasujudu sijdah ndefu, halafu akafanya katika rakaa ya mwisho mfano wa hivyo, kisha akatoa tasliym”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1047) na Muslim (901)].
3- Hadiyth ya Jaabir aliyesema: “Jua lilipatwa enzi ya Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika siku ya joto kali mno. Akawaswalisha Maswahaba wake na akakirefusha kisomo mpaka wakaanza kuanguka. Kisha alirukuu akarefusha, halafu akanyanyuka akarefusha, kisha akarukuu na kurefusha, halafu akasujudu sijdah mbili, kisha akasimama na kufanya mfano wa hayo. Zilikuwa ni rakaa nne na sijdah nne”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (904), Abu Daawuud (1179), An-Nasaaiy (1/217) na Ahmad (3/374)].
Ya pili:
Ni rakaa mbili. Kila rakaa ina kisimamo kimoja, rukuu moja na sijdah mbili kama Sunnah nyinginezo. Anayesema hivi ni Abu Haniyfah. Ibn Hazm amekhiyarisha kati ya namna zote. [Al-Badaai-’i (1/281), Tabyiynul Haqaaiq (1/228), Al-Muhalla (5/95) na Bidaayatul Mujtahid (1/307)]
Hoja za Abu Haniyfah na wenye kukubaliana naye ni:
Hadiyth ya Abu Bakrah aliyesema: “Jua lilipatwa enzi ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Akatoka akiliburura joho lake hadi akaishilia Msikitini. Watu wakamwendea haraka, akaswali nao rakaa mbili”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1063), An-Nasaaiy (3/146) na At-Twayaalsaa (716)].
Wamesema: ”Swalaah yoyote, ni Swalaah iliyozoeleka”. Na katika riwaya ya An-Nasaaiy: “Akaswali rakaa mbili kama wanavyoswali”.
2- Hadiyth ya An Nu’umaan bin Bashiyr aliyesema: “Jua lilipatwa enzi ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Akaanza kuswali rakaa mbili mbili huku akiomba mpaka likaachiliwa”. [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1193), Ahmad (4/267) na At-Twahaawiy. Angalia Al-Irwaa (3/131)].
Ibn Hazm kasema: “Tamshi hili (yaani kukariri rakaa mbili) linawajibisha tuliyoyaeleza”.
· Aina Nyinginezo Za Namna Ya Kuiswali
Imehadithiwa kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliiswali kwa miundo mingineyo. Kati yake ni:
3- Kila rakaa rukuu tatu [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (901), Abu Daawuud (1177) na An-Nasaaiy (3/129) toka kwa ‘Aaishah].
4- Kila rakaa rukuu nne [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (908) na Abu Daawuud (1183)].
Ibn Al-Qayyim anasema: “Maimamu wakubwa hawalioni hilo kuwa ni sahihi, bali wanaliona ni kosa kama Al-Imaam Ahmad, Al-Bukhaariy na Ash-Shaafi’iy”. [Zaadul Ma’ad (1/453) chapa ya Ar-Risaalah]
Ninasema: “Utendaji sahihi zaidi wa Swalaah hii ni kufanya rukuu mbili katika kila rakaa kama walivyosema Jamhuri kutokana na uwazi wa Hadiyth Swahiyh husika. Ama dalili za Abu Haniyfah na waliokubaliana naye, dalili hizi zimetaja rakaa mbili bila uainisho wakati Hadiyth za kundi la kwanza zimeainisha”.
Ama Hadiyth ya An-Nu’umaan bin Bashiyr kuhusu Swalaah ya rakaa mbili mbili, Al-Haafidh anasema katika mjalada wa tatu wa kitabu cha Al-Fat-h kwamba ikiwa Hadiyth hii imehifadhiwa, maana ya neno lake “rakaa mbili mbili” inaweza kuchukuliwa kama rukuu mbili. Ninasema: “Tushajua kwamba Hadiyth hii ni Dhwa’iyf, hivyo hatuhitajii taawili yoyote”.
Ama riwaya zinazozungumzia kuhusu ziada ya rukuu mbili katika rakaa moja, Sheikh wa Uislamu (18/17-18) amesema kwamba hili limepewa udhaifu na Maulamaa weledi wanaosema kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuswali Kusuwf isipokuwa mara moja tu siku alipofariki mwanaye Ibraahiym, na mwanaye huyu hakufa mara mbili, na wala hakuwa na Ibraahiym wawili. Isitoshe, imepokelewa kwa njia ya Tawaatur kwamba Nabiy aliswali Kusuwf siku hiyo kwa rukuu mbili katika kila rakaa.
Al-‘Allaamah Al-Albaaniy katika Al-Irwaa (3/132) amesema: “Kauli ya mwisho kuhusiana na Swalaah ya Kusuwf ni kwamba lililo sahihi thabiti toka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni kuwa Swalaah hii ni rakaa mbili, na kila rakaa ina rukuu mbili. Na haya yamethibiti toka kwa Maswahaba wengi yakielezewa kwenye vitabu vinavyoaminika, njia na riwaya mbalimbali. Ama kinyume na hayo, basi yatakuwa ima Dhwa’iyf au Shaadh, na hayafai kwa hoja”.
· Picha Ya Swalaah Ya Kusuwf Kwa Muhtasari
1- Apige takbiyr, asome du’aa ya ufunguzi, asome isti’aadhah, asome Al-Faatihahh, na kisha asome kiasi cha Suwrat Al-Baqarah.
2- Arukuu rukuu ndefu.
3- Anyanyuke toka kwenye rukuu na aseme: “Sami’a Allaahu liman hamidahu, Rabbanaa walakal Hamdu”.
4- Asisujudu, bali asome Al-Faatihah na Suwrah fupi kidogo kuliko ile ya kwanza.
5- Arukuu tena rukuu ndefu na apunguze kidogo urefu kulinganisha na ile ya kwanza.
6- Anyanyuke toka kwenye rukuu na aseme: “Sami’a Allaahu liman hamidahu, Rabbanaa walakal Hamdu”.
7- Asujudu, kisha akae, halafu asujudu tena.
8- Anyanyuke kwenda rakaa ya pili, kisha afanye kama alivyofanya katika rakaa ya kwanza.
· Je, Husomwa Hwa Sauti Au Kimya Kimya?
Ahmad, Is-Haaq na Maswahibu wawili wa Abu Haniyfah wanasema kwamba ni Sunnah kusoma kwa sauti kinyume na Jamhuri. [Rejea zilizotangulia kuhusiana na namna ya kuswali]
Dalili zao ni:
1- Hadiyth ya ‘Aaishah asemaye: “Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisoma kwa sauti katika Swalaah ya Khusuwf. Anapomaliza kusoma, hupiga takbiyr akarukuu, na anaponyanyuka toka kwenye rukuu husema: “Sami’a Allaahu liman hamidahu, Rabbanaa walakal Hamdu”. Kisha hufanya tena kisomo katika Swalaah ya Kusuwf rukuu nne katika rakaa mbili na sijdah nne”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1065)].
2- Ni Naafilah iliyoruhusiwa kuswaliwa kwa jamaa. Hivyo basi, sehemu ya Sunnah yake ni kusomwa kwa sauti kama ilivyo kwa Swalaah za ‘Iyd, Tarawehe na Kuomba Mvua.
Jamhuri wamesema: “Husomwa kwa sauti katika Swalaah ya Kupatwa Mwezi tu, ama Kupatwa Jua haisomwi kwa sauti”. Hoja yao ni:
1- Yaliyomo kwenye Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas iliyotangulia isemayo: “Akasimama kisimamo kirefu cha kiasi cha kusoma Suwrat Al-Baqarah”. Lakini hili haliwajibishi kuwa hakusoma kwa sauti bali inawezekana kuwa alisikia kutoka kwake Suwrah kadhaa alizozikadiria urefu wake na Al-Baqarah, au alikuwepo sehemu ambayo sauti haikuwa ikimfikia.
2- Yaliyosimuliwa toka kwa ‘Aaishah akisema: “Nilikisia kisomo cha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).“ [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1187) na Al-Bayhaqiy (3/338)].
Wamesema: “Lau angelisoma kwa sauti, pasingehitajika dhana au makisio”. Nao wamejibiwa kwamba kauli hiyo haijathibiti kwa ‘Aaishah, kisha inapingana na kauli yake sahihi inayothibitisha Nabiy kusoma kwa sauti.
3- Hadiyth ya Samurah bin Jun-dub akisema: “Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali Swalaah ya Kupatwa Jua, nami sikuisikia sauti yake”. [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (562), Abu Daawuud (1184), An-Nasaaiy (5/19) na Ibn Maajah (1264)]
Hili linajibiwa kwa Hadiyth iliyotangulia ya Ibn ‘Abbaas. Hadiyth Swahiyh haiwezi kurejeshwa kwa ajili ya Hadiyth hii. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
· Je, Mbali Na Swalaah Ya Kusuwf, Panaweza Kuswaliwa Pakitokea Matukio Ya Kuonyesha Nguvu Za Allaah Kama Matetemeko Na Mengineyo?
Maulamaa wana kauli nne kuhusiana na suala hili:
Ya kwanza:
Imesuniwa kuswali kwa kila janga au tukio la kuogofya kama tetemeko, upepo mkali, radi na mfano wa hayo. Ni kauli ya Abu Haniyfah, Ibn Hazm na riwaya toka kwa Ahmad.
Ya pili:
Haiswaliwi Swalaah yoyote kutokana na matukio isipokuwa Kupatwa Jua na Mwezi tu. Hii ni kauli ya Maalik.
Ya tatu: Haiswaliwi Swalaah yoyote kutokana na matukio isipokuwa Kupatwa Jua na Mwezi na tetemeko la kudumu. Ni kauli ya Hanbali.
Ya nne: Haiswaliwi kwa jamaa isipokuwa Swalaah ya Kupatwa Jua na Mwezi, na kama kuna tukio jingine, basi mtu akae kwake nyumbani aswali na aombe. Ni kauli ya Ash-Shaafi’iy.
Ninasema: “Huenda kauli hii ndio iliyo karibu zaidi na usahihi. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.”
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
033-Swalaah Ya Kuomba Mvua (Al-Istisqaa)
Alhidaaya.com [3]
· Taarifu yake:
“Al-Istisqaa” ni kumwomba Allaah Aiteremshe mvua wakati wa ukame. Maulamaa wote wamekubaliana kwamba hilo ni Sunnah aliyoiweka Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), lakini wamekhitalifiana kuhusiana na Swalaah yenyewe kama tutakavyobainisha.
· Hukmu Ya Swalaah Ya Kuomba Mvua
Ukame ukiingia, ardhi ikakauka na mvua ikapotea, imesuniwa imamu atoke pamoja na watu hadi sehemu maalumu ya kuswalia kama tutakavyoeleza, kisha aswali nao rakaa mbili. Hili ndilo lililothibiti toka kwa Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Imepokelewa toka kwa ‘Abbaad bin Tamiym toka kwa ami yake akisema: “Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka kwenda sehemu ya kuswalia kwa ajili ya kuomba mvua. Alielekea Qiblah na kuswali rakaa mbili na akageuza nguo yake kwa kupindua kulia kuja kushoto.” [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy].
Abu Haniyfah ameenda kinyume katika hili akisema: “Swalaah ya Kuomba Mvua haikusuniwa wala kutoka kwa ajili yake”. [Ibn ‘Aabidiyn (2/184) na Fat-hul Qadiyr (2/57)]
Dalili yake ni yaliyosimuliwa kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliomba mvua bila kuswali kama itakavyokuja.
Hadiyth ni hoja dhidi yake. Na kitendo chake Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) cha kuomba mvua bila Swalaah hakizuii kuwa Nabiy aliyafanya yote mawili, kwani hayapingani.
· Yaliyosuniwa Katika Swalaah Ya Kuomba Mvua
1- Watu watoke pamoja na imamu kwenda sehemu ya kuswalia wakivaa nguo chakavu kidogo, kwa unyenyekevu na kwa kuomba du’aa
Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Abbaas akisema: “Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka akiwa amevaa nguo chakavu, kwa unyenyekevu huku akiomba mpaka sehemu ya kuswalia. Akapanda mimbari, na wala hakukhutubu khutbah yenu hii, lakini aliendelea kufanya du’aa, kuomba kwa unyenyekevu na kupiga takbiyr. Halafu aliswali rakaa mbili kama anavyoswali katika ‘Iyd”. [Al-Albaaniy kasema ni Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1165), At-Tirmidhiy (555), na An-Nasaaiy. Angalia Al-Irwaa (665)].
2- Imamu akhutubu kabla ya Swalaah au baada ya Swalaah juu ya mimbari atakayotayarishiwa
Wenye kusema kwamba Swalaah ya Kuomba Mvua ni Sunnah wamekubaliana kwamba Swalaah hii ina khutbah isipokuwa riwaya katika madhehebu ya Ahmad. Maalik, Ash-Shaafi’iy, Ahmad na Maulamaa wengi wanasema kwamba khutbah inakuwa baada ya Swalaah. [Ad-Dusuwqiy (1/406), Al-Ummu (1/221), Al-Majmu’u (5/77), Al-Mughniy (2/433), na Kash-Shaaful Qina’a (2/69)].
Dalili zao ni:
1- Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Zayd asemaye: “Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka hadi sehemu ya kuswalia, akaomba mvua na kugeuza nguo yake wakati alipoelekea Qiblah. Akaanza na Swalaah kabla ya khutbah, kisha akaelekea Qiblah na kuomba”. [Isnadi yake ni Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (4/41) na asili yake ni kwenye Al-Bukhaariy (1027). Lakini humo hakuna ubainisho wa mahala pa shahidi].
2- Hadiyth ya Abu Hurayrah aliyesema: “Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka siku moja kwa ajili ya kuomba mvua. Akatuswalisha rakaa mbili bila ya adhana au iqaamah. Kisha akatukhutubia, akamwomba Allaah Mtukufu na akageuza nguo yake; kulia akakufanya kushoto na kushoto akakufanya kulia”. [Isnadi yake ni teketeke. Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (2/326) na Ibn Maajah].
Katika riwaya nyingine iliyopokelewa toka kwa Maalik na Ahmad, wao wanasema kwamba khutbah inakuwa kabla ya Swalaah. Hoja yao ni Hadiyth ya ‘Abdullah bin Zayd asemaye: “Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka kwa ajili ya kuomba mvua. Akaelekea Qiblah na kuomba, halafu akaipindua nguo yake. Kisha aliswali rakaa mbili ambapo alisoma kwa sauti ya kusikika”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1024) na Muslim (894)].
Inavyoonekana ni kuwa suala hili lina wasaa. Khutbah inaweza kuwa kabla ya Swalaah au baada ya Swalaah. Chaguzisho hili ni riwaya ya tatu kwa mujibu wa kauli ya Ahmad na chaguo la Ash-Shawkaaniy na wengineo.
Imesuniwa khutbah iendane sambamba na tukio lenyewe. Imamu aonyeshe kumhitajia kidhati Allaah, kujuta na kurejea Kwake. Ni kama alivyosema Ibn ‘Abbaas wakati ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu Anhu) alipomtaka aombe mvua: “Na hii mikono yetu tumeinyoosha Kwako ikiwa imejaa dhambi, na tosi zetu tumezielekeza Kwako tukitubu, basi Tuteremshie mvua”. [Al-Haafidh ameieleza kwenye Al-Fat-h (2/497) na ameinasibisha kwa Az Zubayr bin Bakkaar katika Al-Ansaab]
Na mfano wa maneno kama haya ambayo tutakuja kuyagusia baadaye.
3- Imamu akithirishe kuomba du’aa akiwa amesimama, ameelekea Qiblah, ameinyanyua juu kabisa mikono yake na kuelekeza mgongo wa viganja vyake mbinguni. Watu nao wanyanyue mikono yao na imamu apindue nguo yake.
Imepokelewa toka kwa ‘Abdullah bin Zubayr akisema: “Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka pamoja na watu kwa ajili ya kuwaombea mvua. Akasimama na kumwomba Allaah hali ya kuwa amesimama, kisha akaelekea Qiblah, akalipindua joho lake na watu wakapata mvua”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1023), na Ad-daaramiy (1534)].
Imepokelewa na Anas akisema: “Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa hanyanyui mikono yake miwili kwa lolote analoliomba isipokuwa katika du’aa ya kuomba mvua. Katika du’aa hii, alikuwa akinyanyua mikono mpaka weupe wa kwapa zake huonekana”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1031) na Muslim (895)].
Imepokelewa na Anas akisema: “Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliomba mvua akaelekeza mgongo wa viganja vyake mbinguni”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (896), Abu Daawuud (1171) na Ahmad (3/153)].
Na katika tamshi la Abu Daawuud: “Alikuwa akiomba mvua hivi, akanyoosha mikono yake (akaelekeza matumbo yake chini) mpaka nikaona weupe wa kwapa zake”.
An Nawawiy kasema: “Maulamaa wamesema: “Ni Sunnah kunyanyua mikono miwili na kuelekeza mgongo wa viganja mbinguni katika kila du’aa ya kuomba kuondoshwa janga. Na anapoomba mtu jambo lolote aelekeze viganja vyake mbinguni”.
Mwingine kasema: “Hikma ya kuashiria kwa mgongo wa viganja wakati wa kuomba mvua pasina du’aa nyingine, ni kuweka rajua njema ya kugeuka hali toka juu kuja chini kama ilivyosemwa kuhusiana na kupindua nguo, au ni ishara ya picha ya chenye kuombwa ambacho ni kuteremka mvua kuja ardhini”. [Fat-hul Baariy (3/601)]
Ama watu kunyanyua mikono yao, hayo yako kwenye Hadiyth ya Anas ikizungumzia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuomba mvua siku ya ijumaa juu ya mimbari: “..Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akanyanyua mikono yake akiomba, na watu wakanyanyua mikono yao pamoja naye wakiomba”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1029)].
Ama imamu kupindua nguo yake kulikoelezewa kwenye Hadiyth ya ‘Abdullah bin Zayd, maana yake ni kuuleta upande wa kulia wa nguo yake upande wa kushoto na kinyume chake, na hili limependelewa na Jamhuri ya Maulamaa. Wengine wamesema kuwa ni vizuri kuipindua nguo nje kuifanya ndani, na ndani nje kutokana na Hadiyth ya Ibn Zayd asemaye: “ Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali Swalaah ya kuomba mvua akiwa amejitanda guo la mistari. Akataka kuileta sehemu yake ya chini juu, na ilipomlemea aliipindua juu ya mabega “. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (4/41), Abu Daawuud (1164) na Al-Bayhaqiy (3/351). Angalia Al-Irwaa (3/142)].
Hikma ya yote hayo ni kuweka rajua njema ya kubadilika hali ya mambo, na wakati wa kupindua nguo ni baada ya kumaliza khutba.
4- Du’aa swahiyh za kuomba
(a) Imepokelewa toka kwa Jaabir akisema: “Wanawake waliokuwa wakilia walimjia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:
(( Allaahumma Isqinaa ghaythan mughiythan, mariy-an naafi’an ghayra dhwaarrin ‘aajilan ghayra aajilin)), na hapo hapo mawingu yakafunga. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1169), Al-Haakim (1/327) na Al-Bayhaqiy, na kwa njia yake Al-Bayhaqiy (3/355)].
(b) Imepokelewa toka kwa ‘Amri bin Shu’ayb toka kwa baba yake toka kwa babu yake akisema: “Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa akiomba mvua alikuwa akisema:
((Allaahumma Isqi ‘ibaadaka wa bahaaimaka, wanshur Rahmataka, wa Ahyi baladaka al mayyit)). [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1176)].
(c) Wakati ukame ulipoingia na Nabiy akawaahidi watu kutoka, ‘Aaishah anaelezea akisema: “Alikaa juu ya mimbari, akapiga takbiyr na akamhimidi Allaah ‘Azza wa Jalla kisha akasema: ((Hakika nyinyi mmeshtakia ukame wa nyumba zenu na kuchelewa mvua wakati wake. Na Allaah Subhaanah Amekuamuruni mumwombe, Naye Amekuahidini kuwa Atakujibuni)). Kisha akasema:
(( الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ● الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ)) Laailaaha illa Allaahu Yaf’alu maa Yuriydu. Allaahumma Anta Allaahu laa ilaaha illaa Anta. Anta Al-Ghaniyyu wanahnul fuqaraau, Anzil ‘Alaynaa alghaytha, Waj-’al maa Anzalta lanaa quwwatan wa balaaghan ilaa hiyn)). [Al-Albaaniy kasema ni Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1173) na Al-Haakim (1/328). Angalia Al-Irwaa (668)].
5- Imamu awaswalishe rakaa mbili kama Swalaah ya ‘Iyd na asome kwa sauti
Ni kutokana na Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas iliyotangulia isemayo: “Akaswali rakaa mbili kama anavyoswali ‘Iyd”. [Al-Albaaniy kasema ni Hasan: Tumeitaja nyuma kidogo].
Pia Hadiyth ya ‘Abdullah bin Zayd isemayo: “Kisha akaswali rakaa mbili na akasoma kwa sauti”. [Hadiyth Swahiyh: Tumeitaja nyuma kidogo].
· Kuomba Du’aa Ya Mvua Bila Kuswali
Imethibiti toka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) njia kadhaa za kuomba mvua bila kutoka kwenda kuswali. Kati yake ni:
1- Kuomba du’aa ya mvua katika khutbah ya ijumaa
Imepokelewa toka kwa Anas akisema: “Mtu mmoja aliingia Msikitini siku ya ijumaa - na Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa amesimama anakhutubu – na mtu yule akamwelekea Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa amesimama kisha akamwambia: Ee Nabiy wa Allaah! Mali zimeangamia na mambo yameshindikana, basi tuombee Allaah Atuokoe. Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akanyanyua mikono yake kisha akasema: ((Ee Mola Tuokoe, ee Mola Tuokoe!)). Anas anasema: “Wallaah, hatuoni mbinguni wingu lolote wala vijiwingu vilivyotawanyika, wala hakuna baina yetu na mlima nyumba yoyote. Kisha likachomoza nyuma yake wingu mithili ya ngao ya vita. Lilipofika katikati ya mbingu lilitawanyika, kisha likateremsha mvua. Wallaahi, hatukuliona jua siku sita. Kisha akaingia mtu mwingine kupitia mlango ule – huku Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa amesimama anakhutubu – kisha akamwelekea akiwa amesimama na kumwambia: Ee Nabiy wa Allaah! Mali zimeangamia na mambo yameshindikana, basi tuombee Allaah Aisimamishe. Nabiy wa Allaah Akanyanyua mikono yake kisha akasema: ((Ee Mola! Inyeshe pembezoni mwetu na si juu yetu. Ee Mola! Iteremshe juu ya vilima, milima tambarare, viini vya mabonde na maoteo ya miti)). Mvua ikakatika, tukatoka Msikitini tukitembea kwenye jua.” [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1041) na Muslim (897)].
Katika Hadiyth hii kuna faida kadhaa ambazo ni: kuingiza du’aa ya kuomba mvua kwenye khutbah ya ijumaa, kuiomba du’aa hiyo juu ya mimbari bila kupindua nguo wala kuelekea Qiblah, kuifanya Swalaah ya Ijumaa ni sehemu ya Swalaah ya kuomba mvua na kujuzu kuomba du’aa ya mvua bila Swalaah mahsusi. [Fat-hul Baariy: (2/589) Chapa ya As Salafiyyah]
2- Kuomba du’aa ya mvua siku isiyo ijumaa na bila ya Swalaah
Ni kama ilivyokuja kwenye Hadiyth ya Jaabir aliyesema: “Wanawake wenye kulia walimjia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Nabiy akaomba:
((Allaahumma Isqinaa ghaythan mughiythan, mariy-an naafi’an ghayra dhwaarrin ‘aajilan ghayra aajilin)), mbingu zikafunga)). [Hadiyth Swahiyh: Tumeitaja nyuma kidogo].
3- Kuomba du’aa nje ya Msikiti
Imepokelewa toka kwa ‘Umayr mwachwa huru wa ‘Abul Lahm ya kwamba alimwona Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiomba du’aa ya mvua mbele ya Ahjar Az Zayt karibu na Az Zawraa akiwa amesimama. Anaomba akiwa amenyanyua mikono yake miwili ikiwa mkabala na uso wake na wala haikuvuka kichwa chake. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1168), At-Tirmidhiy (557), An-Nasaaiy (3/159) na Ahmad (5/223)].
· Yanayosemwa Na Kufanywa Wakati Mvua Inaponyesha
1- Imesuniwa kuomba kwa du’aa Swahiyh zilizopokelewa. Kati ya du’aa hizo ni:
(a) Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu Anha) ya kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapoiona mvua husema: ((Allaahumma swayyiban naafi’an)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1032) na Ibn Maajah (3889)].
(b) Pia imepokelewa toka kwa ‘Aaishah akisema kwamba Nabiy alipokuwa akiona mvua husema: ((Rahmatun)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (899) katika sehemu ya Hadiyth].
2- Ni wajibu aamini kwamba wamepata mvua kwa Fadhila za Allaah na Rahma Zake na si kutokana na nyota au sayari
Imepokelewa toka kwa Zayd bin Khalid Al-Juhaniy (Radhwiya Allaahu Anhu) akisema: “Nabiy wa Allaah alituswalisha Swalaah ya Alfajiri huko Al- Hudaybiyah baada ya kunyesha usiku mvua. Alipomaliza Swalaah, aliwaelekea watu akasema: Je, mnajua nini Kasema Mola wenu? Wakasema: " Allaah na Nabiy Wake Ndio wanaojua zaidi". Akasema: Amesema Mola wenu: Amepambaukiwa kati ya Waja Wangu mwenye kuniamini mimi na mwenye kunikufuru. Ama mwenye kusema: Tumepata mvua kwa Fadhila za Allaah na Rahma Zake, basi huyo ni mwenye kuniamini Mimi na mwenye kuzikataa nyota. Ama mwenye kusema: Tumepata mvua kwa mashukio kadha wa kadha ya nyota au sayari, basi huyo amenikufuru Mimi na ameziamini nyota)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (846) na Muslim (71)].
Ikiwa mtu ataamini kwamba mashukio ya nyota yanaleta mvua, basi huu ni ukafiri, kwani huyo anakuwa amemkufuru Allaah. Na kama hakuitakidi hivyo - lakini akasema kwa njia ya majazi nailhali anaamini kwamba mwenye kuleta mvua ni Allaah Peke Yake kwa kuwa mvua imekuwa ni ada yake kunyesha wakati nyota zinaposhuka – basi hiyo inakuwa ni shirki ndogo kwa kuwa ameinasibisha Neema ya Allaah kwa kitu kinginecho, na kwa kuwa Allaah Hakuyafanya mashukio ya nyota kuwa ni sababu ya kunyesha mvua, bali mvua ni kutokana na Fadhila za Allaah na Rahma Zake. Anaizuia Anapotaka na Huiteremsha Anapotaka. [Fat-hul Majiyd (uk. 455-459) kwa mabadilisho kidogo na ufupisho]
3- Imesuniwa kuomba du’aa wakati mvua inaponyesha kwani ni wakati wa uhakika wa kujibiwa du’aa (kama Hadiyth itakuwa ni Swahiyh)
Ni kutokana na yaliyohadithiwa toka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliposema: ((Papieni kupata majibu ya du’aa zenu wakati majeshi yanapokutana, Swalaah inapoqimiwa na mvua inaponyesha)). [Al-Albaaniy kasema ni Hadiyth Swahiyh: Angalia Silsilat As-Swahiyhah (1469) na Swahiyhul Jaami’i (1026)].
4- Imesuniwa aiachie sehemu ya mwili wake ipigwe na mvua
Imepokelewa toka kwa Anas akisema: “Mvua ilitunyeshea tukiwa pamoja na Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Nabiy akaifunua sehemu ya mwili wake ikapigwa na mvua. Tukasema: Ee Nabiy wa Allaah! Kwa nini umefanya hivyo? Akajibu: ((Kwa kuwa bado i-mbichi toka kwa Mola wake Mtukufu)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (898) na Abu Daawuud (5100)].
5- Mvua ikikithiri na madhara yake yakahofiwa
Imesuniwa aombe kwa kunyanyua mikono yake miwili – kama tulivyoeleza kwenye Hadiyth ya Anas ya kuombwa du’aa juu ya mimbari Siku Ya Ijumaa -, aseme: (( Allaahumma hawaalaynaa walaa ‘alaynaa. Allaahumma ‘alal-aakaam, wadh-dhuraab, wabutuunil awdiyah wamanaabit ash-shajarah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1014) na Muslim 897)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
034-Sijdah Ya Kisomo
Alhidaaya.com [3]
· Taarifu Yake:
Sijdah ya kisomo ni sijdah ambayo mtu husujudu kwa kusoma au kusikia Aayah ya Qur-aan Tukufu kati ya Aayah za sijdah.
· Fadhila Yake:
Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah akisema: Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwanadamu anaposoma Aayah ya sijdah akasujudu, shaytwaan hujitenga kando akilia huku akisema: Ee maangamivu yangu! Ameamuriwa kusujudu akasujudu, naye ataipata Pepo, nami niliamuriwa kusujudu nikakataa, nami nitaupata moto)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (81), Ibn Maajah (1052) na Ahmad (9336)].
Kuna Hadiyth nyingi zilizothibiti zinazozungumzia kiujumla kuhusiana na fadhila za sijdah hii. Kati ya hizo ni:
- Hadiyth ya Abu Hurayrah kuhusiana na kufufuliwa na shifaa isemayo: ((Mpaka Atakapotaka Allaah rahma kwa Awatakao kati ya watu wa motoni, Atawaamuru Malaika wawatoe wale waliokuwa wakimwabudu Allaah. Watawatoa na watawajua kutokana na athari za sijdah, kwani Allaah Ameuharamishia moto kuila athari ya sijdah. Watatoka motoni, na mwili wote wa mwanadamu utaliwa na moto isipokuwa athari ya sijdah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (806) na Muslim (182)].
- Hadiyth ya Thawbaan mwachwa huru wa Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambapo alimuuliza Nabiy kuhusu amali ambayo Allaah Atamwingiza kwayo Peponi. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: ((Jilazimishe kukithirisha sijdah, kwani wewe hupati kusujudu sijdah moja kwa ajili ya Allaah, isipokuwa Allaah Hukunyanyulia kwayo daraja moja na Hukupomoshea kwayo kosa moja)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (488), At-Tirmidhiy (388), An-Nasaaiy (2/238) na Ibn Maajah (1423)].
- Hadiyth ya Rabiy’ah bin Ka’ab Al-Aslamiy ya kwamba alimwomba Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) awe pamoja naye peponi, Nabiy akamwambia: ((Jisaidie mwenyewe kwa kukithirisha sijdah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (489), Abu Daawuud (1320), An-Nasaaiy (2/227) na Ahmad (4/59)].
· Hukmu Yake:
Maulamaa wote wamekubaliana kuwa sijdah ya kisomo ipo kisharia kutokana na Aayah na Hadiyth zinazolizungumzia jambo hilo kama Hadiyth ya Ibn ‘Umar asemaye: “Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitusomea Suwrah yenye Aayah ya sijdah, kisha yeye husujudu nasi tunasujudu pamoja naye mpaka mmoja wetu anakosa sehemu ya kuweka paji lake. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1075) na Muslim (575)].
Kisha Maulamaa hao wamekhitalifiana kuhusiana na wajibu wake juu ya kauli mbili:
Ya kwanza:
Ni wajibu. Hii ni kauli ya Ath-Thawriy, Abu Haniyfah, riwaya toka kwa Ahmad na chaguo la Sheikh wa Uislamu Ibn Taymiyah. [Fat-hul Qadiyr (1/382), Ibn ‘Aabidiyn (2/103), Majmu’u Al-Fataawaa (23/139-155) na Al-Inswaaf (2/193)]
Ya pili:
Ni Sunnah, na si wajibu. Ni kauli ya Jamhuri; Maalik, Ash-Shaafi’iy, Al-Awzaa’iy, Al-Layth, Ahmad, Is-Haaq, Abu Thawr, Daawuud na Ibn Hazm. Pia katika Maswahaba ni pamoja na ‘Umar bin Al-Khattwaab, Salmaan, Ibn ‘Abbaas, na ‘Imraan bin Haswiyn. [Al-Majmu’u (4/61), Kash-Shaaf Al-Qinaa (1/445), Al-Mawaahib (2/60), At-Tamhiyd (19/133) na Al-Muhallaa (5/105)]
Wenye kusema ni wajibu wameleta hoja zifuatazo:
1- Kauli Yake Ta’alaa:
((فَمَا لَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ● وَإِذَا قُرِئَ عَلَيْهِمُ الْقُرْآنُ لَا يَسْجُدُونَ))
(( Basi wana nini hawaamini? ● Na wanaposomewa Qur-aan, hawasujudu)). [Al-Inshiqaaq (84:20 na 21)].
Wanasema kwamba mtu halaumiwi isipokuwa kwa kuacha la wajibu.
2- Kauli Yake Ta’alaa:
((فَاسْجُدُوا لِلَّـهِ وَاعْبُدُوا))
((Basi msujudieni Allaah na mwabuduni Yeye)). [An-Najm 53:62)]
3- Kauli Yake Ta’alaa:
((كَلَّا لَا تُطِعْهُ وَاسْجُدْ وَاقْتَرِب))
(( Laa hasha! Usimtii; na sujudu na kurubia (kwa Allaah) )). [Al-‘Alaq (96:19)].
Wanasema kuwa agizo katika aya mbili ni la wajibu.
4- Yaliyomo kwenye Hadiyth ya Abu Hurayrah iliyopita: ((Mwanadamu ameamuriwa kusujudu akasujudu, naye ataipata Pepo)). [Hadiyth Swahiyh: Tumeitaja nyuma kidogo katika mlango huu].
5- Kauli ya ‘Uthmaan: “Hakika sijdah ni wajibu kwa mwenye kusikiliza”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abu Shaybah (4220), ‘Abdul Razzaaq (5906) na Al-Bayhaqiy (2/324)].
Jamhuri wamewajibu:
1- Kulaumiwa katika Aayah ya Suwrat Al-Inshiqaaq kunafungamana na kuacha sijdah kwa kugomea na kibr. Hivyo kunamgusa mwenye kuacha ambaye haamini fadhila yake wala uwepo wake.
2- Kutoa dalili kwa Aayah mbili za mwisho kutazingatiwa ikiwa agizo kwenye Aayah hizo ni la wajibu, na makusudio ya sijdah yawe ni sijdah ya kisomo, na yote mawili hayaingii hapo. [Tuhfat Al-Ahwadhiy (3/172)]
Ninasema: “Imepokelewa toka kwa Zayd bin Thaabit akisema: “Nilimsomea Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) “Wan-Najm”, naye hakusujudu.” Na katika riwaya nyingine: “Hakusujudu yeyote kati yetu”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1072) na Muslim (577)].
“Agizo katika Aayah mbili za mwisho linachukuliwa ima ni la Sunnah, au muradi wake ni sijdah ya Swalaah, au ni la wajibu katika Swalaah ya faradhi, au kwa mujibu wa qaaidah ya Ash-Shaafi’iy ni Sunnah kwa kuzingatia maana zake mbili kwa pamoja”. [Fat-hul-Baariy (2/648) kwa mfanowe]
3- Imehadithiwa kwamba ‘Umar bin Al-Khattwaab alisoma siku ya ijumaa juu ya mimbari Suwrat An-Nahl. Alipofika Aayah ya sijdah, aliteremka akasujudu na watu nao wakasujudu. Ijumaa iliyofuatia, aliisoma sura hiyo hiyo na alipofika Aayah ya sijdah alisema: “Enyi watu! Hakika sisi tunaipita sijdah, mwenye kusujudu basi kafanya la sawa, na asiyesujudu, basi hana makosa”. Na ‘Umar (Radhwiya Allaahu Anhu) hakusujudu. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1077)].
Aliyasema hayo mbele ya hadhira ya Maswahaba, na hakuna yeyote aliyepinga, na ikawa ni Ijma’a kwao wote.
Ninasema: “Sheikh wa Uislamu ana minakasha ya kuzijadili dalili za Jamhuri ya Maulamaa na anayependa anaweza kuipitia. Lililo sahihi zaidi ni kauli ya Jamhuri. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
· Inavyofanyika:
1- Mafuqahaa wamekubaliana kwamba sijdah ya kisomo ni sijdah moja tu.
2- Sijdah inakuwa kwa muundo ule ule wa sijdah ya Swalaah kwa kuweka chini mikono miwili, magoti mawili, miguu miwili, pua na paji la uso. Pia, kwa kuweka mbali vifundo vya mikono na mbavu, na tumbo na mapaja mawili, mbali na kuelekeza vidole Qibla na mengineyo yaliyotangulia.
3- Kwa mujibu wa kauli iliyo sahihi zaidi, haikatazwi kupiga takbiyr ya kuhirimia wala kutoa tasliym. Sheikh wa Uislamu amesema katika Al-Fataawaa (23/165): “Hii ndio Sunnah ijulikanayo toka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Masalaf wote wameishika, na Maimamu mashuhuri wameielezea”.
Ninasema: “Ibn ‘Abdul Barri katika At-Tamhiyd (19/134) amenukuu toka kwa Maalik, Ash-Shaafi’iy, Ahmad na Abu Haniyfah wakisema kwamba tasliym hakuna. Kisha akasema (23/166): Lililohadithiwa kuhusiana na hilo toka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni takbiyr moja, kwani mtu haguri kutoka ‘ibaadah moja kwenda nyingine”.
Ninasema: “Anaashiria Hadiyth ya Ibn ‘Umar aliyesema: “Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitusomea Qur-aan. Akipita Aayah ya sijdah hupiga takbiyr na husujudu sijdah mbili”. [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1413), Al-Bayhaqiy (2/325) na ‘Abdul Razzaaaq (5911). Angalia Al-Irwaa (472)].
Lakini, dalili ya kujuzu kupiga takbiyr wakati wa kusujudu na kunyanyuka toka kwenye sijdah inaweza kupatikana kwenye Hadiyth ya Waail bin Hujr aliyesema kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akinyanyua mikono yake miwili pamoja na takbiyr, na hupiga takbiyr kila anapokwenda chini na kila anaponyanyuka. [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (4/316), Ad-daaramiy (1252) na At-Twayaalsiy (1021). Angalia Al-Irwaa (2/36)].
Jamhuri wanaona ni vyema kupiga takbiyr wakati wa kusujudu na kunyanyuka toka kwenye sijdah.
Ninasema: “Inajuzu kunyanyua mikono miwili pamoja na takbiyr vile vile. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
4- Mwenye kutaka kusujudu sijdah ya kisomo naye hayuko kwenye Swalaah, ni bora zaidi kwake asimame kwanza, kisha apomoke kwenda kwenye sijdah. Hii ni kauli ya Mahanbali, baadhi ya Mahanafi waliofuatia, inakubalika kwa Ash-Shaafi’iy, na ni chaguo la Sheikh wa Uislamu. [Al-Badaai-’i (1/192), Matwaalib Ulin Nuhaa (1/586) na Majmu’u Al-Fataawaa (23/173)]
Wamesema: الخرور “Al-Khuruwr” ni kuporomoka toka kwenye kisimamo. Allaah Amesema:
(( قُلْ آمِنُوا بِهِ أَوْ لَا تُؤْمِنُوا ۚ إِنَّ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ مِن قَبْلِهِ إِذَا يُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ يَخِرُّونَ لِلْأَذْقَانِ سُجَّدًا ))
(( Sema: “Iaminini au msiamini. Hakika wale waliopewa elimu kabla yake wanaposomewa (Qur-aan) wanaporomoka kifudifudi wanasujudu”)). [Al-Israa (17:107)]
Na ikiwa hakufanya na akasujudu bila kusimama, basi hakuna ubaya. Ash-Shaafi’iy na wafuasi wake wengi wanasema kwamba hakuna chochote kinachotegemewa chenye kuthibitisha kusimama huko, bali ni bora kuacha. [Al-Majmu’u (4/65)]
· Je, Ni Sharti Kuwa Twahara Na Kuelekea Qiblah Kwa Ajili Ya Sijdah Ya Kisomo?
Jamhuri ya Maulamaa wanasema kwamba yenye kushurutishwa kwenye Swalaah, hushurutishwa vile vile kwenye sijdah ya kisomo. Wanasema ni lazima mtu awe twahara, aelekee Qiblah pamoja na masharti mengineyo. [Ibn ‘Aabidiyn (2/106), Ad-Dusuwqiy (1/307), Al-Majmu’u (4/63) na Al-Mughniy (1/650)]
Lakini Ibn Hazm na Sheikh wa Uislamu hawakushurutisha hayo kwa kuwa sijdah si Swalaah, bali ni ‘ibaadah. Ni maarufu kwamba kiini cha ‘ibaadah yenyewe haishurutishiwi twahara. Ni kauli ya Ibn ‘Umar, Ash-Shu’abiy na Al-Bukhaariy, nayo ndiyo sahihi.
Linaloonyesha hilo ni Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas asemaye kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisujudu aliposoma An-Najm, akasujudu, na wakasujudu pamoja naye Waislamu, washirikina, majini na watu. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1071) na At-Tirmidhiy (575)].
Al-Bukhaariy amesema kwenye Fat-h (2/644): “Mshirikina ni najisi, hana wudhuu”.
Ash-Shawkaaniy amesema: “Katika Hadiyth zenye kuzungumzia kuhusu sijdah za kisomo, hakuna chochote chenye kuonyesha kwamba mwenye kusujudu ni lazima awe na wudhuu. Waliokuwepo kwenye kisomo cha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) walikuwa wakisujudu pamoja naye, na wala haikunukuliwa kwamba alimwamuru yeyote kati yao kutawadha, na haiwezekani wawe wote na wudhuu. Aidha, washirikina walikuwa wakisujudu pamoja na Nabiy kama ilivyotangulia, nao ni najisi na wudhuu wao haufai. Ama kusitiri uchi na kuelekea Qiblah pamoja na kuweza, hilo limesemwa kuwa linazingatiwa kwa itifaki”. [Naylul Awtwaar (3/125) chapa ya Al-Hadiyth]
Ninasema: “Madhali sijdah si Swalaah, basi si lazima kuelekea Qiblah kama walivyosema Ibn Hazm na Ibn Taymiyah. Lakini hakuna shaka ya kwamba kusujudu mtu akiwa na twahara na akaelekea Qiblah, inakuwa ni bora na ukamilifu zaidi, na haitakikani kuliacha hilo bila ya udhuru. Ama kushurutisha, hilo halitakikani na Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
· Namna Anavyosujudu Mtembeaji Kwa Miguu Na Aliye Kwenye Kipando
Anayesoma au anayesikia Aayah ya sajdah na akawa anatembea kwa miguu au yuko kwenye kipando, kisha akataka kusujudu, basi huyo ataashiria kwa kichwa chake upande wowote ule. Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar ya kwamba aliulizwa kuhusiana na sijdah mtu akiwa juu ya mnyama akajibu akisema: “Sujudu na ashiria”. Hili limesimuliwa na Ibn Abi Shaybah (4210) kwa Sanad Swahiyh. Kundi la Masalafi katika masahibu wa Ibn Mas-’oud na wengineo wamepitisha kwa njia sahihi kwamba mtembeaji huashiria kwa kichwa.
· Yasemwayo Kwenye Sijdah Ya Kisomo
1- Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu Anha) akisema: “Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisema mara nyingi katika sijdah za Qur-aan usiku: ((Sajada wajhiy lil-ladhiy Khalaqahu wa Swawwarahu wa Shaqqa sam-’ahu wa baswarahu bihawlihi wa quwwatihi)). [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1414), At-Tirmidhiy (580) na An-Nasaaiy (2/222). Kuna mvutano kuhusu Sanad yake, nayo kwa hali zote ni Dhwa’iyf. Angalia Fat-hur Rahmaan cha Sheikh wetu Abu ‘Umayr uk. 99. Ninasema: “Kuna Hadiyth mwenza Marfu’u Swahiyh iliyopokelewa toka kwa ‘Aliy kuhusiana na sijdah za Swalaah ambayo imesimuliwa na Muslim”]
2- Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Abbaas akisema: “Alikuja mtu mmoja kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Ee Nabiy wa Allaah! Nilipolala usiku, nilijiona kana kwamba naswali nyuma ya mti, kisha nikasujudu na mti nao ukasujudu kama nilivyosujudu, halafu nikausikia ukisema: Ee Allaah! Niandikie kwayo Kwako thawabu, na Uniondoshee kwayo makosa, na Uniwekee Kwako akiba, na Uitakabalie kwangu kama Ulivyoitakabali kutoka kwa Mja Wako Daawuud”. Ibn ‘Abbaas anaendelea kusema: “Hapo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasoma Aaya ya sajdah akasujudu, kisha nikamsikia anasema mfano wa aliyomwelezea mtu yule kuhusiana na matamshi ya mti”. [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (5790), Ibn Maajah (1053) na wengineo. Ina Hadiyth mwenza ambayo haiiongezei hii ila udhwa’iyf zaidi. Lakini pamoja na hivyo, Sheikh Abul Ashbaal (Rahimahul Laahu) amesema kwamba ni Hadiyth Swahiyh. Angalia Fat-hur Rahmaan uk. 100]
Ninasema: “Hadiyth hizi mbili ni Dhwa’iyf kwa mujibu wa kauli yenye nguvu zaidi. Kuhusu Hadiyth ya kwanza, ipo Hadiyth nyingine mwenza inayohusiana na sijdah za Swalaah. Imam Ahmad ameashiria kutothibiti hilo aliposema: “Ama mimi, nitasema: Subhaana Rabbiyal A’alaa”. Ikiwa mambo ni hivi, basi adhkaari za sijdah ya kisomo zitakuwa ni zile tulizozitaja nyuma katika sijdah ya Swalaah. Kati ya hizo, ni zile za Bibi ‘Aaishah zilizotajwa nyuma kidogo. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
·Ni Nani Mlengwa Wa Hukmu Ya Sijdah Ya Kisomo?
Maulamaa wote wamekubaliana kwamba hukmu ya sijdah ya kisomo inamkusudia msomaji wa Aayah yoyote ya sijdah sawasawa akiwa ndani ya Swalaah au nje ya Swalaah. Halafu wakakhitalifiana kuhusiana na msikiaji, je itampasa kusujudu au la? Wamekhitalifiana juu ya kauli mbili: [Al-Badaai-’i (1/192), Ad-Dusuwqiy (1/307), Bidaayatul Mujtahid (1/329) Al-Majmu’u (4/72) na Matwaalib Ulin Nuhaa (1/582)]
Ya kwanza:
Atasujudu tu hata kama msomaji hakusujudu. Ni kauli ya Abu Haniyfah, Ash-Shaafi’iy na riwaya toka kwa Maalik.
Ya pili:
Hatosujudu isipokuwa tu kama atakusudia kusikiliza na msomaji ambaye anafaa kuwa imamu akasujudu. Ni kauli ya Ahmad na riwaya toka kwa Ahmad. Hoja zao ni:
1- Hadiyth ya Ibn ‘Umar aliposema: “Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitusomea Suwrah yenye Aaya ya sajdah, akasujudu nasi tukasujudu mpaka baadhi yetu wakakosa sehemu ya kuweka paji la uso”. [Hadiyth Swahiyh: Imeshatajwa kwenye mlango wa hukmu ya sijdah ya kisomo].
2- Yaliyosimuliwa ya kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliambiwa: “Fulani alisoma kwako Aayah ya sajdah ukasujudu, nami nimesoma kwako hukusujudu?” Akasema: ((Wewe ulikuwa imamu, na lau ungelisujudu, nasi pia tungesujudu)). [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ash-Shaafi’iy katika Musnadi yake (359) na Al-Bayhaqiy amepokea toka kwake (2/324). Angalia Al-Irwaa (473)].
3- Ibn Mas-’oud alimwambia Tamiym bin Hadhlam – naye ni kijana mdogo- aliposoma Aayah ya sijdah: “Sujudu, wewe ndiye imamu wetu hapo”. [Hadiyth Hasan kwa Sanad zake: Al-Bukhaary ameifanya Hadiyth Mu’allaq (2/648). Na Sa’iyd bin Mansour pamoja na Al-Bukhaariy kwenye At-Taariykhul Kabiyr, wameifanya kuwa Hadiyth Mawswuwl kama ilivyo kwenye At-Taghliyq (2/210). Ina Hadiyth mwenza kwa Al-Bayhaqiy na ‘Abdul Razzaaq ambayo Sheikh wetu amesema kuwa ni Hadiyth Hasan kwenye Fat-hur Rahmaan uk 114]
Hoja hizi zote zinaonyesha kwamba ni Sunnah kwa msikilizaji asujudu kama msomaji atasujudu, na kama hakusujudu, basi haki ya yeye kusujudu haina nguvu ingawa itakuwa bora kusujudu. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
· Sijdah Ya Kisomo Katika Nyakati Zisizoruhusiwa Kuswali
Sijdah ya kisomo inajuzu katika nyakati zisizoruhusiwa kuswali bila ukaraha kwa mujibu wa kauli yenye nguvu zaidi. Tushaeleza nyuma kuwa sijdah si Swalaah, na kwamba Hadiyth zinazozungumzia umarufuku zinahusiana na Swalaah pekee. Hii ni kauli ya Ash-Shaafi’iy na riwaya toka kwa Ahmad. Ibn Hazm kayasema haya haya. [Al-Mughniy (1/623), Al-Muhallaa (5/105) na Bidaayatul Mujtahid (1/328)]
Imesimuliwa toka kwa Ibn ‘Umar akisema kwamba ni karaha lakini Sanad yake ni Dhwa’iyf. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.
· Kukariri Kisomo Au Kuisikia Aayah Ya Sajdah Zaidi Ya Mara Moja
Kama akisoma, au akaisikiliza Aayah ya sajdah zaidi ya mara moja, anaweza kuakhirisha sijdah akaja kusujudu mara moja tu. Ikiwa atasujudu, kisha akasoma tena Aayah ya sijdah, basi itakuwa bora zaidi kwake asujudu mara nyingine tena. Na hii ni kauli ya Jamhuri kinyume na Abu Haniyfah. [Fat-hul Qadiyr (2/22), Ad-Dusuwqiy (1/311), Mughnil Muhtaaj (1/446) na Al-Inswaaf (2/196)]
· Kupitwa Na Sijdah Ya Kisomo
Imesuniwa kwa msomaji na msikilizaji kusujudu moja kwa moja baada ya Aayah ya sajdah hata kama watachelewa kidogo. Lakini kitambo kikirefuka kati ya sajdah na sababu yake, basi hawatosujudu kwa kuwa mahala pake pashapita. Hii ni kauli ya Ash-Shaafi’iy na Hanbali. [Al-Majmu’u (4/71-72) na Kash-Shaaf Al-Qinaa (1/445)]
· Sijdah Ya Kisomo Ndani Ya Swalaah
Imepokelewa toka kwa Abu Raafi’i akisema: “Niliswali pamoja na Abu Hurayrah Swalaah ya ‘Ishaa akasoma إذا السماء انشقت kisha akasujudu. Nikamwambia: Unafanya nini hivi? Akasema: Nilisujudu kwa Aayah hii nyuma ya Abul Qaasim (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), nami nitaendelea kusujudu kwayo mpaka nikutane naye”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (766) na Muslim (578)].
Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah akisema: “’Umar alisujudu kwenye “An-Najm” akasimama, kisha akaiunganishia Suwrah”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdul Razzaaq (5880) na At-Twahaawiy (1/355)].
Katika matukio haya mawili, inaonyesha kwamba imesuniwa kusujudu kwa anayesoma Aayah ya sijdah katika Swalaah yake bila ya kubagua kati ya Swalaah ya Faradhi au ya Sunnah, ni sawa akiwa peke yake au katika Jamaa, au Swalaah ya kimya au ya sauti. Hii ndiyo kauli ya Jamhuri. [Al-Badaai-’i (1/192), Kash-Shaaful Qinaa (1/449) na Mawaahibul Jaliyl (2/65)]
Lakini kwa mujibu wa kauli ya Jamhuri, ni karaha kwa imamu kuisoma katika Swalaah ya kimya ili asije kuwakanganya maamuma. Ash-Shaafi’iy anasema si karaha, bali imesuniwa aikawize sajdah mpaka atakapoimaliza Swalaah ili asiwakanganye maamuma kwa sharti kwamba kitambo kisirefuke. [Al-Majmu’u (4/72) na Nihaayatul Muhtaaj (2/95)]
· Je, Inajuzu Kuiruka Aayah Ya Sijdah Katika Swalaah?
Ni makruhu kwa mwenye kuswali kusoma Aayah nyinginezo na kuiruka Aayah ya sajdah ili asipate kusujudu. Hili limenukuliwa toka kwa kundi la Masalafi kama Ash-Sha’abiy, Ibn Al-Musayyib, Ibn Siyriyn, An-Nakh’iy na Is-Haaq. Jamhuri ya Maulamaa wamelikirihisha hili pia, nalo huitwa: “Katiza sajdah”. [Al-Badaai-’i (1/192), Kash-Shaaful Qinaa (1/449) na Ad-Dusuwqiy (1/309)]
· Faida
Imekirihishwa vile vile mtu kuzikusanya Aayah za sijdah, halafu akazisoma na kusujudu. [Al-Kaafiy cha Ibn Qudaamah (1/160), Al-Mudawwanah (1/111-112) na Rawdhwat At Twaalibiyna (1/323)]
· Ikiwa Sijdah Ni Mwisho Wa Suwrah, Atafanya nini?
Ikiwa Aayah ya sijdah iko mwisho wa Suwrah, mtu atachaguzwa kati ya mambo matatu:
1- Asujudu kisha asimame, halafu aiunganishe na Suwrah nyingine kisha arukuuu. Hili alilifanya ‘Umar (Radhwiya Allaahu Anhu). Alisoma Suwrat Yuwsuf katika Swalaah ya Alfajiri, akarukuu, kisha katika rakaa ya pili akasoma Suwrat An-Najm akasujudu, halafu akasoma إذا السماء انشقت . [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdul Razzaaq (2882) na At-Twahaawiy (1/355)]..
Na hili ndilo bora zaidi.
2- Arukuu, na rukuu itamtosheleza na sajdah.
(a) Imepokelewa toka kwa Naafi’i kwamba Ibn ‘Umar alikuwa anasujudu anapoisoma An Najm katika Swalaah, na kama hakusujudu hurukuu. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdul Razzaaq (5893).
(b) Ibn Mas-’oud aliulizwa kama mtu atarukuu au atasujudu kwenye Suwrah inayoishilia na Aayah ya sajdah akasema: “Kama hakuna kati yako na kati ya sajdah isipokuwa kurukuu, basi ndiyo iliyo karibu”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Shaybah (4371)
Ninasema: “Mahala pa hili ikiwa mtu anaswali peke yake, au akawa ni imamu na akajua kwamba hatowakanganya maamuma. Kama atahofia kuwakanganya, baadhi yao wakasujudu na wengine wakarukuu, basi asifanye hilo. Allaah Ndiye Mjuzi zaidi”.
3- Asujudu, kisha apige takbiyr asimame, halafu arukuu bila ya kusoma Suwrah nyingine.
· Akisoma Aayah Ya Sajdah Juu Ya Mimbari
[Al-Kaafiy cha Ibn Qudaamah (1/160), Al-Mudawwanah (1/111-112) na Rawdhwat At Twaalibiyna (1/323)]
Akipenda anaweza kuteremka akasujudu chini na watu watasujudu pamoja naye, na kama hakusujudu, basi hakuna ubaya kutokana na kitendo cha ‘Umar (Radhwiya Allaahu Anhu). [Hadiyth Swahiyh: Imeshaelezwa katika mlango wa hukmu za sijdah].
Na lau kama ataweza kusujudu juu ya mimbari, basi atasujudu hapo hapo, na watu watasujudu pamoja naye. Na ikiwa khatibu hakusujudu, maamuma hawaruhusiki kusujudu.
·
Mwahala Pa Kusujudu (Aayah za sajdah)
Mwahala (Aayah) pa kusujudu ni 15 katika Qur-aan Tukufu. Hili limeelezewa katika Hadiyth Marfu’u lakini Dhwa’iyf toka kwa ‘Amri bin Al-‘Aaswiy ya kwamba Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimsomea Aayah 15 za sijdah katika Qur-aan, tatu katika hizo zipo katika Suwrah fupi (Mufasswal), na mbili katika Suwrat Al-Hajj. [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1401), Ibn Maajah (1057), Al-Haakim (1/223) na Al-Bayhaqiy (2/214)].
Kati ya Aayah hizi 15, zipo kumi kati yake ambazo Maulamaa wamezipitisha bila hitilafu yoyote, na zipo nne ambazo Maulamaa wamehitalifiana ingawa zimeelezewa katika Hadiyth ambazo ni Swahiyh, na kuna Aayah moja ambayo haikuthibitishwa kwa Hadiyth Swahiyh lakini baadhi ya Maswahaba walikuwa wakisujudu wanapoisoma jambo ambalo linatutuza nyoyo juu ya uhalali wake.
(a) Aayah Za Sijdah Ambazo Maulamaa Hawakukhitilafiana
[Sharhul Ma’aaniy cha At-Twahaawiy (1/359), At-Tamhiyd (19/131) na Al-Muhalla (5/105)]
1- Al-A’araaf katika Neno Lake Ta’alaa:
((إِنَّ الَّذِينَ عِندَ رَبِّكَ لَا يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِهِ وَيُسَبِّحُونَهُ وَلَهُ يَسْجُدُونَ))
[Aayah 206]
2- Ar-Ra’ad katika Neno Lake Ta’alaa:
(( وَلِلَّـهِ يَسْجُدُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَظِلَالُهُم بِالْغُدُوِّ وَالْآصَالِ))
[Aayah 15]
3- An-Nahl katika Neno Lake Ta’alaa:
(( وَلِلَّـهِ يَسْجُدُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ مِن دَابَّةٍ وَالْمَلَائِكَةُ وَهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ • يَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوْقِهِمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ ))
[Aayah 49 na 50]
Imethibiti kwamba ‘Umar aliisoma juu ya mimbari siku ya ijumaa, kisha akateremka akasujudu. [Hadiyth Swahiyh: Tumeielezea kwenye mlango wa Hukmu ya kusujudu].
4- Al-Israa katika Neno Lake Ta’alaa:
(( قُلْ آمِنُوا بِهِ أَوْ لَا تُؤْمِنُوا ۚ إِنَّ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ مِن قَبْلِهِ إِذَا يُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ يَخِرُّونَ لِلْأَذْقَانِ سُجَّدًا • وَيَقُولُونَ سُبْحَانَ رَبِّنَا إِن كَانَ وَعْدُ رَبِّنَا لَمَفْعُولًا • وَيَخِرُّونَ لِلْأَذْقَانِ يَبْكُونَ وَيَزِيدُهُمْ خُشُوعًا))
[Aayah 107-109 ]
5- Maryam katika Neno Lake Ta’alaa:
((أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ مِن ذُرِّيَّةِ آدَمَ وَمِمَّنْ حَمَلْنَا مَعَ نُوحٍ وَمِن ذُرِّيَّةِ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْرَائِيلَ وَمِمَّنْ هَدَيْنَا وَاجْتَبَيْنَا ۚ إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُ الرَّحْمَـٰنِ خَرُّوا سُجَّدًا وَبُكِيًّا))
[Aayah 58]
6- Al Hajji katika Neno Lake Ta’alaa:
((أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ يَسْجُدُ لَهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ وَالنُّجُومُ وَالْجِبَالُ وَالشَّجَرُ وَالدَّوَابُّ وَكَثِيرٌ مِّنَ النَّاسِ ۖ وَكَثِيرٌ حَقَّ عَلَيْهِ الْعَذَابُ ۗ وَمَن يُهِنِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِن مُّكْرِمٍ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَفْعَلُ مَا يَشَاءُ ))
[Aayah 18]
7- Al-Furqaan katika Neno Lake Ta’alaa:
((وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اسْجُدُوا لِلرَّحْمَـٰنِ قَالُوا وَمَا الرَّحْمَـٰنُ أَنَسْجُدُ لِمَا تَأْمُرُنَا وَزَادَهُمْ نُفُورًا))
[Aayah 60]
8- An-Naml katika Neno Lake Ta’alaa:
((أَلَّا يَسْجُدُوا لِلَّـهِ الَّذِي يُخْرِجُ الْخَبْءَ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَيَعْلَمُ مَا تُخْفُونَ وَمَا تُعْلِنُونَ • اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ ))
[Aayah 25 na 26]
9- As-Sajdah katika Neno Lake Ta’alaa:
((إِنَّمَا يُؤْمِنُ بِآيَاتِنَا الَّذِينَ إِذَا ذُكِّرُوا بِهَا خَرُّوا سُجَّدًا وَسَبَّحُوا بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ ))
[Aayah 15]
10- Fusswilat katika Neno Lake Ta’alaa:
((وَمِنْ آيَاتِهِ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ ۚ لَا تَسْجُدُوا لِلشَّمْسِ وَلَا لِلْقَمَرِ وَاسْجُدُوا لِلَّـهِ الَّذِي خَلَقَهُنَّ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ • فَإِنِ اسْتَكْبَرُوا فَالَّذِينَ عِندَ رَبِّكَ يُسَبِّحُونَ لَهُ بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَهُمْ لَا يَسْأَمُونَ))
[Aayah 37 na 38]
(b) Aayah ambazo Maulamaa wamekhitalifiana kusujudu zinaposomwa na ambazo dalili za uthibitisho wake ni swahiyh
11- Swaad katika Neno Lake Ta’alaa:
((قَالَ لَقَدْ ظَلَمَكَ بِسُؤَالِ نَعْجَتِكَ إِلَىٰ نِعَاجِهِ ۖ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ الْخُلَطَاءِ لَيَبْغِي بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَقَلِيلٌ مَّا هُمْ ۗ وَظَنَّ دَاوُودُ أَنَّمَا فَتَنَّاهُ فَاسْتَغْفَرَ رَبَّهُ وَخَرَّ رَاكِعًا وَأَنَابَ ))
[Aayah 24]
Wanaosujudu wakiisoma Aayah hii ni Abu Haniyfah, Ath-Thawriy, Ahmad, Is-Haaq na Abu Thawr. [At-Tamhiyd (19/131), Al-Badaai-’i (1/193), Ad-Dusuwqiy (1/308), Al-Majmu’u (4/60) na Al-Mughniy (1/618)].
Dalili yao ni:
1- Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas aliyesema: “Swaad si katika mahala palipothibiti na kukokotezewa kusujudu, lakini mimi nilimwona Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisujudu hapo”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1069), Abu Daawuud (1409) na At-Tirmidhiy (577)].
2- Imepokelewa toka kwa Mujaahid –kuhusiana na sijdah ya Swaad – akisema: “Nilimuuliza Ibn ‘Abbaas: Ni wapi ilisujudiwa? Akasema: Je, hukusoma:
(( وَوَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ كُلاًّ هَدَيْنَا وَنُوحاً هَدَيْنَا مِن قَبْلُ وَمِن ذُرِّيَّتِهِ دَاوُودَ وَسُلَيْمَانَ وَأَيُّوبَ وَيُوسُفَ وَمُوسَى وَهَارُونَ وَكَذَلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ • وَزَكَرِيَّا وَيَحْيَى وَعِيسَى وَإِلْيَاسَ كُلٌّ مِّنَ الصَّالِحِينَ • وَإِسْمَاعِيلَ وَالْيَسَعَ وَيُونُسَ وَلُوطاً وَكُلاًّ فَضَّلْنَا عَلَى الْعَالَمِينَ • وَمِنْ ءابَائِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ وَإِخْوانِهِمْ وَاجْتَبَيْنَاهُمْ وَهَدَيْنَاهُمْ إِلَى صِراطٍ مُّسْتَقِيمٍ• ذلِكَ هُدَى اللَّهِ يَهْدِى بِهِ مَن يَشَآءُ مِنْ عِبَادِهِ وَلَوْ أَشْرَكُواْ لَحَبِطَ عَنْهُمْ مَّا كَانُواْ يَعْمَلُونَ • أُوْلَـئِكَ الَّذِينَ ءَاتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ فَإِن يَكْفُرْ بِهَا هَـؤُلاءِ فَقَدْ وَكَّلْنَا بِهَا قَوْماً لَّيْسُواْ بِهَا بِكَافِرِينَ • أُوْلَـئِكَ الَّذِينَ هَدَى اللَّهُ فَبِهُدَاهُمُ اقْتَدِهْ قُل لاَّ أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْراً إِنْ هُوَ إِلاَّ ذِكْرَى لِلْعَالَمِينَ))
Na Daawud amekuwa ni katika wale ambao Nabiy wenu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameamuriwa kumfuata, naye alisujudu hapo, na Nabiy wa Allaah alisujudu. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (4807), Ahmad (3215) na Al-Bayhaqiy (2/319)].
3- Imepokelewa na Mujaahid ya kwamba alimuuliza Ibn ‘Abbaas: “Je, ipo sajdah kwenye Swaad? Akajibu: “Ndio, kisha akasoma ووهبنا mpaka akafikia فبهداهم اقتده . Akasema: Yeye ni miongoni mwao. Na Ibn ‘Abbaas akasema: Nilimwona ‘Umar akisoma Swaad juu ya mimbari, akateremka na kusujudu hapo, kisha akapanda tena mimbari”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abu Shaybah (4267), ‘Abdul Razzaaq (5864) na Al-Bayhaqiy (2/319)].
4- Imepokelewa na As-Saaib bin Yaziyd akisema: “Nilimwona ‘Uthmaan akisujudu katika Swaad”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abu Shaybah (4257), ‘Abdul Razzaaq (5864) na Al-Bayhaqiy (2/319)].
· Sajdah Tatu Za Suwrah Fupi (Al-Mufasswal)
Hizi ni Aayah tatu za kusujudu kwa Abu Haniyfah, Ath-Thawriy, Ash-Shaafi’iy na Ahmad. [At-Tamhiyd (19/131), Al-Badaai-’i (1/193), Al-Majmu’u (4/62) na Al-Mughniy (1/617)]
12- An-Najm Aayah ya 62:
((فَاسْجُدُوا لِلَّـهِ وَاعْبُدُوا))
Dalili ya kuthibiti hili ni:
1- Hadiyth ya Abu Mas-’oud ya kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisoma Suwrat An-Najm akasujudu, na hakubaki yeyote katika watu ila alisujudu”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1070) na Muslim (576)].
Hadiyth kama hii iliyopokelewa na Ibn ‘Abbaas tushaitaja nyuma.
2- Kitendo cha ‘Umar cha kusujudu kwenye Suwrah hiyo kama ilivyoelezewa nyuma, na Sanad yake ni Swahiyh.
· Faida:
Kadhalika, imethibiti kuachwa sajdah kwenye Suwrah hiyo. Imepokelewa toka kwa Zayd bin Thaabit ya kwamba alimsomea Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) An-Najm lakini hakusujudu. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1072) na Muslim (577)].
13- Al-Inshiqaaq Aayah 20 na 21:
((وَإِذَا قُرِئَ عَلَيْهِمُ الْقُرْآنُ لَا يَسْجُدُونَ • بَلِ الَّذِينَ كَفَرُوا يُكَذِّبُونَ))
Dalili ni:
1- Ni kusujudu Abu Hurayrah hapo na kauli yake: “Nilisujudu kwa Aayah hii nyuma ya Abul Qaasim (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na nitaendelea kusujudu ikisomwa mpaka nitakapokutana naye”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (766) na Muslim (578)]
2- Pia kasema: “Abu Bakr na ‘Umar walisujudu katika إذا السماء انشقت naإ قرأ باسم ربك الذي خلق , na ni nani aliye bora zaidi kuliko wao?” [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy katika Al-Kubraa (1037), At-Twayaalisiy (2499) na Abul Razzaaq ( 5886)].
3- Imepokelewa kwa njia sahihi toka kwa Ibn ‘Umar, Ibn Mas-’oud na ‘Ammaar. [Angalia athari zilizopokelewa toka kwao katika “Fat-h Ar-Rahmaan Biahkaami Wa Mawaadhi’i Sujuudil Qur-aan” cha Sheikh wetu Abu ‘Umayr (Allaah Amhifadhi) (69,70)]
14- Al-‘Alaq Aayah ya 19:
((كَلَّا لَا تُطِعْهُ وَاسْجُدْ وَاقْتَرِب))
Imetangulia kabla yake Hadiyth ya Abu Hurayrah ya kuthibiti hilo toka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Abu Bakr na ‘Umar.
(c) Aayah ambayo Maulamaa wote wamekhitalifiana na hakuna Hadiyth yoyote Swahiyh inayothibitisha
15- Al-HajjiAayah ya 77:
((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ارْكَعُوا وَاسْجُدُوا وَاعْبُدُوا رَبَّكُمْ وَافْعَلُوا الْخَيْرَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ))
Ni Aayah ambayo Ash-Shaafi’iy na Ahmad wanasujudu wanapoisoma. [At-Tamhiyd (19/131), Al-Majmu’u (4/62) na Al-Mughniy (1/618)]
Kuna Hadiyth ya ‘Uqbah bin ‘Aamir kuhusiana na hili ambapo ‘Uqbah alimuuliza Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama kwenye Al-Hajji kuna sajdah mbili. Nabiy akasema: ((Ndio, asiyesujudu anapoisoma, basi asiisome)). [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1402), At-Tirmidhiy (578) na Ahmad (4/151)]
Ni Hadiyth Dhwa’iyf iliyofanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1402), At-Tirmidhiy (578) na Ahmad (4/151) ingawa Maswahaba wote wameisema wakiwemo ‘Umar bin Al-Khattwaab, ‘Aliy, Ibn ‘Abbaas, Ibn Mas-’oud, Abu Muusa, Abud Dardaai, na ‘Ammaar bin Yaasir (Radhwiya Allaahu Anhum).
