006-Al-An'aam: Aayah Na Mafunzo

 

 

 

006-Al-An'aam

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

Share

000-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Suwrah Al-An'aam

 

 

Aayah Na Mafunzo

 

Alhidaaya.com

 

000-Fadhila Za Suwrah Al-An’aam

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَجَعَلَ الظُّلُمَاتِ وَالنُّورَ ۖ ثُمَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ يَعْدِلُونَ ﴿١﴾

1. AlhamduliLLaah, Himidi Anastahiki Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi na Akajaalia viza na nuru; kisha wale ambao wamekufuru wanawasawazisha wengine na Rabb wao.

 

 

 

Mafunzo:

 

Atw-Twabaraaniy amenukuu kwamba Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amehadithia kuwa: “Suwrah nzima ya Al-An’aam imeteremshwa Makkah, usiku, ikifuatiliwa na Malaika elfu sabini wakinyanyua sauti zao kumsabbih Allaah.”

 

 

 

 

Share

003-Aayah Na Mafunzo: Kauli Za ‘Ulamaa Kuhusu Kuabudiwa Allaah Mbinguni Na Ardhini Naye Anajua Siri Na Dhahiri Na Wanayochuma Waja

 

Aayah Na Mafunzo

 

Al-An’aam

 

Kauli Za ‘Ulamaa Kuhusu Kuabudiwa Allaah (سبحانه وتعالى) Mbinguni Na Ardhini Naye Anajua  Siri Na Dhahiri Na Wanayochuma Waja

 

 

003-Al-An’aam:   Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَهُوَ اللَّـهُ فِي السَّمَاوَاتِ وَفِي الْأَرْضِ ۖ يَعْلَمُ سِرَّكُمْ وَجَهْرَكُمْ وَيَعْلَمُ مَا تَكْسِبُونَ ﴿٣﴾

Na Yeye Ndiye Allaah mbinguni na ardhini, Anajua ya siri yenu na ya dhahiri yenu, na Anajua yale mnayoyachuma. [Al-An’aam (6: 3)]

 

Mafunzo:

 

Wafasiri wa Qur-aan wamekhitilafiana katika kauli nne kuhusu Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

وَهُوَ اللَّـهُ فِي السَّمَاوَاتِ وَفِي الْأَرْضِ ۖ يَعْلَمُ سِرَّكُمْ وَجَهْرَكُمْ وَيَعْلَمُ مَا تَكْسِبُونَ ﴿٣﴾

Na Yeye Ndiye Allaah mbinguni na ardhini, Anajua ya siri yenu na ya dhahiri yenu, na Anajua yale mnayoyachuma. (6:3).

 

 

Kauli ya kwanza:

 

Maana yake ni: Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) ni Ilaah (Apasaye kuabudiwa kwa haki) Anayeabudiwa mbinguni na ardhini kwa sababu Yeye Pekee Ndiye Mwabudiwa wa haki katika ardhi na mbingu, kwa ushahidi wa Kauli Yake (تعالى):

وَهُوَ الَّذِي فِي السَّمَاءِ إِلَـٰهٌ وَفِي الْأَرْضِ إِلَـٰهٌ ۚ  

Na Yeye Ndiye Mwabudiwa wa haki mbinguni na ardhini pia (Ndiye Huyo Huyo) Ilaah. [Az-Zukhruf (43:84)]

 

[Al-Qurtwubiy, Ibn Kathiyr, Ash-Shanqiytwiy, Ibn Al-Anbaariy na wengineo. Taz. Al-Jaami’u li-Ahkaamil-Qur-aan (6/390), Tafsiyr Al-Qur-aan Al-‘Adhwiym (3/240), Adhwaau Al-Bayaan (7/4)]  

 

 

Kauli Ya Pili: 

 

Kwamba maana yake ni: Yeye Allaah Anajua siri zenu mbinguni na ardhini, na ushahidi ni Kauli Yake:

(تعالى)  

 

قُلْ أَنزَلَهُ الَّذِي يَعْلَمُ السِّرَّ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ  

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Ameiteremsha Ambaye Anajua siri katika mbingu na ardhi. [Al-Furqaan (25:6)]

 

Kwa kuzingatia kwamba Kauli Yake: 

 

mbinguni na ardhini[Al-An’aam (6:3)] inahusiana na: Anajua siri zenu.”

