Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi
(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)
Alhidaaya.com [1]
الْمُحِيطُ
الْمُحِيطُ Al-Muhiytw Mwenye Kuzunguka Vyote
|
Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Mwenye elimu ya kila kitu, Rahmah Yake inakizunguka kila kitu, Naye ni Mwenye kutamalaki na kutawala kila kitu.
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
إِن تَمْسَسْكُمْ حَسَنَةٌ تَسُؤْهُمْ وَإِن تُصِبْكُمْ سَيِّئَةٌ يَفْرَحُوا بِهَا ۖ وَإِن تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا لَا يَضُرُّكُمْ كَيْدُهُمْ شَيْئًا ۗ إِنَّ اللَّـهَ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطٌ ﴿١٢٠﴾
Ikikuguseni hasanah (nusura, ushindi) inawachukiza, na likikusibuni baya hulifurahia; na mkisubiri na mkawa na taqwa haitokudhuruni chochote katika hila zao. Hakika Allaah ni Mwenye kuyazunguka wayatendayo. [Aali ‘Imraan (3): 120]
Na pia Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ خَرَجُوا مِن دِيَارِهِم بَطَرًا وَرِئَاءَ النَّاسِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطٌ﴿٤٧﴾
Na wala msiwe kama wale waliotoka majumbani mwao kwa majivuno na kujionyesha kwa watu, na wanazuia njia ya Allaah. Na Allaah ni Mwenye kuyazunguka yote wanayoyatenda. [Al-Anfaal (8): 47]
Links
[1] http://www.alhidaaya.com
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10674&title=34-Sharh%20Asmaa%20Allaah%20Al-Husnaa%20Wa%20Swifaatihi%3A%20%D8%A7%D9%84%D9%92%D9%85%D9%8F%D8%AD%D9%90%D9%8A%D8%B7%D9%8F