Kadhalika, Abu ‘Abdul Rahmaan As-Sulamiy, Abul ‘Aaaliyah na Zurri bin Jaysh. Ibn Qudaamah amesema: “Hatujasikia yeyote aliyeikataa katika enzi yao”.
Ninasema: “Hili linatutuza nyoyo juu ya kuswihi kwake, na Allaah Ndiye Ajuaye zaidi”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
035-Sijdah Ya Kutoa Shukran
Alhidaaya.com [3]
Sijdah ya kutoa shukran ni sijdah anayoifanya mtu wakati inapomjia neema, au inapomwondokea balaa. [Sharhul Minhaaj wa Haashiyatul Qalyuubiy (1/208)]
Imethibiti katika Hadiyth ndefu ya Ka’ab bin Maalik ya kwamba alisujudu ilipomjia habari ya furaha ya kuwa Allaah Kaikubali toba yake. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (4418) na Muslim (2769)].
Aidha, kuna Hadiyth nyingi (ambazo kuna maneno kuhusu Sanad zake) zilizopokelewa toka kwa zaidi ya Maswahaba kumi na mbili ambazo zote zinathibitisha kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisujudu kwa ajili ya kumshukuru Allaah. Kati ya hizo ni Hadiyth ya Abu Bakrah (Radhwiya Allaahu Anhu) isemayo kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), alikuwa anaporomoka kwenda kusujudu kwa ajili ya kumshukuru Allaah linapomjia jambo la furaha au jambo alilobashiriwa kheri. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (2774), At-Tirmidhy (1578), Ibn Maajah (1394) na wengineo kwa Sanad laini. Nimezitaja Hadiyth wenza za kutosha katika kitabu cha Taadhiymu Qadris Swalaat. Unaweza kuzipitia ukitaka].
Haya ndiyo yaliyokubaliwa na Jamhuri ya Maulamaa; Ash-Shaafi’iy, Ahmad, Is-Haaq, Abu Thawr, Ibn Al-Mundhir, na Maswahibu wa Abu Haniyfah. [Rawdhwat At-Twaalibiyna (1/324), Al-Mughniy (1/627) na Al-Fataawaa An-Nahdiyyah (1/135)]
Inafanyika kama inavyofanyika sijdah ya Swalaah kama tulivyoeleza kwenye sijdah ya kisomo. Sijdah hii haina ulazima mtu kuwa twahara au kuelekea Qiblah, kwa kuwa si Swalaah ingawa hayo yanapendeza. Aidha, haina ukaraha kuifanya katika nyakati ambazo ni marufuku kuswali kama tulivyoeleza kwenye mlango wa sijdah ya kisomo.
Haijuzu mtu akiwa ndani ya Swalaah, kwa kuwa sababu yake iko nje ya Swalaah. Ikiwa atasujudu ndani ya Swalaah, basi Swalaah yake itabatilika isipokuwa kama hajui au amesahau. Itachukuliwa ni kama mtu aliyezidisha sijdah kwa kusahau.
Yameelezwa haya na Ash-Shaafi’iy na Hanbali. Mahanbali wanasema kwamba haina ubaya ndani ya Swalaah!! [Al-Majmu’u (40/68) na Al-Furu’u (1/505)] Na hii ni kauli dhwa’iyf, na Allah Ndiye Mjuzi Zaidi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
036-Sijdah Ya Kusahau
Alhidaaya.com [3]
Kusahau katika lugha ya kawaida ni kughafilika na jambo na moyo kuliacha na kwenda kwa jingine. [Lisaan Al-Arab, kidahizo “Sahaa”]
Ama sijdah ya kusahau kiistilahi, ni sijdah inayofanywa kabla ya kutoa tasliym katika Swalaah au baada yake kwa ajili ya kuunga kosa la kuacha jambo au kufanya lililokatazwa bila ya kukusudia. [Al-Iqnaa cha Ash-Sharbyniy (2/89)]
Madhehebu yote yamekubaliana kuhusu kujuzu kwa sijdah ya sahau kwa mtu ambaye limemtokea katika Swalaah yake yale yaliyojiri kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) au mfano wake kwa njia ya kusahau. [Nudhumul Fawaaid Limaa Fiy Hadiythi Dhil Yadayn Minal Fawaaidi cha Al-Haafidh Al-‘Allaaiy uk. 405]
Kuna Hadiyth nyingi Swahiyh zinazozungumzia ujuzifu wa sijdah ya kusahau ambapo humo tutakuta hukumu zake. Ninakuletea hapa ili iwe sahali kuziona na kuyajua masuala husika:
1- Hadiyh ya Abu Hurayrah ya kwamba Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( Swalaah inapoadhiniwa, Shaytwaan hugeuka na kupiga mashuzi kwa sauti ili asiisikie adhana, na adhana inapomalizika huja tena. Inapoqimiwa Swalaah hugeuka, na inapomalizika huja tena akaingia kati ya mtu na nafsi yake akimwambia: Kumbuka kadha, kumbuka kadha, na mtu anakuwa hawezi kukumbuka mpaka anakuwa hajui ni rakaa ngapi kaswali. Na kama mmoja wenu hakujua kaswali ngapi, basi asujudu sijdah mbili akiwa amekaa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1231) na Muslim (389)].
2- Hadiyth ya Abu Hurayrah aliposema: “Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali moja kati ya Swalaah mbili (ima Adhuhuri au Alasiri), akatoa tasliym baada ya rakaa mbili. Kisha akaenda kwa fadhaa kwenye Qiblah cha Msikiti akakiegemea, na watu wakatoka haraka. Na hapo Dhul Yadayn akasimama na kusema: Ee Nabiy wa Allaah! Je, umepunguza Swalaah, au umesahau? Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaangalia kulia na kushoto kisha akasema: Anasema nini Dhul Yadayn? Wakasema: Amesema kweli, hukuswali isipokuwa rakaa mbili. Hapo hapo Nabiy akaswali rakaa mbili, kisha akapiga takbiyr, akasujudu, kisha akapiga takbiyr na kunyanyuka”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1229) na Muslim (373)].
3- Hadiyth ya ‘Imraan bin Haswiyn inayofanana na Hadiyth ya Abu Hurayrah iliyotangulia inayosema: “Akatoa tasliym baada ya rakaa tatu. Alipokumbushwa, aliswali rakaa moja, kisha akatoa tasliym, halafu akasujudu sijdah mbili na kutoa tasliym”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (574), An-Nasaaiy (1/26) na Ibn Maajah (1018)].
4- Hadiyth ya ‘Abdullah bin Buhaynah isemayo kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisimama katika Swalaah ya Adhuhuri bila kukaa tashah-hudi ya kwanza. Alipokamilisha Swalaah yake, alisujudu sijdah mbili akipiga takbiyr katika kila sijdah huku ameketi kabla hajatoa tasliym, na watu wakasujudu pamoja naye kulipia tashah-hudi aliyoisahau. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1224) na Muslim (570)].
5- Hadiyth ya Ibn Mas-’oud aliyesema: “Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali (Ibraahiym kasema: Ima alizidisha au alipunguza), alipotoa tasliym aliulizwa: Je, pametokea jambo katika Swalaah? Akasema: Kwani kuna nini? Wakasema: Umeswali rakaa kadhaa. Akaikunja miguu yake, akaelekea Qiblah, akasujudu sijdah mbili, kisha akatoa tasliym. Halafu akatuelekea kwa uso wake akasema:
Likitokea jambo katika Swalaah nitawajulisheni. Nami bila shaka ni mtu, ninasahau kama mnavyosahau, nami ninaposahau, basi nikumbusheni. Na mmoja wenu akifanya shaka kwenye Swalaah yake, basi ajaribu awezavyo kuangalia alilolifanya sawa, halafu alitimizie, kisha asujudu sijdah mbili”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1226) na Muslim (572)].
Tamshi la Al-Bukhaariy linasema: “Kisha atoe tasliym, halafu asujudu sijdah mbili”. Na katika riwaya: “Aliswali rakaa tano, akasujudu sijdah mbili”.
6- Hadiyth ya Abu Sa’iyd Al-Khudriy asemaye kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Akifanya shaka mmoja wenu kwenye Swalaah yake, kisha asijue ni rakaa ngapi ameswali kama ni tatu au nne, basi aiweke shaka yake kando na ajengee juu ya alilo na uhakika nalo, halafu asujudu sijdah mbili kabla hajatoa tasliym. Na kama atakuwa ameswali rakaa tano, basi sijdah mbili zitaifanya Swalaah yake shufwa, na kama kaswali kutimiza nne, basi sijdah mbili zitakuwa za kumdhili Shaytwaan)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (571), Abu Daawuud (1024), An-Nasaaiy (3/27) na Ibn Maajah (1210)].
Sijdah ya sahau imewekwa katika Swalaah kutokana na sababu tatu:
1- Kupunguza kitu
Pakitokea upungufu katika Swalaah kwa kughafilika au kusahau, chenye kuachwa kitakuwa ima nguzo, au wajibu au Sunnah.
(a) Ikiwa ataiacha nguzo katika rakaa kwa kusahau kisha akaikumbuka kabla ya kuanza kisomo kwenye rakaa inayofuatia, basi itamlazimu arudi kwenye nguzo hiyo, aifanye pamoja na vitendo vinavyofuatia baada yake, kisha itamlazimu asujudu sijdah ya kusahau mwishoni mwa Swalaah yake kama tutakavyokuja kulielezea hilo zaidi katika mahala pake. Na kama hakuikumbuka nguzo hiyo ila baada ya kuanza kisomo katika rakaa inayofuatia, basi rakaa yenye upungufu itabatilika. Itamlazimu aifute, akamilishe Swalaah yake, na kisha asujudu sijdah ya kusahau. [Haya ndiyo waliyoyaeleza Mahanbali, na Madhehebu ya Maalik na Ash-Shaafi’iy yako karibu nao. Angalia Ad-Dusuwqiy (1/293), Al-Majmu’u (4/116), Kash-Shaaful Qinaa (1/402), na Al-Mughniy (2/6)]
Ikiwa atasahau rakaa moja au zaidi, basi atazikamilisha, kisha atasujudu sijdah ya kusahau. Asili ya hili, ni Hadiyth ya Abu Hurayrah – kuhusu kisa cha Dhul Yadayn – na ‘Imraan bin Haswiyn.
(b) Ikiwa atawacha wajibu katika nyajibu za Swalaah kama tashah-hudi ya kati kwa mfano, ataifanya ikiwa ataweza kuiwahi kabla hajaondoka mahala pake na hatolazimiwa na lolote. Na ikiwa ataikumbuka baada ya kuondoka mahala pake na kabla ya kufika kwenye nguzo inayofuatia, basi atarudi ili aifanye, kisha ataikamilisha Swalaah yake na hatosujudu sijdah ya kusahau. Ikiwa ataikumbuka baada ya kuondoka mahala pake na baada ya kufika kwenye nguzo inayofuatia, itakuwa imempomoka na hatorudi ili aifanye, bali atakamilisha Swalaah na atasujudu sijdah ya kusahau.
Asili ya hili ni Hadiyth ya ‘Abdullah bin Buhaynah tuliyoitaja nyuma.
Imepokelewa toka kwa Ziyaad bin ‘Allaaqah akisema: “Al-Mughiyrah bin Shu’ubah alituswalisha. Aliposwali rakaa mbili, alisimama moja kwa moja bila kukaa na walio nyuma yake wakampigia tasbiyh lakini yeye aliwaashiria wasimame. Alipomaliza Swalaah, alitoa tasliym, kisha akasujudu sijdah mbili na kusema: Hivi ndivyo alivyofanya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Na katika riwaya nyingine amesema: “Amesema Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Ikiwa mmoja wenu atapitiliza na akawa tayari ashasimama, basi aikamilishe Swalaah na asujudu sijdah mbili za sahau. Lakini kama hakuwa bado hajasimama vyema, basi akae na hana sijdah ya sahau)). [Hadiyth Swahiyh kwa Sanad zake: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1036), At-Tirmidhiy (365), Ahmad (4/247) na At-Twahaawiy katika Al-Ma’aniy (1/439). Angalia Al-Irwaa (388)].
(c) Ikiwa amewacha lililosuniwa, kuna kauli mbili. Ya kwanza inasema kwamba hatosujudu kwa kuwa yaliyosuniwa hayana ubaya yakiachwa, na ya pili inasema kwamba imesuniwa asujudu lakini si lazima ili asije kuongeza tanzu juu ya shina kutokana na Hadiyth Dhwa’iyf isemayo: ((Kila sahau ina sijdah mbili)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1038), Ibn Maajah (1219), Ahmad (5/285), ‘Abdul Razzaaq (3533), At-Twayaalsiy (997), Al-Bayhaqiy (2/337) na At-Twabaraaniy (2/92). Kuna mvutano katika Sanad yake, kuna udhwa’iyf na mkatiko]
2- Kuzidisha
Ikiwa mwenye kuswali amesahau akazidisha rakaa moja au zaidi katika Swalaah yake, kama atakumbuka kabla hajaimaliza Swalaah, itambidi akae –kwa hali yoyote awayo- asome tashah-hudi, atoe tasliym, kisha asujudu sijdah ya kusahau na kutoa tasliym. Na kama hakukumbuka ila baada ya kutoa tasliym, basi atasujudu sijdah ya kusahau na kutoa tasliym.
Hii ni kutokana na Hadiyth ya Ibn Mas-’oud inayosema kwamba Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali adhuhuri rakaa tano. Akaambiwa: “Je, Swalaah imeongezwa?” Akauliza: “Kivipi? Akaambiwa: “Umeswali tano”, hapo hapo akasujudu sijdah mbili baada ya kutoa tasliym”. [Hadiyth Swahiyh: Tumeitaja nyuma kidogo].
3- Kufanya shaka
Ikiwa mwenye kuswali atafanya shaka kama ameswali rakaa tatu au nne kwa mfano, hapo atajitahidi kuyakumbuka aliyoyafanya katika Swalaah yake. Ikiwa atalitilia nguvu jambo moja kati ya mawili, basi atalishika hilo na atasujudu baada ya tasliym kama ilivyo kwenye Hadiyth iliyotangulia ya Ibn Mas-’oud.
Na kama hakulitilia nguvu lolote kati ya mawili, basi atalishika lenye yakini ambalo ni kuswali zilizo chache, na atasujudu kabla ya tasliym. Hii ni kutokana na Hadiyth iliyotangulia ya Abu Sa’iyd pamoja na Hadiyth ya ‘Abdul Rahmaan bin ‘Awf anayesema: “Nimemsikia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
((Anaposahau mmoja wenu katika Swalaah yake, asijue kama kaswali rakaa moja au mbili, basi ashike kwamba kaswali moja. Na kama hajui kama kaswali rakaa mbili au tatu, basi ashike kwamba kaswali mbili. Na kama hajui kaswali rakaa tatu au nne, basi ashike kwamba kaswali tatu, na kisha asujudu sijdah mbili kabla ya tasliym)). [Kuna ulaini: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhy (398), Ibn Maajah (1209), Al-Haakim (1/325) na Al-Bayhaqiy (2/332). Kuna 'an'anah (fulani toka kwa fulani) ya Ibn Is-Haaq, naye ameingizwa kwenye isnadi bila kuwepo].
[Kitabu cha sijdah ya kusahau cha Sheikh Mahmoud Ghariyb ukurasa wa 17]
1- Ikiwa ni fikra tu zisizo kweli, kama wasiwasi.
2- Ikiwa mtu ana ugonjwa wa wasiwasi kwa namna ambayo haswali Swalaah yoyote ila hufanya shaka.
3- Ikiwa shaka itakuja baada ya kumaliza ‘ibaadah, hatoitia maanani madhali hajayakinisha bali atalifuata alilo na yakini nalo.
Maulamaa wana kauli mbili kuhusiana na hukmu ya sijdah ya kusahau wakati inapopatikana sababu yake: [Fat-hul Qadiyr (1/502), Al-Qawaaniyn (67), Al-Majmu’u (4/152), Al-Mughniy (2/36), Kash-Shaaful Qinaa (1/408), Al-Muhallaa (4/159) na Majmu’u Al-Fataawaa (23/27)]
Kwanza: Ni wajibu
Ni madhehebu ya Hanafi na kauli ya Maalik. Mahanbal na Adh-Dwahiriyyah wamelipitisha hivyo, na ni chaguo la Sheikh wa Uislamu. Hoja yao ni:
1- Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameliamuru jambo hili katika Hadiyth zilizotangulia, na katika baadhi ya Hadiyth ni kwa kufanya shaka tu.
2- Kudumu na kutoacha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kusujudu sijdah mbili za kusahau inapotokea sababu yake.
Ya pili: Ni Sunnah:
Hili ni mashuhuri likipokelewa toka kwa Maalik, Ash-Shaafi’iy na riwaya toka kwa Mahanbali. Hoja yao ni:
1- Yaliyoelezwa katika Hadiyth ya Abu Sa’iyd asemaye: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Akifanya shaka mmoja wenu kwenye Swalaah yake, basi aache shaka na ajengee juu ya yakini. Akiyakinisha ukamilifu, asujudu sijdah mbili. Ikiwa Swalaah yake ni kamili, basi rakaa ya ziada pamoja na sijdah mbili zitakuwa ni Sunnah. Ama ikiwa pungufu, basi rakaa itakuwa ni kamilisho la Swalaah yake na sijdah mbili zitakuwa ni za kumdhili shaytwaan)). [Isnadi yake ni Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1024) na Ibn Maajah (1210). Asili yake ni kutoka kwa Muslim lakini bila ya kutaja neno "sijdah mbili ni Sunnah"].
Wanasema kwamba Hadiyth hapa inaonyesha kwamba sijdah mbili ni Sunnah na wala si wajibu.
Lenye nguvu ni kuwa sijdah hizi ni wajibu. Sheikh wa Uislamu amewajibu wenye kusema ni Sunnah kwa hoja mbili:
1- Tamshi hili “rakaa ya ziada pamoja na sijdah mbili zitakuwa ni Sunnah” haliko katika Hadiyth Swahiyh, na tamshi swahiyh ni: “basi aiweke shaka yake kando na ajengee juu ya alilo na uhakika nalo, halafu asujudu sijdah mbili kabla hajatoa tasliym. Na kama atakuwa ameswali rakaa tano, basi sijdah mbili zitaifanya Swalaah yake shufwa, na kama kaswali kutimiza nne, basi sijdah mbili zitakuwa za kumdhili shaytwaan”, nalo lashurutisha wajibu wa mawili; rakaa na sijdah mbili.
2- Tukijaalia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema, basi maana yake ni kuwa yeye ameamuriwa hilo pamoja na kuweko shaka. Na ikiwa tutakadiria kwamba Swalaah yake ni kamili bila ya kupungua chochote, basi hiyo inakuwa ni ziada katika kitendo chake, naye atalipwa thawabu kama katika Sunnah.
Maulamaa wamekhitalifiana kuhusiana na hili katika kauli tisa kwa mujibu wa Hadiyth Thabiti zinazohusiana na mlango huu:
[Ibn ‘Aabidiyn (1/495), Al-Mabsuwtw (1/219), Al-Qawaaniyna (67), Ad-Dusuwqiy (1/274), Rawdhwat At-Twaalibiyna (1/315), Al-Majmu’u (4/154), Al-Mughniy (2/22), Al-Kaafiy (1/209), Al-Awsatw (3/307) Bidaayatul Mujtahid (1/279) na Naylul Aw-Twaar (3/132-135)]
Ya kwanza:
Sijdah yote ni kabla ya tasliym. Ni kauli ya Abu Hurayrah, Mak-houl, Az-Zuhriy, Ibn Al-Musayyib, Rabiy’ah, Al-Awzaa’iy na Al-Layth. Ni madhehebu mapya ya Ash-Shaafi’iy.
Ya pili:
Sijdah yote ni baada ya tasliym. Ni kauli ya Sa’ad bin Waqqaas, Ibn Mas-’oud, Anas, Ibn Az-Zubayr, na Ibn ‘Abbaas. Pia imesimuliwa toka kwa ‘Aliy, ‘Ammaar, Al-Hasan, An-Nakh’iy na Ath-Thawriy. Ni madhehebu ya Abu Haniyfah na Maswahibu wake.
Ya tatu:
Kama amezidisha kitu atasujudu baada ya tasliym, na kama kapunguza atasujudu kabla ya tasliym. Ni kauli ya Maalik, Al-Mazniy, Abu Thawr na Ash-Shaafi’iy.
Ya nne:
Kila Hadiyth itatumika kwa mujibu wa inavyoeleza, na kama haikueleza kitu, basi atasujudu kabla ya kutoa tasliym. Ni kauli ya Ahmad na Ibn Abu Khaythamah, na ni chaguo la Ibn Al-Mundhir.
Ya tano:
Kila Hadiyth itatumika kwa mujibu wa inavyoeleza, na kama haikueleza kitu, basi atasujudu baada ya kutoa tasliym kama alizidisha, na kabla yake kama alipunguza. Ni kauli ya Is-Haaq bin Raahawiyyah.
Ya sita:
Ni kama iliyotangulia, lakini mwenyewe atachagua kusujudu kabla au baada ya tasliym kama Hadiyth haikuelezea kitu. Ni chaguo la Ash-Shawkaaniy.
Ya saba:
Mwenye kujengea juu ya uchache, atasujudu kabla ya tasliym na mwenye kupima usahihi atasujudu baada ya tasliym. Ni kauli ya Ibn Hibaan.
Ya nane:
Ana khiyari ya kusujudu kabla ya tasliym au baada yake. Hilo limesimuliwa toka kwa ‘Aliy, na ni kauli ya Ash-Shaafi’iy na At-Twabariy.
Ya tisa:
Atasujudu baada ya tasliym isipokuwa mahala pawili ambapo mwenyewe atachagua. Pa kwanza ikiwa atasimama bila kukaa tasha-hudi ya kwanza, na pa pili ni kama hakujua kama ameswali rakaa tatu au nne. Hapa atashika kwamba ameswali zilizo chache na mwenyewe atachagua kusujudu kabla au baada ya tasliym. Ni kauli ya Ibn Hazm na Ahlu Adh-Dhwaahir.
Kupambanua kati ya kuzidisha na kupunguza, na kati ya shaka pamoja na kuhakiki, na shaka pamoja na kujengea juu ya yakini. Hili ni chaguo la Sheikh wa Uislamu Ibn Taymiyah.
[Majmu’u Al-Fataawaa (23/24-25)]
Amesema: “Na hili ni moja ya riwaya toka kwa Ahmad, na madhehebu ya Maalik yako karibu nalo, na si mfano wake. Na hili, pamoja na matumizi yaliyomo ya Hadiyth zote, lakini kuna tofauti ya kimantiki, nayo ni kwamba:
1- Ikiwa ni kupunguza - kama kuacha tasha-hudi ya kwanza - Swalaah itahitajia kuungwa, na cha kuungia kinakuwa kabla ya kutoa tasliym ili Swalaah ikamilike, kwani tasliym ni kuimaliza na kuifunga Swalaah.
2- Ikiwa ni kuzidisha – kama rakaa – basi haikusanywi ziada mbili kwenye Swalaah moja, na sijdah ya sahau itakuwa ni baada ya tasliym, kwa kuwa hilo linamdhili shaytwaan sawa na Swalaah ya kando ambayo ameiungia kwayo upungufu wa Swalaah yake, kwani Nabiy amezifanya sijdah mbili kama rakaa.
3- Vile vile, akifanya shaka na akahakiki, basi ataikamilisha Swalaah yake na atasujudu baada ya tasliym ili kumdhili shaytwaan.
4- Aidha, akitoa tasliym huku akiwa amebakisha sehemu ya Swalaah yake kisha akakamilisha, basi anakuwa ameshaitimiza na tasliym itakuwa ni ziada. Hapa sijdah ya sahau itakuwa baada ya tasliym kwa kuwa ni ya kumdhili shaytwaan.
5- Ikiwa atafanya shaka na hakuweza kujua lipi la uhakika, hapa itakuwa ima ameswali rakaa nne au tano. Kama ameswali tano, sijdah mbili zitaifanya Swalaah yake kuwa shufwa ili awe kama ameswali rakaa sita na si tano, na hii inakuwa kabla ya tasliym.
Ibn Taymiyah kasema: “Kauli hii tunayoishabikia, ndiyo inayotumia Hadiyth zote bila kuacha Hadiyth hata moja pamoja na kutumia Qiyaas Swahiyh kwa lile ambalo halijagusiwa na Hadiyth, na kuliambatisha lisilotajwa na Hadiyth kwa lile linalofanana nalo lililotajwa”.
(a) Ikiwa utapita muda mrefu lakini wudhuu bado anao, Maulamaa wana kauli mbili:
Ya kwanza:
Ataianza tena Swalaah upya. Ni kauli ya Abu Haniyfah, Maalik, Ash-Shaafi’iy na Ahmad. [Al-Mabsuwtw (1/224), Al-Mudawwanah (1/135), Al-Majmu’u (4/156) na Al-Mughniy (2/13)]
Wanasema kwamba Swalaah ni moja na haijuzu kuijenga vipande vipande mbali na muda kurefuka.
Ya pili:
Atajengea juu ya Swalaah yake na atasujudu ikiwa wudhuu haujatenguka. Ni kauli ya Maalik, na kauli ya zamani ya Ash-Shaafi’iy. Pia Yahya bin Sa’iyd Al-Answaariy, Al-Layth, Al-Awzaa’iy, Ibn Hazm na Ibn Taymiyah, isipokuwa yeye ameihusisha na sijdah ya baada ya tasliym. [Al-Mudawwanah (1/135), Al-Muhalla (4/166) na Majmu’u Al-Fataawaa (23/32-35)]
Wanasema kwamba urefu wa muda hauna kidhibiti maalumu, kwani Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitoa tasliym kwa kusahau, akazungumza, akakagua hali, akatoka Msikitini, akaingia nyumbani kwake, kisha akalijua hilo, akatoka na kutimiza kilichopungua katika Swalaah yake, kisha akasujudu sijdah mbili kutokana na sahau aliyoifanya.
Na kwa vile yeye ameamuriwa kuitimiza Swalaah na kusujudu sijdah ya kusahau, imekuwa ni wajibu kutokana na ujumuishi wa kauli yake Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Mwenye kusahau Swalaah, au akalala ikampita, basi kafara yake ni kuiswali anapoikumbuka)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (684), An-Nasaaiy (614) na kwa Al-Bukhaariy mfano wake (597)].
Ninasema: ”Hii ni kauli madhubuti kabisa, lakini mwenye kutaka kuwa salama zaidi, ni vyema aswali upya, nayo ni haki yake. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
(b) Kama wudhuu umemtenguka baada ya kutoa tasliym katika Swalaah aliyoiswali pungufu, basi Swalaah yake ni batili kwa mujibu wa itifaki ya Jamhuri. Ikiwa amesahau kusujudu – baada ya tasliym - kwa kuongeza kitu katika Swalaah yake, inaruhusiwa asujudu hata kama wudhuu umemtenguka, kwa kuwa sijdah mbili ni za kumdhili shaytwaan kama alivyosema Ibn Taymiyah. [Majmu’u Al-Fataawaa (23/36)]
Ninasema: “Yaani atatawadha na kusujudu. Hili ni madhubuti na lenye mwelekeo zaidi”.
[Raddul Muhtaar (1/497), Mawaahibul Jaliyl (2/15), Sharhul Minhaaj (1/204) na Al-Mughniy (2/39)]
Kama mwenye kuswali atasahau zaidi ya mara moja, basi hatosujudu isipokuwa sijdah mbili tu za sahau. Hii ni kwa mujibu wa Jamhuri ya Maulamaa, kwa kuwa haikunukuliwa toka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wala kwa Swahaba yeyote ya kwamba walifanya sijdah ziada kutokana na sahau ya zaidi ya mara moja pamoja na kwamba hilo linaweza kumpata yeyote mwenye kuswali.
Na kwa kuwa lau si maingiliano, basi Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) angelisujudu baada ya kusahau. Na alipokawiza hadi mwisho wa Swalaah, tumejua kwamba alifanya hivyo kwa ajili ya kuzijumuisha sahau zote zilizotendeka ndani ya Swalaah.
Ninasema: “Ama Hadiyth Marfu’u ya Thawbaan: ((Kwa kila sahau sijdah mbili baada ya kutoa tasliym)), ni Dhwa’iyf, haifai”.
[Sharhu Muslim (5/60), Fat-hul Baariy (3/125-126) na Al-Awsatw (3/325)]
Jamhuri ya Maulamaa wanasema kwamba mtu atasujudu sijdah ya sahau katika Swalaah ya Sunnah kama anavyofanya katika Swalaah ya Faradhi kutokana na kutobaguliwa kati ya Swalaah ya Faradhi au ya Sunnah katika Hadiyth husika mbali na kutokuwepo dalili ya ufarikishaji.
Imepokelewa toka kwa Abul ‘Aaliyah akisema: “Nilimwona Ibn ‘Abbaas akisujudu sijdah mbili baada ya Witri yake”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Al-Bukhaariy kasema ni Mu’allaq (3/125-Fat-h) na Ibn Abu Shaybah kasema ni Mawswuul kwa Sanad Swahiyh (2/81)].
Imepokelewa toka kwa ‘Atwaa toka kwa Ibn ‘Abbaas akisema: “Ukipitikiwa kwenye Swalaah ya Sunnah, basi sujudu sijdah mbili”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abil Mundhir katika Al-Awsatw (3/325)].
Katika Swalaah, imamu au maamuma anaweza kupitikiwa na sahau.
(1) Imamu akipitikiwa
(a) Maamuma anaruhusiwa kumzindusha imamu wake kama atasahau. Kwa wanaume inakuwa ni kwa kusema “Subhaanal Laah” na kwa wanawake ni kupiga kikofi. Hii ni kauli ya Jamhuri ya Maulaama kinyume na Maalik. [Fat-hul Qadiyr (1/356), Mawaahibul Jaliyl (2/29), Nihaayatul Muhtaaj (2/44) na Al-Mughniy (2/19)]
Ni kutokana na Hadiyth ya Sahl bin Sa’iyd ya kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Mwenye kupatwa na jambo katika Swalaah yake, basi aseme “Subhaanal Laah”)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1218) na An-Nasaaiy (784)].
Na katika tamshi jingine: ((Likikupateni jambo, basi wanaume waseme “Subhaanal Laah”)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (7190), An-Nasaaiy (793) na Abu Daawuud (940)].
Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Tasbiyh ni kwa wanaume, na kupiga kikofi ni kwa wanawake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1203) na Muslim (422)].
Ama kwa upande wa Maalik, yeye anasema kwamba wanaume na wanawake watasema “Subhaanal Laah” na ni karaha kwa wanawake kupiga kikofi katika Swalaah!! Na Hadiyth ni hoja dhidi yake. Kupiga kikofi ni kupiga kwa tumbo la kiganja chake mgongo wa kiganja kingine kwa ajili ya kumtanabahisha imamu.
(b) Imamu kuitikia uzindushi wa maamuma na maamuma kumfuata.
[Ibn ‘Aabidiyn (1/507), Nihaayatul Muhtaaj (2/75), Al-Khurashiy (1/322) na Al-Mughniy (2/20)]
Jamhuri ya Maulamaa; Hanafi, Ash-Shaafi’iy na Hanbali wanasema kwamba ikiwa imamu atazidisha katika Swalaah, naye akawa na yakini au ikamghilibikia dhana kwamba yeye yuko sawa na huku maamuma wanaona kwamba amekwenda kwenye rakaa ya tano kwa mfano, basi hatowaitikia.
Maalik anasema kwamba ikiwa maamuma ni wengi kwa maana kwamba ni vigumu wao wote kukosea, basi imamu itambidi aachane na yakini yake na awafuate kwenye lile walilomwashiria. Na hii yote ikiwa imamu imemghilibikia dhana au akawa na yakini kwamba yeye yuko sawa. Lakini ikiwa atakuwa na shaka, basi hapo itamlazimu kiwajibu kuwasikiliza maamuma kutokana na Hadiyth ya Dhul Yadayn iliyotangulia. Haya ndiyo waliyosema Jamhuri kuhusiana na shaka kinyume na Mashaafi’i ambao wanaona kwamba imamu ataijengea yakini yake mwenyewe na hatowasikiliza maamuma!!
Ninasema: “Kauli ya Jamhuri ina uzito zaidi, kwa kuwa ushuhuda wa maamuma wanaoaminika, ni uthibitisho tosha. Ikiwa itamghilibikia kwamba maamuma wako sawa, basi atawafuata. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
(c) Imamu akisahau na akasujudu, basi ni lazima maamuma wamfuate.
Hii ni sawasawa ikiwa maamuma atasahau pamoja naye au imamu akasahau peke yake. Ibn Al-Mundhir amesema kwenye Al-Awsatw (3/322): “Maulamaa wote tunaowajua vyema wamekubaliana ya kwamba maamuma anawajibika kusujudu pamoja na imamu pindi imamu anaposahau akasujudu. Hoja yao ni Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) isemayo:
((Hakika si jinginelo, imamu amewekwa ili afuatwe)). [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa nyuma].
Hii ni kwa vile maamuma anamfuata imamu, na hukmu yake ni hukmu yake anaposahau na anapokuwa hakusahau pia.
(d) Imamu akisahau asisujudu, je maamuma watasujudu?
[Al-Awsatw (3/322), Ibn ‘Aabidiyn (1/499), Al-Khurashiy (1/331), Al-Majmu’u (4/143) na Al-Mughniy (1/41)]
Maulamaa wamekhitalifiana katika suala hili. ‘Atwaa, Al-Hasan, An-Nakh’iy, Ath-Thawriy, Abu Haniyfah na Masahibu zake wanaona kwamba ikiwa hakusujudu, basi nao wasisujudu, kwani wakisujudu watakwenda kinyume naye.
Ama Ibn Syriyna, Qataadah, Al-Awzaa’iy, Maalik, Al-Layth, Ash-Shaafi’iy, Abu Thawr na riwaya toka kwa Ahmad, wao wanaona kwamba maamuma watasujudu hata kama imamu wao hakusujudu. Hii ni kwa kuwa jambo hili ni wajibu kwao na kwake na haliwaondokei kwa imamu kuliwacha, bali kila mmoja ni lazima autekeleze wajibu wake na faradhi yake.
(e) Je, maamuma aliyepitwa na baadhi ya rakaa atasujudu imamu wake akisujudu?
Mtu akipata sehemu ya Swalaah ya imamu, na imamu ni lazima asujudu sijdah ya kusahau, hapa Maulamaa wana kauli nne:
[Maulamaa wamekhitalifiana juu ya kiasi cha mtu kumpata imamu kinachomlazimu kumfuata katika sijdah ya sahau. Jamhuri wamesema: “Akiipata nguzo moja kabla hajasujudu sijdah ya sahau, itamlazimu asujudu naye sawasawa ikiwa sahau ilikuwa kabla hajamfuata au baada ya kumfuata”. Maalik anasema: “Kama hakuipata rakaa moja, hatosujudu”. Ninasema: “Hii ndiyo yenye nguvu zaidi. Lakini ikiwa atasahau pamoja na imamu, basi atawajibika kusujudu kwa kusahau mwenyewe na si kwa sahau ya imamu wake. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.]
Ya kwanza:
Atasujudu pamoja na imamu kisha atakamilisha rakaa zilizobakia. Ni kauli ya Ash-Sha’abiy, ‘Atwaa, An-Nakh’iy, Al-Hasan, Ahmad, Abu Thawr, Abu Haniyfah na Masahibu zake. [Al-Awsatw (3/323), Masaail Ahmad cha Abu Daawuud (55) na Al-Aswl (1/234)]
Ya pili:
Ataimaliza Swalaah, kisha atasujudu kwa sahau ya imamu wake. Ni kauli ya Ibn Syriyn na Is-Haaq bin Raahawiyyah. [Al-Awsatw (3/323)]
Ya tatu:
Atasujudu pamoja na imamu, halafu atakamilisha, kisha atasujudu baada ya kumaliza Swalaah yake. Ni kauli ya Ash-Shaafi’iy. [Al-Ummu cha Ash-Shaafi’iy (1/132)]
Ya nne:
Akisujudu imamu kabla ya kutoa tasliym, atasujudu naye lakini akisujudu baada ya tasliym, atasimama aikamilishe Swalaah yake kisha asujudu. Ni kauli ya Maalik, Al-Awzaa’iy na Al-Layth bin Sa’ad. [Al-Awsatw (3/323) na Al-Mudawwanah (1/139)]
Ninasema: “Huenda kauli hii ya mwisho ndiyo iliyo karibu zaidi na neno lake Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Hakika si jinginelo, imamu amewekwa ili afuatwe. Basi akisujudu nanyi sujuduni)). Na nyuma tushasema kwamba kusujudu kabla ya tasliym kunakuwa ni kuunga upungufu, hivyo imepasa kumfuata.
Ama zinazosujudiwa baada ya tasliym, hiyo ni kumdhili shaytwaan. Atasimama akamilishe rakaa zake zilizobakia, kisha atasujudu kwa ajili ya sahau ya imamu wake kutokana na neno lake Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Mlioipata basi swalini, na iliyokupiteni basi itimizeni)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (635) na Muslim (602)].
Na kwa hivi, anakuwa amemfuata imamu kwa upande wa kuwa imamu alisujudu mwishoni mwa Swalaah yake, naye pia kadhalika.
2- Maamuma akisahau nyuma ya imamu
[Al-Awsatw (3/320) na Al-Muhalla (4/167)]
Maamuma akipitikiwa akasahau kitu nyuma ya imamu basi hatosujudu, bali imamu atambebea sahau yake. Hii ndio kauli ya Maulamaa wengi wakiwemo maimamu wanne na wengineo. Kuna Hadiyth Marfu’u iliyokuja kuhusiana na suala hili iliyopokelewa na ‘Umar toka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) isemayo:
((Aliyeko nyuma ya imamu hana sahau. Na ikiwa imamu atasahau, basi ni juu yake sahau na aliyeko nyuma yake. Na ikiwa atasahau nyuma ya imamu, basi hana sahau bali imamu atamtosheleza)). [Hadiyth hii ni Dhwa’iyf na haifai na imefanyiwa “ikhraaj” na Ad Daara Qutwniy (1/377) na Al-Bayhaqiy (2/352)], .lakini wengi wanaitumia.
Ibn Syriyna, Daawoud na Ibn Hazm wako kinyume na hili. Wanasema kwamba maamuma atasujudu akiwa kama yuko peke yake au imamu kwa kuwa agizo la Nabiy la kusujudu sijdah mbili kwa kila mwenye kupitikiwa katika Swalaah yake, halimhusu imamu tu wala maamuma mwenye kuswali peke yake.
Ninasema: “Kauli ya Jamhuri ndiyo yenye uzito zaidi na si Hadiyth Marfu’u. Na hii ni kwa yale aliyoyaelezea Al’Allaamah Al-Albaaniy (Rahimahul Laahu) aliposema: [Irwaaul Ghaliyl (2/132)]
“Sisi tunajua kwa yakini kwamba Maswahaba waliokuwa wakimfuata Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika Swalaah, walikuwa wakisahau sahau za kuwawajibisha kusujudu lau kama wangelikuwa wanaswali mtu peke yake. Na jambo hili hakuna anayeweza kulipinga. Na ikiwa ni hivyo, basi haikunukuliwa kwamba kuna yeyote kati yao aliyesujudu baada ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kutoa tasliym. Na lau kama hilo lingelikuwa linajuzu, basi wangelifanya, na kama wangelifanya basi wangelinukuu. Na kwa kuwa hakuna nukuu yoyote, tunajua kwamba hilo halijuzu na suala liko wazi kabisa. Haya yanatiliwa nguvu na Hadiyth ya Mu’aawiyah bin Al-Hakam ambaye alizungumza ndani ya Swalaah nyuma ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa hajui uharamu wa hilo, lakini Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakumwamuru asujudu sijdah ya kusahau”.
Sijdah ya sahau ni sijdah mbili kama sijdah zile zile za kwenye rakaa. Atapiga takbiyr katika kila kinyanyuko na kiinamo, kisha atatoa tasliym, sawasawa sijdah ikiwa kabla ya tasliym au baada yake.
Ama takbiyr, ni katika Hadiyth ya Ibn Bujaynah isemayo: “Alipoitimiza Swalaah yake, alisujudu sijdah mbili; akapiga takbiyr katika kila sijdah akiwa ameketi kabla ya kutoa tasliym”. [Hadiyth Swahiyh: Tumeitaja mwanzoni mwa mlango huu]. Na hii ni kabla ya tasliym.
Ama baada ya tasliym, hilo limethibiti katika Hadiyth ya Abu Hurayrah isemayo: “…Akaswali rakaa mbili akatoa tasliym, kisha akapiga takbiyr akasujudu, halafu akapiga takbiyr akanyanyuka, kisha akapiga takbiyr akasujudu, halafu akapiga takbiyr akanyanyuka”. [Hadiyth Swahiyh: Tumeitaja mwanzoni mwa mlango huu].
Kwa mujibu wa kauli ya Jamhuri na Hadiyth zinavyoonyesha ni kuwa atatosheka kwa takbiyr ya kusujudu. [Fat-hul Baariy (3/99)]
Maalik amesema: “Ni lazima takbiyr ya kuhirimia kabla ya kusujudu kutokana na ziada iliyopo kwenye Hadiyth ya Abu Hurayrah kuhusiana na kisa cha Dhul Yadayn isemayo: “Ni kwamba alipiga takbiyr akasujudu. Hisham akasema – yaani Ibn Hassan – alipiga takbiyr, kisha akapiga takbiyr, na akasujudu”. Hii ni ziada isiyo ya kawaida na haithibiti.
Ibn ‘Abdul Barri anasema: [Al-Istidhkaar (4/345)]
“Sisi na Jamhuri ya Maulamaa tunasema kwamba kutoa tasliym kwa kusahau hakumtoi mtu katika Swalaah yake wala hakuiharibu. Akiwa kwenye Swalaah yake ataikamilishia, hakuna maana kuhirimia, kwa kuwa haanzi upya Swalaah bali anaitimiza na kuikamilisha. Anayeamuriwa takbiyr ya kuhirimia ni yule anayeanza kuswali”.
Ama kutoa tasliym baada ya sijdah mbili, hilo limethibiti kwenye habari ya Dhul Yadayn, na Hadiyth ya Ibn Mas-’oud toka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ya kwamba aliswali rakaa tano, na Hadiyth ya ‘Imraan bin Haswiyn isemayo: “Akaswali rakaa kisha akatoa tasliym, halafu akasujudu sijdah mbili, kisha akatoa tasliym”. [Hadiyth Swahiyh: Tumeitaja mwanzoni mwa mlango huu].
Maulamaa wana kauli nne kuhusiana na suala hili. [Al-Awsatw cha Ibn Al-Mundhir (3/314-317). Kuna kauli inayothibitisha, inayozuia, inayokhiyarisha na inayofarikisha kati ya sijdah ya baada ya tasliym ambayo husomewa tashah-hudi na kati ya sijdah ya kabla yake ambayo haisomewi tashah-hudi]
Kauli sahihi zaidi ni ile isemayo kwamba mtu hasomi tashah-hudi baada ya sijdah mbili za sahau kwa vile hilo halikuthibiti toka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Aliyesema kuwa inasomwa ametegemea yaliyohadithiwa kwenye Hadiyth ya ‘Imraan bin Haswiyn isemayo kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaswalisha akasahau, kisha akasujudu sijdah mbili, halafu akasoma tashah-hudi, kisha akatoa tasliym. [Hadiyth Shaadh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1039), At-Tirmidhy (395), Ibn Al-Jaaroud (247) na wengineo. Al-Bayhaqiy, Ibn ‘Abdul Barri, Ibn Taymiyah na wengineo wamesema ni Dhwa’iyf. Pia Al’Allaamah Al-Albaaniy kama ilivyo kwenye Al-Irwaa (403)]
Ni Hadiyth Shaadh isiyofaa, na kwa ajili hiyo Sheikh wa Uislamu (23/48) amesema: “Imethibiti kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisujudu baada ya tasliym zaidi ya mara moja kama ilivyo kwenye Hadiyth ya Ibn Mas-’oud wakati aliposwali rakaa tano, na pia katika Hadiyth ya Abu Hurayrah kuhusu Dhul Yadayn na ‘Imraan bin Haswiyn. Lakini hakuna kauli yake hata moja yenye kuamuru kusoma tashah-hudi baada ya sijdah wala kwenye Hadiyth zozote Swahiyh, bali tashah-hudi ni kitendo kirefu kinachoweza kuwa sawa na sijdah mbili au zaidi, na kitendo kama hiki kinastahiki kuhifadhiwa na kusajiliwa kwenye kumbukumbu na kupewa shime na uzito wa kuhadithiwa na kunukuliwa. Na lau kama angelikuwa amesoma tashah-hudi, basi angelieleza hilo yule aliyeeleza kwamba alisujudu, na sababu ya kulitaja hilo ingelikuwa na nguvu zaidi kuliko kuitaja tasliym na takbiyr wakati wa kuinama na kunyanyuka. Na hizi ni kauli nyepesi, wakati tashah-hudi ni kitendo kirefu, basi vipi wanukuu hili na waliache lile?!
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
037-Swalaah Ya Safari
Alhidaaya.com [3]
Maana ya safari katika lugha ya kawaida ni kukata masafa, na kinyume chake ni kusalia mjini anapoishi mtu. Ama kiistilahi, ni kutoka mtu toka makazi yake kwenda sehemu nyingine yenye umbali wa masafa fulani ambayo Maulamaa wamekhitalifiana kuhusu urefu kama tutakavyokuja kueleza.
Kwanza: Kupunguza Swalaah
Kupunguza maana yake ni kuzuia na kutofikia kitu upeo wake na mwisho wake. Ama kiistilahi, ni kuifanya Swalaah ya rakaa nne kuwa rakaa mbili wakati wa safari sawasawa katika hali ya vita au ya amani.
Kupunguza Swalaah wakati wa safari, kumethibiti katika Qur-aan, Hadiyth na Ijma’a. Dalili zake zitakuja wakati tukiuchambua mlango huu Insha-Allaah.
Maulamaa wamekubaliana kwamba inajuzu kupunguza Swalaah safarini. Pia wamekubaliana kwamba Swalaah za Alfajiri na Magharibi hazipunguzwi, lakini wamekhitalifiana kwa upande wa hukmu ya kupunguza Swalaah kama ni wajibu au si wajibu (ruksa). Aidha, wamekhitalifiana kuhusu masharti ya kupunguza na masuala mengineyo husika. Hebu sasa tujaribu kuyachambua masuala haya.
Maulamaa wamekhitalifiana kuhusu hukmu ya kupunguza Swalaah ya rakaa nne kwa kauli mbili:
Ya kwanza:
Kupunguza kumeruhusiwa, nayo ni kauli ya Jamhuri; Maalik, Ash-Shaafi’i na Hanbali. [Ash-Sharhul Kabiyr katika Haashiyat Ad-Dusuwqiy (1/358), Al-Majmu’u (4/337), Kash-Shaaful Qinaa (1/324), Al-Mughniy (2/197), Bidaayatul Mujtahid (1/241), Naylul Awtwaar (3/239) na Al-Haawiy cha Al-Mawruwdiy (2/363-365)]
Kisha hawa wakakhitalifiana juu ya lililo bora kati ya kupunguza, au kuswali kamili, au je mtu anakhiyarishwa?
Ya pili:
Kupunguza ni wajibu na haijuzu kuswali Swalaah kamili. Ni madhehebu ya Hanafi na Ahlu Adh-Dhwaahir, na kauli kwa Maalik. [Al-Badaai-’i (1/91), Fat-hul Qadiyr (1/395), Bidaayatul Mujtahid (1/241), Al-Muntaqaa cha Al-Baajiy (1/260), Al-Muhallaa (4/264), Ma’alimu As-Sunan (1/48) Naylul Awtwaar (3/239)]
Kisha wakakhitalifiana, je akiswali kamili, Swalaah itabatilika au la?
(a) Dalili za wanaosema kwamba si wajibu
Dalili ya kwanza ya Jamhuri:
Kauli Yake Ta’alaa:
((وَإِذَا ضَرَبْتُمْ فِي الْأَرْضِ فَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَقْصُرُوا مِنَ الصَّلَاةِ إِنْ خِفْتُمْ أَن يَفْتِنَكُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ إِنَّ الْكَافِرِينَ كَانُوا لَكُمْ عَدُوًّا مُّبِينًا))
((Na mtakaposafiri katika ardhi basi si dhambi kwenu kufupisha Swalaah mkikhofu kwamba waliokufuru watakushambulieni. Hakika makafiri wamekuwa kwenu ni maadui dhahiri)). [An-Nisaa (4:101)]
Wanasema kuwa Aayah kueleza kwamba hakuna ubaya kunamaanisha kwamba hakuna dhambi, bali jambo ni mubaaha na si la fardhi wala la kufungiwa niya.
Wenye kusema ni wajibu wamewajibu kwa njia tatu:
Njia ya kwanza:
Haikubaliki tamshi la hakuna ubaya kuwa ni mahsusi kwa jambo la mubaaha tu, bali hutumiwa vile vile katika wajibu. Katika hilo ni Kauli Yake Taa’laa:
((إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَائِرِ اللَّـهِ ۖ فَمَنْ حَجَّ الْبَيْتَ أَوِ اعْتَمَرَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَن يَطَّوَّفَ بِهِمَا ۚ وَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَإِنَّ اللَّـهَ شَاكِرٌ عَلِيمٌ))
(( Hakika Asw-Swafaa na Al-Marwah ni katika alama za Allaah. Basi yeyote anayehiji kwenye Nyumba hiyo au akatekeleza ‘Umrah basi hakuna lawama kwake kutufu (vilima) viwili hivyo. Na atakayejitolea kufanya khayr basi hakika Allaah ni Mwenye Kupokea shukurani, Mjuzi wa yote)). [Al-Baqarah (2:158)]
Tamshi la hakuna lawama katika Aayah limekuja katika kusa’i kati ya Swafaa na Marwa katika Hajji, nako ni faradhi.
Limejibiwa hili kwa kusemwa: Aayah imeshuka kwa ajili ya kubainisha kwamba kusa’i ni katika alama, na hiyo ni pale Waislamu walipoona dhiki ya kuifanya kwa vile Waarabu walikuwa wakiifanya enzi ya ujahili. Hivyo Aayah haikushuka kwa ajili ya kubainisha hukmu ya kusa’i!!
Njia ya pili:
Muradi wa kupunguza katika Aayah ni kupunguza umbo la Swalaah wakati wa vita kwa kuacha kusimama na kurukuu.
Limejibiwa hili kwa kusemwa: Muradi wa kupunguza ni kupunguza idadi ya rakaa kwa kuzifanya mbili badala ya nne kwa dalili ya Hadiyth ya Ya’alaa bin Umayyah itakayokuja baadaye. Hadiyth hii inaeleza kwamba alitatizikiwa kupunguza idadi ya rakaa safarini katika hali ya amani kama alivyotatizikiwa ‘Umar. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:
((Ni swadaqah ambayo Allaah Amewapeni, basi ikubalini Swadaqah Yake)). [Hadiyth Swahiyh: Angalia inayofuatia baada yake].
Njia ya tatu:
Katika Aayah kuna sharti ya kuwepo vita, basi kwa nini hamkuisema ili kupunguza kujuzu na badala yake mkaijuzisha katika amani?
Limejibiwa hilo kwa kusemwa kwamba kupunguza katika safari, kumethibitishwa na Sunnah ya Rasuli.
Dalili ya pili ya Jamhuri:
Hadiyth ya Ya’alaa bin Umayyah aliyesema: “Nilimwambia ‘Umar bin Al-Khattwaab:
((فليس عليكم جناح أن تقصروا من الصلاة إن خفتم أن يفتنكم الذين كفروا))
Watu wako kwenye amani!! Akasema: Nimestaajabu kwa hili ulilolistaajabia. Nikaenda kumuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu hilo naye akasema:
((Ni swadaqah ambayo Allaah Amewapeni, basi ikubalini swadaqah Yake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (686), Abu Daawuud (1199), At-Tirmidhy (3037) na Ibn Maajah (1065)].
Wanasema: “Kuelezewa kupunguza kama ni swadaqah, kunaonyesha kujuzu, kwa kuwa swadaqah ni kitu cha khiyari tu, na si cha lazima”.
Wenye kusema ni wajibu wamejibu wakisema:
“Hadiyth ni dalili kwetu na si kwenu, kwa kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameamuru kuikubali swadaqah hii, na agizo lake ni la wajibu, na kila ihsani kwetu ni swadaqah”.
Wamejibiwa:
“Kuna kielelezo zaidi ya kimoja chenye kulibadili agizo toka kwenye ulazima kulipeleka kwenye uzuri na ubora likifanyika!! Kati ya vielelezo hivyo ni kuwa tamshi “swadaqah” linapotolewa, hukusudiwa kwalo swadaqah ya kujitolea na si swadaqah ya lazima”.
Dalili ya tatu ya Jamhuri:
Yaliyosimuliwa toka kwa ‘Aaishah aliposema: “Nilitoka pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwenda ‘Umrah katika mwezi wa Ramadhwaan. Yeye hakufunga nami nikafunga, akapunguza Swalaah nami nikaswali kamili, kisha nilimwambia: Kwa hishma ya wazazi wangu: Wewe hukufunga nami nimefunga, umepunguza Swalaah nami nimeswali kamili. Akaniambia: ((Umefanya vizuri ee ‘Aaishah)). [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ad-daaraqutwniy (2/188) na Al-Bayhaqiy. Ad-daaraqutwniy kaitilia nguvu irsali yake kwenye Al’Ilal].
Wenye kusema ni wajibu wamelijibu hili kwa majibu yafuatayo:
Kwanza: Hadiyth hii ni Dhwa’iyf, haifai kwa hoja.
Pili: Matni yake ina shaka na walakini, kwa kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alifanya ‘Umrah mara nne tu na hakuna yoyote kati ya hizo aliifanya katika mwezi wa Ramadhwaan, bali katika mwezi wa mfungo pili. [Jibu hili linajibiwa kwamba Nabiy alifanya ‘Umrah mbili katika Mwezi wa Ramadhwaan: ‘Umratul Qadhwaa na ‘Umrah ya ukombozi wa mji wa Makkah. Zote mbili zilikuwa katika Ramadhwaan]
Tatu: Sheikh wa Uislamu amesema: “Hadiyth hii kazushiwa ‘Aaishah. [Ameinukulu kwenye Zaad Al-Ma’ad (1/472) chapa ya Ar-Risaalah]
Haiwezekaniki akaswali kinyume na Swalaah ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba wengineo huku akiwaona wakipunguza, halafu yeye peke yake aswali kamili bila sababu kinaishi. Vipi liwe hilo na yeye ndiye asemaye: Swalaah imefaradhiwa rakaa mbili? Ataonekana vipi akizidisha faradhi ya Allaah na kwenda kinyume na Nabiy wa Allaah pamoja na Maswahaba wake?!!”
Dalili ya nne ya Jamhuri:
Yaliyosemwa na ‘Aaishah ya kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akipunguza Swalaah katika safari na kutimiza, na hula na hufunga”. [Hadiyth Munkar: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ad-daaraqutwniy (2/242), (2/189), Ash-Shaafi’iy (518) na Al-Bayhaqiy (3/141, 142) na Sanad yake imeharibika. Sheikh wa Uislamu amesema: “Haya kazushiwa Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)”. Angalia Al-Irwaa (3/3-9)].
Wenye kusema ni wajibu wamejibu wakisema:
“Hili linachukulika kama yeye alipunguza kivitendo na akatimiza kihukmu. Ni kama kauli ya ‘Umar: “Swalaah ya safari ni rakaa mbili kamili bila kupungua”. Hili linajibiwa kwa kusema: “Ni kuwa kuswali kamili katika habari ya ‘Aaishah, kunaonyesha kwamba inajuzu kuiswali Swalaah ya rakaa nne kwa rakaa nne katika safari. Ama kutimiza katika habari ya ‘Umar, kunaonyesha utimilifu kwa upande wa malipo. Habari ya ‘Aaishah haibebeshwi juu ya maneno ya ‘Umar (Radhwiya Allaahu Anhu)”.
Ninasema: “Hadiyth hii ni Munkari na haihitajii taawiyl ya aina yoyote ile”.
Dalili ya tano ya Jamhuri:
Hadiyth ya ‘Abdul Rahmaan bin Yaziyd isemayo: “‘Uthmaan alituswalisha Mina rakaa nne. ‘Abdullah bin Mas-’oud akaelezwa hilo, akavuta kumbukumbu yake nyuma na kusema: Niliswali pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Mina rakaa mbili, niliswali pamoja na Abu Bakr As-Siddiyq Mina rakaa mbili, na niliswali pamoja na ‘Umar Mina rakaa mbili. Basi laiti fungu langu lingekuwa rakaa mbili zenye kukubaliwa badala ya nne” [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1084) na Muslim (695)].
Wamesema: “Yaani, laiti ‘Uthmaan angeliswali rakaa mbili badala ya nne kama alivyokuwa akifanya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Abu Bakri, ‘Umar na ‘Uthmaan mwanzoni mwa Ukhalifa wake. Na makusudio yake ni ukaraha wa kwenda kwake kinyume na alilokuwa akilifanya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahibu wake wawili. Lakini pamoja na haya, Ibn Mas-’oud amewafiki kujuzu kuswali kamili, na kama si hivyo, asingelijuzisha kumfuata yeyote anayeswali kamili”. [Sharhu Muslim cha An Nawawiy (5/204)]
Wenye kusema ni wajibu wamejibu kwa njia hizi:
(a) ’Uthmaan aliswali kamili Minaa kwa kuwa alinuwia kukaa Makkah baada ya Hijjah, na Maswahaba waliyekuwa naye waliswali kamili kwa kuwa nao watakaa Makkah madhali yeye yuko huko.
Hili limejibiwa: “Kukaa Makkah kulikuwa ni marufuku kwa Muhaajirina. Imepokewa kwa njia sahihi kuhusu ‘Uthmaan ya kwamba alikuwa hawaagi wanawake isipokuwa akiwa juu ya mnyama wake, na huharakia akichelea kurejea kwenye hijra yake. Na imethibiti kwamba wakati walipomzingira walimwambia: “Panda mnyama wako wende Makkah”. Akawajibu: “Sitoondoka Madiynah nilikohamia”. [Fat-hul Baariy (2/665) chapa ya As-Salafiyyah]
(b) Imesemwa kwamba ‘Uthmaan aliswali kamili Mina kwa kuwa alikuwa na mke Makkah, kwa dalili kwamba watu walipopinga yeye kuswali Mina rakaa nne aliwaambia: “Enyi watu! Mimi nimeoa Makkah tokea nije, na mimi nimemsikia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
((Mwenye kuoa kwenye mji fulani, basi aswali Swalaah ya mkazi)). [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraj” na Ahmad (1/62) kwa Sanad Dhwa’iyf. Al-Bayhaqiy kaitia kasoro ya kuweko mkatiko].
Hili limejibiwa: “Hadiyth hii imekosolewa kuwa ina mkatiko, haifai kwa hoja.
(c) Imesemwa: ‘Uthmaan aliswali kamili kwa kuwa yeye ni imamu wa Waislamu, na sehemu yoyote anaposhukia anazingatiwa kuwa ni mkazi na nyumbani kwake!!”
Hili limejibiwa: “Kwamba lililo bora zaidi kwa hukmu hii ni Nabiy wa Allaah. Imethibiti kwamba alikuwa akipunguza katika safari zake zote”.
Dalili ya sita ya Jamhuri:
Ni kwamba msafiri akiingia kwenye Swalaah ya mkazi, ataswali rakaa nne kwa makubaliano ya Jamhuri. Na lau kama faradhi yake ni ya kupunguza, msafiri asimfuate mkazi.
Wenye kusema ni wajibu wamejibu wakisema: “Faradhi ya msafiri ni rakaa mbili, na haibadiliki kwa kumfuata mkazi, lakini rakaa mbili za mwisho zinakuwa ni Sunnah, kwa dalili kwamba ikiwa hatokaa baada ya rakaa mbili za kwanza, Swalaah yake itabatilika kwa kuwa ameacha kikao ambacho ni faradhi kwake”.
Hili limejibiwa: “Haikubaliki kuwa rakaa mbili za mwisho kuwa ni Sunnah, na lau kama zingelikuwa ni hivyo, basi isingelikuwa ni wajibu kwake kutimiza nyuma ya imamu mkazi”.
Dalili ya saba ya Jamhuri:
Wametumia kipimo cha kufunga kwa msafiri katika mchana wa Ramadhwaan. Wanasema kuwa kufungua ni ruksa kwake lakini si wajibu, na hali ni hivyo hivyo katika kupunguza Swalaah.
Wenye kusema ni wajibu wamejibu wakisema: “Hiki ni kipimo kisichoendana, hakifai. Kwa kuwa Swiyaam hulipwa, na mfungaji huiachia badali kinyume na rakaa mbili katika Swalaah ya rakaa nne, kwani msafiri huziacha bila badali”.
(b) Dalili za wanaosema kwamba ni wajibu
Dalili ya kwanza: Hadiyth ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu Anha) aliposema: “Swalaah ilifaradhishwa rakaa mbili mbili katika ukazi na safari. Swalaah ya safari ikapitishwa, na ikazidishwa katika Swalaah ya faradhi”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (350) na Muslim (685)].
Jamhuri wamelijibu hili kwa njia mbili:
(a) Muradi wa kufaradhishwa Swalaah rakaa mbili ni kwa aliyetaka kuzifupisha. Zikaongezwa rakaa mbili katika Swalaah ya ukazi kwa njia ya lazima, na Swalaah ya safari ikapitishwa kuwa inajuzu kwa rakaa mbili.
Au muradi mwingine ni kwamba ufaradhi wa Swalaah ulianza kwa rakaa mbili, kisha zikakamilishwa kwa kufanywa nne, na kwa ajili hiyo, ‘Aaishah alikuwa akikamilisha katika safari.
(b) Hadiyth hii ni Mawquwf kwa ‘Aaishah. Hivyo basi, si dalili na hususan yeye hakushuhudia zama za kufaradhishwa Swalaah!!
Hili limejibiwa: “Hadiyth Mawquwf ikiwa haina nafasi ndani yake ya akili kuweza kuingia, basi itakuwa na hukmu ya urufaisho, na hapa ndivyo ilivyo”.
Dalili ya pili: Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas isemayo: ”Allaah Alifaradhisha Swalaah kwa ulimi wa Nabiy wenu rakaa nne kwa mkazi, rakaa mbili kwa msafiri, na rakaa moja vitani”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (687), Abu Daawoud (1247), na An-Nasaaiy (3/169)]
Jamhuri wamejibu: “Hadiyth haichukuliwi kwa mwonekano wake, bali makusudio yake ni kwamba Swalaah ya safari ni rakaa mbili katika hali ya kuzipunguza kwa msafiri. Ama akitaka kutimiza, basi hakuna ubaya ikiwa ni kukusanya kati ya dalili!!
Dalili ya tatu: Hadiyth ya ‘Umar bin Al-Khattwaab aliyesema: “Swalaah ya safari ni rakaa mbili, Swalaah ya Fitr ni rakaa mbili na Swalaah ya Ijumaa ni rakaa mbili kwa ukamilifu bila kupunguza kwa ulimi wa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (3/118), Ibn Maajah (1064) na Ahmad (1/37)].
Jamhuri wamejibu: “Muradi wa ukamilifu ni kuwa malipo ya Swalaah na fadhwla zake yanakuwa kamili bila upungufu. Na taawiyl hii imebidi ije kwa kuwa mwonekano wa Hadiyth unahukumia kwamba Swalaah iwe rakaa mbili katika safari bila kuwa imepunguzwa, na hili linapingana na Qur-aan katika kuiita “Qaswr!!”
Dalili ya nne: Neno lake Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Ni swadaqah ambayo Allaah Amewapeni, basi ikubalini swadaqah Yake) [Hadiyth Swahiyh: Tumeitaja nyuma kidogo].Hadiyth hii ishazungumziwa.
Dalili ya tano: Hadiyth ya Ibn ‘Umar aliyesema: “Nilisuhubiana na Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) safarini. Hakuzidisha zaidi ya rakaa mbili mpaka alipofariki. Nilisuhubiana na Abu Bakr safarini. Hakuzidisha zaidi ya rakaa mbili mpaka alipofariki. Nilisuhubiana na ‘Umar safarini. Hakuzidisha zaidi ya rakaa mbili mpaka alipofariki. Kisha nilisuhubiana na ‘Uthmaan safarini. Hakuzidisha zaidi ya rakaa mbili mpaka alipofariki. Na Allaah Amesema:
لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّـهَ كَثِيرًا
[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (689)] .
Ama tuliyoyaeleza nyuma kuhusu kupunguza ‘Uthmaan Swalaah akiwa Mina, linaloonekana ni kuwa hakuwa akiswali kamili isipokuwa Mina basi kutokana na Hadiyth ya Ibn ‘Umar isemayo: “Nabiy wa Allaah aliswali Mina rakaa mbili, na Abu Bakr baada yake, na ‘Umar baada ya Abu Bakr, na ‘Uthmaan mwanzoni mwa Ukhalifa wake, kisha ‘Uthmaan aliswali baada ya hapo rakaa nne”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1082) na Muslim (694)].
Jamhuri wamejibu: “Kitendo cha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kudumu kwake hakuonyeshi ulazima”.
Dalili ya sita: Rakaa mbili za mwisho inajuzu kuziacha bila kuzifidia, hivyo haijuzu kuzizidisha juu ya rakaa mbili za faradhi, kama lau angezizidisha katika Swalaah ya Alfajiri.
Jamhuri wamejibu: Kuchukulia Swalaah ya Alfajiri kama kipimo hakuendani, kwa kuwa Swalaah ya Alfajiri ni rakaa mbili na haikubali ziada kwa hali yoyote kinyume na Swalaah ya safari, kwani inakubali ziada wakati wa kumfuata mkazi.
Baada ya kuziweka mezani dalili za makundi mawili na kuzijadili, dalili za Jamhuri hazina salama isipokuwa kitendo cha ‘Uthmaan na ‘Aaishah zikilinganishwa na mwonekano wa Hadiyth za ‘Aaishah, ‘Umar na Ibn ‘Abbaas mbali na kudumu Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Makhalifa wake wawili katika kupunguza Swalaah safarini.
Linaloonekana ni kwamba kauli inayosema ni wajibu kupunguza ndiyo yenye nguvu na mwelekeo zaidi. Haingii ndani ya wigo huu aliyemfuata imamu mkazi. Na lau kama mtu atasema kwamba hilo ni Sunnah iliyokokotezwa na haitakikani kuiacha na kwamba kuswali kamili ni makruhu, basi atakuwa hakwenda mbali. Na haya yamenukuliwa toka kwa Sheikh wa Uislamu. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
Maulamaa wamekhitalifiana katika kuainisha masafa ambayo inajuzu kupunguza Swalaah katika kauli tatu:
Ya kwanza: Ni maili 48 sawa na kilometa 85. Hii ni kauli ya Ibn ‘Umar, Ibn ‘Abbaas, Al-Hasan Al-Baswriy na Az-Zuhry. Ni madhehebu ya Maalik, Al-Layth, Ash-Shaafi’iy, Ahmad, Is-Haaq na Abu Thawr. [Al-Qawaaniyn (100), Ad-Dusuwqiy (1/385), Al-Majmu’u (4/322), Al-Haawiy (2/361), Al-Mughniy (2/90) na Kash-Shaaful Qinaa (1/504)] Dalili zao ni:
1- Yaliyosimuliwa toka kwa Ibn ‘Abbaas ikiwa Marfu’u: “Enyi watu wa Makka! Msipunguze chini ya “burudi” nne toka Makkah hadi ‘Asqalaan”. Hadiyth hii ni Munkari, haifai. [Hadiyth Munkari: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ad-daaraqutwniy (148) na Al-Bayhaqiy (3/137). Angalia Al-Irwaa (565)].
2- Yaliyothibiti kwamba Ibn ‘Umar na Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu Anhumaa) walikuwa wakipunguza katika masafa ya “burudi” nne sawa na “farsakha” kumi na sita. [Hadiyth Swahiyh: Al-Bukhaariy kasema ni Mu’allaq (2/659) na Al-Bayhaqiy kasema ni Mawsoul. Angalia Al-Irwaa (568)].
“Al-Burud” ni wingi wa “Al-Bariyd”, nao ni mwendo wa “farsakha” nne, na “farsakha” moja ni sawa na maili tatu, na maili moja ni sawa na takriban kilometa 1.8.
