002-Al-Baqarah: Aayah Na Mafunzo

 

 

 

 

002-Al-Baqarah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

Share

000-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Suwratul-Baqarah

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Fadhila Za Suwratul-Baqarah

 

 

 

Zifuatazo ni fadhila za Suwrah Al-Baqarah kama zilivyopokelewa katika Ahaadiyth mbalimbali:

 

Hadiyth Ya Kwanza:

 

عن ‏ ‏أبي هريرة ‏ رضي الله عنه ‏أن رسول الله ‏ ‏صلى الله عليه وسلم ‏ ‏قال‏: ((لَا تَجْعَلُوا بُيُوتَكُمْ مَقَابِرَ إِنَّ الشَّيْطَانَ يَنْفِرُ مِنَ الْبَيْتِ الَّذِي تُقْرَأُ فِيهِ سُورَةُ الْبَقَرَةِ)) رواه مسلم  

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema: ((Msifanye nyumba zenu makaburi. Kwa hakika shaytwaan haingii nyumba ambayo husomwa humo Suwratul-Baqarah)). [At-Tirmidhiy Hadiyth Hasan Swahiyh] na katika Riwaayah ya Muslim, Hadiyth (780):  ((Shaytwaan anakimbia nyumba inayosomwa ndani yake Suwratul-Baqarah)).

 

 

 

Hadiyth Ya Pili:

 

عَنْ سَهْل بْن سَعْد قَالَ قَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : ((إِنَّ لِكُلِّ شَيْء سَنَامًا وَإِنَّ سَنَام الْقُرْآن سُورَة الْبَقَرَة وَمَنْ قَرَأَهَا فِي بَيْته لَيْلًا لَمْ يَدْخُل الشَّيْطَان بَيْته ثَلَاث لَيَالٍ وَمَنْ قَرَأَهَا نَهَارًا لَمْ يَدْخُل الشَّيْطَان بَيْته ثَلَاثَة أَيَّام)) القاسم الطبراني وأبو حاتموابن حبان في صحيحه، وابن مردويه

Sahl bin Sa’d As-Saa’idiy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kila kitu kina kipeo cha kudhibiti (na kuangaza yaliyo chini) na Al-Baqarah ndio kipeo cha Qur-aan. Atakayesoma Al-Baqarah usiku nyumbani kwake, shaytwaan hatoingia ndani ya nyumba yake nyusiku tatu. Na atakayesoma mchana ndani ya nyumba yake, shaytwaan hatoingia ndani ya nyumba hiyo kwa siku tatu.” [Atw-Twabaraaniy (6/163), Ibn Hibbaan (2/78) na Ibn Mardawayh, Swahiyh At-Targhiyb (2/314)]

 

 

Hadiyth Ya Tatu:

 

عن النَّوَّاسَ بْنَ سَمْعَانَ قال: سَمِعْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((يُؤْتَى بِالْقُرْآنِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَأَهْلِهِ الَّذِينَ كَانُوا يَعْمَلُونَ بِهِ تَقْدُمُهُ سُورَةُ الْبَقَرَةِ وَآلُ عِمْرَانَ وَضَرَبَ لَهُمَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ثَلاثَةَ أَمْثَالٍ مَا نَسِيتُهُنَّ بَعْدُ قَالَ كَأَنَّهُمَا غَمَامَتَانِ أَوْ ظُلَّتَانِ سَوْدَاوَانِ بَيْنَهُمَا شَرْقٌ أَوْ كَأَنَّهُمَا حِزْقَانِ مِنْ طَيْرٍ صَوَافَّ تُحَاجَّانِ عَنْ صَاحِبِهِمَا)) 

Amesimulia An-Nawwaas bin Sam-‘aan (رضي الله عنه):  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Siku ya kufufuliwa, Qur-aan na watu waliokuwa wakiisoma na kutekeleza mafunzo yake, wataletwa mbele wakitangulizwa na Suwratul-Baqarah na Aal-‘Imraan.” Akasema An-Nawwaas: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akatoa mifano mitatu kwa Suwrah mbili hizi na sikusahau mifano hiyo tokea wakati huo. Alisema Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): “Zitakuja kama mawingu mawili au vivuli viwili vyeusi kati yake kuna nuru, au makundi mawili ya ndege waliotandaza mbawa zao wakiruka. Zitawatetea watu wake (wanaoshikamana nazo).” [Muslim]

 

Hadiyth Ya Nne:

 

عن أبي أمامة رضي الله عنه  قال: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((اقْرَءُوا الْقُرْآنَ فَإِنَّهُ يَأْتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ شَفِيعًا لِأَصْحَابِهِ ، اقْرَءُوا الزَّهْرَاوَيْنِ، الْبَقَرَةَ وَسُورَةَ آلِ عِمْرَانَ فَإِنَّهُمَا تَأْتِيَانِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ كَأَنَّهُمَا غَمَامَتَانِ، أَوْ كَأَنَّهُمَا غَيَايَتَانِ، أَوْ كَأَنَّهُمَا فِرْقَانِ ، مِنْ طَيْرٍ صَوَافَّ، تُحَاجَّانِ عَنْ أَصْحَابِهِمَا، اقْرَءُوا سُورَةَ الْبَقَرَةِ فَإِنَّ أَخْذَهَا بَرَكَةٌ وَتَرْكَهَا حَسْرَةٌ وَلَا تَسْتَطِيعُهَا الْبَطَلَةُ)) مسلم

Amesimulia Abuu Umaamah Al-Baahiliy (رضي الله عنه): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Someni Qur-aan kwani itakuja Siku ya Qiyaamah ikiwa ni shafaa’ah (kiombezi) kwa watu wake wanaoisoma na kutekeleza (amri zake). Someni taa mbili: Al-Baqarah na Aal-‘Imraan kwani zitakuja Siku ya Qiyaamah kama kwamba ni maumbile ya mawingu, au sehemu mbili za mawingu, au makundi mawili ya ndege waliotandaza mbawa zao wakiruka. Zitawatetea watu wake (walioshikamana nazo) siku hiyo. Someni Suwratul-Baqarah, kwani kushikamana nayo ni baraka, na kuiacha kwake ni khasara na majuto, na wachawi hawawezi kuihifadhi kwa moyo.” [Muslim (804)] 

 

 

 

 

 

  

 

Share

001-Aayah Na Mafunzo: Herufi Za Mwanzo Katika Baadhi Ya Suwrah

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Herufi Za Mwanzo Katika  Baadhi Ya  Suwrah

الم ﴿١﴾

1. Alif Laam Miym

Mafunzo:

Herufi hizi na nyenginezo kama hizo zinazoanza mwanzoni katika baadhi ya Suwrah, ni katika ‘ilmu ya ghayb ambayo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (Subhaanahuu wa Ta’aalaa) Imehadithiwa kutoka kwa Abuu Bakr, ‘Umar, ‘Uthmaan, ‘Aliy na Ibn Mas‘uwd  (Radhwiya Allaahu ‘anhum) [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

Share

002-Aayah Na Mafunzo: Aina Mbili Za Hidaaya

 

 Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Aina Mbili Za Hidaaya

 

 

ذَٰلِكَ الْكِتَابُ لَا رَيْبَ ۛ فِيهِ ۛ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٢﴾

2. Hiki ni Kitabu kisicho na shaka ndani yake, ni Mwongozo kwa wenye taqwa.

 

Mafunzo:

 

Hudaa, Hidaayah ziko aina mbili;

 

1- Hidaayatut-Tawfiyq:

 

Ni iymaan ambayo mahali pake ni moyoni na ni Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Pekee Awezaye kuiweka katika nyoyo za waja. Dalili ni kauli yake Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa)  Alipomwambia Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye alipendelea kumuongoza ‘Ammi yake Abuu Twaalib katika Uislamu alipokuwa anakaribia kuaga dunia. Allaah Akasema:

 

إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ ﴿٥٦﴾

56. Hakika wewe huwezi kumhidi umpendaye; lakini Allaah Humhidi Amtakaye, Naye Anawajua zaidi wenye kuongoka.” [Al-Qaswasw (28: 56)].

 

Na mfano pia Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

فَإِنَّ اللَّـهَ يُضِلُّ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ ۖ

Basi hakika Allaah Anampotoa Amtakaye na Anamhidi Amtakaye [Faatwir: 8]

 

 

2-Hidaayatul-Irshaad (hidaaya ya kuongoza):

 

Ni kuelekeza, kubainisha, kuongoza njia, kumwongoza mtu katika kutekeleza mema n.k. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٥٢﴾

Na hakika wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) bila shaka unaongoza kuelekea njia iliyonyooka. [Ash-Shuwraa (42 :52)].

 

Na mfano kauli Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

وَأَمَّا ثَمُودُ فَهَدَيْنَاهُمْ فَاسْتَحَبُّوا الْعَمَىٰ عَلَى الْهُدَىٰ فَأَخَذَتْهُمْ صَاعِقَةُ الْعَذَابِ الْهُونِ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿١٧﴾

Na ama kina Thamuwd, Tuliwaongoza, lakini walistahabu upofu kuliko Uongofu. [Fusw-Swilat: 18]

 

 

 

Share

003-Aayah Na Mafunzo: Maana Ya Kusimamisha Swalaah

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Maana Ya Kusimamisha Swalaah

 

الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْغَيْبِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿٣﴾

3. Ambao huamini ya ghayb na husimamisha Swalaah na katika vile Tulivyowaruzuku hutoa.

 

Mafunzo:

Maana ya kusimamisha Swalaah:  Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: “Ni kuswali kwa kuzingatia nguzo na sharti zake.”  Adhw-Dhwahaak amesema kuwa Ibn ‘Abbaas alisema: “Iqamaat Asw-Swalaah maana yake ni kukamilisha rukuu, sujuwd, kusoma Qur-aan, khushuu (unyenyekevu), na kuhudhurisha moyo katika Swalaah.” Qataadah alisema: “Iqamaat Asw-Swalaah maana yake ni kuchunga wakati, wudhuu, rukuu na sujuwd za Swalaah.” Muqaatil bin Hayyaan alisema: “Iqaamat Asw-Swalaah ina maana: Kuchunga wakati, kujitwaharisha kwa ajili yake, kukamilisha rukuu, sujuwd na kusoma Qur-aan, tashahhud na kumwombea rahmah Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hiyo ndiyo Iqaamat Asw-Swalaah.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

 

 

Share

008-Aayah Na Mafunzo: Alama Za Unafiki

Aayah Na Mafunzo:

Al-Baqarah

Alama Za Unafiki

 

 

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَبِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَمَا هُم بِمُؤْمِنِينَ ﴿٨﴾ 

8. Na miongoni mwa watu wako wasemao: ”Tumemuamini Allaah na Siku ya Mwisho” hali ya kuwa si wenye kuamini.

 

Mafunzo:

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ (صلى الله عليه و آله وسلم): ((آيَةُ الْمُنَافِقِ ثلاَثٌ إِذَا حَدَّثَ كَذَبَ وَإِذَا وَعَدَ أَخْلَفَ وَإِذَا اؤْتُمِنَ خَانَ)) متفق عليه . وفي رواية: ((وَإِنْ صَامَ وَصَلَّى وَزَعَمَ أَنَّهُ مُسْلِمٌ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Alama za mnafiki ni tatu: anapozungumza husema uongo, anapotoa ahadi hukhalifu (hatimizi), na anapoaminiwa hufanya khiyana)) [Al-Bukhaariy, Muslim] Na katika riwaaya nyingine: ((Hata akifunga na akiswali na akidai kuwa yeye ni Muislamu)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

 

 

Share

022-Aayah Na Mafunzo: Kumfanyia Allaah anayelingana Naye ni shirki kubwa

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Kumfanyia Allaah anayelingana Naye ni shirki kubwa

 

 

 

الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٢٢﴾

22. Ambaye Amewafanyieni ardhi kuwa ni tandiko na mbingu kuwa ni paa, na Akateremsha kutoka mbinguni maji, Akawatolea kwayo matunda kuwa ni riziki zenu. Basi msimfanyie Allaah waliolingana naye na hali ya kuwa nyinyi mnajua.

 

Mafunzo:

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ سَأَلْتُ ـ أَوْ سُئِلَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ـ أَىُّ الذَّنْبِ عِنْدَ اللَّهِ أَكْبَرُ قَالَ: ((أَنْ تَجْعَلَ لِلَّهِ نِدًّا وَهْوَ خَلَقَكَ))‏‏.‏ قُلْتُ ثُمَّ أَىٌّ قَالَ: ((ثُمَّ أَنْ تَقْتُلَ وَلَدَكَ خَشْيَةَ أَنْ يَطْعَمَ مَعَكَ))‏ قُلْتُ ثُمَّ أَىٌّ قَالَ: ((أَنْ تُزَانِيَ بِحَلِيلَةِ جَارِكَ))‏ قَالَ: وَنَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ تَصْدِيقًا لِقَوْلِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏((‏وَالَّذِينَ لاَ يَدْعُونَ مَعَ اللَّهِ إِلَهًا آخَرَ وَلاَ يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلاَّ بِالْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ‏))

 ‘Abdullaah bin Mas’uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba nilimuuliza au aliulizwa  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Dhambi gani kubwa mbele ya Allaah? Akasema: “Kumfanyia Allaah mlinganishi (kumshirikisha) na hali Yeye Amekuumba.” Nikasema: Kisha ipi? Akasema: “Kumuua mtoto wako kwa khofu ya kutoweza kumpatia chakula chake.”  Nikasema kisha ipi? Akasema: “Kuzini na mke wa jirani yako. Akasema kisha ikateremka Aayah hii kusadikisha kauli ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) : Na wale ambao hawaombi pamoja na Allaah mwabudiwa mwengine na wala hawaui nafsi ambayo Allaah Ameiharamisha (kuuliwa) isipokuwa kwa haki, na wala hawazini.” [Al-Furqaan (25: 68) - Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share

023-Aayah Na Mafunzo: Changamoto Hawezi Yeyote Kuleta Mfano wa Qur-aan

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Changamoto Hawezi Yeyote Kuleta Mfano wa Qur-aan

 

 

 

وَإِن كُنتُمْ فِي رَيْبٍ مِّمَّا نَزَّلْنَا عَلَىٰ عَبْدِنَا فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِّن مِّثْلِهِ وَادْعُوا شُهَدَاءَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٢٣﴾

23. Na ikiwa mko katika shaka kutokana na Tuliyoyateremsha juu ya mja Wetu (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi leteni Suwrah mfano wake, na waiteni mashahidi wenu pasipo na Allaah mkiwa ni wakweli. 

 

فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا وَلَن تَفْعَلُوا فَاتَّقُوا النَّارَ الَّتِي وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ ۖ أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ ﴿٢٤﴾

24. Msipofanya, na wala hamtoweza kufanya, basi ogopeni moto ambao kuni zake ni watu na mawe, umeandaliwa kwa makafiri.

 

Mafunzo:

 

Changamoto kama hiyo Anasema Allaah (Subhanaahu wa Ta’aalaa)

 

أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۖ قُلْ فَأْتُوا بِعَشْرِ سُوَرٍ مِّثْلِهِ مُفْتَرَيَاتٍ وَادْعُوا مَنِ اسْتَطَعْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿١٣﴾

13. Je, wanasema ameitunga (hii Qur-aan)? Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Leteni Suwrah kumi mfano wake zilizotungwa, na iteni muwawezao (wakusaidieni) pasina Allaah mkiwa ni wakweli.  [Huwd: 13]

 

قُل لَّئِنِ اجْتَمَعَتِ الْإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَىٰ أَن يَأْتُوا بِمِثْلِ هَـٰذَا الْقُرْآنِ لَا يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا ﴿٨٨﴾

88. Sema: “Ikiwa watajumuika wanadamu na majini ili walete mfano wa hii Qur-aan; hawatoweza kuleta mfano wake na japokuwa watasaidiana wao kwa wao.”  [Al-Israa: 88]

 

 

Imaam As-Sa’dy (Rahimahu Allaah) amesema:

 

“Na hii ni dalili ya kikomo na burhani ya wazi kuthibitisha aliyokuja nayo Rasuli na akayasadikisha pindi Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anapowapa changamoto ya kuwapinza wana Aadam na majini walete Qur-aan mfano wake, Akawajulisha kwamba hawawezi kuleta mfano wake hata kama watashirikiana wote kufanya hivyo basi hawataweza kamwe!”.

 

 

 

 

 

Share

025-Aayah Na Mafunzo: Miongoni Mwa Neema Za Jannah

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Miongoni Mwa Neema Za Jannah

 

 

وَبَشِّرِ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۖ كُلَّمَا رُزِقُوا مِنْهَا مِن ثَمَرَةٍ رِّزْقًا ۙ قَالُوا هَـٰذَا الَّذِي رُزِقْنَا مِن قَبْلُ ۖ وَأُتُوا بِهِ مُتَشَابِهًا ۖ وَلَهُمْ فِيهَا أَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ ۖ وَهُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٥﴾

25. Na wabashirie wale walioamini na wakatenda mema kwamba watapata Jannaat zipitazo chini yake mito, kila watakaporuzukiwa humo katika matunda kuwa ni riziki husema: “Haya ndiyo yale tuliyoruzukiwa kabla.” Na wataletewa hali ya kuwa yanashabihiana, na watapata humo wake waliotwaharishwa, nao humo ni wenye kudumu.

 

Mafunzo:

 

 قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((إن أول زمرة يدخلون الجنة على صورة القمر ليلة البدر ، ثم الذين يلونهم على أشد كوكب دري في السماء إضاءة ، لا يبولون  ولا يتغوطون ، ولا يتفلون ولا يمتخطون ، أمشاطهم الذهب ، ورشحهم المسك ، ومجامرهم الألوة  الألنجوج ، عود الطيب  وأزواجهم الحور العين ، على خلق رجل واحد ، على صورة أبيهم آدم ، ستون ذراعا في السماء(( البخاري

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kundi la mwanzo watakaongia Jannah watakuwa kama mwezi unapokuwa kamili. Kisha watafuatia ambao watakuwa kama nyota zinazong’ara mbinguni. Hawatakojoa, wala hawatofanya haja kubwa, wala  hawatotema mate, wala hawatopenga kamasi,  vitana vyao vya dhahabu na jasho lao litanukia kama  misk,  vyetezo vyao watatumia udi wa mawardi, wake zao watakuwa ni  Huwrul-‘Ayn wenye macho mazuri makubwa. Watu watakuwa katika umbo la aina ya mtu mmoja, la baba yao Aadam wakiwa dhiraa sitini kwa urefu)) [Al-Bukhaariy]   

 

Mito yake:

 

عَنْ حَكِيم بْن مُعَاوِيَة عَنْ أَبِيهِ قَالَ سَمِعْت رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُول: (( فِي الْجَنَّة بَحْر اللَّبَن وَبَحْر الْمَاء وَبَحْر الْعَسَل وَبَحْر الْخَمْر ثُمَّ تَشَقَّقُ الْأَنْهَار مِنْهَا بَعْد)) وَرَوَاهُ التِّرْمِذِيّ

Imetoka kwa Hakiym bin Mu'aawiyah kutoka kwa baba yake ambaye amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Katika Jannah, kuna bahari ya maziwa, na bahari ya maji, na bahari ya asali na bahari ya mvinyo [wenye ladha]) kisha mito itafunguka humo)) [At-Tirmidhiy]

 

 

 

 

Share

026-Aayah Na Mafunzo: Miongoni Mwa Mifano Ya Allaah Ni Mfano Wa Mbu

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah:

Miongoni Mwa Mifano Ya Allaah Ni Mfano Wa Mbu

 

 

 

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَسْتَحْيِي أَن يَضْرِبَ مَثَلًا مَّا بَعُوضَةً فَمَا فَوْقَهَا ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا فَيَعْلَمُونَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ ۖ وَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا فَيَقُولُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّـهُ بِهَـٰذَا مَثَلًا ۘ يُضِلُّ بِهِ كَثِيرًا وَيَهْدِي بِهِ كَثِيرًا ۚ وَمَا يُضِلُّ بِهِ إِلَّا الْفَاسِقِينَ ﴿٢٦﴾

26. Hakika Allaah Haoni hayaa kupiga mfano wa mbu na ulio zaidi yake (kwa udogo). Basi wale walioamini wanajua kwamba hiyo ni haki kutoka kwa Rabb wao; ama wale waliokufuru husema: “Anataka nini Allaah kwa mfano huu?” (Allaah) Huwapoteza kwayo (mfano huu) wengi na Huwaongoza kwayo wengi na wala Hawapotezi kwayo ila mafasiki.

 

Mafunzo:

 

Makafiri wamefanyia istihzai mifano ya Allaah (Subhanaahu wa Ta’alaa) pale Aliposema:

 

مَثَلُهُمْ كَمَثَلِ الَّذِي اسْتَوْقَدَ نَارًا فَلَمَّا أَضَاءَتْ مَا حَوْلَهُ ذَهَبَ اللَّـهُ بِنُورِهِمْ وَتَرَكَهُمْ فِي ظُلُمَاتٍ لَّا يُبْصِرُونَ ﴿١٧﴾

Mfano wao ni kama mfano wa aliyekoka moto, ulipoyaangaza yaliyopo pembezoni mwake Allaah Akawaondoshea nuru yao na Akawaacha katika viza (hivyo) hawaoni.  [Al-Baqarah: 17]

 

أَوْ كَصَيِّبٍ مِّنَ السَّمَاءِ فِيهِ ظُلُمَاتٌ وَرَعْدٌ وَبَرْقٌ يَجْعَلُونَ أَصَابِعَهُمْ فِي آذَانِهِم مِّنَ الصَّوَاعِقِ حَذَرَ الْمَوْتِ ۚ وَاللَّـهُ مُحِيطٌ بِالْكَافِرِينَ ﴿١٩﴾

Au ni kama mvua kubwa kutoka mbinguni, ndani yake mna viza na radi na umeme, wanatia vidole vyao katika masikio yao kutokana na mingurumo wakikhofu mauti, na Allaah ni Mwenye kuwazunguka kwa ujuzi Wake makafiri. [Al-Baqarah 19]

 

Basi hakika Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:

 

وَلَقَدْ صَرَّفْنَا لِلنَّاسِ فِي هَـٰذَا الْقُرْآنِ مِن كُلِّ مَثَلٍ فَأَبَىٰ أَكْثَرُ النَّاسِ إِلَّا كُفُورًا ﴿٨٩﴾

89. Na kwa yakini Tumesarifu namna kwa namna hii Quraan kwa watu, kwa kila mfano, basi watu wengi kabisa wamekataa kabisa (haki; hawakuacha) isipokuwa kukufuru tu. [Al-Israa: 89]

 

Na:

 

وَلَقَدْ صَرَّفْنَا فِي هَـٰذَا الْقُرْآنِ لِلنَّاسِ مِن كُلِّ مَثَلٍ ۚ وَكَانَ الْإِنسَانُ أَكْثَرَ شَيْءٍ جَدَلًا ﴿٥٤﴾

54. Na kwa yakini Tumesarifu namna kwa namna katika hii Quraan kwa watu, kwa kila mifano. Lakini binaadamu amezidi kuliko kila kitu kwa ubishi.   [Al-Kahf: 54]

 

 

 

 

 

 

Share

027-Aayah Na Mafunzo: Miongoni Mwa Hatari Za Kukata Undugu

 

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Miongoni Mwa Hatari Za Kukata Undugu

 

 

 Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

الَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ اللَّـهِ مِن بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّـهُ بِهِ أَن يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿٢٧﴾

27-Wale wanaovunja ahadi ya Allaah baada ya kuifunga Kwake na wanakata Aliyoyaamrisha Allaah kuungwa, na wanafanya ufisadi katika ardhi, hao ndio wenye khasara.

 

Mafunzo:

 

Makemeo makali ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) yametajwa katika Qur-aan na Sunnah kwa mwenye kukata undugu. Baadhi yake ni kama kulaaniwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala):

 

فَهَلْ عَسَيْتُمْ إِن تَوَلَّيْتُمْ أَن تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَتُقَطِّعُوا أَرْحَامَكُمْ﴿٢٢﴾

Basi huenda nyinyi mkigeuka ndio mfanye ufisadi katika ardhi na kukata jamaa zenu wa uhusiano wa damu?

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّـهُ فَأَصَمَّهُمْ وَأَعْمَىٰ أَبْصَارَهُمْ﴿٢٣﴾

Hao ndio ambao Allaah Amewalaani; Akawafanya viziwi na Akawapofua macho yao. [Muhammad: 22-23]

 

 Na baadhi ya Hadiyth za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

 Jubayr bin Mutw‘im  (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba alimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Hatoingia Jannah mwenye kukata uhusiano wa damu.” [Al-Bukhaariy (5981)]

 

Na pia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

“Hakika Allaah Ameumba viumbe mpaka Alipomaliza ulisimama undugu, ikasema; huyu amesimama anajikinga Kwako na anayemkata, Akasema ndio hivi huridhii Nikimuunga anayekuunga na Ninamkata anayekukata? Akasema sawa. Akasema hilo lako (umekubaliwa ombi lako).” [Al-Bukhaariy]

 

 

 

Share

028-Aayah Na Mafunzo: Kumkufuru Allaah Ilhali Kuna Kufufuliwa Kuhesabiwa Na Kulipwa

Aayah Na Mafunzo

 

Al-Baqarah

 

Kumkufuru Allaah Ilhali Kuna Kufufuliwa Kuhesabiwa Na Kulipwa

 

 

كَيْفَ تَكْفُرُونَ بِاللَّـهِ وَكُنتُمْ أَمْوَاتًا فَأَحْيَاكُمْ ۖ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يُحْيِيكُمْ ثُمَّ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٢٨﴾

28. Vipi mnamkufuru Allaah na hali mlikuwa wafu Akakuhuisheni, kisha Atakufisheni, kisha Atakuhuisheni, kisha Kwake mtarejeshwa?

 

Mafunzo:

 

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba:

وَكُنتُمْ أَمْوَاتًا

“mlikuwa wafu” Kwa maana mlikuwa mchanga kabla ya kukuumbeni.  Basi hivi ni umauti.

فَأَحْيَاكُمْ

“Akakuhuisheni” Kwa maana; Akakuumbeni (mkazaliwa) basi huu ni uhai.

ثُمَّ يُمِيتُكُمْ

“kisha Akakufisheni” Kwa maana mtarudi makaburini, basi huu ni umauti mwengine.

