Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Kwa Ujumla

 

 

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Kwa Ujumla

 

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

 

Share

00-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Na Hakika Wewe Uko Juu Ya Kiwango Adhimu Cha Tabia Njema

 

 

 Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

00-Na Hakika Wewe Uko Juu Ya Kiwango Adhimu Cha Tabia Njema

 

www.alhidaaya.com

 

 

Hakuna sentensi itakayoweza kuelezea mazuri aliyokuja nayo Nabiy wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam); utukufu wake,  daraja yake, elimu na Risala aliyokuja nao pamoja na upana wa hikma zake,  na sifa na akhlaaq (tabia) zake.  

 

Jina lake pekee linatosha kuelezea tabia zake kwani Muhammad maana yake ni "Mwenye kusifiwa." Kwa hiyo bila shaka anamiliki sifa na tabia njema zilizokamilika ambazo hakuna mtu yeyote mwingine aliyemiliki;  ni cheo cha daraja ya juu kabisa hakuna atakayeweza kufikia!  Na si mwengine aliyemsifia kiumbe huyu bali ni Mwenyewe Allaah ('Azza wa Jalla) Anayesema:

 وَإِنَّكَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِيمٍ﴿٤﴾

Na hakika wewe uko juu ya kiwango adhimu cha tabia njema. [Al-Qalam: 4]

 

Swahaba Sa'ad bin Hishaam (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alipomuuliza Mama wa Waumini 'Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa)  kuhusu tabia ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alijibu:

كان خلقه القرآن. ألست تقرأ القرآن (( وَإِنَّكَ لَعَلى خُلُقٍ عَظِيمٍ )) أبو داود والنسائي   

Tabia yake ilikuwa ni Qur-aan, kwani husomi katika Qur-aan )) Na hakika wewe uko juu ya kiwango adhimu cha tabia njema. (( [Abu Daawuwd na An-Nasaaiy]

 

Naye Nabiy (Swalla Allaahu 'alayh wa aalihi wa sallam) akasema:

  ((إِنَّمَا بُعِثْتُ لِأُتَمِّمَ صَالِحَ الأَخْلاقِ‏))

 ((Hakika nimetumwa ili nikamilishe khulqa (tabia) njema)) [Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ameipokea Imaam Ahmad na ameisahihisha Al-Albaaniy Swahiyh Al-Jaami’ (2349), Swahiyh Al-Adab Al-Mufrad (207)]

 

Zitakazofuatia ni baadhi ya sifa na akhlaaq ambazo zinazompelekea Nabiy wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuchukua nafasi adhimu na ya pekee katika ulimwengu huu, pamoja na kuacha athari zake ambazo zimewasisimua na kuwahamasisha watu wengi mno mpaka makafiri wakaingia Uislamu kwazo, na  hazitoweza kubadilika wala kufutika hadi Siku ya mwisho; Swalla Allaahu 'alayh wa aalihi wa sallam.

 

Wabillaahi At-Tawfiyq

 

 

Share

01-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Alijulikana Kabla Ya Unabii Kuwa Ni Mkweli Na Mwaminifu

 

 Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

01-Alijulikana Kabla Ya Unabii Kuwa Ni Mkweli Na Mwaminifu

 

www.alhidaaya.com

 

 

Khulqah yake ya Asw-Swaadiq (mkweli) na Al-Amiyn (Mwaminifu) ilijulikana kabla ya kupewa Unabii kutokana na ukweli wake na uaminifu wake hata akapewa jina la “Asw-Swaadiqul-Amiyn” (Mkweli Mwaminifu):

 

1-Maquraysh wa Makkah walipokuwa wakiijenga upya Al-Ka’bah baada ya kutokea mafuriko makubwa yaliyosababisha maji kuingia ndani ya Msikiti na kubomoka, na pindi walipomaliza kujenga, wakataka kuirudisha Al-Hajar Al-Aswad (Jiwe jeusi) katika kona ya Ka’bah. Makabila manne ya ki-Quraysh  yalikaribia kupigana vita vikubwa kwa kuzozana nani kati yao anayepaswa kuliweka jiwe hilo katika kona yake. Mvutano  huo ukaendelea takriban masiku manne au matano.

Abuu Umayyah bin Mughiyrah Al-Makhzuwmiy ambaye alikuwa mtu mzima wao, akashauri kuwa liwekwe na mtu wa kwanza atakayeingia katika lango la Msikiti, na wote wakaridhika na rai hiyo. Allaah ('Azza wa Jalla) Akajaalia kuwa ni Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aingie na hapo wote wakapiga ukulele: "Huyu Mwaminifu! Sote tumeridhika naye huyu Muhammad."

 

Naye Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa hikma aliyojaaliwa na Allaah ('Azza wa Jalla) akaamrisha kiletwe kitambaa (kikubwa) kisha iwekwe Al-Hajar Al-Aswad katikati kisha akawataka viongozi wa makabila yote; kila mmoja wao akamate kona moja ya kitambaa hicho kisha wanyanyue kwa pamoja, na walipofikia mahali pa kuliweka, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akainyanyua Al-Hajar Al-Aswad kwa mikono yake miwili na kuiweka katika kona ya Al-Ka’bah. Mzozo ukamalizika na watu wakaridhika. [Ar-Rahiyq Al-Makhtuwm, Muhammad Rahmatul-Lil-’Aalamiyn]

 

 

2-Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Alipomteremshia amri hii:

 

وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ ﴿٢١٤﴾

Na onya (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) jamaa zako wa karibu. [Ash-Shu’araa: 214]

 

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipapanda juu ya jabali Swafaa akawaita watu wake na kuwaambia: "Enyi Maquraysh (na riwaayah nyingine enyi Banuu Manaaf, Enyi Banuu fulani na fulani). Je, ikiwa nitawaambieni kuwa wapanda farasi wapo nyuma ya jabali hili wakijitayarisha kukushambulieni, mtanisadiki?" Wote kwa pamoja wakamjibu:

"Bila shaka tutakusadiki, kwa sababu hatujapata kusikia kutoka kwako isipokuwa maneno ya kweli." Akasema: "Basi mimi ni mwonyaji kwenu juu ya adhabu kali iliyo mbele yenu. Okoeni nafsi zenu kutokana na moto…" [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo kwa riwaayah tofauti]

 

 

3-Kauli ya Abu Jahl:

 

“Wa-Allaahi mimi najua vilivyo kuwa yeye ni Mkweli….Tulikuwa tukimwita katika ujana  wake Asw-Swaadiq Al-Amiyn.” (Mkweli Mwaminifu). [Tafsiyr Al-Qurtwubiy]

 

 

4-Imepokelewa kutoka kwa Maswahaba mbali mbali wakihadithia Hadiyth za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakisema: “Amesema Asw-Swaadiq Al-Maswduwq” (mkweli aliyesadikishwa). Mfano ni Hadiyth ya ‘Abdullah bin Mas’uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu):

 

