Back to the homepageBack to the homepage
Alhidaaya Tathmini Shukurani Kumbukumbu Zako
Name or Nickname : *
Email address : *[P]
City :
Country :
Your message : *

Please copy this 4 letters code into the box on the right : (Why this?)


Messages : 1501 to 1520
Page : 76
Number of messages : 1549
on 24/06/2005 at 04:37

Ass.alkm.pongezi na shukran kwa kufungua mtandao huu,kwani waislamu tumo pahali pabaya na dogo tupatalo kutukumbusha na kutuzindua na barka na kheir kubwa.Inshl.Allah awezidishe nguvu ili muendeleze daawa hii.
Tuna omba tafadhali mutuzidishie katika mambo ya wanawake kwani sisi ni dhaifu na nirahisi kuteteleka,tunahitaji makumbusho kwa wengi nakila mara ili tuwe wingi wa iman na khushuu.
Shukran na mabruk kwa mtandao huu.
 
on 24/06/2005 at 04:36

Assalaamu alaykum. Inshaallah wote walioshiriki katika kutengeza website hii na yote yaliyomo, Mwenyezi M'ngu awazidishie kheri, na Inshaallah malipo yake mtayapata Akhera.
Tuzidishieni mawaidha zaidi ya Mashekhe: Nassor Bacho, Othman Maalim na Sheikh Hilaal Kipozeo.
 
on 19/06/2005 at 04:34

aslam alykum
niefurahi sana kwa kazi yenu kubwa mungu akuzidishieni kheri nasi tutajaribu kukutumia makala ambazo tunadhni zitachangia katika kazi hii
 
on 18/06/2005 at 04:24

Ni furaha iliyoje kupata tovuti hii ya hidaaya, Mwenyezi Mungu atawalipa Inshaallah kwa kuleta fikra hii jamil. Napenda kuwashauri wasomaji watembelee na kwenye viungo huko pia kuna mambo, Inshaala Mwenyezi Mungu atujaalie kila la kheri jamii ya Kiislam.
 
on 17/06/2005 at 04:27

BISMILLAH MASHALLAH MASHALLAH MASHALLAH, Mwenye-enzi-mungu akujaze kila la kheri pamoja na jamii yako kwa kuingia fikra ya kuanzisha tovuti hii ya dini yetu ya Kiislam kutunufaisha ndugu zako waislami katika ulimwengu mzima. Jaza yako iko kwa mola wako na nnakuombea wewe na wote wanaoshirikiana nawe kuiendeleza tovuti hii, Inshallah mfanikiwe kwa kila jambo la kheri lenye manufaa mnaloliazimia. Amin
 
on 13/06/2005 at 23:45

ni furaha nzuri sana kwa kutupa huu wakati tumwandikiyeni basi kama mtaweza na muandike habari za jihadi kwa wingisana
 
on 12/06/2005 at 23:42

Asalaam Alaikum Warahamatu llah wabarakatuh amma baad,
Nimefurahi sana kuona ndugu zangu ktk Iman kutoa mchango wao ktk mambo haya ya Dini na Ishaalah ALLAH pekee anajua malipo yake kwao, na ni wajibu kwetu soote kuitumia tovoti hii ili tupate faida yake,maana kwa wakati huu wa mitihani mingi sana kuhusu Dini ni kua kila mmoja alokua na Pc nyumbani basi aitumie fursa hii vizuri kwake na familia yake na pia kwa jamaa zake , kila la kher na ALLAH Karim
Wabilah Tawfiq
 
on 09/06/2005 at 23:38

As-Salaam Alaykum, Pongezi zangu pia kwa waanzishi na waongozaji wa website hii.Allah (SW)atakujaalieni kheri za duniani na Akhera-Amin. Itasaidia sana mkialika watu katika masuala na majibu ili kuongeza ufahamu wa mambo mbali mbali ya maisha. Pia ningeomba mtoe mafunzo yatakayo saidia kupiga vita maovu yanayofanyika katika jamii zetu kama vile malezi/matunzo mabaya ya watoto na wanawake, ndoa zisizo heshimiwa na suala zima la ukimwi. Assalaam Alaykum
 
on 07/06/2005 at 17:17

Alhamdullillah kwa kupata mawaidha mazuri na mafundisha yeje faida duniani na akhera kwa waislamu.
 
on 06/06/2005 at 17:08

AlhamduliLlah,namshukuru Allah kwa kuwajaalia kupata wazo la kuaandaa Wavuti hii ya kiswahili yenye mlengo wa Kisunnah kwani itakuwa ni ukombozi mkubwa kwa waislamu hasa vijana katika kuyaelekea mambo ya dini yao kwa njia iliyo bora na rahisi zaidi.Allah akupeni kheri na baraka nyingi sana.
 
