Al-Ahaadiyth Al-Qudsiyyah

 

 

 

 

 

ِِAl-Ahaadiyth Al-Qudsiyyah

 

Zimekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

 

Share

01-Hadiyth Al-Qudsiy: Mja Wangu Ana Makazi Mazuri Kwangu Ananihimidi

Hadiyth Al-Qudsiy 

Hadiyth Ya 1

Mja Wangu Ana Makazi Mazuri Kwangu Ananihimidi

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ:سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((إِنَّ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ يَقُولُ: إِنَّ عَبْدِي الْمُؤْمِنَ عِنْدِي بِمَنْزِلَةِ كُلِّ خَيْرٍ يَحْمَدُنِي وَأَنَا أَنْزِعُ نَفْسَهُ مِنْ بَيْنِ جَنْبَيْهِ)) مسند أحمد

Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Allaah Aliyetukuka na Jalali Husema: “Hakika mja Wangu Muumini yuko katika kila makazi mazuri Kwangu. Ananihimidi hata Ninapomtoa roho baina pande zake mbili)) [Musnad Ahmad]

 

 

Share

02-Hadiyth Al-Qudsiy: Huruma Zangu Zinashinda Ghadhabu Zangu

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 2  

Huruma Zangu Zinashinda Ghadhabu Zangu

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: (( لَمَّا قَضَى اللَّهُ الْخَلْقَ كَتَبَ فِي كِتَابِهِ عَلَى نَفْسِهِ فَهُوَ مَوْضُوعٌ عِنْدَهُ إِنَّ رَحْمَتِي تَغْلِبُ غَضَبِي)) البخاري , مسلم, النسائي وابن ماجه

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Alipoumba viumbe Aliandika katika kitabu Chake Alichonacho katika Nafsi Yake: Huruma Zangu zinashinda ghadhabu Zangu)) [Al-Bukhaariy, Muslim, an-Nasaaiy na Ibn Maajah]

Share

03-Hadiyth Al-Qudsiy: Allaah Atanyakua Ardhi Na Atakunja Mbingu Katika Mkono Wake Wa Kulia

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 3 

Allaah Atanyakua Ardhi Na Atakunja Mbingu Katika Mkono Wake Wa Kulia

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((يَقْبِضُ اللَّهُ الْأَرْضَ وَيَطْوِي السَّمَاءَ بِيَمِينِهِ ثُمَّ يَقُولُ أَنَا الْمَلِكُ أَيْنَ مُلُوكُ الْأَرْضِ)) البخاري و مسلم

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Atainyakua dunia yote na Atazikunja mbingu kwa kwa Mkono Wake wa kulia kisha Atasema: Mimi Ndiye Mfalme! Wako wapi wafalme wa ardhi?)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share

04-Hadiyth Al-Qudsiy: Binaadamu Amenikadhibisha Na Amenitukana

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 4

 

Binaadamu Amenikadhibisha Na Amenitukana

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ ((قَالَ اللَّهُ كَذَّبَنِي ابْنُ آدَمَ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ ذَلِكَ ، وَشَتَمَنِي وَلَمْ يَكُنْ لَهُ ذَلِكَ ، فَأَمَّا تَكْذِيبُهُ إِيَّايَ ، فَقَوْلُهُ لَنْ يُعِيدَنِي كَمَا بَدَأَنِي وَلَيْسَ أَوَّلُ الْخَلْقِ بِأَهْوَنَ عَلَيَّ مِنْ إِعَادَتِه ،ِ وَأَمَّا شَتْمُهُ إِيَّايَ فَقَوْلُهُ اتَّخَذَ اللَّهُ وَلَدًا وَأَنَا الْأَحَدُ الصَّمَدُ لَمْ أَلِدْ وَلَمْ أُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لِي كُفْئًا أَحَدٌ)) البخاري والنسائ

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema: ((Allaah Amesema: Binaadamu amenikadhibisha na hana haki ya kufanya hivyo, na amenitukana na hana haki ya kufanya hivyo. Ama kunikana kwake ni kusema: Hatonirejesha (tena) kama Alivyoniumba (Hatonifufua kama vile Alivyoniumba). Na kuumba hakukuwa rahisi Kwangu kuliko kumfufua. Ama kunitukana kwake ni kule kusema: Allaah Ana mtoto wakati Mimi ni Ahad (Mmoja Pekee), Asw-Swamad (Aliyekamilika sifa za utukufu Wake, Mkusudiwa haja zote), Sikuzaa wala Sikuzaliwa na hakuna chochote kinachofanana na kulingana Nami)) [Al-Bukhaariy na An-Nasaaiy]

 

 

Share

05-Hadiyth Al-Qudsiy: Mchungaji Anayeadhini Na Kuswali Na Kumuogopa Allaah Ataingizwa Jannah

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 5 

Mchungaji Anayeadhini Na Kuswali Na Kumuogopa Allaah Ataingizwa Jannah

 

  

عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ قَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: (( يَعْجَبُ رَبُّكَ مِنْ رَاعِي غَنَمٍ فِي رَأْسِ شَظِيَّةِ الْجَبَلِ يُؤَذِّنُ بِالصَّلَاةِ وَيُصَلِّي فَيَقُولُ اللَّهُ عَزَّ وَجَلّ :َ انْظُرُوا إِلَى عَبْدِي هَذَا يُؤَذِّنُ وَيُقِيمُ الصَّلَاةَ يَخَافُ مِنِّي قَدْ غَفَرْتُ لِعَبْدِي وَأَدْخَلْتُهُ الْجَنَّةَ)) النسائي بسند صحيح

Kutoka kwa 'Uqbah Ibn 'Aamir (Radhwiya Allaahu ‘anhu)  ambaye amesema: "Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Rabb wenu Anapendezewa na  mchungaji kondoo (na mifugo mengineyo) anayekuwa juu ya kilele cha mlima anapoadhini na akaswali. Allaah Aliyetukuka na Jalali Husema: Angalia huyu ni mja Wangu anaadhini na anaswali; ananiogopa. Nimemghufuria mja Wangu na Nitamuingiza Jannah)) [An-Nasaaiy ikiwa na isnaad nzuri]

 

 

 

Share

06-Hadiyth Al-Qudsiy: Mmoja Katika Waja Wangu Ameniamini Na Mwengine Amenikufuru

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 6

 Mmoja Katika Waja Wangu Ameniamini Na Mwengine Amenikufuru

 

عَنْ زَيْدِ بْنِ خَالِدٍ الْجُهَنِيِّ قَالَ صَلَّى لَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ صَلَاةَ الصُّبْحِ بِالْحُدَيْبِيَةِ عَلَى أَثَرِ سَمَاءٍ كَانَتْ مِنْ اللَّيْلِ فَلَمَّا انْصَرَفَ أَقْبَلَ عَلَى النَّاسِ قَالَ: ((هَلْ تَدْرُونَ مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ؟)) قَالُوا اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ قَالَ :((أَصْبَحَ مِنْ عِبَادِي مُؤْمِنٌ بِي وكَافِرٌ,  فَأَمَّا مَنْ قَالَ مُطِرْنَا بِفَضْلِ اللَّهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَذَلِكَ مُؤْمِنٌ بِي كَافِرٌ بِالْكَوْكَبِ وَأَمَّا مَنْ قَالَ مُطِرْنَا بِنَوْءِ كَذَا وَكَذَا فَذَلِكَ كَافِرٌ بِي مُؤْمِنٌ بِالْكَوْكَبِ)) البخاري والنسائي

Kutoka kwa Zayd bin Khaalid Al-Juhaniyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu)  ambaye amesema:  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)  alituswalisha Swalaah ya Alfajiri (huko) Al-Hudaybiyah baada ya kunyesha mvua usiku. Alipomaliza aliwaelekea watu akasema: ((Je, mnajua Rabb wetu Amesema nini?)) Watu wakasema Allaah na Rasuli Wake ni Wajuzi zaidi. Akasema: ((Mmoja katika waja Wangu ameamka asubuhi akiwa ameniamini na mwengine amenikufuru. Ama aliyesema: tumepewa mvua kwa fadhila za Allaah na Rahmah Zake, huyo ameniamini na amezikanusha nyota; ama aliyesema: tumepewa mvua kwa nyota kadhaa wa kadhaa huyu amenikufuru na ameamini nyota)). [Al-Bukhaariy na An-Nasaaiy]

 

 

 

Share

07-Hadiyth Al-Qudsiy: Mwanaadamu Ameniudhi Anaulaani Wakati Na Hali Wakati Ni Mimi (Nimeuumba)

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 7

Mwanaadamu Ameniudhi Analaani Dahari (Zama) Na Hali Dahari Ni Mimi (Nimeziumba)

 

 

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((قال الله عزَّ وجلَّ:  يُؤْذِينِي إِبِن آدَم يَسُبُّ الدَّهْرَ وأنا الدَّهْرُ بِيَدِي الأمْرُ أُقَلِّبُ اللَّيْلَ وَالنَّهَار))   البخاري و مسلم

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu)  ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Aliyetukuka na Jalali Amesema: Mwanaadamu ameniudhi; analaani dahari (zama) na hali zama ni Mimi (Nimeziumba), Mkononi Mwangu ni amri zote Nageuza usiku na mchana)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Share

08-Hadiyth Al-Qudsiy: Nitamsibu Mja Wangu Homa Duniani Nimpunguzie Sehemu Ya Moto Wa Aakhirah

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 8  

Nitamsibu Mja Wangu Homa Duniani Nimpunguzie Sehemu Ya Moto Wa Aakhirah

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: عَادَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم مَرِيضًا مِنْ وَعَكٍ كَانَ بِهِ، وَمَعَهُ أَبُو هُرَيْرَةَ فَقَالَ النَّبِيُّ  صلى الله عليه وسلم: ((أَبْشِرْ فَإِنَّ اللَّهَ يَقُولُ: هِيَ نَارِي أُسَلِّطُهَا عَلَى عَبْدِي الْمُؤْمِنِ فِي الدُّنْيَا لِتَكُونَ حَظَّهُ مِنَ النَّارِ فِي الْآخِرَةِ )) أحمد وابن ماجه والترمذي – حديث حسن

Kutoka kwa Abu Hurayrah  (Radhwiya Allaahu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)  alimtembelea mgonjwa aliyekuwa na homa. Alikuwa pamoja naye Abu Hurayrah.  Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Akasema: ((Bishara njema! Hakika Allaah  Anasema: Nitamsibu mja Wangu duniani kwa kwa Moto Wangu (homa), ili aepukane na sehemu ya Moto wa Aakhirah)) [Ahmad, Ibn Maajah, At-Tirmidhiy- Hadiyth Hasan]

 

 

 

Share

09-Hadiyth Al-Qudsiy: Subira Katika Mshtuko Wa Kwanza Jazaa Yake Ni Jannah

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 9

Subira Katika Mshtuko Wa Kwanza Jazaa Yake Ni Jannah

 

عَنْ أَبِي أُمَامَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((يَقُولُ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ يَا ابْنَ آدَمَ: إن  َصَبَرْتَ وَاحْتَسَبْتَ عِنْدَ الصَّدْمَةِ الْأُولَى لَمْ أَرْضَ لَكَ ثَوابا دون الْجَنَّةِ)) ابن ماجه

Kutoka kwa Abu Umaamah ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Aliyetukuka na Jalali) Anasema: Ee bin-Aadam! Utakaposubiri na ukategemea thawabu katika mshtuko wa mwanzo, Sitoridhia thawabu yoyote kwa ajili yako ila ya Jannah) [Ibn Maajah]

 

 

Share

10-Hadiyth Al-Qudsiy: Mwenye Kufanya ‘Amali Kwa Kunishirikisha Na Mtu Nitaikanusha