3- Umbali wa “burudi” nne unakuwa na mazito ya safari kati ya kupanda na kushuka. Hivyo inajuzu kupunguza katika masafa hayo lakini si chini ya hapo.
Ya pili: Ni mwendo wa siku tatu na masiku yake kwa kutumia ngamia. Ni kauli ya Ibn Mas-’oud, Suwayd bin Ghaflah, Ash-Sha’abiy, An-Nakh’iy na Ath-Thawriy. Ni madhehebu ya Abu Haniyfah. [Ibn ‘Aabidiyn (2/122), Al-Hidaayah (1/80), Naylul Awtwaar (3/246), na Bidaayatul Mujtahid]
Dalili zao ni:
1- Hadiyth ya ‘Ibn ‘Umar toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) isemayo: ((Asisafiri mwanamke siku tatu ila awe pamoja na maharimu yake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1086) na Muslim (1338)].
2- Hadiyth ya ‘Aliy bin Abiy Twaalib kuhusu kupukusa juu ya khufu mbili isemayo: “Allaah Amezifanya siku tatu na masiku yake kwa msafiri, na siku moja na usiku wake kwa mkazi”. [Hadiyth Swahiyh: Imeelezewa kwenye mlango wa kupukusa juu ya khufu mbili].
Wamesema: “Kufungamana hukmu ya msafiri katika Hadiyth mbili kwa aliyesafiri siku tatu, hakufungamani na kupunguza chini ya hapo!!”.
3- Ni mantiki kwamba tatu ni uchache wa kingi na wingi wa kichache, na haijuzu kupunguza katika safari ndogo!! Ni wajibu mpaka wake uwe uchache wa kingi (nazo ni tatu)!!
Ya tatu: Kupunguza hakuna masafa maalumu, bali mtu hupunguza kwa chochote kijulikanacho kama safari.
Ni kauli ya Adh-Dhwaahiriyyah na chaguo la Sheikh wa Uislamu Ibn Taymiyyah na mwanafunzi wake Ibn Al-Qayyim. [Al-Muhalla (5/10), Majmu’u Al-Fataawaa (24/12-35), Zaad El-Ma’ad, Fat-hul Baariy (2/660) na Al-Mughniy (2/44)]
Dalili zao ni:
1- Kauli Yake Ta’alaa:
((وَإِذَا ضَرَبْتُمْ فِي الْأَرْضِ فَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَقْصُرُوا مِنَ الصَّلَاةِ إِنْ خِفْتُمْ أَن يَفْتِنَكُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ إِنَّ الْكَافِرِينَ كَانُوا لَكُمْ عَدُوًّا مُّبِينًا))
(( Na mtakaposafiri katika ardhi basi si dhambi kwenu kufupisha Swalaah mkikhofu kwamba waliokufuru watakushambulieni. Hakika makafiri wamekuwa kwenu ni maadui dhahiri )).
Mwonekano wa Aayah unaonyesha kwamba kupunguza kunahusiana na safari yoyote ardhini bila ya kuainishwa masafa maalum.
2- Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuainisha mpaka maalumu wa kiwakati au kimahala wa kupunguza Swalaah, bali kafungamanisha hukmu na kile kiitwacho safari tu. Hivyo haijuzu kutofautisha kati ya aina na aina bila dalili ya kisharia, bali la wajibu ni kukiainisha kilichoainishwa na sharia, na kutokiainisha kile kisichoainishwa. Mlango wa kukadiria masafa ya kupunguza Swalaah uko kwa Allaah na Rasuli Wake tu, nao hauingiliwi kwa rai hewa.
3- Imethibiti kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipunguza chini ya masafa yaliyotajwa nyuma kidogo:
(a) Imepokelewa toka kwa Anas akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapotoka mwendo wa maili tatu au farsakha tatu, huswali rakaa mbili”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (691)].
Hii inaonyesha kibayana kwamba kupunguza kunafungamana na safari yoyote ile hata kama itakuwa ni ya maili tatu au farsakha tatu. Al-Haafidh kasema: “Hii ni Hadiyth Swahiyh na bayana zaidi katika hili”.
Jamhuri wamelijibu hili wakisema: “Linachukuliwa hili kwa masafa ya kuanzia kupunguza na si kwa mwisho wa safari!!” Al-Haafidh anasema: “Umbali wa uchukulifu huu haufichikani, pamoja na kwamba Al-Bayhaqiy ameeleza katika riwaya yake kwa njia hii kwamba Yahya bin Zayd amesema: Nilimuuliza Anas kuhusu kupunguza Swalaah. Nilikuwa natoka Basrah kwenda Kuufah nikiswali rakaa mbili mbili mpaka ninapotoka. Anas akasema: Akaitaja Hadiyth. Ikaonekana kwamba alimuuliza kuhusiana na kujuzu kupunguza katika safari, na si mahala pa kuanzia kupunguza”.
(b) Imepokelewa toka kwa Anas akisema: “Niliswali Adhuhuri pamoja na Nabiy Madiynah rakaa nne, na rakaa mbili Dhul Hulayfah”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1089) na Muslim (690) na nyongeza ya (Alasiri) ni yake].
Masafa kati yao ni maili tatu.
(a) Imethibiti toka kwa wawili hao kinyume cha mpaka huo kwa Sanad Swahiyh. Aidha, wengine katika Maswahaba wamekwenda kinyume nao.
(b) Na lau kama tutakubali kwamba haikuthibiti toka kwao isipokuwa dalili walioitoa Jamhuri, na kwamba hakuna aliyekwenda nao kinyume, basi hapo pia hakuna hoja kwa kuwa kunakhalifiana na yaliyothibiti toka kwa Nabiy kama ilivyotangulia.
5- Ama katika Hadiyth: ((Asisafiri mwanamke siku tatu…)), hakuna kinachosema humo kwamba ili safari iwe ni safari ni lazima iwe ya siku tatu, bali maana yake ni kuwa haijuzu mwanamke kusafiri safari hii maalumu bila kuwa na maharimu yake. Kuna Hadiyth Swahiyh Marfu’u toka kwa Abu Hurayrah isemayo: (( Si halali kwa mwanamke anayemwamini Allaah na Siku ya mwisho kusafiri mwendo wa siku moja na usiku bila kuwa na mahramu yake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1088) na Muslim (1939)].
Katika Hadiyth hii, hakuna mpaka wa safari.
Ni kauli ya tatu isemayo kwamba Swalaah hupunguzwa kwa chochote kijulikanacho kama safari sawasawa ikiwa ni ndefu au fupi, na safari hiyo haina mpaka maalumu katika lugha. Hili linarejeshwa kwa watu wenyewe kwa mujibu wa ada na desturi, na linatofautiana kwa kutofautiana zama kimaendeleo kwa upande wa vyombo vya usafiri. Kidhibiti chake ni kusema mtu: “Mimi nasafiri kwenda mji fulani”, na si kusema: “Ninakwenda”, na huko anakokwenda kujulikane kiada kama ni safari kama kuchukua masurufu ya safari na kadhalika. Allah Ndiye Mjuzi Zaidi.
Jamhuri ya Maulamaa; Maalik, Ash-Shaafi’iy na Ahmad wanasema kwamba hairuhusiwi kupunguza isipokuwa katika safari ya wajibu au ya halali, na haijuzu katika safari ya maasia kama ujambazi na mfano wake. [Bidaayatul Mujtahid, (1/244), Al-Majmu’u (4/201), Al-Mughniy (2/101) na Kash-Shaaful Qinaa (1/324)]
Na hili linajengewa juu ya kauli yao kwamba kupunguza ni ruksa, na makusudio yake ni kumpumguzia uzito msafiri, na kwamba ruksa ya kupunguza imetolewa ili imsaidie msafiri kufanikisha malengo yake ya safari. Hivyo haiwi isipokuwa kwa msafiri halali, si kwa msafiri wa safari ya kwenda kumkasirisha Allaah.
Lakini Maulamaa wenye kusema kwamba ni wajibu kupunguza Swalaah ya safari kama Abu Haniyfah, Ibn Hazm, Ibn Taymiyah na wengineo, wanasema kwamba mtu atapunguza katika safari yoyote ile hata kama ni ya maasia, kwa kuwa faradhi yake ni rakaa mbili tu na si nne. Na hii ni kauli kwa Maalik. [Fat-hul Qadiyr (1/47), Al-Kharshiy (1/57), Al-Muhalla (4/267) na Majmu’u Al-Fataawaa (24/110)]
Ninasema: “Kwa yule ambaye kupunguza kwake ni ruksa, haruhusiki kupunguza katika safari ya maasia. Ama mwenye kusema kuwa ni wajibu kupunguza, hatofarikisha kati ya safari halali au safari ya maasia, na hili ndilo lenye nguvu. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
Maulamaa kwa kauli moja wanasema kwamba inajuzu kwa msafiri aanze kupunguza Swalaah baada ya kuyaacha majumba ya mji wake. [Al-Ijma’a cha Ibn Al-Mundhir (39) na Al-Mughniy (2/260)]
Kisha wakakhitalifiana kuhusiana na kujuzu kupunguza kabla ya hilo katika kauli mbili. Kauli sahihi zaidi kati ya mbili ni kuwa haijuzu kupunguza kabla ya kuyaacha majumba. Ni kauli ya Jamhuri. [Ibn ‘Aabidiyn (2/121), Adh-Dhahiyrah (2/365), Al-Majmu’u (4/202) na Kash-Shaaful Qinaa (1/325)]
Nayo inathibitishwa na Hadiyth ya Anas aliyesema: “Niliswali Adhuhuri pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Madiynah rakaa nne, na Dhul Hulayfah rakaa mbili”. [Hadiyth Swahiyh: Tumeitaja nyuma].
Hadiyth hii yaonyesha wazi kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akianza kupunguza Swalaah mara baada tu ya kutoka Madiynah.
Msafiri ataendelea kupunguza Swalaah madhali yuko safarini vyovyote muda urefukavyo. Lakini anapowasili kwenye mji alioukusudia, ni muda gani anaoruhusiwa kupunguza?
Jambo hili limenyamaziwa, halikuzungumzwa. Hakuna Hadiyth yoyote iliyopokelewa toka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inayoeleza wazi kuhusu hilo. Aidha, kipimo cha kuainisha muda huo hakina nguvu kwa Maulamaa. Na kwa ajili hiyo, Maulamaa wamekhitalifiana kuhusiana na suala hili kwa kauli takriban kumi na moja. Zilizo mashuhuri zaidi ni kauli nne ambapo wenye kauli hizi wamejaribu kutolea dalili kupitia matukio ya kupunguza yaliyonukuliwa toka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kauli mashuhuri zaidi ni hizi zifuatazo:
Ya kwanza: Akipanga kukaa zaidi ya siku nne hatopunguza
Hii ni kauli ya Jamhuri; Maalik, Ash-Shaafi’iy na Hanbali, isipokuwa Maalik na Ash-Shaafi’iy wamesema: Ni siku nne zikitolewa siku ya kuingia na ya kutoka. Hanbali wamewekea mpaka Swalaah ishirini na moja. [Ad-Dusuwqiy (1/364), Al-Majmu’u (4/361), Al-Haawiy (2/372), Al-Mughniy (2/132) na Kash-Shaaful Qinaa (1/330)]
Na wametoa dalili kwa haya yafuatayo:
1- Ni kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia Makkah asubuhi ya tarehe nne ya mfungo tatu, kisha akakaa Makkah tarehe nne, tano, sita na saba. Siku ya pili aliswali Alfajiri, kisha akatoka kwenda Mina, na alikuwa akipunguza Swalaah katika siku hizi nailhali ameazimia kukaa. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” kwa maana yake (1564), na Muslim (1240) katika Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas, na Muslim (1218) toka Hadiyth ya Jaabir].
Hili limejibiwa: Kwamba hakuna linaloashiria katika Hadiyth hii kwamba muda huu ndiyo muda mdogo zaidi wa kukaa, kwani imethibiti kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikaa zaidi ya muda huo huku akiendelea kupunguza kama itakavyokuja kubainishwa.
2- Hadiyth ya Al-‘Alaa bin Al-Khadhwramiy asemaye: “Nimemsikia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Mhamiaji atakaa Makkah siku tatu baada ya kumaliza amali ya Hijjah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (1352)].
Wanasema kwamba hili linaonyesha kuwa mwenye kukaa siku tatu hayuko katika hukmu ya mkazi, bali yuko kwenye hukmu ya msafiri.
Wamejibiwa: “Maana ya Hadiyth ni kwamba aliyehama toka Makkah kabla ya ukombozi, ni marufuku kwake kulowea hapo isipokuwa akae siku tatu tu baada ya kumaliza amali zake za Hijjah, asizidishe. Ama msafiri, si karaha kwake kuongeza zaidi ya siku tatu Makkah, lakini vipi kipimo chake kitakuwa? Halafu, katika Hadiyth hakuna ishara yoyote juu ya muda ambao msafiri akikaa atapunguza!!
Isitoshe, Hadiyth inaashiria kwamba zikizidi siku tatu kwa mhamaji, basi ataingia kwenye hukmu ya msafiri na si mkazi, wakati wao wanasema kwamba zikizidi siku tatu kwa msafiri, basi ukaazi wake ni sahihi. Na lau mmoja angelipimiwa kwa mwingine, basi ingelikuwa ni wajibu kwa msafiri apunguze zikizidi siku tatu na si aswali kamili kinyume na kauli yao. [Al-Muhalla (5/24)]
3- Athar ya ‘Umar bin Al-Khattwaab isemayo: “Mayahudi, Wakristo na Majusi waliwekewa muda wa siku tatu Madiynah za kununua na kukidhi mahitajio yao, na haruhusiwi yeyote kati yao kukaa humo kwa zaidi ya siku tatu”. [Isnadi yake ni ya watu madhubuti: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bayhaqiy (3/147-9,209) kwa Sanad ambayo wapokezi wake ni watu madhubuti isipokuwa wamezungumzia kusikia Yahya bin Bakiyr toka kwa Maalik].
Wamesema: “Athar inaonyesha kwamba siku tatu ni mpaka wa safari, na zaidi ya hapo ni mpaka wa ukazi.
Wamejibiwa: “Siku tatu hazionyeshi mpaka wa safari kama tulivyobainisha katika kipengele kilichotangulia”.
4- Ugeni wa msafiri ni siku tatu na baada ya hapo huhesabiwa ni mkazi!!
Wamejibiwa: “Hakuna chenye kuonyesha muda mdogo zaidi wa ukazi kama ilivyo wazi”.
Ya pili: Akipanga kukaa zaidi ya siku kumi na tano hatopunguza
Ni kauli ya Abu Haniyfah, Ath-Thawriy na Al-Muzaniy. [Al-Badaai-’i (1/97,98), Al-Hidaayah (1/81) na Al-Majmu’u (4/364)]
Dalili zao ni:
1- Hadiyth ya Anas isemayo: “Tulitoka Madiynah kwenda Makkah pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Alikuwa akiswali rakaa mbili mbili mpaka tuliporejea Madiynah. Akaulizwa: “Je, mlikaa Makkah siku zozote?” Akajibu: “Tulikaa siku kumi”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1081) na Muslim (693) na tamko jingine ni lake].
Na katika tamshi: “Tulikaa pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) siku kumi tukipunguza Swalaah”. Hili linajibiwa kwa yale yale yaliyotangulia katika Hadiyth ya Jaabir na Ibn ‘Abbaas.
2- Yaliyopokelewa toka kwa Ibn ‘Abbaas akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikaa Makkah mwaka wa ukombozi siku kumi na tano akipunguza Swalaah”. [Ni Dhwa’iyf kwa tamko hili: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1231) na Ibn Maajah (1076). Imekuwa Swahiyh kwa tamko la “kumi na tisa” na litakuja kuelezewa karibuni].
3- Yaliyopokelewa toka kwa Ibn ‘Abbaas na Ibn ‘Umar kwamba wamesema: “Ukisafiri ukafika kwenye mji, na huku umejipangia kukaa siku kumi na tano, basi swali Swalaah kamili. Na kama hujui ni lini utaondoka, basi punguza Swalaah”. [Kalitaja At-Tirmidhy toka kwa Ibn ‘Umar baada ya Hadiyth (548) bila isnadi yake].
Wanasema: “Uainisho huu hausemwi kwa rai ya mtu, bali una hukmu ya Hadiyth Marfu’u!!”.
Wamejibiwa: “Hiyo na kauli ya Swahaba iliyokhalifiwa na wengineo, hivyo haiwezi kuwa dalili. Isitoshe, yaliyothibiti toka kwa Ibn ‘Abbaas na Ibn ‘Umar ni kinyume chake. Ibn ‘Abaaas kasema: “ Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikaa siku kumi na tisa akipunguza, na sisi tukisafiri siku kumi na tisa tunapunguza, na kama tukizidisha tunaswali kamili”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1080)].
Ya tatu: Msafiri ataendelea kupunguza madhali hakupanga kukaa moja kwa moja
Ni kauli ya Al-Hasan, Qataadah na Is-Haaq, na imechaguliwa na Ibn Taymiyah. [Al-Majmu’u (4/365), Majmu’u Al-Fataawaa (24/18) na Al-Muhalla (5/23)]
Dalili zao ni:
1- Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas aliyosema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikaa siku kumi na tisa akipunguza, nasi tunaposafiri tunakaa siku kumi na tisa tunapunguza, lakini tukizidisha tunaswali kamili”. [Hadiyth Swahiyh: Tumeielezea nyuma kidogo].
2- Hadiyth ya Jaabir aliyosema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikaa Tabuk siku ishirini akipunguza Swalaah”. [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (3/295) na Abu Daawuud (1236). Hadiyth hii imetiwa kasoro. Angalia Al-Irwaa (574)].
3- Yaliyosimuliwa toka kwa ‘Imraan bin Haswiyn aliyesema: “Nilishiriki vitani pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na nilikuwa naye katika ukombozi wa Makkah. Akakaa Makkah masiku kumi na nane haswali isipokuwa rakaa mbili akisema: ((Enyi wenyeji! Swalini nne, sisi ni wasafiri)). [Hadiyth Dhwa’iyf: “Takhriyj” yake tushaielezea].
Wanasema: “Hadiyth hizi zinaonyesha kwamba uhakika wa msafiri haufungamani na muda maalumu, bali tunaloona ni kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipunguza katika siku kumi na nane, kumi na tisa na ishirini, kwa kuwa alikuwa ni msafiri”.
Kwa wenye madhehebu matatu yaliyotangulia ni kuwa msafiri anapokaa kwenye mji bila kuwa na nia ya kuendelea na ukaaji huo, halafu asijue ni lini atasafiri au lini atamaliza mambo yake, basi huyo atapunguza Swalaah siku zote. Kigezo chao ni kuwa Masalaf walifanya hivyo.
(a) Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar kwamba alikaa Azerbaijan miezi sita baada ya theluji kuwazingira. Alikuwa akiswali rakaa mbili. [Isnadi yake ni Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bayhaqiy (3/152) na Ahmad (2/83,154) kwa mfano wake kwa mapana kwa Sanad Hasan. Angalia Al-Irwaa (577)].
(b) Imepokelewa toka kwa Abu Al-Minhaal Al-‘Anziy akisema: “Nilimwambia Ibn ‘Abaas: Mimi ninakaa Madiynah mwaka mzima sisafiri”. Akaniambia: “Swali rakaa mbili”. [Isnadi yake ni Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abu Shaybah (2/207)]..
(c) Imepokelewa toka kwa Al-Hasan kwamba Anas bin Maalik alikaa Nisabuor mwaka mmoja au miwili. Alikuwa akiswali rakaa mbili, kisha hutoa tasliym, kisha huswali rakaa mbili, na wala hakusanyi. [Isnadi yake ni Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj" na Ibn Abu Shaybah (5099), na kutoka kwake Ibn Al-Mundhir (1736)].
(d) Imepokelewa toka kwake kwamba ‘Abdur Rahmaan bin Samurah kilimpitia kipindi kimoja au viwili vya baridi kali huko Kabul. Hakuwa akikusanya, na huswali rakaa mbili. [Isnadi yake ni Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj" na Ibn Abu Shaybah (2/13)].
(d) Imepokelewa toka kwa Anas akisema: "Maswahaba wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) walikaa Ram Hormuz miezi tisa wakipunguza Swalaah". [Isnadi yake ni Dhwa’iyf Imefanyiwa “ikhraaj" na Al-Bayhaqiy (3/152). Angalia Al-Irwaa (576)].
(d) Imepokelewa toka kwa Abu Waael akisema: "Tulikuwa pamoja na Masruwk huko Silsilah miaka miwili. Alikuwa na kibarua huko na alikuwa akituswalisha rakaa mbili mpaka alipoondoka". [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj" na Ibn Abu Shaybah (2/208), na ‘Abdu Ar Razzaaq (4357)].
Athar hizi zote zinathibitisha asili hii.
Ya nne: Msafiri atapunguza siku ishirini na masiku yake, kisha baada ya hapo ataswali kamili sawasawa akipanga kuendelea kukaa au bila kupanga
Ni kauli ya Abu Muhammad bin Hazm. Ash-Shawkaaniy kamfuata lakini yeye amepambanua kati ya aliyenuwia kukaa akisema: "Hapunguzi zaidi ya siku nne. Ama yule ambaye hakupanga na hajui lini ataondoka, basi huyo atapunguza siku ishirini, kisha ataswali kamili baada ya hapo. Na hii ni kauli ya Ash-Shaafi'iy". [Mughnil Muhtaaj (1/262)]
Maulamaa wenye kauli hii, wametoa dalili za Maulamaa wa kauli ya tatu isipokuwa wao wameangalia mambo mawili:
La kwanza: Nia ya kukaa haizingatiwi hapa, kwa kuwa nia haziingii katika amali ambazo Allaah Hakuziamuru kama kusafiri na kukaa sehemu, bali nia zinakuwa wajibu katika amali ambazo Allaah Ameziamuru, na hizo hazifai kufanywa bila nia. [Sheikh wa Uislamu Ibn Taymiyah amekubaliana nao juu ya hili. Angalia Al-Muhalla (5/29) na Majmuu Al-Fataawaa (24/41)]
La pili: Kuchunga asili, nako ni kuswali kamili. Wanasema: "Kiukweli ni kuwa asili ni mkazi kuswali kamili, kwa kuwa kupunguza Swalaah kumewekwa kwa msafiri tu. Na mkazi si msafiri, na lau kama si kuthibiti kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa alipunguza Makkah na Tabuk alipokuwa mkazi, basi kuswali kamili ingelikuwa ni wajibu. Hivyo, asili hiyo haiachwi ila kwa dalili, na dalili inaonyesha kupunguzwa Swalaah hadi siku ishirini kama ilivyo katika Hadiyth ya Jaabir. Na hakuna kauli yoyote sahihi inayoeleza kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipunguza akiwa mkazi zaidi ya hivyo mtu akapata kupunguza kwa idadi hiyo. Na hakuna shaka kwamba kupunguza kwake Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika muda huo hakukanushi kwamba alipunguza zaidi ya hapo. Lakini pamoja na hayo, angalizo la asili iliyotajwa ndilo lenye kuhukumia hilo". [Naylul Awtwaar (3/251)]
Hakuna katika Qur-aan Tukufu wala Hadiyh za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) isipokuwa mkazi na msafiri. Ama mlowezi katika nchi ya kigeni, huyu hakosi moja ya hali mbili: Kwanza, ima atakuwa ametua hapo, akatafuta nyumba yake binafsi, akaitia fenicha na samani, na akaishi hapo raha mustarehe. Huyu atakuwa ni mkazi na haruhusiwi kupunguza, si siku nne wala zaidi ya hapo, na halirejewi kwa hili kupunguza Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Swalaah huko Makkah siku nne nailhali yeye anajua kwamba atakaa huko muda huo. Na hii ni kutokana na yale tuliyoyaeleza nyuma kwamba kinachozingatiwa katika safari na ukazi ni mazingira ya ukaaji na utulivu, na si muda. Pili, au ashukie sehemu ambapo hahisi uhuru wala utulivu. Huyu atakuwa ni msafiri wa kupunguza madhali mambo yako hivyo hata zaidi ya siku ishirini.
Kwa mfano mtu anaweza kusafiri toka Mansourah hadi Cairo (Misri) kwa ajili ya haja ambayo anajua kwamba itachukua mwezi mmoja. Akawa wiki moja analala kwa jamaa yake, wiki nyingine kwa rafiki na kadhalika. Huyu hahesabiwi kama mkazi bali msafiri, na anaweza kupunguza apendavyo mwenyewe mpaka arejee kwake au apate sehemu ya kutulia kabisa kama nyumba yake binafsi.
Hii ndiyo kauli yenye nguvu kwa upande wetu katika mas’ala haya, nayo ndiyo yenye kukusanya dalili zote zilizotangulia, nayo iko karibu zaidi na kauli ya tatu ya Maulamaa ambayo inafuatiwa katika nguvu na kauli ya nne. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.
Hairuhusiwi kwa mwanafunzi kupunguza Swalaah akiwa hostelini kwake ikiwa atatulia hapo vyema kwa mujibu wa tuliyotangulia kuyasema kuhusiana na mazingira ya ukazi. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.
Hili ndilo sahihi kwa mujibu wa mwenendo wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Alikuwa akipunguza anapowaswalisha Maswahaba wake na wala hawajulishi kabla ya kuingia kwenye Swalaah kwamba anapunguza, au hata kuwaamrisha kutia niya ya kupunguza. Na haya ndiyo madhehebu ya Abu Haniyfah, Maalik na moja ya kauli mbili katika madhehebu ya Ahmad. [Majmu’u Al-Fataawaa (24/16-21), Al-Hidaayah (1/81), Ash-Sharhu As-Swaghiyr (1/174-na Bughyat As-Saalik) na Al-Mughniy (2/105)]
Na haya tushayaeleza katika mlango wa “Kutofautiana niya kati ya imamu na maamuma”.
Ikiwa msafiri atamfuata imamu mkazi katika Swalaah ya rakaa nne, basi hakosi moja ya mambo matatu:
La kwanza: Ni kuzipata rakaa tatu au nne pamoja na imamu
Hapo itamlazimu amfuate imamu na akamilishe rakaa nne nyuma ya imamu wake. Hii ni kauli ya Jamhuri ya Maulamaa kinyume na Ibn Hazm. [Al-Mughniy (2/151), Al-Muhalla (5/31), na Fat-hul Maalik Bitartiyb At-Tamhiyd (3/132)]
Dalili za Jamhuri ni hizi zifuatazo:
1- Ujumuishi wa kauli yake Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Hakika si jinginelo, imamu amewekwa ili afuatwe, basi msende kinyume naye)). [Hadiyth Swahiyh: “Takhriyj” yake ishaelezwa].
2- Hadiyth ya Muusa bin Salamah Al-Hadhliy aliyesema: “Nilimuuliza Ibn ‘Abbaas vipi niswali kama niko Makkah ikiwa sikuswali nyuma ya imamu?” Akajibu: “Rakaa mbili, Sunnah ya Abal Qaasim (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (688), An-Nasaaiy (3/119) na Ibnu Khuzaymah (951)].
Na katika tamko: “Sisi tukiwa nanyi, tunaswali rakaa nne, na tunaporejea kwenye nyumba tulizofikia, tunaswali rakaa mbili. Akasema: “Hiyo ni Sunnah ya Abal Qaasim (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (1/216), Ibnu Khuzaymah (952) na Al-Bayhaqiy (3/153) kwa njia tofauti].
3- Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar kwamba yeye alikuwa akikaa Makkah siku kumi akipunguza Swalaah. Lakini akiswali pamoja na watu, huswali kama wanavyoswali. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Maalik (196) na ‘Abdul Razzaaq (4381)]
Katika tamshi jingine: “Alikuwa anaposwali na imamu huswali rakaa nne, na kama anaswali peke yake huswali rakaa mbili”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (694)].
La pili: Ni kuipata rakaa moja au mbili pamoja na imamu. Hapa Maulamaa wana kauli mbili.
Ya kwanza: Ni lazima akamilishe nne. Ni madhehebu ya maimamu wanne na wengineo, na ni kauli ya Ibn ‘Umar, Ibn ‘Abbaas na Taabi’iyna. Wametoa dalili zilizotangulia na kwa Hadiyth ya Abu Mujlaz aliyesema: “ Nilimwambia Ibn ‘Umar: “Ikiwa msafiri atazipata rakaa mbili za Swalaah ya wakazi, je zitamtosheleza au itabidi akamilishe nao? Akacheka kisha akasema: “Atakamilisha pamoja nao”. [Al-Albaaniy kasema ni Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bayhaqiy (3/157). Angalia Al-Irwaa (3/22)].
Ya pili: Rakaa mbili tu zitamtosheleza. Ni kauli ya Is-Haaq, Twaawuus, Ash-Sha’abiy na Tamiym bin Hadhlam (Swahibu yake Ibn Mas-’oud) na Abu Muhammad Ibn Hazm.
Ninasema: “Huenda kuswali kamili ni sahihi zaidi kwa kuwa hii ndio kauli ya Ibn ‘Umar na Ibn ‘Abbaas. Hakuna Swahaba yeyote aliyekwenda kinyume nao, na kwa kuwa yeye kaipata jamaa pamoja na imamu mkazi, hivyo itambidi aswali kamili. Lakini panaweza kuja swali: “Ikiwa amenuwiya kupunguza nyuma ya mwenye kuswali kamili na akazipata rakaa mbili – bila kushurutisha mwoano kati ya niya ya imamu na maamuma kama ilivyotangulia- je zitamtosheleza?”
Ninasema: “Hapa ni mahala pa ijtihaad, na madhehebu ya Maswahaba ni bora zaidi kufuatwa. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
La tatu: Ni kupata chini ya rakaa pamoja na imamu
Al-Hasan, An-Nakh’iy, Az-Zuhriy, Qataadah na Maalik wanasema kwamba atapunguza kinyume na Jamhuri. Dalili zao ni:
1- Neno Lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Mwenye kuipata rakaa moja katika Swalaah, basi kaipata Swalaah)). [Hadiyth Swahiyh: “Takhriyj” yake imeelezwa nyuma kidogo].Na huyu anakuwa hakuipata hukmu ya jamaa.
2- Mwenye kuipata rakaa moja ya Swalaah ya Ijumaa, basi ataikamilisha. Ama apataye chini ya hapo, faradhi yake haimwajibikii bali ataswali rakaa nne kama tutakavyokuja kueleza katika mlango wa Swalaah ya Ijumaa.
Ninasema: “Mwelekeo wa hili una nguvu, na Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.”
Ikiwa mkazi anaswali Swalaah ya rakaa nne nyuma ya msafiri, basi ni lazima akamilishe rakaa zote nne baada ya imamu wake kutoa tasliym kwa mujibu wa Maulamaa wote. [Al-Mughniy (2/152)]
Na imesuniwa kwa imamu awajulishe baada ya kutoa tasliym kwa kuwaambia: “Kamilisheni Swalaah yenu, sisi ni wasafiri”.
1- Imepokelewa na Ibn ‘Umar kwamba ‘Umar (Radhwiya Allaahu Anhu) alikuwa anapokwenda Makkah, huwaswalisha watu rakaa mbili kisha husema: “Enyi watu wa Makka! Kamilisheni Swalaah yenu, sisi ni wasafiri”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Maalik (195), Ibn Abi Shaybah (1/419), ‘Abdul Razzaaq (4369) na Al-Baghawiy (1029)].
Imesimuliwa mfano wake Hadiyth Marfu’u ya ‘Imraan bin Huswayn kuhusiana na kisa cha ukombozi wa Makka lakini Hadiyth hii ni Dhwa’iyf. Lakini ‘Umar (Radhwiya Allaahu Anhu) alikifanya kitendo hicho mbele ya Maulamaa Maswahaba na hakuna yeyote aliyempinga. Isitoshe, hakuna aliyekhalifiana naye, na hilo lilikuwa likifanyiwa kazi.
2- Kwa kuwa ni wajibu kwake kuswali rakaa nne, isingeliwezekana aache rakaa yoyote kama lau asingelimfuata msafiri.
Msafiri akiwaswalisha watu wakiwemo wasafiri na wakazi, kisha wudhuu ukamtenguka baada ya rakaa, halafu mkazi akakamata mahala pake, nini kifanyike?
[Fat-hul Maalik Bitabwiyb At-Tamhiyd ‘Alaa Muwattai Maalik (3/133)]
(a) Pamesemwa: “Mkazi atakamilisha Swalaah ya imamu wa kwanza, kisha atawaashiria wanaomfuata wakae, halafu atasimama peke yake ili akamilishe rakaa nne. Baadaye atakaa tasha-hudi, na maamuma wasafiri walio nyuma yake watatoa tasliym. Halafu maamuma wakazi nao watasimama wakamilishe Swalaah peke yao. Hii ni kauli ya Maalik”.
(b) Pamesemwa: “Imamu wa pili atakamilisha Swalaah ya imamu wa kwanza, halafu atarudi nyuma, atamtanguliza msafiri ili amalize Swalaah na wasafiri watatoa tasliym pamoja naye, kisha wakazi watasimama kukamilisha rakaa zao zilizobakia kila mmoja peke yake. Hii ni kauli ya Abu Haniyfah na Maswahibu zake pamoja na Ath-Thawriy”.
(c) Pamesemwa: “Wote watakamilisha Swalaah ya mkazi”. Ni kauli ya Shaafi’iy, Al-Awzaaiy na Al-Layth.
Maulamaa wamekhitalifiana katika mas’-ala haya. Hii ni kutokana na kukhitalifiana mwonekano wa athari zenye kugusia aliyoyafanya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) safarini. Wamekhitalifiana juu ya kauli tano: [Fat-hul Baariy (2/674), Naylul Awtwaar (3/261), Zaad Al-Ma’ad (4738) na Al-Furu’u cha Ibn Muflih (2/59)]
1- Hairuhusiwi kabisa Swalaah za Sunnah safarini
Dalili yake ni Hadiyth ya Ibn ‘Umar aliyesema: “Niliandamana na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), sikumwona akiswali Sunnah za Rawaatib safarini. Na Allaah Anatuambia:
((لقد كان لكم في رسول الله أسوة حسنة))
[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1-11) na Muslim (689)].
Ibn ‘Umar alikuwa anasema anapowaona watu wakiswali Sunnah safarini: “Ningelikuwa ni mwenye kuswali Sunnah, ningeliswali kamili”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (689) na At-Tirmidhiy (544)].
2- Inaruhusiwa Sunnah zote
Waliosema hivi ni Jamhuri. Wametoa dalili kwa Hadiyth zenye kusunisha kiujumla Swalaah zote za Sunnah na za Rawaatib, kuswali Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Dhuhaa siku ya ukombozi wa Makkah na rakaa mbili za Alfajiri wakati walipolala mpaka jua likachomoza.
3- Sunnah zote zinaruhusika lakini za Rawaatib haziruhusiwi
Ni chaguo la Sheikh wa Uislamu na mwanafunzi wake Ibn Al-Qayyim, na kauli ya Ibn ‘Umar. Kigezo chao ni Ibn ‘Umar kukanusha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuswali Sunnah za Rawaatib pasina zinginezo isipokuwa rakaa mbili kutokana na yaliyothibiti toka kwa Ibn ‘Umar kwamba Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali Swalaah za Sunnah juu ya mgongo wa mnyama wake kule alikokuwa akielekea na kuashiria kwa kichwa chake. Ibn ‘Umar alikuwa akilifanya hilo. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1105) na Muslim (700) kwa mfano wake].
4- Za mchana haziruhusiwi lakini za usiku zaruhusiwa
Dalili ni Hadiyth ya ‘Abdullah bin ‘Aamir kwamba baba yake alimweleza kuwa alimwona Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anaswali Sunnah usiku safarini juu ya mnyama wake kule anakoelekea. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1104) na Muslim (689) kwa mfano wake].
Pia, ni kwa kutoacha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuswali Swalaah ya Witr akiwa nyumbani au safarini.
Ninasema: “Lakini kauli hii inachafuliwa na Swalaah ya Dhuhaa aliyoiswali Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) siku ya ukombozi wa Makkah”.
5- Hairuhusiwi Sunnah baada ya Faradhi lakini inajuzu kabla yake na kwa Sunnah zozote
Ni kauli ya Al-Bukhaariy katika Swahiyh yake. Al-Haafidh kaitilia nguvu akisema: “Tofauti kati ya Sunnah za kabla ya Faradhi na baada yake ni kuwa zile za kabla haziingii katika dhana kwamba ni sehemu ya Faradhi kwa kuwa zimejitenga nayo kwa iqaamah, kumngojea imamu na mfano wa hivyo, kinyume na za baada ya Faradhi ambazo aghlabu huhusiana nayo, na zinaweza kuwekwa katika dhana kwamba ni sehemu ya faradhi”.
Ninasema: “Asili ya hili ni kuthibiti kuswali Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) rakaa mbili kabla ya Alfajiri katika safari”.
Pili: Kukusanya Kati Ya Swalaah Mbili
Kukusanya kati ya Swalaah mbili ni kuswali Adhuhuri na Alasiri, au Magharibi na ‘Ishaa kwa pamoja katika wakati wa moja ya Swalaah mbili kwa mkusanyo wa kutanguliza au mkusanyo wa kuchelewesha.
Kukusanya kati ya Swalaah mbili kunajuzu kwa kauli ya Maulamaa wote lakini wamekhitalifiana upande wa miundo ya kukusanya na sifa yake kama tutakavyokuja kuchambua baadaye.
1- Kukusanya safarini:
Maulamaa wamekhitalifiana kuhusiana na hukmu ya kukusanya Swalaah mbili safarini juu ya kauli mbili:
Ya kwanza: Haijuzu kukusanya isipokuwa katika Siku ya Arafah na usiku wa kuweko Mahujaji Muzdalifah. Hii ni kauli ya Abu Haniyfah na riwaya toka kwa Maalik, Al-Hasan na Ibn Syriyn. Dalili yao ni: [Al-Mabsuwtw (1/235), Sharhul Ma’aaniy (1/162), Al-Mudawwanah (1/116) na Al-Mughniy (2/200)]
1- Kauli Yake Ta’alaa:
((إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا))
((Hakika Swalaah kwa Waumini ni fardhi iliyowekwa nyakati maalumu)). [An-Nisaa (:103)]
Nyakati za Swalaah zimethibiti kwa “Tawaaturi”, hivyo haijuzu kuziacha kwa habari ya “Aahaad”.
2- Hadiyth ya Ibn Mas-’oud aliposema: “Sikumwona Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiswali Swalaah yoyote katika wakati usio wake isipokuwa Swalaah mbili: Alipokusanya Magharibi na ‘Ishaa Muzdalifah, na aliposwali Alfajiri siku ile kabla ya wakati wake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1682) na Muslim (1289)].
3- Neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Kupoteza jambo hakupatikani mtu anapolala, lakini kupoteza ni mtu anapokuwa macho)).
Wanasema: “Kitovu cha kulipoteza jambo au kutolipoteza, kimefanywa katika hali ya kuwa macho au usingizini, na hayo hayahusishwi na ukazi au safari, na mkazi na msafiri wako sawa.
Ya pili: Inajuzu kukusanya kati ya Adhuhuri na Alasiri, na kati ya Magharibi na ‘Ishaa. Ni kauli ya Maalik, Ash-Shaafi’iy, Ahmad, Ath-Thawriy, Is-Haaq, Abu Thawr, na Ibn Al-Mundhir. Imesimuliwa na kundi la Maswahaba akiwemo Mu’aadh, Abu Musa, Ibn ‘Abbaas na Ibn ‘Umar. [Al-Mudawwanah (1/116), Bidaayatul Mujtahid (1/248), Al-Majmu’u (4/225), Al-Mughniy (2/200) na Naylul Awtwaar (3/253)]
Dalili yao ni:
1- Hadiyth ya Anas aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaposafiri kabla jua halijapinduka, huchelewesha Adhuhuri hadi wakati wa Alasiri, kisha huteremka na kukusanya Swalaah mbili. Na ikiwa limeshapinduka kabla hajasafiri, huswali Adhuhuri, kisha hupanda mnyama wake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1111) na Muslim (704)].
2- Hadiyth ya Ibn ‘Umar aliyesema: “Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anakusanya kati ya Magharibi na ‘Ishaa mwendo ukiwa mrefu kwake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1106) na Muslim (45)].
3- Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anakusanya Swalaah ya Adhuhuri na Alasiri akiwa safarini, na hukusanya kati ya Magharibi na ‘Ishaa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1107)].
Hadiyth ya Mu’aadh bin Jabal aliyesema: “Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anakusanya kati ya Adhuhuri na Alasiri, na kati ya Magharibi na ‘Ishaa katika vita vya Tabuk. [Akaichelewesha Swalaah siku moja, kisha akatoka, akaswali Adhuhuri na Alasiri kwa pamoja. Kisha akaingia, halafu akatoka, akaswali Magharibi na ‘Ishaa kwa pamoja]”. [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (706), Ibn Maajah (1070) bila nyongeza, Abu Daawuud (1201) na An-Nasaaiy (1/285)].
Hadiyth hizi na nyinginezo zinaonyesha kwa mwonekano wake na ujumuishi wake kwamba inajuzu kukusanya kati ya Swalaah mbili katika safari, sawasawa ikiwa ni “Jam-’u Taqdiym” au “Jam-’u Taakhiyr”.
Wenye kauli ya kwanza wamezichukulia Hadiyth hizi kama ni “ukusanyaji wa kipicha”, nako ni kucheleweshwa Magharibi kwa mfano mpaka mwisho wa wakati wake na kuharakishwa ‘Ishaa mwanzoni mwa wakati wake!!
Hili limetolewa neno lisemalo:” Kukusanya ni ruksa. Na kama kutakuwa kama walivyoeleza, basi ingelikuwa ni dhiki zaidi kuliko kuiswali kila Swalaah katika wakati wake, kwa kuwa mianzo ya nyakati na miisho yake hawaidiriki wajuzi wengi sembuse watu wa kawaida. Aidha, Hadiyth zimekuja zikibainisha wakati mmoja wa Swalaah mbili, na hili ndilo linalofahamika katika tamko la kukusanya”. [Fat-hul Baariy (2/675) chapa ya As-Salafiyyah]
Ama neno lao: “Hatuachi habari “Mutawaatir” kwa Hadiyth hizi, basi sisi tunasema:”Hatuziachi, bali tunazikhusisha nazo, na kuihusisha Mutawaatir na khabar Swahiyh, kunajuzu kwa Ijma’a ya Maulamaa”. [Al-Mughniy (2/201)]
Ama Hadiyth ya Ibn Mas-’oud, inavyoonekana ni kuwa haikusudii Ijma’a kwa pande mbili: Ni kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikusanya baina ya Adhuhuri na Alasiri Arafah, hivyo uainisho huo si sahihi. Halafu hakuna yeyote aliyesema kwamba Alfajiri iliswaliwa kabla ya wakati wake, bali makusudio ni kuharakia zaidi kuiswali.
Isitoshe, kuna wengineo zaidi ya Ibn Mas-’oud walioshuhudia kwa macho yao kukusanya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Swalaah safarini kwingineko kusiko Arafah na Muzdalifah. Na bila shaka, mwenye dalili hutangulizwa kabla ya asiye nayo, naye amekanusha na wengine wamethibitisha, na mthibitishaji hutangulizwa kabla ya mkanushaji pakizingatiwa kwamba Ibn Mas-’oud kasema kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anakusanya kati ya Swalaah mbili safarini. [Isnadi yake ni Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Ya’alaa (5413), At-Twabaraaniy katika Al-Kabiyr (10/39) na At-Twahaawiy katika Sharhul Ma’aaniy (1/160)].
2- Kukusanya mjini anakoishi mtu
Kukusanya Swalaah mbili hakuhusishwi na safari tu, bali inajuzu kukusanya mtu akiwa mjini kwake kwa sababu hizi zifuatazo:
(a) Mvua
Inajuzu kukusanya Adhuhuri na Alasiri, au Magharibi na ‘Ishaa kutokana na mvua kwa mujibu wa kauli ya Jamhuri. Lakini Maalik amekuhusisha kujuzu huko kwa usiku tu na si mchana!! Dalili zao ni hizi zifuatazo:
1- Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikusanya baina ya Adhuhuri na Alasiri, na Magharibi na ‘Ishaa Madiynah bila kuweko vita wala mvua”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (705). Angalia Al-Irwaa (579)].
Hili linatufahamisha na kutuhisisha kwamba kukusanya Swalaah kutokana na mvua kulikuwa kunajulikana wakati wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na lau kama isingelikuwa hivyo, kusingelikuwa na faida ya kukanusha mvua kama ni sababu ya kuruhusu kukusanya Swalaah. [Irwaaul Ghaliyl (3/40)]
2- Imepokelewa toka kwa Naaf’i akisema kwamba Ibn ‘Umar alikuwa anapowakusanya viongozi baina ya Magharibi na ‘Ishaa wakati wa mvua, hukusanya Swalaah hizo pamoja nao. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Maalik (333) na Al-Bayhaqiy kutoka kwake].
3- Imepokelewa toka kwa Hishaam bin ‘Urwah kwamba baba yake ‘Urwah, Sa’iyd bin Al-Musayyib na Abu Bakr bin ‘Abdul Rahmaan bin Al-Haarith bin Hishaam bin Al-Mughyrah Al-Makhzoumiy, walikuwa wakikusanya baina ya Magharibi na ‘Ishaa katika usiku wa mvua, na hawalioni hilo kama tatizo. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bayhaqiy (3/168). Angalia Al-Irwaa (3/40)].
4- Imepokelewa toka kwa Muusa bin ‘Uqbah ya kwamba ‘Umar bin ‘Abdul Aziyz alikuwa akikusanya baina ya Magharibi na ‘Ishaa ya mwisho kama kuna mvua. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bayhaqiy (3/168). Angalia Al-Irwaa (3/40)].
(b) Haja ya dharura
Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Abbaas akisema: “Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali Adhuhuri na Alasiri kwa pamoja Madiynah bila kuwepo vita au mvua”. Abu Kurayb au Sa’iyd akamuuliza: “Kwa nini alifanya hivyo?” Akajibu: “Ili asiusumbue na kuutaabisha umma wake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (705) na Ahmad (1/223)].
Katika hili, pana ruksa kwa wenye nyudhuru ili kuwaondolea tabu na mashaka kinyume na wale wasio na nyudhuru kama hizi. Hii ni kauli ya Ibn Syriyna na Ash-hab mfuasi wa karibu wa Maalik. Al-Khattwaabiy ameisimulia toka kwa Al-Qaffaal Ash-Shaasiy mfuasi wa karibu wa Ash-Shaaf’iy toka kwa Is-Haaq Al-Marouziy toka kwa jumuiko la Maulamaa wa Hadiyth. Ibn Al-Mundhir na Ibn Taymiyah wamelikhitari. [Majmu’u Al-Fataawaa (24/25), Sharhu Muslim cha An-Nawawiy (2/3509), Al-Qawaaniyna (75) na Ma’aalim As-Sunan (2/55)]
Sheikh wa Uislamu amesema: “Ikiwa itakuwa uzito kwa wazalishaji viwandani na wakulima wakati wa Swalaah unapoingia kama maji kuwa mbali nao, au kama watayaendea ili kujitwaharisha kazi yao itasimama, basi wanaweza kuswali katika wakati mmoja kwa kukusanya Swalaah mbili”. [Majmu’u Al-Fataawaa (21/458)]
Mgonjwa ambaye inakuwa uzito kwake kuiswali kila Swalaah katika wakati wake, anaruhusiwa kukusanya kutokana na Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas iliyotangulia na kwa kuchukulia kipimo cha mwanamke mwenye damu ya Istihaadhwah. Inasimuliwa kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwamuru Hamnah bint Jahsh ambaye alikuwa akisumbuliwa sana na damu ya Istihaadhwah kwa kumwambia:
((Ikiwa utahimili kuichelewesha Adhuhuri na kuiwahisha Alasiri, kisha ukaoga wakati unapotwaharika ukaswali Adhuhuri na Alasiri kwa pamoja, halafu ukaichelewesha Magharibi na kuiwahisha isha, kisha ukaoga na kuzikusanya Swalaah mbili, basi fanya)). [Al-Albaaniy kasema ni Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (287), At-Tirmidhiy (128) na Ibn Maajah (627). Angalia Al-Irwaa (188). Inaonekana kama kuipitisha kama Hadiyth Hasan kuna angalizo].
Maalik na Ahmad wamejuzisha mgonjwa kukusanya Swalaah. Sheikh wa Uislamu kalikhitari hilo, lakini Ash-Shaafi’iy kakataa. [Al-Qawaaniyn (75), Al-Mughniy (2/112) na Al-Majmu’u (4/370)]
Kauli ya kujuzu hilo iko wazi, na Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
[Al-Kharshafiy (2/70), Al-Majmu’u (3/375), Al-Inswaaf (2/342), Al-Mughniy (2/132) na Majmu’u Al-Fataawaa (24/54-56)]
1- Akiziswali katika wakati wa Swalaah ya pili (jam’u taakhiyr), basi si sharti kuandamisha baina ya Swalaah mbili zinazokusanywa, bali anaweza kuachanisha kati yao. Kwa mfano, anaweza kuswali Adhuhuri mwanzo wa wakati wa Alasiri, kisha akaichelewesha Alasiri kidogo akaja kuiswali kabla wakati wake haujatoka. Hii ni kauli ya Jamhuri kinyume na baadhi ya Mahanbali.
2- Akiziswali katika wakati wa Swalaah ya kwanza (Jam-’u Taqdiym), Jamhuri wanasema kwamba ni lazima aziswali bila kuziachanisha. Sheikh wa Uislamu Ibn Taymiyah amekhalifiana nao kwa kusema kwamba hilo halishurutishwi. Ni riwaya toka kwa Ahmad, na kauli ya Ash-Shaafi’iy, na hili lakubalika zaidi.
Ibn Taymiyah kasema: “Si sharti kuandamisha kati ya Swalaah mbili, si katika wakati wa Swalaah ya kwanza wala ya pili. Hilo halina mpaka katika sharia, na kulichunga kunaangusha makusudio ya ruksa. Na Sunnah imekuja kwa upana zaidi ya hivyo, kwani Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikusanya mwanzo wa wakati kama alivyofanya ‘Arafah, na wakati mwingine alikusanya katika wakati wa Swalaah ya pili kama alivyofanya Muzdalifah na katika safari zake nyinginezo. Pia, wakati mwingine alikusanya katikati ya nyakati za Swalaah mbili, na katika hali hii zinaweza kuwa mwishoni mwa wakati wa Swalaah ya kwanza, au mwanzoni mwa wakati wa Swalaah ya pili”.
Swalaah ya pili inaweza kuswaliwa wakati wa Swalaah ya kwanza, na ya kwanza wakati wa Swalaah ya pili, yote yanajuzu. Hii ni kwa vile asili ya suala hili ni kuwa wakati unakuwa ni mmoja ikitokea haja, na kutanguliza na kuweka kati ni kwa sababu ya maslaha.
Imesuniwa wakati wa kukusanya Swalaah mbili kutosheka na adhana moja tu na kuqimu kwa kila Swalaah. Katika Hadiyth ya Jaabir, anasema kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali Swalaah mbili Arafah kwa adhana moja na iqama mbili. Akaenda Muzdalifah, akaswali hapo Magharibi na ‘Ishaa kwa adhana moja na iqamah mbili. Hakuswali Sunnah kati yake, kisha akalala kwa ubavu mpaka ilipochomoza Alfajiri. [Hadiyth Swahiyh: Itakuja kamili na “takhriyj” yake katika Mlango wa Hijjah InshaAllaah].
Imepokelewa na Ibn Mas-’oud akisema: “Tukafika Muzdalifah wakati inaadhiniwa ‘Ishaa au muda kidogo kabla yake, akamwamuru mtu mmoja aadhini na kuqimu kisha akaswali Magharibi. Baada yake aliswali rakaa mbili, halafu aliagiza mlo wake wa usiku akala, kisha akamwamuru Uraa aadhini na kuqimu, halafu akaswali ‘Ishaa rakaa mbili….”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1675) na Muslim 1289) kwa mfano wake].
Huu ni mwelekeo wa Ash-Shaafi’iy katika madhehebu yake ya zamani, na riwaya toka kwa Ahmad na Ibn Hazm. Lakini Ath-Thawriy, Ahmad katika riwaya nyingine na Ash-Shaafi’iy katika madhehebu mapya, wanaona kwamba atakusanya Swalaah mbili kwa iqaama mbili tu. Wameishikilia Hadiyth ya Usaamah anayesema: “Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuja Muzdalifah aliteremka, akatawadha, akaufanya vyema wudhuu wake. Halafu Swalaah ikaqimiwa, akaswali Magharibi na kisha kila mtu alimtua ngamia wake nyumbani kwake. Halafu ‘Ishaa ikaqimiwa akaswali, na wala hakuswali Swalaah yoyote baina ya Swalaah mbili”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1672), Muslim (1280) na Ahmad (5/263)].
La sawa ni hayo waliyoyasema hao wa mwanzo kwa kuwa Hadiyth ya Jaabir imejumuisha ziada ya adhana, nayo ni ziada isiyo kanushi, hivyo ni lazima kuikubali. [Naylul Awtwaar (3/263) chapa ya Al-Hadiyth]
Allaah Ndiye Mjuzi zaidi.
Ni sharti kuwepo mpangilio kati ya Swalaah mbili zinazokusanywa, kwa kuwa sharia imekuja na mpangilio maalumu wa nyakati za Swalaah zote. Hivyo, ni wajibu kila Swalaah iwe katika mahala pake ilipopangiwa na sharia kwani Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:
((Swalini kama mnavyoniona nikiswali)).
Lakini, lau kama mtu atasahau, au akawa hajui, au akawakuta watu wanaswali ‘Ishaa huku yeye kanuwia “Jam-’u Taakhiyr”, akaswali nao ‘Ishaa halafu akaswali Magharibi, je itamtosheleza? Mafuqahaa wanasema kwamba haitofaa, Swalaah yake ya ‘Ishaa itakuwa ni batili, na itambidi aswali tena ‘Ishaa baada ya Magharibi. [Sharhul Mumti’i (4/576)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
038-Swalaah Ya Khofu
Alhidaaya.com [3]
[Al-Badaai’u (1/243), Haashiyatul ‘Adawiy (1/296), Rawdhwat At-Twaalibiyna (2/49) na Al-Mughniy (2/402)]
Khofu ni kutarajia adha kutokana na dalili za kuhisika au zinazoonekana wazi. Na makusudio yake hapa ni kupambana na adui au chochote ambacho kinamtia mtu khofu na taharuki.
Swalaah ya Khofu si Swalaah ya kujitegemea yenyewe kama Swalaah ya ‘Iyd au ya Kupatwa Jua na kadhalika, bali ni Swalaah ya kawaida ya faradhi kwa nguzo zake zilezile, masharti yake, Sunnah zake na idadi ya rakaa zake kama inavyokuwa katika hali ya amani. Isipokuwa tu kama itaswaliwa kwa jamaa, itakuwa kwa namna tofauti, na itabeba mambo ambayo haina katika hali ya amani. Na kwa msingi huu, tunaweza kuielezea Swalaah ya Khofu kama ni Swalaah ya Faradhi ambayo wakati wake unaingia na Waislamu wanapambana na adui au wakijilinda na adui.
Swalaah ya Khofu imethibiti kutokana na Neno Lake Ta’alaa:
((وَإِذَا كُنتَ فِيهِمْ فَأَقَمْتَ لَهُمُ الصَّلَاةَ فَلْتَقُمْ طَائِفَةٌ مِّنْهُم مَّعَكَ وَلْيَأْخُذُوا أَسْلِحَتَهُمْ فَإِذَا سَجَدُوا فَلْيَكُونُوا مِن وَرَائِكُمْ وَلْتَأْتِ طَائِفَةٌ أُخْرَىٰ لَمْ يُصَلُّوا فَلْيُصَلُّوا مَعَكَ وَلْيَأْخُذُوا حِذْرَهُمْ وَأَسْلِحَتَهُمْ ۗ وَدَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْ تَغْفُلُونَ عَنْ أَسْلِحَتِكُمْ وَأَمْتِعَتِكُمْ فَيَمِيلُونَ عَلَيْكُم مَّيْلَةً وَاحِدَةً ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِن كَانَ بِكُمْ أَذًى مِّن مَّطَرٍ أَوْ كُنتُم مَّرْضَىٰ أَن تَضَعُوا أَسْلِحَتَكُمْ ۖ وَخُذُوا حِذْرَكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ أَعَدَّ لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا))
((Na utapokuwa upo kati yao, ukawaswalisha, basi lisimame kundi miongoni mwao pamoja nawe, na wachukue silaha zao. Watakaposujudu basi wawe nyuma yenu (kuwalinda). Na lije kundi jingine ambalo halikuswali, liswali pamoja nawe, nao washike hadhari na silaha zao. Wale waliokufuru wanatamani kama mtaghafilika na silaha zenu na vifaa vyenu wakuvamieni mvamio mmoja. Na wala si dhambi kwenu ikiwa mna maudhiko kutokana na mvua au mkiwa wagonjwa kuweka (chini) silaha zenu. Na mshike hadhari zenu. Hakika Allaah Amewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha)). [An-Nisaa (4:102)]
Aidha, imethibiti kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliiswali kama tutakavyokuja kulieleza hilo, na Maulamaa wamekubaliana wote juu ya hili, halafu wakakhitalifiana kuhusiana na kujuzu kwake baada ya kufariki Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Jamhuri ya Maulamaa –kinyume na Abu Yuusuf swahibu yake Abu Haniyfah- wanaona kwamba sharia ya Swalaah hii iko mpaka Siku ya Qiyaamah, na kwamba agizo alilopewa Nabiy ni agizo kwa umma wake pia madhali hakuna dalili ya kulihusisha agizo hilo kwake peke yake. [Al-Badaai’u (1/242), Al-Mudawwanah (1/161), Al-Ummu (1/186) na Al-Mughniy (2/400)]
Pia, kuhusishwa yeye na agizo hakumaanishi kwamba hukmu inamhusu yeye peke yake mbali na kwamba:
1- Kauli yake: ((Swalini kama mnavyoniona nikiswali)), ni jumuishi. [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa mahala pengi].
2- Maswahaba wote kwa pamoja wamekubaliana uwepo wa Swalaah hii baada ya kufariki Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) [Al-Haafidh kainukuu Ijma’a kwenye Al Fat-h (2/498) na Ibn Qudaamah kwenye Al-Mughniy (2/400)]…… na kwa waliosimuliwa kuwa wameiswali ambao ni: [Angalia baadhi ya athar zilizopokelewa toka kwao na takhriyj zake katika Irwaa Al-Ghaliyl (3/42-45)]
(a) ‘Aliy usiku wa vita vya Swaffayn na Al-Hariyr.
(b) Abu Muusa Al-Ash-’ariy na wenzake huko Asbahaan.
(c) Hudhayfah bin Al-Yamaan na Maswahaba akiwemo Sa’ad bin Abi Waqqaas huko Tubrustan.
Ama Al-Mazniy ambaye ni katika wafuasi wa Ash-Shaafi’iy, yeye anaona kwamba Swalaah hii ilikuwepo lakini baadaye iliondoshwa!! Hoja yake ni kuwa katika vita vya Khandaq, zilimpita Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Swalaah, na lau kama Swalaah ya Khofu ingelikuwa inajuzu, basi angeiswali. Amejibiwa kwamba hilo lilikuwa kabla ya kuteremka Aayah ya Swalaah ya hofu kama ilivyo katika Hadiyth ya Abu Sa’iyd isemayo: “Tulizingirwa Siku ya Khandaq…. Na hii ni kabla Allaah ‘Azza wa Jalla Hakuteremsha lolote kuhusu Swalaah ya Khofu”. Hadiyth hii ishaelezewa kwenye mlango wa kulipa Swalaah zilizompita mtu.
Kuna namna nyingi za kuiswali Swalaah ya Khofu zilizothibiti toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) zikiwa na usuwli sita. Hakuna makhitalifiano kati ya Maulamaa kuhusiana na namna yoyote, bali kila moja inafaa kwa kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliiswali mara kadhaa, katika siku tofauti na kwa miundo mbalimbali. Katika kila muundo, alikuwa akiangalia namna itakayochunga Swalaah na kuwalinda zaidi na adui. [Al-Badaai-’i (1/342), Mughnil Muhtaaj (1/301), Al-Mughniy (2/412) na Naylul Awtwaar (3/367 na kurasa zinazofuatia)]
Picha zake ni tofauti lakini maana yake ni moja. Kati ya miundo hiyo ni:
(a) Ikiwa adui hayuko upande wa Qiblah
1- Askari watagawanywa vikosi viwili. Kikosi kimoja kitawekwa mkabala na adui na kingine kitajihami nacho kwa namna ambayo mishale haiwezi kukifikia. Imamu ataanza Swalaah na kikosi hiki, na ataswali nao rakaa moja ikiwa Swalaah ni ya rakaa mbili, au rakaa mbili kama Swalaah ni ya rakaa tatu au nne, kisha atabakia amesimama. Halafu maamuma watakamilisha Swalaah wenyewe kisha watakwenda kusimama mkabala na adui. Halafu kitakuja kikosi kilichokuwa awali mkabala na adui, imamu atawaswalisha kwa rakaa zilizobakia, na anapokaa kwa tashah-hudi, wao watasimama kukamilisha rakaa zilizobakia huku yeye akiwasubiri, na wanapokuja kukaa naye, atatoa tasliym kumaliza nao Swalaah. [Haya ndiyo waliyosema Jamhuri ya Maulamaa. Maalik kasema kwamba imamu hatoi tasliym wala hawangojei, bali anapotoa tasliym wao watakamilisha wenyewe rakaa zilizosalia kwa mujibu wa Hadiyth Mawquwf]
Asili ya hili ni Hadiyth ya Swaaleh bin Khawwaat kuhusiana na walioswali na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Swalaah ya Khofu Siku ya Dhaat Ar Riqa’a isemayo: “Kikosi kimoja kilisimama safu pamoja naye, na kikosi kingine kilisimama safu mkabala wa adui. Akaswali rakaa moja na kikosi kilichosimama naye, kisha akabaki amesimama, na wao wakakamilisha wenyewe. Walipomaliza walikwenda kusimama mkabala wa adui, na kikosi kilichokuwa mkabala na adui kikaenda kwake, akaswali nao rakaa iliyokuwa imesalia katika Swalaah yake. Halafu alibaki amekaa mpaka wakakamilisha wenyewe, kisha akatoa tasliym pamoja nao”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (4130) na Muslim (842)].
Tamshi la Swaaleh bin Khawwaat alilolipokea toka kwa Sahl bin Abi Hatamah linasema kwamba yeye anawangojea akiwa amekaa si amesimama, na ndivyo lilivyo kwenye Swahiyh. Ash-Shaafi’iy na wafuasi wake wanaufuata muundo huu.
2- Imamu ataswali rakaa moja na kikosi cha kwanza, na kikosi kingine kitaelekea upande aliko adui. Kisha kikosi alichokiswalisha rakaa moja kitaondoka kiende kusimama upande aliko adui. Halafu kitakuja kile kikosi kingine, atakiswalisha rakaa moja, halafu kila kikosi kitakamilisha chenyewe rakaa moja.
Asili ya hili ni Hadiyth ya Ibn ‘Umar aliyesema: “Nilishiriki vita eneo la Najd pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Tulimweka adui mkabala wetu na tukapanga safu mbele yao. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasimama kutuswalisha. Kikosi kimoja kikasimama pamoja naye kuswali na kikosi kingine kikamwelekea adui. Rasuli akakiswalisha kikosi alichonacho rakaa kamili. Kisha wakaondoka kwenda kukamata nafasi ya kikosi ambacho bado hakijaswali, wakaja, Rasuli akawaswalisha rakaa kamili halafu akatoa tasliym. Kisha kila kikosi kikajikamilishia chenyewe rakaa moja”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (943) na Muslim (839)].
Mwonekano wa Hadiyth hii ni kuwa wote walikamilisha katika hali moja. Pia yawezekana kwamba kikosi cha pili kilikamilisha baada ya tasliym, halafu wakarejea wale wa mwanzo mahala pao wakakamilisha rakaa. Na hili ndilo lenye nguvu kwa upande wa maana, na kama si hivyo basi ulinzi unaotakikana kuwekwa utakosekana na imamu atabaki peke yake. Riwaya ya Ibn Mas-’oud inalitilia nguvu hili. Inasema: “Kisha akatoa tasliym, na hawa (yaani kikosi cha pili) wakasimama kujikamilishia wenyewe rakaa, wakatoa tasliym kisha wakaondoka. Halafu wakaja wale kwenye sehemu yao wakajikamilishia wenyewe rakaa moja, kisha wakatoa tasliym”. [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Dawuud (1244), At-Twahaawiy (1/184) na Ad-daaraqutwniy. Angalia Al-Irwaa (3/49)].
Mahanafi wanaufuata muundo huu isipokuwa Abu Yuusuf.
3- Imamu ataswali na kikosi kimoja rakaa mbili na atatoa tasliym, kisha ataswali na kingine na kutoa tasliym.
Asili ya hili ni Hadiyth ya Jaabir na Hadiyth ya Abu Bakrah. Jaabir anasema: “Tulikuwa pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) huko Dhaat Ar Riqa’a, na Swalaah ikaqimiwa. Akaswali na kikosi kimoja rakaa mbili kisha wakarudi nyuma, halafu aliswali na kikosi kingine rakaa mbili. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawa ameswali rakaa nne, na watu rakaa mbili”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy ikiwa mu’allaq (4136), na mawsuul kwa Muslim (843). Angalia At-Taghliyq (4/120)].
Tamshi jingine linasema: “Aliswali na kundi la Maswahaba wake rakaa mbili kisha akatoa tasliym, halafu akaswali na jingine rakaa mbili na kutoa tasliym”. [Isnadi yake ni dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ash-Shaafi’iy (506), An-Nasaaiy (3/178), Ad-daaraqutwniy (186) na Al-Bayhaqiy (3/259)].
Abu Bakrah anayatilia nguvu haya akisema kwenye Hadiyth yake: “Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alituswalisha Swalaah ya Khofu. Akaswali rakaa mbili pamoja na baadhi ya Maswahaba wake, kisha akatoa tasliym. Wakarudi nyuma na wakaja wengine wakasimama mahala pao, Nabiy akaswali nao rakaa mbili kisha akatoa tasliym. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawa ameswali rakaa nne, na watu rakaa mbili mbili”. [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (3/179), Abu Dawuud (1248), Al-Bayhaqiy (3/260) na At-Twahaawiy (1/315)].
Hadiyth mbili zinaonyesha kwamba inajuzu kwa mwenye kuswali faradhi kumfuata mwenye kuswali Sunnah. Kwa kuwa rakaa mbili za mwisho zilikuwa ni Sunnah kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na kwa kundi la pili zilikuwa ni faradhi.
4- Imamu ataswali rakaa moja na kikosi kimoja – kingine kikiwa kimemwelekea adui – kisha wataondoka, halafu kitakuja kikosi cha pili na ataswali nacho rakaa moja. Kila kikosi kitatosheka na rakaa moja tu na hawataswali rakaa nyingine.
Asili ya hili ni Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas asemaye: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali Dhiy Qarad, watu wakapanga safu mbili nyuma yake; safu moja nyuma yake moja kwa moja na nyingine mkabala na adui. Akaswali rakaa moja na safu iliyo nyuma yake moja kwa moja, kisha wakarejea hawa kwenda kwenye safu ya wale wengine. Wale wengine wakaja kwenye safu ya hawa, akaswali nao rakaa moja tu na hawakuswali ya pili”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (3/169), Ibn Hibaan (2871) na Ahmad lakini kwake hakuna “na hawakuswali ya pili”!!]
Abu Hurayrah [Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (3035), Ahmad (2/522) na An-Nasaaiy (3/174), na Sanad yake ni Hasan], …Zayd bin Thaabit [Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (3/168) na Ahmad (5/183), na Sanad yake ni Hasan katika Hadiyth wenza],… na Hudhayfah [Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (3/168) na Ahmad (5/183), na Sanad yake ni Hasan katika Hadiyth wenza], …wana Hadiyth kama hii.
Hadiyth nyingine ya Ibn ‘Abbaas inayoonyesha kuswihi kutosheka na rakaa moja inasema: “Allaah (Jalla wa ‘Alaa) Aliifaradhisha Swalaah kwa ulimi wa Nabiy wenu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam); mjini rakaa nne, safarini rakaa mbili, na kwenye khofu (vita) rakaa moja”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (687), Abu Daawuud (1247) na Ahmad (1/237)].
5- Jeshi litagawanywa vikosi viwili. Kikosi kimoja kitasimama safu nyuma ya imamu na kingine kitatazamana na adui. Vikosi vyote viwili vitafunga Swalaah pamoja na imamu, halafu kikosi kilicho nyuma yake kitarukuu na kusujudu pamoja naye huku kikosi kinachotazamana na adui kikibaki kimesimama. Kisha askari walioswali na imamu rakaa mbili watachukua silaha zao waende kusimama mbele ya adui, na wale waliokuwa mbele ya adui watakwenda nyuma ya imamu, watajiswalia wenyewe rakaa moja huku imamu amesimama, halafu atawaswalisha rakaa ya pili. Kisha watakuja waliokwenda kusimama mbele ya adui, watajiswalia wenyewe rakaa moja huku imamu na kikosi kingine wakiwa wamekaa, kisha imamu atatoa tasliym pamoja nao wote.
