SWALI:
ASSALAM ALAYKUM WARAHMATULLAH WABARAKATUH.
SUALA; KUNA UTATANISHI HAPA KUNA MELI IMEPOTEA HAIJULIKANI IMEZAMA AU VIPI(
WABILLAHI TAWFIK. TUNAOMBA HILI SUALA MLIPE KIPA UMBELE KWANI NDIO TUMEKAA HATUJUI TUFANYE NINI.
MAASALAM.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani kwa swali lako zuri na tunamuomba Mola Muweza awe ni mwenye kumrudisha mume salama salimini na Amnusuru na kumhifadhi.
Anapoghibu mume
Katika mas-alah haya Wanachuoni wametofautiana, katika rai na kauli zao walizozitoa ni
Shari'ah inakubali kutenganishwa huko ili kuondoa madhara
Ama kujuzu kwa mwanamke kuomba kutenganishwa na mume aliyeghibu, hapana shaka kuwa kanuni za shari'ah na misingi yake inatilia nguvu
Hivyo ni suala la mwanamke mwenyewe kuangalia uwezo wake wa kungojea na kuvumilia kwa kupotelewa na mume. Kwa hivyo pindi anapohofia fitna atalipeleka suala
Kwa ufupi, tukichukua mfano ikiwa mume kapotea kwa muda wa miezi minne, sita na kuendelea, na mke akaohisi kuwa baada ya muda huo ameona kuwa hawezi tena kuvumilia, basi atakwenda kwa Qaadhi au Shaykh mwenye kuaminika na kupeleka malalamiko yake. Hapo Qaadhi kwa kuangalia maslahi na madhara yaliyopo, anaweza kuamua kumwachisha mke, naye (mke) ataanza eda yake ya miezi 4 na siku 10.
Na Allaah Anajua zaidi
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/57
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F2020&title=Mume%20Hajulikani%20Kama%20Kazama%20Baharini%20Au%20Yuhai%2C%20Je%20Mke%20Akae%20Eda%3F