كِتابُ الأيمان وَالنُّذور
Mlango Wa Viapo Na Nadhiri
Abu Maalik Kamaal Bin As-Sayyid Saalim
Imetarjumiwa na 'Abdullaah Mu'aawiyah (Abu Baasim)
Alhidaaya.com
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
01- Taarifu Ya Viapo
Alhidaaya.com [3]
[Taarifu hii nimeitoa kwenye kitabu cha ndugu yetu kipenzi ‘Iswaam Jaad (Allaah Amhifadhi). Ni kitabu chenye faida kubwa katika Nyanja ya Fiqhi ya Viapo. Kwa hakika nimefaidika sana na kitabu hicho].
الأَيْمَانُ katika lugha ni wingi wa اليَمِيْنُ , na asili yake katika lugha ni mkono. Kisha neno likatumika kwa maana ya kiapo, kwa kuwa watu walipokuwa wanaapizana, kila mmoja kati yao alikuwa akigonganisha mkono wake wa kulia kwa mkono wa kulia wa mwenzake. [Lisaanul ‘Arab na An-Nihaayatu cha Ibn Al-Athiyr].
Na اليَمِينُ katika sharia (kiistilahi), ni kuthibitisha kitu [au jambo] kwa kutaja Jina au Sifa ya Allaah. [Fat-hul Baariy (11/516)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
02- Usharia Wa Kiapo
Alhidaaya.com [3]
Usharia wa kiapo umethibiti katika Qur-aan, Sunnah na Ijma’a.
1- Katika Qur-aan, ni Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَلَا تَنقُضُوا الْأَيْمَانَ بَعْدَ تَوْكِيدِهَا"
“Na wala msivunje viapo baada ya kuvithibitisha. [An-Nahl (16:91)].
Na Neno Lake:
"قدْ فَرَضَ اللَّـهُ لَكُمْ تَحِلَّةَ أَيْمَانِكُمْ"
“Allaah Amekwishakufaridhishieni ukomboaji kwa viapo vyenu”. [At-Tahriym (66:2)].
Na Allaah ‘Azza wa Jalla Amemwamuru Nabiy Wake (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) aape katika mwahala patatu katika Kitabu Chake. Akasema:
"وَيَسْتَنبِئُونَكَ أَحَقٌّ هُوَ ۖ قُلْ إِي وَرَبِّي إِنَّهُ لَحَقٌّ"
53. Na wanakuuliza: Je, hiyo (adhabu na Qiyaamah) ni kweli? Sema: Ndio! Naapa kwa Rabb wangu! Hakika hiyo bila shaka ni kweli. [Yuwnus (10)].
Na:
"قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتَأْتِيَنَّكُمْ"
“Sema: Bali la! Naapa kwa Rabb wangu! Bila shaka itakufikieni”. [Sabai (34:3)].
Na:
"قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتُبْعَثُنَّ"
“Sema: Bali hapana! Naapa kwa Rabb wangu, bila shaka mtafufuliwa”. [At-Taghaabun (64:7)].
2- Na katika Hadiyth, ni neno lake (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam):
" وَالَّذِيْ نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ إِنِّي لأَرْجُو أَنْ تَكُونُوا نِصْفَ أَهْلِ الْجَنَّةِ"
“Naapa kwa Ambaye nafsi ya Muhammad iko Mkononi Mwake, hakika mimi kwa yakini ninatumai mtakuwa nusu ya watu wa Peponi”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (6528) na Muslim (221)].
Na neno lake (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam):
" فَوَالَّذِيْ لَا إِلَهَ غَيْرَهُ إِنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الْجَنَّةِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إِلَّا ذِرَاعٌ فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الْكِتَابُ ...."
“[Basi naapa kwa Ambaye hakuna mungu mwingine ila Yeye tu], hakika mmoja wenu atakuwa akifanya ‘amali ya watu wa Peponi mpaka ikafikia kati yake na Pepo kubakia dhiraa moja, na hapo yaliyoandikwa azali yakamtangulia..”. [Hadiyth Swahiyh. Muslim ameikhariji kwa tamko hili (2643), na At-Tirmidhiy (2137). Na kwa Al-Bukhaariy haina tamko la kiapo (3208)].
Na neno lake (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam):
"مَا بَالُ أَقْوَامٍ يَتَنَزَّهُونَ عَنِ الشَّىْءِ أَصْنَعُهُ، فَوَاللَّهِ إِنِّي لأَعْلَمُهُمْ بِاللَّهِ وَأَشَدُّهُمْ لَهُ خَشْيَةً"
“Wana nini watu hawa wanaacha jambo ninalolifanya? Basi naapa kwa Allaah, hakika mimi kwa yakini ndiye nimjuaye zaidi Allaah kuliko wao, na ndiye mwenye kumwogopa zaidi kuliko wao”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (6101) na Muslim (2356)].
Toka kwa Ibn ‘Umar amesema: “Kiapo cha Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) kilikuwa:
"لاَ وَمُقَلِّبِ الْقُلُوبِ"
“Laa, naapa kwa Mpinduaji wa nyoyo”. [Al-Mughniy (11/160 pamoja na Ash-Sharhul Kabiyr].
Kuna viapo vingine vingi ambavyo tutavigusia baadhi yake katika kitabu hiki In Shaa Allaah.
3- Ama kwa ‘Ijmaa, Umma wote umekubali usharia wa viapo na uthibiti wa hukmu zake.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
03- Viapo Vya Waislamu
Alhidaaya.com [3]
Viapo ambavyo Waislamu wanaviapa na ambavyo vinaweza kuambatana na hukmu za kisharia, tunaweza kuvijumuisha katika aina mbili: [Al-Mabsuwtw (8/126). Angalia pia Majmuw’ul Fataawaa (35/241)].
