Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah - Imaam Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

 

 

 

 200  سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

 

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

 

 

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

 

Share

000-Maswali 200 Na Majibu Ya 'Aqiydah: Utangulizi Wa Mtunzi

 

 

 200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

 

000-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah Utangulizi Wa Mtunzi

 

 

بِسْمِ الله الرَّحْمنِ الرَّحيم

 

الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَجَعَلَ الظُّلُمَاتِ وَالنُّورَ ۖ ثُمَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ يَعْدِلُونَ ﴿١﴾

AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah), Ambaye Ameumba mbingu na ardhi na Akajaalia viza na nuru; kisha wale ambao wamekufuru wanawasawazisha wengine na Rabb wao.

 

هُوَ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن طِينٍ ثُمَّ قَضَىٰ أَجَلًا ۖ وَأَجَلٌ مُّسَمًّى عِندَهُ ۖ ثُمَّ أَنتُمْ تَمْتَرُونَ ﴿٢﴾

Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbeni kutokana na udongo kisha Akahukumu muda maalumu, na uko Kwake muda maalumu uliokadiriwa, kisha nyinyi mnatilia shaka.

 

وَهُوَ اللَّـهُ فِي السَّمَاوَاتِ وَفِي الْأَرْضِ ۖ يَعْلَمُ سِرَّكُمْ وَجَهْرَكُمْ وَيَعْلَمُ مَا تَكْسِبُونَ ﴿٣﴾

Na Yeye ni Allaah mbinguni na ardhini; Anajua ya siri yenu na ya dhahiri yenu; na Anajua yale mnayoyachuma [Al-An’aam: 1-3]

 

 

Na nashuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah Peke Yake Hana mshirika na Ambaye ni:

 أَحَدٌالصَّمَدُ لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ

Mmoja Pekee. (Allaah) ni Aliyekamilika sifa za utukufu Wake Mkusudiwa haja zote. Hakuzaa na wala Hakuzaliwa. Na wala haiwi Awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye. [Al-Ikhlaasw]

 

 بَل لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ كُلٌّ لَّهُ قَانِتُونَ بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَإِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ

Bali ni Vyake vilivyomo mbinguni na ardhini, vyote vinamtii. Mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Anapokidhia jambo basi huliambia Kun! Basi nalo huwa. [Al-Baqarah: 116-117]

 

 وَرَبُّكَ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ وَيَخْتَارُ ۗ مَا كَانَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٦٨﴾

Na Rabb wako Anaumba na Anachagua Atakavyo. Haikuwa wao wana khiari yoyote. Subhaana-Allaah Utakasifu ni wa Allaah na Ametukuka kwa ‘Uluwa kutokana na yale yote wanayomshirikisha. [Al-Qaswasw: 68]

 

لَا يُسْأَلُ عَمَّا يَفْعَلُ وَهُمْ يُسْأَلُونَ

Haulizwi (Allaah) kwa yale Anayoyafanya, lakini wao wataulizwa. [Al-Anbiyaa: 23]

 

وأشهد أن سيدنا ونبينا محمدا عبده ورسوله أرسله بالهدى ودين الحق ليظهره على الدين كله ولو كره المشركون، صلى الله عليه وسلم وعلى آله وصحبه الذين قضوا بالحق وبه كانوا يعدلون، وعلى التابعين لهم بإحسان الذين لا ينحرفون عن السنة ولا يعدلون بل إياها يقتفون وبها يتمسكون وعليها يوالون ويعادون وعندها يقفون، وعنها يذبون ويناضلون وعلى جميع من سلك سبيلهم وقفا أثرهم إلى يوم يبعثون.

 

Na nashuhudia ya kwamba Sayyidinaa na Nabiy wetu, Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni mja na Rasuli Wake. Amemtuma kwa Risala na Mwongozo na Dini ya haki ili Aidhihirishe juu ya dini zote japo watachukia washirikina.

 

Rahmah na amani za Allaah ziwe juu yake, pamoja na Ahli zake na Swahaba zake ambao walihukumu kwa haki  na kwa Dini hiyo walikuwa waadilifu. Na At-Taabi’iyna (waliowafuata) kwa ihsaan mpaka Siku ya Mwisho, ambao walikuwa hawaendi kinyume na Sunnah, bali kwa Sunnah hizo walizifuata na kuzifanyia kazi, pamoja na kushikamana nazo. Na waliwapenda wanazozifanyia kazi, na kuwachukia kwa wenye kuzipuuza, na kwa Sunnah hizo walizilinda na kuzitetea, na wote waliofuata nyayo zao mpaka Siku ya kufufuliwa.

 

أما بعد فهذا مختصر جليل نافع، عظيم الفائدة جم المنافع، يشتمل على قواعد الدين، ويتضمن أصول التوحيد الذي دعت إليه الرسل وأنزلت به الكتب ولا نجاة لمن بغيره يدين، ويدل ويرشد إلى سلوك المحجة البيضاء ومنهج الحق المستبين شرحت فيه أمور الإيمان وخصاله، وما يزيل جميعه أو ينافي كماله، وذكرت فيه كل مسألة مصحوبة بدليلها, ليتضح أمرها وتتجلى حقيقتها ويبين سبيلها، واقتصرت فيه على مذهب السنة والاتباع وأهملت أقوال أهل الأهواء والابتداع، إذ هي لا تذكر إلا للرد عليها، وإرسال سهام السنة عليها، وقد تصدى لكشف عوارها الأئمة الأجلة، وصنفوا في ردها وأبعادها المصنفات المستقلة مع أن الضد يعرف بضده ويخرج بتعريف ضابطه وحده، فإذا طلعت الشمس لم يفتقر النهار إلى استدلال، وإذ استبان الحق واتضح فما بعده إلا الضلال ورتبته على طريقة السؤال ليستيقظ الطالب وينتبه، ثم أردفه بالجواب الذي يتضح الأمر به ولا يشتبه وسميته. "أعلام السنة المنشورة، لاعتقاد الطائفة الناجية المنصورة" والله أسأل أن يجعله ابتغاء وجهه الأعلى، وأن ينفعنا بما علمنا، ويعلمنا ما ينفعنا نعمة منه وفضلا إنه على كل شيء قدير وبعباده لطيف خبير، وإليه المرجع والمصير وهو مولانا فنعم المولى ونعم النصير.

 

Amma Ba’ad, huu ni Mukhtasari mzuri wenye kunufaisha, na wenye faida kubwa, umesheheni manufaa yenye kukusanya juu ya misingi ya Dini. Pia una misingi ya Tawhiyd iliyolinganiwa na Rusuli wote. Na kwa misingi hiyo vitabu vilishushwa. Na wala hafaulu mtu kinyume na misingi hiyo ambayo ndio yenye kumuongoza katika hoja ya wazi, na Manhaj Swahiyh ya haki. Nimeweka wazi mambo ya Iymaan na yanayohusiana nayo, na nimetaja mas-ala yote sambamba na dalili za nasw ili kuweka wazi zaidi uhakika wa misingi hiyo na kubainisha njia zake. Na nimetosheka kwa hoja na mwenendo wa Ahlus-Sunnah wal-Ittibaa’[1]  Nimeacha kauli za watu wa matamanio na uzushi, pamoja na kuwapinza (radd) na kuwapelekea Sunnah Swahiyh zilizobainishwa na Wanazuoni watukufu kwa ajili ya kujibu hoja zao na kuzitupilia mbali kwa kutunga vitabu mbalimbali. Kwa hakika upinzani kujulikana kwa hoja zake, na kutoa dalili kwa taarifu ya udhibiti wake na mpaka wake. Na jua likitoka huna haja ya kutafuta mchana, na haki inapodhihiri na kufunuka hakuna baada yake isipokuwa ni upotevu.

 

Na nimepanga kwa njia ya maswali ili mwanafunzi aamke na kuzinduka, kisha nimeweka majibu yake ambayo yatakuwa wazi bila kumchanganya mwanafunzi au msomaji na nikakiita:  "Miongozo ya Sunnah Swahiyh kwa ‘Aqiydah ya Atw-Twaaifah An-Naajiyah Al-Manswuwrah.[2]

 

Namuomba Allaah (سبحانه وتعالى) Ajaalie kazi hii kuwa ya kutaka Radhi Zake, Atunufaishe kwa elimu, na Atufundishe yanayotufaa, na kutunufaisha kwa neema Zake na fadhila Zake, kwani yeye Allaah (سبحانه وتعالى) ni Qadiyr (Muweza) wa kila kitu,  ni Latwiyf, Mjuzi wa yaliyofichika na ya Dhahiri  na kwake Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) marejeo. Yeye Ndiye Mola Msaidizi wenu, basi Mola Mzuri Alioje, na Mnusuraji Mzuri Alioje!

 

 

 

 

[1] Watu wa Sunnah na ufuataji wa aliyokuja nayo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

[2] Kundi lilookoka na kunusuriwa.

 

 

Share

001-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Jambo Gani La Mwanzo Linalopasa Waja

 

 

 200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

001-Jambo Gani La Mwanzo Linalopasa Waja

 

 

 

 

 

Swali:

ما أول ما يجب على العباد؟

Jambo gani la mwanzo linalopasa waja?

 

 

Jibu: 

 

ج: أول ما يجب على العباد معرفة الأمر الذي خلقهم الله له ، وأخذ عليهم الميثاق به وأرسل به رسله إليهم وأنزل به كتبه عليهم ، ولأجله خلقت الدنيا والآخرة والجنة والنار وبه حقت الحاقة ووقعت والواقعة وفي شأنه تنصب الموازين وتتطاير الصحف وفيه تكون الشقاوة والسعادة وعلى حسبه تقسم الأنوار (ومن لم يجعل الله له نورا فما له من نور).

 

Jambo la mwanzo linalopasa kwa waja ni: Kujua kusudio la Allaah (سبحانه وتعالى) la kuwaumba wao. Kuchukua ahadi nzito kutoka kwao, kuwatumia Rusuli, kuwashushia kwayo vitabu Vyake. Na kwa ajili yake dunia na Aakhirah imeumbwa, na Jannah na Moto, na imehakiki la kuhakiki na litatokea la kutokea na jambo hilo Mizani zitawekwa, na Swahifa zitatawanywa, na kutakuwa na huzuni na furaha, na kwa mnasaba huo kutagawanywa Nuru.

 

وَمَن لَّمْ يَجْعَلِ اللَّـهُ لَهُ نُورًا فَمَا لَهُ مِن نُّورٍ

Na ambaye Allaah Hakumjaalia Nuru, basi hawi na Nuru [An-Nuwr 24:40]

 

 

 

Share

002-Maswali 200 Na Majibu Ya 'Aqiydah: Jambo Gani Ambalo Ni Sababu Ya Allaah Kuumba Viumbe?

 

 200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

 

002-Jambo Gani Ambalo Ni Sababu Ya Allaah Kuumba Viumbe?

 

 

 

Swali:

 

ما هو ذلك الأمر الذي خلق الله الخلق لأجله؟

Ni jambo gani hilo ambalo Allaah (سبحانه وتعالى) ameumba Viumbe kwa ajili yake?

 

Jibu: 

 

ج: قال الله تعالى ( وما خلقنا السماوات والأرض وما بينهما لاعبين ما خلقناهما إلا بالحق ولكن أكثرهم لا يعلمون) وقال تعالى  (وما خلقنا السماء والأرض وما بينهما باطلا ذلك ظن الذين كفروا ) وقال تعالى  (وخلق الله السماوات والأرض بالحق ولتجزى كل نفس بما كسبت وهم لا يظلمون ) وقال تعالى ( وما خلقت الجن والإنس إلا ليعبدون ) الآيات.

 

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema: 

 

وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاءَ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا لَاعِبِينَ ﴿١٦﴾

Na Hatukuumba mbingu na ardhi na yaliyo baina yake kama wenye kufanya mchezo. [Al-Anbiyaa: 16]

 

Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاءَ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا بَاطِلًا ۚ ذَٰلِكَ ظَنُّ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ  

Na wala Hatukuumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake bila kusudio. Hiyo ndio dhana ya wale waliokufuru.  [Swaad: 27]

 

Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَخَلَقَ اللَّـهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ وَلِتُجْزَىٰ كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ﴿٢٢﴾

Na Allaah Ameumba mbingu na ardhi kwa haki, na ili ilipwe kila nafsi kwa yale iliyoyachuma, nao hawatodhulumiwa. [Al-Jaathiyah: 22]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ ﴿٥٦﴾

Na Sikuumba majini na watu wa isipokuwa waniabudu. [Adh-Dhaariyaat: 56]

 
 

 

Share

003-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Nini Maana Ya ‘Abdu (Mja)?

 

  200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

 

003-Nini Maana Ya ‘Abd (Mja)?

 

 

 

Swali:

 

ما معنى العبد؟

 Nini maana ya ‘Abd (Mja)?

 

 

Jibu:

 

ج: العبد إن أريد به المعبد أي المذلل المسخر فهو بهذا المعنى شامل لجميع المخلوقات من العوالم العلوية والسفلية من عاقل وغيره ورطب ويابس ومتحرك وساكن وظاهر وكامن ومؤمن وكافر وبر وفاجر وغير ذلك الكل مخلوق لله عز وجل مربوب له مسخر بتسخيره مدبر بتدبيره ، ولكل منها رسم يقف عليه وحد ينتهي إليه وكل يجري لأجل مسمى لا يتجاوزه مثقال ذرة ( ذلك تقدير العزيز العليم ) تدبير العدل الحكيم ، وإن أريد به العابد المحب المتذلل خص ذلك بالمؤمنين هم عباده المكرمون ، وأولياؤه المتقون ، الذين لا خوف عليهم ولا هم يحزنون.

 

‘Abdu ikiwa linakusudiwa mwenye kutezwa nguvu au mtumwa, litakuwa na maana ya vyote vilivyoumbwa mbinguni na ardhini, vyenye akili na visivyo na akili, vibichi na vikavu, vyenye kutembea na kusimama, vyenye kuonekana au kujificha, mwenye kuamini na asiyeamini, mwema na muovu, na vinginevyo. Vyote hivyo ni viumbe vya Allaah (سبحانه وتعالى) vyenye kulelewa Naye, na vyenye kudhalilishwa Kwake, vyenye kupangwa kwa mpangilio Wake, vyote vyenye kuwa katika mipaka Yake, na kila vyote kupita katika makadirio Yake ambavyo havichupi mipaka Yake japo chembe. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ ﴿٣٨﴾

Hiyo ni takdiri ya Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mjuzi wa yote. [Yaasiyn: 38]

 

Mpangaji kwa uadilifu, Mwingi wa hekima. Na likikusudiwa mja, mpenzi, mwenye kunyenyekea, hivyo atanasibishwa katika kundi la Waumini, miongoni mwa waja Wake Allaah (سبحانه وتعالى) waliokirimiwa na katika vipenzi Vyake wenye taqwa, ambao hawana khofu wala huzuni.

