Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema) - أحادِيثُ عَنْ حُسْنِ الخُلُق

 

أحادِيثُ عَنْ حُسْنِ الخُلُق

 

Hadiyth Kuhusu

 

Husnul-Khuluq (Tabia Njema)  

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

 

Share

01-Hadiyth Husnul-Khuluq: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Ametumwa Kwa Ummah Kukamilisha Husnul-Khuluq

 

 

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

 

Hadiyth Ya  1

 

Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)

Ametumwa Kwa Ummah Ili Kukamilisha Tabia Njema

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ الله عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ‏:‏ ((إِنَّمَا بُعِثْتُ لِأُتَمِّمَ صَالِحَ الأَخْلاقِ‏))

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika nimetumwa ili nikamilishe khulqa (tabia) njema)) [Ahmad na ameisahihisha Al-Albaaniy Swahiyh Al-Jaami’ (2349), Swahiyh Adab Al-Mufrad (207)]

 

 

 

 

Share

02-Hadiyth Husnul-Khuluq: Iymaan Ya Mtu Haikamilikii Ila Kwa Husnul-Khuluq

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

 

Hadiyth Ya 2   

02-Iymaan Ya Mtu Haikamilikii Ila Kwa Husnul-Khuluq

 

Alhidaaya.com

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((أَكْمَلُ الْمُؤْمِنِينَ إِيمَانًا أَحْسَنُهُمْ خُلُقًا  وَخِيَارُكُمْ خِيَارُكُمْ لِنِسَائِهِمْ خُلُقًا)) الترمذي وقال: حديث حسن صحيح

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Muumin aliyekamilika iymaan ni yule aliye na husnul-khuluq (tabia njema) kabisa, na wabora wenu ni wale walio bora kwa wake zao kwa tabia))  [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Swahiyh Hasan]

 

 

 

 

 

Share

03-Hadiyth Husnul-Khuluq: Husnul-Khuluq Inasababisha Miyzaan Ya 'Amali Kuwa Nzito Siku Ya Qiyaamah

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

 

Hadiyth Ya  3

 

Husnul-Khuluq Inasababisha Miyzaan Ya 'Amali Kuwa Nzito Siku Ya Qiyaamah

 

Alhidaaya.com

 

 

عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: (( مَا مِنْ شَىْءٍ أَثْقَلُ فِي الْمِيزَانِ مِنْ حُسْنِ الْخُلُقِ ‏))

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ad-Dardaai kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna kitakachokuwa kizito katika Miyzaan kama Husnul-Khuluq [tabia njema])) [Sunan Abiy Daawuwd, As-Silsilah Asw-Swahiyhah ((2/535), Swahiyh Al-Jaami’ 7=5721, Swahiyh Adab Al-Mufrad (204)]

 

 

 

 

Share

04-Hadiyth Husnul-Khuluq: Sifa Nyepesi Na Amali Aipendayo Zaidi Allaah Na Nzito Katika Miyzaan Siku Ya Qiyaamah

 

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

 

Hadiyth Ya  4

 

Sifa Nyepesi Na Amali Aipendayo Zaidi Allaah Na Nzito Katika Miyzaan Siku Ya Qiyaamah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

عنْ أَنَسٍ قَالَ لَقِيَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَبَا ذَرٍّ فَقَالَ: ((يَا أَبَا ذَرٍّ أَلا أَدُلُّكَ عَلَى خَصْلَتَيْنِ هُمَا أَخَفُّ عَلَى الظَّهْرِ وَأَثْقَلُ فِي الْمِيزَانِ مِنْ غَيْرِهِمَا)) قَالَ:  بَلَى يَا رَسُولَ اللَّهِ . قَالَ: ((عَلَيْكَ بِحُسْنِ الْخُلُقِ وَطُولِ الصَّمْتِ فَوَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ مَا عَمِلَ الْخَلائِقُ عَمَلا أَحَبَّ إِلَى اللَّهِ مِنْهُمَا))

 

Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokutana na Abuu Dharr alisema: ((Ee Abuu Dharr; je, nikujulishe sifa mbili ambazo ni nyepesi mgongoni mwako na nzito katika kabisa katika Miyzaan kuliko nyinginezo?)) Akasema: “Ndio Ee Rasuli wa Allaah.” Akasema: ((Shikimana na Husnul-Khuluq (tabia njema) na ukae kimya mda mrefu (usiongee upuuzi), kwani Naapa kwa Ambaye nafsi ya Muhammad imo Mikononi Mwake, hakuna 'amali za viumbe Azipendazo Allaah kama hizo mbili)) [Al-Mu’jam Al-Awsatw (7287), At-Targhiyb wat-Tarhiyb ya Al-Mundiriy (3/355) kwa daraja ya Hadiyth Jayyid wasimulizi ni wenye kuaminika]

 

Share

05-Hadiyth Husnul-Khuluq: Husnul-Khuluq Inazidisha Umri Wa Mtu

 

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

 

Hadiyth Ya  5

 

Husnul-Khuluq Inazidisha Umri Wa Mtu

 

Alhidaaya.com

 

 

عن عائشة أم المومنينن رضي الله عنها عن النبي صلى الله عليه وسلم: ((...صِلةُ الرَّحِمِ وحُسنُ الخُلُقِ وحُسنُ الجِوارِ يَعمُرانِ الدِّيارَ، ويَزيدانِ في الأعمارِ))

Imepokelewa kutoka kwa Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kuunga undugu na Husnul-Khuluq (tabia njema) na kumfanyia wema jirani inaamirisha nyumba na inaongeza umri)) [Ahmad na ameisahihisha Al-Albaaniy katika As-Silsilah Asw-Swahiyhah (519), Swahiyh At-Targhiyb (2524)] 

 

Share

06-Hadiyth Husnul-Khuluq: Aliye Kipenzi Cha Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) Na Atakayekuwa Karibu Naye Siku Ya Qiyaamah

 

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

 

Hadiyth Ya 6

 

Aliye Kipenzi Cha Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) Na Atakayekuwa Karibu Naye

Siku Ya Qiyaamah

 

Alhidaaya.com

 

 

ن جابر رضي اللَّه عنه أَن رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال: (( إِن مِنْ أَحَبِّكُم إِليَّ ، وَأَقْرَبِكُمْ مِنِّي مَجلساً يَومَ القِيَامَةِ، أَحَاسِنَكُم أَخلاقا)) الترمذي حديث حسن

Imetoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu)  kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika walio vipenzi kwangu na watakaokuwa karibu na mimi siku ya Qiyaamah ni wale wenye husnul-khuluq (tabia njema))) [At-Tirmidhiy – Hadiyth Hasan]. .

 

 

Share

07-Hadiyth Husnul-Khuluq: Husnul-Khuluq Ni Sababu Ya Kuingizwa Jannah

 

 

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

 

Hadiyth Ya  7

 

Husnul-Khuluq Ni Sababu Ya Kuingizwa Jannah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

عن أَبِي هُرَيْرَةَ‏:‏ سُئِلَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم‏:‏ مَا أَكْثَرُ مَا يُدْخِلُ الْجَنَّةَ‏؟‏ قَالَ‏:‏ ((تَقْوَى اللهِ، وَحُسْنُ الْخُلُقِ)) قَالَ‏:‏ وَمَا أَكْثَرُ مَا يُدْخِلُ النَّارَ‏؟‏ قَالَ‏:‏ ((الأَجْوَفَانِ‏:‏ الْفَمُ وَالْفَرْجُ‏.))

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa: “Jambo gani zaidi litakalokuwa ni sababu ya kumwingiza mtu Jannah?” Akasema: ((Taqwa (kumcha Allaah) na Husnul-Khuluq (tabia njema)). Na akulizwa: “Jambo gani zaidi litakalokuwa ni sababu ya kumwingiza mtu Motoni?” Akasema; ((Mdomo na sehemu za siri)) [Al-Adab Al-Mufrad, Swahiyh Ibn Maajah (3443)], Swahiyh At-At-Tirmidhiy (2004)]

 

Share

08-Hadiyth Husnul-Khuluq: Amedhaminiwa Jannah (Pepo) Mwenye Husnul-Khuluq

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

 

