SWALI:
Asalam aleykum,
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 28 nilifanya uzinzi kipindi cha nyuma lakin toka mwaka 2006 mwishon nilitubu na kujiweka mbali na zinaa mpaka sasa je, maomdi ninayoomba kwa mwenyezi mungu anipe mume awe mwaminif kama mimi nitapata?
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kutubia, kujirekebisha baada ya kuasi kwako. Ni jambo linalofahamika kuwa Allaah Aliyetukuka ni Msamehevu
Ikiwa umefanya madhambi, ukatubia ni kama kwamba huna tena madhambi tena hivyo kuwa msafi
Bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:
Tawbah [2]
Na Allaah Anajua zaidi.
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/67
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/nasiha_tawbah
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F4670&title=Nilikuwa%20Muasi%20Kisha%20Nimetubu%20Namuomba%20Allaah%20Mume%20Mwema%20%20Je%20Allaah%20Ataitikia%20Du%E2%80%99aa%20Yangu%3F%20