 

 

Share

004-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: 'Ibaadah Ni Nini?

 

 

  200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

 

004-‘Ibaadah Ni Nini?

 

 

 

Swali:

ماهي العبادة؟

‘Ibaadah ni nini?

 

Jibu:

 

العبادة هي: اسم جامع لكل مايحبه الله ويرضاه من الأقوال والأعمال الظاهرة والباطنة والبراءة مما ينافي ذلك ويضاده

Neno ‘Ibaadah ni: Jina lenye kukusanya kila jambo Alipendalo Allaah (سبحانه وتعالى) na kuliridhia, miongoni mwa kauli za wazi na za ndani, na kuepukana na yale Asioyaridhia na matakwa Yake.

 

 

 

Share

005-Maswali 200 Na Majibu Ya 'Aqiydah: Wakati Gani 'Amali Inakuwa 'Ibaadah?

 

    200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

005-Wakati Gani 'Amali Inakuwa 'Ibaadah?

 

 

 

Swali:

 

متى يكون العمل عبادة؟

Wakati gani ‘amali (matendo) inakuwa ‘Ibaadah?

 

 

Jibu:

 

ج: إذا كمل فيه شيئان وهما كمال الحب مع كمال الذل قال الله تعالى (والذين آمنوا أشد حبا لله) وقال تعالى  (إن الذين هم من خشية ربهم مشفقون) وقد جمع الله تعالى بين ذلك في قوله   (إنهم كانوا يسارعون في الخيرات ويدعوننا رغبا ورهبا وكانوا لنا خاشعين)

 

Matendo yanakuwa Ibaadah yanapotimia ndani yake mambo mawili nayo ni: Ukamilifu wa upendo pamoja na ukamilifu wa unyenyekevu.

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

 وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّـهِ  

Na wale walioamini wana mapenzi zaidi kwa Allaah [Al-Baqarah: 165]

 

Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِنَّ الَّذِينَ هُم مِّنْ خَشْيَةِ رَبِّهِم مُّشْفِقُونَ ﴿٥٧﴾

Hakika wale ambao kwa kumuogopa Rabb wao, bado ni wenye kuchelea (Adhabu Yake). [Al-Muuminuwn: 57]

 

Na mambo hayo Allaah (سبحانه وتعالى) Ameyakusanya katika Aayah kwa kusema:

إِنَّهُمْ كَانُوا يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَيَدْعُونَنَا رَغَبًا وَرَهَبًا ۖ وَكَانُوا لَنَا خَاشِعِينَ ﴿٩٠﴾

Hakika wao walikuwa wakikimbilia katika mambo ya khayr na wakituomba kwa raghba na khofu, na walikuwa wenye kutunyenyekea. [Al-Anbiyaa: 90]

 

  

 

Share

006-Maswali 200 Na Majibu Ya 'Aqiydah: Nini Alama Ya Mapenzi Ya Mja Kwa Rabb Wake?

 

  200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

006-Nini Alama Ya Mapenzi Ya Mja Kwa Rabb Wake?

 

 

 

 

Swali: 

 

Nini alama ya mapenzi ya mja kwa Rabb Wake (عز وجل)

 

Jibu:

 

 

ج: علامة ذلك: أن يحب ما يحبه الله تعالى ويبغض ما يسخطه فيمتثل أوامره ويجتنب مناهيه ويوالي أولياءه ويعادي أعداءه ;ولذا كان أوثق عرى الإيمان الحب في الله والبغض فيه.

Dalili ya hilo ni, mja kupenda yale Anayopenda Allaah (سبحانه وتعالى) na kuchukia Anayoyachukia kwa kutekeleza amri Zake, kujitenga na makatazo Yake, kupenda vipenzi Vyake, na kuchukia maadui Zake. Na kwa kufanya hivyo itakuwa ni kamba madhubuti ya Iymaan, kupenda kwa ajili ya Allaah (سبحانه وتعالى) na kuchukia kwa ajili Yake.

 

 

 

 

Share

007-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Kwa Yepi Waja Wamejua Yale Anayoyapenda Na Kuyaridhia Allaah?

 

  200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

 

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

007-Kwa Yepi Waja Wamejua Yale Anayoyapenda Na Kuyaridhia Allaah?

 

 

 

 

Swali:

 

بماذا عرف العباد ما يحبه الله ويرضاه ؟

 

Kwa yepi waja wamejua yale Anayoyapenda Allaah (سبحانه وتعالى) na kuyaridhia?

 

Jibu:

 

 

ج: عرفوه بإرسال الله تعالى الرسل وإنزاله الكتب آمرا بما يحبه الله ويرضاه ناهيا عما يكرهه ويأباه وبذلك قامت عليهم حجته الدامغة, وظهرت حكمته البالغة قال الله تعالى (رسلا مبشرين ومنذرين لئلا يكون للناس على الله حجة بعد الرسل)  وقال تعالى (قل إن كنتم تحبون الله فاتبعوني يحببكم الله ويغفر لكم ذنوبكم والله غفور رحيم )

 

Wamejua kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kuleta Rusuli na kuteremsha Vitabu Akiamrisha Anayopenda Allaah, kuyaridhia, kukataza Asiyoyapenda na kuyachukia. Na kwa sababu hiyo, hoja zenye nguvu zilisimama juu yao, na hikmah Yake Allaah (سبحانه وتعالى) ikadhihirika kwa kusema:

 

رُّسُلًا مُّبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَى اللَّـهِ حُجَّةٌ بَعْدَ الرُّسُلِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا ﴿١٦٥﴾

Rusuli ni wabashiriaji na waonyaji ili pasikuweko kutoka kwa watu hoja yoyote juu ya Allaah baada ya (kuletwa) Rusuli. Na Allaah daima ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [An-Nisaa: 165]

 

Pia Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

 

قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣١﴾

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Aal-‘Imraan: 31]

 

 

 

Share

008-Maswali 200 Na Majibu Ya 'Aqiydah: Sharti Za 'Ibaadah Ni Ngapi?

 

  200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

008-Sharti Za Ibaadah Ni Ngapi

 

 

 

 

Swali:

كم شروط العبادة؟

 

 Sharti za ‘Ibaadah ni ngapi?

 

Jibu:

 

ثلاثة: الأول: صدق العزيمة وهو شرط في وجودها ,والثاني :إخلاص النية ,والثالث :موافقة الشرع الذي أمر الله تعالى أن لا يدان إلا به ,وهما شرطان في قبولها.

 

  • Kuna sharti tatu:
  • Kuwa na niyyah ya ukweli, ndio sharti la kuwepo kwake
  • Kuwa na niyyah safi

 

Liendane na shariy’ah ambayo Allaah Ameamrisha kutohukumiwa isipokuwa na kwazo, nazo ni sharti mbili za kukubaliwa kwake.

 

 

 

 

Share

009-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Niyyah Ya Kweli Ni Ipi?

 

  200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

009-Niyyah Ya Kweli Ni Ipi

 

 

 

Swali:

ما هو صدق العزيمة؟

Ni ipi hiyo niyyah ya kweli?

 

Jibu: 

 

ج: هو ترك التكاسل والتواني وبذل الجهد في أن يصدق قوله بفعله قال الله تعالى  (يا أيها الذين آمنوا لم تقولون ما لا تفعلون كبر مقتا عند الله أن تقولوا ما لا تفعلون)

 

Hayo ni kuacha uvivu na kuakhirisha akhirisha (mambo) na kutoa juhudi katika kusadikisha kauli yake na vitendo vyake. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لِمَ تَقُولُونَ مَا لَا تَفْعَلُونَ﴿٢﴾

Enyi walioamini!  Kwanini mnasema yale msiyoyafanya?

كَبُرَ مَقْتًا عِندَ اللَّـهِ أَن تَقُولُوا مَا لَا تَفْعَلُونَ﴿٣﴾

Ni chukizo kubwa mno mbele ya Allaah kwamba mnasema yale msiyoyafanya.

[Asw-Swaff: 2-3]

 

 

 

Share

010-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Nini Maana Kuitakasa Niyyah (Ikhlaasw)

 

  200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

010-Nini Maana Kuitakasa Niyyah (Ikhlaasw)

 

 

 

 

Swali:

 

  ما معنى إخلاص النية ؟

 

Nini maana ya kuitakasa Niyyah?  (Ikhlaasw)

 

 

Jibu:

 

ج: هو أن يكون مراد العبد بجميع أقواله وأعماله الظاهرة وإلباطنة ابتغاء وجه الله تعالى قال الله عز وجل  (وما أمروا إلا ليعبدوا الله مخلصين له الدين حنفاء) وقال تعالى  (وما لأحد عنده من نعمة تجزى إلا ابتغاء وجه ربه الأعلى)  وقال تعالى (إنما نطعمكم لوجه الله لا نريد منكم جزاء ولا شكورا)  وقال تعالى  (من كان يريد حرث الآخرة نزد له في حرثه ومن كان يريد حرث الدنيا نؤته منها وما له في الآخرة من نصيب) وغيرها من الآيات.

 

Maana yake ni kuwa kusudio la mja katika kauli na matendo, yawe ya dhahiri au ya siri ni kwa ajili ya kutaka radhi za Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kauli ya Allaah Anayosema:

 

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ ﴿٥﴾

 

Na hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Allaah wenye kumtakasia Dini, wenye kujiengua na upotofu kuelemea Dini ya haki na wasimamishe Swalaah na watoe Zakaah; na hiyo ndiyo Dini iliyosimama imara. [Al-Bayyinah: 5]

 

Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

  

 وَمَا لِأَحَدٍ عِندَهُ مِن نِّعْمَةٍ تُجْزَىٰ ﴿١٩﴾

Na hali hakuna mmoja yeyote aliyemfanyia fadhila yoyote hata amlipe.

 

إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ رَبِّهِ الْأَعْلَىٰ ﴿٢٠﴾

Isipokuwa kutaka Wajihi wa Rabb wake Mwenye ‘Uluwa Aliyetukuka kabisa kuliko vyote. [Al-Layl: 19-20]

 

Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

  

  إِنَّمَا نُطْعِمُكُمْ لِوَجْهِ اللَّـهِ لَا نُرِيدُ مِنكُمْ جَزَاءً وَلَا شُكُورًا﴿٩﴾

Hakika sisi tunakulisheni kwa ajili ya Wajihi wa Allaah, hatukusudii kwenu jazaa na wala shukurani. [Al-Insaan: 9]

 

Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 مَن كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ الْآخِرَةِ نَزِدْ لَهُ فِي حَرْثِهِ ۖ وَمَن كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ الدُّنْيَا نُؤْتِهِ مِنْهَا وَمَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِن نَّصِيبٍ﴿٢٠﴾

Yeyote atakaye mavuno ya Aakhirah Tutamzidishia katika mavuno yake. Na yeyote atakaye mavuno ya dunia, Tutampa humo, lakini Aakhirah hatokuwa na fungu lolote. [Ash-Shuwraa: 20]

 

Na Aayah nyinginezo.

 

 

 

Share

011-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Shariy'ah Ipi Ya Dini Allaah Ameamrisha Kufuata?

 

  200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

 

 

011-Shariyah Ipi Ya Dini Allaah Ameamrisha Kufuata?

 

 

Swali:

 

س: ماهو الشرع الذي أمر الله تعالى أن لا يدان إلا به ؟

Ni shariy’ah ipi ambayo Allaah Ameamrisha kutofuata dini isipokuwa kwayo?

 

 

Jibu:

 

 

ج: هي الحنيفية ملة إبراهيم عليه السلام قال الله تبارك وتعالى  (إن الدين عند الله الإسلام)  وقال تعالى  (أفغير دين الله يبغون وله أسلم من في السماوات والأرض طوعا وكرها) وقال تعالى  (ومن يرغب عن ملة إبراهيم إلا من سفه نفسه) وقال تعالى  (ومن يبتغ غير الإسلام دينا فلن يقبل منه وهو في الآخرة من الخاسرين) وقال تعالى  (أم لهم شركاء شرعوا لهم من الدين ما لم يأذن به الله) وغيرها من الآيات.

 

Ni ile shariy’ah bora ambao ni millah (Dini) ya Nabiy Ibraahiym (عليه السلام).  Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:   

 

إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّـهِ الْإِسْلَامُ ۗ

Hakika Dini mbele ya Allaah ni Uislamu. [Aal-‘Imraan: 19]

 

 

Na Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:  

 

 أَفَغَيْرَ دِينِ اللَّـهِ يَبْغُونَ وَلَهُ أَسْلَمَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَإِلَيْهِ يُرْجَعُونَ ﴿٨٣﴾

Je, wanataka dini isiyokuwa ya Allaah, na hali amejisalimisha Kwake kila aliye katika mbingu na katika ardhi akipenda asipende na Kwake watarejeshwa. [Aal-‘Imraan: 83]

 

Na Anasema tena Allaah (سبحانه وتعالى):  

 

 وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٨٥﴾

Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake; naye katika Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika. [Aal-‘Imraan: 85]

 

Na Anasema tena Allaah (سبحانه وتعالى):

وَمَن يَرْغَبُ عَن مِّلَّةِ إِبْرَاهِيمَ إِلَّا مَن سَفِهَ نَفْسَهُ ۚ  

Na ni nani atakayejitenga na mila ya Ibraahiym isipokuwa anayeitia nafsi yake upumbavu? [Al-Baqarah: 130]

 

Na Anasema tena Allaah (سبحانه وتعالى):

 أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّـهُ ۚ  

Je, wanao washirika waliowaamuru Dini yale ambayo Allaah Hakuyatolea idhini? [Ash-Shuwraa: 21]

  

 

Na Aayah nyinginezo.

 

 

 

 

Share

012-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Dini Ya Kiislamu Ina Daraja Ngapi?

 

 

  200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

012-Dini Ya Kiislamu Ina Daraja Ngapi

 

 

 

 

Swali:

 

كم مراتب دين الإسلام

 

Dini ya Kiislamu ina daraja ngapi?

 

 

Jibu:

 

 هو ثلاث مراتب الإسلام والإيمان والإحسان وكل واحد منها إذا أطلق شمل الدين كله.

 

Dini ya Kiislamu ina darajja tatu nazo ni: Uislamu, Iymaan, na Ihsaan na kila fungu katika hayo matatu linapoachwa linakusanya mafungu yote ya Dini.