عن أبي عبْدِ الرَّحْمن عبدِ الله بنِ مسعودٍ رضي الله عنه قال: حدَّثَنا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم وهُوَ الصَّادقُ المَصْدوق: ((إنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ في بَطْنِ أُمِّه أرْبعينَ يوْماً نُطْفَةً، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذلك، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذلك، ثُمَّ يُرْسَلُ إليه المَلكُ فَيَنْفخُ فيه الرُّوحَ ويُؤمَرُ بأرْبَعِ كلماتٍ: بِكَتْبِ رِزْقِهِ وأَجَلِهِ وعَمَلِهِ وشَقيٌّ أو سَعيدٌ، فَوَاللهِ الَّذي لا إله غَيْرُهُ إنَّ أَحَدَكُمْ ليَعْمَلُ بعَمَلِ أهْلِ الجَنَّةِ حتى ما يكُونَ بَيْنَهُ وبَيْنَها إلا ذِرَاعٌ، فَيَسْبِقُ عَليْه الكِتابُ فَيَعْمَلُ بعَملِ أَهْلِ النَّارِ فَيَدْخُلُها. وإنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهل النَّارِ حتى ما يَكُونَ بَيْنَهُ وبَيْنَها إلا ذِرَاعٌ، فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الكتابُ، فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أهل الجنَّةِ فَيَدْخُلُها)) رواه البخاري ومسلم

 

Kutoka kwa Abuu 'Abdir-Rahmaan 'Abdillaah bin Mas‘uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: “Ametusimulia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ambaye ni mkweli mwenye kuaminiwa: “Hakika kila mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake siku arubaini akiwa ni mkusanyiko wa mbegu (za uzazi za mama na baba), kisha arubaini zifuatazo huwa ni donge la damu, kisha arubaini zijazo huwa pande la nyama, kisha Allaah Humtuma Malaika kwake na kumpulizia roho (yake). Na (Malaika huyo) anaamrishwa maneno manne; Kuandika rizki yake, ajali yake (umri atakaoishi duniani), amali zake, mtu muovu au mwema. Wa-Allaahi naapa kwa Yule Ambaye hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Yeye, hakika mmoja wenu huenda afanye ‘amali za watu wa Jannah hadi ikawa baina yake na Jannah ni dhiraa na kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya ‘amali ya watu wa motoni akaingia motoni. Na mmoja wenu hufanya ‘amali za watu wa motoni hadi ikawa baina yake na moto ni dhiraa na hapo kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya ‘amali ya watu wa Jannah akaingia Jannah)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Pia Hadiyth ya   Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) Al-Bukhaariy Kitaab Al-Fitan, na wengineo.

 

 

5-Allaah ('Azza wa Jalla) Mwenyewe Amethitibisha kuwa ni Asw-Swaadiq (mkweli) Anaposema:

 

وَالَّذِي جَاءَ بِالصِّدْقِ وَصَدَّقَ بِهِ ۙ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُتَّقُونَ﴿٣٣﴾

Na yule aliyekuja na ukweli na wakausadikisha - hao ndio wenye taqwa. [Az-Zumar: 33]

 

Amesema Mujaahid na Qataadah na wengineo kuhusu: “Na yule aliyekuja na ukweli “Huyo ni Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]  

 

 

Share

02-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Akijali Mno Umma Wake Na Akiwakhofia Adhabu

 

 

 

 Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

02-Akijali Mno Umma Wake Na Akiwakhofia Adhabu

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Nabiy wetu Muhammad   (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akijali mno Ummah wake huu wa Kiislamu, akikhofia na kujali Waumini wasipatwe na shari au  balaa au adhabu yoyote ile. Hadiyth ifuatayo ni dalili mojawapo ya kujali kwake kwa Ummah huu wa Kiislamu:

 

 

عنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم تَلاَ قَوْلَ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ فِي إِبْرَاهِيم: ((‏رَبِّ إِنَّهُنَّ أَضْلَلْنَ كَثِيرًا مِنَ النَّاسِ فَمَنْ تَبِعَنِي فَإِنَّهُ مِنِّي)) الآيَةَ‏.‏ وَقَالَ عِيسَى عَلَيْهِ السَّلاَمُ:((إِنْ تُعَذِّبْهُمْ فَإِنَّهُمْ عِبَادُكَ وَإِنْ تَغْفِرْ لَهُمْ فَإِنَّكَ أَنْتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ‏)) فَرَفَعَ يَدَيْهِ وَقَالَ" ((اللَّهُمَّ أُمَّتِي أُمَّتِي)) وَبَكَى فَقَالَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ: يَا جِبْرِيلُ اذْهَبْ إِلَى مُحَمَّدٍ وَرَبُّكَ أَعْلَمُ فَسَلْهُ مَا يُبْكِيكَ فَأَتَاهُ جِبْرِيلُ   عَلَيْهِ الصَّلاَةُ وَالسَّلاَمُ  فَسَأَلَهُ فَأَخْبَرَهُ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بِمَا قَالَ‏.‏ وَهُوَ أَعْلَمُ‏.‏ فَقَالَ اللَّهُ يَا جِبْرِيلُ اذْهَبْ إِلَى مُحَمَّدٍ فَقُلْ إِنَّا سَنُرْضِيكَ فِي أُمَّتِكَ وَلاَ نَسُوءُكَ.

 

 

Amesimulia ‘Abdullaah bin ‘Amru bin Al-‘Aasw (رضي الله عنه):  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisoma kauli ya Allaah (عزّ وجلّ) kuhusu Nabiy Ibraahiym:

 

رَبِّ إِنَّهُنَّ أَضْلَلْنَ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ ۖ فَمَن تَبِعَنِي فَإِنَّهُ مِنِّي ۖ  

Rabb wangu! Hakika hao (masanamu) wamepoteza watu wengi.  Basi atakayenifuata, huyo yuko nami. [Ibraahiym: 36]

 

Na amesema ‘Iysaa (عليه السلام):

 

إِن تُعَذِّبْهُمْ فَإِنَّهُمْ عِبَادُكَ ۖ وَإِن تَغْفِرْ لَهُمْ فَإِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١١٨﴾

Ukiwaadhibu, basi bila shaka hao ni Waja Wako, na Ukiwaghufuria basi hakika Wewe Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote [Al-Maaidah: 118]

 

Akanyanyua mikono yake akisema: “Ee Allaah! Ummah wangu! Ummah Wangu!  Akalia, kisha Allaah (عزّ وجلّ) Akasema: “Ee Jibriyl! Nenda kwa Muhammad, na Rabb wako Anajua zaidi, kisha muulize kitu kigani kinachomliza? Basi Jibriyl akamwendea (صلى الله عليه وآله وسلم) akamuuliza (sababu ya kulia kwake), na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamjulisha, na Allaah Anajua zaidi, Hapo Allaah Akasema: “Ee Jibriyl! Nenda kwa Muhammad na mwambie: Hakika Sisi Tutaridhia Ummah wako wala Hatutaudhika nawe.” [Muslim]

 

Imaam An-Nawawiy (رحمه الله) amesema katika Sharh Muslim: “Hadiyth hii imejumuisha aina za faida zikiwemo: Bainisho kamilifu la huruma zake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa Ummah wake, na kujali kutunza maslahi yao, na kutilia hima mambo yao. Na hii ni bishara adhimu kwa Ummah huu kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Ameuzidishia (Ummah) Sharaf (taadhima)  kutokana na ambayo Allaah (سبحانه وتعالى)  Amemuahidi Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم)  katika kauli Yake: “Tutaridhia Ummah wako wala Hatutaudhika nawe.”  Na hii ni Hadiyth itoayo matarajio makubwa kabisa kwa Ummah huu.