 

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 10

Mwenye Kufanya ‘Amali Kwa Kunishirikisha Na Mtu Nitaikanusha

 

عنْ ابي هريرة رضي الله عنه أنَّه صلَّى الله عليه وسلَّم قال: ((قال الله تعالى: أنا أغْنى الشُّركاء عن الشِّرْك، فمَن عمل عملاً أشْرَك فيه معي غيري تركتُه وشِرْكه))    

Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Allaah Ta’aalaa Anasema: ‘‘Mimi ni mwenye kujitosheleza kabisa, Sihitaji msaada wala mshirika. Kwa hiyo, yule afanyaye ‘amali kwa kunishirikisha na mtu, Nitaikanusha pamoja na mshirika wake.”)) Yaani: hatopata ujira wowote kwa ‘amali hiyo. [Muslim (2985), Ibn Maajah (4202)]

Share

11-Hadiyth Al-Qudsiy: Watu Wa Mwanzo Kuulizwa Qiyaamah: Shahidi, ‘Aalim Na Mtoaji Mali

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 11

Watu Wa Mwanzo Kuulizwa Qiyaamah: Shahidi, ‘Aalim Na Mtoaji Mali

  

عَنْ أبي هريرة رضي الله عنه قال: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهم عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ ((إِنَّ أَوَّلَ النَّاسِ يُقْضَى يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَلَيْهِ رَجُلٌ اسْتُشْهِدَ فَأُتِيَ بِهِ فَعَرَّفَهُ نِعَمَهُ فَعَرَفَهَا قَالَ: فَمَا عَمِلْتَ فِيهَا؟ قَالَ: قَاتَلْتُ فِيكَ حَتَّى اسْتُشْهِدْتُ، قَالَ: كَذَبْتَ وَلَكِنَّكَ قَاتَلْتَ لِأَنْ يُقَالَ جَرِيءٌ فَقَدْ قِيلَ ثُمَّ أُمِرَ بِهِ فَسُحِبَ عَلَى وَجْهِهِ حَتَّى أُلْقِيَ فِي النَّارِ، وَرَجُلٌ تَعَلَّمَ الْعِلْمَ وَعَلَّمَهُ وَقَرَأَ الْقُرْآنَ فَأُتِيَ بِهِ فَعَرَّفَهُ نِعَمَهُ فَعَرَفَهَا قَالَ: فَمَا عَمِلْتَ فِيهَا؟ قَالَ: تَعَلَّمْتُ الْعِلْمَ وَعَلَّمْتُهُ وَقَرَأْتُ فِيكَ الْقُرْآنَ، قَالَ: كَذَبْتَ وَلَكِنَّكَ تَعَلَّمْتَ الْعِلْمَ لِيُقَالَ عَالِمٌ وَقَرَأْتَ الْقُرْآنَ لِيُقَالَ هُوَ قَارِئٌ فَقَدْ قِيلَ ثُمَّ أُمِرَ بِهِ فَسُحِبَ عَلَى وَجْهِهِ حَتَّى أُلْقِيَ فِي النَّارِ، وَرَجُلٌ وَسَّعَ اللَّهُ عَلَيْهِ وَأَعْطَاهُ مِنْ أَصْنَافِ الْمَالِ كُلِّهِ فَأُتِيَ بِهِ فَعَرَّفَهُ نِعَمَهُ فَعَرَفَهَا قَالَ: فَمَا عَمِلْتَ فِيهَا؟ قَالَ: مَا تَرَكْتُ مِنْ سَبِيلٍ تُحِبُّ أَنْ يُنْفَقَ فِيهَا إِلَّا أَنْفَقْتُ فِيهَا لَكَ قَالَ كَذَبْتَ وَلَكِنَّكَ فَعَلْتَ لِيُقَالَ هُوَ جَوَادٌ فَقَدْ قِيلَ ثُمَّ أُمِرَ بِهِ فَـسُحِبَ عَـلَى وَجْهِهِ ثُمَّ أُلْقِيَ فِي النَّارِ ))

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi sallam) akisema: ((Wa mwanzo kuhesabiwa Siku ya Qiyaamah ni mtu aliyekufa shahidi katika vita, ataletwa na kujulishwa neema alizoneemeshwa na baada ya kuzijua ataulizwa (na Allaah): “Umezifanyia kazi gani neema hizi?” Atasema: “Nimepigana jihaad kwa ajili Yako mpaka nikafa shahidi.” Ataambiwa: “Umesema uongo, bali ulipigana ili isemwe kuwa wewe ni jasiri na imeshasemwa.” Kisha itaamrishwa abururwe kwa uso wake na kuingizwa Motoni. Na mtu (mwengine) 'Aalim aliyejifundisha Dini akaijua vizuri, akasoma na Qur-aan, ataletwa na kujulishwa neema alizoneemeshwa, kisha ataulizwa; “Umezifanyia kazi gani neema hizi?” Atasema: “Nimejifunza elimu nikafundisha na kwa ajili Yako nikasoma Qur-aan.” Ataambiwa: “Umesema uongo, bali ulijifunza elimu ili isemwe kuwa wewe ni ‘Aalim. Ukasoma Qur-aan ili isemwe kuwa wewe ni msomaji (mzuri), na imeshasemwa.” Kisha itaamrishwa abururwe kwa uso wake na kuingizwa Motoni. Na mtu (mwengine) Allaah Amempa wasaa, akampa kila aina ya mali, ataletwa na kujulishwa juu ya neema alizoneemeshwa, kisha ataulizwa: “Umezifanyia kazi gani neema hizi?” Atasema: “Sijaacha njia Unayopenda mtu atoe katika mali yake ila mimi nimetoa kwa ajili Yako.” Ataambiwa: “Umesema uongo, bali umetoa ili isemwe kuwa wewe ni mkarimu na imeshasemwa. Kisha itaamrishwa abururwe kwa uso wake na kuingizwa Motoni”. [Muslim] 

 

 

Share

12-Hadiyth Al-Qudsiy: Toa (Mali Katika Njia ya Allaah) Ee Mwana Aadam Nami Nitakupa

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 12

Toa (Mali Katika Njia ya Allaah) Ee Mwana Aadam Nami Nitakupa

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ ((قَالَ اللَّهُ أَنْفِقْ يَا ابْنَ آدَمَ أُنْفِقْ عَلَيْكَ)) البخاري ومسلم

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema:  Rasuli wa Allaah Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam amesema:  ((Allaah Amesema:  Toa (mali katika njia ya Allaah) ee mwana Aadam, Nami Nitakupa)) [Al-Bukhaariy Na Muslim]

 

Share

13-Hadiyth Al-Qudsiy: Mja Hakuonekana Na Kheri Yoyote Isipokuwa Kuamrisha Watu Wasamehe Wenzie

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 13

Mja Hakuonekana Na Kheri Yoyote Isipokuwa Kuamrisha Watu Wasamehe Wenzie

 

 

عَنْ أَبِي مَسْعُودٍ الأنصاري رضي الله عنه قال: قال رسول اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ((حُوسِبَ رَجُلٌ مِمَّنْ كَانَ قَبْلَكُمْ فَلَمْ يُوجَدْ لَهُ مِنْ الْخَيْرِ شَيْءٌ إِلاَّ أَنَّهُ كَانَ يُخَالِطُ النَّاسَ وَكَانَ مُوسِرًا فَكَانَ يَأْمُرُ غِلْمَانَهُ أَنْ يَتَجَاوَزُوا عَنْ الْمُعْسِرِ قَالَ:  قَالَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ : نَحْنُ أَحَقُّ بِذَلِكَ مِنْهُ تَجَاوَزُوا عَنْهُ)) البخاري, مسلم والنسائي

Kutoka kwa Abu Mas’uwd Al-Answaariy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema:   Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mtu mmoja katika wale waliokutangulieni alitakiwa ajieleze. Hakuonekana na kheri yoyote isipokuwa alikuwa akiamiliana na kuchanganyikana na watu, na alivyokuwa ni tajiri akiwaamrisha wafanyakazi wake wamuachie (wamsamehe) mtu mwenye shida (asilipe deni lake). (Akasema Rasuli) Allaah (‘Azza wa Jalla) Akasema:  Sisi Tuna haki zaidi kuliko yeye kumsamehe)) [Al-Bukhaariy, Muslim na An-Nasaaiy]

 

Share

14-Hadiyth Al-Qudsiy: Jilinde Na Moto Japo Kwa Nusu Tende Au Neno Jema

 

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth ya 14

Jilinde Na Moto Japo Kwa Nusu Tende Au Neno Jema

 

 

عن عَدِيَّ بْنَ حَاتِمٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ يَقُولُ كُنْتُ عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَجَاءَهُ رَجُلَانِ أَحَدُهُمَا يَشْكُو الْعَيْلَةَ وَالْآخَرُ يَشْكُو قَطْعَ السَّبِيلِ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ((أَمَّا قَطْعُ السَّبِيلِ فَإِنَّهُ لَا يَأْتِي عَلَيْكَ إِلَّا قَلِيلٌ حَتَّى تَخْرُجَ الْعِيرُ إِلَى مَكَّةَ بِغَيْرِ خَفِيرٍ وَأَمَّا الْعَيْلَةُ فَإِنَّ السَّاعَةَ لَا تَقُومُ حَتَّى يَطُوفَ أَحَدُكُمْ بِصَدَقَتِهِ لَا يَجِدُ مَنْ يَقْبَلُهَا مِنْهُ ثُمَّ لَيَقِفَنَّ أَحَدُكُمْ بَيْنَ يَدَيْ اللَّهِ لَيْسَ بَيْنَهُ وَبَيْنَهُ حِجَابٌ وَلَا تَرْجُمَانٌ يُتَرْجِمُ لَهُ ثُمَّ لَيَقُولَنَّ لَهُ أَلَمْ أُوتِكَ مَالًا فَلَيَقُولَنَّ بَلَى ثُمَّ لَيَقُولَنَّ أَلَمْ أُرْسِلْ إِلَيْكَ رَسُولًا فَلَيَقُولَنَّ بَلَى فَيَنْظُرُ عَنْ يَمِينِهِ فَلَا يَرَى إِلَّا النَّارَ ثُمَّ يَنْظُرُ عَنْ شِمَالِهِ فَلَا يَرَى إِلَّا النَّارَ فَلْيَتَّقِيَنَّ أَحَدُكُمْ النَّارَ وَلَوْ بِشِقِّ تَمْرَةٍ فَإِنْ لَمْ يَجِدْ فَبِكَلِمَةٍ طَيِّبَةٍ)) البخاري

Kutoka kwa ‘Adiyy bin Haatim (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye alisema: Nilikuwa kwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) na wakamjia watu wawili. Mmoja alikuwa akilalamika umaskini, mwengine akilalamika juu ya uporaji wa njiani. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) akasema: Ama kwa uporaji wa njiani, karibu wakati utafika ambapo misafara itaweza kwenda Makkah bila ya walinzi, ama kwa umaskini Saa (Qiyaamah) haitofika kabla mmoja wetu hajachukua swadaqah yake na kuzunguka bila ya kumpa mtu wa kuipokea. Kisha hapo mmoja wenu atasimama mbele ya Allaah bila ya pazia baina yake na Allaah na bila ya mtarujumani (mtu wa kufasiri). Kisha atamuuliza; Je, sikukuletea utajiri? Atasema: Naam. Tena Atasema (Allaah) sikukuletea Rasuli? Atasema: Naam. Ataangalia kulia hatoona chochote isipokuwa Moto, kisha atatazama kushoto hatoona chochote isipokuwa Moto, kwa hivyo muache kila mmoja katika nyinyi ajilinde na Moto japo kwa (kutoa swadaqa) nusu ya kokwa ya tende, na ikiwa hakupata basi kwa (kutamka) neno jema)) [Al-Bukhaariy]