 

 

Hadiyth inayothibitisha hayo:

 

عَن عُمَر رضي اللهُ عنه:  أبَيْنَما نَحْنُ جُلْوسٌ عِنْدَ رسُولِ الله صلى الله عليه وسلم ذات يَوْم  إذْ طَلَعَ عَلَيْنَا رَجُلٌ شَدِيدُ بَياضِ الثِّيَاِبِ شَديدُ سَوَادِ الشَّعْرِ، لا يُرَى عليه أَثَرُ السَّفَرِ ولا يَعْرِفُهُ مِنَّا أَحَدٌ، حَتى جَلَسَ إلى النَّبِّي صلى الله عليه وسلم، فأسْنَدَ رُكْبَتَيْهِ إلى رُكْبَتَيْهِ ووَضَعَ كَفَّيْهِ على فَخِذَيْهِ، وقال: يا محمَّدُ أَخْبرني عَن الإسلامِ، فقالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((الإسلامُ أَنْ تَشْهَدَ أَنْ لا إلهَ إلا اللهُ وأَنَّ محمِّداً رسولُ الله، وتُقِيمَ الصَّلاةَ، وتُؤتيَ الزَّكاةَ، وتَصُومَ رَمَضان، وتَحُجَّ الْبَيْتَ إن اسْتَطَعتَ إليه سَبيلاً)). قالَ صَدَقْتَ. فَعَجِبْنا لهُ يَسْأَلُهُ ويُصَدِّقُهُ، قال : فَأَخْبرني عن الإِيمان. قال: ((أَن تُؤمِنَ باللهِ، وملائِكَتِهِ وكُتُبِهِ، ورسُلِهِ، واليَوْمِ الآخِرِ، وتُؤمِنَ بالْقَدَرِ خَيْرِهِ وشَرِّهِ)) قال صدقت. قال : فأخْبرني عَنِ الإحْسانِ. قال:(( أنْ تَعْبُدَ الله كَأَنَّكَ تَرَاهُ فإنْ لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ فإنَّهُ يَرَاك)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ  

Kutoka kwa 'Umar (رضي الله عنه)  ambaye amesema: Siku moja tulikuwa tumekaa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) , hapo alitokea  mtu ambaye  nguo zake zilikuwa nyeupe pepe na nywele zake zilikuwa nyeusi sana; hakuwa na alama  ya machofu ya safari na wala hapakuwa na hata mmoja katika sisi aliyemtambua. Alienda akakaa karibu na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaweka magoti yake karibu na magoti yake na akaweka viganja vyake juu ya mapaja yake kisha akasema; Ee Muhammad! Niambie kuhusu Uislamu.  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Uislamu ni kukiri kuwa hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa  Allaah na Muhammad ni Rasuli Wake, kusimamisha Swalaah, kutoa Zakaah, kufunga (Swawm) za Ramadhaan na kutekeleza Hijjah  kwa mwenye uwezo)) Akasema (yule mtu yaani Jibriyl) – “Umesema kweli”. Tulipigwa na mshangao kwa kumuuliza  kwake Nabiy na kumsadikisha.  Na akasema tena: Niambie  kuhusu Iymaan.  Akasema: ((Ni kumwamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Rusuli Wake na Siku ya Qiyaamah, na  kuamini ya kuwa kheri na shari zinatoka Kwake)). Akasema: “Umesema kweli”. Akasema: “Hebu nielezee kuhusu Ihsaan”.  Akasema Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): (( Ni kumwabudu Allaah kama vile unamuona na kama humuoni basi Yeye Anakuona…)) [Muslim]

 

 

Share

013-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Nini Maana Ya Uislamu?

 

  200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

013-Nini Maana Ya Uislamu?

 

 

 

Swali:

 

ما معنى الإسلام

Ni nini maana ya Uislamu?

 

 

 

Jibu:

 

 

ج: معناه الاستسلام لله بالتوحيد والانقياد له بالطاعة والخلوص من الشرك قال الله تعالى (ومن أحسن دينا ممن أسلم وجهه لله) وقال تعالى (ومن يسلم وجهه إلى الله وهو محسن فقد استمسك بالعروة الوثقى)  وقال تعالى  (فإلهكم إله واحد فله أسلموا وبشر المخبتين)

 

Maana yake ni kujisalimisha kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kumpwekesha na kufuata maamrisho yake kwa utii na kuepukana na shirki kama Allaah (سبحانه وتعالى)  Anavyosema:

 

وَمَنْ أَحْسَنُ دِينًا مِّمَّنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ وَاتَّبَعَ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۗ وَاتَّخَذَ اللَّـهُ إِبْرَاهِيمَ خَلِيلًا ﴿١٢٥﴾

Na nani aliye bora zaidi kwa Dini kuliko yule aliyejisalimisha kwa Allaah naye ni mtendaji mazuri na akafuata millah ya Ibraahiym aliyejiengua na upotofu akaelemea Dini ya haki. Na Allaah Amemchukua Ibraahiym kuwa ni kipenzi. [An-Nisaa: 125]

 

 

Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):  

 

 وَمَن يُسْلِمْ وَجْهَهُ إِلَى اللَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ ۗ وَإِلَى اللَّـهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ ﴿٢٢﴾

Na anayeusalimisha uso wake kwa Allaah, naye akawa ni mtenda ihsaan, basi kwa yakini ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika. Na kwa Allaah ni hatima ya mambo yote. [Luqmaan: 22]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

  فَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ فَلَهُ أَسْلِمُوا ۗ وَبَشِّرِ الْمُخْبِتِينَ ﴿٣٤﴾

Kwa hiyo Mwabudiwa wenu wa haki ni Ilaah Mmoja Pekee, basi kwake jisalimisheni. Na wabashirie wanyenyekevu. [Al-Hajj: 34] 

 

 

 

Share

014-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Dalili Ipi Inayojulisha Kujumuisha Mojawapo Ya Nguzo Za Kiislamu

 

  200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

014-Dalili Ipi Inayojulisha Kujumuisha Mojawapo Ya Nguzo Za Kiislamu

 

 

 

 

Swali:

 

   ما الدليل على شموله الدين كله عند الإطلاق

Ni ipi dalili inayojulisha kujumuisha mojawapo ya mafungu hayo (ya Dini Ya Kiislamu) kuwa ndio Dini yote?

 

 

Jibu:

 

 

ج: قال الله تعالى  (إن الدين عند الله الإسلام) وقال النبي صلى الله عليه وسلم  (بدأ الإسلام غريبا وسيعود غريبا كما بدأ) وقال صلى الله عليه وسلم   (أفضل الإسلام إيمان بالله) وغير ذلك كثير.

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

 

إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّـهِ الْإِسْلَامُ ۗ

Hakika Dini mbele ya Allaah ni Uislamu [Aal-‘Imraan: 19]

 

Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:

 

 ((بَدَأَ الإِسْلامُ غَرِيبًا ، وَسَيَعُودُ كَمَا بَدَأَ غَرِيبًا...))

((Uislamu ulianza ukiwa mgeni na utaondoka ukiwa ni mgeni kama ulivyoanza)). [Muslim, Kitaabul-Iymaan Juz 145]

 

Na akasema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

((أفضل الإسلام إيمان بالله))

((Uislamu bora kwa mtu ni kumwamini Allaah)) [Ahmad 4/114, Atw-Twabaraniy katika Al-Kabiyr kutoka katika Hadiyth ya ‘Amru bin ‘Absa, al-Haythamiy katika kitabu chake ‘Al-Mujma’ (1/63) kuwa watu waliopokea ni thiqah (waaminifu)]

 

 

Share

015-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Dalili Ipi Ya Kujulisha Nguzo Za Kiislamu Kwa Upana

 

  200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

015-Dalili Ipi Ya Kujulisha Nguzo Za Kiislamu Kwa Upana?

 

 

 

Swali:

 

  ما الدليل على تعريفه بالأركان الخمسة عند التفصيل

Ni ipi dalili ipi ya kujuilsha nguzo za Kiislamu kwa upana?

 

 

Jibu:

 

ج: قوله صلى الله عليه وسلم في حديث سؤال جبريل إياه عن الدين (الإسلام أن تشهد أن لا إله إلا الله  وأن محمدا رسول الله وتقيم الصلاة وتؤتي الزكاة وتصوم رمضان وتحج البيت إن استطعت إليه سبيلا)  وقوله صلى الله عليه وسلم (بني الإسلام على خمس)   فذكر هذه غير أنه قدم الحج على صوم رمضان وكلاهما في الصحيحين.

 

Ni kauli ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) wakati Jibriyl alipomuuliza kuhusiana na Dini.

((Uislamu ni kukiri kuwa hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na Muhammad ni Rasuli Wake, kusimamisha Swalaah, kutoa Zakaah, kufunga (Swawm) Ramadhwaan na kutekeleza Hijjah kwa mwenye uwezo))   [Al-Bukhaariy ( 1/114)  na (8/513) na Muslim (8)]

 

 

Na kauli yake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

((بُنِيَ الإِسْلاَمُ عَلَى خَمْسٍ))

((Uislamu umejengwa kwa nguzo tano)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Katika Hadiyth hii Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ametanguliza kutaja Hijjah juu ya Swawm ya Ramadhwaan, na zote Hadiyth hizo mbili ni Swahiyh kwa Imaam al-Bukhaariy na Imaam Muslim.

 

 

 

 

Share

016-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Nafasi Ya Shahaadah Mbili Katika Dini?

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

016-Ni Ipi Nafasi Ya Shahaadah Mbili Katika Dini?

 

 

 

Swali:

س: ما محل الشهادتين من الدين

 

Ni ipi nafasi ya shahaadah mbili katika Dini?

 

 

Jibu:

 

 

ج: لا يدخل العبد في الدين إلا بهما

قال الله تعالى ( إنما المؤمنون الذين آمنوا بالله ورسوله )

 وقال النبي صلى الله عليه وسلم  ( أمرت أن أقاتل الناس حتى يشهدوا أن لا إله إلا الله وأن محمدا عبده ورسوله )  الحديث وغير ذلك كثير.

 

Mtu haingii katika Dini isipokuwa kwa Shahaadah hizo mbili. Allaah Anasema: 

 

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ

Hakika Waumini ni wale waliomwamini Allaah na Rasuli Wake [An-Nuwr (24: 62)]

 

 Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema:

 

((أُمِرْتُ أن أقاتِل الناسَ حتى يَشهدُوا أن لا إله إلا الله ، أنَّ محمداً رسولُ الله...)

((Nimeamrishwa kupigana na watu mpaka washuhudie kuwa hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah na kwamba Muhammad ni Rasuli Wake)) [Al-Bukhariy na Muslim Hadiyth ya ‘Abdullaahi bin ‘Umar (رضي الله عنهما)]

 

Na Hadiyth nyenginezo zaidi ya hiyo.

 

 

Share

017-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ipi Dalili Ya Kushuhudia Kuwa Hakuna Mwabudiwa Wa Haki Ila Allaah?

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

017-Ipi Dalili Ya Kushuhudia  Kuwa Hakuna Mwabudiwa Wa Haki Ila Allaah?

 

 

 

Swali:

 

س: ما دليل شهادة أن لا إله إلا الله  

 

Ipi Dalili Ya Kushuhudia  Kuwa Hakuna Mwabudiwa Wa Haki Ila Allaah?

 

 

Jibu:

 

ج: قول الله تعالى  (شهد الله أنه لا إله إلا هو والملائكة وأولو العلم قائما بالقسط لا إله إلا هو العزيز الحكيم)

 وقوله تعالى (فاعلم أنه لا إله إلا الله)

وقوله تعالى  (وما من إله إلا الله)  

وقوله تعالى (ما اتخذ الله من ولد وما كان معه من إله)  الآيات

وقوله تعالى  (قل لو كان معه آلهة كما يقولون إذا لابتغوا إلى ذي العرش سبيلا)

 الآيات وغيرها.

Ni kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):  

 

شَهِدَ اللَّـهُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٨﴾

Allaah Ameshuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye; na (pia) Malaika na wenye elimu (kwamba Allaah) ni Mwenye kusimamisha (uumbaji Wake) kwa uadilifu. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Aal-‘Imraan (3:18)]

 

Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ  

Basi jua kwamba: laa ilaaha illa-Allaah (hapana muabudiwa wa haki ila Allaah) [Muhammad (47:19)]

 

 

Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

  وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا اللَّـهُ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ ﴿٦٥﴾

Na hakuna Muabudiwa wa haki yeyote isipokuwa Allaah Mmoja Pekee, Asiyepingika. [Swaad (38:65)]

 

Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

مَا اتَّخَذَ اللَّـهُ مِن وَلَدٍ وَمَا كَانَ مَعَهُ مِنْ إِلَـٰهٍ ۚ  

Allaah Hakujifanyia mwana yeyote, na wala hakukuwa pamoja Naye mwabudiwa yeyote. [Al-Muuwminuwn (23:91)]

 

Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

قُل لَّوْ كَانَ مَعَهُ آلِهَةٌ كَمَا يَقُولُونَ إِذًا لَّابْتَغَوْا إِلَىٰ ذِي الْعَرْشِ سَبِيلًا ﴿٤٢﴾

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Kama ingelikuwa pamoja Naye waabudiwa kama wasemavyo; basi hapo wangelitafuta njia ya kumfikia Mwenye ‘Arshi. [Al-Israa (17:42)]

 

Na Aayah nyenginezo.

 

 

Share

018-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah:Ni Nini Maana Ya Shahaadah Ya Laa Ilaaha Illa-Allaah

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

018-Ni Nini Maana Ya Shahaadah Ya Laa Ilaaha Illa-Allaah

 

 

 

Swali:     

 

س: ما معنى شهادة أن لا إله إلا الله

 

Ni Nini Maana Ya Shahaadah Ya Laa Ilaaha Illa-Allaah?

 

 

Jibu:

 

ج: معناها: نفي استحقاق العبادة عن كل ما سوى الله وإثباتها لله عز وجل وحده لا شريك له في عبادته كما أنه ليس له شريك في ملكه

قال الله تعالى  (ذلك بأن الله هو الحق وأن ما يدعون من دونه هو الباطل وأن الله هو العلي الكبير)

 

Maana yake ni: kukanusha kustahiki ‘ibaadah kwa kila kisichokuwa Allaah (سبحانه وتعالى) na kuithibitisha kwa Allaah (عز وجل)  ni Mmoja Pekee Hana mshirika katika kuabudiwa Kwake, kama ambavyo Allaah (سبحانه وتعالى) Hana mshirika katika ufalme Wake.

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:   

ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْحَقُّ وَأَنَّ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِ هُوَ الْبَاطِلُ وَأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ ﴿٦٢﴾

Hivyo ni kwa kuwa Allaah Ndiye wa Haki, na kwamba vile wanavyoomba badala Yake ndiyo batili, na kwamba Allaah Ndiye Mwenye ‘Uluwa Uliotukuka, Mkubwa Kabisa. [Al-Hajj (22:62)]

 

 

 

 

Share

019-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Yepi Masharti Ya Laa Ilaaha Illa Allaah?

