Vipi Uweze Kuhifadhi Qur-aan?
كَيْفَ تَحْفَظُ الْقُرآن؟
Alhidaaya.com [1]
06-Zingatia Aayah Zinazoshabihiana (Aayaat Al-Mutashaabihaat)
06-Zingatia Aayah Zinazoshabihiana (Aayaat Al-Mutashaabihaat)
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
اللَّـهُ نَزَّلَ أَحْسَنَ الْحَدِيثِ كِتَابًا مُّتَشَابِهًا مَّثَانِيَ
Allaah Ameteremsha kauli nzuri kabisa, Kitabu; zinazoshabihiana ibara zake, zenye kukaririwa kila mara. [Az-Zumar (39: 23)]
Anayehifadhi Qur-aan aghlabu hutatizwa na kubabaika katika Aayah zinazoshabihiana katika Qur-aan. Kushabihiana kwake kunatofautiana ima kwa kutangulia neno au maneno, au kunatofautiana katika herufi au irabu n.k. Utakapozitambua na kuzihifadhi sawa sawa kauli hizo, basi utajiepusha na kutatizwa huko In Shaa Allaah. Kuna vitabu kwa lugha ya Kiarabu ambavyo vimetaja Aayah hizo laiti kama vingefasiriwa vitabu hivyo kwa lugha ya Kiswahili. Miongoni mwa Vitabu hivyo ni vifuatavyo:
Mifano michache ya kauli za Allaah (سبحانه وتعالى) zinazoshabihiana ni kama ifautavyo:
i-Mfano wa kwanza:
وَمَا أُهِلَّ بِهِ لِغَيْرِ اللَّـهِ ۖ
[Al-Baqarah (2: 173)]
Aayah hii katika Suwratul Baqarah ni pekee iliyotanguliza neno la بِهِ kabla ya لغير الله.
Ama kwengineko kama katika Suwratul-Maaidah (5:3) Suwratul-An-aam (6: 145) Suwratun-Nahl (16:115) imekuwa tofauti na hiyo Aayah ya Suwratul-Baqarah kwa kuwa neno la بِهِ limekuja baada ya لغير الله
وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ
Pia katika Suwratun-Nahl haikuanzia na: !$tBur.
ii-Mfano wa pili:
Zingatia kauli za Allaah (سبحانه وتعالى) zifuatazo jinsi zilivyoshabihiana na tofauti zake:
y7Ï9ºs ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانُوا يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَيَقْتُلُونَ النَّبِيِّينَ بِغَيْرِ الْحَقِّ ۗ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ ﴿٦١﴾
[Al-Baqrah (2: 61)]
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانُوا يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَيَقْتُلُونَ الْأَنبِيَاءَ بِغَيْرِ حَقٍّ ۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ ﴿١١٢﴾
[Aal-‘Imraan (3: 112)]
Kauli zifuatazo zimeshabihiana lakini zimetofautiana katika irabu; ya kwanza imetajwa kwa fat-haa na pili kwa kasra.
لَّقَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ فَقِيرٌ وَنَحْنُ أَغْنِيَاءُ ۘ سَنَكْتُبُ مَا قَالُوا وَقَتْلَهُمُ الْأَنبِيَاءَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَنَقُولُ ذُوقُوا عَذَابَ الْحَرِيقِ ﴿١٨١﴾
[Aal-‘Imraan (3: 181)]
فَبِمَا نَقْضِهِم مِّيثَاقَهُمْ وَكُفْرِهِم بِآيَاتِ اللَّـهِ وَقَتْلِهِمُ الْأَنبِيَاءَ بِغَيْرِ حَقٍّ
[An-Nisaa (4: 155)]
iii-Mfano wa tatu:
Aayah zilizoshabihiana lakini zimetafautiana kidogo katika kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى) kuhusu Nabiy Zakariyyah (عليه السلام) na Maryam mama wa Nabiy ‘Iysaa (عليه السلام) katika Suwratul-’Imraan:
قَالَ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَقَدْ بَلَغَنِيَ الْكِبَرُ وَامْرَأَتِي عَاقِرٌ ۖ قَالَ كَذَٰلِكَ اللَّـهُ يَفْعَلُ مَا يَشَاءُ ﴿٤٠﴾
[Aal-‘Imraan (3: 40)]
قَالَتْ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي وَلَدٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِي بَشَرٌ ۖ قَالَ كَذَٰلِكِ اللَّـهُ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ ۚ
[Aal-‘Imraan: (3: 47)]
iv-Mfano wa nne:
وَلَقَدْ صَرَّفْنَا لِلنَّاسِ فِي هَـٰذَا الْقُرْآنِ مِن كُلِّ مَثَلٍ
[Al-Israa (17: 89)]
Hapa tunaona kwamba neno لِلناَّسِ limetangulia. Ama katika Aayah ifuatayo limekuja baadaye.
وَلَقَدْ صَرَّفْنَا فِي هَـٰذَا الْقُرْآنِ لِلنَّاسِ مِن كُلِّ مَثَلٍ
[Al-Kahf (18: 54)]
v-Mifano mingi mno imo katika Qur-aan iliyokuwa katika hali kama hizo, na vinginevyo. Na pia nyingi hutofautiana pale inapomalizika Aayah; mfano Aayah mbili zinazofuatiana katika Suwratul-Maaidah:
لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٦٢﴾
[Al-Maaidah (5: 62)]
لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَصْنَعُونَ ﴿٦٣﴾
[Al-Maaidah (5: 63)]
Kisha katika Aayah Namba 79 imetofautiana tena:
لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ ﴿٧٩﴾
[Al-Maaidah (5: 79)]
Zingatia pia Asmaa na Swifaat za Allaah (سبحانه وتعالى) zinavyomalizika ambazo mara nyingi zimetajwa mbili mbili, huwa zinatofautiana mara kwa mara. Asmaa na Swifaat za Allaah (سبحانه وتعالى) zimekariri zaidi katika Suwratun-Nisaa. Pia aina za adhabu zinavvyotajwa mwishoni mwa Aayah. Almuradi darsa hili ni pana mno inahitaji mijalada ya vitabu! Inatosheleza kwamba anayehifadhi Qur-aan atambue swala hii na awe makini mwenyewe katika kutambua kauli na maneno hayo.
Links
[1] http://www.alhidaaya.com
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10723&title=06-Vipi%20Uweze%20Kuhifadhi%20Qur-aan%3F%20%28%D9%83%D9%8E%D9%8A%D9%92%D9%81%D9%8E%20%D8%AA%D9%8E%D8%AD%D9%92%D9%81%D9%8E%D8%B8%D9%8F%20%D8%A7%D9%84%D9%92%D9%82%D9%8F%D8%B1%D8%A2%D9%86%29%3A%20Zingatia%20Aayah%20Zinazoshabihiana%20%28Aayaat%20Al-Mutashaabihaat%29