 

Na amesema Imaam Ad-Daaniyy: Na imesemwa kuwa maana yake ni: Yeye Ndiye Mwabudiwa mbinguni na ardhini.

 

Na kadhaalika, Al-Ashmuwniyy kaunga mkono ufafanuzi huo.

 

Na amesema An-Nahhaas kuwa kauli hiyo ni bora katika yaliyoelezwa juu ya Aayah hiyo.

 

[Al-Muktafaa Fiy Al-Waqf Wal-Ibtidaa Fiy KitaabiLLaah ‘Azza Wa Jalla (273), Manaaru Al-Hudaa Fiy Bayaan Al-Waqf Wal-Ibtidaa (265). Adhwaau Al-Bayaan Fiy Iydhwaah Al-Qur-aan bil-Qur-aan (4/7)]   

 

 

Kauli Ya Tatu:

 

Kwamba maana yake ni:  Yeye Allaah, Ambaye Yeye Yuko mbinguni na katika ardhi, Anajua siri zenu na ya dhahiri yenu katika ardhi.  Naye Yuko juu ya ‘Arsh Yake Akiwa juu ya Viumbe Vyake wote, Akiwa Anajua siri za watu wa ardhini na ya dhahiri yao, hakuna kinachofichika Kwake katika hayo. Na ushahidi ni Kauli Yake (تعالى):

 

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ﴿١٦﴾

Je, mnadhani mko katika amani na (Allaah) Aliyeko mbinguni kwamba Hatokudidimizeni ardhini, tahamaki hiyo inatikisika?

 

 

أَمْ أَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ﴿١٧﴾

Au mnadhani mko katika amani na (Allaah) Aliyeko mbinguni kwamba Hatokutumieni tufani ya mawe? Basi mtajua vipi Maonyo Yangu!

 

[Al-Mulk (67:16-17)]

 

 

Na Kauli Yake (تعالى):

 

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ ﴿٥﴾

Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah), Yuko juu (Istawaa) ya ‘Arsh. [Twaahaa (20:5)]

 

 

Kauli Ya Nne: 

 

Ina maana kutangulizwa na kuakhirishwa, yaani: Yeye Allaah Anajua siri zenu na ya dhahiri yenu mbinguni na ardhini. Na hii ni kauli ya Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) .

 

Kauli iliyo na nguvu kabisa katika kauli hizo nne ni:

 

Kauli ya kwanza ambayo ni kauli ya wengi katika Mufassariyn, pamoja na kwamba kuna uwezekano wa kauli nyingine katika hizo kwa sababu kila kauli ina ushahidi wake katika Qur-aan.

 

Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah (رحمه الله) amesema: “Maimaam wakubwa kama Imaam Ahmad na wengineo wameifasiri kwamba: “Kuwa Yeye ni Mwabudiwa mbinguni na ardhini.” [Al-Furqaan Bayna Awliyaair-Rahmaan Wa-Awliyaa Ash-Shaytwaan (244)]

 

Ibn Kathiyr (رحمه الله)  amesema “Kauli iliyo sahihi kabisa ni kwamba: “Allaah Anaombwa mbinguni na ardhini, yaani Anaabudiwa,   Anapwekeshwa, Anakiriwa kwa Uabudiwa na Anaitwa Allaah. Naye Anaombwa na wote kwa utashi na khofu isipokuwa wakanushaji katika majini na wanaadamu.”  [Tafsiyr Al-Qur-aan Al-‘Adhwiym, (3/240)]  

 

 

Share

012-Aayah Na Mafunzo: Rahma Za Allaah Zinashinda Ghadhabu Zake

Aayah Na Mafunzo

 

www.alhidaaya.com

 

 

Al-An’aam 12

 

 

012-Rahma Za Allaah Zinashinda Ghadhabu Zake

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

قُل لِّمَن مَّا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ قُل لِّلَّـهِ ۚ كَتَبَ عَلَىٰ نَفْسِهِ الرَّحْمَةَ ۚ لَيَجْمَعَنَّكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۚ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٢﴾

Sema: Ni vya nani vilivyomo mbinguni na ardhini? Sema: Ni vya Allaah. Amejiwajibishia Nafsi Yake Rahmah. Bila shaka Atakukusanyeni Siku ya Qiyaamah, hapana shaka yoyote ndani yake. Wale ambao wamekhasiri nafsi zao basi wao hawaamini. [Al-An'aam: 12]

 

 

 