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

019-Yepi Masharti Ya Laa Ilaaha Illa Allaah?

 

 

 

Swali    

 

س: ما هي شروط شهادة أن لا إله إلا الله التي لا تنفع قائلها إلا باجتماعها فيه

 

Yepi Masharti Ya Laa Ilaaha Illa Allaah ambayo hayamnufaishi anayeitamka isipokuwa kwa kukusanyika ndani yake masharti hayo?

 

Jibu:

 

ج: شروطها سبعة:

 

الأول: العلم بمعناها نفيا وإثباتا

 

والثاني: استيقان القلب بها

 

الثالث: الانقياد لها ظاهرا وباطنا

 

الرابع: القبول لها فلا يرد شيئا من لوازمها ومقتضياتها

 

الخامس: الإخلاص فيها

 

السادس: الصدق من صميم القلب لا باللسان فقط

 

السابع: المحبة لها ولأهلها, والموالاة والمعاداة لأجلها.

 

Masharti yake ni saba:

 

 

Kwanza: Kujua maana yake, kukataa na kuthibitisha.

 

Pili: Kukubalika kwa moyo.

 

Tatu: Kuitekeleza kwa dhahiri na siri.

 

Nne: Kuyakubali bila kuacha kitu miongoni mwa yanayoambatana nayo.

 

Tano: Ikhlaasw ndani yake.

 

Sita: Kusadikisha moyoni sio kwa ulimi tu.

 

Saba: Kupenda msharti hayo, na kuwapenda watu wenye kushikamana nayo na kuchukia watu wasiofuata na kuwaenzi wenye kuyaenzi masharti hayo.

 

 

 

 

 

Share

020-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ipi Dalili Kuthibitisha Masharti Hayo Kupitia Qur-aan Na Sunnah?

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

020-Ipi Dalili Kuthibitisha Masharti Hayo Kupitia Qur-aan Na Sunnah?

 

 

Swali:

 

س: ما دليل اشتراط العلم من الكتاب والسنة

 

Ipi dalili kuthibitisha masharti hayo kupitia Qur-aan na Sunnah?

 

Jibu:

 

ج: قول الله تعالى ( إلا من شهد بالحق ) أي بلا إله إلا الله ( وهم يعلمون ) بقلوبهم معنى ما نطقوا به بألسنتهم وقول النبي صلى الله عليه وسلم ( من مات وهو يعلم أن لا إله إلا الله دخل الجنة )

 

 

Ni kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى) Anayosema:

 

 إِلَّا مَن شَهِدَ بِالْحَقِّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿٨٦

isipokuwa yule aliyeshuhudia kwa haki, nao wanaju. [Az-Zukhruf (43:86)]

 

Maana yake ni kwamba: Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, hali wakijua.  

 

Kukiri kwa nyoyo zao ina maana hawakutamka kwa ndimi zao.  

 

Na kauli ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema:

 

مَنْ مَاتَ وَهُوَ يَعْلَمُ أَنَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ دَخَلَ الْجَنَّةَ

 

((Mwenye kufa na hali anajua kuwa laa ilaaha illa-Allaah ataingia peponi)) [Muslim na Ahmad]

 

 

Share

021-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Kushurutisha Yakini Toka Qur-aan Na Sunnah?

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

021-Ni Ipi Kushurutisha Yakini Toka Qur-aan Na Sunnah?

 

 

Swali:  

س: ما دليل اشتراط اليقين من الكتاب والسنة 

 

Ni ipi kushurutisha yakini toka Qur-aan na Sunnah?

 

Jibu:

 

ج: قول الله عز وجل ( إنما المؤمنون الذين آمنوا بالله ورسوله ثم لم يرتابوا ) إلى قوله ( أولئك هم الصادقون ) وقول النبي صلى الله عليه وسلم ( أشهد أن لا إله إلا الله وأني رسول الله لا يلقى الله بهما عبد غير شاك فيهما إلا دخل الجنة ) وقال صلى الله عليه وسلم لأبي هريرة ( من لقيت وراء هذا الحائط يشهد أن لا إله إلا الله مستيقنا بها قلبه فبشره بالجنة ) كلاهما في الصحيح .

 

Ni kauli ya Allaah  (عزَّ وجلَّ):

 

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ لَمْ يَرْتَابُوا وَجَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ ﴿١٥﴾

Hakika Waumini ni wale waliomwamini Allaah na Rasuli Wake, kisha wakawa si wenye shaka, na wakafanya jihaad kwa mali zao na nafsi zao katika njia ya Allaah. Hao ndio  wakweli. [Al-Hujuraat (49:15)]

 

Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema mwenye kusema:

 

 ((أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَنِّى رَسُولُ اللَّهِ لاَ يَلْقَى اللَّهَ بِهِمَا عَبْدٌ غَيْرَ شَاكٍّ إلاَّ دَخَلَ الْجَنَّةِ))

Nashuhudia kwamba hapana ilaaha isipokuwa Allaah na kwamba mimi ni Rasuli wa Allaah, mja yoyote hakutani na Allaah bila kuwa na shaka ndani yake (shahaadah hizo mbili) isipokuwa ataingia peponi . [Muslim Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه)]

 

 

Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  alimwambia Abu Hurayrah  (رضي الله عنه)   kwamba:

 

((مَنْ لَقِيتُ مِنْ وَرَاءِ هَذَا الْحَائِطِ يَشْهَدُ أَنْ لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ مُسْتَيْقِنًا بِهِ قَلْبُهُ بَشَّرْتُهُ بِالْجَنَّةَ))

 Utakaekutana naye nyuma ya ukuta huu, hali ya kuwa anashuhudia kuwa laa ilaaha illa-Allaah, kwa dhati ya moyo wake, basi mpe biashara ya pepo. [Imepokewa na Muslim-Kitabul Iyman 31].

 

Hadiyth zote hizo mbili ni sahihi.

 

 

Share

022-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ipi Dalili Ya Sharti La Kufuata, Kwa Mujibu Wa Qur-aan Na Sunnah?

 

  200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

022-Ipi Dalili Ya Sharti La Kufuata, Kwa Mujibu Wa Qur-aan Na Sunnah?

 

 

Swali:

 

س: ما دليل اشتراط الانقياد من الكتاب والسنة 

 

Ni ipi dalili ya sharti la kufuata, kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah?

 

Jibu:

 

ج: قال الله تعالى ( ومن يسلم وجهه إلى الله وهو محسن فقد استمسك بالعروة الوثقى ) وقال النبي صلى الله عليه وسلم ( لا يؤمن أحدكم حتى يكون هواه تبعا لما جئت به ).

 

Ni kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى) Anayosema:

 

وَمَن يُسْلِمْ وَجْهَهُ إِلَى اللَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ ۗ وَإِلَى اللَّـهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ ﴿٢٢﴾

 

Na anayesilimisha uso wake kwa Allaah, naye ni mtenda wema, basi kwa yakini ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika. Na kwa Allaah ni mwisho wa mambo yote. [Luqmaan (31:22)]

 

 

Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  akasema:

 

  ((لاَيُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى يَكُونَ هَواهُ تَبَعَاً لِمَا جِئْتُ بِهِ))

Haamini mmoja mwenu mpaka hawaa (matamanio) yake yawe ni kufuata nilichokuja nacho. [Imepokewa na Ibn Abi ‘Asim katika kitabu Sunnah, Al-Baghwi katika Sharhi Sunnah, Al-Khatwib katika At-Taarikh (4/369), Ibn Batwa katika Al-Inabah kitabul Imaan na sanad yake imepita kwa Naim bin Hammad ambaye ni dhaifu, kama ilivyo pokewa kutoka kwa ibn ‘Amru ambaye ni Jahala (hafahamiki), Hadiyth hii ipo katika 40 Nawawi na amesema kuwa ni sahihi. Ibn Rajab alishindana nae kwa kusema: usahihi wake uko mbali kwa kuwa Naim ameipokea peke yake, wametofautiana katika sanad yake kama vile katika sanad yupo ‘Uqbah bin ‘Awf ambaye hafahamiki vile vile].

 

 

Share

023-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Dalili Ipi Ya Kushurutisha Kukubali Toka Qur-aan na Sunnah?

 

200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

023-Dalili  Ipi Ya Kushurutisha Kukubali Toka Qur-aan na Sunnah?

 

 

Swali:

 

س: ما دليل اشتراط القبول من الكتاب والسنة 

    

Ni ipi dalili ya kushurutisha kukubali toka Qur-aan na Sunnah?

 

 

Jibu: 

 

ج: قال الله تعالى في شأن من لم يقبلها( احشروا الذين ظلموا وأزواجهم وما كانوا يعبدون ) إلى قوله( إنهم كانوا إذا قيل لهم لا إله إلا الله يستكبرون ويقولون أئنا لتاركوا آلهتنا لشاعر مجنون )الآيات.

وقال النبي صلى الله عليه وسلم( مثل ما بعثني الله به من الهدى والعلم كمثل الغيث الكثير أصاب أرضا فكان منها نقية قبلت الماء فأنبتت الكلأ والعشب الكثير وكان منها أجادب أمسكت الماء فنفع الله به الناس فشربوا وسقوا وزرعوا, وأصاب منها طائفة أخرى إنما هي قيعان لا تمسك ماء ولا تنبت كلأ, فذلك مثل من فقه في دين الله ونفعه ما بعثني الله به فعلم وعلم ومثل من لم يرفع بذلك رأسا ,ولم يقبل هدى الله الذي أرسلت به ).

 

Ni kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى) kuhusu hali ya asiyekubali:

 

احْشُرُوا الَّذِينَ ظَلَمُوا وَأَزْوَاجَهُمْ وَمَا كَانُوا يَعْبُدُونَ ﴿٢٢

 

(Malaika wataamrishwa): Wakusanyeni wale waliodhulumu na wenziwao na yale waliyokuwa wakiyaabudu.

 

Mpaka katika kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِنَّهُمْ كَانُوا إِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ يَسْتَكْبِرُونَ ﴿٣٥﴾ وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُو آلِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍ ﴿٣٦﴾

 

Wao walipokuwa wakiambiwa: Laa ilaaha illa Allaah (hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah), wakitakabari. Na wanasema: Je, sisi kweli tuache waabudiwa wetu kwa ajili ya mshairi majnuni?! [Asw-Swaffaat (37:22-36)]

 

 

Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema:

 

مَثَلُ مَا بَعَثَنِي اللَّهُ بِهِ مِنْ الْهُدَى وَالْعِلْمِ كَمَثَلِ الْغَيْثِ الْكَثِيرِ أَصَابَ أَرْضًا فَكَانَ مِنْهَا نَقِيَّةٌ قَبِلَتْ الْمَاءَ فَأَنْبَتَتْ الْكَلاَ وَالْعُشْبَ الْكَثِيرَ وَكَانَتْ مِنْهَا أَجَادِبُ أَمْسَكَتْ الْمَاءَ فَنَفَعَ اللَّهُ بِهَا النَّاسَ فَشَرِبُوا وَسَقَوْا وَزَرَعُوا وَأَصَابَتْ مِنْهَا طَائِفَةً أُخْرَى إِنَّمَا هِيَ قِيعَانٌ لاَ تُمْسِكُ مَاءً وَلاَ تُنْبِتُ كَلاَ فَذَلِكَ مَثَلُ مَنْ فَقُهَ فِي دِينِ اللَّهِ وَنَفَعَهُ مَا بَعَثَنِي اللَّهُ بِهِ فَعَلِمَ وَعَلَّمَ وَمَثَلُ مَنْ لَمْ يَرْفَعْ بِذَلِكَ رَأْسًا وَلَمْ يَقْبَلْ هُدَى اللَّهِ الَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ" قَالَ أَبُو عَبْد اللَّهِ قَالَ إِسْحَاقُ وَكَانَ مِنْهَا طَائِفَةٌ قَيَّلَتْ الْمَاءَ قَاعٌ يَعْلُوهُ الْمَاءُ وَالصَّفْصَفُ الْمُسْتَوِي مِنْ الأَرْضِ.

 

 

Mfano wa kile alichonituma Allaah kutokana na uongofu na elimu, ni kama mfano wa mvua nyingi, iliyonyeshea ardhi na ikawa nzuri iliyokubali maji, yakaota malisho na majani mengi na Allaah akawanufaisha watu kwa maji ya kunywa na kunywesha wanyama na wakalimia/wakandisha mazao, na kundi lingine likawa halina kitu, na huo ni mfano wa ardhi ambayo haina kitu nyeupe isiyoshika maji wala kuota malisho. Mfano huo ni kama mfano wa mtu aliyejifunza Dini ya Allaah na akanufaisha kwa kile alichompa akajifunza na akafundisha, na mfano wa ambaye hajainua kichwa kwa hilo na wala hajakubali mwongozo wa Allaah ambao nimetumwa nao" [Al-Bukhaariy (69) na Muslim (2282)]

 

 

Share

024-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Dalili Ipi Ya Kushurutisha Ikhlaasw Katika Qur-aan Na Sunnah?

 

200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

024-Dalili Ipi Ya Kushurutisha Ikhlaasw Katika Qur-aan Na Sunnah?

 

 

 

Swali:

 

س: ما دليل اشتراط الإخلاص من الكتاب والسنة 

 

Ni ipi dalili ya kushurutisha ikhlaasw katika Qur-aan na Sunnah?

 

 

Jibu:

 

ج: قال الله تعالى( ألا لله الدين الخالص )وقال تعالى( فاعبد الله مخلصا له الدين )وقال النبي صلى الله عليه وسلم
( أسعد الناس بشفاعتي من قال لا إله إلا الله خالصا من قلبه )وقال صلى الله عليه وسلم( إن الله تعالى حرم على النار من قال لا إله إلا الله يبغي بذلك وجه الله ).

 

 

Ni kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى)

 

أَلَا لِلَّـهِ الدِّينُ الْخَالِصُ ۚ  ﴿٣﴾

Tanabahi! Ni ya Allaah Pekee Dini iliyotakasika. [Az-Zumar (39:3)]

  

Na Aayah nyingine Allaah Anasema:

 

فَاعْبُدِ اللَّـهَ مُخْلِصًا لَّهُ الدِّينَ ﴿٢﴾

Basi mwabudu Allaah kwa kumtakasia Dini Yeye. [Az-Zumar (39:2)]

 

Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: 

 

(( أسعد الناس بشفاعتي من قال لا إله إلا الله خالصا من قلبه ))

“Mwenye furaha zaidi ya kupata shifaa yangu ni yule mwenye kusema: Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, kwa kutakasa moyo wake”. [Imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslim 99]

 

Akasema tena Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)

 

(( إن الله تعالى حرم على النار من قال لا إله إلا الله يبغي بذلك وجه الله )).

