Back to the homepageBack to the homepage
Alhidaaya Tathmini Shukurani Kumbukumbu Zako
Name or Nickname : *
Email address : *[P]
City :
Country :
Your message : *

Please copy this 4 letters code into the box on the right : (Why this?)


Messages : 1381 to 1400
Page : 70
Number of messages : 1549
on 16/06/2007 at 14:26

SHUKRANI KWA WOTE WALIYOANZISHA WEBSITE HII..
MOLA AWAPE JAZA KUBWA ..PIA AWAPE NGUVU YA KUZIDI KUENDESHA KAZI HII YA KIISLAMU..
WABILAH AL TAWFIQ..
 
on 15/06/2007 at 14:25

Assalaam alaykum.. Shukran za dhati ziende kwa Mola wetu mpenzi pamoja na kipenzi chetu Mtume(SAW).. Mtume amesema (Asieshukuru watu basi hana shkurani kwa Allah )kwa hiyo sina budi kuwashukuru sana viongozi wa tovuti hii kwa juhudi zao na napenda kuwapa pongezi kubwa,kwa kweli sisi hatuna la kuwalipa isipokuwa tunasema Allah atakulipeni ujira ulio mkubwa hapa duniani na Akhera..amiyn.
Maoni yangu ni.. Nawashauri viongozi wetu watuanzishie "ALHIDAAYA ONLINE" japo wiki mara moja ili waweze kutuunganisha sisi wapenzi wa tovuti hii kuweza kupeana fikra na mawazo mbali mbali kuhusu UISLAM WETU na mengineyo.
Na nawashauri ndugu zangu kuitumia fursa hii adhimu kwa ihsani kubwa kabisa na tuwaombee viongozi wetu hawa dua ili waiendeleze tovuti hii kwa ufanisi mkubwa.
Wabillahi-taufiq.
 
on 02/06/2007 at 14:23

asalam alaykum ndugu wa kiislam mungu aliuekupen ujuz wa kuweza kufungua website hii nzur sana na imepangika hasa na inaelimisha sana na kuwakumbusha watu kwa mambo mengi ya mungu na mtume wake ila nilikua namalalamiko au maombi kwa upande mwengine mana nakumbuka nilikua nikifungua sehem ya qur-an nampata msomaj mmmoja anaitwa minshawwi lakin nashangaa mumemtoa naomba kwa hisan yenu kama kuna uwezekano mumrejeshe na ishallah mungu ataleta heri zaid juu ya uma wa kislam usijekupotea na watu kijisahau masaalam
 
on 31/05/2007 at 14:22

Assalam Aleikum,

Alhamdullilah kwa Website hii hakika ina manufaa sana. Allah Barik ili muzidi kuiendeleza.
 
on 29/05/2007 at 14:21

Assalaamu Alaykum,
Napenda kutoa shukrani zangu kwa ndugu wanaoiendesha Ahidaaya, pia Namuomba Allah Akulipeni mema mnayostahiki kutokana na kazi hii adhimu mnayoiendesha, AAmmiyn.
 
on 29/05/2007 at 14:20

Napenda kuwashukuru watayarishaji hii tovuti kwani tunafaidika sana Mungu awajaze kila la kheri mzidi kutunufaisha.
 
on 14/05/2007 at 14:19

Asalaam alaikum
ALLAH awajalie zaidi mzidi kutuelimisha.
Maoni yangu ni kuanzishwa kwa kipengere kuhusu TIBA ASILIA kama mboga,matunda,habat soda,asali, maziwa n.k.katika kujitibu maradhi mbalimbali angalau kwa wiki mara moja mnaongelea KISUKARI then wiki nyingine labda PRESSURE.
ALLAH awafanyie wepesi,
Shukran, SABAH
 
on 09/05/2007 at 14:18

Assalam Aleykum

Natoa shukran kubwa kwa kutuletea mtandao huu, nimepata faida nyingi na nimeelimika sana kuhusu dini yetu tukufu.