 

Mafunzo:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: (( لَمَّا قَضَى اللَّهُ الْخَلْقَ كَتَبَ فِي كِتَابِهِ عَلَى نَفْسِهِ فَهُوَ مَوْضُوعٌ عِنْدَهُ إِنَّ رَحْمَتِي تَغْلِبُ غَضَبِي)) البخاري   مسلم  النسائي وابن ماجه

Kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه)  ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: ((Allaah Alipoumba viumbe Aliandika katika kitabu Chake Alichonacho katika Nafsi Yake: Rahmah Zangu zinashinda ghadhabu Zangu)) [Al-Bukhaariy, Muslim, an-Nasaaiy na Ibn Maajah]

 

 

 

 

 

Share

073-Aayah Na Mafunzo: Israafiyl Yuko Tayari Anasubiri Amri Ya Allaah Ya Kupuliza Baragumu La Qiyaamah

Aayah Na Mafunzo

 

www.alhidaaya.com

 

Al-An’aam 73

 

073-Malaika Israafiyl Yuko Tayari Anasubiri Amri Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Ya Kupuliza Baragumu La Qiyaamah

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۖ وَيَوْمَ يَقُولُ كُن فَيَكُونُ ۚ قَوْلُهُ الْحَقُّ ۚ وَلَهُ الْمُلْكُ يَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ ۚ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ ۚ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْخَبِيرُ ﴿٧٣﴾

Naye Ndiye Ambaye Ameumba mbingu na ardhi kwa haki. Na Siku Atakaposema: Kun! Basi (jambo) huwa! Kauli Yake ni haki. Ni Wake Yeye tu ufalme Siku litakapopulizwa baragumu. Mjuzi wa ghaibu na dhahiri. Naye Ni Mwenye Hikmah wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [Al-An'aam: 73]

 

 

 

Mafunzo:

 

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Israafiyl ameliweka baragumu mdomoni mwake huku ameelekeza kipaji chake cha uso juu akisubiri amri ya kulipuliza.” [Muslim].

 

Share

094-Aayah Na Mafunzo: Kila Moja Atafika Siku Ya Qiyaamah Pekee Akiwa Uchi Kama Alivyozaliwa Na Akiacha Kila Kitu Nyuma Yake

Aayah Na Mafunzo

 

www.alhidaaya.com

 

Al-An’aam 94

 

094-Kila Moja Atafika Siku Ya Qiyaamah Pekee Akiwa Uchi Kama Alivyozaliwa

Na Akiacha Kila Kitu Nyuma Yake

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَلَقَدْ جِئْتُمُونَا فُرَادَىٰ كَمَا خَلَقْنَاكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَتَرَكْتُم مَّا خَوَّلْنَاكُمْ وَرَاءَ ظُهُورِكُمْ ۖ وَمَا نَرَىٰ مَعَكُمْ شُفَعَاءَكُمُ الَّذِينَ زَعَمْتُمْ أَنَّهُمْ فِيكُمْ شُرَكَاءُ ۚ لَقَد تَّقَطَّعَ بَيْنَكُمْ وَضَلَّ عَنكُم مَّا كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ﴿٩٤﴾

 

Na kwa yakini mmetujia mmoja mmoja kama Tulivyokuumbeni mara ya kwanza, na mmeyaacha nyuma yenu yote Tuliyokuruzukuni. Na Hatuwaoni pamoja nanyi waombezi wenu ambao mlidai kwamba wao ni washirika wenu. Kwa yakini yamekatika (mahusiano) baina yenu na yamekupoteeni mliyokuwa mkidai. [Al-An'aam: 94]

 

 

Mafunzo:

 

عَنْ عَائِشَةَ (رضي الله عنها)  قَالَتْ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((يُحْشَرُ النَّاسُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ حُفَاةً عُرَاةً غُرْلا)) قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ، النِّسَاءُ وَالرِّجَالُ جَمِيعًا يَنْظُرُ بَعْضُهُمْ إِلَى بَعْضٍ؟  قَالَ: ((يَا عَائِشَةُ! الأَمْرُ أَشَدُّ مِنْ أَنْ  يُهِمَّهُم ذلِكَ)) وَفِي رِواية: ((ألأَمْرُ أَهَمُّ مِنْ أَنْ يَنْظُرَ بَعْضُهُمْ إِلَى بَعْضٍ)) متفق عليه

                                                                                                                                              Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (رضي الله عنها) ambaye amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Watu watafufuliwa Siku ya Qiyaamah ilhali hawana viatu, wako uchi, ni mazunga [hawakutahiriwa])). Nikamuuliza: Ee Rasuli wa Allaah! Wanaume na wanawake wote watatazamana? Akasema: ((Ee ‘Aaishah! Hali itakuwa ngumu mno hata hawatoweza kushughulika na jambo hilo!))

