Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Fadhila Zake Mbalimbali

 

 

 

 

 

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Fadhila Zake Mbalimbali

 

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

 

Share

00-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Na Fadhila Za Allaah Juu Yako Daima Ni Adhimu

 

 

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

00-Na Fadhila Za Allaah Juu Yako Daima Ni Adhimu

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Allaah ('Azza wa Jalla) Amefadhilisha baadhi ya Manabii juu ya wengine kama Anavyosema:

 

وَرَبُّكَ أَعْلَمُ بِمَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ وَلَقَدْ فَضَّلْنَا بَعْضَ النَّبِيِّينَ عَلَىٰ بَعْضٍ ۖ وَآتَيْنَا دَاوُودَ زَبُورًا ﴿٥٥﴾

Na Rabb wako Anawajua vilivyo waliomo katika mbingu na ardhi. Na kwa yakini Tumewafadhilisha baadhi ya Manabii juu ya wengineo. Na Tukampa Daawuwd Zabuwr [Al-Israa: 55]

 

Na Amefadhilisha baadhi ya Rusuli juu ya wengineo kama Anavyosema pia:

 

تِلْكَ الرُّسُلُ فَضَّلْنَا بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۘ مِّنْهُم مَّن كَلَّمَ اللَّـهُ ۖ وَرَفَعَ بَعْضَهُمْ دَرَجَاتٍ ۚ وَآتَيْنَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ وَأَيَّدْنَاهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ ۗ  

Hao ni Rusuli, Tumewafadhilisha baadhi yao juu ya baadhi. Miongoni mwao kuna aliyesemeshwa na Allaah, na Akawapandisha baadhi yao vyeo. Na Tukampa ‘Iysaa mwana wa Maryam hoja bayana na Tukamtia nguvu kwa Ruwhil-Qudus (Jibriyl (عليه السلام [Al-Baqarah: 253]

 

Nini Tofauti Ya Rasuli Na Nabiy?

 

‘Ulamaa wamesema mengi kuhusu tofauti baina ya Rasuli na Nabiy. Wakakubaliana wengi wao kwamba Rasuli ni ambaye ameteremshiwa shariy’ah na akaamrishwa kubalighisha. Ama Nabiy ni ambaye ametumwa na Allaah ('Azza wa Jalla) bila kuteremshiwa shariy’ah mpya naye hutumia shariy’ah  ya Rasuli aliyemtangulia.

 

Shaykhul-Islaam ibn Taymiyyah amesema:  “Rasuli ni ambaye aliyetumwa kwa kaumu makafiri waliokanusha. Nabiy ni aliyetumwa kwa Waumini kwa shariy’ah ya Rasuli wa kabla yake awafunze na awahakumu baina yao kama Anavyosema Allaah ('Azza wa Jalla):

 

إِنَّا أَنزَلْنَا التَّوْرَاةَ فِيهَا هُدًى وَنُورٌ ۚ يَحْكُمُ بِهَا النَّبِيُّونَ الَّذِينَ أَسْلَمُوا لِلَّذِينَ هَادُوا  

Hakika Tumeteremsha Tawraat humo mna mwongozo na nuru; ambayo kwayo, Nabiy waliojisalimisha (kwa Allaah), waliwahukumu Mayahudi...  [Al-Maaidah: 44]

 

Kwa ufupi ni kuwa kila Rasuli ni Nabiy lakini si kila Nabiy ni Rasuli. Na ‘Ulamaa wamekubaliana kwamba Rasuli ni bora kuliko Nabiy.  Hivyo Rasuli ana daraja kubwa kuliko Nabiy. 

 

Na katika ambao Allaah ('Azza wa Jalla) Amewafadhilisha juu ya wengine ni ambao wanaojulikana kwa Ulul-‘Azmi (wenye azimio la subira katika da'wah [ulinganiaji]) kama Anavyosema Allaah ('Azza wa Jalla):

 

فَاصْبِرْ كَمَا صَبَرَ أُولُو الْعَزْمِ مِنَ الرُّسُلِ

Basi subiri (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kama walivyosubiri wenye azimio madhubuti miongoni mwa Rusuli  [Al-Ahqaaf: 38]

 

 

Na walio mashuhuri kama walivyokubaliana baadhi ya 'Ulamaa ni ambao wametajwa katika kauli ya Allaah ('Azza wa Jalla):

 

وَإِذْ أَخَذْنَا مِنَ النَّبِيِّينَ مِيثَاقَهُمْ وَمِنكَ وَمِن نُّوحٍ وَإِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ۖ وَأَخَذْنَا مِنْهُم مِّيثَاقًا غَلِيظًا ﴿٧﴾

Na pale Tulipochukua kutoka kwa Manabii fungamano lao na kutoka kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na kutoka kwa Nuwh, na Ibraahiym, na Muwsaa, na ‘Iysaa mwana wa Maryam; na Tukachukua kutoka kwao fungamano gumu. [Al-Ahzaab: 7]

 

 

Na Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amefadhilishwa kwa fadhila adhimu na nyingi mno kama Anavyosema Allaah (‘Azza wa Jalla) katika kauli Yake: 

 

  وَكَانَ فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكَ عَظِيمًا ﴿١١٣﴾

Na fadhila za Allaah juu yako daima ni adhimu. [An-Nisaa: 113]

 

Tutaendelea kutaja fadhila za Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika makala zinazofuata.

 

WabiLLaahi At-Tawfiyq

 

 

Share

01-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kiumbe Bora Kabisa Wa Kwanza Kufufuliwa Na Kwanza Kuomba Ash-Shafaa’ah

 

Fadhila Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

01-Kiumbe Bora Kabisa Wa Kwanza Kufufuliwa

Na Kwanza Kuomba Ash-Shafaa’ah

 

www.alhidaaya.com

 

 

Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni kiumbe bora kabisa, na wa kwanza kufufuliwa na wa kwanza atakayeruhusiwa kuomba Ash-Shafaa’ah (uombezi) Siku ya Qiyaamah:

 

عن أَبُي هُرَيْرَةَ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَنَا سَيِّدُ وَلَدِ آدَمَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَأَوَّلُ مَنْ يَنْشَقُّ عَنْهُ الْقَبْرُ وَأَوَّلُ شَافِعٍ وَأَوَّلُ مُشَفَّعٍ " رواه مسلم  

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: ((Mimi ni Bwana wa mtoto wa Aadam Siku ya Qiyaamah, na (mimi) wa kwanza ambaye kaburi lake litapasuka, na wa kwanza wa kushufai, na wa kwanza ambaye atakayeombewa Ash-Shafaa’ah)) [Muslim]

 

An-Nawawiy akasema katika Sharh Swahiyh Muslim: “Hadiyth hii ni dalili ya ubora wake Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam juu ya viumbe wote wengineo kwa sababu madhehebu ya Ahlus-Sunnah wanawafikiana kwamba bin Aadam ni bora kuliko Malaika, naye Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam ni bora kuliko bin Aadam wengineo.”

 

 

Share

02-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ametumwa Kwa Walimwengu Wote

Fadhila Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

02-Ametumwa Kwa Walimwengu Wote

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا كَافَّةً لِّلنَّاسِ بَشِيرًا وَنَذِيرًا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٢٨﴾

Na Hatukukutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa kwa watu wote uwe mbashiriaji na muonyaji, lakini watu wengi hawajui. [Sabaa: 28]

 

 

Ina maana: Kwa walimwengu wote ambao watahesabiwa matendo yao. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

 

Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

  وَكَانَ النَّبِيُّ يُبْعَثُ إِلَى قَوْمِهِ خَاصَّةً، وَبُعِثْتُ إِلَى النَّاسِ عَامَّةً

Na alikuwa Nabiy akitumwa kwa watu wake pekee, lakini mimi nimetumwa kwa watu wote.” [Hadiyth ya Jaabir bin ‘Abdillaah (رضي الله عنه) -Al-Bukhaariy (5011)]  

 

Kwa hiyo yeye ni pekee aliyetumwa kwa walimwengu wote wakiwemo majini na  bin Aadam; wakiwa ni waarabu, waajemi, wahindi, waafrika na kadhaalika kama alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

وَبُعِثْتُ إِلَى كُلِّ أَحْمَر وَأَسْوَد

((… Na nimetumwa kwa (bin Aadam) wekundu wote na weusi)) [Muslim]

 

 

Mujaahid amesema:  “Hii inamaanisha: Kwa majini na kwa bin Aadam.”  Wengineo wamesema: “Kwa Waarabu na wasio Waarabu.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

 

Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Alimuamrisha Rasuli Wake  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aseme:

 

قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا  

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi ni Rasuli wa Allaah kwenu nyinyi nyote.  [Al-A’raaf: 158]

 

 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

تَبَارَكَ الَّذِي نَزَّلَ الْفُرْقَانَ عَلَىٰ عَبْدِهِ لِيَكُونَ لِلْعَالَمِينَ نَذِيرًا ﴿١﴾

Amebarikika Ambaye Ameteremsha kwa mja Wake pambanuo (la haki na batili) ili awe muonyaji kwa walimwengu. [Al-Furqaan: 1]

 

Share

03-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) Ni Nabiy Wa Mwisho

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم) 

03-Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) Ni Nabiy Wa Mwisho

www.alhidaaya.com

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amethibitisha katika Qur-aan kwamba Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni Nabiy wa mwisho baada ya Manabii na Rusuli wote, kuanzia Nabiy Aadam ('Alayhis-Salaam) mpaka Nabiy ‘Iysaa ('Alayhis-Salaam) kisha wa mwisho kabisa ndiye Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَـٰكِن رَّسُولَ اللَّـهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا ﴿٤٠﴾

Hakuwa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) baba wa yeyote miongoni mwa wanaume wenu, lakini ni Rasuli wa Allaah na ni mwisho wa Manabii. Na Allaah daima ni Mjuzi wa kila kitu. [Al-Ahzaab: 30]

 

Wafasiri wa Qur-aan wamesema kwamba inamaanisha hakuna tena Wahyi na Risala kutoka mbinguni, kwa maana Qur-aan ni Kitabu cha mwisho na uthibitiso Wake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema pia katika kauli Yake Aliyoiteremsha pindi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliposimama Siku ya ‘Arafah kuwakhutubia Maswahaba katika Hijjah yake ya kuaga:

 

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ۚ  

Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na Nimekutimizieni neema Yangu, na Nimekuridhieni Uislamu uwe Dini yenu.  [Al-Maaidah: 3]

 

Na uthibitisho mwengine ni katika Hadiyth zake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):  

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضى الله عنه) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إِنَّ مَثَلِي وَمَثَلَ الأَنْبِيَاءِ مِنْ قَبْلِي كَمَثَلِ رَجُلٍ بَنَى بَيْتًا فَأَحْسَنَهُ وَأَجْمَلَهُ، إِلاَّ مَوْضِعَ لَبِنَةٍ مِنْ زَاوِيَةٍ، فَجَعَلَ النَّاسُ يَطُوفُونَ بِهِ وَيَعْجَبُونَ لَهُ، وَيَقُولُونَ هَلاَّ وُضِعَتْ هَذِهِ اللَّبِنَةُ قَالَ فَأَنَا اللَّبِنَةُ، وَأَنَا خَاتِمُ النَّبِيِّينَ )) البخاري ومسلم

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mfano wangu na mfano wa Mananbii wa kabla yangu ni kama mfano wa mtu aliyejenga nyumba akaifanya nzuri na kuipamba isipokuwa sehemu moja ya tofali katika kona. Watu wakawa wanalizunguka na kustaabishwa uzuri wake na husema: “Je, hili tofali litajazwa sehemu yake?” Basi mimi ndio tofali, nami ndiye Nabiy wa mwisho)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Na pia:

 

عن أَنَس بْن مَالِكٍ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: (( إِنَّ الرِّسَالَةَ وَالنُّبُوَّةَ قَدِ انْقَطَعَتْ فَلاَ رَسُولَ بَعْدِي وَلاَ نَبِيَّ)) ‏ قَالَ فَشَقَّ ذَلِكَ عَلَى النَّاسِ فَقَالَ: ((لَكِنِ الْمُبَشِّرَاتُ))‏.‏ قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ وَمَا الْمُبَشِّرَاتُ؟  قَالَ: ((رُؤْيَا الْمُسْلِمِ وَهِيَ جُزْءٌ مِنْ أَجْزَاءِ النُّبُوَّةِ)) حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ غَرِيبٌ الترمذي وصححه الالباني (2272)

 

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamb Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Risala za Unabii zimekatika, kwa hiyo hakuna Rasuli baada yangu wala Nabiy)). Akasema (Anas) Ikawa (khabari) nzito kwa watu kisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Isipokuwa Mubash-shiraat [wabashiriaji])) Wakasema: Ee Rasuli wa Allaah? Nini Mubash-shiraat? Akasema: ((Ndoto ya Muislamu nayo ni chembe ya sehemu  katika sehemu ya Unabiy)) [Hadiyth Hasan, Swahiyh Ghariyb At-Tirmidhiy (2272) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy, na katika Irwaa Al-Ghaliyl kwa daraja ya Swahiyh kwa sharti ya Imaam Muslim, na Imaam Al-Waadi’iy katika Swahiyh Al-Musnad pia kwa daraja ya Swahiyh kwa sharti ya Imaam Muslim]

 

Share

04-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Asemayo Ni Wahyi Kutoka Kwa Allaah

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

04-Asemayo Ni Wahyi Kutoka Kwa Allaah

 

www.alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa): 

 

وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣﴾

Na wala hatamki kwa hawaa.

 

 

إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ﴿٤﴾

Hayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa. [An-Najm: 3-4]

 

 

Imaam As-Sa’dy amesema: “Yaani matamko yake hayatokani na hawaa (matamanio) ya nafsi yake.”

 

Na katika Hadiyth:

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو، قَالَ كُنْتُ أَكْتُبُ كُلَّ شَىْءٍ أَسْمَعُهُ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أُرِيدُ حِفْظَهُ فَنَهَتْنِي قُرَيْشٌ وَقَالُوا:   "أَتَكْتُبُ كُلَّ شَىْءٍ تَسْمَعُهُ وَرَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بَشَرٌ يَتَكَلَّمُ فِي الْغَضَبِ وَالرِّضَا؟" فَأَمْسَكْتُ عَنِ الْكِتَابِ فَذَكَرْتُ ذَلِكَ لِرَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَأَوْمَأَ بِأُصْبُعِهِ إِلَى فِيهِ فَقَالَ: ((اكْتُبْ فَوَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ مَا يَخْرُجُ مِنْهُ إِلاَّ حَقٌّ)) السلسلة الصحيحة  4 / 45

 

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr ibn Al-‘Aasw (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nilikuwa naandika kila nilichokisia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), nikakusudia kuyahifadhi, lakini Maquraysh walinikataza wakasema:  “Je, unaandika kila unachomsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye ni bin Aadam tu anaongea kwa ghadhabu na kwa furaha?” Nikaacha kuandika kisha nikamtajia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaashiria kidole chake mdomoni mwake akasema: ((Andika! Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi mwake, hakuna kinachotoka humu isipokuwa haki)) [Abuu Daawuwd na ameisahihisha Al-Albaaniy katika As-Silsilah Asw-Swahiyhah (4/45) (1032)]

 

Na Wahyi ni aina tatu kama walivyosema ‘Ulamaa akiwemo Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) katika Majmuw’ Fataawaa: Kwanza ni Maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika Qur-aan. Pili ni Maneno ya Allaah ('Azza wa Jalla) katika Hadiyth Al-Qudsiy na tatu ni maneno ayasemayo yeye Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo Allaah ('Azza wa Jalla) Anamfunulia Wahyi nayo ni katika Hadiyth zilizothibiti usahihi wake, kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

 

وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ﴿٤٤﴾

Na Tumekuteremshia Ukumbusho (Qur-aan) ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao huenda wakapata kutafakari. [An-Nahl: 44]

 

Kwa maana: Imeteremshwa Al-Quraan ili iwe wazi kufahamika kwa watu yale ambayo yamefichika maana zake na hukmu zake. [At-Tafsiyr Al-Muyassar]

 

Naye Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

((أَلَا إِنِّي أُوتِيتُ الْقُرْآنَ وَمِثْلَهُ مَعَهُ)) صحيح رواه أبو داود

((Hakika mimi nimepewa Qur-aan na mfano wake)) [Hadiyth Swahiyh, Abuu Daawuwd]

 

Share

05-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Katumwa Kuwa Ni Rahmah Kwa Ulimwengu

Fadhila Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

05-Katumwa Kuwa Ni Rahmah Kwa Ulimwengu

 

www.alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِّلْعَالَمِينَ ﴿١٠٧﴾

Na Hatukukutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa ni rahmah kwa walimwengu. [Al-Anbiyaa: 107]

 

 

Ibn ‘Abaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: “Allaah Amemtuma Nabiy Wake Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa ni rahmah kwa ulimwengu mzima; Waumini na makafiri. Ama Muumini miongoni mwao ni ambaye Allaah Amemwongoza kupitia kwake na Akamwingiza Jannah (Peponi) kwa sababu ya kumwamini kwake, na kwa kufanyia kazi yale aliyokuja nayo kutoka kwa Allaah. Ama kafiri ni vile kucheleweshewa balaa(na adhabu) ambazo zilikuwa zikawateremkea ummah za awali zilizokanusha waliowafikishia Risala kabla yao.” [Tafsiyr Atw-Twabariy, Ibn Kathiyr]

 

 

Rahmah kwa Waumini pia ni vile kuwatoa kutoka katika kiza na kuwaingiza katika mwanga kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

رَّسُولًا يَتْلُو عَلَيْكُمْ آيَاتِ اللَّـهِ مُبَيِّنَاتٍ لِّيُخْرِجَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۚ وَمَن يُؤْمِن بِاللَّـهِ وَيَعْمَلْ صَالِحًا يُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۖ قَدْ أَحْسَنَ اللَّـهُ لَهُ رِزْقًا﴿١١﴾

Ni Rasuli anakusomeeni Aayaat za Allaah zinazobainisha; ili kuwatoa wale walioamini na wakatenda mema kutoka kwenye viza kuingia katika Nuru. Na yeyote anayemwamini Allaah na akatenda mema, Atamuingiza Jannaat zipitazo chini yake mito ni wenye kudumu humo abadi. Allaah Amekwishamfanyia rizki nzuri kabisa. [Atw-Twalaaq: 11]

 

Na mifano katika Hadiyth:

 

 عَنْ عَمْرِو بْنِ أَبِي قُرَّةَ، قَالَ كَانَ حُذَيْفَةُ بِالْمَدَائِنِ فَكَانَ يَذْكُرُ أَشْيَاءَ قَالَهَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم لأُنَاسٍ مِنْ أَصْحَابِهِ فِي الْغَضَبِ فَيَنْطَلِقُ نَاسٌ مِمَّنْ سَمِعَ ذَلِكَ مِنْ حُذَيْفَةَ فَيَأْتُونَ سَلْمَانَ فَيَذْكُرُونَ لَهُ قَوْلَ حُذَيْفَةَ فَيَقُولُ سَلْمَانُ: "حُذَيْفَةُ أَعْلَمُ بِمَا يَقُولُ" فَيَرْجِعُونَ إِلَى حُذَيْفَةَ فَيَقُولُونَ لَهُ:  "قَدْ ذَكَرْنَا قَوْلَكَ لِسَلْمَانَ فَمَا صَدَّقَكَ وَلاَ كَذَّبَكَ" ‏.‏ فَأَتَى حُذَيْفَةُ سَلْمَانَ وَهُوَ فِي مَبْقَلَةٍ فَقَالَ: "يَا سَلْمَانُ مَا يَمْنَعُكَ أَنْ تُصَدِّقَنِي بِمَا سَمِعْتُ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم؟" فَقَالَ سَلْمَانُ: "إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَغْضَبُ فَيَقُولُ فِي الْغَضَبِ لِنَاسٍ مِنْ أَصْحَابِهِ وَيَرْضَى فَيَقُولُ فِي الرِّضَا لِنَاسٍ مِنْ أَصْحَابِهِ ،   أَمَا تَنْتَهِي حَتَّى تُوَرِّ ثَ رِجَالاً حُبَّ رِجَالٍ وَرِجَالاً بُغْضَ رِجَالٍ وَحَتَّى تُوقِعَ اخْتِلاَفًا وَفُرْقَةً وَلَقَدْ عَلِمْتَ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم خَطَبَ فَقَالَ: ((أَيُّمَا رَجُلٍ مِنْ أُمَّتِي سَبَبْتُهُ سَبَّةً أَوْ لَعَنْتُهُ لَعْنَةً فِي غَضَبِي - فَإِنَّمَا أَنَا مِنْ وَلَدِ آدَمَ أَغْضَبُ كَمَا يَغْضَبُونَ وَإِنَّمَا بَعَثَنِي رَحْمَةً لِلْعَالَمِينَ - فَاجْعَلْهَا عَلَيْهِمْ صَلاَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ))‏ ‏

   

 

‘Amr bin Abiy Qurrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: “Hudhayfah alikuwa Madaayin akawa anataja mambo ambayo aliyasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa katika ghadhabu kwa watu katika Maswahaba zake. Watu waliomsikia Hudhayfah walikuwa wakimwendea Salmaan na kumwambia mambo aliyoyasema Hudhayfah.  Salmaan akawa anasema: “Hudhayfah anajua zaidi aliyoyasema.” Kisha wao humjibu Hudhayfah na kumwambia: “Tumemtajia Salmaan yale uliyoyasema, lakini hakukusadiki wala hakukukanusha.” Kisha Hudhayfah akamwendea Salmaan ambaye alikuwa katika shamba lake la mboga akasema: “Ee Salmaan, kitu gani kilichokuzuia usinisadikishe uliyoyasikia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)?” Salmaan akasema: “Hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akighadhibika na huwaambia watu kati ya Maswahaba zake (maneno) ya ghadhabu, na huwa katika furaha na hapo huwasemesha watu kwa furaha.  Je, hivi hutoacha mpaka utie mapenzi ya watu katika nyoyo za watu na utie chuki za watu katika nyoyo za watu hadi usababishe watu kukhitilafiana na kufarikiana? Unajua kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikhutubia akasema: ((Ikiwa kuna mtu yeyote katika Ummah wangu ambaye nilimtolea lugha isiyo nzuri nilipokuwa katika ghadhabu au kumlaani - basi hakika mimi ni katika wana Aadam, hughadhibika kama mnavyoghadhibika. Hakika Allaah Amenitumia kuwa ni rahmah kwa walimwengu. (Ee Allaah) Ijaalie (ghadhabu au laana yangu) iwe du’aa (ya kuwatakasa, ujira na kikurubishho kwa Allaah),  Siku ya Qiyaamah)) [Sunan Abiy Daawuwd na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Abiy Daawuwd, As-Silsilah Asw-Swahiyhah, Swahiyh Al-Jaami’

 

 

Ama rahmah kwa makafiri ni kama mfano wa Hadiyth:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ قِيلَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ ادْعُ عَلَى الْمُشْرِكِينَ قَالَ: ((إِنِّي لَمْ أُبْعَثْ لَعَّانًا وَإِنَّمَا بُعِثْتُ رَحْمَةً)) مسلم  

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba ilisemwa: Ee Rasuli wa Allaah! Omba du’aa dhidi ya makafiri.” Akasema: ((Hakika mimi sikutumwa kuwa ni mwenye kuomba laana  bali hakika nimetumwa kuwa ni rahmah)) [Muslim]

 

Mfano wa rahmah kwa wanyama ni Hadiyth:

 

عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ:  كُنَّا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي سَفَرٍ فَانْطَلَقَ لِحَاجَتِهِ فَرَأَيْنَا حُمَّرَةً مَعَهَا فَرْخَانِ فَأَخَذْنَا فَرْخَيْهَا فَجَاءَتِ الْحُمَّرَةُ فَجَعَلَتْ تَفْرُشُ فَجَاءَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ: ((مَنْ فَجَعَ هَذِهِ بِوَلَدِهَا رُدُّوا وَلَدَهَا إِلَيْهَا)) ‏.‏ وَرَأَى قَرْيَةَ نَمْلٍ قَدْ حَرَّقْنَاهَا فَقَالَ: ((مَنْ حَرَّقَ هَذِهِ)) ‏.‏ قُلْنَا نَحْنُ ‏.‏ قَالَ: ((إِنَّهُ لاَ يَنْبَغِي أَنْ يُعَذِّبَ بِالنَّارِ إِلاَّ رَبُّ النَّارِ))

 

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdur-Rahmaan bin ‘Abdillaah kutoka kwa baba yake amesema: Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) safarini, akaondoka kwenda kujisaidia. Tukamuona ndege akiwa na (vitoto vyake) viwili vidogo. Tukavichukua vidogo. Yule ndege akaja akawa anatandaza mbawa zake. Kisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaja na akasema: ((Nani aliyemtia majonzi  huyu kwa kwa kumpotezea vidogo vyake? Mrudishieni vidogo vyake)) Akaona pia mdudu chungu wa shamba tuliyemuunguza, akasema: ((Nani kamuunguza?)) Tukasema: “Sisi.” Akasema: ((Hakika haijuzu yeyote kuadhibu kwa moto isipokuwa Rabb wa moto)) [Sunan Abiy Daawuwd (2765), ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Abiy Daawuwd, As-Silsilah Asw-Swahiyhah]  

 

 

Na pia rahmah yake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika kuchinja wanyama:

 

عَنْ شَدَّادِ بْنِ أَوْسٍ، قَالَ ثِنْتَانِ حَفِظْتُهُمَا عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إِنَّ اللَّهَ كَتَبَ الإِحْسَانَ عَلَى كُلِّ شَىْءٍ فَإِذَا قَتَلْتُمْ فَأَحْسِنُوا الْقِتْلَةَ وَإِذَا ذَبَحْتُمْ فَأَحْسِنُوا الذَّبْحَ وَلْيُحِدَّ أَحَدُكُمْ شَفْرَتَهُ فَلْيُرِحْ ذَبِيحَتَهُ))

 

Imepokelewa kutoka kwa Shaddaad bin Aws (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: “Mambo mawili nimeyahifadhi kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Hakika Allaah Ameamrisha kufanya wema katika kila jambo, basi mkiua ueni vizuri, na mkichinja chinjeni vyema, na atie makali kisu chake anayetaka kuchinja ili amuondoshee adhabu kichinjwa chake)) [Muslim, Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaa’iy, Ibn Maajah na Ad-Daarimiy]

 

Share

06-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Amechaguliwa Kutoka Kizazi Cha Nabiy Ismaa’iyl Kisha Katika Nasaba Na Kabila Bora Kabisa

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

06-Amechaguliwa Kutoka Kizazi Cha Nabiy Ismaa’iyl

Kisha Katika Nasaba Na Kabila Bora Kabisa.

 

www.alhidaaya.com

 

 

Nabiy Ismaa’iyl ('Alayhis-Salaam) pamoja na mama yake Haajar walikuwa ni watu wa mwanzo kabisa kuishi Makkah baada ya Nabiy Ibraahiym ('Alayhis-Salaam) kuwaacha katika bonde la Makkah ambako hapakuwa na maisha yoyote. Kisha baada ya Nabiy Ibraahiym ('Alayhis-Salaam)  kujenga Al-Ka’bah, pamoja na mwanawe Nabiy Ismaa’iyl ('Alayhis-Salaam) akawaacha hapo Makkah na Nabiy Ismaa’iyl ('Alayhis-Salaam) akaoa na ndipo kizazi chake kikaendelea na kuendelea mpaka kufikia kuzaliwa Nabiy wa mwisho, naye ni Nabiy wetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Amethibitisha hayo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hadiyth:

 

عَنْ وَاثِلَةَ بْنِ الأَسْقَعِ، رضى الله عنه قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((إِنَّ اللَّهَ اصْطَفَى مِنْ وَلَدِ إِبْرَاهِيمَ إِسْمَاعِيلَ وَاصْطَفَى مِنْ وَلَدِ إِسْمَاعِيلَ بَنِي كِنَانَةَ وَاصْطَفَى مِنْ بَنِي كِنَانَةَ قُرَيْشًا وَاصْطَفَى مِنْ قُرَيْشٍ بَنِي هَاشِمٍ وَاصْطَفَانِي مِنْ بَنِي هَاشِمٍ))‏ ‏ قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ‏.

Imepokelewa kutoka kwa Waathilah bin Al-Asqa’ akisema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Allaah Amemteua Ismaa’iyl katika wana wa Ibraahiym, na Amemteua  Kinaanah kutoka wana wa Ismaa’iyl, na Amemteua  Quraysh kutokana na Kinaanah na Ameteua Baniy Haashim kutokana na Quraysh na Ameniteua mimi kutokana na Baniy Haashim)) [At-Tirmidhiy, ameisahihisha Imaam Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (3605)]

 

Na pia:

 

عَنْ الْمُطَّلِبِ بْنِ أَبِي وَدَاعَةَ قَالَ: جَاءَ الْعَبَّاسُ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَكَأَنَّهُ سَمِعَ شَيْئًا فَقَامَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى الْمِنْبَرِ فَقَالَ:  ((مَنْ أَنَا؟)) فَقَالُوا:  أَنْتَ رَسُولُ اللَّهِ عَلَيْكَ السَّلَامُ، قَالَ:  ((أَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، إِنَّ اللَّهَ خَلَقَ الْخَلْقَ فَجَعَلَنِي فِي خَيْرِهِمْ فِرْقَةً، ثُمَّ جَعَلَهُمْ فِرْقَتَيْنِ فَجَعَلَنِي فِي خَيْرِهِمْ فِرْقَةً، ثُمَّ جَعَلَهُمْ قَبَائِلَ فَجَعَلَنِي فِي خَيْرِهِمْ قَبِيلَةً،  ثُمَّ جَعَلَهُمْ بُيُوتًا فَجَعَلَنِي فِي خَيْرِهِمْ بَيْتًا وَخَيْرِهِمْ نَسَبًا)) قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ

Kutoka kwa ‘Al-Mutw-twalib bin Abiy Wadaa’ah amesema: Al-‘Abbaas alikuja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kama kwamba alisikia jambo, basi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasimama katika minbari akasema: ((Je, mimi ni nani?)) Wakasema: “Wewe ni Rasuli wa Allaah ‘Alaykas-salaam.” Akasema: ((Mimi ni Muhammad bin ‘Abdillaah bin ‘Abdil-Mutw-twalib. Hakika Allaah Ameumba viumbe Akanijaalia kuwa katika kundi bora lao. Kisha Akawafanya kuwa katika makundi mawili, Akanijaalia kuwa katika kundi bora kati ya hayo (mawili). Kisha Akafanya makabila Akanijaalia kuwa katika kabila bora kati ya hayo. Kisha Akafanya nyumba Akanijaalia kuwa ni mbora wao katika hizo kwa kabila na unasaba)) [At-Tirmidhiy - Swahiyh Al-Jaami’ (1472)]

 

Nasaba ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) inayomalizikia kwa ‘Adnaan inakubalika kuwa ni Swahiyh kwa ‘Ulamaa  wote wa Siyrah na wale wanaodurusu nasaba za watu mashuhuri, nayo ni kama ifuatavyo:

 

Muhammad bin ‘Abdillaah bin ‘Abdil-Muttwalib bin Haashim bin ‘Abd-Manaaf bin Quswayy  bin Kilaab bin Murrah bin Ka’ab bin Luayy bin Ghaalib bin Fihr bin Maalik bin Nadhwar bin Kinaanah bin Khuzaymah bin Mudrikah bin Ilyaas bin Madhwar bin Nizaar bin Ma’di bin ‘Adnaan.

 

Kisha inaendelea mpaka kufikia kwa Nabiy Ismaa’iyl ('Alayhis-Salaam).

 

Na katika Hadiyth ndefu ya ‘Abdullaah bin ‘Abbaas pindi Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipomwandikia barua mfalme wa Roma kisha mfalme huyo akawa anamuuliza Abuu Sufyaan maswali kadhaa kuhusu Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):    

 

ثُمَّ قَالَ لِتُرْجُمَانِهِ قُلْ لَهُ كَيْفَ نَسَبُ هَذَا الرَّجُلِ فِيكُمْ قُلْتُ هُوَ فِينَا ذُو نَسَبٍ‏.

…kisha (mfalme wa Roma akamuuliza mwenye kutarjumi. “Muulize, je, huyo mtu (yaani Nabiy Muhammad Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anatokana na nasaba gani?” Nikajibu: “Anatokana na nasaba bora kabisa kati yetu.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Share

07-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Allaah Na Malaika Wanamswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Na Amri Kwa Waumini Wamswalie

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

07-Allaah Na Malaika Wanamswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

Na Amri Kwa Waumini Wamswalie

 

www.alhidaaya.com

 

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

 

إِنَّ اللَّـهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ ۚ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٥٦﴾

Hakika Allaah na Malaika Wake wanamswalia Nabiy. Enyi walioamini mswalieni na msalimieni kwa maamkizi ya amani na kwa tasliymaa.  [Al-Ahzaab 33: 56]

 

Maana ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): Ni kumsifia kwa Malaika, kumteremshia rahmah na baraka, fadhila n.k.

 

Maana ya Malaika Wake kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni kumuombea kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  du’aa Amghufurie na Amteremshie baraka.  