 

Share

15-Hadiyth Al-Qudsiy: Suwratul Faatihah - Nimeigawa Swalaah Baina Yangu Na Mja Wangu Nusu Mbili

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 15

 

Suwratul Faatihah - Nimeigawa Swalaah Baina Yangu Na Mja Wangu Nusu Mbili

 

 

  

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((مَنْ صَلَّى صَلَاةً لَمْ يَقْرَأْ فِيهَا بِأُمِّ الْقُرْآنِ فَهِيَ خِدَاجٌ)) ثَلَاثًا غَيْرُ تَمَامٍ فَقِيلَ لِأَبِي هُرَيْرَةَ إِنَّا نَكُونُ وَرَاءَ الْإِمَامِ فَقَالَ اقْرَأْ بِهَا فِي نَفْسِكَ فَإِنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:  ((قَالَ اللَّهُ تَعَالَى قَسَمْتُ الصَّلَاةَ بَيْنِي وَبَيْنَ عَبْدِي نِصْفَيْنِ وَلِعَبْدِي مَا سَأَلَ فَإِذَا قَالَ الْعَبْدُ (الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ) قَالَ اللَّهُ تَعَالَى حَمِدَنِي عَبْدِي وَإِذَا قَالَ (الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ)  قَالَ اللَّهُ تَعَالَى أَثْنَى عَلَيَّ عَبْدِي وَإِذَا قَالَ (مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ) قَالَ مَجَّدَنِي عَبْدِي وَقَالَ مَرَّةً فَوَّضَ إِلَيَّ عَبْدِي فَإِذَا قَالَ (إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ) قَالَ هَذَا بَيْنِي وَبَيْنَ عَبْدِي وَلِعَبْدِي مَا سَأَلَ)) مسلم, مالك, الترمذي, أبو داود, النسائي وابن ماجه

 

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayeswali Swalaah bila ya kusoma humo mama wa Qur-aan (Suwratu Al-Faatihah) huwa haikutimia (ina kasoro) [na alikariri mara tatu] haikutimia. Mtu mmoja alimwambia Abuu Hurayrah: (Hata) tukiwa nyuma ya Imaam? Akasema: Isome mwenyewe (kimya kimya) kwani nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Allaah Ta’aalaa Amesema: Nimeigawa Swalah baina Yangu na mja Wangu nusu mbili, mja Wangu atapata yale aliyoyaomba. Mja anaposema (Himidi zote Anastahiki Allaah) Rabb (Mola) wa walimwengu). Allaah Ta’aalaa Husema: Mja Wangu kanihimidi (kanisifu). Na anaposema (Mwingi wa Rahmah – Mwenye kurehemu). Allaah Ta’aalaa Husema: Mja wangu kanitukuza, na anaposema (Mfalme wa siku ya malipo). Allaah Ta’aalaa Husema: Mja wangu kanipa heshima. Na mara moja alisema: Mja wangu kazikubali nguvu Zangu. Na anaposema (Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada) Husema: Hii ni baina Yangu na mja Wangu na mja Wangu atapata kile alichokiomba. Na anaposema: (Tuongoze njia iliyonyooka. Njia ya wale Uliowaneemesha, sio ya walioghadhibikiwa wala waliopotea). Husema: Hii ni ya mja Wangu na mja Wangu atapata kile alichokiomba)) [Muslim, Maalik, At-Tirmidhiy, Abu Daawuwd, An-Nasaaiy na Ibn Maajah]  

Share

16-Hadiyth Al-Qudsiy: Kitu Cha Kwanza Kinachohesabiwa Katika ‘Amali Za Mja Ni Swalah

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 16

Cha Kwanza Kinachohesabiwa Katika ‘Amali Za Mja Ni Swalaah

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ َقَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ ((إِنَّ أَوَّلَ مَا يُحَاسَبُ بِهِ الْعَبْدُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مِنْ عَمَلِهِ صَلاتُهُ، فَإِنْ صَلُحَتْ فَقَدْ أَفْلَحَ وَأَنْجَحَ ، وَإِنْ فَسَدَتْ فَقَدْ خَابَ وَخَسِرَ، فَإِنْ انْتَقَصَ مِنْ فَرِيضَتِهِ شَيْءٌ قَالَ الرَّبُّ عَزَّ وَجَلَّ : انْظُرُوا هَلْ لِعَبْدِي مِنْ تَطَوُّعٍ-  فَيُكَمَّلَ بِهَا مَا انْتَقَصَ مِنْ الْفَرِيضَةِ ثُمَّ يَكُونُ سَائِرُ عَمَلِهِ عَلَى ذَلِكَ)) الترمذي و أبوا داود والنسائي وابن ماجه وأحمد

Imepokelewa na Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: “Nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Cha kwanza kinachohesabiwa katika ‘amali za mja Siku ya Qiyaamah ni Swalaah zake. Zikiwa zimetimia, hapo tena atakuwa kaneemeka na kafuzu, na zikiwa zina kasoro atakuwa kaanguka na kala khasara. Ikiwa pana upungufu katika Swalaah zake za fardhi Atasema Rabb (Mola) ‘Azza wa Jalla: “Angalia ikiwa mja Wangu ana Swalaah zozote za Sunnah ambazo zinaweza kufidia zile zilizopungua?”. Hapo tena amali yake iliyobaki itaangaliwa hivyo hivyo)) [At-Tirmidhiy, Abu Daawuwd, An-Nasaaiy, Ibn Maajah na Ahmad]

 

Share

17-Hadiyth Al-Qudsiy: Malaika Wanaotafuta Vikao Vya Watu Wanaomdhukuru Allaah Kisha Allaah Huwaghufuria

 

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 17 

Malaika Wanaotafuta Vikao Vya Watu Wanaomdhukuru

 Allaah Kisha Allaah Huwaghufuria

 

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ ((إِنَّ لِلَّهِ عَزَّ وَجَلَّ مَلَائِكَةً سَيَّارَةً فُضُلًا يَبْتَغُونَ مَجَالِسَ الذِّكْر، وَإِذَا وَجَدُوا مَجْلِسًا فِيهِ ذِكْرٌ قَعَدُوا مَعَهُمْ فَحَضَنَ بَعْضُهُمْ بَعْضًا بِأَجْنِحَتِهِمْ حَتَّى يَمْلَئُوا مَا بَيْنَهُمْ وَبَيْنَ سَمَاءِ الدُّنْيَا، فَإِذَا تَفَرَّقُوا عَرَجُوا أَوْ صَعِدُوا إِلَى السَّمَاءِ، قَالَ : فَيَسْأَلُهُمْ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ وَهُوَ أَعْلَمُ: مِنْ أَيْنَ جِئْتُمْ؟ فَيَقُولُون:َ جِئْنَاكَ مِنْ عِنْدِ عِبَادٍ لَكَ فِي الْأَرْضِ يُسَبِّحُونَكَ وَيُكَبِّرُونَكَ وَيَحْمَدُونَكَ وَيُهَلِّلُونَكَ وَيَسْأَلُونَكَ، قَالَ: وَمَاذَا يَسْأَلُونِي؟ قَالُوا: يَسْأَلُونَكَ جَنَّتَكَ، قَالَ: وَهَلْ رَأَوْا جَنَّتِي؟ قَالُوا: لَا أَيْ رَبِّ، قَالَ: فَكَيْفَ لَوْ قَدْ رَأَوْا جَنَّتِي؟ قَالُوا: وَيَسْتَجِيرُونَكَ ، قَالَ: مِمَّ يَسْتَجِيرُونِي؟ قَالُوا: مِنْ نَارِكَ يَا رَبِّ، قَالَ: وَهَلْ رَأَوْا نَارِي؟ قَالُوا: لَا، قَالُوا: وَيَسْتَغْفِرُونَكَ، قَالَ: فَيَقُول:ُ قَدْ غَفَرْتُ لَهُمْ وَأَعْطَيْتُهُمْ مَا سَأَلُوا وَأَجَرْتُهُمْ مِمَّا اسْتَجَارُوا، قَالَ: فَيَقُولُونَ: رَبِّ فِيهِمْ فُلَانٌ عَبْدٌ خَطَّاءٌ إِنَّمَا مَرَّ فَجَلَسَ مَعَهُمْ،  قَالَ: فَيَقُولُ قَدْ غَفَرْتُ لَهُمْ هُمْ الْقَوْمُ لَا يَشْقَى بِهِمْ جَلِيسُهُمْ)) البخاري , مسلم , الترمذي والنسائي

 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah (عزّ وجلّ) Anao Malaika chungu nzima ambao wanakwenda huku na kule wakitafuta vikao vya kumdhukuru Allaah, na wanapopata kikao, wanakaa na watu hao huku wakikunja mbawa zao baina yao, na kuijaza sehemu ya baina yao na uwingu wa dunia. (Watu) wanapoondoka, (Malaika) hupanda mbinguni. Akasema (Nabiy): Hapo tena Allaah (عزّ وجلّ) Huwauliza ijapokuwa Anayajua yote: “Mnatoka wapi?” Wao hujibu: “Tunatoka kwa baadhi ya waja wako duniani, walikuwa wanakusabbih na kukabbir na kuhallil na kukuhimidi na wanakuomba fadhila Zako.” (Allaah) Husema: “Wananiomba nini?” (Malaika hujibu): “Wanakuomba Jannah Yako. (Allaah) Husema: “Wameiona Jannah Yangu?”  Husema: “La, Ee Rabb”. (Allaah) Husema: “Ingekuwaje kama wangaliona Jannah Yangu!?”  (Malaika) Husema: “Wanaomba himaya Yako”. (Allaah) Husema: “Wanataka kuhamiwa kutokana na nini Kwangu?” (Malaika) Husema: “Kutokana na Moto Wako ee Rabb”. (Allaah) Husema: “Je, wameuona Moto Wangu?”  Husema: “La.” (Allaah) Husema: “Je, ingekuwaje kama wangeuona Moto Wangu!?” Husema: “Wanaomba maghfirah Yako”. (Allaah) Husema: “Nimewaghufuria na Nimewapa himaya ya yale wanayotaka wahamiwe.” (Malaika) husema: “Ee Rabb! Miongoni mwao yumo fulani, mja wako muovu ambaye alikuwa akipita tu na akakaa nao.” (Allaah) Husema: “Nimewaghufuria wote (pamoja naye), hao ni watu ambao akaaye nao hataadhibiwa.” [Al-Bukhaariy, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy]

 

 

Share

18-Hadiyth Al-Qudsiy: Swawm Ni Yangu Na Ni Mimi Ndiye Ninayelipa

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 18

Swawm Ni Yangu Na Ni Mimi Ndiye Ninayelipa

 

 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَال: ((يَقُولُ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ: الصَّوْمُ لِي وَأَنَا أَجْزِي بِهِ، يَدَعُ شَهْوَتَهُ وَأَكْلَهُ وَشُرْبَهُ مِنْ أَجْلِي، وَالصَّوْمُ جُنَّةٌ وَلِلصَّائِمِ فَرْحَتَانِ، فَرْحَةٌ حِينَ يُفْطِرُ وَفَرْحَةٌ حِينَ يَلْقَى رَبَّهُ، وَلَخُلُوفُ فَمِ الصَّائِمِ أَطْيَبُ عِنْدَ اللَّهِ مِنْ رِيحِ الْمِسْكِ))  البخاري و مسلم و مالك والترمذي والنسائي وابن ماجه 

