Fataawaa: Udhwhiyyah (Kuchinja)

 

 

 

 

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

 

 

 

Share

01-Imaam Ibn Baaz: Hukmu Ya Kuchinja (Udhwhiyah) Kwa Mwenye Uwezo

Hukmu Ya Kuchinja (Udhwhiyah) Kwa Mwenye Uwezo

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

 

Amesema Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah):

 

“Udhwhiyah ni Sunnah Muakkadah (Iliyosisitizwa) imewekewa Shariy'ah kwa wanaume na wanawake, na inatosheleza kwa mwanamme na watu wake wa nyumbani na kwa mwanamke na watu wake wa nyumbani.”

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (18/38)]

 

 

 

Share

02-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Akinunua Mnyama Wa Udhwhiyah Kisha Akapata Maradhi Achinjwe

 

Akinunua Mnyama Wa Udhwhiyah Kisha Akapata Maradhi Achinjwe

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

 

Atakayenunua kichinjwa na kumchunga kisha akapata maradhi au kuvunjika mguu wake je, huchinjwa?

 

JIBU:

 

 

Atakayeainisha kichinjwa na kusema: “Hiki ndicho kichinjwa changu huwa ndio kichinjwa.”

 

a-Akipatwa na maradhi au kuvunjika na ikiwa wewe ndiye uliyesababisha basi hatochinjwa na yapasa kununua mbadala wake au kilicho bora zaidi.

 

b-Na ikiwa wewe hukusababisha basi atafaa.

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (25/99)]

 

 

Share

03-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Hukumu ya Udhwhiya kwa Maiti

 

Hukumu ya Udhwhiya kwa Maiti

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah) amesema:

 

 

a-Udhwhiya ni kwa walio hai. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  alikuwa na ndugu waliokufa kabla lakini hakuwachinjia.

 

 

b-Atakapousia mtu kabla ya kufa kwake achinjiwe basi usia wake utafuatwa  na atachinjiwa.

 

c-Achinje mtu kwa ajili yake na watu wa nyumbani kwake na anuie hilo walio hai na waliokufa.

 

d-Maiti kupwekeka na Udhwhiya si katika Sunnah.

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (25/11]

Share

04-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Inafaa Kumkosoa Anayechinja Kwa Ajili Ya Maiti

 

Inafaa Kumkosoa Anayechinja Kwa Ajili Ya Maiti?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Je katika hali hiyo (kuchinja kwa asiyekuwa Allaah) tunatakiwa kumkosoa aliyechinja kwa ajili ya maiti?

 

 

JIBU:

 

 

Lau mtu akifanya hivyo hatutomkosoa bali tutamuelekeza kile kilicho bora zaidi nayo ni dua'a kwa maiti.

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (25/122)]

 

 

Share

05-Imaam Ibn 'Uthaymiyn; Mwanamke Anafaa Kuchinja?

 

Mwanamke Anafaa Kuchinja?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

 

Je Mwanamke Anaruhusiwa Kuchinja Kichinjwa?

 

 

JIBU:

 

 

Inajuzu mwanamke kuchinja kichinjwa kwani asili ni mwanamke kushirikiana na mwanamme katika ‘Ibaadah.

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (25/81)]

 

 

Share

06-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Aliyeoa Na Kuishi Na Baba Yake Udhwhiya Ya Baba Yake Inamtosheleza?

 

Aliyeoa Na Kuishi Na Baba Yake Udhwhiya Ya Baba Yake Inamtosheleza?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Kijana aliyeoa mwenye mali anayekaa na babake je Udhwhiyah (kichinjo) ya babake kitamtosheleza?

 

JIBU:

 

 

a-Sunnah ni mtu kuchinja kwa ajili yake na watu wa nyumbani kwake wakubwa kwa wadogo.

 

b-Ama ikiwa kila mmoja anakaa nyumba yake tofauti basi kila mmoja anatakiwa achinje alipo (kivyake).

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (25/38)]

 

 

Share

07-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Kukopa kwa Ajili ya Udhwhiya Inafaa?

 

Kukopa kwa Ajili ya Udhwhiya Inafaa?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

 

Fakiri ambaye hana chochote mkononi pindi 'Iydul-Adhw-haa  inapofika lakini ni mwenye kutarajia kupokea mshahara wake wa mwezi basi na akope achinje kisha alipe?

 

 

JIBU:

 

 

Kama hatoweza kulipa kwa muda wa karibu basi haifai kwake kukopa ili achinje kwani hili litamfanya ashughulike na kulipa deni.

