Utengenezaji Sambusa Za Nyama Na Jinsi Ya Kuzihifadhi
Takriban Sambusa 350
Vipimo
Pastries za sambusa - *350 takriban
Nyama ya kusaga - 4 Kilo
Pilipili mbichi ilosagawa - *3 Vijiko vya kulia
Jira (bizari pilau/cumini) - 3 vijiko vya kulia
Dania (gilgilani/coriander) - 3 vijiko vya kulia
Bizari mchanganyiko au bizari mchuzi - 1 kijiko cha kulia
Pilipili manga - 1 kijiko cha kulia
Ndimu - 7 takriban kamua
Vidonge vya supu - 5
Chumvi - *1 kijiko cha kulia
Vitunguu vilokatwakatwa (chopped) - 10 kiasi vya kiasi
Kotimiri (fresh coriander chopped) - 7 – 8 misongo
Mafuta ya kukaangia - Nusu karai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
6. Tayarisha gundi kwa kuchanganya unga kiasi katika kibakuli na maji.
7. Chukua pastry moja, kunja mkunjo wa kwanza kufanya kifuko. Jaliza kiasi vijiko viwili vya chai kisha kunja kama muelekezo wa picha. Tahadhari usibakishe uwazi pembezoni. Weka kidole gumba katika corner ya pastry pale unapokunja ili ubane pastry isibakie uwazi.
8. Kunja mkunjo wa pili kwa kukuilekeza pastry sambamba na ukingoni mwa pastry, huku umebana uwazi wa mfuko ili nyama isitoke. Elekeza sambamba na ukingoni wa pili. Endelea hivyo mpaka mwishowe ibakie kisehemu ndogo tu ya pastry.Tia gundi ubane vizuri sehemu zote za wazi.
9. Panga katika sahani kisha zihifadhi katika mifuko ya kuhifadhi chakula katika freezer.
10. Unapotaka kuzipika, ikiwa zinatoka katika freezer, zipike kwa mafuta ya dafudafu (Si yaliyochemka zitaungua sambusa kabla ya kuiva). Isipokuwa ikiwa unazipika fresh ndio mafuta yanaweza kuwa yameshika moto.
11. Zikibadilika rangi kuwa hudhurungi (golden brown) epua uzichuje mafuta katika chujio, kisha weka katika sahani uliyoweka tissue za jikoni zizidi kuchuja mafuta.
12. Panga katika sahani ya kupakulia zikiwa tayari.
Vidokezo:
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/46
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7312&title=Utengenezaji%20Sambusa%20Za%20Nyama%20Na%20Jinsi%20Ya%20Kuzihifadhi