 

“Allaah ameharamisha moto kwa aliyetamka hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, kwa hali ya kutaka radhi ya Allaah kwa hilo” [Imepokewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

Share

025-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Dalili Ipi Ya Kushurutisha Qur-aan na Sunnah?

 

 200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

025-Dalili Ipi Ya Kushurutisha Qur-aan na Sunnah?

 

 

Swali:

 

س: ما دليل الصدق من الكتاب والسنة 

Ni ipi dalili ya Kushurutisha Qur-aan na Sunnah?

 

 

Jibu:

 

ج: قال الله تعالى( ألم أحسب الناس أن يتركوا أن يقولوا آمنا وهم لا يفتنون ولقد فتنا الذين من قبلهم فليعلمن الله الذين صدقوا وليعلمن الكاذبين )إلى آخر الآيات وقال النبي صلى الله عليه وسلم( ما من أحد يشهد أن لا إله إلا الله وأن محمدا رسول الله صدقا من قلبه إلا حرمه الله على النار )وقال للأعرابي الذي علمه شرائع الإسلام إلى أن قال والله لا أزيد عليها ولا أنقص منها فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم( أفلح إن صدق ).

 

Ni kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) inayosema:

 

 

الم ﴿١﴾

Alif Laam Miym.

 

أَحَسِبَ النَّاسُ أَن يُتْرَكُوا أَن يَقُولُوا آمَنَّا وَهُمْ لَا يُفْتَنُونَ ﴿٢﴾

Je, wanadhani watu kwamba wataachwa kwa kuwa wanasema: Tumeamini, nao ndio wasijaribiwe? 

 

وَلَقَدْ فَتَنَّا الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۖ فَلَيَعْلَمَنَّ اللَّـهُ الَّذِينَ صَدَقُوا وَلَيَعْلَمَنَّ الْكَاذِبِينَ ﴿٣﴾

Kwa yakini Tuliwajaribu wale wa kabla yao. Na kwa yakini Allaah Atawatambulisha wale walio wakweli, na kwa hakika Atawatambulisha walio waongo. [Al-'Ankabuwt: (29:1-3)]

 

وقال النبي صلى الله عليه وسلم:

( ما من أحد يشهد أن لا إله إلا الله وأن محمدا رسول الله صدقا من قلبه إلا حرمه الله على النار )وقال للأعرابي الذي علمه شرائع الإسلام إلى أن قال والله لا أزيد عليها ولا أنقص منها فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم( أفلح إن صدق ).

 

Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:

 

“Hakuna mtu yeyote mwenye kushuhudia kuwa hapana mwabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah na Muhammad ni Rasuli Wake kwa ukweli moyoni mwake isipokuwa Allaah Atamharamishia moto”. [Imepokewa na Al-Bukhaariy katika Kitaabul-'Ilm (128), Muslim Kitaabul-Imaan (32) Tamko ni la Al-Bukhaariy katika Hadiyth ya Anas].

 

Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia bedui ambae alimfundisha shariy’ah ya Uislamu mpaka yule bedui aliposema:

 

Naapa kwa Allaah sitazidisha na wala sitopunguza juu ya hayo, na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Amefaulu ikiwa ni mkweli". [Imepokewa na Al-Bukhaariy-Kitaabul-Imaan (16) na Muslim (43)].

 

 

 

Share

026-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Dalili Ipi Ya Kushurutisha Mahaba Toka Qur-aan na Sunnah?

 

 200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

026-Dalili Ipi Ya Kushurutisha Mahaba Toka Qur-aan na Sunnah?

 

 

 

Swali:

 

س: ما دليل اشتراط المحبة من الكتاب والسنة 

Ni ipi dalili ya Kushurutisha mahaba toka Qur-aan na Sunnah?

 

Jibu:

 

ج: قال الله تعالى ( يا أيها الذين آمنوا من يرتد منكم عن دينه فسوف يأتي الله بقوم يحبهم ويحبونه ) وقال النبي صلى الله عليه وسلم ( ثلاث من كن فيه وجد بهن حلاوة الإيمان أن يكون الله ورسوله أحب إليه مما سواهما وأن يحب المرء لا يحبه إلا لله وأن يكره أن يعود في الكفر بعد إذ أنقذه الله منه كما يكره أن يقذف في النار ).

 

Allaah (سبحانه وتعالىAmesema:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَن يَرْتَدَّ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّـهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ أَذِلَّةٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ يُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوْمَةَ لَائِمٍ ۚ ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٥٤﴾

Enyi walioamini! Yeyote atakayeritadi miongoni mwenu akaacha Dini yake, basi Allaah Ataleta watu (badala yao) Atakaowapenda nao watampenda, wanyenyekevu kwa Waumini, washupavu juu ya makafiri, wanafanya Jihaad katika Njia ya Allaah na wala hawakhofu lawama za mwenye kulaumu. Hiyo ni Fadhila ya Allaah, Humpa Amtakaye. Na Allaah Ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote. [Al-Maaidah: (5:54)]

 

Na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

( ثلاث من كن فيه وجد بهن حلاوة الإيمان أن يكون الله ورسوله أحب إليه مما سواهما وأن يحب المرء لا يحبه إلا لله وأن يكره أن يعود في الكفر بعد إذ أنقذه الله منه كما يكره أن يقذف في النار ).

 

"Mambo matatu yawapo ndani yake (mtu) atapata ladha ya Iymaan: Kuwa  Allaah na Rasuli Wake wanapendeza zaidi kuliko  wengine.

Pili: kumpenda mtu kwa ajili ya Allaah pekee.

Tatu: Na achukie kurudi katika ukafiri, baada ya Allaah kumwokoa na ukafiri huo, kama ambavyo anachukia kutupwa katika moto". 

 

 

Share

027-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Dalili Ya Kupenda Kwa Ajili Ya Allaah Na Kuchukia Kwa Ajili Yake?

 

 

 200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

027-Ni Ipi Dalili Ya Kupenda Kwa Ajili Ya Allaah Na Kuchukia Kwa Ajili Yake? 

 

Swali:

س: ما دليل الموالاة لله والمعاداة لأجله 

 

Ni ipi dalili ya kupenda kwa ajili ya Allaah na kuchukia kwa ajili Yake?

 

Jibu:

 

ج: قال الله عز وجل( يا أيها الذين آمنوا لا تتخذوا اليهود والنصارى أولياء بعضهم أولياء بعض ومن يتولهم منكم فإنه منهم )إلى قوله( إنما وليكم الله ورسوله والذين آمنوا )إلى آخر الآيات. وقال تعالى( يا أيها الذين آمنوا لا تتخذوا آباءكم وإخوانكم أولياء إن استحبوا الكفر على الإيمان )الآيتين. وقال تعالى( لا تجد قوما يؤمنون بالله واليوم الآخر يوادون من حاد الله ورسوله )الآية. وقال تعالى( يا أيها الذين آمنوا لا تتخذوا عدوي وعدوكم أولياء )إلى آخر السورة وغير ذلك من الآيات.

 

Ni kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٥١﴾

Enyi walioamini! Msifanye Mayahudi na Manaswara marafiki wandani na walinzi. Wao kwa wao ni marafiki wandani. Na yeyote atakayewafanya marafiki wao wandani, basi hakika yeye ni miongoni mwao. Hakika Allaah Haongoi watu madhalimu.

فَتَرَى الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ يُسَارِعُونَ فِيهِمْ يَقُولُونَ نَخْشَىٰ أَن تُصِيبَنَا دَائِرَةٌ ۚ فَعَسَى اللَّـهُ أَن يَأْتِيَ بِالْفَتْحِ أَوْ أَمْرٍ مِّنْ عِندِهِ فَيُصْبِحُوا عَلَىٰ مَا أَسَرُّوا فِي أَنفُسِهِمْ نَادِمِينَ ﴿٥٢﴾

Utawaona wale ambao katika nyoyo zao mna maradhi (ya unafiki) wanakimbilia kwao wakisema: Tunakhofu usitusibu mgeuko. Basi asaa Allaah Akaleta ushindi au jambo (jengine) litokalo Kwake, wakawa wenye kujuta kwa waliyoyaficha katika nafsi zao.

وَيَقُولُ الَّذِينَ آمَنُوا أَهَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ أَقْسَمُوا بِاللَّـهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ ۙ إِنَّهُمْ لَمَعَكُمْ ۚ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فَأَصْبَحُوا خَاسِرِينَ ﴿٥٣﴾

Na hapo walioamini watasema (wanafiki wakifichuka): Je, hawa ndio wale ambao waliapa kwa Allaah kwa viapo vyao thabiti vya nguvu, kwamba wao wapo pamoja nanyi? Zimeporomoka amali zao, na wamekuwa wenye kukhasirika.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَن يَرْتَدَّ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّـهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ أَذِلَّةٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ يُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوْمَةَ لَائِمٍ ۚ ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٥٤﴾

Enyi walioamini! Yeyote atakayeritadi miongoni mwenu akaacha Dini yake, basi Allaah Ataleta watu (badala yao) Atakaowapenda nao watampenda, wanyenyekevu kwa Waumini, washupavu juu ya makafiri, wanafanya Jihaad katika Njia ya Allaah na wala hawakhofu lawama za mwenye kulaumu. Hiyo ni Fadhila ya Allaah, Humpa Amtakaye. Na Allaah Ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote. 

إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ رَاكِعُونَ ﴿٥٥﴾

Hakika Rafiki wenu Mlinzi ni Allaah na Rasuli Wake na wale walioamini, ambao wanasimamisha Swalaah na wanatoa Zakaah hali ya kuwa wananyenyekea. [Al-Maaidah: (5:51-55)]

 

Na Allaah Amesema:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا آبَاءَكُمْ وَإِخْوَانَكُمْ أَوْلِيَاءَ إِنِ اسْتَحَبُّوا الْكُفْرَ عَلَى الْإِيمَانِ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ﴿٢٣﴾

Enyi walioamini! Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu marafiki wandani ikiwa wanapendelea ukafiri badala ya imaan. Na atakayewafanya marafiki wandani miongoni mwenu, basi hao ndio madhalimu. [At-Tawbah: (9:23)]

 

Na Allaah Akasema tena:

 

 

لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ ۚ ﴿٢٢﴾

Hutokuta watu wanaomuamini Allaah na Siku ya Mwisho kuwa wanafanya urafiki na kuwapenda wanaompinga Allaah na Rasuli Wake, japo wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. [Al-Mujaadalah: (58:22)]

 

Na Aayah nyingine Allaah Anasema:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاءَ ﴿١﴾

Enyi walioamini! Msifanye adui Wangu na adui wenu kuwa marafiki  [Al-Mumtahinah: (60:1)]

 

 

Na Aayah nyenginezo.

 

Share

028-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Dalili Ya Kuushuhudilia Kwamba Muhammad Ni Rasuli Wa Allaah?

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

028-Ni Ipi Dalili Ya Kuushuhudilia Kwamba Muhammad Ni Rasuli Wa Allaah?

 

 

 

Swali:

 

س: ما دليل شهادة أن محمدا رسول الله 

 

Ni ipi dalili ya kuushuhudilia kwamba Muhammad ni Rasuli wa Allaah?

 

Jibu:

 

ج: قول الله تعالى( لقد من الله على المؤمنين إذ بعث فيهم رسولا من أنفسهم يتلو عليهم آياته ويزكيهم ويعلمهم الكتاب والحكمة )الآية. وقوله تعالى( لقد جاءكم رسول من أنفسكم عزيز عليه ما عنتم حريص عليكم بالمؤمنين رءوف رحيم ).وقوله تعالى( والله يعلم إنك لرسوله )وغيرها من الآيات.

 

Ni kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): 

 

لَقَدْ مَنَّ اللَّـهُ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ إِذْ بَعَثَ فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْ أَنفُسِهِمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ  ﴿١٦٤﴾

Kwa yakini Allaah Amewafanyia fadhila Waumini pale Alipomtuma kwao Rasuli miongoni mwao wenyewe, anawasomea Aayaat Zake na anawatakasa na anawafunza Kitabu na Hikmah (Sunnah). [Aal-'Imraan: (3:164)]

 

Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿١٢٨﴾

Kwa yakini amekujieni Rasuli anayetokana na nyinyi wenyewe, yanamtia mashaka (na huzuni) yanayokutaabisheni, anakujalini, kwa Waumini ni mwenye huruma mno, mwenye rehma. [At-Tawbah: (9:128)].

 

Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَاللَّـهُ يَعْلَمُ إِنَّكَ لَرَسُولُهُ ﴿١﴾

Na Allaah Anajua kuwa wewe ni Rasuli Wake. [Al-Munaafiquwn: (63:1)].

 

 

Na Aayah nyinginezo.

 

 

Share

029-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Nini Maana Ya Kushuhudia Ya Kuwa Muhammad Ni Rasuli Wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)?

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

029-Nini Maana Ya Kushuhudia Ya Kuwa Muhammad Ni Rasuli Wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)?

 

Swali:

 

س: ما معنى شهادة أن محمدا رسول الله صلى الله عليه وسلم 

 

Nini maana ya Kushuhudia ya kuwa Muhammad ni Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)?

 

Jibu:

 

ج: هو التصديق الجازم من صميم القلب المواطئ لقول اللسان بأن محمدا عبده ورسوله إلى كافة الناس إنسهم وجنهم( شاهدا ومبشرا ونذيرا وداعيا إلى الله بإذنه وسراجا منيرا )فيجب تصديقه في جميع ما أخبر به من أنباء ما قد سبق وأخبار ما سيأتي وفيما أحل من حلال وحرم من حرام والامتثال والانقياد لما أمر به والكف والانتهاء عما نهى عنه واتباع شريعته والتزام سنته في السر والجهر مع الرضا بما قضاه والتسليم له وأن طاعته هي طاعة الله ومعصيته معصية الله ;لأنه مبلغ عن الله رسالته ولم يتوفه الله حتى كمل به الدين وبلغ البلاغ المبين وترك أمته على المحجة البيضاء ليلها كنهارها لا يزيغ عنها بعده إلا هالك وفي هذا الباب مسائل ستأتي إن شاء الله.

 

Ni kukubali moja kwa moja ndani ya moyo, sambamba na kutamka kwa ulimi kwamba Muhammad ni mja na Rasuli Wake kwa watu wote bin-Aadam na majini

 

 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ شَاهِدًا وَمُبَشِّرًا وَنَذِيرًا ﴿٤٥﴾

Ee Nabiy! Hakika Sisi Tumekutuma uwe shahidi, na mbashiriaji na mwonyaji.