Asili ya muundo huu ni Hadiyth ya Abu Hurayrah ambaye aliulizwa kuhusu Swalaah ya Khofu akajibu: "Nilikuwa na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika vita vile. Nabiy wa Allaah akawagawanya watu makundi mawili. Kundi moja likasimama pamoja naye, na kundi jingine likamwelekea adui nailhali migongo yao imeelekea Qiblah. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akapiga takbiyr na wao wote wakapiga naye takbiyr (walio pamoja naye na waliomwelekea adui). Kisha Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akarukuu rukuu moja, na kundi alilo nalo likarukuu, kisha akasujudu na kundi alilonalo likasujudu huku wale wengine wakiwa wamesimama kuelekeana na adui. Halafu Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisimama na watu wa kundi lililoswali naye wakachukua silaha zao, kisha wakaenda kinyumenyume mpaka wakasimama mbele kukabiliana na adui. Halafu likaja kundi lililokuwa mkabala na adui, wakarukuu na kusujudu nailhali Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kasimama kama alivyo, kisha wakasimama. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akarukuu rakaa nyingine na wao wakarukuu pamoja naye, akasujudu wakasujudu pamoja naye. Halafu likaja kundi lililokuwa limeelekeana na adui, wakarukuu na wakasujudu nailhali Nabiy wa Allaah amekaa pamoja na alio nao. Kisha ikaja tasliym, na Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatoa tasliym, na wote wakatoa tasliym. Watu wakasimama wakiwa wameshiriki wote Swalaah pamoja naye". [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Dawuud (1241), An-Nasaaiy (3/173) na Ahmad (2/320)].
(b) Ikiwa adui yuko upande wa Qiblah
6- Imamu atawagawa vikosi viwili, atahirimia Swalaah pamoja nao wote, atasoma, atarukuu na ataitadili pamoja nao wote. Kisha atasujudu na kikosi kimoja huku kingine kikichunga mpaka atakaposimama imamu toka kwenye sijdah, na hapo kikosi kingine kitasujudu, na baada ya kusujudu, watamfata imamu kwenye kisimamo. Katika rakaa ya pili, imamu atafanya hivyo hivyo lakini watakaolinda mara hii ni wale waliosujudu naye katika rakaa ya kwanza. Halafu atakaa nao tashahhudi na kutoa tasliym pamoja nao wote.
Asili ya muundo huu ni Hadiyth ya Jaabir aliyesema: “Niliswali pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Swalaah ya vitani. Tulijipanga safu mbili: safu moja nyuma ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) huku adui akiwa kati yetu na Qiblah. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akapiga takbiyr ya kuhirimia Swalaah, nasi sote tukapiga. Kisha akanyanyua kichwa chake toka kwenye rukuu, nasi sote tukanyanyuka. Akateremka kwenda sijdah pamoja na safu iliyomfuatia, na safu ya nyuma ikasimama mkabala na adui. Na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomaliza kusujudu na ikasimama safu inayomfuatia, safu ya nyuma iliteremka kwenda sijdah kisha wakasimama. Kisha safu ya nyuma ikaja mbele na ya mbele ikaenda nyuma, Nabiy akarukuu, nasi sote tukarukuu. Halafu akanyanyua kichwa chake toka kwenye rukuu, nasi sote tukanyanyua, akateremka kwenda sijdah pamoja na safu inayomfuatia ambayo ilikuwa nyuma katika rakaa ya kwanza. Kisha safu ya nyuma ikasimama kumwelekea adui, na Nabiy alipomaliza sijdah pamoja na safu inayomfuatia, safu ya nyuma iliteremka kwenda sijdah wakasujudu, halafu Nabiy akatoa tasliym, nasi sote tukatoa tasliym. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (840) na Abu Dawuud (1241)].
Hadiyth mfano wa hii ya Abu ‘Ayyash Az-Zuraqiy iko, nayo ni Hadiyth Swahiyh ambayo imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Dawuud (1236), An-Nasaaiy (3/176), Ahmad (4/59) na wengineo].
[Al-Badaai-’i (1/244), Rawdhwat At-Twaalibiyna (2/60), Al-Mughniy (2/416) na Kash-Shaaful Qinaa (1/18)]
1- Vita vikiumana watu wakashindwa kuswali jamaa kwa miundo iliyotangulia, na wakawa na matarajio ya kutulia hali kabla ya kutoka wakati wa Swalaah, hapo itakuwa vyema kuikawiza.
2- Ikiwa muda utabakia wa kuweza kuswali, wataswali kwa kuashiria lakini kama muda hakuna, kila mmoja ataswali peke yake kiasi awezavyo. Wakiweza kurukuu na kusujudu watafanya, au wanaweza kuswali huku wanatembea kwa miguu au kwenye vipando wakiwa wameelekea Qiblah au bila kuelekea. Hawatalipa Swalaah utulivu unaporejea si kwa wakati uliopo kwao wala kwa ujao.
Asili ya hili ni Neno Lake Ta’alaa:
((فَإِنْ خِفْتُمْ فَرِجَالًا أَوْ رُكْبَانًا ۖ فَإِذَا أَمِنتُمْ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَمَا عَلَّمَكُم مَّا لَمْ تَكُونُوا تَعْلَمُونَ))
((Mkikhofu (swalini) huku mnatembea au mmepanda kipando. Mtakapokuwa katika amani mdhukuruni Allaah kama Alivyokufunzeni yale mliyokuwa hamuyajui)). [Al-Baqarah (2:239)]
Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar akisema: “Ikiwa kizaazaa kitakuwa zaidi ya hapo, basi wataswali kwa kusimama wakitembea au wakiwa kwenye vipando, wameelekea qiblah au bila kuelekea”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (4535), Ibn Maajah (1258) na Maalik (442)].
Al-Bukhaary kaongeza: “Amesema Naafi’i: Simwoni ‘Abdullah bin ‘Umar amelisema hilo isipokuwa toka kwa Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)”.
Wakishindwa kurukuu na kusujudu, basi watazifanya kwa ishara, na ishara ya sijdah itakuwa ya chini zaidi kuliko ya rukuu.
Ninasema: “Rakaa moja itatosheleza, na Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
3- Ikiwa mapambano na adui yatawashughulisha mpaka wakati wa Swalaah ukatoka, basi hakuna ubaya na Swalaah yao wataiswali pale watakapoweza. Ni kama ilivyotokea kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika vita vya Khandaq. Alishughulishwa yeye na Maswahaba zake hadi Swalaah ya Alasiri ikawapita wakaja kuiswali baada ya Magharibi. Hadiyth kuhusiana na hili tumeitaja kwenye mlango wa kulipa Swalaah zilizompita mtu.
Mtu akiwa mjini kwake, akakabiliwa na khofu toka kwa adui dhalimu kafiri, auMuislamu katili, au mafuriko, au moto, au mnyama mkali na kadhalika, basi anaruhusiwa kuswali Swalaah ya Khofu. Hii ni kauli ya Maulamaa wengi kama Abu Haniyfah, Maalik, Ash-Shaafi’iy, Ahmad, Al-Awzaa’iy na Ibn Hazm. [Al-Ummu (1/186), Al-Mudawwanah (1/161), Al-Mughniy (2/302), Twarhu At-Tashriyb (3/141), Naylul Awtwaar (3/377-378) na Al-Muhalla (5/33-43)]
Wanasema ni kutokana na Kauli Yake Ta’alaa:
((وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِن كَانَ بِكُمْ أَذًى مِّن مَّطَرٍ أَوْ كُنتُم مَّرْضَىٰ أَن تَضَعُوا أَسْلِحَتَكُمْ ۖ وَخُذُوا حِذْرَكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ أَعَدَّ لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا ))
((Na wala si dhambi kwenu ikiwa mna maudhiko kutokana na mvua au mkiwa wagonjwa kuweka (chini) silaha zenu. Na mshike hadhari zenu. Hakika Allaah Amewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha)). [An-Nisaa (4:102)]
Na hili halikuhusishwa na safari. [Ila kwa mwenye kusema kwamba makusudio ya Kauli Yake Ta’alaa وإذا ضربتم في الأرض فليس عليكم جناح أن تقصروا من الصلاة ni Swalaah ya Khofu, na si kupunguza Swalaah. Huyo, atajengea kwamba hilo limehusishwa na safari tu]
Ikiwa pataulizwa: Je, Hadiyth zote zilizotangulia zinahusiana na safari tu? Patajibiwa kwamba safari ni wasifu usio na kadiri, hauna sharti wala sababu, na kama si hivyo, basi ingelazimu kwamba asiswali isipokuwa wakati wa kutishiwa na adui kafiri!!
Mtu akiswali Swalaah ya Khofu mjini kwake, basi ataiswali kwa idadi kamili ya rakaa zake kwa muundo wowote kati ya miundo iliyoelezewa, na hii ni kwa imamu na maamuma.
Lakini je, itafaa kuswali rakaa moja mjini kwa mujibu wa Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas isemayo: “Allaah Jalla wa ‘Alaa Aliifaradhisha Swalaah kwa ulimi wa Nabii wenu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam); mjini rakaa nne, safarini rakaa mbili, na kwenye khofu (vita) rakaa moja?” [Hadiyth Swahiyh: Takhriyj yake tumeitaja nyuma kidogo].
Na je, kujuzu kuswali Swalaah ya Khofu kwa kuashiria wakati mambo yanaposhitadi kunaitilia nguvu Hadiyth hii?
Haya ni ya kutafitiwa zaidi. Ibn Hazm kwa mujibu wa mwonekano wa Hadiyth, hakujuzisha kuswali rakaa moja isipokuwa safarini tu. Basi nawe litafiti hili.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
039-Swalaah Ya Jamaa
Alhidaaya.com [3]
Maana ya Swalaah Ya Jamaa ni kuiswali Swalaah pamoja na watu. [Jawaahir Al-Ikliyl (1/76)]
(a) Swalaah ya Jamaa ina fadhla kubwa kabisa, na kwa ajili hiyo, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameihimizia na kubainisha fadhla zake katika Hadiyth mbalimbali. Kati ya hizo ni:
1- Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Swalaah ya Jamaa inaizidi Swalaah ya mtu peke yake kwa daraja ishirini na saba)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (645) na Muslim (650)].
2- Imepokelewa toka kwa Abu Sa’iyd Al-Khudriy akisema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Kuswali kwa Jamaa ni sawa na kuswali Swalaah ishirini na tano. Na anapoiswali kwenye ardhi mahame isokaliwa, akatimiza rukuu yake na sijdah yake, basi zinafikia Swalaah hamsini)). [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (560), Ibn Maajah (788) na Al-Haakim (1/208)].
3- Imepokelewa toka kwa ‘Uthmaan bin ‘Affaan ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Mwenye kutawadha kwa ajili ya Swalaah na akautimiliza wudhuu, kisha akatembea kwenda kwenye Swalaah ya Faradhi, akaiswali pamoja na watu au pamoja na Jamaa au Msikitini, basi Allaah Humghufiria madhambi yake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (232), An-Nasaaiy (2/111) na Ahmad (1/67)].
4- Na katika Hadiyth Marfu’u ya Abu Hurayrah:
((Na hiyo ni kuwa yeye akitawadha vizuri kama inavyotakiwa, kisha akatoka kwenda Msikitini na hakuna kimtoacho isipokuwa Swalaah tu, basi hatokanyaga hatua isipokuwa hunyanyuliwa kwayo daraja moja na hupomoshewa kwayo kosa moja. Na anaposwali, Malaika huendelea kumwombea rahma madhali ataendelea kubakia sehemu aliyoswalia (wakisema): “Ee Mola, Mpe rahma na baraka. Ee Mola, Mrehemu. Na mmoja wenu haachi kuwa ndani ya Swalaah madhali yu katika kuisubiri Swalaah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (647) na Muslim (649)].
5- Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Lau watu wangelijua yaliyomo ndani ya adhana na safu ya kwanza, kisha wasipate njia ya kulipata hilo ila kwa kura, basi wangelipiga kura. Na lau wangelijua yaliyomo ndani ya kuwahi mapema, basi wangelishindana. Na lau wangelijua yaliyomo ndani ya Swalaah ya ‘Ishaa na Alfajiri, basi wangeziendea japo kwa kutambaa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (615) na Muslim (437)].
6- Imepokelewa toka kwa ‘Uthmaan kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Mwenye kuswali ‘Ishaa katika Jamaa, basi ni kama aliyesimama nusu ya usiku, na mwenye kuswali Alfajiri katika Jamaa basi ni kama aliyeswali usiku wote)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (656), Abu Daawuud (555), At-Tirmidhiy (221) na Ahmad (1/58)].
(b) Swalaah ya Jamaa ndiyo maana ya dini na nembo ya Uislamu kiasi ambacho ikiwa watu wa mjini wataiacha, basi watapigwa vita, na watu wa vitongojini watalazimishwa. [Al-Mughniy (2/176) na Al-Majmu’u (4/193)]
Swalaah Ya Jamaa Katika (Swalaah za) Faradhi
Maulamaa wamekhitalifiana kuhusu hukmu ya Swalaah ya Jamaa kwa wanaume kwa kauli nyingi ambazo tunaweza kuzifupisha katika kauli mbili zifuatazo:
Ya kwanza:
Swalaah ya Jamaa ni faradhi kwa kila mtu binafsi isipokuwa kwa udhuru. Kauli hii imesimuliwa toka kwa Ibn Mas-’oud na Abu Muusa. Pia kaisema ‘Atwaa, Al-Awzaa’iy na Abu Thawr. Ni madhehebu ya Ibn Hazm na chaguo la Sheikh wa Uislamu ingawa wamekhitalifiana kati yao kama je Jamaa ni sharti ya kuswihi Swalaah au si sharti? [Al-Mughniy (2/176), Kash-shaaful Qina’a (1/454), Al-Badaai-’i (1/155), Al-Muhalla (4/188), na Majmu’u Al-Fataawaa (23/239)]
Dalili zao ni hizi:
1- Kauli Yake Ta’alaa:
((وَإِذَا كُنتَ فِيهِمْ فَأَقَمْتَ لَهُمُ الصَّلَاةَ فَلْتَقُمْ طَائِفَةٌ مِّنْهُم مَّعَكَ وَلْيَأْخُذُوا أَسْلِحَتَهُمْ فَإِذَا سَجَدُوا فَلْيَكُونُوا مِن وَرَائِكُمْ وَلْتَأْتِ طَائِفَةٌ أُخْرَىٰ لَمْ يُصَلُّوا فَلْيُصَلُّوا مَعَكَ وَلْيَأْخُذُوا حِذْرَهُمْ وَأَسْلِحَتَهُمْ ۗ وَدَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْ تَغْفُلُونَ عَنْ أَسْلِحَتِكُمْ وَأَمْتِعَتِكُمْ فَيَمِيلُونَ عَلَيْكُم مَّيْلَةً وَاحِدَةً ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِن كَانَ بِكُمْ أَذًى مِّن مَّطَرٍ أَوْ كُنتُم مَّرْضَىٰ أَن تَضَعُوا أَسْلِحَتَكُمْ ۖ وَخُذُوا حِذْرَكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ أَعَدَّ لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا))
((Na utapokuwa upo kati yao, ukawaswalisha, basi lisimame kundi miongoni mwao pamoja nawe, na wachukue silaha zao. Watakaposujudu basi wawe nyuma yenu (kuwalinda). Na lije kundi jingine ambalo halikuswali, liswali pamoja nawe, nao washike hadhari na silaha zao. Wale waliokufuru wanatamani kama mtaghafilika na silaha zenu na vifaa vyenu wakuvamieni mvamio mmoja. Na wala si dhambi kwenu ikiwa mna maudhiko kutokana na mvua au mkiwa wagonjwa kuweka (chini) silaha zenu. Na mshike hadhari zenu. Hakika Allaah Amewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha)). [An Nisaa (4:102)]
Wanasema kwamba Allaah Ameamuru kuswaliwe Jamaa katika hali ya vita na khofu, hivyo katika hali ya usalama inakuwa na uzito na ulazima zaidi. Aidha, vitendo vingi vya Swalaah vimesamehewa katika Swalaah ya vita ili Jamaa ipatikane, na kama si kuwa kwake wajibu, basi visingesamehewa.
2- Kauli Yake Ta’alaa:
((وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَارْكَعُوا مَعَ الرَّاكِعِينَ))
((Na simamisheni Swalaah na toeni Zakaat na rukuuni pamoja na wanaorukuu (katika utiifu))). [Al-Baqarah (2:43)]
Na hili linakuwa katika hali ya ushirika na wengine katika rukuu, na hivyo limekuwa agizo la kuswali Swalaah kwa Jamaa, nalo ni agizo wazi la wajibu.
3- Hadiyth ya Abu Hurayrah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Naapa kwa Ambaye nafsi yangu iko Mkononi Mwake! Hakika mimi nilikusudia niamuru zikusanywe kuni ziwashwe moto, halafu niamuru Swalaah iadhiniwe, kisha nimwamuru mtu awaswalishe watu name nitoke niende kwa watu nikawachomee nyumba zao. Naapa kwa Ambaye nafsi yangu iko Mkononi Mwake! Lau kama mmoja wao anajua kwamba atapata kinofu kinono, au vijishale viwili vizuri vya kulengea shabaha, basi hakika angehudhuria ‘Ishaa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (644) na Muslim (651)].
Wanasema kwamba Hadiyth yaonyesha kwamba Jamaa ni Fardhi ‘Ayni ( ya mtu mwenyewe binafsi), kwa kuwa lau kama ingekuwa ni Sunnah, basi anayeiacha asingetishiwa kuchomewa nyumba, na lau kama ingelikuwa ni Fardhi Kifaaya (ya kutoshelezana), basi ingetosha Rasuli kuiswali na watu alionao.
Kutoa dalili kwa Hadiyth hii kwamba Jamaa ni wajibu kwa kila mtu binafsi kumejibiwa kwa njia kadhaa. Kati yake ni kuwa:
- Wakusudiwa hapa ni wanafiki na si Waumini.
- Rasuli alikusudia lakini hakufanya, na kama ingelikuwa ni wajibu basi asingewaacha.
- Makusudio ni Swalaah ya Ijumaa kama ilivyo kwenye riwaya nyingine na kadhalika.
Wenye kusema ni wajibu wamezijibu njia hizi zote kwa majibu marefu ambayo hatuwezi kuyaeleza hapa. Unaweza kuyaangalia kwenye rejea husika. [Angalia Fat-hul Baariy (2/148-151), Ihkaamul Ahkaam cha Ibn Daqiyq Al-‘Iyd (1/166) na Al-Muhalla (4/191)]
4- Hadiyth ya Abu Hurayrah aliyesema: “Mtu mmoja kipofu alimjia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Mimi sina mtu wa kuniongoza kunipeleka Msikitini. Akamtaka idhini Rasuli amruhusu aswalie nyumbani naye akamruhusu. Alipogeuka kuondoka alimwita na kumuuliza: Je unaisikia adhana? Akasema ndio. Akamwambia: Basi ijibu”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (653), An-Nasaaiy (2/109) na wengineo]
5- Hadiyth ya Maalik bin Al-Huwayrith aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alituambia nikiwa nimemjia na kundi la watu wangu:
((Wakati wa Swalaah ukiingia, basi mmoja wenu awaadhinie, na mkubwa wenu awaswalishe)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (631) na Muslim (674)]
6- Hadiyth ya Abud Dardaai ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Hakuna watu watatu katika kijiji au jangwa ambao hawasimamishi Swalaah isipokuwa Shaytwaan huwatawala. Basi shikamana na Jamaa, kwani mbwa mwitu humla kondoo wa mbali)). [Tumeitaja katika mlango wa hukmu ya adhana]
7- Yaliyosimuliwa toka kwa Ibn ‘Abbaas kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Mwenye kusikia adhana kisha asiijibu, basi huyo hana Swalaah isipokuwa kwa udhuru)). [Imetiwa ila kuwa Mawquwf. Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (551), Ibn Maajah (794), Al-Haakim (1/245) na Al-Bayhaqiy (3/57, 174). Yeye katilia nguvu kuwa ni Mawquwf, na hili ndilo Swahiyh. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi]
La sahihi ni kuwa Hadiyth hii ni Mawquwf.
8- Imepokelewa toka kwa ‘Abdullah bin Mas-’oud akisema: “ Hakika hakukuwa na yeyote kati yetu anayebaki nyumbani asiende kuswali isipokuwa mnafiki ambaye unafiki wake ushajulikana au mtu mgonjwa. Ikiwa mtu mgonjwa, hutembea akishikiliwa na watu wawili mpaka akahudhuria Swalaah”. Anasema: “Hakika Rasuli wa Allaah ametufundisha Sunnah za uongofu, na kati ya Sunnah za uongofu ni kuswali kwenye Msikiti unaoadhiniwa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (654), Abu Daawuud (550), An Nasaaiy (2/108) na Ibn Maajah (777) kwa konteksi ndefu zaidi]
Hili limejibiwa: Kwamba hii ni kauli ya Swahaba na haina zaidi ya kuelezea udumifu katika Swalaah ya Jamaa na kutoiacha. Na kauli kama hii haitolewi hoja ya ulazima wa jambo. Isitoshe, kuna dalili katika Hadiyth ya Abu Hurayrah ya kuwa wanaohusishwa na makamio ya kuchomewa nyumba ni wanafiki.
Ya pili: Swalaah ya Jamaa si wajibu kwa kila mtu binafsi. Ni kauli ya Jamhuri; Abu Haniyfah, Maalik na Ash-Shaafi’iy ingawa wamekhitalifiana kati yao kama je Jamaa ni Sunnah tu, au Sunnah Iliyokokotezwa, au ni Fardhi Kifaayah? [Al-Badaai-’i (1/155), Ibn ‘Aabidiyn (1/371), Al-Qawaaniyna (69), Al-Khurashiy (2/16), Al-Majmu’u (4/184) na Mughnil Muhtaaj (1/229)]
Hoja zao ni:
1- Neno la Rasuli Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam:
((Swalaah ya Jamaa inaishinda Swalaah ya mtu peke yake kwa daraja ishirini na saba)) na zingine zenye maana kama hii. Wanasema kwamba uzidiano unaonyesha kwamba Swalaah mbili zinashirikiana katika asili ya ubora na hii inaonyesha kwamba si wajibu kwa kila mtu binafsi. Haisemwi: “Kulifanya la wajibu ni bora kuliko kuliacha”, wala haisemwi: “Tamshi lake “af-‘alu” laweza kuja kuthibitisha sifa ya upande mmoja wa kitu na kuikanusha ya upande mwingine, na “afdwalu” yenye kudhifiwa kwenye Swalaah ya mtu pweke hivyo hivyo. Kwa kuwa hili linaswihi katika “af-‘alu” moja kwa moja bila kukutanishwa na “min”. Na hata baadhi ya matamshi yaliyopo kwa Muslim yanasema: ((Huizidi Swalaah ya kuswali peke yake)), na hili latueleza wazi kwamba inasihi mtu kuswali peke yake. [Twarhu At-Tathriyb cha Al-‘Iraaqiy]
Wa mwanzo wamejibu wakisema kwamba uzidiano ni kwa Swalaah ya mwenye udhuru – kwa kukusanya baina ya dalili -, nayo inakuwa chini ya Swalaah ya Jamaa kwa ubora.
2- Hadiyth ya Yazid bin Al-Aswad kuhusu kisa cha watu wawili walioswali nyumbani walikofikia, wakaenda Msikitini na hawakuswali. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawaambia: ((Msifanye, mkiswali nyumbani kwenu mlikofikia, kisha mkaja kwenye Msikiti wa Jamaa, basi swalini pamoja nao, kwani Jamaa inakuwa ni Sunnah kwenu)). [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa katika mlango wa nyakati marufuku kuswali]
Wanasema: “Rasuli hakuwakanushia kuswali nyumbani kwao walikofikia”.
Limejibiwa: “Hili ni tukio la kibinafsi ambapo inawezekana wakawa na udhuru wa kuacha kuswali Jamaa.
3- Hadiyth ya Abu Muusa aliyesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Watu wenye malipo makubwa zaidi katika Swalaah ni wale wenye kutembea toka mbali kisha wa mbali zaidi. Na yule anayengojea Swalaah mpaka akaswali na imamu ana malipo makubwa zaidi kuliko yule anayeswali kisha akalala)) [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (651) na Muslim (662)]
Na katika tamko la Muslim: “Mpaka aiswali katika Jamaa na imamu”.
Hadiyth iko wazi kwamba anayeswali peke yake na anayeswali Jamaa wanashirikiana katika asili ya malipo.
Ninasema: “Hii ndiyo hoja yao yenye nguvu zaidi kwa mujibu wa mwono wangu”.
4- Hadiyth ya Ibn ‘Umar kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema katika vita vya Khaybar:
((Mwenye kula mti huu –yaani kitunguu saumu- basi asikurubie kabisa Msikiti wetu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (853) na Muslim (561)]….na Hadiyth nyingine zenye maana sawa na hii.
Wamesema: “Hadiyth hii inalazimisha moja ya mawili: Ima iwe kula vitu hivi inaruhusika na Swalaah ya Jamaa iwe si wajibu kwa mtu binafsi yake, au Swalaah ya Jamaa iwe ni wajibu kwa mtu binafsi yake, na mtu asiruhusiwe kula vitu hivi. [Ihkaamul Ahkaami Sharhi ‘Umdatil Ahkaam cha Ibn Daqiyq Al-‘Iyd (1/119)]
Jamhuri wanasema kwamba mtu anaruhusiwa kula vitu hivi na Jamaa inakuwa si wajibu kwake kwa kuwa inajuzu kuiacha kutokana na kula vitu hivi. Lakini wamejibiwa kwamba Jamaa ni wajibu na haitimu ila kwa kuacha kula kitunguu saumu, hivyo ni lazima kuacha kukila wakati wa Swalaah.
5- Inawezekana kutolea dalili kwa Hadiyth ya mtu aliyeswali nyuma ya Mu’aadh aliyerefusha sana kisomo. Mtu yule akajitoa kwenye Swalaah, akaswali peke yake, kisha akaenda kumshtakia kwa Rasuli Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam, na Rasuli hakukipinga kitendo chake cha kuacha Jamaa. [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa katika mlango wa “kukhitalifiana nia ya imamu na maamuma” katika sharti za kuswihi Swalaah]
Hili linajibiwa kwamba kurefusha imamu ni udhuru wa kuacha Jamaa.
Hakuna shaka kwamba kukusanya kati ya Hadiyth zilizotangulia kiasi inavyowezekana ni jambo la lazima. Nukta ambayo Hadiyth hizi zinakutania bila kukiacha chochote –kwa mwono wangu- ni kusema kwamba Swalaah ya Jamaa ni fardhi ya kutoshelezana kama alivyosema Ash-Shaafi’iy Rahimahul Laahu. Hii ndio kauli sahihi yenye uwiano mzuri zaidi. Lakini inatakikana ijulikane kwamba haipotezi Jamaa na kuiatilisha bila ya udhuru, isipokuwa mnyimwa kheri na mkosa bahati.
[Nimeitoa kwenye kitabu changu cha Fiqhu As-Sunna Lin-Nisaai ukurasa wa 146-149 kwa mabadilisho kidogo. Angalia Al-Badaai-’i (1/155), Ash-Sharhu As-Swaghiyr (1/156), Mughnil Muhtaaj (1/229) na Al-Mughniy (2/202)]
Kwa mujibu wa Ijma’a ya Maulamaa, Swalaah ya Jamaa si wajibu kwa wanawake lakini sheria inawaruhusu kuswali Jamaa kwa mujibu wa kauli ya Jamhuri.
Swalaah ya mwanamke katika Jamaa inakuwa kwa aina mbili:
1- Mwanamke aswalishwe na mwanamke mwenzake. Hili linaruhusika kutokana na mambo matatu:
(a) Ujumuishi wa Hadiyth zilizotangulia kuhusiana na fadhila za Swalaah ya Jamaa. Na asili ni kuwa ((Wanawake ni ndugu moja na wanaume)). [Hasan kwa Sanad tofauti. Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (236), At-Tirmidhiy (113) na Ahmad (6/256)]
(b) Hakuna katazo lolote la wanawake kuswalishana wenye.
(c) Kutendwa hilo na baadhi ya Maswahaba wanawake kama Ummu Salamah na ‘Aaishah. Imepokelewa toka kwa Rabtwah Al-Hanafiyyah kwamba ‘Aaishah aliwaswalisha na akasimama kati yao katika Swalaah ya faradhi. [Swahiyh kwa Hadiyth wenza: Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdul Razzaaq (3/141), Ad-daaraqutwniy (1/404) na Al-Bayhaqiy (3/131)]
Na imepokelewa toka kwa ‘Ammaar Ad-Dahniy toka kwa mwanamke katika watu wake aitwaye Hujayrat toka kwa Ummu Salamah kwamba aliwaswalisha akasimama katikati yao. [Swahiyh kwa Hadiyth wenza: Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdul Razzaaq (3/140), Ad-daaraqutwniy (1/405) na Al-Bayhaqiy (3/131)]
Kutokuwepo mpingaji wa kitendo hiki cha Maswahaba hawa akina mama, kunaonyesha kwamba inajuzu kisheria mwanamke kuwa imamu wa wenzake. Imepokelewa kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliamuru Ummu Waraqah aweke mwadhini wa kumwadhinia, na akamwamuru awaswalishe watu wa nyumbani kwake. [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (592), Ibn Khuzaymah (3/89), Al-Bayhaqiy (3/130) na Ad-daaraqutwniy (1/403)]
Hadiyth hii ni Dhwa’iyf, na haya ndiyo waliyoyasema Mashafii na Mahanbali.
2- Mwanamke aswalishwe na mwanamume. Ni sawa akiswalishwa peke yake, au pamoja na wanawake wenzake, au nyuma ya Jamaa ya wanaume. Haya yanajuzu kutokana na Hadiyth nyingi. Kati ya hizo ni:
- Hadiyth ya Anas aliyesema: “Niliswali mimi pamoja na yatima katika nyumba yetu nyuma ya Rasuli Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam, na mama yangu –Ummu Salamah- akiwa nyuma yetu”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (727) na Muslim (658)]
- Hadiyth ya Ummu Salamah aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapotoa tasliym, wanawake husimama anapomaliza tasliym yake, naye hukaa kidogo mahala pake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (870), Abu Daawuud (1040), An-Nasaaiy (2/66) na Ibn Maajah (932)]
1- Mtu anaweza kuswali Jamaa yeye na mke tu faraghani au na yeyote katika maharimu zake, kwa kuwa inajuzu kukaa naye faraghani kwingineko kokote.
2- Haijuzu mwanamume kumswalisha mwanamke ajnabiya peke yake kutokana na ujumuishi wa kauli yake Rasuli Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam: ((Asikae kabisa mwanamume na mwanamke faraghani, kwani watatu wao ni shaytwaan)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (1171) na Ahmad (172)]
3- Mwanamume anaweza kuliswalisha kundi la akina mama, kwa kuwa wingi wao huondosha ufaragha, hakuna katazo lililoripotiwa, na baadhi ya Masalaf wameripotiwa kulitenda hilo. Lakini hili litafanyika ikiwa patasalimika na fitna, na kama fitna ipo, basi haijuzu, kwani Allaah Hapendi ufisadi.
Hukumu zaidi kuhusiana na Swalaah ya Jamaa ya akina mama zitakuja kuelezewa mbeleni Insha-Allaah.
Mafuqahaa wamekubaliana kwamba uchache wa idadi ya kufanyika Jamaa ni watu wawili, yaani imamu na maamuma. Kwa hawa wawili, fadhila ya Jamaa hupatikana. Na hii ni kwa Hadiyth zifuatazo:
1- Hadiyth ya Maalik bin Al-Huwayrath aliyesema: “Watu wawili walimjia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakitaka kusafiri. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawaambia: ((Ikiwa mmeshatoka, basi adhinini, kisha kimuni Swalaah, halafu awaswalisheni mkubwa wenu zaidi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (630) na Muslim (674)]
2- Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas kuhusiana na kisa cha kulala kwake pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa khalati yake Maymounah isemayo: “Akasimama kuswali, nami nikatawadha kiasi alivyotawadha yeye, kisha nikaja na kusimama kushotoni kwake, akanigeuza na kunileta kuliani kwake. Halafu aliswali rakaa nyingi, kisha akalala kwa ubavu”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (138) na Muslim (763)]
3- Imepokelewa toka kwa Abu Sa’iyd Al-Khudriy kwamba mtu mmoja alikuja baada ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kumaliza kuswali. Rasuli akasema: ((Nani atamtolea swadaqah huyu?)) Mtu mmoja akasimama na kuswali naye. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (574), At-Tirmidhiy (220), Ad-daaramiy (1368) na Ahmad (10980)]
4-Tumeeleza kwenye mlango wa Swalaah ya usiku namna Ibn Mas-’oud na Hudhayfah walivyoswali na Rasuli Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam.
Kisha Maulamaa wamekhitalifiana kama Jamaa inapatikana katika Swalaah ya faradhi ikiwa kuna imamu na kijana mdogo mpambanuzi. La sahihi ni kwamba Jamaa inapatikana kutokana na Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas. Isitoshe, hakuna dalili ya kufarikisha kati ya Swalaah ya Sunnah na ya faradhi katika hilo, na mtoto mdogo mpambanuzi anaweza kuwa imamu ikiwa anaswali Sunnah kama itakavyokuja. Hivyo inajuzu mtoto kuwa maamuma wa mswaliji faradhi aliyebaleghe. Haya ni madhehebu ya Hanafi na Ash-Shaafi’iy na riwaya toka kwa Ahmad. [Al-Badaai-’i (1/156), Mughnil Muhtaaj (1/229) na Al-Mughniy (2/178). Angalia Haashiyat Ad-Dusuwqiy (1/319) na Jawaahir Al-Ikliyl (1/76). Wamaalik wametofautisha kati ya faradhi na Sunnah!! Na Hadiyth iliyotangulia ya Abu Sa’iyd ni hoja dhidi yao]
Swalaah ya Jamaa inaweza kuswaliwa mahala popote palipo twahara; nyumbani, jangwani au Msikitini. Ni kwa neno lake Rasuli Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam:
((Ardhi imefanywa kwangu ni sehemu ya kuswalia na kujitwaharishia. Na mtu yeyote katika umma wangu ambaye Swalaah imemwadilia, basi aswali)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (335) na Muslim (521) kutoka Hadiyth ya Jaabir]
Na neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwaambia watu wawili: ((Mkiswali nyumbani kwenu mlikofikia, kisha mkaja kwenye Msikiti wa Jamaa, basi swalini pamoja nao, kwani Jamaa inakuwa ni Sunnah kwenu)). [Hadiyth Swahiyh: Takhriyj yake imeshatajwa]
Isipokuwa kuswali Swalaah za faradhi kwa Jamaa Msikitini inakuwa ni bora zaidi kuliko sehemu nyingine. Ni kwa Hadiyth ya Zayd bin Thaabit ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Swalini enyi watu majumbani mwenu, kwani bora ya Swalaah ni mtu kuswali nyumbani kwake isipokuwa Swalaah ya faradhi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (731) na Muslim (781)]
Kuongezea na hilo ni kuwa kuswaliwa Msikitini huiongezea nguvu nembo ya Swalaah, hudhihirisha wingi wa Waislamu, na mtu hupata thawabu za kukanyaga hatua kwenda Msikitini.
Kuna nyudhuru jumuiya na nyudhuru binafsi zinazoruhusu kutohudhuria Jamaa Msikitini. Ubainisho wa hili ni kama ifuatavyo:
(a) Nyudhuru jumuiya
1,2- Mvua na tope zinazomletea mtu uzito wa kutoka kwenda Msikitini
Imepokelewa toka kwa Naafi’i kwamba Ibn ‘Umar aliadhini kwa ajili ya Swalaah katika usiku wenye baridi na upepo kisha akasema: “Swalini majumbani”. Kisha akasema: “Ikiwa usiku ni wa baridi na mvua, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akimwamuru mwadhini aseme: “ Swalini majumbani”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (666) na Muslim (697)]
Imepokelewa toka kwa Jaabir akisema: “Tulitoka pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika safari, mvua ikatunyeshea na akasema: ((Aswali atakaye kati yenu kwenye hema yake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (698), Abu Daawuud (1065) na At-Tirmidhiy (409)]
Lakini kama atatoka kwenda kwenye Jamaa, basi itakuwa ni bora zaidi kutokana na Hadiyth ya Abu Sa’iyd Al-Khudriy aliyesema: “Lilikuja wingu na mvua ikanyesha mpaka dari likavuja (lilikuwa ni la majani ya mtende). Swalaah ikaqimiwa, nami nikamwona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisujudu kwenye maji na tope na nikaona athari ya tope kwenye paji lake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (669) na Muslim (1167)]
Hakika Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alihudhuria Jamaa ingawa mvua ilikuwepo na tope na akasujudu juu yake.
3- Baridi kali
Ni ile inayopita kiwango kilichozoeleka kwa watu. Hadiyth ya Ibn ‘Umar inayogusia hili tushaielezea nyuma takriban.
Imepokelewa toka kwa Na’iym An-Nahhaam kwamba iliadhiniwa Alfajiri katika siku ya baridi naye akiwa katika guo la mke akasema: “Laiti mwadhini angelinadi: Na mwenye kukaa, basi hana makosa”. Na hapo mwadhini wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akanadi mwishoni mwa adhana yake: Na mwenye kukaa, basi hana makosa”. Na hii ni katika enzi ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika adhana za mwisho mwisho. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (4/220), ‘Abdul Razzaaq (1927) na Al-Bayhaqiy (1/398)]
Zaidi ya nyudhuru hizi, Maulamaa wameongezea udhuru wa kiza kinene ambapo mtu anakuwa hawezi kuiona njia yake kuelekea Msikitini.
An-Nawawiy kasema: “Masahibu zetu wamesema: Jamaa hupomoka kwa nyudhuru sawasawa tukisema kwamba ni Sunnah, au Fardhi Kifaayah, au Fardhi ‘Ayn. Kwa kuwa, hata sisi tukisema kwamba ni Sunnah, basi inakuwa ni kokotezwa na ni karaha kuiacha kama ilivyobainika nyuma. Na kama ataiacha kwa udhuru, basi ukaraha utaondoka, na hii haimaanishi kwamba kama ataiacha Jamaa kwa udhuru atazipata fadhila zake, bali bila shaka fadhila hizo hazipati. Maana yake inakuwa ni kupomoka madhambi na ukaraha”. [Al-Majmu’u cha An-Nawawiy]
(b) Nyudhuru binafsi
4- Ugonjwa
Ni ule wenye kumpa mtu uzito wa kuweza kwenda Msikitini kwa ajili ya Jamaa. Ibn Al-Mundhir kasema: “Siyajui makhitalifiano yoyote kati ya Maulamaa kuhusu kutokwenda mgonjwa kwenye Jamaa kutokana na ugonjwa, na kwa vile Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipougua, hakwenda Msikitini na akasema: ((Mwamrisheni Abu Bakri aswalishe watu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (664) na Muslim (418)]
Na ikiwa ugonjwa ni mdogo usioleta tabu kama kuuma gego, maumivu kidogo ya kichwa au homa ya mbali, basi huo si udhuru. Kidhibiti ni uzito unaompata mgonjwa mithili ya uzito wa kutembea kwenye mvua”. [Al-Majmu’u cha An-Nawawiy (4/205)]
Na kama atapiga moyo konde, akaenda Msikitini na ugonjwa wake kama ataweza, basi ni bora zaidi. Imepokelewa toka kwa Ibn Mas-’oud akisema: “Hakika hakukuwa na yeyote kati yetu anayebaki nyumbani asiende kuswali isipokuwa mnafiki ambaye unafiki wake ushathibiti au mtu mgonjwa. Ikiwa mtu mgonjwa, hutembea akishikiliwa na watu wawili mpaka akahudhuria Swalaah”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (654) na wengineo, nasi tushaitaja]
5- Ila kama upofu na mfano wake
Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimruhusu Thawbaan bin Maalik aswalie nyumbani kwake wakati alipomwambia: “Ee Rasuli wa Allaah! Macho yangu hayaoni, na mimi ninawaswalisha watu wangu. Mvua inaponyesha, bonde linalotenganisha kati yangu na wao hufurika nami nashindwa kwenda Msikiti wao, nikabaki kuwaswalisha watu wangu”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (425) na Muslim (33)]
Huyu, ana nyudhuru mbili kwa pamoja; upofu na mvua. Na katika tamshi la Hadiyth ya Anas: “Mtu mmoja katika Answar aliniambia: Mimi siwezi kuswali nawe. Alikuwa ni pandikizi la mtu”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (670) na Abu Daawuud (657)]
Baadhi ya Maulamaa wanauchukulia upandikizi wa mtu na utipwatipwa kama ni udhuru. Na hata kipofu, kama hakupata wa kumwongoza kwenda naye Msikitini, huo unakuwa ni udhuru kwake wa kutohudhuria Jamaa kwa mujibu wa Jamhuri. Lakini Mahanafi wanampa udhuru kwa hali yoyote hata kama ana mtu wa kumpeleka Msikitini. [Ibn ‘Aabidiyn (1/373), Ad-Dusuwqiy (1/391) na Kash-Shaaful Qina’a (1/497)]
6- Khofu
Ni kama mtu kujikhofia kutokana na mtawala, dhalimu, adui, mwizi na kadhalika. Au hata kuyaogopea mali yake, au mke wake, au wale alio na jukumu la kuwalinda. Hili ni katika udhuru wa kutohudhuria Jamaa kwa Maulamaa ingawa wamekhitalifiana katika baadhi ya vipengele. [Ibn ‘Aabidiyn (1/374), Mughnil Muhtaaj (1/235) na Al-Mughniy (1/631)]
Na mhimili wa haya ni Hadiyth Marfu’u toka kwa Ibn ‘Abbaas isemayo:
((Mwenye kusikia adhana, kisha asizuiliwe na udhuru wowote kuiendea –Wakauliza: Ni upi udhuru Ee Rasuli wa Allaah? Akasema: Ni khofu au ugonjwa- basi Swalaah yake aliyoiswali haitokubaliwa)). [Hadiyth Dhwa’iyf: Takhriyj yake imeshatangulia katika mlango wa hukmu ya Swalaah ya Jamaa]
Tumeshaeleza kwamba Hadiyth hii si Swahiyh.
7- Kutengwa chakula kwa mwenye njaa
Imepokelewa toka kwa Naafi’i toka kwa Ibn ‘Umar akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Akitengewa mmoja wenu mlo wa usiku na Swalaah ikaqimiwa, basi anzeni na chakula. Asiharakie mpaka amalize kula)). Ibn ‘Umar alikuwa akitengewa chakula na Swalaah inaqimiwa. Haendi kuswali mpaka amalize kula huku akikisikia kisomo cha imamu. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (673) na Muslim (559)]
Jamhuri ya Maulamaa wamelichukulia neno lake: “basi anzeni na chakula” kama ni Sunnah, kisha wakakhitalifiana. Kuna wanaolihusisha hilo na aliyebanwa na njaa, na hili ni mashuhuri kwa Ash-Shaafi’iy. Wengine kama Ath-Thawriy, Ahmad na Is-Haaq hawalihusishi na njaa bali wanalijengea juu ya kitendo cha Ibn ‘Umar. Ibn Hazm kapetuka hayo akisema kwamba akiswali kisha akaja kula, basi Swalaah yake ni batili!! Wengine wanaona ni bora kuanza na Swalaah kwa yule ambaye hana hamu sana ya kula, na hili limenukuliwa toka kwa Maalik na Maswahibu zake wakisema: “Kama ataharakia kula kisha akaswali, basi ni Sunnah kuiswali tena!!” [Fat-hul Baariy (2/188) kwa mabadilisho kidogo]
Ninasema: “Ama kusuniwa kuiswali tena, hili halina dalili. Ama kutanguliza kula kabla ya Swalaah kuwa ni Sunnah na si wajibu, dalili yake ni Hadiyth ya ‘Amri bin ‘Umayyah aliyesema: “ Nilimwona Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akila paja la mbuzi kwa kukata vinofu, akaitwa kwenye Swalaah, akasimama na kukitupa kisu. Akaswali na wala hakutawadha”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (675) na Muslim (355)]
8- Kubanwa na haja ndogo au kubwa
Ni kwa Hadiyth ya ‘Aaishah aliyesema: “Nimemsikia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
((Msiswali chakula kikiwa tayari, au mtu akibanwa na haja ndogo au kubwa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (560), Abu Daawuud (89) na Ahmad (6/43)]
Imepokelewa toka kwa ‘Abdullah bin Al-Arqam ya kwamba alitoka kwenda kuhiji au kufanya ‘Umrah akiwa pamoja na watu, na alikuwa akiwaswalisha. Na siku moja, aliqimu Swalaah –Swalaah ya Alfajiri- kisha akasema: “Mmoja wenu atangulie –naye akaenda msalani- kwani nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “
((Akitaka mmoja wenu kwenda msalani na Swalaah ikaqimiwa, basi aende kwanza msalani)). [Swahiyh kwa Sanad tofauti: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (88), An-Nasaaiy (2/110), At-Tirmidhiy (142), Ibn Maajah (616) na wengineo]
Kubanwa na haja ndogo au kubwa ni nyudhuru mbili ambazo kila moja hupomosha Jamaa kwa makubaliano ya Maulamaa wote kutokana na dalili zilizotangulia. Kwa kuwa mtu akiswali huku amebanwa na moja kati ya haja mbili, basi anakuwa mbali na khushuu ya Swalaah, na anakuwa haizingatii tena Swalaah yake.
9- Kula kitunguu maji, kitunguu saumu, “shallots” na mfano wake kama harufu yake itabakia
Huu ni udhuru wa kutokwenda kwenye Jamaa ili watu na Malaika wasiudhike. Imepokelewa toka kwa Jaabir kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Mwenye kula kitunguu saumu hichi))-, Akasema mara nyingine: ((Mwenye kula kitunguu maji, kitunguu saumu na “shallots”- basi asiukaribie kabisa Msikiti wetu, kwani Malaika wanaudhika na yale yanayowaudhi wanadamu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (854) na Muslim (564) na tamko ni lake]
Makusudio hapa ni kuvila vitu hivi vikiwa vibichi. Kama vikipikwa akavila, basi hakuna ubaya kwani sababu ya kukerwa na harufu inakuwa haipo. Imepokelewa toka kwa ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu Anhu) akisema juu ya mimbar: “ Kisha nyinyi enyi watu mnakula mimea miwili, siioni isipokuwa ni mibaya; kitunguu hiki na kitunguu saumu. Mimi nimemwona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anapomkuta mtu ana harufu yake Msikitini, humwamuru atoke kwenda Al-Baqiy’i. Mwenye kuvila, basi avile vikiwa vimepikwa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (567) na An-Nasaaiy (2/43) kwa ufupi]
Maulamaa wamemjumuisha kwenye udhuru huu mtu mwenye kufanya kazi yenye harufu mbaya kama mchinjaji na muuza nyama, muuza mafuta na kadhalika. Pia mtu mwenye maradhi ya kuwakera watu kama ukoma na mbalanga. [Ad-Dusuwqiy (1/389), Mughnil Muhtaaj (1/236) na Kash-Shaaful Qina’a (1/497)]
Ninasema: “Wenye kustahiki zaidi kuingizwa kwenye orodha hii ni wavutaji sigara ambao wamekuwa wengi hivi leo. Watu hukerwa nao zaidi kuliko wanavyokereka na mlaji kitunguu na kitunguu saumu. Hii ni pamoja na kwamba asili ya kitunguu na kitunguu saumu ni halali kinyume na uvutaji sigara. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
Jingine waliloliongezea Maulamaa katika nyudhuru za kutokwenda kwenye Jamaa ni kutopata nguo ya kujisitiri uchi, bali Ash-Shaafi’iy na baadhi ya Mahanafi wanasema kwamba ikiwa ana nguo yenye hadhi sawa na wenzake atakwenda kwenye Jamaa, na kama hana basi asitoke. [[Ad-Dusuwqiy (1/380), Mughnil Muhtaaj (1/236) na Kash-Shaaful Qina’a (1/496)]
Mafuqahaa wa Kishafii na Kihanbali wanaona kwamba bi harusi kupelekwa kwa mume ni udhuru unaomruhusu mume kubakia awe na mke, na asitoke kwenda Jamaa kwa muda wa siku saba ikiwa mke ni bikra, na siku tatu ikiwa mke mkuu!! Mashafii wamelihusisha hili la kutokwenda Jamaa na Swalaah za usiku tu!! [Mughnil Muhtaaj (1/236) na Kash-Shaaful Qina’a (1/497)]
Ninasema: “Hili ni kosa, alilolielezea Ash-Shaafi’iy ni ukaraha. Na kiini cha kosa hili ni kutoifahamu vizuri Hadiyth ya Anas. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Ni Sunnah ikiwa mtu atamwolea mke mkuu bikra, akae kwa bikra siku saba, kisha agawe siku. Na akimwolea bikra mke mkuu, akae kwa mke mkuu siku tatu, kisha agawe siku)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (5214) na Muslim (1461)]
Maana ya Hadiyth hii ni wazi kwamba kama mtu ana mke mkuu akaoa bikra, basi atalala kwa bikra siku saba, kisha atazigawa siku kwa wakeze kwa usawa, na hakuna hapa kinachopinga kwamba asitoke kwenda kuswali. Pia, kama ana mke bikra akao mke mkuu, atakaa kwa mke mkuu siku tatu.
Linalobainisha kwa uwazi zaidi kwamba haya ndiyo makusudio ya kukaa ni kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomwoa Ummu Salamah, alikaa kwake siku tatu na akasema:
((Watu wako hawatapata madhaliliko kwa sababu yako, ukitaka nitalala kwako siku saba, na nikilala kwako siku saba, nitalala pia siku saba kwa wake zangu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (1460), Abu Daawuud (2122), Ibn Maajah (1917) na Maalik (1123)]
1- Kuacha kazi wakati wa Swalaah unapoingia
Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa ni mwenye kuwahudumia wakeze, na wakati wa Swalaah unapoingia hutoka kwenda kuswali”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (676), At-Tirmidhiy (2489) na Ahmad (6/49)]
2,3- Kutawadha nyumbani, kwenda kwa miguu Msikitini, na kukithirisha hatua na kuzihesabu
Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Mwenye kujitwaharisha nyumbani kwake, kisha akatembea kwa miguu kwenda katika nyumba kati ya Nyumba za Allaah ili kutekeleza faradhi kati ya Faradhi za Allaah, basi hatua zake mbili zinakuwa; moja yao inapomosha dhambi na nyingine inanyanyua daraja)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (666)]
Na imepokelewa toka kwa Abu Musa Al-Ash’ariyy ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Mtu mwenye malipo makubwa zaidi katika Swalaah, ni yule anayetembea toka mbali, kisha wa mbali zaidi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (651) na Muslim (662)]
Na imepokelewa toka kwa Anas akisema: “Banu Salamah walitaka wahamie kwenye Msikiti wa karibu zaidi, na Rasuli wa Allaah hakupenda mji kubaki mahame bila watu akasema:
((Enyi Banu Salamah! Je, hamzihesabu hatua zenu?)). Wakabakia [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1887), Ibn Maajah (784) na Ahmad (3/106)]
Na katika tamshi la Hadiyth ya Jaabir: “Akatukataza akisema:
((Hakika nyinyi mnapata kila hatua daraja)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (664) na Ahmad (3/336)]
Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Je, niwaonyesheni jambo ambalo Allaah Hufuta kwalo makosa na Hunyanyua kwalo daraja?)) Wakasema: “Tuonyeshe Ee Rasuli wa Allaah. Akasema: ((Kuutimiliza wudhuu pamoja na ukali wa baridi na maumivu ya viungo, kukithirisha hatua kwenda Msikitini, na kusubiri Swalaah baada ya Swalaah, basi hayo ndiyo ya kuazimiwa kweli)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (251), At-Tirmidhiy (51), An-Nasaaiy (1/89) na Ahmad (2/235)]
Imepokelewa kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Mwenye kwenda Msikitini mwanzo wa mchana au mwisho wa usiku, Allaah Humwandalia mashukio Peponi kila anapokwenda mwanzo wa mchana au mwisho wa usiku)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (662) na Muslim (669)]
4- Kuharakia kwenda Msikitini na kuiwahi Swalaah
Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah akisema kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Na lau wangelijua yaliyomo katika kuiwahi Swalaah, basi wangelishindana. Na lau wangelijua yaliyomo kwenye Swalaah ya ‘Ishaa na Alfajiri, basi wangeziendea japo kwa kutambaa. Na lau wangelijua yaliyomo kwenye safu ya kwanza, basi wangelipiga kura)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (720) na Muslim (437)]
Na imepokelewa kutoka kwake vile vile akisema kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
((Na anapoingia Msikitini, anakuwa ndani ya Swalaah madhali Swalaah ndiyo inayomzuia)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (477) na Muslim (649) kwa ufupi]
5- Kwenda Msikitini kwa miguu na kwa utulivu bila haraka
Imepokelewa toka kwa Abu Qataadah akisema: “Tulipokuwa tukiswali pamoja na Rasuli Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam, mara ghafla alisikia zogo la watu. Alipomaliza kuswali aliuliza: Mna nini? Wakasema: Tumekimbilia Swalaah. Akawaambia: ((Msifanye. Mnapokuja kwenye Swalaah kuweni watulivu, mnachokipata kiswalini, na mnachokikosa kikamilisheni)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (635) na Muslim (603)]
Imepokelewa toka kwa Abu Hurayra kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Mnapoisikia adhana, basi nendeni kwa miguu katika Swalaah. Jipambeni kwa utulivu na umakini, na wala msifanye haraka. Mnachokipata kiswalini, na mnachokikosa kikamilisheni)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (636) na Muslim (602)]
6- Kusoma adhkaar zilizothibiti wakati wa kutoka na kuingia Msikitini
Atasema anapotoka: “Ee Mola! Nijaalie nuru katika moyo wangu, na nuru katika ulimi wangu, na Ujaalie nuru katika masikio yangu, na Unijaalie nuru katika macho yangu, na Unijaalie nuru nyuma yangu na nuru mbele yangu, na Ujaalie nuru juu yangu na nuru chini yangu. Ee Mola Nipe nuru”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (6316) na Muslim (763)]
Na atasema wakati anapoingia kwa mguu wake wa kulia: “Bismillaah. Ee Allaah Mrehemu Muhammad”. [Hadiyth Hasan Lighayrih: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abus Sunniy (88). Ina Hadiyth wenza na angalia Swahiyh Al-Kalim At-Twayyib (63)]
Na “Ee Allaah! Nifungulie milango ya Rehma Yako”.
7- Kutoshikanisha vidole akiwa Msikitini isipokuwa kwa haja
Kwa kuwa mtu anakuwa ndani ya hukmu ya Swalaah madhali amekaa akiisubiri Swalaah, na mwenye kuswali haijuzu kwake kushikanisha vidole kama ilivyotangulia katika mlango wa mambo yaliyokirihishwa katika Swalaah. Maana ya hili tunaipata katika Hadiyth ya Abu Hurayrah ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Akitawadha mmoja wenu nyumbani kwake kisha akaenda Msikitini, basi anakuwa ndani ya Swalaah mpaka arejee. Basi na asifanye hivi, na akashikanisha baina ya vidole vyake)). [Hadiyth Hasan kwa Sanad tofauti: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Haakim (1/206). Ina Hadiyth wenza kwa Ahmad (3/42), Ad-daaramiy (1406) Ibn Khuzaymah (439) na wengineo]
Hadiyth hii ina mvutano, na kuifanya Hasan kuna nguvu zaidi.
Ama Hadiyth ya ‘Abdullah bin ‘Amri iliyoelezewa na Al-Bukhaariy kwa anwani isemayo: “Kushikanisha vidole Msikitini na kwingineko” isemayo kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ee ‘Abdullah bin ‘Amri! Utafanya nini ukibakia baina ya watu wasio na kheri, na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akashikanisha kati ya vidole vyake)) [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (466), Abu Daawuud (4342) na Ibn Maajah (3957)]…. na mfano wake, ni kuwa uhakiki unasema kwamba hakuna mgongano kati ya Hadiyth mbili, kwa kuwa linalokatazwa ni kufanya hilo kwa njia ya mchezo. Makusudio ya yaliyomo ndani ya Hadiyth ni kuiga na kutoa taswira ya maana katika nafsi kwa picha ya hisia. Au yawezekana kusema: “Katazo limehusishwa tu na mtu anapokuwa ndani ya Swalaah, au anapokuwa anaisubiri kwa kuwa hapo anahukumiwa kuwa yuko kwenye Swalaah. Na Hadiyth ya Ibn ‘Amri na mfano wake hazina hayo. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi. [Angalia Fat-hul Baariy (1/566) chapa ya Al-Ma-’arifah]
8- Kuswali rakaa mbili za maamkizi ya Msikiti
Hili lishazungumzwa kirefu katika mlango wa Swalaah za Sunnah.
9- Kutoswali Sunnah Swalaah inapoqimiwa
Ni kwa Hadiyth ya Abu Hurayrah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Swalaah inapoqimiwa, hapana Swalaah ila ya faradhi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (710), Abu Daawuud (1266), An-Nasaiy (2/116), At-Tirmidhiy (421) na Ibn Maajah (1151)]
Imepokelewa toka kwa ‘Abdullah bin Bahiynah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwona mtu anaswali rakaa mbili baada ya Swalaah kuqimiwa. Rasuli alipomaliza Swalaah, watu walimzonga mtu yule, na Rasuli akamwambia: ((Je, Asubuhi ni rakaa nne? Je, Asubuhi ni rakaa nne?)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (663-711), An-Nasaaiy (2/117) na Ibn Maajah (1153)]
Katika tamshi jingine: ((Mmoja wenu anakurubia kuswali Alfajiri rakaa nne)).
Na kama atahirimia Swalaah ya Sunnah kabla ya iqaama, kisha ikaqimiwa naye yuko ndani ya Swalaah, basi kauli adilifu zaidi ni kusema: Akijua kuwa ataimaliza Swalaah kabla imamu hajahirimia, basi ataikamilisha, na kama si hivyo, basi ataivunja kutokana na Hadiyth hii. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi. [Angalia madhehebu ya Maulamaa: Ibn ‘Aabidiyn (1/479), Jawaahir Al-Ikliyl (1/77), Mughnil Muhtaaj (1/252) na Al-Mughniy (1/456)]
(10) Kutotoka Msikitini baada ya kuadhiniwa na kabla ya Swalaah ya faradhi isipokuwa kwa dharura
Imepokelewa toka kwa Abu Ash-Sha’athai akisema: “Tulikuwa tumekaa Msikitini pamoja na Abu Hurayrah. Mwadhini akaadhini, na mtu mmoja akasimama akaanza kutoka Msikitini. Abu Hurayrah akamwandama kwa jicho mpaka akatoka nje, kisha akasema: “Ama huyu, bila shaka amemwasi Abal Qaasim Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (655), Abu Daawuud (536), An-Nasaaiy (2/29), At-Tirmidhiy (204) na Ibn Maajah (733)]
Kama kuna dharura inayoshurutisha mtu kutoka, basi hakuna ubaya. Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka baada ya Swalaah kuqimiwa na watu kunyoosha safu. Alikuwa ashasimama sehemu yake ya kuswalia, na tulipokuwa tunasubiri apige takbiyr, aliondoka na kutuambia: Bakini kama mlivyo. Tukabakia kama tulivyo mpaka akatutokea tena huku kichwa chake kikitona maji. Alikuwa kaoga”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (639) na Muslim (605)]
11-Asisimame mtu -Swalaah inapoqimiwa- ila baada ya kumwona imamu
Imepokelewa toka kwa Abu Qatadah akisema kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Inapoqimiwa Swalaah msisimame mpaka mnione)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (637) na Muslim (604)]
Fiqh ya suala hili ishaelezwa kwenye mlango wa adhana.
12- Kumwomba ruksa mume ya kwenda Msikitini na mume asimkatalie
Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
((Mke akimwomba ruksa mmoja wenu ya kwenda Msikitini, basi asimzuie)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (5238) na Muslim (442)]
Kasema tena Ibn ‘Umar: “Mke wa ‘Umar alikuwa anahudhuria Jamaa ya Swalaah ya Alfajiri na ‘Ishaa Msikitini. Akaulizwa: Kwa nini unatoka nawe wajua kwamba ‘Umar anachukia hilo na analifanyia wivu? Akasema: Kipi kinamzuia anikataze? Akasema: Kinachomzuia asinikataze ni Kauli ya Rasuli wa Allaah Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam: ((Msiwazuie vijakazi wa Allaah na Misikiti ya Allaah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (900), Muslim (442) kwa ufupi na wengineo]
Ruksa hii wanayopewa wake na waume zao ya kwenda Msikitini ni wajibu kwa wanaume kuitoa kutokana na katazo la wazi la kuwazuia, ikiwa hakuna visababisho vya fitna kama kujishaua, kujitia manukato na kujipodoa. Kama lipo lolote katika hivyo, si lazima kuwapa ruksa na inakuwa ni haramu kutoka. [Jaami’u Ahkaamin Nisaa cha Sheikh wetu (1/279)]
Inaweza kusemwa: Ruksa iliyotajwa si ya wajibu, kwa kuwa lau ingelikuwa ni wajibu, basi maana ya kuomba ruksa isingelikuwepo kwa kuwa ruksa haipatikani ila atakapokuwa mwenye kuombwa ruksa ni mwenye kuchaguzwa katika kukubali au kukataa. [Fat-hul Baariy (2/404) chapa ya As-Salafiyyah] Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
13- Wajiweke mbali na manukato, kujipamba na mambo yote ya kufitinisha
Imepokelewa toka kwa Zaynab mke wa ‘Abdullah bin Mas-’oud akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alituambia:
((Akienda mmoja wenu Msikitini, basi asiguse manukato)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (443) na An-Nasaaiy katika Al-Kubraa (9425)]
Na imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
((Msiwazuie vijakazi wa Allaah na Misikiti ya Allaah. Na watoke bila kujitia chochote)). [Hadiyth Swahiyh Lighayrih: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (2/438) na Abu Daawuud (565)]
14- Wasichanganyike na wanaume wakati wa kuingia au kutoka Msikitini
Kwa ajili ya sababu hii, wanawake katika enzi ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) walikuwa wakiharakia kutoka baada ya kumalizika Swalaah. Ummu Salamah amesema: “Rasuli wa Allaah alipokuwa anatoa tasliym, wanawake husimama wakati anapoimalizia tasliym yake, na yeye hukaa sehemu yake kidogo kabla hajasimama. Tunaona -na Allaah Anajua zaidi- kwamba kufanya hivyo ni ili wanawake wapate nafasi ya kutoka kabla mwanamume yeyote hajawakuta”.
[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (870)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
040-Uimamu Na Hukmu Zake
Alhidaaya.com [3]
· Fadhla Ya Uimamu
Imepokelewa toka kwa Jaabir akisema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
((Halitaacha kundi katika Umma wangu kuwa linaipigania haki na likiwashinda maadui mpaka kukurubia Siku ya Qiyaamah. Anasema: Atateremka ‘Iysaa bin Maryam (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam), na Amiri wao atasema: Njoo utuswalishe, naye atasema: Hapana, hakika nyinyi kwa nyinyi ni Maamiri. Ni Takrima ya Allaah kwa Umma huu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (156) na Ahmad (3/384)].
· Nani Anastahiki Zaidi Uimamu? Je, Ni Mweledi Zaidi Wa Kusoma Au Mtaalamu Aliyebobea Taaluma Ya Dini?
Maulamaa wana mielekeo miwili kuhusiana na suala hili: [Al-Mabsuutw (1/41), Al-Mudawwanah (1/83), Al-Majmuu (4/180) na Al-Mughniy (2/134)].
Wa kwanza:
Msomaji mweledi zaidi anastahiki.
Ni kauli ya Abu Haniyfah na Maswahibu zake, Ath-Thawriy na Ahmad. Dalili yao ni:
1- Hadiyth ya Abu Saiyd Al-Khudriyy aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Watu wakiwa watatu, basi awaswalishe mmoja wao, na mwenye haki zaidi ya kuswalisha ni yule aliyewazidi wenzake kwa kisomo)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (672), An-Nasaaiy (2/77) na Ahmad (3/24)].
2- Hadiyth ya Abu Mas-’oud Al-Answaariy aliyesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Awaswalishe watu mwenye kukisoma zaidi Kitabu cha Allaah. Kama kisomo chao kiko sawa, basi awaswalishe mjuzi zaidi wa Sunnah. Kama wako sawa katika Sunnah, basi aliyehajiri mwanzo. Na kama wako sawa katika Hijrah, basi aliyetangulia katika Uislamu. Na mtu asimwongoze mtu katika madaraka yake ila kwa idhni yake, na asikae nyumbani kwake juu ya kiti chake ila kwa idhni yake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (673), Abu Daawuud (582), At-Tirmidhiy (235), An-Nasaaiy (2/76) na Ibn Maajah (980)].
3- Hadiyth ya ‘Amri bin Salamah ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( Swalini Swalaah fulani katika wakati fulani, na swalini Swalaah fulani katika wakati fulani, na wakati wa Swalaah unapoingia, basi mmoja wenu aadhini, na awaswalisheni mweledi wenu zaidi wa Qur-aan))…..Wakaangalia, na hakukuwepo stadi zaidi wa kusoma kuliko mimi, kwa kuwa nilikuwa nikipata ‘ilmu toka kwa wasafiri. Wakanitanguliza mbele umri wangu ukiwa miaka sita au saba hivi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (4302), Abu Daawuud (585), An-Nasaaiy (2/80) na Ahmad (3/475)]. Hadiyth
4- Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar akisema: “Muhaajiryna wa awali walipofika Al-‘Uswbah (ni sehemu iliyoko Qubaa) kabla ya kuja Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Saalim aliyekuwa mtumwa wa Abu Hudhayfah alikuwa akiwaswalisha, naye alikuwa mweledi zaidi wao wa kusoma”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (692) na Abu Daawuud (588)].
Saalim alikuwa wakati huo bado ni mtumwa hajaachwa huru, lakini aliwaswalishwa pamoja na kuwa wao ni waungwana.
Wa pili:
Mtaalamu aliyebobea taaluma ya dini anastahiki zaidi kuliko msomaji stadi.
Ni kauli ya Maalik na Ash-Shaafi’iy, na riwaya toka kwa Abu Haniyfah na Ahmad. Dalili yao ni:
1- Ni kuwa linaweza kumtokea jambo ndani ya Swalaah ambalo hawezi kujua afanye vipi isipokuwa kwa kuwa na ujuzi, hivyo mjuzi anakuwa ni bora zaidi. Ni kama imamu au Kadhi Mkuu.
2- Wamezijibu Hadiyth zilizotangulia kwa kusema kuwa stadi zaidi wa kusoma katika Maswahaba ndiye mtaalamu zaidi wa taaluma ya dini, kwa kuwa walikuwa hawasomi Aayah kumi mpaka wafahamu maana zake na yaliyomo ndani yake kati ya elimu na amali. Nao wamejibiwa kuwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “ Kama kisomo chao kiko sawa, basi awaswalishe mjuzi zaidi wa Sunnah” linatoa dalili kwamba msomaji stadi ndiye wa kutangulizwa bila mpinzani.
3- Ni Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kumtanguliza Abu Bakr awaswalishe watu wakati ugonjwa ulipomzidia, na Abu Bakr hakuwa stadi wao zaidi. Wamejibiwa kwamba kutangulizwa Abu Bakr kulikuwa ni ishara ya kuteuliwa kuwa Khaliyfah, na Khaliyfah ana haki zaidi na uimamu hata kama mwingine ni stadi zaidi wa usomaji kuliko yeye.
· Lenye Nguvu:
Mweledi zaidi wa kusoma ndiye anayestahiki zaidi kuwa imamu lakini kwa sharti kwamba awe anajua yote yanayopasa kuyajua kuhusu Swalaah. Na kama hayajui hayo, basi asiwe imamu kwa itifaki ya Maulamaa. [Fat-hul Baariy (2/171). Chapa ya Al-Maarifah].
Kisha swali linabaki: Nini makusudio ya msomaji mweledi zaidi?
Jamhuri wanasema kwamba ni yule anayesoma vizuri zaidi. Baadhi ya Mahanbali wanasema ni yule aliyehifadhi zaidi.
Ninasema: “Naam, ni yule aliyehifadhi zaidi kutokana na Hadiyth zilizotangulia zinavyohabarisha, lakini kwa sharti kwamba kisomo chake kiwe sahihi na madhubuti, na kila herufi itoke kwenye ala yake (makhraji yake).