 

 

 

Share

03-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Alisisitiza Mno Umma Wake Kuhusu Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

03-Alisisitiza Mno Ummah Wake Kuhusu Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

www.alhidaaya.com

 

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesisitiza mno Husnul-Khuluq (tabia njema) katika Hadiyth nyingi, miongoni mwazo ni ambazo zinabashiria Al-Jannah (Pepo) na pia kuwa karibu naye huko Peponi:  

 

 

1-Aliye na Husnul-Khuluq ni kipenzi cha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na atakuwa karibu naye Jannah:

 

عن جابر رضي اللَّه عنه أَن رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال: (( إِن مِنْ أَحَبِّكُم إِليَّ ، وَأَقْرَبِكُمْ مِنِّي مَجلساً يَومَ القِيَامَةِ، أَحَاسِنَكُم أَخلاقا)) الترمذي حديث حسن

 

Imetoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu)  kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika walio vipenzi kwangu na watakaokuwa karibu na mimi siku ya Qiyaamah ni wale wenye tabia njema)) [At-Tirmidhiy – Hadiyth Hasan].

 

 

2-Taqwa na Husnul-Khulq ndio sababu kuu ya kumwingiza mtu Jannah:

 

عن أَبِي هُرَيْرَةَ‏:‏ سُئِلَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم‏:‏ مَا أَكْثَرُ مَا يُدْخِلُ الْجَنَّةَ‏؟‏ قَالَ‏:‏ ((تَقْوَى اللهِ، وَحُسْنُ الْخُلُقِ)) قَالَ‏:‏ وَمَا أَكْثَرُ مَا يُدْخِلُ النَّارَ‏؟‏ قَالَ‏:‏ ((الأَجْوَفَانِ‏:‏ الْفَمُ وَالْفَرْجُ‏.))

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa: “Jambo gani zaidi litakalokuwa ni sababu ya kumwingiza mtu Jannah?” Akasema: ((Taqwa (kumcha Allaah) na Husnul-Khuluq (tabia njema)). Na akulizwa: “Jambo gani zaidi litakalokuwa ni sababu ya kumwingiza mtu Motoni?” Akasema; ((Mdomo na sehemu za siri)) [Al-Adab Al-Mufrad, Swahiyh Ibn Maajah (3443)], Swahiyh At-At-Tirmidhiy (2004)]

 

 

3-Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amedhamini Jannah kwa anayeacha mabishano na kusema uongo na mwenye khulqa njema:

 

عَنْ أَبِي أُمَامَةَ البَاهِلي (رضي الله عنه) قَال: قَال رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((أَنَا زَعِيم بَيْت فِي رَبَض الْجَنَّة لِمَنْ تَرَكَ الْمِرَاء وَإِنْ كَانَ مُحِقًّا، وَبِبَيْتٍ فِي وَسَط الْجَنَّة لِمَنْ تَرَكَ الْكَذِب وَإِنْ كَانَ مَازِحًا، وَبِبَيْتٍ فِي أَعْلَى الْجَنَّة لِمَنْ حَسُنَ خُلُقه)) حديث صحيح رواه أبو داود بإسناد صحيح

Imepokelewa kutoka kwa Abu Umaamah Al-Baahiliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:  ((Mimi ni mdhamini wa nyumba ya kando ya Jannah kwa anayeacha mabishano [wenye shaka] hata kama ni mwenye haki, na ni mdhamini wa nyumba iliyo katikati ya Jannah kwa anayeacha uongo japo ni kwa mzaha, na mdhamini wa nyumba iliyo mahala pa juu zaidi ya Jannah kwa ambaye tabia yake ni njema)). [Hadiyth Swahiyh ameipokea Abu Daawuwd isnaad yake ni Swahiyh]

 

 

4-Husnul-Khuluq (tabia njema) inasababisha Miyzaan ya matendo kuwa nzito Siku ya Qiyaamah:

 

عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: (( مَا مِنْ شَىْءٍ أَثْقَلُ فِي الْمِيزَانِ مِنْ حُسْنِ الْخُلُقِ ‏))

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ad-Dardaai kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna kitakachokuwa kizito katika Miyzaan kama Husnul-Khuluq [tabia njema])) [Sunan Abiy Daawuwd, As-Silsilah Asw-Swahiyhah ((2/535), Swahiyh Al-Jaami’ 7=5721, Swahiyh Adab Al-Mufrad (204)]

 

 

Na pia:

 

عنْ أَنَسٍ قَالَ لَقِيَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَبَا ذَرٍّ فَقَالَ: ((يَا أَبَا ذَرٍّ أَلا أَدُلُّكَ عَلَى خَصْلَتَيْنِ هُمَا أَخَفُّ عَلَى الظَّهْرِ وَأَثْقَلُ فِي الْمِيزَانِ مِنْ غَيْرِهِمَا)) قَالَ:  بَلَى يَا رَسُولَ اللَّهِ . قَالَ: ((عَلَيْكَ بِحُسْنِ الْخُلُقِ وَطُولِ الصَّمْتِ فَوَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ مَا عَمِلَ الْخَلائِقُ عَمَلا أَحَبَّ إِلَى اللَّهِ مِنْهُمَا))

 

Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokutana na Abuu Dharr alisema: ((Ee Abuu Dharr; je, nikujulishe sifa mbili ambazo ni nyepesi mgongoni mwako na nzito katika kabisa katika Miyzaan kuliko nyinginezo?)) Akasema: “Ndio Ee Rasuli wa Allaah.” Akasema: ((Shikimana na Husnul-Khuluq (tabia njema) na ukae kimya mda mrefu (usiongee upuuzi), kwani Naapa kwa Ambaye nafsi ya Muhammad imo Mikononi Mwake, hakuna 'amali za viumbe Azipendazo Allaah kama hizo mbili)) [Al-Mu’jam Al-Awsatw (7287), At-Targhiyb wat-Tarhiyb ya Al-Mundiriy (3/355) kwa daraja ya Hadiyth Jayyid wasimulizi ni wenye kuaminika]

 

 

5-Husnul-Khuluq inazidisha umri wa mtu:

 

عن عائشة أم المومنينن رضي الله عنها عن النبي صلى الله عليه وسلم: ((...صِلةُ الرَّحِمِ وحُسنُ الخُلُقِ وحُسنُ الجِوارِ يَعمُرانِ الدِّيارَ، ويَزيدانِ في الأعمارِ))