 

Maana ya Waumini kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni kumuombea kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) du’aa na amani. Juu ya hivyo Waumini kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) inawarudia wenyewe thawabu tele kutokana na fadhila zilizotajwa katika Hadiyth kadhaa za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), miongoni mwazo ni:

 

عنْ عبد اللَّه بن عمرو بن العاص رضي اللَّه عنْهُمَا أنَّهُ سمِع رسُول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يقُولُ: ((مَنْ صَلَّى عَلَيَّ صَلاَةً، صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ بِهَا عشْراً))  رواهُ مسلم

Imetoka kwa 'Abdullaah bin 'Amru bin Al'-Aasw (رضي الله عنهما)  kwamba kamsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Atakayeniswalia mara moja, Allaah Atamswalia mara kumi)) [Muslim]

 

Na pia:

 

عن ابن مسْعُودٍ رضي اللَّه عنْهُ أنَّ رسُول اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال: ((أَوْلى النَّاسِ بي يوْمَ الْقِيامةِ أَكْثَرُهُم عَليَّ صلاةً)) رواه الترمذي وقال: حديثٌ حسنٌ

Imetoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Watu wa mwanzo kwangu (watakaokuwa karibu yangu) siku ya Qiyaamah ni wale wanaoniswalia sana))  [At-Tirmidhy na kasema ni Hadiyth Hasan]

 

 

Na pia:

 

عنْ أبي هُريْرةَ رضي اللَّه عنهُ أنَّ رسُولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال: ((ما مِنْ أحد يُسلِّمُ علَيَّ إلاَّ ردَّ اللَّه علَيَّ رُوحي حَتَّى أرُدَّ عَليهِ السَّلامَ)) رواهُ أبو داود بإسناد صحيحٍ

Imetoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hapana yeyote atakayeniswalia ila Allaah Hurudishia mimi roho yangu hadi nimrudishie salaam (huyo aliyenisalimia))) [Abuu Daawuwd kwa IsnaadHasan]

 

 

Share

08-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Swalaah Zetu Hazitimii Ila Baada Kutamka Shahada Mbili Na Kumswalia

 Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

08-Swalaah Zetu Hazitimii Ila Baada Kutamka Shahada Mbili Na Kumswalia

www.alhidaaya.com

 

 

Katika Swalaah zetu tunapokaa kikao cha Tashahhud, huwa tunamtaja Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kushuhudia kwamba yeye ni Rasuli wa Allaah na kisha tunamswalia kwa kutamka Swalaah inayojulikana kwa ni Swalaatul-Ibraahimiyyah.  Kikako cha Tashahhud ni mojawapo ya nguzo za Swalaah ambayo bila ya kufanya hivyo, Swalaah haitimii.

 

Tunavyotamaka tashahhud na aina za kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):  

 

 

 التَّحِيّـاتُ للهِ وَالصَّلَـواتُ والطَّيِّـبات، السَّلامُ عَلَيـكَ أَيُّهـا النَّبِـيُّ وَرَحْمَـةُ اللهِ وَبَرَكـاتُه، السَّلامُ عَلَيْـنا وَعَلـى عِبـادِكَ الصَّـالِحـين، أَشْـهَدُ أَنْ لا إِلـهَ إِلاّ الله، وَأَشْـهَدُ أَنَّ مُحَمّـداً عَبْـدُهُ وَرَسـولُه

 

At-tahiyyaatu liLLaahi, was-swalawaatu, wat-twayyibaatu, Assalaamu ‘alayka ayyuhan-Nnabiyyu warahmatu-Allaahi wa Barakaatuh, Assalaamu ‘alaynaa wa ’alaa ‘IbaadiLLaahis-swaalihiyn. Ash-hadu an-laa ilaaha illa-Allaah wa ash-hadu anna Muhammadan ‘Abduhu wa Rasuwluhu

 

Maamkuzi mema na Rehma na mazuri yote (ni kwa Allaah), amani ziwe juu yako ee Nabiy na Rehma za Allaah na Baraka Zake,  amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Allaah walio wema. Nashuhudia (kwa kuamini moyoni na kukiri) kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, na nashuhudia (kwa kuamini moyoni na kukiri) kwamba Muhammad ni mja Wake na ni Rasuli Wake. [Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Mas-‘uwd (رضي الله عنه)  - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (2/311), Muslim (1/301)]

 

 اللّهُـمَّ صَلِّ عَلـى مُحمَّـد وَعَلـى آلِ مُحمَّد كَمـا صَلَّيـتَ عَلـى إبْراهـيمَ وَعَلـى آلِ إبْراهـيم إِنَّكَ حَمـيدٌ مَجـيد، اللّهُـمَّ بارِكْ عَلـى مُحمَّـد وَعَلـى آلِ مُحمَّـد كَمـا بارِكْتَ عَلـى إبْراهـيمَ وَعَلـى آلِ إبْراهيم إِنَّكَ حَمـيدٌ مَجـيد .

 

Allaahumma Swalli ‘alaa Muhammad wa ‘alaa aali Muhammad, kamaa Swallayta ‘alaa Ibraahiyma wa ‘alaa aali Ibraahiyma, Innaka Hamiydun Majiyd. Allaahumma Baarik ‘alaa Muhammad, wa ‘alaa aali Muhammad, kamaa Baarakta ‘alaa  Ibraahiyma wa ‘alaa  aali Ibraahiyma, Innaka Hamiydun Majiyd.

 

 

Ee Allaah! Mswalie Muhammad, na jamaa wa Muhammad, kama Ulivyomswalia Ibraahiym na juu ya jamaa zake Ibraahiym, hakika Wewe ni Mwenye Kusifika Mtukufu. Ee Allaah! Mbariki Muhammad na jamaa zake Muhammad kama Ulivyombariki Ibraahiym na juu ya jamaa zake Ibraahiym, hakika Wewe ni Mwenye Kusifika Mtukufu. [Hadiyth ya Ka’ab bin ‘Ujrah (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (6/408)]

 

 

اللّهُـمَّ صَلِّ عَلـى مُحمَّـدٍ وَعَلـى أَزْواجِـهِ وَذُرِّيَّـتِه كَمـا صَلَّيْـتَ عَلـى آلِ إبْراهـيم، وَبارِكْ عَلـى مُحمَّـدٍ وَعَلـى أَزْواجِـهِ وَذُرِّيَّـتِه كَمـا بارِكْتَ عَلـى آلِ إبْراهـيم إِنَّكَ حَمـيدٌ مَجـيد

 

Allaahumma Swalli ‘alaa Muhammad, wa ‘alaa azwaajihi wa dhurriyaatihi, kamaa Swallayta ‘alaa aali Ibraahiyma, wa Baarik ‘alaa Muhammad, wa ’alaa azwaajihi wa dhurriyaatihi, kamaa Baarakta ‘alaa aali Ibraahiyma, Innaka Hamiydun Majiyd

 

Ee Allaah! Mswalie Muhammad na wake zake na kizazi chake, kama Ulivyowaswalia jamaa zake Ibraahiym, na Mbariki Muhammad na wake zake na kizazi chake kama Ulivyowabariki jamaa zake Ibraahiym, hakika Wewe ni Mwenye Kusifika Mtukufu. [Hadiyth ya Abu Humayd As-Saa’adiy Al-Mundhir (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (6/407), Muslim (1/306) na tamashi lake]

 

 

 

Share

09-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kapewa Majina Kadhaa Ya Kusifiwa Na Allaah

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

09-Kapewa Majina Kadhaa Ya Kusifiwa Na Allaah

www.alhidaaya.com

 

 

عن جبير بن مطعم رضي الله عنه أن رسول اللهصلى الله عليه وسلم قال: ((إنَّ لِيْ أَسْمَاءً، أَنَا مُحَمَّدٌ، وَأَنَا أَحْمَدُ، وَأَنَا المَاحِي الَّذِي يَمْحُو الله بِيَ الكُفْرَ، وَأَنَا الحَاشِرُ الَّذِي يُحْشَرُ النَّاسُ عَلَى قَدَمَيَّ، وَأَنَا العَاقِبُ الَّذِي لَيْسَ بَعْدَهُ أَحَدٌ))

 

 وفي لفظ  ((وَنَبِيُّ التَّوبَةِ، وَنَبِيُّ الرَّحْمَةِ)) . متفق عليه.

 

Imepokelewa kutoka kwa Jubayr bin Mutw’im (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mimi nina majina kadhaa: Mimi ni Muhammad na mimi ni Ahmad, na mimi ni Al-Maahiy (mfutaji) ambaye Allaah Hufuta kufru kupitia kwangu, na mimi ni Al-Haashir (mkusanyaji) ambaye watu watakusanywa mbele ya miguu yangu (Siku ya Qiyaamah), na mimi ni Al-‘Aaqib (Wa mwisho) ambaye hakuna baada yake mtu (Nabiy))   [Muslim]

 

Na katika lafdhi nyengine:  ((Na Nabiy wa Tawbah na Nabiy wa Rahmah)) [Muslim]

 

 

 

  

Share

10-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Aliyepata Ummah Wa Watu Wengi Kuliko Manabii Wote

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

10-Aliyepata Ummah Wa Watu Wengi Kuliko Manabii Wote

www.alhidaaya.com

 

 

 

 

عن اِبْن عَبَّاسٍ عَنْ اَلنَّبِيِّ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) أَنَّهُ قَالَ: ((عُرِضَتْ عَلَيَّ الأُمَمُ فَرَأَيْتُ اَلنَّبِيَّ وَمَعَهُ اَلرَّهْطُ، وَالنَّبِيَّ وَمَعَهُ اَلرَّجُلُ وَالرَّجُلاَنِ، وَالنَّبِيَّ وَلَيْسَ مَعَهُ أَحَدٌ، إِذْ رُفِعَ لِي سَوَادٌ عَظِيمٌ فَظَنَنْتُ أَنَّهُمْ أُمَّتِي، فَقِيلَ لِي هَذَا مُوسَى وَقَوْمُهُ، فَنَظَرْتُ فَإِذَا سَوَادٌ عَظِيمٌ، فَقِيلَ لِي هَذِهِ أُمَّتُكَ، وَمَعَهُمْ سَبْعُونَ أَلْفًا يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ بِغَيْرِ حِسَابٍ وَلاَ عَذَابٍ))

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema: ((Ummah zote zilipitishwa mbele yangu, nikamuona Nabiy akiwa na kundi dogo la watu, na Nabiy akiwa na mtu mmoja au wawili, na Nabiy akiwa hana mtu yeyote. Kisha nikaonyeshwa idadi kubwa ya watu niliodhania ni katika Ummah wangu, lakini nikaambiwa: Huyo ni Muwsaa na watu wake. Kisha nikatazama nikaona kundi kubwa ambalo nikaamibwa: Hawa ni watu wako, na pamoja nao humo, ni watu elfu sabiini watakaoingia Jannah (Peponi) bila hesabu wala adhabu)) [Al-Bukhaariy (3410) Muslim (220)]

 

Share

11-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Allaah Amemfanya Kuwa Khaliyl Wake

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

11-Allaah Amemfanya Kuwa Khaliyl Wake

 

www.alhidaaya.com

 

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ الْحَارِثِ النَّجْرَانِيِّ، قَالَ حَدَّثَنِي جُنْدَبٌ ، قَالَ سَمِعْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَبْلَ أَنْ يَمُوتَ بِخَمْسٍ وَهُوَ يَقُولُ: ((إِنِّي أَبْرَأُ إِلَى اللَّهِ أَنْ يَكُونَ لِي مِنْكُمْ خَلِيلٌ فَإِنَّ اللَّهَ تَعَالَى قَدِ اتَّخَذَنِي خَلِيلاً كَمَا اتَّخَذَ إِبْرَاهِيمَ خَلِيلاً وَلَوْ كُنْتُ مُتَّخِذًا مِنْ أُمَّتِي خَلِيلاً لاَتَّخَذْتُ أَبَا بَكْرٍ خَلِيلاً، أَلاَ وَإِنَّ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ كَانُوا يَتَّخِذُونَ قُبُورَ أَنْبِيَائِهِمْ وَصَالِحِيهِمْ مَسَاجِدَ أَلاَ فَلاَ تَتَّخِذُوا الْقُبُورَ مَسَاجِدَ إِنِّي أَنْهَاكُمْ عَنْ ذَلِكَ ))‏.‏

Imetoka kwa ‘Abdullah bin Al-Haarith An-Najraaniyy ambaye amesema:  “Jundub amenihadithia kwamba: Nimemsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema kabla siku tano za kufariki kwake:  ((Mimi niko huru mbele ya Allaah kwenu kuwa na Khaliyl.  Kwani Allaah Ta’aalaa Amenifanya kuwa Khaliyl kama Alivyomfanya Ibraahiym kuwa Khaliyl. (Rafiki kipenzi mwandani) Na ingelikuwa kumfanya mtu katika ummah wangu kuwa Khaliyl basi ningelimfanya Abuu Bakr kuwa Khaliyl (wangu). Tahadharini! Walio kabla yenu walikuwa wakifanya makaburi ya Manabii wao na watu wema wao kuwa ni mahali pa ‘ibaadah! Basi msifanye makaburi kuwa ni mahala pa ‘ibaadah hakika mimi nakukatazeni hivyo!)) [Muslim]

 

Maana ya Khaliyl: Amesema Shaykhul-Islaam ibn Taymiyyah:  “Ukhaliyl ni mapenzi kamilifu yanayolazimikana na ‘Ubuwdiyyah: (kumwabudu Allaah kikamilifu), na kutoka kwa Rabb Subhaanahu, ni ukamilifu wa  Ar-Rubuwbiyyah (Uola) kwa waja Wake wanaompenda Naye Anawapenda” [Risaalah Al-‘Ubuwdiyyah]

 

 

Sifa hiyo aliyopewa Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis-salaam) kuwa ni Khaliyl wa Allaah imethibiti katika kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَمَنْ أَحْسَنُ دِينًا مِّمَّنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ وَاتَّبَعَ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۗ وَاتَّخَذَ اللَّـهُ إِبْرَاهِيمَ خَلِيلًا ﴿١٢٥﴾

Na nani aliye bora zaidi kwa Dini kuliko yule aliyejisalimisha kwa Allaah naye ni mtendaji mazuri na akafuata millah ya Ibraahiym aliyejiengua na upotofu akaelemea Dini ya haki. Na Allaah Amemchukua Ibraahiym kuwa ni kipenzi. [An-Nisaa: 125]

 

Na Hadiyth nyenginezo:

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((لَوْ كُنْتُ مُتَّخِذًا مِنْ أَهْلِ الأَرْضِ خَلِيلاً لاَتَّخَذْتُ ابْنَ أَبِي قُحَافَةَ خَلِيلاً وَلَكِنْ صَاحِبُكُمْ خَلِيلُ اللَّهِ ))

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:  ((Ingelikuwa kumfanya mtu katika dunia hii kuwa Khaliyl, basi ningelimfanya Ibn Abiy Quhaafah (Abu Bakr Asw-Swiddiyq Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa ni Khalily (wangu) lakini Swahibu wenu ni Khaliyl wa Allaah)) [Muslim]

 

Katika usimulizi wa Sunan Ibn Maajah, Wakiy’ amesema kuhusu “Swahib wenu” amekusudia yeye mwenyewe Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

 

Na katika Riwaayah nyengine:

 

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم : ((أَلاَ إِنِّي أَبْرَأُ إِلَى كُلِّ خِلٍّ مِنْ خِلِّهِ وَلَوْ كُنْتُ مُتَّخِذًا خَلِيلاً لاَتَّخَذْتُ أَبَا بَكْرٍ خَلِيلاً إِنَّ صَاحِبَكُمْ خَلِيلُ اللَّهِ ‏))

 

((Mimi niko huru kutokana na utegemezi wa marafiki wote wapenzi na wandani. Ingelikuwa napaswa kumfanya mtu kuwa Khaliyl (Rafiki kipenzi mwandani), basi ningelimfanya Abuu Bakr. Hakika Allaah Amemfanya Swahib yenu kuwa Khaliyul Wake)) [Muslim]

 

 

 

Share

12-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Amefunguliwa Kifua Chake Kuoshwa Kwa Zamzam Na Kujazwa Hikma Na Iymaan

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

12-Amefunguliwa Kifua Chake Kuoshwa Kwa Zamzam Na Kujazwa Hikma Na Iymaan 

 

www.alhidaaya.com

 

 

أَنَسُ بْنُ مَالِكٍ كَانَ أَبُو ذَرٍّ رضى الله عنه يُحَدِّثُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((فُرِجَ سَقْفِي وَأَنَا بِمَكَّةَ، فَنَزَلَ جِبْرِيلُ  عَلَيْهِ السَّلاَمُ   فَفَرَجَ صَدْرِي، ثُمَّ غَسَلَهُ بِمَاءِ زَمْزَمَ، ثُمَّ جَاءَ بِطَسْتٍ مِنْ ذَهَبٍ مُمْتَلِئٍ حِكْمَةً وَإِيمَانًا، فَأَفْرَغَهَا فِي صَدْرِي، ثُمَّ أَطْبَقَهُ، ثُمَّ أَخَذَ بِيَدِي فَعَرَجَ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا‏.‏ قَالَ جِبْرِيلُ لِخَازِنِ السَّمَاءِ الدُّنْيَا: افْتَحْ‏.‏ قَالَ: مَنْ هَذَا؟  قَالَ: جِبْرِيلُ))

Imepokelewa kutoka kwa Anas kwamba Abuu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Paa la nyumba yangu lilifunguliwa nilipokuwa Makkah (usiku wa Israa wal-Mi’raaj) akateremka Jibriyl (‘alayhis-salaam) akafungua kifua changu kisha akakiosha kwa maji ya Zamzam. Kisha akaleta chombo cha dhahabu kilichojaa Hikmah na Iymaan  akamwaga ndani ya kifua changu kisha akikufnga.  Kisha akanikamata mkono wangu  akapanda mbingu ya dunia (ya karibu).  Jibrily akamwambia Mlinzi wa mbingu ya dunia afungue mlango.  Mlinzi akasema “Nani?” Akajibu:  “Jibriyl.” [Al-Bukhaariy] 

 

Pia:

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَتَاهُ جِبْرِيلُ صلى الله عليه وسلم وَهُوَ يَلْعَبُ مَعَ الْغِلْمَانِ فَأَخَذَهُ فَصَرَعَهُ فَشَقَّ عَنْ قَلْبِهِ فَاسْتَخْرَجَ الْقَلْبَ فَاسْتَخْرَجَ مِنْهُ عَلَقَةً فَقَالَ هَذَا حَظُّ الشَّيْطَانِ مِنْكَ ‏.‏ ثُمَّ غَسَلَهُ فِي طَسْتٍ مِنْ ذَهَبٍ بِمَاءِ زَمْزَمَ ثُمَّ لأَمَهُ ثُمَّ أَعَادَهُ فِي مَكَانِهِ وَجَاءَ الْغِلْمَانُ يَسْعَوْنَ إِلَى أُمِّهِ - يَعْنِي ظِئْرَهُ - فَقَالُوا إِنَّ مُحَمَّدًا قَدْ قُتِلَ ‏.‏ فَاسْتَقْبَلُوهُ وَهُوَ مُنْتَقَعُ اللَّوْنِ ‏.‏ قَالَ أَنَسٌ وَقَدْ كُنْتُ أَرَى أَثَرَ ذَلِكَ الْمِخْيَطِ فِي صَدْرِهِ ‏.‏

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik kwamba  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa akicheza na watoto wenzake alijiwa na Jibriyl (‘alayhis-salaam), akamchukua na kumlaza chini, kisha akampasua kifua chake na kuutoa nje moyo wake na kutoa kutoka ndani ya moyo huo kipande cha damu iliyoganda akasema: “Hicho ni kipande cha shaytwaan mwako.”  Kisha akauosha kwa maji ya Zamzam yaliyokuwemo ndani ya chombo cha dhahabu, kisha akaurudisha moyo mahali pake. Watoto waliokuwa wakicheza pamoja naye walikimbia mpaka nyumbani kwa mama yake yaani mnyonyeshaji wake (Bibi Haliymah As-Sa’diyyah), wakasema: “Muhammad keshauliwa!” Wakamkimbilia wakamkuta   (amekaa mzima hana chochote isipokuwa) rangi ya uso wake ilikuwa imebadilika na kugeuka (nyeupe).  Anas akasema: “Mimi mwenyewe niliona alama za mishono (ya sindano) katika kifua chake.”  [Muslim]

 

Share

13-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Waumini Wanapaswa Kumpenda Kuliko Nafsi Zao

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

13-Waumini Wanapaswa Kumpenda Kuliko Nafsi Zao

www.alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):  

 

النَّبِيُّ أَوْلَىٰ بِالْمُؤْمِنِينَ مِنْ أَنفُسِهِمْ ۖ  

Nabiy ana haki zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao. Na wake zake ni mama zao.  [Al-Ahzaab: 6]

 

Na katika Hadiyth inayohusiana na kauli hiyo ya Allaah (عزّ وجلّ):

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ  رضى الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ‏ ((مَا مِنْ مُؤْمِنٍ إِلاَّ وَأَنَا أَوْلَى النَّاسِ بِهِ فِي الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ، اقْرَءُوا إِنْ شِئْتُمْ‏: ((النَّبِيُّ أَوْلَى بِالْمُؤْمِنِينَ مِنْ أَنْفُسِهِمْ‏)) فَأَيُّمَا مُؤْمِنٍ تَرَكَ مَالاً فَلْيَرِثْهُ عَصَبَتُهُ مَنْ كَانُوا، فَإِنْ تَرَكَ دَيْنًا أَوْ ضِيَاعًا فَلْيَأْتِنِي وَأَنَا مَوْلاَهُ))  البخاري   

 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna Muumini yeyote isipokuwa mimi nina haki zaidi kwake (ya kupendwa na kutiiwa) kuliko watu wote duniani na Aakhirah. Someni mkipenda:

 

النَّبِيُّ أَوْلَىٰ بِالْمُؤْمِنِينَ مِنْ أَنفُسِهِمْ ۖ  

Nabiy ana haki zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao. Na wake zake ni mama zao.  [Al-Ahzaab: 6]

 

Na Muumini yeyote aliyeacha mali basi na warithi jamaa zake. Na ikiwa ameacha deni  au Watoto masikini, basi na waje kwangu (niwalipie madeni yao na niwahudumie) mimi ni mlinzi wao.  [Al-Bukhaariy]     

 

Na Hadiyth nyenginezo za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

عبد اللَّهِ بْنَ هِشَامٍ قَالَ، كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم وَهْوَ آخِذٌ بِيَدِ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ فَقَالَ لَهُ عُمَرُ يَا رَسُولَ اللَّهِ لأَنْتَ أَحَبُّ إِلَىَّ مِنْ كُلِّ شَىْءٍ إِلاَّ مِنْ نَفْسِي‏.‏ فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: ((لاَ وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ حَتَّى أَكُونَ أَحَبَّ إِلَيْكَ مِنْ نَفْسِكَ)) فَقَالَ لَهُ عُمَرُ فَإِنَّهُ الآنَ وَاللَّهِ لأَنْتَ أَحَبُّ إِلَىَّ مِنْ نَفْسِي‏.‏ فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: ((الآنَ يَا عُمَرُ))

 

Amesimulia ‘Abdullaah bin Hishaam (رضي الله عنه):  Tulikuwa pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) naye ameushika mkono wa ‘Umar bin Al-Khattwaab. ‘Umar akamwambia: Ee Rasuli wa Allaah, hakika wewe ni kipenzi zaidi kwangu kuliko kitu chochote isipokuwa nafsi yangu.  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hapana, (haiwezekani hivyo). Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, mpaka niwe kipenzi zaidi kwako kuliko nafsi yako.” ‘Umar (رضي الله عنه)  akamwambia:  Basi kwa sasa Wa-Allaahi wewe ni kipenzi zaidi kwangu kuliko nafsi yangu. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hivi sasa ee ‘Umar (umekuwa Muumini wa kweli).” [Al-Bukhaariy]

 

Na pia:

 

عَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللّه عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قال: ((لا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى أَكونَ أحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ وَالِدِهِ وَوَلَدِه وَالنَّاسِ أَجْمَعينَ )) متفق عليه

Imesimuliwa na Anas bin Maalik kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: ((Hatoamini mmoja wenu mpaka niwe (mimi Muhammad) kipenzi chake kuliko mwanawe na wazazi wake na kuliko watu wote)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

Share

14-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Manabii Na Rusuli Wote Walifungamana Ahadi Naye Kumwamini

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

14-Manabii Na Rusuli Wote Walifungamana Ahadi Naye Kumwamini

www.alhidaaya.com

 

 

 Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ النَّبِيِّينَ لَمَا آتَيْتُكُم مِّن كِتَابٍ وَحِكْمَةٍ ثُمَّ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مُّصَدِّقٌ لِّمَا مَعَكُمْ لَتُؤْمِنُنَّ بِهِ وَلَتَنصُرُنَّهُ ۚ قَالَ أَأَقْرَرْتُمْ وَأَخَذْتُمْ عَلَىٰ ذَٰلِكُمْ إِصْرِي ۖ قَالُوا أَقْرَرْنَا ۚ قَالَ فَاشْهَدُوا وَأَنَا مَعَكُم مِّنَ الشَّاهِدِينَ ﴿٨١﴾

Na pindi Alipochukua Allaah fungamano kwa Manabii (akawaambia) Kwa yale niliyokupeni kutoka kitabu na hikmah, kisha akakujieni Rasuli (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) mwenye kusadikisha yaliyo pamoja nanyi; ni juu yenu kumwamini na kumnusuru. (Kisha Allaah): Akasema Je, mmekiri na mmekubali kuchukua juu ya hayo fungamano zito Langu? Wakasema: Tumekiri. (Allaah) Akasema: Basi shuhudieni na Mimi Niko pamoja nanyi katika wenye kushuhudia.   [Aal-‘Imraan: 81]

 

 

Na katika Hadiyth:

 

 

عن جابر بن عبد الله رضي الله عنهما: أَنَّ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِكِتَابٍ أَصَابَهُ مِنْ بَعْضِ أَهْلِ الْكُتُبِ، فَقَرَأَهُ على النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَغَضِبَ وَقَالَ: ((أَمُتَهَوِّكُونَ فِيهَا يَا ابْنَ الْخَطَّابِ؟ وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لَقَدْ جِئْتُكُمْ بِهَا بَيْضَاءَ نَقِيَّةً، لَا تَسْأَلُوهُمْ عَنْ شَيْءٍ فَيُخْبِرُوكُمْ بِحَقٍّ فَتُكَذِّبُوا بِهِ، أَوْ بِبَاطِلٍ فَتُصَدِّقُوا بِهِ، وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لَوْ أَنَّ مُوسَى كَانَ حَيًّا، مَا وَسِعَهُ إِلَّا أَنْ يَتْبَعَنِي‏))  رواه أحمد، وحسنه الألباني في إرواء الغليل 

 

Kutoka kwa Jaabir Bin ‘Abdillaah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba ‘Umar Ibn Al-Khatw-twaab (رضي الله عنهما) alimwendea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa na Maandishi aliyoyapata kutoka kwa Ahlul-Kitaab. Akamsomea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), lakini Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaghadhibika akasema: ((Je unachanganyikiwa (Dini yako) ee ibn Al-Khatw-twaab? Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, nimekujieni na (Risala ya Uislaam)  ikiwa ni angavu na safi kabisa. Usiwaulize lolote wasije wakakuambia jambo la  kweli nawe ukalikanusha, au wasije kukuambia jambo la uongo nawe ukaliamini. Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikoni Mwake, angeliuwa Muwsaa yuko hai, basi asingelikuwa na chaguo isipokuwa kunifuata mimi)) [Imaam Ahmad [14736] na ameipa daraja ya Hasan Imaam Al-Albaani katika Irwaa Al-Ghaliyl (6/34)]

 

 

Pia imethibitika kuwa Nabiy ‘Iysaa (عليه السلام) atateremka duniani kabla ya Qiyaamah na atahukumu kwa Dini ya Kiislamu:

 

 

عن أبي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لَيُوشِكَنَّ أَنْ يَنْزِلَ فِيكُمُ ابْنُ مَرْيَمَ حَكَمًا عَدْلاً، فَيَكْسِرَ الصَّلِيبَ، وَيَقْتُلَ الْخِنْزِيرَ، وَيَضَعَ الْجِزْيَةَ، وَيَفِيضَ الْمَالُ حَتَّى لاَ يَقْبَلَهُ أَحَدٌ، حَتَّى تَكُونَ السَّجْدَةُ الْوَاحِدَةُ خَيْرًا مِنَ الدُّنْيَا وَمَا فِيهَا)) ثُمَّ يَقُولُ أَبُو هُرَيْرَةَ وَاقْرَءُوا إِنْ شِئْتُمْ: ((‏وَإِنْ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ إِلاَّ لَيُؤْمِنَنَّ بِهِ قَبْلَ مَوْتِهِ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكُونُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا‏))‏

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu iko Mikononi Mwake, hivi karibuni atateremka kwenu mwana wa Maryam ('Iysaa) akiwa ni kiongozi muadilifu na atavunja misalaba, na kuua nguruwe, na ataondosha jizyah (ushuru kutoka kwa wasio Waislamu ambao wamo katika himaya ya serikali ya Waislamu). Kisha kutakuwa na mali nyingi hadi itafikia kuwa hakuna mtu wa kupokea swadaqh. Wakati huu sijdah moja itakuwa ni bora kwao kuliko maisha haya na yote yaliyomo (katika dunia).” Kisha Abuu Huraryah akasema: Someni mkipenda:  

 

وَإِن مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ إِلَّا لَيُؤْمِنَنَّ بِهِ قَبْلَ مَوْتِهِ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكُونُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا ﴿١٥٩﴾

Na hakuna yeyote katika Ahlil-Kitaabi ila atamwamini kabla ya kufa kwake. Na Siku ya Qiyaamah atakuwa shahidi juu yao. (4: 159)[Al-Bukhaariy]

 

Na pia:

 

 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ:  قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((أَنَا أَوْلَى النَّاسِ بِعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ فِي الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ، وَالأَنْبِيَاءُ إِخْوَةٌ لِعَلاَّتٍ، أُمَّهَاتُهُمْ شَتَّى، وَدِينُهُمْ وَاحِدٌ))

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Mimi ni awlaa (bora  na karibu zaidi) kwa ‘Iysaa mwana wa Maryam dunina na Aakhirah na Manabii wote ni ndugu, mama zao wanatofautiana lakini Dini yao ni moja)) [Al-Bukhaariy]

 

Share

15-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kitabu Chake (Qur-aan) Kimejumuisha Vitabu Vyote Vya Mbinguni

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

15- Kitabu Chake (Qur-aan) Kimejumuisha Vitabu Vyote Vya Mbinguni

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Qur-aan imejumuisha na kusadikisha yote yaliyoteremshwa katika Tawraat, Injiyl na Zaabuwr kama Anavyosema Allaah :(سبحانه وتعالى)  

 

وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ الْكِتَابِ وَمُهَيْمِنًا عَلَيْهِ ۖ فَاحْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ ۖ  

Na Tumekuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Kitabu kwa haki kinachosadikisha Vitabu vilivyokuwa kabla yake na chenye kudhibiti, kushuhudia na kuhukumu juu yake (hivyo Vitabu). Basi hukumu baina yao kwa yale Aliyoyateremsha Allaah.   [Al-Maaidah: 48]

 

 

Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema kuhusu:

 

وَمُهَيْمِنًا عَلَيْهِ

Yaani: Kinadhibiti Vitabu viliyo kabla yake.

 

Na Imaam As-Sa’dy amesema kuhusu

وَمُهَيْمِنًا عَلَيْهِ

Yaani: Kinajumuisha yaliyojumuishwa katika Vitabu vya awali.

 

Na katika Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):   

 

عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ، أَنَّ ابْنَ عَبَّاسٍ رضى الله عنهما قَالَ: كَيْفَ تَسْأَلُونَ أَهْلَ الْكِتَابِ عَنْ شَىْءٍ، وَكِتَابُكُمُ الَّذِي أُنْزِلَ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَحْدَثُ، تَقْرَءُونَهُ مَحْضًا لَمْ يُشَبْ وَقَدْ حَدَّثَكُمْ أَنَّ أَهْلَ الْكِتَابِ بَدَّلُوا كِتَابَ اللَّهِ وَغَيَّرُوهُ وَكَتَبُوا بِأَيْدِيهِمُ الْكِتَابَ وَقَالُوا هُوَ مِنْ عِنْدِ اللَّهِ‏ لِيَشْتَرُوا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلاً، أَلاَ يَنْهَاكُمْ مَا جَاءَكُمْ مِنَ الْعِلْمِ عَنْ مَسْأَلَتِهِمْ، لاَ وَاللَّهِ مَا رَأَيْنَا مِنْهُمْ رَجُلاً يَسْأَلُكُمْ عَنِ الَّذِي أُنْزِلَ عَلَيْكُمْ‏.‏

 

Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: “Kwanini mnawauliza Ahlul-Kitaab jambo lolote ilhali Kitabu chenu ambacho kimeteremshwa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ni kipya (na cha karibuni)? Mnakisoma kikiwa ni kisafi, hakikupotoshwa wala kubadilishwa. Na mmeshajulishwa (na Allaah) kwamba Ahlul-Kitaab wamebadilisha Vitabu vya Allaah na wakavigeuza na wakaandika kwa mikono yao Kitabu wakasema “Hiki ni kutoka kwa Allaah ili wabadilishe kwa thamani ndogo.’” Je haikuwafikia ilmu kuwakataza msiwaulize lolote?  Hapana, wa-Allaahi hatujapata kuona mtu yeyote kutoka  kwao anayewauliza nyinyi yale yaliyoteremshwa kwenu.”  [Al-Bukhaariy Kitaab Al-I’tiswaam Bil-Kitaabi Was-Sunnah]

 

Share

16-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Allaah Hakumwita Kwa Jina Lake Katika Qur-aan Kama Walivoitwa Manabii Wengineo

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

16-Allaah Hakumwita Kwa Jina Lake Katika Qur-aan Kama Walivoitwa Manabii Wengineo

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Kwa sababu ya utukufuu wake na heshima kubwa Aliyopewa, ni Nabiy pekee ambaye Allaah ('Azza wa Jalla) Hakumwita kwa jina lake bali Alimwita  kwa cheo chake cha Rasuli au Nabiy; mifano michache ifuatayo:  

 

يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ  

Ee Rasuli! Balighisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako.  [Al-Maaidah: 67]

 

Na pia,

 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ شَاهِدًا وَمُبَشِّرًا وَنَذِيرًا ﴿٤٥﴾

Ee Nabiy! Hakika Sisi Tumekutuma uwe shahidi, na mbashiriaji na mwonyaji. [Al-Ahzaab: 45]

 

Na pia,

 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَطَلِّقُوهُنَّ لِعِدَّتِهِنَّ وَأَحْصُوا الْعِدَّةَ ۖ  

Ee Nabiy!  Mtakapowataliki wanawake, basi watalikini katika wakati wa eda (twahaarah) zao, na hesabuni barabara eda.  [Atw-Twalaaq: 1]

 

 

Na hata katika hali nyengine Allaah ('Azza wa Jalla) Alimwita kwa sifa fulani badala ya jina lake, mfano:

 

 

يَا أَيُّهَا الْمُزَّمِّلُ﴿١﴾

Ee uliyejifunika. [Al-Muzzammil: 1]

 

يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ﴿١﴾

Ee mwenye kujigubika! [Al-Muddath-thir: 1]

 

 

Lakini jina lake Amelitaja Allaah ('Azza wa Jalla) katika hali ya kujulishwa kuhusu khabari zake ndipo Amemtaja kwa jina lake, mfano watu kujulishwa kuwa yeye ni Rasuli wa Allaah, wala sio kumwita kwa "Yaa Muhammad".