Hadiyth Ya  8

 

Amedhaminiwa Jannah (Pepo) Mwenye Husnul-Khuluq

 

Alhidaaya.com

 

 

 

عَنْ أَبِي أُمَامَةَ البَاهِلي (رضي الله عنه) قَال: قَال رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((أَنَا زَعِيم بَيْت فِي رَبَض الْجَنَّة لِمَنْ تَرَكَ الْمِرَاء وَإِنْ كَانَ مُحِقًّا، وَبِبَيْتٍ فِي وَسَط الْجَنَّة لِمَنْ تَرَكَ الْكَذِب وَإِنْ كَانَ مَازِحًا، وَبِبَيْتٍ فِي أَعْلَى الْجَنَّة لِمَنْ حَسُنَ خُلُقه)) حديث صحيح رواه أبو داود بإسناد صحيح

Imepokelewa kutoka kwa Abu Umaamah Al-Baahiliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:  ((Mimi ni mdhamini wa nyumba ya kando ya Jannah kwa anayeacha mabishano [wenye shaka] hata kama ni mwenye haki, na ni mdhamini wa nyumba iliyo katikati ya Jannah kwa anayeacha uongo japo ni kwa mzaha, na mdhamini wa nyumba iliyo mahala pa juu zaidi ya Jannah kwa ambaye ana husnul-khuluq (tabia njema)). [Hadiyth Swahiyh ameipokea Abu Daawuwd isnaad yake ni Swahiyh]

 

 

Share

09-Hadiyth Husnul-Khuluq: Husnul-Khuluq Inampatisha Mtu Daraja La Mwenye Swawm Na Qiyaam

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

 

Hadiyth Ya 9  

 

Husnul-Khuluq Inampatisha Mtu Daraja La Mwenye Swawm Na Qiyaam  

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Qiyaam : Kisimamo Cha Usiku Kuswali 

 

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : سَمِعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : ((  إنَّ المُؤْمِنَ لَيُدْرِكُ بحُسْنِ خُلُقِه دَرَجَةَ الصَّائِمِ القَائِمِ )) رواه أَبُو داود .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakika Muumini anafikia kwa husnul-khuluq yake (tabia njema) daraja ya mfungaji (Swawm) mwenye kusimama usiku." [Abu Daawuud]

 

 

Share

10-Hadiyth Husnul-Khuluq: Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) Alikuwa Na Husnul-Khuluq Kuliko Watu Wote

 

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

 

Hadiyth Ya  10

 

Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) Alikuwa Na Husnul-Khuluq Kuliko Watu Wote

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

وعن أنس رضي الله عنه ، قال : كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم أحْسَنَ النَّاس خُلُقاً . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa ni mwenye husnul-khuluq (tabia njema) kuliko watu wote." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share

11-Hadiyth Husnul-Khuluq: Wema Ni Katika Husnul-Khuluq

 

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

 

Hadiyth Ya  11

 

Wema Ni Katika Husnul-Khuluq

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

وعن النَّوَاس بنِ سمعان  رضي الله عنه ، قَالَ : سألتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم عن البِرِّ وَالإثم ، فَقَالَ : ((  البِرُّ : حُسنُ الخُلقِ ، والإثمُ : مَا حاك في صدرِك ، وكَرِهْتَ أن يَطَّلِعَ عَلَيْهِ النَّاسُ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa An-Nawwaas bin sam'aan (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu wema na dhambi akasema: "Wema ni Husnul-Khuluq (Tabia njema) na dhambi ni iliokera nafsini mwako na ukachukia watu kuiona." [Muslim]

 

Share

12-Hadiyth Husnul-Khuluq: Aliye Mbora Kabisa Ni Mwenye Husnul-Khuluq

 

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

 

Hadiyth Ya 12

Aliye Mbora Kabisa Ni Mwenye Husnul-Khuluq

 

Alhidaaya.com

 

 

 

عن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما ، قَالَ : لَمْ يكن رسولُ الله صلى الله عليه وسلم فَاحِشاً وَلاَ مُتَفَحِّشاً ، وكان يَقُولُ : ((  إنَّ مِنْ خِيَارِكُمْ أحْسَنَكُمْ أخْلاَقاً )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillah bin 'Amru bin Al-'aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: "Hakuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni mwenye kuzungumza maneno machafu wala kuyasikiliza." Na alikuwa akisema: "Hakika aliye bora miongoni mwenu ni yule mwenye husnul-khuluq (tabia nzuri)" [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na Ahmad].