Imepokelewa kutoka kwa Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kuunga undugu na Husnul-Khuluq (tabia njema) na kumfanyia wema jirani inaamirisha nyumba na inaongeza umri)) [Ahmad na ameisahihisha Al-Albaaniy katika As-Silsilah Asw-Swahiyhah (519), Swahiyh At-Targhiyb (2524)] 

 

 

6-Iymaan ya mtu haikamilikii ila kwa Husnul-Khuluq (tabia njema):

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((أَكْمَلُ الْمُؤْمِنِينَ إِيمَانًا أَحْسَنُهُمْ خُلُقًا  وَخِيَارُكُمْ خِيَارُكُمْ لِنِسَائِهِمْ خُلُقًا)) الترمذي وقال: حديث حسن صحيح

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Muumin aliyekamilika iymaan ni yule aliye na tabia njema kabisa, na wabora wenu ni wale walio bora kwa wake zao kwa tabia))  [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Swahiyh Hasan]

 

 

Hizo ni baadhi ya Hadiyth nyingi zenye kusisitiza Husnul-Khuluq baina ya watu kwa ujumla, kwa mke na mume, na hata kwa makafiri.

 

Share

04-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Akidhikika Pindi Waumini Wanapopata Shida, Akiwajali, Mpole Na Mwenye Huruma Mno

  

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

004-Akidhikika Pindi Waumini Wanapopata Shida,

Akiwajali, Mpole Na Mwenye Huruma Mno  

 

www.alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿١٢٨﴾

Kwa yakini amekujieni Rasuli anayetokana na nyinyi wenyewe, yanamtia mashaka (na huzuni) yanayokutaabisheni, anakujalini, mwenye huruma kwa Waumini ni mwenye huruma mno, mwenye rahmah. [At-Tawbah: 128]

 

Imaam As-Sa’diy amesema: 

لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ

Kwa yakini amekujieni Rasuli anayetokana na nyinyi wenyewe, yanamtia mashaka (na huzuni) yanayokutaabisheni.

 

Yaani: Wanamjua hali yake na wanajimakinisha kuchukua (ujumbe) kutoka kwake wala hawamwendei kinyume katika utiifu, naye ni (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwanasihi nasaha nzuri kabisa na akiwaendea mbio kuwafanikishia maslahi yao. Akidhikika na yale yanayokutieni mashaka na yanayokutaabisheni.

حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ

anakujalini, mwenye huruma kwa Waumini ni mwenye huruma mno, mwenye rahmah.

 

Akikupendeleeni khayr na akifanya juhudi kukufikieni hizo khayr na akitilia hima kuongoka kwenu kufikia iymaan na akichukia shari kukufikieni na akifanya juhudi zisikufikieni shari hizo. Mpole na mwenye huruma mno, akiwahurumia kuliko wazazi wao wanavyowahurumia.

[Tafsiyr Imaam As-Sa'dy]

 

Katika ambayo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anayojali na kuyakhofia kwa Waumini ni kuwakinga na moto. Kama ilivyothibiti katika Hadiyth:

 

عَنْ جَابِرٍ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((مَثَلِي وَمَثَلُكُمْ كَمَثَلِ رَجُلٍ أَوْقَدَ نَارًا فَجَعَلَ الْجَنَادِبُ وَالْفَرَاشُ يَقَعْنَ فِيهَا وَهُوَ يَذُبُّهُنَّ عَنْهَا وَأَنَا آخِذٌ بِحُجَزِكُمْ عَنِ النَّارِ وَأَنْتُمْ تَفَلَّتُونَ مِنْ يَدِي)) مسلم

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mfano wangu na mfano wenu ni kama mtu ambaye anayewasha moto kisha wadudu na nondo wala nguo wakawa wanaanguka humo kisha yeye (huyo mtu) anajaribu kuwatoa humo nami huku nawazuia migongo yao isiangukie katika moto lakini mnateleza mikononi mwangu)) [Muslim]

 

Share

05-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Akiwapendelea Waumini Yaliyo Mepesi Katika ‘Amali Zao Na Katika Da’wah

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

05-Akiwapendelea Waumini Yaliyo Mepesi Katika ‘Amali Zao Na Katika Da’wah

 

www.alhidaaya.com

 

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwapendelea Maswahaba kutenda yaliyo mepesi na hakuwatakia wataabike katika ‘amali zao wala katika kutaamuli na watu katika Da’wah. Hadiyth ya Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amesema:

 

كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا أَمَرَهُمْ أَمَرَهُمْ مِنَ الأَعْمَالِ بِمَا يُطِيقُونَ قَالُوا: ((إِنَّا لَسْنَا كَهَيْئَتِكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّ اللَّهَ قَدْ غَفَرَ لَكَ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ‏.‏ فَيَغْضَبُ حَتَّى يُعْرَفَ الْغَضَبُ فِي وَجْهِهِ ثُمَّ يَقُولُ: ((إِنَّ أَتْقَاكُمْ وَأَعْلَمَكُمْ بِاللَّهِ أَنَا))

 

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapowaamrisha (Waumini) jambo katika 'amali aliwaamrisha (mepesi) ambayo walikuwa na uwezo nao wakawa wanasema: “Sisi si kama wewe, Allaah Amekughufuria madhambi yako yaliyotangulia na ya baadae.”  Akaghadhibika mpaka ghadhabu ikadhihirika usoni mwake kisha akasema: ((Mimi ni mwenye taqwa zaidi yenu, na namjua zaidi Allaah kulikoni nyinyi)) [Al-Bukhaariy]  

 

 

Na katika Da’wah (ulinganiaji):

 

عَنْ أَنَسِ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((يَسِّرُوا وَلاَ تُعَسِّرُوا وَبَشِّرُوا ولاَ تُنَفِّرُوا)) متفق عليه

 

Imepokelewa kutoka kwa Anas (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Sahilisheni wala msifanye uzito, wapendekezeni watu khayr na muwabashirie wala msiwakimbize)). [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Na katika ‘Ibaadah: Hadiyth ya ‘Abdullaah Ibn ‘Amru Ibn Al-‘Aasw:

 