 

مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّـهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ ۖ  

Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni Rasuli wa Allaah. Na wale walio pamoja naye ni wakali zaidi dhidi ya makafiri; wanahurumiana baina yao [Al-Fat-h]

 

Na pia,

 

وَمَا مُحَمَّدٌ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ ۚ  

Na Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) si yeyote isipokuwa ni Rasuli tu. Wamekwishapita kabla yake Rusuli.  [Aal-‘Imraan: 144]

 

 

Na pia:

 

 

مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَـٰكِن رَّسُولَ اللَّـهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ ۗ

Hakuwa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)  baba wa yeyote miongoni mwa wanaume wenu, lakini ni Rasuli wa Allaah na ni mwisho wa Manabii.  [Al-Ahzaab: 40]

 

 

 

Mifano ya Manabii walioitwa kwa majina yao katika hali ya kuitwa na kutajwa khabari zao:

 

 

 وَقُلْنَا يَا آدَمُ اسْكُنْ أَنتَ وَزَوْجُكَ الْجَنَّةَ وَكُلَا مِنْهَا رَغَدًا حَيْثُ شِئْتُمَا وَلَا تَقْرَبَا هَـٰذِهِ الشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٣٥﴾

Na Tukasema: Ee Aadam, kaa wewe na mkeo (Hawaa) Jannah na kuleni humo maridhawa popote mpendapo na wala msiukaribie mti huu; mtakuwa miongoni mwa madhalimu. [Al-Baqarah: 35]

 

 

 قِيلَ يَا نُوحُ اهْبِطْ بِسَلَامٍ مِّنَّا وَبَرَكَاتٍ عَلَيْكَ وَعَلَىٰ أُمَمٍ مِّمَّن مَّعَكَ ۚ

Pakasemwa: “Ee Nuwh!  Teremka (jahazini) kwa amani kutoka Kwetu na Baraka nyingi juu yako, na juu za umati zilio pamoja na wewe. [Huwd: 48]

 

 

وَنَادَيْنَاهُ أَن يَا إِبْرَاهِيمُ ﴿١٠٤﴾

Tukamwita: “Ee Ibraahiym. [Asw-Swaffaat: 104]

 

 

يَا زَكَرِيَّا إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَامٍ اسْمُهُ يَحْيَىٰ لَمْ نَجْعَل لَّهُ مِن قَبْلُ سَمِيًّا ﴿٧﴾

 

. (Akaambiwa): “Ee Zakariyyaa! Hakika Sisi Tunakubashiria ghulamu jina lake Yahyaa, Hatukupata kabla kumpa jina hilo yeyote.” [Maryam: 7]

 

 

يَا يَحْيَىٰ خُذِ الْكِتَابَ بِقُوَّةٍ ۖ وَآتَيْنَاهُ الْحُكْمَ صَبِيًّا ﴿١٢﴾

(Alipofikia kimo cha kufahamu aliambiwa) “Ee Yahyaa!  Chukua Kitabu kwa nguvu.” Na Tukampa Al-Hukma (hikma, ufahamu wa shariy’ah, elimu n.k) angali mtoto. [Maryam: 12]

 

 

Katika hali ya kumwita Muwsaa (‘Alayhis-salaam):

 

 

قَالَ يَا مُوسَىٰ إِنِّي اصْطَفَيْتُكَ عَلَى النَّاسِ بِرِسَالَاتِي وَبِكَلَامِي فَخُذْ مَا آتَيْتُكَ وَكُن مِّنَ الشَّاكِرِينَ ﴿١٤٤﴾

 

(Allaah) Akasema: “Ee Muwsaa hakika Mimi Nimekuteua juu ya watu kwa ujumbe Wangu na maneno Yangu. Basi pokea Niliyokupa na kuwa miongoni mwa wanaoshukuru.”  [Al-A’raaf: 144]

 

 

Katika hali ya kujulisha khabari zake. Mfano wachawi walipomwambia Nabiy Muwsaa (‘Alayhis-salaam):

 

 

قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِمَّا أَن تُلْقِيَ وَإِمَّا أَن نَّكُونَ نَحْنُ الْمُلْقِينَ ﴿١١٥﴾

(Wachawi) Wakasema: Ee Muwsaa, ima utupe wewe au tuwe sisi wa (kwanza) kutupa.   [Al-A’raaf: 115]

 

 

Mfano wa katika hali ya kumwita Nabiy ‘Iysaa (‘Alayhis-salaam):

 

وَإِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ أَأَنتَ قُلْتَ لِلنَّاسِ اتَّخِذُونِي وَأُمِّيَ إِلَـٰهَيْنِ مِن دُونِ اللَّـهِ ۖ قَالَ سُبْحَانَكَ مَا يَكُونُ لِي أَنْ أَقُولَ مَا لَيْسَ لِي بِحَقٍّ ۚ إِن كُنتُ قُلْتُهُ فَقَدْ عَلِمْتَهُ ۚ تَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِي وَلَا أَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِكَ ۚ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ ﴿١١٦﴾

Na pindi Allaah Atakaposema: Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam!  Je, wewe uliwaambia watu: ‘Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni waabudiwa wawili badala ya Allaah? (‘Iysaa) Atasema: Utakasifu ni Wako hainipasi mimi kusema yasiyo kuwa haki kwangu; ikiwa nimesema hayo basi kwa yakini Ungeliyajua; Unayajua yale yote yaliyomo katika nafsi yangu; na wala mimi sijui yale yaliyomo katika Nafsi Yako; hakika Wewe ni Mjuzi wa ghayb. [Al-Maaida: 116]

 

Na katika hali ya kujulisha khabari zake:

 

قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ اللَّـهُمَّ رَبَّنَا أَنزِلْ عَلَيْنَا مَائِدَةً مِّنَ السَّمَاءِ تَكُونُ لَنَا عِيدًا لِّأَوَّلِنَا وَآخِرِنَا وَآيَةً مِّنكَ ۖ وَارْزُقْنَا وَأَنتَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ ﴿١١٤﴾

. Akasema ‘Iysaa mwana wa Maryam: Ee Allaah, Rabb wetu, Tuteremshie meza iliyotandazwa chakula kutoka mbinguni ili iwe kwetu ni sikukuu kwa wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu; na iwe Aayah (ishara, hoja) itokayo Kwako; basi Turuzuku; kwani Wewe ni Mbora wa wenye kuruzuku. [Al-Maaidah: 114]

 

 

Share

17-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Swahaba Walikatazwa Kumwita Kama Wanavyoitana Wao Kwa Wao Au Kwa Jina Lake

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

17-Swahaba Walikatazwa Kumwita Kama Wanavyoitana Wao Kwa Wao Au Kwa Jina Lake

 

www.alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

لَّا تَجْعَلُوا دُعَاءَ الرَّسُولِ بَيْنَكُمْ كَدُعَاءِ بَعْضِكُم بَعْضًا ۚ قَدْ يَعْلَمُ اللَّـهُ الَّذِينَ يَتَسَلَّلُونَ مِنكُمْ لِوَاذًا ۚ فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٦٣﴾

Msifanye wito wa Rasuli baina yenu kama wito wa nyinyi kwa nyinyi. Kwa yakini Allaah Anawajua miongoni mwenu wale wanaoondoka kwa kunyemelea. Basi watahadhari wale wanaokhalifu amri yake, isije kuwasibu fitnah au ikawasibu adhabu iumizayo. [An-Nuwr: 63]

 

Adhw-Dhwahaak amesema kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya-Allaahu ‘anhumaa) kwamba amesema: “Walikuwa wakisema: “Yaa Muhammad, Yaa Abal-Qaasim” basi Allaah Akawakataza hivyo kwa sababu ya kumtukuza Nabiy Wake, baada ya hapo wakawa wanasema: “Yaa Nabiyya-Allaah, Yaa Rasuwla-Allaah.” Mujaahid na Sa’iyd bin Jubayr (Rahimahumaa-Allaah) nao pia wamsema hivyo. [Tafsiyr Ibn Kathiyr].

 

Imaam As-Sa’dy (Rahimahu-Allaah) naye amesema kuhusu kusudio la Aayah hiyo kwamba: Msiseme: “Yaa Muhammad bin ‘Abdillaah” Kama mnavyoitana wenyewe kwa wenyewe bali (Allaah) Amemtukuza na Akamfadhilisha na Akamtofautisha na wengineo wamwite: “Yaa Rasuwla-Allaah, Yaa Nabiyya-Allaah.”

 

 

Share

18-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Allaah Alipojulisha Khabari Zake Alimtaja Kwa Sifa Tukufu Kabisa

  Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

18-Allaah Alipotaka Kujulisha Khabari Zake Alizijulisha Bila Kumtaja Jina,

Isipokuwa Alimtaja Kwa Sifa Tukufu Ya ‘Ubuwdiyyah

 

www.alhidaaya.com

 

 

Allaah ('Azza wa Jalla) Alipotaka kujulisha khabari za Nabiy Wake, Alizijulisha bila ya kumtaja kwa jina lake kwa ajili ya kumtukuza Nabiy Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Akamtaja kwa kumpa sifa tukufu nayo ni sifa ya Al-‘Ubuwdiyyah[1] (kumwabudu Allaah kikamilifu).  Basi Allaah ('Azza wa Jalla) Akamtaja kwa sifa hiyo katika Aayah kadhaa za Qur-aan; miongoni mwanzo ni pale Alipomuelezea katika safari ya Al-Israa wal-Mi’raaj; Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَىٰ بِعَبْدِهِ لَيْلًا مِّنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ لِنُرِيَهُ مِنْ آيَاتِنَا ۚ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ ﴿١﴾

Utakasifu ni wa Ambaye Amemsafirisha usiku mja Wake kutoka Al-Masjid Al-Haraam mpaka Al-Masjid Al-Aqswaa ambao Tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake; ili Tumuonyeshe baadhi ya Aayaat (miujiza, ishara, dalili) Zetu. Hakika Yeye (Allaah) ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote. [Al-Israa: 1]

 

Na Akasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kuhusu safari hiyo hiyo ya Al-Israa Wal-Mi’raaj:

 

فَأَوْحَىٰ إِلَىٰ عَبْدِهِ مَا أَوْحَىٰ ﴿١٠﴾

(Allaah) Akamfunulia Wahy mja Wake yale Aliyomfunulia Wahy. [An-Najm: 10]

 

Na katika hali ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kumwabudu na kumuomba du’aa Rabb wake:

 

وَأَنَّهُ لَمَّا قَامَ عَبْدُ اللَّـهِ يَدْعُوهُ كَادُوا يَكُونُونَ عَلَيْهِ لِبَدًا﴿١٩﴾

Na kwamba mja wa Allaah (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) aliposimama kumwomba (Rabb wake), walikaribia kumzonga. [Al-Jinn: 19]

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

تَبَارَكَ الَّذِي نَزَّلَ الْفُرْقَانَ عَلَىٰ عَبْدِهِ لِيَكُونَ لِلْعَالَمِينَ نَذِيرًا ﴿١﴾

Amebarikika Ambaye Ameteremsha kwa mja Wake pambanuo (la haki na batili) ili awe muonyaji kwa walimwengu. [Al-Furqaan: 1]

 

Na pia Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي أَنزَلَ عَلَىٰ عَبْدِهِ الْكِتَابَ وَلَمْ يَجْعَل لَّهُ عِوَجًا ۜ﴿١﴾

AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah) Ambaye Amemteremshia mja Wake (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Kitabu na wala Hakukifanya ndani yake kiwe kombo. [Al-Kahf: 1]

 

Na pia Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

هُوَ الَّذِي يُنَزِّلُ عَلَىٰ عَبْدِهِ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ لِّيُخْرِجَكُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ بِكُمْ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿٩﴾

Yeye Ndiye Yule Anayemteremshia mja Wake Aayaat bayana ili Akutoeni katika viza na kukuingizeni kwenye Nuru. Na hakika Allaah kwenu ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu. [Al-Hadiyd: 9]

 

Na pia Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَإِن كُنتُمْ فِي رَيْبٍ مِّمَّا نَزَّلْنَا عَلَىٰ عَبْدِنَا فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِّن مِّثْلِهِ وَادْعُوا شُهَدَاءَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٢٣﴾

Na ikiwa mko katika shaka kutokana na Tuliyoyateremsha juu ya mja Wetu (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi leteni Suwrah mfano wake, na waiteni mashahidi wenu pasipo na Allaah mkiwa ni wakweli. [Al-Baqarah: 23]

 

 

 

[1] Maana Ya Al-‘Ubuwdiyyah kwa upana kidogo: Unyenyekevu, mapenzi, khofu ya adhabu za Allaah na kutaraji rahma za Allaah, utiifu na udhalili kwa Allaah Aliyetukuka, na kutovuka mipaka Yake, na kutekeleza maamrisho Yake na kujizuia na makatazo Yake, kwa kujikurubisha kwa Allaah na kutaka thawabu Zake na kujihadhari na ghadhabu na ikabu Zake.

 

 

 

Share

19-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Swahaba Walitahadharishwa Kuporomoka ‘Amali Zao Kwa Kumwita Kwa Sauti Ya Juu

 Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

19-Swahaba Walitahadharishwa Kuporomoka ‘Amali Zao Kwa Kumwita Kwa Sauti Ya Juu

www.alhidaaya.com

 

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Aliwafunza adabu Swahaba wasimwite Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa sauti ya juu. Na Akawawekea tahadharisho la kuporomoka ‘amali zao pindi wakifanya hivyo. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَرْفَعُوا أَصْوَاتَكُمْ فَوْقَ صَوْتِ النَّبِيِّ وَلَا تَجْهَرُوا لَهُ بِالْقَوْلِ كَجَهْرِ بَعْضِكُمْ لِبَعْضٍ أَن تَحْبَطَ أَعْمَالُكُمْ وَأَنتُمْ لَا تَشْعُرُونَ﴿٢﴾

Enyi walioamini! Msipandishe sauti zenu juu ya sauti ya Nabiy, na wala msiseme naye kwa sauti ya juu, kama mnavyosemezana wenyewe kwa wenyewe kwa sauti za juu; zisije zikaporomoka ‘amali zenu nanyi hamhisi.

 

Wakajaribiwa, na wao  wakatii amri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) wakawa wana khofu kuongea na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  kwa sauti ya juu hadi wengine wakawa wanaweka kijiwe mdomoni ili kiwazuie kumwita kwa sauti ya juu. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِنَّ الَّذِينَ يَغُضُّونَ أَصْوَاتَهُمْ عِندَ رَسُولِ اللَّـهِ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ امْتَحَنَ اللَّـهُ قُلُوبَهُمْ لِلتَّقْوَىٰ ۚ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ عَظِيمٌ﴿٣﴾

Hakika wale wanaoteremsha sauti zao mbele ya Rasuli wa Allaah, hao ndio ambao Allaah Amejaribu nyoyo zao kwa ajili ya taqwa. Watapata maghfirah na ujira adhimu.

 

Na mabedui nao ambao hakuwa na ustaarabu wakafunzwa adabu pia kutokumwita ovyo ovyo: Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِنَّ الَّذِينَ يُنَادُونَكَ مِن وَرَاءِ الْحُجُرَاتِ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ﴿٤﴾

Hakika wale wanaokuita (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) nyuma ya vyumba, wengi wao hawatii akilini.

 

وَلَوْ أَنَّهُمْ صَبَرُوا حَتَّىٰ تَخْرُجَ إِلَيْهِمْ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٥﴾

Na lau kwamba wao wangelisubiri mpaka ukawatokea, bila shaka ingelikuwa ni khayr kwao. Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

[Al-Hujuraat: 1-4]

 

Share

20-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kumuona Kwake Katika Ndoto Ni Kumuona Hakika

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

20-Kumuona Kwake Katika Ndoto Ni Kumuona Hakika

www.alhidaaya.com

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ:  قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ رَآنِي فِي الْمَنَامِ فَقَدْ رَآنِي فَإِنَّ الشَّيْطَانَ لاَ يَتَمَثَّلُ بِي))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayeniona katika ndoto basi hakika ameniona [ameniota] kwani shaytwaan hajifananishi na mimi)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share

21-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Allaah (عزّ وجلّ) Ameapia Kwa Uhai Wake

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

21-Allaah (عزّ وجلّ) Ameapia Kwa Uhai Wake

www.alhidaaya.com

 

Allaah (‘Azza wa Jalla)      Hajapatapo kuapia kwa uhai wa mtu yeyote katika waja Wake isipokuwa kwa uhai wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), hii ni kutokana na Sharaf na taadhima kubwa Aliyomjaalia Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

لَعَمْرُكَ إِنَّهُمْ لَفِي سَكْرَتِهِمْ يَعْمَهُونَ﴿٧٢﴾

Naapa kwa uhai wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم!) Hakika wao walikuwa katika ulevi wao wanatangatanga kwa upofu. [Al-Hijr: 72]

 

 

Imehadithiwa kutoka kwa ‘Amr bin Maalik An-Nakriy kutoka kwa Abuu Al-Jawzaa kwamba Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema:  “Allaah Hajapatapo kuumba wala kuanzisha wala kuunda roho ambayo ni kipenzi Kwake kama roho ya Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Wala sijapatapo kusikia Allaah Ameapia uhai wa yeyote ghairi yake.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]   

 

 

Share

22-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Rasuli Pekee Ambaye Allaah Ameahidi Kuhifadhi Kitabu Chake Al-Qur-aan

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

22-Rasuli Pekee Ambaye Allaah Ameahidi Kuhifadhi Kitabu Chake Al-Qur-aan

www.alhidaaya.com

 

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameteremshiwa Kitabu cha mwisho ambacho ni Qur-aan ambayo haibadiliki wala haiwezekani kugeuzwa wala kupotoshwa mpaka Siku ya Qiyaamah, kinyume na Vitabu vya awali ambayo vimepotoshwa kwa kubadilishwa, kupugunzwa na kuongezwa maneno yasiyokuwa ya Allaah ('Azza wa Jalla). Basi Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ameahidi Mwenyewe kuihifadhi Qur-aan kama Anavyosema: 

 

إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ

Hakika Sisi Tumeteremsha Adh-Dhikra (Qur-aan) na hakika Sisi bila shaka ndio Wenye kuihifadhi. [Al-Hijr: 9]

 

Ama Vitabu vya awali, Allaah Aliwaachia Wanazuoni wa Ahlul-Kitaabi wahifadhi kama Anavyosema:

 

 

إِنَّا أَنزَلْنَا التَّوْرَاةَ فِيهَا هُدًى وَنُورٌ ۚ يَحْكُمُ بِهَا النَّبِيُّونَ الَّذِينَ أَسْلَمُوا لِلَّذِينَ هَادُوا وَالرَّبَّانِيُّونَ وَالْأَحْبَارُ بِمَا اسْتُحْفِظُوا مِن كِتَابِ اللَّـهِ وَكَانُوا عَلَيْهِ شُهَدَاءَ ۚ فَلَا تَخْشَوُا النَّاسَ وَاخْشَوْنِ وَلَا تَشْتَرُوا بِآيَاتِي ثَمَنًا قَلِيلًا ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ ﴿٤٤﴾

Hakika Tumeteremsha Tawraat humo mna mwongozo na nuru; ambayo kwayo, Nabiy waliojisalimisha (kwa Allaah), waliwahukumu Mayahudi. Na (kadhalika) wanachuoni waswalihina na wanachuoni mafuqahaa wa dini kwa sababu waliyokabidhiwa kuhifadhi Kitabu cha Allaah; na wakawa mashahidi juu yake. Basi msiwaogope watu, bali Niogopeni Mimi, na wala msibadilishe Aayaat Zangu kwa thamani ndogo. Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri. [Al-Maaidah: 44]

 

Lakini haikuwezekana kuhifadhika bali vimepotoshwa kwa kupunguzwa na kugeuzwa na kuongezwa, na dalili kadhaa zimethibiti miongoni mwazo ni Kauli za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

وَإِنَّ مِنْهُمْ لَفَرِيقًا يَلْوُونَ أَلْسِنَتَهُم بِالْكِتَابِ لِتَحْسَبُوهُ مِنَ الْكِتَابِ وَمَا هُوَ مِنَ الْكِتَابِ وَيَقُولُونَ هُوَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ وَمَا هُوَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ وَيَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿٧٨﴾

Na hakika miongoni mwao kuna kundi wanaopotosha Kitabu kwa ndimi zao (wanaposoma) ili mdhanie kuwa hayo ni yanayotoka katika Kitabu, na hali hayo si yenye kutoka katika Kitabu, na wanasema: Hayo ni kutoka kwa Allaah; na hali hayo si kutoka kwa Allaah na wanamsingizia uongo Allaah na wao wanajua. [Aal-‘Imraan: 78]

 

Na,

 

فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ يَكْتُبُونَ الْكِتَابَ بِأَيْدِيهِمْ ثُمَّ يَقُولُونَ هَـٰذَا مِنْ عِندِ اللَّـهِ لِيَشْتَرُوا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۖ فَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا كَتَبَتْ أَيْدِيهِمْ وَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا يَكْسِبُونَ ﴿٧٩﴾

Basi ole kwa wale wenye kuandika kitabu kwa mikono yao; kisha wakasema: Hiki ni kutoka kwa Allaah ili wabadilishe kwa thamani ndogo. Basi ole wao kwa yale yaliyoandikwa na mikono yao, na ole wao kwa yale wanayoyachuma. [Al-Baqarah: 79]

 

 Na,

 

وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ إِذْ قَالُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ عَلَىٰ بَشَرٍ مِّن شَيْءٍ ۗ قُلْ مَنْ أَنزَلَ الْكِتَابَ الَّذِي جَاءَ بِهِ مُوسَىٰ نُورًا وَهُدًى لِّلنَّاسِ ۖ تَجْعَلُونَهُ قَرَاطِيسَ تُبْدُونَهَا وَتُخْفُونَ كَثِيرًا ۖ وَعُلِّمْتُم مَّا لَمْ تَعْلَمُوا أَنتُمْ وَلَا آبَاؤُكُمْ ۖ قُلِ اللَّـهُ ۖ ثُمَّ ذَرْهُمْ فِي خَوْضِهِمْ يَلْعَبُونَ ﴿٩١﴾

Na hawakumkadiria Allaah kama inavyostahiki kumkadiria, pale waliposema: Allaah Hakuteremsha chochote kwa mtu. Sema: Nani aliyeteremsha Kitabu ambacho amekuja nacho Muwsaa, (chenye) nuru na mwongozo kwa watu. Mnakifanya kurasa kurasa mkizifichua na mkificha mengi. [Al-An’aam: 91]

 

Na,

 

أَفَتَطْمَعُونَ أَن يُؤْمِنُوا لَكُمْ وَقَدْ كَانَ فَرِيقٌ مِّنْهُمْ يَسْمَعُونَ كَلَامَ اللَّـهِ ثُمَّ يُحَرِّفُونَهُ مِن بَعْدِ مَا عَقَلُوهُ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿٧٥﴾

Je, mnatumai kwamba watakuaminini na hali lilikuwa kundi miongoni mwao linasikia maneno ya Allaah kisha linayageuza baada ya kuyaelewa na hali wanajua? [Al-Baqarah: 75]

 

Na,

 

فَبِمَا نَقْضِهِم مِّيثَاقَهُمْ لَعَنَّاهُمْ وَجَعَلْنَا قُلُوبَهُمْ قَاسِيَةً ۖ يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِ ۙ وَنَسُوا حَظًّا مِّمَّا ذُكِّرُوا بِهِ ۚ  

Kwa sababu ya kuvunja kwao fungamano lao, Tuliwalaani na Tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu. Wanageuza maneno (ya Allaah) kutoka mahali pake, na wakasahu sehemu ya yale waliyokumbushwa.  [Al-Maaidah: 13]

 

 Na dalili mojawapo katika Hadiyth:  

 

عَنْ  إبن عَبَّاسٍ رضى الله عنهما قَالَ: كَيْفَ تَسْأَلُونَ أَهْلَ الْكِتَابِ عَنْ شَىْءٍ، وَكِتَابُكُمُ الَّذِي أُنْزِلَ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَحْدَثُ، تَقْرَءُونَهُ مَحْضًا لَمْ يُشَبْ وَقَدْ حَدَّثَكُمْ أَنَّ أَهْلَ الْكِتَابِ بَدَّلُوا كِتَابَ اللَّهِ وَغَيَّرُوهُ وَكَتَبُوا بِأَيْدِيهِمُ الْكِتَابَ وَقَالُوا هُوَ مِنْ عِنْدِ اللَّهِ‏ لِيَشْتَرُوا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلاً،  

 

Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: “Kwanini mnawauliza Ahlul-Kitaab jambo lolote ilhali Kitabu chenu ambacho kimeteremshwa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ni kipya (na cha karibuni)? Mnakisoma kikiwa ni kisafi, hakikupotoshwa wala kubadilishwa. Na mmeshajulishwa (na Allaah) kwamba Ahlul-Kitaab wamebadilisha Vitabu vya Allaah na wakavigeuza na wakaandika kwa mikono yao Kitabu wakasema “Hiki ni kutoka kwa Allaah ili wabadilishe kwa thamani ndogo.’”    [Al-Bukhaariy Kitaab Al-I’tiswaam Bil-Kitaabi Was-Sunnah]

 

Share

23-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Rasuli Pekee Aliyetumwa Kufunza Na Kutakasa Ummah Kwa Kitabu Cha Allaah Na Sunnah Zake

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

23-Rasuli Pekee Aliyetumwa  Kufunza Na Kutakasa Ummah

Kwa Kitabu Cha Allaah Na Sunnah Zake.

www.alhidaaya.com

 

 

Ni Rasuli pekee ambaye Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amemtuma kufunza na kutakasa watu wake si kwa kutokana na Kitabu cha Allaah pekee, bali na kwa Sunnah zake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa sababu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

 

وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣﴾

Na wala hatamki kwa hawaa.

إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ﴿٤﴾

Hayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa. [An-Najm: 3-4]

 

Na imethibiti katika Hadiyth zake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa amepewa Qur-aan na yanayofanana nayo; Yaani: Sunnah zake:

 

عَنِ الْمِقْدَامِ بْنِ مَعْدِيكَرِبَ، عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَنَّهُ قَالَ: (أَلَا إِنِّي أُوتِيتُ الْقُرْآنَ وَمِثْلَهُ، أَلَا يُوشِكُ رَجُلٌ يَنْثَنِي شَبْعَانًا عَلَى أَرِيكَتِهِ يَقُولُ: "عَلَيْكُمْ بِالْقُرْآنِ فَمَا وَجَدْتُمْ فِيهِ مِنْ حَلَال فَأَحِلُّوهُ وَمَا وَجَدْتُمْ فِيهِمِنْ حَرَامٍ فَحَرِّمُوهُ...)) رواه أبو داود والترمذي والحاكم وصححه وأحمد بسند صحيح

Kutoka kwa Miqdaad bin Ma’dikarib (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Tanabahi! Hakika nimepewa Qur-aan na inayofanana nayo (Sunnah) Tanabahi! Utafika wakati mtu aliyeshiba mno ataegemea kwenye kochi na kusema: “Shikamaneni na Qur-aan, mtakayokuta humo ya halali halalisheni, na mtakayokuta ya haramu haramisheni.” [Imepokewa na Abuu Daawuwd, na At-Tirmidhiy, na Al-Haakim na ameisahihisha Ahmad kwa isnaad Swahiyh].

 

 

Na Kauli za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) zifuatazo zinathibitisha kupewa Kitabu na Sunnah:

 

لَقَدْ مَنَّ اللَّـهُ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ إِذْ بَعَثَ فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْ أَنفُسِهِمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿١٦٤﴾

Kwa yakini Allaah Amewafanyia fadhila Waumini pale Alipomtuma kwao, Rasuli miongoni mwao, anawasomea Aayaat Zake na anawatakasa na anawafunza Kitabu na Hikmah (Sunnah); japokuwa walikuwa kabla katika upotofu bayana. [Aal-‘Imraan: 164]

 

‘Ulamaa wamekubaliana kwamba maana mojawapo ya Al-Hikmah ni Sunnah zake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَاذْكُرْنَ مَا يُتْلَىٰ فِي بُيُوتِكُنَّ مِنْ آيَاتِ اللَّـهِ وَالْحِكْمَةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ لَطِيفًا خَبِيرًا ﴿٣٤﴾

Na kumbukeni yale yanayosomwa majumbani mwenu katika Ayaat za Allaah na Hikmah (Sunnah), hakika Allaah daima ni Mwenye kudabiri mambo kwa ulatifu, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [Al-Ahzaab: 34]

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

هُوَ الَّذِي بَعَثَ فِي الْأُمِّيِّينَ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ﴿٢﴾

Yeye Ndiye Aliyepeleka Rasuli kwa wasiojua kusoma wala kuandika miongoni mwao anawasomea Aayaat Zake na Anawatakasa, na Anawafunza Kitabu na Hikmah na japo walikuwa hapo kabla katika upotofu bayana. [Al-Jumu’ah: 2]

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

كَمَا أَرْسَلْنَا فِيكُمْ رَسُولًا مِّنكُمْ يَتْلُو عَلَيْكُمْ آيَاتِنَا وَيُزَكِّيكُمْ وَيُعَلِّمُكُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُعَلِّمُكُم مَّا لَمْ تَكُونُوا تَعْلَمُونَ ﴿١٥١﴾

Kama Tulivyomtuma kwenu Rasuli anayetokana na nyinyi, anawasomea Aayaat Zetu na anakutakaseni na anakufunzeni Kitabu na Hikmah (Sunnah), na anakufundisheni mambo ambayo hamkuwa mkiyajua. [Al-Baqarah: 151]

 

Share

24-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ameruhusiwa Kuingiza Jannah Watu Sabiini Elfu Katika Ummah Wake

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

24-Ameruhusiwa Kuingiza Jannah Watu Sabiini Elfu Katika Ummah Wake

www.alhidaaya.com

 

 

Hadiyth ifuatayo imethibitisha kwamba Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni Rasuli Pekee ambaye ataruhusiwa kuingiza watu sabiini elfu katika Ummah wake:

 

Hadiyth maarufu ya ‘Ukaashah kuhusu Ruqyah (kinga na tiba:

 

عَنْ حُصَيْنِ بْنِ عَبْدِ اَلرَّحْمَنِ قَالَ: كُنْتُ عِنْدَ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ فَقَالَ: أَيُّكُمْ رَأَى الْكَوْكَبَ اَلَّذِي اِنْقَضَّ الْبَارِحَةَ؟ فَقُلْتُ أَنَا. ثُمَّ قُلْتُ: أَمَّا إِنِّي لَمْ أَكُنْ فِي صَلاةٍ وَلَكِنِّي لُدِغْتُ. قَالَ: فَمَا صَنَعْتَ؟ قُلْتُ: اِرْتَقَيْتُ. قَالَ: فَمَا حَمَلكَ عَلَى ذَلِكَ؟ قُلْتُ: حَدِيثٌ حَدَّثَنَاهُ اَلشَّعْبِيُّ. قَالَ: وَمَا حَدَّثَكُمْ؟ قُلْتُ: حَدَّثَنَا عَنْ بُرَيْدَةَ بْنِ الْحُصَيْبِ أَنَّهُ قَالَ: لاَ رُقْيَةَ إِلاَّ مِنْ عَيْنٍ أَوْ حُمَةٍ. قَالَ: قَدْ أَحْسَنَ مَنِ اِنْتَهَى إِلَى مَا سَمِعَ. وَلَكِنْ حَدَّثَنَا اِبْنُ عَبَّاسٍ عَنْ اَلنَّبِيِّ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) أَنَّهُ قَالَ: ((عُرِضَتْ عَلَيَّ الأُمَمُ فَرَأَيْتُ اَلنَّبِيَّ وَمَعَهُ اَلرَّهْطُ وَالنَّبِيَّ وَمَعَهُ اَلرَّجُلُ وَالرَّجُلاَنِ، وَالنَّبِيَّ وَلَيْسَ مَعَهُ أَحَدٌ، إِذْ رُفِعَ لِي سَوَادٌ عَظِيمٌ فَظَنَنْتُ أَنَّهُمْ أُمَّتِي، فَقِيلَ لِي هَذَا مُوسَى وَقَوْمُهُ، فَنَظَرْتُ فَإِذَا سَوَادٌ عَظِيمٌ، فَقِيلَ لِي هَذِهِ أُمَّتُكَ، وَمَعَهُمْ سَبْعُونَ أَلْفًا يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ بِغَيْرِ حِسَابٍ وَلاَ عَذَابٍ)) ثُمَّ نَهَضَ فَدَخَلَ مَنْزِلَهُ فَخَاضَ اَلنَّاسُ فِي أُولَئِكَ فَقَالَ بَعْضُهُمْ: فَلَعَلَّهُمْ اَلَّذِينَ صَحِبُوا رَسُولَ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) ، وَقَالَ بَعْضُهُمْ فَلَعَلَّهُمْ اَلَّذِينَ وُلِدُوا فِي الإِسْلامِ فَلَمْ يُشْرِكُوا بِاَللَّهِ شَيْئًا وَذَكَرُوا أَشْيَاءَ. فَخَرَجَ عَلَيْهِمْ رَسُولُ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَأَخْبَرُوهُ فَقَالَ: ((هُمُ اَلَّذِينَ لاَ يَسْتَرْقُونَ وَلاَ يَكْتَوُونَ وَلاَ يَتَطَيَّرُونَ وَعَلَى رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ)) فَقَامَ عُكَّاشَةُ بْنُ مُحْصَنٍ فَقَالَ: اُدْعُ اَللَّهَ أَنْ يَجْعَلَنِي مِنْهُمْ. فَقَالَ: ((أَنْتَ مِنْهُمْ)) ثُمَّ قَامَ رَجُلٌ آخَرُ فَقَالَ: اُدْعُ اَللَّهَ أَنْ يَجْعَلَنِي مِنْهُمْ. فَقَالَ: ((سَبَقَكَ بِهَا عُكَّاشَةُ)) البخاري ومسلم

Huswayn bin ‘Abdir-Rahmaan amehadithia: Siku moja nilipokuwa na Sa’iyd bin Jubayr, aliuliza: “Nani miongoni mwenu aliyeona kimondo (nyota inayofukuza shaytwaan) jana usiku?” Nikajibu: “Mimi nimeiona.” Kisha nikaelezea kwamba sikuwa nikiswali wakati ule sababu nilidonelewa na nge mwenye sumu. Akasema: “Kisha ukafanya nini?” Nikajibu: “Nilifanya Ruqyah (kujitibu). Akauliza: “Kitu gani kimekupeleka ufanye hivyo?” Nikasema: “Ni Hadiyth niliyoisikia kutoka kwa Ash-Sha’biyy.” Akauliza: “Amekuhadithieni nini Ash-Sha’biyy?” Nikajibu: “Ameripoti kutoka kwa Buraydah bin Al-Huswayb amesema kwamba Ruqyah hairuhusiwi isipokuwa kwa ajili ya kijicho na kudonelewa (na mdudu sumu).” (Sa’iyd bin Jubayr) akasema: “Amefanya vyema kukomea kwenye aliyosikia (yaani: kufanyia kazi jambo kwa ujuzi kinyume na ujahili). Lakini Ibn ‘Abbaas ametusimulia kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Ummah zote zilipitishwa mbele yangu, nikamuona Nabiy akiwa na kundi dogo la watu, na Nabiy akiwa na mtu mmoja au wawili, na Nabiy akiwa hana mtu yeyote. Kisha nikaoneshwa idadi kubwa ya watu niliodhania ni katika Ummah wangu, lakini nikaambiwa: Huyo ni Muwsaa na watu wake. Kisha nikatazama nikaona kundi kubwa ambalo nikaamibwa: Hawa ni watu wako, miongoni mwao ni watu elfu sabini watakaoingia Jannah bila hesabu wala adhabu)). Kisha akainuka kuingia nyumbani kwake (na nyuma yake) watu wakaanza kujadiliaina ni nani hao watakaoweza kuwa. Wengineo wakasema: “Labda ni Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)” Wengine wakasema: “Labda ni wale waliozaliwa katika Uislamu na hawakumshirikisha Allaah kwa chochote.” (Wakataja mengine kadhaa) Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akatoka na kuja na wakamwambia (waliyokuwa wakiyajadili). Akasema: ((Ni wale ambao wasiotafuta kufanyiwa Ruqyah, wala kujichoma chuma cha moto, wala hawaamini twiyaarah (itikadi ya mkosi au nuksi), bali wanamtegemea Rabb wao na kutawakali Kwake Pekee)) ‘Ukaashah bin Mihswan akasimama akasema:  “Muombe Allaah niwe mmoja wao.” Akasema:  ((Wewe ni mmoja wao)). Kisha mtu mwengine akasimama akasema: Muombe Allaah niwe mmoja wao (pia). Akasema: ((‘Ukaashah amekutangulia)) [Al-Bukhaariy (3410) Muslim (220)]

 

Share

25-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Atakuwa Sayyid (Bwana) Wa Watu Siku Ya Qiyaamah

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

25-Atakuwa Sayyid (Bwana) Wa Watu Siku Ya Qiyaamah

www.alhidaaya.com

 

 

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ أَنَا سَيِّدُ وَلَدِ آدَمَ وَلاَ فَخْرَ وَأَنَا أَوَّلُ مَنْ تَنْشَقُّ الأَرْضُ عَنْهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلاَ فَخْرَ وَأَنَا أَوَّلُ شَافِعٍ وَأَوَّلُ مُشَفَّعٍ وَلاَ فَخْرَ وَلِوَاءُ الْحَمْدِ بِيَدِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلاَ فَخْرَ ‏"‏ ‏.

