Piga Hesabu Za Zakaah Yako Unayotaka Kutoa Kwa Kutumia Kikokotoo (Calculator) Ya Kuhesabu Zakaah Yako
Mtumwa anapomtumikia bwana wake huwa hana budi kutekeleza amri zote. Juu ya hivyo, atakapoambiwa ya kwamba utumwa wake unamalizika baada ya kumtumikia bwana, basi atafanya juhudi zake kumridhisha matakwa yake ili apate uhuru wake.