ثُمَّ يُحْيِيكُمْ

“kisha Atakuhuisheni” Kisha Atakufufueni Siku ya Qiyaamah; kwa maani huu ni uhai mwengine. Basi hivyo ni kufa (umauti) mara mbili na uhai mara mbili kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

قَالُوا رَبَّنَا أَمَتَّنَا اثْنَتَيْنِ وَأَحْيَيْتَنَا اثْنَتَيْنِ

Watasema: “Rabb wetu! Umetufisha mara mbili na Umetuhuisha mara mbili [Ghaafir: 11] [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

Imaam As-Sa’dy (Rahimahu Allaah) amesema: “Hili ni swali la kustaajabisha na onyo kali kwamba: Vipi iwe kwenu mnakufuru Allaah Ambaye Amekuumbeni na hali hamkuwa chochote hapo mwanzo, kisha Akakuneemesheni kila aina za neema, kisha Atakufisheni utakapofika wakati wenu ulioandikwa mfe, kisha Atakulipeni makaburini kisha Atakuhuisheni baada ya kufufuliwa na kukusanywa, kisha Kwake mtarudishwa Atakulipeni jazaa kamilifu. Basi madamu mko katika mageuzo Yake  na mabadiliko Yake, na chini ya amri Zake za kidini, na kisha baada ya  hapo kuna malipo; je, hivi inapasa kwenu mumkufuru? Na je, hii nini kama si ujahili mkuu kabisa na ujinga wa hali ya juu. Bali inayokupaseni ni kumcha Yeye na kumshukuru, na kumwamini na kuogopa adhabu Yake na kutaraji thawabu Zake.”

 

 

Share

029-Aayah Na Mafunzo: 'Aqiydah Ya Salaf Kuhusu Maana ya Istiwaa

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

'Aqiydah Ya Salaf Kuhusu Maana ya Istiwaa

 

 

هُوَ الَّذِي خَلَقَ لَكُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ فَسَوَّاهُنَّ سَبْع سَمَاوَاتٍ ۚ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٢٩﴾ 

29. Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbieni vyote vilivyomo ardhini kisha Istawaakuzielekea mbingu na Akazifanya timilifu mbingu saba, Naye kwa kila kitu ni Mjuzi.

 

Mafunzo:

 

 

Istawaa: Inamaanisha Yuko juu kabisa kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa)

 

Faida: Msimamo wa Salaf katika tafsiyr ya Aayah hiyo ni kama uliopokelewa kuwa, Ja’far bin ‘Abdillaah na wengine miongoni mwao walisema: “Tulikuwa kwa Imaam Maalik bin Anas basi akatokea mtu akamuuliza? Ee Abaa ‘Abdillaah! Allaah (Ta’aalaa) Anasema:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ ﴿٥﴾

Mwingi wa rahmah juu ya ‘Arshi Istawaa. [Twaaha  (20: 5)]. 

 

Je, vipi Istawaa? Basi Imaam Maalik hakuwahi kughadhibika kutokana na kitu chochote kile kama alivyoghadhibika kutokana na swali la mtu huyo, kisha [Imaam Maalik] akatazama chini na huku akikwaruzakwaruza kwa kijiti kilichokuwa kwenye mkono wake mpaka akarowa jasho, kisha akanyanyua kichwa chake na kukirembea kile kijiti kisha akasema: ‘Vipi’ ni ghayr ma’quwl (hakutambuliki), na Al-Istiwaa ghayr maj-huwl (si jambo lisilojulikana), na kuamini hilo ni waajib (lazima), na kuuliza (au kuhoji hilo) ni bid’ah (uzushi); na nina khofu kuwa wewe ni mzushi! Akaamrisha mtu huyo atolewe, basi akatolewa. [Imesimuliwa kwenye Al-Hilyah (6/325-326) na pia imesimuliwa na Abuu ‘Uthmaan Asw-Swaabuniy katika ‘Aqiydatu As-Salaf Asw-haab Al-Hadiyth uk. (17-18), kutoka kwa Ja’far bin ‘Abdillaah]

 

Share

031-Aayah Na Mafunzo: Nabiy Aadam ('Alayhis-Salaam) kufunzwa Majina Ya Vitu Vyote

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Nabiy Aadam ('Alayhis-Salaam) kufunzwa Majina Ya Vitu Vyote

 

 

وَعَلَّمَ آدَمَ الْأَسْمَاءَ كُلَّهَا ثُمَّ عَرَضَهُمْ عَلَى الْمَلَائِكَةِ فَقَالَ أَنبِئُونِي بِأَسْمَاءِ هَـٰؤُلَاءِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٣١﴾

31. Na Akamfunza Aadam majina yote (ya kila kitu), kisha Akavionesha mbele ya Malaika; Akasema: “Niambieni majina ya hivi mkiwa ni wakweli.”

 

قَالُوا سُبْحَانَكَ لَا عِلْمَ لَنَا إِلَّا مَا عَلَّمْتَنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ ﴿٣٢﴾

32. Wakasema: Subhaanak Utakasifu ni Wako! Hatuna elimu isipokuwa Uliyotufunza; hakika Wewe Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.

 

 قَالَ يَا آدَمُ أَنبِئْهُم بِأَسْمَائِهِمْ ۖ فَلَمَّا أَنبَأَهُم بِأَسْمَائِهِمْ قَالَ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ إِنِّي أَعْلَمُ غَيْبَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَأَعْلَمُ مَا تُبْدُونَ وَمَا كُنتُمْ تَكْتُمُونَ ﴿٣٣﴾

33. Akasema: “Ee Aadam, wajulishe kwa majina yao.” Basi alipowatajia majina yao; (Allaah) Akasema: “Je, Sikuwaambieni kuwa hakika Mimi Najua ghaibu ya mbingu na ardhi na Najua mnayoyadhihirisha na mliyokuwa mkiyaficha.

 

Mafunzo:

 

Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Watakusanyika Waumini Siku ya Qiyaamah na Watasema: Lau tungetafuta kuombewa shafaa’ah kwa Rabb wetu! Watakwenda kwa Aadam na watasema: Wewe ndio baba wa watu, Amekuumba Allaah kwa Mkono Wake na Akaamrisha Malaika wakusujudie, na Akakufundisha majina ya vitu vyote, basi tuombee kwa Rabb wako ili Atupe faraja kutokana na sehemu yetu hii? Atasema: Mimi siwezi kufanya mnaloomba! Na atakumbuka makosa yake na ataona hayaa, atasema: Mfuateni Nuwh, hakika yeye ndiye Rasuli wa kwanza Aliyemtuma Allaah kwa watu ardhini. Watamfuata. Naye atasema: Siwezi kufanya mnaloomba! Na atakumbuka kumuomba kwake Allaah kwa jambo asilokuwa na ujuzi nalo.  Naye ataona hayaa na atasema: Nendeni kwa Khaliylur-Rahmaan. Watakwenda kwa Ibraahiym. Naye atawaambia: Siwezi kufanya mnaloomba! Nendeni kwa Muwsaa mja ambaye Allaah Alizungumza naye na Akampa Tawraat. Muwsaa atasema: Siwezi kufanya mnaloomba!  Atakumbuka kuwa aliwahi kumuua mtu bila ya haki na ataona hayaa kwa Rabb wake.  Atasema: Nendeni kwa ‘Iysaa kwani ni mja wa Allaah na Rasuli Wake na neno Lake na Roho Yake. Naye atasema: Siwezi kufanya mnaloomba! Nendeni kwa Muhammad, ni mja aliyefutiwa makosa yaliyotangulia na yajayo. Watakuja kwangu na nitakwenda kwa Rabb wangu kumuomba idhini (ya maombi), nitapewa idhini. Nitakapomuona Rabb wangu nitasujudu na Ataniacha hivyo hivyo mpaka Atakavyo. Kisha itasemwa: Inua kichwa chako na omba utapewa! Na sema yatasikilizwa (uyasemayo)! Na omba shafaa‘ah utapewa! Nitainua kichwa changu na nitamhimidi kwa Himdi Zake Atakazonifundisha, kisha nitaomba na Atanikubalia idadi kubwa ya watu, nitawaingiza Jannah. Kisha nitarudi tena Kwake. Nitakapomuona Rabb wangu, nitafanya kama mara ya kwanza, kisha nitaomba na Atanikubalia idadi kubwa ya watu nitawaingiza Jannah. Kisha nitarejea mara ya tatu, kisha nitarudi mara ya nne kisha nitasema: Hakuna watu waliobakia motoni isipokuwa Qur-aan imewazuia na watawajibika kubakia humo.” [Al-Bukhaariy (4476)]

 

 

 

Share

034-Aayah Na Mafunzo: Maasi Ya Kwanza Ni Kibri. Hatoingia Jannah Mwenye Chembe Ya Kibri

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Maasi Ya Kwanza Ni Kibri. Hatoingia Jannah Mwenye Chembe Ya Kibri

 

 

 

وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ أَبَىٰ وَاسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ الْكَافِرِينَ ﴿٣٤﴾

34. Na pale Tulipowaambia Malaika: “Msujudieni Aadam.” Wakasujudu isipokuwa Ibliys alikataa na akatakabari na akawa miongoni mwa makafiri.

 

Mafunzo:

 

Qataadah alisema kuhusu kauli ya Allaah: Wakasujudu isipokuwa Ibliys alikataa na akatakabari na akawa miongoni mwa makafiri.” “Ibliys ni adui wa Allaah. Alimwonea wivu Aadam kwa sababu Allaah Alimtukuza Aadam. Alisema (Ibliys). “Nimeumbwa kwa moto naye (Aadam) kaumbwa kwa udongo!” Kwa hiyo kosa la kwanza kufanywa lilikuwa ni kibri, kwani adui wa Allaah alikuwa na kibri sana kumsujudia Aadam.” Mimi (Ibn Kathiyr) nasema: yameandikwa katika Swahiyh: “Hakuna atakayeingia Jannah mtu ambaye ana kiburi chenye uzito sawa na punje ya khardali.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

 

Share

042-Aayah Na Mafunzo: Sifa Za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Katika Tawraat

Aayah Na Mafunzo:

Al-Baqarah

Sifa Za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Katika Tawraat

 

 

وَلَا تَلْبِسُوا الْحَقَّ بِالْبَاطِلِ وَتَكْتُمُوا الْحَقَّ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٤٢﴾

42. Na wala msichanganye haki kwa batili na mkaficha haki; na hali mnajua

 

Mafunzo:

Atwaa bin Yaasir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba: Nilikutana na ‘Abdullaah bin ‘Amr bin Al-‘Aasw (Radhwiya Allaahu ‘anhu)  nikasema: Nielezee sifa za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) zilizopo katika Tawraat. Akasema: Sawa. Wa-Allaahi hakika amesifiwa kwenye Tawraat kwa baadhi ya sifa katika Qur-aan. Ee Nabiy! Hakika Sisi Tumekutuma uwe shahidi na mbashiriaji na mwonyaji na ngao ya Waumini. Wewe ni mja na Rasuli Wangu. Na nikakuita mwenye kutawakkal. Yeye si mwenye maneno makali wala si msusuwavu, wala hazui ovu kwa ovu, wala halipizi uovu kwa uovu lakini anasamehe na kuachilia mbali. Na Allaah Hatomfisha mpaka asimamishe mila iliyojikunja kwa kusema: Laa ilaaha illa Allaah [hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah] na afungue kwayo macho yaliyopofuka, na masikio yasiyosikia, na nyoyo zilizofungwa. [Al-Bukhaariy (2125)]. 

 

Share

043-Aayah Na Mafunzo: Nguzo Tano Za Kiislamu Umuhimu Wa Swalaah Na Zakaah

Aayah Na Mafunzo

 

Al-Baqarah

 

Nguzo Tano Za Kiislamu Umuhimu Wa Swalaah Na Zakaah

 

 

 

وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَارْكَعُوا مَعَ الرَّاكِعِينَ ﴿٤٣﴾

43. Na simamisheni Swalaah na toeni Zakaah na rukuuni pamoja na wanaorukuu (katika utiifu).

 

Mafunzo:

 

Nguzo tano za Uislamu zimetajwa katika Hadiyth ifuatayo:

 

Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: amesema: “Uislamu umejengwa juu ya nguzo tano; Kushuhudia kwamba hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, na kwamba Muhammad ni Rasuli Wake, na kusimamisha Swalaah, na kutoa Zakaah, na kutekeleza Hajj, na kufunga Swiyaam Ramadhwaan.” [Al-Bukhaariy (8)]

 

Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amesisitiza mno katika Qur-aan nguzo mbili; Swalaah na kutoa Zakaah.

 

Miongoni mwa kusisitizwa Swalaah ni kwamba ni jambo la kwanza mja kuulizwa Siku ya Qiyaamah:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ َقَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ ((إِنَّ أَوَّلَ مَا يُحَاسَبُ بِهِ الْعَبْدُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مِنْ عَمَلِهِ صَلاتُهُ فَإِنْ صَلُحَتْ فَقَدْ أَفْلَحَ وَأَنْجَحَ وَإِنْ فَسَدَتْ فَقَدْ خَابَ وَخَسِرَ فَإِنْ انْتَقَصَ مِنْ فَرِيضَتِهِ شَيْءٌ قَالَ الرَّبُّ عَزَّ وَجَلَّ انْظُرُوا هَلْ لِعَبْدِي مِنْ تَطَوُّعٍ فَيُكَمَّلَ بِهَا مَا انْتَقَصَ مِنْ الْفَرِيضَةِ ثُمَّ يَكُونُ سَائِرُ عَمَلِهِ عَلَى ذَلِكَ)) الترمذي و أبوا داود والنسائي وابن ماجه وأحمد

Imepokelewa na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Kitu cha kwanza kinachohesabiwa katika ‘amali za mja wa Allaah Siku ya Qiyaamah ni Swalaah zake. Zikiwa zimetimia, hapo tena atakuwa kaneemeka na kafuzu, na zikiwa zina kasoro atakuwa kaanguka na kala khasara. Ikiwa pana upungufu katika Swalaah zake za fardhi Allaah (‘Azza wa Jalla) Atasema: “Tazama ikiwa mja wangu ana Swalaah zozote za Sunnah ambazo zinaweza kufidia zile zilizopungua, hapo tena ‘amali yake iliyobaki itaangaliwa hivyo hivyo)) [At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy, Ibn Maajah na Ahmad]

 

Na kuhusu Zakaah:

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayepewa mali kisha asitoe Zakaah yake, basi mali hiyo Siku ya Qiyaamah itageuzwa kuwa joka dume lenye upara, mwenye madoa mawili machoni (kutokana na wingi wa sumu aliyonayo), atajizungusha katika mwili wa mtu huyo, kisha atamkaba shingoni huku akimwambia: "Mimi ndiyo hazina yako uliyokuwa ukiikusanya, mimi ndiyo mali yako", kisha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaisoma Aayah hii:

 

وَلَا يَحْسَبَنَّ الَّذِينَ يَبْخَلُونَ بِمَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ هُوَ خَيْرًا لَّهُم ۖ بَلْ هُوَ شَرٌّ لَّهُمْ ۖ سَيُطَوَّقُونَ مَا بَخِلُوا بِهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ  

180. Wala wasidhani kabisa wale wanaofanya ubakhili kwa yale Aliyowapa Allaah katika fadhila Zake kwamba hayo ni kheri kwao, bali ni shari kwao. Watafungwa kongwa yale waliyoyafanyia ubakhili Siku ya Qiyaamah. [Aal ‘Imraan 180 – Hadiyth katika Al-Bukhaariy na Muslim]

Share

047-Aayah Na Mafunzo: Ummah Bora Ni Ummah Wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Ummah Bora Ni Ummah Wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

 

 

 يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَنِّي فَضَّلْتُكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٤٧﴾

47. Enyi wana wa Israaiyl! Kumbukeni neema Yangu Niliyokuneemesheni na hakika Mimi Nimekufadhilisheni juu ya walimwengu wote.

Mafunzo:

Kufadhilishwa kwa hao Baniy Israaiyl juu ya walimwengu wote; makusudio yake ni walimwengu wa zama zao kwani inafahamika kuwa ummah uliokuwa bora kuliko ummah zote ni ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa dalili ya kauli ya Allaah (Ta’aalaa): Mmekuwa ummah bora kabisa uliotolewa (mfano) kwa watu; mnaamrisha mema na mnakataza munkari na mnamwamini Allaah. Na lau wangeliamini Ahlul-Kitaabi ingelikuwa ni bora kwao, miongoni mwao wanaoamini na wengi wao ni mafasiki.” [Aal-‘Imraan (3: 110)]

 

 

 

Share

057-Aayah Na Mafunzo: Uyoga Ni Aina Ya Manna Ni Shifaa Ya Macho

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Uyoga Ni Aina Ya Manna Ni Shifaa Ya Macho

 

 

وَظَلَّلْنَا عَلَيْكُمُ الْغَمَامَ وَأَنزَلْنَا عَلَيْكُمُ الْمَنَّ وَالسَّلْوَىٰ ۖ كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ ۖ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿٥٧﴾ 

57. Na Tukakufunikeni kwa mawingu na Tukakuteremshieni Al-Manna na As-Salwaa. (Tukakwambieni): “Kuleni katika vizuri Tulivyokuruzukuni.” Hawakutudhulumu Sisi lakini walikuwa wakizidhulumu nafsi zao.

 

Mafunzo:

Faida: Sa’iyd bin Zayd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Al-Kama-ah (uyoga) ni aina ya  manna na maji yake ni shifaa (ponyo) ya macho.”  [Al-Bukhaariy (4478)]

 

Share

058-Aayah Na Mafunzo: Ubadilishaji Wa Maana Ya Hittwah: Tuondolee Uzito Wa Madhambi

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Ubadilishaji Wa Maana Ya Hittwah

 

 

وَإِذْ قُلْنَا ادْخُلُوا هَـٰذِهِ الْقَرْيَةَ فَكُلُوا مِنْهَا حَيْثُ شِئْتُمْ رَغَدًا وَادْخُلُوا الْبَابَ سُجَّدًا وَقُولُوا حِطَّةٌ نَّغْفِرْ لَكُمْ خَطَايَاكُمْ ۚ وَسَنَزِيدُ الْمُحْسِنِينَ ﴿٥٨﴾

58. Na pindi Tuliposema: “Ingieni mji huu (Quds) na kuleni humo maridhawa popote mpendapo, na ingieni katika mlango wake huku mmeinama kunyenyekea na semeni “Hittwah" (Tuondolee uzito wa madhambi); Tutakughufurieni makosa yenu na Tutawazidishia (thawabu) wafanyao ihsaan.

 

 

Mafunzo:

 

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Wana wa Israaiyl waliamrishwa kuingia kupitia mlangoni huku wainame na wanyenyekee na waseme ‘Hittwah’ (Tuondolee uzito wa madhambi). Lakini waliingia kinyumenyume wakipotosha maneno wakisema: Habbat fiy sha’rah (mbegu katika unywele).” [Al-Bukhaariy]

 

 

Share

065-Aayah Na Mafunzo: Maana Ya As-Sabt Na Mayahudi Kuvunja Shariy’ah Yake

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Maana Ya As-Sabt Na Mayahudi Kuvunja Shariy’ah Yake

 

 

وَلَقَدْ عَلِمْتُمُ الَّذِينَ اعْتَدَوْا مِنكُمْ فِي السَّبْتِ فَقُلْنَا لَهُمْ كُونُوا قِرَدَةً خَاسِئِينَ ﴿٦٥﴾

65. Na kwa yakini mlikwishawajua wale miongoni mwenu waliotaadi mipaka ya As-Sabt Tukawaambia: “Kuweni manyani waliobezwa.”

 

 

Mafunzo:

 

As-Sabt maana yake asili, ni mapumziko na hivyo Siku hiyo yao ya mapumziko (Jumamosi), Mayahudi waliwekewa shariy’ah wasivue samaki lakini walikhalifu amri kwa kutumia njama na ujanja wakavua samaki kumuasi Allaah, basi Allaah Akawaghadhibikia na kuwageuza manyani.

 

Share

066-Aayah Na Mafunzo: Kumuasi Allaah Katika Aliyoyaharamisha Kunastahiki Adhabu

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Kumuasi Allaah Katika Aliyoyaharamisha Kunastahiki Adhabu

 

 

فَجَعَلْنَاهَا نَكَالًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهَا وَمَا خَلْفَهَا وَمَوْعِظَةً لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٦٦﴾

66. Tukaifanya kuwa ni adhabu ya kuonya kwa waliokuweko zama zao na wataokuja baada yao na ni mawaidha kwa wenye taqwa.

 

Mafunzo:

 

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Msifanye makosa waliyoyafanya Mayahudi wakakiuka Aliyoyaharamisha Allaah kwa hila ndogo ndogo.” [Imaam Abuu ‘Abdillaah bin Batwwah; Irwaa Al-Ghaliyl (5/375) – Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

 

Share

067-Aayah Na Mafunzo: Kisa Cha Al-Baqarah (Ng’ombe)

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Kisa Cha Al-Baqarah (Ng’ombe)

 

 

وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تَذْبَحُوا بَقَرَةً ۖ قَالُوا أَتَتَّخِذُنَا هُزُوًا ۖ قَالَ أَعُوذُ بِاللَّـهِ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْجَاهِلِينَ ﴿٦٧﴾

67. Na pindi Muwsaa alipowaambia kaumu wake: “Hakika Allaah Anakuamuruni mchinje ng’ombe.” Wakasema: “Unatufanyia mzaha?” Akasema: “Najikinga kwa Allaah kuwa  miongoni mwa wajinga.”  

 

قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا هِيَ ۚ قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ لَّا فَارِضٌ وَلَا بِكْرٌ عَوَانٌ بَيْنَ ذَٰلِكَ ۖ فَافْعَلُوا مَا تُؤْمَرُونَ ﴿٦٨﴾

68. Wakasema: “Tuombee kwa Rabb wako Atubainishie ni ng’ombe wa aina gani huyo?” (Muwsaa) Akasema: “Hakika Yeye (Allaah) Anasema kwamba ng’ombe mwenyewe si mpevu wala si mchanga, bali ni wa katikati baina ya hao, basi fanyeni mnavyoamrishwa.”

 

قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا لَوْنُهَا ۚ قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ صَفْرَاءُ فَاقِعٌ لَّوْنُهَا تَسُرُّ النَّاظِرِينَ ﴿٦٩﴾

69. Wakasema: “Tuombee kwa Rabb wako Atubainishie rangi yake?” (Muwsaa) Akasema: “Hakika Yeye (Allaah) Anasema kwamba ni ng’ombe wa rangi ya njano iliyoiva mno, rangi yake huwapendeza wanaotazama.”

 

 قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا هِيَ إِنَّ الْبَقَرَ تَشَابَهَ عَلَيْنَا وَإِنَّا إِن شَاءَ اللَّـهُ لَمُهْتَدُونَ ﴿٧٠﴾

70. Wakasema: “Tuombee kwa Rabb wako Atubainishie ni ng’ombe wa aina gani huyo? Kwa hakika ng’ombe wametutatiza na hakika sisi In-Shaa-Allaah  tutakuwa wenye kuongoka.”

 

قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ لَّا ذَلُولٌ تُثِيرُ الْأَرْضَ وَلَا تَسْقِي الْحَرْثَ مُسَلَّمَةٌ لَّا شِيَةَ فِيهَا ۚ قَالُوا الْآنَ جِئْتَ بِالْحَقِّ ۚ فَذَبَحُوهَا وَمَا كَادُوا يَفْعَلُونَ ﴿٧١﴾

71. (Muwsaa) Akasema: ”Hakika Yeye (Allaah) Anasema kwamba ni ng’ombe ambaye hakutiishwa; kwa kulima ardhi wala kwa kumwagilia maji shamba; ni kamilifu hana dosari.” Wakasema: “Sasa umekuja na haki.” Basi wakamchinja na hawakuwa wenye kukaribia kufanya hivyo. 

 

وَإِذْ قَتَلْتُمْ نَفْسًا فَادَّارَأْتُمْ فِيهَا ۖ وَاللَّـهُ مُخْرِجٌ مَّا كُنتُمْ تَكْتُمُونَ ﴿٧٢﴾

72. Na pindi mlipoiua nafsi, kisha mkakhitilafiana kwayo, na Allaah ni Mwenye kutoa hayo mliyokuwa mkiyaficha.

 

فَقُلْنَا اضْرِبُوهُ بِبَعْضِهَا ۚ كَذَٰلِكَ يُحْيِي اللَّـهُ الْمَوْتَىٰ وَيُرِيكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿٧٣﴾

73. Tukasema: “Mpigeni (huyo maiti) kwa baadhi ya sehemu yake (huyo ng’ombe).” Hivyo ndivyo Allaah Anavyohuisha wafu na Anakuonyesheni Aayaat (miujiza, dalili) Zake huenda mkatia akilini.

 

 

Mafunzo:

 

Kuhusu Aayah (67- 73); kulikuweko na mtu aliyepooza (asiyekuwa wa kawaida) na alikuwa na mali nyingi. Hakuwa na mrithi isipokuwa jamaa yake mmoja. Mrithi huyo alimuua huyo bwana ili apate kurithi mali. Kisha akachukua mwili wake akautupa nje na nyumba ya mtu mmoja kumsingizia. Siku ya pili  akadai kulipiza kisasi, pakatokea mzozano na watu walikaribia kuuana. Mwishowe wakasema “Mnaye Rasuli wa Allaah mwendeeni.” Walipomwendea Nabiy Muwsaa akawaambia: “Hakika Allaah Anakuamuruni mchinje ng’ombe.” Wakafanya ugumu wa kutii amri hii kwa kubishana na wakazidi kufanyiwa ugumu kumtafuta ng’ombe mwenye sifa fulani. Wasingebishana basi ingewatosheleza kuchinja ng’ombe yoyote yule.  Ng’ombe mwenye sifa hizo akapatikana kwa mtu mmoja pekee naye akataka alipwe dhahabu iliyojaza ngozi ya ng’ombe. Wakamlipa na wakamchinja na kisha wakachukua sehemu ya ng’ombe kumpigia huyo mtu aliyeuliwa, akazindukana na wakamuuliza nani aliyemuua? Akamuashiria mrithi wake, basi hakuruhusiwa tena kumrithi. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]  

 

 

Share

081-Aayah Na Mafunzo: Madhambi Madogo Yanajikusanya Mpaka Yanaangamiza

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Madhambi Madogo Yanajikusanya Mpaka Yanaangamiza

 

 

 

بَلَىٰ مَن كَسَبَ سَيِّئَةً وَأَحَاطَتْ بِهِ خَطِيئَتُهُ فَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٨١﴾

81. Ndio! Yeyote aliyechuma uovu na yakamzunguka kwayo makosa yake; basi hao ni watu wa motoni, wao humo ni wenye kudumu.