 

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (Radhwiya-Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mimi Sayyid (Bwana) katika wana wa Aadam Siku ya Qiyaamah wala sijifakharishi kwa kujigamba. Na ni wa kwanza ambaye ardhi itanipasukia Siku ya Qiyaamah wala sijifakharishi kwa kujigamba. Na wa kwanza ambaye nitashufai na wa kwanza ambaye nitakubaliwa shufaa yangu wala sijifakharishi kwa kujigamba, na katika mkono wangu kutakuwepo na bango la sifa, wala sijifakharishi kwa kujigamba)) [Ibn Maajah ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Ibn Maajah (3496), Swahiyh At-Targhiyb (3643)]

 

Share

26-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Alifikishwa Mbingu Ya Saba Katika Safari Ya Usiku Mmoja Ya Israa Wal-Mi’raaj

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

26-Alifikishwa Mbingu Ya Saba Katika Safari Ya Usiku Mmoja Ya Israa Wal-Mi’raaj

www.alhidaaya.com

 

Tukio la miujiza ya Allaah (‘Azza wa Jalla) la Al-Israa wal Mi’raaj ambalo amemjaalia Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) asafiri usiku mmoja tu na kumfikisha mbingu ya saba.  Dalili ya safari hiyo ya mijuzia ni katika Quraan ni kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَىٰ بِعَبْدِهِ لَيْلًا مِّنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ لِنُرِيَهُ مِنْ آيَاتِنَا ۚ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ ﴿١﴾

 

Utakasifu ni wa Ambaye Amemsafirisha usiku mja Wake kutoka Al-Masjid Al-Haraam mpaka Al-Masjid Al-Aqswaa ambao Tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake; ili Tumuonyeshe baadhi ya Aayaat (miujiza, ishara, dalili) Zetu. Hakika Yeye (Allaah) ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.  [Al-Israa: 1]

 

Na pia Kauli Zake Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala): 

 

ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّىٰ ﴿٨﴾

Kisha akakurubia na akashuka.

 

فَكَانَ قَابَ قَوْسَيْنِ أَوْ أَدْنَىٰ ﴿٩﴾

Kisha akawa kiasi cha umbali wa mipinde miwili au karibu zaidi.

 

فَأَوْحَىٰ إِلَىٰ عَبْدِهِ مَا أَوْحَىٰ ﴿١٠﴾

(Allaah) Akamfunulia Wahy mja Wake yale Aliyomfunulia Wahy.

 

مَا كَذَبَ الْفُؤَادُ مَا رَأَىٰ ﴿١١﴾

Moyo haukukadhibisha yale aliyoyaona.

 

أَفَتُمَارُونَهُ عَلَىٰ مَا يَرَىٰ ﴿١٢﴾

Je, mnambishia kuhusu yale aliyoyaona?

 

وَلَقَدْ رَآهُ نَزْلَةً أُخْرَىٰ ﴿١٣﴾

Na kwa yakini amemuona (Jibriyl) katika uteremko mwingine.

 

عِندَ سِدْرَةِ الْمُنتَهَىٰ ﴿١٤﴾

Kwenye mkunazi wa mpaka wa mwisho kabisa.  

 

عِندَهَا جَنَّةُ الْمَأْوَىٰ ﴿١٥﴾

Karibu yake kuna Jannah ya Al-Ma-waa.

 

إِذْ يَغْشَى السِّدْرَةَ مَا يَغْشَىٰ ﴿١٦﴾

Ulipoufunika mkunazi huo unachokifunika

 

مَا زَاغَ الْبَصَرُ وَمَا طَغَىٰ ﴿١٧﴾

Jicho lake halikukengeuka wala halikupinduka mipaka.

 

لَقَدْ رَأَىٰ مِنْ آيَاتِ رَبِّهِ الْكُبْرَىٰ ﴿١٨﴾

Kwa yakini aliona miongoni mwa Aayaat (ishara, dalili) za Rabb wake kubwa kabisa. [An-Najm: 8-18]

 

Na Hadiyth kadhaa ziloelezea kuhusu safari hiyo; miongoni mwazo ni zifuatazo ambazo alipofika mbingu ya saba ndipo ilipofaridhishwa Swalaah tano kwa Waislamu:

 

‘Abdullaah bin Mas’uwd alisema, “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipewa vitu vitatu: alipewa Swalaah tano, alipewa Aayah mbili za kumalizia Suwrah ya Al-Baqarah na kusamehewa kwa madhambi ya wale watu ambao hawamshirikishi Allaah miongoni mwa ummah wake.” [Muslim Namba 329].

 

 

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: “Allaah Alinipa ufunuo na Akasema kuwa Ummah wangu wanawajibika kuswali Swalaah khamsini (50) kila siku; usiku na mchana. Nilishuka kwenda kwenye mbingu ya Muwsaa (‘Alayhis-Salaam) akaniluza: “Lipi Rabb wako Amekupatia kwa ajili ya ummah wako?” Nikasema: “Swalaah Khamsini.”  Akasema: “Rejea kwa Rabb wako na omba Akupunguzie katika idadi hiyo ya Swalaah, maana watu wako hawawezi kubeba mzigo huo mzito. Kama vile nilivyotiwa katika mtihani na wana wa Israaiyl na nikawajaribu nikawaona kuwa walikuwa dhaifu sana na hawawezi kubeba mzigo kama huo.”  Hivyo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimgeukia Jibriyl (‘Alayhis-Salaam) kama vile akitaka kupata ushauri wake juu ya hilo. Jibriyl (‘Alayhis-Salaam) akasema: “Ndiyo, sawa, kama unataka hivyo.” Na wakarejea tena juu kwa Allaah.” [Al-Bukhaariy, Juzuu 9 Namba 608].

 

 

Kisha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Nilirejea kwa Rabb wangu na kusema, “Ee Rabb wangu, Fanya vitu viwe vyepesi kwa ajili ya Ummah wangu. Allaah Alipunguza  idadi ya Swalaah khamsini na kuwa tano kwa ajili yangu. Nilishuka chini nikaenda kwa Muwsaa (‘Alayhis-Salaam) ambaye alisema: “Hakika watu wako hawataweza kubeba mzigo huu mzito. Rejea kwa Rabb wako umwombe afanye wepesi wa hilo, Ee Muhammad! Mimi nilijaribu kuwalingania Ummah wangu wana Israaiyl ili wafanye kidogo zaidi ya hayo, lakini hawakuweza kuyafanya hayo bali waliishia kukata tamaa.” [Al-Bukhaariy, Juzuu 9 Namba 608]. 

 

 

Basi nikawa natangatanga kati ya mbingu ya Muwsaa na kwa Rabb wangu mwisho Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akasema: “Kuna Swalaah tano kila siku, usiku na mchana Ee Muhammad. Kila Swalaah imebeba uzito wa Swalaah kumi, na hivyo hizo ni khamsini vile vile. Mtu yeyote anayetia niyyah ya kufanya jambo zuri na asipolifanya basi atapata thawabu kwa hilo, na kama atalifanya hilo tendo, basi itaandikwa thawabu kumi kwa hilo. Wakati ambapo mtu aliyenuia kufanya uovu na akaacha kuufanya haitasajiliwa hiyo na kama atafanya uovu huo basi utasajiliwa uovu mmoja tu. Hapo nikashuka kwa Muwsaa (‘Alayhis-Salaam) na kumwambia hayo, Muwsaa akasema: “Nenda kwa Rabb wako ili afanye mambo yawe mepesi zaidi.” Juu ya kauli hiyo Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Nimekuwa nikienda kwa Rabb wangu mara kwa mara hadi naona aibu kusimama mbele yake. [Muslim].

 

Juu ya hilo Jibriyl (‘Alayhis-Salaam) akasema: ”Kwa jina la Allaah! Shuka sasa!”  Kisha Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaamka akiwa ndani ya Masjid Al-Haraam (Msikiti Mtukufu wa Makkah)” [Swahiyh Al-Bukhaariy, Juzuu 9 Namba 608]

 

Na pia ndani ya maelezo ya Al-Bukhaariy kuna maelezo zaidi kuwa: “…nilipoondoka nilisikia sauti:  “Nimetoa amri Yangu na kisha nimewapunguzia uzito Waja Wangu.”

 

 

Share

27-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Atakuwa Wa Kwanza Na Ummah Wake Kuvuka Swiraatw

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

27-Atakuwa Wa Kwanza Na Ummah Wake Kuvuka Swiraatw

www.alhidaaya.com

 

Kutoka katika Hadiyth ndefu kabisa iliyothibiti kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Ummah wake tutakuwa wa kwanza kabisa kuvuka Asw-Swiraatw:

 

عَنْ عَطَاءِ بْنِ يَزِيدَ اللَّيْثِيِّ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، أَنَّ النَّاسَ، قَالُوا يَا رَسُولَ اللَّهِ هَلْ نَرَى رَبَّنَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ هَلْ تُضَارُّونَ فِي الْقَمَرِ لَيْلَةَ الْبَدْرِ ‏"‏‏.‏ قَالُوا لاَ يَا رَسُولَ اللَّهِ‏.‏ قَالَ ‏"‏ فَهَلْ تُضَارُّونَ فِي الشَّمْسِ لَيْسَ دُونَهَا سَحَابٌ ‏"‏‏.‏ قَالُوا لاَ يَا رَسُولَ اللَّهِ‏.‏ قَالَ ‏"‏ فَإِنَّكُمْ تَرَوْنَهُ كَذَلِكَ، يَجْمَعُ اللَّهُ النَّاسَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَيَقُولُ مَنْ كَانَ يَعْبُدُ شَيْئًا فَلْيَتَّبِعْهُ‏.‏ فَيَتْبَعُ مَنْ كَانَ يَعْبُدُ الشَّمْسَ الشَّمْسَ، وَيَتْبَعُ مَنْ كَانَ يَعْبُدُ الْقَمَرَ الْقَمَرَ، وَيَتْبَعُ مَنْ كَانَ يَعْبُدُ الطَّوَاغِيتَ الطَّوَاغِيتَ، وَتَبْقَى هَذِهِ الأُمَّةُ فِيهَا شَافِعُوهَا ـ أَوْ مُنَافِقُوهَا شَكَّ إِبْرَاهِيمُ ـ فَيَأْتِيهِمُ اللَّهُ فَيَقُولُ أَنَا رَبُّكُمْ‏.‏ فَيَقُولُونَ هَذَا مَكَانُنَا حَتَّى يَأْتِيَنَا رَبُّنَا فَإِذَا جَاءَنَا رَبُّنَا عَرَفْنَاهُ فَيَأْتِيهِمُ اللَّهُ فِي صُورَتِهِ الَّتِي يَعْرِفُونَ فَيَقُولُ أَنَا رَبُّكُمْ‏.‏ فَيَقُولُونَ أَنْتَ رَبُّنَا‏.‏ فَيَتْبَعُونَهُ وَيُضْرَبُ الصِّرَاطُ بَيْنَ ظَهْرَىْ جَهَنَّمَ، فَأَكُونُ أَنَا وَأُمَّتِي أَوَّلَ مَنْ يُجِيزُهَا، وَلاَ يَتَكَلَّمُ يَوْمَئِذٍ إِلاَّ الرُّسُلُ، وَدَعْوَى الرُّسُلِ يَوْمَئِذٍ اللَّهُمَّ سَلِّمْ سَلِّمْ‏.‏

 

Kutoka kwa ‘Atwaa’ bin Yaziyd Al-Laythiy kuwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Watu (yaani Maswahaba) walisema:  “Ee Rasuli wa Allaah! Je, tutamuona Rabb wetu Siku ya Qiyaama?” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  akasema: ((Je, mna shida yoyote ya kuuona mwezi usiku ambao mwezi ni mpevu?)) Wakasema: “Hapana ee Rasuli wa Allaah.” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Je, mna shida ya kuliona jua siku isiyokuwa na mawingu?)) Wakasema: “Hapana  ee Rasuli wa Allaah.”  Akasema: ((Hakika nyinyi mtamuona, kama hivyo. Allaah Atawakusanya watu wote Siku ya Qiyaamah, Naye Atasema: “Yeyote aliyekuwa akiabudu kitu (duniani) akifuate hicho (kitu)”  Kwa hiyo, yule aliyekuwa akiabudu jua atalifuata jua; na yeyote aliyekuwa akiuabudu mwezi ataufuata mwezi; na yeyote aliyekuwa akiabudu twaghuti  atamfuata twaghuti. Na utabakia Ummah huu peke yake na watu wake wazuri na wanafiki miongoni mwao)). Allaah Atakuja kwao na kusema: “Mimi Ndiye Rabb wenu.” Wao (watu watamkanusha) kwa kusema: “Hii ni sehemu yetu, nasi tutaketi hapa mpaka atakapokuja Rabb wetu. Pindi Atakapokuja tutamjua.” Kwa hivyo, Allaah Atakuja kwao katika Surah Yake ambayo wataijua, Naye Atasema: “Mimi Ndiye Rabb wenu.” Watu watasema: “Wewe Ndiye Rabb wetu.” Nao (watu) watamfuata. Kisha Asw-Swiraatw (Njia) itawekwa juu ya Moto (wa Jahannam).. Mimi na Ummah wangu tutakuwa wa kwanza kuivuka na hakuna atakayezungumza Siku hiyo isipokuwa Rusuli. Na Du‘aa ya Rusuli Siku hiyo itakuwa:

اللَّهُمَّ سَلِّمْ سَلِّمْ

 

Allaahumma Sallim (Ee Allaah! Jaalia salama, Jaalia salama)) [Al-Bukhaariy]

 

 

 

Share

28-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Atakuwa Wa Kwanza Kuingia Jannah Pamoja Na Ummah Wake

 

 

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

28-Atakuwa Wa Kwanza Kuingia  Jannah Pamoja Na Ummah Wake

www.alhidaaya.com

 

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) atakuwa wa kwanza kuingia Jannah (Peponi):

 

 

عَنْ ثَابِتٍ، عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ آتِي بَابَ الْجَنَّةِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَأَسْتَفْتِحُ فَيَقُولُ الْخَازِنُ مَنْ أَنْتَ فَأَقُولُ مُحَمَّدٌ ‏.‏ فَيَقُولُ بِكَ أُمِرْتُ لاَ أَفْتَحُ لأَحَدٍ قَبْلَكَ ‏"‏مسلم

 

Imepokelewa kutoka kwa Thaabit kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Nitaufikia mlango wa Jannah Siku ya Qiyaamah, utafunguliwa kisha mlinzi wake atauliza: “Nani wewe?” Nitasema: Mimi Muhammad. Atasema: Nimeamrishwa kukufungulia wewe tu si mwenginewe kabla yako)) [Muslim]

 

 Na katika Hadiyth nyengine atakuwa wa kwanza kugonga mlango wa Jannah:

 

 

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ أَنَا أَكْثَرُ الأَنْبِيَاءِ تَبَعًا يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَأَنَا أَوَّلُ مَنْ يَقْرَعُ بَابَ الْجَنَّةِ ‏"‏ ‏.‏مسلم

 

Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Miongoni mwa Manabii, mimi nitakuwa ndiye mwenye wafuasi wengi kabisa Siku ya Qiyaamah na wa kwanza kuugonga mlango wa Jannah)) [Muslim]

 

Na pia Ummah wake tutakuwa wa kwanza kuingia Jannah:

 

 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ نَحْنُ الآخِرُونَ الأَوَّلُونَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَنَحْنُ أَوَّلُ مَنْ يَدْخُلُ الْجَنَّةَ بَيْدَ أَنَّهُمْ أُوتُوا الْكِتَابَ مِنْ قَبْلِنَا وَأُوتِينَاهُ مِنْ بَعْدِهِمْ فَاخْتَلَفُوا فَهَدَانَا اللَّهُ لِمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ مِنَ الْحَقِّ فَهَذَا يَوْمُهُمُ الَّذِي اخْتَلَفُوا فِيهِ هَدَانَا اللَّهُ لَهُ - قَالَ يَوْمُ الْجُمُعَةِ - فَالْيَوْمُ لَنَا وَغَدًا لِلْيَهُودِ وَبَعْدَ غَدٍ لِلنَّصَارَى ‏"‏ ‏.‏ البخاري ، مسلم  

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Sisi ni (Ummah) wa mwisho lakini ni wa kwanza siku ya Qiyaamah. Sisi ni wa kwanza kuingia Jannah ingawa wao (Mayahudi na Manaswara) walipewa Kitabu kabla yetu nasi tumepewa baada yao. Allaah Ametuongoza katika haki katika waliyokhitilafiana kwa idhini Yake. Hii ni siku (Ijumaa) waliyokhitilafiana, nasi Allah Ametuongoza nayo Hivyo watu wanatufuata kwani kesho (Jumamosi) ni siku ya Mayahudi na inayofuatia (Jumapili) ni ya Manaswara)) [Al-Bukhaariy, Muslim  na wengineo]

 

Share

29-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Rasuli Pekee Atakayeruhusiwa Ash-Shafaa'ah Ummah Wake

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

29-Rasuli Pekee Atakayeruhusiwa Ash-Shafaa'ah (Uombezi) Kwa Ummah Wake

www.alhidaaya.com

 

 

Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) atakuwa Rasuli pekee atakayekubaliwa ash-shafaa'ah yake (uombezi) Siku ya Qiyaamah.  Atakapokuwa amesujudu kisha ataamrishwa kuinuka na kuomba ash-shafaa'ah:

  

 

عَنْ أَنَسٍ ، رَضِيَ اللهُ عَنْهُ ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى الله عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ ، قَالَ يَجْتَمِعُ المُؤْمِنُونَ يَوْمَ القِيَامَةِ فَيَقُولُونَ : لَوِ اسْتَشْفَعْنَا إلى رَبِّنَا ، فَيَأْتُونَ ادَمَ ، فَيَقُولُونَ : أَنْتَ أَبو النَّاسِ ، خَلَقَكَ اللهُ بِيَدِهِ ، وَأَسْجَدَ لَكَ مَلائِكَتَهُ ، وَعَلَّمَكَ أَسْماءَ كُلِّ شَيْءٍ ، فاشْفَعْ لَنا عِنْدَ رَبِّكَ ، حَتَّى يُرِيحَنا مِنْ مَكَانِنا هَذا ، فَيَقُولُ : لَسْتُ هُنَاكُمْ ـ وَيَذْكُرُ ذَنْبَهُ ، فَيَسْتَحْيي ـ ائْتُوا نُوحاً ؛ فَإِنَّهُ أَوَّلُ رَسُولٍ بَعَثَهُ اللهُ إِلي أَهْلِ الأَرْض ، فَيَأْتُونَهُ ، فَيَقُولُ : لَسْتُ هُنَاكُمْ ـ ويَذْكُرُ سُؤالَهُ رَبَّهُ مَا لَيْسَ لَهُ بِهِ عِلْمٌ ، فَيَسْتَحْيي ـ فَيَقُولُ : اؤْتُوا خَلِيلَ الرَّحْمنِ ، فَيَأْتُونَهُ ، فَيَقُولُ : لَسْتُ هُنَاكُم ، اؤْتُوا موسى ، عَبْداً كَلَّمَهُ اللهُ ، و أَعْطَاهُ التَّوْرَاةَ . فَيَأْتُونَهُ ، فَيَقُولُ : لَسْتُ هُنَاكُمْ ـ وَيَذْكُرُ قَتْلَ النَّفْسِ بِغَيْرِ نَفْسٍ ، فَيَسْتَحْيي مِنْ رَبِّهِ ـ فَيَقُولُ : اؤْتُوا عِيسَى ، عَبْدَ اللهِ وَرَسُولَهُ ، وَكَلِمَةَ اللهِ وَرُوحَهُ . فَيَأْتُونَهُ ، فَيَقُولُ : لَسْتُ هُنَاكُمْ ، اؤْتُوا مُحَمَّداً ، ـ صَلَّى الله عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ ـ عَبْداً غَفَرَ اللهُ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ وَمَا تَأَخَّرَ ، فَيَأْتُونَنِي ، فَأَنْطَلِقُ حَتَّي أَسْتَأْذِنَ عَلَي رَبِّي فَيُؤْذَنُ . فإذا رَأَيْتُ رَبِّي وَقَعْتُ سَاجداً ، فَيَدَعُني مَا شَاءَ اللهُ ، ثُمَّ يُقَالُ : ارْفَعْ رَأْسَكَ ، وسَلْ تُعْطَهُ ، وَقُلْ يُسْمَعْ ، واشْفَعْ تُشَفَّعْ . فَأَرْفَعُ رَأْسي ، فَأَحْمَدُهُ بِتَحْمِيدٍ يُعَلِّمُنِيهِ ، ثُمَّ أَشْفَعُ ، فَيحُدُّ لي حَدّاً ، فَأُدْخِلُهُمْ الجَنَّةَ . ثُمَّ أَعُودُ إِلَيْهِ ، فإِذا رَأَيْتُ رَبِّي ( فَأَقَعُ ساجداً ) مِثْلَهُ ، ثُمَّ أَشْفَعُ فَيَحُدُّ لِي حَدّاً ، فَأُدْخِلُهُمُ الجَنَّةَ . ثُمَّ أَعُودُ الثالِثةَ ، ثُمَّ أَعُودُ الرَّابعة ، فَأقُولُ : مَا بَقِي في النَّارِ إِلَّا مَنْ حَبَسَهُ القُرْانُ ، ووَجَبَ عَلَيْهِ الخُلُودُ

 

Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Watakusanyika Waumini Siku ya Qiyaamah na Watasema: Lau tungetafuta kuombewa shafaa’ah kwa Rabb wetu! Watakwenda kwa Aadam na watasema: Wewe ndio baba wa watu, Amekuumba Allaah kwa Mkono Wake na Akaamrisha Malaika wakusujudie, na Akakufundisha majina ya vitu vyote, basi tuombee kwa Rabb wako ili Atupe faraja kutokana na sehemu yetu hii? Atasema: Mimi siwezi kufanya mnaloomba! Na atakumbuka makosa yake na ataona hayaa, atasema: Mfuateni Nuwh, hakika yeye ndiye Rasuli wa kwanza Aliyemtuma Allaah kwa watu ardhini. Watamfuata. Naye atasema: Siwezi kufanya mnaloomba! Na atakumbuka kumuomba kwake Allaah kwa jambo asilokuwa na ujuzi nalo.  Naye ataona hayaa na atasema: Nendeni kwa Khaliylur-Rahmaan. Watakwenda kwa Ibraahiym. Naye atawaambia: Siwezi kufanya mnaloomba! Nendeni kwa Muwsaa mja ambaye Allaah Alizungumza naye na Akampa Tawraat. Muwsaa atasema: Siwezi kufanya mnaloomba!  Atakumbuka kuwa aliwahi kumuua mtu bila ya haki na ataona hayaa kwa Rabb wake.  Atasema: Nendeni kwa ‘Iysaa kwani ni mja wa Allaah na Rasuli Wake na neno Lake na Roho Yake. Naye atasema: Siwezi kufanya mnaloomba! Nendeni kwa Muhammad, ni mja aliyefutiwa makosa yaliyotangulia na yajayo. Watakuja kwangu na nitakwenda kwa Rabb wangu kumuomba idhini (ya maombi), nitapewa idhini. Nitakapomuona Rabb wangu nitasujudu na Ataniacha hivyo hivyo mpaka Atakavyo. Kisha itasemwa: Inua kichwa chako na omba utapewa! Na sema yatasikilizwa (uyasemayo)! Na omba shafaa‘ah (uombezi) utapewa! Nitainua kichwa changu na nitamhimidi kwa Himdi Zake Atakazonifundisha, kisha nitaomba na Atanikubalia idadi kubwa ya watu, nitawaingiza Jannah. Kisha nitarudi tena Kwake. Nitakapomuona Rabb wangu, nitafanya kama mara ya kwanza, kisha nitaomba na Atanikubalia idadi kubwa ya watu nitawaingiza Jannah. Kisha nitarejea mara ya tatu, kisha nitarudi mara ya nne kisha nitasema: Hakuna watu waliobakia motoni isipokuwa Qur-aan imewazuia na watawajibika kubakia humo.” [Al-Bukhaariy (4476)]

 

Na  Hadiyth ifuatayo kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) atakuwa na du’aa makhsusi ya kuombea Ummah wake ash-shafaa’ah (uombezi): 

 

عن أبي هريرة رَضِيَ اللَّهُ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ لِكُلِّ نَبِيٍّ دَعْوَةٌ، فَأُرِيدُ إِنْ شَاءَ اللَّهُ أَنْ أَخْتَبِيَ دَعْوَتِي شَفَاعَةً لأُمَّتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ ‏"‏‏.‏

Kutoka kwa Abuu Huraryah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kila Nabiy na du’aa inayotaqabailiwa, nami nataka In Shaa Allaah nihifadhi du'aa yangu kwa ajili ya kuwaonbea shafaa'ah (uombezi) Ummah wangu Siku ya Qiyaamah)) [Al-Bukhaariy]

 

 Na pia:

 

عَنْ آدَمَ بْنِ عَلِيٍّ، قَالَ سَمِعْتُ ابْنَ عُمَرَ، رضى الله عنهما يَقُولُ إِنَّ النَّاسَ يَصِيرُونَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ جُثًا، كُلُّ أُمَّةٍ تَتْبَعُ نَبِيَّهَا، يَقُولُونَ يَا فُلاَنُ اشْفَعْ، حَتَّى تَنْتَهِيَ الشَّفَاعَةُ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَذَلِكَ يَوْمَ يَبْعَثُهُ اللَّهُ الْمَقَامَ الْمَحْمُودَ‏.‏

 Kutoka kwa Aadam bin ‘Aliy ambaye amesema: Nilimsikia Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) akisema: “Siku ya Qiyaamah, watu wataangukia kupiga magoti na kila Ummah utafuata Nabiy wake wakisema: “Ee fulani tuombee ash-shafaa’ah (uombezi)!” Mpaka shafaa’ah (ya hakika) itafika kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na hiyo ndiyo siku ambayo Allaah Atakayompandisha cheo kitukufu cha kusifiwa (Al-Maqaamah Al-Mahmuwdah).” [Al-Bukhaariy] 

 

Share

30-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ummah Wake Utakuwa Wa Kwanza Kuhukumiwa Siku Ya Qiyaamah

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

30-Ummah Wake Utakuwa Wa Kwanza Kuhukumiwa Siku Ya Qiyaamah

www.alhidaaya.com

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، وَعَنْ رِبْعِيِّ بْنِ حِرَاشٍ، عَنْ حُذَيْفَةَ، قَالاَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ أَضَلَّ اللَّهُ عَنِ الْجُمُعَةِ مَنْ كَانَ قَبْلَنَا فَكَانَ لِلْيَهُودِ يَوْمُ السَّبْتِ وَكَانَ لِلنَّصَارَى يَوْمُ الأَحَدِ فَجَاءَ اللَّهُ بِنَا فَهَدَانَا اللَّهُ لِيَوْمِ الْجُمُعَةِ فَجَعَلَ الْجُمُعَةَ وَالسَّبْتَ وَالأَحَدَ وَكَذَلِكَ هُمْ تَبَعٌ لَنَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ نَحْنُ الآخِرُونَ مِنْ أَهْلِ الدُّنْيَا وَالأَوَّلُونَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ الْمَقْضِيُّ لَهُمْ قَبْلَ الْخَلاَئِقِ ‏"‏ ‏.‏ وَفِي رِوَايَةِ وَاصِلٍ الْمَقْضِيُّ بَيْنَهُمْ ‏.‏

  

Kutoka kwa Abuu Hurayrah na Abuu Rib-‘iyy bin Hiraash kutoka kwa Hudhayfah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ilikuwa ni Ijumaa ambayo Allaah Aliigeuza kutoka kwa walio kabla yetu. Mayahudi wakawa na Siku ya Jumamosi na Manaswara Siku ya Jumapili. Allaah Akatuletea na kutuongoza sisi Siku ya Ijumaa (siku tukufu ya Swalaah ya jamaah) Akajaalia Ijumaa, Jumamosi na Jumapili (kuwa ni siku tukufu). Kwa utaratibu huu wao (Mayahudi na Manaswara) watakuja baada yetu Siku ya Qiyaamah. Sisi (ni Ummah) wa mwisho katika watu wa dunia, lakini wa kwanza miongoni mwa viumbe kuhukumiwa Siku ya Qiyaamah)) na katika riwaayah nyengine:  ((Kuhukumiwa miongoni mwao)) [Al-Bukhaariy]

 

Share

31-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kumtii Yeye Ni Sawa Na Kumtii Allaah

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

31-Kumtii Yeye Ni Sawa Na Kumtii Allaah

 

www.alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):  

 

مَّن يُطِعِ الرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ اللَّـهَ ۖ وَمَن تَوَلَّىٰ فَمَا أَرْسَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا ﴿٨٠﴾

Atakayemtii Rasuli basi kwa yakini amemtii Allaah. Na atakayekengeuka basi Hatukukutuma kuwa mlinzi juu yao. [An-Nisaa: 80]

 

Na katika Hadiyth:

عَنْ أبي هُرَيْرة رضى الله عنه  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ مَنْ أَطَاعَنِي فَقَدْ أَطَاعَ اللَّهَ، وَمَنْ عَصَانِي فَقَدْ عَصَى اللَّهَ، وَمَنْ أَطَاعَ أَمِيرِي فَقَدْ أَطَاعَنِي، وَمَنْ عَصَى أَمِيرِي فَقَدْ عَصَانِي ‏"‏‏.‏

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)  amehadithia kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayenitii basi atakuwa amemtii Allaah, na atakayeniasi atakuwa amemuasi Allaah, na atakayemtii Amiri wangu (kiongozi niliyemteua), atakuwa amenitii mimi na atakayemuasi atakuwa ameniasi mimi)) [Al-Bukhaariy, Muslim, An-Nasaaiy, Ibn Maajah]

 

 Na katika Hadiyth nyengine:

 

عن عبدالله بن عمر رضي الله عنه أنه كان يومًا من الأيامِ عندَ رسولِ اللهِ صلَّى اللهُ عليهِ وسلمَ وهو في نفرٍ من أصحابِه فقال: ((ألستم تعلمون أنِّي رسولُ اللهِ؟)) قالوا: "بلى يا رسولَ اللهِ نشهدُ أنك رسولُ اللهِ" قال: ((ألستم تعلمونَ أن اللهَ تعالَى أنزلَ في كتابِه أنَّ مَن أطاعَني فقد أطاع اللهَ؟)) قالوا: "بلى نشهدُ أن مَن أطاعَك فقد أطاع اللهَ" قال: ((فإنَّ مِن طاعتي أن تطيعوا أئمَّتَكم فإن صلُّوا قُعودًا فصلُّوا قُعودًا))

‘Abdullaah bin ‘Umar (رضي الله عنهما) amehadithia kwamba siku moja alikuwa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) pindi alipokuwa na baadhi ya Maswahaba akasema: ((Je si mnajua kuwa mimi ni Rasuli wa Allaah?)) Wakasema: “Bila shaka ee Rasuli wa Allaah tunashuhudia kuwa wewe ni Rasuli wa Allaah.”  Akasema: ((Je, si mnajua kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Ameteremsha katika Kitabu Chake kuwa “Atakayenitii mimi atakuwa amemtiia Allaah?” Wakasema: “Bila shaka tunashuhudia kuwa atakayekutii wewe atakuwa amemtii Allaah.” Akasema: ((Miongoni mwa kunitii ni Imaam wenu wanaposwali wakiwa wamekaa kitako, basi nanyi mswali kwa kukaa kitako)) [Musnad Ahmad ni Hadiyth Swahiyh taz Asw-Swahiyh Al-Musnad, (761), na riwaayah nyengine Taz Swahiyh Ibn Hibbaan (2109), Swiffatusw-Swalaah ya Al-Albaaniy (1/87)]

 

 

 

Share

32-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Hatajwi Ila Anaswaliwa (Anaombewa Rahmah Na Amani)

 

 Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

32-Hatajwi Ila Anaswaliwa (Anaombewa Rahmah Na Amani)

www.alhidaaya.com

 

 

Kila anapotajwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Waislamu wanapasa kumswalia, naye Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akakemea asiyefanya hivyo katika Hadiyth:

 

 

 عنْ أبي هُريْرةَ رضي اللَّه عنهُ قال: قال رسُولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم: ((رَغِم أنْفُ رجُلٍ ذُكِرْتُ عِنْدَهُ فَلَمْ يُصَلِّ علَيَّ))  رواهُ الترمذي وقالَ : حديثٌ حسنٌ .

Imetoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Amepata khasara mtu ambaye nimetajwa kwake na hakuniswalia)) [At-Tirmidhiy na kasema Hadiyth Hasan]

 

Na pia,

 

 وعن علِيٍّ رضي اللَّه عنْهُ قال: قال رسُولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم: ((الْبخِيلُ من ذُكِرْتُ عِنْدَهُ فَلَم يُصَلِّ علَيَّ)) رواهُ الترمذي وقالَ : حديثٌ حسنٌ صحيحٌ .

Imetoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Bakhili ni yule ambaye nimetajwa kwake na hakuniswalia)) [At-Tirmidhiy na kasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

Share

33-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ana Ujira Usiokatika Anasifika Na Maarufu Mno

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

33-Ana Ujira Usiokatika Anasifika Na Maarufu Mno

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

وَإِنَّ لَكَ لَأَجْرًا غَيْرَ مَمْنُونٍ ﴿٣﴾

 

Na hakika wewe bila shaka una ujira usiokatika. [Al-Qalam: 3]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

وَرَفَعْنَا لَكَ ذِكْرَكَ ﴿٤﴾

 

Na Tukanyanyulia juu utajo wako (ukawa mwenye kusifika mno)?  [Ash-Sharh: 4]

 

Allaah (سبحانه وتعالى)  Amemfadhilisha na kumkirimu Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kutajwa mno na kusifiwa na akawa maarufu ulimwenguni.  Hutajwa katika kila Adhaana ya Swalaah, katika Iqaamah, katika khutbah za Ijumaa, katika kutamka Shahaadah, na hutajwa ndani ya Swalaah na kila zinapotajwa Hadiyth zake, na anaswaliwa katika kuomba du’aa ambapo du’aa haitaqabaliwi bila ya kumswalia yeye kwanza, na huswaliwa pia inapomalizika du’aa, na katika hali nyingi mbali mbali, na Hadiyth zifuatazo zinathibitisha:

 

عن ابي سعيد الخدري رضي الله عنه ان رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: أتاني جبريلُ فقال: إنَّ ربِّي وربَّك يقولُ لك: كيف رفَعْتُ ذِكْرَك ؟ قال: اللهُ أعلَمُ قال: إذا ذُكِرْتُ ذُكِرْتَ معي

Imepokelewa kutoka kwa Sa’idy Al-Khudriyy (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:  “Amenijia Jibriyl akasema: Hakika Rabb wangu na Rabb Wako Anasema: Vipi umenyanyuliwa juu utajo wako? Akasema: Allaah Anajua zaidi. Akasema: (Allaah Anasema): Kila nnapotajwa, nawe unatajwa pamoja nami.” [Ibn Jariyr, Ibn Abiy Haatim, Ibn Hibbaan na Ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Ibn Hibbaan 3382]

 

Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema ) (kuhusu maana ya):  “Sitajwi isipokuwa unatajwa pamoja Nami”;  katika Adhaan, Iqaamah, Tashahhud, Siku ya Ijumaa, kwenye Minbari (khutbah), Siku ya ’Iydul-Fitwr, Siku ya ’Iydul- Adhw-haa, Ayyaamut-Tashriyq, Siku ya ’Arafah, katika Jamarah, katika Swafaa Wal Marwah, katika Khutbah za Nikaah, Mashariki ya ardhi na Magharibi, na kwamba lau mtu akamwabudu Allaah akaamini Jannah na Moto na kila kitu lakini hashuhudii  kwamba Muhammad ni Rasuli wa Allaah,  basi hakuna kitakachomfaa na atakuwa ni kafiri. [Tafsiyr Al-Qurtwubiy]

 

Naye Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:

 ((الْبَخِيلُ مَنْ ذُكِرْتُ عِنْدَهُ فَلَمْ يُصَلِّ عَلَيَّ))

((Bakhili ni yule ambaye nikitajwa haniswalii))  [Hadiyth ya ‘Aliy bin Abi Twaalib (رضي الله عنه)   - At-Tirmidhiy (5/551) [3546], na wengineo na angalia: Swahiyh Al-Jaami’ (3/25) [2787] na Swahiyh At-Tirmidhiy (3/177)]

 

Share

34-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Amekubaliwa Ombi Lake Kutoka Mbingu Ya Saba Kupunguziwa Swalaah Khamsiyn Kwa Ummah Wake

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

34-Amekubaliwa Ombi Lake Kutoka Mbingu Ya Saba

Kupunguziwa Swalaah Khamsiyn Kwa Ummah Wake

 

www.alhidaaya.com

 

 

Juu ya kuwa Swalaah ni nguzo muhimu kabisa katika nguzo za Kiislamu, na ni msingi wa Dini, na kama alivyosema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu mtu asiyeswali kwamba mwenye kuiacha amekufuru kwani baina ya mtu na shirki na ukafiri ni Swalaah, lakini Allaah (عزّ وجلّ)  Alimuitikia Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم)  ombi lake la kupunguziwa Ummah wake Swalaah hizo kutoka khamsini kwa siku hadi tano. Na fardhi hii amefaridhishwa nayo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  kutoka mbingu ya saba, jambo ambalo hakuna Nabiy yeyote aliyefadhilishwa kama hivi:

 

 

قالَ أَنَسُ بْنُ مَالِكٍ وَابْنُ حَزْمٍ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ فَرَضَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ عَلَى أُمَّتِي خَمْسِينَ صَلاَةً فَرَجَعْتُ بِذَلِكَ حَتَّى أَمُرَّ بِمُوسَى عَلَيْهِ السَّلاَمُ فَقَالَ مَا فَرَضَ رَبُّكَ عَلَى أُمَّتِكَ قُلْتُ فَرَضَ عَلَيْهِمْ خَمْسِينَ صَلاَةً ‏.‏ قَالَ لِي مُوسَى فَرَاجِعْ رَبَّكَ عَزَّ وَجَلَّ فَإِنَّ أُمَّتَكَ لاَ تُطِيقُ ذَلِكَ ‏.‏ فَرَاجَعْتُ رَبِّي عَزَّ وَجَلَّ فَوَضَعَ شَطْرَهَا فَرَجَعْتُ إِلَى مُوسَى فَأَخْبَرْتُهُ فَقَالَ رَاجِعْ رَبَّكَ فَإِنَّ أُمَّتَكَ لاَ تُطِيقُ ذَلِكَ ‏.‏ فَرَاجَعْتُ رَبِّي عَزَّ وَجَلَّ فَقَالَ هِيَ خَمْسٌ وَهِيَ خَمْسُونَ لاَ يُبَدَّلُ الْقَوْلُ لَدَىَّ ‏.‏ فَرَجَعْتُ إِلَى مُوسَى فَقَالَ رَاجِعْ رَبَّكَ فَقُلْتُ قَدِ اسْتَحْيَيْتُ مِنْ رَبِّي عَزَّ وَجَلَّ ‏"‏ ‏.‏

 

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik na Ibn Hazmi kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:  “Allaah (عزّ وجلّ) Amefaridhisha kwa Ummah wangu Swalaah khamsini, nikarudi nikiwa nimezikubali mpaka nikafikia kwa Muwsaa (عليه السلام) akauliza: Rabb wako Amefaridhisha nini kwa Ummah wako? Nikasema: Amewafaridhisha Swalaah khamsini.  Akaniambia: Rudi kwa Rabb wako Allaah (عزّ وجلّ) kwani ummah wako hawataziweza. Nikarudi kwa Rabb wangu Allaah (عزّ وجلّ) Akapunguza idadi fulani nikarudi kwa Muwsaa na kumjulisha akasema: Rejea kwa Rabb wako kwani Ummah wako hawataziweza. Nikarudi kwa Rabb wangu Allaah (عزّ وجلّ) mwisho Akasema: Hizo ni tano lakini (thawabu zake) ni khamsini; Haibadilishwi Kwangu kauli. Nikarudi kwa Muwsaa akasema: Rejea kwa Rabb wako, nikasema: Hakika ninamstahi Rabb wangu Allaah (عزّ وجلّ) [An-Nisaaiy, Ibn Maajah]

 

 

Share

35-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Allaah Amemtunza Na Kumuongoza Na Kumtimizia Mahitaji Yake

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

35-Allaah Amemtunza Na Kumuongoza Na Kumtimizia Mahitaji Yake

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

أَلَمْ يَجِدْكَ يَتِيمًا فَآوَىٰ ﴿٦﴾

Je, kwani Hakukukuta yatima, Akakupa makazi?

 

 

وَوَجَدَكَ ضَالًّا فَهَدَىٰ ﴿٧﴾

Na Akakukuta mpotevu Akakuongoza?

 

 

وَوَجَدَكَ عَائِلًا فَأَغْنَىٰ ﴿٨﴾

Na Akakukuta mhitaji, Akakutosheleza? [Adhw-Dhwuhaa: 6-8]

Share

36-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Allaah Hakuwaadhibu Au Kuwaangamiza Makafari Kwa Sababu Ya Uwepo Wakee

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

36-Allaah Hakuwaadhibu Au Kuwaangamiza Makafari Kwa Sababu Ya Kuweko Kwake

 

www.alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

  وَإِذْ قَالُوا اللَّـهُمَّ إِن كَانَ هَـٰذَا هُوَ الْحَقَّ مِنْ عِندِكَ فَأَمْطِرْ عَلَيْنَا حِجَارَةً مِّنَ السَّمَاءِ أَوِ ائْتِنَا بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٣٢﴾

Na pindi waliposema: “Ee Allaah! Kama haya ni haki kutoka Kwako; basi Tunyeshee mvua ya mawe kutoka mbinguni, au Tuletee adhabu iumizayo.”

 

وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُعَذِّبَهُمْ وَأَنتَ فِيهِمْ ۚ وَمَا كَانَ اللَّـهُ مُعَذِّبَهُمْ وَهُمْ يَسْتَغْفِرُونَ﴿٣٣﴾

Na Allaah Hakuwa wa kuwaadhibu na hali wewe (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uko nao. Na Allaah Hakuwa wa kuwaadhibu hali wao wanaomba maghfirah. [Al-Anfaal: 32- 33]

 

Imaam As-Sa’diy  (رحمه الله)  amesema:  “Kutokana na kauli yao hiyo (ya Aayah 32 ya kuomba adhabu) ni dhahiri kuwa wao ni wajinga wapumbavu, madhalimu. Lau kama Allaah Angewaharakazia adhabu basi wasingebakia kuishi. Lakini Allaah Amewakinga na adhabu kwa sababu ya uwepo wa Rasuli miongoni mwao. Basi uwepo wa Rasuli ni amani kwao kutokana na adhabu.”

 

Share

37-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Amefutiwa Madhambi Yake Yote Yaliyotangulia Na Ya Yaliyo Mbele Yake

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

37-Amefutiwa Madhambi Yake Yote Yaliyotangulia Na Ya Yaliyo Mbele Yake

 

www.alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (عزّ وجلّ):

 

 إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُّبِينًا ﴿١﴾ لِّيَغْفِرَ لَكَ اللَّـهُ مَا تَقَدَّمَ مِن ذَنبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ وَيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكَ وَيَهْدِيَكَ صِرَاطًا مُّسْتَقِيمًا ﴿٢﴾

Hakika Tumekupa ushindi (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم ambao ni) ushindi wa dhahiri. Ili Allaah Akughufurie yale yaliyotangulia katika madhambi yako na yale yanayokuja; na Akutimizie neema Yake juu yako na Akuongoze njia iliyonyooka. [Al-Fat-h: 1-2]

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akafurahi mno kuteremshiwa kwake Aayah hiyo kama ilivyothibiti katika Hadiyth:

 

عَنْ أَنَسٍ، رضى الله عنه قَالَ أُنْزِلَتْ عَلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلمَ ‏:‏ ‏((ليغْفِرَ لَكَ اللَّهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِكَ وَمَا تَأَخَّر))َ  مَرْجِعَهُ مِنَ الْحُدَيْبِيَةِ فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ لَقَدْ أُنْزِلَتْ عَلَىَّ آيَةٌ أَحَبُّ إِلَىَّ مِمَّا عَلَى الأَرْضِ ثُمَّ قَرَأَهَا النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم عَلَيْهِمْ فَقَالُوا هَنِيئًا مَرِيئًا يَا نَبِيَّ اللَّهِ قَدْ بَيَّنَ اللَّهُ لَكَ مَاذَا يُفْعَلُ بِكَ فَمَاذَا يُفْعَلُ بِنَا فَنَزَلَتْ عَلَيْهِ: ((ليُدْخِلَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الأَنْهَارُ))  حَتَّى بَلَغَ ‏:‏ ‏((‏فوزًا عَظِيمًا ))‏  قَالَ هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ  ‏.‏

 

Anas bin Maalik amehadithia kwamba: Tulipokuwa tunarudi kutoka Hudaybiyah, iliteremshwa kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

 

لِّيَغْفِرَ لَكَ اللَّـهُ مَا تَقَدَّمَ مِن ذَنبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ وَيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكَ وَيَهْدِيَكَ صِرَاطًا مُّسْتَقِيمًا﴿٢﴾

Ili Allaah Akughufurie yale yaliyotangulia katika madhambi yako na yale yanayofuatia; na Akutimizie neema Yake juu yako na Akuongoze njia iliyonyooka.

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hakika nimeteremshiwa Aayah ambayo ni kipenzi mno kuliko chochote kilichoko duniani.” Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akawasomea Aayah hiyo, wakasema: Hongera kwako ee Nabiy wa Allaah, hakika Allaah Amekubainishia Atakalokufanyia, lakini je Atatufanyia nini sisi? Hapo ikateremshwa: 

 

لِّيُدْخِلَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَيُكَفِّرَ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عِندَ اللَّـهِ فَوْزًا عَظِيمًا﴿٥﴾

Ili Awaingize Waumini wa kiume na Waumini wa kike Jannaat zipitazao chini yake mito, ni wenye kudumu humo, na Awafutie maovu yao; na kukawa huko mbele ya Allaah, ni kufuzu adhimu. [Al-Fat-h: 5]

 

 [At-Tirmidhiy Amesema Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

Share

38-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Nabiy Pekee Aliyetakwa Afuate Mwongozo Na Vigezo Vya Manabii Wengineo

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

38-Nabiy Pekee Aliyetakwa  Afuate Mwongozo Na Vigezo Vya Manabii Wengineo

 

www.alhidaaya.com

 

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Alimuamrisha Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) afuate mwongozo na vigezo vya Manabii wengineo; jambo ambalo hakuna Nabiy mwengine aliyeamrishwa kufanya hivyo. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى) baada ya kuwataja Manabii kumi na nane katika Aayah zilizofuatana za Suwrah Al-An’aam:

 

  وَتِلْكَ حُجَّتُنَا آتَيْنَاهَا إِبْرَاهِيمَ عَلَىٰ قَوْمِهِ ۚ نَرْفَعُ دَرَجَاتٍ مَّن نَّشَاءُ ۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ ﴿٨٣﴾

Na hiyo ndio hoja Yetu Tuliyompa Ibraahiym juu ya watu wake.  Tunampandisha cheo Tumtakaye. Hakika Rabb wako ni Mwenye hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.

 

وَوَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ ۚ كُلًّا هَدَيْنَا ۚ وَنُوحًا هَدَيْنَا مِن قَبْلُ ۖ وَمِن ذُرِّيَّتِهِ دَاوُودَ وَسُلَيْمَانَ وَأَيُّوبَ وَيُوسُفَ وَمُوسَىٰ وَهَارُونَ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿٨٤﴾

Na Tukamtunukia Is-haaq, na Ya’quwb. Wote Tukawahidi. Na Nuwh Tulimhidi kabla. Na katika dhuria wake Daawuwd, na Sulaymaan, na Ayyuwb, na Yuwsuf, na Muwsaa, na Haaruwn. Na hivyo ndivyo Tulipavyo wafanyao ihsaan.

 

وَزَكَرِيَّا وَيَحْيَىٰ وَعِيسَىٰ وَإِلْيَاسَ ۖ كُلٌّ مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿٨٥﴾

Na Zakariyyaa, na Yahyaa, na ‘Iysaa, na Ilyaas. Wote ni miongoni mwa Swalihina.

 

وَإِسْمَاعِيلَ وَالْيَسَعَ وَيُونُسَ وَلُوطًا ۚ وَكُلًّا فَضَّلْنَا عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٨٦﴾

Na Ismaa’iyl, na Al-Yasa’a na Yuwnus, na Luutw. Na wote Tuliwafadhilisha juu ya walimwengu.

وَمِنْ آبَائِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ وَإِخْوَانِهِمْ ۖ وَاجْتَبَيْنَاهُمْ وَهَدَيْنَاهُمْ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٨٧﴾

Na katika baba zao, na dhuriya wao, na ndugu zao. Na Tukawateua na Tukawaongoza kuelekea njia iliyonyooka.

 

ذَٰلِكَ هُدَى اللَّـهِ يَهْدِي بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۚ وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٨٨﴾

Hiyo ndiyo hidaaya ya Allaah, kwa hiyo, Humwongoza Amtakaye kati ya waja Wake. Na kama wangemshirikisha bila shaka yangeporomoka yale waliyokuwa wakitenda. [Al-An’aam: 83-88]

 

Na hii ni dalili ya kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Amemfadhilisha kuliko Manabii wengineo kama alivyosema Imaam As-Sa’dy  (رحمه الله):

“Inamaanisha: Fuata nyuma ee Rasuli Mkarimu mwendo wa hawa Manabii waliokhitariwa, na fuata millah zao. Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akafuata vigezo vyao akaongoka kwa hidaaya ya Rusuli (wote) wa kabla yake, na akakusanya kila aina ya mazuri yao. Ikamkusanyikia kwake fadhila na khulqa zikawapita walimwengu wote. Akawa Sayyid wa Rusuli wote, na Imaam wa wenye kumcha Allaah, basi   Swalaah za Allaah ziwe juu yake pamoja na Manabii wote wengineo.  Na kutokana na hivyo, Maswahaba wakatoa dalili kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ni Rasuli mbora kabilsa kuliko wote.  [Tafsiyr As-Sa’dy (Uk 263)]

 

 

 

Share

39-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Amepewa Al-Kawthar (Mto Ulioko PeponiWenye Kheri Nyingi)

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

39-Amepewa Al-Kawthar (Mto Ulioko Peponi Wenye Kheri Nyingi)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

عَنْ أَنَسٍ (رضي الله عنه) : ((إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ)) أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: ((هُوَ نَهْرٌ فِي الْجَنَّةِ))

Anas (رضي الله عنه) amehadithia (kuhusu Kauli Yake Allaah): “Hakika Sisi Tumekupa Al-Kawthar”; kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Huo ni Mto katika Jannah.” [Al-Bukhaariy, At-Tirmidhiy]  

 

 

 

عَنْ أَنَسٍ، قَالَ: بَيْنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ذَاتَ يَوْمٍ بَيْنَ أَظْهُرِنَا إِذْ أَغْفَى إِغْفَاءَةً ثُمَّ رَفَعَ رَأْسَهُ مُتَبَسِّمًا فَقُلْنَا: مَا أَضْحَكَكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟  قَالَ: ((أُنْزِلَتْ عَلَىَّ آنِفًا سُورَةٌ ))‏. فَقَرَأَ: (( بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ * إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ * فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ * إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ الأَبْتَرُ)).‏ ثُمَّ قَالَ: ((أَتَدْرُونَ مَا الْكَوْثَرُ؟)). فَقُلْنَا اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ.‏ قَالَ: ((فَإِنَّهُ نَهْرٌ وَعَدَنِيهِ رَبِّي عَزَّ وَجَلَّ عَلَيْهِ خَيْرٌ كَثِيرٌ هُوَ حَوْضٌ تَرِدُ عَلَيْهِ أُمَّتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ آنِيَتُهُ عَدَدُ النُّجُومِ فَيُخْتَلَجُ الْعَبْدُ مِنْهُمْ فَأَقُولُ رَبِّ إِنَّهُ مِنْ أُمَّتِي‏.‏ فَيَقُولُ مَا تَدْرِي مَا أَحْدَثَتْ بَعْدَكَ))‏.‏ زَادَ ابْنُ حُجْرٍ فِي حَدِيثِهِ بَيْنَ أَظْهُرِنَا فِي الْمَسْجِدِ‏.‏ وَقَالَ:‏ ((مَا أَحْدَثَ بَعْدَكَ))‏.

 

Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Siku moja Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa pamoja nasi akawa amepitiwa na lepe la usingizi kisha akanyanyua kichwa chake juu huku akitabasamu, tukasema: Ni kitu gani kimekufurahisha ee Rasuli wa Allaah? Akasema: “Imeniteremkia sasa hivi Suwrah: (Akaisoma Suwrah Al-Kawthar).

 

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ * إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ * فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ * إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ الأَبْتَرُ *

 [Al-Kawthar: (108)]  

 

Kisha akasema: “Je, mnajua ni nini Al-Kawthar?” Tukajibu: Allaah na Rasuli Wake Ndio Wajuao zaidi. Akasema: “Huo ni mto ambao Allaah (عزّ وجلّ) Ameniahidi. Una kheri nyingi sana, nao una hodhi lake ambalo Ummah wangu watakusudia kulifikia Siku ya Qiyaamah. Vyombo vyake (au bilauri) ni idadi ya nyota. Mja miongoni mwao atatolewa mbali atengwe. Nitasema: Ee Rabb! Hakika yeye ni katika Ummah wangu!  Allaah Atasema: Hujui nini alizusha baada yako!”

 

Ibn Hujri amezidisha katika Hadiyth yake: Alikuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amekaa kitako pamoja nasi Msikitini. Na (Allaah) Atasema: “Hujui walichokizusha baada yako!” [Muslim – Kitaab Asw-Swalaah - Mlango wa hoja anayesema kuwa Al-Basmalah ni Aayah katika kila mwanzo wa Suwrah isipokuwa Suwrah Al-Baraa (At-Tawbah)] 

 

 

Share

40-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Allaah Amemsifu Kuwa Ni Mpole Na Mwenye Rehma Kwa Ummah Wake

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

40- Allaah Amemsifu Kuwa Ni Mpole Na Mwenye Rehma Kwa Ummah Wake

www.alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

فَبِمَا رَحْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ لِنتَ لَهُمْ ۖ وَلَوْ كُنتَ فَظًّا غَلِيظَ الْقَلْبِ لَانفَضُّوا مِنْ حَوْلِكَ ۖ فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاسْتَغْفِرْ لَهُمْ وَشَاوِرْهُمْ فِي الْأَمْرِ ۖ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚإِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَوكِّلِينَ ﴿١٥٩﴾

Basi ni kwa rahmah kutoka kwa Allaah umekuwa mpole kwao (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Na lau ungelikuwa mjeuri mwenye moyo mgumu wangelitawanyika mbali nawe. Basi wasamehe na waombee maghfirah na washauri katika mambo. Na unapoazimia basi tawakali kwa Allaah. Hakika Allaah Anapenda wanaotawakali. [Aal-‘Imraan: 159]

 

Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿١٢٨﴾

Kwa yakini amekujieni Rasuli anayetokana na nyinyi wenyewe, yanamtia mashaka (na huzuni) yanayokutaabisheni, anakujalini, mwenye huruma kwa Waumini ni mwenye huruma mno, mwenye rahmah. [At-Tawbah: 128]

 

 

 

 

Share

41-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Nabiy Pekee Aliyejaaliwa Fadhila Tele Za Kumswalia

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم) 

41-Nabiy Pekee Aliyejaaliwa Fadhila Tele Za Kumswalia

www.alhidaaya.com

 

 

قال رَسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ صَلَّى عَلَيَّ صَلَاةً صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ بِهَا عَشْرًا))

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Atakayeniswalia mara moja basi Allaah Atamswalia mara kumi)) [Hadiyth ya Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)  - Muslim (1/288) [408] Amesema Al-Bukhaariy katika Swahiyh yake: Abul Al-‘Aaaliyah amesema: “Swalaah ya Allaah ni kumsifu kwake mbele ya Malaika na Swalaah ya Malaika ni du’aa”]

 

وَقال رَسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((لا تجعلوا قبري عيدا، وصلوا علي فإن صلاتكم تبلغني حيث كنتم))

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Msilifanye kaburi langu kuwa ni mahali pa kurejewa rejewa, na niswalieni kwani kuniswalia kwenu kunanifikia popote mlipo)) [Hadiyth ya Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)   - Abu Daawuwd (2/218) [2042], Ahmad (2/367) na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Swahiyh  Abi Daawuwd (2/383)]

 

 

وَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ لِلَّهِ مَلائِكَةً سَيَّاحِينَ فِي الأَرْضِ يُبَلِّغُونِي مِنْ أُمَّتِي السَّلام))

Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Hakika Allaah Ana Malaika wanamzunguka katika ardhi, wananiletea salamu kutoka kwa Ummah wangu))  [Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Mas-‘uwd (رضي الله عنه)  -  An-Nasaaiy (3/43), Al-Haakim (2/421) na ameisahihisha  katika Swahiyh An-Nasaaiy  (1/274)]

 

 

وَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم َ: ((مَا مِنْ أحَدٍ يُسَلِّمْ علَيَّ إلاَّ رَدَّ اللهُ رُوحِي حَتَّى أَرُدَّ عَلَيْهِ السَّلامَ))

Na pia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Hakuna mtu yeyote anayeniswalia ila Allaah hunirudisha roho yangu ili nimrudishie salamu))  [Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه)  - Abu Daawuwd  (2041), na Al-Albaaniy (رحمه الله) ameipa daraja ya Hasan katika Swahiyh Abi Daawuwd (1/283)]

 

Share

42-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Ni Kigezo Kizuri Kwa Anayetaka Kufaulu Aakhirah

 

Fadhila Za  Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

42-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Ni Kigezo Kizuri Kwa Anayetaka Kufaulu Aakhirah

 

www.alhidaaya.com

 

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Amemjaalia Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa na tabia njema zilokamilika nazo ni kigezo kwa yeyote yule anayetaka kufuzu Aakhirah kwa kuingizwa Jannah (Peponi) na kuepushwa na Moto. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ  

Kwa yakini mna kigezo kizuri kwa Rasuli wa Allaah kwa mwenye kumtaraji Allaah na Siku ya Mwisho  [Al-Ahzaab: 21]

 

Imaam As-Sa’dy (رحمه الله) amesema kuhusu kauli hiyo ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

“Mwenye kufuata kigezo chake amefuata njia ya kumfikisha katika Utukufu wa Allaah na hiyo ndio Njia Iliyonyooka. Na kigezo hicho kizuri hukifuata  na kupata tawfiyq kwa mwenye kumtaraji Allaah na Siku ya Mwisho, kwa sababu ya kuwa kwake na iymaan, khofu ya Allaah, kutaraji thawabu na khofu ya adhabu Yake, basi hujihimiza kufuata kigezo cha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).” [Tafsiyr As-Sa’dy]

 

 

 

 

Share

43-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Iymaan Hazitimii Bila Ya Kufuata Na Kutekeleza Hukmu Yake (صلى الله عليه وآله وسلم)

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

43-Iymaan Hazitimii Bila Ya Kufuata Na Kutekeleza

Hukmu Yake (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

 فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٦٥﴾

Basi Naapa kwa Rabb wako, hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni mwamuzi katika yale wanayozozana baina yao, kisha wasipate katika nyoyo zao karaha katika yale uliyohukumu na wajisalimishe, kwa kujisalimisha kikamilifu. [An-Nisaa: 65]

 

 

Kisa cha Maswahaba kilichosababisha kuteremshwa Aayah hiyo tukufu:

 

عَنْ عُرْوَةَ بْنِ الزُّبَيْرِ، أَنَّ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ الزُّبَيْرِ، حَدَّثَهُ أَنَّ رَجُلاً مِنَ الأَنْصَارِ خَاصَمَ الزُّبَيْرَ عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي شِرَاجِ الْحَرَّةِ الَّتِي يَسْقُونَ بِهَا النَّخْلَ، فَقَالَ الأَنْصَارِيُّ: سَرِّحِ الْمَاءَ‏ يَمُرُّ، فَأَبَى عَلَيْهِمْ، فَاخْتَصَمُوا عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم لِلزُّبَيْرِ: ‏"‏ اسْقِ يَا زُبَيْرُ ثُمَّ أَرْسِلِ الْمَاءَ إِلَى جَارِكَ ‏"‏ ‏.‏ فَغَضِبَ الأَنْصَارِيُّ فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَنْ كَانَ ابْنَ عَمَّتِكَ، فَتَلَوَّنَ وَجْهُ نَبِيِّ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ثُمَّ قَالَ: ‏"‏ يَا زُبَيْرُ اسْقِ ثُمَّ احْبِسِ الْمَاءَ حَتَّى يَرْجِعَ إِلَى الْجَدْرِ ‏"‏ ‏.‏ فَقَالَ الزُّبَيْرُ: وَاللَّهِ إِنِّي لأَحْسِبُ هَذِهِ الآيَةَ نَزَلَتْ فِي ذَلِكَ:‏ فَلاَ وَرَبِّكَ لاَ يُؤْمِنُونَ حَتَّى يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لاَ يَجِدُوا فِي أَنْفُسِهِمْ حَرَجًا

‘Urwa bin Zubayr (رضي الله عنه)  amehadithia kwamba ‘Abdullaah bin Zubayr alimhadithia kwamba, bwana mmoja katika Answaar, alikhitilafiana naye mbele ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu maeneo ya kumwagia maji ya Harra ambayo wanamwagilia maji mitende yao. Answaari akasema: “Acha maji yatiririke.” Lakini (Zubayr) alikataa kufanya hivyo na gomvi likaletwa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) naye akamwambia Zubayr: “Ee Zubayr, mwagilia maji (mitende yako) na acha maji yatiririke kwa jirani yako.”  Answaari akaghadhibika na kusema: “Ee Rasuli wa Allaah! (umetoha hukmu hiyo) kwa kuwa ni bin wa ammat (Shangazi) yako?”  Hapo uso wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ukabadilika rangi (kwa ghadhabu). Basi hapo akasema: “Ee Zubayr mwagilia maji (mitende yako) kisha izuie hadi ipande juu katika kuta.” Zubayr akasema: “Wa-Allaahi, nadhani kuwa Aayah hii imeteremka kwa ajili hiyo.”

 

 فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٦٥﴾

Basi Naapa kwa Rabb wako, hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni mwamuzi katika yale wanayozozana baina yao, kisha wasipate katika nyoyo zao karaha katika yale uliyohukumu na wajisalimishe, kwa kujisalimisha kikamilifu. [An-Nisaa: 65 - Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Share

44-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) : Baina Ya Nyumba Yake Na Minbar Yake Amefanyiwa Kipande Cha Pepo Rawdhwatul-Jannah

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

44-Baina Ya Nyumba Yake Na Minbar Yake Amefanyiwa

Kipande Cha Pepo Rawdhwatul-Jannah

www.alhidaaya.com

 

 

Allaah (عز وجل) Amemfanyia Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)  kipande cha Jannah (Pepo) baina ya nyumba yake na Minbar yake. Na nyumba yake hiyo ni ile ambayo ilikuwa ni ya Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها):  

 

 

عنْ أَبِى هُرَيْرَةَ رضى الله عنه عَنِ النَّبِىِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ : ( مَا بَيْنَ بَيْتِى وَمِنْبَرِى رَوْضَةٌ مِنْ رِيَاضِ الْجَنَّةِ )  

Kutoka kwa Abiu Hurayrah (رضي الله عنه)  kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Baina ya nyumba yangu na Minbari yangu kuna Rawdhwah kutoka Rawdhwah ya Jannah)) yaani kipande cha Peponi. [Al-Bukhaari (1196), Muslim (1391)]

 

 

Na ‘Ulamaa wamekubaliana kwamba katika hiyo Rawdhwatul-Jannah, ni mustahabb (inapendekezwa) kumdhukuru Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kila aina ya kumdhukuru; kuswali rakaa mbili, pindi mtu anapojaaliwa kutembelea Masjdi An-Nabawiy (Msikiti wa Nabiy ulioko Madiynah). Lakini kwa hali ilivyo sasa ya msongamano mkubwa wa watu, mtu anaweza kuswali katika maeneo ya kando ili kuepusha zahma na madhara kwa Waislamu na bila shaka hupata thawabu na fadhila zake sawasawa bila ya upungufu wowote wa fadhila za hicho kipande cha Rawdhwatul-Jannah, bali kwa sababu ya niyyah njema ya kuepusha msongamano baina ya Waislamu, huenda mtu akalipwa malipo zaidi kutokana na niyyah yake njema.  