· Angalizo:
Haitakikani Kumfanya Imamu Asiyestahiki Uimamu Kwa Kuwa Tu Anaghani Mno Anaposoma
Imepokelewa toka kwa ‘Abbaas Al-Ghaffaariy akisema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiyaeleza mambo sita anayoyakhofia juu ya Umma wake: Watoto wadogo kuendesha dola, kukithiri polisi na vyombo vya usalama, watawala kula hongo, kukata ukoo, kuua bila kujali, na mashabiki wenye kuifanya Qur-aan zumari. Wanamtanguliza mtu ambaye si mjuzi wao wala mbora wao awaghanie nyimbo))”. [Hasan kwa Sanad tofauti: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Twabaraaniy katika Al-Kabiyr (18/37), Ahmad (3/494) na Al-Bukhaariy katika At-Taariykh (7/80). Ina Hadiyth wenza zenye kuitilia nguvu].
Makusudio ya ughaniji unaolaumiwa hapa, ni ule wa chumvi ya kulazimisha unaopetuka qaaidah za lugha na tajwiydi, wa madoido ziada, wa kurembesha, na wa mahadhi yanayochukiwa na Maulamaa.
· Mtu Asiingie Kuswalisha Wakati Imamu Mteule Yupo Ila Kwa Ruksa Yake
Ni kutokana na neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) – katika Hadiyth ya Ibn Mas-’oud iliyotangulia punde - ((Na mtu asimwongoze mtu katika madaraka yake ila kwa idhni yake)). [Hadiyth Swahiyh: Tumeitaja nyuma kidogo]
Imamu wa Msikiti kapewa mamlaka yake na wahusika, na kwa hivyo haijuzu mtu mwingine aswalishe ila kwa idhni yake, na kama si hivyo basi itakuwa ni fujo na migogoro. Wahusika inawabidi wamteue imamu anayefaa na anayestahiki kazi hiyo, na kama si hivyo, basi watapewa uimamu wahafidhi mamluki wasioswalisha itakikanavyo na wasiojua hukumu zake!!
· Ustahikivu Wa Uimamu Kiufupi
Ikiwa Msikiti una imamu mteule wa kudumu, basi huyo ndiye wa kuswalisha, na kama hayuko, basi atatangulizwa msomaji stadi na mjuzi zaidi wa Fiqhi ya Swalaah. Kama watu watalingana, basi atangulizwe mjuzi na mwelewa zaidi wao wa Sunnah. Wakilingana, basi aliyewatangulia wote kwa Hijrah, na kama watalingana, basi mkubwa wao zaidi kiumri. [Hijrah ni kuhama toka nchi ya Makafiri kwenda nchi ya Kiislamu. Hijrah hii inaendelea mpaka Siku ya Qiyaamah, haina ukomo].
Haya ndiyo yanayofahamika kutokana na maneno ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliyomwambia Maalik bin Al Huwayrath pamoja na watu aliokuwa nao wakati walipotaka kurejea kwa watu wao:
((Swalini kama mlivyoniona nikiswali. Na Swalaah inapowadia, basi mmoja wenu aadhini, na mkubwa wenu zaidi kiumri awaswalishe)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (631) na Muslim (674)].
· Si Sharti Imamu Awe Yule Aliyewapiku Wote
Bali unajuzu uimamu wa kila ambaye uimamu wake unaswihi kumswalisha imamu anayestahiki zaidi uimamu kuliko yeye. Ni kama Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliposwali nyuma ya Abu Bakr wakati wa maradhi yake aliyofia. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (684)].
Aidha, Rasuli aliswali rakaa ya pili ya Swalaah ya Alfajiri nyuma ya ‘Abdul Rahmaan bin ‘Awf. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim toka Hadiyth ya Al-Mughiyrah].
· Watu Ambao Uimamu Wao Unaswihi
1- Kipofu
Imepokelewa toka kwa Muhammad bin Ar-Rubay’i ya kwamba ‘Utbaan bin Maalik alikuwa akiwaswalisha watu wake naye ni kipofu, na kwamba alisema: “Ee Rasuli wa Allaah! Hakika inakuwa ni giza na mafuriko na mimi ni mtu kipofu, basi swali ee Rasuli wa Allaah nyumbani kwangu katika sehemu ambayo nitaifanya kuwa ndio kijimsikiti changu. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwendea kisha akamuuliza: ((Ni wapi unataka niswali?)). Akamwonyesha sehemu ya nyumba, na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaswali hapo. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (667) na Muslim (33)].
Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimpa Ibn Maktoum uongozi wa kuswalisha watu Madiynah. [Swahiyh Lighayrih: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Hibaan (2134) na Abu Ya’alaa (4456). Ina Hadiyth mwenza ya Ibn ‘Abbaas].
· Faida
Kwa mujibu wa kauli yenye nguvu, inajuzu kwa mwenye ulemavu wowote kumswalisha mzima asiye na ulemavu, kwa kuwa hakuna tofauti kati yake na kipofu. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi. [Angalia As-Saylu Al-Jarraar (1/253)].
2- Mtumwa na aliyewahi kuwa mtumwa
Imepokelewa na Ibn ‘Umar akisema: “Muhaajiriyn wa awali walipofika Al-‘Uswbah (ni sehemu iliyoko Qubaa) kabla ya kuja Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Saalim aliyekuwa mtumwa wa Abu Hudhayfah alikuwa akiwaswalisha, naye alikuwa mweledi zaidi wao wa kusoma”. [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa nyuma kidogo].
Maswahaba wakubwa wa Kikureshi, wote kwa pamoja, waliafiki kumtanguliza Saalim, na wakati huo alikuwa ni mtumwa, hajaachwa huru bado. Kutangulizwa huku kunatoa dalili ya kujuzu mtumwa kuwa imamu.
Imepokelewa toka kwa Naafi’i bin ‘Abdul Haarith ya kwamba ‘Umar alimwambia: “Ni nani unayemtumia kuwaongoza watu wa Bondeni?” Akasema: “Ni Ibn Abzaa”. Akauliza: “Ni nani Ibn Abzaa?” Akasema: “Alikuwa ni katika watumwa wetu”. Akauliza: “Umewawekea mtumwa wa zamani kuwaongoza?” Akajibu: “Ni msomaji mzuri wa Kitabu cha Allaah ‘Azza wa Jalla na mjuzi wa taaluma ya mirathi”. ‘Umar akasema: “Ama mimi, hakika nimemsikia Nabiy wenu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Hakika Allaah Huwanyanyua kwa Kitabu hiki watu, na Huwashusha wengine kwacho)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (817), Ibn Maajah (218) na Ahmad (1/35)].
Kwa haya, Jamhuri wanaona kwamba uimamu wa mtumwa unaswihi kinyume na Maalik.
2- Mtoto mtambuzi
Tumeshaeleza nyuma kwamba ‘Amri bin Salamah aliwaswalisha watu wake akiwa mtoto wa miaka sita au saba wakati Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipowaamuru awaswalishe mwingi wao kwa kisomo.
Ash-Shaafi’iy pekee ndiye anayekubali hili kinyume na Jamhuri wanaokataa, lakini Hadiyth inawarudi wenyewe. Na mwenye kusema kwamba hao walilifanya hilo kwa ijtihada yao wenyewe na Rasuli hakuliona, basi hakutenda haki, kwa kuwa haiwezekani likapitishwa jambo lisilojuzu wakati Wahyi bado unashuka. Ni kama Abu Sa’iyd na Jaabir walivyotoa dalili ya kujuzu kumwagia maji ya uzazi nje ya utupu wa mwanamke kwa kuwa wao walilifanya katika enzi ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na kama hilo lingekuwa limekatazwa, basi Qur-aan ingelikataza. [Fat-hul Baariy (8/23) chapa ya Al-Maarifah].
3- Fasiki
Katika kauli mbili sahihi zaidi za Maulamaa, fasiki anafaa kuwa imamu. Hii ni kauli ya Abu Haniyfah, Ash-Shaafi’iy na riwaya toka kwa Ahmad. [Al-Mabsuutw (1/40), Al-Majmu’u (4/123) na Al-Inswaaf (2/252)].
Yanayoarifu hilo ni:
(a) Ujumuishi wa Hadiyth zilizotangulia katika kumtanguliza msomaji zaidi wa Kitabu cha Allaah.
(b) Hadiyth ya Abu Hurayrah ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Wanawaswalisheni, na kama watafanya sawa, basi thawabu mtapata nyinyi, na kama wakikosea, basi thawabu mtapata nyinyi, na wao watabeba makosa yao)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (294) na Ahmad (2/355)].
(C) Hadiyth ya ‘Ubaydullah bin ‘Uday bin Al-Khayyar ya kwamba aliingia kwa ‘Uthmaan bin ‘Affaan (Radhwiya Allahu Anhu) akiwa amezingirwa akamwambia: “Wewe ni imamu mkuu, na yamekufika haya tunayoyaona. Anatuswalisha imamu wa fitna, nasi twahofia kuwa tunafanya makosa”. Akamwambia: Swalaah ndiyo amali bora kabisa wanayoifanya watu. Na kama watu watafanya amali bora, basi fanya nao, lakini wakifanya ubaya, basi uepuke ubaya wao.“ [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (695) na ‘Abdul Razzaaq (1991)].
(d) Maswahaba akiwemo Ibn ‘Umar, waliswali nyuma ya Al-Hajjaaj bin Yuusuf, naye ni fasiki mbaya kabisa. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1660) na An-Nasaaiy (5/254)].
Lakini pamoja na kujuzu, ni karaha kuswali nyuma yake kutokana na Hadiyth ya Thawbaan aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Kwa hakika ninauogopea Umma wangu viongozi wa dini wapotoshi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (2229), Abu Daawuud (4252) na Ahmad (6/278)].
Ikiwezekana kumfuata asiye fasiki, basi inatakikana kumwacha fasiki, na kama haiwezekani kwa kuwa Jamaa yaweza kutatizika, basi itajuzu kumfuata kama ilivyotangulia. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
· Faida
Haijuzu kuswalishwa na kafiri kwa kuwa Swalaah yake haiswihi kwake mwenyewe. Allaah Anasema:
((وَلَقَدْ أُوحِيَ إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكَ لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ))
(( Kwa yakini umefunuliwa Wahy na kwa wale walio kabla yako kwamba: “Ukifanya shirki bila shaka zitaporomoka ‘amali zako na bila shaka utakuwa miongoni mwa waliokhasirika”)). [Az-Zumar (:65)]
Na Anasema tena:
((وَقَدِمْنَا إِلَىٰ مَا عَمِلُوا مِنْ عَمَلٍ فَجَعَلْنَاهُ هَبَاءً مَّنثُورًا))
(( Na Tutayaendea yale waliyoyatenda ya ‘amali yoyote ile, Tutayafanya chembechembe za vumbi zinazoelea hewanizinazotawanyika )). [Al-Furqaan (25:23)]
5- Asiyejulikana itikadi yake wala hali yake
Maimamu wote wanne na wengineo wamekubaliana kwamba Swalaah inaswihi nyuma ya imamu asiyejulikana kuwa anafanya mambo ya bid-’a au ufasiki, na kwamba si sharti ya kufuata kwamba maamuma ajue itikadi ya imamu wake wala kumjaribu kwa kumuuliza itikadi yake, bali ataswali nyuma ya asiyejulikana hali yake. [Majmu’u Al-Fataawaa cha Sheikh wa Uislamu (23/351)].
Hii ni kutokana na neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Wanawaswalisheni, wakifanya sawa basi thawabu ni zenu, na wakikosea basi thawabu ni zenu na makosa ni juu yao)). [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa nyuma kidogo].
Na Anas bin Maalik anasema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:
((Mwenye kuswali Swalaah yetu, akaelekea Qiblah chetu na akala kichinjwa chetu, basi huyo ni Muislamu mwenye Dhima ya Allaah na Dhima ya Rasuli Wake. Basi msimfanyie Allaah udanganyifu katika Dhima Yake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1/391), Abu Daawuud (2641), At-Tirmidhiy (2608) na An-Nasaaiy (2/105)].
Ibn Hazm kasema: [Al-Muhallaa (4/51)].
“Akiswali nyuma ya mtu anayedhani kuwa ni Muislamu, kisha akajua kwamba ni kafiri au anacheza tu, au hajabaleghe, basi Swalaah yake ni kamili, kwa kuwa Allaah Hakumkalifisha kuyajua yaliyomo ndani ya nyoyo za watu, bali tumekalifishwa yale tuyaonayo kidhahiri. Hivyo, tunaloamrishwa Swalaah inapoqimiwa ni kuswalishwa na mtu tunayemwona kidhahiri, na mwenye kufanya hivyo, basi anakuwa ameswali kama ilivyoamrishwa..”.
Lakini Jamhuri wamesema: “Ni lazima aswali tena akija kujua kwamba imamu wake ni kafiri”.
4- Mwanamke kuswalisha Jamaa ya wanawake
Katika mlango wa hukmu ya Jamaa ya wanawake, tulieleza kwamba ‘Aaishah na Ummu Salamah waliwaswalisha wanawake wenzao.
Ama mwanamume na kijana kuswalishwa na mwanamke, hilo haliswihi kwa mujibu wa kauli ya Jamhuri ya Masalaf na Makhalaf kutokana na neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliposema:
((Hawatofaulu watu waliomtawalisha mwanamke juu yao)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (4425), At-Tirmidhiy (2262) na An-Nasaaiy (8/227)].
Na pia ni kuwa haikuthibiti toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba alijuzisha mwanamke kumswalisha mwanamume au wanaume mbali na kuwa hakuna tukio lolote kuhusu jambo hili lililotokea enzi ya Rasuli wala enzi ya Maswahaba wala enzi ya Taabi’iyna.
Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliziweka safu zao nyuma ya safu za wanaume kuchelea fitna. Hivyo, mwanamume kumfuata mwanamke ni kinyume na haya yaliyotajwa. Na huwezi kusema kwamba asili ni kufaa hilo!! Kwa kuwa sisi tunasema: “ Yamekuja yenye kuarifu kwamba wanawake hawafai kuongoza jambo lolote, na hili ni katika jumla ya mambo, bali ndilo la juu na tukufu zaidi”. [As-Saylu Al-Jarraar (1/250)].
· Mwenye Kuwaswalisha Watu Na Wao Wanamchukia
Imepokelewa na Abu Umaamah akisema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Watu watatu Swalaah zao hazivuki masikio yao (hazikubaliwi kabisa): Mtumwa aliyetoroka mpaka arejee, mwanamke aliyelala nailhali mumewe ameghadhibika naye, na imamu anayeongoza watu na wao wanamchukia)). [Hasan kwa Sanad tofauti: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (360). Ina Hadiyth mwenza kwa Abu Daawuud (593) na Ibn Maajah (970)].
Makamio haya ni mahususi kwa mtu ambaye watu wanamchukia kwa sababu ya dini yake, kwenda kwake kinyume na Sunnah au mengineyo mengi ambayo yamekuwa ni mtihani katika zama zetu hizi toka kwa maimamu ambao hima yao kubwa ni kujikita Misikitini ili kupata mishahara. Wengi wao hawaijui dini, na wamekuwa chanzo cha matatizo yote na kwa watu wao. Tunajilinda kwa Allaah na yenye kuchusha.
Ama imamu mwenye kusimamisha Sunnah, basi madhambi watayapata wanaomchukia. Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimpa Usamah madaraka awaongoze watu, lakini watu hao waliupinga na kuukosoa uongozi wake. Rasuli akasema:
((Kama mnaukosoa na kuupinga uongozi wake, basi mshaukosoa na kuupinga uongozi wa baba yake kabla yake. Basi naapa kwa Allaah! Hakika yeye alikuwa anastahiki uongozi, na hakika yeye ni katika watu wanaopendeka zaidi kwangu, na hakika huyu bila shaka, ni katika watu wanaopendeka zaidi kwangu baada yake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (4250) na Muslim (2426)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
041-Mahala Pa Kusimama Imamu Na Maamuma
Alhidaaya.com [3]
[1] Swalaah ya imamu na maamuma mmoja tu
Akiswali mtu mmoja tu na imamu, basi atasimama sambamba upande wake wa kulia –bila kurudi kidogo nyuma kama anavyosema Ash-Shaafi’iy- kutokana na yaliyomo ndani ya kisa cha Ibn ‘Abbaas aliposwali na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Kisha akasimama kuswali (yaani Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)), nami nikasimama na kufanya kama alivyofanya. Kisha nikaenda na kusimama pembeni yake, naye akaweka mkono wake wa kulia juu ya kichwa changu, akalikamata sikio langu la kulia na kulisokota. Kisha akaswali…”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (183) na Muslim (763)].
Na katika riwaya nyingine: [Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (1/330) kwa Sanad Swahiyh lakini riwaya hii kidhahiri ni “Shaadhah”].
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipoelekea kwenye Swalaah yake, nilirejea nyuma, Rasuli akaswali, na alipomaliza aliniambia: ((Vipi wewe? Nakuweka pembeni yangu nawe warudi nyuma!)). Hadiyth
Na Jaabir anasema katika kisa chake cha kuswali na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Akaja, akatawadha, kisha akasimama akaswalia nguo moja aliozifunga ncha zake kinyume. Nami nikasimama nyuma yake, akalikamata sikio langu na kuniweka kuliani kwake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (766) na Ahmad (3/351)].
Na katika kisa cha Swalaah ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) -katika maradhi yake ya kifo- pembeni mwa Abu Bakr, ‘Aaishah amesema: “ Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akakaa sambamba pembeni mwa Abu Bakr. Abu Bakr akawa anaswali kwa Swalaah ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na watu wanaswali kwa Swalaah ya Abu Bakr”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (683) na Muslim (418)].
[2] Swalaah ya imamu na watu wawili au zaidi
- Wakiswali watu wawili na imamu, watasimama nyuma yake safu moja kwa makubaliano ya Maswahaba Maulamaa na waliofuatia baada yao kinyume na Ibn Mas-’oud na Maswahibu zake wawili. Hii ni kutokana na Hadiyth ya Jaabir aliyesema: “Kisha nikaja mpaka nikasimama kushotoni mwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), akaukamata mkono wangu akanizungusha na kunisimamisha kuliani kwake. Kisha akaja Jabbar bin Swakhr, akatawadha, halafu akaja na kusimama kushotoni mwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaikamata mikono yetu sote, akatusukuma na kutusimamisha nyuma yake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (3006) katika Hadiyth ndefu, Ibn Maajah (973) na Ahmad (3/421)].
Naye Anas anasema: “Tuliswali mimi na yatima katika nyumba yetu nyuma ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na mama yangu –Ummu Sulaym- yuko nyuma yetu”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (727) na Muslim (658)].
Ama Ibn Mas-’oud, yeye alikuwa anaona kwamba mmoja asimame kuliani mwa imamu na mwingine kushotoni. Al-Aswad na ‘Alqa’mah waliswali pamoja na ‘Abdullah bin Mas-’oud nyumbani kwake. Wanahadithia hilo wakisema: “..Tukaenda ili tusimame nyuma yake, akatukamata mikono yetu, akamweka mmoja wetu kuliani kwake na mwingine kushotoni kwake. Aliporukuu, tuliweka mikono yetu juu ya magoti yetu. Anasema: Akaipiga mikono yetu, akapandanisha kati ya viganja vyake viwili, kisha akaviingiza baina ya mapaja yake mawili, halafu akasema: Hivi ndivyo alivyofanya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (534), Abu Daawuud (613) na An-Nasaaiy (2/49)].
Lakini kundi la Maulamaa akiwemo Ash-Shaafi’iy linasema kwamba Hadiyth hii ya Ibn Mas-’oud ni Mansuwkh, kwa kuwa alijifundisha Swalaah hii toka kwa Rasuli akiwa Makkah ambako utendaji na hukmu ulikuwa ni tofauti, nazo kwa sasa zimeachwa, na hukmu hii ilikuwa ni miongoni mwazo. Na Rasuli alipofika Madiynah aliiacha. Na ikiwa tutajaalia kwamba historia ya tukio haijulikani, basi Hadiyth hii haina ubavu wa kuzipinga Hadiyth zilizotangulia. [Naylul Aw-Twaar na Al-Muhalla].
- Wakiswali watu zaidi ya watatu na imamu, basi wote watasimama nyuma yake kwa Ijma’a ya Maulamaa. Hadiyth zenye kubainisha hili ni nyingi mno hazihesabiki.
- Haijuzu maamuma kumtangulia imamu, kwa kuwa haiswihi kumfuata imamu isipokuwa kama yuko mbele ya maamuma. Jamhuri wanasema kwamba mwenye kumtangulia imamu Swalaah yake ni batili. Lakini Maalik, Is-Haaq, Abu Thawr na Daawuud wanaona kwamba inajuzu kama nafasi itakuwa finyu, na wengine wanasema kwa hali yoyote yajuzu. [Ibn ‘Aabidiyn (1/551), Ad-Dusouqiy (1/331), Mughnil Muhtaaj (1/490), Kash-Shaaful Al-Qinaa’a (1/485), na Al-Inswaaf (2/280)].
[3] Swalaah pembeni ya imamu kwa aliyekosa nafasi Msikitini
Anayeingia Msikitini, akakuta Msikiti umejaa na safu zimekamilika, anaruhusiwa kuzipenya safu kwenda kwa imamu kusimama pembeni yake. Hili alilifanya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika maradhi yake wakati Abu Bakr alipokuwa anaswalisha watu. “Abu Bakri alipomwona, alirejea nyuma, naye akamwashiria aendelee kama alivyo. Rasuli akakaa sambamba pembeni ya Abu Bakri”. [Hadiyth Swahiyh: Tumeitaja nyuma kidogo].
Na pia kisa cha kwenda Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa Bani ‘Amri bin ‘Awf ili kuwasuluhisha, na akamkuta Abu Bakri anawaswalisha watu. Kisa kinasema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaja na watu wako kwenye Swalaah. Akajipenyeza mpaka akasimama kwenye safu……”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (684) na Muslim (421)].
Na katika tamshi la Muslim: “Akazipenya safu mpaka akasimama mbele ya safu ya mbele”.
[4] Swalaah ya mwanamke na imamu
Mwanamke akiswali na imamu, basi atasimama nyuma ya safu za wanaume hata kama hakuna wanawake wenzake. Atasimama peke yake kwenye safu ya mwisho. Na kama ataswali yeye peke yake na imamu, basi atasimama nyuma yake, na si kuliani kwake.
Ummu Salamah anasema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapotoa tasliym, wanawake husimama anapomaliza tasliym yake, naye hukaa kidogo mahala pake kabla hajasimama. Tunaona –na Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi- kwamba hilo ni ili wanawake waondoke kabla mwanamume yeyote hajawakuta”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (870), Abu Daawuud (1040), An-Nasaaiy (2/66) na Ibn Maajah (932)].
Na Anas amesema: “Niliswali mimi na yatima nyuma ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na mama yangu Ummu Sulaym yuko nyuma yetu”. [Hadiyth Swahiyh: Tumeitaja nyuma kidogo].
Naye Ibn Mas-’oud amesema: “Wanaume na wanawake wa Bani Israa’iyl walikuwa wakiswali pamoja. Mwanamke mwenye mpenzi wake, alikuwa akivaa visigino virefu ili apate kimo zaidi mbele ya mpenzi wake, na hapo wakateremshiwa hedhi”. Ibn Mas-’oud alikuwa akisema: “Wawekeni nyuma pale Alipowarudisha Allaah”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdul Razzaaq (5115) na At-Twabaraaniy (9384)].
Na kama wataswali imamu, mwanamume mmoja na mwanamke mmoja, basi mwanamume atasimama sambamba kuliani mwa imamu, na mwanamke atasimama peke yake nyuma yao. Imepokelewa toka kwa Anas kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimswalisha yeye pamoja na mwanamke. Rasuli akamweka yeye kuliani kwake, na mwanamke nyuma yao kidogo. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (269) na Ibn Abu Shaybah (2/88)].
· Faida
Ikiwa mwanamke atavunja miiko kwa kuswali mbele ya safu za wanaume, basi Swalaah yake itajuzu kwa mujibu wa kauli ya Jamhuri. Lakini Hanafi wanasema kuwa Swalaah ya wanaume ndiyo itakuwa batili, na si ya mwanamke!!.
Ninasema:
“La sahihi ni kuwa Swalaah yake mwanamke ndiyo inayobatilika kutokana na Hadiyth isemayo: ((Mwenye kuswali peke yake nyuma ya safu, hana Swalaah)), na kwa kusimama Ummu Salamah peke yake nyuma ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Anas na yatima. Na hili linatujulisha kwamba Swalaah yake hubatilika akiswali mbele ya wanaume au akiwa nao pamoja. Lakini hili ni kama hakuna dharura ya kufanya hivyo”.
[5] Swalaah ya mwanamke na wanawake wenzake
Mwanamke akiswalisha jamaa ya wanawake wenzake, basi atasimama katikati yao, hatokuwa mbele ya safu yao ya kwanza. Hili ni sitara zaidi kwake. Imepokelewa toka kwa Rabtwah Al-Hanafiyyah akisema kwamba ‘Aaishah aliwaswalisha na akasimama katikati yao katika Swalaah ya faradhi. [Hadiyth Swahiyh kwa Hadiyth wenza zenye kuitilia nguvu: Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdul Razzaaq (3/141), Ad-Daara Qutwniy (1/404) na Al-Bayhaqiy (3/131)].
Imepokelewa toka kwa Hujayrah toka kwa Ummu Salamah kwamba aliwaswalisha na akawa katikati yao. [Hadiyth Swahiyh kwa Hadiyth wenza zenye kuitilia nguvu: Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdul Razzaaq (3/140), Ad-Daara Qutwniy (1/405) na Al-Bayhaqiy (3/131)].
Na ikiwa mwanamke atawaswalisha wenzake na akasimama mbele yao, basi kwa mujibu wa mwono wenye nguvu zaidi, Swalaah yake itakuwa ni sahihi yenye kutosheleza kwa kuwa hakuna dalili ya kuibatwilisha. Lakini hilo litakuwa ni kinyume cha ubora. Allaah Ndiye Mjuzi zaidi.
[6] Wanaposimama watoto wa kiume katika Swalaah
Imesimuliwa kwamba: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiwaweka wanaume mbele ya watoto, na watoto nyuma yao, na akina mama nyuma ya watoto.” Lakini ni Dhwa’’iyf, haifai. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (677) na Ahmad (5/341) toka kwa Abu Maalik Al Ash-ariy].
Imamu Al-Albaaniy amesema: “Ama kuwaweka watoto nyuma yao, sikupata katika hili isipokuwa Hadiyth hii, na hoja haisimami kwayo. Basi mimi sioni ubaya watoto kusimama pamoja na watu wazima ikiwa safu itakuwa na nafasi. Na Swalaah ya yatima pamoja na Anas nyuma ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni hoja juu ya hilo”. [Tamaam Al-Minnah ukurasa wa 282].
Ninasema: “Hadiyth ya Anas kuhusu kuswali yeye pamoja na yatima nyuma ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) tushaielezea. Na lau kama watoto wangelikuwa wanazuiwa kusimama safu moja na wanaume, basi Anas angelisimama kuliani mwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na yatima angesimama nyuma yao, na Ummu Sulaym naye nyuma yao wote. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.”
· Swalaah Ya Imamu Na Maamuma Katika Sehemu Ya Mnyanyuko
1- Imamu kuwa juu na maamuma chini
Ni karaha kwa imamu kuwa juu na maamuma kuwa chini. Hii ni kauli ya Jamhuri, ni sawasawa kuwa juu kwake ni kwa haja au bila haja. Imepokelewa toka kwa Hammaam: “Kwamba Hudhayfah aliwaswalisha watu huko Al-Madaain akiwa sehemu ya juu. Abu Mas-’oud (Muanswaar) akaikamata kanzu yake akamvuta. Alipomaliza Swalaah alimwambia: “Je, hujui kwamba wao walikuwa wakikatazwa hilo?” Akasema: “Naam. Nilikumbuka uliponivuta”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (597), Ibn Khuzaymah (1523), Al-Haakim (1/210) na Al-Bayhaqiy (3/108). Hakuna kinachoogopewa humo isipokuwa “an-‘anah” ya Al-A’amash].
Ash-Shaafi’iy kasema: “Ninapendelea kwa imamu anayewafundisha maamuma wake Swalaah, aswalishe juu ya kitu kilichonyanyuka ili wamwone na kufuatilisha vitendo vyake”. Na hili ni kwa riwaya toka kwa Ahmad kwa Hadiyth ya Sahl bin Sa’ad wakati alipoulizwa kuhusu mimbari akasema: “Kisha nikamwona Rasuli wa Allaah akiswali juu yake (yaani vigogo vya mimbari). Akapiga takbiyr akiwa juu yake, kisha akarukuu akiwa juu yake, halafu akateremka kinyumenyume na kusujudu juu ya mimbari asili, kisha akarudi. Alipomaliza aliwaelekea watu na kuwaambia: “Enyi watu! Mimi nimefanya hivi ili munifuate na mjifunze ninavyoswali”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (917) na Muslim (544)].
Ninasema: “Ikiwa kuna faida ya imamu kusimama sehemu iliyonyanyuka kama kuwafundisha watu na mfano wake, basi hakuna ubaya kutokana na Hadiyth hii. Pia kama hilo litalazimu kama kujaa sehemu ya juu ya Msikiti aliko imamu na watu wengine wakaswalia chini”.
2- Maamuma kuwa juu na imamu kuwa chini
Hakuna dalili ya kuzuia maamuma kuswali juu na imamu chini na hususan ikiwa itabidi kama kujaa sehemu ya chini ya Msikiti na wengine wakaswalia juu. Lakini kuswalia huko ni lazima kuwe kwa namna ambayo maamuma anaweza kumsikia imamu, kumfuata na kwenda naye sambamba akiwa nyuma yake. Hatakiwi kuwa mbele yake ila kwa udhuru. Hili linatiliwa nguvu na kitendo cha Abu Hurayrah. Alikuwa juu ya jengo lililo juu ya Msikiti, na alikuwa akimfuata imamu. [Isnadi yake ni Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abi Shaybah (2/223), ‘Abdul Razzaaq (4888) na Al-Bayhaqiy (3/111)].
Na imepokelewa toka kwa Sa’iyd bin Sulaym akisema: “Nilimwona Saalim bin ‘Abdallah akiswali Swalaah ya Magharibi juu ya paa la Msikiti akiwa na mtu mwingine, yaani akimfuata imamu”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Shaybah (2/233)].
· Kumfuata Imamu Nyuma Ya Kizuizi
Ikiwa maamuma ataswali nje ya Msikiti na imamu yuko ndani, au akaswali ndani ya Msikiti lakini kipo kizuizi kati yao, basi itajuzu ikiwa safu zitaungana. Maimamu wote wamekubaliana juu ya hili. [Majmu’u Al-Fataawaa (23/407)].
Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), alikuwa anaswali usiku katika chumba chake na ukuta wa chumba ukiwa mfupi. Watu walikuwa wakikiona kiwiliwili chake na kumfuata katika Swalaah yake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (729) na Muslim (782)].
Chumba hicho ni mkeka uliokuwa ukimwekea kizuizi usiku Msikitini kama ilivyo kwenye baadhi ya riwaya za Hadiyth.
Imepokelewa toka kwa Jublah bin Abi Sulaymaan akisema: “Nilimwona Anas bin Maalik akiswali kwenye nyumba ya Abu ‘Abdullah iliyo juu ya Msikiti na yenye mlango wa kuingilia Msikitini. Alikuwa akiswali Ijumaa hapo na akimfuata imamu”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abu Shaybah (2/223) ‘Abdul Razzaaq (5455) na Al-Bayhaqiy (3/111)].
Ikiwa watapanga safu na kukawa kati yao na safu nyingine barabara ambayo watu wanapita, au mto wa kupita meli, basi hili lina kauli mbili ambazo ni riwaya toka kwa Ahmad. Kauli ya kwanza inasema kuwa hilo halifai kama asemavyo Abu Haniyfah, na ya pili inasema kwamba inajuzu kama wasemavyo Maalik na Ash-Shaafi’iy. [Majmu’u Al-Fataawaa (23/407) na Al-Mughniy]..
Kauli hii ndiyo yenye nguvu zaidi kwa kuwa hakuna Hadiyth au Ijma’a yoyote yenye kuzuia hilo. Al-Hasan kasema: “Hakuna ubaya ukiswali na kati yako na imamu kuna mto”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy ikiwa Mu’allaq (2/250-Fat-h), ‘Abdul Razzaaq kaifanya Mawsuul (5453) na Ibn Abu Shaybah (2/149)].
Lakini inatakikana maamuma aweze kujua vitendo vya imamu kama kusikia takbiyr ya imamu au kuiona safu ya mbele. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipowaona Maswahaba zake wanajiweka weka nyuma aliwaambia:
((Njooni mbele mnifuate, na wa nyuma wenu wawafuate wa mbele wenu. Hawataacha watu kuwa wanajiweka weka nyuma mpaka Allaah Awaweke nyuma)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (438), Abu Daawuud (480) An-Nasaaiy (2/83) na Ibn Maajah (978)].
Na kwa ajili hiyo, Ibn Mujlaz anasema: “Atamfuata imamu hata kama kutakuweko barabara au ukuta kati yao ikiwa atasikia takbiyr ya imamu”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Al-Bukhaariy kasema ni Mu’allaq (2/250-Fat-h), na Ibn Abu Shaybah kasema ni Mawswuwl (2/223) kwa Sanad Swahiyh].
Ninasema: “Haifichikani kwamba sababu ya utengano huu ni dharura kama kujaa Msikiti na viwanja vilivyoungana. Na kama si hivyo, basi asili ni kuungana safu na kukurubiana. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.”
· Angalizo:
Swalaah ya kumfuata imamu kwa njia ya idhaa (redio) haifai.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
042-Safu Na Hukmu Zake
Alhidaaya.com [3]
· Safu Bora Zaidi Kwa Upande Wa Wanaume Na Wanawake
Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Safu bora zaidi ya wanaume ni ya kwanza, na ya shari yake zaidi ni ya mwisho, na safu bora zaidi ya wanawake ni ya mwisho, na ya shari yake zaidi ni ya kwanza)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (440), Abu Daawuud (678), At-Tirmidhiy (224), An-Nasaaiy (2/93) na Ibn Maajah (1000)].
Ninasema: “Safu ya mwisho ya wanawake kuwa ni bora zaidi mahala pake ni pale wanawake wanapokuwa wanaswali nyuma ya safu za wanaume. Na ikiwa wanaswali nyuma ya mwanamke, au na imamu mwanamume katika mahala palipotenganishwa na wanaume, basi safu yao bora itakuwa ni ya kwanza. Hii ni kutokana na ujumuishi wa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Hakika Allaah na Malaika Wake Wanazitakia rahma safu za mwanzo)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (664), An-Nasaaiy (2/90) na Ibn Maajah (997)].
Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
· Fadhila Za Safu Ya Kwanza
Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Na lau wangelijua yaliyoko kwenye safu ya mbele, basi wangelipiga kura)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (720) na Muslim (437-439)].
Na katika tamshi la Muslim: ((..ingelifanyika kura)).
· Fadhila Ya Upande Wa Kulia Wa Safu
Imepokelewa toka kwa Al-Barrai akisema: “Tulikuwa tunaposwali nyuma ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), tunapenda kuwa kulia kwake akituelekea kwa uso wake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (709), Abu Daawuud (615), An-Nasaaiy (2/94) na Ibn Maajah (1006)].
Imepokelewa kwa njia Marfu’u toka kwa ‘Aaishah akisema: “Hakika Allaah na Malaika Wake Huwatakia rahma walioko kuumeni mwa safu”. [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (676) na Ibn Maajah (1005). Al-Bayhaqiy kaitia dosari matni yake (3/103) akisema kwamba haikuhifadhiwa. Al-Albaaniy kaipitisha kwenye Tamaam Al-Minnah (uk. 228), nayo ni kama walivyosema. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi].
Lakini Hadiyth hii haikuhifadhiwa kwa tamshi hili.
· Wanaosimama Nyuma Ya Imamu
Imepokelewa toka kwa Ibn Mas-’oud (Radhwiya Allahu Anhu) akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Wasimame nyuma yangu wale wenye akili na wajuzi miongoni mwenu, kisha wale wanaowafuatia (mara tatu). Na jiepusheni na vurugu za sokoni)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” Muslim (432), Abu Daawuud (675), na At-Tirmidhiy (228)].
Hadiyth hii inatuarifu kwamba wa kuwa nyuma ya imamu ni mtu mweledi zaidi kisha mjuzi zaidi. Kwa kuwa imamu anastahiki zaidi kuwa karibu na mtu huyo, kwani anaweza kumhitajia akamate uimamu badala yake, na pia anaweza kumkumbusha kama atasahau kitu ambacho wengine hawawezi. Aidha, weledi hao wataitoa picha halisi ya Swalaah, wataihifadhi na watu watajifunza kutoka kwao. Na kwa ajili hiyo, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapenda Muhaajiruwna na Answaar wakae nyuma yake ili wajifunze kutoka kwake. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Maajah (977), Ahmad (3/100) na wengineo].
· Kukamilisha Safu Ya Kwanza Kisha Inayoifuatia
Imepokelewa toka kwa Anas kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Kamilisheni safu ya kwanza kisha inayoifuatia, na kama kuna upungufu, basi uwe kwenye safu ya mwisho)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (2/93) na Abu Daawuud (671)].
Na imepokelewa toka kwa Jaabir bin Samrah akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitutokea akasema: ((Mbona nawaona mnanyanyua mikono yenu kana kwamba ni mikia ya farasi waliochacharika? Tulieni katika Swalaah)). Akasema: Kisha akatutokea akatuona tumejigawa mafungu mafungu akatuambia: (( Kwa nini msipange safu kama wanavyopanga safu Malaika mbele ya Mola wao?)) Tukasema: Ee Rasuli wa Allaah! Ni vipi Malaika wanapanga safu mbele ya Mola wao? Akasema: ((Wanaikamilisha safu ya kwanza na wanazinyoosha safu zao)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (430), Abu Daawuud (661), An-Nasaaiy (2/92) na Ibn Maajah (992)].
· Wajibu Wa Kunyoosha Safu Na Kuziba Mianya
Kuna Hadiyth nyingi Swahiyh zinazozungumzia suala hili. Kati yake ni:
1- Hadiyth ya An-Nu’umaan bin Bashiyr aliyesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika mtazinyoosha safu zenu, au Allaah Atakhitilafisha kati ya nyuso zenu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (717) na Muslim (436)].
Maana ya: “Allaah Atakhitilafisha kati ya nyuso zenu”, ni kuwa Ataingiza uadui na chuki kati yenu, na nyoyo zenu zitakhitalifiana. Kwa kuwa kukhitalifiana kidhahiri, ni sababu ya kukhitalifiana kindani. Maana hii inatiliwa nguvu na:
2- Hadiyth ya Abu Mas-’oud aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akipapasa mabega yetu katika Swalaah na kutuambia: ((Simameni sawa na msikhitalifiane, la sivyo nyoyo zenu zitakhitalifiana)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (432), Abu Dawuud (674), An-Nasaaiy (2/87) na Ibn Maajah (976)].
3- Imepokelewa toka kwa Anas toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba kasema: ((Lingamanisheni safu zenu, kwani hakika mimi nawaoneni kwa nyuma yangu)). Mmoja wetu alikuwa akilinatisha bega lake na bega la mwenzake, na unyayo wake kwa unyayo wake. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (725) na Muslim (434)].
4- Anas anasema kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (( Zinyorosheni sawa safu zenu, ziwekeni karibu karibu, na kuweni sambamba kwa shingo zenu. Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu iko Mkononi Mwake, hakika mimi namwona Shaytwaan anaingia kupitia mianya ya safu kana kwamba ni kondoo wadogo weusi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (667), An-Nasaaiy (2/92), na Ahmad (3/260)].
5- Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Lingamanisheni safu, yawekeni mabega sambamba, zibeni mianya, kuweni laini ndugu zenu wakiwashika mikono, na wala msiache nafasi wazi kwa Shaytwaan. Na mwenye kuunga safu, Allaah Humuunga, na mwenye kuikata safu, Allaah Humkata)). [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (666), An-Nasaaiy (2/93) na Ahmad (2/97)].
6- Imepokelewa toka kwa Anas kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Zisawazisheni safu zenu, kwani kuzisawazisha safu ni sehemu ya kuisimamisha Swalaah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” kwa tamko hili na Al-Bukhaariy (723), na kwa jingine Muslim (434), na wengineo].
• Imamu anatakiwa yeye mwenyewe azinyoroshe safu au awaamuru maamuma wafanye hivyo, na asihirimie Swalaah ila baada ya safu kulingamana sawa. Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar akisema: “Umar alikuwa hahirimii mpaka safu zilingamane sawa, huwapa jukumu kwa hilo watu”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdul Razzaaq (2439)].
· Faida
An-Nawawiy kasema kwenye Al-Majmu’u (4/297): “Kama mwenye kuingia kwenye safu atakuta mwanya au nafasi wazi, basi ataingia. Ikiwa safu ya mbele imepwaya, basi anaweza kuipasua safu ya nyuma yake iliyo jaa ili kuziba pengo, kwa kuwa hilo ni kosa la maamuma wa mwanzo”.
· Ukaraha Wa Kupanga Safu Kati Ya Nguzo
Imepokelewa toka kwa ‘Abdul Hamiyd bin Mahmoud akisema: “Niliswali pamoja na Anas bin Maalik siku ya Ijumaa. Tukasogezwa kwenye nguzo, nasi tukasogea mbele na tukarudi nyuma. Anas akasema: Tulikuwa tukijiepusha na hili katika enzi ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (673), An-Nasaaiy (2/94), At-Tirmidhiy (229) na Ahmad (3/131). Imeelezwa kama ni Dhwa’iyf kwa vipimo visivyokubalika].
Hili linatiliwa nguvu na Hadiyth ya Mu’aawiyah bin Murrah toka kwa baba yake akisema: “Tulikuwa tukikatazwa kupanga safu kati ya nguzo wakati wa uhai wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na tunafukuzwa tuwe mbali nazo kabisa”.[Isnadi yake ni Laini: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Maajah (1002), Ibn Khuzaymah (1567), Ibn Hibaan (2219) na Al-Haakim (1/218). Inatiliwa nguvu na Hadiyth ya kabla yake].
Na kwa ajili hiyo, ni karaha kwa maamuma kusimama kati ya nguzo za Msikiti kwa kuwa nguzo hizo huzikata safu zao. Lakini ikiwa safu ni fupi ya kuweza kujaza nafasi kati ya nguzo mbili, basi hakuna ukaraha kwa kuwa safu haikatwi. Ibn Mas-’oud, An-Nakh’iy, Ibn Al-Mundhir toka kwa Hudhayfah na Ibn ‘Abbaas wamelikirihisha hilo wakati ambapo Ibn Syriyna, Maalik na Aswhaabu Ar Ra’ay wameliruhusu. Wamesema kwamba hakuna dalili yoyote inayozuia hilo!! [Al-Awsatw cha Ibn Al-Mundhir (4/181-182)].
Na hakuna shaka yoyote kwamba Hadiyth ya Anas ina hukmu ya Umarfu’u, na inatiliwa nguvu na Hadiyth ya Qurrah bin Qays. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.
Ama ikiwa ni imamu na maamuma mmoja tu, basi hakuna ukaraha wa kusimama baina ya nguzo mbili kwa sababu tuliyokwishaieleza. Hili linatiliwa nguvu na Hadiyth ya Ibn ‘Umar aliyesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia nyumbani akiwa pamoja na Usamah bin Zayd, ‘Uthmaan bin Twalha na Bilaal. Akapotea huko kwa muda kisha akatoka. Nilikuwa mtu wa kwanza kuingia baada yake, nikamuuliza Bilaal: Ameswalia wapi? Akasema: Kati ya nguzo mbili za mbele”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (504) na Muslim (1329)].
· Anayeswali Peke Yake Nyuma Ya Safu
Asili katika Swalaah ya Jamaa ni kuwa maamuma wanatakiwa wawe kwenye safu zilizopangana sawa kama ilivyoelezwa. Na ikiwa maamuma ataswali peke yake nyuma ya safu, basi Maulamaa wamekhitalifiana kuhusiana na hukmu ya Swalaah yake katika kauli tatu:
Ya kwanza:
Ni kwamba Swalaah yake haiswihi. Ni kauli ya Ahmad, Is-Haaq, An-Nakh’iy, Ibn Abu Shaybah na Ibn Al-Mundhir. [Al-Awsatw (4/183), Al-Mughniy (2/211) na Al-Mumti’i (4/376)].
Dalili zao ni hizi zifuatazo:
1- Hadiyth ya ‘Aliy bin Shaybaan aliyesema: “Tulitoka mpaka tukafika kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), tukampa Bay-’ah na tukaswali nyuma yake. Halafu tuliswali nyuma yake Swalaah nyingine, na alipomaliza alimwona mtu mmoja anaswali peke yake nyuma ya safu. Alipomaliza, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasimama mbele yake na kumwambia: (( Ielekee Swalaah yako, hakuna Swalaah kwa aliye nyuma ya safu)). [Hadiyth Swahiyh kwa isnadi nyingine: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Maajah (1003), Ahmad (3/23), na Ibn Hibaan (2202)].
2- Hadiyth ya Waabiswah bin Ma’abad ya kwamba mtu mmoja aliswali peke yake nyuma ya safu. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwamuru aswali tena upya. [Hadiyth Swahiyh kwa Sanad tofauti: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (230,231), Abu Daawuud (682), Ibn Maajah (1004) na Ahmad (4/228). Angalia Al-Irwaa (541)].
Wamesema: “Lau kama Swalaah yake ingelikuwa imeswihi, basi asingemwamuru aiswali tena. Kwa kuwa kufanya upya ni wajibiko na taklifu katika jambo ambalo limeshafanywa na kumalizika, na lau kama si kuharibika kwake, asingelimkalifisha kulifanya tena upya”.
Ya pili:
Swalaah yake inaswihi, lakini ni karaha kusimama peke yake bila ya udhuru. Ni kauli ya Abu Haniyfah na Maswahibu zake, Maalik, Al-Awzaaiy na Ash-Shaafi’iy. [Al-Badaai-’i (1/218), Mughnil Muhtaaj (1/247), Jawaahirul Ikliyl (1/80), na Al-Awsatw (4/183)].
Dalili zao ni:
1- Hadiyth ya Abu Bakrah ambaye alimwahi Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa katika rukuu. Akarukuu kabla hajafika kwenye safu. Akalieleza hilo kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Rasuli akamwambia: ((Allaah Akuzidishie pupa, lakini usifanye tena)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (783), Abu Daawuud (683), An-Nasaaiy (2/118) na Ahmad (5/39)].
Wamesema: “Abu Bakrah aliifanya nguzo moja ya Swalaah nyuma ya safu lakini hakuamuriwa kuswali tena upya. Alilokatazwa ni kutokifanya tena kitendo hicho, kana kwamba ameelekezwa kwa lile lililo bora zaidi. Wamelitolea dalili hilo ya kwamba agizo la kuiswali tena upya Swalaah kwenye Hadiyth ya Waabiswah ni agizo la Sunnah, ikiwa ni kukusanya kati ya dalili mbili”.
Wa mwanzo wamejibu wakisema: Zinaweza kukusanywa kwa njia nyingine. [Fat-hul Baariy (2/314) chapa ya As-Salafiyyah, na Majmu’u Al-Fataawaa (23/397)].
Nayo ni kuwa Hadiyth ya Abu Bakrah ni mahsusi kwa ujumuishi wa Hadiyth ya Waabiswah. Mwenye kuanza kuswali peke yake nyuma ya safu, kisha akaingia kwenye safu kabla ya kusimama toka kwenye rukuu, basi si lazima aswali tena kama ilivyo kwenye Hadiyth ya Abu Bakrah. Na kama si hivyo, basi ni lazima airejeshe tena kwa mazingatio ya ujumuishi wa Hadiyth za Waabiswah na ‘Aliy bin Shiybaan.
2- Ni kwamba Ibn ‘Abbaas wakati Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomzungusha toka kushoto hadi kulia – na Hadiyth hii ishazungumzwa mara nyingi - alikuwa ameswali peke yake nyuma yake kwa sehemu ndogo ya Swalaah!! Wanasema: Chenye kuharibu Swalaah hakina tofauti kati ya kingi chake na kichache chake.!!
Wamejibiwa: Kwa mfano wa yaliyotangulia katika Hadiyth ya Abu Bakrah ni kuwa hakuna madhara yoyote kwa picha hii ndogo ya mtu kusimama peke yake nyuma ya safu kabla hajaingia.
3- Wameuchukulia ukanushi kwenye neno lake: “Hakuna Swalaah kwa aliye nyuma ya safu”, kama ni ukanushi wa ukamilifu na si ukanushi wa kuswihi.
Hili limejibiwa kwamba asili ni kukanusha uwepo, - na hili haliwezekani - kisha kukanusha uswihifu mpaka dalili ithibitishe kutowezekana kwake, na hapo pataelekewa kwenye ukanushi wa ukamilifu. Na hapa hakuna dalili vile vile. Kisha hili linakataliwa kwa amri yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ya kuswali tena kama ilivyotangulia.
4- Kuswali Ummu Sulaym peke yake kwenye safu nyuma ya Anas na yatima wakimfuata Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Limejibiwa kwamba hii ni hoja dhaifu isiyoweza kuipinga hoja ya katazo. Kwani kusimama mwanamke nyuma ya safu ya wanaume ni Sunnah amuriwa. Na lau kama mwanamke atasimama kwenye safu ya wanaume, basi hilo litakuwa ni makruhu, na halifai kwa kipimo. Halafu isitoshe, mwanamke huyo alisimama peke yake nyuma ya safu kwa kuwa hakukuweko mwanamke mwingine wa kusimama naye, na lau kama angelikuweko, basi angelazimika kusimama pamoja naye, na hukmu yake ingelikuwa ni ya mwanamume anayeswali peke yake nyuma ya safu ya wenzake. [Majmu’u Al-Fataawaa (23/395)].
Ya tatu:
Ikiwa atasimama peke yake kwa sababu ya udhuru, Swalaah itaswihi na kama si hivyo, itabatilika. Ni kauli ya Al-Hasan Al-Baswriy na Hanafi. Imekhitariwa na Sheikh wa Uislamu na mwanafunzi wake Ibn Al-Qayyim, na imetiliwa nguvu na Ibn ‘Uthaymiyn. [Al-Badaai-’i (1/218), Al-Inswaaf (2/289), Majmu’u Al-Fataawaa (23/396), I’ilaam Al-Muwaqqi’iyna (2/41), Tahdhiyb As Sunan (2/266-Al’Awn) na Al-Mumti’i (4/383)].
Hoja yao ni dalili za kauli ya pili lakini wamesema kwamba ukanushi wa kuswihi hauwi isipokuwa kwa kitendo kilichoharamishwa, au kwa kuacha wajibu. Na qaaidah inasema: Wajibu haupo kwa kushindwa.
Ninasema: “Huenda hii ndio kauli inayokubalika zaidi, kisha kauli ya kwanza. Allaah Ndiye Mjuzi zaidi.”
· Rai
“Ninalolihisi ndani ya nafsi yangu ni kuwa muradi wa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Anayeswali peke yake nyuma ya safu hana Swalaah)), ni kuwa anayekusudiwa ni yule mwenye kuswali nyuma ya safu za watu kivyake, na hapo Hadiyth itakuwa haina mushkil. Lakini sikupata yeyote aliyetangulia mwenye ufahamu huu (ingawa ufahamu huu una nguvu na unakubaliana na Uswuul za Sharia). Hivyo siwezi kuthubutu kulikata hilo. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
· Aliyeingia Akakuta Safu Zimejaa, Nini Afanye?
[Al-Badaai-’i (1/218), Fat-hul Qadiyr (1/309), Jawaahirul Ikliyl (1/80), Mughnil Muhtaaj (1/248), Al-Majmu’u (4/297), Kash-Shaaful Qinaa (1/490), Al-Inswaaf (2/289), Al-Mughniy (2/216), Al-Awsatw (4/185) na Al-Mumti’i (4/383)].
Mtu anatakiwa ajiepushe kuswali peke yake nyuma ya safu kiasi inavyowezekana ili asiingie kwenye ukaraha uliozungumzwa na Jamhuri. Swalaah itafaa kwa mujibu wa kauli ya Hanafi:
1- Akikuta nafasi katika safu ya mwisho atasimama hapo.
2- Akikuta nafasi kwenye safu ya mbele, atazipasua safu ili aifikie kwa kuwa waliotangulia wamefanya kosa la kutoijaza. Na kama hakupata nafasi isipokuwa kusimama pembeni ya imamu, basi atafanya hivyo. Dalili za hili zishaelezwa nyuma.
3- Kama hakuna mtu wa kusimama naye, je atamvuta mtu toka kwenye safu ili asimame naye?
Maulamaa wamekhitalifiana kuhusiana na hili. Hanafi, Hanbali na Ash-Shaafi’i wamelijuzisha. Pia imepokelewa toka kwa ‘Atwaa na An-Nakh’iy. Hii ni kwa vile kuna udharura wa kufanya hivyo. Ash-Shaafi’iy kalifungamanisha hilo na kuidadisi hali ya mvutwa kama ni mtu wa kukubali au la ili kuepusha mgogoro. Ahmad na Is-Haaq wanaona ni bora kumgusa ili arudi nyuma badala ya kumvuta.
Ninasema: “Asili ya kujuzu kumvuta mtu nyuma toka kwenye safu, ni Hadiyth ya Ubayya bin Ka’ab iliyoelezwa nyuma wakati alipomvuta mtu na kusimama mahala pake. Alipomaliza alimwambia: “Hakika hii ni amri toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwetu ya kwamba tumfuate..” [Hadiyth Swahiyh: Imeelezwa kwenye kipengele cha “Nani anayemfuata imamu?”]
Lakini kuna matahadharisho mengineyo yanakuja.
Maalik anaona ni makruhu mtu kumvuta mwingine akasema: Ataswali peke yake, na mwenye kuvutwa asikubali, na hili limepokelewa toka kwa Al-Awzaaiy, na ni chaguo la Sheikh wa Uislamu. Katika kuvuta huku, kuna matahadharisho ambayo ni:
1- Kutamletea tashwishi mvutwaji.
2- Mvutwaji atafanyiwa kosa kwa kutolewa sehemu aliyokwishaanza kuizoea.
3- Kutaacha nafasi kwenye safu na huenda hili likawa ni mlango wa kuikata safu. Makemeo juu ya hili yashaelezwa nyuma.
4- Safu nzima itafanyiwa kosa, kwa kuwa watasogea kwa ajili ya kujaza mwanya.
Ninasema: “Ni bora asimvute mtu, bali aswali peke yake kutokana na udhuru. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
043-Masuala Yanayohusiana Na Sifa Ya Swalaah Ya Jamaa
Alhidaaya.com [3]
· Sutrah Ya Imamu Ni Sutrah Kwa Maamuma
Jamhuri ya Maulamaa wanasema kwamba sutrah ya imamu ni sutrah kwa walio nyuma yake. Maana ya kusema hivi ni mambo mawili:
1- Kwamba kama hakikuingia kati ya imamu na sutrah kitu cha kuikatizia Swalaah, basi Swalaah ya maamuma ni sahihi na haiathiriwi na chochote chenye kupita katika baadhi ya safu zao wala kati yao na imamu. Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas inasema: “Nilielekea nikiwa nimepanda punda jike na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anaswali na watu Mina bila kuwepo ukuta. Nikapita mbele ya baadhi ya safu, nikashuka na kumwachilia punda aende zake kujilia. Nikaingia kwenye safu na hakuna yeyote aliyenilalamikia”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (76) na Muslim (504)].
2- Kwamba kikipita chenye kukatizia Swalaah kati ya imamu na sutrah yake, basi kitakata Swalaah yake na Swalaah yao. Imepokelewa toka kwa ‘Amri bin Shu’ayb toka kwa baba yake toka kwa babu yake akisema: “Tulishuka pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) toka pande za Adhakhar. Swalaah ikawadia, naye akaswali akielekea ukuta kama Qiblah chake. Sisi tulisimama nyuma yake, na mara akatokeza mnyama akipita mbele yake. Rasuli akawa anamzuia mpaka tumbo lake likaambata ukuta, na mnyama ikabidi apite nyuma yake”. [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (708), Ibn Maajah (3603) na Ahmad (2/196)].
Na lau kwamba sutrah yake si sutrah yao, basi kusingelikuweko tofauti kati ya kupita mnyama huyo mbele yake na nyuma yake. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
· Hukmu Ya Imamu Kusoma Basmalah "بسم الله " Kwa Sauti Katika Swalaah Ya Kusoma Kwa Sauti
Suala hili ni moja kati ya masuala yajulikanayo zaidi, yenye mikwamo ya kifiqhi, yenye kuzungumzwa zaidi kwenye midahalo na yenye kuandikwa sana kwenye vitabu. [Nasbu ar Raayah (1/336)].
Na kwa ajili hiyo, kundi la Maulamaa wameliandikia kiainishi na kipambanuzi suala hili. Kiufupi, Maulamaa wana kauli mbili katika suala hili:
Ya kwanza: Ni Sunnah kuisoma kimya. Ni kauli ya Hanbali na Aswhaabu Ar Ra’ay, na ni chaguo la Sheikh wa Uislamu. At-Tirmidhiy kasema: “Maulamaa wengi katika Maswahaba wakiwemo Abu Bakr, ‘Umar, ‘Uthmaan na ‘Aliy walikuwa wakilifanya hili pamoja na Taabi’iyna waliokuja baada yao. Ibn Al-Mundhir kalitaja toka kwa Ibn Mas-’oud, Ibn Az Zubayr na ‘Ammaar (Radhi za Allaah ziwe juu yao wote). Aidha, wamelisema hili akina Al-Awzaaiy, Ath-Thawriy na Ibn Al-Mubaarak. [Al-Mabsuutw (1/15), Al-Mughniy (1/345) na Kash-Shaaful Qinaa (1/335). Ninasema: “Ama imamu Maalik, yeye hasomi basmalah mwanzoni mwa Swalaah. Angalia Al-Mudawwanah (1/64)”].
Hoja yao ni:
1- Hadiyth ya Anas: “Kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Abu Bakr na ‘Umar, walikuwa wanafungua Swalaah kwa Al-Hamdu lil-Laahi Rabbi Al-‘Aalamiyna”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (743) na Muslim (399)].
Na katika riwaya ya Muslim toka kwake: “Niliswali pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Abu Bakr, ‘Umar na ‘Uthmaan, nami sikumsikia yeyote kati yao akisoma Bismil-Laahi Ar Rahmaan Ar Rahiym”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (399)].
Riwaya ya kwanza imehojiwa kwa kusemwa kuwa maana ya neno lake “wanafungua Swalaah kwa Al-Hamdu lil-Laahi Rabbi Al-‘Aalamiyna” ni Suwrat Al-Faatihah kabla ya Suwrah nyingine. Hapa basmalah haikanushwi wala haithibitishwi.
Ama riwaya ya pili, hii hata kama isnadi yake ni Swahiyh, lakini baadhi ya Maulamaa wameizungumzia kwa upande wa kwamba msimulizi kaichukulia riwaya ya kwanza hivyo, akakosea. Iliyohifadhiwa ni riwaya ya kwanza. [Angalia Fat-hul Baariy (2/266-267)].
2- Hadiyth ya ‘Aaishah isemayo: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiifungua Swalaah kwa takbiyr na kusoma “Al-Hamdu Lil-Laahi Rabbi Al-‘Aalamiyna”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (498)].
Wamesema: “Iko wazi kwamba basmalah haisomwi kwa sauti, na inaiunga mkono Hadiyth ya Anas”.
3-Yaliyosimuliwa toka kwa Ibn ‘Abdillaah bin Al-Mughaffal aliyesema: “Baba yangu alinisikia nikisema: Bismil Laahi Ar Rahmaan Ar Rahiym akaniambia: Uzushi, tahadhari na uzushi. Mimi sikumwona Swahaba yeyote wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ila alikuwa anachukia sana uzushi katika Uislamu. Mimi niliswali pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Abu Bakr, ‘Umar na ‘Uthmaan na sikumsikia yeyote kati yao akiitamka, basi nawe usiitamke. Ukiswali basi sema: “Al-Hamdu Lil-Laahi Rabbi Al ’Aalamiyna”. [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (244) na An-Nasaaiy (2/135)].
Imejibiwa kwamba ni Dhwa’iyf, haifai kutolewa dalili.
4- Ni Neno Lake Allaah ‘Azza wa Jalla katika Al-Hadiyth Al-Qudsiy:
((Nimeigawanya Swalaah kati Yangu na kati ya Mja Wangu nusu mbili, na Mja Wangu atapata ayaombayo. Akisema mja: Al-Hamdu Lil-Laahi Rabbi Al ’Aalamiyna, Allaah Ta’alaa Husema: Mja Wangu amenihimidi…)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (395), Abu Daawuud (821), At-Tirmidhiy (2953), An-Nasaaiy (2/135) na Ibn Maajah (838)]..
Imetolewa hoja na yule aliyesema kwamba basmalah haisomwi kabisa kwenye Swalaah.
5- Hapana shaka kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwa akiisoma kabisa kwa sauti, usiku au mchana, mara tano kila siku, akiwa safarini au mjini kwake. Haiwezekani akafanya hivyo kisha hilo likafichika kwa Makhalifa Waongofu au Maswahaba wengineo, au watu wa mji wake katika enzi hizo bora. [Zaadul Ma’ad (1/206-207)].
Ya pili: Ni Sunnah isomwe kwa sauti. Hili ni mashuhuri kwa Ash-Shaafi’iy. Hoja yake ni:
1- Aliyoyasimulia Na’iym Al-Mujmir akisema: “Niliswali nyuma ya Abu Hurayrah akasoma: Bismil Laahi Ar Rahmaan Ar Rahiym. Halafu akasoma Al-Faatihahh hadi ((غير المغضوب عليهم ولا الضالين )) akasema: Aamiyn, na watu wakaitikia Aamiyn. Na anasema kila anaposujudu: Allaahu Akbar. Na anaposimama toka kikao cha rakaa mbili husema: Allaahu Akbar. Na anapotoa tasliym husema: Naapa kwa Yule Ambaye Nafsi yangu iko Mkononi Mwake! Hakika mimi nawafananishieni Swalaah ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (2/134), Ahmad (2/497), Ibn Khuzaymah (499) na Ibn Hibaan (1797)]
Hili limejibiwa kwa kusemwa kuwa kuna uwezekano wa kuwa Abu Hurayrah amewafananishia Swalaah ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika sehemu kubwa ya Swalaah na si katika sehemu zote, pakizingatiwa kwamba kuna wengineo waliopokea toka kwa Na’iym toka kwa Abu Hurayrah bila kutaja basmalah. Hivyo Hadiyth haiko wazi ya kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisoma basmalah kwa sauti.
2- Hadiyth ya Qataadah aliyesema: “Anas aliulizwa: Vipi kilikuwa kisomo cha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)? Akasema: Kilikuwa ni “madda”, kisha akasoma بسم الله الرحمن الرحيم na anavuta الرحمن na anavuta الرحيم . [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (5046)].
Hili limejibiwa kwamba haliko wazi kama Anas alilisikia hili toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika Swalaah, bali lililothibiti toka kwake ni kuwa hakuwa akiisoma kwa sauti kama ilivyotangulia.
3- Yaliyosimuliwa toka kwa Ibn ‘Abbaas: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiifungua Swalaah yake kwa بسم الله الرحمن الرحيم . [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (245) na wengineo. Angalia Hadiyth nyinginezo katika mlango wake ambazo hazikosi maneno katika Nasbu Ar Raayah (1/328)].
Imejibiwa, kwa kuwa ni Dhwa’iyf, haifai kwa hoja. Kisha upo uwezekano ndani yake wa kusomwa kwa siri au kwa sauti.
· Lenye Nguvu Zaidi
Kutokana na hoja zilizotangulia, tunaona kwamba hakuna katika kuisoma basmalah kwa sauti katika Swalaah, Hadiyth Swahiyh bayana yenye uzito sawa wa kidalili na Hadiyth ya Anas ya kutosomwa kwa sauti. Hivyo basi, ni bora kuisoma kimya kimya. Lakini pamoja na hivyo, la sawa zaidi ni kuwa kinachosomwa kimya kimya, kinaweza kuruhusiwa kusomwa kwa sauti kwa ajili ya maslaha muhimu kama vile imamu kuwafundisha maamuma. Pia mtu anaweza kuacha lililo bora zaidi kwa ajili ya kuziunganisha nyoyo na kuliunganisha neno kwa ajili ya kuchelea watu kulikimbia lenye maslaha kwao. [Majmuu Al-Fataawaa (22/436). Angalia Nasbu Ar Raayah (1/328)].
Angalizo:
Ni vyema ijulikane kwamba makhitalifiano katika suala hili si makubwa sana. Haitakikani kwa watu kuwa na ukereketwa wa kupita kiasi chake. Na kwa ajili hiyo, Sheikh wa Uislamu amesema: “Ama kuwa na kasumba na suala hili na mengineyo, hilo ni katika nembo za mifarakano na makhitilafiano ambayo tumekatazwa. Mwenye kulipigia debe hilo, basi huyo anazidi kuzisimika bendera za kuufarikisha umma kwa suala hili ambalo ni moja kati ya masuala yenye makhitilafiano madogo mno. Ni kazi tu ya Shaytwaan anayechochea watu wabebe bendera za mifarakano”. [Majmuu Al-Fataawaa (22/405)].
· Maamuma Kusoma Al-Faatihahh Nyuma Ya Imamu
Hili lina kauli tatu za Maulamaa:
Ya kwanza: Maamuma hasomi si katika Swalaah ya kusoma kimya kimya wala Swalaah ya kusoma kwa sauti. Ni kauli ya Abu Haniyfah na masahibu zake. [Al-Mabsuutw (1/200) na Al-Badaai-’i (1/103)]. Dalili yao ni:
1- Yaliyosimuliwa toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Mwenye imamu, basi kisomo cha imamu ni kisomo kwake)). [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Maajah (850) na Ahmad (14166). Fat-hul Qadiyr (1/339)].
Kwa kuwa ni Dhwa’iyf kwa pande zake zote, haifai kwa dalili.
2- Hadiyth ya ‘Imraan bin Haswiyn ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali Adhuhuri, kisha mtu mmoja akawa anasoma nyuma yake: سبح اسم ربك الأعلى. Alipomaliza aliuliza: Nani aliyesoma? Au: Msomaji ni nani kati yenu? Mtu yule akasema: ((Hakika nilidhani kwamba baadhi yenu ni wenye kunipokonya Suwrah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (398), An-Nasaaiy (917) na Abu Daawuud (828)].
Lengo la kusema hivi ni kukataza kunyanyua sauti wakati maamuma anaposoma Suwarah nyuma ya imamu katika Swalaah ya kusoma kwa sauti ya chini kama inavyoonekana!!.
3- Kusoma Al-Faatihahh si wajibu kimsingi – kwa upande wao - hivyo kwa maamuma ndio kabisa!! Hili linapingwa kabisa kama ilivyo wazi.
Ya pili:
Ataisoma katika Swalaah ya kimya kimya na si katika Swalaah ya kusoma kwa sauti. Ni kauli ya Jamhuri na chaguo la Sheikh wa Uislamu. [Al-Mughniy (1/330), Kash-Shaaful Qinaa (1/464), Mawaahibul Jaliyl (1/537) na Majmu’u Al-Fataawaa].
Hoja ya kauli hii ni:
1- Neno Lake Ta’alaa:
((وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُوا لَهُ وَأَنصِتُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ))
((Na inaposomwa Qur-aan, basi isikilizeni kwa makini na bakieni kimya (mzingatie) ili mpate kurehemewa)). [Al-A’araaf (7:204)].
2- Hadiyth: ((Hakika amefanywa imamu ili afuatwe. Anapopiga takbiyr basi nanyi pigeni takbiyr [Na anaposoma, basi nyamazeni] )). [Wahafidhi wakuu wa Hadiyth wameitia doa ziada hii: Muslim kaifanyia “ikhraaj” (404), Abu Daawuud (603), na An-Nasaaiy (931)].
3- Hadiyth ya Ibn Shihaab toka kwa Ibn Ukaymah toka kwa Abu Hurayrah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimaliza Swalaah ambayo alisoma kwa sauti kisha akauliza: ((Je, mmoja wenu kasoma nami hivi punde?)) Akasema mtu mmoja: Ndio, ee Rasuli wa Allaah. Akasema: ((Mimi nasema, kwa nini napokonywa kisomo?)). Akasema: Watu wakaacha kusoma pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika Swalaah ambazo Rasuli anasoma kwa sauti wakati walipolisikia hilo toka kwake. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (826), At-Tirmidhiy (312), An-Nasaaiy (2/140) na Ibn Maajah (848)].
Baadhi yao wamesema: Hadiyth hii ni yenye kunasikhi kisomo nyuma ya imamu katika Swalaah za kusoma kwa sauti!!
4- Hadiyth: ((Mwenye imamu, basi kisomo cha imamu ni kisomo kwake)). [Hadiyth Dhwa’iyf:Tumeitaja nyuma kidogo].
Wamesema: Muradi ni kwa Swalaah za kusoma kwa sauti.