 

 

Mafunzo:

 

Abdullaah bin Mas‘uwd  (Radhiwya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Tahadharini na madhambi madogo, kwa sababu yanajikusanya kwa mtu mpaka yanamuangamiza.” Kisha akapiga mfano: “Kama vile mfano wa watu waliopiga kambi katika ardhi tambarare kisha wakaja watumishi wao, mmoja wao akakusanya kuni na mwengine akakusanya kuni mpaka zikawa nyingi za kutosha kisha wakakoka moto na wakapika walivyovitia humo.” [Musnad Ahmad (5/312); Swahiyh Al-Jaami’ (2687)]

 

 

 

 

Share

083-Aayah Na Mafunzo: ‘Amali Bora Kabisa Kuswali Kwa Wakati Wake Kuwafanyia Wema...

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

‘Amali Bora Kabisa Kuswali Kwa Wakati Wake Kuwafanyia Wema Wazazi Na Jihaad

 

 

 

وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَ بَنِي إِسْرَائِيلَ لَا تَعْبُدُونَ إِلَّا اللَّـهَ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَقُولُوا لِلنَّاسِ حُسْنًا وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ ثُمَّ تَوَلَّيْتُمْ إِلَّا قَلِيلًا مِّنكُمْ وَأَنتُم مُّعْرِضُونَ ﴿٨٣﴾ 

83. Na pindi Tulipochukua fungamano ya wana wa Israaiyl (Tukawaambia): “Msiabudu isipokuwa Allaah; na muwafanyie ihsaan wazazi wawili, na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini; na semeni na watu kwa uzuri na simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah;” kisha mkakengeuka ila wachache miongoni mwenu na hali nyinyi mnapuuza.

 

 

Mafunzo:

 

Ibn Mas‘uwd  (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba: Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah, ‘amali gani bora kabisa?  Akasema: “Kuswali kwa wakati wake.”  Nikasema: Kisha ipi? Akasema: “Kuwatendea wema wazazi wawili” Nikasema: Kisha ipi? Akasema: “Jihaad katika njia ya Allaah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share

087-Aayah Na Mafunzo: Uthibitisho Kuwa Ruwhul-Qudus Ni Jibriyl ('Alayhis-Salaam)

Aayah Na Mafunzo

 

Al-Baqarah

 

Uthibitisho Kuwa Ruwhul-Qudus Ni Jibriyl ('Alayhis-Salaam)

 

 Alhidaaya.com

 

وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَقَفَّيْنَا مِن بَعْدِهِ بِالرُّسُلِ ۖ وَآتَيْنَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ وَأَيَّدْنَاهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ ۗ أَفَكُلَّمَا جَاءَكُمْ رَسُولٌ بِمَا لَا تَهْوَىٰ أَنفُسُكُمُ اسْتَكْبَرْتُمْ فَفَرِيقًا كَذَّبْتُمْ وَفَرِيقًا تَقْتُلُونَ ﴿٨٧﴾

87. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa Kitabu na Tukafuatisha Rusuli baada yake. Na Tukampa ‘Iysaa mwana wa Maryam hoja bayana na Tukamtia nguvu kwa Ruwhil-Qudus (Jibriyl (عليه السلام. Je, basi kila anapokujieni Rasuli kwa yale yasiyoyapenda nafsi zenu, mlitakabari; basi kundi mlilikadhibisha na kundi mnaliua.

 

Mafunzo:

 

Uthibitisho kwamba Jibriyl (‘Alayhis-salaam) ni Ruwh Al-Qudus: ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amehadithia kwamba: Rasuli wa Allaah alijenga minbar ndani ya Masjid ambapo Hasan bin Thaabit (mshairi maarufu) alikuwa akimtetea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) (kwa mashairi yake). Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Yaa Allaah! Msaidie Hasan kwa Ruwh Al-Qudus kama alivyomlinda Rasuli Wako.” [Al-Bukhaariy]

 

Pia, Ibn Mas‘uwd  (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Ruwh Al-Qudus alinifahamisha kuwa hakuna roho itakayokufa mpaka imalizike rizki yake na muda wake, kwa hiyo mcheni Allaah na mtakeni rizki katika hali iliyo bora.” [As-Sunnah: (14/304), ameisahihisha Al-Albaaniy katika Mushkilat Al-Faqar (15), Swahiyh Al-Jaami’ (2085) Hadiyth kutoka Abuu Umaamah Al-Baahiliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu)]

 

 

Share

102-Aayah Na Mafunzo: Atakayemwendea Mchawi Amekufuru

 

 

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Atakayemwendea Mchawi Amekufuru

 

 

 

وَاتَّبَعُوا مَا تَتْلُو الشَّيَاطِينُ عَلَىٰ مُلْكِ سُلَيْمَانَ ۖ وَمَا كَفَرَ سُلَيْمَانُ وَلَـٰكِنَّ الشَّيَاطِينَ كَفَرُوا يُعَلِّمُونَ النَّاسَ السِّحْرَ وَمَا أُنزِلَ عَلَى الْمَلَكَيْنِ بِبَابِلَ هَارُوتَ وَمَارُوتَ ۚ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَا إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْ ۖ فَيَتَعَلَّمُونَ مِنْهُمَا مَا يُفَرِّقُونَ بِهِ بَيْنَ الْمَرْءِ وَزَوْجِهِ ۚ وَمَا هُم بِضَارِّينَ بِهِ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَيَتَعَلَّمُونَ مَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ ۚ وَلَقَدْ عَلِمُوا لَمَنِ اشْتَرَاهُ مَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ ۚ وَلَبِئْسَ مَا شَرَوْا بِهِ أَنفُسَهُمْ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿١٠٢﴾

102. Na wakafuata yale waliyoyasoma mashaytwaan juu ya ufalme wa Sulaymaan; na Sulaymaan hakukufuru lakini mashaytwaan ndio waliokufuru; wanafundisha watu sihiri na yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili katika (mji wa) Baabil; Haaruwt na Maaruwt. Nao wawili hawamfundishi yeyote mpaka waseme: “Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru.” Kisha wakajifunza kutoka kwa hao wawili yenye kupelekea kufarikisha kwayo baina ya mtu na mkewe. Na wao hawawezi kamwe kumdhuru yeyote kwayo isipokuwa kwa idhini ya Allaah; na wanajifunza yanayowadhuru na wala hayawanufaishi; na kwa yakini walijua kwamba atakayechuma haya hatopata katika Aakhirah fungu lolote, na ni ubaya ulioje walichojiuzia nafsi zao, lau wangelikuwa wanajua.

 

Mafunzo:

 

Uharamisho wa kufanya sihri dalili ni Hadiyth: “Atakayemuendea mtabiri au mchawi akasadiki asemayo, atakuwa amekufuru aliyoteremshiwa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).” [Tafsiyr Ibn Kathiyr; Hadiyth ina isnaad ya upokezi Swahiyh na kuna Hadiyth zinazokubaliana na hii] 

 

Na Sihri ni katika madhambi saba yanayoangamiza:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((اجْتَنِبُوا السَّبْعَ الْمُوبِقَاتِ)) قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ وَمَا هُنَّ؟  قَالَ: ((الشِّرْكُ بِاللَّهِ وَالسِّحْرُ وَقَتْلُ النَّفْسِ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلاَّ بِالْحَقِّ وَأَكْلُ الرِّبَا وَأَكْلُ مَالِ الْيَتِيمِ وَالتَّوَلِّي يَوْمَ الزَّحْفِ وَقَذْفُ الْمُحْصَنَاتِ الْمُؤْمِنَاتِ الْغَافلاَتِ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Jiepusheni na mambo saba yanayoangamiza!)) Wakauliza: Ni yepi hayo yaa Rasuwla Allaah? Akawaambia: ((Ni kumshirikisha Allaah, sihri [uchawi], kuua nafsi Aliyoiharamisha Allaah isipokuwa kwa haki, kula ribaa, kula mali ya yatima, kukimbia wakati wa kupambana na adui na kuwatuhumu uzinifu wanawake Waumini waliohifadhika walioghafilika)). [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Share

116-Aayah Na Mafunzo: Kumsingizia Allaah Subhanaahu Wa Ta’aalaa Kuwa Ana Mwana Ni Kumshutumu Allaah

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Kumsingizia Allaah Subhanaahu Wa Ta’aalaa Kuwa Ana Mwana Ni Kumshutumu Allaah

 

 

وَقَالُوا اتَّخَذَ اللَّـهُ وَلَدًا ۗ سُبْحَانَهُ ۖ بَل لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ كُلٌّ لَّهُ قَانِتُونَ ﴿١١٦﴾

116. Na wakasema: “Allaah Amejichukulia mwana.” Subhaanah! Utakasifu ni Wake. Bali ni Vyake vilivyomo mbinguni na ardhini, vyote vinamtii.

 

 

Mafunzo:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: (قَالَ اللَّهُ: كَذَّبَنِي ابْنُ آدَمَ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ ذَلِكَ، وَشَتَمَنِي وَلَمْ يَكُنْ لَهُ ذَلِكَ، أَمَّا تَكْذِيبُهُ إِيَّاىَ أَنْ يَقُولَ إِنِّي لَنْ أُعِيدَهُ كَمَا بَدَأْتُهُ، وَأَمَّا شَتْمُهُ إِيَّاىَ أَنْ يَقُولَ اتَّخَذَ اللَّهُ وَلَدًا، وَأَنَا الصَّمَدُ الَّذِي لَمْ أَلِدْ وَلَمْ أُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لِي كُفُؤًا أَحَدٌ))

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah  (رضي الله عنهما)amesema:  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: “Allaah Amesema: Mwana Aadam amenikadhibisha, wala hapaswi hilo! Na amenishutumu mja wangu na wala hapaswi hilo! Ama kunikadhibisha kwake, amedai kuwa Sitoweza kumrudisha (kumfufua) kama alivyokuwa. Ama kunishutumu, ni kudai kuwa Nina mwana na ilhali   Mimi ni Asw-Swamad (Aliyekamilika sifa za utukufu Wake, Mkusudiwa haja zote) Ambaye Sikuzaa wala Sikuzaliwa na hakuna chochote kinachofanana na kulingana Nami.”   [Al-Bukhaariy]

 

 

Share

120-Aayah Na Mafunzo: Tahadharisho La Kuwaiga Makafiri

Aayah Na Mafunzo

 

Al-Baqarah

 

Tahadharisho La Kuwaiga Makafiri

 

 

 

وَلَن تَرْضَىٰ عَنكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ ۗ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّـهِ هُوَ الْهُدَىٰ ۗ وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُم بَعْدَ الَّذِي جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ ۙ مَا لَكَ مِنَ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ ﴿١٢٠﴾

120. Na hawatoridhika nawe Mayahudi wala Manaswara mpaka ufuate mila zao. Sema: “Hakika mwongozo wa Allaah ndio mwongozo (pekee).” Na ukifuata hawaa zao baada ya yale ambayo yaliyokujia katika elimu, basi hutopata kutoka kwa Allaah mlinzi yeyote wala mwenye kunusuru.

 

Mafunzo:

 

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameonya kuwafuata Mayahudi na Manaswara katika Hadiyth:

 

خَالِفُوا الْمُشْرِكِينَ أَحْفُوا الشَّوَارِبَ وَأَوْفُوا اللِّحَى

“Kuweni kinyume na washirikina, punguzeni masharubu na fugeni ndevu.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Na pia:

 

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((لَتَتَّبِعُنَّ سَنَنَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ شِبْرًا بِشِبْرٍ وَذِرَاعًا بِذِرَاعٍ حَتَّى لَوْ دَخَلُوا فِي جُحْرِ ضَبٍّ لاَتَّبَعْتُمُوهُمْ)) ‏ قُلْنَا يَا رَسُولَ اللَّهِ آلْيَهُودَ وَالنَّصَارَى؟ قَالَ: ((‏فَمَنْ؟))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Sa’iyd Alkhudriyy (رضي الله عنه) ambaye amesema:  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mtafuata nyendo za wale waliokuja kabla yenu hatua kwa hatua mpaka itafika wakiingia katika shimo la kenge, na nyinyi mtaingia pia.” (Maswahaba) wakasema: Ee Rasuli wa Allaah, je, unamaanisha Mayahudi na Manaswara?  Akasema: “Hivyo nani basi mwengine?” [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

Pia amesema Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

مَنْ تَشَبَّهَ بِقَوْمٍ فَهُوَ مِنْهُمْ

 “Anayejishabihisha na watu, basi naye ni miongoni mwao.” [Ahmad, Swahiyh Abiy Daawuwd (4031), na wengineo]

 

Share

121-ِِِAayah Na Mafunzo: Maana Ya Kuisoma Qur-aan Ipasavyo Kusomwa

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Maana Ya Kuisoma Qur-aan Ipasavyo Kusomwa

 

 

الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَتْلُونَهُ حَقَّ تِلَاوَتِهِ أُولَـٰئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۗ وَمَن يَكْفُرْ بِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿١٢١﴾

121. Wale Tuliowapa Kitabu wanakisoma kwa haki ipasavyo ya kusomwa kwake; hao ndio wanaokiamini, na atakayekikanusha basi hao ndio waliokhasirika.

 

 

Mafunzo:

 

 

Maana ya “kuisoma haki ipasavyo kusomwa”: ‘Umar bin Al-Khattwaab (رضي الله عنه) amesema: “Anapopita mtu panapotajwa Jannah, anamuomba Allaah Jannah, na anapopita panapotajwa moto anajikinga nao kwa Allaah.” 

 

Na Hudhayfah bin Al-Yamaan amehadithia kuhusu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba alipokuwa akiswali, pale anapopita Aayah ya rahmah aliomba rahmah, anapopita Aayah ya adhabu anajikinga nayo, anapopita Aayah ya kumsabihi Allaah anamsabihi (kumtukza) [Swahiyh Ibn Maajah (1119)]

 

Ibn Mas‘uwd (رضي الله عنه) amesema maana yake ni: “Anahalalisha Aliyohalalisha Allaah, na Anaharamisha Aliyoyaharamisha Allaah na anasoma kama Alivyoteremsha Allaah wala hapotoshi maneno sehemu zake wala hafanyii taawiyl lolote humo isiyokuwa taawiyl yake.” (Taawiyl: kukwepesha maana yake ya kihakika kwa kuipa maana ndogo au tofauti, ishara ambayo ni tofauti na maana ya juu; ni kukanusha maana).

 

Na Al-Hasan Al-Baswriy amesema: “Wanaifanyia kazi shariy’ah (hukmu) zake na wanaamini mutashaabih zake (mutashaabih: zilizofanana) na wanapeleka yanayowatatiza kufahamu kwa ‘Ulamaa wake.”

 
Pia, baadhi ya ‘Ulamaa wamesema kuwa: Ni kuisoma kwa hukmu zake za tajwiyd, kufahamu maana yake, kuifanyia kazi maamrisho yake, kujiepusha makatazo yake, kujifundisha na kuifundisha. Hali kadhaalika kusabbih kila panapotajwa Tasbiyh, kumtukuza Allaah (عزّ وجلّ), kuomba Rahmah, kuomba maghfirah, kuomba kuingizwa Jannah (Peponi) na kuomba kinga ya Moto kila panapotajwa hayo.

 

 

 

Share

135-Aayah Na Mafunzo: Dini Ya Nabiy Ibraahiym Ndio Dini Ya Kiislamu

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Dini Ya Nabiy Ibraahiym Ndio Dini Ya Kiislamu

 

 

 

وَقَالُوا كُونُوا هُودًا أَوْ نَصَارَىٰ تَهْتَدُوا ۗ قُلْ بَلْ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۖ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٣٥﴾

135. Na wakasema: “Kuweni Mayahudi au Manaswara mtaongoka.” Sema:  “Bali (tunafuata) mila ya Ibraahiym aliyeelemea haki na wala hakuwa katika washirikina.” [Al-Baqarah: 135]

 

 

Mafunzo:

 

Amesimulia Ibn Umar (رضي الله عنهما) kwamba: Zayd bin ‘Amr bin Nufayl, alitoka kuelekea Sham, akiulizia kuhusu dini ili aifuate. Akakutana na mwanazuoni wa ki-Yahudi, akamuuliza kuhusu dini na akasema: Mimi huenda nikaingia dini yenu, basi nielezee. Akasema: Huwezi kuwa katika dini yetu mpaka uchukue fungu lako katika ghadhabu za Allaah. Akasema Zayd: Mimi hakuna ninachokikimbia ila ghadhabu za Allaah, wala sivumilii ghadhabu za Allaah kwa kitu chochote, na vipi nitaweza! Je, utanielekeza (dini) nyingine? Akasema (mwanachuoni wa ki-Yahudi): Sijui ila Dini iliyotakasika, akasema Zayd: Ni (dini) ipi hiyo iliyotakasia? Akasema: Dini ya Ibraahiym, hakuwa Myahudi wala Mnaswara, wala haabudu ila Allaah. Akatoka Zayd akakutana na mwanazuoni wa ki-Naswara, akamuuliza kama vile (alivyomuuliza Myahudi), akasema: Huwezi kuwa katika dini yetu mpaka uchukue fungu lako katika laana za Allaah. Akasema: Mimi hakuna nnachokimbia ila nakimbia laana za Allaah, wala sivumilii laana za Allaah wala ghadhabu zake kwa chochote, na vipi nitaweza! Je, utanielekeza (dini) nyingine? Akasema: sijui ila (Dini) iliyotakasika. Akasema: Ni ipi hiyo (Dini) iliyotakasika? Akasema: Dini ya Ibraahiym, hakuwa Myahudi wala Mnaswara wala haabudu ila Allaah. Basi Zayd alipoona maneno yao kuhusu Ibraahiym  (عليه السلام)  aliondoka sehemu hiyo, na alipokuwa nje aliinua mikono yake akasema; “Ee Allaah mimi nashuhudia niko katika Dini ya Ibraahiym.” [Al-Bukhaariy (3827)]

 

Share

142-Aayah Na Mafunzo: Ahlul-Kitaab Wanatuhusudu Kwa Siku Ya Ijumaa Na Qiblah Chetu

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Ahlul-Kitaab Wanatuhusudu Juu Ya Siku Ya Ijumaa Na Qiblah Chetu

 

 

 

سَيَقُولُ السُّفَهَاءُ مِنَ النَّاسِ مَا وَلَّاهُمْ عَن قِبْلَتِهِمُ الَّتِي كَانُوا عَلَيْهَا ۚ قُل لِّلَّـهِ الْمَشْرِقُ وَالْمَغْرِبُ ۚ يَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿١٤٢﴾

142. Watasema wapumbavu miongoni mwa watu: “Nini kilichowageuza kutoka Qiblah chao ambacho walikuwa wakikielekea!” Sema: “Mashariki na Magharibi ni ya Allaah, Anamwongoza Amtakaye kuelekea njia iliyonyooka.”

 

Mafunzo:

 

 

Amehadithia ‘Aaishah (رضي الله عنها) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alizungumzia juu Ahlul-Kitaab akasema: “Hawatuhusudu juu ya kitu kama wanavyotuhusudu juu ya Siku ya Ijumaa ambayo Allaah Ametupa hidaaya na wao wakapotoshwa kutokana nayo. Na kwa Qiblah ambacho Allaah Ametuongoza kwacho na wao walipotoshwa kutokana nacho, na kwa kauli yetu ya ‘Aamiyn’ ya Imaam.” [Ahmad (6/134)].

 

 

Share

143-Aayah Na Mafunzo: Ummah Bora Na Adilifu Ni Ummah Wa Kiislamu

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Ummah Bora Na Adilifu Ni Ummah Wa Kiislamu  

 

 

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا ۗ وَمَا جَعَلْنَا الْقِبْلَةَ الَّتِي كُنتَ عَلَيْهَا إِلَّا لِنَعْلَمَ مَن يَتَّبِعُ الرَّسُولَ مِمَّن يَنقَلِبُ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ ۚ وَإِن كَانَتْ لَكَبِيرَةً إِلَّا عَلَى الَّذِينَ هَدَى اللَّـهُ ۗ وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُضِيعَ إِيمَانَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِالنَّاسِ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿١٤٣﴾

143. Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah bora na adilifu ili muwe mashahidi juu ya watu na awe Rasuli shahidi juu yenu. Na Hatukukifanya Qiblah ambacho ulikuwa ukikielekea (Baytul-Maqdis) isipokuwa Tupate kumpambanulisha yule anayemfuata Rasuli miongoni mwa mwenye kugeuka akarudi nyuma. Na hakika ilikuwa ni jambo gumu isipokuwa kwa wale ambao Allaah Amewaongoza. Na Allaah Hakuwa Mwenye kupoteza iymaan yenu (Swalaah), hakika Allaah kwa watu, bila shaka ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu.

 

 

Mafunzo:

 

Masjid hiyo waliyoswali Swahaba wakageuza Qiblah chao kuelekeza Al-Ka’bah wakiwa ndani ya Swalaah, ndio inayojulikana kama Masjd Al-Qiblatayni (Msikiti wa Qiblah mbili) Yaani; kuelekea kwao ndani ya Swalaah moja, kwanza Baytul-Maqdis (Palestina) kisha kuelekea kwao Al-Ka’bah baada ya kuteremshwa Aayah hii ya 143 Al-Baqarah.

 

Kuhusu kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah bora na adilifu ili muwe mashahidi juu ya watu na awe Rasuli shahidi juu yenu”, Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ataitwa Nuwh Siku ya Qiyaamah ataulizwa: Je, umebalighisha ujumbe? Atasema: Naam. Wataitwa watu wake wataulizwa: Je, alikufikishieni ujumbe? Watasema: Hakutujia mwonyaji wala hakuna aliyetumwa kwetu. Ataulizwa Nuwh: Nani mwenye kukushuhudia hayo? Atasema: Muhammad na Ummah wake.  Akasema: Hiyo ndio maana kauli Yake: “Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah bora na adilifu ili muwe mashahidi juu ya watu na awe Rasuli shahidi juu yenu.” Akasema: “Waswatwaa, maana yake ni uadilifu basi mtatoa ushahidi (kuhusu Nuwh) kubalighisha ujumbe na kisha nitakuwa shahidi wenu.”  [Ahmad (3/32) na Al-Bukhaariy pia kama hivyo (4487)]

 

 

Share

152-Aayah Na Mafunzo: Ukimdhukuru Allaah Naye Atakukumbuka

 

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

 Ukimdhukuru Allaah Naye Atakukumbuka

 

 

فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ وَاشْكُرُوا لِي وَلَا تَكْفُرُونِ﴿١٥٢﴾

152. Basi nidhukuruni na Mimi Nitakukumbukeni; na nishukuruni wala msinikufuru.

 

 

Mafunzo:

 

Fadhila za kumdhukuru Allaah ni nyingi mno, miongoni mwazo ni: 

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ (( يَقُولُ اللَّهُ تَعَالَى: أَنَا عِنْدَ ظَنِّ عَبْدِي بِي وَأَنَا مَعَهُ إِذَا ذَكَرَنِي، فَإِنْ ذَكَرَنِي فِي نَفْسِهِ ذَكَرْتُهُ فِي نَفْسِي، وَإِنْ ذَكَرَنِي فِي مَلَإٍ ذَكَرْتُهُ فِي مَلَإٍ خَيْرٍ مِنْهُمْ، وَإِنْ تَقَرَّبَ إِلَيَّ بِشِبْرٍ تَقَرَّبْتُ إِلَيْهِ ذِرَاعًا، وَإِنْ تَقَرَّبَ إِلَيَّ ذِرَاعًا تَقَرَّبْتُ إِلَيْهِ بَاعًا، وَإِنْ أَتَانِي يَمْشِي أَتَيْتُهُ هَرْوَلَةً)) البخاري، مسلم، الترمذي و ابن ماجه

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema, ((Allaah Ta’aalaa, Anasema: Mimi ni vile mja Wangu anavyonidhania. Niko pamoja naye Anaponikumbuka katika nafsi yake, Ninamkumbuka  katika nafsi Yangu, anaponikumbuka katika hadhara, Ninamkumbuka katika hadhara bora zaidi. Na anaponikaribia shibiri Ninamkaribia dhiraa; anaponikaribia dhiraa, Ninamkaribia pima, anaponijia kwa mwendo (wa kawaida) ninamwendea mbio)) [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na Ibn Maajah]

 

 

 

Na pia amesema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): 

 

((أَلَا أُنَبِّئُكُمْ بِخَيْرِ أَعْمَالِكُمْ وَأَزْكَاهَا عِنْدَ مَلِيكِكُمْ وَأَرْفَعِهَا فِي دَرَجَاتِكُمْ وَخَيْرٌ لَكُمْ مِنْ إِنْفَاقِ الذَّهَبِ وَالْوَرِقِ وَخَيْرٌ لَكُمْ مِنْ أَنْ تَلْقَوْا عَدُوَّكُمْ فَتَضْرِبُوا أَعْنَاقَهُمْ وَيَضْرِبُوا أَعْنَاقَكُمْ؟)) قَالُوا: بَلَى. قَالَ: ((ذِكْرُ اللَّهِ تَعَالَى)).

 

((Hivi niwaambieni khabari ya matendo yenu bora, na ambayo ni masafi mno, mbele ya Mola wenu, na ambayo ni ya juu mno katika daraja zenu, na ambayo ni bora kwenu kuliko kutoa dhahabu na fedha, na ambayo ni bora kuliko kukutana na adui zenu, mkawapiga shingo zao, nao wakakupigeni shingo zenu?)) Wakasema: [Maswahaba]: Ndio. Akasema: ((Ni kumdhukuru Allaah Ta’aalaa)) [ Hadiyth ya ‘Abu Dardaa ‘Uwaymir bin ‘Aamir (رضي الله عنه) - At-Tirmidhiy (5/459) [3377], Ibn Maajah (2/1246) [3790], na angalia Swahiyh Ibn Maajah (2/316) na Swahiyh At-Tirmidhiy (3/139)]

 

Share

153-Aayah Na Mafunzo: Kuomba Msaada Kwa Subira Na Swalaah

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Kuomba Msaada Kwa Subira Na Swalaah

 

 

  

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الصَّابِرِينَ ﴿١٥٣﴾

153. Enyi walioamini! Tafuteni msaada kwa subira na Swalaah; hakika Allaah Yu pamoja na wanaosubiri.

 

 

Mafunzo:

 

Miongoni mwa fadhila za subira na Swalaah: Swuhayb bin Sinaan (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ajabu ya jambo la Muumin kwamba kila jambo lake ni kheri. Na halipatikani hili isipokuwa kwa Muumin. Anapofikwa na jambo zuri hushukuru nayo ni kheri kwake na anapofikwa na jambo lenye madhara husubiri nayo ni kheri kwake.” [Muslim: (2999)]

 

Pia, Abuu Faraas Rabiy'ah bin Ka'ab Al-Aslamiy (رضي الله عنه) ambaye alikuwa mtumishi wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amehadithia: Nililala na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) usiku mmoja nikamletea maji ya kutawadha, akaniambia: “Omba utakacho!” Nikasema: Nataka kuandamana na wewe Jannah! Akasema: “Hutaki lolote lingine?” Nikasema: Ni hilo tu. Akasema: “Basi nisaidie (ili hilo liwezekane) kwa kuzidisha kusujudu (Kuswali).” [Muslim] 

 

 

Share

155-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Dhikru Ya Istirjaa'

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Fadhila Za Dhikru Ya Istirjaa’

(Hakika sisi ni wa Allaah, na hakika sisi Kwake wenye kurejea)

 

www.alhidaaya.com

 

 

وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ ۗ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ ﴿١٥٥﴾

155. Na bila shaka Tutakujaribuni kwa kitu katika khofu na njaa na upungufu wa mali na nafsi na mazao. Na wabashirie wenye kusubiri.