كُنْتُ أَصُومُ الدَّهْرَ وَأَقْرَأُ الْقُرْآنَ كُلَّ لَيْلَةٍ - قَالَ - فَإِمَّا ذُكِرْتُ لِلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم وَإِمَّا أَرْسَلَ إِلَىَّ فَأَتَيْتُهُ فَقَالَ لِي‏"‏أَلَمْ أُخْبَرْ أَنَّكَ تَصُومُ الدَّهْرَ وَتَقْرَأُ الْقُرْآنَ كُلَّ لَيْلَةٍ‏"‏‏.‏ قُلْتُ بَلَى يَا نَبِيَّ اللَّهِ وَلَمْ أُرِدْ بِذَلِكَ إِلاَّ الْخَيْرَ.‏ قَالَ ‏"‏فَإِنَّ بِحَسْبِكَ أَنْ تَصُومَ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ ثَلاَثَةَ أَيَّامٍ ‏"‏.‏ قُلْتُ يَا نَبِيَّ اللَّهِ إِنِّي أُطِيقُ أَفْضَلَ مِنْ ذَلِكَ ‏.‏ قَالَ ‏"‏ فَإِنَّ لِزَوْجِكَ عَلَيْكَ حَقًّا وَلِزَوْرِكَ عَلَيْكَ حَقًّا وَلِجَسَدِكَ عَلَيْكَ حَقًّا - قَالَ - فَصُمْ صَوْمَ دَاوُدَ نَبِيِّ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَإِنَّهُ كَانَ أَعْبَدَ النَّاسِ"‏‏.‏ قَالَ قُلْتُ يَا نَبِيَّ اللَّهِ وَمَا صَوْمُ دَاوُدَ قَالَ ‏"‏كَانَ يَصُومُ يَوْمًا وَيُفْطِرُ يَوْمًا‏"‏.‏ قَالَ ‏"‏وَاقْرَإِ الْقُرْآنَ فِي كُلِّ شَهْرٍ‏"‏ ‏.‏ قَالَ قُلْتُ يَا نَبِيَّ اللَّهِ إِنِّي أُطِيقُ أَفْضَلَ مِنْ ذَلِكَ قَالَ ‏"‏ فَاقْرَأْهُ فِي كُلِّ عِشْرِينَ "‏‏.‏ قَالَ قُلْتُ يَا نَبِيَّ اللَّهِ إِنِّي أُطِيقُ أَفْضَلَ مِنْ ذَلِكَ قَالَ ‏"‏فَاقْرَأْهُ فِي كُلِّ عَشْرٍ‏"‏ ‏.‏ قَالَ قُلْتُ يَا نَبِيَّ اللَّهِ إِنِّي أُطِيقُ أَفْضَلَ مِنْ ذَلِكَ ‏.‏ قَالَ ‏"‏ فَاقْرَأْهُ فِي كُلِّ سَبْعٍ وَلاَ تَزِدْ عَلَى ذَلِكَ ‏.‏ فَإِنَّ لِزَوْجِكَ عَلَيْكَ حَقًّا وَلِزَوْرِكَ عَلَيْكَ حَقًّا وَلِجَسَدِكَ عَلَيْكَ حَقًّا"‏.‏ قَالَ فَشَدَّدْتُ فَشُدِّدَ عَلَىَّ.‏ قَالَ وَقَالَ لِيَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏"‏إِنَّكَ لاَ تَدْرِي لَعَلَّكَ يَطُولُ بِكَ عُمْرٌ"‏.‏ قَالَ فَصِرْتُ إِلَى الَّذِي قَالَ لِيَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَلَمَّا كَبِرْتُ وَدِدْتُ أَنِّي كُنْتُ قَبِلْتُ رُخْصَةَ نَبِيِّ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم.‏

 

“Nilikuwa nikifunga mwaka mzima, na nikisoma Qur-aan kila usiku. Alipojulishwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaniita kwake nikaenda. Akasema: ((Nimesikia kwamba unafunga (Swawm) mwaka mzima na unasoma (unakhitimisha) Qur-aan kila usiku?)) Nikasema: Ndio ee Rasuli wa Allaah. Wala sitaki lolote ila khayr tu. Akasema: ((Inakutosheleza ukifunga katika kila mwezi siku tatu…)) Kisha akasema: ((Na usome Qur-aan (ukhitimishe) kila mwezi)). Akasema: Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah, mimi hakika naweza kufanya vizuri zaidi ya hivyo. Akasema: ((Basi soma katika siku saba na usizidishe juu ya hivyo, kwani mke wako ana haki na wewe, na wageni wako wana haki kwako, na mwili wako una haki kwako)). Akasema: Kila nikimkazania (nizidishe ‘ibaadah) alikuwa akinikazania (nipunguze). Akasema: Akaniambia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Huenda umri ukawa mrefu kwako)) Nikaendeleza (‘ibaadah) kama alivyoniambia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Nilipokuwa mkubwa kiumri nilipendelea kufuata rukhsa aliyonipa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]

 

Share

06-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Miongoni Mwa Hayaa Zake Alimsitahi Allaah Alipofaradhisha Swalaah Tano

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

06-Miongoni Mwa Hayaa Zake Alimsitahi Allaah Alipofaradhisha  Swalaah Tano 

www.alhidaaya.com

 

 

Pindi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipopandishwa mbinguni siku ya Israa Wal-Mi’raaj ambako ndipo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Alimfaradhishia nguzo ya Swalaah kwa Waislamu, na wakati alipopewa amri hiyo ya Swalaah akiwa anarejea, Nabiy Muwsaa ('Alayhis-Salaam) akamtaka arudi kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ili zipunguzwe hizo Swalaah tano, lakini  Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimstahi Rabb wake (‘Azza wa Jalla). Hadiyth ifuatayo imethibitisha: 

   

 أَنَسُ بْنُ مَالِكٍ وَابْنُ حَزْمٍ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((فَرَضَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ عَلَى أُمَّتِي خَمْسِينَ صَلاَةً فَرَجَعْتُ بِذَلِكَ حَتَّى أَمُرَّ بِمُوسَى عَلَيْهِ السَّلاَمُ فَقَالَ: مَا فَرَضَ رَبُّكَ عَلَى أُمَّتِكَ؟ قُلْتُ فَرَضَ عَلَيْهِمْ خَمْسِينَ صَلاَةً‏.‏ قَالَ لِي مُوسَى: فَرَاجِعْ رَبَّكَ عَزَّ وَجَلَّ فَإِنَّ أُمَّتَكَ لاَ تُطِيقُ ذَلِكَ‏.‏ فَرَاجَعْتُ رَبِّي عَزَّ وَجَلَّ فَوَضَعَ شَطْرَهَا فَرَجَعْتُ إِلَى مُوسَى فَأَخْبَرْتُهُ فَقَالَ: رَاجِعْ رَبَّكَ فَإِنَّ أُمَّتَكَ لاَ تُطِيقُ ذَلِكَ.‏ فَرَاجَعْتُ رَبِّي عَزَّ وَجَلَّ فَقَالَ: هِيَ خَمْسٌ وَهِيَ خَمْسُونَ لاَ يُبَدَّلُ الْقَوْلُ لَدَىَّ‏.‏ فَرَجَعْتُ إِلَى مُوسَى فَقَالَ رَاجِعْ رَبَّكَ فَقُلْتُ قَدِ اسْتَحْيَيْتُ مِنْ رَبِّي عَزَّ وَجَلَّ))

 

