SW
mimi nina mume lakini hanipi matumizi kabisa na pesa anayo je nikimuacha ni mbaya manake hataki kuniacha na tuna mda wa miezi sita toka tuowane na mimi namtimizia kila kitu lakini hanisaidii kwa lolote je nifanye nini? Asanteni ndugu zangu waislam
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa dada yetu aliyeuliza swali
Yaonyesha kwa hakika kuwa tunahitaji katika jamii yetu malezi ya kijamii kwa kiasi kikubwa. Tatizo hili huenda limeanza kuanzia katika majumba ya wazazi wetu nasi tukayarithi kwa ujumla wake. Kisha tatizo jengine linakuja katika mas-ala ya kuchagua mchumba. Hapa huwa tunakosea
Mbali na hayo, hatufundishwi majumbani kwetu namna ya kuishi na mume au mume kuishi vyema na mke. Kwa ajili hiyo huwa linapotokea tatizo huwa mara moja kutaka ima kuacha au kuachwa bila ya kuchukua hatua zifaazo. Katika maisha ya wanandoa ni wajibu na si ihsani kwa mume kumpatia yote anayohitajia mke katika mambo ya dharura na msingi wa maisha
Ama kwa mujibu wa hayo uliyotuelezea tunaweza kukupatia ushauri ufuatao:
Katika kila hali tunamuomba Allaah Aliyetukuka Akusahilishie jambo lako
Na Allaah Anajua zaidi
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/60
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F2607&title=Mume%20Hampi%20Matumizi%20Wala%20Kumsaidia%20Kwa%20Lolote%20Afanyeje%3F