1- الْقَسَمُ “Kiapo”: Hiki ni kile ambacho mwenye kuapa anakusudia kwacho kumtukuza mwenye kuapiwa, na aina hii haifai isipokuwa kwa Allaah Ta’aalaa tu, kwani Yeye Ndiye Mstahiki wa Kutukuzwa kwa Dhati Yake kwa namna ambayo haijuzu kuvunja hishma ya Jina Lake kwa hali yoyote.
2- الشَّرْطُ وَالْجَزَاءُ “Sharti na Jazaa” (yaani sharti na tokeo lake, kwa maana ya kufungamanisha tendo na uwepo wa kitu au kutokuwepo kwake). Hili kwa mujibu wa Fuqahaa ni kiapo kwa kuwa linabeba maana ya kiapo ijapokuwa wabobezi wa lugha hawaitambui maana hii. Kati ya viapo vya aina hii ni pamoja na yamini ya nadhiri, yamini ya talaka, yamini ya kufanya la haramu, yamini ya dhwihaar na mfano wake.
Katika mlango huu, tutaiangalia kwa kina zaidi aina ya kwanza na baadhi ya picha za aina ya pili. Picha zake zilizobaki zimetajwa katika mahala mbalimbali husika katika Vitabu vya Fiqh.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
04- Haifai Kuapa Kila Wakati
Alhidaaya.com [3]
[At-Tafsiyr Al-Kabiyr ya Ar-Raaziy (6/75), 30/83) na Al-Mabsuwtw (8/127)]
Allaah Ta’aalaa Amesema:
"وَلَا تُطِعْ كُلَّ حَلَّافٍ مَّهِينٍ"
“Na wala usimtii kila mwingi wa kuapa, dhalili”. [Al-Qalam (68:10)].
الحَلَّافُ kwa mujibu wa walivyomwelezea baadhi ya Mufassiruna, ni mwingi wa kuapa katika haki na baatwil, na kwa tabia hiyo ya kuapa ovyo ovyo, inatosha kuwa alama ya kujiweka mbali na mtu huyo. Na Allaah ‘Azza wa Jalla Amesema:
"وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ"
“Na hifadhini yamini zenu”. [Al-Maaidah (5:89)].
Muradi wa Aayah hii ni jizuieni kuapa apa – kwa mujibu wa kauli ya mmoja wa Mufassiruna-, kwani linalotazamiwa baada ya kuapa ni kuhifadhi jema lililoapiwa, au kwa maana ya jizuieni msiape bila sababu yoyote.
Waarabu walikuwa wakimsifu mtu kutokana na uchache wa kuapa kwake kama alivyosema Kathiyr:
قَلِيْلُ الأَلَايَا حَافِظٌ لِيَمِيْنِهِ فَإِنْ سَبَقَتْ مِنْهُ الأَلِيَّة ُ بَرَّتِ
“Ni mchache mno wa kuapa, alindaye kiapo chake, na kama kiapo chake kimemtangulia, basi hukiheshimu akakitekeleza”.
Na hikma ya watu kuamuriwa kuapa kwa ufinyu iwezekanavyo, ni kuwa mtu anayeapa kwa Allaah kwa kila kichache na kingi, basi ulimi wake utazoea hilo, na kiapo hakitakuwa na uzito wala thamani kwenye moyo wake, na hatokuwa na muamana wa kuthubutu kuapa kiapo cha uongo. Na hapo lengo asili la kiapo litapoteza mwelekeo. Na kwa ajili hiyo, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) amekirihisha kuapa katika kuuza na kununua kwa kusema:
"الْحَلِفُ مَنْفَقَةٌ لِلسِّلْعَةِ مَمْحَقَةٌ لِلرِّبْحِ"
“Kiapo ni chuuzo la bidhaa, futo la baraka ya faida”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (2087) na Muslim (1606)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
05- Kiapo Hakiapiwi Ila Kwa Allaah Tu
Alhidaaya.com [3]
Toka kwa Ibn ‘Umar kuwa Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) alimpata ‘Umar bin Al-Khattwaab akiwa anakwenda na msafara huku akiapa kwa baba yake. Akamwambia:
"ألاَ إِنَّ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ يَنْهَاكُمْ أَنْ تَحْلِفُوا بِآبَائِكُمْ فَمَنْ كَانَ حَالِفًا فَلْيَحْلِفْ بِاللَّهِ أَوْ لِيَصْمُتْ"
“Jua utambue kwamba Allaah ‘Azza wa Jalla Anakukatazeni kuapa kwa baba [mababu] zenu, na mwenye kuapa, basi na aape kwa Allaah, au anyamaze”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (6646) na Muslim (1646)].
Hadiyth hii inadulisha mambo mawili: [Fat-hul Baariy (11/533)].
La Kwanza: Inakataza kuapa kwa asiye Allaah. Katika Hadiyh hii ya ‘Umar, mababu wamehusishwa kwa kuwa ndio walioapiwa, au wamehusishwa kwa kuwa ndio waliokuwa wakiapiwa zaidi kwa ushahidi wa neno la Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) katika riwaayah nyingine isemayo:
"وَكَانَتْ قُرَيْشٌ تَحْلِفُ بِآبَائِهَا"
“Na Maquraysh walikuwa wakiapa kwa mababu zao”. [Al-Bukhaariy (3836) na Muslim (1636)].
Na linadulisha ujumla wa katazo la kuapia kwa chochote kisicho Allaah neno lake Rasuli:
"مَنْ كَانَ حَالِفًا فَلاَ يَحْلِفْ إِلاَّ بِاللَّه"
“Mwenye kuapa, basi asiape kwa kingine chochote isipokuwa kwa Allaah tu”.
La Pili: Kwamba mwenye kuapa kwa asiye Allaah, akaapa kwa chochote kile, basi kiapo chake hakifungiki, ni sawa akiapia kwa chenye kustahiki kutukuzwa utukuzo usiobeba maana ya ‘ibaadah kama Manabii, Malaika, ‘Ulamaa, watu wema, mababu na Al-Ka’abah, au kisicho stahiki kutukuzwa kama watu wa kawaida, au chenye kustahiki kudharauliwa na kudhalilishwa kama Mashaytwaan na vingine vyenye kuabudiwa kinyume na Allaah. Kigezo cha kutofungika kiapo chake hapa ni kuwa hakuapa kwa Allaah, wala kwa lenye kuwakilisha Dhati Yake.