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye alisema: ((Allaah Aliyetukuka na Jalali Anasema: Swawm ni Yangu na ni Mimi ndiye ninayelipa. (Mtu) huacha matamanio yake, chakula chake, kinywaji chake kwa ajili Yangu. Swawm ni ngao, na yule anayefunga ana furaha mbili; Furaha anapofuturu na furaha anapokutana na Mola wake. Mbadiliko wa harufu ya pumzi zake (kutoka mdomoni) ni bora kwa Allaah kuliko harufu ya misk)) [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik, At-Tirmdihiy, An-Nasaaiy na Ibn Maajah]

 

Share

19-Hadiyth Al-Qudsiy: Mimi Ni Vile Mja Wangu Anavyonidhania. Niko Pamoja Naye Anaponikumbuka

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 19

Mimi Ni Vile Mja Wangu Anavyonidhania. Niko Pamoja Naye Anaponikumbuka

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ (( يَقُولُ اللَّهُ تَعَالَى: أَنَا عِنْدَ ظَنِّ عَبْدِي بِي وَأَنَا مَعَهُ إِذَا ذَكَرَنِي، فَإِنْ ذَكَرَنِي فِي نَفْسِهِ ذَكَرْتُهُ فِي نَفْسِي ، وَإِنْ ذَكَرَنِي فِي مَلَإٍ ذَكَرْتُهُ فِي مَلَإٍ خَيْرٍ مِنْهُمْ ، وَإِنْ تَقَرَّبَ إِلَيَّ بِشِبْرٍ تَقَرَّبْتُ إِلَيْهِ ذِرَاعًا، وَإِنْ تَقَرَّبَ إِلَيَّ ذِرَاعًا تَقَرَّبْتُ إِلَيْهِ بَاعًا، وَإِنْ أَتَانِي يَمْشِي أَتَيْتُهُ هَرْوَلَةً)) البخاري , مسلم, الترمذي و ابن ماجه

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema, ((Allaah Ta’aalaa, Anasema: Mimi ni vile mja Wangu anavyonidhania. Niko pamoja naye Anaponikumbuka katika nafsi yake, Ninamkumbuka  katika nafsi Yangu, anaponikumbuka katika hadhara, Ninamkumbuka katika hadhara bora zaidi. Na anaponikaribia shibiri Ninamkaribia dhiraa; anaponikaribia dhiraa, Ninamkaribia pima, anaponijia kwa mwendo (wa kawaida) ninamwendea mbio)) [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na Ibn Maajah]

 

Share

20-Hadiyth Al-Qudsiy: Malipo Ya Niyyah Ya Kufanya Hasanaat Na Maovu

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 20 

Malipo Ya Niyyah Ya Kufanya Hasanaat Na Maovuu

 

عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِيمَا يَرْوِي عَنْ رَبِّهِ عَزَّ وَجَلَّ قَال: ((إِنَّ اللَّهَ كَتَبَ الْحَسَنَاتِ وَالسَّيِّئَاتِ ثُمَّ بَيَّنَ ذَلِكَ، فَمَنْ هَمَّ بِحَسَنَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا كَتَبَهَا اللَّهُ لَهُ عِنْدَهُ حَسَنَةً كَامِلَةً،  فَإِنْ هُوَ هَمَّ بِهَا فَعَمِلَهَا كَتَبَهَا اللَّهُ لَهُ عِنْدَهُ عَشْرَ حَسَنَاتٍ إِلَى سَبْعِ مِائَةِ ضِعْفٍ، إِلَى أَضْعَافٍ كَثِيرَةٍ،  وَمَنْ هَمَّ بِسَيِّئَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا كَتَبَهَا اللَّهُ لَهُ عِنْدَهُ حَسَنَةً كَامِلَةً، فَإِنْ هُوَ هَمَّ بِهَا فَعَمِلَهَا، كَتَبَهَا اللَّهُ لَهُ سَيِّئَةً وَاحِدَةً)) البخاري و مسلم

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kutokana na yale aliyoyapokea kwa Rabb wake Tabaaraka Wa Ta’aalaa kwamba amesema: “Hakika Allaah Ameandika hasanaat (mazuri) na maovu kisha Akayabainisha. Basi atakayetilia hima kufanya hasanah (zuri) moja, kisha asiweze kuifanya, basi Allaah Atamwandikia (thawabu za) hasanah moja kamilifu.  Na ikiwa ametilia hima kuifanya kisha akaifanya, basi Allaah Atamwandikia hasanaat kumi hadi mara mia saba maradufu zaidi ya hayo. Na akitilia hima kufanya ovu moja kisha asifanye, basi Allaah Atamuandikia hasanah moja kamilifu. Na ikiwa akitilia hima akalifanya, basi Allaah Atamuandikia ovu moja.” [Al-Bukhaariy na Muslim kwa herufi hizi]

 

 

 

Share

21-Hadiyth Al-Qudsiy: Nimeikataza Nafsi Yangu Dhulma Na Nimeiharamisha Kwenu Kwa Hivyo Msidhulumiane

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 21

Nimeikataza Nafsi Yangu Dhulma Na Nimeiharamisha Kwenu Kwa Hivyo Msidhulumiane

 

عن أبي ذَرٍّ الْغِفاريِّ رضي الله عنه، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم فيما يَرْويهِ عن رَبِّهِ عَزَّ وجَلَّ أَنَّهُ قال: 

(( يا عِبادي إنِّي حَرَّمْتُ الظُلْمَ على نَفْسِي وَ جعَلْتُهُ بَيْنَكُمْ مُحَرَّماً فلا تَظَالَمُوا.

يا عِبادي كُلُّكُمْ ضالٌّ إلا مَنْ هَدَيْتُهُ، فاسْتَهدُوني أهْدِكُمْ.

يا عِبادِي كُلُّكُمْ جائعٌ إلا مَنْ أطْعَمْتُهُ، فاسْتَطْعِمُوني أُطْعِمْكُم.

يا عِبادِي كُلُّكُمْ عَارٍ إلا مَنْ كَسَوْتُهُ، فاسْتكْسوني أَكسُكُم.

يا عِبادِي إِنَّكُمْ تُخْطِئُونَ بالليْلِ والنَّهارِ، وأنا أَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَميعاً، فاسْتَغْفِرُوني أُغْفِر لكُمْ.

يا عِبادِي إِنَّكُمْ لنْ تبْلغُوا ضُرِّي فتَضُرُّوني، ولن تبْلُغُوا نفْعي فَتَنْفعُوني.

يا عِبادِي لوْ أَنَّ أَوَّلَكُمْ وآخِرَكُمْ وإنْسَكُمْ وجِنَّكُمْ كانُوا عَلَى أَتْقَى قَلْبِ رَجُلٍ واحدٍ مِنْكُمْ ما زادَ ذلك في مُلْكي شَيئاً.

يا عِبادِي لوْ أَنَّ أَوَّلكُمْ وآخِرَكُمْ وإنْسَكُمْ وجِنَّكُمْ كانُوا عَلَى أَفْجَرِ قَلْبِ رَجُلٍ وَاحدٍ مِنْكُمْ ما نَقَصَ ذَلِكَ مِنْ مُلْكي شَيئاً.

يا عِبادِي لوْ أَنَّ أَوَّلَكُمْ وآخِرَكُمْ وإنْسَكُمْ وجنَّكُمْ قاموا في صَعِيدٍ وَاحِدٍ، فَسَأَلُوني، فأَعْطَيْتُ كلَّ واحدٍ مَسْأَلَتَهُ ما نَقَصَ ذلك مِمَّا عِنْدِي إلا كما يَنْقُصُ الْمِخْيَطُ إذا أُدْخِلَ الْبَحْرَ.

يا عِبادِي إنَّما هي أعمَالُكُمْ أُحْصِيها لَكُمْ ثُمَّ أُوَفِّيكُمْ إيَّاها، فَمَنْ وَجَدَ خيْراً فَلْيَحْمَدِ اللهَ، ومَنْ وَجَدَ غَيْرَ ذلك فَلا يَلومَنَّ إلا نَفْسَه)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ     

Imepokelewa kutoka kwa Abu Dharr Al-Ghifaariyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisimulia yale aliyopokea kutoka kwa  Rabb wake (Aliyetukuka na Jalaali) ((Enyi waja Wangu, Nimeikataza nafsi Yangu dhulma na Nimeiharamisha kwenu (hiyo dhulma), kwa hivyo msidhulumiane.

Enyi waja Wangu, nyote mumepotea isipokuwa wale Niliowaongoza, kwa hivyo tafuteni muongozo kutoka Kwangu Nitakuongozeni. 

Enyi waja Wangu nyote mna njaa isipokuwa wale Niliowalisha, kwa hivyo tafuteni chakula kutoka Kwangu na Nitakulisheni.

Enyi waja Wangu, nyote mko uchi isipokuwa wale niliowavika nguo, kwa hivyo tafuteni vazi kutoka Kwangu Nitakuvisheni.

Enyi waja Wangu, mnafanya makosa usiku na mchana, na Ninaghufuria dhambi zote, kwa hivyo ombeni maghfirah kutoka Kwangu Nitakughufurieni.

Enyi waja Wangu hamuwezi kunidhuru Mimi wala kuninufaisha.  

Enyi waja Wangu, ingekuwa wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binaadamu katika nyinyi na majini katika nyinyi akawa mwenye taqwa kama moyo wa mwenye taqwa katika nyinyi, haitaongeza chochote katika ufalme Wangu.

Enyi waja Wangu, angelikuwa wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binaadam katika nyinyi na majini katika nyinyi akawa mbaya kama moyo mbaya wa mtu miongoni mwenu (mtu mbaya kupita kiasi) haitonipunguzia chochote katika ufalme Wangu.

Enyi waja Wangu ingelikuwa wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binaadam katika nyinyi na majini katika nyinyi mkasimama pahala pamoja na mkaniomba, na Nikawapa kila mmoja alichoomba, haitonipunguzia katika nilicho Nacho zaidi kuliko sindano inavyopunguza bahari inapochovywa.

Enyi waja Wangu, ni vitendo vyenu ninavyovihesabu, kwa ajili yenu Nikakulipeni. Kwa hivyo anayekuta kheri amhimidi Allaah na yule anayekuta kinyume chake basi ajilaumu mwenyewe)) [Muslim]

 

Share

22-Hadiyth Al-Qudsiy: Fadhila Za Kutembelea Mgonjwa, Kumlisha Aliye Na Njaa Na Kunywesha Aliye Na Kiu

Hadiyth Al-Qudisy

Hadiyth Ya 22

Fadhila Za Kutembelea Mgonjwa, Kumlisha Aliye Na Njaa Na Kunywesha Aliye Na Kiu

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((إِنَّ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ يَقُولُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ: يَا ابْنَ آدَمَ مَرِضْتُ فَلَمْ تَعُدْنِي،  قَالَ: يَا رَبِّ كَيْفَ أَعُودُكَ وَأَنْتَ رَبُّ الْعَالَمِينَ؟ قَالَ: أَمَا عَلِمْتَ أَنَّ عَبْدِي فُلَانًا مَرِضَ فَلَمْ تَعُدْهُ؟ أَمَا عَلِمْتَ أَنَّكَ لَوْ عُدْتَهُ لَوَجَدْتَنِي عِنْدَهُ؟  يَا ابْنَ آدَمَ، اسْتَطْعَمْتُكَ فَلَمْ تُطْعِمْنِي ، قَالَ: يَا رَبِّ وَكَيْفَ أُطْعِمُكَ وَأَنْتَ رَبُّ الْعَالَمِينَ؟  قَالَ: أَمَا عَلِمْتَ أَنَّهُ اسْتَطْعَمَكَ عَبْدِي فُلَانٌ فَلَمْ تُطْعِمْهُ؟ أَمَا عَلِمْتَ أَنَّكَ لَوْ أَطْعَمْتَهُ لَوَجَدْتَ ذَلِكَ عِنْدِي؟  يَا ابْنَ آدَمَ اسْتَسْقَيْتُكَ فَلَمْ تَسْقِنِي، قَالَ: يَا رَبِّ كَيْفَ أَسْقِيكَ وَأَنْتَ رَبُّ الْعَالَمِينَ؟ قَالَ اسْتَسْقَاكَ عَبْدِي فُلَانٌ فَلَمْ تَسْقِهِ، أَمَا إِنَّكَ لَوْ سَقَيْتَهُ وَجَدْتَ ذَلِكَ عِنْدِي؟)) مسلم