 

 

 

Share

45-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Amepewa Al-Wasiylah (Heshima Maalum) Na Al-Maqaam Al-Mahmuwd (Cheo Cha Kusifika) Siku Ya Qiyaamah

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

45-Amepewa Al-Wasiylah (Heshima Maalum)

Na Al-Maqaam Al-Mahmuwd (Cheo Cha Kusifika) Siku Ya Qiyaamah

 

www.alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

وَمِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَّكَ عَسَىٰ أَن يَبْعَثَكَ رَبُّكَ مَقَامًا مَّحْمُودًا ﴿٧٩﴾

Na katika usiku, amka uswali (tahajjud) kuisoma (Qur-aan); ni ziada ya Sunnah kwako Asaa Rabb wako Akakuinua cheo kinachosifika. [Al-Israa: 79]

 

 

Nayo ni Ash-Shafaa’ah (Uombezi) Siku ya Qiyaamah baada ya kisimamo kirefu mno cha watu katika mkusanyiko wa viumbe wote. Watu watamwendea Nabiy Aadam, Nuwh, Ibraahiym, Muwsaa na ‘Iysaa  (عليهم السلام) wawaombe Ash-Shafaa’ah lakini kila mmoja atakataa kwa kutoa udhuru wake, na kila mmoja atawaambia Ummah wake wapeleke ombi   kwa Nabii mwenginewe mpaka watu wamfikie Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) wamuombe, na hapo ndipo atakapoinama kusujudu na kumuomba Rabb Wake Ash-Shafaa’ah,  na Allaah (عز وجل) Atamkubalia Shafaa yake, basi mahali hapo ndipo pakaitwa “Al-Maqaam Al-Mahmuwd” [Cheo cha Kusifika] kwa kuwa viumbe wote watamsifu Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa sababu Shafaa’ah yake ndio sababu yao kufanyiwa wepesi kisimamo chao kirefu mno Siku hiyo ya Mkusanyiko. Hadiyth ifutayo inathibitisha:

 

 

عن ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا يَقُولُ : ( إِنَّ النَّاسَ يَصِيرُونَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ جُثًا ، كُلُّ أُمَّةٍ تَتْبَعُ نَبِيَّهَا يَقُولُونَ : يَا فُلانُ اشْفَعْ ، يَا فُلانُ اشْفَعْ ، حَتَّى تَنْتَهِيَ الشَّفَاعَةُ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَذَلِكَ يَوْمَ يَبْعَثُهُ اللَّهُ الْمَقَامَ الْمَحْمُودَ ) رواه البخاري  

Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما) amesema: Watu watasubiri wakiwa watapiga magoti Siku ya Qiyaamah, na kila Ummah utamfuata Nabiy wake wakisema: “Ee fulani tuombee Ash-Shafaa’ah (kwa Allaah), mpaka ombi la Ash-Shafaa’ah litamfikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), na hiyo ndio siku ambayo Allaah Atamuinua katika Al-Maqaam Al-Mahmuwd (Cheo Cha Kusifika) [Al-Bukhaariy]

 

Miongoni mwa amali zikatazosababisha kupata Ash-Shafaa’ah ya Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

 

1-Kuitikia Mwadhini na kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ، أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ ‏ " إذَا سَمِعْتُمْ الْمُؤَذِّنَ فَقُولُوامِثْلَ مَا يَقُولُ ، ثُمَّ صَلُّوا عَلَيَّ ، فَإِنَّهُ مَنْ صَلَّى عَلَيَّ صَلاةً صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ بِهَا عَشْرًا . ثُمَّ سلُوا اللَّه لي الْوسِيلَةَ ، فَإِنَّهَا مَنزِلَةٌ في الجنَّةِ لا تَنْبَغِي إِلاَّ لعَبْدٍ منْ عِباد اللَّه وَأَرْجُو أَنْ أَكُونَ أَنَا هُو ، فَمنْ سَأَل ليَ الْوسِيلَة حَلَّتْ لَهُ الشَّفاعَةُ

Abdullaah bin ‘Amruw (رضي الله عنهما)  kwamba kamsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) akisema: ((Mtakapomsikia muadhini basi semeni kama anavyosema, kisha niswalieni, kwani mwenye kuniswalia mara moja Allaah Atamswalia mara kumi, na kisha niombeeni (kupata) ‘wasiylah’ ambayo ni manzila (heshima maalum) huko Jannah. Haitomstahikia isipokua mja mmoja katika waja wa Allaah, nami ninatarajia kuwa mja huyo, na mwenye kuniombea “Al-Wasiylah” atapata uombezi (wangu Siku ya Qiyaamah)) [Muslim (1/288)

 

 

2-Kuitikia Mwadhini na kumuombea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  du’aa iliyothibiti:

 

وَعَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   قَالَ : {مَنْ قَالَ حِينَ يَسْمَعُ اَلنِّدَاءَ : اَللَّهُمَّ رَبَّ هَذِهِ اَلدَّعْوَةِ اَلتَّامَّةِ،  وَالصَّلَاةِ اَلْقَائِمَةِ،  آتِ مُحَمَّدًا اَلْوَسِيلَةَ وَالْفَضِيلَةَ،  وَابْعَثْهُ مَقَامًا مَحْمُودًا اَلَّذِي وَعَدْتَهُ، حَلَّتْ لَهُ شَفَاعَتِي يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ}  أَخْرَجَهُ اَلْأَرْبَعَةُ

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kusoma anaposikia Adhana:

 اَللَّهُمَّ رَبَّ هَذِهِ اَلدَّعْوَةِ اَلتَّامَّةِ،  وَالصَّلَاةِ اَلْقَائِمَةِ،  آتِ مُحَمَّدًا اَلْوَسِيلَةَ وَالْفَضِيلَةَ،  وَابْعَثْهُ مَقَامًا مَحْمُودًا اَلَّذِي وَعَدْتَهُ

Allaahumma Rabba haadhihid-dda’watit-ttaamah, wasw-Swaalaatil qaaimah, aati Muhammada  al-wasiylata wal fadhwiylah, wab-‘ath-hu maqaaman mahmuwdan alladhiy wa’adtah.

(Ee Allaah, Rabb wa mwito huu uliotimia, na Swalaah iliyosimama, mpe (Nabiy) Muhammad al-Wasiylah (cheo, heshima maalumu, daraja), na fadhila, na mfikishe daraja yenye kuhimidiwa, ambayo Umemuahidi).

Ash-Shafaa’ah (Uombezi) wangu umehalalika kwake Siku ya Qiyaamah.” [Imetolewa na Al-Arba’ah]

 

 

3-Kuimarika katika Tawhiyd ya Allaah (عز وجل)

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ أَنَّهُ قَالَ قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ : مَنْ أَسْعَدُ اَلنَّاسِ بِشَفَاعَتِكَ؟ قَالَ: ((مَنْ قَالَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اَللَّهُ خَالِصًا مِنْ قَلْبِهِ))

Abuu Hurayrah (رضي اَللَّهُ عَنْهُ) alimesema: Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) “Nani atakayefanikiwa zaidi na shafaa’ah yako? Akajibu: ((Atakayesema

لاَ إِلَهَ إِلاَّ اَللَّهُ

Laa ilaaha illa-Allaah

hali ya kuwa na niyyah safi moyoni mwake)) [Al-Bukhaariy]

 

 

4-Kuzidishia Kusujudu (Kuswali Nawaafil):

 

Imehadithiwa na mmoja wa Mtumishi wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba:

كان ممَّا يقولُ للخادمِ : ألكَ حاجةٌ ؟ قال : حتى كان ذاتَ يومٍ فقال : يا رسولَ اللهِ ! حاجتي ، قال : و ما حاجتك ؟ قال : حاجَتي أن تشفعَ لي يومَ القيامةِ  قال : و من دلَّكَ على هذا ؟ قال : ربِّي ، قال : أما لا ، فأعنِّي بكثرةِ السجودِ

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akimwambia Mtumishi wake: “Je unahitaji lolote?” Hadi siku moja (Mtumishi) akasema: “Ee Rasuli wa Allaah nina haja!” Akauliza: “Nini haja yako?” akasema: “Haja yangu uniombee Shafaa Siku ya Qiyaamah.”  Akamuuliza: Nani aliyekuongoza kuomba hilo?” Akasema: “Rabb Wangu.” Akasema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Basi nisaidie kwa kuzidisha kusujudu (kuswali)” [As-Silsilah Asw-Swahiyha 2102], Swahiyh Al-Musnad (1497])

 

Pia,

 

 عن أبي فراس رَبِيعَة بْن كَعْبٍ الْأَسْلَمِيُّ رضي الله عنه    خادم رسول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: كُنْتُ أَبِيتُ مَعَ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَأَتَيْتُهُ بِوَضُوئِهِ وَحَاجَتِهِ، فَقَالَ لِي: ((سَلْني)) فَقُلْتُ: أَسْأَلُكَ مُرَافَقَتَكَ فِي الْجَنَّةِ، قَالَ: ((أَوْ غَيْرَ ذَلِكَ؟))  قُلْتُ: هُوَ ذَاكَ، قَالَ: ((فَأَعِنِّي عَلَى نَفْسِكَ بِكَثْرَةِ السُّجُودِ)) رواه مسلم في  صحيحه

Kutoka kwa Abuu Firaas Rabiy'ah bin Ka'ab Al-Aslamiy mtumishi wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  ambaye amesema: "Nililala na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  usiku mmoja nikamletea maji ya kutawadha, akaniambia: ((Niombe utakacho)) Nikasema: "Nataka kuandamana na wewe Jannah. Akasema: ((Hutaki lolote lingine?)) Nikasema: "Ni hilo tu."  Akasema:  ((Basi nisaidie (ili hilo liwezekane) kwa kuzidisha kusujudu [Kuswali])) [Muslim katika Swahiyh yake] 

 

 

 

 

Share

46-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Allaah Ametanguliza Kumtaja Yeye Katika Qur-aan Kabla Ya Manabii Wengineo

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

46-Allaah Ametanguliza Kumtaja Yeye Katika Qur-aan Kabla Ya Manabii Wengineo

 

www.alhidaaya.com

 

 

Miongoni mwa fadhila zake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ni kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) amemtanguliza Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kumtaja kabla ya Manabii wengineo au kumlinganisha na Manabii wengine katika Aayaat za Qur-aan kadhaa, miongoni mwazo ni kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَإِذْ أَخَذْنَا مِنَ النَّبِيِّينَ مِيثَاقَهُمْ وَمِنكَ وَمِن نُّوحٍ وَإِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ۖ وَأَخَذْنَا مِنْهُم مِّيثَاقًا غَلِيظًا ﴿٧﴾

Na pale Tulipochukua kutoka kwa Manabii fungamano lao na kutoka kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na kutoka kwa Nuwh, na Ibraahiym, na Muwsaa, na ‘Iysaa mwana wa Maryam; na Tukachukua kutoka kwao fungamano gumu. [Al-Ahzaab: 7]

 

Na pia Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِنَّا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ كَمَا أَوْحَيْنَا إِلَىٰ نُوحٍ وَالنَّبِيِّينَ مِن بَعْدِهِ ۚ وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَعِيسَىٰ وَأَيُّوبَ وَيُونُسَ وَهَارُونَ وَسُلَيْمَانَ ۚ وَآتَيْنَا دَاوُودَ زَبُورًا ﴿١٦٣﴾

Hakika Tumekufunulia Wahy (ee Muhammadصلى الله عليه وآله وسلم) kama Tulivyomfunulia Wahy Nuwh na Manabii baada yake. Na Tumemfunulia Wahy Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na dhuriya, na ‘Iysaa na Ayyuwb na Yuwnus na Haaruwn, Na Sulaymaan. Na Tumempa Daawuwd Zabuwr. [An-Nisaa: 163]

 

Share

47-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ametumwa Kutimiza Akhlaaq (Tabia) Njema

 

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

47-Ametumwa Kutimiza Akhlaaq (Tabia) Njema

www.alhidaaya.com

 

 

Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ametumwa kutimiza Akhlaaq (tabia):

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ الله عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ‏:‏ ((إِنَّمَا بُعِثْتُ لِأُتَمِّمَ صَالِحَ الأَخْلاقِ‏))

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)  amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)    amesema: ((Hakika nimetumwa ili nikamilishe khulqa (tabia) njema)) [Ahmad na ameisahihisha Al-Albaaniy Swahiyh Al-Jaami’ (2349), Swahiyh Adab Al-Mufrad (207)]

 

Ni fadhila adhimu kabisa kujaaliwa yeye mtu mmoja, Nabiy wa mwisho ili akhlaaq hizo ziwe kigezo wa walimwengu wote waliobakia mpaka Siku ya Mwisho ili kwa atakayemwamini na kumfuata iwe ni sababu ya kufaulu kwake duniani na Aakhirah.

 

Hivyo basi, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akadhihirisha Akhlaaq zake ambazo ni kigezo na sifa za kujinasabisha nazo Muumin wa kweli na akataja katika Hadiyth zake kadhaa kuwa Akhlaaq njema ni sababu kuu ya kumfikisha mtu katika Jannaatul-Firdaws karibu naye, na haya ndio mafanikio adhimu kabisa ya kupaswa kuyaazimia kwa nguvu. Mfano wa Hadiyth aliyothibitisha kabisa kuwa Akhlaaq njema zitakuwa ni nzito kabisa katika Miyzaan ya mja Siku ya Qiyaamah:

 

عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: (( مَا مِنْ شَىْءٍ أَثْقَلُ فِي الْمِيزَانِ مِنْ حُسْنِ الْخُلُقِ ‏))

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ad-Dardaai kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna kitakachokuwa kizito katika Miyzaan kama Husnul-Khuluq [tabia njema])) [Sunan Abiy Daawuwd, As-Silsilah Asw-Swahiyhah (2/535), Swahiyh Al-Jaami’ (5721), Swahiyh Adab Al-Mufrad (204)]

 

 

Bonyeza kiungo kifuatacho upate Hadiyth tele zenye kutaja Akhlaaq (tabia) zake (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

 

 

Share

48-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Amepewa Funguo Za Hazina Za Ulimwengu Wote

 

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

48-Amepewa Funguo Za Hazina Za Ulimwengu Wote

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم خَرَجَ يَوْمًا فَصَلَّى عَلَى أَهْلِ أُحُدٍ صَلاَتَهُ عَلَى الْمَيِّتِ، ثُمَّ انْصَرَفَ إِلَى الْمِنْبَرِ فَقَالَ ‏ "‏ إِنِّي فَرَطٌ لَكُمْ، وَأَنَا شَهِيدٌ عَلَيْكُمْ، وَإِنِّي وَاللَّهِ لأَنْظُرُ إِلَى حَوْضِي الآنَ، وَإِنِّي أُعْطِيتُ مَفَاتِيحَ خَزَائِنِ الأَرْضِ ـ أَوْ مَفَاتِيحَ الأَرْضِ ـ وَإِنِّي وَاللَّهِ مَا أَخَافُ عَلَيْكُمْ أَنْ تُشْرِكُوا بَعْدِي، وَلَكِنْ أَخَافُ عَلَيْكُمْ أَنْ تَنَافَسُوا فِيهَا ‏"‏‏.‏

 

Kutoka kwa ‘Uqbah bin ‘Aamir (رضي الله عنه) amesema: Siku moja Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikwenda nje na akaongoza Swalaah za maiti; Mashuhadaa wa Uhd, kisha akapanda katika Minbar akasema: “Mimi nitaandaa njia kwa ajili yenu kama muasisi na nitakuwa Shahidi kwa ajili yenu. Na wa-Allaahi, ninaiona Al-Hawdhw (chemchemi ya Al-Kawthar) sasa hivi na nimepewa funguo za hazina zote za ardhi (au funguo za ardhi). Na Wa-Allaahi, hakika mimi sikhofu kuwa mtamshirikisha Allaah baada ya kufa kwangu, lakini nakhofu kuwa mtagombana baina yenu kwa ajili ya vitu vya kidunia.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Kupewa Hazina Za Ulimwengu: Ni kuongezeka na kupanuka Uislamu, na kujaaliwa ushindi mkubwa na mateka ya mali, kwa sababu unapopatikana ushindi wa nchi ni sawa na kumiliki mali na hazina zake.

 

 

Share

49-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Nabiy Pekee Aliyepewa Kauli Za Kusherehi Kitabu Chake

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

49-Nabiy Pekee Aliyepewa Kauli Za Kusherehi Kitabu Chake

 

 

www.alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

  وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ﴿٤٤﴾

 (Tumewatuma) Kwa hoja bayana na vitabu. Na Tumekuteremshia Ukumbusho (Qur-aan) ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao huenda wakapata kutafakari. [An-Nahl: 44]

 

 

Maana yake: “Tumekuteremshia Qur-aan ee Rasuli, ili uwabainishie wazi watu yaliyofichikia katika maana zake, hukmu zake na ili wazingatie (Aayaat) na waongoke kwayo.” [Tafsiyr Al-Muyassar]

 

Hivyo basi anayoyasema katika kusherehi Aayaat za Qur-aan ni Wahyi Aliofunuliwa Na Allaah (سبحانه وتعالى) Ambaye Anasema:

 

 

مَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣﴾

Na wala hatamki kwa hawaa.

إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ﴿٤﴾

Hayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa. [An-Najm: 3-4]

 

Akasema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  kuthibitisha hayo katika Hadiyth:

 

((أَلَا إِنِّي أُوتِيتُ الْقُرْآنَ وَمِثْلَهُ مَعَهُ)) صحيح رواه أبو داود

((Hakika mimi nimepewa Qur-aan na mfano wake)) [Hadiyth Swahiyh, Abuu Daawuwd]

 

 

 

Share

50-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Amepewa Na Amejaaliwa Mambo Kadhaa Ambayo Manabii Wengineo Hawakupewa

 

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

50-Amepewa Na Amejaaliwa Mambo Kadhaa Ambayo Manabii Wengineo Hawakupewa

Alhidaaya.com

 

 

 

Miongoni mwa mambo ambayo Amejaaliwa na kupewa Nabiy Muhammad  (صلى الله عليه وآله وسلم)  pasi na Manabii wengineo ni:

 

 

1-Kujaaliwa Swafu zake (katika Swalaah za Jamaa) kuwa ni kama Swafu za Malaika.

 

 

2-Amehalalishiwa ghanima (ngawira na mateka ya vita).

 

 

3-Amejaaliwa ardhi kuwa ni twahara. Kwa maana yanapokosekana maji ya kutawadhia Waislamu hufanya Tayammum.

 

 

4-Amejaaliwa ardhi kuwa ni Masjid (Msikiti) kwa maana mtu anaweza kuswali popote katika ardhi madamu ni mahali pasafi; anaweza kuswali njiani, darasani, uwanjani na kadhaalika.

 

 

5-Amepewa Jawaami’ul-Kalim’ (mkusanyiko wa maneno machahe lakini yenye maana pana).

 

 

 

6-Ataruhusiwa Ash-Shafaa’’ah (Uombezi) Siku ya Qiyaamah kuwashufai watu na kuwaingiza Jannah.

 

 

7-Ataruhusiwa kuwaingiza Jannah watu elfu sabiini bila ya kuhesabiwa na bila kuadhibiwa; bonyeza kiungo kifuatacho:

 

24-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ameruhusiwa Kuingiza Jannah Watu Sabiini Elfu Katika Ummah Wake

 

 

8-Amenusuriwa kwa kutiwa khofu na kizaazaa katika nyoyo za makafiri; kwa maana Allaah (سبحانه وتعالى) Ametia kiwewe na khofu kubwa katika nyoyo za makafiri hadi waogope kupigana vita au wanyon’gonyee na kushindwa kupigana na Waumini.

 

 

9-Ametumwa kwa Ulimwengu wote, kwani Manabii wengineo walitumwa kwa kaumu zao tu.

 

 

Hadiyth zifuatazo zimethibitisha hayo:

 

 

Kunusuriwa Kwa Kiwewe, Kuhalalishiwa Ghanima, Kupewa Ash-Shafaa’ah, Kutumwa Wa Walimwengu Wote:

 

عن جَابِرُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((أُعْطِيتُ خَمْسًا لَمْ يُعْطَهُنَّ أَحَدٌ قَبْلِي،  نُصِرْتُ بِالرُّعْبِ مَسِيرَةَ شَهْرٍ، وَجُعِلَتْ لِيَ الأَرْضُ مَسْجِدًا وَطَهُورًا، فَأَيُّمَا رَجُلٍ مِنْ أُمَّتِي أَدْرَكَتْهُ الصَّلاَةُ فَلْيُصَلِّ، وَأُحِلَّتْ لِيَ الْمَغَانِمُ وَلَمْ تَحِلَّ لأَحَدٍ قَبْلِي، وَأُعْطِيتُ الشَّفَاعَةَ، وَكَانَ النَّبِيُّ يُبْعَثُ إِلَى قَوْمِهِ خَاصَّةً، وَبُعِثْتُ إِلَى النَّاسِ عَامَّةً))

Jaabir bin Abdillaah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Nimepewa mambo matano hakupewa yoyote kabla yangu; Nimenusuriwa na (kutiwa) kiwewe (nyoyoni mwa maadui) kwa mwendo wa mwezi. Na nimefanyiwa ardhi kuwa sehemu ya kufanyia ‘ibaadah na kujitwaharishia, basi mtu mtu yeyote katika ummah wangu akifikiwa na Swalaah, aswali. Na nimehalalishiwa ngawira hazikuwa halali kwa yeyote kabla yangu. Na nimepewa shafaa’ah (maombezi Siku ya Qiyaamah). Na alikuwa Nabiy akitumwa kwa watu wake pekee, lakini mimi nimetumwa kwa watu wote.” [Al-Bukhaariy (5011)]  

 

Kupewa Jawaami’ul-Kalimi, Kunusuriwa Kwa Kiwewe, Kuhalalishiwa Ghanima, Kufanyiwa Ardhi Kuwa Ni Twahara Na Masjid, Kutumwa Kwa Walimwengu Wote, Kufanywa Nabiy Wa Mwisho:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)  قَالَ:  ((فُضِّلْتُ عَلَى الأَنْبِيَاءِ بِسِتٍّ:  أُعْطِيتُ جَوَامِعَ الْكَلِمِ، وَنُصِرْتُ بِالرُّعْبِ، وَأُحِلَّتْ لِيَ الْغَنَائِمُ، وَجُعِلَتْ لِيَ الأَرْضُ طَهُورًا وَمَسْجِدًا، وَأُرْسِلْتُ إِلَى الْخَلْقِ كَافَّةً، وَخُتِمَ بِيَ النَّبِيُّونَ))

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraryah (رضي الله عنه)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: ((Nimefadhilishwa juu ya Manabii kwa mambo sita; nimepewa ‘Jawaami’al-Kalimi’  na nimenusuriwa kwa kutiwa kiwewe na khofu (katika nyoyo za maadui) na nimehalalishiwa ghanima  na nimefanyiwa ardhi kuwa kitoharishi na Masjid (mahali pa kuswali), na nimetumwa kwa viumbe wote, na Manabii wamekhitimishwa kwangu))[Muslim]

 

 

Kujaaliwa Swafu Kama Swafu Za Malaikah, Ardhi Kuwa ni Msikiti, Ardhi Kuwa Twahara: 

 

عَنْ حُذَيْفَةَ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ فُضِّلْنَا عَلَى النَّاسِ بِثَلاَثٍ جُعِلَتْ صُفُوفُنَا كَصُفُوفِ الْمَلاَئِكَةِ وَجُعِلَتْ لَنَا الأَرْضُ كُلُّهَا مَسْجِدًا وَجُعِلَتْ تُرْبَتُهَا لَنَا طَهُورًا إِذَا لَمْ نَجِدِ الْمَاءَ ‏"‏ ‏.‏ وَذَكَرَ خَصْلَةً أُخْرَى ‏.‏

 

Imepokelewa kutoka kwa Hudhayfah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Tumefadhilishwa kuliko watu wengine katika mambo matatu: Safu zetu zimefanywa katika safu za Malaika, ardhi yote imefanywa kwetu kuwa Msikiti na mchanga wake umefanywa twahara kwetu ikiwa hakuna maji.” Na akataja fadhila nyengine. [Muslim].

 

Swafu kama za Malaika zimetajwa katika Hadiyth:

 

عَنْ جَابِرِ بْنِ سَمُرَةَ، قَالَ خَرَجَ عَلَيْنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ ‏"‏ مَا لِي أَرَاكُمْ رَافِعِي أَيْدِيكُمْ كَأَنَّهَا أَذْنَابُ خَيْلٍ شُمْسٍ اسْكُنُوا فِي الصَّلاَةِ ‏"‏ ‏.‏ قَالَ ثُمَّ خَرَجَ عَلَيْنَا فَرَآنَا حَلَقًا فَقَالَ ‏"‏ مَا لِي أَرَاكُمْ عِزِينَ ‏"‏ ‏.‏ قَالَ ثُمَّ خَرَجَ عَلَيْنَا فَقَالَ ‏"‏ أَلاَ تَصُفُّونَ كَمَا تَصُفُّ الْمَلاَئِكَةُ عِنْدَ رَبِّهَا ‏"‏ ‏.‏ فَقُلْنَا يَا رَسُولَ اللَّهِ وَكَيْفَ تَصُفُّ الْمَلاَئِكَةُ عِنْدَ رَبِّهَا قَالَ ‏"‏ يُتِمُّونَ الصُّفُوفَ الأُوَلَ وَيَتَرَاصُّونَ فِي الصَّفِّ ‏"‏ ‏.‏

Imepokelewa toka kwa Jaabir bin Samrah akisema: “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitutokea akasema: ((Mbona nawaona mnanyanyua mikono yenu kana kwamba ni mikia ya farasi waliochacharika? Tulieni katika Swalaah)). Akasema: Kisha akatutokea akatuona tumejigawa mafungu mafungu akatuambia: ((Kwa nini msipange safu kama wanavyopanga safu Malaika mbele ya Rabb wao?)) Tukasema: Ee Rasuli wa Allaah! Ni vipi Malaika wanapanga safu mbele ya Rabb wao? Akasema: ((Wanaikamilisha safu ya kwanza na wanazinyoosha safu zao)). [Muslim, Abuu Daawuwd (661), An-Nasaaiy (2/92), Ibn Maajah (992)].

 

 

 

 

Share

51-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Amefunuliwa Wahyi Mbingu Ya Saba; Suwrah Na Aayah Mbili Ambazo Hajapewa Nabii Yoyote Kabla Yake

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

51-Amefunuliwa Wahyi Mbingu Ya Saba; Suwrah Na Aayah Mbili

Ambazo Hajapewa Nabii Yoyote Kabla Yake  

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) amepewa katika Qur-aan Suwrah Al-Faatihah na Aayah mbili za mwisho wa Suwratul-Baqarah, ambazo hajapatapo kupewa mfano wa kama Aayah hizo Nabiy mwenginewe kabla yake.  Juu ya hivyo, Aayah hizo amefunuliwa nazo Wahyi akiwa mbingu ya Saba katika safari ya Israa wal-Mi’raaj:

 

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ بَيْنَمَا جِبْرِيلُ قَاعِدٌ عِنْدَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم سَمِعَ نَقِيضًا مِنْ فَوْقِهِ فَرَفَعَ رَأْسَهُ فَقَالَ: ((هَذَا بَابٌ مِنَ السَّمَاءِ فُتِحَ الْيَوْمَ لَمْ يُفْتَحْ قَطُّ إِلاَّ الْيَوْمَ، فَنَزَلَ مِنْهُ مَلَكٌ فَقَالَ: هَذَا مَلَكٌ نَزَلَ إِلَى الأَرْضِ لَمْ يَنْزِلْ قَطُّ إِلاَّ الْيَوْمَ، فَسَلَّمَ وَقَالَ أَبْشِرْ بِنُورَيْنِ أُوتِيتَهُمَا لَمْ يُؤْتَهُمَا نَبِيٌّ قَبْلَكَ، فَاتِحَةُ الْكِتَابِ وَخَوَاتِيمُ سُورَةِ الْبَقَرَةِ لَنْ تَقْرَأَ بِحَرْفٍ مِنْهُمَا إِلاَّ أُعْطِيتَهُ)) ‏.‏

Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)   amehadithia kwamba: Jibriyl   (عليه السلام)  alipokuwa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  alisikia sauti kutoka juu. Jibriyl   (عليه السلام) akatazama juu akasema: “Huu mlango wa mbinguni umefunguliwa na haujapatapo kufunguliwa isipokuwa leo.” Malaika akateremka humo akasema: “Huyu Malaika ameteremka ardhini, hajapatapo kuteremka kamwe isipokuwa leo.” Akasalimia kisha   akasema: “Pokea bishara ya nuru mbili ulizopewa ambazo hakuna Nabiy aliyepewa kabla yako; Ufunguo wa Kitabu (Al-Faatihah), na Aayah (mbili) za mwisho wa Suwratul-Baqarah.  Hutosoma herufi humo ila utapewa barakah zake ziliomo.” [Muslim]

 

 

Imaam Muslim amenukuu katika Swahiyh yake kuwa Aayah hizi mbili alipewa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) alipofika kikomo mbingu ya saba katika Safari ya Al-Israa Wal-Mi’raaj pamoja na kupewa Swalaah tano na msamaha kwa mtu asiyemshirikisha Allaah na yeyote au chochote.

 

 

 

Share

52-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ametumwa Kubashiria Na Kuonya Walimwengu

 

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

52-Ametumwa Kubashiria Na Kuonya Walimwengu

 

www.alhidaaya.com

 

 

Kama ilivyotangulia fadhila ya kuwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ametumwa kwa Walimwengu wote, basi kubashiria na kuonya kwake hali kadhalika ni kwa ajili ya ulimwengu mzima na si kaumu yake tu kama ilivyokuwa desturi ya Manabii wengineo kabla yake:

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):   

 

تَبَارَكَ الَّذِي نَزَّلَ الْفُرْقَانَ عَلَىٰ عَبْدِهِ لِيَكُونَ لِلْعَالَمِينَ نَذِيرًا ﴿١﴾

Amebarikika Ambaye Ameteremsha kwa mja Wake pambanuo (la haki na batili) ili awe muonyaji kwa walimwengu. [Al-Furqaan: 1]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

أَكَانَ لِلنَّاسِ عَجَبًا أَنْ أَوْحَيْنَا إِلَىٰ رَجُلٍ مِّنْهُمْ أَنْ أَنذِرِ النَّاسَ وَبَشِّرِ الَّذِينَ آمَنُوا أَنَّ لَهُمْ قَدَمَ صِدْقٍ عِندَ رَبِّهِمْ ۗ قَالَ الْكَافِرُونَ إِنَّ هَـٰذَا لَسَاحِرٌ مُّبِينٌ﴿٢﴾

Je, imekuwa ni ajabu kwa watu kwamba Tumemfunulia Wahy mtu miongoni mwao kwamba: Waonye watu na wabashirie wale walioamini kwamba watapata cheo kitukufu mbele ya Rabb wao. Makafiri wakasema: Hakika huyu bila shaka ni mchawi bayana. [Yuwnus: 2]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَأَرْسَلْنَاكَ لِلنَّاسِ رَسُولًا ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا ﴿٧٩﴾

Na Tumekutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa watu uwe Rasuli na inatosheleza Allaah kuwa ni Mwenye kushuhudia yote. [An-Nisaa: 79]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَـٰذَا الْقُرْآنُ لِأُنذِرَكُم بِهِ وَمَن بَلَغَ ۚ

Na nimefunuliwa Wahy hii Qur-aan ili nikuonyeni kwayo na kila itakayomfikia.[Al-An’aam: 19]

 

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ شَاهِدًا وَمُبَشِّرًا وَنَذِيرًا ﴿٤٥﴾

Ee Nabiy! Hakika Sisi Tumekutuma uwe shahidi, na mbashiriaji na mwonyaji.

 

وَدَاعِيًا إِلَى اللَّـهِ بِإِذْنِهِ وَسِرَاجًا مُّنِيرًا ﴿٤٦﴾

Na mlinganiaji kwa Allaah kwa idhini Yake; na siraji kali yenye nuru.

 

وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ بِأَنَّ لَهُم مِّنَ اللَّـهِ فَضْلًا كَبِيرًا ﴿٤٧﴾

Na wabashirie Waumini kwamba watapata kutoka kwa Allaah fadhila kubwa.