 

 

Share

13-Hadiyth Husnul-Khuluq: Ujira Mara Mbili Kwa Kumfunza Husnul-Khuluq Kijakazi

 

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

 

Hadiyth Ya 13

 

Ujira Mara Mbili Kwa Kumfunza Husnul-Khuluq Kijakazi    

 

Alhidaaya.com

 

عَنْ أَبِي مُوسَى الأَشْعَرِيِّ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ إِذَا أَدَّبَ الرَّجُلُ أَمَتَهُ فَأَحْسَنَ تَأْدِيبَهَا، وَعَلَّمَهَا فَأَحْسَنَ تَعْلِيمَهَا ثُمَّ أَعْتَقَهَا فَتَزَوَّجَهَا، كَانَ لَهُ أَجْرَانِ، وَإِذَا آمَنَ بِعِيسَى ثُمَّ آمَنَ بِي، فَلَهُ أَجْرَانِ، وَالْعَبْدُ إِذَا اتَّقَى رَبَّهُ وَأَطَاعَ مَوَالِيَهُ، فَلَهُ أَجْرَانِ ‏"‏‏.‏

Imepokewa kwa Abu Muwsaa Al-Ash‘ariyy  (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)  kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Pindi mtu anapomfundisha adabu nzuri kabisa kijakazi wake, akamsomesha kwa kuboresha elimu yake, kisha akamuacha huru na kumuoa, atakuwa na ujira mara mbili. Na pindi mtu atakapomuamini ‘Iysaa, kisha akaniamimi mimi, naye atakuwa na ujira mara mbili. Na mtumwa atakapomcha Rabb wake (akawa na Taqwa) na akawatii mabwana zake, basi atakuwa na ujira mara mbili”. [Al-Bukhaariy]

 

Share

14-Hadiyth Husnul-Khuluq: Inawatosheleza Watu Husnul-Khuluq Kulikoni Mali

 

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

 

Hadiyth Ya  14

 

Inawatosheleza Watu Husnul-Khuluq Kulikoni Mali

 

Alhidaaya.com

 

 

 

وَعَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِنَّكُمْ لَا تَسَعُونَ اَلنَّاسَ بِأَمْوَالِكُمْ، وَلَكِنْ لِيَسَعْهُمْ بَسْطُ اَلْوَجْهِ، وَحُسْنُ اَلْخُلُقِ} أَخْرَجَهُ أَبُو يَعْلَى، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Nyinyi hamuwezi kuwatosheleza watu kwa mali zenu, lakini iwatoshe wao kutoka kwenu uchangamfu wa uso na khulqa (tabia) njema.” [Imetolewa na Abuu Ya’laa na akaisahihisha Al-Haakim]

 

Share

15-Hadiyth Husnul-Khuluq: Du’aa Ee Allaah Umeboresha Umbo Langu Boresha Khulqa Zangu

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

 

Hadiyth Ya 15

 

Du’aa Ee Allaah Umeboresha Umbo Langu Boresha Khulqa Zangu

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 عَنِ اِبْنِ مَسْعُودٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {اَللَّهُمَّ كَمَا أَحْسَنْتَ خَلْقِي، فَحَسِّنْ خُلُقِي} رَوَاهُ أَحْمَدُ وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّان َ

Kutoka kwa Ibn Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema:

اَللَّهُمَّ كَمَا أَحْسَنْتَ خَلْقِي، فَحَسِّنْ خُلُقِي

“Ee Allaah! Kama Ulivyofanya umbo langu kuwa bora nitengenezee tabia yangu.” [Imetolewa na Ahmad na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

Share

16-Hadiyth Husnul-Khuluq: Du'aa: Kujikinga Na Khulqa Ovu Za Kuchukiza

 

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

 

Hadiyth Ya 16

Du’aa Kujikinga Na Khulqa (Tabia) Ovu Za Kuchukiza

 

Alhidaaya.com

 

 

عَن زيادِ بْن عِلاقَةَ عن عمِّه، وَهُوَ قُطبَةُ بنُ مالِكٍ، t، قَال: كَانَ النَّبيُّ ﷺ يقُولُ: اللَّهمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِن منْكَرَاتِ الأَخلاقِ، والأعْمَالِ والأَهْواءِ رواهُ الترمذي وقال: حديثُ حَسَنٌ.