· Faida:
Mwislamu Akimwapia Nduguye Kwa Allaah, Basi Inatakikana Amsadiki Hata Kama Atajua Kinyume Cha Ukweli Wa Jambo.
Toka kwa Abu Hurayrah amesema, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) amesema:
"رَأَى عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ عَلَيْهِ السَّلاَمُ رَجُلاً سَرَقَ، فَقَالَ عِيسَى أسَرَقْتَ قَالَ كَلاَّ وَالَّذِي لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ. فَقَالَ عِيسَى آمَنْتُ بِاللَّهِ وَكَذَّبْتُ عَيْنيْ"
“‘Iysaa bin Maryam (‘Alayhis Salaam) alimwona mtu ameiba. ‘Iysaa akamwambia: Umeiba? Akasema hapana la hasha, naapa kwa Ambaye hapana mwingine wa kuabudiwa isipokuwa Yeye. ‘Iysaa akasema: Nimemwamini Allaah, na nimelikadhibisha jicho langu”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (3444) na Muslim (2368)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
06- Kuapa Kwa Majina Na Sifa Za Allaah
Alhidaaya.com [3]
[Al-Mughniy (11/182) na Al-Majmuw’u (18/22)].
Hakuna makhitalifiano yoyote kati ya ‘Ulamaa kuwa kiapo kinafungika kwa mwenye kusema "وَاللهِ" , au "بِاللهِ" , au "تَاللهِ" , na ni juu yake kafara kama atakivunja kiapo chake. Na pia kinafungika kwa kuapa kwa Jina lolote kati ya Majina Yake Subhaanah Ambayo haitwi Kwayo mwingine yoyote isipokuwa Yeye tu kama [الرَّحْمنُ] “Ar-Rahmaan”, au [الْأَوَّلُ الَّذِيْ لَيْسَ قَبْلَهُ شَيْءٌ] “Wa Mwanzo Ambaye hakuna kabla Yake kitu” , au [رَبُّ الْعَالَمِيْنَ] “Mola wa walimwengu”, au [الْحَيُّ الَّذِيْ لاَ يَمُوْتُ] “Aliye Hai Ambaye Hafi” , na mfano wa hayo.
Ama majina ambayo huitwa kwayo asiye Allaah kwa majazi na ambayo pia hunasibishwa kwa Allaah Ta’aalaa kama الْخَالِقُ , الرَّزَّاقُ , الرَّبُّ , الرَّحِيْمُ , الْقَاهِرُ na mfano wake, haya yote huitwa kwayo asiye Allaah kwa majazi kwa ushahidi wa Neno Lake Ta’aalaa:
"وَتَخْلُقُونَ إِفْكًا"
“Na mnaunda uzushi”. [Al-‘ Ankabuwt (29:17)].
Na Neno Lake:
"أَتَدْعُونَ بَعْلًا وَتَذَرُونَ أَحْسَنَ الْخَالِقِينَ"
“Mnamwomba (sanamu linaloitwa) ba-’alaa, na mnaacha Mbora wa wenye kuumba?". [As-Swaaffaat (37:125)].
Na Neno Lake:
"ارْجِعْ إِلَىٰ رَبِّكَ"
“Rejea kwa bwana wako”. [Yuwsuf (12:50)].
Na:
"اذْكُرْنِي عِندَ رَبِّكَ"
“Nikumbuke mbele ya bwana wako”. [Yuwsuf (12:42)].
Majina haya ikiwa atakusudia kwayo Jina la Allaah au akajiropokea tu bila uainisho, basi kinakuwa ni kiapo, kwa kuwa kwa kuyataja, Yananasibika Kwake Allaah. Na kama akikusudia asiye Allaah Ta’aalaa, basi haiwi kiapo, kwa kuwa yanatumika kwa wengineo. Hivyo unasibisho wa majina haya kwa Allaah, utategemea niya ya mwapaji.
Ama majina ambayo anaitwa kwayo Allaah Ta’aalaa na wengineo na wala hayanasibiki Kwake tu kwa kuitwa kama aliye hai, mjuzi, mkarimu na mfano wake, haya, ikiwa atakusudia kwayo kuapa kwa Jina la Allaah Ta’aalaa, basi kiapo kinazingatiwa. Na kama ataita au akakusudia asiye Allaah, basi hakizingatiwi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
07- Kuapa Kwa Sifa Za Allaah (تعالى)
Alhidaaya.com [3]
(a) Kwa mujibu wa Jumhuwri ya ‘Ulamaa, inajuzu kuapa kwa Sifa kati ya Sifa za Dhati ya Allaah Subhaanah ambazo hakusudiwi Kwazo mwingine Zaidi Yake Ta’aalaa kama Ujalali Wake, Kibri Chake, Uadhama Wake, na ‘Izzati Yake, na kiapo kinafungika Kwazo.
Toka kwa Anas amesema: Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) amesema:
"لاَ تَزَالُ جَهَنَّمُ تَقُولُ هَلْ مِنْ مَزِيدٍ حَتَّى يَضَعَ رَبُّ الْعِزَّةِ فِيهَا قَدَمَهُ فَتَقُولُ قَطْ قَطْ وَعِزَّتِكَ. وَيُزْوَى بَعْضُهَا إِلَى بَعْضٍ"
“Jahannam itaendelea kusema: Je, kuna zaidi [watu kuja kuingia]? Mpaka Rabbu wa ‘Izzah Atakapoweka ndani yake Mguu Wake, na hapo itasema: Inatosha, inatosha, naapa kwa ‘Izzati Yako. Na sehemu zake zitakutanishwa zenyewe kwa zenyewe”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (6661) na Muslim (2848)].