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik na Ibn Hazm kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:  ((Allaah ('Azza wa Jalla) Alifaradhisha Swalaah khamsini kwa Ummah wangu, nikazikubali na nikarejea hadi nilipopita kwa Muwsaa ('Alayhis-Salaam) ambaye alisema:  Je, Rabb wako Amekufaradhishia nini kwa Ummah wako? Nikasema: Amewafaridhisha Swalaah khamsini. Muwsaa akaniambia: Rudi kwa Rabb wako ‘Azza wa Jalla kwani ummah wako hawatoziweza hizo.  Nikamrejea Rabb wangu Allaah ('Azza wa Jalla)  Naye Akanipunguzia idadi zake, nikarudi kwa Muwsaa nikamwelezea akasema: Rudi kwa Rabb wako  kwani ummah wako hawatoziweza hizo. Nikarudi kwa Rabb wangu Allaah ('Azza wa Jalla) Akasema: Hizo (Swalaah) ni tano lakini ni thawabu khamisini na Kauli Yangu haibadiliki.  Nikarudi kwa Muwsa akasema: Rudi kwa Rabb wako. Nikasema: Hakika namstahi Rabb wangu Allaah 'Azza wa Jalla)) [A-Nasaaiy, Ibn Maajah na katika riwaayah ndefu ya Al-Bukhaariy]

 

 

Share

07-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Miongoni Mwa Hayaa Zake: Alikuwa Akiwastahi Maswahaba Zake Kuwaambia Waondoke Nyumbani Kwake

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

07-Miongoni Mwa Hayaa Zake:

Alikuwa Akiwastahi Maswahaba Zake Kuwaambia Waondoke Nyumbani Kwake

 

www.alhidaaya.com

 

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa ni mwenye kustahi na kuona hayaa mno na amethibitisha hayo Swahaba wake mtukufu:

 عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رضى الله عنه قَالَ كَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم أَشَدَّ حَيَاءً مِنَ الْعَذْرَاءِ فِي خِدْرِهَا‏.‏

Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: “Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa ni mwenye kuona hayaa mno kuliko  msichana asiyevunja ungo.  [Al-Bukhaariy, na Muslim]   

 

 

Alisitahi na kuona hayaa kuwataka Maswahaba waondoke siku ya Nikaah yake na Mama wa Waumini Zaynab bint Jahsh, siku ambayo palikuwa na karamu nyumbani kwake. Maelezo kama yalivyokuja katika Hadiyth kwenye Al-Bukhaariy:

 

عَنْ أَنَسٍ رضى الله عنه قَالَ: "بُنِيَ عَلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم بِزَيْنَبَ ابْنَةِ جَحْشٍ بِخُبْزٍ وَلَحْمٍ فَأُرْسِلْتُ عَلَى الطَّعَامِ دَاعِيًا فَيَجِيءُ قَوْمٌ فَيَأْكُلُونَ وَيَخْرُجُونَ، ثُمَّ يَجِيءُ قَوْمٌ فَيَأْكُلُونَ وَيَخْرُجُونَ، فَدَعَوْتُ حَتَّى مَا أَجِدُ أَحَدًا أَدْعُو فَقُلْتُ: يَا نَبِيَّ اللَّهِ مَا أَجِدُ أَحَدًا أَدْعُوهُ، قَالَ: ((ارْفَعُوا طَعَامَكُمْ)) وَبَقِيَ ثَلاَثَةُ رَهْطٍ يَتَحَدَّثُونَ فِي الْبَيْتِ، فَخَرَجَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَانْطَلَقَ إِلَى حُجْرَةِ عَائِشَةَ فَقَالَ: ((السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ أَهْلَ الْبَيْتِ وَرَحْمَةُ اللَّهِ)) فَقَالَتْ: وَعَلَيْكَ السَّلاَمُ وَرَحْمَةُ اللَّهِ، كَيْفَ وَجَدْتَ أَهْلَكَ بَارَكَ اللَّهُ لَكَ؟  فَتَقَرَّى حُجَرَ نِسَائِهِ كُلِّهِنَّ، يَقُولُ لَهُنَّ كَمَا يَقُولُ لِعَائِشَةَ، وَيَقُلْنَ لَهُ كَمَا قَالَتْ عَائِشَةُ، ثُمَّ رَجَعَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَإِذَا ثَلاَثَةُ رَهْطٍ فِي الْبَيْتِ يَتَحَدَّثُونَ، وَكَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم شَدِيدَ الْحَيَاءِ، فَخَرَجَ مُنْطَلِقًا نَحْوَ حُجْرَةِ عَائِشَةَ فَمَا أَدْرِي آخْبَرْتُهُ أَوْ أُخْبِرَ أَنَّ الْقَوْمَ خَرَجُوا، فَرَجَعَ حَتَّى إِذَا وَضَعَ رِجْلَهُ فِي أُسْكُفَّةِ الْبَابِ دَاخِلَةً وَأُخْرَى خَارِجَةً أَرْخَى السِّتْرَ بَيْنِي وَبَيْنَهُ، وَأُنْزِلَتْ آيَةُ الْحِجَابِ"   البخاري

 

Imepokelewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba iliandaliwa karamu ya mkate kwa nyama siku ya Nikaah ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Zaynab bint Jahsh, nikatumwa kualika watu (wahudhurie karamu), basi watu wakaanza kuhudhuria (kwa makundi). Wakawa wanakula na kuondoka. Kundi lingine likawa linahudhuria kula na kuondoka. Nikaendelea kualika watu mpaka nikakosa tena watu wa kuwaalika. Nikasema: Ee Nabiy wa Allaah! Sipati tena watu wa kuwaalika! Akasema: ((Chukua chakula kilichobakia)). Kisha kundi la watu watatu wakawa wamebakia nyumbani kwake wakipiga gumzo. Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaondoka kwenda chumbani kwa ‘Aaishah akasema:  ((Assalaamu ‘Alaykum Ahlal-Bayt wa RahmatuLLaah)). Akajibu: “Wa ‘Alaykas-Salaam wa RahmatuLLaah. Je, umemkutaje mke wako Baaraka Allaahu Laka?” Kisha akaingia vyumbani mwa wake zake wote na akawaambia vile vile kama alivyomwambia ‘Aaishah nao wakasema vile vile kama alivyosema ‘Aaishah. Kisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akarudi na kukuta kundi la wale watu watatu bado wangaliko wakiwa wanapiga gumzo. Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa ni mtu mwenye kuona hayaa mno basi akatoka nje (kwa mara ya pili) kisha akaingia chumbani mwa ‘Aaishah. Sikumbuki kama nilimjulisha kuwa watu wameshaondoka. Akarudi na pindi alipofikia tu mlangoni, akavuta pazia baina yangu na yake, hapo Aayah ya hijaab ikateremshwa.” [Al-Bukhaariy]

 