 

الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّـهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ﴿١٥٦﴾

156. Wale ambao unapowafika msiba husema: “Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea.”

 

أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ ﴿١٥٧﴾

 

Mafunzo:

 

Muislamu apatapo msiba au janga lolote lile ikiwa ni kufiwa, maradhi, kupata khasara katika mali, mateso, maafa ya aina yoyote n.k. basi hapo hapo aombe du’aa hii:

 

إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ, اللَّهُمَّ أْجُرْنِي فِي مُصِيبَتِي وَأَخْلِفْ لِي خَيْرًا مِنْهَا

 

 

Dalili ni Hadiyth ya Ummuu Salamaah (رضي الله عنها) ambaye amehadithia:  Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Hakuna Muislamu anayefikwa na msiba akasema Alivyoamrishwa na Allaah: (Hakika sisi ni wa Allaah, na hakika sisi Kwake wenye kurejea, ee Allaah, nilipe kwa msiba wangu na nipe badala yake kilicho bora kuliko huo [msiba]), basi hakuna ila Allaah Atampa kilicho bora kuliko (msiba huo).” Abuu Salamah alipofariki nilisema: Muislamu gani ni bora kuliko Abuu Salamah ambaye familia yake ilikuwa ya kwanza kuhajiri kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)?. Kisha nikasema (du’aa hiyo) na Allaah Akanipa Rasulu-Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) badala yake…. [Muslim (910)]

 

 

Share

163-Aayah Na Mafunzo: Aayah Mojawapo Yenye Jina Adhimu Kabisa La Allaah

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Aayah Mojawapo Yenye Jina Adhimu Kabisa La Allaah

 

www.alhidaaya.com

 

 

وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿١٦٣﴾

163.  Na Ilaah wenu (Allaah) ni Ilaah Mmoja, hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu.

 

 

Mafunzo:

 

عَنْ أَسْمَاءَ بِنْتِ يَزِيدَ (رضي الله عنها) أَنَّ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((اسْمُ اللَّهِ الأَعْظَمُ فِي هَاتَيْنِ الأَيَتَيْنِ ((وَإِلَهُكُمْ إِلَهٌ وَاحِدٌ لاَ إِلَهَ إلاَّ هُوَ الرَّحْمَنُ الرَّحِيمُ)) وَفَاتِحَةِ آلِ عِمْرَانَ ((الم اللَّهُ لاَ إِلَهَ إلاَّ هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّوم))

 

Kutoka kwa Asmaa bint Yaziyd  (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Jina Adhimu kabisa la Allaah limo katika Aayah zifuatazo: “Na Ilaah wenu (Allaah) ni Ilaah Mmoja, hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Mwingi wa rahmah, Mwenye kurehemu.” (Al-Baqarah: 163) na na ufunguo (mwanzo) wa ‘Aal-‘Imraan: “Alif Laam Allaah, hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Aliyehai daima, Msimamia kila kitu (Aal-‘Imraan: 1-2) [Swahiyh At-Tirmidhiy (3478), Swahiyh Ibn Majaah (3123),  Swahiyh Al-Jaami’ (980),  Swahiyh Abiy Daawuwd (1496) Swahiyh At-Targhiyb (1642)]

 

 

Share

165-Aayah Na Mafunzo: Allaah Na Rasuli Wake Wanastahiki Kupendwa Kuliko Yeyote Yule

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Allaah Na Rasuli Wake Wanastahiki Kupendwa Kuliko Yeyote Yule

 

 www.alhidaaya.com

 

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّـهِ ۗ وَلَوْ يَرَى الَّذِينَ ظَلَمُوا إِذْ يَرَوْنَ الْعَذَابَ أَنَّ الْقُوَّةَ لِلَّـهِ جَمِيعًا وَأَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعَذَابِ ﴿١٦٥﴾

165. Na miongoni mwa watu wako wenye kuchukua asiyekuwa Allaah na kuwafanya kuwa ni wanaolingana (na Allaah) wanawapenda kama kumpenda Allaah. Na wale walioamini wana mapenzi zaidi kwa Allaah. Na lau wangelitambua wale waliodhulumu watakapoona adhabu kwamba nguvu zote ni za Allaah; na kwamba hakika Allaah ni Mkali wa kuadhibu.

 

 

Mafunzo:

 

وَلَهُمَا عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((ثَلاثٌ مَنْ كُنَّ فِيهِ وَجَدَ بِهِنَّ حَلاوَةَ الإِيمَانِ: أَنْ يَكُونَ اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَحَبَّ إِلَيْهِ مِمَّا سِوَاهُمَا، وَأَنْ يُحِبَّ الْمَرْءَ لاَ يُحِبُّهُ إِلاَّ لِلَّهِ، وَأَنْ يَكْرَهَ أَنْ يَعُودَ فِي الْكُفْرِ بَعْدَ إِذْ أَنْقَذَهُ اللَّهُ مِنْهُ  كَمَا يَكْرَهُ أَن ْيُقْذَفَ فِي النَّار))

Nao Al-Bukhaariy na Muslim wamerekodi Hadiyth kutoka kwake Anas(رضي الله عنه)  amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Mambo matatu atakayekuwa nayo, atapata utamu wa Iymaan: Allaah na Rasuli Wake wawe vipenzi zaidi kwake kuliko wengineo, ampende mtu na wala asimpende isipokuwa kwa ajili ya Allaah, na achukie kurudi katika ukafiri baada ya Allaah kumwokoa kutoka huko kama anavyochukia kuingizwa motoni)) [Al-Bukhaariy na Muslim]  

 

 

Share

172-Aayah Na Mafunzo: Du’aa Ya Mwenye Kula Haraam Haikubalilwi

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Du’aa Ya Mwenye Kula Haraam Haikubalilwi

 

www.alhidaaya.com

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ وَاشْكُرُوا لِلَّـهِ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ ﴿١٧٢﴾

172. Enyi walioamini! Kuleni vizuri Tulivyokuruzukuni na mshukuruni Allaah mkiwa mnamwabudu Yeye Pekee.

Mafunzo:

 

 

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Enyi watu! Hakika Allaah ni Mzuri na Hapokei ila kilicho kizuri. Na Allaah Amewaamrisha Waumini kama Alivyowaamrisha Rasuli Anaposema: “Enyi Rusuli! Kuleni katika vizuri na tendeni mema, hakika Mimi kwa yale myatendayo ni Mjuzi.” [Al-Muuminuwn (23: 51)] Na Anasema: “Enyi walioamini! Kuleni vizuri Tulivyokuruzukuni.” Kisha akataja kisa cha mtu aliyekuwa safarini akiwa katika hali ya uchafu na mavumbi akiinua mikono yake mbinguni akiomba: Eee Rabb! Ee Rabb! Na hali chakula chake ni haramu, kinywaji chake ni haramu na kajengeka mwili wake kwa haramu vipi atakubaliwa du'aa yake?’ [Muslim]   

 

Share

185-Aayah Na Mafunzo: Mwezi Wa Ramadhwaan Ni Mwezi Wa Qur-aan

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Mwezi Wa Ramadhwaan Ni Mwezi Wa Qur-aan

 

 www.alhidaaya.com

 

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ۖ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۗ يُرِيدُ اللَّـهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّـهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿١٨٥﴾

Mwezi wa Ramadhwaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe mwongozo kwa watu na hoja bayana za mwongozo na pambanuo (la haki na batili). Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi na afunge. Na atakayekuwa mgonjwa au safarini, basi (inapaswa kulipa) idadi sawa katika masiku mengineyo. Allaah Anakutakieni mepesi na wala Hakutakieni magumu; na ili mkamilishe idadi na ili mumkabbir Allaah kwa kuwa Amekuongozeni na ili mpate kushukuru. [Al-Baqarah: 185]

 

 

Mafunzo:

 

 

“Alikuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ajwad (mkarimu) wa watu, na alikuwa ajwad zaidi katika Ramadhwaan wakati anapokutana na Jibriyl (‘Alayhis Salaam), alikuwa - Jibriyl (‘Alayhis Salaam)- akimjia Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam kila usiku wa Ramadhwaan akimdurusisha Qur-aan” [Imepokelewa na Al-Bukhaariy, kitabu cha Swawm, mlango alikuwa (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mkarimu (mbora) zaidi katika Ramadhwaan, Hadiyth namba 1179]

 

Share

186-Aayah Na Mafunzo: Ramadhwaan, Swiyaam Na Yanayohusu Duaa

 

Aayah Na Mafunzo:

 

Al-Baqarah

 

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ ﴿١٨٦﴾

Na watakapokuuliza Waja Wangu kuhusu Mimi, basi (waambie) hakika Mimi Niko Karibu (kwa ujuzi). Naitikia duaa ya muombaji anaponiomba. Hivyo basi waniitikie Mimi na waniamini Mimi, wapate kuongoka. [Al-Baqarah (2:186)]

 

 

 

Mafunzo:

 

Ramadhwaan, Swiyaam Na Yanayohusu Duaa

 

1-Ramadhwaan Ni Mwezi Wa Duaa Na Duaa Ya Mwenye Swawm Inaitikiwa:

 

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (رحمه الله) amesema: “Faida zinapatikana kutokana na Aayah hii. Kwanza: Kwamba kuna uwezekano mkubwa katika Swiyaam (funga) kuitikiwa duaa, kwa sababu Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja Aayah hii baada ya kutaja Aayah za Swiyaam, khasa vile Anavotaja mwishoni mwa kutaja Aayaat za Swiyaam. Pili: Baadhi ya watu wa ilimu wamesema kwamba inaweza kupatikana katika humo faida nyengineyo, kwamba duaa iombwe mwisho wa Siku ya Swawm (kabla ya kufuturu). [Tafsiyr Imaan Ibn ‘Uthaymiyn]

 

Na Hadiyth kadhaa zimethibitisha kuitikiwa duaa ya mwenye Swawm, miongoni mwazo ni:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((ثَلاثَةٌ لا تُرَدُّ دَعْوَتُهُمْ الإِمَامُ الْعَادِلُ وَالصَّائِمُ حِينَ يُفْطِرُ وَدَعْوَةُ الْمَظْلُومِ )) 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه):   Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Watatu duaa zao hazirejeshwi: Imaam (kiongozi)  mtenda haki, mwenye Swawm wakati anapofungua, na duaa ya aliyedhulumiwa.” [Imesimuliwa na At-Tirmidhiy Hadiyth nambari (2525), na Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh katika Swahihy At-Tirmidhiy Hadiyth nambari (2050)]

 

Na pia:

 

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ ، قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وسلم: ((إِنَّ لِلَّهِ تَبَارَكَ وَتَعَالَى عُتَقَاءَ فِي كُلِّ يَوْمٍ وَلَيْلَةٍ)) يَعْنِي: فِي َمَضَانَ وَإِنَّ لِكُلِّ مُسْلِمٍ فِي كُلِّ يَوْمٍ وَلَيْلَةٍ دَعْوَةً مُسْتَجَابَةً)) 

 

Amesimulia Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: “Allaah Ana watu wa kuwaacha huru na moto kila siku na usiku, na kila mja kati yao ana dua inayojibiwa.” [Imesimuliwa na Ahmad (7401). Na Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh katika Swahihy Al-Jaami’i (2169), Swahiyh At-Targhiyb Wat-Tarhiyb (1002)]

 

 

2-Kuomba Duaa Kwa Allaah (عزّ وجلّ) Pekee Bila Ya Kumshirikisha:

 

Swahaba walikuwa wanamuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) maswali mbalimbali. Allaah (سبحانه وتعالى) Ameyataja katika Qur-aan na Akatoa majibu kwa kutanguliza kumwambia Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) aseme kuwajibu Swahaba “Sema!”. Mifano michache:

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ ...  

“Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema…” [Al-Baqarah (2:219)]

 

يَسْأَلُكَ النَّاسُ عَنِ السَّاعَةِ ۖ قُلْ ...

“Watu wanakuuliza kuhusu Saa (Qiyaamah). Sema…” [Al-Ahzaab (33:63)]

 

وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ ...  

“Na wanakuuliza kuhusu hedhi. Sema…” [Al-Baqarah (2:222)]

 

Na maswali yote mengineyo katika Qur-aan, jibu la Allaah (سبحانه وتعالى) limeanzia hivyo hivyo: “Sema….” isipokuwa swali hili ambalo Allaah (عزّ وجلّ) Analijibu Mwenyewe moja kwa moja Anaposema: 

فَإِنِّي قَرِيبٌ

“Basi hakika Mimi ni Niko karibu.”

 

 

Hivyo ni kwa sababu Allaah (سبحانه وتعالى) Anadhihirisha kwamba Yuko karibu kabisa na hakuhitaji mtu kuomba duaa kupitia kwa mtu yeyote ili isije kuwa ni kumshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى) katika kuabudiwa Kwake, kwa sababu duaa ni ibaada kama alivyosema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth aliyosimulia Nu’umaan bin Bashiyr  (رضي الله عنه)  kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  katika kauli yake  Allaah (سبحانه وتعالى)

وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚ

“Na Rabb wenu Amesema: “Niombeni, Nitakuitikieni.”  Amesema: “Duaa ni ibaada.” Kisha akasoma Aayah hiyo tukufu.   [Ghaafir (40:60)] [Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, na Ahmad – Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

Basi watanabahi na wazingatie na wamche Allaah wanaomshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى) katika duaa zao kupitia viumbe kama wafanyavyo wenye kutufu makaburi kuwaomba wafu, jambo ambalo linaingia katika shirki kubwa ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Haisamehi pindi mtu akifariki bila ya kutubia.

 

 

 

3-Madamu Utamuomba Allaah Pekee Atakauitikia

 

Du’aa hupokelewa tu madamu Muislamu atamkabili Allaah (تعالى) bila ya kumshirikisha: Salmaan (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Rabb wenu (تبارك وتعالى) (Aliyebarikika na Aliyetukuka), Yuhai, Mkarimu, Anastahi kutoka kwa mja Wake anaponyanyua mikono yake kisha Airudishe sifuri.” [Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy na Ibn Maajah]

 

Pia; Abuu Sa’iyd (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna Muislamu atakayeomba du’aa ambayo haina dhambi wala kukata undugu wa uhusiano wa damu isipokuwa Allaah Atampa mojawapo ya matatu; ima Amharakishie du’aa yake, au Amuwekee akiba Aakhirah au ima Amuepushe nayo ovu kama hilo.” Wakasema: Basi tutazidisha (kuomba du’aa). Akasema: “Allaah Mwingi zaidi (wa kuongeza).” [Ahmad]

 

 

 

 

 

Share

187-Aayah Na Mafunzo: Ruhusa Ya Kula Na Kunywa Usiku Wa Ramadhwaan

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

 

Ruhusa Ya Kula Na Kunywa Usiku Wa Ramadhwaan  

 

www.alhidaaya.com

 

 

أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَائِكُمْ ۚ هُنَّ لِبَاسٌ لَّكُمْ وَأَنتُمْ لِبَاسٌ لَّهُنَّ ۗ عَلِمَ اللَّـهُ أَنَّكُمْ كُنتُمْ تَخْتَانُونَ أَنفُسَكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ وَعَفَا عَنكُمْ ۖ فَالْآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُوا مَا كَتَبَ اللَّـهُ لَكُمْ ۚ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ ۚ وَلَا تُبَاشِرُوهُنَّ وَأَنتُمْ عَاكِفُونَ فِي الْمَسَاجِدِ ۗ تِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ فَلَا تَقْرَبُوهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ ﴿١٨٧﴾

187. Mmehalalishiwa usiku wa kufunga Swiyaam kujamiiana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu na nyinyi ni vazi kwao. Allaah Anajua kwamba nyinyi mlikuwa mkijifanyia khiyana nafsi zenu, hivyo Akapokea tawbah yenu na Akakusameheni. Basi sasa waingilieni na tafuteni Aliyokuandikieni Allaah kwenu. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe (mapambazuko) wa Alfajiri kutokana na uzi mweusi (wa kiza cha usiku). Kisha timizeni Swiyaam mpaka usiku. Na wala msiwaingilie hali ya kuwa nyinyi wenye kukaa i’tikaaf Misikitini. Hiyo ni mipaka ya Allaah basi msiikaribie. Hivyo ndivyo Allaah Anavyobainisha Aayaat (na hukmu) Zake kwa watu wapate kuwa na taqwa.

 

Maswahaba walitatanishwa na kushindwa kuelewa maana ya neno uzi mweupe kutokana na uzi mweusi.” ‘Adiyy bin Haatim (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Ilipoteremshwa Aayah: mpaka ubainike kwenu uzi mweupe (mapambazuko) wa Alfajiri kutokana na uzi mweusi (wa kiza cha usiku)”, Nilichukua uzi mmoja mweupe na mmoja mweusi nikaweka chini ya mto wangu lakini haikunibainikia. Nikamwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلمasubuhi nikamwelezea. Akasema: “Hakika hiyo (imekusudiwa) ni kiza cha usiku na weupe wa Alfajiri” [Al-Bukhaariy Na Muslim]

 

 

Share

191-Aayah Na Mafunzo: Utukufu Wa Masjid Al-Haraam Na Maharamisho Yake

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Utukufu Wa Masjid Al-Haraam Na Maharamisho Yake

 

 www.alhidaaya.com

 

 

وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُم مِّنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ ۚ وَالْفِتْنَةُ أَشَدُّ مِنَ الْقَتْلِ ۚ وَلَا تُقَاتِلُوهُمْ عِندَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ حَتَّىٰ يُقَاتِلُوكُمْ فِيهِ ۖ فَإِن قَاتَلُوكُمْ فَاقْتُلُوهُمْ ۗ كَذَٰلِكَ جَزَاءُ الْكَافِرِينَ ﴿١٩١﴾

191. Na wauweni popote muwakutapo, na watoeni popote walipokutoeni. Na fitnah ni mbaya zaidi kuliko kuua. Na wala msipigane nao kwenye Al-Masjidil-Haraam mpaka wakupigeni humo, watakapokupigeni basi wauweni. Namna hivi ndivyo jazaa ya makafiri.

 

 

Mafunzo

 

 

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika mji huu Ameuharamishwa Allaah tokea Siku Aliyoumba mbingu na ardhi. Hivyo, ni sehemu tukufu kwa amri ya Allaah mpaka Siku ya Qiyaamah. Kupigana kwake kulihalalishwa kwangu tena kwa saa chache mchana. Hivyo, ni sehemu tukufu kwa amri ya Allaah mpaka Siku ya Qiyaamah. Miti yake isikatwe na majani yasing’olewe. Endapo mtu atataja mapigano yaliyofanywa na Rasuli wa Allaah kuwa ni hoja inayoruhusu watu kupigana katika mji huo, basi semeni kuwa: Allaah Alimruhusu Rasuli Wake lakini hakukuruhusuni nyinyi.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share

197-Aayah Na Mafunzo: Miezi Ya Hajj Na Haramisho La Maasi

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Miezi Ya Hajj Na Haramisho La Maasi

 

 

 

الْحَجُّ أَشْهُرٌ مَّعْلُومَاتٌ ۚ فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ ۗ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ يَعْلَمْهُ اللَّـهُ ۗ وَتَزَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَىٰ ۚ وَاتَّقُونِ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٧﴾

197. Hajj ni miezi maalumu. Na atakayekusudia kuhiji (akahirimia), basi asifanye tendo la ndoa wala ufasiki wala mabishano katika Hajj. Na lolote mlifanyalo katika ya kheri Allaah Analijua. Na chukueni masurufu. Na hakika bora ya masurufu ni taqwa. Na nicheni Mimi enyi wenye akili!

 

 

Mafunzo:

 

Kuhusu miezi ya Hajj; Ibn ‘Umar (رضي الله عنه) alisema: Ni Shawwaal, Dhul-Qa’dah na siku kumi za mwanzo za Dhul-Hijjah. [Fat-hul-Baariy (3/491)]

Na kuhusu kubishana, imeharamsihwa khaswa katika Hajj na masiku yote yote mengineyo; Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mimi ni mdhamini wa nyumba ya kando ya Jannah kwa anayeacha mabishano hata kama ni mwenye haki, na ni mdhamini wa nyumba iliyo katikati ya Jannah kwa anayeacha uongo japo ni kwa mzaha, na mdhamini wa nyumba iliyo mahala pa juu zaidi ya Jannah kwa ambaye tabia yake ni njema.” [Abuu Daawuwd kwa isnaad Swahiyh]

 

 

Share

201-Aayah Na Mafunzo: Miongoni Du’aa Alizokuwa Akiomba Sana Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

 

Miongoni Mwa Du’aa Alizokuwa Akiomba Sana Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 وَمِنْهُم مَّن يَقُولُ رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ ﴿٢٠١﴾

201. Na miongoni mwao kunawasemao: “Rabb wetu Tupe katika dunia mazuri na katika Aakhirah mazuri na Tukinge na adhabu ya moto.”

 

 

Mafunzo:

 

 عَنْ أَنَسٍ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: كَانَ أَكْثَرُ دُعَاءِ رَسُولِ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم: ((رَبَّنَا آتِنَا فِي اَلدُّنْيَا حَسَنَةً, وَفِي اَلْآخِرَةِ حَسَنَةً, وَقِنَا عَذَابَ اَلنَّارِ)) مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ.‏

Imepokelewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiomba sana du’aa: ((Rabbanaa Aatinaa fid-duniya hasanatan wa fil-Aakhirati hasanatan wa Qinaa ‘adhaaban-naar))  [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share

203-Aayah Na Mafunzo: Kumdhukuru Allaah Kwa Wingi Masiku Ya Tashriyq

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Kumdhukuru Allaah Kwa Wingi Masiku Ya Tashriyq

 

 

وَاذْكُرُوا اللَّـهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ ۚ فَمَن تَعَجَّلَ فِي يَوْمَيْنِ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ وَمَن تَأَخَّرَ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ لِمَنِ اتَّقَىٰ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ ﴿٢٠٣﴾

203. Na mdhukuruni Allaah katika siku za kuhesabika. Atakayeharakisha kuondoka katika siku mbili, basi hakuna dhambi juu yake; na atakayetaakhari basi hakuna dhambi juu yake; kwa mwenye kuwa na taqwa. Na mcheni Allaah na jueni kwamba Kwake mtakusanywa.

 

 

Mafunzo:

 

Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Siku za kuhesabika ni siku za tashriyq (11, 12, 13 Dhul-Hijjah) na siku zinazojulikana ni siku za kumi za mwanzo za Dhul-Hijjah. [Al-Qurtwubiy: 3.3]

 

 

 

Share

205-Aayah Na Mafunzo: Miongoni Mwa Ufisadi Katika Ardhi Shirki Na Bid’ah

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

 

www.alhidaaya.com

 

Miongoni Mwa Ufisadi Katika Ardhi Shirki Na Bid’ah  

 

وَإِذَا تَوَلَّىٰ سَعَىٰ فِي الْأَرْضِ لِيُفْسِدَ فِيهَا وَيُهْلِكَ الْحَرْثَ وَالنَّسْلَ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الْفَسَادَ ﴿٢٠٥﴾ 

205. Na anapoondoka hufanya bidii katika ardhi ili afisidi humo na aangamize mimea na vizazi.  Na Allaah Hapendi ufisadi.

 

 

Mafunzo:

 

Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema: “Kwa ujumla shirki na kumwomba du’aa asiyekuwa Allaah na kumwabudu ghairi Yake, au kumtii au kumfuata (mwongozi) asiyekuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni ufisadi mkubwa kabisa katika ardhi, hakuna kutengenea watu wake isipokuwa mpaka iwe Allaah Ndiye Mwabudiwa Pekee na kuombwa du’aa Yeye na kumtii na ittibaa’ (kufuata mwongozo wa) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) [Majmuw’ Al-Fataawa 25/15)]

 

Pia kuleta na kueneza bid’ah katika Dini. Amethadharisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

 مَنْ أَحْدَثَ فِي أَمْرِنَا هَذَا مَا لَيْسَ مِنْهُ فَهُوَ رَدٌّ

((Atakayezusha katika jambo letu hili (Dini yetu) basi litarudishwa.)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share

208-Aayah Na Mafunzo: Hatua Za Shaytwaan Na Fadhila Za Kutokumfuata

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

 

www.alhidaaya.com

 

Hatua Za Shaytwaan Na Fadhila Za Kutokumfuata

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿٢٠٨﴾

208. Enyi walioamini! Ingieni katika Uislamu kikamilifu, na wala msifuate hatua za shaytwaan. Hakika yeye kwenu ni adui wa wazi.