Na katika Hadiyth ya Abu Hurayrah –katika kuelezea mtu wa mwisho atakayetoka motoni-,:
"فَلاَ يَزَالُ يَدْعُو اللَّهَ. فَيَقُولُ لَعَلَّكَ إِنْ أَعْطَيْتُكَ أَنْ تَسْأَلَنِي غَيْرَهُ. فَيَقُولُ لاَ وَعِزَّتِكَ لاَ أَسْأَلُكَ غَيْرَهُ"
“Na ataendelea kumwomba Allaah bila kuchoka. [Allaah] Atamwambia: Je haiwezekani Nikikupa utaniomba jingine? Atasema laa, naapa kwa Nguvu Zako zisizoshindika (‘Izzati Yako), sitokuomba jingine zaidi ya hilo”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (6573) na Muslim (183)].
Na katika mapokezi ya Abu Hurayrah, Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) anasema:
"بَيْنَا أَيُّوبُ يَغْتَسِلُ عُرْيَانًا فَخَرَّ عَلَيْهِ جَرَادٌ مِنْ ذَهَبٍ، فَجَعَلَ أَيُّوبُ يَحْتَثِي فِي ثَوْبِهِ، فَنَادَاهُ رَبُّهُ يَا أَيُّوبُ، أَلَمْ أَكُنْ أَغْنَيْتُكَ عَمَّا تَرَى قَالَ بَلَى وَعِزَّتِكَ وَلَكِنْ لاَ غِنَى بِي عَنْ بَرَكَتِكَ"
“Wakati Ayyuwb alipokuwa anaoga uchi, nzige wa dhahabu walimwangukia. Ayyuwb akaanza kuwakusanya kwenye nguo zake. Mola wake akamwita: Ee Ayyuwb! Je, Sijakupa vya kutosha kiasi cha wewe kutowahitajia hivyo? Akasema: Na’am, naapa kwa ‘Izzati Yako, lakini siwezi kutosheka na Baraka Zako”. [Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (279) na Muslim (2806)].
Na toka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) alikuwa anasema:
"أَعُوذُ بِعِزَّتِكَ الَّذِيْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ، الَّذِيْ لاَ يَمُوتُ وَالْجِنُّ وَالإِنْسُ يَمُوتُونَ"
“Najilinda kwa “Izzat Yako Ambaye hapana mwingine wa kuabudiwa isipokuwa Wewe tu, Ambaye Hafi, hali ya kuwa majini na wana wa Aadam wanakufa”. [Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (7383) na Muslim (2717)].
Katika Hadiyth hii, kuna dalili kwamba inajuzu kujilinda kwa Sifa kati ya Sifa za Allaah, na pia katika kuapa, kwa kuwa yote mawili hayawi isipokuwa kwa Allaah tu.
(b) Ama Sifa za Vitendo vya Allaah Ta’aalaa, hili tushaligusia nyuma katika Hadiyth ya Ibn ‘Umar isemayo: “Kiapo cha Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) kilikuwa:
"لاَ وَمُقَلِّبِ الْقُلُوبِ"
“Laa, naapa kwa Mpinduaji wa nyoyo”. [Hadiyth Swahiyh].
Ibn Al-’Arabiy (Rahimahul Laah) amesema: “Katika Hadiyth hii, tunapata kuelewa kuwa inajuzu kuapa kwa Vitendo vya Allaah kama Atasifiwa Navyo bila kutaja Jina Lake. Na kama mtu ataapa kwa Sifa kati ya Sifa Zake, au kwa Kitendo kati ya Vitendo Vyake bila uainisho, basi hakiwi ni kiapo kutokana na tuliyoyasema nyuma katika neno lake Rasuli:
"مَنْ كَانَ حَالِفًا فَلْيَحْلِفْ بِاللَّهِ أَوْ لِيَصْمُتْ"
“Mwenye kuapa, basi aape kwa Allaah, au anyamaze”.
Na kama akiapa kwa Sifa kati ya Sifa za Allaah, basi kinakuwa ni kiapo, na akikivunja, basi ni lazima atoe kafara. Hivi hivi wamesema ‘Ulamaa wa Kimaalik na Kishaafi’iy toka kwa Maalik na Ash-Shaafi’iy mpaka enzi yetu ya leo”. [‘Aaridhwat Al-Ahwaziy (7/23].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
08- Kuapa Kwa Qur-aan
Alhidaaya.com [3]
Qur-aan ni Maneno ya Allaah ambayo hayakuumbwa. Na Maneno ya Allaah ni Sifa kati ya Sifa Zake. Na kwa ajili hiyo, Jumhuwri ya ‘Ulamaa –kinyume na Abu Haniyfah- wanasema kuwa inajuzu kuapa kwa Qur-aan, na mtu akiapa kwayo, basi kiapo kinafungika. Kutilia nguvu hili ni kuwa, kuomba kinga (kusema A’uwdhu bil Laah) hakuwi isipokuwa kwa Allaah tu, mbali na kuthibiti hilo toka kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) kuwa alikuwa anaomba kinga kwa baadhi ya Sifa za Allaah Ta’aalaa. Alikuwa anasema:
"أَعُوذُ بِوَجْهِكَ..."
“Najilinda kwa Wajihi Wako…”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (4628) na wengineo kutoka Hadiyth ya Jaabir].
Na:
"أَعُـوْذُ بِكَلِـماتِ اللّهِ التّـامّاتِ..."
“Najilinda kwa Maneno ya Allaah Yaliyotimia…”. [Hadyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2708) na wengineo toka Hadiyth ya Khawlah bint Hakiym].
Na:
"أَعُوْذُ بِرِضَاكَ مِنْ سَخَطِكَ"
“Najilinda kwa Radhi Zako kutokana na Hasira Zako”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (486) na wengineo toka Hadiyth ya ‘Aaishah].