Ya tatu:
Ni lazima aisome katika Swalaah ya kimya kimya na katika Swalaah ya kusoma kwa sauti. Ni kauli ya Ash-Shaafi’iy – katika madhehebu mapya - na wafuasi wake na Ibn Hazm. Imekhitariwa na Ash-Shawkaaniy na Ibn ‘Uthaymiyn. [Al-Ummu (1/93), Al-Majmu’u (3/322), Al-Muhalla (3/236), Al-Furu’u (1/428), Naylul Awtwaar (2/250) na Al-Mumti’i (4/247)].
Kauli hii ndiyo yenye nguvu zaidi kutokana na dalili zifuatazo:
1- Hadiyth ya ‘Ubaadah bin Swaamit ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hana Swalaah asiyesoma Faatihahtul Kitaab)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (756) na Muslim (394)].
2- Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba kasema: ((Mwenye kuswali Swalaah yoyote bila kusoma Ummul Qur-aan, basi Swalaah hiyo ni pungufu, -mara tatu- haikutimu)). Abu Hurayrah akaulizwa: Hata tukiwa nyuma ya imamu? Akasema: Isome katika nafsi yako”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (395), Abu Daawuud (821), At-Tirmidhiy (2953), An-Nasaaiy (2/135) na Ibn Maajah (838)].
Hadiyth hizi mbili zinauweka ujumuishi wa Aayah Tukufu na Hadiyth: ((Na anaposoma, basi nyamazeni)) katika umahususi isipokuwa maamuma kusoma Al-Faatihahh. Hii ni pamoja na kuwa ziada ya ((Na anaposoma, basi nyamazeni)), ni katika ziada ambayo wahafidhi wakubwa wa Hadiyth wamekhitalifiana kwa upande wa usahihi wake. Abu Daawuud kasema: “Haikuhifadhiwa”. Hivyo hivyo kasema Ibn Mu’iyn, Abu Haatim Ar-Raaziy, Ad-daaraqutwniy na Abu ‘Aliy An-Niysaabuuriy. Kukubaliana wahafidhi wote hawa juu ya udhwa’iyf wake, kunatangulizwa juu ya uSwahiyh wake na hususan panapozingatiwa kwamba hakuna Sanad Swahiyh iliyosimuliwa. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi. [Sharhu Muslim cha An-Nawawiy (4/123). Chapa ya Ihyaau At-Turaath Al’Arabiy].
Kinachotilia nguvu uainisho na ubainisho huu ni:
3- Hadiyth ya ‘Ubaadah bin As-Swaamit akisema: “Tulikuwa nyuma ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika Swalaah ya Alfajiri. Rasuli wa Allaah akasoma, na kisomo kikawa kizito kwake. Alipomaliza alisema: ((Je, nyinyi mnasoma nyuma ya imamu wenu?)). Tukasema: Na’am, lakini haraka haraka ee Rasuli wa Allaah. Akasema: ((Msifanye isipokuwa Faatihahtul Kitaab, kwani hana Swalaah asiyeisoma)). [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (823), Al-Bukhaariy katika mlango wa “Sehemu ya kisomo” (63,64), At-Tirmidhiy (311) na wengineo].
4- Imepokelewa toka kwa mtu mmoja katika Maswahaba wa Rasuli akisema: “Amesema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Huenda nyinyi mnasoma nyuma ya imamu, na imamu anasoma?)) Wakasema: Ni kweli tunafanya hivyo. Akasema: ((Basi msifanye isipokuwa kama mmoja wenu anasoma Ummul Kitaab)). Au alisema: ((Faatihahtul Kitaab)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (5/60), Al-Bukhaariy (63) katika mlango wa “Sehemu ya kisomo” na Al-Bayhaqiy (2/166)].
5- Ama yale waliyodai ya kwamba Hadiyth ya Abu Hurayrah imezinasikhi Hadiyth zenye kuamuru kusoma, basi Al-Haazimiy naye katika kitabu cha “Al-I’itibaar” kurasa za 72-75, amedai kinyume chake kwa kuzifanya Hadiyth wajibishi ni zenye kuzinasikhi Hadiyth katazishi. Na kiukweli ni kuwa hakuna dalili yoyote kuhusiana na hili au lile, bali lililo wajibu ni kurejea kwenye qaaidah za kukusanya (Al-Jam’u) au umilishi (At-Tarjiyh). Hii ni juu ya kwamba kauli yake: “Watu wakaacha kusoma katika pale aliposoma kwa sauti” imedarijiwa toka kauli ya Az-Zuhriy kama ilivyo katika riwaya ya Ahmad (2/240) na wengineo. Al-Bukhaariy amekubaliana na hili katika kitabu chake cha Taarikhuhu pamoja na Abu Daawuud, Ya’aquub bin Yuusuf, Adh-Dhahliy, Al-Khattwaabiy na wengineo. An-Nawawiy kasema: “Hili halina khilafu kabisa kati yao”.
Ninasema: “Ikiwa ni hivyo, basi hakuna hoja tena, na mapingamizi yote yameanguka. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi”.
· Ni Wakati Gani Maamuma Anasoma Al-Faatihahh Nyuma Ya Imamu Wake?
[Naylul Awtwaar (2/251) chapa ya Al-Hadiyth kwa mabadilisho kidogo].
Tushajua kwamba kusoma Al-Faatihahh ni nguzo ya lazima katika kila rakaa sawasawa kwa imamu, kwa anayeswali peke yake na kwa maamuma. Hivyo basi, ni wakati gani maamuma ataisoma katika Swalaah ya kisomo cha sauti? Baadhi wamesema ni pale anaponyamaza imamu kati ya Al-Faatihahh na Suwrah. Wengine wamesema ataisoma nyuma ya imamu Aayah baada ya Aayah, na hili ni bora zaidi kwa kuwa isti’aadhah (أعوذ بالله من الشيطان الرجيم) ambayo mahala pake ni baada ya takbiyr ya kuhirimia Swalaah haitocheleweshwa, na pia haitorudiwa tena wakati mtu anapotaka kusoma Al-Faatihahh ikiwa aliileta isti’aadhah mahala pake mwanzoni, na akaichelewesha Al-Faatihahh mpaka pale imamu atakaposoma Suwrah. Isitoshe, itamtosheleza “Aamiyn” moja tu wakati yeye na imamu wanapomaliza kusoma Al-Faatihahh.
· Kuitikia “Aamiyn” Kwa Sauti Kwa Imamu Na Maamuma Katika Swalaah Ya Kisomo Cha Sauti
Imepokelewa toka kwa Abu Hurayra kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Imamu akisema “Aamiyn” basi nanyi semeni “Aamiyn”, kwani yeyote ambaye “Aamiyn” yake itawafikiana na “Aamiyn” ya Malaika, ataghufiriwa madhambi yake yaliyotangulia)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (870) na Muslim (410)].
Imepokelewa toka kwa Waael bin Hujar akisema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisoma: غير المغضوب عليهم ولا الضالين akasema: Aamiyn, na akaivuta kwayo sauti yake”. [Hadiyth Swahiyh kwa Sanad tofauti: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (248), Abu Daawuud (932), Ahmad (4/315) na wengineo, nayo ina Sanad tofauti].
At-Tirmidhiy kasema: “Hivi ndivyo walivyosema Maulamaa wengi katika Maswahaba wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Taabi’iyna na waliofuata baada yao. Wanaona mwanamume anyanyue sauti yake kwa “Aamiyn” na asiifiche. Haya pia ndiyo wayasemayo akina Ash-Shaafi’iy, Ahmad na Is-Haaq”.
Na imepokelewa toka kwa Ibn Jariyj toka kwa ‘Atwaa akisema: “Nilimwambia: Je, Ibn Az-Zubayr alikuwa akiitikia “Aamiyn” baada ya Al-Faatihahh? Akasema: Na’am, na walio nyuma yake pia mpaka Msikiti hurindima”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdul Razzaaq (2640) na Ash-Shaafi’iy kama ilivyo kwenye Musnadi wake (230)].
· Je, Maamuma Ataitikia “Aamiyn” Sambamba Na Imamu Au Baada Yake?
Baadhi ya Maulamaa wanaona kwamba maamuma asiitikie ila baada ya kuitikia imamu wake kutokana na mwonekano wa Hadiyth isemayo: ((Hakika si jinginelo, imamu amefanywa kuwa imamu ili afuatwe)). Na Hadiyth isemayo: ((Imamu akiitikia “Aamiyn”, nanyi itikieni “Aamiyn”)).
Lakini kauli yenye nguvu ni kuitikia maamuma baada ya imamu kusema ولا الضالين kwa kuwa hili limekuja wazi. Katika Hadiyth ya Abu Muusa Al-Ash’ariy, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Akipiga takbiyr, nanyi pigeni takbiyr, na akisema غير المغضوب عليهم ولا الضالين basi semeni: “Aamiyn, Allaah Atakupendeni)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (404), Abu Daawuud (972), An-Nasaaiy (2/196) na Ibn Maajah (901)].
Na hii pia ni kwa ajili ya kwenda pamoja kwa “Aamiyn” ya imamu, maamuma na Malaika, na hapo wakapata maghfirah kwa Idhni ya Allaah Mtukufu.
· Ni Karaha Imamu Kurefusha Swalaah Kama Itakuwa Ni Uzito Kwa Baadhi Ya Maamuma
Imepokelewa toka kwa Abu Mas-’oud akisema: “Mtu mmoja alisema: Ee Rasuli wa Allaah! Hakika mimi ninajichelewesha sana na Swalaah ya Alfajiri kwa kuwa fulani huirefusha sana. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akakasirika, sikumwona akiwa ameghadhibika sehemu yoyote kama alivyokuwa ameghadhibika siku hiyo. Kisha akasema: ((Enyi watu! Hakika miongoni mwenu wapo wenye kuwakimbiza watu. Basi yeyote atakayeswalisha watu, basi afupishe Swalaah, kwani nyuma yake yuko mdhoofu, mzee na mwenye jambo linalomsubiri)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (704) na Muslim (466)].
Na mtu yule aliposwali nyuma ya Mu’aadh na Mu’aadh akasoma Al-Baqarah au An-Nisaai, alikwenda kulalamika kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Rasuli akasema: ((Ee Mu’aadh! Je, unawakimbiza watu wewe? –mara tatu- Kwa nini usiswalishe kwa سبح اسم ربك na والشمس وضحاها na والليل إذا يغشى )). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (705) na Muslim (465)].
Ninasema: “Na hii ni kama inakuwa ni uzito kwa baadhi ya maamuma. Ikiwa imamu atajua kwamba wameridhika na urefushaji, basi hakuna ukaraha. Makusudio kiujumla, ni imamu kuchunga hali ya maamuma wake. Katika Hadiyth ya Ibn ‘Umar ni kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akituamuru kukhafifisha Swalaah, naye hutuswalisha kwa kusoma As-Swaaffaat.” [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (2/95), Ahmad (2/26) na wengineo].
Imepokelewa toka kwa Jaabir bin Samura akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali Swalaah kama mnavyoswali Swalaah zenu hivi leo, lakini yeye alikuwa akikhafifisha. Swalaah yake ilikuwa ni nyepesi zaidi kuliko Swalaah yenu. Alikuwa anasoma katika Swalaah ya Alfajiri Al-Waaqiah au Suwrah nyinginezo mfano wake”. [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (5/104), Ibn Khuzaymah (531), ‘Abdul Razzaaaq (2720) na wengineo].
Ibn Mas-’oud amezitaja Suwrah ishirini za Al-Mufasswal. Anasema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anakutanisha kati yake Suwrah mbili katika kila rakaa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (775) na Muslim (722)].
Hivyo basi, kidhibiti cha kurefusha au kufupisha Swalaah ni hali ya maamuma na ridhaa yao, pamoja na kuitimiliza Swalaah bila ya kupunguza nguzo yake yoyote. Anas amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiifupisha Swalaah na kuitimiliza”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (706) na Muslim (469)].
Na anasema tena: “Sikuswali kamwe nyuma ya imamu yeyote mwenye kukhafifisha zaidi na mwenye kuitimiliza Swalaah zaidi kuliko Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na hakika alikuwa anaposikia mtoto analia, hukhafifisha kuchelea mama yake kubabaika”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (708) na Muslim (469)].
· Kumkumbusha Imamu Kama Kisomo Kitamkanganya
Kama kisomo kitamkanganya imamu, basi maamuma ana wajibu wa kumkumbusha. Jamhuri imelipendelea hilo kutokana na Hadiyth ya Al-Masuur bin Yaziyd Al-Asadiy Al-Maalikiy aliyesema: “Nilimshuhudia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisoma kwenye Swalaah, kisha akaacha kitu hakukisoma. Mtu mmoja akamwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Umeacha Aayah kadha wa kadha. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: ((Mbona usinikumbushe?!)). [Hadiyth Hasan kwa mwega wa nyingine: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (907), Al-Bukhaariy katika “Sehemu ya Kisomo” (194) na Ibn Khuzaymah (1648). Ina Hadiyth mwenza].
Hili pia linatolewa ushahidi na Hadiyth ya Ibn ‘Umar ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali Swalaah ambapo alisoma na kutatizikiwa. Alipomaliza alimuuliza Ubayya: ((Umeswali nasi?)) Akajibu: Na’am. Akamwambia: ((Nini kilikuzuia?)). [Hadiyth Hasan kwa mwega wa nyingine: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (907), Ibn Hibaan (1/316-Ihsaan) kwa Sanad Hasan. Abu Haatim ameiweka sawa irsali yake (1/77), na inatolewa ushahidi na iliyo kabla yake].
· Angalizo
Imamu akikosea katika usomaji, haitakikani kumrekebisha isipokuwa kama kosa litakuwa ni lenye kubadili maana. Imepokelewa toka kwa Ubayya bin Ka’ab ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: ((Mimi nimesomeshwa Qur-aan kwa lahaja saba, hakuna kati yake isipokuwa ni bainifu na toshelezi. Nikisema: Ghafuwran Rahiyman, au nikasema: Samiy-’an ‘Aliyman, au nikasema: ‘Aliyman Samiy-’an, basi Allaah Yuko hivyo, madhali Aayah ya adhabu haikumaliziwa kwa rahma, au Aayah ya rahma kwa adhabu)). [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (5/41, 51), Abu Daawuud (1477) na Adh-dwiyaau katika Al-Mukhtaarah (1173)].
· Ni Karaha Kwa Maamuma Kufanyiana Tashwishi Kwa Kisomo Na Takbiyr
Imepokelewa toka kwa Abu Sa’iyd akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikaaa ‘itikaaf Msikitini akawasikia wakisoma kwa sauti. Akafunua pazia na kuwaambia: ((Jueni kwamba kila mmoja wenu ni mwenye kumnong’oneza Mola wake, basi msiudhiane nyinyi kwa nyinyi, wala baadhi yenu wasisome kwa sauti za juu zaidi kuliko wenzao.)) Au akasema: ((Katika Swalaah)). [Hadiyth Swahiyh Bitwuruqihi: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1332), Ahmad (3/94) na wengineo. Angalia As-Swahiyhah (1597, 1603)].
Hadiyth ya ‘Imraan bin Haswiyn imeelezwa katika milango iliyopita kuhusiana na mtu aliyesoma nyuma yake سبح اسم ربك الاعلى , na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: ((Hakika nilidhani baadhi yenu watanipokonya Suwrah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (398) na wengineo. Imeelezwa nyuma kidogo].
· Wajibu Wa Kumfuata Imamu Na Uharamu Wa Kumtangulia
Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah akisema: ((Hakika si jinginelo, imamu amewekwa ili afuatwe. Akipiga takbiyr, basi nanyi pigeni takbiyr, akirukuu nanyi rukuuni, na akisema: Sami’a Allaahu liman hamidah, basi semeni: Rabbaanaa walakal hamdu, akisujudu nanyi sujuduni. Na akiswali kwa kukaa, nanyi nyote swalini kwa kukaa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (734) na Muslim (414, 416)].
Na katika tamshi la Muslim: ((Msimtangulie imamu, akipiga takbiyr basi pigeni takbiyr…)). Hadiyth
Na imepokelewa vile vile toka kwa Abu Hurayrah ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hivi haogopi mmoja wenu akinyanyua kichwa chake kabla ya imamu, Allaah kukigeuza kichwa chake kuwa cha punda, au Allaah kuifanya sura yake sura ya punda?!)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (691) na Muslim (427)].
Hadiyth hizi zinaonyesha kwamba ni haramu kumtangulia imamu katika Swalaah. Jamhuri wanasema kwamba Swalaah ya mwenye kumtangulia imamu ni sahihi lakini anakuwa ni mwenye kupata madhambi. Ahmad na Ahlu Adh-Dhwaahir wamesema kwamba Swalaah yake itabatilika. Pia Ibn ‘Umar kasema hivyo hivyo. [Fat-hul Baariy (2/215)].
· Pia Haijuzu Kwenda Naye Sambamba
Imepokelewa na Al-Barraai akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaposema: Sami’a Allaahu liman hamidah, hainamishi yeyote kati yetu mgongo wake mpaka Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) awe ameteremka na kusujudu, kisha tunaporomoka kusujudu baada yake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (690) na Muslim (474)].
Ama kuachwa nyuma na imamu, ikiwa itakuwa kwa udhuru kama ugonjwa na mfano wake, basi hakuna ubaya. Na kama mtu atafanya makusudi kujichelewesha, basi inakuwa ni makruhu. Baadhi ya Maulamaa wamesema kuwa ikiwa ataachwa na imamu kwa zaidi ya nguzo moja, basi Swalaah yake ni batili kutokana na ujumuishi wa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Hakika si jinginelo, imamu amewekwa ili afuatwe)). Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
· Je, Imamu Atafuatwa Kama Kazidisha Katika Swalaah?
Ni kama imamu kusahau akaenda rakaa ya tano na maamuma wakampigia tasbiyh asiwajali akiwa na uhakika kwamba hakusahau. Kwa hili, Sheikh wa Uislamu amesema: “Ikiwa watasimama pamoja naye bila kujua, basi Swalaah zao hazitabatilika. Lakini ikiwa watajua, basi haitakikani kumfuata, bali watamsubiri mpaka atakapokuja kutoa tasliym pamoja nao, au watatoa tasliym kabla yake, lakini kumsubiri ni bora zaidi.”
Ninasema:
“Mtu anaweza kusema: Watamfuata kutokana na ujumuishi wa dalili zenye kuamuru kumfuata, na kwa vile Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliponyanyuka kwenda rakaa ya tano, Maswahaba walisimama na Rasuli hakuwaamuru wakae kama imamu atasimama kwenda rakaa ya tano. Suala hapa ni ijtihaad tu, basi nawe tafiti. Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.”
Imamu Akiswali Kwa Kukaa Kutokana Na Udhuru
Tumeshaeleza nyuma kwamba inaswihi mtu mzima wa afya kumfuata mgonjwa. Ikiwa watu wenye kuweza kusimama wataswalishwa na imamu aliyekaa kutokana na udhuru, je watasimama au watakaa? Maulamaa wana kauli mbili katika suala hili:
Ya kwanza:
Ni lazima na wao pia waswali kwa kukaa. Ni kauli ya Ahmad, Is-Haaq, Al-Awzaa’iy, Ibn Al-Mundhir, Daawuud na Ibn Hazm. Ni kauli iliyosimuliwa toka kwa Jaabir, Abu Hurayrah, Usayd bin Khudhayr na Qays bin Fahd. Kwa upande wao, hakuna Swahaba yeyote aliyejulikana kwenda kinyume na hilo. [Al-Mughniy (2/162), Al-Furu’u (2/578), Al-Awsatw (4/205), Al-Muhalla na Naylul Awtwaar (3/203)].
Wametoa dalili kwa haya yafuatayo:
1- Hadiyth ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu Anha) akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali nyumbani kwake akishtakia kuumwa, akaswali kwa kukaa, na watu nyuma yake wakaswali kwa kukaa. Aliwaashiria wakae, na alipomaliza alisema: ((Hakika si jinginelo, imamu amewekwa ili afuatwe. Akirukuu nanyi rukuuni, na akinyanyuka, nanyi nyanyukeni. Na akiswali kwa kukaa, basi nanyi swalini kwa kukaa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (688) na Muslim (412)].Kuna Hadiyth ya Anas na Abu Hurayrah kama hii.
2- Hadiyth ya Jaabir aliyesema: “Rasuli wa Allaah alishtakia kuumwa tukaswali nyuma yake akiwa amekaa huku Abu Bakr akiwasikilizisha watu takbiyr yake. Akatugeukia akatuona tumesimama, akatuashiria, tukakaa na tukaswali nyuma yake kwa kukaa. Alipotoa tasliym alisema: ((Mmekurubia hivi punde kufanya kitendo cha Wafursi na Warumi. Wanawasimamia wafalme wao wakiwa wamekaa, basi msifanye. Wafateni maimamu wenu. Akiswali kwa kusimama, basi swalini kwa kusimama, na akiswali kwa kukaa basi nanyi swalini kwa kukaa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (413), Abu Daawuud (606), An-Nasaaiy (3/9) na Ibn Maajah (1240)].
Ya pili:
Haijuzu wao kuswali kwa kukaa, bali wataswali kwa kusimama. Kauli hii imeungwa mkono na wengi akiwemo Abu Haniyfah na Ash-Shaafi’iy. [Fat-hul Qadiyr (1/261), Al-Mabsuutw (1/218), Sharhul Ma’aaniy (1/406), Al-Ummu (1/151), Al-Majmu’u (4/164), Al-Ihkaam cha Ibn Daqiyq Al-’Abdu (1/225) na Twarhu At-Tathriyb (2/334)].
Dalili zao ni:
1- Kujibu dalili za wa kauli ya kwanza. Hapa wao wana njia tatu:
(a) Dai la kuwa Hadiyth hizo ni mansukh. Iliyozinasikhi ni Hadiyth ya ‘Aaishah kuhusu Abu Bakr kuwaswalisha watu wakati Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa mgonjwa. Hadiyth inasema: “Kisha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alijihisi kidogo nafuu, akatoka kwa ajili ya Swalaah ya Adhuhuri akiwa kati ya watu wawili, mmoja wao akiwa ‘Abbaas. Abu Bakr alikuwa anawaswalisha watu, na Abu Bakr alipomwona, alianza kurudi nyuma, na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwashiria kwamba asirudi na kusema: Niketisheni pembeni yake, nao wakamkalisha pembeni ya Abu Bakr. Abu Bakr akaanza kuswali akimfuata Rasuli (akiwa amesimama), na watu wakimfuata Abu Bakr, huku Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa amekaa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (687) na Muslim (418)].
Wamesema: “Na hili lilikuwa katika maradhi ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliyofia. Na Abu Bakr aliswali nyuma yake na watu wakiwa wamesimama, na hii inaonyesha kwamba hukmu ya mwanzo imenasikhiwa”.
Hili limejibiwa kwa njia hizi zifuatazo:
1- Ni kwamba Abu Bakr alikuwa ndiye imamu na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amefungamanishwa naye kama ilivyo kwenye baadhi ya riwaya. Hili limeandamizwa kwa kusemwa kwamba riwaya hizi lau kama zingelikuwa ni sahihi, basi lingechukuliwa kwa Swalaah nyingi, kwani Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliugua kwa muda wa siku kumi na mbili zenye jumla ya Swalaah 60.
2- Imamu Ahmad kasema: “Hakuna ndani yake hoja, kwa kuwa Abu Bakr alikuwa ameianza Swalaah akiwa amesimama. Na kama aliianza kwa kusimama, basi nao waliswali kwa kusimama. Akaashiria kuoanisha kati ya Hadiyth mbili kwa kuichukulia Hadiyth ya kwanza kwamba aliianza Swalaah kwa kukaa, na kuichukulia Hadiyth ya pili kwamba aliianza Swalaah kwa kusimama, halafu akaishiwa nguvu za kusimama akakaa. Anasema: Pale itakapowezekana kuoanisha kati ya Hadiyth, basi itakuwa ni wajibu, na naskh haitokuwepo.
Hili limeandamiziwa kwa kusemwa kwamba linajibiwa na yaliyoko kwenye Hadiyth ya Jaabir na ya ‘Aaishah ambapo Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaashiria Maswahaba wake wakae baada ya kuwa wameanza Swalaah kwa kusimama. Uandamizi huu umejibiwa kwa kusemwa kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa ameianza Swalaah kwa kukaa, na wao iliwalazimu wakae kwa kukaa kwake kinyume na kumfuata kwao Abu Bakr, kwani imamu wao huyu, aliianza Swalaah kwa kusimama, hivyo iliwalazimu kusimama, na wakaendelea kusimama.
3- Ni kwamba hamna ndani ya Hadiyth linaloashiria kwamba watu walikuwa wamesimama na Abu Bakr amekaa. Pengine wao ndio walikuwa wamekaa. Linaloonyesha hilo ni kwamba watu walikuwa wakiifuata Swalaah ya Abu Bakr, na kama wangekuwa wamesimama, basi wasingeliifuata Swalaah yake isipokuwa safu ya kwanza, kwa kuwa safu hii itakuwa imezikinga safu nyingine zisimwone. Haya kayasema Ibn Hazm.
Al-‘Iraaqiy kaliandamiza hili kwa njia kadhaa. Kati yake ni kwamba Maswahaba waliianza Swalaah kwa kusimama nyuma ya Abu Bakr. Na mwenye kudai kwamba waliibadili hali hii, basi na alete dalili. Na kama hilo lingefanyika, basi lingenukuliwa bila shaka. Kasema pia kwamba muradi wa wao kumfuata Abu Bakr, ni kuifuata sauti yake na si kwa kumwona.
4- Tukichukulia kwa nadharia tete kwamba imethibiti kuwa Maswahaba waliswali kwa kusimama nyuma ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) huku yeye akiwa amekaa, basi hilo haliarifu naskh, bali linaarifu kuruhusika hilo tu na kubainisha kwamba agizo la kuwaamuru wakae, ni agizo la Sunnah na si agizo la wajibu.
Hili limejibiwa kwa kusemwa: Hili linakataliwa. Amri haiwi ya Sunnah ikiwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameisisitizia kwa kuiashiria akiwa kwenye Swalaah, pia akaizungumzia kwa maneno ya wazi baada ya tasliym, na kisha akakifananisha kitendo chao na kitendo cha makafiri wa kimajusi. Vielelezo vyote hivi vinaonyesha kwamba katazo ni la uharamishaji.
(b) Dai la kuwa hilo linamhusu Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) peke yake. Na hili ndilo mashuhuri katika kauli ya Maalik na kundi la Maswahibu zake. [Kwa ajili ya hili, madhehebu ya Maalik yanasema kwamba Swalaah ya mwenye kuweza kusimama haiswihi asilani akiswalishwa na imamu aliyekaa. Angalia Al-Mudawwanah (1/81) na Mawaahibul Jaliyl (2/97)].
Wameitilia nguvu kwa yaliyosimuliwa kwa njia Marfu’u katika Hadiyth iliyofanyiwa “ikhraaj” na Ad-daaraqutwniy ambayo isnadi yake ni mbovu: ((Asiswalishe tena yeyote baada yangu kwa kukaa)), na kwamba hakuna Khalifa yeyote aliyeswalisha watu kwa kukaa!!
Limejibiwa hili kwamba asili ni kuwa umahususi unakuwa haupo mpaka iwepo dalili ya kuuthibitisha, na Hadiyth iliyosimuliwa ni Dhwa’iyf, haifai. Ama kutoa dalili ya Makhalifa kutoswalisha kwa kukaa, dalili hiyo ni dhwa’iyf zaidi, kwani kuacha kitu hakuonyeshi kwamba ni haramu, na huenda wao walitosheka kuwatanguliza watu wenye kuweza kusimama kuswalisha.
(c) Kuliawilisha neno lake: ((Basi swalini kwa kukaa)) wakisema: “Linachukuliwa kwa maana ya: Akikaa kwa tashah-hudi, basi nanyi kaeni kwa tashah-hudi!!
Limejibiwa kwamba huku ni kuipindisha habari na kuitoa nje ya ujumuishi wake bila dalili, na konteksi ya Hadiyth inamzuia aliyekwishafahamu kukimbilia kwenye taawiyl hii. Kati ya vyenye kuzuia, ni Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwapa ishara ya kukaa, na pia kuwaelezea sababu ya kujifananisha na hilo na makafiri wa kimajusi.
2- (Kati ya dalili za wenye kupinga maamuma kuswali kwa kukaa) ni kwamba kusimama ni nguzo kwa maamuma mwenye kuiweza. Haijuzu kuiacha kama zilivyo nguzo nyinginezo.
3- Kila mmoja miongoni mwao ana faradhi yake. Faradhi ya imamu ni kukaa, na faradhi ya maamuma ni kusimama.
· Hoja Yenye Nguvu Katika Suala Hili
Hakuna shaka yoyote kwamba kauli zote mbili zina uzito wa kuzingatika ingawa kauli ya kwanza ndiyo yenye uzito zaidi pamoja na kuzingatiwa hali ya imamu wakati anapoanza Swalaah. Kama ataianza kwa kukaa, basi ni lazima maamuma wakae, na kama ameianza kwa kusimama, itawalazimu kusimama. Lakini kama atalazimika kukaa kutokana na udhuru, je watakaa au watasimama? Hapa ni mahala pa ijtihaad, ingawa sababu ya kujifananisha na Wafursi na Warumi inatilia nguvu kukaa kwao.
Ama kukimbilia kwenye naskh, mimi hili silioni kama ni lenye nguvu kutokana na baadhi ya miono iliyotangulia, na kwa kuwa kulisema hilo kunahitajia naskh mara mbili. Ni kuwa asili katika hukmu ya mwenye kuweza kusimama ni kuwa asiswali kwa kukaa, na kusimama kumenasikhiwa kwenda kwenye kukaa kwa yule ambaye imamu wake ameswali kwa kukaa. Hivyo dai la naskh ya kukaa baada ya hapo linahukumia kufanyika naskh mara mbili, na hili liko mbali, bali linakwenda kinyume na qaaidah ya hukmu.
Na dai la naskh linajibiwa vile vile ya kwamba Maswahaba wanne walilifanya hilo – inasemekana sita - na hakuna yeyote aliyelikataa kwa mujibu wa inavyojulikana kwao mpaka Ibn Hibaan akasema: “Kwangu mimi ni aina ya Ijma’a ambayo wote wamekubaliana juu ya kujuzu kwake”.
· Kuibalighisha Takbiyr Ya Imamu Kama Itahitajika
Inajuzu mtu kuibalighisha takbiyr ya imamu ikiwa hilo litahitajika. Ni kama Msikiti kuwa mkubwa na sauti ya imamu kushindwa kufika kwenye safu za mwisho. Asili ya uhalali wa hili kama litahitajika, ni kitendo cha Abu Bakr wakati alipowaswalisha watu wakati wa maradhi ya kifo cha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama ilivyo kwenye Hadiyth ya ‘Aaishah isemayo: “Abu Bakr (Radhwiya Allaahu Anhu) akarudi nyuma, na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akakaa pembeni mwake, na Abu Bakr akiwabalighishia watu takbiyrah”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (712) na Muslim (418)].
Ama kubalighisha nyuma ya imamu bila haja, hilo ni bid-’a isiyopendeza kwa makubaliano ya maimamu. [Majmu’u Al-Fataawaa cha Sheikh wa Uislamu (23/403)]. Allaah Ndiye Mjuzi zaidi.
· Imamu Kumweka Mtu Mwingine Badali yake
Imamu akitokewa na udhuru ndani ya Swalaah kama kutengukwa na wudhuu au akakumbuka kwamba ana hadathi au mfano wa hilo, hapo itambidi amtangulize mtu kati ya maamuma atakayekamilisha Swalaah badala yake. Asili ya hili ni:
1- Hadiyth ya Sahl bin Sa’ad kuhusu kisa cha kwenda Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ukoo wa ‘Amri bin ‘Awf ili kusuluhisha kati yao, na Abu Bakr alipowaswalisha watu. Hadiyth inasema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaja na watu wanaswali. Kisha Abu Bakr akarudi nyuma mpaka akaingia sawa kwenye safu, na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatangulia akaswalisha…..”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (684) na Muslim (431)].
2- Hadiyth ya ‘Amr bin Maymoun kuhusiana na kisa cha kudungwa kisu ‘Umar akiwa ndani ya Swalaah. Hadiyth inasema: “ Na hakuchelewa ila alipiga takbiyr. Nikamsikia akisema: Ameniuwa – au amenila mbwa -, wakati alipomchoma. ’Umar akaukamata mkono wa ‘Abdul Rahman bin ‘Auf akamtanguliza. Na ‘Abdul Rahmaan akawaswalisha Swalaah khafifu..” [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (3700)].
Tukio hili lilikuwa mbele ya Maswahaba, nao waliridhia ‘Umar kumtanguliza ‘Abdul Rahmaan badala yake ili akamilishe nao Swalaah. Hakuna yeyote aliyelipinga hilo, na hivyo limekuwa ni Ijma’a.
3- Imepokelewa toka kwa Khalid bin Al-Lajlaaj ya kwamba siku moja ‘Umar bin Al-Khattwaab aliwaswalisha watu. Na alipokaa kwenye rakaa mbili za mwanzo, alirefusha kikao. Na alipoanza kunyanyuka, alirejea nyuma, akaukamata mkono wa mtu mmoja kati ya maamuma na kumtanguliza mahala pake. [Isnadi yake ni laini: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Al-Mundhir katika Al-Awsatw (4/241) na Al-Bayhaqiy (3/114)].
Akaeleza kwamba alimpitia mmoja wa wakeze, kisha akauhisi umajimaji ndani ya Swalaah.
4- Imepokelewa toka kwa Abu Raziyn akisema: “ ‘Aliy alituswalisha kisha damu ya pua ikamtoka. Akamkamata mtu akamtanguliza, naye akarudi nyuma”. [Isnadi yake ni Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdul Razzaaq (3670), Ibn Al-Mundhir (4/242) na Al-Bayhaqiy (3/114)].
· Hapa Kuna Mas-ala Mawili:
(a)
Aliyekamata mahala pa imamu, je ataitimiza Swalaah yake yeye au Swalaah ya imamu wake aliyemtanguliza? [Angalia Al-Muhalla cha Ibn Hazm (4/220)].
Faida ya mas-ala haya inadhihiri pale mwenye kuchukua mahala pa imamu atakapokuwa ametanguliwa kwa rakaa moja kwa mfano kisha akakamata nafasi ya imamu katika rakaa ya pili. Linaloonekana kuwa na nguvu zaidi ni kuwa ataikamilisha rakaa hiyo ya pili pamoja nao, kisha anapomaliza kusujudu sijdah mbili, atawaashiria wakae, halafu yeye atasimama kwenda rakaa yake ya pili. Anapoitimiza, atakaa na kusoma tashah-hudi, halafu atasimama, na maamuma watasimama pamoja naye ili kukamilisha rakaa mbili zilizosalia, au rakaa moja kama Swalaah ni ya Magharibi. Na ikiwa Swalaah ni ya Alfajiri, atafanya hivyo hivyo kwa kutoa tasliym pamoja nao.
Abu Haniyfah na Maalik wamesema: “ Bali atawaswalisha Swalaah ya imamu wa kwanza. Kuweka wazi hili ni kuwa ataswali nao rakaa yake ya kwanza (ambayo ni ya pili kwao), kisha atakaa tashah-hudi juu ya hukmu ya Swalaah ya imamu wa kwanza!! Kisha atakamilisha nao Swalaah.
Na hapa kuna angalizo. Ni kuwa imamu wa kwanza aliyetoka, uimamu wake ushabatilika na maamuma watakuwa wanamfuata imamu mpya, na imamu huyu haswali isipokuwa Swalaah yake mwenyewe. Hivyo watamfuata katika lile linalowalazimu, na hawatamfuata katika lile lisilowalazimu, na watasimama pale walipofikia na watamngoja mpaka afikie pale walipofikia wao, halafu hapo watamfuata. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
(b)
Imamu akiwaswalisha watu kisha akakumbuka kwamba alikuwa na hadathi baada ya kumaliza Swalaah
Jamhuri akiwemo Maalik, Ash-Shaafi’iy, Ahmad, Abu Thawr, Al-Mazniy na wengineo wamesema kwamba yeye ataswali tena lakini maamuma hawataswali. Lakini kundi jingine akiwemo Abu Haniyfah na Maswahibu zake, Ath-Thawriy na wengineo wamesema kwamba wote wataswali tena upya.
Kauli ya kwanza ya Jamhuri ndiyo yenye nguvu zaidi, nayo imesimuliwa toka kwa ‘Umar, mwanawe ‘Abdullah, ‘Uthmaan na ‘Aliy. [Al-Awswat cha Ibn Al-Mundhir (4/212)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
044-Hukmu Za Aliyetanguliwa
Alhidaaya.com [3]
· Kuipata Jamaa
Kuipata Jamaa kuko kwa aina mbili:
1- Kuipata fadhla ya Jamaa:
Hii hupatikana kwa kushirikiana maamuma na imamu katika sehemu ya Swalaah yake hata kama itakuwa ni katika kikao cha mwisho kabla ya tasliym. Hii ni kauli ya Jamhuri: Hanafi, Hanbali, Ash-Shaafi’iy na baadhi ya wafuasi wa Maalik. [Ibn ‘Aabidiyn (1/483), Ad-Dusuwqiy (1/320), Mughnil Muhtaaj (1/231) na Kash-Shaaful Qinaa (1/460)].
Hili ni sahihi kwa kuwa lau kama asingelipata fadhla ya Jamaa kwa hilo, basi angelizuiliwa kumfuata, kwa kuwa wakati huo inakuwa ni ziada bila faida. Hili linatiliwa nguvu na kauli ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inayosema: ((Mnapoisikia adhana, basi nendeni kwa miguu katika Swalaah. Kuweni watulivu na makini, na wala msifanye haraka. Mnachokipata kiswalini, na mnachokikosa kikamilisheni)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (636) na wengineo. Imeshatajwa nyuma].
Imepokelewa toka kwa mtu mmoja wa Madiynah akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisikia mchakato wa viatu vyangu akiwa kwenye sijdah. Alipomaliza kuswali aliuliza: ((Ni nani huyu niliyesikia mchakato wa viatu vyake?)) Nikasema: Ni mimi ee Mjumbe wa Allaah. Akasema: ((Umefanya nini?)). Akasema: Nimekukuta umesujudu, nami nikasujudu. Akasema: ((Hivyo hivyo fanyeni, lakini msiihesabu. Mwenye kunikuta nimerukuu, au nimesimama, au nimesujudu, basi awe pamoja nami katika hali niliyopo)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (1/284) kwa Sanad Swahiyh. Ina Hadiyth mwenza kwa At-Tirmidhiy (591) kwa Sanad Dhwa’iyf, na nyingine kwa Abu Daawuud].
Lakini thawabu zake zinakuwa chini ya thawabu za yule aliyeipata Swalaah tokea mwanzoni. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.
2- Kuipata hukmu ya Jamaa na matokeo yake:
Muradi wa hukmu ya Jamaa ni kuthibiti hukmu husishwa kwa kuzingatiwa kuwa yeye ni mwenye kumfuata imamu kama kusujudu naye kama alisahau kitu, au kuswali kwake Ijumaa rakaa mbili na mfano wa hivyo.
Kauli dhahiri zaidi ya Maulamaa ni kwamba hukmu ya Jamaa haithibiti ila kwa kuipata rakaa kamili pamoja na imamu [ juu ya mvutano mashuhuri kuhusu ni kipi hasa hupatikania kwacho rakaa. Litafafanuliwa hili, si mbali sana] kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Mwenye kuipata rakaa katika Swalaah, basi kaipata Swalaah)). [Hadiyth Swahiyh: Takhriyj yake ishaelezwa, nayo imepitishwa na Al-Bukhaariy na Muslim].
Hii ni kauli ya Maalik, na chaguo la Sheikh wa Uislamu. [Ad-Dusuwqiy (1/320) na Majmuu Al-Fataawaa (23/330, 331)].
· Kuipata Rakaa
Maulamaa wametofautiana kuhusiana na kiasi ambacho maamuma anakuwa ni mwenye kuhesabiwa kwamba ameipata rakaa pamoja na imamu wake katika kauli mbili mashuhuri:
Ya kwanza:
Rakaa hupatikana kwa kuiwahi rukuu pamoja na imamu
Hii ni kauli ya Jamhuri ya Maulamaa na wengineo. [Al-Mabsoutw (2/95), Fat-hul Qadiyr (1/483), Al-Mudawwanah, Al-Umm (1/135), Al-Majmu’u (4/111), Al-Mughniy (1/299), Al-Furuw’u (1/587), Twarhu At-Tathriyb (2/365), na Hukmu Man Adraka Ar Rukuw’u cha Asw-Swan-’aaniy].
Kauli kama hii kaisema Ibn ‘Umar, Ibn Mas-’oud, Zayd bin Thaabit na Maswahaba wengineo. Hoja ya kauli hii ni:
1- Hadiyth ya Abu Hurayrah ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwenye kuipata rakaa ya Swalaah, basi ameipata Swalaah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (850) na Muslim (607)]. Wamelichukulia tamshi la “rakaa” kwamba linakusudiwa rukuu.
2- Uchukulifu huu wameutilia nguvu kwa riwaya ya Ibn Khuzaymah kwa Hadiyth ya Abu Hurayrah kwa tamshi la: ((Mwenye kuipata rakaa ya Swalaah [kabla imamu hajanyoosha mgongo wake] basi ameipata)). [Munkari kwa tamko hili: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Khuzaymah (1595), Al-Bayhaqiy (2/89), Ad Daaraqutwniy (1/346) na Al-‘Uqayliy kwenye Adh-Dhwu’afaa (4/398). Ziada imefanywa katika maneno ya Az-Zuhriy, na Al-Bukhaariy kaifanyia “ikhraaj” katika Juz’u Al-Qira-ati ukurasa wa 47 kwa njia hiyo hiyo bila ziada].
Wamesema kwamba hili linaonyesha kuwa makusudio ya rakaa ni rukuu!!
3- Hadiyth Marfu’u iliyohadithiwa toka kwa Abu Hurayrah: ((Mkifika kwenye Swalaah nasi tumesujudu, basi sujuduni lakini msiihesabie kitu, na mwenye kuipata rakaa basi ameipata Swalaah)). [Hadiyth Munkari: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (893), Ad-daaraqutwniy (1/347), Al-Haakim (1/216) na Al-Bayhaqiy (2/89). Katika Sanad yake yuko Yahya bin Abu Sulaymaan. Al-Bukhaariy kasema: “Ni Hadiyth Munkari”. Abu Haatim kasema: “Ni Hadiyth Mudhwtwarib, haina nguvu”. Lakini Al-Albaaniy ameiimarisha katika Al-Irwaa (2/261) na Asw-Swahiyhah (1188) kwa vigezo visivyo imara].
4- Hadiyth ya Abu Bakrah ya kwamba alimwahi Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwenye rukuu, naye akarukuu kabla hajafika kwenye safu. Akalieleza hilo kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na Rasuli akamwambia: ((Allaah Akuzidishie pupa lakini usifanye tena)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (783) na wengineo].
Wamesema: Ni wazi kuwa rakaa ilihesabiwa, na kwa hivyo hakuamuriwa kuirejesha, na haiwezekani kwamba aliisoma Al-Faatihahh ndani yake. Ama neno lake: ((Lakini usifanye tena)), hilo ni katazo la kuingia kwenye Swalaah kabla ya kuifikia safu.
5- Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar akisema: “Ukija na imamu yuko kwenye rukuu, nawe ukaweka mikono yako juu ya magoti yako kabla hajanyanyua kichwa chake, basi umeipata”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (1/243) na Al-Bayhaqiy (2/90)].
6- Imepokelewa toka kwa Zayd bin Wahab akisema: “Nilitoka pamoja na ‘Abdullah bin Mas-’oud toka nyumbani kwake kwenda Msikitini. Tulipofika katikati ya Msikiti, imamu alirukuu, na ‘Abdullah akapiga takbiyr kisha akarukuu nami nikarukuu pamoja naye. Kisha tukajivuta mbele tukiwa kwenye rukuu mpaka tukaifikilia safu, na watu wakanyanyua vichwa vyao. Imamu alipomaliza Swalaah, nilisimama – nikidhani kwamba sikuipata rakaa - na ‘Abdullah akanikamata mkono, akanikalisha na kuniambia: Hakika umeipata”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (1/255), Atw-Twahaawiy (1/397) na Al-Bayhaqiy (2/90)].
7- Imepokelewa toka kwa Abu Umaamah bin Sahl akisema: “Nilimwona Zayd bin Thaabit ameingia Msikitini na watu wako kwenye rukuu. Akatembea hata asiweze kuifikia safu akiwa amerukuu. Akapiga takbiyr na kurukuu, kisha akajisogeza akiwa kwenye rukuu mpaka akafika kwenye safu”.
Na katika tamko jingine toka kwa Khaarijah bin Zayd: “ Kisha rakaa hiyo huhesabiwa, sawasawa akiifikia safu au hakuifikia”. [Hadiyth Swahiyh: Riwaya ya kwanza imefanyiwa “ikhraaj” na At-Twahaawiy (1/398), na ya pili imefanyiwa na Al-Bayhaqiy (2/91) na wengineo. Angalia Al-Irwaa (2/264)].
Ya pili:
Haihesabiwi rakaa ambayo aliyetanguliwa hakusoma Al-Faatihahh nyuma ya imamu.
Ni kauli ya Al-Bukhaariy na Ibn Hazm pamoja na Taqiyyu Ad Diyn As Subkiy ambaye ni katika wafuasi wa Ash-Shaafi’iy. Ash-Shawkaaniy, Al-‘Allaamah Al-Mu’allamiy Al-Yamaaniy na wengineo wameitilia nguvu kauli hii. [Al-Qiraa-at Khalfal Imaam (164), Al-Muhalla (3/243), Naylul Awtwaar (2/ ) na Wahal Yudriku Al Maamuum Ar rak-’at cha Al-Mu’allamiy (uk 43)].
Hoja zao ni:
1- Kauli ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Mnapoisikia adhana, basi nendeni kwenye Swalaah, na ni juu yenu kuwa watulivu na wastahivu, na wala msifanye haraka. Mlichokipata kiswalini, na kilichokupiteni basi kikamilisheni)). [Hadiyth Swahiyh: Imeshaelezwa nyuma].
Wamesema: Mwenye kuipata rukuu, basi ashapitwa na kisimamo na kisomo cha Al-Faatihahh, na vyote viwili ni faradhi ambayo Swalaah haitimii ila kwavyo. Na kauli ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inaamuru kuyalipa yaliyopita na kuyakamilisha. Hivyo haijuzu kukihusisha kitu katika hayo bila kuwepo kauli nyingine, na hakuna njia ya kupatikana kwake.
2- Ama Hadiyth isemayo: ((Mwenye kuipata rakaa katika Swalaah, basi ameipata Swalaah)), hii ni haki na hoja inayowarudi wenyewe. Kwa kuwa pamoja na hivyo, hakupomoki kukilipa ambacho mtu hakukipata katika Swalaah bila khilafu yoyote. Na katika Hadiyth hakuna kwamba mwenye kuipata rukuu anakuwa amekipata kisimamo.
Ninasema: “Wamelichukulia neno “rakaa” kwa maana ya rakaa kamili, na huu ndio uhalisia wa tamko.”
3- Ama nyongeza: “kabla imamu hajanyoosha mgongo wake”, hii haiswihi. Na ukomo wa jambo ni kuwa mmoja wa wasimulizi ilimpitikia dhana kwamba maana ya Hadiyth ni: “Mwenye kuipata rukuu pamoja na imamu, basi kaipata rakaa”, na hapo akaongeza ziada hii kwa ajili ya kubainisha zaidi kwa mujibu wa dhana yake. Baadhi yao wamejuzisha ya kuwa ziada hii ni ya Az Zuhriy ambayo imewakanganya baadhi ya wenye ufahamu mdogo.
4- Vile vile Hadiyth: ((Mkifika kwenye Swalaah nasi tumesujudu…)), Hadiyth hii ni Dhwa’iyf, haifai kwa hoja.
5- Ama Hadiyth ya Abiy Bakrah, wao hapo hawana hoja kabisa, kwa kuwa hakuna linalobainisha kwamba alitosheka na rakaa hiyo, na kwamba hakuilipa.
6- Ama athar kutoka kwa Maswahaba, hizo zinapingwa na kauli ya Abu Hurayrah isemayo: “Kwamba haihesabiwi rakaa mpaka asome Ummul Qur-aan”. Na kauli ya baadhi yao, si hoja kwa mwingine.
· Kauli Yenye Nguvu Zaidi
Baada ya kuzipitia dalili za makundi mawili, ninaloliona mimi ni kuwa hoja za Jamhuri, hoja kama hizi haziwezi kuturidhisha kuwa zina nguvu ya kutengua nguzo za kisimamo na kusoma Al-Faatihahh, kwa kuwa asili ni kubakia Hadiyth juu ya ujumuishi wake, na kuibeba dhima ya Swalaah kikamilifu. Na’am, hatupingi kuwa kauli ya kwamba mtu huipata rakaa ina nguvu kutokana na kuungwa mkono na kundi la Maswahaba Wasomi, na pia hatumlaumu yeyote mwenye kuona hivyo.
Ama mimi, bado ningali natafakuri. Lakini, naona kuwa mwenye kuingia akamkuta imamu amerukuu, basi atangoja mpaka aitadili, kisha atajiunga naye lakini hatohesabu chochote kwa ajili ya kuondokana na mvutano na kuwa salama na dini yake. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.
Faida Zinazohusiana Na Mas-ala Yaliyopita (Kwa Mujibu Wa Kauli Ya Jamhuri).
[1] Je, anaweza mtu kurukuu kabla ya kuifikia safu ili aipate rukuu?
Tumeshaeleza nyuma kwamba Abu Bakrah aliporukuuu kabla ya kuifikia safu, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia: ((Allaah Akuzidishie pupa lakini usifanye tena)). [Hadiyth Swahiyh: Imeshaelezwa nyuma kidogo].
Akamkataza asije kurukuu tena kabla ya kufika kwenye safu.
Ama Hadiyth ya ‘Abdullah bin Az Zubayr ya kwamba alisema juu ya mimbari: “ Akiingia mmoja wenu Msikitini na watu wamerukuu, basi arukuu wakati anapoingia, kisha ajisogeze akiwa kwenye rukuu mpaka aingie kwenye safu, kwani hilo ni Sunnah”, [Wapokezi wake wanaaminika: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Haakim (1/214), Ibn Khuzaymah (1571) na Al-Bayhaqiy (3/106) kupitia kwa Ibn Jariyj toka kwa ‘Atwaa. Na Ibn Jariyj huyu ni mdanganyifu, na kaitaja kuwa ni fulani toka kwa fulani (‘an-’anah) tukijua kwamba baadhi yao wanaichukulia riwaya yake toka kwa ‘Atwaa kama ni Mawswuul] tunakuta kwamba kuna maneno kidogo yaliyosemwa kuhusiana na Isnadi yake, na pia kuna mvutano kuhusiana na Umarfu’u wa neno lake “hilo ni Sunnah”. Isitoshe, vyovyote iwavyo, kauli hiyo haina uimara wowote wa kuikinza Hadiyth Swahiyh ya Abu Bakrah. Tunakubali kwamba hili limethibiti kwa kitendo cha Ibn Mas-’oud na wengineo, lakini pia katazo limethibiti toka kwa Maswahaba wengineo kama Abu Hurayrah na Ubayya bin Ka’ab.
Lililo bora ni mtu asirukuu kabla ya kuifikia safu kutokana na usahihi wa katazo la kufanya hivyo na udhaifu wa rai kinzani. Na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ashasema: ((Mlichokipata kiswalini, na kilichokupiteni basi kikamilisheni)). [Hadiyth Swahiyh: Imeshaelezwa nyuma kidogo].
[2] Je, ni sharti atulizane kwenye rukuu ili aipate rakaa? [Al-Mubdi’u (2/48), Al-Inswaaf (2/224) na Al-Majmuw’u (4/113)].
Baadhi ya Mafuqahaa wamesema kwamba ni lazima maamuma atulizane kwenye rukuu kabla imamu hajanyanyuka kupita mpaka wa rukuu yenye kutosheleza na akusanyike pamoja naye kwenye utulizano. Lakini wengi wamesema kwamba ataipata rakaa kwa kurukuu ikiwa yeye ametulizana, na wengine wameliachilia, hawakuweka sharti ya kutulizana.
[3] Akifanya shaka ya kuipata rukuu pamoja na imamu [Al-Inswaaf (2/224) na Al-Majmu’u (4/114)]
La sahihi ni kwamba haipati kwa kuwa kiasili haipo, na kwa kuwa hukmu ya kuhesabiwa rakaa, ni kwa kuipata rukuu kwa wenye kusema hivyo. Hivyo haipatikani ila kwa yakini.
Na imesemwa: Anakuwa ni mwenye kuipata, kwa kuwa asili ni kubakia rukuu ya imamu na kutoitadili mpaka ithibitike kuwa ameitadili kihakika.
[4] Je, inamtosheleza takbiyrah moja tu wakati wa kuiwahi rukuu? [Al-Inswaaf (2/224), Al-Majmu’u (4/112) na Qawaaid Ibn Rajab (Al-Qaaidah 18)]
Akimwahi imamu katika rukuu, basi takbiyrah moja tu itamtosheleza. Atapiga takbiyrah ya kuhirimia, nayo itamtosheleza na takbiyrah ya kurukuu. Na kama atapiga takbiyrah mbili; moja ya kuhirimia na nyingine ya kurukuu, basi itakuwa ni bora zaidi.
·Faida:
Ni lazima aipige takbiyrah ya kuhirimia akiwa amesimama. Na kama ataitamka takbiyrah yote au sehemu yake baada ya kuinama, basi haitofaa kwa kuwa atakuwa ameileta mahala pasipo pake, na kusimama pia ni nguzo ya Swalaah.
[5] Je, imamu atasubiri kama atahisi mtu anaingia ili aipate rukuu au Jamaa?
Inafaa kisharia kwa imamu kuirefusha zaidi rakaa ya kwanza kuliko ya pili ili watu waweze kuipata rakaa ya kwanza kama alivyokuwa akifanya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Imepokelewa toka kwa Abu Qataadah akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisoma katika rakaa mbili za mwanzo Ummul Kitaab na Suwrah mbili, na katika rakaa mbili za mwisho Faatihahtul Kitaab. Baadhi ya nyakati alikuwa akisoma kwa sauti tumsikie, na alikuwa akirefusha zaidi rakaa ya kwanza kuliko rakaa ya pili. Hivi hivi katika Alasiri, na hivi hivi Alfajiri [Tukapata uhakika kwamba anataka watu waipate rakaa ya kwanza]”.[ Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (776), Muslim (451) na Abu Daawuud (798) na nyongeza ni yake mwenyewe].
Imepokelewa toka kwa Abu Sa’iyd akisema: “ Swalaah ilikuwa inaqimiwa, kisha mtu akaenda Al-Baqiy na kufanya shughuli zake, halafu akatawadha, kisha akaja na kumkuta Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) bado yuko katika rakaa ya kwanza kutokana na kuirefusha”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (454), An-Nasaaiy (2/164) na Ibn Maajah (825)].
Na hapa ndipo walipoichukulia dalili baadhi ya wenye kusema kwamba rakaa inapatikana kwa kuiwahi rukuu. Dalili ni kuwa imamu akihisi kwamba kuna mtu anaingia naye yuko kwenye rukuu, basi amngoje ili aipate rakaa kama hilo halitowataabisha maamuma. Kalisema hili Ash-Shaafi’iy, Ahmad na Is-Haaq. [Al-Mughniy (1/236) na Naylul Awtwaar (3/166)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
045-Jamaa Zaidi Ya Moja Ndani Ya Msikiti Mmoja
Alhidaaya.com [3]
[Ibn ‘Aabidiyn (1/331), Al-Badaai-’i (1/153), Ad-Dusuuqiy (1/332), Al-Mughniy (2/180), Kash-Shaaful Qinaa (1/457), Al-Majmu’u (4/221), Al-Ummu (1/180) na Al-Awsatw (4/215)].
Msikiti haukosi kuwa na moja kati ya hali mbili:
[1] Msikiti ulioko kwenye soko, au barabarani au kwenye mapitio ya watu ambapo huingia humo kundi baada ya kundi. Msikiti huu inajuzu kukariri Jamaa bila ya ukaraha kwa makubaliano ya Maulamaa.
[2] Msikiti wenye menejimenti kamili na imamu mteule
Msikiti huu ndio mahala pa makhitalifiano kati ya Maulamaa. [Waliojuzisha kukariri Jamaa bila ya ukaraha ni ‘Atwaa, Al-Hasan, An-Nakh-’iy, Qataadah, Ahmad na Is-Haaq. Lakini Jamhuri wamelifanya makruhu zimazima ingawa wamevutana kati yao katika kuainisha ukaraha huo].
Kulihakiki hili kiuwazi ni kusema kuwa kukariri Jamaa kwenye Msikiti kama huu kuna hali mbili:
Hali ya kwanza:
Liwe jambo la kutokezea tu. Kiasili ni kwamba watu wote huswali pamoja na imamu mteule isipokuwa kwa yule aliyechelewa kwa udhuru. Wakati mwingine huingia watu wawili au watatu wakamkuta imamu ashatoa tasliym, na hawa wataruhusika kuswali Jamaa nyingine bila ya ukaraha. Asili ya hili ni Hadiyth ya Abu Sa’iyd Al-Khudriy ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwona mtu akiswali peke yake akasema: ((Je, hakuna mtu wa kumtolea swadaqah huyu akaswali pamoja naye?)). [Hadiyth Swahiyh kwa Sanad zake. Abu Daawuud (574), At-Tirmidhiy (220), Ahmad (3/5, 45) na wengineo].
Anas bin Maalik alilifanya hilo. Imepokelewa toka kwa Abu ‘Uthmaan akisema: “Alitujia Anas Ibn Maalik katika Msikiti wa Banu Tha-’alabah akauliza: Je, mshaswali? (Ilikuwa Swalaah ya Alfajiri) Tukasema: Ndio. Akamwambia mtu mmoja: Adhini. Akaadhini na kuqimu, kisha akaswali katika Jamaa”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (1/321), ‘Abdul Razzaaq (3417) na Ibn Al-Mundhir (4/215)].
Imepokelewa toka kwa Salamah bin Kuhayl ya kwamba Ibn Mas-’oud aliingia Msikitini akakuta watu washaswali. Akaswali Jamaa na ‘Al-Qamah, Al-Aswad na Masruwq. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (2/323) na Ibn Al-Mundhir. Ina Hadiyth mwenza kwa ‘Abdul Razzaaq (2884)].
Hakuna Swahaba yeyote aliyejulikana kwamba amewapinga, na Swalaah ya Jamaa kama tulivyoeleza nyuma, inaizidi kwa daraja Swalaah ya mtu peke yake.
Hali ya pili:
Liwe jambo lililozoeleka, la kila siku, lililokubaliwa. Ni kama kukubaliana kila kundi (wenye mapote tofauti au mfano wake) liswali upande fulani wa Msikiti, au katika wakati maalumu tofauti na kundi jingine. Hili bila shaka lina ukaraha kwa kuwa halikuweko wakati wa enzi ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wala kizazi cha mwanzo, linasambaratisha umoja kati ya Waislamu, na linawavuta watu kuwa wavivu na magoigoi wa kuhudhuria na kuiwahi Jamaa ya kwanza kwa kisingizio cha kusubiri Jamaa ya pili.
Hili ndilo angalizo na tamshi la Maalik na Ash-Shaafi’iy wakati walipochukizwa na kukariri Jamaa ndani ya Msikiti mmoja. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.
·Aliyeswali Peke Yake Kisha Akaja Msikitini Kwenye Jamaa, Basi Aswali Jamaa Na Watu
Hili ni jambo linalopendeza kwa ajili ya kupata fadhla ya Jamaa. Katika milango ya nyuma, tulielezea neno la Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa watu wawili ambao hawakuswali aliowaona nyuma ya safu. (walikuwa washaswali nyumbani walikofikia). Aliwaambia: ((Msifanye. Mkiswali nyumbani mlikofikia, kisha mkaja kwenye Msikiti wenye Jamaa, basi swalini pamoja nao, kwani kwenu hiyo ni Sunnah)). [Hadiyth Swahiyh: Imeelezewa mara nyingi].
Imepokelewa toka kwa Abu Dharri kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliniuliza: ((Utafanya nini ukiwa unatawaliwa na viongozi wanaochelewesha Swalaah na wakati wake, au wanaiua Swalaah na wakati wake?)) Nikasema: “Unaniamuru nini?” Akasema: ((Swali Swalaah katika wakati wake, na kama utaipata pamoja nao, basi swali, kwani hiyo ni Sunnah kwako)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (648). Imeshaelezewa nyuma].
Maulamaa wote wamekubaliana juu ya kupendeza kuiswali Swalaah mara nyingine kwa Jamaa. Wamelielezea hilo kwa uchambuzi kwenye vitabu tanzu. Kati ya hayo, wameitoa kando Swalaah ya Magharibi –Hanafi, Maalik na Hanbali- [Ibn ‘Aabidiyn (1/479), Al-Badaai-’i (1/287), Ad Dusuuqiy (1/320), Al-Mawaahib (2/84), Al-Mughniy (2/111), na Kash-Shaaful Qina’a (1/212)] wakisema kwamba hairejeshwi kwa kuwa ni Witri ya mchana, na pia Witri. Haya yashaelezewa kirefu nyuma.
· Ikiwa Ameswali Faradhi Kwa Jamaa, Je Ataswali Tena Kama Ataikuta Jamaa?
[Vitabu rejea vilivyotangulia pamoja na Al-Muhadh-dhab (1/102) na Asnaa Al-Matwaalib (1/212)].
Inavyoelekea ni kuwa hilo limesuniwa pia. Ash-Shaafi’iy na Hanbali wamelisema hili, kwa kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwaambia watu wale wawili: ((Mkiswali)), kunathibitisha kuswali mtu peke yake au kwa Jamaa, na kwa ujumuishi wa neno lake: ((kwani kwenu hiyo ni Sunnah)). Maalik amelikataa hilo la kuswali tena isipokuwa kama litafanyika kwenye Msikiti Mtakatifu wa Makkah, Msikiti wa Nabiy na Baytul Maqdis (Al-Masjid Al-Aqswaa) kutokana na ubora wa Misikiti hiyo. Kauli ya kuswali mara nyingine ndiyo yenye nguvu zaidi. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
046-Yanayofanyika Baada Ya Kumalizika Swalaah
Alhidaaya.com [3]
· Imamu Awaelekee Watu Baada Ya Kutoa Tasliym Na Akae Kidogo Kabla Hajaondoka
Imepokelewa toka kwa Samurah bin Jun-dub akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapomaliza kuswali, hutuelekea kwa uso wake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (845) na Muslim (2275)].
Hikma ya kuwaelekea maamuma kama inavyosemwa ni kuwafundisha mambo wanayoyahitajia kama ilivyo kwenye Hadiyth ya Zayd bin Khaalid Al-Juhaniy isemayo: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alituswalisha Swalaah ya Alfajiri huko Al-Hudaybiyah baada ya mvua kunyesha usiku. Alipomaliza kuswali, aliwaelekea watu na kuwaambia: ((Je, mnajua nini Kasema Mola wenu?)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (846) na Muslim (71)].
Kuna mengine yaliyosemwa kuhusiana na hikma ya hilo. Vyovyote iwavyo, hiyo ni Sunnah inayostahiki kufuatwa. Imesuniwa katika kuwaelekea, kuwe karibu zaidi kwa upande wake wa kuume. Imepokelewa toka kwa Al-Barraa akisema: “Tulipokuwa tunaswali nyuma ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), tulikuwa tunapenda tuwe kuliani mwake, akituelekea kwa uso wake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (709) na Abu Daawuud (615)].
· Faida
Imesuniwa kwa imamu kabla hajawaelekea watu, akae akiwa ameelekea Qiblah kiasi cha kusema: “Allaahumma Anta as Salaam waminka as Salaam, Tabaarakta yaa Dhal Jalaali wal Ikraam”. Hivi ndivyo alivyokuwa akifanya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Ni kama ilivyo kwenye Swahiyh Muslim (592) toka kwa ‘Aaishah na toka kwa Al Barraa bin ‘Aazib akisema: “Nilipeleleza Swalaah nilizoswali pamoja na Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Nikagundua kwamba muda takriban uko sawa wa kisimamo chake, kurukuu kwake na kuitadili kwake baada ya kurukuu, kusujudu kwake, kikao chake baina ya sijdah mbili, kusujudu kwake na kikao chake baina ya tasliym na kuondoka”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (471), Abu Daawuud (854), An-Nasaaiy (3/66) na Ahmad (4/294)].
Imepokelewa na Ummu Salamah akisema kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikaa mahala pake muda kidogo. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (849), Abu Daawuud (1040), An-Nasaaiy (3/67) na Ibn Maajah (932)].
· Wanawake Waondoke Haraka Mara Tu Baada Ya Swalaah Kumalizika
Imepokelewa toka kwa Ummu Salamah ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikaa mahala pake muda kidogo. Ibn Shihaab amesema: “Tunaona – na Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi – ili wamalizike wanawake wenye kuondoka”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (849), Abu Daawuud (1040), An-Nasaaiy (3/67) na Ibn Maajah (932)].
Na kasema tena Ummu Salamah: “Akina mama wakati wa enzi ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), walikuwa wanapotoa tasliym katika Swalaah ya faradhi husimama. Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na wanaume walioswali, alikuwa akibakia hapo hapo alipo muda autakao. Na Rasuli wa Allaah anaposimama, na wanaume nao husimama”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (866) na wengineo].
Mahala pa kufanyika hili ni pale wanawake wanaposwali nyuma ya wanaume moja kwa moja, na ukawa mlango wa kutokea wote ni mmoja. Ama ikiwa kuna mlango maalum wa wanawake na sehemu yao maalum ya kuswalia ambapo wanaume hawawezi kuwaona, basi ni haki yao kubakia hapo waliposwalia ili kuleta tasbiyh, tahmiyd, tahliyl na nyiradi nyinginezo zinazofanywa kila baada ya Swalaah, kwa kuwa Malaika huwaombea rahma madhali wako kwenye sehemu waliyoswalia, na madhali wudhuu haujawatenguka. [Mfano wa haya yako kwenye Jaami’u Ahkaam An Nisaa cha Sheikh wetu Allaah Amhifadhi (1/287). Angalia kitabu changu cha Fiqhu As-Sunnah Lin-Nisai ukurasa wa 156].
Ninasema: “Linalopendeza ni kuwepo mlango maalumu wa akina mama – na hususan katika wakati huu wa fitna- ambao wanaume hawaruhusiwi kabisa kuingilia. Na asili ya hili ni kauli ya ‘Umar bin Al-Khattwaab aliposema: “Bora tungeuacha mlango huu kwa wanawake”. Ibn ‘Umar hakuingilia tena mlango huo mpaka alipokufa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (463) toka kwa Naafi’i toka kwa ‘Umar. Nayo inachukulika kwamba ameichukua toka kwa Ibn ‘Umar. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi].
· Yanayosemwa Wakati Wa Kutoka Msikitini
Imepokelewa toka kwa Abu Humayd au Abu Asyad (Radhwiya Allaahu Anhu) akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Anapoingia mmoja wenu Msikitini, basi amtolee salaam Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kisha aseme: “Allaahumma Iftah liy abwaaba Rahmatika”. Na anapotoka aseme: “Allaahumma inniy as-aluka min Fadhwlika”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (713), Abu Daawuud (465) na An-Nasaaiy (3/53)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
047-Baadhi Ya Hukmu Za Msikiti
Alhidaaya.com [3]
Msikiti bora zaidi kuliko mingine:
Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Swalaah moja ndani ya Msikiti wangu huu, ni bora zaidi kuliko Swalaah 1000 kwenye Msikiti mwingine, isipokuwa Al-Masjid Al-Haraam)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1190)].
· Misikiti Bora Zaidi
Ni Al-Masjidul Haraam, kisha Msikiti wa Rasuli, halafu Al-Masjidul Aqswaa kutokana na Hadiyth hii na zinazofuatia.
· Safari Haifungwi Isipokuwa Kuiendea Misikiti Mitatu
Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Safari haifungwi isipokuwa kuiendea Misikiti Mitatu: Msikiti wangu huu, Masjidul Haraam na Masjidul Aqswaa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1189) na Muslim (1397)].
· Ubora Wa Kujenga Misikiti
Imepokelewa toka kwa ‘Uthmaan bin ‘Affaan ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwenye kujenga Msikiti kwa ajili ya Allaah, akitafuta kwa hilo Uso wa Allaah, basi Allaah Atamjengea nyumba peponi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (450) na Muslim (533)].
· Ukaraha Wa Kuipamba Misikiti Na Kurefusha Sana Majenzi Yake Zaidi Ya Inavyohitajia
Imepokelewa toka kwa Anas ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Qiyaamah hakitosimama mpaka watu wajifakharishie kwa misikiti)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (449), An-Nasaaiy (689), Ibn Maajah (739) na Ahmad (11931)].