Kutoka Kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: ((Hakika Allaah ‘Aliyetukuka na Jalali Atasema siku ya Qiyaamah: Ee mwana wa Adam, Niliumwa na usije kunitembelea? Atasema: Ee Rabb (Mola), vipi nije kukutembelea nawe ni Rabb wa ulimwengu? Atasema: Kwani ulijua kuwa mja wangu fulani alikuwa mgonjwa na hukwenda kumtembelea! Hukujua kuwa  ungekwenda ungalinikuta Niko pamoja naye?  Ee mwana wa Adam, Nilikuomba chakula na hukunipa. Atasema: Ee Rabb, vipi nitakupa chakula na Wewe ni Rabb wa ulimwengu? Atasema: Kwani hukujua kuwa mja wangu fulani alikuomba chakula na hukumpa? Hukujua kuwa ungalimpa chakula ungalikuta hayo (jazaa) kwangu mimi? Ee mwana wa Aadam, nilikuomba maji na hukunipa. Atasema: Ee Rabb, vipi nitakupa maji na Wewe ni Rabb wa ulimwengu? Atasema: Mja wangu fulani alikuomba maji na hukumpa. Hukujua kwamba ungalimpa maji ungalikuta hayo (jazaa) Kwangu Mimi)) [Muslim]  

 

 

Share

23-Hadiyth Al-Qudsiy: Kiburi Ni Joho Langu Na Utukufu Ni Kanzu Yangu Atakayeshindana Nami Nitamvurumisha Motoni

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 23 

Kiburi Ni Joho Langu Na Utukufu Ni Kanzu Yangu,

Atakayeshindana Nami Nitamvurumisha Motoni

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ هَنَّادٌ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((قَالَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ الْكِبْرِيَاءُ رِدَائِي وَالْعَظَمَةُ إِزَارِي فَمَنْ نَازَعَنِي وَاحِدًا مِنْهُمَا قَذَفْتُهُ فِي النَّارِ)) أبو داود ، ابن ماجه و أحمد

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:  ((Allaah Amesema: Kiburi ni joho Langu,  na utukufu ni kanzu Yangu, yule ashindanaye na Mimi katika kimoja katika hayo nitamvurumisha Motoni)) [Abu Daawuwd, Ibn Maajah na Ahmad]

 

Share

24-Hadiyth Al-Qudsiy: Waliokhasimiana Hazipokelewi Amali Zao Hadi Wapatane

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 24 

Waliokhasimiana Hazipokelewi ‘Amali Zao Hadi Wapatane

 

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: (( تُعْرَضُ أَعْمَالُ النَّاسِ فِي كُلِّ جُمُعَةٍ مَرَّتَيْنِ، يَوْمَ الِاثْنَيْنِ وَيَوْمَ الْخَمِيسِ، فَيُغْفَرُ لِكُلِّ مُؤْمِنٍ إِلَّا عَبْدًا بَيْنَهُ وَبَيْنَ أَخِيهِ شَحْنَاءُ، فَيُقَالُ أَنْظِرُوا هَذَيْنِ حَتَّى يَصْطَلِحَا)) مسلم, مالك و أبي داود

Abuu Huraryah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesimulia kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla amesema: ((‘Amali za watu huwekwa wazi mara mbili kwa wiki siku ya Jumatatu na Alkhamiys. Hughufuriwa kila Muumini isipokuwa mja aliyekuwa na ukhasama baina yake na nduguye (Muislamu). Husemwa: Wangojeeni hawa hadi wapatane)) [Muslim, Maalik na Abu Daawuud]

 

Share

25-Hadiyth Al-Qudsiy: Watu Watatu Watakaokuwa Wagomvi Wa Allaah Siku Ya Qiyaamah

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 25

Watu Watatu Watakaokuwa Wagomvi Wa Allaah Siku Ya Qiyaamah

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:  ((قَالَ اللَّهُ ثَلَاثَةٌ أَنَا خَصْمُهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ، رَجُلٌ أَعْطَى بِي ثُمَّ غَدَرَ، وَرَجُلٌ بَاعَ حُرًّا فَأَكَلَ ثَمَنَهُ،  وَرَجُلٌ اسْتَأْجَرَ أَجِيرًا فَاسْتَوْفَى مِنْهُ وَلَمْ يُعْطِ أَجْرَهُ)) البخاري, أحمد وابن ماجه

Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Amesema: Kuna watu watatu watakaokuwa wagomvi Wangu Siku ya Qiyaamah; Mtu aliyetoa neno lake (ahadi) kwa Jina Langu na asitekeleze, mtu aliyemuuza mtu huru na pesa akazitumia; na mtu aliyeajiri mfanyakazi wakakubaliana kisha asimpe ujira wake”. [Al-Bukhaariy, Ahmad na Ibn Maajah]

 

 

Share

26-Hadiyth Al-Qudsiy: Usijfanye Duni Kwa Kuogopa Watu Kusema Jambo Kwani Allah Ana Haki Zaidi Ya Kuogopwa

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 26  

Usijfanye Duni Kwa Kuogopa Watu Kusema Jambo Kwani Allah Ana Haki Zaidi Ya Kuogopwa    

 

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((لَا يَحْقِرَنَّ أَحَدُكُمْ نَفْسَهُ إِذَا رَأَى أَمْرًا لِلَّهِ فِيهِ مَقَالٌ أَنْ يَقُولَ فِيهِ، فَيُقَالُ لَهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ:  مَا مَنَعَكَ أَنْ تَقُولَ فِيهِ؟ فَيَقُولُ رَبِّ! خَشِيتُ النَّاسَ، قَالَ: فَأَنَا أَحَقُّ أَنْ تَخْشَى)) مسند أحمد

Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy amehadithia kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Asijifanye duni mmoja wenu atakapoona jambo la Allaah ambalo angeliweza kusema kitu juu yake lakini asiseme (aogope), kwa hivyo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Humwambia siku ya Qiyaamah: Kipi kilichokuzuia usiseme kitu kuhusu jambo kadhaa wa kadhaa? Husema: Nikiogopa watu. Kisha Mola Atasema: Ni mimi Ndiye ninayepaswa kuogopwa.” [Musnad Ahmad]

 

Share

27-Hadiyth Al-Qudsiy: Wapendanao Kwa Ajili Ya Allaah Watawekwa Katika Kivuli Cha Allaah Siku Ya Qiyaamah

Hadiyth Qudsiy

Hadiyth Ya 27

Wapendanao Kwa Ajili Ya Allaah Watawekwa Katika Kivuli Cha Allaah Siku Ya Qiyaamah

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((إِنَّ اللَّهَ يَقُولُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ: أَيْنَ الْمُتَحَابُّونَ بِجَلَالِي؟ الْيَوْمَ أُظِلُّهُمْ فِي ظِلِّي يَوْمَ لَا ظِلَّ إِلَّا ظِلِّي)) البخاري ومالك

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah Atasema siku ya Qiyaamah: Wako wapi wale wapendanao kwa (ajili ya) utukufu Wangu? Leo Nitawaweka kwenye kivuli Changu siku ambayo hakuna kivuli isipokuwa kivuli Changu]. [Al-Bukhaariy na Maalik]

 

 

Share

28-Hadiyth Al-Qudsiy: Allaah Akimpenda Mja Au Akimchukia, Humuamrisha Jibriyl

Hadiyth Qudsiy

Hadiyth Ya 28

Allaah Akimpenda Mja Au Akimchukia, Humuamrisha Jibriyl

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((إِنَّ اللَّهَ إِذَا أَحَبَّ عَبْدًا دَعَا جِبْرِيلَ فَقَالَ: إِنِّي أُحِبُّ فُلَانًا فَأَحِبَّهُ، قَالَ:  فَيُحِبُّهُ جِبْرِيلُ، ثُمَّ يُنَادِي فِي السَّمَاءِ فَيَقُولُ: إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ فُلَانًا فَأَحِبُّوهُ، فَيُحِبُّهُ أَهْلُ السَّمَاء، قَالَ: ثُمَّ يُوضَعُ لَهُ الْقَبُولُ فِي الْأَرْضِ، وَإِذَا أَبْغَضَ عَبْدًا دَعَا جِبْرِيلَ فَيَقُولُ: إِنِّي أُبْغِضُ فُلَانًا فَأَبْغِضْهُ، قَالَ: فَيُبْغِضُهُ جِبْرِيلُ ثُمَّ يُنَادِي فِي أَهْلِ السَّمَاءِ: إِنَّ اللَّهَ يُبْغِضُ فُلَانًا فَأَبْغِضُوهُ، قَالَ: فَيُبْغِضُونَهُ ثُمَّ تُوضَعُ لَهُ الْبَغْضَاءُ فِي الْأَرْضِ)) البخاري, مسلم والترمذي

 Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Akimpenda mja Humuita Jibriyl na Husema: Hakika Mimi Nampenda fulani kwa hivyo (nawe) mpende! Akasema (Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): Basi Jibriyl humpenda. Kisha Jibriyl hutangaza mbinguni, akisema: Allaah Anampenda fulani kwa hivyo mpendeni! Basi wakaazi wa mbinguni humpenda. Akasema: Kisha hujaaliwa mapenzi (na watu) duniani. Na Allaah Akimchukia mja (wake) Humuita Jibriyl na Husema: Namchukia fulani, nawe mchukie! Kwa hivyo Jibriyl naye humchukia. Kisha hunadi kwa wakaazi wa mbinguni: Allaah Anamchukia fulani kwa hivyo mchukieni! Basi (watu) humchukia na hujaaliwa kuwa ni chukizo duniani)) [Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhiy]

Share

29-Hadiyth Al-Qudsiy: Allaah Anatangaza Vita Dhidi Ya Mwenye Kumfanyia Uadui Kipenzi Chake

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 29

Allaah Anatangaza Vita Dhidi Ya Mwenye Kumfanyia Uadui Kipenzi Chake

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ اللَّهَ قَال:َ مَنْ عَادَى لِي وَلِيًّا فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالْحَرْبِ، وَمَا تَقَرَّبَ إِلَيَّ عَبْدِي بِشَيْءٍ أَحَبَّ إِلَيَّ مِمَّا افْتَرَضْتُ عَلَيْهِ،  وَمَا يَزَالُ عَبْدِي يَتَقَرَّبُ إِلَيَّ بِالنَّوَافِلِ حَتَّى أُحِبَّهُ، فَإِذَا أَحْبَبْتُهُ كُنْتُ سَمْعَهُ الَّذِي يَسْمَعُ بِهِ، وَبَصَرَهُ الَّذِي يُبْصِرُ بِهِ، وَيَدَهُ الَّتِي يَبْطِشُ بِهَا، وَرِجْلَهُ الَّتِي يَمْشِي بِهَا، وَإِنْ سَأَلَنِي لَأُعْطِيَنَّهُ، وَلَئِنْ اسْتَعَاذَنِي لَأُعِيذَنَّهُ، وَمَا تَرَدَّدْتُ عَنْ شَيْءٍ أَنَا فَاعِلُهُ تَرَدُّدِي عَنْ نَفْسِ الْمُؤْمِنِ يَكْرَهُ الْمَوْتَ وَأَنَا أَكْرَهُ مَسَاءَتَهُ)) البخاري