وَدَاعِيًا إِلَى اللَّـهِ بِإِذْنِهِ وَسِرَاجًا مُّنِيرًا ﴿٤٦﴾

Na mlinganiaji kwa Allaah kwa Idhini Yake, na siraji kali yenye nuru. [Al-Ahzaab: (33:45-46)]

 

Kwa hiyo  inapasa kumsadikisha katika yote aliyoyaeleza, habari zilizopita na habari zijazo, katika aliyohalalisha, na aliyoharamisha kufuata na kunyenyekea aliyoyaamrisha, kujizuia na kukoma kwa aliyoyakataza, kufuata shariy’ah yake na kulazimu Sunnah yake katika siri na jahara pamoja na kuridhia hukumu yake na kujisalimisha kwake, na kuwa kumtii yeye ni kumtii Allaah, kwa kuwa yeye ni mfikishaji wa Allaah na kumuasi yeye ni kumuasi Allaah, na kuwa Allaah hakumfikisha hadi alipokamilisha dini  na akafikisha kufikisha kwa bayana akaacha uma wake kwenye uwanja mweupe usiku wake ni kama mchana wake hapotei (njia) hiyo baada yake, isipokuwa upotevu, katika mlango huu kuna maswali yatakuja In shaa Allaah.

 

 

Share

030-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Yepi Masharti Ya Kuwa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Ni Rasuli Wake?

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

030-Yepi Masharti Ya Kuwa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Ni Rasuli Wake?

 

 

 

س: ما شروط شهادة أن محمدا رسول الله صلى الله عليه وسلم وهل تقبل الشهادة الأولى بدونها 

 

ج: قد قدمنا لك أن العبد لا يدخل في الدين إلا بهاتين الشهادتين وأنهما متلازمتان فشروط الشهادة الأولى هي شروط في الثانية كما أنها هي شروط في الأولى.

 

 

Share

031-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Dalili Ya Swalaah Na Zakaah?

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

031-Ni Ipi Dalili Ya Swalaah Na Zakaah?

 

 

Swali:

 

س: ما دليل الصلاة والزكاة 

 

Ni ipi dalili ya Swalaah na Zakaah?

 

Jibu:

 

ج: قال الله تعالى( فإن تابوا وأقاموا الصلاة وآتوا الزكاة فخلوا سبيلهم )وقال تعالى( فإن تابوا وأقاموا الصلاة وآتوا الزكاة فإخوانكم في الدين )وقال تعالى( وما أمروا إلا ليعبدوا الله مخلصين له الدين حنفاء ويقيموا الصلاة ويؤتوا الزكاة )الآية وغيرها.

 

Ni kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَخَلُّوا سَبِيلَهُمْ ۚ ﴿٥﴾

Lakini wakitubu, na wakasimamisha Swalaah na wakatoa Zakaah, basi waachieni huru njia zao. [At-Tawbah: (9:5)]

 

Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَإِخْوَانُكُمْ فِي الدِّينِ ۗ ﴿١١﴾

Wakitubu, na wakasimamisha Swalaah, na wakatoa Zakaah, basi ni ndugu zenu katika Dini. [At-Tawbah: (9:11)]

 

Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَۚ  ﴿٥﴾

Na hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Allaah hali ya kuwa ni wenye kumtakasia Dini, wenye kujiengua na upotofu kuelemea Dini ya haki, na wasimamishe Swalaah na watoe Zakaah. [Al-Bayyinah: (98:5)]

 

 

Share

032-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Dalili Ya Swaum?

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

032-Ni Ipi Dalili Ya Swaum?

 

 

Swali:

 

س: ما دليل الصوم 

Ni ipi dalili ya Swaum?

 

Jibu:

 

ج: قال الله تعالى( يا أيها الذين آمنوا كتب عليكم الصيام كما كتب على الذين من قبلكم )وقال تعالى( فمن شهد منكم الشهر فليصمه ) الآيات, وفي حديث الأعرابي: أخبرني ما فرض الله علي من الصيام. فقال( شهر رمضان إلا أن تطوع شيئا )الحديث.

 

Ni kauli ya Allaah(سبحانه وتعالى):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٨٣﴾

Enyi walioamini! Mmefaridhishwa Swiyaam kama ilivyofaridhishwa kwa walio kabla yenu mpate kuwa na taqwa. [Al-Baqarah: (2:183)]

 

Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ۖ ﴿١٨٥﴾

Kwa hiyo atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi na afunge. [Al-Baqarah: (2:185)]

 

Na katika kauli ya Bedui:

 

Nijulishe nini Allaah amenifaradhishia mimi kutokana na Swaum? Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamjibu:

"Amefaradhisha mwezi wa Ramadhwaan, isipokuwa kujitolea (Swaum ya Sunnah)".

 

 

Share

033-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Dalili Ya Hajj?

 

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

033-Ni Ipi Dalili Ya Hajj?

 

 

 

Swali:

 

Ni ipi dalili ya Hajj?

س: ما دليل الحج  

Jibu:

 

ج: قال الله تعالى( وأتموا الحج والعمرة لله )وقال تعالى( ولله على الناس حج البيت من استطاع إليه سبيلا )وقال النبي صلى الله عليه وسلم( إن الله تعالى كتب عليكم الحج )الحديث في الصحيحين وتقدم حديث جبريل وحديث( بني الإسلام على خمس )وغيرها كثير.

 

Ni kauli ya Allaah(سبحانه وتعالى):

وَأَتِمُّوا الْحَجَّ وَالْعُمْرَةَ لِلَّـهِ ۚ 

Na timizeni Hajj na ‘Umrah kwa ajili ya Allaah. [Al-Baqarah: (2:196)]

 

Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ  ﴿٩٧﴾ 

Na kwa ajili ya Allaah imewajibika watu watekeleze Hajj katika nyumba (Al-Ka’bah) hiyo kwa mwenye uwezo. [Aal-'Imraan: (3:97)]

 

Na kauli ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema:

 

( إن الله تعالى كتب عليكم الحج )

"Hakika Allaah amekufaradhishieni nyinyi Hajj". (Hadiyth ipo katika Swahiyh mbili. Bukhaariy na Muslim).[Imepokewa na Al-Bukhaariy katika Kitaabul-Iymaan mlango wa Zakkah (46), Muslim (11) katika Hadiyth ya Twalha Ibn ‘Ubaydullah]

 

Na Hadiyth ya Jibriyl imetangulia kuelezea na Hadiyth kuhusiana na:

 ( بني الإسلام على خمس )

"Uislamu umejengwa kwa nguzo tano".

 

 

Share

034-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Hukumu Ya Mtu Mwenye Kupinga Mojawapo Ya Nguzo Za Kiislamu?

 

200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

034-Ni Ipi Hukumu Ya Mtu Mwenye Kupinga Mojawapo Ya Nguzo Za Kiislamu?

 

 

Swali:

س: ما حكم من جحد واحدا منها أو أقر به واستكبر عنه 

Ni ipi hukumu ya mtu mwenye kupinga mojawapo, au akakiri na akafanya kiburi hizo?

 

Jibu:

ج: يقتل كفرا كغيره من المكذبين والمستكبرين مثل إبليس وفرعون.

 

Anauwawa kwa kukufuru, kama mwingine miongoni mwa wapingaji na wenye kiburi kama mfano wa Ibliys na Firawn.

 

 

Share

035-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Hukumu Ya Mwenye Kukubali Halafu Akaacha kwa Uvivu Au Kuibadili?

 

200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

035-Ni Ipi Hukumu Ya Mwenye Kukubali Halafu Akaacha kwa Uvivu Au Kuibadili?

 

 

Swali:

س: ما حكم من أقر بها ثم تركها لنوع تكاسل أو تأويل 

Ni ipi hukumu ya mwenye kukubali halafu akaacha kwa uvivu au kuibadili?

 

Jibu:

 

ج: أما الصلاة  فمن أخرها عن وقتها بهذه الصفة فإنه يستتاب فإن تاب وإلا قتل حدا لقوله تعالى :(فان تابوا وأقاموا الصلاة وآتوا الزكاة فخلوا سبيلهم)  وحديث (أمرت أن أقاتل الناس)  الحديث وغيرها

 أما الزكاة  فإن كان مانعها ممن لا شوكة له أخذها الإمام منه قهرا ,ونكله بأخذ شيء من ماله لقوله صلى الله عليه وسلم:( ومن منعها فإنا آخذوها وشطر ماله معها ) الحديث ,وإن كانوا جماعة ولهم شوكة وجب على الإمام قتالهم حتى يؤدوها للآيات والأحاديث السابقة وغيرها وفعله أبو بكر والصحابة رضي الله عنهم أجمعين.

أما الصوم  فلم يرد فيه شيء ولكن يؤدبه الإمام أو نائبه بما يكون زاجرا له ولأمثاله .

أما الحج  فكل عمر العبد وقت له لا يفوت إلا بالموت والواجب فيه المبادرة ,وقد جاء الوعيد الأخروي في التهاون فيه, ولم ترد فيه عقوبة خاصة في الدنيا. 

 

Ama swalaah kuichelewesha nje ya wakati wake kwa sifa yake, atatakiwa kutubia, na kama hataki atauwawa kwa kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَخَلُّوا سَبِيلَهُمْ ۚ ﴿٥﴾

Lakini wakitubu, na wakasimamisha Swalaah na wakatoa Zakaah, basi waachieni huru njia zao.[At-Tawbah: (9:5)].

 

Na kauli yake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

(أمرت أن أقاتل الناس)

"Nimeamrishwa kupigana na watu mpaka washuhudie Allaah” [Al-Bukhaariy, Muslim, Tirmidhiy, Nasaai na Ibn Majah].

 

Na ama Zakaah, ikiwa mtu atajizuia kutoa na hana silaha, Imam atamlazimisha kutoa Zakaah, na kumuadabisha kwa kuchukua chochote kutokana na mali yake hiyo, kwa kauli ya  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

"Na mwenye kujizuia kutotoa Zakaah, basi mimi nitaichukua kwa nguvu, na kuchukua sehemu ya mali yake kama faini”. [Imepokewa na Ahmad 5/2,3, Abu Dawuwd 1575, An-Nasaai 2515, Ibn Abi Shaybah 1613, AbduRazzaq 1814, Al-Baihaqi 4/105, Al-Hakim 1/398].

 

Wakiwa wengi na wana silaha ni wajibu wa Imam  kupambana nao mpaka walipe Zakaah, kwa mujibu wa Aayah  na Hadiyth tulizotangulia kuzitaja na nyinginezo. Abu Bakar (Radhwiya Allaahu 'anhu) na Swahaaba wengine walifanya hivyo. Ama kuhusu swawm hakuna dalili iliyopokelewa kuelezea, ila ataadabishwa na Imam au Naibu wake, kwa kumkemea na mfano wake, ama Hijjah ni kwa kila umri wa mtu alioupanga kuhiji, na haupiti mpaka afe tu. Ila inamlazimu kuhiji haraka na kuna kemeo kali la Aakherah kuhusiana na kuzembea kwake, japo duniani hakuna adhabu maalumu iliyotajwa.

 

 

Share

036-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Nini Maana Ya Iymaan?

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

036-Nini Maana Ya Iymaan?

 

 

Swali:

س: ماهو الإيمان

Ni ipi Iymaan?

 

Jibu:

 

ج: الإيمان قول وعمل قول القلب واللسان وعمل القلب واللسان والجوارح ويزيد بالطاعة وينقص بالمعصية ويتفاضل أهله فيه.

 

Iymaan ni kauli na matendo, kauli ya moyo na ulimi na ni tendo la moyo, ulimi pamoja na viungo, na Iymaan inaongezeka kwa ucha-Mungu na kupungua kwa maasi na watu huzidiana kwa Iymaan zao.

 

 

Share

037-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Dalili Ya Kauli na Matendo?

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

 

037-Ni Ipi Dalili Ya Kauli na Matendo?

 

 

Swali:

 

س: ما الدليل على كونه قولا وعملا

Ni ipi dalili ya kauli na matendo?

 

Jibu:

 

ج: قال الله تعالى( ولكن الله حبب إليكم الإيمان وزينه في قلوبكم )الآية وقال تعالى( فآمنوا بالله ورسوله )وهذا معنى الشهادتين اللتين لا يدخل العبد في الدين إلا بهما, وهي من عمل القلب اعتقادا ,ومن عمل اللسان نطقا لا تنفع إلا بتواطئهما وقال تعالى( وما كان الله ليضيع إيمانكم )يعني صلاتكم إلى بيت المقدس قبل تحويل القبلة, سمى الصلاة كلها إيمانا وهي جامعة لعمل القلب واللسان والجوارح.

وجعل النبي صلى الله عليه وسلم الجهاد وقيام ليلة القدر وصيام رمضان وقيامه وأداء الخمس وغيرها من الإيمان, وسئل النبي صلى الله عليه وسلم: أي الأعمال أفضل؟ قال( إيمان بالله ورسوله ).

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amesema:

 

وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ حَبَّبَ إِلَيْكُمُ الْإِيمَانَ وَزَيَّنَهُ فِي قُلُوبِكُمْ َ﴿٧﴾

Lakini Allaah Amekupendezesheeni Iymaan, na Akaipamba katika nyoyo zenu [Al-Hujuraat: (49:7)]

 

Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ  ﴿١٥٨﴾

Basi mwaminini Allaah na Rasuli Wake; [Al-A'raaf: (7:157)]

 

Hii ndio maana ya shahaadah mbili ambazo mja hawezi kuingia katika dini isipokuwa kwa hizo nayo ni amali ya moyo kuitakidi na amali ya ulimi ni kutamka. Na hazinufaishi mpaka ziwe zimetulia katika moyo na ulimi.

 

Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُضِيعَ إِيمَانَكُمْ ۚ  ﴿١٤٣﴾

Na Allaah Hakuwa Mwenye Kupoteza Iymaan yenu. [Al-Baqarah: (2:143)]

 

Kwa maana ya kwamba Allaah hawezi kupoteza Swaalah zenu mlizokuwa mkielekea Baytil-Maqdis (Jerusalem) kabla ya kugeuzwa qibla na kuwa Makkah. Swaalah yote imeitwa ni Iymaan, nayo inakusanya matendo ya moyo, ulimi na viungo.

 

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaifanya Jihaad, kisimamo cha Laylatul-Qadri, kufunga Swawm ya Ramadhwaan na kisimamo chake, kuswali Swaalah tano na nyinginezo ni katika Iymaan. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa hivi: Ni matendo gani bora zaidi? Nabiy akajibu ni: "Kumuamini Allaah na Rasuli Wake". [Imepokewa na Al-Bukhaariy (26) na Muslim (83) katika Hadiyth ya Abu Huraiyrah]

 

 

Share

038-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Dalili Ya Kuzidi Iymaan Na Kupungua?