Na imepokelewa toka kwa Ibn ‘Abbaas kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Sikuamrishwa kujenga misikiti kama ngome)). Yaani: Kunyanyua majengo yake kupita kiasi ya inavyohitajia. [Ibn ‘Abbaas kasema: Hakika mtaipamba kama walivyopamba Mayahudi na Manasara]. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (448), Ibn Hibaan (1615), Al-Bayhaqiy (2/438) Abu Ya-’alaa (2454) na ‘Abdul Razzaaq (5127)].
Imepokelewa kwamba ‘Umar aliamrisha kujenga misikiti akisema: “Wahifadhi watu kutokana na mvua, na tahadhari usije kupaka rangi nyekundu au njano, watu wakaondokewa na khushuu kwa kushughulishwa na hilo”. [Al-Bukhaariy kaitolea maelezo katika mlango wa “Kujenga Msikiti” kwa kulitaja bayana jina la msimulizi wake (Swiyghat Al-Jazm)].
· Kuisafisha Misikiti Na Kuitia Vinukizo
Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameamuru kujenga misikiti kwenye mitaa yenye watu, na akaamuru isafishwe na itiwe vinukizo. [Hadiyth Mursal: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (455), At-Tirmidhiy (594) na Ibn Maajah (759). Katika Sanad yake kuna mvutano kuhusiana na Hisham bin ‘Urwah. Lililo sawa -kama alivyosema Ad-daaraqutwniy katika Al’ilal- ni upokezi toka kwa Hisham toka kwa baba yake bila kumtaja ‘Aaishah. Angalia Al-Iswaabah (5/361)].
Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah kwamba mtu mmoja mweusi –au mwanamke mweusi- alikuwa akisafisha Msikiti akafa, na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamuulizia. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (458) na Muslim (956)].
Na katika tamko jingine toka kwa Abu Hurayrah: “Mwanamke alikuwa akiokota vijitaka na vijiti Msikitini”. [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Khuzaymah (1300) na wengineo].
Na imepokelewa toka kwa Anas akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliona kohozi kwenye Qiblah cha Msikiti, akaghadhibika mno mpaka uso wake ukawa mwekundu. Mwanamke mmoja wa Kiansari akasimama na kulikwangua, kisha akaweka mahala pake kinukizo. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Uzuri ulioje wa kitendo hiki!!)). [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (2/25) na Ibn Maajah (762)].
· Kuihifadhi Na Taka Na Uchafu
Imepokelewa toka kwa Anas bin Maalik ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Misikiti hii haifai kwa jingine lolote kati ya mkojo huu wala uchafu, bali Misikiti ni kwa ajili ya kumdhukuru Allaah na kusoma Qur-aan)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (537) kuhusiana na mtu aliyekojoa Msikitini].
Na toka kwa Anas vile vile kwamba Rasuli wa Allaah amesema: ((Kutema mate Msikitini ni dhambi, na kafara yake ni kuyafukia)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (552), Abu Daawuud (475), At-Tirmidhiy (572) na An-Nasaaiy (2/51)].
Imepokelewa toka kwa Abu Dharri toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Amali za Umma wangu zilionyeshwa kwangu; njema zake na mbaya zake, nikakuta katika amali zake njema adha inayoondoshwa njiani, na nikakuta katika amali zake mbaya kohozi lililopo Msikitini halifukiwi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (553)].
Katika sharhu yake, An-Nawawiy amesema: “Hadiyth hii inaonyesha kwamba ubaya huu na sifa hii hasi, hakuhusiani tu na aliyetema kohozi, bali anaingia yeye na kila aliyeliona akaliacha bila kulifukia, au kulikwangua au mfano wake”.
Na hili linatiliwa nguvu na Hadiyth ya Ibn ‘Umar ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliona mate kwenye ukuta wa Qiblah akayakwangua. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (406) na Muslim (547)].
· Faida
Afanye Nini Aliyelazimika Kutema Kohozi Akiwa Ndani ya Swalaah?
Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliona kohozi kwenye Qiblah cha Msikiti. Akawaelekea watu na kusema: ((Inakuwaje mmoja wenu asimame kumwelekea Mola wake halafu ateme kohozi mbele Yake? Je, anapenda mmoja wenu aelekewe kisha atemewe kohozi usoni? Basi ikiwa mmoja wenu atatema kohozi, ateme kushotoni mwake chini ya mguu wake, na kama hatoweza, basi afanye hivi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (550), An-Nasaaiy (1/163) na Ibn Maajah (1022)]. Akatemea kwenye nguo yake, kisha akaipangusia yenyewe kwa yenyewe.
· Marufuku Kunadia Kilichopotea Msikitini
Misikiti ni sehemu ya ‘’ibaadah, dhikri, na matendo ya utiifu. Haifai kunadiwa humo kitu alichopoteza mtu. Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah akisema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwenye kumsikia mtu akinadia kitu alichopoteza Msikitini, basi aseme: “Kamwe Allaah Asikurejeshee”, kwani Misikiti haikujengwa kwa ajili ya hilo)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (568), Abu Daawuud (4790) na Ibn Maajah (767)].
· Marufuku Kuuza Na Kununua Msikitini
Imepokelewa toka kwa ‘Abdullah bin ‘Amri ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikataza kuuza na kununua Msikitini, kuimbwa humo mashairi, kunadiwa humo kilichopotea, na kunyoa ndevu siku ya Ijumaa kabla ya Swalaah. [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1079), At-Tirmidhiy (322), An-Nasaaiy (2/47) na Ibn Maajah (766)].
Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mkimwona mwenye kuuza au kununua Msikitini, basi semeni: Kamwe Allaah Asikutilie faida biashara yako)). [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (1321)].
Jamhuri wamelichukulia katazo katika Hadiyth hizi kama katazo makruhu.
· Faida
Ama kuuza mbele ya mlango wa Msikiti (nje yake), huko kunajuzu bila ya ukaraha wowote. Dalili ya hili ni Hadiyth ya Ibn ‘Umar ya kwamba ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu Anhu) aliliona guo zuri la mistari mistari linauzwa mbele ya mlango wa Msikiti akasema: “Ee Rasuli wa Allaah!! Ungelinunua hili ukalivaa siku ya Ijumaa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (886) na Muslim (2068)].
· Marufuku Kuimba Mashairi Yasiyo Ya Kimaadili Msikitini
Tumeshaieleza Hadiyth Marfu’u ya ‘Abdullah bin ‘Amri isemayo: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikataza kuuza na kununua Msikitini na kuimbwa humo mashairi”.
Katazo hili linahusiana na uimbaji wa mashairi yasiyo na maadili mema, na yenye kuvuka mpaka wa uwastani kiasi cha kuutoa Msikiti nje ya lengo la kujengwa kwake. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimruhusu Hassan bin Thaabit kuwaanikia mapagani maovu yao Msikitini. Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah akisema: “ ’Umar alimpitia Hassan akiwa anaimba Msikitini. Hassan akamwangalia kwa jicho la chaki kisha akasema: “Hakika nilikuwa naimba na yumo humu aliye mbora kuliko wewe”. Kisha akamgeukia Abu Hurayrah akamwambia: “Nakuapia Allaah. Je, umemsikia Rasuli wa Allaah akisema: ((Nijibie mimi (shutuma za makafiri). Ee Allaah! Mtilie nguvu kwa Roho Mtakatifu)). Akasema: “Na’am”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (453) na Muslim (2485)].
· Marufuku Kupaza Sauti Msikitini
Katika Hadiyth ya As-Saaib bin Zayd ni kwamba ‘Umar aliwaona watu wawili toka Taif wakizungumza kwa sauti akasema: “Mngelikuwa ni wenyeji ningewaadhibu vikali. Mnanyanyua sauti zenu kwenye Msikiti wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)!!”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (470)].
Tumetangulia kusema nyuma kidogo kwamba ni marufuku kwa wenye kuswali kufanyiana tashwishi, na kunyanyua sauti hata kama ni kwa kusoma Qur-aan.
Ninasema: “Hili linachukuliwa ikiwa unyanyuaji wa sauti utakuwa ni wa kukera. Ikiwa haukeri, basi utaruhusiwa kwa ajili ya maslaha kama kudai haki na mfano wake. Ni kama ilivyo kwenye Hadiyth ya Ka’ab bin Maalik ya kwamba alimdai Ibn Abiy Hadrad deni lake ndani ya Msikiti, sauti zao zikapanda mpaka Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawasikia akiwa nyumbani kwake. Kisha akawatokea. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (457)]. Hadiyth inaendelea kueleza kwamba hakuwakataza hilo. Pia inaruhusiwa kunyanyua sauti kwa ajili ya kutoa ‘ilmu au kuelezea jambo.
· Inajuzu Kuzungumzia Maneno Yenye Faida Msikitini
Imepokelewa toka kwa Jaabir bin Samurah akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa hanyanyuki toka kwenye sehemu yake aliyoswalia Swalaah ya Alfajiri mpaka jua linapochomoza, na jua linapochomoza husimama”. Anasema: “Walikuwa wanazungumza, wakiyagusia masuala ya ujahilia, wakicheka na Rasuli akitabasamu”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (670)].
· Inajuzu Kula, Kunywa na Kulala Msikitini
Imepokelewa toka kwa ‘Abdullah bin Al-Haarith akisema: “Katika enzi ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), tulikuwa tunakula mkate na nyama Msikitini”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Maajah (3300)].
Na imethibiti kwamba mwanamke mmoja mweusi alikuwa akiishi Msikitini. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (439)].
Na pia Ahlus Swafah. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (6452) na At-Tirmidhiy (479)].
Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar akisema kwamba alikuwa akilala Msikitini naye ni kijana kapera. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (7031), Muslim (2479) na wengineo kwa mfano wake].
· Inajuzu Kucheza Msikitini Kwa Maslaha
Imepokelewa na ‘Aaishah akisema: “Wahabeshi walikuja wakicheza siku ya ‘Iyd. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaniita, nami nikaweka kichwa changu juu ya mabega yake, nikawa natizama wanavyocheza mpaka nikaondoka mwenyewe”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (5190) na Muslim (892), na tamko ni lake].
· Ni Marufuku Kushikanisha Vidole Msikitini
Hili tushalielezea kirefu nyuma.
· Inajuzu Kumwingiza Mpagani Msikitini Kwa Ajili Ya Maslaha Isipokuwa Msikiti Mtakatifu Wa Makkah
Ni kwa Hadiyth ya Abu Hurayrah kuhusiana na kisa cha kumfungia Thumaamah bin Athaal –wakati huo alikuwa ni mpagani- kwenye nguzo moja kati ya nguzo za Msikiti. Kisa kinaeleza kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliamuru aachiliwe katika siku ya tatu. “Akachomoka akaenda kwenye mtende ulioko karibu na Msikiti, akaoga, kisha akaingia Msikitini, akasilimu. [Hadiyth Swahiyh: “Takhriyj” yake ishaelezwa kwenye mlango wa kukoga].
Ama Msikiti Mtakatifu wa Makkah, mpagani haruhusiwi kuingia humo kwa Neno Lake Ta’alaa:
((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْمُشْرِكُونَ نَجَسٌ فَلَا يَقْرَبُوا الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ بَعْدَ عَامِهِمْ هَـٰذَا ۚ وَإِنْ خِفْتُمْ عَيْلَةً فَسَوْفَ يُغْنِيكُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ إِن شَاءَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ حَكِيمٌ))
((Enyi walioamini! Hakika washirikiana ni najisi, basi wasikaribie Al-Masjid Al-Haraam baada ya mwaka wao huu. Na mkikhofu umasikini basi Allaah Atakutajirisheni kutokana na fadhila Zake Akitaka. Hakika Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote)). [At-Tawbah (9:28)]
Hii ni kauli ya Ash-Shaafi’iy na Ibn Hazm. [Al-Muhalla (4/243)].
· Ni haramu Kujenga Misikiti Juu Ya Makaburi
Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Amewalaani Mayahudi na Manaswara. Wameyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa Misikiti)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1330) na Muslim (531)].
Imepokekewa toka kwa Jun-dub akisema: “Nimemsikia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema kabla hajafariki kwa siku tano: ((Jueni kwamba, hakika waliopita kabla yenu walikuwa wakiyafanya makaburi ya Manabii wao na watu wao wema kuwa Misikiti. Basi jueni, msije mkayafanya makaburi kuwa Misikiti. Hakika mimi nawakatazeni na hilo)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (532), An-Nasaaiy katika Al-Kubraa (11123) na Ahmad (1/195)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
048-Swalaah Ya Ijumaa
Alhidaaya.com [3]
[Mlango huu umechomolewa kwa muhtasari toka kitabu changu cha Allam-’atu Fiy Aadaab Wa Ahkaamil Jum-’at].
· Miongoni Mwa Fadhla Za Siku Ya Ijumaa
1- Siku ya Ijumaa ndiyo siku bora zaidi kwa Allaah Ta’aalaa:
Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Halichomozi jua wala kuchwa juu ya siku iliyo bora zaidi kuliko siku ya Ijumaa)). [Hadiyth Swahiyh Lighayrihi: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (2/457), ‘Abdul Razzaaq (5563), Ibn Hibaan (2759) na Al-Baghawiy (1062). Ina Hadiyth wenza].
Na Allaah Mtukufu Ameiapia katika Kitabu Chake Akisema:
((وَشَاهِدٍ وَمَشْهُودٍ))
((Na Naapa kwa shahidi na kinachoshuhudiwa)). [Al-Buruwj (85:3)]
Abu Hurayrah kasema: “Siku iliyoahidiwa ni siku ya Qiyaamah, na yenye kushuhudia ni Siku ya Ijumaa, na yenye kushuhudiwa ni siku ya Arafah”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Jariyj (30/82), Al-Haakim (2/519) na Al-Bayhaqiy (3/170). Imesimuliwa ikiwa Marfu’u, lakini si Swahiyh].
2- Allaah Mtukufu Alifanya matukio makubwa katika siku hii
Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Siku njema kabisa iliyochomokezewa na jua ni Siku ya Ijumaa. Katika siku hii, aliumbwa Aadam, aliingizwa peponi, alitolewa humo, alikubaliwa toba, alikufa na ndiyo siku ya kusimama Qiyaamah. Hakuna mnyama yoyote isipokuwa anakuwa ni mwenye kusikiliza katika Siku ya Ijumaa mpaka jua lichomoze kwa ajili ya kukiogopea Qiyaamah isipokuwa mwanadamu. Katika siku hii, kuna saa ambayo Muislamu haisadifu akiwa {amesimama} anaswali na akamwomba Allaah jambo lolote, isipokuwa Humpa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (584) kwa ufupi, Maalik (1/108) na kwa njia yake Abu Daawuud (1046) na At-Tirmidhiy (491)].
3- Ni siku ya sikukuu kwa Waislamu ambapo Allaah Aliwakamilishia Dini Yake na Akawatimizia Neema Yake
Imepokelewa toka kwa Twaariq bin Shihaab akisema: “Mtu mmoja katika Mayahudi alikuja kwa ‘Umar bin Al-Khattwaab akamwambia: Ee Amiri wa Waumini! Kuna Aayah katika Kitabu chenu mnaisoma. Lau ingeliteremshwa kwetu jamii ya Mayahudi, basi tungeliifanya siku hiyo sikukuu. Akasema:
الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ۚ
‘Umar akasema: Hakika tumeijua siku hiyo, na mahala ambapo Aayah iliteremka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa amesimama Arafah Siku ya Ijumaa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (45), Muslim (3017), At-Tirmidhiy (3043) na An-Nasaaiy (8/114)].
Imepokelewa toka kwa Anas ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Alinijia Jibriyl na mithili ya kioo cheupe, kwenye kioo hicho kuna doa jeusi. Nikasema: Ee Jibriyl! Nini hii? Akasema: Hii ni Ijumaa, Allaah Ameifanya ni sikukuu kwako na kwa Umma wako)). [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Ya’alaa (4213) na wengineo kwa Sanad Hasan].
4- Kuna fadhla kubwa za kuiswali na kuihudhuria
Baadhi ya fadhila hizo tutazieleza katika mahala pake Insha-Allaah.
· Yanayofanywa Usiku Wa Kuamkia Ijumaa Na Katika Siku Yenyewe
1- Ni karaha kuuhusisha usiku wa Ijumaa kwa Swalaah au mchana wake kwa Swaum
Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Msiuhusishe usiku wa Ijumaa kwa Swalaah kutofautisha na masiku mengine, wala msiihusishe siku ya Ijumaa kwa Swaum kutofautisha na siku nyingine isipokuwa iwe katika Swaum anayoifunga mmoja wenu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (1144), An-Nasaaiy katika Al-Kubraa (2751) na Ahmad (2/444). Na asili yake ni katika Al-Bukhaariy (1985) bila kutaja Swalaah].
2- Imesuniwa kusoma Suwrat As Sajdah na Suwrat Al-Insaan katika Swalaah ya Alfajiri yake
Ni kwa Hadiyth ya Abu Hurayrah ya kwamba: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisoma katika Swalaah ya Alfajiri ya Siku ya Ijumaa Alif Laam Miym Tanziyl (As Sajdah) katika rakaa ya kwanza, na katika rakaa ya pili
((هَلْ أَتَىٰ عَلَى الْإِنسَانِ حِينٌ مِّنَ الدَّهْرِ لَمْ يَكُن شَيْئًا مَّذْكُورًا))"
[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (891), Muslim (880) na wengineo].
· Maangalizo Mawili
[Majmu’u Al-Fataawaa (24/205) na Zaad Al-Ma’ad (1/375)].
(a) Watu wengi ambao hawakuelimika, wanadhani kwamba makusudio ni kuihusisha Swalaah hii kwa sijdah ya ziada na huiita sijdah ya Ijumaa. Na kama mmoja wao hakuisoma Suwrah hii, basi husoma Suwrah nyingine yenye sijdah. Hili ni kosa, na lililo sawa ni kuwa sijdah imekuja kwa kufuata agizo na si makusudio yake kwamba mwenye kuswali akusudie kuisoma.
(b) Haikusuniwa kusoma kwenye Swalaah hiyo Suwrah nyingine ya sajdah kwa makubaliano ya Maulamaa wote.
3- Imesuniwa kukithirisha kumswalia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
Imepokelewa toka kwa Aws akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika katika masiku yenu bora kabisa ni Siku ya Ijumaa. Siku hiyo aliumbwa Aadam, siku hiyo litapulizwa baragumu, na siku hiyo kuna mngurumo wa kutisha. Basi kithirisheni kuniombea rahma, kwani maombi yenu huonyeshwa kwangu)). Mtu mmoja akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Vipi sisi kukuombea wewe rahma kunaonyeshwa kwako nawe ushaoza? Akasema: ((Hakika Allaah ‘Azza wa Jalla Ameiharamishia ardhi [kuila] miili ya Manabii)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1047), An-Nasaaiy (3/91), Ibn Maajah (1085) Ahmad (4/8) na wengineo].
4- Imesuniwa kusoma Suwrat Al-Kahf
Ni kwa Hadiyth ya Abu Sa’iyd ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwenye kusoma Suwrat Al-Kahf Siku ya Ijumaa, basi itamwangazia nuru ya kati ya Ijumaa mbili)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Haakim (2/368) na Al-Bayhaqiy (3/249)].
5- Kukithirisha du’aa kwa matarajio ya kusadifiana na saa ya kujibiwa
Tushaielezea Hadiyth Marfu’u ya Abu Hurayrah isemayo: ((Katika siku hii, kuna saa ambayo Muislamu haisadifu akiwa {amesimama} anaswali na akamwomba Allaah jambo lolote, isipokuwa Humpa)). [Hadiyth Swahiyh: Tushaielezea nyuma kidogo].
· Saa Ya Kujibiwa Ni Saa Ya Mwisho Baada Ya Alasiri ya Siku ya Ijumaa Kwa Kauli Yenye Nguvu
Ni kwa Hadiyth ya Jaabir isemayo: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Siku ya Ijumaa ni kumi na mbili (yaani saa). Hapatikani Muislamu anayemwomba Allaah Azza wa Jalla chochote isipokuwa Allaah Azza wa Jalla Humpa. Basi ipanieni kimakusudi saa ya mwisho baada ya Alasiri)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1047) na An-Nasaaiy (3/99), na tamko ni lake].
Na imepokelewa toka kwa Anas akisema kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (( Ipanieni kimakusudi saa ambayo hutarajiwa katika Siku ya Ijumaa baada ya Alasiri mpaka kuchwa jua)). [Hadiyth Hasan kwa Sanad tofauti: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (489), na kwa njia ya Al-Baghawiy (1051). Angalia Swahiyh At-Targhiyb (793)].
· Hukmu ya Swalaah ya Ijumaa
Swalaah ya Ijumaa ni Fardhi ‘Ayn kwa kila Muislamu aliyebaleghe isipokuwa yule ambaye dalili imemtoa kando. Asili ya ufaradhi wake ni kutoka kwenye Qur-aan, Sunnah na Ijma’a ya Umma:
1- Allaah Amesema:
(( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ))
(( Enyi walioamini! Inaponadiwa kwa ajili ya Swalaah siku ya Ijumaa, kimbilieni kumdhukuru Allaah na acheni kuuza na kununua. Hivyo ni kheri kwenu mkiwa mnajua)). [Al-Jum-‘ah (62:9)]
2- Imepokelewa toka kwa Hafswah ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kwenda Ijumaa ni wajibu kwa kila aliye baleghe, na ni lazima kwa mwenye kwenda Ijumaa akoge)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na An Nasaaiy (3/89), Abu Daawuud (342), Ibn Al-Jaaruwd (287) na Al-Bayhaqiy (3/172)].
3- Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar na Abu Hurayrah ya kwamba wamemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa juu ya vigogo vya mimbari yake akisema: ((Watakoma watu kuacha Swalaah za Ijumaa, au Allaah Atawapiga muhuri kwenye nyoyo zao, kisha watakuwa ni miongoni mwa wenye kughafilika)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (865), An-Nasaaiy (3/88), Ibn Maajah (794) na Ad-daaramiy (1570)].
4- Imepokelewa toka kwa Abul Ja’ad Adw-Dwamariy akisema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwenye kuacha ijumaa tatu bila ya udhuru, basi atapigwa muhuri kwenye moyo wake)). [Hadiyth Swahiyh kwa Sanad zake: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1052), At-Tirmidhiy (500), An-Nasaaiy (3/88) na Ibn Maajah (1125)].
5- Imepokelewa toka kwa Ibn Mas-’oud ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaambia watu wasiokwenda Ijumaa: ((Nilikusudia nimwamuru mtu aswalishe watu, kisha mimi niende kuwachomea moto watu wasiohudhuria Ijumaa nyumba zao)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (4398), An-Nasaaiy (2/100), Ad-daaramiy (2/171), Ibn Maajah (2041) na Ahmad (6/100)].
6- Waislamu wote wamekubaliana juu ya wajibu wa Ijumaa. Lakini mvutano ulioko ni je, Ijumaa ni Fardhi ‘Ayn au Fardhi Kifaayah? [Al-Mughniy (2/111) chapa ya Al-Fikr na Badaai’u As-Swanaai’i (1/256)]..
Na kutokana na dalili zilizotangulia, inabainika kwamba ni Fardhi ‘Ayn. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.
· Walio Nje Ya Wigo Wa Wajibu
Ni mtoto, mwanamke, mtumwa anayemilikiwa, mgonjwa, msafiri na wengineo wenye nyudhuru. Ikiwa yeyote katika hawa ataiswali, basi Swalaah yake ni sahihi na faradhi ya Adhuhuri itamwondokea.
Imepokelewa toka kwa Twaariq bin Shihaab kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ijumaa ni haki wajibu kwa kila aliye baleghe isipokuwa wanne: Mtumwa mmilikiwa, mwanamke, mtoto na mgonjwa)). [Hadiyth Hasan kwa Sanad zake: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1067), Ad-daaraqutwniy (2/3) na Al-Bayhaqiy (3/183). Angalia Al-Irwaa (3/57)].
Imepokelewa na Jaabir kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Anayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho, basi ni juu yake Ijumaa Siku ya Ijumaa isipokuwa mgonjwa, au msafiri, au mwanamke au mtoto au mtumwa)).
Nyudhuru nyingine zinazomruhusu Muislamu asiende kuswali Ijumaa ni baridi na mvua. Ni kwa Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas: “Ni kwamba yeye alimwambia mwadhini wake katika siku ya mvua kubwa: Utakaposema
أشهد أن لا إله إلا الله أشهد أن محمدا رسول الله , basi usiseme: حي على الصلاة , bali sema: صلوا في بيوتكم (swalini majumbani mwenu). Watu wakawa kana kwamba wameshangazwa na hilo naye akawauliza: Mnashangazwa na hili? Hakika alilifanya hili aliyekuwa mbora kuliko mimi. Hakika Ijumaa ni azma, na mimi nimeona tabu kuwatoeni, mkatembea kwenye tope na utelezi”. [Hadiyth Swahiyh: “Takhriyj” yake ishaelezwa].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
049- Maandalizi Kwa Ajili Ya Swalaah Ya Ijumaa
Alhidaaya.com [3]
Kuoga
Ni wajibu kwa mwenye kwenda katika Swalaah ya Ijumaa – katika waliowajibikiwa - aoge kwa mujibu wa kauli mbili sahihi za Maulamaa. Na hii ni kwa mujibu wa dalili tulizokwishazieleza katika mlango wa yenye kuwajibisha ghusl. Kati yake ni Hadiyth ya Abu Sa’iyd ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kuoga Siku ya Ijumaa ni wajibu kwa kila Muislamu aliyebaleghe)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (879) na Muslim (846)].
Na Hadiyth ya Ibn ‘Umar ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Akija mmoja wenu Ijumaa, basi aoge)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (877) na Muslim (84)].
Linalofahamika kutokana na Hadiyth hizi ni kwamba si wajibu kuoga kwa asiyehudhuria Ijumaa, kwani hakuna umuhimu huo kwa aliyesameheka kwenda Ijumaa. Haya wameyasema Jamhuri. [Fat-hul Baariy (2/417) na Al-Awsatw (4/48)].
· Faida Mbili:
1- Aliyepatwa na hadathi ndogo baada ya kuoga
Huyu kutamtosheleza kutawadha, kwani hadathi huiathiri twahara ndogo tu na wala haiathiri kusudio la kuoga ambalo ni kuutakasa mwili na kuondosha harufu. Aidha, kuoga huko ni kama kuoga janaba ambako hakutenguliwi na hadathi. [Al-Mughniy (2/99)].
2- Aliyepatwa na janaba Siku ya Ijumaa, basi josho moja tu litamtosheleza.
Mtu huyu litamtosheleza josho moja kwa janaba na Ijumaa kama atayanuwia yote mawili. Hii na kauli ya Maulamaa wengi ambao wamesema: “Tumekuta kwamba wudhuu mmoja na tayammumi moja, hutosheleza hadathi zote zenye kutengua wudhuu, na josho moja hutosheleza janaba zaidi ya moja, na josho moja hutosheleza hedhi ya masiku kadhaa, na twawafu moja hutosheleza ‘Umrah na Hajji katika qiraan. Hivyo ni lazima iwe hivyo kwa kila lenye kuwajibisha kuoga”.
Lakini Ibn Hazm amekwenda kinyume na hili akisema kwamba ni wajibu kila kimoja kiwe na josho lake maalum, na ameikosoa kirefu kauli hiyo ya Jamhuri. [Al-Awsatw (4/43), Al-Majmu’u (4/365), Al-Mughniy (2/99) na Al-Muhalla (2/45)].
Yaliyosuniwa Kabla Ya Kwenda Ijumaa
1- Kujitia manukato – kama anayo - isipokuwa kwa aliyehirimia na kwa mwanamke
Imepokelewa toka kwa Salmaan akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Haogi mtu Siku ya Ijumaa, akajitwaharisha kiasi awezavyo kujitwaharisha, akajipaka mafuta katika mafuta yake, akajitia manukato ya nyumbani kwake, kisha akatoka na asiingie kati ya watu wawili, halafu akaswali aliyoandikiwa, kisha akanyamaza wakati imamu anakhutubu, isipokuwa hughufiriwa yaliyo kati yake na Ijumaa nyingine)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (883), Abu Daawuud (1113), Ad-daaramiy (1541) na Al-Baghawiy (1058)]
Ama mwenye kuhirimia, huyo haijuzu kutumia manukato kama itakavyokuja kuelezwa katika mlango wa Hijjah.
Ama mwanamke, kuna dalili kochokocho zenye kuthibitisha uharamu wa kutoka akiwa amejitia manukato hata kama ni kwenda Msikitini kwa Swalaah. Kati yake ni Hadiyth ya Zaynab Ath-Thaqafiyyah toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) isemayo: ((Akihudhuria mmoja wenu ‘Ishaa ( Msikiti: katika riwaya nyingine) basi asijitie manukato usiku huo)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (443) na An- Nasaaiy (2/260)].
2- Kupiga mswaki
Ni kwa Hadiyth Marfu’u ya Abu Sa’iyd: ((Kuoga Siku ya Ijumaa ni wajibu kwa kila aliyebaleghe, apige mswaki na ajitie manukato akipata)). [Hadiyth Swahiyh: Tumeitaja nyuma kidogo].
Na kwa ujumla wa neno lake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Lau si kuchelea uzito juu ya Umma wangu, basi ningeliwaamuru wapige mswaki kila Swalaah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (887) na Muslim (578)].
3- Kujipamba kwa nguo maridadi zaidi, na nguo bora zaidi ni nyeupe
Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah na Abu Sa’iyd wakisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwenye kuoga Siku ya Ijumaa, akavaa nguo zake zilizo nzuri zaidi, akajitia manukato kama anayo, kisha akaenda Ijumaa, hayo yanakuwa ni kafara kwa yaliyoko kati yake na kati ya Ijumaa ya kabla yake)). [Hadiyth Swahiyh Lighayrihi: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (343), Ahmad (3/81), Al-Haakim (1/283) na Ibn Hibaan (2767)].
Na nguo bora zaidi ni nyeupe kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Vaeni katika nguo zilizo nyeupe, kwani hizo ndizo nguo bora zaidi kwenu, na wakafinini kwazo maiti wenu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (3878), At-Tirmidhiy (994), An-Nasaaiy (8/205), Ibn Maajah (1472) na Ahmad (1/247)].
4- Kujiepusha na chenye kukera watu kwa harufu yake
Ni kama kula kitunguu maji, kitunguu saumu na mfano wake au kuvuta sigara. Haya tushayaeleza katika mlango wa Swalaah ya Jamaa.
Wanayotakiwa Kuyafanya Maamuma Kabla Ya Khutbah
1,2- Kwenda mapema Msikitini na kujiweka karibu na imamu
Imepokelewa na Abu Hurayrah aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Inapokuwa Siku ya Ijumaa, kunakuwa na Malaika katika kila mlango wa Msikiti wakisajili wa mwanzo na anayefuatia. Imamu anapokaa, hukunja madaftari yao na huja kusikiliza khutbah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (3211) na Muslim (850)].
Pia Abu Hurayrah kapokea akisema kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwenye kuoga Siku ya Ijumaa josho la janaba kisha akaenda, basi ni kama ametoa swadaqah ngamia. Na mwenye kwenda katika saa ya pili, basi ni kama ametoa swadaqah ng’ombe. Na mwenye kwenda saa ya tatu, basi ni kama ametoa swadaqah kondoo mwenye pembe. Na mwenye kwenda saa ya nne, basi ni kama ametoa swadaqah kuku. Na mwenye kwenda saa ya tano, basi ni kama ametoa swadaqah yai. Na imamu anapotoka, Malaika huhudhuria kusikiliza khutbah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (881) na Muslim (850)].
Na imepokelewa na Samurah bin Jun-dub ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hudhurieni khutbah, na mkurubieni imamu, kwani hakika mtu ataendelea kujiweka mbali mpaka awekwe nyuma peponi hata kama ataingia)). [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1108) na Ahmad (5/10)].
3- Kwenda kwa miguu bila kutumia kipando isipokuwa kama atalazimika
Imepokelewa toka kwa Aws bin Aws ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwenye kuoga Siku ya Ijumaa na akasafisha kichwa chake, akatoka mwanzo wa wakati na akawahi mwanzo wa khutbah, na akatembea kwa miguu asipande kipando, na akawa karibu na imamu, na akasikiliza na kunyamaza, basi anapata kwa kila hatua amali ya mwaka; Swawm yake na Swalaah yake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (496), An-Nasaaiy (3/95), Abu Daawuud (345), na Ibn Maajah (1087)].
Imepokelewa toka kwa ‘Ubaabah bin Rifaa-’at akisema: “ Abu ‘Absi alinikuta nikienda Ijumaa akaniambia: “Nimemsikia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Mtu ambaye miguu yake itachafuka kwa vumbi katika Njia ya Allaah, basi Allaah Humharamishia moto)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (907)].
4- Kuswali Swalaah ya Maamkizi ya Msikiti kabla ya kukaa
Imepokelewa toka kwa Jaabir akisema: “Mtu mmoja aliingia Siku ya Ijumaa na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anakhutubu. Rasuli akamuuliza: ((Je, umeswali?)). Akasema: Hapana. Akamwambia: ((Basi swali rakaa mbili)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (930) na Muslim (875)].
Na katika tamko jingine: ((Simama uswali rakaa mbili, na uzifupishe)). Hii inamaanisha kwamba ikiwa alikaa bila ya kuswali, basi imesuniwa asimame aziswali – hata kama imamu anakhutubu - na azifupishe. Anaweza kuongeza Sunnah nyinginezo kiasi awezavyo kabla imamu hajapanda mimbari kwa mujibu wa Jamhuri ya Maulamaa. [Sharhu Muslim cha An-Nawawiy (3/385)]. Na hii ni kwa Hadiyth ya Salmaan iliyotajwa mara nyingi nyuma isemayo: ((Kisha akaswali alichoandikiwa, halafu akanyamaza wakati imamu anazungumza, isipokuwa hughufiriwa yaliyo kati yake na Ijumaa nyingine)). [Hadiyth Swahiyh: “Takhriyj” yake ishaelezwa].
· Faida:
Ijumaa haina Sunnah ya Qabliyyah
Adhana inapomalizika, haijuzu kabisa watu kusimama ili kuswali Qabliyyah. [Isipokuwa kama atakuja baada ya kumalizika adhana. Hapo anaweza kuswali Maamkizi ya Msikiti, kisha akae, au kama alisahau kama ilivyotangulia].
Hii ndio kauli sahihi zaidi ya Maulamaa. Imesemwa na Hanafiy, Maalik, Ash-Shaafi’iy na wafuasi wake wengi - kinyume na An-Nawawiy na wengineo -. Ni mashuhuri kwa Ahmad. [Al-Fataawaa Al-Kubraa cha Sheikh wa Uislamu (2/351), Zaad Al-Maad (1/433) na Twarhu At-Tathriyb (3/41)].
Na hili linathibitishwa na Sunnah, kwani Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anatoka nyumbani kwake, na anapopanda mimbari, Bilaal alikuwa anaanza moja kwa moja kuadhini adhana ya Ijumaa. Anapomaliza, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaanza kukhutubu bila mapumziko. Na hili lilikuwa linashuhudiwa na wote. Hivyo basi, ni wakati gani walikuwa wanaswali Sunnah? Na yeyote anayedhani kwamba walikuwa wote wanasimama kuswali rakaa mbili baada ya Bilaal kumaliza adhana, basi huyo upeo wake wa Sunnah ni mfinyu mno.
Linalotilia nguvu haya, ni Hadiyth ya Ibn ‘Umar asemaye: “Niliswali pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) rakaa mbili kabla ya Adhuhuri, na rakaa mbili baada ya Adhuhuri, na rakaa mbili baada ya Magharibi, na rakaa mbili baada ya ‘Ishaa, na rakaa mbili baada ya Ijumaa”. [Hadiyth Swahiyh: “Ishaelezwa kwenye mlango wa Sunnah za Rawaatib].
Hii ni matni inayojieleza wazi kwamba Ijumaa kwa Maswahaba, imejitenga kando peke yake mbali na Adhuhuri. Na kwa vile hakuitaja Sunnah ila baada yake, imebainika kwamba haina Sunnah ya kabla yake. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.
5- Kutokukusanyika kwa ajili ya darsa kabla ya Ijumaa
Ni kwa Hadiyth ya ‘Amri bin Shu’ayb toka kwa baba yake toka kwa babu yake ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kununua au kuuza Msikitini, kunadiwa kilichopotea, na kuimbwa mashairi. Na amekataza kukusanyika kwa darsa mfano wa Swalaah Siku ya Ijumaa. [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1079) na wengineo].
Kukusanyika huku kunaweza kuwa kwa kukaa kwenye halaqah (mduara) au kukusanyika kwa aina yoyote kwa ajili ya darsa. Na hayo yote yanaingia ndani ya katazo lililopo kwenye Hadiyth. [Angalia Allam-’atu fiy Hukmi Al Ijtimaa liddarsi Qabla Al Jum’at Cha Muhammad Muusa Nasr].
Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
050-Adhana Ya Ijumaa
Alhidaaya.com [3]
· Adhana Khatibu Anapokaa Juu Ya Mimbari
Imepokewa toka kwa As-Saaib bin Yazid akisema: “Mwanzo wa adhana ya Siku ya Ijumaa ulikuwa wakati imamu anapokaa juu ya mimbari Siku ya Ijumaa wakati wa enzi ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Abu Bakri na ‘Umar (Radhwiya Allaahu Anhum). Ulipokuwa ukhalifa wa ‘Uthmaan (Radhwiya Allaahu Anhu) – na watu wakaongezeka – ‘Uthmaan aliamuru adhana ya tatu Siku ya Ijumaa, nayo ikaadhiniwa hapo Az Zawraa, na jambo likathibiti hivyo. Watu hawakumkosoa kwa hilo, lakini walimkosoa aliposwali Swalaah kamili Mina”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (916), Abu Daawuud (1087), At-Tirmidhiy (516), An-Nasaaiy (3/101) na Ibn Maajah (1135)].
Katika Hadiyth hii kuna faida mbili:
Ya kwanza: Kwamba adhana Siku ya Ijumaa inakuwa baada ya imamu kukaa juu ya mimbari.
Ya pili: Kwamba Sunnah ni adhana moja tu kwa Ijumaa wakati imamu anapokaa. Ama kitendo cha ‘Uthmaan (Radhwiya Allaahu Anhu), si vizuri kukifuata katika wakati wetu wa sasa. Yeye aliongeza adhana ya kwanza kwa sababu ya kimantiki, nayo ni kuongezeka watu na nyumba zao kuwa mbali na Msikiti wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Alitaka kuwajulisha kuingia wakati wa Swalaah kama ilivyo kwa Swalaah nyingine za Faradhi. Akaijumuisha adhana hiyo na Ijumaa na akaubakisha umahususi wake na adhana baada ya khatibu kukaa. Basi yeyote ambaye hakuitizama sababu hii na akashikamana na adhana ya ‘Uthmaan kibubusa, basi hawi ni mwenye kumfuata Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), bali anakuwa ni mwenye kumkhalifu, kwa kuwa hakutizama kwa jicho la mazingatio sababu hiyo ambayo lau kama isingelikuweko, basi ‘Uthmaan asingeiongezea juu ya Sunnah ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Makhalifa wake wawili.
Na ni jambo lililo wazi kabisa kwamba ujulisho wa kuingia wakati wa Swalaah katika zama yetu ya sasa unapatikana bila kuongeza adhana hii, kwani mtu anaweza kusikia adhana ya Ijumaa baada ya kila mita chache anazotembea zikitokea Misikiti mbalimbali yenye vipaza sauti, pamoja na watu wengi kuwa na saa za kutegesha wakati na mfano wake.[Angalia Al-Ajwibat An-Naafi’at cha Al-Albaaniy Allaah Amrehemu uk. 28].
Pamoja na yote haya, Ibn ‘Umar alikuwa akimkosoa ‘Uthmaan kwa adhana ya kwanza akisema: “Hakika Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa anapanda mimbari, Bilaal huadhini, na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anapomaliza khutba huqimu Swalaah. Na adhana ya kwanza ni bid-’a”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (2/48)].
Kiufupi, kama itapatikana sababu ya kuwepo adhana ya ‘Uthmaan (Radhwiya Allaahu Anhu), basi itafanywa kwa haja na maslaha. Lakini kama hakuna, basi Sunnah ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba wake wawili isipetukwe. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.
· Adhana Ya Ijumaa Ina Nyakati Mbili:
(a) Baada ya kupinduka jua na imamu kukaa juu ya mimbari
Jamhuri ya Maulamaa wanasema kwamba wakati wa Ijumaa na wakati wa Adhuhuri, ni baada ya jua kupinduka kwa kuwa Ijumaa ni badala ya Adhuhuri!!. Iispokuwa tu wao wamependelea iwahishwe mwanzo wa wakati wake baada ya kupinduka jua. Dalili zao ni:
1- Hadiyth ya Salamah bin Al-Akwa’a aliyesema: “Tulikuwa tunaswali Ijumaa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) jua linapopinduka, kisha tunarejea kukifuatilia kivuli”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (4168) na Muslim (860)].
2- Hadiyth ya Anas: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaswali Ijumaa wakati jua linapopinduka”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (903), Abu Daawuud (1084), At-Tirmidhiy (503) na Ahmad (3/128)].
(b) Kabla ya kupinduka jua anapokaa imamu juu ya mimbari
Imaam Ahmad ameujuzisha wakati huu na ameutolea dalili kwa Hadiyth mbili zilizotangulia. Udhahiri wake ni kuwa Swalaah ndiyo iliyokuwa ikiswaliwa wakati jua linapopinduka, na adhana ilikuwa ni kabla yake. Hadiyth hizo mbili zimewekwa wazi na..
3- Hadiyth ya Jaabir bin ‘Abdullaah aliyesema: “ Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaswali Ijumaa, kisha tunakwenda kwa ngamia wetu, tunawapumzisha wakati jua linapopinduka, yaani kuwanyunyizia maji”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (858), An-Nasaaiy (3/100) na Ahmad (3/331)].
Kuna athari nyingi Swahiyh toka kwa Maswahaba (Radhwiya Allaahu Anhum) zinazotaarifu kujuzu adhana kabla ya jua kupinduka. Kati ya athari hizo ni:
4- Imepokelewa toka kwa Abu Raziyn amesema: “Tulikuwa tunaswali Ijumaa pamoja na ‘Aliy. Wakati mwingine tunakikuta kivuli cha kupinduka jua, na wakati mwingine hatukikuti”. [Isnadi yake ni Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abu Shaybah (2/18)].
5- Imepokelewa toka kwa ‘Abdullaah bin Salamah akisema: “‘Abdullaah (yaani: Ibn Mas-’oud) alituswalisha Ijumaa wakati wa Dhuhaa na akatuambia: Nimewaogopeeni joto”. [Isnadi yake ni Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abu Shaybah (2/17). Kuna maneno kuhusu huyu ‘Abdullah bin Salamah, lakini riwaya yake haifanyiwi hofu kwa matukio aliyoyahudhuria na kuyashuhudia].
6- Imepokelewa toka kwa Bilaal Al-‘Absiy: “Kwamba ‘Ammaar aliwaswalisha watu Ijumaa na watu wako makundi mawili. Baadhi wanasema jua limepinduka, na wengine wanasema halijapinduka”. [Isnadi yake ni Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abu Shaybah (2/18)].
7- Imepokelewa toka kwa Sammak bin Harb akisema: “ An-Nu’umaan bin Bashiyr alikuwa akituswalisha Ijumaa baada ya jua kupinduka”. [Isnadi yake ni Hasan: Al-Bukhaariy ameitaja ishara (2/449), na Ibn Abu Shaybah ameiunga (2/18)].
· Ni Marufuku Kuuza Baada Ya Adhana Ya Ijumaa
Ni kwa Neno Lake Ta’alaa:
(( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ))
(( Enyi walioamini! Inaponadiwa kwa ajili ya Swalaah Siku ya Ijumaa, kimbilieni kumdhukuru Allaah na acheni kuuza na kununua. Hivyo ni kheri kwenu mkiwa mnajua)). [Al-Jum-‘ah (62:9)]
Na katazo kwa mujibu wa Jamhuri ya Maulamaa, linajumuisha kuuza, kufunga ndoa na mikataba mingineyo. Mahanbali wamesema na kuungwa mkono na Ibn Hazm kwamba mengine yote hayakatazwi isipokuwa kuuza tu.
Na je inafaa kuuza baada ya adhana? Kuna kauli mbili za Maulamaa zilizojengewa juu ya msingi wa kwamba je katazo linahukumia kutohalalika mauzo au kuhalalika? Jamhuri wanasema kwamba mauzo ni halali, kwa kuwa katazo halimo ndani ya mauzo yenyewe, bali nje yake, kwa kuwa yakifanyika yatamzuia mtu asiende Ijumaa. Hivyo mauzo kiasili ni halali lakini yanakuwa na ukaraha wa tahriym.
Ni mashuhuri kwa Maalik na Hanbali kwamba mauzo hayafai na hayakubaliki.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
051-Khutbah Ya Ijumaa Na Hukmu Zinazomkhusu Khatibu
Alhidaaya.com [3]
· Hukmu Yake
Jamhuri ya Maulamaa wanasema kwamba khutbah ya Ijumaa ni sharti ya kuswihi Ijumaa. [Al-Badaai-’i (1/262), Ibn ‘Aabidiyn (1/567) na Al-Mughniy (2/74)].
Dalili zao ni hizi zifuatazo:
1- Ni Neno Lake Ta’alaa:
(( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ))
(( Enyi walioamini! Inaponadiwa kwa ajili ya Swalaah siku ya Ijumaa, kimbilieni kumdhukuru Allaah na acheni kuuza na kununua. Hivyo ni kheri kwenu mkiwa mnajua)). [Al-Jum-‘ah (62:9)]
Na “Dhikr” katika Aayah ni khutbah kwa mambo mawili:
(a) Ni kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
(( فإذا خرج الامام حضرت الملائكة يستمعون الذكر))
((Na imamu anapotoka, Malaika huhudhuria wakasikiliza khutba)). [Hadiyth Swahiyh: Al-Bukhaariy kasema ni “Mu’allaq” (2697) na Muslim (1718) na wengineo wamesema ni “Mawsuwl”].
Khutbah imeitwa dhikr. Na juu ya hilo, ikiwa kwenda kwa ajili ya khutbah ni lazima, nayo ni njia, basi khutbah inakuwa ni lazima, nayo ndio lengo.
(b) Ni kwamba Allaah Mtukufu Ameamuru kwenda kwenye khutbah tokea pale inapoadhiniwa. Na kwa “Tawaatur” isiyo na shaka, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anakhutubu mara tu baada ya adhana. Na kwa hilo, imejulikana kwamba kwenda kwenye khutbah ni wajibu.
2- Ni kudumu Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kutoa khutbah kila Ijumaa, na kamwe hakuwahi kuswali bila khutbah.
3- Kuharamishwa kuzungumza wakati wa khutbah na wajibu wa kuisikiliza khutbah.
Ikiulizwa: Dalili hizi hazionyeshi juu ya shurutisho?! Itajibiwa: Swalaah hii imekuwa ni wajibu kwa sifa hii ambayo Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliendelea nayo. Kwa hiyo, mwenye kukusuru kinyume na ilivyokuwa ikifanyika, basi anakuwa hakufanya lililo wajibu juu yake, na hili li wazi katika shurutisho. Na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwenye kufanya amali yoyote isiyohusiana na amri yetu, basi ni batili)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (862), Abu Daawuud (1093), An-Nasaaiy (3/109, 110), At-Tirmidhiy (507) na Ahmad (5/87)].
Hili linaonyesha kwamba kama hakukhutubu, ataswali rakaa nne, na Ijumaa si rakaa nne, hivyo inakuwa ni Adhuhuri.
· Ni Lazima Akhutubu Khutbah Mbili Kwa Kusimama, Na Akae Kidogo Kati Yake Ila Kama Ana Udhuru
Hii ndio kauli ya Jamhuri kinyume na Hanafi. Wajibu wa hili uko wazi –kama ilivyotangulia- kutokana na kudumu kwa kitendo chenye kubainisha sifa ya Swalaah hii ya wajibu, mbali na kutonukuliwa kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitosheka na khutbah moja, na kwamba alikhutubu akiwa amekaa. Imepokelewa toka kwa Jaabir bin Samurah: “Kwamba Rasuli wa Allaah alikuwa anakhutubu kwa kusimama, kisha anakaa, halafu anasimama na kukhutubu. Basi yeyote atakayekueleza kwamba alikuwa anakhutubu kwa kukaa, basi huyo ameongopa. Hakika – Wallaah – niliswali pamoja naye zaidi ya Swalaah elfu mbili”.
Katika riwaya nyingine: “Sikumwona ila amesimama”.
Imepokelewa toka kwa Ka’ab bin ‘Ajrah kwamba yeye: “Aliingia Msikitini – huku ‘Abdullaah bin Al-Hakam anakhutubu kwa kukaa – akasema: Mwangalieni khabithi huyu anakhutubu kwa kukaa nailhali Allaah Anasema:
وَإِذَا رَأَوْا تِجَارَةً أَوْ لَهْوًا انفَضُّوا إِلَيْهَا وَتَرَكُوكَ قَائِمًا ۚ”
[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (864), An-Nasaaiy (3/102) na Ibn Abu Shaybah].
· Kiasi Kitoshelezacho Khutbah
Maulamaa wamekhitalifiana kuhusu kiasi kitoshelezacho khutba. Kiuhakiki ni kusemwa: [Ar-Rawdhwat An-Naddiyyat uk. 137].
“Kisha jua kwamba khutbah ya kisharia, ni ile aliyokuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameizoea ya kuwatia watu utashi na kuwatia khofu. Hii kiuhalisia, ndio kiini cha khutbah ambacho kwa ajili yake khutbah imewekwa. Ama kuweka sharti ya kumhimidi Allaah, au kumswalia Rasuli wa Allaah, au kusoma kitu katika Qur-aan, haya yote yako nje ya kusudio kuu la uwepo wa khutbah. Na kukubaliwa mfano wa hayo katika khutbah yake Rasuli, hakuonyeshi kwamba ndio makusudio ya wajibu na sharti la lazima. Na yeyote aliye mwadilifu, atakuwa hana shaka yoyote kwamba kusudio kuu ni mawaidha bila ya yale yanayotokea kabla yake kati ya himdi kwa Allaah na Swalaah kwa Rasuli. Ilikuwa ni katika ada endelevu ya Waarabu kwamba mmoja wao anapotaka kusimama mbele ya hadhira na kusema neno, huanza neno lake kwa kumsifu Allaah na Rasuli Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Ni uzuri na ubora ulioje wa hili!! Lakini, hilo sio kusudio bali kusudio ni yale yanayofuatia. Na bila shaka, yeyote mwenye umbile salama, atapinga na kukataa ikiwa mtu atasimama mbele ya baraza kwa ajili ya kulihutubia, na hotuba yake isiwe na kingine chochote zaidi ya kumhimidi Allaah na kumswalia Rasuli tu.
Na tukikubaliana na haya, basi tunajua kwamba mawaidha kwenye khutbah ya Ijumaa ndio dhamira kuu ya mazungumzo, na khatibu akilifanya, anakuwa amefanya jambo la kisharia. Na ikiwa atatanguliza sifa kwa Allaah na kwa Rasuli Wake, au akaingiza ndani ya khutbah yake qaraa za Qur-aan, basi inakuwa ni utimilifu na uzuri zaidi”.
Ninasema: “Ni Sunnah kama itakavyokuja mbele”.
· Yaliyosuniwa Kwenye Khutbah
1- Kuianza kwa kumhimidi Allaah na kumsifu, na kumswalia Rasuli Wake na kutashahudia
Imepokelewa toka kwa Jaabir akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akimhimidi Allaah na kumsifu katika khutbah ya Siku ya Ijumaa [kwa Sifa Anazostahiki, kisha anasema: Man Yahdihi Allaahu falaa mudhwilla lahu, waman Yudhwlil falaa haadiya lahu, wakhayrul hadiyth, Kitaabu Allaah]”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (867)].
Na katika Hadiyth ya Abu Humayd As Saa’idiy: “Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisimama jioni baada ya Swalaah, akatashahudia, na akamsifu Allaah kwa Sifa Anazostahiki kisha akasema: Ammaa ba’adu”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (926)].
Imesuniwa aanze kwa khutbah ya haja. Imepokelewa toka kwa Ibn Mas-’oud akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametufundisha katika khutbah ya haja tuseme: “Alhamdu li-Laahi nahmaduhu wa nasta’iynuhu wa nastaghfiruhu, wa na’uwdhu bil Laahi min shuruwri anfusinaa wa sayyiaati a-’amaalinaa. Man Yahdihi Allaahu falaa mudhwilla lahu, waman Yudhwlil falaa Haadiya lahu. Wa ash-hadu an laa ilaaha illa Allaahu wahdahu laa shariyka Lahu, wa ash-hadu anna Muhammadan ‘Abduhu wa Rasuuluhu. [Kisha akasoma Aayah tatu]:
(( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ))
(( يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالًا كَثِيرًا وَنِسَاءً ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالْأَرْحَامَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا))
(( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا ● يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَالَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗوَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا))
[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (2118), At-Tirmidhiy (1105), An-Nasaaiy (6/89) na Ibn Maajah (1892)].
Imepokelewa toka kwa Jaabir akisema: “
Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapokhutubu, macho yake huwa mekundu, sauti yake huwa juu, na ghadhabu zake hushitadi kana kwamba anaonya watu na jeshi (la uvamizi) akisema: Litawavamieni asubuhi au jioni. Na anasema: ((Nimetumwa mimi, na Qiyaamah kama viwili hivi)), na hukutanisha baina ya kidole chake cha shahada na cha kati. Na husema: ((Ammaa ba’adu. Hakika Maneno yaliyo bora kabisa ni Kitabu cha Allaah, na Uongofu ulio bora kabisa ni Uongofu wa Muhammad, na shari ya mambo ni yale yenye kuzushwa, na kila chenye kuzushwa ni bid-’a, na kila upotevu ni motoni..)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (867), An-Nasaaiy (3/188), Ibn Maajah (45) na Ahmad (3/319)].
Na imepokelewa kwa njia sahihi kwamba ‘Umar bin Al-Khattwaab na Ibn Mas-’oud (Radhwiya Allaahu Anhumaa), walikuwa wakifungulia kwa maneno haya khutbah ya Ijumaa na khutbah nyinginezo.
2- Kuipa khutbah uzito na kunyanyua sauti
Ni kama ilivyotangulia kwenye Hadiyth ya Jaabir isemayo: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapokhutubu, macho yake huwa mekundu, sauti yake huwa juu, na ghadhabu zake hushitadi kana kwamba anaonya watu kuwa watavamiwa na jeshi akisema: Litawavamieni asubuhi au jioni”.
3- Kuifupisha khutbah na kuirefusha Swalaah
Imepokelewa toka kwa ‘Ammaar bin Yaasir akisema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Hakika mtu kurefusha Swalaah na kufupisha khutbah yake, ni alama ya weledi wake. Basi irefusheni Swalaah hii, na fupisheni khutbah hizi, kwani baadhi ya maneno ni kama uchawi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (869), Ahmad (4/263), Ad-daaramiy (1556) na wengineo].
Na imepokelewa toka kwa Jaabir bin Samrah akisema: “Niliswali pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Swalaah yake ilikuwa ni ya wastani, na khutbah yake ni ya wastani”.
Na katika riwaya: “Harefushi mawaidha Siku ya Ijumaa, bali yanakuwa ni maneno machache”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (866), Abu Daawuud (1107) na riwaya nyingine ni yake, At-Tirmidhiy (507), An-Nasaaiy (3/110) na Ibn Maajah (1106)].
Ninasema: “Kuna faida mbili katika kufupisha khutbah: Kwanza hakumchoshi msikilizaji, na pili kunamfanya aielewe vyema na kuifahamu vizuri zaidi. Lakini weledi na umahiri wa khatibu, unaweza kuifanya kuwa ndefu kwa mujibu wa suala linalozungumziwa. Imethibiti kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anakhutubu kwa kusoma Suwrat “Qaaf” na “Tabaaraka”, na hii ni pamoja na kuzisoma kwa tartiyl na kusimama kwenye kila Aayah. Hili bila shaka lilikuwa likiirefusha khutbah. Makusudio kiujumla, ni kuchunga hali ya watu na haja yao. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi”.
4- Kusoma Aayah za Qur-aan ndani ya khutbah
(a) Imepokelewa toka kwa Jaabir bin Samurah akisema: “ Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikaa baina ya khutbah mbili, na huwakumbusha watu, na husoma Aayah za Qur-aan”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (862) na Abu Daawuud (1094)].
(b) Imepokelewa toka kwa Swafwaan bin Ya’alaa toka kwa baba yake: “Kwamba yeye alimsikia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasoma juu ya mimbari "ونادوا يا مالك" “. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (3266) na Muslim (871)].
(c) Imepokelewa toka kwa Ummu Hishaam akisema: “Sikuihifadhi Suwrat Qaaf isipokuwa toka kwenye kinywa cha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), akikhutubu kwayo kila Ijumaa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (872) na Ahmad (6/463)].
5- Kuteremka toka juu ya mimbari anaposoma Aayah ya sijdah
Hili limethibiti toka kwa ‘Umar bin Al-Khattwaab, Abu Muusa Al-Ash-’ariy na ‘Ammaar bin Yaasir. Haya yashaelezwa kwenye mlango wa sijdah ya kisomo.
6- Kuwaombea du’aa Waislamu ndani ya khutbah
Inasimuliwa toka kwa Samrah: “Kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiwaombea maghfirah Waumini katika kila Ijumaa”. Lakini ni Dhwa’iyf mno, haifai kwa dalili ingawa Maulamaa wanaitumia. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bazzaar katika Al-Majma’a (2/190), na katika Sanad yake, kuna mtu ameachwa].
Pamoja na hayo, kuna faida ya kupendeza kuomba du’aa katika khutbah kutokana na Hadiyth ya ‘Ammaarah bin Ra-ayat: “ Ya kwamba yeye alimwona Bishr bin Marwaan juu ya mimbari akinyanyua mikono yake (akiomba) akasema: Allaah Ainyime mikono hii miwili kheri zote. Hakika nilimwona Rasuli wa Allaah haongezi zaidi ya kufanya hivi, na akaashiria kwa kidole chake cha shahada”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (874), An-Nasaaiy (3/108), Abu Daawuud (1104), At-Tirmidhiy (515) na Ibn Maajah (1103)].
Katika hili, kuna faida mbili:
1- Kuthibitisha kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiomba katika khutbah yake.
2- Ukaraha wa imamu kunyayua mikono yake anapoomba juu ya mimbari, na kwamba Sunnah ni kuashiria kwa kidole chake cha shahada. Na hili linatiliwa nguvu na Hadiyth ya Sahl bin Sa’ad aliyesema: “ Sikumwona kamwe Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akinyoosha mikono yake wakati anaomba juu ya mimbari yake wala juu ya mimbari nyingine yoyote, lakini nilimwona akifanya hivi, na akaashiria kidole chake cha shahada, na akakifunga cha kati na gumba”. [Hadiyth Hasan kwa iliyoitangulia: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1105) kwa Sanad laini. Hadiyth iliyotangulia, inaitolea ushuhuda].
Na hii ni moja ya mielekeo miwili kwa Hanbali, nao umekhitariwa na Sheikh wa Uislamu. [Al-Ikhtiyaaraat uk. 80].
· Zindusho:
Kuomba du’aa katika Swalaah ya kuomba mvua, kunatolewa nje ya tuliyoyaeleza, kwani lililothibiti katika Swalaah hiyo ni kunyanyua mikono miwili kama ilivyotangulia katika mlango husika. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
· Mambo Anayoruhusiwa Kuyafanya Khatibu Wakati Wa Khutbah
1- Kuegemea fimbo au mfano wake
Katika Hadiyth ya Al-Hakam bin Hazan Al-Kalfiyy – katika kisa cha kwenda kwake kwa Rasuli akiwa na wajumbe: “ Tukakaa hapo masiku kadhaa ambapo tulihudhuria Ijumaa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Akasimama akiegemea fimbo au upinde, akamhimidi Allaah na akamsifu”. [Hadiyth Swahiyh kwa Hadiyth wenza: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1096), Ahmad (4/212), Abu Ya’alaa (12/204) na Ibn Khuzaymah (1452). Ina Hadiyth wenza].
Na katika Hadiyth ya Fatmah bint Qays –kuhusu kisa cha Al-Jassaasah (mnyama mwenye nywele nyingi mwili mzima)..Rasuli wa Allaah akasema: –na akagonga kwa fimbo yake kwenye mimbari– ((Hii ni Twaybah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (2942), Abu Daawuud (4326), At-Tirmidhiy (2253) na Ibn Maajah (4074)].
2- Kuzungumza na yeyote amtakaye katika hadhira kwa haja
Ni kama kumwamuru aliyeingia aswali rakaa mbili za maamkizi ya Msikiti, au kumwamuru mwenye kuziruka shingo za watu akae, au kumuuliza mtu jambo fulani, au kumjibu anayemuuliza, au kumwamuru mtu aingie na mfano wa hayo.
Hayo yote yamethibiti toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Baadhi yake yashaelezwa nyuma na mengineyo yako njiani.
3- Kuwahimiza watu watoe swadaqah kwa masikini wakimwona
Imepokelewa toka kwa Abu Sa’iyd Al-Khudriyy akisema: “Alikuja mtu mmoja Siku ya Ijumaa akiwa katika hali mbaya sana (wakati Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anakhutubu). Rasuli wa Allaah akamuuliza: ((Umeswali?)). Akasema: Hapana. Akamwambia: ((Swali rakaa mbili)), na akawahimiza watu kumtolea swadaqah. Wakazikusanya chini nguo zao, na Rasuli akampa nguo mbili kati ya zilizokusanywa”. [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (3/106)].
Tanbihi:
Kutoa swadaqah kwa masikini wakati wa khutbah, kunaweza kufanyika ikiwa khatibu amenyamaza. Ama desturi iliyozagaa kwenye Misikiti ya kupita mhudumu wa Msikiti na kapu au sanduku kwa Waumini kwa ajili ya kukusanya swadaqah – huku imamu anakhutubu -, hakuna shaka ya kwamba jambo hilo si la kisharia kutokana na ujumuishi wa Hadiyth zenye kuamuru kuisikiliza khutbah, zenye kuharamisha kuzungumza au kufanya vitendo visivyo na maana wakati wa khutbah kama tutakavyokuja kuzungumza.
4- Kuikata khutbah ili kulishughulikia jambo lililomtokea kisha arudi kwenye khutbah
Kuna Hadiyth nyingi zinazohusiana na hili. Kati ya Hadiyth hizo ni Hadiyth ya Jaabir bin ‘Abdullah –kuhusu kisa cha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuanza kuitumia mimbari baada ya kuwa akikhutubu juu ya kigogo cha mtende- : “Ilipokuwa Siku ya Ijumaa, alisogea juu ya mimbari. Kigogo cha mtende kikapiga ukelele, kama anavyolia mtoto mdogo. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akateremka, akakikumbatia, nacho kinalia kilio cha kunung’unika cha mtoto anayebembelezwa. Kilikuwa kinalia kutokana na khutbah kilichokuwa kikiisikia”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (3584)].
Na Hadiyth ya Abu Rifa’at aliyesema: “Nilifika kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa anakhutubu nikasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Kuna mtu mgeni amekuja anaulizia kuhusu dini yake, haijua dini yake ni ipi. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akanigeukia, akaacha kukhutubu, akanijia, na akaleta kiti ambacho nadhani miguu yake ni ya chuma. Akakaa na akaanza kunifundisha aliyofundishwa na Allaah. Kisha akarudi kwenye khutbah yake akaikamilisha hadi mwisho wake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (876) na An-Nasaaiy (8/220)].
5- Kutenganisha baina ya khutbah na Swalaah ili kulishughulikia jambo lililomtokezea
Imepokelewa toka kwa Anas akisema: “ Hakika nilimwona mtu akimzungumzisha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa amesimama baina yake na Qiblah baada ya kuqimiwa Swalaah. Aliendelea kuzungumza naye, na hakika niliwaona baadhi yetu wakisinzia kutokana na muda mrefu wa kusimama Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na mtu huyo”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (643) na Muslim (376)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
052-Wanayotakiwa Kuyafanya Maamuma Wakati Wa Khutbah
Alhidaaya.com [3]
1- Wajisogeze karibu na khatibu
Imepokelewa toka kwa Samrah bin Jun-dub ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hudhurieni khutbah, na mkurubieni khatibu, kwani hakika mtu hatoacha kujiweka mbali mpaka awekwe nyuma peponi hata kama ataingia)). [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1108) na wengineo].
Na imepokewa toka kwa Aws bin Aws toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Mwenye kuoga Siku ya Ijumaa na akasafisha kichwa chake, akatoka mwanzo wa wakati na akawahi mwanzo wa khutbah, na akatembea kwa miguu asipande kipando, na akawa karibu na imamu, na akasikiliza na kunyamaza, basi anapata kwa kila hatua amali ya mwaka)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (345), At-Tirmidhiy (496), An-Nasaaiy (3/95) na Ibn Maajah (1087)].
2- Wamwelekee khatibu kwa nyuso zao wakati anapotoa khutbah
Imesuniwa maamuma wamwelekee khatibu wakati anapokhutubu kwa nyuso zao. Hili halina uthibitisho wowote sahihi uliorufaishwa kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), lakini imethibiti toka kwa Ibn ‘Umar ya kwamba imamu alikuwa hakai isipokuwa yeye humwelekea. [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdul Razzaaq (5391), na kwa njia ya Ibn Al-Mundhir (4/74) na Al-Bayhaqiy (3/199)].
Na imepokelewa toka kwa Anas ya kwamba yeye alikuja Siku ya Ijumaa, akaegemea ukutani, na akamwelekea imamu. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (2/118), na Ibn Al-Mundhir toka kwake (4/74)].
At-Tirmidhiy kasema (2/283): “ Hili walilifanya Maulamaa katika Maswahaba wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na wengineo; walikuwa wakipendelea kumwelekea imamu wakati anakhutubu”.
3- Waisikilize khutbah na wasizungumze wakati inaendelea
Tumeeleza katika Hadiyth ya Salmaan kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Haogi mtu Siku ya Ijumaa, kisha akanyamaza wakati imamu anakhutubu, isipokuwa hughufiriwa yaliyo kati yake na Ijumaa nyingine)). [Hadiyth Swahiyh: Imeelezwa nyuma kidogo].
Na imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ukimwambia mwenzako nyamaza Siku ya Ijumaa na imamu anakhutubu, basi umejiharibia)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (934) na Muslim (851)].
Na katika Hadiyth ya ‘Amri bin Shu’ayb toka kwa baba yake toka kwa babu yake ikiwa Marfu’u: (( Na aliyejiharibia, na akaziruka shingo za watu, basi thawabu zake ni nakisi)). [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (347) na Ibn Khuzaymah (1810)].
Jamhuri ya Maulamaa wameharamisha watu waliohudhuria khutbah kuzungumzishana.
Faida Mbili:
Ya kwanza:
Ikiwa baadhi ya hadhira wataongea, basi inajuzu kuwanyamazisha kwa ishara. Imepokelewa toka kwa Anas akisema: “Wakati Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa amesimama anakhutubu siku moja juu ya mimbari, mtu mmoja alisimama na kusema: Lini kitasimama Qiyaamah ee Nabii wa Allaah? Rasuli hakumjibu, na watu wakamwashiria akae, naye akakataa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (6167), Ibn Al-Mundhir (1807) na Ibn Khuzaymah (1796)].
Ninasema: “Kumjibu aliyetoa salaam hujumuishwa na hili pia, hakuwi ila kwa kuashiria”.
La pili:
Inajuzu kuzungumza na khatibu wakati anakhutubu kwa haja, sawasawa kwa kuanza kumsemesha au kumjibu kama atamsemesha mtu. Anas amesema katika Hadiyth: “Bedui mmoja wa majangwani alikuja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa anakhutubu Siku ya Ijumaa na kusema: Ee Rasuli wa Allaah! Mifugo imeangamia”. [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa katika mlango wa Swalaah ya kuomba mvua].
Na katika kisa cha Sulayk Al-Ghatwafaaniy, alipoingia Msikitini akakaa – na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anakhutubu -, Rasuli alimuuliza: ((Je, umeswali rakaa mbili?)). Akasema: Hapana. Akamwambia: ((Simama uswali rakaa mbili)). [Hadiyth Swahiyh: “Takhriyj” yake ishaelezwa].
4- Mtu asiziruke shingo za watu wala asitenganishe kati ya watu wawili
Imepokelewa toka kwa ‘Abdullah bin Bisr akisema: “Alikuja mtu mmoja akiziruka shingo za watu. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: ((Kaa. Hakika umewaudhi watu na umechelewa)). [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1118), An-Nasaaiy (3/103) na Ahmad (4/188)].
Na pia Hadiyth ya ‘Abdullah bin ‘Amri tuliyoielezea: (( Na aliyejiharibia, na akaziruka shingo za watu, basi thawabu zake ni nakisi)). [Hadiyth Hasan: Imetajwa nyuma kidogo].