Na mfano wa haya ni mengi. [Al-Mughniy (11/193) na Majmuw’ul Fataawaa (35/237). Ibn Al-Hammaam na Al-‘Ayniy wameungana na madhehebu ya Jumhuwri ya kufungika kiapo kwa kuapa kwa Qur-aan. Angalia Al-Fiqhul Islaamiy wa Adillatuhu (3/379)].
· Zindusho
Mwenye kuapa kwa Musw-haf, ikiwa anakusudia kwao Qur-aan iliyoandikwa ndani yake ambayo ni Maneno ya Allaah, basi itajuzu. Lakini akikusudia karatasi zilizoandikwa, basi haijuzu. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْر
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
09- Mwenye Kuapa Kwa Kusema: لَعَمْرُ الله “Naapa kwa Uhai wa Allaah”
Alhidaaya.com [3]
Imekuja katika Hadiyth ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa): Watu waliomzushia uzushi wa zinaa na wakasema waliyoyasema na Allaah Akamtakasa na uzushi huo, Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) alisimama na akataka udhuru toka kwa ‘Abdillaah bin Ubayya, na Usayd bin Khudhayr akasimama na kumwambia Sa’ad bin ‘Ubaadah:
" لَعَمْرُ الله لَنقْتُلَنَّه "
“Naapa kwa Uhai wa Allaah, lazima tutamuua”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (6662)].
"العَمْرُ" ina maana ya uhai. Mwenye kusema "لَعَمْرُ اللهِ" ni kama ameapa kwa Kubakia Milele Allaah, na hili linajuzu kwa ‘Ulamaa wote, na kiapo kinafungika kutokana na Hadiyth iliyotangulia. Katika Hadiyth hii, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) alikikubali kiapo cha Usayd (Radhwiya Allaah ‘anhu) cha "لَعَمْرُ اللهِ" na wala hakumkataza.
Na Allaah Ta’aalaa Amesema:
"لَعَمْرُكَ إِنَّهُمْ لَفِي سَكْرَتِهِمْ يَعْمَهُونَ"
15. Naapa kwa uhai wako (ee Muhammad صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمَ). Hakika wao walikuwa katika ulevi wao wanatangatanga kwa upofu. [Al-Hijr (72)].
Ikathibiti kwalo kuwa ni tamko la kisharia. Kisha kwa kuwa maana yake ni: “Naapa kwa Usalio wa Milele wa Allaah”, au: “Naapa kwa Uhai wa Allaah”. Kiapo hiki kinakuwa kwa Sifa ya Dhati ya Allaah, hivyo kinakuwa ni chenye kujuzu.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
010- Mwenye Kusema: وَعَهْدِ اللَّـهِ “Naapa kwa Ahadi ya Allaah”
Alhidaaya.com [3]
‘Ulamaa wamekhitalifiana kuhusiana na aliyesema: “Naapa kwa Ahadi ya Allaah”, au “Ni juu yangu Ahadi”, je kiapo chake kinafungika? Wana kauli tatu katika hili:
Kauli Ya Kwanza: Kiapo Kinafungika Kwa Kuapa Kwa Ahadi Ya Allaah
Ni kauli ya Al-Hasan, Twaawuws, Ash-Sha-‘abiy, Al-Awzaa’iy, Maalik na Ahmad. Hoja yao ni:
1- Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَأَوْفُوا بِعَهْدِ اللَّـهِ إِذَا عَاهَدتُّمْ وَلَا تَنقُضُوا الْأَيْمَانَ بَعْدَ تَوْكِيدِهَا"
“Na timizeni Ahadi ya Allaah mnapoahidi, na wala msivunje viapo baada ya kuvithibitisha”. [An-Nahl (16:91)].
Kauli Yake Ta’aalaa hapa haikutanguliwa na chochote isipokuwa kutajwa Ahadi, na kwa hivyo, imejulikana kuwa ni kiapo. Wamejibiwa hoja yao hii kwa kuambiwa kuwa hailazimu kuatwifiwa viapo kwa Ahadi kuwa ndio iwe kiapo.
2- Toka kwa Ibn Mas-‘uwd, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) amesema:
"مَنْ حَلَفَ عَلَى يَمِينٍ كَاذِبَةٍ، لِيَقْتَطِعَ بِهَا مَالَ رَجُلٍ مُسْلِمٍ أَوْ قَالَ أَخِيهِ لَقِيَ اللَّهَ وَهْوَ عَلَيْهِ غَضْبَانُ ". فَأَنْزَلَ اللَّهُ تَصْدِيقَهُ: إِنَّ الَّذِينَ يَشْتَرُونَ بِعَهْدِ اللَّـهِ وَأَيْمَانِهِمْ ثَمَنًا قَلِيلًا"
“Mwenye kuapa kiapo cha uongo ili aweze kupora kwacho mali ya mtu Muislamu, au alisema nduguye (Muislamu), basi atakutana na Allaah hali ya kuwa Amemkasirikia)). Allaah Akateremsha uthibitisho Wake [kwa hilo Akisema]: Hakika wale wanaobadilisha Ahadi ya Allaah na viapo vyao kwa thamani ndogo”.
Hapa Allaah Ameipa ahadi umahususi na kipaumbele kuliko viapo vingine, na hii inaonyesha uhakika wa kuiapia. Na kwa kuwa pia Ahadi ya Allaah ni yale ambayo Ameyawajibisha juu ya Waja Wake na yale Aliyowapa Waja Wake kama Alivyosema:
"وَمِنْهُم مَّنْ عَاهَدَ اللَّـهَ"
“Na miongoni mwao wako waliomuahidi Allaah”.
3- Ahadi inaitwa vile vile yamini. Inakuwa kama vile amesema: “Naapa kwa Yamini ya Allaah”. Na ile ni yamini, na ndivyo ilivyo hapa pia.
4- Maana yake inachukulika kama: Maneno ya Allaah, nayo ni Sifa Yake.
5- Ada na mazoea ya matumizi yamelithibitisha. Hivyo ni lazima liwe yamini kwa kulitaja.