 

Katika riwaayah nyingine imesema: ((Hali itakuwa ngumu mno kiasi kwamba hawatoweza kutazamana)). [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Bin Aadam husema: “Mali yangu, mali yangu! Lakini mali gani uliyonayo isipokuwa uliyokwishaila ukaimaliza, au uliyoivaa ikachakaa, au uliyoitolea swadaqah ikatangulia (kuwa akiba yako ya Aakhirah). Ama nyingineyo utoandoka duniani na kuwaachia watu.” [Muslim].

 

Share

098-Aayah Na Mafunzo: Nyota Zimeumbwa Kwa Ajili Ya Matatu Mapambo Ya Mbingu Kupiga Mashaytwaan Kuongoza Njia

Aayah Na Mafunzo

 

www.alhidaaya.com

 

Al-An’aam 98

 

098-Nyota Zimeumbwa Kwa Ajili Ya Matatu

Mapambo Ya Mbingu Kupiga Mashaytwaan Kuongoza Njia

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

وَهُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ النُّجُومَ لِتَهْتَدُوا بِهَا فِي ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۗ قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٩٧﴾

 Na Yeye Ndiye Aliyekufanyieni nyota ili zikusaidieni kujua mwendako katika viza vya bara na bahari. Kwa yakini Tumezifasili waziwazi ishara na vielelezo kwa watu wanaojua. [Al-An’aam: 97]

 

 

Mafunzo:

 

Amesimulia Qataadah (رضي الله عنه): “Allaah Ameumba hizi nyota kwa malengo matatu; (i) mapambo ya mbingu (ii) vimondo vya (kuwafukuza na kuwapiga) shaytwaan, (iii) alama za kuongoza njia (wasafiri wa majangwani na baharini). Basi atakayefasiri vingine amekosea na atakuta patupu Aakhirah (atakosa thawabu) kwani atakuwa amebeba asio na elimu nayo kwa kuchupa mipaka ya ujuzi Wake.” [Al-Bukhaariy]

 

Nyota zimeumbwa kwa ajili ya mambo hayo tu. Basi Hadiyth hii inawakanusha wanajimu (watabiri wa nyota) jambo ambalo ni la kumshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى) nayo ni Shirki kubwa ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Haisamehe.

 

 

 

 

 

Share

103-Aayah Na Mafunzo: Macho Hayamzunguki Allaah Bali Yeye Anayazunguka Macho Yote

 

Aayah Na Mafunzo

 

www.alhidaaya.com

 

Al-An’aam 103

 

103-Suala La ‘Aqiydah: Macho Hayamzunguki Allaah (سبحانه وتعالى)  

Bali Yeye Anayazunguka Macho Yote

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ ۖ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ ﴿١٠٣﴾

Macho hayamzunguki (hayamdiriki) bali Yeye Anayazunguka macho yote, Naye Ni Mwenye Kudabiri mambo kwa ulatifu, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. (6:103).

 

 

 

Mafunzo:

 

Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) Hakumuona Allaah (سبحانه وتعالى):

 

  

Masruwq  (رضي الله عنه)  amehadithia kwamba: Nilimwambia ‘Aaishah (رضي الله عنها) : Ee Mama! Je Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake? Akasema: Hayo uliyoyasema yamefanya nywele zangu zisimame kunisisimka mwili! Tambua kwamba mtu akikutajia mambo matatu yafuatayo basi yeye ni muongo! Atakayesema kwamba Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) amemuona Rabb wake, kisha akasoma:

 

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ ۖ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ ﴿١٠٣﴾

Macho hayamzunguki (hayamdiriki) bali Yeye Anayazunguka macho yote, Naye Ni Mwenye Kudabiri mambo kwa ulatifu, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. (6:103).