Makamio haya hayatamgusa mtu aliyekuta mwanya kati ya watu wawili, kwa kuwa uzembe umefanywa na wao, na mrukaji hatakuwa na makosa. Pia kwa aliyepatikana na haja ikabidi atoke, kisha akataka kurudi kwenye nafasi yake.
Katika Hadiyth Marfu’u ya Salmaan: “ Kisha akaenda na asiingie kati ya watu wawili, halafu akaswali aliyoandikiwa, kisha imamu anapotoka akasikiliza, basi hughufiriwa yaliyo kati yake na Ijumaa nyingine”. [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa nyuma kidogo].
Kutenganisha kati ya wawili inakuwa ni pamoja na kukaa kati yao, au kumtoa mmoja wao na kukaa mahala pake. Pia kunaweza kuwa kwa kuwaruka tu, na ziada iliyopo katika urukaji huu, ni kunyanyua miguu juu ya vichwa vyao na mabega yao.
5- Mtu asimsimamishe mtu na kukaa mahala pake
Imepokelewa toka kwa Jaabir toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Kamwe asimsimamishe mmoja wenu mtu Siku ya Ijumaa, kisha aende yeye akakae mahala pake, lakini aseme: Fungueni nafasi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (2177), Ahmad (3/295), na kama hii hii katika Swahiyh Mbili toka kwa Ibn ‘Umar].
Kusema: “Fungueni nafasi”, ni pale wakati khatibu bado hajaanza kuzungumza, na kama ameanza basi ni kwa ishara.
6- Akisinzia basi akakae sehemu nyingine
Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar akisema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Akisinzia mmoja wenu [katika majilisi yake Siku ya Ijumaa], basi ahame toka majilisi yake [kwenda kwingine])). [Hadiyth Hasan kwa Sanad tofauti: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1119), At-Tirmidhiy (526), Ahmad (2/22) na wengineo].
Hikma ya kubadilisha sehemu ni kwamba msogeo huondosha usingizi. Pia yawezekana hikma ikawa ni kuihama tu sehemu ambayo mghafala umempata kwa kulala, ingawa mlalaji hana makosa. [Naylul Awtwaar (3/298)].
7- Je, inajuzu “Al-Ihtibaa” wakati wa khutbah?
“Al-Ihtibaa” ni kuisimamisha miundi miwili na kuizungushia nguo, au kuifumbata mikono miwili juu ya magoti na kuyafanya mhimili wa kujiegemezea. Ibn Al-Athiyr amesema: “Hilo limekatazwa kwa kuwa kikao hiki huleta usingizi na kumfanya mtu asiisikie khutbah mbali na kuhatarisha uvunjifu wa wudhuu wake”.
Imesimuliwa toka kwa Mu’aadh bin Anas toka kwa baba yake: “Kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza “Al-Ihtibaa” Siku ya Ijumaa na imamu anakhutubu”. [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1110), At-Tirmidhiy (514) na Ahmad (3/439)].
Hadiyth hii ina mvutano, na kauli yenye nguvu inasema kuwa ni Dhwa’iyf”. Na kwa ajili hiyo, Maulamaa wengi wameruhusu “Al-Ihtibaa”.
Ninasema: “Ikiwa ni hivyo, basi kuacha ni bora hata kama Hadiyth ni Dhwa’iyf. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi”.
8- Akikumbuka Swalaah ya Faradhi aliyoisahau au alilala ikampita..
Atasimama na kuilipa hata kama imamu anakhutubu. Ni kwa Hadiyth ya Anas ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwenye kusahau Swalaah [au akalala ikampita], basi aiswali anapoikumbuka, haina kafara isipokuwa hilo)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (597) na Muslim (684)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
053-Yanayotendwa Katika Swalaah Ya Ijumaa
Alhidaaya.com [3]
· Kiasili Swalaah Ya Ijumaa Ni Rakaa Mbili
Si nne zilizopunguzwa. Ni kwa Hadiyth ya ‘Umar bin Al-Khattwaab aliyesema: “Swalaah ya Adhw-haa ni rakaa mbili, na Swalaah ya Fitri ni rakaa mbili, na Swalaah ya Safari ni rakaa mbili, na Swalaah ya Ijumaa ni rakaa mbili kiukamilifu bila kupunguza kwa ulimi wa Nabii wenu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (1/232), Ibn Maajah (1063) na Ahmad (1/37). Angalia Al-Irwaa (3/106)].
Maulamaa wote wamekubaliana kwamba Swalaah ya Ijumaa ni rakaa mbili.
· Kilichosuniwa Kusomwa Kwenye Swalaah Ya Ijumaa
Imepokelewa toka kwa Raafi’i kwamba Abu Hurayrah aliswalisha Ijumaa, na akasoma baada ya Suwratil Jum-’ah katika rakaa ya pili: (( إذا جاءك المنافقون)) . Akasema: “Nikamwahi Abu Hurayrah wakati alipoondoka nikamwambia: Wewe umesoma Suwrah mbili ambazo ‘Aliy bin Abiy Twaalib alikuwa akiziswalishia huko Kufa”. Abu Hurayrah akasema: “Hakika mimi nimemsikia Rasuli wa Allaah akiziswalishia Siku ya Ijumaa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (877), At-Tirmidhiy (519), Abu Daawuud (1121) na Ibn Maajah (1118)].
Na imepokelewa toka kwa An-Nu’umaan bin Bashiyr akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anasoma kwenye ‘Iyd Mbili na kwenye Ijumaa: سبح اسم ربك الأعلى na هل أتاك حديث الغاشية [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (878), At-Tirmidhiy (533), Abu Daawuud (1122) na An-Nasaaiy (3/112)].
· Aliyetanguliwa Katika Swalaah Ya Ijumaa
Atakayefika katika Swalaah ya Ijumaa, atajiunga na imamu katika hali yoyote atakayomkuta nayo. Na kama ataipata rakaa moja pamoja na imamu [kwa mujibu wa makhitilafiano tuliyoyazungumzia kuhusu upatikanaji wa rakaa], basi ataiongezea nyingine baada ya imamu kutoa tasliym. Na kama hakuzipata rakaa mbili kama kuwakuta wako kwenye sijdah au kwenye kikao cha tashah-hud [au kwenye rukuu kwa yule asiyehesabu kwamba rakaa inapatikana kwenye rukuu] katika rakaa ya pili, basi huyo ataswali nne. Hili ndilo walilolifutu Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar akisema: “Mtu akiipata rakaa Siku ya Ijumaa, basi atakamilisha na nyingine moja, na kama atawakuta wako tashah-hud, basi ataswali nne”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdul Razzaaq (5471), Ibn Abiy Shaybah (2/37) na Al-Bayhaqiy (3/204)].
Imepokelewa pia toka kwa Ibn Mas-’oud akisema: “ Mwenye kuipata rakaa, basi ameipata Ijumaa, na ambaye hakuipata Ijumaa, basi aswali nne”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdul Razzaaq (5477), Ibn Abiy Shaybah (2/37) na Al-Bayhaqiy (3/204)].
Aidha, Sheikh wa Uislamu ameisimulia toka kwa Anas akisema: “Hakuna Swahaba yeyote ajulikanaye kwamba amekwenda kinyume na hili, na ni wengi tu waliosema kwamba hilo ni Ijma’a ya Maswahaba”. Nalo pia ni kauli ya Jamhuri: Maalik, Ash-Shaafi’iy, Ahmad na wengineo.
· Kufurika Msikiti Katika Swalaah Ya Ijumaa
1- Ikiwa mtu atakosa nafasi kutokana na kujaa Msikiti hadi pomoni, kama ataweza kurukuu na kusujudu kwa namna awezayo, basi atafanya hata kama ni juu ya mgongo wa mwenzake au kwa kuashiria. Hili litamtosheleza kwa kuwa ndio ukomo wa uwezo wake, na halitofautishwi na mtu kushindwa kurukuu au kusujudu kwa sababu ya ugonjwa, au vita na kadhalika. ‘Umar bin Al-Khattwaab kasema: “Msongamano ukizidi, basi na asujudu mmoja wenu juu ya mgongo wa nduguye”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdul Razzaaq (5469), At-Twayalsiy (70), na kwa njia yake Ahmad (1/32) na Al-Bayhaqiy (3/183)].
Hii ni kauli ya Ath-Twawriy, Ash-Shaafi’iy, Ahmad, Is-Haaq, Asw-haabu Ar-Raay na wengineo.
2- Msikiti ukisongeka, viwanja vyake vikajaa, na safu zikashikana, hapo inajuzu kuswali kwenye vichochoro, au nyumba zilizoshikana na safu, na hata juu ya paa la Msikiti. Na lau kama ukuta utazuia kati ya mtu na imamu au mfano wake, basi haidhuru. Na hili lishaelezwa katika mlango wa Swalaah ya Jamaa.
· Sunnah Baada Ya Ijumaa
Imesuniwa – baada ya Swalaah ya Ijumaa – mtu aswali rakaa mbili au nne, na kuswalia nyumbani ni bora zaidi. Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayekuwa ni mwenye kuswali kati yenu baada ya Ijumaa, basi aswali baada yake rakaa nne [Na kama kitu kitakuharakiza, basi swali rakaa mbili Msikitini, na rakaa mbili ukirejea] )). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (822), Abu Daawuud (1131), At-Tirmidhiy (523), An-Nasaaiy (3/113) na Ibn Maajah (1132)].
Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa haswali baada ya Ijumaa mpaka aondoke na kuswali rakaa mbili nyumbani kwake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Humaydiy (976), na kutoka kwake Ibn Al-Mindhir (1878). Na asili yake ni katika Al-Bukhaariy (937) na Muslim (882)].
Mas-ala Mbalimbali
· Idadi Ambayo Kwayo Ijumaa Inaswihi
[Angalia Al-Awsatw (4/29), Al Maw-‘idhwat Al Hasanah cha Swiddiyq Khan na Al-Ajwibat Al-Hasanah uk. 76-78.].
Swalaah ya Ijumaa ni Faradhi kati ya Faradhi za Allaah Mtukufu, ni alama kati ya alama za Uislamu, na ni Swalaah kati ya Swalaah nyinginezo. Basi yeyote mwenye kushurutisha iwepo ndani ya Swalaah hii idadi zaidi ya ile ya kuruhusu kuswalika Jamaa, basi alete dalili, na dalili hakuna. Na la ajabu ni kuwepo kauli nyingi zilizosemwa katika kukadiria idadi inayotakikana hadi kufikia kauli kumi na tano. [Al-Haafidh amezitaja katika Al Fat-h (2/490)].
Katika kauli zote hizi, hakuna hata dalili moja iliyotolewa isipokuwa kauli isemayo: Hufanyika kwa idadi ya zinavyofanyika Jamaa nyinginezo, yaani kwa mtu mmoja pamoja na imamu. Iwaje? Na masharti yamethibiti kwa dalili maalumu zinazoarifu kwamba kama sharti haipo, basi mshurutishwa naye anakuwa hayupo. Kwa hiyo, kuthibitisha masharti hayo kwa kisicho dalili kimsingi, ni kujiingiza vibaya kwenye hatari, na uthubutu wa kumwongopea Allaah, Rasuli Wake na Sharia Yake.
Na lau kama Allaah Mtukufu Angelikuwa na muradi katika idadi fulani pasina nyingine, basi Angelibainisha hilo katika Kitabu Chake, au kupitia ulimi wa Nabii Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
· Sunnah Ni Kuwa Zisiswaliwe Ijumaa Kwenye Misikiti Mbalimbali Katika Mji Mmoja Ila Kwa Dharura
Dharura ni kama kutotosha Msikiti mmoja kutokana na wingi wa Waumini na mfano wa hilo. Na kama si hivyo, basi hapakukhitilafiwa ya kwamba Ijumaa haikuwa ikiswaliwa katika enzi ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na katika enzi ya Makhalifa Waongofu isipokuwa katika Msikiti wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) tu, na haikuwa ikiswaliwa kwenye Misikiti mingine.
Ama tuyaonayo leo ya kukithiri kwa wingi Misikiti ambayo Ijumaa zinaswaliwa ikiwemo Misikiti midogo iliyoko barabarani na kwenye vichochoro jirani, huku pakiwepo uwezekano wa kuachana nayo kwa watu kwenda kuswali kwenye Misikiti mikubwa, basi bila shaka hili ni katika jambo lenye kuugawa umma huu mgawanyo wa kusikitisha, na kuitoa Ijumaa toka kwenye kiini chake. [Angalia: Al-Awsatw (4/116), Iswlaahu Al-Masaajid cha Al-Qaasimiy (uk. 60-62), Al-Mughniy (2/92) na Majmu’u Al-Fataawaa (24/208)].
· Ijumaa Na ‘Iyd Vikikutana Siku Moja
Ikikutana Siku ya Ijumaa na Siku ya ‘Iyd, Maulamaa wana kauli mbili kuhusu aliyeswali ‘Iyd siku hiyo:
Ya kwanza: Ni lazima aswali Ijumaa pia
Hii ni kauli ya Maulamaa wengi. [Al-Mudawwanah (1/153), Al-Majmu’u (4/320), Tabyiyn Al-Haqaaiq (1/224), At-Tamhiyd (10/272), Al-Awsatw (4/291) na Al-Muhalla (3/303)].
Lakini Mashaafi’i wameiondosha kwa wanavijiji tu na si kwa watu waishio mijini. Hoja za kauli hii ni:
1- Ujumla wa Kauli Yake Ta’alaa:
(( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ))
(( Enyi walioamini! Inaponadiwa kwa ajili ya Swalaah siku ya Ijumaa, kimbilieni kumdhukuru Allaah na acheni kuuza na kununua. Hivyo ni kheri kwenu mkiwa mnajua)). [Al-Jum-‘ah (62:9)].
2- Dalili zilizotangulia kuhusu wajibu wa Swalaah ya Ijumaa.
3- Kwa vile hizo ni Swalaah mbili za faradhi (juu ya kuwepo makhitalifiano kuhusiana na wajibu wa Swalaah ya ‘Iyd), basi faradhi moja haiwezi kuanguka kwa sababu ya nyingine kama Adhuhuri na ‘Iyd.
4- Ruksa ya kuacha Ijumaa kwa aliyeswali ‘Iyd, inawahusu wale tu waliowajibikiwa na Ijumaa katika wakazi wa majangwani na vijijini. Imepokelewa na Abu ‘Ubayd mwachwa huru wa Ibn Azhar akisema: “Niliswali ‘Iyd pamoja na ‘Uthmaan bin ‘Affaan, na hiyo ilikuwa Siku ya Ijumaa. Akaswali kabla ya khutbah, kisha akakhutubu akasema: Enyi watu! Hakika hii ni siku ambayo zimewakusanyikieni ‘Iyd mbili. Basi mwenye kutaka kuisubiri Ijumaa katika watu wa maeneo ya miinuko, basi na asubiri, na mwenye kupenda kurudi, basi nimemruhusu” [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (5572), Maalik (1/141), na kutoka kwake Ash-Shaafi’iy kwenye Al-Umm (1/239) na ‘Abdul Razzaaq (5732)].
Ya pili:
Atakuwa hana Ijumaa, lakini imesuniwa kwa imamu kuisimamisha ili aihudhurie mwenye kutaka na yule ambaye hakuwahi kuswali ‘Iyd.
Ni kauli ya Jamhuri ya Mahanbali, nayo imesimuliwa toka kwa ‘Umar, ‘Uthmaan, ‘Aliy, Ibn ‘Umar, Ibn ‘Abbaas na Ibn Az-Zubayr (Radhwiya Allaahu Anhum). [Al-Mughniy (2/265), Al-Inswaaf (2/403), Kash-Shaaful Qinaa’a (2/41), na Majmu’u Al-Fataawaa (24/211)].
Kauli hii katika dalili yake, imetegemea Hadiyth mbili Marfu’u Dhwa’iyf pamoja na baadhi ya athar Swahiyh.
1- Yaliyosimuliwa toka kwa Iyaas bin Abiy Ramlah aliyesema: “Nilimshuhudia Mu’aawiyah bin Abiy Sufyaan akimuuliza Zayd bin Arqam akisema: Je, ulihudhuria pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ‘Iyd Mbili zilizokutana siku moja? Akajibu: Ndio. Akauliza: Ni vipi alifanya? Akasema: Aliswali ‘Iyd, kisha akatoa ruksa kwa Ijumaa kwa kusema: ((Mwenye kutaka kuswali, basi aswali)). [Ni Dhwa’iyf mno: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1070), An-Nasaaiy (3/194) Ibn Maajah (1310) na Ahmad (4/372)].
2- Yaliyosimuliwa toka kwa Abu Hurayrah ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika zimekusanyika katika siku yenu hii ‘Iyd Mbili. Basi mwenye kutaka itamtosheleza na Ijumaa, na sisi tutaswali Ijumaa)). [Ni Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1073), Ibn Maajah (1/13) na Al-Haakim (2/288). Maulamaa kadhaa wameitia dosari kama Ahmad, Ad-Daara Qutwniy na Ibn ‘Abdul Barri. Ina Hadiyth mwenza kwa Ibn Maajah (1312) toka kwa Ibn ‘Umar, na Sanad yake ni Dhwa’iyf].
3- Ni athar ya ‘Uthmaan iliyotangulia ambapo anasema: “Na mwenye kupenda kurudi, basi nimemruhusu”.
Ama kauli ya kundi la kwanza isemayo kwamba hili ni mahsusi kwa watu wa majangwani ambao Ijumaa kwao si wajibu, panaweza kuulizwa: “Ikiwa ni hivyo, basi nini faida ya kauli yake “nimemruhusu”?!
4- ‘Atwaa amesema: “ Ibn Az-Zubayr alituswalisha siku ya ‘Iyd katika siku ya Ijumaa mwanzoni mwa mchana. Kisha tukaenda Ijumaa naye hakutokeza, tukaswali peke yetu. Ibn ‘Abbaas alikuwa Taif, na aliporudi tulimwelezea hilo naye akasema: Ameipata Sunnah”. [Ibn Az-Zubayr akalisikia hilo na kusema: Nilimwona ‘Umar bin Al-Khattwaab zinapokutanika ‘Iyd Mbili, hufanya kama hivi]. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1071), toka kwa ‘Atwaa, An-Nasaaiy (3/194) na Ibn Khuzaymah (1465) toka kwa Wahab bin Kaysaan. Katika baadhi ya Sanad, kuna neno “ameipata” tu bila neno “Sunnah”. Kulithibitisha hili kunahitajia utafiti zaidi. Alaa kulli haal, sisi tunatolea dalili kwa kitendo cha Maswahaba pale ambapo hakuna aliyekwenda kinyume miongoni mwao].
Na kauli ya Swahaba: Ameipata Sunnah, ina hukmu ya Umarufu’u kwa kauli yenye nguvu.
5- Katika kukitimiza kisa cha Ibn Az-Zubayr kupitia kwa Hishaam bin ‘Urwah toka kwa Wahab bin Kaysaan, Hisham amesema: “Nikalieleza hilo kwa Naafi’i, naye akasema: Lilielezwa kwa Ibn ‘Umar, naye hakulipinga”. [Isnadi yake ni Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (2/7)].
6- Imepokelewa toka kwa Abu ‘Abdul Rahmaan As-Sulamiy akisema: “Zilikutana ‘Iyd Mbili wakati wa ‘Aliy. Akawaswalisha Swalaah ya ‘Iyd, kisha akakhutubu juu ya mnyama wake akasema: Enyi watu! Aliyeswali miongoni mwenu ‘Iyd, basi ameiswali Ijumaa yake bila shaka”. Na katika riwaya nyingine: “Mwenye kupenda kuswali Ijumaa, basi aswali, na anayetaka kukaa, basi akae. [Sufyaan kasema: yaani akae nyumbani kwake]”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (2/7), ‘Abdul Razzaaq (5731) na Ibn Al-Mundhir (4/290)].
7- Wamesema: Hakuna katika Maswahaba hawa, aliyejulikana kwamba amekwenda kinyume na hukmu hii.
Jamhuri wamejibu kuhusu athar hizi wakisema kwamba zinachukulika kwa watu wa majangwani ambao Ijumaa kwao si wajibu!!
Ibn ‘Abdul Barri kasema: “Athar hizi zikibeba uwezekaniko wa taawiyl tuliyoitaja, basi haitojuzu kwa Muislamu kuipomosha faradhi ya Ijumaa kwa yule ambaye ni wajibu kwake”.
Ninasema: “Lenye nguvu ni kwamba Ijumaa hupomoka kwa aliyeswali ‘Iyd kwa mujibu wa athar tulizozitaja za Maswahaba, na kwa kutopatikana athar zenye kukhalifiana na hizi toka kwa yeyote kati yao. Na hii bila shaka inazatiti mwega wa Umarufu’u tukizingatia kwamba kauli ya Ibn ‘Abbaas “Ameipata Sunnah” ina hukmu ya Umarufu’u. Ama kuzibebesha athar zote hizi juu ya yule ambaye Ijumaa si wajibu kwake, basi hiyo ni wazi kuwa ni takilifu. Ikiwa athar ya ‘Uthmaan itakuwa salama, basi kwa mwingine inaweza isiwe salama kama inavyoonekana. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi”.
· Imesuniwa Kwa Imamu Aitishe Ijumaa
Na hii ili aswali kwa mwenye kutaka na kwa yule ambaye hakuwahi kuswali ‘Iyd. Hili linapatikana toka kwenye Hadiyth iliyoelezwa nyuma ya An-Nu’umaan bin Bashiyr inayosema kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anasoma katika Swalaah ya ‘Iyd na Swalaah ya Ijumaa Suwrat Al-A’alaa na Suwrat Al-Ghaashiyah. Anasema: “Na inapokutana ‘Iyd na Ijumaa katika siku moja, anazisoma Suwrah hizi mbili katika Swalaah mbili”. [Hadiyth Swahiyh: “Takhriyj” yake imeshaelezwa].
· Aliyeswali ‘Iyd, Na Asiswali Ijumaa, Je Adhuhuri Kwake Ni Lazima?
Imekuja katika athar ya ‘Atwaa – katika kisa cha Ibn Az-Zubayr -: “Akaswali Ijumaa rakaa mbili baada ya Swalaah ya fitr, kisha hakuongeza juu ya Swalaah hizo mpaka akaswali Alasiri. Akasema: Ama Mafuqahaa, wao hawakuzungumza kuhusu hilo. Ama kwa asiye faqihi, yeye kakilaumu alichokifanya Ibn Az Zubayr. Akasema: Mimi hakika nilimlaumu kwa hilo, na nikaswali Adhuhuri siku hiyo, mpaka tulipokuja kujua kwamba ‘Iyd Mbili ilikuwa zinapokutana vile vile, huswaliwa Swalaah moja”. [Isnadi yake ni Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdul Razzaaq (5725) na Abu Daawuud (1072) kwa ufupi].
Ash-Shawkaaniy kasema: “Inavyoonyesha ni kuwa hakuswali Adhuhuri, na kwa kuwa Ijumaa inapopomoka kwa njia kati ya njia za kuhalalisha, basi si lazima kuswali Adhuhuri kwa ambaye imempomokea. Ni wazi kwamba wanaosema hivyo ni wale wenye kusema kuwa Ijumaa ndio asili, na wewe unajua fika kwamba Alilolifaradhisha Allaah Mtukufu kwa Waja Wake katika Siku ya Ijumaa, ni Swalaah ya Ijumaa. Hivyo basi, kulazimisha Adhuhuri kwa aliyeiacha kwa udhuru au bila udhuru, kunahitajia dalili, na hakuna dalili ifaayo kuishikilia juu ya hilo kwa ninavyofahamu mimi”. [Naylul Awtwaar (3/336)].
Ninasema: “ Ama kuipomosha Adhuhuri kwa yule ambaye hakuswali Ijumaa baada ya kuwa ameswali ‘Iyd, mimi sijui kama kuna Swahaba yeyote aliyelikubali hilo. Na hii pakizingatiwa kuwa imekuja toka kwa ‘Atwaa mwenyewe akisema: “Zilikutana ‘Iyd Mbili katika enzi ya Ibn Az-Zubayr, akawaswalisha ‘Iyd, kisha akawaswalisha Ijumaa Swalaah ya Adhuhuri rakaa nne”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (2/7)].
Roho hairidhiki wala kutulia kwa kuipomosha Adhuhuri. Lililo bora ni mtu kwenda Ijumaa ili aondokane na mvutano huu. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.
· Ijumaa Ikiwafikiana na Siku Ya ‘Arafah
Mahujaji hawaswali Ijumaa, bali wanaswali Adhuhuri na Alasiri kwa kukusanya na kupunguza. Na kabla ya hapo, imamu huwakhutubia khutbah ya ‘Arafah kama alivyofanya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hayo yatakuja kwenye mlango wa Hijjah Insha Allaah.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
054-Swalaah Ya ‘Iyd Mbili
Alhidaaya.com [3]
· Hikma Ya Kuwekwa ‘Iyd Mbili
Ni kwamba kila watu wana siku yao maalumu ambapo hujipamba na kutoka majumbani mwao wakiwa na mapambo yao. [Hujjat Allaah Al-Baalighah cha Ad-Dahlawiy (2/23)].
Imepokelewa toka kwa Anas (Radhwiya Allaahu Anhu) akisema: “ Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuja, na watu wa Madiynah wana siku mbili wanazozisherehekea katika ujahilia, naye akasema: ((Nimewajieni, nanyi mna siku mbili mnazozisherehekea katika ujahilia. Na hakika Allaah Amewabadilishieni kwa siku nyingine bora zaidi kuliko hizo: Siku ya Kuchinja, na Siku ya Fitwri)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1134), An-Nasaaiy (3/179), Ahmad (3/103), Al-Baghawiy (1098) na wengineo].
“Yaani, kwa kuwa siku za Fitwr na kuchinja zimewekwa na Allaah Mtukufu, na ndizo Alizozichagua kwa Waja Wake, na kwa kuwa huja baada ya kutekeleza nguzo mbili adhimu kati ya nguzo za Uislamu ambazo ni Hijjah na Swiyaam. Na ndani ya nguzo hizi mbili, Allaah Huwaghufiria mahujaji na wafungaji, na Hueneza Rahma Zake kwa Viumbe Wake wote watiifu.
Ama siku za Nayrouz na Marjani, siku hizi zilichaguliwa na watawala wa enzi hizo kutokana na uwastani wa majira ya wakati na hali ya hewa, au kwa faida nyinginezo za mpito. Bila shaka tofauti iko wazi kati ya faida mbili kwa mwenye kulitaamuli hilo”. [Al Fat-hu Ar Rabbaaniy bitartiyb Musnadi Ahmad cha Al-Bannaa (6/119)].
· Hukmu Ya Swalaah Ya ‘Iyd Mbili
Maulamaa wamekhitalifiana kuhusu hukmu ya Swalaah ya ‘Iyd Mbili katika kauli tatu:
Ya kwanza:
Ni wajibu kwa kila mtu binafsi (Fardhu ‘Ayn)
Ni kauli ya Abu Haniyfah, moja ya kauli za Ash-Shaafi’iy, na riwaya toka kwa Ahmad. Pia ni kauli ya baadhi ya wafuasi wa Maalik, na ni chaguo la Sheikh wa Uislamu. [Al-Badaai-’i (1/273), Ibn ‘Aabidiyn (2/166), Ad-Dusuwqiy (1/396), Al-Inswaaf (2/240), Majmu’u Al-Fataawaa (23/161) na As-Subul Al-Jarraar (1/315)].
Dalili zao ni:
1- Kauli Yake Ta’alaa:
((فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ))
((Basi swali kwa ajili ya Rabb wako na chinja kwa ajili Yake)). [Al-Kawthar (108:2)]
Agizo hapa ni la wajibu.
2- Kauli Yake Ta’alaa:
((شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ۖوَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۗ يُرِيدُ اللَّـهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّـهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ))
Mwezi wa Ramadhwaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe mwongozo kwa watu na hoja bayana za mwongozo na pambanuo (la haki na batili). Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi na afunge. Na atakayekuwa mgonjwa au safarini, basi (inapaswa kulipa) idadi sawa katika masiku mengineyo. Allaah Anakutakieni mepesi na wala Hakutakieni magumu; na ili mkamilishe idadi na ili mumkabbir Allaah kwa kuwa Amekuongozeni na ili mpate kushukuru. [Al-Baqarah: 185]
Agizo la kupiga takbiyr katika ‘Iyd Mbili ni agizo la Swalaah yenye kukusanya takbiyr iliyozoeleka, na takbiyr za ziada kwenye rakaa ya kwanza na ya pili.
3- Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwajibika na Swalaah hii katika ‘Iyd Mbili, na hakuiacha katika ‘Iyd yoyote ile, na Makhalifa wake na Waislamu waliendelea na Swalaah hii baada yake.
4- Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaamuru watu kutoka kwa ajili ya Swalaah hii hata wanawake, wanawali na wenye hedhi. (Wenye hedhi aliwaamuru wakae kando na sehemu ya kuswalia). Hata pia alimwamuru asiye na abaya aazime kwa mwenzake. Haya yatakuja kuzungumziwa.
5- Swalaah hii ni moja kati ya utambulisho adhimu na bayana wa Uislamu, hivyo imekuwa ni wajibu kama Swalaah ya Ijumaa. Na kwa ajili hiyo, ni lazima kuwapiga vita wenye kukataa katakata kuiswali.
6- Swalaah hii inaipomosha Swalaah ya Ijumaa ikiwa zitawafikiana katika siku moja kama ilivyotangulia. Na kisicho wajibu hakiwezi kukipomosha kilicho wajibu.
Ya pili:
Ni wajibu kwa kutoshelezana (Fardhu Kifaayah)
Ikiwa baadhi wataiswali, basi itawapomokea waliobaki. Ni kauli ya Hanbali na baadhi ya Mashaafi’i. [Al-Mughniy (2/304), Kash-Shaaful Qina’a (2/50) na Al-Majmu’u (5/2). An-Nawawiy amedai kwamba kuna Ijma’a ya Maulamaa wote kwamba Swalaah hii si Fardhi ‘Ayn (kila mtu binafsi), lakini hayo yamevunjwa nguvu katika yaliyozungumzwa nyuma].
Hoja zao ni dalili zile zile zilizotolewa na kundi la kauli ya kwanza lakini wamesema: “Si lazima kwa kila mtu binafsi kwa kuwa Swalaah haijawekewa adhana. Si wajibu kwa mtu binafsi sawa na Swalaah ya Janazah, na kama ingelikuwa hivyo, basi ingelazimu mtu aisikilize khutbah yake kama khutbah ya Ijumaa.
Ya tatu:
Ni Sunnah iliyokokotezwa lakini si wajibu. Ni kauli ya Maalik, Ash-Shaafi’iy na wafuasi wao wengi. [Ad-Dusuwqiy (1/396), Jawaahirul Ikliyl (1/101), na Al-Majmu’u (5/2)].
Hoja yao ni:
1- Neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kumwambia bedui wakati alipomtajia Swalaah tano akasema: “Je, kuna jingine zaidi ya hilo juu yangu?” Akasema: ((Hapana, ila ukilifanya la Sunnah)), na mengine yaliyo ndani ya maana hii. [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa nyuma mara nyingi].
2- Swalaah hii ni Swalaah yenye rukuu na sijdah na haikuwekewa adhana!! Hivyo si wajibu kisharia kama ilivyo Swalaah ya Dhuhaa.
· Kauli Yenye Nguvu
Ni kauli ya kwanza kutokana na dalili zake zilizotajwa. Ama kusema kwamba ni Sunnah iliyokokotezwa, kauli hii ni dhaifu. Ama swali la bedui kwa Rasuli, hilo halina hoja, kwa kuwa Rasuli kazitaja Swalaah tano kimahususi ili kuzisisitizia, kuonyesha ulazima wake wa kudumu, na kukariri kwake usiku na mchana. Ama nyinginezo, uwajibu wake ni wa nadra kama Swalaah ya maiti, nadhiri na kadhalika.
Ama kusema kwamba Swalaah hii ni Fardhi ya Kutoshelezana, usemi huu haukai sawa. Kisha katika kutoshelezana, hupatikana ndani yake maslaha ya mtu binafsi kwa kufanya wengine kama kuzika maiti, au kupambana na adui. Lakini katika siku ya ‘Iyd, hakuna maslaha maalumu ambayo baadhi ya watu huyafanya wengine wakafaidika, bali Swalaah ya ‘Iyd imetangaziwa mkusanyiko mkubwa zaidi kuliko wa Swalaah ya Ijumaa pale ambapo hata wanawake wameamuriwa kwenda kuihudhuria, lakini hawakuamuriwa kuhudhuria Swalaah ya Ijumaa ingawa ruksa ipo. Rasuli kasema: ((Kuswali majumbani mwenu ni bora zaidi kwenu)). Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.
· Wakati Wa Swalaah Ya ‘Iyd Mbili
Wakati wa Swalaah ya ‘Iyd huanza baada ya kunyanyuka jua kiasi cha urefu wa mkuki (yaani baada ya kupita wakati wa ukaraha), na humalizika kwa kupinduka jua. Haya ndiyo waliyoyasema Jamhuri (Hanafi, Maalik na Hanbali). [Ibn ‘Aabidyna (1/583), Ad-Dusuuqiy (1/396) na Kash-Shaaful Qina’a (2/50). Ash-Shaafi’iy kajuzisha Swalaah mwanzo wa jua kuchomoza].Imepokelewa toka kwa ‘Abdullah bin Bisr –Swahiba wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) – ya kwamba alitoka pamoja na watu siku ya ‘Iyd el Fitwr au ‘Iyd el Adhw-haa. Akalalamikia imamu kuchelewesha chelewesha na kusema: “Hakika sisi tulikuwa tumeshamaliza saa yetu hii”. Na hiyo ni wakati wa Swalaah ya Adh-dhuhaa. [Hadiyth Swahiyh: Al-Bukhaariy kaitolea maelezo (2/456) na Abu Daawuud kaiunganisha(1135), Ibn Maajah (1317), Al-Haakim (1/295) na Al-Bayhaqiy (3/282)].
· Faida
Ni bora Swalaah ya ‘Iyd el Adh-haa iswaliwe mwanzoni mwa wakati ili watu wapate nafasi nzuri ya kwenda kuchinja baada ya Swalaah. Ama Swalaah ya ‘Iyd el Fitwr, imesuniwa kuichelewesha kidogo na wakati huu ili watu wawahi kutoa zakaatul fitwr. [Vitabu mama vya fiqh vilivyotangulia].
· Hukmu Yake Ikiwa Wakati Wake Umepita
Kuna picha tatu za kupita wakati wa Swalaah ya ‘Iyd: [Al-Badaai-’i (1/276), Ad-Dusuuqiy (1/396-400), Bidaayatul Mujtahid (1/321), Al-Majmu’u (5/27), Al-Mughniy (2/324) na Majma’ul Anhur (1/169)].
Ya kwanza:
Watu wasijue kwamba ni ‘Iyd ila baada ya kupinduka jua
Huu ni udhuru wenye kujuzisha kuichelewesha hadi siku ya pili sawasawa ikiwa ni ‘Iyd el Fitwr au ‘Iyd el Adh-haa. Hili ndilo walilolisema Jamhuri kutokana na Hadiyth ya Abu ‘Umayr bin Anas toka kwa wenzake wengi kati ya Maswahaba wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambao wanashuhudia: “Kwamba wao waliuona mwezi jana, akawaamuru wafungue, na wakipambaukiwa waende kwenye kiwanja chao cha kuswalia”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1157), An-Nasaaiy (3/180) na Ibn Maajah (1653)].
Ya pili:
Waicheleweshe (wote) Swalaah ya ‘Iyd na wakati wake bila ya udhuru uliotangulia
Ikiwa ni ‘Iyd el Fitwr, basi kimsingi itakuwa ishapomoka na haitalipwa. Ama ikiwa ni ‘Iyd el Adh-haa, basi itajuzu kuiakhirisha mpaka siku ya tatu ya kuchinja, kwa maana kwamba itajuzu kuilipa siku ya pili au siku ya tatu kuanzia jua linapopanda mpaka mwanzo wa kupinduka, sawasawa ikiwa kuichelewesha kulikuwa ni kwa udhuru au bila udhuru. Lakini watu wataandamwa na dhana ya kuwa wamefanya vibaya ikiwa walichelewesha bila udhuru.
Ya tatu:
Iswaliwe katika wakati wake wa siku ya kwanza lakini ikawapita baadhi ya watu
Hanafi na Maalik wanasema kwamba haijuzu kisharia kuilipa kwa kuwa ni Swalaah ambayo imewekewa wakati wake maalum na kwa mipaka maalumu. Ni lazima vikamilike vyote ukiwemo wakati. Lakini Ash-Shaafi’iy amejuzisha kuilipa katika wakati wowote aupendao mtu, na kwa namna yoyote, sawasawa akiswali peke yake au kwa jamaa, kwa mujibu wa qaaidah yake ya kuhalalisha kuilipa Sunnah yoyote.
Hanbali naye kasema kwamba ni marufuku kuilipa lakini kaongeza: “Atachaguzwa; akitaka ataiswali rakaa nne, ima kwa tasliym moja au kwa tasliym mbili”.
Ninasema: “Kauli hii ya Hanbali ni dhaifu, na msingi wake ni kuifananisha na Ijumaa!!”
· Lenye Nguvu
Ninaloliona katika picha hizi zote tatu ni kwamba mwenye kupitwa na Swalaah ya ‘Iyd kwa udhuru, basi anaweza kuilipa katika siku ya pili. Na kama si kwa udhuru, basi hatoilipa kwa mujibu wa yaliyoelezwa katika mlango wa kulipa Swalaah zilizompita mtu. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.
· Mahala Inaposwaliwa
Imepokelewa toka kwa Abu Sa’iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu Anhu) akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anatoka siku ya Fitwr na Adh-haa kwenda katika kiwanja cha kusalia, na jambo la kwanza analolianza ni Swalaah”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (956), Muslim (889) na An-Nasaaiy (3/187)].
Na Sunnah iendeleayo kwa Swalaah ya ‘Iyd mbili, ni kuwa iwe kwenye “Muswallaa”, yaani kwenye jangwa au kiwanja kipana, kwa kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Swalaah moja katika Msikiti wangu huu ni bora kuliko Swalaah 1000 katika misikiti mingineyo isipokuwa Al-Masjid Al-Haraam)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1190) na Muslim (1394)].
Lakini pamoja na fadhla hii kubwa, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka na akauacha”. [Al-Madkhal cha Ibn Al-Hajji (2/283)].
Isipokuwa kama kutakuwepo udhuru kama mvua [Kuhusiana na hili, kuna Hadiyth Marfu’u ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali nao msikitini waliponyeshewa na mvua, lakini ni Dhwa’iyf], na mfano wake, au baadhi ya watu kushindwa kutoka kwa sababu ya utu uzima au ugonjwa, hapo itakuwa hapana ubaya kuiswalia msikitini.
Inapasa ijulikane kwamba lengo la Swalaah ni kujumuika Waislamu mahala pamoja. Haitakikani viwepo viwanja vingi katika maeneo yaliyokaribiana bila haja kama tunavyoshuhudia katika baadhi ya miji ya Kiislamu. “Bali hata baadhi ya viwanja hivi, vimekuwa ni mimbari za kivyama za kusambaratisha umoja wa Waislamu. Walaa hawla walaa quwwata illaa bi Allaah”. [Ahkaamul ‘Iydayn (uk. 24) cha Sheikh ‘Aliy Hasan ‘Abdul Hamiyd, Allaah Amhifadhi].
· Faida: Swalaah ya ‘Iyd Makkah
Lililo bora ni kuswalia kwenye Al-Masjid Al-Haraam, kwani viongozi wa dini hawakuacha kuendelea kuswalia ‘Iyd mjini Makkah kwenye Al-Masjid Al-Haraam, na hilo ni bora zaidi kuliko kutoka kwenda kuswalia jangwani. [Al-Majmu’u cha An-Nawawiy (5/524)].
· Kutoka Kwenda Uwanja Wa Kuswalia Na Adabu Zake
1- Ni Sunnah kuoga kabla ya kutoka
Imepokelewa toka kwa Naafi’i kwamba Ibn ‘Umar: “Alikuwa anaoga siku ya Fitwr kabla ya kwenda uwanja wa kuswalia”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Maalik (426), na kutoka kwake Ash-Shaafi’iy (73) na ‘Abdul Razzaaq (5754)].
‘Aliy bin Abiy Twaalib aliulizwa kuhusiana na kuoga akasema: “ Ni Siku ya Ijumaa, Siku ya Arafah, Siku ya Kuchinja, na Siku ya Fitwr”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ash-Shaafi’iy (114), na kupitia kwake Al-Bayhaqiy (3/278)].
2- Kujipamba na kuvaa nguo nzuri
Asili ya kupendelewa hili ni Hadiyth ya Ibn ‘Umar aliyesema: “’Umar alilichukua juba la hariri linalouzwa sokoni, akamwendea Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kumwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Nunua hili ujipambe nalo kwa ‘Iyd na kwa wageni wanaokuja toka nje”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (886), Muslim (2068) na wengineo].
Hadiyth. “Kutokana na Hadiyth hii, imejulikana kwamba kujipamba siku ya ‘Iyd ni ada iliyokuwa imezoeleka kwao, na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakulikemea jambo hilo, na kubakia kwake kumetambulika”. [Haashiyat Assandiy ‘Alaa An-Nasaaiy (3/181)].
Na imepokelewa toka kwa Ibn ‘Abbaas ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Alikuwa anavaa burdah jekundu siku ya ‘Iyd”. [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh: Angalia As-Swahiyha (1279)].
3- Kula kabla ya kutoka kwenda uwanja wa kuswalia na hasahasa katika ‘Iyd el Fitwr
Anas amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa hatoki siku ya Fitwr mpaka ale tende”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (953), At-Tirmidhiy (543), Ibn Maajah (1754) na Ahmad (3/126)].
Na Buraydah kasema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa hatoki siku ya Fitwr mpaka ale, na siku ya kuchinja hali mpaka arudi, na hula sehemu ya mnyama wake aliyemchinja”. [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (542), Ibn Maajah (1756) na Ahmad (5/352)].
Hikma ya kula kabla ya kutoka kwenda kuswali ‘Iyd el Fitwr ni ili asidhani mwenye kudhani kwamba haifai kula mpaka amalize kuswali ‘Iyd. Na katika ‘Iyd el Adh-haa, huakhirisha kula ili kifungua kinywa chake kiwe kwa mnyama wake aliyemchinja. [Al Fat-h (2/447), Al-Mughniy (2/371) na Zaad El Maad (1/441)].
4- Kupiga takbiyr katika ‘Iyd zote mbili tokea pale anapoanza kutoka nyumbani
Allaah Amesema:
(( يُرِيدُ اللَّـهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّـهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ))
((Allaah Anakutakieni mepesi na wala Hakutakieni magumu; na ili mkamilishe idadi na ili mumkabbir Allaah kwa kuwa Amekuongozeni na ili mpate kushukuru)). [Al-Baqarah (2:185)]
Na imetaarifiwa juu ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba yeye: “Alikuwa anatoka siku ya ‘Iyd el Fitwr, na hupiga takbiyr mpaka anapofika uwanja wa kuswalia, na mpaka amalize Swalaah, na anapomaliza Swalaah, huikata takbiyr”. [Mursal, na ina Hadiyth wenza: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (1/487). Angalia Asw-Swahiyhah (170)].
Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar: “Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anatoka kwenda ‘Iyd mbili pamoja na Al-Fadwl bin ‘Abbaas, ‘Abdullah, Al-‘Abbaas, ‘Aliy, Ja’afar, Al-Hasan, Al-Husayn, Usaamah bin Zayd, Zayd bin Haarithah, na Ayman bin Ummu Ayman (Radhwiya Allaahu Anhuum) huku akiinyanyua sauti yake kwa tahliyl na takbiyr”. [Al Albaaniy kasema ni Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bayhaqiy (3/279). Angalia Al-Irwaa (3/123)].
Hivyo basi, kwa mujibu wa makubaliano ya maimamu wanne, inajuzu kwa kila mmoja kupiga takbiyr kwa sauti wakati anapotoka kwenda kuswali ‘Iyd. [Majmu’u Al Fataawaa (24/220)].
Lakini, baadhi ya Maulamaa wametanabahisha kwamba haijuzu katika upigaji takbiyr, kujumuika watu wote katika sauti moja kama wanavyofanya watu hivi leo. [Kati ya waliolisema hili ni Al’Allaamah Al-Albaaniy –kama ilivyo kwenye Asw-Swahiyhah (1/121)-, Ibn Baaz na Ibn ‘Uthaymiyn Allaah Awarehemu wote].
Ninasema: “Kujuzu mjumuiko huu wa watu katika sauti moja kunaweza kutolewa dalili kwa yale aliyoyatolea maelezo Al-Bukhaariy kwa kulitaja bayana jina la mhusika Ibn ‘Umar kwamba: “Ibn ‘Umar alikuwa anapiga takbiyr katika quba lake huko Mina, watu walioko msikitini wakaweza kumsikia na wao wakapiga takbiyr, na walioko masokoni nao wakapiga takbiyr mpaka Mina yote ikatikisika kwa takbiyr. Na akina mama walikuwa wakipiga takbiyr nyuma ya sauti ya Bin ‘Uthmaan na ‘Umar bin ‘Abdul ‘Aziyz masiku ya tashriyq pamoja na wanaume msikitini.
Hivyo, mas-ala ni mahala pa ijtihaad na kuangalia, haitakikani kugombana na kushikana mashati kwa ajili yake.
· Tamko La Takbiyr
Hakuna Hadiyth yoyote Marfu’u iliyoripotiwa toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusiana na tamko la takbiyr, lakini imethibiti toka kwa Ibn Mas-’oud ya kwamba yeye alikuwa anasema:
(( الله أكبر الله أكبر، لا إله إلا الله، والله أكبر الله أكبر ولله الحمد)).
[Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (2/168)].
Na Ibn ‘Abbaas alikuwa anasema: “
(( الله أكبر الله أكبر، الله أكبر ولله الحمد، الله أكبر وأجل، الله أكبر على ما هدانا)).
[Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bayhaqiy (3/315)].
Na Salmaan (Radhwiya Allaahu Anhu) alikuwa akisema: “ Pigeni takbiyr:
(( الله أكبر, الله أكبر، الله أكبر كبيرا)).
[Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bayhaqiy (3/316)].
Ama waliyoyaongeza watu wa kawaida na wafuasi wao katika zama hizi kwenye takbiyr katika tunayoyasikia na kuyajua, hayo yametungwa tu na hayana asili yoyote. Al-Haafidh katika Al Fat-h kasema (2/536): “Hakika pamezushwa katika zama hizi ziada katika hilo isiyo na asili yoyote”.
Ninasema: “Katika zama zao ilikuweko (ziada), na sisi hivi leo tuna tungo za mahadhi na nyimbo. Allaahu Atusaidie”.
· Faida
Wakati wa takbiyr katika ‘Iyd el Adh-haa, unaanzia tokea Alfajiri ya siku ya ‘Arafah hadi mwisho wa masiku ya Tashriyq. Hivi ndivyo walivyofanya Jamhuri ya Salaf, Mafuqahaa wa Maswahaba na Maimamu. [Majmu’u Al-Fataawaa (24/220). Angalia Irwaaul Ghaliyl (3/125)].
Wengine wamesema kuwa wakati wa takbiyr huanza baada ya Swalaah lakini hawana dalili ya kuthibitisha. Al-Bukhaariy (2/461) katoa maelezo kwa kulitaja bayana jina la mhusika Ibn ‘Umar akisema: “Ibn ‘Umar alikuwa anapiga takbiyr Mina katika masiku hayo, na baada ya Swalaah, juu ya tandiko lake, katika nyumba yake ya mapumziko, katika baraza lake na barabara zote zilizokuwepo wakati huo”.
5- Wanawake – hata wenye hedhi- watoke na watoto
Imepokelewa toka kwa Ummu ‘Atwiyyah akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alituamuru tuwatoe katika Fitwr na Adh-haa wasichana waliovunja ungo karibuni, wenye hedhi, na wanawali. Ama wenye hedhi, hao watajitenga kando na uwanja wa Swalaah lakini watashuhudia kheri na du’aa ya Waislamu. Nikasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Mmoja wetu anaweza kuwa hana jilbabu. Akasema: Basi ukhti yake amvalishe jilbabu lake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (971) na Muslim (890)].
Ni lazima wanawake wawajibike na adabu za kutoka ikiwa ni pamoja na kutojitia manukato na kujikwatua kama inavyojulikana. Ama watoto, Ibn ‘Abbaas aliulizwa: “Je, uliswali ‘Iyd pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)?” Akasema: “Na’am, lau si hadhi yangu kwake, nisingeliweza kuiswali kutokana na utoto wangu”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (977)].
Lakini, inatakikana wawe pamoja nao watu wa kuwadhibiti wasicheze na kuruka ruka huku na kule na mfano wa hayo sawasawa kama wataswali au la.
6- Kupita njia tofauti wakati wa kwenda kuswali
Imepokelewa toka kwa Jaabir bin ‘Abdallah akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapita njia tofauti inapokuwa siku ya ‘Iyd”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (986)].
Na imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapotoka kwenda ‘Iyd, hurudi kwa njia nyingine tofauti na ile aliyotokea”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Maajah (1301), Ad-daaramiy (1613), Ahmad (8100), Ibn Khuzaymah (1468), Ibn Hibaan (2815), na Al-Bayhaqiy (3/308). Al-Bukhaariy (943) ameitaja kwa kufuatilia Hadiyth ya Jaabir iliyotangulia –nayo ni kwa njia hiyo hiyo!!- Amesema: “Na Hadiyth ya Jaabir ni Swahiyh zaidi”].
Hivyo Maulamaa wengi wamependelea kwenda uwanja wa kuswalia kwa njia na kurudi kwa njia nyingine kwa ajili ya kumwigiza Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
7- Imesuniwa kwenda kwa miguu badala ya kutumia kipando ila kwa dharura
Imepokelewa toka kwa ‘Aliy (Radhwiya Allaahu Anhu) akisema: “Katika Sunnah, utoke kwenda kwenye ‘Iyd kwa miguu”. [Al-Albaaniy kasema ni Hadiyth Hasan. Angalia Swahiyh At-Tirmidhiy (1/164) cha Al-Albaaniy].
Kuna udhwa’iyf ndani ya Hadiyth hii lakini ipo Hadiyth yake mwenza ya Ibn ‘Umar isemayo: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anatoka kwenda ‘Iyd kwa miguu na anarudi kwa miguu”. [Al-Albaaniy kasema ni Hadiyth Hasan. Angalia Swahiyh Ibn Maajah (1071) cha Al-Albaaniy].
Na hii ni endapo uwanja wa kuswalia upo karibu na haiwi uzito kuufikia kwa miguu. Lakini mtu akihitaji kipando, basi hapana ubaya. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.
8- Imesuniwa kwenda mapema
Na hii ni baada ya watu kuswali Alfajiri ili kukaa sehemu zao, na waendelee kupiga takbiyr mpaka imamu atoke kwa ajili ya Swalaah. [Angalia Sharhu As-Sunnah cha Al-Baghawiy (4/302)].
· Hakuna Sunnah Kabla Ya Swalaah Ya ‘Iyd Wala Baada Yake
Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Abbaas akisema: “Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali siku ya Fitwr rakaa mbili, hakuswali kabla yake wala baada yake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (989), At-Tirmidhiy (537), An-Nasaaiy (3/193) na Ibn Maajah (1291)].
Ibn Al-‘Arabiy kasema: “Lau kuswali Sunnah kwenye uwanja wa kuswalia kungelifanywa, basi kungelinukuliwa. Na aliyejuzisha, anaona kwamba huo ni wakati huria wa Swalaah, na mwenye kuacha, anaona kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakulifanya, na mwenye kumfuata Rasuli, basi huyo ameongoka”.
Al-Haafidh kasema: “Ama kuswali tu Sunnah, hakuna katazo lolote lililothibiti kwa dalili maalum isipokuwa kama hilo litakuwa katika wakati wa karaha ambao uko katika masiku yote. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi”. [Fat-hul Baariy (2/552)].
Ninasema: “Baadhi ya watukufu wanaona kwamba uwanja wa kuswalia ‘Iyd ni Msikiti. Hivyo mtu anapoingia hapo, asikae mpaka aswali rakaa mbili. Dalili ni Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwazuia wenye hedhi kukaa hapo na kuwaamuru kujitenga kando. [Hili kalisema Al-’Allaamah Ibn ‘Uthaymiyn Allaah Amrehemu].
Na hapa kuna mtizamo. Kutolea dalili ya kuzuiwa wenye hedhi kunajibiwa kwa kusema kwamba muradi ni wao kujitenga na Swalaah kama ilivyotangulia katika mlango wa twahara. Isitoshe, ardhi yote ni Msikiti na inajuzu kuswali Sunnah ya maamkizi ya Msikiti wakati mtu anapotaka kuswali kwenye sehemu yoyote ya ardhi!! Alaa kulli haal, lau kama Maswahaba wangelikuwa wanaswali maamkizi kwenye uwanja wa kuswalia ‘Iyd, basi lingenukuliwa hilo kama alivyogusia Ibn Al-‘Arabiy. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi. Lakini, lau watu wataswalia Msikitini, basi hakuna shaka juu ya ruksa ya kuswali rakaa hizo za maamkizi”.
· Swalaah Ya ‘Iyd Haina Adhana Wala Iqaamah
Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Abbaas na Jaabir (Radhwiya Allaahu Anhumaa) wakisema: “Haikuwa ikiadhiniwa siku ya Fitwr wala siku ya Adh-haa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (960) na Muslim (886)].
Imepokelewa toka kwa Jaabir bin Samrah (Radhwiya Allaahu Anhu) akisema: “Niliswali pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ‘Iyd mbili, si mara moja, si mara mbili, bila adhana wala iqaamah”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (887), Abu Daawuud (1148) na At-Tirmidhiy (532)].
Ibn Al-Qayyim kasema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapofika sehemu ya kuswalia, anaanza kuswali bila adhana wala iqaamah, wala kusemwa: Aswalaatu Jaami’ah. Na Sunnah, kisifanywe chochote katika hayo”. Na juu ya haya, adhana kwa ajili ya ‘Iyd mbili, ni bid-’a. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.
· Namna Ya Kuswali Swalaah Ya ‘Iyd
Swalaah ya ‘Iyd ni rakaa mbili. Ni kwa Hadiyth ya ‘Umar (Radhwiya Allaahu Anhu) aliyesema: “Swalaah ya safari ni rakaa mbili, na Swalaah ya Adh-haa ni rakaa mbili, na Swalaah ya Fitwri ni rakaa mbili, kiukamilifu bila kupunguza kwa ulimi wa Nabii wenu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).” [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (3/183) na Ahmad (1/37). Ishatajwa nyuma].
Inaswaliwa katika picha ifuatayo:
1- Ataianza kwa takbiyrah ya kuhirimia kama zilivyo Swalaah nyinginezo.
2- Kisha baada ya takbiyrah ya kuhirimia, atapiga takbiyrah nyingine saba kabla hajaanza kusoma. Haikupokelewa toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba alikuwa ananyanyua mikono yake wakati akipiga takbiyrah za Swalaah ya ‘Iyd, lakini Ibn Al-Qayyim kasema: “Ibn ‘Umar - ingawa ametopea katika kuifuata Sunnah - alikuwa akinyanyua mikono kwa kila takbiyrah”. [Zaad El-Ma’ad (1/441)].
Ninasema: “Anayeona kwamba Ibn ‘Umar hafanyi hili ila kwa tawqiyf toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), basi anaweza kunyanyua mikono yake, na kama si hivyo, basi bora ya uongofu, ni uongofu wa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)”.
3- Haikupokelewa toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) dhikr maalumu wakati anaponyamaza baina ya takbiyrah hizi, lakini Ibn Mas-’oud kasema: “ Baina ya kila takbiyrah mbili ni Himdi kwa Allaah ‘Azza wa Jalla na Sifa kwa Allaah”. [Isnadi yake ni Hasan. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bayhaqiy (3/291)].
4- Kisha ataanza kusoma Al-Faatihahh – baada ya takbiyrah 7- halafu Suwrah. Imesuniwa asome ق والقرآن المجيد katika rakaa ya kwanza, na katika rakaa ya pili asome اقتربت الساعة وانشق القمر kama ilivyothibiti toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (891), An-Nasaaiy katika Al-Kubraa (11550), At-Tirmidhiy (534), na Ibn Maajah (1282)].
Na huenda alisoma kwenye rakaa mbili سبح اسم ربك الأعلى na هل أتاك حديث الغاشية
[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (878), na nyingine toka kwa An-Nu’umaan bin Bashiyr. Imetajwa nyuma kidogo].
5- Na baada ya kisomo, atayafanya mengineyo ya rakaa katika umbile lake la kawaida.
6- Atapiga takbiyrah ya kusimama kwenda rakaa ya pili.
7- Halafu atapiga baada yake takbiyrah tano kwa namna iliyotangulia katika rakaa ya kwanza.
8- Atasoma Al-Faatihahh na Suwrah tuliyoieleza.
9- Kisha ataikamilisha Swalaah yake na kutoa tasliym.
Hii ni kauli ya Maulamaa wengi katika Maswahaba na kisha waliokuja baada yao kuhusu sifa ya Swalaah ya ‘Iyd mbili. Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu Anha): “Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akipiga takbiyrah katika Fitwr na Adh-haa; takbiyrah saba katika rakaa ya kwanza, na tano katika rakaa ya pili, mbali na takbiyrah mbili za rukuu”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1150), Ibn Maajah (1280) na Ahmad (6/70)].
Imepokelewa na ‘Amri bin Shu’ayb toka kwa baba yake toka kwa babu yake akisema: “ Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipiga takbiyrah ya ‘Iyd: saba katika rakaa ya kwanza, kisha akasoma, halafu akasoma, kisha akapiga takbiyrah wakarukuu, halafu akasujudu, kisha akasimama akapiga takbiyrah tano, halafu akasoma, kisha akapiga takbiyrah akarukuu, halafu akasujudu”. [Al-Albaaniy kasema ni Hadiyth Hasan. Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1152) na Ibn Maajah (1278). Angalia Al-Irwaa (3/108-112)].
· Khutbah Ni Baada Ya Swalaah, Na Mtu Ana Ruksa Ya Kuondoka Baada Ya Swalaah Au Kubaki Akaisikiliza
Ni Sunnah kwa imamu akhutubu khutbah moja tu baada ya Swalaah – na si khutbah mbili – [Yaliyosimuliwa ya kuwa zilikuwa ni khutbah mbili, ni Dhwa’iyf mno. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi] …kwa kusimama chini na si juu ya mimbari. Hivi ndivyo alivyofanya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Makhalifa Waongofu baada yake.
1- Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaah Anhu) akisema: “Nilihudhuria ‘Iyd pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Abu Bakr, ‘Umar na ‘Uthmaan (Radhwiya Allaahu Anhum). Wote hao walikuwa wanaswali kabla ya khutbah”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (962) na Muslim (884)].
2- Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar: “Kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Abu Bakr na ‘Umar, walikuwa wakiswali ‘Iyd mbili kabla ya khutbah”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (963) na Muslim (888)].
3- Imepokelewa toka kwa Abu Sa’iyd Al-Khudriy akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anatoka siku ya ‘Iyd na Adh-haa kwenda uwanja wa kuswalia. La kwanza analoanza nalo ni Swalaah, kisha huondoka pale aliposwalishia, akasimama kuwaelekea watu – na watu wamekaa kwenye safu zao - kisha akawapa mawaidha, akawausia na akawaamuru. Na kama anataka kuamuru kikosi kiende sehemu fulani basi hukiamuru, au kuamuru jambo lolote huamuru, kisha huondoka”. Abu Sa’iyd kasema: “Watu waliendelea na hayo mpaka nilipotoka na Marwaan – naye ni Gavana wa Madiynah - kwenda kwenye Adh-haa au Fitwr. Tulipofika sehemu ya kuswalia, tulishtukizwa kuona mimbari iliyotengenezwa na Kuthayr bin As-Swalt, naye Marwaan ghafla akataka kuipanda kabla ya Swalaah. Nikaikamata nguo yake nikamvuta, naye akanivuta, akapanda na kukhutubu kabla ya Swalaah. Nikamwambia: Mmebadili, Wallaahi. Akasema: Ee Abu Sa’iyd! Unayoyajua hayapo tena. Nikasema: Ninayoyajua Wallaah ni bora zaidi kuliko nisiyoyajua. Akasema: Hakika watu hawakuwa wakikaa kutusikiliza baada ya Swalaah, nami nikaifanya kabla ya Swalaah”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (956) na Muslim (889)].
Kusikiliza khutbah hii si lazima, na imesuniwa kwa imamu awakhiyarishe waliohudhuria baina ya kusikiliza au kuondoka ikiwa ni kukiiga kitendo cha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Imepokelewa toka kwa ‘Abdullah bin As Saaib akisema: “ Nilihudhuria ‘Iyd pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Alipomaliza Swalaah alisema: ((Hakika sisi tunakhutubu. Basi anayetaka kukaa asikilize khutbah akae, na anayetaka kuondoka, basi aondoke”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (1155), An-Nasaaiy (3/185) na Ibn Maajah (1290)].
· Faida
Khutbah ya ‘Iyd ni kama khutbah nyinginezo. Hufunguliwa kwa Himdi, na Kumsifu Allaah Mtukufu. Hakuna Hadiyth Swahiyh inayoelezea kwamba inafunguliwa kwa takbiyrah.
· Je, Watu Hupongezana Kwa ‘Iyd?
Sheikh wa Uislamu amesema kwenye Al-Fataawaa (24/253): “Ama kupongezana siku ya ‘Iyd kwa kuambiana wakati wanapokutana baada ya Swalaah ya ‘Iyd: “Taqabbala Allaahu minnaa waminkum” au “Ahaala ‘alayka”, na mfano wa hayo, hili limesimuliwa toka kwa baadhi ya Maswahaba ya kwamba walikuwa wakilifanya. [Al-Haafidh kasema kwenye Al-Fat-h: (2/517): “Tumesimulia katika Al-Mahaamaliyyaat kwa isnadi Hasan toka kwa Jubayr bin Nafiyr akisema: Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) walikuwa wanapokutana siku ya ‘Iyd huambiana: “Taqabbala Allaahu minnaa wa minka”. Ibn Qudaamah amenukulu kwenye Al-Mughniy (2/259) mfano wake toka kwa Abu Umaamah na wengineo katika Maswahaba wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na amenukulu toka kwa Ahmad akiisifia vizuri Hadiyth ya Abu Umaamah. Angalia Tamaam Al-Minnah uk. 354-356].
Maimamu kama Ahmad na wengineo wameliruhusu lakini Ahmad kasema: Mimi sianzi kumpongeza mtu, na ikiwa mtu atanianza, basi ninamjibu. Na hii ni kwa vile kujibu maamkizi ni wajibu, ama kuanza pongezi, hili ni jambo ambalo halikuamuriwa na pia si jambo ambalo limekatazwa. Basi mwenye kulifanya ana kiigizo, na mwenye kuliacha basi ana kiigizo. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi”.
“Na hakuna shaka kwamba pongezi hizi ni katika akhlaqi njema, ni picha nzuri ya kijamii kati ya Waislamu, zina athari nzuri katika kuimarisha mahusiano na mtangamano, na kueneza roho ya mapenzi kati ya Waislamu. Linaloweza kusemwa kwa uchache kuhusiana na hili ni umpongeze anayekupongeza, na unyamaze kama atanyamaza”. [Waqafaatun Lis Swaaimiyna cha Sheikh Salmaan Al-‘Awdah (uk.99) akikizungumzia kitabu cha Ahkaamul ‘Iydayn cha Hishaam Al-Burghush (uk. 57)].
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/284
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9588&title=02-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20%D9%83%D9%90%D8%AA%D9%8E%D8%A7%D8%A8%D9%8F%20%D8%A7%D9%8E%D9%84%D8%B5%D9%91%D9%8E%D9%84%D9%8E%D8%A7%D8%A9%D9%90%20-%20Kitabu%20Cha%20Swalaah%20%20
[3] http://www.alhidaaya.com/
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9662&title=000-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Swalaah
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9663&title=001-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Kwanza%3A%20Swalaah%20Tano
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9664&title=002-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Baadhi%20Ya%20Dalili%20Za%20Makundi%20Mawili
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9670&title=003-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Hukmu%20Za%20Kidunia%20Kwa%20Asiyeswali
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9671&title=004-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Swalaah%20Ni%20Wajibu%20Kwa%20Nani%3F
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9672&title=005-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Nyakati%20Za%20Swalaah
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9673&title=006-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Masuala%20Yanayohusiana%20Na%20Nyakati%20Za%20Swalaah%20
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9674&title=007-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Kulipa%20Swalaah%20Zilizopita%20
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9675&title=008-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Nyakati%20Zisizoruhusiwa%20Kuswali
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9691&title=009-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Adhana%20Na%20Iqaamah
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9692&title=010-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Kwanza%3A%20Adhana
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9695&title=011-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Pili%3A%20Iqaamah
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9696&title=012-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Masharti%20Ya%20Kuswihi%20Swalaah
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9697&title=013-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Mahala%20Palipokatazwa%20Kuswalia
[18] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9698&title=014-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Sehemu%20Ya%20Mwili%20Inayopasa%20Kusitiriwa%20
[19] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9699&title=015-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Niya
[20] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9700&title=016-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Nguzo%20Za%20Swalaah%20
[21] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9709&title=017-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Waajibati%20Za%20Swalaah
[22] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9710&title=018-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Sunnah%20Za%20Swalaah
[23] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9713&title=019-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Mambo%20Yaliyoruhusiwa%20Ndani%20Ya%20Swalaah
[24] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9714&title=020-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Yaliyokatazwa%20Ndani%20Ya%20Swalaah
[25] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9715&title=021-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Yenye%20Kubatwilisha%20Swalaah
[26] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9716&title=022-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Qunuwt%20Katika%20Swalaah%20Za%20Faradhi
[27] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9721&title=023-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Swalaah%20Za%20Sunnah%20%28Tatwawwu%E2%80%99%E2%80%99u%29
[28] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9726&title=024-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Swalaah%20Ya%20Witr
[29] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9730&title=025-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Qiyaamul%20Layl
[30] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9865&title=026-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Qiyaam%20Ramadhwaan%20%28Tarawehe%29
[31] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9866&title=027-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Swalaat%20Adh-dhuhaa
[32] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9867&title=028-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Swalaat%20Al-Istikhaarah
[33] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9868&title=029-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Swalaat%20At-Tasbiyh
[34] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9869&title=030-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Swalaah%20Ya%20Tahiyyatul%20Masjid%20
[35] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9870&title=031-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Swalaah%20Ya%20Tawbah
[36] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9871&title=032-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Swalaah%20Ya%20Kupatwa%20Jua%20%28Kusuwf%29
[37] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9872&title=033-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Swalaah%20Ya%20Kuomba%20Mvua%20%28Al-Istisqaa%29%20
[38] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9873&title=034-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Sijdah%20Ya%20Kisomo
[39] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9886&title=035-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Sijdah%20Ya%20Kutoa%20Shukran%20
[40] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9887&title=036-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Sijdah%20Ya%20Kusahau%20
[41] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9888&title=037-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Swalaah%20Ya%20Safari
[42] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9890&title=038-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Swalaah%20Ya%20Khofu
[43] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9891&title=039-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Swalaah%20Ya%20Jamaa
[44] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9898&title=040-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Uimamu%20Na%20Hukmu%20Zake%20
[45] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9901&title=041-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Mahala%20Pa%20Kusimama%20Imamu%20Na%20Maamuma
[46] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9902&title=042-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Safu%20Na%20Hukmu%20Zake
[47] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9903&title=043-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Masuala%20Yanayohusiana%20Na%20Sifa%20Ya%20Swalaah%20Ya%20Jamaa%20
[48] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9918&title=044-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Hukmu%20Za%20Aliyetanguliwa
[49] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9919&title=045-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Jamaa%20Zaidi%20Ya%20Moja%20Ndani%20Ya%20Msikiti%20Mmoja%20
[50] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9920&title=046-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Yanayofanyika%20Baada%20Ya%20Kumalizika%20Swalaah
[51] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9921&title=047-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Baadhi%20Ya%20Hukmu%20Za%20Msikiti
[52] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9924&title=048-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Swalaah%20Ya%20Ijumaa%20%20
[53] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9925&title=049-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Maandalizi%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Swalaah%20Ya%20Ijumaa
[54] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9926&title=050-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Adhana%20Ya%20Ijumaa
[55] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9927&title=051-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Khutbah%20Ya%20Ijumaa%20Na%20Hukmu%20Zinazomkhusu%20Khatibu
[56] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9928&title=052-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Wanayotakiwa%20Kuyafanya%20Maamuma%20Wakati%20Wa%20Khutbah%20
[57] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9929&title=053-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Yanayotendwa%20Katika%20Swalaah%20Ya%20Ijumaa%20
[58] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9931&title=054-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Swalaah%3A%20Swalaah%20Ya%20%E2%80%98Iyd%20Mbili