Kauli Ya Pili: Kiapo Hakifungiki Kwa Kuapa Kwa Ahadi Ya Allaah Ila Tu Mtu Akinuwia
Hii ni kauli ya Ash-Shaafi’iy. Hoja yake ni kuwa neno hili hutumika kwa maana nyingine isiyo yamini (kama Usia wa Allaah kwa Waja Wake kwa kufuata Maamrisho Yake na mengineyo). Hivyo haligeuki na kubeba maana ya yamini ila kwa niya.
Kauli Ya Tatu: Kuapa Kwa Ahadi Ya Allaah Si Yamini
Ni kauli ya Abu Haniyfah na Ibn Hazm. Hoja zao ni:
1- Kuapa kwa Ahadi ya Allaah si kuapa kwa Sifa za Allaah ambazo inajuzu kuapa kwazo.
2- Yamini haiwi ila kwa Allaah tu.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
011- Mwenye Kusema: أَقْسَمْتُ “Nimeapa” au أُقْسِمُ “Ninaapa”
Alhidaaya.com [3]
1- Mwenye kusema: “Ninaapa kwa Allaah” au “Nimeapa kwa Allaah”, basi hiki ni kiapo bila mvutano wowote, ni sawa mtu amenuwia yamini au hakunuwia. Kwa kuwa akisema: “Kwa Allaah” na hakusema: “Naapa”, basi inakuwa ni kiapo kwa kukadiria kitenzi kabla yake (naapa). Halafu matumizi ya kiada na kimazoea yamelazimisha hivyo. Allaah ‘Azza wa Jalla Amesema:
"فَيُقْسِمَانِ بِاللَّـهِ"
“Kisha waape kwa Allaah”. [Al-Maaidah (5:107)].
Na Amesema tena:
"وَأَقْسَمُوا بِاللَّـهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ"
“Na waliapa kwa Allaah kwa viapo vya nguvu”. [Al-An’aam (6:109)].
2- Akisema: أُقْسِمُ “Ninaapa” au أَقْسَمْتُ “Nimeapa”, je kitakuwa ni kiapo?
Kuna kauli tatu kuhusu hili:
Kauli Ya Kwanza: Ni Yamini Kwa Vyovyote
Ni madhehebu ya Hanafiy na Ahmad, na Ibn Qudaamah ameyatilia nguvu. Dalili zao ni:
1- Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas toka kwa Abu Hurayrah -kuhusu kisa cha mtu aliyemhadithia Rasuli (Swalla Allaah ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) njozi yake na Abu Bakr akaifasiri. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia:
" أَصَبْتَ بَعْضًا وَأَخْطَأْتَ بَعْضًا " . فَقَالَ : أَقْسَمْتُ - بِأَبِي أَنْتَ وأمي- لَتُحَدِّثَنِّي مَا الَّذِي أَخْطَأْتُ . فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : " لاَ تُقْسِمْ "
“Umepatia sehemu na umekosea sehemu”. Akasema: Nimekuapia -kwa baba yangu na mama yangu- utanieleza lipi nimekosea. Rasuli akamwambia: “Usiape”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (2293), Abu Daawuwd (3268), na Ibn Maajah (3918) kwa tamko hili. Na katika Swahiyh Mbili kwa tamko la: “Wa Allaah, hakika utanieleza”].
Hapa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amelihesabu neno la Abu Bakr “Nimeapa” kuwa yamini. Likathibiti kwa hivyo kimatumizi na kwa ada ya kisharia.
2- Katika mkasa wa Bi ‘Aaishah kuzushiwa tuhuma kwamba amezini, Abu Bakr (Radhwiya Allaah ‘anhu) alimwambia ‘Aaishah:
"أَقْسَمْتُ عَلَيْكِ يَا بُنَيَّةُ إِلاَّ رَجَعْتِ إِلَى بَيْتِكِ"
“Nimekuapia na nakusihi ee mwanangu urudi nyumbani kwako”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (4757)].
3- Katika kisa cha ‘Abdul Rahmaan bin Abiy Bakr pamoja na wageni wa Abu Bakr walipokataa kula chakula, Abu Bakr akaja, na ‘Abdul Rahmaan akajificha kwa kumwogopa, Abu Bakr akasema:
"يَا غُنْثَرُ أَقْسَمْتُ عَلَيْكَ إِنْ كُنْتَ تَسْمَعنِي"
“We mpumbavu wee, nimekuapia kama unanisikia [toka huko ulikojificha]”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2057)].
4- Neno Lake Ta’aalaa:
"إِذْ أَقْسَمُوا لَيَصْرِمُنَّهَا مُصْبِحِينَ • وَلَا يَسْتَثْنُونَ"
“Walipoapa kuwa bila shaka watayavuna (mazao yake) watakapopambaukiwa asubuhi • Na wala hawakusema In-Shaa Allaah”. [Al-Qalam (68: 18 na 19)].
Allaah Hakusema: “Wakaapa kwa Allaah”. Hivyo Ameizingatia ni yamini, na kusema “In -Shaa Allaah” kunakuwa ndani ya yamini.
5 - Ni kuwa yamini haijuzu ila kwa Allaah ‘Azza wa Jalla tu. Hivyo, haifai kuapa isipokuwa kwa Allaah tu. Ni kama Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَاسْأَلِ الْقَرْيَةَ"
“Na uliza mji”. [Yuwsuf (12:82)].
“Yaani watu wa mji”. Na Waarabu wanakijua kiapo kwa njia hii (bila kumtaja Allaah).
Kauli Ya Pili: Ni Yamini Kama Atanuwiya Kuapa Kwa Allaah, Kama Hakunuwiya Basi Si Kiapo.
Ni madhehebu ya Al-Hudhayl bin Zufar –Faqiyh mkubwa wa Kihanafiy, Is-Haaq, Maalik na Ibn Al-Mundhir. Kwa kuwa inaweza kubeba kiapo kwa Allaah au kwa kitu kingine. Hivyo haiwi yamini mpaka aielekeze kwenye hali ya kuwajibisha kafara.