 

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (25/110)]

 

 

 

 

 

Share

08-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Hikma Ya Kujizuia Kukata Nywele, Kucha Kwa Mwenye Kunuia Kuchinja

 

Hikma Ya Kujizuia Kukata Nywele, Kucha Kwa Mwenye Kunuia Kuchinja

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Ni ipi hekima kwa anayetaka kufanya Udhwhiya kujizuia kukata nywele zake, kucha na kutoa kitu katika ngozi?

 

 

JIBU:

 

 

a-Miongoni mwa neema za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  kwa waja Wake ni kuwa pindi wanapoondoka watu kwenye kuhiji na kufanya ‘ibaadah na kuacha waliyoacha ni kuwa Allaah Amewaamrisha waliobaki kushirikiana na Hujaji kwa kuacha kufanya baadhi ya mambo kwa ajili ya kujikurubisha kwa Allaah.

 

 

b-Mchinjaji anashirikiana na Hujaji katika baadhi ya matendo ya ‘ibaadah nayo ni kujikurubisha kwa Allaah kwa kuchinja. Mtu huyu anayetaka kuchinja anashirikiana na Hujaji katika sifa za Ihraam nazo ni kujizuia na kukata nywele na kucha.

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (25/139)]

 

 

Share

09-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Mnyama Yupi Bora Kwa Udhwhiya Aliye Mnene, Mwenye Mafuta Mengi Au Mwenye Thamani?

 

Mnyama Yupi Bora Kwa Udhwhiya Aliye Mnene,

Mwenye Mafuta Mengi Au Mwenye Thamani?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Ni kipi bora katika Udhwhiya? Je, ni mnyama mkubwa wa kiwiliwili mwenye mafuta mengi au mwenye thamani kubwa?

 

 

JIBU:

 

 

Tukiangalia manufaa ya Udhwhiya ni kuwa mnyama mkubwa mwenye nyama nyingi anakuwa ni bora.

 

 

Na tukiangalia ukweli wa kutaabadi kwa ajili ya Allaah ('Azza wa Jalla)  tutasema mwenye thamani kubwa ni bora.

 

Hata hivyo angalia kilicho kizuri zaidi kwa moyo wako na ufanye na ukiona kuwa nafsi yako inazidi iymaan na kujidhalilisha kwa Allaah ('Azza wa Jalla)  kwa kutoa thamani zaidi basi fanya hivyo.

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (25/35)]

 

 

Share

10-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Unapochinja Unatakiwa Kusema Nini?

 

Unapochinja Unatakiwa Kusema Nini?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Unasema nini unapochinja?

 

JIBU:

 

Anasema mtu anapotaka kuchinja:

 

بسم الله والله اكبر، اللهم هذا منك ولك اللهم هذه عني و عن اهل بيتي  

((BismiLLaah, wa Allaahu Akbar, Ee Allaah hii ni kutoka Kwako na kwa ajili Yako, Ee Allaah hii ni kutoka kwangu na kwa kutoka kwa ahli yangu))

 

 

 [Majmuw’ Al-Fataawaa (25/55)]

 

 

Share

11-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Wakati Wa Kutamka Du’aa Ya Kuchinja Na Sifa Yake

 

Wakati Wa Kutamka Du’aa Ya Kuchinja Na Sifa Yake

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Ni wakati gani wa kutamka hayo (du’aa ya kuchinja) na sifa yake ni ipi?

 

JIBU:

 

 

Wakati wa kusema hayo (du’aa ya kuchinja) ni pindi mnyama anapokalishwa (kwa ajili ya kuchinjwa) na sifa yake ni kusema:

بسم الله والله اكبر، اللهم هذا منك ولك اللهم  هذا عن فلان  

((BismiLLaah, wa Allaahu Akbar, Ee Allaah hii ni kutoka Kwako na kwa ajili Yako, Ee Allaah hii ni kutoka kwa fulani))

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (25/56)]

 

Share

12-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Akisahau Kutamka Du’aa Ya Kuchinja Afanyeje? Kichinjo Kinakuwa Haraam Kuliwa

 

Akisahau Kutamka Du’aa Ya Kuchinja Afanyeje? Kichinjo Kinakuwa Haraam Kuliwa

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

 

Mtu anaposahau kutamka du’aa ya kuchinja anatakiwa afanye nini?

 

 

JIBU:

 

Atakayesahau kusema hana madhambi lakini kichinjo kinakuwa haraam na haifai kuliwa.

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (25/56)]

 

 

 

Share

13-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Wakati Na Siku Za Kupasa Udhwhiya (Kuchinja)

 

Wakati Na Siku Za Kupasa Udhwhiya (Kuchinja)

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

 

Wakati wa Udhwhiya ni baada ya Swalaah ya  'Iyd (Al-Adhwhaa) hadi kuzama kwa jua siku ya kumi na tatu, kwa maana ni siku nne (jumla); Siku ya ‘Iyd na siku tatu baada ya hapo.

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (25/12)]

 

Share