 

Na akasoma pia:

 

وَمَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُكَلِّمَهُ اللَّـهُ إِلَّا وَحْيًا أَوْ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ أَوْ يُرْسِلَ رَسُولًا فَيُوحِيَ بِإِذْنِهِ مَا يَشَاءُ ۚ إِنَّهُ عَلِيٌّ حَكِيمٌ﴿٥١﴾

Na wala haikuwa kwa mtu yeyote kwamba Allaah Amsemeze isipokuwa kwa Wahy au kutoka nyuma ya kizuizi, au Hutuma Mjumbe, kisha Anamfunulia Wahy Ayatakayo kwa Idhini Yake. Hakika Yeye Ni Mwenye ‘Uluwa, Mwenye Hikmah wa yote. (42:51).

 

 

Kisha akaendelea kusema: Na atakayesema kwamba Nabiy anajua yatakayotokea kesho basi ni muongo. Kisha Akasoma:

 

وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَّاذَا تَكْسِبُ غَدًا ۖ

Na nafsi yoyote haijui nini itachuma kesho, na nafsi yoyote haijui itafia katika ardhi gani.  (31:34).

 

 

Kisha akasema: Na atakayesema kuwa Nabiy ameficha aliyofunuliwa Wahyi (na maamrisho) basi ni muongo! Kisha akasoma:

 

يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ وَإِن لَّمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ ۚ  

Ee Rasuli! Balighisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako. Na usipofanya, basi utakuwa hukubalighisha ujumbe Wake.  

(5:67).

 

 

Kisha akasema: Lakini Nabiy alimuona Jibriyl katika umbile lake khalisi mara mbili. [Al-Bukhaariy]

 

 

Kwa upande mwengine Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Allaah, na akasema kuwa Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake mara mbili. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]  

 

Al-Haafidhw, Ibn Hajar amesema: “Maelezo ya Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) yamekuja katika hali ya kutodhibitiwa (hayaelezi kama Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake kwa macho yake au vipi) wakati kauli za Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها)  na wenziwe zimedhibitiwa kwa kusema Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) hakumuona Allaah “Kwa macho yake.” Tunaweza kuunganisha kauli hizo mbili kwa kusema Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها)  alikataa muono “Kwa macho yake” na kauli ya Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kuwa ni kamuona kiroho.” [Fat-hul-Baariy, 8/608]  

 

 

Na Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kwa riwaaya nyingine  alisema kuwa Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake wakati akiwa katika usingizi, na hii ni ndoto ya kweli. Na kauli ya Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها)  inakataa, na kwamba Rasuli hakumuona Rabb wake wakati yeye akiwa macho, lakini kauli hiyo haikatazi kuwa  Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake akiwa usingizini Alichokana hapa ni kuwa Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) hakumuona Allaah kwa macho yake meupe, akiwa macho.  

 

Wale ambao wanao msimamo kuwa Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake kwa macho yake meupe wanaleta Hadiyth dhaifu. Hakuna Hadiyth Swahiyh ambayo inaeleza ya kuwa Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake kwa macho yake akiwa macho. Wenye msimamo huo wanaleta Hadiyth ya At-Tirmidhiy ambayo Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) anasema kuwa Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake. ‘Ikrimah alimuuliza: “Vipi Aayah ambayo inasema:

 

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ ۖ

Macho hayamzunguki (hayamdiriki) bali Yeye Anayazunguka macho yote

 

 

Alijibu, kuwa ni wakati tu Allaah amezungukwa na Nuru, lakini Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake mara mbili. “Hadiyth hii ni dhaifu.”

 

Kwa hali hiyo, hakuna mgongano wa kauli, na Allaah Anajua zaidi [Sharh ya Uswuwl Al-I’itiqaad cha Al-Laalika’iy, (93/512), As-Sunnah (1/181) na Swifaat Al-Maqdisiy ukurasa (109-111]   

 

Hapa kunathibitishwa kuwa Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) hakumuona Rabb wake wakati alipopelekwa Al-Israa Wal Mi’raaj, na hii ndio ‘Aqiydah ya Ahlus-Sunnah wal- Jamaa’ah kuwa Allaah Haonekani duniani, kinyume na ‘Aqiydah ya Masufi wanaoamini kuwa Allaah Anaonekana duniani kwa kuegemeza tukio hilo la Al-Israa Wal Mi’raaj.