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

038-Ni Ipi Dalili Ya Kuzidi Iymaan Na Kupungua?

 

 

Swali:

 

س: ما الدليل على زيادة الإيمان ونقصانه

Ni ipi dalili ya kuzidi Iymaan na kupungua?

 

Jibu:

 

ج: قوله تعالى( ليزدادوا إيمانا مع إيمانهم )(وزدناهم هدى )( ويزيد الله الذين اهتدوا هدى )( والذين اهتدوا زادهم هدى )( ويزداد الذين آمنوا إيمانا )( فأما الذين آمنوا فزادتهم إيمانا )( فاخشوهم فزادهم إيمانا )( وما زادهم إلا إيمانا وتسليما )وغير ذلك من الآيات, وقال صلى الله عليه وسلم( لو أنكم تكونون في كل حالة كحالتكم عندي لصافحتكم الملائكة ) أو كما قال.

Ni kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

لِيَزْدَادُوا إِيمَانًا مَّعَ إِيمَانِهِمْ ۗ ﴿٤﴾

Ili wazidi imaan pamoja na imaan zao. [Al-Fat-h: (48:4)]

 

Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

وَزِدْنَاهُمْ هُدًى ﴿١٣﴾

Na Tukawazidishia hidaya. [Al-Kahf: (18:13)].

 

Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

وَيَزِيدُ اللَّـهُ الَّذِينَ اهْتَدَوْا هُدًى ۗ  ﴿٧٦﴾

Na Allaah Atawazidishia hidaaya wale wenye kushika uongofu.[ Maryam: (19:76)].

 

Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَالَّذِينَ اهْتَدَوْا زَادَهُمْ هُدًى ﴿١٧﴾

Na wale waliohidika, Anawazidishia Hidaya. [Muhammad: (47:17)]

 

Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 وَيَزْدَادَ الَّذِينَ آمَنُوا إِيمَانًا

Na iwazidishie iymaan wale walioamini. [Al-Muddaththir: (74:31)].

 

Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا فَزَادَتْهُمْ إِيمَانًا ﴿١٢٤﴾

Ama wale walioamini huwazidishia iymaan. [At-Tawbah: (9:124)].

 

Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُوا لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَانًا ﴿١٧٣﴾

Hakika watu wamejumuika dhidi yenu, basi waogopeni. (3:173).

 

Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

وَمَا زَادَهُمْ إِلَّا إِيمَانًا وَتَسْلِيمًا ﴿٢٢﴾

Na haikuwazidishia isipokuwa imaan na kujisalimisha. [Al-Ahzaab: (33:22)].

 

Na Aayah nyenginezo.

 

وقال صلى الله عليه وسلم( لو أنكم تكونون في كل حالة كحالتكم عندي لصافحتكم الملائكة ) أو كما قال.

Na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

"Lau nyinyi mngedumu na hali hii, kama mlivyo hali zenu kwangu, basi Malaika wangekupeni mikono”. [Imepokewa na Muslim (2750)].

 

Au kama alivyosema

 

 

Share

039-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Dalili Ya Kuzidiana Iymaan Kwa Wenye Kuamini?

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

039-Ni Ipi Dalili Ya Kuzidiana Iymaan Kwa Wenye Kuamini?

 

 

Swali:

 

س: ما الدليل على تفاضل أهل الإيمان فيه

 

Ni ipi dalili ya kuzidiana iymaan kwa wenye kuamini?

 

Jibu:

 

ج: قال تعالى( والسابقون السابقون أولئك المقربون )-إلى-( وأصحاب اليمين ما أصحاب اليمين )وقال تعالى( فأما إن كان من المقربين فروح وريحان وجنة نعيم وأما إن كان من أصحاب اليمين فسلام لك من أصحاب اليمين )وقال تعالى( فمنهم ظالم لنفسه ومنهم مقتصد ومنهم سابق بالخيرات بإذن الله )الآيات, وفي حديث الشفاعة( أن الله يخرج من النار من كان في قلبه وزن دينار من إيمان ,ثم من كان في قلبه نصف دينار من إيمان )- وفي رواية يخرج من النار من قال لا إله إلا الله وكان في قلبه من الخير ما يزن شعيرة ثم يخرج من النار من قال لا إله إلا الله وكان في قلبه من الخير ما يزن برة ثم يخرج من النار من قال لا إله إلا الله وكان في قلبه من الخير ما يزن ذرة .

 

 

Ni kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَالسَّابِقُونَ السَّابِقُونَ ﴿١٠﴾

Na waliotangulia mbele, watatangulia mbele.

أُولَـٰئِكَ الْمُقَرَّبُونَ ﴿١١﴾

Hao ndio watakaokurubishwa.

Mpaka katika kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

وَأَصْحَابُ الْيَمِينِ مَا أَصْحَابُ الْيَمِينِ ﴿٢٧﴾

Na watu wa kuliani, je, ni nani watu wa kuliani? [Al-Waaqi'ah: (56:10-27)]

 

Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

فَأَمَّا إِن كَانَ مِنَ الْمُقَرَّبِينَ ﴿٨٨﴾

Basi akiwa miongoni mwa waliokurubishwa.

فَرَوْحٌ وَرَيْحَانٌ وَجَنَّتُ نَعِيمٍ ﴿٨٩﴾

Basi mapumziko ya raha na manukato na Jannah ya neema.

وَأَمَّا إِن كَانَ مِنْ أَصْحَابِ الْيَمِينِ ﴿٩٠﴾

Na kama akiwa miongoni mwa watu wa kuliani.

فَسَلَامٌ لَّكَ مِنْ أَصْحَابِ الْيَمِينِ ﴿٩١﴾

Basi (ataambiwa): Salaam juu yako uliye katika watu wa kuliani. [Al-Waaqi'ah: (56:88-91)]

 

Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

ثُمَّ أَوْرَثْنَا الْكِتَابَ الَّذِينَ اصْطَفَيْنَا مِنْ عِبَادِنَا ۖ فَمِنْهُمْ ظَالِمٌ لِّنَفْسِهِ وَمِنْهُم مُّقْتَصِدٌ وَمِنْهُمْ سَابِقٌ بِالْخَيْرَاتِ بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ  ﴿٣٢﴾

Kisha Tukawarithisha Kitabu wale Tuliowakhitari miongoni mwa Waja Wetu. Basi miongoni mwao yupo mwenye kudhulumu nafsi yake, na miongoni mwao yupo aliye wastani, na miongoni mwao yupo aliyesabiki kwa mambo mengi ya kheri kwa Idhini ya Allaah. [Faatwir: (35:32)]

 

Na katika Hadiyth ya Shifaa:

 

“Hakika Allaah Atamtoa mtu motoni mwenye nusu dinari ya Iymaan”. [Imepokewa na Al-Bukhaariy (7439) na Muslim (183)].

 

Na katika riwaayah nyingine:

 

“Atatolewa motoni mwenye kusema hapana Mungu ila Allaah, na akawa moyoni mwake kuna kheri ya uzani wa shayiri, kisha atatoka mwenye kutamka shahaadah na katika moyo wake kuna uzani wa kheri Mfano punje ya ngano, kisha atatolewa mwenye kutamka Shahaadah na ndani ya moyo wake kuna uzani wa kheri, mfano wa punje ya mahindi”. [Imepokewa na Muslim (193)-Kitaabul-Imaan].

 
 
 
Share

040-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Dalili Inayojulisha Iymaan inakusanya Mfumo Mzima Wa Dini?

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

 

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

040-Ni Ipi Dalili Inayojulisha Iymaan inakusanya Mfumo Mzima Wa Dini?

 

 

Swali:

 

س: ما الدليل على أن الإيمان يشمل الدين كله عند الإطلاق

 

Ni ipi dalili inayojulisha Iymaan inakusanya mfumo mzima wa dini?

 

Jibu:

 

ج: قال النبي صلى الله عليه وسلم في حديث وفد عبد القيس:( آمركم بالإيمان بالله وحده قال أتدرون ما الإيمان بالله وحده؟ قالوا الله ورسوله أعلم. قال: شهادة أن لا إله إلا الله وأن محمدا رسول الله ,وإقام الصلاة ,وإيتاء الزكاة ,وأن تؤدوا من المغنم الخمس ).

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema katika Hadiyth ya ujumbe wa ‘Abdul-Qais: "Ninakuamrisheni kumuamini Allaah Pekee.”

Akawauliza! Je, mnajua nini maana ya kumuamini Allaah Pekee? Wakamjibu: “Allaah na Rasuli Wake ndio Wajuzi zaidi”.

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema:

 

"Ni kutoa Shahaadah mbili, kusimamisha Swalaah, kutoa Zakkah na kutekeleza miongoni mwa ngawira kutoa tano yake" [Imepokewa na Al-Bukhaariy (17) na Muslim (17)].

 

 

Share

041-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Dalili Inayojulisha Juu Ya Nguzo Sita Za Iymaan?

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

041-Ni Ipi Dalili Inayojulisha Juu Ya Nguzo Sita Za Iymaan?

 

 

Swali:

 

س: ما الدليل على تعريف الإيمان بالأركان الستة عند التفصيل

 

Ni ipi dalili inayojulisha juu ya nguzo sita za Iymaan?

 

Jibu:

 

ج: قول النبي صلى الله عليه وسلم لما قال جبريل عليه السلام أخبرني عن الإيمان قال( أن تؤمن بالله وملائكته وكتبه ورسله واليوم الآخر وتؤمن بالقدر خيره وشره )

Ni kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pale Jibriyl (‘Alayhi Salaam) alipomwambia nipe habari kuhusiana na Iymaan Nabiy alimtajia kwa kusema:

 

"Ni Kumuamini Allaah, Malaaikah Wake, Vitabu Vyake, Rasuli Wake, Siku ya Mwisho na kuamini Qadari Yake (Allaah) ya kuwa kheri na shari vinatoka Kwake (Subhaanahu wa Ta'aalaa). [Imepokewa na Muslim-Kitaabul-Iymaan].

 

 

Share

042-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Kwa Ujumla Ni Ipi Dalili Yake Katika Qur-aan?

 

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

042-Kwa Ujumla Ni Ipi Dalili Yake Katika Qur-aan?

 

Swali:

س: ما دليلها من الكتاب جملة

 

Kwa ujumla ni ipi dalili yake Katika Qur-aan?

 

Jibu:

 

ج: قول الله تعالى( ليس البر أن تولوا وجوهكم قبل المشرق والمغرب ولكن البر من آمن بالله واليوم الآخر والملائكة والكتاب والنبيين )وقوله تعالى( إنا كل شيء خلقناه بقدر )وسنذكر إن شاء الله دليل كل على انفراده.

Ni kauli ya Allaah  (عزَّ وجلَّ):

 

لَّيْسَ الْبِرَّ أَن تُوَلُّوا وُجُوهَكُمْ قِبَلَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَلَـٰكِنَّ الْبِرَّ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالْكِتَابِ وَالنَّبِيِّينَ ﴿١٧٧﴾ 

Sio wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa Mashariki na Magharibi, lakini wema ni mwenye kuamini Allaah na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii [Al-Baqarah: (2:177)]

 

Na kauli ya Allaah  (عزَّ وجلَّ):

 

إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ ﴿٤٩﴾

Hakika Sisi Tumekiumba kila kitu kwa Qadar (makadirio, majaaliwa). [Al-Qamar: (54:49)]

 

 

Na tutaendelea kutaja kila dalili kwa upana wake In shaa Allaah.

 

 

Share

043-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Nini Maana Ya Kumuamini Allaah ('Azza wa Jalla)

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

043-Nini Maana Ya Kumuamini Allaah ('Azza wa Jalla)

 

Swali:

س: ما معنى الإيمان بالله عز وجل

 

Nini maana ya kumuamini Allaah ('Azza wa Jalla)?

 

Jibu:

ج: هو التصديق الجازم من صميم القلب بوجود ذاته تعالى الذي لم يسبق بضد ولم يعقب به هو الأول فليس قبله شيء ,والآخر فليس بعده شيء والظاهر فليس فوقه شيء والباطن فليس دونه شيء حي قيوم أحد صمد( لم يلد ولم يولد ولم يكن له كفوا أحد )وتوحيده بإلهيته وربوبيته وأسمائه وصفاته.

 

Ni kukubali moja kwa moja kwa moyo kwamba Allaah Yupo  Ambaye Hana Mshirika, Yeye Ndie  Mwanzo  hakuna kabla Yake, Naye Ndie wa Mwisho  hana baada Yake kitu, Yeye Ndie wa Dhahiri Hana juu Yake kitu chochote, Yeye Ndie wa Siri Hana ndani Yake kitu chochote, Yu Hai, Msimamizi, wa Pekee, Mwenye Kukusiwa, (Hakuzaa wala Hakuzaliwa. Na wala haiwi Awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye). Na kumpwekesha Yeye kwa Uungu Wake na usimamizi Wake, pamoja na majina Yake na Sifa Zake.

 

 

Share

044-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Hiyo Tawhiyd Ya Uungu?

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

044-Ni Ipi Hiyo Tawhiyd Ya Uungu?

 

Swali:

س: ما هو توحيد الإلهية

Ni Ipi hiyo Tawhiyd ya Uungu?

 

Jibu:

ج: هو إفراد الله عز وجل بجميع أنواع العبادة الظاهرة والباطنة قولا وعملا ونفي العبادة عن كل ما سوى الله تعالى كائنا من كان كما قال تعالى( وقضى ربك ألا تعبدوا إلا إياه )وقال تعالى( واعبدوا الله ولا تشركوا به شيئا )وقال تعالى( إنني أنا الله لا إله إلا أنا فاعبدني وأقم الصلاة لذكري )وغير ذلك من الآيات, وهذا قد وفت به شهادة أن لا إله إلا الله.

 

Ni kumpwekesha Allaah ('Azza wa Jalla) kwa aina zote za ‘ibaadah za dhahiri na za ndani kwa kauli na vitendo. Na kutohusisha ‘ibaadah kwa kila asiye kuwa Allaah.

 

Ni kauli ya Allaah  (عزَّ وجلَّ):

وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ ﴿٢٣﴾

Na Rabb wako Ameamuru kwamba: Msiabudu isipokuwa Yeye Pekee [Al-Israa: (17:23)]

 

Na kauli ya Allaah  (عزَّ وجلَّ):

وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ  ﴿٣٦﴾

Na mwabuduni Allaah wala msimshirikishe na chochote. [An-Nisaa: (4:36)

 

Na kauli ya Allaah  (عزَّ وجلَّ):

 

إِنَّنِي أَنَا اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدْنِي وَأَقِمِ الصَّلَاةَ لِذِكْرِي ﴿١٤﴾

Hakika Mimi Ni Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi. Basi niabudu, na simamisha Swalaah kwa ajili ya kunidhukuru. [Twaahaa: (20:14)].