Inshalla mungu awabariki na muzidi kutuongoza tujue vizuri njia ya haki.
 
on 09/05/2007 at 14:16

Mola awabariki.awape afya na uwezo wa kuzidi kutuelimisha na Mola awatakabalie hii kazi tukufu.

Shukran
Saada.
 
on 08/05/2007 at 14:14

Assalam Aleykum

Natoa shukran kubwa kwa kutuletea mtandao huu, nimepata faida nyingi na nimeelimika sana kuhusu dini yetu tukufu.

Inshalla mungu awabariki na muzidi kutuongoza tujue vizuri njia ya haki.
 
on 08/05/2007 at 13:42

Assalamu alaykum waanzilishi na wasomaji wa AlHidaaya wote.
Napenda kuwapongeza wale wote walioanzisha mtandao huu kwa kweli M/Mungu awalipe kila la kheri kw dunia na akhera.
Maoni yangu ni kwamba tunaomba mutuwekee TV on-line kuhusu khabari za Uislamu n Waislmu ulimwenguni.
Ahsanteni ,
WABILLAHI TAWFIQI
 
on 28/04/2007 at 13:29

Asalamu aleykum shukrani zangu nyingi ziwafikie waanzilishi wa al hidaaya,kwani kwa muda mfupi nimepata faida sana ya makala hii na naona hasara kwa yaliyonipita,vipi nitazipata makala za mwanzo ili nifaidike na makala ya mwanzo?
 
on 21/04/2007 at 13:28

Assalaamu 'alaykum yaa ahlal Hidaaya
Alhamdulillahi Wasswalatu Wassalaamu 'alaa Ashrafil Anbiyaa
Amma ba'ad
tunamshukuru Allah kwa juhudi zenu mnazo zifanya za kutuelimisha na kutukumbusha dini yetu kwa njia nyepesi na nzuri ya website yenu ya Alhidaaya ambayo ina ma'alumati mengi yaliyo sahihi yenye faida.Maanshaa aalh.

sisi hatuna cha kawalipa ila kuwombea du'aa Mwenyeezi Mungu awajaze kila la kheri na awape nguvu muendelee kutuelimisha

Kwani kila tunachowauliza mwatujibu ,tunakuombeni msivunjike moyo kutuelimisha .kwani tunakuombeeni mwenyezi mungu awalipe kila la kheri dunia wal akhira. inshaa aalah "Aamiin"
 
on 10/04/2007 at 13:26

Allahu Barik
 
on 14/03/2007 at 13:24

A/S watayarishaji na wausika wa mtandao huu wa alhidaaya, pamoja na waslimu wote wanaotembelea
mtandaohuu. Ningependa kumshukuru ALLAH (SWA) kwa kunipatia nafasi hii ya kuniwezesha kutoa maelezo yangu.La pili nawashukuru watayarishaji
wa makala haya yaliyomo hapa.Masheikh nawashukuru kuyajali matakwa yetu na nawaombea pepo na msamaha kwa (ALLAH).natumaini mtatuongezea khutba za ijumaa za ndugu yetu s. nuurdin (kinsh)ambayo wakina mama waliopo nyumbani husikiliza kama khutba ya ijumaa.
 
on 12/03/2007 at 13:16

Assalaamualeikum, kwa mara nyingine tena narudi kwenyed kitabu hiki cha wageni, ambayo ina wasomaji wengi duniani kote, lengo la kurudi ni kutoa tena maoni na kuwashukuru saana uongozi wa ALHIDAAYA,kwa kazi zao ya kuwakutanisha waislam ktk jumba mmoja ambapo waislam wanapata nafasi ya kuzungumza na kuwasiliana vizuri kabisa,


ya pili ni kutoa ushauri au maoni ya kuwa ingekwepo siku au hata wiki mmoja tuwe tunajadili mas'ala fulaani inayo wahusu waislaam kote duniani, kulichanganua vizuri saana kila mmoja angechangia maoni yake nathani mtakubaliana nami, mada inge andaliwa na uongozi wa ALHIDAAYA.Na kutayarishwa vizuri saana. wassalaamualeikum,
 