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema: ((Yeyote yule atakayefanya uadui kwa kipenzi changu Nitatangaza vita dhidi yake. Mja Wangu hanikaribii na kitu chochote Ninachokipenda kama ‘amali nilizomfaridhishia, na mja Wangu huzidi kunikaribia kwa ‘amali za Sunnah ili nimpende. Ninapompenda, huwa masikio yake yanayosikilizia, macho yake anayoonea, mikono yake anayonyoshea, miguu yake anayotembelea nayo, lau angeniomba kitu bila shaka ningempa, lau angeniomba himaya bila shaka ningelimkinga, na sisiti juu ya kitu chochote kama ninavyosita (kuichukua) roho ya mja Wangu Muumin: Anachukia mauti nami Nachukua kumdhuru)) [Al-Bukhaariy]

 

Share

30-Hadiyth Al-Qudsiy: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Pekee Ataweza Kutuombea Shafaa’ah

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 30

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Pekee

Ataweza Kutuombea Shafaa’ah  Siku Ya Qiyaamah

 

عَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:  يَجْتَمِعُ الْمُؤْمِنُونَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَيَقُولُونَ: لَوْ اسْتَشْفَعْنَا إِلَى رَبِّنَا،  فَيَأْتُونَ آدَمَ فَيَقُولُونَ: أَنْتَ أَبُو النَّاسِ خَلَقَكَ اللَّهُ بِيَدِهِ وَأَسْجَدَ لَكَ مَلَائِكَتَهُ وَعَلَّمَكَ أَسْمَاءَ كُلِّ شَيْءٍ فَاشْفَعْ لَنَا عِنْدَ رَبِّكَ حَتَّى يُرِيحَنَا مِنْ مَكَانِنَا هَذَا.  فَيَقُولُ: لَسْتُ هُنَاكُمْ وَيَذْكُرُ ذَنْبَهُ فَيَسْتَحِي ، ائْتُوا نُوحًا فَإِنَّهُ أَوَّلُ رَسُولٍ بَعَثَهُ اللَّهُ إِلَى أَهْلِ الْأَرْضِ ،   فَيَأْتُونَهُ فَيَقُولُ لَسْتُ هُنَاكُمْ وَيَذْكُرُ سُؤَالَهُ رَبَّهُ مَا لَيْسَ لَهُ بِهِ عِلْمٌ. فَيَسْتَحِي فَيَقُولُ: ائْتُوا خَلِيلَ الرَّحْمَنِ فَيَأْتُونَهُ فَيَقُولُ: لَسْتُ هُنَاكُمْ،  ائْتُوا مُوسَى عَبْدًا كَلَّمَهُ اللَّهُ وَأَعْطَاهُ التَّوْرَاةَ.  فَيَأْتُونَهُ فَيَقُولُ: لَسْتُ هُنَاكُمْ وَيَذْكُرُ قَتْلَ النَّفْسِ بِغَيْرِ نَفْسٍ فَيَسْتَحِي مِنْ رَبِّهِ فَيَقُولُ: ائْتُوا عِيسَى عَبْدَ اللَّهِ وَرَسُولَهُ وَكَلِمَةَ اللَّهِ وَرُوحَهُ فَيَقُولُ: لَسْتُ هُنَاكُمْ ،  ائْتُوا مُحَمَّدًا صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَبْدًا غَفَرَ اللَّهُ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ وَمَا تَأَخَّرَ،  فَيَأْتُونِي،  فَأَنْطَلِقُ حَتَّى أَسْتَأْذِنَ عَلَى رَبِّي فَيُؤْذَنَ لِي ،  فَإِذَا رَأَيْتُ رَبِّي وَقَعْتُ سَاجِدًا فَيَدَعُنِي مَا شَاءَ اللَّهُ ثُمَّ يُقَالُ: ارْفَعْ رَأْسَكَ وَسَلْ تُعْطَهْ،  وَقُلْ يُسْمَعْ   وَاشْفَعْ تُشَفَّعْ،  فَأَرْفَعُ رَأْسِي فَأَحْمَدُهُ بِتَحْمِيدٍ يُعَلِّمُنِيهِ ثُمَّ أَشْفَعُ فَيَحُدُّ لِي حَدًّا فَأُدْخِلُهُمْ الْجَنَّةَ.  ثُمَّ أَعُودُ إِلَيْهِ فَإِذَا رَأَيْتُ رَبِّي مِثْلَهُ ثُمَّ أَشْفَعُ فَيَحُدُّ لِي حَدًّا فَأُدْخِلُهُمْ الْجَنَّةَ.  ثُمَّ أَعُودُ الرَّابِعَةَ فَأَقُولُ: مَا بَقِيَ فِي النَّارِ إِلَّا مَنْ حَبَسَهُ الْقُرْآنُ وَوَجَبَ عَلَيْهِ الْخُلُودُ)) البخاري،  مسلم، مالك،    الترمذي وابن ماجه

Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Watakusanyika Waumini Siku ya Qiyaamah na Watasema: Lau tungetafuta kuombewa shafaa’ah kwa Rabb wetu! Watakwenda kwa Aadam na watasema: Wewe ndio baba wa watu, Amekuumba Allaah kwa Mkono Wake na Akaamrisha Malaika wakusujudie, na Akakufundisha majina ya vitu vyote, basi tuombee kwa Rabb wako ili Atupe faraja kutokana na sehemu yetu hii? Atasema: Mimi siwezi kufanya mnaloomba! Na atakumbuka makosa yake na ataona hayaa, atasema: Mfuateni Nuwh, hakika yeye ndiye Rasuli wa kwanza Aliyemtuma Allaah kwa watu ardhini. Watamfuata. Naye atasema: Siwezi kufanya mnaloomba! Na atakumbuka kumuomba kwake Allaah kwa jambo asilokuwa na ujuzi nalo.  Naye ataona hayaa na atasema: Nendeni kwa Khaliylur-Rahmaan. Watakwenda kwa Ibraahiym. Naye atawaambia: Siwezi kufanya mnaloomba! Nendeni kwa Muwsaa mja ambaye Allaah Alizungumza naye na Akampa Tawraat. Muwsaa atasema: Siwezi kufanya mnaloomba!  Atakumbuka kuwa aliwahi kumuua mtu bila ya haki na ataona hayaa kwa Rabb wake.  Atasema: Nendeni kwa ‘Iysaa kwani ni mja wa Allaah na Rasuli Wake na neno Lake na Roho Yake. Naye atasema: Siwezi kufanya mnaloomba! Nendeni kwa Muhammad, ni mja aliyefutiwa makosa yaliyotangulia na yajayo. Watakuja kwangu na nitakwenda kwa Rabb wangu kumuomba idhini (ya maombi), nitapewa idhini. Nitakapomuona Rabb wangu nitasujudu na Ataniacha hivyo hivyo mpaka Atakavyo. Kisha itasemwa: Inua kichwa chako na omba utapewa! Na sema yatasikilizwa (uyasemayo)! Na omba shafaa‘ah utapewa! Nitainua kichwa changu na nitamhimidi kwa Himdi Zake Atakazonifundisha, kisha nitaomba na Atanikubalia idadi kubwa ya watu, nitawaingiza Jannah. Kisha nitarudi tena Kwake. Nitakapomuona Rabb wangu, nitafanya kama mara ya kwanza, kisha nitaomba na Atanikubalia idadi kubwa ya watu nitawaingiza Jannah. Kisha nitarejea mara ya tatu, kisha nitarudi mara ya nne kisha nitasema: Hakuna watu waliobakia motoni isipokuwa Qur-aan imewazuia na watawajibika kubakia humo.” [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik, At-Tirmidhiy na Ibn Maajah]

 

 

 

Share

31-Hadiyth Al-Qudsiy: Mashuhadaa Wako Hai Jannah Wanatamani Kurudi Duniani Kupigana Tena Fiy SabiliLLaah

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 31 

Mashuhadaa Wako Hai Jannah Wanatamani Kurudi Duniani

Kupigana Tena Fiy SabiliLLaah

 

عَنْ مَسْرُوقٍ قَالَ سَأَلْنَا عَبْدَ اللَّهِ عَنْ هَذِهِ الْآيَةِ:  ((وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ أَمْوَاتًا بَلْ أَحْيَاءٌ عِنْدَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ))  قَالَ أَمَا إِنَّا قَدْ سَأَلْنَا عَنْ ذَلِكَ فَقَالَ:  ((أَرْوَاحُهُمْ فِي جَوْفِ طَيْرٍ خُضْرٍ لَهَا قَنَادِيلُ مُعَلَّقَةٌ بِالْعَرْشِ تَسْرَحُ مِنْ الْجَنَّةِ حَيْثُ شَاءَتْ ثُمَّ تَأْوِي إِلَى تِلْكَ الْقَنَادِيلِ فَاطَّلَعَ إِلَيْهِمْ رَبُّهُمْ اطِّلَاعَةً فَقَالَ: هَلْ تَشْتَهُونَ شَيْئًا؟  قَالُوا: أَيَّ شَيْءٍ نَشْتَهِي وَنَحْنُ نَسْرَحُ مِنْ الْجَنَّةِ حَيْثُ شِئْنَا؟ فَفَعَلَ ذَلِكَ بِهِمْ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ،  فَلَمَّا رَأَوْا أَنَّهُمْ لَنْ يُتْرَكُوا مِنْ أَنْ يُسْأَلُوا قَالُوا: يَا رَبِّ! نُرِيدُ أَنْ تَرُدَّ أَرْوَاحَنَا فِي أَجْسَادِنَا حَتَّى نُقْتَلَ فِي سَبِيلِكَ مَرَّةً أُخْرَى،  فَلَمَّا رَأَى أَنْ لَيْسَ لَهُمْ حَاجَةٌ تُرِكُوا)) مسلم،  الترمذي، النسائي وابن ماجه

Masruwq (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Tulimuuliza ‘Abdullaah kuhusu Aayah: ((Wala usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika njia ya Allaah ni wafu, bali wahai, kwa Rabb wao wanaruzukiwa)) [Aal-‘Imraan 3: 169] Akasema: Ama tuliuliza kuhusu Aayah hiyo akasema: (Nabiy Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Roho zao zimo ndani ya ndege wa kijani wenye kandili zinazoning’inia kutoka kwenye ‘Arsh wanatembea Jannah huria popote wapendapo, tena hujibanza kwenye hizo kandili. Rabb wao Aliwatupia jicho na Akasema: Je, Mnataka chochote? Wakasema: Tutake nini tena na tunajifaragua tutakavyo Jannah? Alifanya hivyo (Rabb) mara tatu. Walipoona hawataachiwa kuulizwa (tena) walisema: Yaa Rabb! Tungependa roho zetu Uzirejeshe katika viwiliwili vyetu ili tuweze tena kupigana kwa ajili Yako. Tena (Rabb) Alipoona hawahitaji chochote waliachiwa)) [Muslim, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy na Ibn Maajah]

 

Share

32-Hadiyth Al-Qudsiy: Mtu Anayejiua Anaharamishwa Jannah (Haingii Peponi)

Hadiyth Al-Qudisy

Hadiyth ya 32

Mtu Anayejiua Anaharamishwa Jannah (Haingii Peponi)

 

عَنْ جُنْدَبُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((كَانَ فِيمَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ رَجُلٌ بِهِ جُرْحٌ، فَجَزِعَ فَأَخَذَ سِكِّينًا فَحَزَّ بِهَا يَدَهُ، فَمَا رَقَأَ الدَّمُ حَتَّى مَاتَ، قَالَ اللَّهُ تَعَالَى: بَادَرَنِي عَبْدِي بِنَفْسِهِ حَرَّمْتُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ)) البخاري