 

وَلَا تُطِعِ الْكَافِرِينَ وَالْمُنَافِقِينَ وَدَعْ أَذَاهُمْ وَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا ﴿٤٨﴾

Na wala usiwatii makafiri na wanafiki, na achilia mbali maudhi yao, na tawakali kwa Allaah. Na Allaah Anatosheleza kuwa Mdhamini. [Al-Ahzaab: 45-48]

 

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ وَإِن لَّمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ ۚ وَاللَّـهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ ﴿٦٧﴾

Ee Rasuli! Balighisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako. Na usipofanya, basi utakuwa hukubalighisha ujumbe Wake. Na Allaah Atakuhifadhi dhidi ya watu. Hakika Allaah Haongoi watu makafiri [Al-Maaidah: 67]

 

 

Bonyeza kiungo kifuatacho upate faida  inayohusiana na maudhui ya fadhila hii:

 

 

02-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ametumwa Kwa Walimwengu Wote

 

 

 

 

Share

53-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Amepewa Ummah Bora Kabisa

 Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

53-Amepewa Ummah Bora Kabisa  

 

www.alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):   

 

كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ ۗ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُم ۚ مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿١١٠﴾

Mmekuwa Ummah bora kabisa uliotolewa (mfano) kwa watu; mnaamrisha mema na mnakataza munkari na mnamwamini Allaah. Na lau wangeliamini Ahlul-Kitaabi ingelikuwa ni bora kwao, miongoni mwao wanaoamini na wengi wao ni mafasiki [Aal-‘Imraan: 110]

 

 

Na Hadiyth zinathibitisha na kufafanua zaidi:  

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَة َ رضى الله عنه ((‏كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ‏)) قَالَ خَيْرَ النَّاسِ لِلنَّاسِ، تَأْتُونَ بِهِمْ فِي السَّلاَسِلِ فِي أَعْنَاقِهِمْ حَتَّى يَدْخُلُوا فِي الإِسْلاَمِ‏.‏

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kuhusu:    

 ‏كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ‏

"Mmekuwa Ummah bora kabisa uliotolewa (mfano) kwa watu"

 

Kasema:  “Watu bora kabisa kati ya watu, mtawajia kwa minyororo katika shingo zao mpaka waingie Uislamu.” [Al-Bukhaariy]

 

تَأْتُونَ بِهِمْ فِي السَّلاَسِلِ فِي أَعْنَاقِهِمْ حَتَّى يَدْخُلُوا فِي الإِسْلاَمِ‏

Maana ya: “Mtawajia kwa minyororo katika shingo zao mpaka waingie Uislamu.”

 

“Ni matekwa waliokamatwa na Waislamu, basi Allaah huwaongoza na kuingia katika Uislaam kwa hivyo wanafaidika na kuingia Peponi. Hii ni katika neema adhimu na fadhila za Allaah  juu ya matekwa kisha wakaingia Uislamu na hawakuuawa na makafiri.” [Imaam Ibn Baaz – Sharh Riyaadhw Asw-Swaalihiyn]

 

 

Na pia:

 

عَنْ بَهْزِ بْنِ حَكِيمٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ، أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ فِي قَوْلِهِ كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ ‏ قَالَ ‏"‏ إِنَّكُمْ تُتِمُّونَ سَبْعِينَ أُمَّةً أَنْتُمْ خَيْرُهَا وَأَكْرَمُهَا عَلَى اللَّهِ ‏"‏

Kutoka kwa Bahz bin Haakim, kutoka baba yake, kutoka kwa babu yake kwamba kamsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema kuhusu kauli ya Allaah:

‏كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ‏

Mmekuwa Ummah bora kabisa uliotolewa (mfano) kwa watu

Nyinyi ni  umaliziaji wa mataifa sabini, nyie ndiye bora zaidi, na ndiyo (Ummah) mtukufu bora mbele ya Allaah. [Hadiyth Hasan At-Tirmidhiy]

 

Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):   

 

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا ۗ

Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah bora na adilifu ili muwe mashahidi juu ya watu na awe Rasuli shahidi juu yenu. [Al-Baqrah: 143]

 

 

Share

54-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Anaombewa Du’aa Na Kuswaliwa Katika Kila Aina Za Ibaadah Za Waumini

 

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

54-Anaombewa Du’aa Na Kuswaliwa Katika Kila Aina Za Ibaadah Za Waumini

 

www.alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

وَرَفَعْنَا لَكَ ذِكْرَكَ ﴿٤﴾

Na Tukanyanyulia juu utajo wako (ukawa mwenye kusifika mno)?  [Ash-Sharh: 4]

 

Allaah (عز وجل) Amemjaalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) fadhila adhimu kabisa nayo ni fadhila za kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika hali mbalimbali ya maisha ya Muislamu; katika Swalaah zote za faradhi na za Sunnah, namo ni katika Adhana na Iqaamah na katika kikao cha Tashahhud, katika Swalaah ya Jeneza, anapotajwa katika vikao vya elimu, zinapotajwa Hadiyth zake, katika ‘ibaada za Hajj na ‘Umrah, katika kuomba du’aa, katika Adhkaar za asubuhi na jioni, baada ya kutawadha, watu wanapokhutubia katika Minbar, zinapofungwa Nikaah,  Siku ya Ijumaa imeamrishwa kukithirisha kumswalia, na katika,  hali nyenginezo. Juu ya hivyo  imeamrishwa kuwa pindi inapoadhiniwa aombewe du’aa na kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Kumswalia kote huko humrudia fadhila zake kwa Muislamu anayetekeleza amri hii:

 

 

1-Baada Ya Kutawadha:

 

أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ  

Ash-hadu an laa ilaaha illa-Allaah, Wahdahu laa shariyka Lahu wa ash-hadu anna Muhammadan ‘Abduhu wa Rasuwluhu

 

2-Katika Adhana:

 

 

اللهُ أكبَر اللهُ أكبر، الله أكبر اللهُ أكبر، أشهدُ أنْ لا إلهَ إلَّا الله، أشهدُ أنْ لا إلهَ إلَّا الله، أشهدُ أنَّ محمدًا رسولُ الله، أشهدُ أنَّ محمدًا رسولُ الله، حيَّ على الصَّلاة، حيَّ على الصَّلاة، حيَّ على الفلاح، حيَّ على الفلاح، اللهُ أكبر اللهُ أكبر، لا إلهَ إلَّا الله

 

Allaahu Akbar Allaahu Akbar, Allaahu Akbar Allaahu Akbar, Ash-hadu an laa ilaaha illa-Allaah, Ash-hadu an laa ilaaha illa-Allaah,   Ash-hadu anna Muhammadan Rasuwlu-Allaah, Ash-hadu anna Muhammadan Rasuwlu-Allaah, Hayya ‘alas-Swalaah, Hayya ‘alas-Swalaah, Hayya ‘alal-Falaah, Hayya ‘alal-Falaah,   Allaahu Akbar Allaahu Akbar, laa ilaaha illa-Allaah

 

 

3-Anaombewa Du’aa Na Anaswaliwa Inapoadhiniwa:

 

 

وَعَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم   قَالَ : {مَنْ قَالَ حِينَ يَسْمَعُ اَلنِّدَاءَ : اَللَّهُمَّ رَبَّ هَذِهِ اَلدَّعْوَةِ اَلتَّامَّةِ،  وَالصَّلَاةِ اَلْقَائِمَةِ،  آتِ مُحَمَّدًا اَلْوَسِيلَةَ وَالْفَضِيلَةَ،  وَابْعَثْهُ مَقَامًا مَحْمُودًا اَلَّذِي وَعَدْتَهُ، حَلَّتْ لَهُ شَفَاعَتِي يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ}  أَخْرَجَهُ اَلْأَرْبَعَةُ

 

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kusoma anaposikia Adhana:

 

 اَللَّهُمَّ رَبَّ هَذِهِ اَلدَّعْوَةِ اَلتَّامَّةِ،  وَالصَّلَاةِ اَلْقَائِمَةِ،  آتِ مُحَمَّدًا اَلْوَسِيلَةَ وَالْفَضِيلَةَ،  وَابْعَثْهُ مَقَامًا مَحْمُودًا اَلَّذِي وَعَدْتَهُ

Allaahumma Rabba haadhihid-dda’watit-ttaamah, wasw-Swaalaatil qaaimah, aati Muhammada  al-wasiylata wal fadhwiylah, wab-‘ath-hu maqaaman mahmuwdan alladhiy wa’adtah.

 

(Ee Allaah, Rabb wa mwito huu uliotimia, na Swalaah iliyosimama, mpe (Nabiy) Muhammad al-Wasiylah (cheo, heshima maalumu, daraja), na fadhila, na mfikishe daraja yenye kuhimidiwa, ambayo Umemuahidi).

Ash-Shafaa’ah (Uombezi) wangu umehalalika kwake Siku ya Qiyaamah.” [Imetolewa na Al-Arba’ah]

 

 

Na pia,

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ، أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ ‏ " إذَا سَمِعْتُمْ الْمُؤَذِّنَ فَقُولُوامِثْلَ مَا يَقُولُ ، ثُمَّ صَلُّوا عَلَيَّ ، فَإِنَّهُ مَنْ صَلَّى عَلَيَّ صَلاةً صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ بِهَا عَشْرًا . ثُمَّ سلُوا اللَّه لي الْوسِيلَةَ ، فَإِنَّهَا مَنزِلَةٌ في الجنَّةِ لا تَنْبَغِي إِلاَّ لعَبْدٍ منْ عِباد اللَّه وَأَرْجُو أَنْ أَكُونَ أَنَا هُو ، فَمنْ سَأَل ليَ الْوسِيلَة حَلَّتْ لَهُ الشَّفاعَةُ

‘Abdullaah bin ‘Amruw (رضي الله عنهما)  kwamba kamsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) akisema: ((Mtakapomsikia muadhini basi semeni kama anavyosema, kisha niswalieni, kwani mwenye kuniswalia mara moja Allaah Atamswalia mara kumi, na kisha niombeeni (kupata) ‘wasiylah’ ambayo ni manzila (heshima maalum) huko Jannah. Haitomstahikia isipokua mja mmoja katika waja wa Allaah, nami ninatarajia kuwa mja huyo, na mwenye kuniombea “Al-Wasiylah” atapata uombezi (wangu Siku ya Qiyaamah)) [Muslim (1/288)

 

 

4-Katika Iqaamah:

 

اللهُ أكبر اللهُ أكبر، أشهدُ أنْ لا إلهَ إلَّا الله، أشهدُ أنَّ محمدًا رسولُ الله، حيَّ على الصَّلاة، حيَّ على الفلاح، قد قامتِ الصَّلاةُ، قد قامتِ الصَّلاة، اللهُ أكبر اللهُ أكبر، لا إلهَ إلَّا الله

 

Allaahu Akbar Allaahu Akbar, Ash-hadu an laa ilaaha illa-Allaah, Ash-hadu anna Muhammadan Rasuwlu-Allaah, Hayya ‘alas-Swalaah, Hayya ‘alal-Falaah, Qad Qaamatis-Swalaah  Qad Qaamatis-Swalaah, Allaahu Akbar Allaahu Akbar, laa ilaaha illa-Allaah

 

 

5-Katika Kikao Cha Tashahhud:

 

 

التَّحِيّـاتُ للهِ وَالصَّلَـواتُ والطَّيِّـبات، السَّلامُ عَلَيـكَ أَيُّهـا النَّبِـيُّ وَرَحْمَـةُ اللهِ وَبَرَكـاتُه، السَّلامُ عَلَيْـنا وَعَلـى عِبـادِكَ الصَّـالِحـين، أَشْـهَدُ أَنْ لا إِلـهَ إِلاّ الله، وَأَشْـهَدُ أَنَّ مُحَمّـداً عَبْـدُهُ وَرَسـولُه

At-tahiyyaatu liLLaahi, was-swalawaatu, wat-twayyibaatu, Assalaamu ‘alayka ayyuhan-Nnabiyyu warahmatu-Allaahi wa Barakaatuh, Assalaamu ‘alaynaa wa ’alaa ‘IbaadiLLaahis-swaalihiyn. Ash-hadu an-laa ilaaha illa-Allaah wa ash-hadu anna Muhammadan ‘Abduhu wa Rasuwluhu

 

اللّهُـمَّ صَلِّ عَلـى مُحمَّـد وَعَلـى آلِ مُحمَّد كَمـا صَلَّيـتَ عَلـى إبْراهـيمَ وَعَلـى آلِ إبْراهـيم إِنَّكَ حَمـيدٌ مَجـيد، اللّهُـمَّ بارِكْ عَلـى مُحمَّـد وَعَلـى آلِ مُحمَّـد كَمـا بارِكْتَ عَلـى إبْراهـيمَ وَعَلـى آلِ إبْراهيم إِنَّكَ حَمـيدٌ مَجـيد .

Allaahumma Swalli ‘alaa Muhammad wa ‘alaa aali Muhammad, kamaa Swallayta ‘alaa Ibraahiyma wa ‘alaa aali Ibraahiyma, Innaka Hamiydun Majiyd. Allaahumma Baarik ‘alaa Muhammad, wa ‘alaa aali Muhammad, kamaa Baarakta ‘alaa  Ibraahiyma wa ‘alaa  aali Ibraahiyma, Innaka Hamiydun Majiyd.

 

 

6-Du’aa Haipandi Mbinguni Bila Ya Kumswalia Mwanzo Na Mwisho Wa Du’aa:

 

 

عَنْ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ (رضي الله عنه)  قَالَ: "إِنَّ الدُّعَاءَ مَوْقُوفٌ بَيْنَ السَّمَاءِ وَالأَرْضِ لاَ يَصْعَدُ مِنْهُ شَيْءٌ حَتَّى تُصَلِّيَ عَلَى نَبِيِّكَ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)"

Imepokelewa kutoka kwa ‘Umar bin Khattwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu): “Hakika du’aa inasimama baina ya mbingu na ardhi haipandi masafa yoyote mpaka umswalie Nabiy wako (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)." [Swahiyh At-Tirmidhiy (486), Swahiyh At-Targhiyb (1676)]

 

 

7-Kukithirisha Kumswalia Siku Ya Ijumaa:

 

عَنْ أَوْسِ بْنِ أَوْسٍ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ مِنْ أَفْضَلِ أَيَّامِكُمْ يَوْمَ الْجُمُعَةِ، فَأَكْثِرُوا عَلَيَّ مِنْ الصَّلاةِ فِيهِ، فَإِنَّ صَلاَتَكُمْ مَعْرُوضَةٌ عَلَيَّ)) قَالوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ وَكَيْفَ تُعْرَضُ صَلاتُنَا عَلَيْكَ وَقَدْ أَرَمْتَ؟  قَالَ: يَقُولُ:  بَلِيتَ  قَالَ: ((إِنَّ اللَّهَ تَبَارَكَ وَتَعَالَى حَرَّمَ عَلَى الأَرْضِ أَجْسَادَ الأَنْبِيَاءِ)) رواه ابو داوُود بِاِسنادٍ صحيح

Imepokelewa kutoka kwa Aws bin Aws (رضي الله عنه)  ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه  وآله وسلم ) amesema: ((Hakika siku zenu zilizo bora mno ni siku ya Ijumaa, basi kithirisheni kuniswalia siku hiyo, hakika Swalaah zenu huwa naletewa)). Maswahaba wakauliza: “Ee Rasuli wa Allaah! Vipi Swalaah zetu kuwa unaletewa na ilihali wakati huo utakuwa umeshaoza?” Akajibu: ((Hakika Allaah Ameiharamisha ardhi kula viwiliwili vya Manabii)). [Abuu Daawuwd kwa Isnaad Swahiiyh]

 

 

Share

55-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Aliwaimamisha Manabii Wote Katika Swalaah Siku Ya Israa Wal Miaraaj

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

55-Aliwaimamisha Manabii Wote Katika Swalaah Siku Ya Israa Wal Miaraaj

 

Alhidaaya.com

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipofika Masjid Al-Aqswaa aliwasalisha Manabii wote wengine nyuma yake. Hadiyth ndefu yenye maelezo yafuatayo:

 

فلمَّا أَتَى النبيُّ صلَّى اللهُ عليهِ وسلَّمَ المسجدَ الأَقْصَى قامَ يصلِّي ، فالتَفَتَ ثُمَّ التَفَتَ فإِذَا النبيُّونَ أجمعونَ يُصَلُّونَ مَعَهُ . فلمَّا انصرفَ جِيءَ بِقَدَحَيْنِ ، أحدُهُما عن اليَمِينِ والآخَرُ عَنِ الشِّمالِ ، في أَحَدِهما لَبَنٌ وفي الآخَرِ عَسَلٌ ، فأخذَ اللَّبَنَ فَشربَ مِنْهُ ، فقال الذي كان مَعَهُ القَدَحُ : أَصَبْتَ الفِطْرَةَ

Pindi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipofika Masjid Al-Aqwswaa alisimama kuswali, akageuka kisha akageuka, tahamaki Manabii wote walikuweko kuswali naye.  Alipomaliza akaletewa vyombo viwili, kimoja kuliani na kingine kushotoni. Kimojawapo kina maziwa na kingine kina asali. Akachukua maziwa akanywa, basi aliyekuwa naye (Jibriyl) alimwamba “Umeongozwa katika fitwrah.”  [Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Abaaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ameikhariji Ahmad Isnaad yake ni Swahiyh, na Imaam Ibn Kathiyr katika Tafsiyr yake]

 

 

Share

56-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ummah Wake Utashudhuia Umati Zote Za Nyuma

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

56-Ummah Wake Utashudhuia Umati Zote Za Nyuma

Alhidaaya.com

 

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا ۗ

Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah bora na adilifu ili muwe mashahidi juu ya watu na awe Rasuli shahidi juu yenu. [Al-Baqarah: 143]

 

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ يَجِيءُ نُوحٌ وَأُمَّتُهُ فَيَقُولُ اللَّهُ تَعَالَى هَلْ بَلَّغْتَ فَيَقُولُ نَعَمْ، أَىْ رَبِّ‏.‏ فَيَقُولُ لأُمَّتِهِ هَلْ بَلَّغَكُمْ فَيَقُولُونَ لاَ، مَا جَاءَنَا مِنْ نَبِيٍّ‏.‏ فَيَقُولُ لِنُوحٍ مَنْ يَشْهَدُ لَكَ فَيَقُولُ مُحَمَّدٌ صلى الله عليه وسلم وَأُمَّتُهُ، فَنَشْهَدُ أَنَّهُ قَدْ بَلَّغَ، وَهْوَ قَوْلُهُ جَلَّ ذِكْرُهُ ‏(( ‏وَكَذَلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ‏)) وَالْوَسَطُ الْعَدْلُ ‏"‏‏.‏ البخاري

 

Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ataitwa Nuwh Siku ya Qiyaamah ataulizwa: Je, umebalighisha ujumbe? Atasema: Naam. Wataitwa watu wake wataulizwa: Je, alikufikishieni ujumbe? Watasema: Hakutujia mwonyaji wala hakuna aliyetumwa kwetu. Ataulizwa Nuwh: Nani mwenye kukushuhudia hayo? Atasema: Muhammad na Ummah wake.  Akasema: Hiyo ndio maana kauli Yake:

 

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ  

Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah bora na adilifu ili muwe mashahidi juu ya watu. Akasema: “Waswatwaa, maana yake ni uadilifu basi mtatoa ushahidi (kuhusu Nuwh) kubalighisha ujumbe na kisha nitakuwa shahidi wenu.”  [Ahmad (3/32) na Al-Bukhaariy pia kama hivyo (4487)]

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَجَاهِدُوا فِي اللَّـهِ حَقَّ جِهَادِهِ ۚ هُوَ اجْتَبَاكُمْ وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ ۚ مِّلَّةَ أَبِيكُمْ إِبْرَاهِيمَ ۚ هُوَ سَمَّاكُمُ الْمُسْلِمِينَ مِن قَبْلُ وَفِي هَـٰذَا لِيَكُونَ الرَّسُولُ شَهِيدًا عَلَيْكُمْ وَتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ ۚ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَاعْتَصِمُوا بِاللَّـهِ هُوَ مَوْلَاكُمْ ۖ فَنِعْمَ الْمَوْلَىٰ وَنِعْمَ النَّصِيرُ ﴿٧٨﴾

Na fanyeni jihaad katika njia ya Allaah kama inavyostahiki kufanyiwa jihaad. Yeye Ndiye Amekuteueni na Hakukufanyieni ugumu wowote ule katika Dini. Mila ya baba yenu Ibraahiym. Yeye (Allaah) Ndiye Aliyekuiteni Waislamu hapo zamani na pia katika hii (Qur-aan). Ili Rasuli (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) awe shahidi juu yenu, nanyi muwe mashahidi juu ya watu.  [Al-Hajj: 78]

 

Imaam As-Sa’diy amesema kuhusu kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ

nanyi muwe mashahidi juu ya watu.  

 

Kwa sababu ya kuwa kwenu nyinyi Waislamu ni Ummah bora kabisa uliotolewa kwa watu, Ummah wa wastani kwa uadilifu, basi mtashahudia Rusuli wote kwamba wamebalighisha ujumbe kwa Ummah zao, na mtashuhudia kwa Ummah zote kwamba Rusuli wao wamebalighisha ujumbe kutokana na yale ambayo Allaah Amekujulisheni katika Kitabu Chake (Qur-aan). [Tafsiyr As’Sa’diy]

 

Ummah wa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa ni Ummah bora kabisa ni kutokana na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ ۗ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُم ۚ مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿١١٠﴾

Mmekuwa Ummah bora kabisa uliotolewa (mfano) kwa watu; mnaamrisha mema na mnakataza munkari na mnamwamini Allaah. Na lau wangeliamini Ahlul-Kitaabi ingelikuwa ni bora kwao, miongoni mwao wanaoamini na wengi wao ni mafasiki [Aal-‘Imraan:110]

 

 

 

 

Share

57-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Dini Yake Ndio Itakayoshinda Dini Zote

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

57-Dini Yake Ndio Itakayoshinda Dini Zote

 

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا﴿٢٨﴾

Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad  (صلى الله عليه وآله وسلم kwa mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote. Na Allaah Anatosha kuwa ni Shahidi. [Al-Fat-h:28]

 

Qiyaamah hakitasimama hadi Dini ya Kiislaam ishinde Dini zote, na hii imeshaanza kudhihirika ulimwenguni kutokana na matukio kadhaa yaliyosababisha watu wengi kuingia katika Uislaam. 

 

Na katika Dalili kumi kubwa za kusimama Qiyaamah zipo Hadiyth kadhaa zinazoelezea hayo mojawapo ifuatayo:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَة قَالَ : قَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ  ((يَنْزِل عِيسَى اِبْن مَرْيَم فَيَقْتُل الْخِنْزِير وَيَمْحُو الصَّلِيب وَتُجْمَع لَهُ الصَّلَاة وَيُعْطِي الْمَال حَتَّى لَا يُقْبَل وَيَضَع الْخَرَاج وَيَنْزِل الرَّوْحَاء فَيَحُجّ مِنْهَا أَوْ يَعْتَمِر أَوْ يَجْمَعهُمَا))  أحمد

Kutoka kwa Abu Hurayrah ambaye amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)    amesema: ((‘Iysaa mwana wa Maryam atateremka na kuua nguruwe, atavunja misalaba, ataimamisha watu katika Swalaah ya Jamaa, na kutoa mali hadi hakuna atakayetaka kupokea tena. Ataondosha jizya (kodi) na atakwenda Ar-Rawhaa ambako ataelekea kutekeleza Hajj, ‘Umrah au zote mbili)) [Ahmad]

 

Imaam Atw-Twabariy amesema  kuhusu kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ ۚ

 

Ili Aishindishe juu ya dini zote.

 

“Hivyo ni kubatilisha millah (dini) zote hadi kwamba hakutakuwa na Dini nyingine isipokuwa hiyo, na hivyo ndivyo ilivyokuwa mpaka ‘Iysaa mwana wa Maryam ashuke na kumuua Ad-Dajaal, hapo Dini zote zitabatilishwa isipokuwa Dini ya Allaah aliyomtuma nayo Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)   na Uislaam ushinde juu ya dini zote."

 

 

Na Hadiyth nyenginezo zifuatazo:   

 

 عَنْ تَمِيمٍ الدَّارِيِّ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَيَبْلُغَنَّ هَذَا الْأَمْرُ مَا بَلَغَ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَلَا يَتْرُكُ اللَّهُ بَيْتَ مَدَرٍ وَلَا وَبَرٍ إِلَّا أَدْخَلَهُ اللَّهُ هَذَا الدِّينَ بِعِزِّ عَزِيزٍ أَوْ بِذُلِّ ذَلِيلٍ عِزًّا يُعِزُّ اللَّهُ بِهِ الْإِسْلَامَ وَذُلًّا يُذِلُّ اللَّهُ بِهِ الْكُفْرَ

Tamiym Ad-Daariyy amesimulia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)   amesema: “Jambo hili (Uislaam) hakika litafika kila mahali palipoguswa na usiku na mchana. Allaah Hatoacha  nyumba au makazi isipokuwa Allaah Ataingizi Dini hii kwa ‘izza (utukufu) ambao watukufu watajaaliwa taadhima na wadhalili watadhalilika. Allaah Atawapa utukufu watukufu kwa Uislaam na Atawadhalilisha wadhalili kwa Ukafiri. [Ahmad]       

 

Na pia,

 

عَن الْمِقْدَاد بن الْأسود قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: " يَقُولُ لَا يَبْقَى عَلَى ظَهْرِ الْأَرْضِ بَيْتُ مَدَرٍ وَلَا وَبَرٍ إِلَّا أَدْخَلَهُ اللَّهُ كلمة الاسلام بعز عَزِيز أَو ذل ذليل إِمَّا يعزهم الله عز وَجل فَيَجْعَلُهُمْ مِنْ أَهْلِهَا أَوْ يُذِلُّهُمْ فَيَدِينُونَ لَهَا  رَوَاهُ أَحْمد

Miqdaad bin Al-Aswad amesimulia: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akisema: “Haitasalia juu ya ardhi (duniani) nyumba ya udongo wala  hema la nywele za ngamia isipokuwa Allaah Ataingiza humo neno la Islaam kwa ‘izza (utukufu) ambao watukufu watajaaliwa taadhima na wadhalili watadhalilika ima Allaah  (‘Azza wa Jalla)  Awape utukufu wakazi na kuwajaalia wawe katika watu Wake, au Awadhalilishe na wawe duni mbele Yake.”  [Ahmad, Swahiyh Ibn Maajah (6701)]

 

 

Na Kauli Zake nyenginezo Allaah (سبحانه وتعالى):

 

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ﴿٩﴾

Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote, japo watakirihika washirikina. [Asw-Swaff: 9]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ﴿٣٣﴾

Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote, japo watakirihika washirikina. [At-Tawbah: 33]

 

 

 

Share

58-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Masiyh Dajjaal Haingii Katika Mji Wake Madiynah

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) 

 

58-Masiyh Dajjaal Haingii Katika Mji Wake Madiynah 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Pindi atakapotokeza Masiyh Dajjaal kama ni alama mojawapo kubwa za Qiyaamah, ataenea ulimwengu mzima isipokuwa mji wa Madiynah kutokana na utukufu wa mji huu na utukufu wake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Hadiyth kadhaa zimetaja kuhusu Masiyh Dajjaal na fitnah zake miongoni mwazo ni hizi zinazotaja kutokuweza kuingia Madiynah:

 

 

 عن أَنَس بْن مَالِكٍ رضى الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ لَيْسَ مِنْ بَلَدٍ إِلاَّ سَيَطَؤُهُ الدَّجَّالُ، إِلاَّ مَكَّةَ وَالْمَدِينَةَ، لَيْسَ لَهُ مِنْ نِقَابِهَا نَقْبٌ إِلاَّ عَلَيْهِ الْمَلاَئِكَةُ صَافِّينَ، يَحْرُسُونَهَا، ثُمَّ تَرْجُفُ الْمَدِينَةُ بِأَهْلِهَا ثَلاَثَ رَجَفَاتٍ، فَيُخْرِجُ اللَّهُ كُلَّ كَافِرٍ وَمُنَافِقٍ ‏"‏‏.‏

 

Amesimulia Anas bin Maalik (رضي الله عنه)   kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: “Hakuna mji hata mmoja ambao Dajjaal hatoingia isipokuwa Makkah na Madiynah, na hakutakuwa na njia (za Makkah na Madiynah) ila watasimama kwa safu Malaika wakiilinda dhidi yake. Kisha Madiynah itatetemeka mitetemeko mitatu pamoja na watu wake, hapo Allaah Atawatoa makafiri na wanafiki wote kwayo.”

 

 

Pia,

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم‏.‏ ‏ "‏ عَلَى أَنْقَابِ الْمَدِينَةِ مَلاَئِكَةٌ، لاَ يَدْخُلُهَا الطَّاعُونُ وَلاَ الدَّجَّالُ ‏"‏‏.‏

 

Amesimulia Abu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Katika milango inayoingia Madiynah kuna Malaika wenye kulinda njia zake. Madiynah haingiwi na tauni wala Dajjaal.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Pia,

 

  عَنْ أَبِي بَكْرَةَ رضى الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ لاَ يَدْخُلُ الْمَدِينَةَ رُعْبُ الْمَسِيحِ الدَّجَّالِ، لَهَا يَوْمَئِذٍ سَبْعَةُ أَبْوَابٍ، عَلَى كُلِّ باب مَلَكَانِ ‏"‏‏.‏

 

Amesimulia Abu Bakrah (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Madiynah haitafikiwa na khofu itakayoletwa na Al-Masiyh Dajjaal. Na wakati huo Madiynah itakuwa na milango saba, kila mlango utakuwa na Malaika wawili, wanaolinda.”

 

 

Maelezo mafupi kuhusu Masiyh Dajjaal:

 

 

Masiyh Ad-Dajjaal ni mtu miongoni mwa wana wa Aadam.  Atadhihiri duniani akiwa ni alama kubwa mojawapo za Qiyaamah. Sifa zake kadhaa zimetajwa miongoni mwazo ni kwamba atakuwa ni mtu mwenye jicho moja na baina ya macho yake kuna herufi zisizoungana za  ك ف ر  (ka fa ra)  au كافر   (kaafir) kwa herufi za kuungana. Kila Muislamu anayejua kusoma au asiyejua kusoma ataweza kusoma neno hilo.