 

Na Aayah nyenginezo.

 

 Mpaka hapo shahaadah yake itakuwa imekamilika.

 

 

Share

045-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Nini Kinyume Cha Tawhiyd Ya Uungu?

 

 200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

045-Nini Kinyume Cha Tawhiyd Ya Uungu?

 

Swali:

س: ما هو ضد توحيد الإلهية

Nini kinyume cha Tawheed ya Uungu?

 

Jibu:

ج: ضده الشرك وهو نوعان شرك أكبر ينافيه بالكلية وشرك أصغر ينافي كماله.

 

Kinyume chake ni kumshirikisha Allaah, nayo ina aina mbili:

(i)                     Shirki kubwa inayopinga mambo yote.

(ii)                   Shirki ndogo inayopinga ukamilifu wake.

 

 

Share

046-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Shirki Kubwa?

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

 

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

046-Ni Ipi Shirki Kubwa?

 

 

 

Swali:

س: ما هوالشرك الأكبر

Ni ipi shirki kubwa?

 

Jibu:

 

: هو اتخاذ العبد من دون الله ندا يسويه برب العالمين يحبه كحب الله ويخشاه كخشية الله ويلتجئ إليه ويدعوه ويخافه ويرجوه ويرغب إليه ويتوكل عليه أو يطيعه في معصية الله أو يتبعه على غير مرضاة الله وغير ذلك قال تعالى( إن الله لا يغفر أن يشرك به ويغفر ما دون ذلك لمن يشاء ومن يشرك بالله فقد افترى إثما عظيما )وقال تعالى( ومن يشرك بالله فقد ضل ضلالا بعيدا )وقال تعالى( ومن يشرك بالله فقد حرم الله عليه الجنة ومأواه النار )وقال تعالى( ومن يشرك بالله فكأنما خر من السماء فتخطفه الطير أو تهوي به الريح في مكان سحيق )وغير ذلك من الآيات

وقال النبي صلى الله عليه وسلم( حق الله على العباد أن يعبدوه ولا يشركوا به شيئا وحق العباد على الله أن لا يعذب من لا يشرك به شيئا )وهو في الصحيحين, ويستوي في الخروج بهذا الشرك عن الدين المجاهر به ككفار قريش وغيرهم, والمبطن له كالمنافقين المخادعين الذين يظهرون الإسلام ويبطنون الكفر, قال الله تعالى( إن المنافقين في الدرك الأسفل من النار ولن تجد لهم نصيرا إلا الذين تابوا وأصلحوا واعتصموا بالله وأخلصوا دينهم لله فأولئك مع المؤمنين )وغير ذلك من الآيات.

 

 

Ni mtu kumfanya kiumbe sawa na Allaah katika ushirika wa kumuomba kinyume cha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala). Anampenda mfano wa kumpenda Allaah, anamuogopa kama anavyomuogopa Allaah, anakimbilia kwake na kumuomba, anamuogopa na kumtegemea, au kumtii katika kumuasi Allaah au kumfuata katika yasiyompendeza Allaah na mengineyo.

 

Ni kauli ya Allaah  (عزَّ وجلَّ):

 

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدِ افْتَرَىٰ إِثْمًا عَظِيمًا ﴿٤٨﴾

Hakika Allaah Haghufurii kushirikishwa, lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae. Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amezua dhambi kuu kabisa. [An-Nisaa: (4:48)]

 

Na kauli ya Allaah  (عزَّ وجلَّ):

 

وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا ﴿١١٦﴾

Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amepotoka upotofu wa mbali. [An-Nisaa: (4:116)]

 

Na kauli ya Allaah  (عزَّ وجلَّ):

 

إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ﴿٧٢﴾

Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Jannah, na makazi yake yatakuwa ni motoni. Na madhalimu hawatopata yeyote mwenye kunusuru. [Al-Maaidah: (5:72)]

 

Na kauli ya Allaah  (عزَّ وجلَّ):

 

وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَكَأَنَّمَا خَرَّ مِنَ السَّمَاءِ فَتَخْطَفُهُ الطَّيْرُ أَوْ تَهْوِي بِهِ الرِّيحُ فِي مَكَانٍ سَحِيقٍ ﴿٣١﴾

Na yeyote anayemshirikisha Allaah, basi ni kama kwamba ameporomoka kutoka mbinguni, wakamnyakua ndege au upepo ukamtupa mahali mbali mno. [Al-Hajj: (22:31)]

 

Na Aayah nyenginezo.

 

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“Haki ya Allaah kwa waja ni kumuabudu Yeye bila kumshirikisha na kitu chochote na haki ya waja kwa Allaah ni kutomuadhibu yule ambae hamshirikishi Allaah na kitu chochote”.

Hadiyth hiyo ipo katika Swahiyh mbili [Al-Bukhaariy (2856) na Muslim (30)].

 

Na wanalingana katika shirki hii kutoka katika dini mwenye kujidhihirisha kwayo kama makafiri wakikuraishi na wengineyo, na wenye kuficha ukafiri wao kama wanafiki na kujidhahirisha na Uislamu. Allaah  (عزَّ وجلَّ) Anasema:

 

إِنَّ الْمُنَافِقِينَ فِي الدَّرْكِ الْأَسْفَلِ مِنَ النَّارِ وَلَن تَجِدَ لَهُمْ نَصِيرًا ﴿١٤٥﴾

Hakika wanafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa katika moto, na wala hutompata kwa ajili yao mwenye kunusuru.

 

إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا وَأَصْلَحُوا وَاعْتَصَمُوا بِاللَّـهِ وَأَخْلَصُوا دِينَهُمْ لِلَّـهِ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَسَوْفَ يُؤْتِ اللَّـهُ الْمُؤْمِنِينَ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿١٤٦﴾

Isipokuwa wale waliotubu, na wakarekebisha mwenendo wao, na wakashikamana na Allaah, na wakakhalisisha Dini yao kwa ajili ya Allaah, basi hao watakuwa pamoja na Waumini. Na Allaah Atawapa Waumini ujira mkubwa kabisa. [An-Nisaa: (4:145-146)]

 

 

 

Share

047-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Hiyo Shirki Ndogo?

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

047-Ni Ipi Hiyo Shirki Ndogo?

 

 

Swali:

س: ما هو الشرك الأصغر

Ni Ipi hiyo shirki ndogo?

 

Jibu:

 

ج: هو يسير الرياء الداخل في تحسين العمل المراد به الله تعالى قال الله تعالى ( فمن كان يرجو لقاء ربه فليعمل عملا صالحا ولا يشرك بعبادة ربه أحدا )وقال النبي صلى الله عليه وسلم( أخوف ما أخاف عليكم الشرك الأصغر )فسئل عنه فقال( الرياء )ثم فسره بقوله صلى الله عليه وسلم( يقوم الرجل فيصلي فيزين صلاته لما يرى من نظر رجل إليه ) ومن ذلك الحلف بغير الله كالحلف بالآباء والأنداد والكعبة والأمانة وغيرها قال صلى الله عليه وسلم( لا تحلفوا بآبائكم ولا بأمهاتكم ولا بالأنداد )وقال صلى الله عليه وسلم( لا تقولوا والكعبة ولكن قولوا ورب الكعبة )وقال صلى الله عليه وسلم( لا تحلفوا إلا بالله) وقال صلى الله عليه وسلم( من حلف بالأمانة فليس منا )وقال صلى الله عليه وسلم( من حلف بغير الله فقد كفر أو أشرك )وفي رواية( وأشرك )ومنه قول ما شاء الله وشئت قال النبي صلى الله عليه وسلم للذي قال له ذلك ( أجعلتني لله ندا بل ما شاء والله وحده )ومنه قول لولا الله وأنت وما لي إلا الله وأنت وأنا داخل على الله وعليك ونحو ذلك, قال صلى الله عليه وسلم( لا تقولوا ما شاء الله وشاء فلان ولكن قولوا ما شاء الله ثم شاء فلان )قال أهل العلم ويجوز لولا الله ثم فلان ,ولا يجوز لولا الله وفلان.

 

Ni kufanya jambo jema kwa niyyah ya kujionyesha. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

 

 فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا ﴿١١٠﴾

Hivyo anayetaraji kukutana na Rabb wake, basi na atende amali njema na wala asimshirikishe yeyote katika ibaada za Rabb wake. [Al-Kahf: (18:110)]

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“Kitu ninachokihofia zaidi kwenu ni shirki ndogo”.

 

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaulizwa kuhusiana na Shirki hiyo na Nabiy akasema:

 

"Ni kujionyesha".

 

Kisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaelezea shirki hiyo kwa kusema:

 

"Ni mtu kuswali na kuirembesha Swalaah hiyo baada ya kuona jicho la mtu likimwangalia yeye”.

 

Na miongoni mwa shirki ndogo ni mtu kuapa kwa asiyekuwa Allaah kama vile kuapa kwa baba zake, au wapenzi wake, au Al-Ka'abah na Amana na vinginevyo.

 

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"Msiape viapo kwa baba zenu, wala kwa mama zenu, au kwa vipenzi vyenu".

 

Na Nabiy (Swalla Allaau 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"Msiseme na Al-Ka'abah, ila semeni na Rabb wa Al-Kaabah".

 

Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema:

 

"Msiape isipokuwa kwa Allaah".

 

Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

“Mwenye kuapa kwa dhamana sio katika sisi”.

 

Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

“Mwenye kuapa kwa asiyekuwa Allaah, hakika amekufuru au amemshirikisha Allaah”.

 

Na katika riwaayah nyingine:

 

“Na akamshirikisha”.

 

Na katika kauli yake Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni: lile Analotaka Allaah na wewe Nabiy.

 

Kauli hii alimwambia yule ambae amesema kwa kiapo hicho kwa kumwambia:

“Je umenifanya mimi ni mshirika wa Allaah? Bali sema Akitaka Allaah Pekee.”

 

Na kauli nyingine ni: Lau sio Allaah na wewe, Nina nini mimi na Allaah, na mimi nipo katika miliki ya Allaah na wewe na wengineo,  na mfano wa hayo.

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akasema:

 

"Msiape kwa kusema Akitaka Allaah na fulani, lakini semeni: Akitaka Allaah, kisha fulani”.

 

Wanachuoni wamesema: Inafaa kusema Akitaka Allaah kisha fulani, na sio kusema Akitaka Allaah na fulani.

 

 

Share

048-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Tofuati Kati ya (waw)-na Na Thumma (kisha) Katika Matamshi Haya?

 

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

048-Ni Ipi Hiyo Tofauti Kati ya (waw)-na Na Thumma (kisha) Katika Matamshi Haya?

 

 

Swali:

س: ما الفرق بين الواو وثم في هذه الألفاظ

Ni ipi tofuati kati ya (waw)-na na thumma (kisha) katika matamshi haya?

 

Jibu:

ج: لأن العطف بالواو يقتضي المقارنة والتسوية فيكون من قال ما شاء الله وشئت قارنا مشيئة العبد بمشيئة الله مسويا بها بخلاف العطف بثم المقتضية للتبعية فمن قال ما شاء الله ,ثم شئت فقد أقر بأن مشيئة العبد تابعة لمشيئة الله تعالى لا تكون إلا بعدها كما قال تعالى( وما تشاءون إلا أن يشاء الله ) وكذلك البقية.

Kwa sababu herufi ya Waw (na) inafahamisha usawa. Mfano: Mtu akisema hivi: Akipenda Allaah na wewe, inajulisha usawa kati ya mja na Allaah katika kupenda kwa pamoja. Kinyume cha Thumma inajulisha baada.

 

Mfano: Mtu akisema: Akipenda Allaah halafu wewe. Inajulisha baada ya kutaka Allaah ndio atake mja, na hapa haijulishi pamoja. 

Ni kauli ya Allaah  (عزَّ وجلَّ):

وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا﴿٣٠﴾

Na hamtoweza kutaka isipokuwa Atake Allaah. Hakika Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote. [Al-Insaan: (76:30)]

 

 

 

 

Share

049-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Nini Tawhiyd Rubuwbiyyah?

 

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

049-Ni Nini Tawhiyd Rubuwbiyyah?

 

 

Swali:

س: ما هو توحيد الربوبية

Ni Nini Tawhiyd Rubuwbiyyah?

 

Jibu:

ج: هو الإقرار الجازم بأن الله تعالى رب كل شيء ومليكه وخالقه ومدبره والمتصرف فيه لم يكن له شريك في الملك ,ولم يكن له ولي من الذل ولا راد لأمره ولا معقب لحكمه ولا مضاد له ولا مماثل له ولا سمي له ولا منازع في شيء من معاني ربوبيته ومقتضيات أسمائه وصفاته, قال الله تعالى( الحمد لله الذي خلق السماوات والأرض وجعل الظلمات والنور )الآيات بل السورة كلها وقال تعالى( الحمد لله رب العالمين )وقال تعالى( قل من رب السماوات والأرض قل الله قل أفاتخذتم من دونه أولياء لا يملكون لأنفسهم نفعا ولا ضرا قل هل يستوي الأعمى والبصير أم هل تستوي الظلمات والنور أم جعلوا لله شركاء خلقوا كخلقه فتشابه الخلق عليهم قل الله خالق كل شيء وهو الواحد القهار )الآيات

 

وقال تعالى( الله الذي خلقكم ثم رزقكم ثم يميتكم ثم يحييكم هل من شركائكم من يفعل من ذلكم من شيء سبحانه وتعالى عما يشركون )وقال تعالى( هذا خلق الله فأروني ماذا خلق الذين من دونه )وقال تعالى( أم خلقوا من غير شيء أم هم الخالقون أم خلقوا السماوات والأرض بل لا يوقنون )الآيات وقال تعالى( رب السماوات والأرض وما بينهما فاعبده واصطبر لعبادته هل تعلم له سميا )وقال تعالى( ليس كمثله شيء وهو السميع البصير )وقال تعالى( وقل الحمد لله الذي لم يتخذ ولدا ولم يكن له شريك في الملك ولم يكن له ولي من الذل وكبره تكبيرا )وقال تعالى( قل ادعوا الذين زعمتم من دون الله لا يملكون مثقال ذرة في السماوات ولا في الأرض وما لهم فيهما من شرك وما له منهم من ظهير ولا تنفع الشفاعة عنده إلا لمن أذن له حتى إذا فزع عن قلوبهم قالوا ماذا قال ربكم قالوا الحق وهو العلي الكبير ).

 

 

 

Share