 

 

Mafunzo:

عَنْ سَبْرَةَ بْنِ أَبِي فَاكِهٍ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: ((إِنَّ الشَّيْطَانَ قَعَدَ لاِبْنِ آدَمَ بِأَطْرُقِهِ ، فَقَعَدَ لَهُ بِطَرِيقِ الإِسْلاَمِ فَقَالَ: تُسْلِمُ وَتَذَرُ دِينَكَ وَدِينَ آبَائِكَ وَآبَاءِ أَبِيكَ؟ فَعَصَاهُ فَأَسْلَمَ ، ثُمَّ قَعَدَ لَهُ بِطَرِيقِ الْهِجْرَةِ فَقَالَ: تُهَاجِرُ وَتَدَعُ أَرْضَكَ وَسَمَاءَكَ؟ وَإِنَّمَا مَثَلُ الْمُهَاجِرِ كَمَثَلِ الْفَرَسِ فِي الطِّوَلِ،  فَعَصَاهُ فَهَاجَرَ، ثُمَّ قَعَدَ لَهُ بِطَرِيقِ الْجِهَادِ فَقَالَ: تُجَاهِدُ فَهُوَ جَهْدُ النَّفْسِ وَالْمَالِ فَتُقَاتِلُ فَتُقْتَلُ فَتُنْكَحُ الْمَرْأَةُ وَيُقْسَمُ الْمَالُ؟ فَعَصَاهُ فَجَاهَدَ‏)) ‏.‏ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم : ((فَمَنْ فَعَلَ ذَلِكَ كَانَ حَقًّا عَلَى اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ أَنْ يُدْخِلَهُ الْجَنَّةَ ،  وَمَنْ قُتِلَ كَانَ حَقًّا عَلَى اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ أَنْ يُدْخِلَهُ الْجَنَّةَ ،  وَإِنْ غَرِقَ كَانَ حَقًّا عَلَى اللَّهِ أَنْ يُدْخِلَهُ الْجَنَّةَ ، أَوْ وَقَصَتْهُ دَابَّتُهُ كَانَ حَقًّا عَلَى اللَّهِ أَنْ يُدْخِلَهُ الْجَنَّةَ))‏

 

Imepokelewa kutoka kwa Sabrah bin Abiy Faakih (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba kamsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Hakika shaytwaan humkalia mwana Aadam katika njia zake. Humkalia katika njia ya Islaam husema: “Hivi utaingia katika Uislamu uache dini  yako na dini ya baba yako na ya babu zako?” Lakini akamuasi akasilimu. Kisha akamkalia njia ya hijrah. Akasema: “Hivi utahajiri uache nchi yako na mbingu zake? Hakika mwenye kuhajiri ni kama farasi aliyefungwa kwenye kigingi.” Lakini akamuasi akahajiri. Kisha akamkalia njia ya jihaad akasema: “Hivi utapigana jihaad ugharimu uhai wako na mali yako. Utapigana na utauliwa, na mkeo ataolewa na mali yako itagawanywa.” Lakini akamuasi akapigana jihaad)) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Atakayefanya hivyo atakuwa na haki kwa Allaah (‘Azza wa Jalla) Amuingize Jannah. Na atakayeuliwa atakuwa na haki kwa Allaah (‘Azza wa Jalla) Amiuingize Jannah. Atakayezama atakuwa na haki kwa Allaah Amuingize Jannah. Atakayeangushwa na mnyama wake akavunjika shingo, atakuwa na haki kwa Allaah Amuingize Jannah)).

 

[An-Nasaaiy – Kitaab Al-Jihaad na ameisahihisha Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) katika Swahiyh An-Nasaaiy (3134), na taz. Swahiyh Al-Jaami’ (1652)]

Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema: “Kila Alichokiharamisha Allaah (Ta’aalaa) ni katika hatua za shaytwaan, ikiwa ni kutakabari, au kuongopa, au isthzai au mengineo, kwa sababu huyaamrisha na huyaitia na huyalingania.” [Tafsiyr Al-Faatihah wal Baqarah (2/234)]  

 

 

Share

213-Aayah Na Mafunzo: Ummah Wetu Ni Wa Mwisho Lakini Wa Kwanza Kuhukumiwa Na Kuingizwa Jannah

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Ummah Wetu Ni Wa Mwisho Na Wa Kwanza Kuhukumiwa Na Kuingizwa Jannah

 www.alhidaaya.com

 

كَانَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً فَبَعَثَ اللَّـهُ النَّبِيِّينَ مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ وَأَنزَلَ مَعَهُمُ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِيَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ فِيمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ ۚ وَمَا اخْتَلَفَ فِيهِ إِلَّا الَّذِينَ أُوتُوهُ مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۖ فَهَدَى اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا لِمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِهِ ۗ وَاللَّـهُ يَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٢١٣﴾

213. Watu walikuwa ummah mmoja kisha Allaah Akatuma Nabiy wabashiriaji na waonyaji na Akateremsha pamoja nao Kitabu kwa haki ili kihukumu baina ya watu katika ambayo wamekhitilafiana kwayo. Na hawakukhitilafiana katika hayo isipokuwa wale waliopewa hicho (Kitabu) baada ya kuwajia hoja bayana kwa kufanyiana baghi na uhusuda baina yao. Allaah Akawaongoza wale walioamini kuendea haki katika yale waliyokhitilafiana, kwa idhini Yake. Na Allaah Humwongoza Amtakaye kuelekea njia iliyonyooka.

 

Mafunzo:

Hudhayfah bin Al-Yamaan (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah Aliwapoteza waliokuwa kabla yetu kutokujua Siku ya Ijumaa. Ilikuwa Mayahudi siku ya Jumamosi na ikawa Manaswara siku ya Jumapili, Akaja Allaah kwetu Akatuongoza (kuifahamu) siku ya Ijumaa Akafanya Ijumaa na Jumamosi na Jumapili na vile vile wao watatufuata sisi siku ya Qiyaamah. Na sisi ni wa mwisho katika watu wa dunia na wa kwanza Siku ya Qiyaamah watakaohukumiwa kabla ya viumbe (wengine).” [Al-Bukhaariy (1415) na katika riwaayah nyengine; “Sisi (Waislamu) watu wa kwanza kuingia Jannah…” [‘Abdur-Raazzaaq (1/82) Tafsiyr Ibn Kathiyr].

 

 

Share

214-Aayah Na Mafunzo: Kuipata Jannah Si Wepesi Inahitaji Juhudi Ya ‘Amali Na Kujizuia Maasi

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Kuipata Jannah Si Wepesi Inahitaji Juhudi Ya ‘Amali Na Kujizuia Maasi

 

  www.alhidaaya.com

 

 

أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَأْتِكُم مَّثَلُ الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلِكُم ۖ مَّسَّتْهُمُ الْبَأْسَاءُ وَالضَّرَّاءُ وَزُلْزِلُوا حَتَّىٰ يَقُولَ الرَّسُولُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ مَتَىٰ نَصْرُ اللَّـهِ ۗ أَلَا إِنَّ نَصْرَ اللَّـهِ قَرِيبٌ ﴿٢١٤﴾

214. Je, mnadhani kwamba mtaingia Jannah na hali bado haijakufikieni (mitihani) kama ya wale waliopita kabla yenu? Iliwagusa dhiki za umasikini na maafa ya magonjwa na njaa na wakatetemeshwa mpaka Rasuli na wale walioamini pamoja naye wanasema: “Lini itafika nusura ya Allaah?” Tanabahi! Hakika nusura ya Allaah iko karibu.

 

 

Mafunzo:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((لَمَّا خَلَقَ اللَّهُ الْجَنَّةَ وَالنَّارَ أَرْسَلَ جِبْرِيلَ إِلَى الْجَنَّةِ فَقَال: انْظُرْ إِلَيْهَا وَإِلَى مَا أَعْدَدْتُ لِأَهْلِهَا فِيهَا،  قَالَ:  فَجَاءَهَا وَنَظَرَ إِلَيْهَا وَإِلَى مَا أَعَدَّ اللَّهُ لِأَهْلِهَا فِيهَا.  قَالَ:  فَرَجَعَ إِلَيْهِ قَالَ: فَوَعِزَّتِكَ لَا يَسْمَعُ بِهَا أَحَدٌ إِلَّا دَخَلَهَا، فَأَمَرَ بِهَا فَحُفَّتْ بِالْمَكَارِهِ، فَقَالَ: ارْجِعْ إِلَيْهَا فَانْظُرْ إِلَى مَا أَعْدَدْتُ لِأَهْلِهَا فِيهَا،  قَالَ: فَرَجَعَ إِلَيْهَا فَإِذَا هِيَ قَدْ حُفَّتْ بِالْمَكَارِهِ،  فَرَجَعَ إِلَيْهِ فَقَالَ: وَعِزَّتِكَ لَقَدْ خِفْتُ أَنْ لَا يَدْخُلَهَا أَحَدٌ. قَالَ: اذْهَبْ إِلَى النَّارِ فَانْظُرْ إِلَيْهَا وَإِلَى مَا أَعْدَدْتُ لِأَهْلِهَا فِيهَا،  فَإِذَا هِيَ يَرْكَبُ بَعْضُهَا بَعْضًا،  فَرَجَعَ إِلَيْهِ فَقَالَ: وَعِزَّتِكَ لَا يَسْمَعُ بِهَا أَحَدٌ فَيَدْخُلَهَا، فَأَمَرَ بِهَا فَحُفَّتْ بِالشَّهَوَاتِ فَقَالَ: ارْجِعْ إِلَيْهَا فَرَجَعَ إِلَيْهَا فَقَالَ: وَعِزَّتِكَ لَقَدْ خَشِيتُ أَنْ لَا يَنْجُوَ مِنْهَا أَحَدٌ إِلَّا دَخَلَهَا)) الترمذي و قال حديث حسن صحيح – ابو داود والنسائي

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Alipoumba Jannah na moto, Alimtuma Jibriyl Jannah Akimwambia: Iangalie na angalia matayarisho Niliyoyaandaa  kwa ajili ya wakazi wake. Akasema: Kwa hivyo alikuja kuiangalia na kuangalia maandalizi Aliyoyaandaa Allaah kwa ajili ya wakazi Wake. Akasema: Akarejea kwa Allaah na kusema: Naapa kwa Utukufu Wako, hakuna atakayesikia (habari yake) ila tu ataingia (Jannah). Kisha Akaamrisha izungushwe mambo magumu watu wasiyoyapenda, Akasema: Rejea na angalia yale Niliyoyaandaa kwa ajili ya wakazi wake. Akasema: Kisha akarejea na akakuta imezungukwa na mambo magumu watu wasiyoyapenda. Hapo alirejea kwa Allaah na akasema: Naapa kwa Utukufu Wako, nina khofu hakuna hata mtu mmoja atakayeingia. Akasema: Nenda motoni ukauangalie na uangalie Niliyoyaandaa kwa ajili ya wakazi wake. Akaona ulikuwa na matabaka moja juu ya tabaka jingine. Akarejea kwa Allaah na akasema: Naapa kwa Utukufu Wako hakuna hata mmoja ausikiae (sifa zake) atakayeingia. Kisha Allaah Aliamrisha Uhusishwe na matamanio ya nafsi). Kisha Allaah Akamuambia: Rejea tena (motoni). Alirejea tena na akasema: Naapa kwa Utukufu, wako nakhofia kuwa hapatokuwa na yeyote atakayenusurika nao)) [At-Tirmidhiy, akasema ni Hadiyth Hasan, na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy]

 

 

Share

216-Aayah Na Mafunzo: Muumini Khasa Ni Mwenye Kuamini Majaaliwa Ya Khayr Na Shari

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

 

Muumini Khasa Ni Mwenye Kuamini Majaaliwa Ya Khayr Na Shari

 

www.alhidaaya.com

 

 

 كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ وَهُوَ كُرْهٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَن تُحِبُّوا شَيْئًا وَهُوَ شَرٌّ لَّكُمْ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٢١٦﴾

216. Mmeandikiwa shariy’ah kupigana vita nako kunachukiza mno kwenu. Na asaa mkachukia jambo na hali lenyewe ni khayr kwenu. Na asaa mkapenda jambo na hali lenyewe ni la shari kwenu. Na Allaah Anajua na nyinyi hamjui.

 

 

Mafunzo:

 

قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم:" عَجَبًا لأمرِ المؤمنِ إِنَّ أمْرَه كُلَّهُ لهُ خَيرٌ وليسَ ذلكَ لأحَدٍ إلا للمُؤْمنِ إِنْ أصَابتهُ سَرَّاءُ شَكَرَ فكانتْ خَيرًا لهُ وإنْ أصَابتهُ ضَرَّاءُ صَبرَ فكانتْ خَيرًا لهُ ". رواهُ مُسْلِمٌ.

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ajabu ya hali ya Muumini kuwa mambo yake yote ni khayr; anapofikwa na furaha hushukuru na huwa khayr kwake, na anapofikwa na matatizo husubiri na huwa ni khayr kwake, na haiwi hivyo (sifa hiyo) ila kwa Muumini)) [Muslim]

 

 

Share

219-Aayah Na Mafunzo: Kafara Ya Niyyah Ya Kucheza Kamari Ni Kutoa Swadaqah

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Kafara Ya Niyyah Ya Kucheza Kamari Ni Kutoa Swadaqah

 

 

 يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَا أَكْبَرُ مِن نَّفْعِهِمَا ۗ وَيَسْأَلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَ قُلِ الْعَفْوَ ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ ﴿٢١٩﴾

219. Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema: “Katika viwili hivyo mna dhambi kubwa na (baadhi ya) manufaa kwa watu. Na dhambi yake viwili hivyo ni kubwa kuliko manufaa yake.” Na wanakuuliza nini watoe. Sema: “Yaliyokuzidieni.” Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat (na  shariy’ah) ili mpate kutafakariMafunzo:

 

Mafunzo:

 

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mwenye kuapa akasema katika kiapo chake: Naapa kwa Laata na ‘Uzzaa (majina ya waabudiwa wa uongo) aseme: Laa ilaaha illa Allaah. Na atakayemwambia mwenzake: Njoo tuchezeshe kamari, basi atoe swadaqah.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Share

221-Aayah Na Mafunzo: Mwanamke Huolewa Kwa Sifa Nne…

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

 

www.alhidaaya.com

 

Mwanamke Huolewa Kwa Sifa Nne….

 

وَلَا تَنكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ ۚ وَلَأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ ۗ وَلَا تُنكِحُوا الْمُشْرِكِينَ حَتَّىٰ يُؤْمِنُوا ۚ وَلَعَبْدٌ مُّؤْمِنٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ ۗ أُولَـٰئِكَ يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَى الْجَنَّةِ وَالْمَغْفِرَةِ بِإِذْنِهِ ۖ وَيُبَيِّنُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٢٢١﴾

221. Na wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni. Na wala msiwaozeshe (wanawake wa Kiislamu) wanaume washirikina mpaka waamini. Na mtumwa Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni. Hao wanaita katika moto na Allaah Anaita katika Al-Jannah na maghfirah kwa idhini Yake. Na Anabainisha Aayaat (na shariy’ah) Zake ili wapate kukumbuka.

 

 

Mafunzo:

 

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mwanamke huolewa kwa (sifa) nne; mali yake (utajiri), nasaba yake, na uzuri wake na Dini yake, lakini shikilia mwenye Dini utaneemeka.”  [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share

222-Aayah Na Mafunzo: Hukmu Ya Haramisho La Kujimai Na Mwanamke Akiwa Katika Hedhi Au Nifaas Ni Moja

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

 

Hukmu Ya Haramisho La Kujimai Na Mwanamke Akiwa Katika Hedhi Au Nifaas Ni Moja

 

www.alhidaaya.com

 

 

وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ ۖ وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ ۖ فَإِذَا تَطَهَّرْنَ فَأْتُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ أَمَرَكُمُ اللَّـهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ ﴿٢٢٢﴾ 

222. Na wanakuuliza kuhusu hedhi. Sema: “Hiyo ni dhara; basi waepukeni wanawake katika hedhi. Wala msiwakaribie kujimai nao mpaka watwaharike. Watakapotwaharika basi waendeeni kupitia pale Alipokuamrisheni Allaah.” Hakika Allaah Anapenda wenye kutubia na Anapenda wenye kujitwaharisha.

 

 

Mafunzo:

 

Kuruhusiwa kufanya kila jambo isipokuwa kujimai.

 

عن  أنس رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ الْيَهُودَ كَانُوا إِذَا حَاضَتِ الْمَرْأَةُ؛ لَمْ يُؤَاكِلُوهَا. فَقَالَ النَّبِيُّ -صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((اصْنَعُوا كُلَّ شَيْءٍ إِلاَّ النِّكَاحَ)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Imepokelewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mayahudi walikuwa hawali na mwanamke anapokuwa katika hedhi. Lakini Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Fanyeni naye kila jambo isipokuwa kujimai)) [Muslim]

 

Haramisho la kumuingilia:

 

Mwenye kumuingia mwenye hedhi au mwanamke kwenye dubur (uchi wa nyuma) au kumwendea mtabiri na kumuamini kwa anayosema basi amekufuru kwa aliyoteremshiwa Muhammad.” [Swahiyh At-Tirmidhiy (135), Swahiyh Ibn Maajah (528), As-Silsilah Asw-Swahiyhah (7/1130)].

 

Imaam Ibn Taymiyyah amesema:

 

"Kuwaingilia wenye nifasi ni kama kumwingilia mwenye hedhi, na hilo ni haramu kwa makubaliano ya Maimaam. [Al-Fataawaa (21/624)]

 

 

Share

223-Aayah Na Mafunzo: (1) Haramisho La Kumuingilia Mwanamke Kwa Nyuma (2) Duaa Ya Kujimai

 

 

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

 

(1) Haramisho La Kumuingilia Mwanamke Kwa Nyuma (2) Duaa Ya Kujimai

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّىٰ شِئْتُمْ ۖ وَقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّكُم مُّلَاقُوهُ ۗ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٢٢٣﴾

223. Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu (panapotoka kizazi) vyovyote mpendavyo. Na kadimisheni (mema) kwa ajili ya nafsi zenu. Na mcheni Allaah na jueni kwamba hakika nyinyi ni wenye kukutana Naye. Na wabashirie Waumini.

 

Mafunzo:

 

Haramisho la kumuingilia mwanamke kupitia dubur (uchi wa nyuma) yameharamishwa katika Hadiyth zifuatazo:

 

“Allaah Hatomtazama mwanamume mwenye kumuingilia mkewe kwa nyuma.” [An-Nasaaiy na Ibn Hibbaan kwa Isnaad nzuri].

 

"Amelaaniwa mwenye kumuingilia mwanamke kwa nyuma." [Ahmad, Abuu Daawuwd na Ibn 'Adiy]

 

"Mwenye kumuingia mwenye hedhi au mwanamke kwa nyuma au kumwendea mchawi na kumuamini kwa anayosema basi amekufuru kwa aliyoteremshiwa Muhammad." [Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na Ibn Maajah, na Isnadi yake ni Sahihi].

 

Faida: Kuhusu kauli ya Allaah “Na kadimisheni (mema) kwa ajili ya nafsi zenu.“ Yaani, jikurubisheni kwa Allaah kwa ‘amali njema na kumuingilia mke kwa kutaja Jina la Allaah kwa kusema, BismiLLaah – kabla ya kuanza jimai na kutaraji kupata kizazi chema; Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Iwapo mmoja wenu atamuingilia mke wake kisha akasema:

بِسْمِ الله اللّهُـمَّ جَنِّبْنا الشَّيْـطانَ، وَجَنِّبِ الشَّـيْطانَ ما رَزَقْـتَنا

BismiLLaah, Allaahumma Jannibnash-shaytwaan wa Jannibish-shaytwaan maa Razaqtanaa’  (Kwa Jina la Allaah, Ee Allaah! Tulinde na shaytwaan pia kilinde Ulichoturuzuku kutokana na shaytwaan) basi iwapo watakuwa wameandikiwa kupata mtoto, shaytwaan hatoweza kumdhuru)) [Al-Bukhaariy kama ilivyo katika Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

 

Share

224-Aayah Na Mafunzo: Makatazo Ya Kuendeleza Viapo Vya Makosa

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Makatazo Ya Kuendeleza Viapo

 

وَلَا تَجْعَلُوا اللَّـهَ عُرْضَةً لِّأَيْمَانِكُمْ أَن تَبَرُّوا وَتَتَّقُوا وَتُصْلِحُوا بَيْنَ النَّاسِ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٢٤﴾

224. Na wala msifanye (Jina la) Allaah kuwa ni nyudhuru ya viapo vyenu kukuzuieni katika kutenda wema na kuwa na taqwa na kusuluhisha baina ya watu. Na Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 Mafunzo :

Kutoka kwa Naafi’ kwamba Ibn ‘Umar alikuwa akisema katika Al-Iylaa (mwanamume kuapa kutokukutana na mkewe) Aliyoitaja Allaah (تعالى).

 

Makatazo ya kuendeleza viapo vya makosa: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Wa-Allaahi! Ni dhambi zaidi kwa Allaah, mmoja wenu anapotekeleza kiapo chake kuhusu (kuvunja uhusiano) na jamaa zake kuliko (kuvunja kiapo na) kulipa kafara (fidia) kama inavyotakiwa na Allaah katika hali kama hizi.” [Muslim]

 

 

 

Share

227-Aayah Na Mafunzo: Haramisho La Mwanamke Kuomba Talaka Bila Sababu

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Haramisho La Mwanamke Kuomba Talaka Bila Sababu

 

 

 

وَإِنْ عَزَمُوا الطَّلَاقَ فَإِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿٢٢٧﴾

227. Na wakiazimia talaka, basi hakika Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

Mafunzo:

 

Mwanamke haifai kuomba talaka bila ya sababu:  

 

عَنْ ثَوْبَان مَوْلَى رَسُول اللَّه – صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ – عَنْ النَّبِيّ – صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ – أَنَّهُ قَالَ :((أَيّمَا اِمْرَأَة سَأَلَتْ زَوْجهَا الطَّلَاق فِي غَيْر مَا بَأْس حَرَّمَ اللَّه عَلَيْهَا رَائِحَة الْجَنَّة))  الترمذي و قال حديث حسن

Kutoka kwa Thawbaan amesema kwamba: Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mwanamke yeyote anayemuomba mumewe talaka bila ya sababu yoyote, Allaah Amemharimishia harufu ya Pepo” [At-Tirmidhiy na kasema Hadiyth Hasan]

 

Na riwaayah nyengine amesema:

 

“Mwanamke yeyote mwenye kumuomba mumewe talaka pasi na kosa lolote basi Jannah itakuwa haram kwake wala hatosikia harufu yake.” [Al-Bukhaariy, Muslim, Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy na Ibn Maajah].

 

 

 

 

Share

228-Aayah Na Mafunzo: Miongoni Mwa Haki Za Mume Na Mke

Aayah Na Mafunzo

 Al-Baqarah

 

Miongoni Mwa Haki Za Mume Na Mke

 

 

 

وَالْمُطَلَّقَاتُ يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ ثَلَاثَةَ قُرُوءٍ ۚ وَلَا يَحِلُّ لَهُنَّ أَن يَكْتُمْنَ مَا خَلَقَ اللَّـهُ فِي أَرْحَامِهِنَّ إِن كُنَّ يُؤْمِنَّ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ وَبُعُولَتُهُنَّ أَحَقُّ بِرَدِّهِنَّ فِي ذَٰلِكَ إِنْ أَرَادُوا إِصْلَاحًا ۚ وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٢٨﴾

228. Na wanawake waliotalikiwa wabakie kungojea zipite hedhi (na twahara) tatu. Na wala si halali kwao kuficha Aliyoumba Allaah katika matumbo yao ikiwa wao ni wenye kumwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Na waume zao wana haki kuwarejea katika muda huo ikiwa wakitaka suluhu. Nao wake wana haki kama ambayo (ya waume zao) iliyo juu yao kwa mujibu wa shariy’ah. Na wanaume wana daraja zaidi juu yao. Na Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.

 

Mafunzo:

 

عن جابر (رضي الله عنه) عن النبي صلى الله عليه وسلم: أنه قال في حجة الوداع: ((واتَّقُوا اللهَ في النِّساءِ، فإنهن عندكم عَوَانٌ، ولكم عليهن ألا يُوطِئْنَ فُرُشكم أحدا تكرهونه، فإن فَعَلْن فاضربوهن ضَرْبا غير مُبَرِّح، ولهن رزْقُهنَّ وكِسْوتهن بالمعروف))

Kutoka kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema katika Hijja ya kuaga: ((Mcheni Allaah kuhusu wanawake kwani wao ni wasaidizi wenu.  Mnayo haki juu yao kuwa wasimuruhusu mtu msiyempenda kukanyaga zulia lenu. (kuingia katika nyumba) Lakini wakifanya hivyo, mnaruhusiwa kuwatia adabu ndogo. Wao wana haki kwenu kwamba muwatimizie matumizi yao na nguo kwa njia ya kuridhisha)) [Muslim]

 

Na pia:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((لاَ يَفْرَكْ مُؤْمِنٌ مُؤْمِنَةً إِنْ كَرِهَ مِنْهَا خُلُقًا رَضِيَ مِنْهَا آخَرَ))  مسلم

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu)   kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Muumin [mume] asimchukie Muumin [mke]. Asipompendelea kwa tabia fulani ataridhika naye kwa tabia nyingine)) [Muslim]

 

Share

229-Aayah Na Mafunzo: Hukmu Ya Khul’u Ni Kurudisha Mahari Kutokuvuka Mipaka

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Hukmu Ya Khul’u Ni Kurudisha Mahari Kutokuvuka Mipaka

 

 

الطَّلَاقُ مَرَّتَانِ ۖ فَإِمْسَاكٌ بِمَعْرُوفٍ أَوْ تَسْرِيحٌ بِإِحْسَانٍ ۗ وَلَا يَحِلُّ لَكُمْ أَن تَأْخُذُوا مِمَّا آتَيْتُمُوهُنَّ شَيْئًا إِلَّا أَن يَخَافَا أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ اللَّـهِ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ اللَّـهِ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا فِيمَا افْتَدَتْ بِهِ ۗ تِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ فَلَا تَعْتَدُوهَا ۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ اللَّـهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٢٢٩﴾

229. Talaka ni mara mbili. Hivyo kuzuia kwa mujibu wa shariy’ah au kuachia kwa ihsaan. Wala si halali kwenu kuchukua chochote katika mlivyowapa wanawake, isipokuwa wote wawili wakikhofu kuwa hawatoweza kusimamisha mipaka ya Allaah. Mtakapokhofu kuwa wote wawili hawatoweza kusimamisha mipaka ya Allaah; basi hakuna lawama juu yao katika ambacho amejikombolea kwacho. Hiyo ni mipaka ya Allaah basi msitaadi. Na atakayetaadi mipaka ya Allaah basi hao ndio madhalimu.

 

Mafunzo:

 

Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amehadithia kwamba: Mke wa Thaabit bin Qays alimfuata Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: Ee Rasuli wa Allaah,  Thaabit bin Qays simlaumu katika tabia wala Dini, lakini mimi nakhofia ukafiri katika Uislamu (kutokutekeleza haki zake). Basi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Utamrejeshea shamba lake?” Akasema: Ndio. Akasema kumwambia Qays: “Kubali shamba na umtaliki.” [Al-Bukhaariy (5273)].

Khul‘u: kujivua kutoka katika ndoa na kurudisha mahari.

