Dua Za Kujitoharisha
SWALI:
Assalam Aleikum
naomba tafadhali unisaidie na Dua ya Janaba na piya Dua ya Hedhi (wakati wa kujitoharisha).
shukran
ma'asalaam
JIBU:
AlhamduliLLah, Waswalaatu Was-salaam 'alaa Rasuli-Llah صلى الله عليه وآله وسلم Amma ba'ad,
Hakuna uthibitisho wowote katika mafundisho ya Sunnah ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kwamba kuna du'aa khaswa ya janaaba au ya hedhi, ila tu anapofanya wudhuu husema Bismillah kutokana na Hadiythi ifuatayo.
((عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال لا وضوء لمن لم يذكر اسم الله تعالى)) رواه أبو داود.
((Imetoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه kwamba amesema Mtume صلى الله عليه وسلم Hakuna wudhuu kwa asiyetaja jina la Allaah سبحانه وتعالى )) Abu Dawuud
Na kwavile ghuslu (josho) huanza mtu kwa wudhuu basi inafaa kuanza kwa kusema Bismillah.
Ama baada ya kutoka kufanya wudhuu imethibitika
((عن عمر بن الخطاب رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ما منكم من أحد يتوضأ فيسبغ الوضوء ثم يقول أشهد أن لا إله إلا الله وحده لا شريك له وأشهد أن محمداً عبده ورسوله اللهم اجعلني من التوابين واجعلني من المتطهرين إلا فتحت له أبواب الجنة الثمانية يدخل من أيها شاء )) رواه الترمذي
((Imetoka kwa 'Umar رضي الله عنه kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم kasema: Hakuna katika mmoja wenu atakayetawadha akautengeneza wudhuu kikamilifu, kisha akasema :
(Ash-hadu alla Ilaaha illa Allaah wahdahu laa shariyka
“Nakiri kwa moyo na kwa kauli kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu peke yake, wala Hana mshirika wake, na ninakiri kwamba Muhammad صلى الله عليه وسلم ni mja wake na ni Mtume wake” “Ewe Mwenyezi Mungu nijaalie niwe miongoni mwa wale wanaoomba msamaha, na nijaalie miongoni mwa wale waliosafi" isipokuwa atafunguliwa milango minane ya pepo aingie wowote autakao )) At-Tirmidhiy
Na Allaah Anajua Zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