Aayah hizo ziloteremshwa ni:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَدْخُلُوا بُيُوتَ النَّبِيِّ إِلَّا أَن يُؤْذَنَ لَكُمْ إِلَىٰ طَعَامٍ غَيْرَ نَاظِرِينَ إِنَاهُ وَلَـٰكِنْ إِذَا دُعِيتُمْ فَادْخُلُوا فَإِذَا طَعِمْتُمْ فَانتَشِرُوا وَلَا مُسْتَأْنِسِينَ لِحَدِيثٍ ۚ إِنَّ ذَٰلِكُمْ كَانَ يُؤْذِي النَّبِيَّ فَيَسْتَحْيِي مِنكُمْ ۖ وَاللَّـهُ لَا يَسْتَحْيِي مِنَ الْحَقِّ ۚ وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ ۚ ذَٰلِكُمْ أَطْهَرُ لِقُلُوبِكُمْ وَقُلُوبِهِنَّ ۚ وَمَا كَانَ لَكُمْ أَن تُؤْذُوا رَسُولَ اللَّـهِ وَلَا أَن تَنكِحُوا أَزْوَاجَهُ مِن بَعْدِهِ أَبَدًا ۚ إِنَّ ذَٰلِكُمْ كَانَ عِندَ اللَّـهِ عَظِيمًا ﴿٥٣﴾

Enyi walioamini! Msiingie nyumba za Nabiy isipokuwa mkipewa idhini ya kwenda kula si kungojea kiive. Lakini mtakapoitwa, basi ingieni, na mkimaliza kula, tawanyikeni, na wala msikae kujiliwaza kwa mazungumzo. Hakika hiyo ilikuwa inamuudhi Nabiy, naye anakustahini, lakini Allaah Hasitahi (kubainisha) haki. Na mnapowauliza wake zake haja, waulizeni nyuma ya pazia. Hivyo ni utwaharifu zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao. Na haipasi kwenu kumuudhi Rasuli wa Allaah. Na wala kuwaoa wake zake baada yake abadani. Hakika jambo hilo mbele ya Allaah ni kubwa mno.

 

إِن تُبْدُوا شَيْئًا أَوْ تُخْفُوهُ فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا ﴿٥٤﴾

Mkidhihirisha kitu chochote au mkikificha, basi hakika Allaah daima ni Mjuzi wa kila kitu.

 

لَّا جُنَاحَ عَلَيْهِنَّ فِي آبَائِهِنَّ وَلَا أَبْنَائِهِنَّ وَلَا إِخْوَانِهِنَّ وَلَا أَبْنَاءِ إِخْوَانِهِنَّ وَلَا أَبْنَاءِ أَخَوَاتِهِنَّ وَلَا نِسَائِهِنَّ وَلَا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ ۗ وَاتَّقِينَ اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدًا ﴿٥٥﴾

Si dhambi juu yao wanawake kuonana na baba zao, na wala watoto wao wa kiume, na wala kaka zao, na wala watoto wa kiume wa kaka zao, na wala watoto wa kiume wa dada zao, na wala wanawake wenzao (wa Kiislamu), na wala iliyowamiliki mikono yao ya kulia. Na mcheni Allaah. Hakika Allaah daima ni Mwenye kushuhudia kila kitu. 

[Al-Ahzaab: 53-55]

 

Share

08-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Miongoni Mwa Hayaa Zake Alistahi Maswahaabiyaat Katika Kuwaelekeza Jinsi Ya Kutwaharisha Hedhi

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

00-Miongoni Mwa Hayaa Zake Alistahi Maswahaabiyaat

Katika Kuwaelekeza Jinsi Ya Kutwaharisha Hedhi

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) alimstahi mwanamke aliyemjia kumuuliza swala la hedhi yake, basi kwa kusitahi, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alifunika uso wake baada ya kumjibu mwanamke huyo. Hadiyth inaelezea:

 

 عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ سَأَلَتِ امْرَأَةٌ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَيْفَ تَغْتَسِلُ مِنْ حَيْضَتِهَا قَالَ فَذَكَرَتْ أَنَّهُ عَلَّمَهَا كَيْفَ تَغْتَسِلُ ثُمَّ تَأْخُذُ فِرْصَةً مِنْ مِسْكٍ فَتَطَهَّرُ بِهَا ‏.‏ قَالَتْ كَيْفَ أَتَطَهَّرُ بِهَا قَالَ: ((تَطَهَّرِي بِهَا ‏.‏ سُبْحَانَ اللَّهِ)) ‏.‏ وَاسْتَتَرَ - وَأَشَارَ لَنَا سُفْيَانُ بْنُ عُيَيْنَةَ بِيَدِهِ عَلَى وَجْهِهِ  قَالَ: قَالَتْ عَائِشَةُ وَاجْتَذَبْتُهَا إِلَىَّ وَعَرَفْتُ مَا أَرَادَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَقُلْتُ تَتَبَّعِي بِهَا أَثَرَ الدَّمِ ‏.‏ وَقَالَ ابْنُ أَبِي عُمَرَ فِي رِوَايَتِهِ فَقُلْتُ تَتَبَّعِي بِهَا آثَارَ الدَّمِ ‏.‏

 Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) ambaye amesema: Mwanamke alimuuliza Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) vipi kuoga kujitwaharisha baada ya kumaliza hedhi yake. Akataja kuwa alimfundisha vipi kuoga kisha akamwambia achukue kipande cha pamba aweke misk  kwa ajili ya kujitwaharisha. Aksema: Vipi nijitwaharishe nacho? Akasema: ((Jitwaharishe nacho Subhaana Allaah!)) (Nabiy Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)   akajifunika uso wake. Sufyaan bin ‘Uyaynah akaonyesha jinsi alivyojifunika uso wake. Akasema ‘Aaishah: Nikamvuta mwanamke kwangu kwani nilifahamu alivyokusudia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), nikasema: Pakaza pamba hiyo katika sehemu zenye athari ya damu. Na Ibn ‘Umar katika Hadiyth yake (ametaja maneno ya ‘Aaishah)  Pakaza katika sehemu zenye athari ya damu.  [Muslim]

 

 

 

Share

09-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Mtu Bora Kabisa, Mkarimu Mno Na Shujaa

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

09-Mtu Bora Kabisa, Mkarimu Mno Na Shujaa

www.alhidaaya.com

 

 

عَنْ أَنَسٍ، رضى الله عنه قَالَ كَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم أَحْسَنَ النَّاسِ وَأَشْجَعَ النَّاسِ وَأَجْوَدَ النَّاسِ، وَلَقَدْ فَزِعَ أَهْلُ الْمَدِينَةِ، فَكَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم سَبَقَهُمْ عَلَى فَرَسٍ، وَقَالَ: ((وَجَدْنَاهُ بَحْرًا))

Imepokelewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa mtu bora kabisa, shujaa kabisa na mkarimo mno kuliko watu wengineo. Pindi watu wa Madiyna walipofazaika (kwa khofu), Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipanda farasi akatangulia mbele yao na akasema: ((Tumempata farasi huyu haraka kabisa))  [Al-Bukhaariy]

 

Na katika Hadiyth nyengine:

 