Kutoka kwa Jundub bin ‘Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhu)  ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Alikuweko miongoni wa wale waliokutangulieni mtu ambaye alijeruhiwa. Alikuwa na maumivu makubwa kwa hivyo alichukua kisu akajikata mkononi mwake, damu haikusita kutoka mpaka akafa. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akasema: Mja wangu kaniwahi kwa (kuitoa) nafsi yake; nimemuharamishia yeye Jannah)) [Al-Bukhaariy]

 

Share

33-Hadiyth Al-Qudsiy: Mwenye Kusubiri Anapoondokewa Na kipenzi Chake Hulipwa Jannah

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 33

 Mwenye Kusubiri Anapoondokewa Na kipenzi Chake Hulipwa Jannah

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((يَقُولُ اللَّهُ تَعَالَى مَا لِعَبْدِي الْمُؤْمِنِ عِنْدِي جَزَاءٌ إِذَا قَبَضْتُ صَفِيَّهُ مِنْ أَهْلِ الدُّنْيَا ثُمَّ احْتَسَبَهُ إِلَّا الْجَنَّةُ)) البخاري

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Ta’aalaa Anasema: Haitokuwa jazaa ya mja wangu Muumini Ninapomchukulia kipenzi chake bora katika ahli wa duniani kisha akastahamili kwa ajili Yangu, haitakua ila ni (kumuingiza) Jannah)) [Al-Bukhaariy]

Share

34-Hadiyth Al-Qudsiy: Mwenye Kupenda Kukutana Na Allaah Na Anayechukia Kukutana Naye

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 34

Mwenye Kupenda Kukutana Na Allaah Na Anayechukia Kukutana Naye   

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:  ((قَالَ اللَّهُ إِذَا أَحَبَّ عَبْدِي لِقَائِي أَحْبَبْتُ لِقَاءَهُ وَإِذَا كَرِهَ لِقَائِي كَرِهْتُ لِقَاءَهُ)) البخاري و مالك

 Imepokelewa kutoka kwa Abua Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Amesema: Mja wangu akipenda kukutana na Mimi, Nami Hupenda kukutana naye; na akikirihika (akichukia) kukutana na Mimi, basi nami Hukirihika kukutana naye)) [Al-Bukhaariy na Maalik]

Share

35-Hadiyth Al-Qudsiy: Mtu Aliyewausia Wanawe Wamuunguze Baada Ya Kufariki Kwa kukhofu Adhabu Ya Allaah

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 35

Mtu Aliyewausia Wanawe Wamuunguze Baada Ya Kufariki Kwa kukhofu Adhabu Ya Allaah

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((كَانَ رَجُلٌ يُسْرِفُ عَلَى نَفْسِهِ فَلَمَّا حَضَرَهُ الْمَوْتُ قَالَ لِبَنِيهِ: إِذَا أَنَا مُتُّ فَأَحْرِقُونِي ثُمَّ اطْحَنُونِي،  ثُمَّ ذَرُّونِي فِي الرِّيحِ،  فَوَاللَّهِ لَئِنْ قَدَرَ عَلَيَّ رَبِّي لَيُعَذِّبَنِّي عَذَابًا مَا عَذَّبَهُ أَحَدًا.  فَلَمَّا مَاتَ فُعِلَ بِهِ ذَلِكَ،  فَأَمَرَ اللَّهُ الْأَرْضَ فَقَالَ: اجْمَعِي مَا فِيكِ مِنْهُ فَفَعَلَتْ،  فَإِذَا هُوَ قَائِمٌ،  فَقَال:َ مَا حَمَلَكَ عَلَى مَا صَنَعْتَ؟ قَالَ: يَا رَبِّ خَشْيَتُكَ.  فَغَفَرَ لَهُ)) البخاري، مسلم، النسائي و ابن ماجه

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mtu alifanya maasi makubwa na wakati mauti yalipomfikia aliwausia wanawe akiwaambia: Nitapokufa, nichomeni, munisage na mulitawanye jivu langu baharini kwani, wa-Allaahi, Allaah Atakaponipata, Ataniadhibu adhabu ambayo hajapata kuadhibiwa mtu mwingine. (Wanawe) walifanya walivyousiwa. Kisha Allaah Aliiamrisha ardhi kwamba: “Toa kile ulichokichukua.” Mara hapo akasima.  (Allaah) Akamuambia: Kitu gani kilichokufanya ufanye hayo uliyofanya? (Yule mtu) akasema: Yaa Rabb wangu! Ni kukukhofu Wewe. Basi Allaah Akamghufuria))  [Al-Bukhaariy, Muslim, An-Nasaaiy na Ibn Maajah]

 

Share

36-Hadiyth Al-Qudsiy: Mja Aliyerudia Kufanya Madhambi Allaah Akamghufuria

Hadiyth Al-Qudsiy

 

Hadiyth Ya 36

 

Mja Aliyerudia Kufanya Madhambi Allaah Akamghufuria

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِيمَا يَحْكِي عَنْ رَبِّهِ عَزَّ وَجَلَّ قَالَ: ((أَذْنَبَ عَبْدٌ ذَنْبًا فَقَالَ: اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي ذَنْبِي،  فَقَالَ تَبَارَكَ وَتَعَالَى:  أَذْنَبَ عَبْدِي ذَنْبًا فَعَلِمَ أَنَّ لَهُ رَبًّا يَغْفِرُ الذَّنْبَ وَيَأْخُذُ بِالذَّنْبِ ثُمَّ عَادَ فَأَذْنَبَ فَقَالَ:  أَيْ رَبِّ اغْفِرْ لِي ذَنْبِي،  فَقَالَ تَبَارَكَ وَتَعَالَى: عَبْدِي أَذْنَبَ ذَنْبًا فَعَلِمَ أَنَّ لَهُ رَبًّا يَغْفِرُ الذَّنْبَ وَيَأْخُذُ بِالذَّنْبِ ثُمَّ عَادَ فَأَذْنَبَ فَقَالَ: أَيْ رَبِّ اغْفِرْ لِي ذَنْبِي،  فَقَالَ تَبَارَكَ وَتَعَالَى: أَذْنَبَ عَبْدِي ذَنْبًا فَعَلِمَ أَنَّ لَهُ رَبًّا يَغْفِرُ الذَّنْبَ وَيَأْخُذُ بِالذَّنْبِ. اعْمَلْ مَا شِئْتَ فَقَدْ غَفَرْتُ لَكَ)) البخاري و مسلم

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuhusu mambo aliyohadithia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kutoka kwa Rabb Wake (‘Azza wa Jalla) kwamba ((Mja wa Allaah alifanya dhambi na akasema: Ee Rabb nighufurie dhambi zangu. Na yeye Allaah (Tabaaraka wa Ta’aalaa) Akasema: Mja wangu kafanya dhambi kisha kajua kwamba anaye Rabb Ambaye Anaghufuria dhambi na Anayeadhibu kwa kufanya dhambi. Kisha akarudi tena kufanya dhambi akasema: Ee Rabb nighufurie dhambi zangu. Na yeye Allaah (Tabaaraka wa Ta’aalaa) Akasema: Mja wangu kafanya dhambi kisha kajua kwamba anaye Rabb Ambaye Anaghufuria dhambi na Anayeadhibu kwa kufanya dhambi. Kisha akarudia tena dhambi na akasema: Ee Rabb nighufurie dhambi zangu. Na yeye Allaah (Tabaaraka wa Ta’aalaa) Akasema: Mja wangu kafanya dhambi kisha kajua kwamba anaye Rabb Ambaye Anaghufuria dhambi na Anayeadhibu kwa kufanya dhambi. (Allaah Akasema): Fanya utakavyo, kwani Nimekughufuria)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Share

37-Hadiyth Al-Qudsiy: Ee bin Aadam! Sitojali Dhambi Zako Madamu Utanikaribia Kuomba Maghfirah

 

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 37

Ee Bin-Aadam! Sitojali Dhambi Zako Madamu Utanikaribia Kuomba Maghfirah

 

عن أَنَسُ بْنُ مَالِكٍ قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((قَالَ اللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى يَا ابْنَ آدَمَ،  إِنَّكَ مَا دَعَوْتَنِي وَرَجَوْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ عَلَى مَا كَانَ فِيكَ وَلَا أُبَالِي، يَا ابْنَ آدَمَ لَوْ بَلَغَتْ ذُنُوبُكَ عَنَانَ السَّمَاءِ ثُمَّ اسْتَغْفَرْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ وَلَا أُبَالِي، يَا ابْنَ آدَمَ إِنَّكَ لَوْ أَتَيْتَنِي بِقُرَابِ الْأَرْضِ خَطَايَا ثُمَّ لَقِيتَنِي لَا تُشْرِكُ بِي شَيْئًا لَأَتَيْتُكَ بِقُرَابِهَا مَغْفِرَةً))    

Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Allaah (Tabaaraka wa Ta’aalaa) Amesema: Ee bin-Aadam! Hakika ukiniomba na ukanitaraji (kwa malipo) Nitakughufuria yale yote uliyonayo na wala Sijali, Ee bin-Aadam! Lau zingefikia dhambi zako ukubwa wa mbingu, kisha ukaniomba maghfirah, Ningekughufuria bila ya kujali (kiasi cha madhambi uliyoyafanya). Ee bin-Aadam! Hakika ungenijia na madhambi yakaribiayo ukubwa wa ardhi, kisha ukakutana nami na hali hukunishirikisha chochote, basi Nami Nitakujia na maghfirah yanayolinga nayo.” [At-Tirmidhiy na Shaykh Al-Albaaniy kaipa daraja ya Hasan]

 

 

Share

38-Hadiyth Al-Qudsiy: Allaah Huteremka Katika Mbingu Ya Dunia Thuluthi Ya Mwisho Ya Usiku Kuwaitikia Waja

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 38  

Allaah Huteremka Katika Mbingu Ya Dunia Thuluthi Ya Mwisho Ya Usiku

Kuwaitikia Waja 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((يَنْزِلُ رَبُّنَا تَبَارَكَ وَتَعَالَى كُلَّ لَيْلَةٍ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا حِينَ يَبْقَى ثُلُثُ اللَّيْلِ الْآخِرُ يَقُولُ: مَنْ يَدْعُونِي فَأَسْتَجِيبَ لَهُ، مَنْ يَسْأَلُنِي فَأُعْطِيَهُ، مَنْ يَسْتَغْفِرُنِي فَأَغْفِرَ لَهُ)) البخاري و مسلم

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu)  kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Tabaaraka wa Ta’aalaa Huteremka (kwa namna inavyolingana na utukufu Wake) kila siku katika mbingu ya dunia inapobakia thuluthi ya mwisho ya usiku na Husema: Nani ananiomba du’aa Nimuitike? Nani Ananiomba jambo Nimpe? Nani ananiomba maghfirah Nimghufurie?)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Share

39-Hadiyth Al-Qudsiy: Nimewatayarishia Waja Wangu Jannah Ambayo Hawajapata Kuona Wala Kusikia Wala Kuyawaza

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 39

Nimewatayarishia Waja Wangu Huko Jannah Ambayo

Hawajapata Kuyaona Wala Kusikia Wala Kuyawaza

 

  عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((قَالَ اللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى: أَعْدَدْتُ لِعِبَادِي الصَّالِحِينَ مَا لَا عَيْنٌ رَأَتْ وَلَا أُذُنٌ سَمِعَتْ وَلَا خَطَرَ عَلَى قَلْبِ بَشَرٍ)) قَالَ أَبُو هُرَيْرَةَ اقْرَءُوا إِنْ شِئْتُمْ: (( فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَا أُخْفِيَ لَهُمْ مِنْ قُرَّةِ أَعْيُنٍ)) البخاري، مسلم، الترمذي وابن ماجه