Kutoka kwa Ziyaad bin ‘Ilaaqah kutoka kwa ‘Amm yake naye ni Qutwabah bin Maalik. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akiomba:

 

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ مُنْكَرَاتِ الاَخْلاَقِ وَالاَعْمَالِ وَالاَهْوَاءِ

Allaahumma inniy a’uwdhu bika min munkaraatil-akhlaaqi wal a’-maali wal ahwaai

Ee Allaah, hakika najikinga Kwako tabia ovu za kuchukiza na matendo na matamanio

 

[At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Al-Haakim, At-Twabaraniy -  Swahiyh At-Tirmidhiy (3/184)]

 

Na pia,

 اللَّهُمَّ جَنِّبْنِي مُنْكَرَاتِ الاَخْلاَقِ وَالاَهْوَاءِ وَالاَعْمَالِ والأدْوَاءِ

Allaahumma jannibniy munkaraatil-akhlaaqi, wal ahwaahi, wal-a’maali, wal adwaai

Ee Allaah niepushe tabia ovu za kuchukiza na matamanio na na matendo, na maradhi

 

[Al-Haakim na kasema Swahiyh kwa sharti ya Muslim na ameikubali Adh-Dhahabiy.  Kitabus-Sunnah (13)  na ameipa daraja ya Swahiyh Al-Albaaniy]

 

Share

17-Hadiyth Husnul-Khuluq: Ee Allaah Niongoze Katika Husnul-Khuluq Na Niepushe Akhlaaq Mbaya

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

 

Hadiyth Ya  17

 

Ee Allaah Niongoze Katika Husnul-Khuluq Na Niepushe Akhlaaq Mbaya

 

Alhidaaya.com

 

Du’aa hii ni miongoni mwa du’aa za kufungulia Swalaah Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)

 

عَنْ عَلِيِّ بْنِ أَبِي طَالِبٍ، عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَنَّهُ كَانَ إِذَا قَامَ إِلَى الصَّلاَةِ قَالَ ‏"‏

 

‘Aliy bin Abiy Twaalib (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa pindi anaposimama kuanza  Swalaah alikuwa akiomba:

 

وَجَّهـتُ وَجْهِـيَ لِلَّذي فَطَرَ السَّمـواتِ وَالأَرْضَ حَنـيفَاً وَمـا أَنا مِنَ المشْرِكين، إِنَّ صَلاتـي، وَنُسُكي، وَمَحْـيايَ، وَمَماتـي للهِ رَبِّ العالَمين، لا شَريـكَ لَهُ وَبِذلكَ أُمِرْتُ وَأَنا مِنَ المسْلِـمين. اللّهُـمَّ أَنْتَ المَلِكُ لا إِلهَ إِلاّ أَنْت، أَنْتَ رَبِّـي وَأَنـا عَبْـدُك، ظَلَمْـتُ نَفْسـي وَاعْـتَرَفْتُ بِذَنْبـي فَاغْفِرْ لي ذُنوبي جَميعاً إِنَّـه لا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إلاّ أَنْت، وَاهْدِنـي لأَحْسَنِ الأَخْلاقِ لا يَهْـدي لأَحْسَـنِها إِلاّ أَنْـت، وَاصْـرِف عَـنّْي سَيِّئَهـا، لا يَصْرِفُ عَـنّْي سَيِّئَهـا إِلاّ أَنْـت، لَبَّـيْكَ وَسَعْـدَيْك، وَالخَـيْرُ كُلُّـهُ بِيَـدَيْـك، وَالشَّرُّ لَيْـسَ إِلَـيْك، أَنا بِكَ وَإِلَيْـك، تَبـارَكْتَ وَتَعـالَيتَ، أَسْتَغْـفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَـيك