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ قَالَ كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ  أَحْسَنَ النَّاسِ وَكَانَ أَجْوَدَ النَّاسِ وَكَانَ أَشْجَعَ النَّاسِ وَلَقَدْ فَزِعَ أَهْلُ الْمَدِينَةِ ذَاتَ لَيْلَةٍ فَانْطَلَقَ نَاسٌ قِبَلَ الصَّوْتِ فَتَلَقَّاهُمْ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَاجِعًا وَقَدْ سَبَقَهُمْ إِلَى الصَّوْتِ وَهُوَ عَلَى فَرَسٍ لِأَبِي طَلْحَةَ عُرْيٍ فِي عُنُقِهِ السَّيْفُ وَهُوَ يَقُولُ" ((لَمْ تُرَاعُوا لَمْ تُرَاعُوا)) قَالَ: ((وَجَدْنَاهُ بَحْرًا)) أَوْ ((إِنَّهُ لَبَحْرٌ)) .‏ قَالَ: وَكَانَ فَرَسًا يُبَطَّأُ   مسلم  
 

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa mtu bora kabisa, na mkarimu mno kuliko watu wengineo, na shujaa kabisa. Usiku mmoja, watu wa Madiynah walifazaika kwa khofu (ya mshindo wa sauti). Wakatoka watu kuelekea mshindo wa sauti lakini Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alishafika kabla yao sehemu ya sauti hiyo, akakutana nao akasema: ((Msikhofu! Msikhofu!)) Naye alikuwa amepanda farasi wa Abuu Twalhah, farasi huyo alikuwa hana tandiko lake  na shingoni mwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  kulikuwa na panga akasema: ((Nimeshampata farasi kwa haraka kama (kasi ya mawimbi ya) bahari)) Au ((Hakika hiyo (sauti ya mshindo) ni (mfoko wa) bahari)) [Al-Bukhaariy]

 

 

 

Share

10-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Alikuwa Na Mwili Mlaini Kabisa Na Wenye Kutoa Harufu Nzuri Mno Ya Manukato

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

10-Alikuwa Na Mwili Mlaini Kabisa Na Wenye Kutoa  Harufu Nzuri Mno Ya Manukato  

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

عن أَنَسٌ رضي الله عنه قال: مَا شَمِمْتُ عَنْبَرًا قَطُّ وَلاَ مِسْكًا وَلاَ شَيْئًا أَطْيَبَ مِنْ رِيحِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَلاَ مَسِسْتُ شَيْئًا قَطُّ دِيبَاجًا وَلاَ حَرِيرًا أَلْيَنَ مَسًّا مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم

Kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Sijapatapo kusikia ‘ambar au misk wala harufu yoyote nyengine yenye harufu nzuri kama harufu ya mwili wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Na sijapatapo kugusa makhmeli wala hariri iliyo laini kabisa kulikono mwili wa Rasuli wa Allaah  Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)) [Muslim]

 

 

‘Ambar = Aina ya mafuta mazito yenye manukato mazuri kabisa.

 

Misk = Aina ya mafuta mazito yenye manukato mazuri.  Miski ziko rangi mbili:  nyeupe na nyeusi. Hii ndio iliyotajwa katika Sunnah kwa ajili ya wanawake kujitwaharisha hedhi zao.

 

 

 Na pia:

 

 عن جَابِرِ بْنِ سَمُرَةَ، قَالَ صَلَّيْتُ مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم صَلاَةَ الأُولَى ثُمَّ خَرَجَ إِلَى أَهْلِهِ وَخَرَجْتُ مَعَهُ فَاسْتَقْبَلَهُ وِلْدَانٌ فَجَعَلَ يَمْسَحُ خَدَّىْ أَحَدِهِمْ وَاحِدًا وَاحِدًا - قَالَ - وَأَمَّا أَنَا فَمَسَحَ خَدِّي - قَالَ - فَوَجَدْتُ لِيَدِهِ بَرْدًا أَوْ رِيحًا كَأَنَّمَا أَخْرَجَهَا مِنْ جُؤْنَةِ عَطَّارٍ ‏.‏

Kutoka kwa Jaabir Bin Samurah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: “Niliswali pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Swalaah ya mwanzo kisha akatoka kwenda kwa ahli zake nami nikatoka kwenda naye. Akakutana na watoto (njiani). Akawagusa mashavu yao mmmoja mmoja. Akanigusa mimi pia shavu langu nikahisi ubaridi au harufu ya mkono wake kama vile umetolewa kutoka mfuko wa mafuta ya manukato mazuri.”  [Muslim

Share

11-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Mifano Ya Ukarimu Wake: Akitoa Swadaqah Hadi Kwamba Alipofariki Hakuacha Dirham Wala Dinari

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

11-Mifano Ya Ukarimu Wake:

 

Akitoa Swadaqah Hadi Kwamba Alipofariki Hakuacha Dirham Wala Dinari

 

www.alhidaaya.com

 

 

Kutoa kwake swadaqah Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kulikuwa hadi alipofariki hakuwa na chochote cha kumiliki wala dirham wala dinari kama ilivyothibiti katika Hadiyth:

 

عَنْ عَمْرِو بْنِ الْحَارِثِ، خَتَنِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَخِي جُوَيْرِيَةَ بِنْتِ الْحَارِثِ قَالَ مَا تَرَكَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عِنْدَ مَوْتِهِ دِرْهَمًا وَلاَ دِينَارًا وَلاَ عَبْدًا وَلاَ أَمَةً وَلاَ شَيْئًا، إِلاَّ بَغْلَتَهُ الْبَيْضَاءَ وَسِلاَحَهُ وَأَرْضًا جَعَلَهَا صَدَقَةً‏.‏

 

Imepokelewa kutoka kwa ‘Amruw bin Al-Haarith, kaka yake mke wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Alipofariki Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuacha dirham wala dinari, wala mtumwa wala kijakazi, isipokuwa baghala wake mweupe (aliyekuwa akimpanda), na silaha na kipande cha ardhi alichokitolea swadaqah.”  [Al-Bukhaariy]

 

Share

12-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Mifano Ya Ukarimu Wake: Akitoa Bila Kukhofia Umasikini

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

12-Mifano Ya Ukarimu Wake: Akitoa Bila Kukhofia Umasikini

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitoa swadaqah kila mara bila ya kukhofu umasikini:

 

 

 

عَنْ مُوسَى بْنِ أَنَسٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: مَا سُئِلَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عَلَى الإِسْلاَمِ شَيْئًا إِلاَّ أَعْطَاهُ. قَالَ: فَجَاءَهُ رَجُلٌ فَأَعْطَاهُ غَنَمًا بَيْنَ جَبَلَيْنِ فَرَجَعَ إِلَى قَوْمِهِ فَقَالَ: "يَا قَوْمِ أَسْلِمُوا فَإِنَّ مُحَمَّدًا يُعْطِي عَطَاءً لاَ يَخْشَى الْفَاقَةَ"

Imepokelewa kutoka kwa Muwsaa bin Anas kutoka kwa baba yake kwamba: Hakupata kuombwa kitu Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ajili ya Uislamu isipokuwa alitoa.”  Akasema:  “Alimjia mtu akampa kundi la mifugo ya (kondoo na mbuzi). Akarudi kwa watu wake na kusema: “Enyi watu wangu! Silimuni katika Uislamu kwani Muhammad anatoa swadaqah bila ya kukhofia ufukara.” [Muslim]

 

 

Share