Kauli Ya Tatu: Si Yamini, Ni Sawa Akinuwiya Au Asinuwiye.
Ni kauli ya Ash-Shaafi’iy, Ibn Hazm, Al-Hasan, Az-Zuhriy, Qataadah, na Abu ‘Ubayd. Kwa kuwa yamini haifungiki ila kwa Jina Tukuzwa au Sifa Tukuzwa ili Mwapiwa Ahudhurishwe, na hapa Hakutajwa.
Al-Khattwaabiy amelitolea dalili dhehebu hili kwa Hadiyth iliyotangulia nyuma kidogo ya tafsiri ya Abu Bakr ya njozi mbele ya Rasuli. Na hii ni kwa kuwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameamuru mtu kutekeleza kiapo chake ili kujisafisha nacho. Na lau kama neno lake (Abu Bakr) “nimeapa” lingekua kiapo, basi angelimwamuru awajibike nacho.
Dalili hii imeandamiziwa kwa jibu lisemalo kwamba katika riwaayah ya Swahiyh mbili imeelezwa kwamba Abu Bakr aliitamka yamini wazi bayana akisema: “Wa Allaah, utanieleza”. Rasuli akamwambia: “Usiape”.
Kauli Yenye Nguvu:
Kwa mujibu wa hoja hizo, inaonekana kuwa mwenye kusema “nimeapa” basi neno lake hilo linazingatiwa kama yamini iliyofungika. Lakini, inatakikana yamini hii ifungwe kwa masharti mawili. Kwanza mwapaji aape kwa khiyari yake mwenyewe, na pili akusudie kuapa, asiwe anatamka tu na mfano wa hivyo. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
012-Mwenye Kusema: أَشْهَدُ باللَّـهِ “Ninashuhudia kwa Allaah”
au أَشْهَدُ “Ninashuhudia”
Alhidaaya.com [3]
1- Mwenye kusema: “Ninashuhudia kwa Allaah”, basi tamshi lake hili ni kiapo kwa mujibu wa rai ya Fuqahaa wote. Kwa kuwa neno: “Kwa Allaah” linatosha peke yake kuwa kiapo kwa kuwa linamaanisha: “Ninaapa kwa Allaah”. Tumeshasema nyuma kwamba katika Neno Lake Ta’aalaa:
"أَن تَشْهَدَ أَرْبَعَ شَهَادَاتٍ بِاللَّـهِ"
“Atakapotoa ushahidi mara nne kwa kiapo cha Allaah”. [An-Nuwr (24:8)]… ni kwamba “Li’aan” (mume kumtuhumu mkewe kuwa amezini kwa kutamka shahaadah) kwa mujibu wa ‘Ulamaa wengi ni viapo vinavyotiliwa nguvu kwa kumshuhudilia Allaah. Lakini Ash-Shaafi’iy amekhitalifiana na wenzake kwa kuifungamanisha kauli yake hii na niya.
2- Ama akisema: “Ninashuhudia”, hapa ‘Ulamaa wamekhitalifiana kama kitakuwa ni kiapo katika kauli tatu kama zile zile za suala lililotangulia. Mashiko ya mwenye kulizingatia neno “Ninashuhudia” kuwa kiapo, ni Neno Lake Ta’aalaa:
"إِذَا جَاءَكَ الْمُنَافِقُونَ قَالُوا نَشْهَدُ إِنَّكَ لَرَسُولُ اللَّـهِ"
“Watakapokujia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) wanafiki wakisema: Tunashuhudia kwamba wewe bila shaka ni Rasuli wa Allaah”.
Kisha Akasema baada ya kauli hii:
"اتَّخَذُوا أَيْمَانَهُمْ جُنَّةً فَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ"
“Wamefanya viapo vyao kuwa ni ngao, hivyo wakazuia Njia ya Allaah”. [Al-Munaafiquwn (63: 1 na 2)]. Wamesema: Allaah Ameuita ushuhuda wao kiapo.
‘Ulamaa wengine wamejibu hoja hii wakisema kuwa Aayaat haziko bayana kutolewa dalili juu ya hili kwa kuwepo uwezekano wa kuwa Kauli Yake Ta’aalaa:
اتَّخَذُوا أَيْمَانَهُمْ “Wamevifanya viapo vyao” hairejei ikafungamana na Kauli Yake:
نَشْهَدُ إِنَّكَ لَرَسُولُ اللَّـهِ “Tunashuhudia kwamba wewe bila shaka ni Rasuli wa Allaah, bali inarejea kwenye sababu ya kuteremshwa Aayaat, nayo ni kuwa ‘Abdullaah bin Ubayya aliapa aliyoyasema. Yamesemwa haya na Al-Qurtubiy.
Ninasema: “Kauli hii ya ‘Ulamaa hawa pengine inatiliwa nguvu na Hadiyth ya Ibn Mas-‘uwd aliyeripoti kwamba: “Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa: Ni watu wapi walio bora zaidi? Akasema:
" قَرْنِي ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ ثُمَّ الَّذِي يَلُونَهُمْ ثُمَّ يَجِيءُ قَوْمٌ تَسبِقُ شَهَادَة أحدِهمْ يَمِينه وَيَمِينه شَهَادَته"
“Ni kizazi changu [cha Maswahaba], kisha wale wanaowafuatia [cha Taabi’iyna], kisha kizazi kinachowafuatia [cha baada ya Taabi’iyna]. Halafu watakuja watu ambao ushahidi wa mmoja wao utatangulia kiapo chake, na kiapo chake ushahidi wake”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (6658) na Muslim (2533)].
Al-Haafidh kasema: “Mpishano wa maana uko wazi kati ya yamini na ushahidi”. [Fat-hul Baariy (11/544)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
013- Mwenye Kusema: وَايْمُ اللَّهِ “Waiymul Laah”
Alhidaaya.com [3]
Yamini inafungika kwa kusema hivyo. Hili limethibiti toka kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Katika Hadiyth ya ‘Aaishah, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
" وَايْمُ اللَّهِ، لَوْ أَنَّ فَاطِمَةَ بِنْتَ مُحَمَّدٍ سَرَقَتْ لَقَطَعَ مُحَمَّدٌ يَدَهَا"
“Naapa kwa Allaah, lau Faatwimah bint Muhammad angeiba, basi Muhammad angeukata mkono wake”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (6788) na Muslim (1688)].
