Hadiyth Ya 39
إنَّ الله تَجاوَزَ لِي عَنْ أُمَّتي الْخَطَأَ والنِّسْياَنَ
Allaah Amesamehe Kwa Ajili Yangu Ummah Wangu Kukosea Na Kusahau
عَن ابْنِ عَبَّاسِ رَضِيَ الله عَنْهُما: أن رَسُوَل اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إنَّ الله تَجاوَزَ لِي عَنْ أُمَّتي: الْخَطَأَ، والنِّسْياَنَ، وَمَا اسْتُكْرِهُوا عَلَيْهِ)) حَدِيثٌ حَسَنٌ، رَوَاهُ ابْنُ مَاجَهْ وَالْبَيْهَقِيّ وَغيرهما
Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah Amewasamehe (au ameachilia mbali kuwatia hesabuni) kwa ajili yangu ummah wangu kwa kukosea, kusahau, na yale wanayoyafanya kwa kulazimishwa kwa nguvu.” [Ibn Maajah, Al-Bayhaqiy na wasiokuwa hao wawili]