on 05/06/2005 at 17:06

Assalam alaykum, nawashukuru wamiliki wa website hii ya Al hidaaya, ni Allah (s.w) pekee anayeweza kuwalipa kwa kazi yenu nzuri na kutusogea karibu zaidi utajo na ukumbusho wake. Muzidi kuendelea zaidi kutuletea mazuri ya dini yetu na Allah (s.w) awabariki na sote pia, Amin
 
on 04/06/2005 at 17:04

Namshukura ALLAH kwakuwezesha ndugu zangu nyinyi kwa bidii zenu za kutambaza na kufanya kazi njema.INSHA ALLAH nasi wengine tujibidishe kwa kazi ya ALLAH pale popote tulipo.Hii ni ukumbii bora na muzidi wala tusirudi nyuma,masha allah.ALLAH BARIK FIY
 
on 02/06/2005 at 17:02

asalamu aleikum, nina furahi kwa kuona site hii ya kiislamu katika lugha ya kiswahili, na kutoa mafundisho sahih ya ahlil sunnah wal jamaa, mungu awazidishie imani ya wenye kufungua website hii na wenye kusoma inshaallah
 
on 01/06/2005 at 16:59

Asalaam Aleikum, Mwenyezimungu Inshaalah Aendeleyee kuwaongoza na kukujaalieni muendelee muwe na niya na juhudi za kuueneza Uisalaam wa ukweli sio wa akina madevu na suruwali za combat. Maasallaam
 
on 29/05/2005 at 16:57

Nimependezewa sana na kazi inayofanywa na wenye mtandao huu. Ishaallah mola awape nguvu na uwezo zaidi wa kueneza dini yetu na Ishaallah tutafanikiwa. Amin.
 
on 27/05/2005 at 16:55

UMUHIMU WA HABARI KATIKA UISLAMU
Yoyote anayefahamu yaliyomo katika Qur-ani japo kidogo atajua umuhimu wa habari katika Uislamu,inatosha kukumbuka kisa cha Nabii Suleiman na Ndege wake “Hud-hud”, pia Qur-ani yote ni visa vya Mitume waliotangulia ambavyo kutokana na umuhimu wake Allah alimsimulia Mtume wake,akamwambia:
((?????? ??????? ???????? ??????? C??????? E???C ??????????C ???????? ????C C?????A????????? ????E? ???? ??E????? ?????? C?U?C????????)).

Kwa hivyo hapana budi Waislamu hasa Mashekhe na Walimu wa vyuo watumie nafasi zao kuelimisha jamii madhara ya majanga tafauti yanayotokea Ulimwenguni likiwamo suala la UKIMWI.
E???? E?????I?C???? .....????I???? ?????? I?????C? E?? ????????C? C????UU??UU??C??UU?? 18/?E?? C?EC??/1426?U UUUU 27/?C??/2005?

MASUALA YA KUJIPIMA
(1)-Kwa nafasi yako kama Imamu au Mwalimu,Jee unahisi kuna haja ya kuweka sheria ya lazima ya kupima Aids kabla ya ndoa,kama jawabu ndio au siyo,orodheza sababu zako.

(2)- Taja njia ambazo Maimamu na Walimu hutumia katika kulielezea suala la Ukimwi,na kwa kiwango gani hufanikiwa na yepi matatizo yanayowakumba katika kufanikisha suala hilo?

(3)- Kwa mtazamo wako,kwa kiwango gani Uislamu umechangia kupunguza janga la Ukimwi? Eleza kwa kifupi kwa njia ya madondoo.
 
on 26/05/2005 at 16:52

Mash-Allah . I really loved the person who came up with this website.This is an inspiration to our muslim sisters and brothers. Thank you so much.
 
on 25/05/2005 at 16:49

may Allah(s.w),give you all the fortitude to continue in enlighting islam! i found this site very useful,keep it up!
 
on 25/05/2005 at 16:44

nashukuru kwa kuanzishwa kwa web site hii. mimi shida yangu natafuta mchumba wakuoa.
 
on 25/05/2005 at 16:42

Assalaama-alaykum, Napenda kutoa shukrani zanzu za dhati kwa wale wote walioshiriki kuanzisha Website hii. Kwani katika uislam hakuna jambo lenye kheri kama kukumbushana. Na insha-allah msione tabu kushirikiana na watu mbalimbali wanaotembelea kwenye ukumbi huu iwapo kutatakiwa msaada wowote wa kuendeleza mambo ya kheri kama haya. M.Mungu akupeni kila la kheri na akuzidishieni elimu Insha-Allah, Jazaa-kumul-llah kheyr.
 
Messages : 1501 to 1520
Page : 76
Number of messages : 1549