 

 

Atakuja kuwafitinisha watu na fitnah yake itakuwa ni fitnah kubwa kabisa haijapata kutokea tangu Allaah (‘Azza wa Jalla) kumuumba Aadam kwa sababu Allaah Atamjaalia uwezo wa kufanya miujiza mikubwa ambayo itawashangaza na kuwachanganya watu wasio na iymaan. Ama Waumini hawatapotoshwa na Masiyd Dajjaal. Na ndio maana Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaifanya du’aa ya kujikinga na fitnah za Masiyh Dajjaal katika Swalaah kuwa ni jambo la muhimu mno.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share

59-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ujira Wa Ummah Wake Ni Zaidi Kuliko Ujira Wa Umati Za Nyuma

 

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

59-Ujira Wa Ummah Wake Ni Zaidi Kuliko Ujira Wa Umati Za Nyuma

 

Alhidaaya.com

 

 

Kutokana na Rahmah za Allaah (سبحانه وتعالى) na Fadhila zake kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), Amejaalia Ummah wa Kiislamu kupata fadhila hii ya kuwa thawabu za ‘amali za Waumini ni nyingi kulikoni thawabu za ‘amali walizotenda Umati zilizotangulia. Hadiyth na Kauli za Allaah (سبحانه وتعالى) zimethibiti hayo kama ifuatavyo:

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ رضى الله عنهما أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ إِنَّمَا مَثَلُكُمْ وَالْيَهُودُ وَالنَّصَارَى كَرَجُلٍ اسْتَعْمَلَ عُمَّالاً فَقَالَ مَنْ يَعْمَلُ لِي إِلَى نِصْفِ النَّهَارِ عَلَى قِيرَاطٍ قِيرَاطٍ فَعَمِلَتِ الْيَهُودُ عَلَى قِيرَاطٍ قِيرَاطٍ، ثُمَّ عَمِلَتِ النَّصَارَى عَلَى قِيرَاطٍ قِيرَاطٍ، ثُمَّ أَنْتُمُ الَّذِينَ تَعْمَلُونَ مِنْ صَلاَةِ الْعَصْرِ إِلَى مَغَارِبِ الشَّمْسِ عَلَى قِيرَاطَيْنِ قِيرَاطَيْنِ، فَغَضِبَتِ الْيَهُودُ وَالنَّصَارَى وَقَالُوا نَحْنُ أَكْثَرُ عَمَلاً وَأَقَلُّ عَطَاءً، قَالَ هَلْ ظَلَمْتُكُمْ مِنْ حَقِّكُمْ شَيْئًا قَالُوا لاَ‏.‏ فَقَالَ فَذَلِكَ فَضْلِي أُوتِيهِ مَنْ أَشَاءُ ‏"‏‏.‏

 Amesimulia ‘Abdillaahi bin ‘Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنهما)   kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: “Hakika mfano wenu na mfano wa Mayahudi na Manaswara ni mfano wa mtu aliyewaajiri vibarua, akawaambia: ‘Nani atakayenifanyia kazi kuanzia asubuhi mpaka mchana (saa sita) kwa Qiraatw moja?’ Mayahudi walikubali na kutekeleza kazi hiyo kwa Qiraatw moja; na kisha Manaswara wakafanya kazi mpaka Swalaah ya Alasiri kwa Qiraatw; na sasa nyinyi Waislamu mnafanya kazi kuanzia Swalaah ya Alasiri mpaka machweo kwa Qiraatw mbili kila mmoja.” Mayahudi na Manaswara walighadhibika, na wakasema: ‘Kwa nini tufanye kazi zaidi kwa malipo duni? Mwajiri (Allaah) Akawauliza: “Je, Nimenyakua haki yenu? Wakasema: ‘Hapana.’ Akasema: Hiyo ni Fadhila Yangu, Ninampatia Nimtakaye." [Al-Bukhaariy]

 

Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَآمِنُوا بِرَسُولِهِ يُؤْتِكُمْ كِفْلَيْنِ مِن رَّحْمَتِهِ وَيَجْعَل لَّكُمْ نُورًا تَمْشُونَ بِهِ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٨﴾ لِّئَلَّا يَعْلَمَ أَهْلُ الْكِتَابِ أَلَّا يَقْدِرُونَ عَلَىٰ شَيْءٍ مِّن فَضْلِ اللَّـهِ ۙ وَأَنَّ الْفَضْلَ بِيَدِ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ ﴿٢٩﴾

 

28. Enyi walioamini! Mcheni Allaah, na muaminini Rasuli Wake. (Allaah) Atakupeni sehemu mbili kati ya rahmah Zake, na Atakuwekeeni nuru mnatembea nayo, na Atakughufurieni; na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. 29. Ili wajue Ahlul-Kitaabi kwamba hawana uwezo wa chochote katika fadhila za Allaah, na kwamba fadhila zimo Mkononi mwa Allaah Humpa Amtakaye, na Allaah ni Mwenye fadhila adhimu. [Al-Hadiyd: 28 – 29]

 

 

Na pindi Ahlul-Kitaab wakisilimu kwa kumuamini Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), basi wameahidiwa kupata ujira mara mbili katika ‘amali zao kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ مِن قَبْلِهِ هُم بِهِ يُؤْمِنُونَ ﴿٥٢﴾ وَإِذَا يُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ قَالُوا آمَنَّا بِهِ إِنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّنَا إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلِهِ مُسْلِمِينَ ﴿٥٣﴾ أُولَـٰئِكَ يُؤْتَوْنَ أَجْرَهُم مَّرَّتَيْنِ بِمَا صَبَرُوا وَيَدْرَءُونَ بِالْحَسَنَةِ السَّيِّئَةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿٥٤﴾

52. Wale Tuliowapa Kitabu kabla yake, wao wanaiamini (Qur-aan). 53. Na wanaposomewa husema: Tumeiamini, hakika hiyo ni haki kutoka Rabb wetu, hakika Sisi kabla yake tulikuwa Waislamu waliojisalimisha. 54. Hao watapewa ujira wao mara mbili kwa vile walivyosubiri, na wanazuia ubaya kwa wema, na katika vile Tulivyowaruzuku hutoa. [Al-Qaswasw: 52 – 54]

 

 

Na Hadiyth ifuatayo inaunga mkono:

 

 

حدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ بْنُ عُيَيْنَةَ، حَدَّثَنَا صَالِحُ بْنُ حَىٍّ أَبُو حَسَنٍ، قَالَ سَمِعْتُ الشَّعْبِيَّ، يَقُولُ حَدَّثَنِي أَبُو بُرْدَةَ، أَنَّهُ سَمِعَ أَبَاهُ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ ثَلاَثَةٌ يُؤْتَوْنَ أَجْرَهُمْ مَرَّتَيْنِ الرَّجُلُ تَكُونُ لَهُ الأَمَةُ فَيُعَلِّمُهَا فَيُحْسِنُ تَعْلِيمَهَا، وَيُؤَدِّبُهَا فَيُحْسِنُ أَدَبَهَا، ثُمَّ يُعْتِقُهَا فَيَتَزَوَّجُهَا، فَلَهُ أَجْرَانِ، وَمُؤْمِنُ أَهْلِ الْكِتَابِ الَّذِي كَانَ مُؤْمِنًا، ثُمَّ آمَنَ بِالنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَلَهُ أَجْرَانِ، وَالْعَبْدُ الَّذِي يُؤَدِّي حَقَّ اللَّهِ وَيَنْصَحُ لِسَيِّدِهِ ‏"‏‏.‏ ثُمَّ قَالَ الشَّعْبِيُّ وَأَعْطَيْتُكَهَا بِغَيْرِ شَىْءٍ وَقَدْ كَانَ الرَّجُلُ يَرْحَلُ فِي أَهْوَنَ مِنْهَا إِلَى الْمَدِينَةِ‏.‏

Imepokewa kwa babake Abu Burdah (رضي الله عنه) amesema: “Watu watatu watapewa ujira wao mara mbili: Mtu aliye na kijakazi, naye akamsomesha inavyotakiwa na akamfundisha adabu njema, kisha akamuacha huru na kumuoa. Mtu huyo atapata ujira mara mbili. Na Muumini miongoni mwa Ahlul-Kitaab, ambaye alikuwa Muumini, kisha akamuamini Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), naye atakuwa na ujira mara mbili. Na mtumwa anayetekeleza haki za Allaah na akawa na ikhlasi kwa bwanake”.  [Al-Bukhaariy]

 

 

 

Share

60-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kitabu Chake (Qur-aan) Kimepewa Majina Na Sifa Kadhaa

 

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

60-Kitabu Chake (Qur-aan) Kimepewa Majina Na Sifa Kadhaa

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Al-Qur-aan aliyoteremshiwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ina Majina na Sifa kadhaa. Miongoni mwayo ni Uhai, Burhani (dalili za wazi) na Nuru. Majina na Sifa hizo Amezitaja Allaah (سبحانه وتعالى) katika Qur-aan kwenye Aayah mbali mbali; mfano wa Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى) ni: 

 

يَا أَهْلَ الْكِتَابِ قَدْ جَاءَكُمْ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمْ كَثِيرًا مِّمَّا كُنتُمْ تُخْفُونَ مِنَ الْكِتَابِ وَيَعْفُو عَن كَثِيرٍ ۚ قَدْ جَاءَكُم مِّنَ اللَّـهِ نُورٌ وَكِتَابٌ مُّبِينٌ ﴿١٥﴾

Enyi Ahlal-Kitaab! Hakika amekwishakujieni Rasuli Wetu anayekubainishieni mengi katika yale mliyokuwa mkiyaficha katika Kitabu, na anasamehe mengi. Kwa yakini imekufikieni kutoka kwa Allaah Nuru na Kitabu kinachobainisha. [Al-Maaidah: 15]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَكُم بُرْهَانٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَأَنزَلْنَا إِلَيْكُمْ نُورًا مُّبِينًا ﴿١٧٤﴾

Enyi watu!  Kwa yakini imekujieni burhani kutoka kwa Rabb wenu na Tumekuteremshieni Nuru bayana.  [An-Nisaa: 174]

 

Na pia Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَالنُّورِ الَّذِي أَنزَلْنَا ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ﴿٨﴾

Basi muaminini Allaah na Rasuli Wake na Nuru (Qur-aan) Tuliyoiteremsha, na Allaah kwa yale myatendayo ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [At-Taghaabun: 8]

 

 

Na kuhusu Uhai Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

وَكَذَٰلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ رُوحًا مِّنْ أَمْرِنَا ۚ مَا كُنتَ تَدْرِي مَا الْكِتَابُ وَلَا الْإِيمَانُ وَلَـٰكِن جَعَلْنَاهُ نُورًا نَّهْدِي بِهِ مَن نَّشَاءُ مِنْ عِبَادِنَا ۚ وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٥٢﴾ صِرَاطِ اللَّـهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ أَلَا إِلَى اللَّـهِ تَصِيرُ الْأُمُورُ﴿٥٣﴾

Na hivyo ndivyo Tulivyokuletea Ruwh (Qur-aan) kutoka amri Yetu. Hukuwa uajua nini Kitabu wala iymaan, lakini Tumeifanya ni Nuru, Tunaongoa kwayo Tumtakaye miongoni mwa waja Wetu. Na hakika wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) bila shaka unaongoza kuelekea njia iliyonyooka. Njia ya Allaah Ambaye ni Vyake Pekee vyote vilivyomo mbinguni na vyote vilivyomo ardhini. Tanabahi! Kwa Allaah Pekee yanaishia mambo yote. [Ash-Shuwraa: 52-53]

 

 

Baadhi Ya Majina Na Sifa Za Qur-aan:

 

 

Al-Kitaab

الكتاب

Al-Furqaan

الفرقان

An-Nuwr

النور

Ar-Ruwh

الروح

Al-Hadiyth

الحديث

Al-Burhaan

البرهان

Ar-Rahmah

الرحمة

At-Tanziyl

التنزيل

Adh-Dhikr

الذّكر

Al-Kalaam

الكلام

Al-Maw’idhwah

الموعظة

Al-Haadiy

الهادي

Al-Mubaarak

المبارك

Al-Haqq

الحق

Al-Bayaan

البيان

Al-Muniyr

المنير

Ash-Shifaa

الشفاء

Al-‘Adhwiym

العظيم

Al-Kariym

الكريم

Al-Majiyd

المجيد

Al-‘Aziyz

العزيز

Al-Bashiyr

البشير

Al-Muhaymin

المهيمن

An-Ni’mah

النعمة

Al-Qaswasw

القصص

As-Siraaj

السراج

Al-Habl

الحبل

Al-Hukm

الحكم

At-Tibyaan

التبيان

An-Nadhiyr

النذير

Al-Hakiym

الحكيم

Adh-Dhikraa

الذكرى

Al-Miyzaan

الميزان

At-Tadhkirah

التذكرة

Al-Yaqiyn

اليقين

Ahsanul-Hadiyth

احسن الحديث

Al-Mathaaniy

المثاني

Al-Kitaab Al-Mutashaabihah

الكتاب المتشابه

Al-Qayyim

القيّم

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share

61-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Hukmu Zake Za Shariy’ah Ni Sawa Na Hukmu Za Qur-aan

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

61-Hukmu Zake Za Shariy’ah Ni Sawa Na Hukmu Za Qur-aan

 

Alhidaaya.com

 

 

Hukmu za Shariy’ah anazotoa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ni sawa na hukmu za Qur-aan kwa sababu Allaah (سبحانه وتعالى) Amemteremshia Qur-aan kisha Akamtaka yeye Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) awabainishie watu ili Qur-aan na hukmu zake zifahamike kwa watu. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ﴿٤٤﴾

 (Tumewatuma) Kwa hoja bayana na vitabu. Na Tumekuteremshia Ukumbusho (Qur-aan) ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao huenda wakapata kutafakari. [An-Nahl: 44]

 

Na Allaah (سبحانه وتعالى) Akamjaalia kumpa  mfano wa Qur-aan, kisha  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  akatahadharisha watu wasije kudai kuwa Qur-aan inawatosheleza kama wanavyodai kundi potofu linalojulikana kwa Qur-aaniyyuwn wanaoamini Qur-aan lakini wanapinga Ahaadiyth za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

 

((أَلَا إِنِّي أُوتِيتُ الْقُرْآنَ وَمِثْلَهُ، أَلَا يُوشِكُ رَجُلٌ يَنْثَنِي شَبْعَانًا عَلَى أَرِيكَتِهِ يَقُولُ: "عَلَيْكُمْ بِالْقُرْآنِ فَمَا وَجَدْتُمْ فِيهِ مِنْ حَلَال فَأَحِلُّوهُ وَمَا وَجَدْتُمْ فِيهِمِنْ حَرَامٍ فَحَرِّمُوهُ... ((رواه أبو داود والترمذي والحاكم وصححه وأحمد بسند صحيح

“Tanabahi! Hakika nimepewa Qur-aan na inayofanana nayo (Sunnah) Tanabahi! Utafika wakati mtu aliyeshiba mno ataegemea kwenye kochi na kusema: “Shikamaneni na Qur-aan, mtakayokuta humo ya halaal halalisheni, na mtakayokuta ya haraam haramisheni.” [Imepokewa na Abu Daawuwd, na At-Tirmidhiy, na Al-Haakim na ameisahihisha Ahmad kwa isnaad Swahiyh].

 

Na akasema pia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth:

 

عَنْ أَبي هريرةَ رضي الله عنه: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((كُلُّ أُمَّتِي يَدخُلُونَ الجَنَّةَ إلا مَنْ أبَى)). قيلَ: وَمَنْ يَأبَى يَا رَسُول الله؟ قَالَ: ((مَنْ أَطَاعَنِي دَخَلَ الجَنَّةَ، وَمَنْ عَصَانِي فَقَدْ أبَى)). رواه البخاري

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amesimulia: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: “Ummah wangu wote wataingia Jannah isipokuwa atakayekataa.” Akaulizwa: Ni yupi atakayekataa Ee Rasuli wa Allaah? Akajibu: “Atakayenitii mimi ataingia Jannah, na atakayeniasi basi amekataa.” [Al-Bukhaariy]

 

Na kumtii kwake amri na hukmu zake ni sawa na kumtii Allaah (سبحانه وتعالى) kama Anavyoamrisha Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَالرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿١٣٢﴾

Na mtiini Allaah na Rasuli mpate kurehemewa. [Aal-‘Imraan: 132]

 

Na katika Hadiyth:

 

 

عَنْ أبي هُرَيْرة رضى الله عنه  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ مَنْ أَطَاعَنِي فَقَدْ أَطَاعَ اللَّهَ، وَمَنْ عَصَانِي فَقَدْ عَصَى اللَّهَ، وَمَنْ أَطَاعَ أَمِيرِي فَقَدْ أَطَاعَنِي، وَمَنْ عَصَى أَمِيرِي فَقَدْ عَصَانِي ‏"‏‏.‏

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)  amehadithia kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayenitii basi atakuwa amemtii Allaah, na atakayeniasi atakuwa amemuasi Allaah, na atakayemtii Amiri wangu (kiongozi niliyemteua), atakuwa amenitii mimi na atakayemuasi atakuwa ameniasi mimi.” [Al-Bukhaariy, Muslim, An-Nasaaiy, Ibn Maajah]

  

Na Aayah nyenginezo kadhaa zinazothibitisha kuwa inapasa kumtii Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kila alichokuja nacho na kuwaamrisha Waumini, na kwamba ana haki ya kutoa hukmu ikawatosheleza Waislamu. Miongoni mwa Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى) ni zifuatazo:

 

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا﴿٦٥﴾

“Basi Naapa kwa Rabb wako, hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni mwamuzi katika yale wanayozozana baina yao, kisha wasipate katika nyoyo zao karaha katika yale uliyohukumu na wajisalimishe, kwa kujisalimisha kikamilifu.” [An-Nisaa: 65]

 

 

Na pia,

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا ﴿٥٩﴾

Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Rasuli na wenye madaraka katika nyinyi. Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Rasuli mkiwa mnamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri zaidi. [An-Nisaa: 59] 

 

 

Na pia,

 وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ

Na lolote analokupeni Rasuli ((صلى الله عليه وآله وسلم  basi lichukueni, na analokukatazeni, basi acheni. Na mcheni Allaah. [Al-Hashr: 7]

 

Na pia,

 

وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ ۗ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا ﴿٣٦﴾

Na haiwi kwa Muumini mwanamume na wala kwa Muumini mwanamke, Anapohukumu Allaah na Rasuli Wake jambo lolote, iwe wana hiari katika jambo lao.  Na anayemuasi Allaah na Rasuli Wake, basi kwa yakini amepotoka upotofu bayana. [Al-Ahzaab: 36]

 

 

Na kwa kuwa ayasemayo ni Wahyi kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

مَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣﴾ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ﴿٤﴾

Na wala hatamki kwa hawaa. Hayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa. [An-Najm: 3-4]

 

 

 

 

Share

62-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ametumwa Kuondosha Yaliyokuwa Na Mashaka Na Magumu Kwa Watu

 

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

62-Ametumwa Kuondosha Yaliyokuwa Na Mashaka Na Magumu Kwa Watu

 

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الرَّسُولَ النَّبِيَّ الْأُمِّيَّ الَّذِي يَجِدُونَهُ مَكْتُوبًا عِندَهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ يَأْمُرُهُم بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَاهُمْ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَائِثَ وَيَضَعُ عَنْهُمْ إِصْرَهُمْ وَالْأَغْلَالَ الَّتِي كَانَتْ عَلَيْهِمْ ۚ فَالَّذِينَ آمَنُوا بِهِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُوا النُّورَ الَّذِي أُنزِلَ مَعَهُ ۙ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿١٥٧﴾

Wale wanomfuata Rasuli; Nabiy asiyejua kusoma wala kuandika ambaye wanamkuta ameandikwa kwao katika Tawraat na Injiyl, anawaamrisha mema na anawakataza munkari, na anawahalalishia vizuri na anawaharamishia maovu, na anawaondoshea mizigo yao na minyororo iliyokuwa juu yao. Basi wale waliomwamini na wakamtukuza, na wakamnusuru na wakafuata nuru (Qur-aan) ambayo imeteremshwa pamoja naye; hao ndio wenye kufaulu.  [Al-A’raaf: 157]

 

Imaam Ibn Kathiyr ameeleza katika Tafsiyr yake:

Kuhusu Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

وَيَضَعُ عَنْهُمْ إِصْرَهُمْ وَالْأَغْلَالَ الَّتِي كَانَتْ عَلَيْهِمْ ۚ  

Na anawaondoshea mizigo yao na minyororo iliyokuwa juu yao.

 

Maana yake: Yeye Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) amewasahilishia watu kwa kuwandoshea yaliyo na taklifu.  Na minyororo iliyokuwa juu yao ni kwamba Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) amekuja kwa upole, ulaini na Dini nyepesi kama ilivyotajwa katika Hadiyth kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:

أُرْسِلْتُ بِحَنِيفِيَّةٍ سَمْحَةٍ

 

Nimetumwa kwa Dini Ya Haniyfah (kuelemea haki tu) na (Dini) ya sahali ya uvumilivu.  [Musnad Ahmad na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Asw-Swahiyhah)

 

Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipowatuma Yemen amiri wawili Mu’aadh bin Jabal na Abu Muwsaa Al-Ash’ariyy  (رضي الله عنهما) aliwausia:

يَسِّرَا وَلَا تُعَسِّرَا وَبَشِّرَا وَلَا تُنَفِّرَا وَتَطَاوَعَا وَلَا تَخْتَلِفَا

 

Rahisisheni mambo kwa watu (kuhusu mambo ya Dini) wala msifanye magumu na toeni habari njema na msiwakimbize, na mtiiane (msikizane) wala msikhitilafiane.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Abu Barzah Al-Aslamiy Swahaba wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Niliambatana na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) nikaona jinsi gani alivyokuwa na usahali wa mambo. Ummah zilokuwa kabla yetu walifanyiwa mambo mazito katika Shariy’ah zao lakini Allaah Amefanya Shariy’ay ya jumuisho na sahali kwa Ummah huu, kama ilivyo kauli ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

إِنَّ اللَّهَ تَجَاوَزَ لأُمَّتِي عَمَّا وَسْوَسَتْ أَوْ حَدَّثَتْ بِهِ أَنْفُسَهَا، مَا لَمْ تَعْمَلْ بِهِ أَوْ تَكَلَّمْ ‏

“Hakika Allaah Amesamehe Ummah wangu (zile amali mbaya) ambazo nafsi zao huwanong’oneza au kupendekeza maadamu hawatatenda au kuzungumza.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Na pia amesema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

 رُفِع عَنْ أُمَّتِي اَلْخَطَأَ، وَالنِّسْيَانَ، وَمَا اسْتُكْرِهُوا عَلَيْهِ  رَوَاهُ اِبْنُ مَاجَهْ   

Umma wangu umeondoshewa kukosea, kusahau na walilolazimishwa.”  [Imetolewa na Ibn Maajah]  

 

 

Share

63-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Allaah (سبحانه وتعالى) Amemfunulia Wahyi Kwa Aina Zaidi Ya Moja

 

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

63-Allaah (سبحانه وتعالى) Amemfunulia Wahyi Kwa Aina Zaidi Ya Moja

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَمَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُكَلِّمَهُ اللَّـهُ إِلَّا وَحْيًا أَوْ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ أَوْ يُرْسِلَ رَسُولًا فَيُوحِيَ بِإِذْنِهِ مَا يَشَاءُ ۚ إِنَّهُ عَلِيٌّ حَكِيمٌ﴿٥١﴾

Na wala haikuwa kwa mtu yeyote kwamba Allaah Amsemeze isipokuwa kwa Wahy au kutoka nyuma ya kizuizi, au Hutuma Mjumbe, kisha Anamfunulia Wahy Ayatakayo kwa idhini Yake; hakika Yeye ni Mwenye ‘Uluwa, Ametukuka,  Mwenye hikmah wa yote. [Ash-Shuwraa: 51]

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) pekee ambaye Wahyi wake kutoka kwa Allaah (عز وجل) ulikuwa ni wa aina kadhaa miongoni mwazo ni aina zifuatazo:

 

 

Aina Ya Kwanza Na Ya Pili: -Kama kwa sauti ya kengele, au kupitia Jibriyl (عليه السلام) kwa umbile la mtu:  

 

 

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يُوسُفَ، قَالَ أَخْبَرَنَا مَالِكٌ، عَنْ هِشَامِ بْنِ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ الْمُؤْمِنِينَ ـ رضى الله عنهاأَنَّ الْحَارِثَ بْنَ هِشَامٍ ـ رضى الله عنه سَأَلَ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ يَا رَسُولَ اللَّهِ كَيْفَ يَأْتِيكَ الْوَحْىُ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ أَحْيَانًا يَأْتِينِي مِثْلَ صَلْصَلَةِ الْجَرَسِ ـ وَهُوَ أَشَدُّهُ عَلَىَّ ـ فَيُفْصَمُ عَنِّي وَقَدْ وَعَيْتُ عَنْهُ مَا قَالَ، وَأَحْيَانًا يَتَمَثَّلُ لِيَ الْمَلَكُ رَجُلاً فَيُكَلِّمُنِي فَأَعِي مَا يَقُولُ ‏" قَالَتْ عَائِشَةُ رضى الله عنها وَلَقَدْ رَأَيْتُهُ يَنْزِلُ عَلَيْهِ الْوَحْىُ فِي الْيَوْمِ الشَّدِيدِ الْبَرْدِ، فَيَفْصِمُ عَنْهُ وَإِنَّ جَبِينَهُ لَيَتَفَصَّدُ عَرَقًا‏.‏

 

Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها) Al-Haarith bin Hishaam alimuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) “Ee Rasuli wa Allah! Wahyi unakujia vipi?” Rasuli wa Allaah akajibu:  “Wakati fulani unanijia kama sauti ya kengele, aina hii ya Wahyi ni ngumu zaidi kwangu kuliko zote na kisha hali hiyo hunipitia baada ya kuwa nimeshafahamu kile nilichofunuliwa. Wakati mwingine Malaika huja katika umbile la mtu, hunizungumzisha na kuzingatia anayosema.” ‘Aaishah amesema: Kwa hakika nilimwona (Rasuli wa Allaah صلى الله عليه وآله وسلم) akiletewa Wahyi siku ya baridi kali na akaona jasho likimdondoka usoni (baada ya kumalizika Wahyi). [Al-Bukhaariy]

 

 

Aina Ya Tatu: Allaah (عز وجل) kumsemesha moja kwa moja nyuma ya pazia mfano vile alipoongea naye pindi Alipompandisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) mpaka mbingu ya saba katika safari ya muujiza ya Al-Israa Wal-Mi’raaj akamfaridhisha na Ummah wake Swalaah tano.

 

 

Pia kama ilivyoelezewa katika Hadiyth ifuatayo:

 

 عنْ أَبِي قِلاَبَةَ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ أَتَانِي اللَّيْلَةَ رَبِّي تَبَارَكَ وَتَعَالَى فِي أَحْسَنِ صُورَةٍ قَالَ أَحْسَبُهُ قَالَ فِي الْمَنَامِ فَقَالَ يَا مُحَمَّدُ هَلْ تَدْرِي فِيمَ يَخْتَصِمُ الْمَلأُ الأَعْلَى قَالَ قُلْتُ لاَ ‏.‏ قَالَ فَوَضَعَ يَدَهُ بَيْنَ كَتِفَىَّ حَتَّى وَجَدْتُ بَرْدَهَا بَيْنَ ثَدْيَىَّ أَوْ قَالَ فِي نَحْرِي فَعَلِمْتُ مَا فِي السَّمَوَاتِ وَمَا فِي الأَرْضِ قَالَ يَا مُحَمَّدُ هَلْ تَدْرِي فِيمَ يَخْتَصِمُ الْمَلأُ الأَعْلَى قُلْتُ نَعَمْ ‏.‏ قَالَ فِي الْكَفَّارَاتِ ‏.‏ وَالْكَفَّارَاتُ الْمُكْثُ فِي الْمَسَاجِدِ بَعْدَ الصَّلَوَاتِ وَالْمَشْىُ عَلَى الأَقْدَامِ إِلَى الْجَمَاعَاتِ وَإِسْبَاغُ الْوُضُوءِ فِي الْمَكَارِهِ وَمَنْ فَعَلَ ذَلِكَ عَاشَ بِخَيْرٍ وَمَاتَ بِخَيْرٍ وَكَانَ مِنْ خَطِيئَتِهِ كَيَوْمَ وَلَدَتْهُ أُمُّهُ وَقَالَ يَا مُحَمَّدُ إِذَا صَلَّيْتَ فَقُلِ اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ فِعْلَ الْخَيْرَاتِ وَتَرْكَ الْمُنْكَرَاتِ وَحُبَّ الْمَسَاكِينِ وَإِذَا أَرَدْتَ بِعِبَادِكَ فِتْنَةً فَاقْبِضْنِي إِلَيْكَ غَيْرَ مَفْتُونٍ قَالَ وَالدَّرَجَاتُ إِفْشَاءُ السَّلاَمِ وَإِطْعَامُ الطَّعَامِ وَالصَّلاَةُ بِاللَّيْلِ وَالنَّاسُ نِيَامٌ ‏"‏ ‏.‏

 

Kutoka kwa Abu Qilaabah kutoka kwa Ibn ‘Abbaas amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Alinijia Rabb wangu (تبارك وتعالى) usiku mmoja kwa Sura nzuri kabisa.”  (Mmoja wa msimuliaji) alisema:  Nadhani alisema ilikuwa katika ndoto. “Kisha Akasema: Ee Muhammad!  Je, unajua kundi lilotukuka kabisa linajishughulisha na nini?”  Akasema: “Nikasema hapana! Akaweka Mkono Wake baina ya mabega yangu hadi nikahisi kupoza kwa kwake kwa ubaridi kati ya kifua changu.”  Au alisema: “Kwenye koo langu. Kwa hivyo nilijua yaliyomo mbinguni na yaliyomo duniani. Akasema: Ee Muhammad! Je, unajua kundi lilotukuka kabisa linajishughulisha na nini?  Nikasema: Naam, katika Mukaffaraat (‘amali zinazofuta madhambi) na ‘amali zinazofuta madhambi ni kukaa Msikitini baada ya Swalaah na kutembea kwa miguu kuelekea Swalaah za Jamaa na Isbaagh Al-Wudhwuu (kutawadha kikamilifu pamoja na kuwepo uzito na ugumu), na atakayefanya hivyo ataishi kwa kheri na atakufa kwa kheri, madhambi yake yatakuwa kama siku aliyomzaa mama yake (hana madhambi).  Akasema (pia): Ee Muhammad, utakaposwali sema:

 

 اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ فِعْلَ الْخَيْرَاتِ، وَتَرْكَ الْمُنْكَرَاتِ، وَحُبَّ الْمَسَاكِينِ  وَإِذَا أَرَدْتَ  بِعِبَادِكَ فِتْنَةَ  فَاقْبِضْنِي إِلَيْكَ غَيْرَ مَفْتُونٍ

 

Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba kufanya mema yote, kuacha munkari zote, na kuwapenda masikini, na Unapotaka kuwatia waja wako majaribuni (fitnah), basi Nifishe mimi bila kujaribiwa.   

 

Akasema: Na kupandishwa daraja ni kueneza Salaam na kulisha chakula na Swalaah za usiku watu wanpokuwa wamelala.” [At-Tirmidhiy]

 

 

 

Aina Ya Nne: Ndoto Ya Kweli

 

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ الْمُؤْمِنِينَ، أَنَّهَا قَالَتْ أَوَّلُ مَا بُدِئَ بِهِ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم مِنَ الْوَحْىِ الرُّؤْيَا الصَّالِحَةُ فِي النَّوْمِ، فَكَانَ لاَ يَرَى رُؤْيَا إِلاَّ جَاءَتْ مِثْلَ فَلَقِ الصُّبْحِ، ثُمَّ حُبِّبَ إِلَيْهِ الْخَلاَءُ

 

Amesimulia ‘Aaishah (Mama wa Waumini): (رضي الله عنها):  Wahyi kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ulianza kwa ndoto njema usingizini na alikuwa haoni ndoto isipokuwa ni kweli kama ulivyo mwanga wa mchana, na alipendezeshwa kujitenga. [Al-Bukhaariy]

 

 

Aina Ya Tano: Kumjia Jibriyl (عليه السلام) kwa umbo lake. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَلَقَدْ رَآهُ بِالْأُفُقِ الْمُبِينِ ﴿٢٣﴾

Na kwa yakini alimuona (Jibriyl) katika upeo wa macho ulio bayana. [At-Takwiyr: 23]

 

Na pia Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَلَقَدْ رَآهُ نَزْلَةً أُخْرَىٰ ﴿١٣﴾ عِندَ سِدْرَةِ الْمُنتَهَىٰ ﴿١٤﴾ عِندَهَا جَنَّةُ الْمَأْوَىٰ ﴿١٥﴾

 

Na kwa yakini amemuona (Jibriyl) katika uteremko mwingine. Kwenye mkunazi wa mpaka wa mwisho kabisa. Karibu yake kuna Jannah ya Al-Ma-waa. [An-Najm: 13 – 15]

 

Na kuhusu Kuali hizo za Allaah (سبحانه وتعالى), Aaishah (رضي الله عنها)  alisema katika Hadiyth ndefu:

 

 

  أَنَا أَوَّلُ هَذِهِ الْأُمَّةِ سَأَلَ عَنْ ذَلِكَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ : إِنَّمَا هُوَ جِبْرِيلُ لَمْ أَرَهُ عَلَى صُورَتِهِ الَّتِي خُلِقَ عَلَيْهَا غَيْرَ هَاتَيْنِ الْمَرَّتَيْنِ رَأَيْتُهُ مُنْهَبِطًا مِنْ السَّمَاءِ سَادًّا عِظَمُ خَلْقِهِ مَا بَيْنَ السَّمَاءِ إِلَى الْأَرْضِ

 

Mimi ndiye wa kwanza wa Ummah huyu ambaye alimuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu hilo (kumuona Jibriyl), akasema: “Hakika yeye ni Jibriyl. Sijawahi kumwona katika umbo lake la asili ambalo aliumbwa nalo isipokuwa kwa nyakati hizo mbili (zinazokusudiwa katika  Aayah hizo); Nilimwona akishuka kutoka mbinguni na kujaza (angani) kutoka mbinguni kuja duniani kwa umbo lake kubwa mno la mwili.” [Muslim]  

 

 

 

 

 

Share

64-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Majini Wameitika Risala Yake Na Wakalingania Majini Wenzao

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

64-Majini Wameitika Risala Yake Na Wakalingania Majini Wenzao

 

Alhidaaya.com

 

 

Miongoni mwa fadhila zake Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ni kwamba hata Majini waliposikiliza Qur-aan waliisifu Qur-aan kuwa ni ya ajabu na wakaiamini. Anasema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):

 

قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا﴿١﴾ يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ ۖ وَلَن نُّشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا﴿٢﴾

 

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Nimefunuliwa Wahy kwamba kundi miongoni mwa majini lilisikiliza; wakasema: ‘Hakika sisi tumeisikia Qur-aan ya ajabu. Inaongoza kwenye uongofu, basi tukaiamini, na wala hatutomshirikisha Rabb   wetu na yeyote. [Al-Jinn: 1 – 2]

 

Bali wakawalingania majini wenzao kwa yafuatayo baada ya wao kwanza kuisikiliza Qur-aan kwa makini:

 

  • Wanyamaze na wasikilize kwa makini.

 

  • Wakasadikisha yaliyokuja kabla ya Qur-aan.

 

  • Wakawalingania waisadiki Qur-aan kwa kuwa inaongoza katika haki (Uislaam) na katika njia iliyonyooka.

 

  • Wamwitikie Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na waitikie wito wa Allaah.

 

  • Waiamini Qur-aan na wamwamini Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na wamwamini Allaah (عَزَّ وَجَلَّ).  

 

  • Kisha wakawahamasisha kuwa pindi wakifanya hivyo wataghufuriwa madhambi yao na wataepushwa na adhabu.

 

  • Kisha wakawaonywa majini wenzao kwamba pindi wasipoitikia wito huo wa Allaah na Rasuli Wake (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), basi hawataweza kuepukana na adhabu ya Allaah (عَزَّ وَجَلَّ) na watabakia kuwa katika upotofu wa dhahiri.

 

Kauli za Allaah (عَزَّ وَجَلَّ):

 

 

وَإِذْ صَرَفْنَا إِلَيْكَ نَفَرًا مِّنَ الْجِنِّ يَسْتَمِعُونَ الْقُرْآنَ فَلَمَّا حَضَرُوهُ قَالُوا أَنصِتُوا ۖ فَلَمَّا قُضِيَ وَلَّوْا إِلَىٰ قَوْمِهِم مُّنذِرِينَ﴿٢٩﴾ قَالُوا يَا قَوْمَنَا إِنَّا سَمِعْنَا كِتَابًا أُنزِلَ مِن بَعْدِ مُوسَىٰ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ وَإِلَىٰ طَرِيقٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٣٠﴾ يَا قَوْمَنَا أَجِيبُوا دَاعِيَ اللَّـهِ وَآمِنُوا بِهِ يَغْفِرْ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمْ وَيُجِرْكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٣١﴾ وَمَن لَّا يُجِبْ دَاعِيَ اللَّـهِ فَلَيْسَ بِمُعْجِزٍ فِي الْأَرْضِ وَلَيْسَ لَهُ مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءُ ۚأُولَـٰئِكَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ﴿٣٢﴾

Na pale Tulipowaelekeza kwako (ee Muhammadصلى الله عليه وآله وسلم) ) kundi miongoni mwa majini wakisikiliza kwa makini Qur-aan; walipoihudhuria, walisema: Bakieni kimya msikilize! Ilipomalizika; waligeuka kurudi kwa kaumu yao wakiwa wenye kuonya. Wakasema: Enyi kaumu yetu! Hakika sisi tumesikia Kitabu kimeteremshwa baada ya Muwsaa, kinachosadikisha yaliyo kabla yake, kinaongoza kwenye haki na kuelekea njia iliyonyooka. Enyi kaumu yetu! Mwitikieni mlinganiaji wa Allaah, na mwaminini!  (Allaah) Atakughufurieni madhambi yenu, na Atakukingeni na adhabu iumizayo. Na yeyote asiyemuitikia mlinganiaji wa Allaah, basi hawezi kushinda kukwepa katika ardhi na hatokuwa na walinzi badala ya Allaah.  Hao wamo katika upotofu bayana. [Al-Ahqaaf (46): 29 – 32]

 

 

Share