 

Wajjahtu wajhiya liLLadhiy fatwaras-samaawaati wal ardhwa haniyfan wamaa ana minal mushrikiyn. Inna swalaatiy, wanusuky, wamahyaaya wamamaatiy liLLaahi Rabbil ‘aalamiyn. Laa shariyka Lahu wabidhaalika umirtu wa anaa minal Muslimiyn. Allaahumma Antal-Maliku laa ilaaha illa Anta. Anta Rabbiy wa ana ‘abduka, dhwalamtu nafsiy wa’taraftu bidhambiy faghfirly dhunuwbiy jamiy’an innahu laa yaghfirudh-dhunuwba illa Anta. Wahdiniy liahsanil-akhlaaqi laa yahdiy liahsanihaa illa Anta, waswrif ‘annyi sayyiahaa laa yaswrif ‘anniy sayyiahaa illa Anta. Labbayka wasa’dayka walkhayru kulluhu biyadika, wash-sharru laysa Ilayka, ana bika wa Ilayka, Tabaarakta wa Ta’aalayta, astaghfiruka wa atuwbu Ilayka

 

Nimeuelekeza uso wangu kwa yule Ambaye Ameanzisha mbingu na ardhi hali ya kuelemea katika haki, na sikuwa mimi ni katika washirikina, hakika Swalaah yangu na kuchinja kwangu na uhai wangu, na kufa kwangu ni kwa Allaah Rabb walimwengu, Hana mshirika, na kwa hilo nimeamrishwa nami ni katika Waislamu. Ee Allaah, Wewe Ndiye Mfalme, hapana  mwabudiwa wa haki ila Wewe, Wewe Ndiye Rabb wangu na mimi ni mja Wako. Nimedhulumu nafsi yangu, na nimekiri madhambi yangu kwa hivyo nighufurie madhambi yangu yote, hakika haghufurii madhambi, ila Wewe.  Na niongoze kwenye husnul-khuluq (tabia njema) kwani haongozi kwenye husnul-khuluq (tabia njema)  ila Wewe. Niepushe na tabia mbaya, kwani hakuna mwenye uwezo wa kuniepusha na tabia mbaya ila Wewe.  Naitikia mwito Wako, na nina furaha kukutumikia, na kheri zote ziko mikononi Mwako, na shari haitoki Kwako, mimi nimepatikana kwa ajili Yako, na nitarudi Kwako, Umebarikika na Umetukuka, nakuomba maghfira na narudi Kwako kutubia [Muslim] 

 

Bonyeza Upate Du’aa Kwa Sauti:

 

Bonyeza Hapa Usikilize

 

 

Share

18-Hadiyth: Husnul-Khuluq: Wengi Watakaoingizwa Jannah Ni Wenye Husnul-Khuluq

 

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

 

Hadiyth Ya  18

  Wengi Watakaoingizwa Jannah Ni Wenye Husnul-Khuluq

 

 

Alhidaaya.com

 

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {أَكْثَرُ مَا يُدْخِلُ اَلْجَنَّةَ تَقْوى اَللَّهِ وَحُسْنُ اَلْخُلُقِ} أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mengi yanayowaingiza watu Jannah ni kuwa na taqwa Allaah na khulqa (tabia)  njema.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na akaisahihisha Al-Haakim]

 

 

 

Share

19-Hadiyth Husnul-Khuluq: Ubakhili Na Khulqa Mbaya Hazijumuiki Kwa Muumini

 

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

 

Hadiyth Ya  19

Ubakhili Na Khulqa Mbaya Hazijumuiki Kwa Muumini

 

Alhidaaya.com

 

 

وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ ‏ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏{خَصْلَتَانِ لَا يَجْتَمِعَانِ فِي مُؤْمِنٍ: اَلْبُخْلُ، وَسُوءُ اَلْخُلُقِ} أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَفِي سَنَدِهِ ضَعْفٌ

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mambo mawili hayajumuiki kwa Muumini: ubakhili na khulqa (tabia) mbaya.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na katika isnaad yake kuna udhaifu]

 