 

Kadhaalika, Aayah hiyo vilevile haikanushi kuonekana Allaah Qiyaamah, bali Qiyaamah Allaah Ataonekana katika kisimamo cha Qiyaamah katika Jannah (Peponi) kwa dalili nyingi kutoka katika Qur-aan na Sunnah, kinyume na ‘Aqiydah ya makundi potofu yanayoamini kuwa Allaah Hatoonekana Aakhirah.

 

 

Share

158-Aayah Na Mafunzo: Miongoni Mwa Alama Kuu Za Qiyaamah Kuchomoza Jua Magharibi Ad-Dajjaal Mnyama Mkubwa Kuongea

 

Aayah Na Mafunzo

 

www.alhidaaya.com

 

Al-An’aam 158

 

158-Miongoni Mwa Alama  Kuu Za Qiyaamah

Kuchomoza Jua Magharibi Ad-Dajjaal Mnyama Mkubwa Kuongea

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن تَأْتِيَهُمُ الْمَلَائِكَةُ أَوْ يَأْتِيَ رَبُّكَ أَوْ يَأْتِيَ بَعْضُ آيَاتِ رَبِّكَ ۗ يَوْمَ يَأْتِي بَعْضُ آيَاتِ رَبِّكَ لَا يَنفَعُ نَفْسًا إِيمَانُهَا لَمْ تَكُنْ آمَنَتْ مِن قَبْلُ أَوْ كَسَبَتْ فِي إِيمَانِهَا خَيْرًا ۗ قُلِ انتَظِرُوا إِنَّا مُنتَظِرُونَ ﴿١٥٨﴾

Je, wanangojea nini isipokuwa Malaika wawafikie (kuwatoa roho), au Awafikie Rabb wako (kuwahukumu), au ziwajie baadhi ya Aayaat za Rabb wako? Siku zitakapokuja baadhi ya Alama (za Qiyaamah) za Rabb wako haitoifaa nafsi iymaan yake, ikiwa haikuamini kabla au haikuchuma katika Iymaan yake kheri yoyote. Sema: Ngojeeni hakika nasi tunangojea. [Al-An'aam: 158]

 

Mafunzo:

 

Aayah hii tukufu imetaja kuwa kutatokea alama kabla ya kusimama Qiyaamah; alama ambazo wale wasioamini kabla ya kutokea alama hizo, watakapotaka kuamini, basi Iymaan zao hazitawafaa lolote kwa kuwa hawatakubaliwa kuamini kwao. Mifano ya hayo ni jua kuchomoza kutoka upande wa Magharibi badala ya kuchomoza kutoka Mashariki kwa Hadiyth ifuatayo:

 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayetubu kabla ya kuchomoza jua upande wa Magharibi, Allaah Atamkubalia tawbah yake.” [Muslim]

 

Na pia: Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Matatu yakitokea, basi nafsi haitofaa iymaan yake tena ikiwa haikuamini kabla au haikuchuma kheri yoyote; kuchomoza jua upande wa Magharibi, kutokeza kwa Ad-Dajjaal, na mnyama mkubwa wa ardhi (atakyesemesha watu).” [Ibn Jariyr na Ahmad].

 

Na Hadiyth ifuatayo imetaja alama zote kumi:

 

Amesimulia Hudhayfah Bin Asiyd (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa chumbani nasi tulikuwa chini yake, akachungulia na kutuuliza:   “Mnajadiliana nini?” Tukasema: (Tunajadili kuhusu) Saa (Qiyaamah). Hapo akasema: Saa (Qiyaamah) hakitatokea mpaka zionekane Alama (au Ishara) kumi: Kudidimia kwa Mashariki na Magharibi, Kudidimia Bara la Arabu, Moshi, (Masiyh) Ad-Dajjaal, Mnyama mwitu mkubwa wa ardhi (atakayewasemesha watu), Ya-ajuwj na Ma-ajuwj,  Kuchomoza jua upande wa Magharibi,   Moto utakaotokea  upande wa chini ya ‘Aden utakaowasukuma watu (kufikia Ardhi ya Mkusanyiko).”  Shu'bah   amesema na amenihadithia   ‘Abdul-‘Aziyz bin Rufa’y kutoka kwa Abiy Atw-Twufayl kutoka kwa Abiy Sariyhah Hadiyth kama hiyo  ila Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakuitaja (alama ya kumi) lakini alisema kuwa katika kumi, mojawapo ni kuteremka Nabiy ‘Iysaa  bin Maryam alayhi  (عليه السلام)  na katika riwaaya nyengine ni: Upepo mkali utakaowaendesha watu na kutupwa   baharini. [Muslim]

 

 

Na ‘Ulamaa wametaja alama hizo kubwa kumi ingawa wamekhitilafiana katika mpangilio wake na kuzitaja kwake nazo ni:

 

-Kuja kwa Mahdi.