 

Kutaadi mipaka ya Allaah amekataza pia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliposema: “Allaah Ameweka mipaka, hivyo msipindukie, na Ametoa maamrisho hivyo msiyadharau, na kuyaharamisha baadhi ya mambo, hivyo msifanye makosa. Ameacha baadhi ya mambo bila ya kuyawekea shariy’ah kwa kuwahurumia, si kwa sababu Aliyasahau, basi msiulizie khabari zake.” [Ad-Daaraqutwniy (4/298)]

 

Share

230-Aayah Na Mafunzo: Haramisho La Kuhalalisha Ndoa Baada Ya Talaka Tatu

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

 

Haramisho La Kuhalalisha Ndoa Baada Ya Talaka Tatu

 

www.alhidaaya.com 

 

 

 فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا تَحِلُّ لَهُ مِن بَعْدُ حَتَّىٰ تَنكِحَ زَوْجًا غَيْرَهُ ۗ فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يَتَرَاجَعَا إِن ظَنَّا أَن يُقِيمَا حُدُودَ اللَّـهِ ۗ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ يُبَيِّنُهَا لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٢٣٠﴾

230. Na akimtaliki (mara ya tatu) basi hatokuwa halali kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwengine. Akimtaliki (au akifariki) hapatokuwa dhambi juu yao wawili kurejeana wakidhani kwamba watasimamisha mipaka ya Allaah. Na hiyo ni mipaka ya Allaah Anaibainisha kwa watu wanaojua.

 

Mafunzo:

 

Haifai kufunga nikaah ya uongo kwa ajili kuhalalisha nikaah baada ya talaka tatu. Amelaaniwa afanyaye hivyo; Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amemlaani anayefanya tahliyl (mhalalishaji) na mhalalishiwa wale wanaokula ribaa na wanaotoa ribaa.” [At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah na Ahmad].

 

Faida nyengine:

 

‘Aaishah (رضي الله عنها) amehadithia: Mke wa Rifaa’ah Al-Qurdhwiy alikuja wakati mimi na Abuu Bakr tulikuwa na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: Nilikuwa mke wa Rifaa‘ah, lakini aliniacha na ilikuwa talaka isiyorejewa. Kisha niliolewa na ‘Abdur-Rahmaan bin Az-Zubayr lakini dhakari yake ilikuwa haina nguvu. Kisha akachukua ncha ya nguo yake akaonesha ulaini wa dhakari yake (kuwa mfano wa udogo wa dhakari). Khaalid bin Sa’iyd bin Al-‘Aasw ambaye alikuwa mlangoni akisubiri kuruhusiwa kuingia alisema: Yaa Abaa Bakr! Kwanini humzuii huyu mwanamke kusema wazi mbele ya Rasuli wa Allaah?  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akacheka, kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamuuliza yule mwanamke: “Je, unataka kurudi kuolewa na Rifaa’ah? Basi, huwezi mpaka uonje ‘usaylah yake naye aonje ‘usaylah yako (yaani mjamiiane kikamlifu na mumeo wa sasa).” [Ahmad (6/34) na Al-Bukhaariy na Muslim na An-Nasaaiy walinukuu Hadiyth hii kwa maneno ya Muslim kuwa Rifaa’ah alimtaliki mkewe kwa talaka ya tatu na ya mwisho]. Maana ya ‘usaylah ni kitendo cha jimai kama ilivyo dalili ya Hadiyth: “Fahamu kuwa ‘usaylah ni kuingiliana kimwili.” [Ahmad (6/62)]

 

 

Share

233-Aayah Na Mafunzo: Faida Za Kumnyonyesha Mtoto

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

 

Faida Za Kumnyonyesha Mtoto

www.alhidaaya.com

 

 

 

 

 

وَالْوَالِدَاتُ يُرْضِعْنَ أَوْلَادَهُنَّ حَوْلَيْنِ كَامِلَيْنِ ۖ لِمَنْ أَرَادَ أَن يُتِمَّ الرَّضَاعَةَ ۚ وَعَلَى الْمَوْلُودِ لَهُ رِزْقُهُنَّ وَكِسْوَتُهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ لَا تُكَلَّفُ نَفْسٌ إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَا تُضَارَّ وَالِدَةٌ بِوَلَدِهَا وَلَا مَوْلُودٌ لَّهُ بِوَلَدِهِ ۚ وَعَلَى الْوَارِثِ مِثْلُ ذَٰلِكَ ۗ فَإِنْ أَرَادَا فِصَالًا عَن تَرَاضٍ مِّنْهُمَا وَتَشَاوُرٍ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا ۗ وَإِنْ أَرَدتُّمْ أَن تَسْتَرْضِعُوا أَوْلَادَكُمْ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِذَا سَلَّمْتُم مَّا آتَيْتُم بِالْمَعْرُوفِ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٢٣٣﴾ 

233. Na wazazi wa kike wanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili, kwa mwenye kutaka kutimiza kunyonyesha. Na ni juu ya mzazi wa kiume kuwapatia chakula chao na nguo kwa mujibu wa ada. Hailazimishwi nafsi ila kwa iliwezalo. Asidhuriwe mzazi wa kike kwa ajili ya mwanawe, na wala mzazi wa kiume kwa ajili ya mwanawe. Na juu ya mrithi (wa baba) mfano wa hivyo. Watakapotaka kumwachisha kunyonya kwa maridhiano baina yao wawili na mashauriano basi hapana dhambi juu ya wawili hao. Na mtakapotaka kutafuta wa kuwayonyesha watoto wenu, basi si dhambi kwenu ikiwa mtalipa mlichoahidi kwa mujibu wa shariy’ah. Na mcheni Allaah na jueni kwamba hakika Allaah kwa myatendayo ni Mwenye kuona.

 

Mafunzo:

Faida Za Kunyonyesha:

Mama  anafaa atambue kwamba kumnyonyesha mtoto ni jambo lenye kumpatia faida nyingi mtoto pamoja na mama yake, kwani ni jambo la asili Alilojaaliya Allaah (Subhanaahu wa Ta’aalaa) kwa rahma Yake kubwa na Hikma Yake na bila shaka faida zake hakuna anayezipinga kwani hata madaktari wametambua faida nyingi baada ya utafiti. Baadhi ya hizo faida ni:  

 

 

Faida kwa mtoto

  1. Mtoto anakingika na maradhi mengi ya kila aina.
  2. Imepatikana asilimia ndogo ya vifo vya watoto wanaonyonyeshwa vifuani.
  3. Asilimia kubwa imeonekana kuwa watoto wanaonyonyeshwa huwa ni wenye akili kubwa (mahodari) na wenye utulivu zaidi.
  4. Maziwa ya mama ni chakula kamili anachokihitaji mtoto katika miezi yake ya mwanzo.
  5. Maziwa ya mama yako tayari wakati wowote na yako katika hali ya joto linalomfaa mtoto.
  6. Huenda maziwa ya kutengenezwa yakamfanyia mtoto mzio (allergy), ama maziwa ya kifuani hayana matatizo kama hayo.
  7. Hupata hamu ya kupenda kula zaidi (appetite).      

 

Faida kwa mzazi

  1. Mama atapata himaya kutokana na maradhi ya saratani (cancer)
  2. Fuko la uzazi hurudi katika hali yake ya kawaida baada ya kunyonyesha.
  3. Mwili wa mama hupunguka uzito uliomzidi.     
  4. Ni njia ya kupunguza masarifu ya hela kwa kununua badala yake maziwa ya sinai  (ya kutengenezwa) na pia kuepukana na malipo ya hospitali kutokana na utafiti ulioonekana kwamba asilimia kubwa ya watoto wasionyonyeshwa hupata maradhi mara kwa mara.
  5. Kujipunguzia kazi za kutengeneza maziwa ya sinai (ya kutengenezwa) na kupata faida ya wakati zaidi, kwani ya kifuani yako tayari hayahitaji wakati wa kutengeneza, mbali pia kujiepusha na kazi za kukosha chupa na vifaa vya maziwa ya sinai.
  6. Wakati wowote, mahali popote yako tayari hana haja mama ya kubeba chupa za maziwa anapotoka nje au anapokuwa safarini.

 

Faida baina ya mama na mtoto

  1. Mtoto na mama wote kupata utulivu na kutulia nafsi.
  2. Huathiri mapenzi baina yao yakawa makubwa zaidi.
  3. Mama huridhika kuwa ameitumia Rahma na neema ya Allah (Subhaana wa Ta'aalah) na hutosheka kuwa ametimiza wajibu wake kwa mwanawe kwani wengi wanaoacha kunyonyesha huja kujuta baadaye. 

 [Imekusanywa na Alhidaaya.com]

 

 

Share

234-Aayah Na Mafunzo: Hikma Ya Eda Ya Mjane Kuwa Miezi Minne Na Siku Kumi

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

 

 

Hikma Ya Eda Ya Mjane Kuwa Miezi Minne Na Siku Kumi

 

 www.alhidaaya.com

 

وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا ۖ فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا فَعَلْنَ فِي أَنفُسِهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿٢٣٤﴾

234. Na wale wanaofishwa miongoni mwenu na wakaacha wake, hao wake wangojee peke yao (eda) miezi minne na siku kumi. Watakapofikia muda wao, si dhambi kwao katika yale waliyoyafanya katika nafsi zao kwa ada ya shariy’ah. Na Allaah kwa yale myatendayo ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.

Mafunzo:

 

Hikma ya kufaridhiwa eda miezi minne na siku kumi:  Sa’iyd bin Muswayyib, Abuu ‘Aaliyah na wengineo wamesema kuwa: Hikma ya kuifanya eda ya mjane kuwa ni miezi minne na siku kumi ni kuwa yawezekana kuwepo mimba. Mwanamke anaposubiri kwa kipindi hicho itathibitika kama ana mimba. Na dalili ni Hadiyth ifuatayo:

عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: حَدَّثَنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم -وَهُوَ الصَّادِقُ الْمَصْدُوقُ: ((إِنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ فِي بَطْنِ أُمِّهِ أَرْبَعِينَ يَوْمًا نُطْفَةً، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يُرْسَلُ إلَيْهِ الْمَلَكُ فَيَنْفُخُ فِيهِ الرُّوحَ،  رواه البخاري ومسلم

Kutoka kwa Abuu 'Abdir-Rahmaan 'Abdillaah bin Mas-‘uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: “Ametusimulia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ambaye ni mkweli mwenye kuaminiwa: “Hakika kila mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake siku arubaini akiwa ni mkusanyiko wa mbegu (za uzazi za mama na baba), kisha arubaini zifuatazo huwa ni donge la damu, kisha arubaini zijazo huwa pande la nyama, kisha Allaah Humtuma Malaika kwake na kumpulizia roho yake))   [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share

236-Mataa'u (Kiliwazo, Kitoka Nyumba, Masurufu) Ya Kumpa Mke Anayetalikiwa

Aayah Na Mafunzo

 

Al-Baqarah

 

 Mataa'u  au Mut'ah Atw-Twalaaq (Kiliwazo, Kitoka Nyumba, Masurufu)

Ya Kumpa Mke Anayetalikiwa

 

www.alhidaaya.com

 

 

لَّا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِن طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ مَا لَمْ تَمَسُّوهُنَّ أَوْ تَفْرِضُوا لَهُنَّ فَرِيضَةً ۚ وَمَتِّعُوهُنَّ عَلَى الْمُوسِعِ قَدَرُهُ وَعَلَى الْمُقْتِرِ قَدَرُهُ مَتَاعًا بِالْمَعْرُوفِ ۖ حَقًّا عَلَى الْمُحْسِنِينَ ﴿٢٣٦﴾

236. Hakuna dhambi kwenu mkiwatalaki wanawake ambao hamkuwagusa au kuwabainishia kwao mahari. Wapeni kiliwazo kwa mwenye wasaa kadiri ya uwezo wake na mwenye dhiki kadiri ya uwezo wake. Maliwaza kwa mujibu wa ada, ni haki kwa wafanya ihsaan.

 

 

وَإِن طَلَّقْتُمُوهُنَّ مِن قَبْلِ أَن تَمَسُّوهُنَّ وَقَدْ فَرَضْتُمْ لَهُنَّ فَرِيضَةً فَنِصْفُ مَا فَرَضْتُمْ إِلَّا أَن يَعْفُونَ أَوْ يَعْفُوَ الَّذِي بِيَدِهِ عُقْدَةُ النِّكَاحِ ۚ وَأَن تَعْفُوا أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ ۚ وَلَا تَنسَوُا الْفَضْلَ بَيْنَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٢٣٧﴾ 

237. Na mkiwataliki kabla ya kuwagusa na mkawa mmeshawabainishia kwao mahari, basi (wapeni) nusu ya hayo mliyobainisha isipokuwa wakisamehe au asamehe yule ambaye fungamano ya ndoa liko mikononi mwake. Na mkisamehe ni ukaribu zaidi ya taqwa. Na wala msisahau fadhila baina yenu. Hakika Allaah kwa myatendayo ni Mwenye kuona.

 

 

Mafunzo:

 

Mukhtasari Wa Mataa'u  au Mut'ah Atw-Twalaaq (Kiliwazo, Kitoka Nyumba, Masurufu) Ya Kumpa Mke Anayeachwa

 

Hali Ya 1:

Nikaah imefungwa, maingiliano hayakutendeka, mahari hayakubainishwa.

Hukmu Yake: Kadiri ya uwezo wa mume na pia mwanamke hahitaji kukaa eda.

 

Hali Ya 2:

Nikaah imefungwa, maingiliano hayakutendeka, mahari yamebainishwa.

Hukmu Yake: Nusu Ya mahari yaliyobainishwa. Pia hana haja ya kukaa eda.

 

Hali Ya 3:

Nikaah imefungwa, maingiliano yametendekea, mahari yamebainishwa.

Hukmu yake: Apewe mahari kamili.

 

Hali ya 4:

Nikaah imefungwa, maingiliano yametendeka, mahari hayakubainishwa.

Hukmu yake: Apewe mahari yanayolingana na mahari waliopewa wanawake wengine katika familia yake.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share

238-Aayah Na Mafunzo: Umuhimu Wa Kuhifadhi Swalaah Ya Alasiri

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

 

 

Umuhimu Wa Kuhifadhi Swalaah Ya Alasiri

 www.alhidaaya.com

 

 

حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ﴿٢٣٨﴾

238. Shikamaneni na Swalaah na khaswa Swalaah ya katikati (Alasiri), na simameni mbele ya Allaah katika hali ya utiifu.

 

 

Mafunzo:

 

Umuhimu wa Swalaah ya ‘Alasiri: Ibn ‘Umar (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mwenye kupitwa na Swalaah ya Alasiri ni kama amedhulumiwa watu wake na mali yake.” [Al-Bukhaariy (552)]

 

 

 

Share

245-Aayah Na Mafunzo: Kutoa Kwa Ajili Ya Allaah Ni Kuzidishwa Mali Na Fadhila Tele Nyenginezo

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Kutoa Kwa Ajili Ya Allaah Ni Kuzidishwa Mali Na Fadhila Tele Nyenginezo

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

مَّن ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا فَيُضَاعِفَهُ لَهُ أَضْعَافًا كَثِيرَةً ۚ وَاللَّـهُ يَقْبِضُ وَيَبْسُطُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٢٤٥﴾

245. Ni nani atakayemkopesha Allaah mkopo mzuri kisha (Allaah) Amzidishie mzidisho mwingi. Na Allaah Anakunja na Anakunjua, na Kwake mtarejeshwa.

 

 

Fadhila tele zimetajwa katika Qur-aan na Sunnah kuhusu kutoa mali katika njia ya Allaah; miongoni mwazo ni

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((مَا نَقَصَتْ صَدَقَةٌ مِنْ مَالٍ  وَمَا زَادَ اللَّهُ عَبْدًا بِعَفْوٍ إلاَّ عِزًّا  وَمَا تَوَاضَعَ أَحَدٌ لِلَّهِ إِلاَّ رَفَعَهُ اللَّهُ عَزَّ وَ جَلَّ)) مسلم        

  

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu)  kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kutoa swadaqah hakupunguzi mali, Allaah Humzidishia mja ‘izzah (utukufu) kwa ajili ya kusamehe kwake.  Na   yeyote anayenyenyekea kwa ajili ya Allaah, Allaah (عزّ وجلّ) Atampandisha Daraja [Atamtukuza] [Muslim]

 

 

 

Pia:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((مَا مِنْ يَوْمٍ يُصْبِحُ الْعِبَادُ فِيهِ إلاَّ مَلَكَانِ يَنْزِلاَنِ فَيَقُولُ أَحَدُهُمَا: اللَّهُمَّ أَعْطِ مُنْفِقًا خَلَفًا. وَيَقُولُ الأَخَرُ: اللَّهُمَّ أَعْطِ مُمْسِكًا تَلَفًا)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)  kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Kila siku inayowapambaukia watu kuna Malaika wawili wanateremka, mmoja wao akiomba: Ee Allaah! Mwenye kutoa [sadaka] mlipe zaidi. Na mwengine huomba: Ee Allaah! Mwenye kuzuia mpe hasara)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share

252-Aayah Na Mafunzo: Miongoni Mwa Fadhila Za Nabiy Ni Kupewa Mambo Matano

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Miongoni Mwa Fadhila Za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

Ni Kupewa Mambo Matano Ambayo Hakupewa Nabiy Yeyote

 

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa):

 

تِلْكَ آيَاتُ اللَّـهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِالْحَقِّ ۚ وَإِنَّكَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٢٥٢﴾

252. Hizo ni Aayaat za Allaah Tunakusomea (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa haki. Na hakika wewe ni miongoni mwa Rusuli.

 

 

Mafunzo:

 

عن جَابِرُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((أُعْطِيتُ خَمْسًا لَمْ يُعْطَهُنَّ أَحَدٌ قَبْلِي،  نُصِرْتُ بِالرُّعْبِ مَسِيرَةَ شَهْرٍ، وَجُعِلَتْ لِيَ الأَرْضُ مَسْجِدًا وَطَهُورًا، فَأَيُّمَا رَجُلٍ مِنْ أُمَّتِي أَدْرَكَتْهُ الصَّلاَةُ فَلْيُصَلِّ، وَأُحِلَّتْ لِيَ الْمَغَانِمُ وَلَمْ تَحِلَّ لأَحَدٍ قَبْلِي، وَأُعْطِيتُ الشَّفَاعَةَ، وَكَانَ النَّبِيُّ يُبْعَثُ إِلَى قَوْمِهِ خَاصَّةً، وَبُعِثْتُ إِلَى النَّاسِ عَامَّةً))

Jaabir bin Abdillah amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Nimepewa mambo matano hakupewa yoyote kabla yangu; Nimenusuriwa na (kutiwa) kiwewe (nyoyoni mwa maadui) kwa mwendo wa mwezi. Na nimefanyiwa ardhi kuwa sehemu ya kufanyia ‘ibaadah na kujitwaharishia, basi mtu mtu yeyote katika ummah wangu akifikiwa na Swalaah, aswali. Na nimehalalishiwa ngawira hazikuwa halali kwa yeyote kabla yangu. Na nimepewa shafaa’ah (maombezi Siku ya Qiyaamah). Na alikuwa Nabiy akitumwa kwa watu wake pekee, lakini mimi nimetumwa kwa watu wote.” [Al-Bukhaariy (5011)]  

 

 

 

Share

253-Aayah Na Mafunzo: Aina Mbali Mbali Za Kufadhilishwa Manabii

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

 

Aina Mbali Mbali Za Kufadhilishwa Manabii

 

 www.alhidaaya.com

 

 

تِلْكَ الرُّسُلُ فَضَّلْنَا بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۘ مِّنْهُم مَّن كَلَّمَ اللَّـهُ ۖ وَرَفَعَ بَعْضَهُمْ دَرَجَاتٍ ۚ وَآتَيْنَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ وَأَيَّدْنَاهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ ۗ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا اقْتَتَلَ الَّذِينَ مِن بَعْدِهِم مِّن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ وَلَـٰكِنِ اخْتَلَفُوا فَمِنْهُم مَّنْ آمَنَ وَمِنْهُم مَّن كَفَرَ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا اقْتَتَلُوا وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَفْعَلُ مَا يُرِيدُ ﴿٢٥٣﴾

253. Hao ni Rusuli, Tumewafadhilisha baadhi yao juu ya baadhi. Miongoni mwao kuna aliyesemeshwa na Allaah, na Akawapandisha baadhi yao vyeo. Na Tukampa ‘Iysaa mwana wa Maryam hoja bayana na Tukamtia nguvu kwa Ruwhil-Qudus (Jibriyl (عليه السلام. Na lau Angelitaka Allaah wasingelipigana wale wa baada yao, baada ya kuwajia hoja bayana. Lakini walikhitalifiana, basi miongoni mwao ambao walioamini na miongoni mwao waliokufuru. Na lau Angelitaka Allaah wasingelipigana lakini Allaah Anafanya Ayatakayo.

 

Mafunzo:

 

Maana inayokusudiwa katika Aayah hii ni Hadiyth ambayo Swahiyh mbili ziliikusanya kutoka kwa Abuu Hurayrah ambaye amehadithia: Wakati fulani Muislamu na Yahudi walikuwa wakibishana. Yahudi akaapa: “Hapana! Naapa kwa (Allaah) Ambaye Alimteua Muwsaa (عليه السلام) kuwa mbora kwa walimwengu wote.” Muislamu aliinua mkono wake akampiga Yahudi kibao usoni, kisha akasema: “Amemzidi Muhammad pia ewe khabithi!” Yahudi akaenda kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumlalamikia. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Msinifidhalishe zaidi juu ya Manabii kwani watu watapoteza fahamu Siku ya kufufuliwa (Qiyaamah) na nitakuwa wa kwanza kuzindukana na nitamkuta Muwsaa ameshika nguzo ya ‘Arsh. Sitojua kama Muwsaa (عليه السلام) alizindukana kabla yangu ama kulimtosha kupoteza kwake fahamu kulikompata mlimani. Hivyo misnitukuze juu ya Manabii.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

 

Share

254-Aayah Na Mafunzo: Kukimbilia Kutoa Swadaqah Kabla Ya Kufariki

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Kukimbilia Kutoa Swadaqah Kabla Ya Kufariki

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa:)

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِمَّا رَزَقْنَاكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ يَوْمٌ لَّا بَيْعٌ فِيهِ وَلَا خُلَّةٌ وَلَا شَفَاعَةٌ ۗ وَالْكَافِرُونَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٢٥٤﴾

254. Enyi walioamini! Toeni katika Tulivyokuruzukuni kabla haijafika Siku ambayo hakutokuweko mapatano humo wala urafiki wala uombezi. Na makafiri wao ndio madhalimu.

 

 

Mafunzo:

 

عن أبي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النَّبِيِّ (صلى الله عليه و آله وسلم) فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ, أَيُّ الصَّدَقَةِ أَعْظَمُ أَجْرًا؟ قَالَ: ((أَنْ تَصَدَّقَ وَأَنْتَ صَحِيحٌ شَحِيحٌ تَخْشَى الْفَقْرَ وَتَأْمُلُ الْغِنَى وَلاَ تُمْهِلُ حَتَّى إِذَا بَلَغَتْ الْحُلْقُومَ قُلْتَ لِفُلاَنٍ كَذَا وَلِفلاَنٍ كَذَا وَقَدْ كَانَ لِفُلاَنٍ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه)  amesema: “Mtu mmoja alikuja kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwuliza: Ee Rasuli wa Allaah! Ni sadaka ipi yenye ujira mkubwa zaidi?  Akasema: ((Ni utoe swadaqah nawe umzima, unataka mali bado, unakhofia ufukara na unatarajia utajiri. Wala usichelewe mpaka roho ikafika kwenye koo, ukaanza kusema: fulani ana haki kadhaa na fulani ana haki kadhaa na fulani alikuwa ana haki kadhaa)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na Anasema Allaah ('Azza wa Jalla):

 

وَأَنفِقُوا مِن مَّا رَزَقْنَاكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ فَيَقُولَ رَبِّ لَوْلَا أَخَّرْتَنِي إِلَىٰ أَجَلٍ قَرِيبٍ فَأَصَّدَّقَ وَأَكُن مِّنَ الصَّالِحِينَ﴿١٠﴾

Na toeni katika yale Tuliyokuruzukuni kabla hayajamfikia mmoja wenu mauti akasema: “Rabb wangu! Lau Ungeliniakhirisha mpaka muda wa karibu hivi, basi ningetoa swadaqah na ningelikuwa miongoni mwa Swalihina.” [Al-Munaafiquwn: 10]

 

 

 

 

 

Share

255-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Aayatul-Kursiyy Na Kuweko Jina Tukufu Kabisa La Allaah

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Fadhila Za Aayatul-Kursiyy Na Kuweko Jina Tukufu Kabisa La Allaah

 

 

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ ﴿٢٥٥﴾

255. Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Aliyehai daima, Msimamia kila kitu. Haumchukui usingizi wala kulala. Ni Vyake pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Nani huyu ambaye anashufai mbele Yake bila ya idhini Yake. Anajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawawezi kufikia kuelewa chochote kuhusu ujuzi Wake isipokuwa kwa Alitakalo. Imeenea Kursiyy Yake mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo. Naye ni Mwenye Uluwa, Ametukuka, Adhimu; Mkuu kabisa.

 

Mafunzo:

 

Aayah hii ndiyo Aayah adhimu kabisa katika Qur-aan kwa dalili ya Hadiyth ya Muslim (810) kutoka kwa ‘Abdullaahi bin Rabaah Al-Answaariy kutoka kwa ‘Ubayy bin Ka’ab ambaye amehadithia: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Yaa Abal-Mundhir! Hivi unajua ni Aayah gani ndani ya Kitabu cha Allaah kuwa ni adhimu kabisa?” Akasema: Nikasema: Allaah na Rasuli Wake ni wajuzi zaidi. “Yaa Abal-Mundhir! Hivi unajua ni Aayah gani ndani ya Kitabu cha Allaah kuwa ni adhimu kabisa?” Akasema: Nikasema: Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Aliyehai daima, Msimamia kila kitu” (mpaka mwisho wa Aayah). Akasema Ubayy: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akanipiga kifuani kisha akasema: “Wa-Allaahi upongezwe kwa ‘ilmu yako yaa Abal-Mundhir.” [Muslim] na katika mapokezi ya Ahmad imeendelea: “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, Aayah hii ina ulimi na midomo miwili ambao inamtukuza Mfalme (Allaah) katika mguu wa Arsh.”  [Swahiyh At-Targhiyb (1471)]

 

Pia, zimetajwa katika Sunnah, fadhila zake kadhaa, zifutazo ni baadhi yake:

 

“Atakayeisoma anapoamka asubuhi itamkinga na majini mpaka itakapofika jioni. Na atakayeisoma jioni atakingwa nao mpaka asubuhi.” [Al-Haakim (1/562) Taz. Swahiyh At-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/273)]

 

”Atakayezisoma mara tatu asubuhi na jioni  zitamtosheleza kwa kila kitu.” [Abuu Daawuwd (4/322) [5082], At-Tirmidhiy (5/567) [3575], Taz. Swahiyh At-Tirmidhiy (3/182)]

 

Pia, Aayah hii ina Jina tukufu kabisa la Allaah katika kauli Yake (تعالى): ”Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Aliyehai daima, Msimamia kila kitu” na  dalili ni:

 

Abuu Umaamah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:  ”Jina Tukufu  kabisa la Allaah  Ambalo likiombewa kwalo Anaitikia limo katika Suwrah tatu; Al-Baqarah, Aal-‘Imraan, na Twaahaa’. [At-Tirmdhiy, Silsilah Asw-Swahiyhah (746)] Na mapokezi mengineyo yaliyothibitisha kuhusu Ismul-A’dhwam (Jina tukufu kabisa).