Share

20-Hadiyth Husnul-Khuluq: Ukorofi Ni Khulqa Mbaya

 

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

 

Hadiyth Ya 20

 

Ukorofi Ni Khulqa Mbaya

 

Alhidaaya.com

 

 

وَعَنْ عَائِشَةَ ‏رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا‏ قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏قَالَ: {اَلشُّؤْمُ: سُوءُ اَلْخُلُقِ} أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ وَفِي إِسْنَادِهِ ضَعْفٌ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Ukorofi ni khulqa (tabia) mbaya.”  [Imetolewa na Ahmad na katika isnaad yake kuna udhaifu]

 

Faida:

 

Shari anazopata Mwana -Aadam ni kutokana na khulqa (tabia) zake mbaya. Hadiyth hii inaonyesha kuwa khulqa nzuri au mbaya za mtu zinatokana na chaguo lake binafsi.

 

Share

21-Hadiyth Husnul-Khuluq: Muumini Ni Kioo Kwa Muumini Mwenzake Kwa Husnul-Khuluq

 

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

 

Hadiyth Ya 21

Muumini Ni Kioo Kwa Muumini Mwenzake Kwa Husnul-Khuluq

 

Alhidaaya.com

 

 

 

عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {اَلْمُؤْمِنُ مِرْآةُ اَلْمُؤْمِنِ} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ بِإِسْنَادٍ حَسَنٍ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Muumini ni kioo cha ndugu yake Muumini.” [Imetolewa na Abuu Daawud kwa isnaad Hasan]

  

Faida:

 

Mtu anajifunza kuonekana kwake iwe ni uzuri au ubaya pindi anapojiangalia katika kioo. Vivyo hivyo, Muislaam ndio kioo cha Muislaam mwenzake na anatakiwa ajifunze kutoka kwa mwenzake kwa khulqa (tabia) alizonazo ili apendeze kwa Allaah na kwa watu baada ya kuondokana na khulqa yake mbaya.

 

 

Share

22-Hadiyth Husnul-Khuluq: Allaah Anamchukua Mwenye Khulqa Mbaya Za Maneno Maovu

Hadiyth: Husnul-Khuluq (Tabia Njema)

 

Hadiyth Ya 22

Allaah Anamchukua Mwenye Khulqa Mbaya Za Maneno Maovu

 

Alhidaaya.com

 

 

 

وَعَنْ أَبِي اَلدَّرْدَاءِ‏ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏{إِنَّ اَللَّهَ يُبْغِضُ اَلْفَاحِشَ اَلْبَذِيءَ} أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَصَحَّحَهُ

وَلَهُ مِنْ حَدِيثِ اِبْنِ مَسْعُودٍ ‏رَفَعَهُ‏: {لَيْسَ اَلْمُؤْمِنُ بِالطَّعَّانِ، وَلَا اَللَّعَّانُ، وَلَا اَلْفَاحِشَ، وَلَا اَلْبَذِيءَ} وَحَسَّنَهُ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ، وَرَجَّحَ اَلدَّارَقُطْنِيُّ وَقْفَهُ

Kutoka kwa Abuu Ad-Dardaa (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakika Allaah Anamchukia muovu, mwenye maneno mabaya.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na akaisahihisha]

 

Pia amepokea kutoka katika Hadiyth ya Ibn Mas-‘uwd marfuw’: “Muumini si mtukanaji, wala si mlaanifu, wala mchafu, wala si mwenye maneno mabaya.” [Na amesema ni Hasan na akaisahihisha Al-Haakim. Ad-Daaraqutwniy ameitilia nguvu kuwa ni Marfuw’]

 

Faida:

 

Hadiyth hii inatuelekeza kuwa si katika khulqa (tabia) ya Muumini kuwaita nduguze majina mabaya au kuwalaani. Hata hivyo inaruhusiwa kumtukana na kumlaani yule aliyelaaniwa na Allaah na Rasuli wake. Au kutaja kwa ujumla laana ya Allaah kwa makafiri. Watu wenye kufanya mambo mabaya na machafu. Vinginevyo si halaal kumlaani mtu kwa kumtaja jina lake.

 

 

 

Share