-Kutokeza kwa Masiyh Ad-Dajjaal.

-Kuteremka kwa Nabiy ‘Iysaa na (عليه السّلام).

-Kuchomoza kwa Yaajuwj na Maajuwj.

-Ka’bah kubomolewa na kutoka Moshi.

-Kutoweka Qur-aan nyoyoni mwa Waumini na Miswahafu.

-Jua kuchomoza Magharibi.

-Kutokeza mnyama mkubwa atakayewasemesha watu.

-Mididimizo mitatu ya ardhi: Mdidimizo wa Mashariki, Magharibi na katika Jaziyrah ya Arabia.

-Moto utakaotoka kutoka Yemen utawapeleka watu kufika katika Ardhi ya Mkusanyiko.

 

 

 

 

 

 

 

   

 

 

 

 

Share

160-Aayah Na Mafunzo: Mja Akitia Niyyah Kutenda Jema Analipwa Moja, Akitimiza Analipwa Mara Kumi, Ovu Haliandikiwi Mpaka Alitende Na Huhesabiwa Moja

 

Aayah Na Mafunzo

 

 

www.alhidaaya.com

 

 

Al-An’aam 160

 

160-Miongoni Mwa Rahma Za Allaah  Ni Kwamba Mja Akitia Niyyah Kutenda Jema Analipwa Moja Na Akitimiza  Analipwa Mara Kumi Na Ovu Haliandikiwi Mpaka Alitende Na Huhesabiwa Moja

 

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

مَن جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا ۖ وَمَن جَاءَ بِالسَّيِّئَةِ فَلَا يُجْزَىٰ إِلَّا مِثْلَهَا وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿١٦٠﴾

Atakayekuja na ‘amali njema basi atapata (thawabu) kumi mfano wake. Na Atakayekuja na ovu basi hatolipwa ila mfano wake, nao hawatodhulumiwa. [Al-An'aam: 160]

 

 

Mafunzo:

 

Rahmah Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Kwa Waumini Kuongezewa Thawabu Mara Kumi Kwa ‘Amali Njema Moja Na Kuandikiwa Dhambi Moja Tu Kwa Tendo Ovu:

 

Ukitia niyyah kutenda amali moja lakini ukawa hukujaaliwa kuitenda utaandikiwa moja. Utakapoweza kuitenda utalipwa mara kumi yake.

Ukitia niyyah kutenda uovu haitoandikwa kwanza kwa kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Anampa mja muhula ajirudi  ili asitende uovu au dhambi. Na atakapolitenda basi ataandikiwa dhambi moja.

 

 

Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:Allaah Ameandika mema na mabaya, kisha Akayabainisha, basi atakayetia niyyah kutenda jema kisha asilifanye, ataandikiwa jema moja kamili. Atakapofanya hima na akalitenda, ataandikiwa mema kumi hadi kuzidi mia saba na ziada nyingi. Na atakayetia niyyah kufanya kitendo kibaya kisha asikifanye, ataandikiwa jema moja kamili. Atakapokifanya, ataandikiwa dhambi moja.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Share

162-Aayah Na Mafunzo: Du’aa Mojawapo Ya Kufungulia Swalaah

 

Aayah Na Mafunzo

 

www.alhidaaya.com

 

Al-An’aam:  162

 

162-Du’aa Mojawapo Ya Kufungulia Swalaah

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٦٢﴾

Sema: Hakika Swalaah yangu, na ‘Ibaadah yangu ya kuchinja, na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah Pekee Rabb wa walimwengu.

 

 

لَا شَرِيكَ لَهُ ۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ ﴿١٦٣﴾

Hana mshirika, na kwa hayo ndio nimeamrishwa, nami ni Muislamu wa kwanza (katika ummah huu).

 

 

Mafunzo:

 

Faida: Aayah (6: 161- 162) ni mojawapo ya du’aa ya kufungulia Swalaah: Pia Aayah hii ni dalili mojawapo ya haramisho la kuchinja kwa kukusudia asiyekuwa Allaah (سبحانه وتعالى).

