SWALI:
ASSALAMU ALEYKUM
NATOWA SHUKURANI NYINGI KWA M.MUNGU PIA NA TOA SHUKURANI KWA NDUGU ZANGU WOTE WA AL HIDAAYA M.MUNGU AWAJAZI MAJAZI MEMA INSHAALLAH KWA KUTUELIMISHA NDUGU ZENU WA KISLAM.
SIFA ZOTE ANASTAHIKI M.MUNGU AMBAE AMENIWEZESHA KUULIZA SWALI ILIYOJAA MOYONI SIKUNYINGI NA MI HII MARA YANGU YA KWANZA KUJITOKEZA AL HAMDULILLAH.
BISMILLAH.. Mimi ni msichana wa miaka 22 ambae sijaolewa bado nimeka miaka 2 sasa nalala peke yangu pia nimefurahi kuwa nachumba peke yangu maana nafanya ibada kwa utulivu na swali, na soma qur.an [2] na soma dua ya kujikinga nyiradi na kwa kweli na mtegemea ALLAH zaidi ya kila kitu sasa bibi yangu alikuja kututembelea sasa tangu aje sina raha maana namsikia kila mara akimwambia mama msichana sio vizuri kulala peke yake.. sasa mama analala na mimi kweli na mpenda mama yangu na si kama na kata kulala na mimi isipokuwa na mpenda zaidi ALLAH na naogopa adhabu yake ndio maana nimeuliza suali ili nitumie hikma kumwambia mama yangu. mama yangu analala nami nawakati yuko na baba tangu miaka kadhaa mama halali na baba sasa analala na mi nami najua nivibaya nikimwacha nitapata dhambi maana baba saa ingine anakuja katika hali ya matamanio kumtaka nami nashindwa lakufanya najifanya nimelala na mama anamkatalia kumpa haki yake jee ni sawa nimwache tu alale kwangu...? pia huyo jida yangu anataka nilale na mdogo wangu wakike sikatai ila hafanyi ibada ata niki mpa nasaha na shindwa kuelewa pia si kulala tu ata saa zozote nikika ndani kufanya ibada huyu jida{bibi} yangu ana gomba pia mama anagomba eti nitapata majini nashindwa kuelewa nifanyaje sina raha nashindwa kumu abudu ALLAH Vizuri ata kufanya ibada ya usiku nashindwa nahofia kum bughudhi mama kalala pia ana kaa mpaka saa 6 ama 7 za usiku kuangalia tv kuamka alfajir nikimwamsha ananinyamazia
ninge penda munijibu mapema ili nitatue hii mtihani pia ningependa muni send kwenye e-mail yangu iwe uwepesi kwangu kusoma. pia wasome waislam wenzangu
SHUKRAN WA FI AMANILLAH
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukran dada yetu kwa swali lako
Nasaha yetu ya kwanza katika tatizo
Subira mara zote inaleta kheri ndio Waswahili wanasema: “Subira huvuta kheri”. Tutambue kuwa hakuna dhiki ambazo zinadumu milele katika maisha ya mwanadamu, kwani baada ya dhiki inakuja faraja. Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema: “Hakika pamoja na uzito upo wepesi” (94: 6). Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Muhifadhi Allaah, utampata Yuko mbele yako. Mjue Allaah katika neema, Atakujua katika shida. Ujue kwamba hakika lenye kukukosa halikuwa ni la kukupata, na la kukupata halikuwa ni lenye kukukosa. Na ujue kwamba ushindi waja kwa kusubiri na kwamba faraja yaja baada ya dhiki, na hakika baada ya mazito huja mepesi” (Ahmad).
Kwa hivyo, awali ya yote usijitie dhiki kwa yanayokukumba katika mitihani kwani hiyo ni Sunnah ya Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa waja wake. Ukilinganisha mtihani wako huu na wengine kama wewe utajikuta kuwa wewe wako ni mdogo
Nasaha ya pili, usitoke katika utii kwa mamako maadamu hajakuamrisha kumuasi Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) na Mtume wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema: “Na Tumemuusia mtu kwa wazazi wake wawili. Mama yake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumwachisha ziwa baada ya miaka miwili. (Tumemuusia): Nishukuru Mimi na wazazi wako. Ni kwangu Mimi ndiyo marudio. Na pindi wakikushikilia kunishirikisha na ambayo huna ilimu nayo, basi usiwatii. Lakini kaa nao kwa wema duniani” (31: 14 – 15).
Na Akasema tena: “Na Mola wako Ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima. Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu, Warehemu kama walivyo nilea utotoni” (17: 23 – 24).
Hizi ni ayah ambazo zinatuhimiza
Ni muhimu zaidi kutatua tatizo la mamako, kwani
Hata ikiwa hatakuwa ni mwenye kubadilika muache alale huko chumbani nawe ukiinuka usiku unaweza kwenda sehemu ambayo kuna nafasi ili kufanya ibada yako. Au pale pale chumbani bila ya kuwasha taa ili usimsumbue mamako au kuwasha kandili au mshumaa. Ikiwa yeye haswali hata ukimuamsha
Njia nyengine ni kukubali dada yako alale nawe chumba kimoja kwani
Muombe Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Akuepushe na balaa, shida na huo mtihani ukuondokee na uwe katika hali nzuri hapa duniani na Kesho Akhera. Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Akupe subira ya kuweza kukumbana na mitihani hiyo.
Na Allah Anajua zaidi
Links
[1] http://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/213
[2] http://qur.an/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F322&title=Ukilala%20Peke%20Yako%20Chumbani%20Unapata%20Jini%20Wa%20Mahaba%3F