on 06/03/2007 at 14:14

Alhamdulilahi namshukuru muumba,ndugu yangu abdullah hayoyote usemayo ni ya kweli kabisa hayana shaka ni kweli na ni dhima kwa Mwenyeezi Mungu kwa haoo wayafanyayo,Na kila mtu ataulizwa vipi alichuma maishani mwake kwa kile alichokitia tumboni kwake,LAKINI sasa nduguyangu abdullah unapo ongea kuhusu mass-ala haya jitahid usi point watu fulani au kabila fulani huo sio utaratibu wa kufahamishana kwa maana hata UK kuna makabila mingi na jamii tofauti yana fanya hivyo hivyo,pokea nasaha hizi kwa kukumbuswa kwa ajili ya allha. JITAHID

asalaam `alaykum
 
on 05/03/2007 at 14:12

Maneno yako Dada Suhayla ni ya kweli kabisa. Huu ndio umekua mpango mkubwa sana wa watu kujipatia pesa za bure, na kusema uongo. Hapa Minnesota kuna ndugu wa Somali wengi sana. Na mambo kama hayo hufanyika sana ili wapate food stamps and pesa. Nina iman kuwa sio sawa, lakini binaadamu waona kupata tuu hawafikirii na mbele za Allah..Wabillahi Tawfiq
 
on 04/03/2007 at 14:11

Assalamu Aleykum Warahmatullahi Wabarakatu.

Alhamdulillahi, namshukuru MwenyeziMungu(swt) kwa neema zake zote alizoturuzuku na kutujaalia sisi tukawa miongoni mwa Waislamu.Ama baada ya kumshukuru Allah (swt) ningepende kuwashukuru nanyi pia kwa jumla na sadakatul jaariyah yenu hii tukufu munayoifanya.Inshaallah Allah awabariki,awalipe mema ya hapa duniani na kesho Akhera na awaongoze kwenye kheri juu ya kheri na imani inayoendelea na kuthibitika vizuri pasi na kushuka pamoja na waislamu wote kwa jumla.

Ama maoni yangu nikuhusu mawaidha.Ningependa sana kama kutakuwa na uwezekano mukaweka mawaidha yanayozungumzia maisha ya waislamu wanawoishi inchi za kimagharibi na tabia wanazozitumia za kusema kuwa wamewachana wala hawakuwachana ili kupata pesa na marupurupu kwa serikali.Nijambo lakusikitisha sana kuona hivyo ambayo sasa imekuwa kama kawaida ya baadhi ya waislamu huku,ambapo kwakufanya hivyo wanaichafua dini yetu tukufu ambayo ni ya Allah.Kama mutapata mashekhe wazungumzie haya na madhara yake kwa Audio.maana watu wengine huwa sisana kukaa na kusoma.kusikiliza inakuwa nikwepesi kwa ndugu zetu wengine.

WASSALAMA ALEYKUM WARAHMA TU LLAHI WABARAKATU:
 
on 02/03/2007 at 14:10

As'salaam alaykum warahmatu L-lwahi Warakatuh.

InshaAllah sifa njema ana stahiki Allah mola mlezi wa walimwengu na Sala na salam zimfikie kipenzi chetu Mtume Muhammad Swala L-lwahu alayhi wasalaam.

Kama Waislam ni wajibu wetu kushukuru kwa kile tunacho tunacho jaaliwa na Allah, na kama hivyo basi pia niwajibu wetu kuwakumbuka nanyi kwa kutanguliza Du'aa kwa kuwaombea kwa Allah awajaalie Iyman zaidi katika kuisambaza dini ya Kiislam.

Hakika tunanufaika sana na mambo mbali mbali ambayo mnayo tutaarishia kwa yakini ya kuwa katika njia bora na imara katika Uislam.

Tunawaombea Kheyr na Barka kutoka kwa Mwenyeezi Mungu Subhanahu Wataala. na pia awalinde na awape Radhi zake Amiyn.
 
Messages : 1381 to 1400
Page : 70
Number of messages : 1549