 

Kuhusu kauli ya Allaah (تعالى): ((Imeenea Kursiyy Yake mbingu na ardhi)) Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: “Iwapo mbingu saba na ardhi saba zingekunjuliwa na kulazwa sambamba, basi zingefikia kipimo cha (udogo wa) pete katika jangwa, kulinganisha na ‘Arsh.” [Ibn Abiy Haatim (3/981)]

 

 

Share

257-Aayah Na Mafunzo: Du’aa Ya Kuomba Kutolewa Kizani Na Kuingia Katika Nuru

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

 

Du’aa Ya Kuomba Kutolewa Kizani Na Kuingia Katika Nuru

 

www.alhidaaya.com

 

 

 اللَّـهُ وَلِيُّ الَّذِينَ آمَنُوا يُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَوْلِيَاؤُهُمُ الطَّاغُوتُ يُخْرِجُونَهُم مِّنَ النُّورِ إِلَى الظُّلُمَاتِ ۗ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٥٧﴾

257. Allaah ni Mlinzi Msaidizi wa wale walioamini, Anawatoa kutoka katika viza na kuwaingiza katika Nuru. Na wale waliokufuru marafiki wao wandani ni twaghuti, huwatoa kutoka katika Nuru na kuwaingiza katika viza. Hao ni watu wa motoni wao humo ni wenye kudumu.

 

Mafunzo:

 

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas’uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitufundisha maneno mengine lakini hakuyafundisha kama alivyokuwa akitufundisha tashahhud: 

 

((اللَّهُمَّ أَلِّفْ بَيْنَ قُلُوبِنَا وَأَصْلِحْ ذَاتَ بَيْنِنَا وَاهْدِنَا سُبُلَ السَّلاَمِ وَنَجِّنَا مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ وَجَنِّبْنَا الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَبَارِكْ لَنَا فِي أَسْمَاعِنَا وَأَبْصَارِنَا وَقُلُوبِنَا وَأَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا وَتُبْ عَلَيْنَا إِنَّكَ أَنْتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ وَاجْعَلْنَا شَاكِرِينَ لِنِعْمَتِكَ مُثْنِينَ بِهَا قَابِلِيهَا وَأَتِمَّهَا عَلَيْنَا))

Allaahumma allif bayna quluwbinaa, wa Aswlih dhaata bayninaa, wahdinaa subulas-ssalaami, wanajjinaa minadhw-dhwulumaati ilan-nnuwri, wa jannibnal-fawaahisha maa dhwahara minhaa wamaa batwan, wa Baarik-lanaa fiy asmaa’inaa, wa abswaarinaa, wa quluwbinaa, wa azwaajinaa, wa dhurriyaatinaa, watub ‘alaynaa Innaka Antat-Tawaabur-Rahiym, waj-’alnaa shaakiriyna lini’matika muthniyna bihaa qaabiliyhaa wa atimmahaa ‘alaynaa

 

Ee Allaah! Unganisha baina ya nyoyo zetu, na Suluhisha yaliyo baina yetu, na Tuongoze njia za amani, na Tuokoe kutokana na viza Utuingize katika Nuru, na Tuepushe machafu ya dhahiri na ya siri, na Tubarikie katika kusikia kwetu na kuona kwetu, nyoyo zetu, na wake zetu, na vizazi vyetu, na Tupokelee tawbah zetu, hakika Wewe ni At-Tawwaabur-Rahiym  (Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye Kurehemu), na Tujaalie kuwa wenye kushukuru neema Zako, wenye kuzielezea kwa uzuri, wenye kuzipokea (kwa shukrani), na Zitimize kwetu.

 

[Abuu Daawuwd, Al-Haakim akasema ‘Swahiyh kwa sharti ya Muslim, na ameikubali Adh-Dhahabiy (1/265) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Adab Al-Mufrad (490)].

 

 

Share

261-Aayah Na Mafunzo: Kutoa Mali Kwa Ajili Ya Allaah Ni Kuzidishiwa Mara Mia Saba

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

 

Kutoa Mali Kwa Ajili Ya  Allaah Ni Kuzidishiwa Mara Mia Saba

 

www.alhidaaya.com

 

 

 Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

مَّثَلُ الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ كَمَثَلِ حَبَّةٍ أَنبَتَتْ سَبْعَ سَنَابِلَ فِي كُلِّ سُنبُلَةٍ مِّائَةُ حَبَّةٍ ۗ وَاللَّـهُ يُضَاعِفُ لِمَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٦١﴾ 

261. Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Allaah ni kama mfano wa punje moja ya mbegu iliyotoa mashuke saba, katika kila shuke kuna punje mia. Na Allaah Humzidishia Amtakaye; na Allaah ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote.

 

Mafunzo:

 

Faida: Thawabu za kutoa kwa ajili ya Allaah: Aayaah kadhaa na Hadiyth zimetaja fadhila za kutoa mfano wa Hadiyth ni: ‘Uqbah bin ‘Amru bin Tha’alabah Abuu Mas‘uwd (رضي الله عنه) amehadithia kuwa mtu alitoa ngamia na hatamu yake kwa ajili ya Allaah, na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Siku ya Qiyaamah utakuwa na ngamia mia saba pamoja na hatamu zao.” [Swahiyh An-Nasaaiy (3187)]

 

Pia: Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Kutoa swadaqah hakupunguzi mali, Allaah Hamzidishii mja msamaha ila Humpa utukufu, na yeyote anayenyenyekea kwa ajili ya Allaah, Allaah Aliyetukuka Atampandisha Daraja.” [Muslim] 

 

 

Share

262-Aayah Na Mafunzo: Anayesimbulia Alichotoa Hatotazamwa Na Allaah Siku Ya Qiyaamah

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Anayesimbulia Alichotoa Hatotazamwa Na Allaah Siku Ya Qiyaamah

 

 

 

الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ثُمَّ لَا يُتْبِعُونَ مَا أَنفَقُوا مَنًّا وَلَا أَذًى ۙ لَّهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٢٦٢﴾

262. Wale wanaotoa mali zao katika njia ya Allaah kisha hawafuatishii kwa waliyoyatoa masimbulizi wala udhia watapa ujira wao kwa Rabb wao, na wala hakuna khofu juu yao na wala hawatohuzunika.

 

Mafunzo:

 

 

Abuu Dharr (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Watu watatu Allaah Hatowazungumzisha Siku ya Qiyaamah, wala Hatowatazama, wala Hatowatakasa, na watapata adhabu inayoumiza.” Akayakariri maneno hayo mara tatu. Abuu Dharr akasema: Wamepita patupu na wamekhasirika! Ni nani hao Ee Rasuli wa Allaah?  Akasema: “Al-Musbil (mwenye kuburuza nguo yake), mwenye kutoa kisha akasimbulia alichokitoa, na mwenye kuuza bidhaa zake kwa kutumia kiapo cha uongo.” [Muslim]

 

 

 

Share

264-Aayah Na Mafunzo: Mfano Anayetoa Swadaqah Kwa Riyaa Kuwa Hapati Thawabu

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Mfano Anayetoa Swadaqah Kwa Riyaa (Kujionyesha) Kuwa Hapati Thawabu

 

 Alhidaaya.com

 

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُبْطِلُوا صَدَقَاتِكُم بِالْمَنِّ وَالْأَذَىٰ كَالَّذِي يُنفِقُ مَالَهُ رِئَاءَ النَّاسِ وَلَا يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ صَفْوَانٍ عَلَيْهِ تُرَابٌ فَأَصَابَهُ وَابِلٌ فَتَرَكَهُ صَلْدًا ۖ لَّا يَقْدِرُونَ عَلَىٰ شَيْءٍ مِّمَّا كَسَبُوا ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ ﴿٢٦٤﴾

264. Enyi walioamini! Msibatilishe swadaqah zenu kwa masimbulizi na udhia kama yule ambaye anatoa mali yake kwa kujionyesha kwa watu wala hamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Basi mfano wake ni kama jabali juu yake pana udongo, kisha likapigwa na mvua kubwa ikaliacha tupu. Hawana uwezo juu ya lolote katika waliyoyachuma. Na Allaah Haongoi watu makafiri.

 

 

Mafunzo:

 

عنْ ابي هريرة رضي الله عنه أنَّه صلَّى الله عليه وسلَّم قال: ((قال الله تعالى: أنا أغْنى الشُّركاء عن الشِّرْك، فمَن عمل عملاً أشْرَك فيه معي غيري تركتُه وشِرْكه))    

Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Allaah Ta’aalaa Anasema: Mimi Ni Mwenye kujitosheleza kabisa, Sihitaji msaada wala mshirika. Kwa hiyo, yule afanyaye amali kwa kunishirikisha na mtu, Nitaikanusha pamoja na mshirika wake.”  Yaani: hatopata ujira wowote kwa amali hiyo. [Muslim (2985), Ibn Maajah (4202)]

 

 

Share

265-Aayah Na Mafunzo: Mfano Wa Anayetoa Swadaqah Kwa Ikhlaasw Hulipwa Maradufu

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Mfano Wa Anayetoa Swadaqah Kwa Ikhlaasw Hulipwa Maradufu

 

www.alhidaaya.com

 

 

  وَمَثَلُ الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ وَتَثْبِيتًا مِّنْ أَنفُسِهِمْ كَمَثَلِ جَنَّةٍ بِرَبْوَةٍ أَصَابَهَا وَابِلٌ فَآتَتْ أُكُلَهَا ضِعْفَيْنِ فَإِن لَّمْ يُصِبْهَا وَابِلٌ فَطَلٌّ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٢٦٥﴾

265. Na mfano wa wale wanaotoa mali zao kutafuta radhi za Allaah na kujithibitisha nafsi zao ni kama mfano wa bustani iliyoko pahala paliponyanyuka; ikafikiwa hiyo bustani na mvua kubwa, ikatoa mazao yake maradufu, na hata kama haikufikiwa na mvua kubwa basi mvua ndogo huitosheleza. Na Allaah kwa muyatendayo ni Mwenye kuona.

 

Mafunzo:

 

Pia anayetoa kwa ikhlaasw na kwa kuficha kabisa swadaqah yake atakuwa miongoni mwa watu saba watakaokuwa katika kivuli cha Allaah ('Azza wa Jalla) Siku ambayo hakutokuwa na kivuli isipokuwa kivuli Chake.

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ   ((سَبْعَةٌ يُظِلُّهُمْ اللَّهُ فِي ظِلِّهِ يَوْمَ لا ظِلَّ إِلا ظِلُّهُ: الإِمَامُ الْعَادِلُ، وَشَابٌّ نَشَأ فِي عِبَادَةِ رَبِّهِ، وَرَجُلٌ قَلْبُهُ مُعَلَّقٌ فِي الْمَسَاجِدِ، وَرَجُلَانِ تَحَابَّا فِي اللَّهِ اجْتَمَعَا عَلَيْهِ وَتَفَرَّقَا عَلَيْهِ، وَرَجُلٌ طَلَبَتْهُ امْرَأَةٌ ذَاتُ مَنْصِبٍ وَجَمَالٍ فَقَالَ إِنِّي أَخَافُ اللَّهَ، وَرَجُلٌ تَصَدَّقَ بِصَدَقَةٍ فَأَخْفَاهَا حَتَّى لا تَعْلَمَ شِمَالُهُ مَا تُنْفِقُ يَمِينُهُ، وَرَجُلٌ ذَكَرَ اللَّهَ خَالِيًا فَفَاضَتْ عَيْنَاهُ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Watu saba Allaah  Atawafunika katika kivuli Chake, Siku ambayo hakutokuwa na kivuli ila kivuli Chake: Imaam muadilifu, kijana ambaye amekulia katika ‘Ibaadah ya Rabb wake, Mtu ambaye moyo wake umeambatana na Misikiti, watu wawili wanaopendana kwa ajili ya Allaah; wanakutana kwa ajili Yake na wanafarikiana kwa ajili Yake, mwanamme aliyetakwa na mwanamke mwenye hadhi na mrembo wa kuvutia akasema: "Mimi namkhofu Allaah!" Mtu aliyetoa Swadaqah yake akaificha hadi kwamba mkono wake wa kushoto usijue nini ulichotoa mkono wake wa kulia, na mtu aliyemdhukuru Allaah kwa siri macho yake yakatokwa machozi)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Share

266-Aayah Na Mafunzo: Mfano Wa Tajiri Anayemuasi Allaah Mpaka Zikapotea ‘Amali Zake

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Mfano Wa Tajiri Anayemuasi Allaah Mpaka Zikapotea ‘Amali Zake

 

www.alhidaaya.com

 

 

 أَيَوَدُّ أَحَدُكُمْ أَن تَكُونَ لَهُ جَنَّةٌ مِّن نَّخِيلٍ وَأَعْنَابٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ لَهُ فِيهَا مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ وَأَصَابَهُ الْكِبَرُ وَلَهُ ذُرِّيَّةٌ ضُعَفَاءُ فَأَصَابَهَا إِعْصَارٌ فِيهِ نَارٌ فَاحْتَرَقَتْ ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ ﴿٢٦٦﴾

 

266. Je! Anapenda mmoja wenu awe ana bustani ya mitende na mizabibu ipitayo chini yake mito; anayo humo kila aina ya mazao; ukamfikia uzee, naye ana kizazi dhaifu; kisha ikapigwa na kimbunga cha moto kikaiteketeza? Hivyo ndivyo Allaah Anavyobainisha Aayaat (ishara, zingatio n.k) kwenu mpate kutafakari.

 

 

Mafunzo:

 

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ،‏.‏ قَالَ وَسَمِعْتُ أَخَاهُ أَبَا بَكْرِ بْنَ أَبِي مُلَيْكَةَ، يُحَدِّثُ عَنْ عُبَيْدِ بْنِ عُمَيْرٍ، قَالَ:  قَالَ عُمَرُ رضى الله عنه يَوْمًا لأَصْحَابِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم:  فِيمَ تَرَوْنَ هَذِهِ الآيَةَ نَزَلَتْ ‏ ((أَيَوَدُّ أَحَدُكُمْ أَنْ تَكُونَ لَهُ جَنَّةٌ‏))‏ قَالُوا اللَّهُ أَعْلَمُ‏.‏ فَغَضِبَ عُمَرُ فَقَالَ: قُولُوا نَعْلَمُ أَوْ لاَ نَعْلَمُ‏.‏ فَقَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ: فِي نَفْسِي مِنْهَا شَىْءٌ يَا أَمِيرَ الْمُؤْمِنِينَ‏.‏ قَالَ عُمَرُ: يَا ابْنَ أَخِي قُلْ وَلاَ تَحْقِرْ نَفْسَكَ‏.‏ قَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ: ضُرِبَتْ مَثَلاً لِعَمَلٍ‏.‏ قَالَ عُمَرُ أَىُّ عَمَلٍ قَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ لِعَمَلٍ‏.‏ قَالَ عُمَرُ: لِرَجُلٍ غَنِيٍّ يَعْمَلُ بِطَاعَةِ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ، ثُمَّ بَعَثَ اللَّهُ لَهُ الشَّيْطَانَ فَعَمِلَ بِالْمَعَاصِي حَتَّى أَغْرَقَ أَعْمَالَهُ‏.‏ ‏(‏فَصُرْهُنَّ‏)‏ قَطِّعْهُنَّ‏.‏

 

Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: Nilimsikia kaka yake Abuu Bakr bin Abiy Mulaykah akihadithia kutoka kwa ‘Ubayd bin ‘Umayr kwamba: Siku moja ‘Umar (رضي الله عنه) aliwaambia Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Mnadhani Aayah hii imeteremka kwa ajili ya nani?” “Je, Anapenda mmoja wenu awe ana bustani…” Wakasema: “Allaah Ndiye Mjuzi.” ‘Umar akakasirika akasema: “Semeni tunajua au hatujui!.” Ibn ‘Abbaas akasema: Nimefikiri jambo katika nafsi yangu Ee Amiyrul-Muuminiyn.” ‘Umar akasema: “Ee mtoto wa ndugu yangu! Sema wala usiidharau nafsi yako.” Ibn ‘Abbaas akasema: “Imepigiwa mfano wa matendo.” ‘Umar akasema: “Matendo gani?” Ibn ‘Abbaas akasema: “Matendo.” ‘Umar akasema: “(Mfano) wa mtu tajiri anayemtii Allaah kisha Allaah Akamtumia shaytwaan, akafanya maasi mpaka ‘amali zake zote zikapotea” [Al-Bukhaariy]

 

 

Share

267-Aayah Na Mafunzo: Makatazo Ya Kutoa Swadaqah Ya Vitu Vibovu

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

 

Makatazo Ya  Kutoa Swadaqah Ya Vitu Vibovu

 

www.alhidaaya.com

 

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا كَسَبْتُمْ وَمِمَّا أَخْرَجْنَا لَكُم مِّنَ الْأَرْضِ ۖ وَلَا تَيَمَّمُوا الْخَبِيثَ مِنْهُ تُنفِقُونَ وَلَسْتُم بِآخِذِيهِ إِلَّا أَن تُغْمِضُوا فِيهِ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ حَمِيدٌ ﴿٢٦٧﴾

267. Enyi walioamini! Toeni katika vizuri mlivyochuma na katika ambavyo Tumekutoleeni kutoka katika ardhi. Na wala msikusudie vibaya kutoka humo mkavitoa na hali nyinyi wenyewe si wenye kuvichukuwa isipokuwa kuvifumbia macho. Na jueni kwamba hakika Allaah ni Mkwasi, Mwenye kustahiki kuhimidiwa.

 

Mafunzo:

 

 قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّ اللَّهَ طَيِّبٌ لاَ يَقْبَلُ إِلاَّ طَيِّبًا))

 

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:  

(Enyi watu, hakika Allaah ni Mzuri na Hapokei ila kilicho kizuri. [Muslim]

 

Share

268-Aayah Na Mafunzo: Tofauti Ya Taathira Ya Shaytwaan Na Ya Malaika Kwa Mwana Aadam

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Tofauti Ya Taathira Ya  Shaytwaan Na Ya Malaika Kwa Mwana Aadam

 www.alhidaaya.com

 

 

الشَّيْطَانُ يَعِدُكُمُ الْفَقْرَ وَيَأْمُرُكُم بِالْفَحْشَاءِ ۖ وَاللَّـهُ يَعِدُكُم مَّغْفِرَةً مِّنْهُ وَفَضْلًا ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٦٨﴾

268. Shaytwaan anakutishieni ufukara na anakuamrisheni machafu, (ubakhili), na Allaah Anakuahidini maghfirah kutoka Kwake na fadhila. Na Allaah ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote.

 

Mafunzo:

 

‘Abdullaah bin Mas‘uwd  (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika shaytwaan humwathiri mwana wa Aadam na Malaika pia humauthiri. Ama kuhusu athari za shaytwaan ni kutisha kwa mambo ya shari na kukadhibisha haki. Ama athari za Malaika ni ahadi ya mwisho mwema na kuamini haki. Yeyote anayeoona haya (athari za Malaika) basi ajue kuwa ni kutoka kwa Allaah na Amhimidi Allaah. Na anayeona ya mwanzo basi aombe kinga kwa Allaah dhidi ya shaytwaan.” Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasoma: “Shaytwaan anakutishieni ufukara na anakuamrisheni machafu, (ubakhili), na Allaah Anakuahidini maghfirah kutoka Kwake na fadhila.” [Ibn Haatim (3/1090) katika Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

 

Share

269-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Kujaaliwa Hikmah Na Du’aa Ya Kuomba Hikmah

 

Al-Baqarah

Fadhila Za Kujaaliwa Hikmah Na Du’aa Ya Kuomba Hikmah

 

 www.alhidaaya.com

 

 

يُؤْتِي الْحِكْمَةَ مَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُؤْتَ الْحِكْمَةَ فَقَدْ أُوتِيَ خَيْرًا كَثِيرًا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٢٦٩﴾

269. Humpa hikmah Amtakaye. Na anayepewa hikmah basi kwa yakini huwa amepewa khayr nyingi. Na hawakumbuki (na kuwaidhika) isipokuwa wenye akili.

 

Mafunzo:

 

Ibn Mas‘uwd  (رضي الله عنه) amehadithia kwamba alimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Hapana hasad ila katika mawili; mtu aliyeruzukiwa mali na Allaah na akaitumia kwa uadilifu, na mtu aliyepewa hikmah na Allaah na anahukmu kwayo na anawafundisha wengine.” [Ahmad (1/432) katika Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

الَّهُمَّ آتِنِي الْحِكْمَةَ الَّتِي مَنْ أُوتِيَهَا فَقَدْ أُوتِيَ خَيْرًا كَثِيرًا

Allaahumma aatinil-hikmatallaty man uwtiyahaa faqad uwtiya khayran kathiyraa

Ee Allaah, Nipe Hikma ambayo atakayepewa basi kwa yakini amepewa khayr nyingi. [Ad-Du’aa Minal-Kitaabi was Sunnah li Sa’iyd bin Wahf Al-Qahtwaaniy]

 

 

Share

271-Aayah Na Mafunzo: Anayetoa Swadaqah Kwa Kuficha Atakuwa Chini Ya Kivuli Cha Allaah

 

 

Al-Baqarah

Anayetoa Swadaqah Kwa Kuficha Atakuwa Chini Ya Kivuli Cha Allaah

 www.alhidaaya.com

 

إِن تُبْدُوا الصَّدَقَاتِ فَنِعِمَّا هِيَ ۖ وَإِن تُخْفُوهَا وَتُؤْتُوهَا الْفُقَرَاءَ فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۚ وَيُكَفِّرُ عَنكُم مِّن سَيِّئَاتِكُمْ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿٢٧١﴾

 271. Mkidhihirisha swadaqah basi ni vizuri hivyo, na mkizificha na kuwapa mafakiri, basi hilo ni kheri kwenu. Na Atakufutieni katika maovu yenu. Na Allaah kwa yale myatendayo ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika

 

 

Mafunzo:

 

Thawabu za kuficha ‘amali ya kutoa kwa ajili ya Allaah; Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:  ((Watu saba Allaah  Atawafunika katika kivuli Chake, Siku ambayo hakutokuwa na kivuli ila kivuli Chake: Imaam muadilifu, kijana ambaye amekulia katika ‘Ibaadah ya Rabb wake, Mtu ambaye moyo wake umeambatana na Misikiti, watu wawili wanaopendana kwa ajili ya Allaah; wanakutana kwa ajili Yake na wanafarikiana kwa ajili Yake, mwanamme aliyetakwa na mwanamke mwenye hadhi na mrembo wa kuvutia akasema: "Mimi namkhofu Allaah!" Mtu aliyetoa Swadaqah yake akaificha hadi kwamba mkono wake wa kushoto usijue nini ulichotoa mkono wake kulia, na mtu aliyemdhukuru Allaah kwa siri macho yake yakatokwa machozi)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Share

272-Aayah Na Mafunzo: Kutoa Swadaqah Kutaraji Wajihi Wa Allaah Ni Kupandishwa Daraja

 

 

Al-Baqarah

Kutoa Swadaqah Kutaraji Wajihi Wa Allaah Ni Kupandishwa Daraja

 Alhidaaya.com 

 

لَّيْسَ عَلَيْكَ هُدَاهُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۗ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ فَلِأَنفُسِكُمْ ۚ وَمَا تُنفِقُونَ إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ اللَّـهِ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لَا تُظْلَمُونَ ﴿٢٧٢﴾

272. Si juu yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwaongoa, lakini Allaah Humwongoa Amtakaye. Na chochote cha kheri mtoacho basi ni kwa ajili ya nafsi zenu. Na hamtoi ila kutaka Wajhi wa Allaah. Na chochote mtoacho katika kheri mtalipwa kamilifu nanyi hamtodhulumiwa.

Mafunzo:

 

Fadhila za kutoka swadaqah: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwambia Sa’d bin Abiy Waqqaasw (رضي الله عنه) alipomzuru mgonjwa (na mapokezi mengine alipokuwa Hijjatul-Widaa’): “Hutatoa swadaqah na huku ukitarajia Wajihi wa Allaah ila utapanda daraja ya juu kwa sababu yake ikiwa ni pamoja na kile unachokitoa kwenye kinywa cha mkeo.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Share

273-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Anayejizuia Na Kustahi Kuombaomba

 

Al-Baqarah

 Fadhila Za Anayejizuia Na Kustahi Kuombaomba

www.alhidaaya.com

 

 

لِلْفُقَرَاءِ الَّذِينَ أُحْصِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ لَا يَسْتَطِيعُونَ ضَرْبًا فِي الْأَرْضِ يَحْسَبُهُمُ الْجَاهِلُ أَغْنِيَاءَ مِنَ التَّعَفُّفِ تَعْرِفُهُم بِسِيمَاهُمْ لَا يَسْأَلُونَ النَّاسَ إِلْحَافًا ۗ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ ﴿٢٧٣﴾

273. (Swadaqah ni) Kwa ajili ya mafakiri waliozuilika katika njia ya Allaah hawawezi kwenda huku na kule katika ardhi (kutafuta rizki); asiyewajua huwadhania kuwa ni matajiri kutokana na staha ya kujizua kwao, unawatambua kwa alama zao, hawaombi watu kwa ung’ang’anizi. Na chochote mtoacho katika kheri basi Allaah kwacho ni Mjuzi.

Mafunzo:

 

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Si maskini anayewazungukia watu anarudishwa na tonge moja au mawili na tende moja au tende mbili, lakini maskini ni yule ambaye hapati chenye kumtosheleza, wala hajulikani ili apewe swadaqah wala hasimami kuwaomba watu.” [Al-Bukhaariy (1479)]

 

Abuu Sa’iyd alisema: “Mama yangu alinituma kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuomba msaada, lakini nilipofika nilikaa kitako, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliniangalia na kuniambia: “Yeyote anayeridhika, Allaah Atamtajirisha. Yule anayejistahi Allaah Atamfanya aheshimike. Anayewaomba watu ambapo ana kiasi kidogo, atakuwa ombaomba.” [Imaam Ahmad (3/9) - Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

Share

274-Aayah Na Mafunzo: Kutoa Swadaqah Hata Riyali Moja Ni Kheri

 

 

Al-Baqarah

Kutoa Swadaqah Hata Riyali Moja Ni Kheri

 

www.alhidaaya.com

 

 Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُم بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ سِرًّا وَعَلَانِيَةً فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ﴿٢٧٤﴾

274. Wale wanaotoa mali zao usiku na mchana, kwa siri na kwa dhahiri; watapata ujira wao kwa Rabb wao, na wala hakuna khofu juu yao na wala wao hawatohuzunika.