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Tabaaraka wa Ta’aalaa Amesema: Nimewatayarishia waja Wangu wema kile ambacho jicho lolote halijapata kuona na sikio lolote halijapata kusikia na wala haijapata kupita katika moyo wa binaadamu)) Akasema Abuu Hurayrah: Kwa hivyo, soma ukitaka: Basi nafsi yoyote haijui yaliyofichiwa katika yanayoburudisha macho. Ni jazaa kwa yale waliyokuwa wakiyatenda)) [As-Sajdah: 32:17] [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na Ibn Maajah]

 

Share

40-Hadiyth Al-Qudsiy: Mambo Yaliyozungushiwa Jannah Na Moto

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 40  

Mambo Yaliyozungushiwa Jannah Na Moto

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((لَمَّا خَلَقَ اللَّهُ الْجَنَّةَ وَالنَّارَ أَرْسَلَ جِبْرِيلَ إِلَى الْجَنَّةِ فَقَال: انْظُرْ إِلَيْهَا وَإِلَى مَا أَعْدَدْتُ لِأَهْلِهَا فِيهَا،  قَالَ:  فَجَاءَهَا وَنَظَرَ إِلَيْهَا وَإِلَى مَا أَعَدَّ اللَّهُ لِأَهْلِهَا فِيهَا.  قَالَ:  فَرَجَعَ إِلَيْهِ قَالَ: فَوَعِزَّتِكَ لَا يَسْمَعُ بِهَا أَحَدٌ إِلَّا دَخَلَهَا، فَأَمَرَ بِهَا فَحُفَّتْ بِالْمَكَارِهِ، فَقَالَ: ارْجِعْ إِلَيْهَا فَانْظُرْ إِلَى مَا أَعْدَدْتُ لِأَهْلِهَا فِيهَا،  قَالَ: فَرَجَعَ إِلَيْهَا فَإِذَا هِيَ قَدْ حُفَّتْ بِالْمَكَارِهِ،  فَرَجَعَ إِلَيْهِ فَقَالَ: وَعِزَّتِكَ لَقَدْ خِفْتُ أَنْ لَا يَدْخُلَهَا أَحَدٌ. قَالَ: اذْهَبْ إِلَى النَّارِ فَانْظُرْ إِلَيْهَا وَإِلَى مَا أَعْدَدْتُ لِأَهْلِهَا فِيهَا،  فَإِذَا هِيَ يَرْكَبُ بَعْضُهَا بَعْضًا،  فَرَجَعَ إِلَيْهِ فَقَالَ: وَعِزَّتِكَ لَا يَسْمَعُ بِهَا أَحَدٌ فَيَدْخُلَهَا، فَأَمَرَ بِهَا فَحُفَّتْ بِالشَّهَوَاتِ فَقَالَ: ارْجِعْ إِلَيْهَا فَرَجَعَ إِلَيْهَا فَقَالَ: وَعِزَّتِكَ لَقَدْ خَشِيتُ أَنْ لَا يَنْجُوَ مِنْهَا أَحَدٌ إِلَّا دَخَلَهَا)) الترمذي و قال حديث حسن صحيح – ابو داود والنسائي

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Alipoumba Jannah na moto, Alimtuma Jibriyl Jannah Akimwambia: Iangalie na angalia matayarisho Niliyoyaandaa  kwa ajili ya wakaazi wake. Akasema: Kwa hivyo alikuja kuiangalia na kuangalia maandalizi Aliyoyaandaa Allaah kwa ajili ya wakaazi Wake. Akasema: Akarejea kwa Allaah na kusema: Naapa kwa Utukufu Wako, hakuna atakayesikia (habari yake) ila tu ataingia (Jannah). Kisha Akaamrisha izungushwe mambo magumu watu wasiyoyapenda, Akasema: Rejea na angalia yale Niliyoyaandaa kwa ajili ya wakaazi wake. Akasema: Kisha akarejea na akakuta imezungukwa na mambo magumu watu wasiyoyapenda. Hapo alirejea kwa Allaah na akasema: Naapa kwa Utukufu Wako, nina khofu hakuna hata mtu mmoja atakayeingia. Akasema: Nenda motoni ukauangalie na uangalie Niliyoyaandaa kwa ajili ya wakaazi wake. Akaona ulikuwa na matabaka moja juu ya tabaka jengine. Akarejea kwa Allaah na akasema: Naapa kwa Utukufu Wako hakuna hata mmoja ausikiae (sifa zake) atakayeingia. Kisha Allaah Aliamrisha Uhusishwe na shahawa, matamanio ya nafsi). Kisha Allaah Akamuambia: Rejea tena (motoni). Alirejea tena na akasema: Naapa kwa Utukufu, wako nakhofia kuwa hapatakuwa na yeyote atakayenusurika nao)) [At-Tirmidhiy akasema ni Hadiyth Hasan, na Abu Daawuwd na An-Nasaaiy]

 

Share

41-Hadiyth Al-Qudsiy: Jannah Na Moto Vilishindana Allaah Akahukumu Baina Yake

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 41

Jannah Na Moto Vilishindana Allaah Akahukumu Baina Yake

 

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((احْتَجَّتْ الْجَنَّةُ وَالنَّارُ فَقَالَتْ النَّارُ: فِيَّ الْجَبَّارُونَ وَالْمُتَكَبِّرُونَ،  وَقَالَتْ الْجَنَّةُ: فِيَّ ضُعَفَاءُ النَّاسِ وَمَسَاكِينُهُمْ،  قَالَ: فَقَضَى بَيْنَهُمَا: إِنَّكِ الْجَنَّةُ رَحْمَتِي أَرْحَمُ بِكِ مَنْ أَشَاءُ،  وَإِنَّكِ النَّارُ عَذَابِي أُعَذِّبُ بِكِ مَنْ أَشَاءُ،  وَلِكِلَاكُمَا عَلَيَّ مِلْؤُهَا)) البخاري،  مسلم و الترمذي

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Jannah na moto vilishindana. Moto ulisema: Ndani yangu wamo wenye kujifanya majabari na wenye kutakabari.  Jannah ikasema: Ndani yangu wamo watu dhaifu na maskini. Akasema: Allaah Akahukumu baina yao: (Akasema): Wewe Jannah ni rahmah Zangu, kupitia kwako wewe Humrehemu Nimtakaye. Nawe moto ni adhabu Yangu, kupitia kwako wewe ninawaadhibu wale niwatakao na kila mmoja katika nyinyi mtajaa)) [Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhiy]

 

Share

42-Hadiyth Al-Qudsiy: Watu Wa Jannah Watapata Ridhaa Ya Allaah

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 42 

Watu Wa Jannah Watapata Ridhaa Ya Allaah

 

 

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ اللَّهَ تَبَارَكَ وَتَعَالَى يَقُولُ لِأَهْلِ الْجَنَّةِ: يَا أَهْلَ الْجَنَّةِ!  فَيَقُولُونَ لَبَّيْكَ رَبَّنَا وَسَعْدَيْكَ،   فَيَقُولُ: هَلْ رَضِيتُمْ؟  فَيَقُولُونَ وَمَا لَنَا لَا نَرْضَى وَقَدْ أَعْطَيْتَنَا مَا لَمْ تُعْطِ أَحَدًا مِنْ خَلْقِكَ،   فَيَقُولُ:  أَنَا أُعْطِيكُمْ أَفْضَلَ مِنْ ذَلِكَ،   قَالُوا: يَا رَبِّ وَأَيُّ شَيْءٍ أَفْضَلُ مِنْ ذَلِكَ؟  فَيَقُولُ: أُحِلُّ عَلَيْكُمْ رِضْوَانِي فَلَا أَسْخَطُ عَلَيْكُمْ بَعْدَهُ أَبَدًا)) البخاري،  مسلم و الترمذي

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Tabaaraka wa Ta’aalaa Atawaambia watu wa Jannah: Enyi watu wa Jannah! Watasema: Labeka Rabb wetu tuko chini ya amri Yako na kheri zote zimo katika Mikono Yako. Kisha Atasema: Je, mmeridhika?  Watasema: Vipi tusiridhike na hali Umetupa ambayo Hukumpa yeyote mwengine katika viumbe Vyako? Kisha Atasema:  Nitakupeni kilichobora kuliko hayo. Watasema: Ee Rabb, ni kipi kilicho bora kuliko haya? Atasema: Nitafanya ridhaa (mapenzi) Yangu iwateremkie na baada ya hapo Sitoghadhibika nanyi tena abadan)) [Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhy]

 

Share

43-Hadiyth Al-Qudsiy: Nani Aapaye Kwamba Allaah Hatomghufuria Fulani?

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 43

Nani Aapaye Kwamba Allaah Hatomghufuria Fulani?

 

 

عَنْ جُنْدَبٍ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَدَّثَ ((أَنَّ رَجُلًا قَالَ: وَاللَّهِ لَا يَغْفِرُ اللَّهُ لِفُلَانٍ ، وَإِنَّ اللَّهَ تَعَالَى قَالَ: مَنْ ذَا الَّذِي يَتَأَلَّى عَلَيَّ أَنْ لَا أَغْفِرَ لِفُلَانٍ ، فَإِنِّي قَدْ غَفَرْتُ لِفُلَانٍ وَأَحْبَطْتُ عَمَلَكَ))  أَوْ كَمَا قَالَ – مسلم

Imepokelewa kutoka kwa Jundabi (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amehadithia: ((Mtu mmoja alisema: Wa-Allaahi,  Allaah Hatomghufuria fulani kwa haya, Allaah Ta’aalaa Akasema: Ni nani huyo aapaye kwa Jina Langu kuwa Sitamghufuria fulani? Basi kwa yakini Nimemghufuria (huyo) fulani na Nimeporomosha 'amali zako.)) (au kama alivyosema). [Muslim]

 

Share

44-Hadiyth Al-Qudsiy: Sifa Za Anayependeza Zaidi Kwa Allaah

 

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 44

Sifa Za Anayependeza Zaidi Kwa Allaah  

  عَنْ أَبِي أُمَامَةَ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:  ((إِنَّ أَغْبَطَ أَوْلِيَائِي عِنْدِي لَمُؤْمِنٌ خَفِيفُ الْحَاذِ ذُو حَظٍّ مِنْ الصَّلَاةِ أَحْسَنَ عِبَادَةَ رَبِّهِ وَأَطَاعَهُ فِي السِّرِّ وَكَانَ غَامِضًا فِي النَّاسِ لَا يُشَارُ إِلَيْهِ بِالْأَصَابِعِ وَكَانَ رِزْقُهُ كَفَافًا فَصَبَرَ عَلَى ذَلِكَ)) ثُمَّ نَقَرَ بِيَدِهِ فَقَالَ:  ((عُجِّلَتْ مَنِيَّتُهُ قَلَّتْ بَوَاكِيهِ قَلَّ تُرَاثُهُ)) الترمذي (وكذلك  أحمد وابن ماجه ) وإسناده حسن

Abuu Umaamah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba Allaah Amesema: “Hakika anayependeza zaidi Kwangu ni Muumini mwenye hali duni, mswalihina mwenye kumwabudu vizuri kabisa na kumcha kwa siri, ambaye si maarufu kwa watu na wala hatambuliki na ambaye rizki yake ni ndogo kiasi cha kumtosheleza tu, lakini anastahamili hali hiyo.” Kisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akatikisa mkono wake akasema: “Kama mauti yangemfikia mapema asingekuwa na watu wengi wa kumlilia, na urithi wake ungelikuwa mdogo sana.”  [At-Tirmidhiy, Ahmad na Ibn Maajah, Isnaad yake Hasan] 

 

Share