 

Du’aa Mojawapo Ya Kufungulia Swalaah:

 

وَجَّهـتُ وَجْهِـيَ لِلَّذي فَطَرَ السَّمـواتِ وَالأَرْضَ حَنـيفَاً وَمـا أَنا مِنَ المشْرِكين، إِنَّ صَلاتـي، وَنُسُكي، وَمَحْـيايَ، وَمَماتـي للهِ رَبِّ العالَمين، لا شَريـكَ لَهُ وَبِذلكَ أُمِرْتُ وَأَنا مِنَ المسْلِـمين.

 

Wajjahtu wajhiya liLLadhiy fatwaras-samaawaati wal ardhwa haniyfan wamaa ana minal mushrikiyn. Inna swalaatiy, wanusuky, wamahyaaya wamamaatiy liLLaahi Rabbil ‘aalamiyn. Laa shariyka Lahu wabidhaalika umirtu wa anaa minal Muslimiyn.

 

Nimeuelekeza uso wangu kwa yule Ambaye Ameanzisha mbingu na ardhi hali ya kuelemea katika haki, na sikuwa mimi ni katika washirikina, hakika Swalaah yangu na kuchinja kwangu na uhai wangu, na kufa kwangu ni kwa Allaah Rabb walimwengu, Hana mshirika, na kwa hilo nimeamrishwa nami ni katika Waislamu. 

Na katika riwaaya nyenginezo inaishia kwa:

 

وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ

nami ni Muislamu wa kwanza.

 

Kisha Du'aa inaendelea:

 

اللّهُـمَّ أَنْتَ المَلِكُ لا إِلهَ إِلاّ أَنْت، أَنْتَ رَبِّـي وَأَنـا عَبْـدُك، ظَلَمْـتُ نَفْسـي وَاعْـتَرَفْتُ بِذَنْبـي فَاغْفِرْ لي ذُنوبي جَميعاً إِنَّـه لا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إلاّ أَنْت، وَاهْدِنـي لأَحْسَنِ الأَخْلاقِ لا يَهْـدي لأَحْسَـنِها إِلاّ أَنْـت، وَاصْـرِف عَـنّْي سَيِّئَهـا، لا يَصْرِفُ عَـنّْي سَيِّئَهـا إِلاّ أَنْـت، لَبَّـيْكَ وَسَعْـدَيْك، وَالخَـيْرُ كُلُّـهُ بِيَـدَيْـك، وَالشَّرُّ لَيْـسَ إِلَـيْك، أَنا بِكَ وَإِلَيْـك، تَبـارَكْتَ وَتَعـالَيتَ, أَسْتَغْـفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَـيك

 

Allaahumma Antal-Maliku laa ilaaha illa Anta. Anta Rabbiy wa ana ‘abduka, dhwalamtu nafsiy wa’taraftu bidhambiy faghfirly dhunuwbiy jamiy’an innahu laa yaghfirudh-dhunuwba illa Anta. Wahdiniy liahsanil-akhlaaqi laa yahdiy liahsanihaa illa Anta, waswrif ‘annyi sayyiahaa laa yaswrif ‘anniy sayyiahaa illa Anta. Labbayka wasa’dayka walkhayru kulluhu biyadika, wash-sharru laysa Ilayka, ana bika wa Ilayka, Tabaarakta wa Ta’aalayta, astaghfiruka wa atuwbu Ilayka

 

Ee Allaah, Wewe Ndiye Mfalme, hapana  mwabudiwa wa haki ila Wewe, Wewe Ndiye Rabb wangu na mimi ni mja Wako. Nimedhulumu nafsi yangu, na nimekiri madhambi yangu kwa hivyo nighufurie madhambi yangu yote, hakika haghufurii madhambi, ila Wewe.  Na niongoze kwenye tabia nzuri kwani haongozi kwenye tabia nzuri ila Wewe. Niepushe na tabia mbaya, kwani hakuna mwenye uwezo wa kuniepusha na tabia mbaya ila Wewe.  Naitikia mwito Wako, na nina furaha kukutumikia, na kheri zote ziko mikononi Mwako, na shari haitoki Kwako, mimi nimepatikana kwa ajili Yako, na nitarudi Kwako, Umebarikika na Umetukuka, nakuomba maghfirah na narudi Kwako kutubia [Hadiyth ya ‘Aliy bin Abi Twaalib  (رضي الله عنه) - Muslim (1/534)]

 

Share