 

Mafunzo:

 

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mtu alisema: Nitatoa swadaqah usiku. Alitoka usiku na swadaqah yake ikamfikia mkononi mwa mzinzi mwanamke (bila ya kujua). Asubuhi, watu wakahadithia: Mzinzi amepewa swadaqah! Yule mtu akasema: Allaahumma Himdi ni Zako, kwa (kumpa swadaqah) mzinzi mwanamke. Leo usiku nitatoa swadaqah tena. Akatoa swadaqah yake na (bila kujua) ikafika mikononi mwa tajiri. Asubuhi yake (watu) wakahadithia: Usiku uliopita tajiri kapewa swadaqah! Akasema: Allaahumma Himdi ni Zako kwa (kumpa swadaqah) tajiri. Usiku nitatoa swadaqah. Hivyo alitoka na swadaqah yake (na bila ya kujua) ikamfikia mikononi mwa mwizi. Siku ya pili yake wakahadithia watu: Usiku uliopita mwizi alipewa swadaqah! Akasema: Allaahumma Himdi ni Zako, (nimempa swadaqah) mzinzi mwanamke, tajiri na mwizi. Kisha alimjia mtu na kumwambia: Swadaqah ulizotoa zimekubaliwa. Ama kuhusu mwanamke mzinzi, inaweza kumfanya kuacha uzinifu. Ama kuhusu tajiri, itamfanya kujifunza na kumfanya kutumia utajri wake aliopewa na Allaah. Ama mwizi inaweza kumfanya kuacha wizi.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share

275-Aayah Na Mafunzo: Adhabu Za Anayekula Ribaa Kurushiwa Mawe Mdomoni

 

Al-Baqarah

Adhabu Za Anayekula Ribaa Kurushiwa Mawe Mdomoni

 

www.alhidaaya.com

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

الَّذِينَ يَأْكُلُونَ الرِّبَا لَا يَقُومُونَ إِلَّا كَمَا يَقُومُ الَّذِي يَتَخَبَّطُهُ الشَّيْطَانُ مِنَ الْمَسِّ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا إِنَّمَا الْبَيْعُ مِثْلُ الرِّبَا ۗ وَأَحَلَّ اللَّـهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا ۚ فَمَن جَاءَهُ مَوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّهِ فَانتَهَىٰ فَلَهُ مَا سَلَفَ وَأَمْرُهُ إِلَى اللَّـهِ ۖ وَمَنْ عَادَ فَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٧٥﴾

275. Wale wanaokula ribaa hawatosimama (Siku ya Qiyaamah) ila kama anavyosimama yule aliyezugwa na shaytwaan kwa kuguswa na kupatwa. Hivyo kwa sababu wao wamesema: “Hakika biashara ni kama ribaa.” Na Allaah Amehalalisha biashara na Ameharamisha ribaa. Basi atakayefikiwa na mawaidha kutoka kwa Rabb wake akakoma (kula ribaa); basi ni yake yale yaliyopita, na hukumu yake iko kwa Allaah. Na atakayerudia basi hao ni watu wa motoni, wao humo ni wenye kudumu.

 

Mafunzo:

 

Samurah bin Jundub (رضي الله عنه) amehadithia Hadiyth ndefu kuhusu ndoto ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) (katika msafara wake wa Israa wal-Mi’raaj pamoja na Jibriyl ((عليه السلام “Tukafika kwenye mto. Nilidhani alisema: Mto ulikuwa mwekundu kama damu, na tukamuona mtu akiogelea mtoni, na kwenye kingo zake alikuwepo mtu mwengine aliyejikusanyia mawe mengi. Mtu ndani ya mto aliogelea kisha akaja kwa mtu aliyekusanya mawe na kufungua kinywa chake, na yule mtu mwengine akitupa mawe kinywani mwake.” Tafsiri yake kwamba huyo ni mla ribaa. [Fat-h Al-Baariy (3295)]

 

 

Share

276-Aayah Na Mafunzo: Ribaa Haizidishi Bali Inapunguza Na Kufilisi Mali

Al-Baqarah

Ribaa Haizidishi Bali Inapunguza Na Kufilisi Mali

 www.alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa:)

 

 يَمْحَقُ اللَّـهُ الرِّبَا وَيُرْبِي الصَّدَقَاتِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ ﴿٢٧٦﴾

276. Allaah Huifuta baraka (mali ya) ribaa na Huzibariki swadaqah. Na Allaah Hapendi kila kafiri apapiae madhambi.

 

Mafunzo:

 

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia:  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Yeyote anayetoa swadaqah inayolingana na tende, kutokana na mali ya halali, na Allaah Hakubali isipokuwa kilicho kizuri na safi, basi hakika Allaah Hukipokea kwa Mkono Wake wa kulia kisha Hukiinua kwa mtoaji, kama mtu anayemfuga mwanafarasi wake, mpaka inakuwa (swadaqah) hiyo kama mlima.” [Muslim katika kitaab cha Zakaah]

 

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakithirishi yeyote katika ribaa ispokuwa huwa mwisho wa jambo lake ni kupungukiwa na kufilisika katika mali.” [Ibn Maajah kutoka kwa Ibn Mas‘uwd  (رضي الله عنه)]

 

Share

278-Aayah Na Mafunzo: Matahadharisho Ya Ribaa Na Adhabu Zake

 

Al-Baqarah

Matahadharisho Ya Ribaa Na Adhabu Zake

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَذَرُوا مَا بَقِيَ مِنَ الرِّبَا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿٢٧٨﴾

278. Enyi walioamini! Mcheni Allaah na acheni yaliyobakia katika ribaa ikiwa nyinyi ni Waumini

 

 

 

Mafunzo:

 

‘Awn bin Abi Juhayf amehadithia kutoka kwa baba yake kuwa alinunua kijana (mtumwa) anayejua kuumika (hijaamah). Akasema: “Hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amekataza (kuchukua) thamani ya damu (malipo yatokanayo na kuumika), na thamani ya mbwa, na chumo la malaya na amemlaani mla ribaa na muwakilishi wake na mtu anayechora (ngozi za watu kwa kutia rangi ndani yake na mchorajwi na mchonga vinyago.” [Al-Bukhaariy]

 

 “Dirhamu ya ribaa anayokula mtu na huku anajua ni mbaya zaidi kuliko kuzini mara thelathini na sita.” [Ahmad]

 

“Ribaa ina milango 73 iliyo nyepesi na sahali ni mtu kumuoa mamake.” [Al-Haakim]

 

“Jiepusheni na mambo saba yenye kuangamiza… kula ribaa.”  [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Share

279-Aayah Na Mafunzo: Anayeshughulika Na Ribaa Ajitangazie Vita Na Allaah

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Anayeshughulika Na Ribaa Ajitangazie Vita Na Allaah

www.alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa:

 

فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا فَأْذَنُوا بِحَرْبٍ مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۖ وَإِن تُبْتُمْ فَلَكُمْ رُءُوسُ أَمْوَالِكُمْ لَا تَظْلِمُونَ وَلَا تُظْلَمُونَ ﴿٢٧٩﴾

279. Na msipofanya basi tangazeni vita kutoka kwa Allaah na Rasuli Wake. Na mkitubu basi mtapata rasilimali zenu msidhulumu na wala msidhulumiwe

 

Mafunzo:

 

Ilipoteremka Aayah Namba (2: 275) Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema; “Yeyote asiyejizuia kufanya mukhaabarah (kukodisha shamba kwa malipo ya kugawana sehemu ya mazao) basi apokee tangazo la vita kutoka kwa Allaah na Rasuli Wake.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr] 

 

Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه) amehadithia: Alikuja Bilaal kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na aina ya tende nzuri. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamuuliza: “Umetoa wapi hizi?” Akasema: Tulikuwa tuna tende mbaya nikaziuza pishi mbili kwa pishi moja (ya tende nzuri). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hapana! Hiyo ndiyo ribaa. Usifanye hivyo! Lakini ukitaka kununua basi uza tende zisizo nzuri kisha (kwa pesa) nunua tende nzuri kwa bei uliyopatia.” [Muslim]

 

Share

280-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Anayempa Muda Mdaiwa Au Kusamehe Deni

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Fadhila Za Anayempa Muda Mdaiwa Au Kusamehe Deni

 

 

 

 وَإِن كَانَ ذُو عُسْرَةٍ فَنَظِرَةٌ إِلَىٰ مَيْسَرَةٍ ۚ وَأَن تَصَدَّقُوا خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٢٨٠﴾

280. Na ikiwa (mdaiwa) ni mwenye hali ngumu, basi (mdai) angoje mpaka afarijike. Na mkifanya deni kuwa ni swadaqah basi ni kheri kwenu mkiwa mnajua.

 

 

Mafunzo:

 

 

Ubaydullaah bin ‘Abdillaah alimsikia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Kulikuwa na tajiri anawakopesha watu, basi akiona mtu hawezi kumlipa deni kwa hali mbaya aliyokuwa nayo anawaambia vijana wake: Msameheni huenda Allaah Atatusamehe. Basi Allaah Akamsamehe.” [Al-Bukhaariy]

 

Abuu Hurayrah amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayemuakhirishia mwenye usiri (wa kulipa deni) au akamsamehe, Allaah Atamfunika kivuli Siku ya Qiyaamah chini ya kivuli cha ‘Arshi Yake, Siku ambayo hakutokuwa na kivuli isipokuwa kivuli Chake.” [At-Tirmdihy]

 

Sulaymaan bin Buraydah amehadithia kwamba baba yake alisema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Yeyote anayempa muda mdaiwa anayekabiliwa na matatizo, basi kila siku atalipwa sawa na kutoa swadaqah.” [Ahmad]

 

Hudhayfah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Siku ya Qiyaamah, mmoja wa waja wa Allaah ataitwa mbele Yake na Atamuuliza: Umefanya ‘amali gani kwa ajili yangu katika maisha yako? Atajibu: Ee Rabb wangu! Sikuwahi katika uhai wangu kufanya ‘amali kwa ajili Yako iliyo sawa na chembe ndogo! (Ataulizwa na atajibu) Mara tatu, kisha mara ya tatu atasema: Ee Rabb wangu! Ulinijaalia mali na nilikuwa nafanya biashara. Nilikuwa mpole, nikiwapa masharti mepesi wenye uwezo na nikiwapa muda wa kulipa wadaiwa. Allaah Atamwambia: Mimi Ndiye Mwenye haki zaidi ya kutoa masharti mepesi kwa hiyo, ingia Jannah!.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Share

281-Aayah Na Mafunzo: Aayah Ya Mwisho Kuteremshwa

Aayah Na Mafunzo

 

Al-Baqarah: 281 : Aayah Ya Mwisho Kuteremshwa

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَاتَّقُوا يَوْمًا تُرْجَعُونَ فِيهِ إِلَى اللَّـهِ ۖ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿٢٨١﴾

281. Na iogopeni Siku mtakayorejeshwa ndani yake kwa Allaah, kisha kila nafsi italipwa kamilifu iliyoyachuma nao hawatodhulumiwa

 

 

Mafunzo:

 

 

Wengi kati ya ‘Ulamaa wamekiri kwamba hii ni Aayah ya mwisho  kuteremshwa. Na miongoni mwa Salaf waliokiri ni Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما), na Sa’iyd  bin Jubayr (رحمه الله) kwa Riwayaah mbalimbali kwamba baada kuteremshwa Aayah hii yakapatika masiku kadhaa kisha akafariki Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) [An-Nasaaiy – Tafsiyr Ibn Kathiyr].

 

 

Na Imaam As-Sa’dy (رحمه الله) amesema: “Hii ni Aayah ya mwisho iliyoteremshwa katika Qur-aan, na ikafanywa ni hatima ya hukmu hizi za maamrisho na makatazo kwa sababu humo mna ahadi za kutenda mema na kheri, na only la kutenda maovu, na kwamba anayejua kwamba yeye atarejeshwa kwa Allaah, basi Atamlipa kwa dogo na kubwa (aliyoyatenda) na yaliyodhahiri na ya siri na kwamba Allaah Hatomdhulumu uzito wa chembe ya hardali (au atomu), basi itamwajibika awe na raghbah (utashi, matumaini) na khofu. Na bila kuyajua hayo moyoni kutakuwa hakuna sababu ya kuyatekeleza.”

 

Share

282-Aayah Na Mafunzo: Aayah Ya Deni, Maana Ya Upungufu Wa Akili Kwa Wanawake

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Aayah Ya Deni Maana Ya Upungufu Wa Akili Kwa Wanawake

www.alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا تَدَايَنتُم بِدَيْنٍ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى فَاكْتُبُوهُ ۚ وَلْيَكْتُب بَّيْنَكُمْ كَاتِبٌ بِالْعَدْلِ ۚ وَلَا يَأْبَ كَاتِبٌ أَن يَكْتُبَ كَمَا عَلَّمَهُ اللَّـهُ ۚ فَلْيَكْتُبْ وَلْيُمْلِلِ الَّذِي عَلَيْهِ الْحَقُّ وَلْيَتَّقِ اللَّـهَ رَبَّهُ وَلَا يَبْخَسْ مِنْهُ شَيْئًا ۚ فَإِن كَانَ الَّذِي عَلَيْهِ الْحَقُّ سَفِيهًا أَوْ ضَعِيفًا أَوْ لَا يَسْتَطِيعُ أَن يُمِلَّ هُوَ فَلْيُمْلِلْ وَلِيُّهُ بِالْعَدْلِ ۚ وَاسْتَشْهِدُوا شَهِيدَيْنِ مِن رِّجَالِكُمْ ۖ فَإِن لَّمْ يَكُونَا رَجُلَيْنِ فَرَجُلٌ وَامْرَأَتَانِ مِمَّن تَرْضَوْنَ مِنَ الشُّهَدَاءِ أَن تَضِلَّ إِحْدَاهُمَا فَتُذَكِّرَ إِحْدَاهُمَا الْأُخْرَىٰ ۚ وَلَا يَأْبَ الشُّهَدَاءُ إِذَا مَا دُعُوا ۚ وَلَا تَسْأَمُوا أَن تَكْتُبُوهُ صَغِيرًا أَوْ كَبِيرًا إِلَىٰ أَجَلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ أَقْسَطُ عِندَ اللَّـهِ وَأَقْوَمُ لِلشَّهَادَةِ وَأَدْنَىٰ أَلَّا تَرْتَابُوا ۖ إِلَّا أَن تَكُونَ تِجَارَةً حَاضِرَةً تُدِيرُونَهَا بَيْنَكُمْ فَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَلَّا تَكْتُبُوهَا ۗ وَأَشْهِدُوا إِذَا تَبَايَعْتُمْ ۚ وَلَا يُضَارَّ كَاتِبٌ وَلَا شَهِيدٌ ۚ وَإِن تَفْعَلُوا فَإِنَّهُ فُسُوقٌ بِكُمْ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ وَيُعَلِّمُكُمُ اللَّـهُ ۗ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٢٨٢﴾ 

282. Enyi walioamini! Mtakapokopeshana deni mpaka muda maalumu uliopangwa, basi liandikeni. Na aandike baina yenu mwandishi kwa uadilifu. Na wala asikatae mwandishi kuandika kama Allaah Alivyomfunza. Basi aandikishe kwa imla yule ambaye ana haki (mdai) na amuogope Allaah, Rabb wake, na wala asipunguze humo kitu chochote. Basi ikiwa yule ambaye ana haki amepumbaa kiakili au mnyonge, au hawezi kuandikisha mwenyewe, basi aandikishe msimamizi wake kwa uadilifu. Na mshuhudishe mashahidi wawili wanaume miongoni mwenu. Na ikiwa hakuna wanaume wawili, basi mwanamme mmoja na wanawake wawili katika wale mnaowaridhia miongoni mwa mashahidi, ili kama mmoja wao hao wanawake wawili akikosea (akasahau), basi mmoja wao atamkumbusha mwengine. Na mashahidi wasikatae watapoitwa. Na wala msichukie kuliandika (deni) dogo au kubwa mpaka muda wake. Hivyo kwenu ndiyo uadilifu upasavyo mbele ya Allaah na ndio unyoofu zaidi kwa ushahidi; na ni karibu zaidi ili msiwe na shaka; isipokuwa itakapokuwa biashara taslimu mnayoiendesha baina yenu, basi si dhambi kwenu msipoiandika. Na shuhudisheni mnapouziana. Na wala asidhuriwe mwandishi wala shahidi; na mkifanya basi hakika huo ni ufasiki kwenu. Na mcheni Allaah, na Allaah Anakufunzeni, na Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi

 

Mafunzo:

 

Hii ni Aayah ndefu kabisa kuliko zote katika Qur-aan na Aayah hii inajulikana kwa ‘Aayatud-dayn’  (Aayah ya deni).

 

Kuhusu upungufu wa akili na Dini kwa wanawake imekusudiwa katika maelezo yanayoendeleza Hadiyth “…Ama upungufu katika akili yake ni ushahidi wa wanawake wawili kwamba ni sawa na ushahidi wa mwanamme mmoja, na huo ndio udhaifu wa akili. Ama upungufu katika Dini, wanawake wakati mwengine (katika hedhi) hawaswali na kufunga Swiyaam mwezi wa Ramadhwaan.” [Muslim]

 

 

Share

283-Aayah Na Mafunzo: Ruhusa Ya Kitu Rehani

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Ruhusa Ya Kuweka Kitu Rehani

www.alhidaaya.com

 

 Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَإِن كُنتُمْ عَلَىٰ سَفَرٍ وَلَمْ تَجِدُوا كَاتِبًا فَرِهَانٌ مَّقْبُوضَةٌ ۖ فَإِنْ أَمِنَ بَعْضُكُم بَعْضًا فَلْيُؤَدِّ الَّذِي اؤْتُمِنَ أَمَانَتَهُ وَلْيَتَّقِ اللَّـهَ رَبَّهُ ۗ وَلَا تَكْتُمُوا الشَّهَادَةَ ۚ وَمَن يَكْتُمْهَا فَإِنَّهُ آثِمٌ قَلْبُهُ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ ﴿٢٨٣﴾

283. Na mkiwa safarini na hamkumpata mwandishi, basi (mdai) akabidhiwe rahani. Na ikiwa mmoja wenu amewekewa amana na mwengine, basi airudishe yule ambaye ameaminiwa amana ya mwenzake; na amche Allaah, Rabb wake; na wala msifiche ushahidi; na mwenye kuuficha basi hakika moyo wake ni wenye kutenda dhambi. Na Allaah kwa mnayoyatenda ni Mjuzi.

 

Mafunzo:

 

‘Aaishah (رضي الله عنها) amehadithia kwamba “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alinunua chakula kwa Yahudi lakini akamlipa muda ujao (deni). Na akaweka rehani nguo yake ya vita iliyotengenezwa kwa chuma.”

 

Sumurah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mkono wa mkopaji utabeba mzigo wa kile ulichochukua mpaka utakapolipa.” [Ahmad, Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy katika Al-Kubraa na Ibn Maajah]

 

 

 

 

Share

285-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Aayah Mbili Za Mwisho Suwratul-Baqarah

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Fadhila Za Aayah Mbili Za Mwisho Suwratul-Baqarah

 www.alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa:

 

آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ ۚ كُلٌّ آمَنَ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ ۚ وَقَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ ﴿٢٨٥﴾

285. Rasuli ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Rabb wake na Waumini (pia). Wote wamemwamini Allaah, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake, na Rusuli Wake. (Nao husema): “Hatutofautishi baina ya yeyote kati ya Rusuli Wake.” Na wakasema: “Tumesikia na tumetii, tunakuomba maghfirah Rabb wetu na Kwako ni mahali pa kuishia.

 

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ ۗ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِ ۖ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا ۚ أَنتَ مَوْلَانَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴿٢٨٦﴾  

286. Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake. Itapata (thawabu) iliyoyachuma, na ni dhidi yake (kwa maovu) iliyojichumia. “Rabb wetu Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Rabb wetu, Usitubebeshe mzigo kama Ulivyoubebesha juu ya wale waliokuwa kabla yetu. Rabb wetu, Usitutwike tusiyoyaweza, na Tusamehe, na Tughufurie na Turehemu, Wewe ni Mola Mlinzi wetu, basi Tunusuru dhidi ya watu makafiri.

 

Mafunzo:

 

 

Fadhila Za Aayah Mbili Za Mwisho Suwrah Al-Baqarah:

 

 

1-Kutokuhesabiwa katika kusahau na kukosea.

 

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:

 

إنَّ اللَّهَ تجاوزَ عن أمَّتيَ الخطأَ والنِّسيانَ ومَا استُكرِهُوا عليه

“Ummah wangu umenyanyuliwa makosa na kusahau na wanayo shurutishwa.” [Ibn Maajah, Ibn Hibbaan, Ad-Daraqutwniy, At-Twabaraniy na Al-Haakim, Irwaa Al-Ghaliyl (1027)]

 

 

2-Atakayezisoma zitamtosheleza:

 

 عن أَبِي مَسْعُودٍ الأَنْصَارِيِّ، قَالَ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: ((الآيَتَانِ مِنْ آخِرِ سُورَةِ الْبَقَرَةِ مَنْ قَرَأَ بِهِمَا فِي لَيْلَةٍ كَفَتَاهُ))

Abuu Mas‘uwd Al-Answaariyy ‘Uqbah bin ‘Amr bin Tha’labah (رضي الله عنه) amesimulia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayesoma usiku Aayah mbili za mwisho wa Suwratul-Baqarah zitamtosheleza.” Yaani: zinamtosheleza kumkinga na kila baya na lenye kumdhuru. [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

3-Hakuna Nabiy aliyepewa Aayah hizi isipokuwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)  

 

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ بَيْنَمَا جِبْرِيلُ قَاعِدٌ عِنْدَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم سَمِعَ نَقِيضًا مِنْ فَوْقِهِ فَرَفَعَ رَأْسَهُ فَقَالَ: ((هَذَا بَابٌ مِنَ السَّمَاءِ فُتِحَ الْيَوْمَ لَمْ يُفْتَحْ قَطُّ إِلاَّ الْيَوْمَ، فَنَزَلَ مِنْهُ مَلَكٌ فَقَالَ: هَذَا مَلَكٌ نَزَلَ إِلَى الأَرْضِ لَمْ يَنْزِلْ قَطُّ إِلاَّ الْيَوْمَ، فَسَلَّمَ وَقَالَ أَبْشِرْ بِنُورَيْنِ أُوتِيتَهُمَا لَمْ يُؤْتَهُمَا نَبِيٌّ قَبْلَكَ، فَاتِحَةُ الْكِتَابِ وَخَوَاتِيمُ سُورَةِ الْبَقَرَةِ لَنْ تَقْرَأَ بِحَرْفٍ مِنْهُمَا إِلاَّ أُعْطِيتَهُ)) ‏.‏

Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesimulia:   Jibriyl (عليه السّلام) alipokuwa na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisikia sauti kutoka juu. Jibriyl (عليه السّلام) akatazama juu akasema: “Huu mlango wa mbinguni umefunguliwa na haujapatapo kamwe kufunguliwa isipokuwa leo.” Malaika akateremka humo akasema: “Huyu Malaika ameteremka ardhini, hajapatapo kuteremka kamwe isipokuwa leo.” Akasalimia kisha   akasema: “Pokea bishara ya Nuru mbili ulizopewa ambazo hakuna Nabiy aliyepewa kabla yako; Ufunguo wa Kitabu (Al-Faatihah), na Aayah (mbili) za mwisho wa Suwratul-Baqarah.  Hutosoma herufi humo ila utapewa barakah zake ziliomo.” [Muslim]

 

 

4-Aayah mbili hizi amepewa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa mbingu ya saba.

 

Hadiyth ya Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه):

 

لَمَّا أُسْرِيَ بِرَسُولِ اللّهِ صلى الله عليه وسلم انْتُهِيَ بِهِ إِلَى سِدْرَةِ الْمُنْتَهَى. وَهِيَ فِي السَّمَاءِ السَّادِسَةِ. إِلَيْهَا يَنْتَهِي مَا يُعْرَجُ بِهِ مِنَ الأَرْضِ. فَيُقْبَضُ مِنْهَا. وَإِلَيْهَا يُنْتَهِى مَا يُهْبَطُ بِهِ مِنْ فَوْقِهَا. فَيُقْبَضُ مِنْهَا. قَالَ: {إِذْ يَغْشَى السِّدْرَةَ مَا يَغْشَى} [النجم: 16] قَالَ: فَرَاشٌ مِنْ ذَهَبٍ. قَالَ: فَأُعْطِيَ رَسُولُ اللّهِ صلى الله عليه وسلم ثَلاَثاً: أُعْطِيَ الصَّلَوَاتِ الْخَمْسَ. وَأُعْطِيَ خَوَاتِيمَ سُورَةِ الْبَقَرَةِ. وَغُفِرَ لِمَنْ لَمْ يُشْرِكْ بِالله مِنْ أُمَّتِهِ شَيْئاً الْمُقْحِمَاتُ (رواه مسلم) .

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipopelekwa safari ya usiku mbinguni (Al-Israa Wal-Mi’raaj), aliishia Sidratul-Muntahaa (Mkunazi wa mpaka wa mwisho kabisa) katika mbingu ya sita ambapo huishia kila kitu (hakuna ajuaye ‘ilmu ya baada ya hapo isipokuwa Allaah). Ambapo pia kunaishia kila kinachopanda kutoka ardhini (amali za watu n.k) na kushikiliwa humo, na kinapoishia kila kitu  kinachoteremka kutoka juu yake na kushikiliwa hapo. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِذْ يَغْشَى السِّدْرَةَ مَا يَغْشَىٰ ﴿١٦﴾

Ulipoufunika mkunazi huo unachokifunika [An-Najm: 16]

 

(Msimulizi) Akasema: Vipepeo vya dhahabu. Akasema: Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akapewa (mambo) matatu: Akapewa Swalaah tano za kila siku. Na akapewa hitimisho la Suwrah Al-Baqarah. Na kughufuriwa katika Ummah wake ambaye hamshirikishi Allaah na chochote.  [Muslim]

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share