Na katika Hadiyth ya Abu Hurayrah toka kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) -kuhusu kisa cha Nabiy Sulaymaan (‘Alayhis Salaam) ambapo aliapa kuwa atawazungukia wakeze 90 [usiku mmoja na kila mmoja atamzalia mtoto mpanda farasi atakayepigana Jihaad]-, Rasuli anasema:
"وَايْمُ الَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ لَوْ قَالَ إِنْ شَاءَ اللَّهُ، لَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فُرْسَانًا أَجْمَعُونَ "
“Naapa kwa Ambaye nafsi ya Muhammad iko Mkononi Mwake, lau angesema: In Shaa Allaah, basi wangelipigana Jihaad katika Njia ya Allaah wakiwa wote wapanda farasi”. [Hadiyth Swahiyhy. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (6639) na Muslim (1654)].
Asili ya " وَايْمُ اللَّهِ " ni " أَيْمٌنُ الله" aymunul Laah, nalo ni jina linalotumika kwa kiapo kwa maana ya “Yamini ya Allaah”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
014- Kuapa Kwa Asiye Allaah Ni Shirki
Alhidaaya.com [3]
Toka kwa Ibn ‘Umar kwamba alimsikia mtu mmoja akisema: Laa, naapa kwa Al-Ka’abah. Ibn ‘Umar akamwambia: Haapiwi asiye Allaah, kwani hakika mimi nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
"مَنْ حَلَفَ بِغَيْرِ اللَّهِ فَقَدْ أَشْرَكَ"
“Mwenye kuapa kwa asiye Allaah, basi hakika amefanya shirki”. [Hadiyth Hasan. Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (1535) na Abu Daawuwd (3251)].
Inatiliwa nguvu na Hadiyth ya Qutaylah –Mwanamke toka Juhaynah- :
"أَنَّ يَهُودِيًّا، أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ إِنَّكُمْ تُنَدِّدُونَ وَإِنَّكُمْ تُشْرِكُونَ تَقُولُونَ مَا شَاءَ اللَّهُ وَشِئْتَ وَتَقُولُونَ وَالْكَعْبَةِ . فَأَمَرَهُمُ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا أَرَادُوا أَنْ يَحْلِفُوا أَنْ يَقُولُوا " وَرَبِّ الْكَعْبَةِ " . وَيَقُولُونَ " مَا شَاءَ اللَّهُ ثُمَّ شِئْتَ "
“Kwamba Myahudi mmoja alikwenda kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: Hakika nyinyi mnamfanyia Allaah ulinganishi na viumbe, na hakika nyinyi mnamfanyia washirika. Mnasema: Alitakalo Allaah na ulitakalo [mnafanya sawa Matashi ya Allaah na matashi ya binadamu]. Na mnasema: Naapa kwa Al-Ka’abah. Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawaamuru [Maswahaba] waseme wanapotaka kuapa: Naapa kwa Mola wa Al-Ka’abah, na waseme: Alitakalo Allaah, kisha ulitakalo”. [Matashi ya mja yaje baada ya Matashi ya Allaah]. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na An-Nasaaiy (7/6) na Ahmad (6/371)].
Katazo la kuapa kwa asiye Allaah limekuja katika Hadiyth kadhaa. Kati ya Hadiyth hizo ni:
1- Hadiyth ya Abu Hurayrah. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لَا تَحْلِفُوا بِآبَائِكُمْ وَلَا بِأُمَّهَاتِكُمْ وَلَا بِالْأَنْدَادِ وَلَا تَحْلِفُوا إلا بِاللَّهِ، وَلَا تَحْلِفُوا إِلَّا وَأَنْتُمْ صَادِقُونَ"
“Msiape kwa baba zenu, wala kwa mama zenu, wala kwa viumbe wanaolinganishwa na Allaah. Na wala msiape isipokuwa kwa Allaah, na wala msiape isipokuwa mnasema kweli”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3248) na An-Nasaaiy (7/5)].
2- Toka kwa ‘Abdur Rahmaan bin Samurah amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
" لَا تَحْلِفُوا بِالطَّوَاغِي وَلَا بِآبَائِكُمْ"
“Msiape kwa masanamu wala kwa baba zenu”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1648), An-Nasaaiy (7/7) na Ibn Maajah (2095)].
3- Toka kwa Ibn Az Zubayr:
"أَنَّ عُمَرَ [17] لَمَّا كَانَ بِالْمَخْمَصِ مِنْ عُسْفَانَ اسْتَبَقَ النَّاسُ فَسَبَقَهُمْ عُمَرُ ، فقَالَ ابْنُ الزُّبَيْرِ : فَانَتهَزْتُ فَسَبَقْتُهُ ، فَقُلْتُ : سَبَقْتُه وَالْكَعْبَةِ، ثُمَّ انتهَزَ فَسَبَقَنِي ، فَقَالَ : سَبَقْتُه وَاللَّهِ ، ثُمَّ أَنَاخَ فَقَالَ : أَرَأَيْتَ حَلِفَكَ بِالْكَعْبَةِ ، وَاللَّهِ لَوْ أَعْلَمُ أَنَّكَ فَكَّرْتَ فِيهَا قَبْلَ أَنْ تَحْلِفَ لَعَاقَبْتُكَ ، احْلِفْ بِاللَّهِ فَأْثَمْ أو أبْرُرْ"
Kwamba ‘Umar alipokuwa Mahmasw akitokea ‘Usfaan, watu walishindana na ‘Umar akawatangulia. Ibn Az-Zubayr akasema: Nikavizia nafasi, nami nikamtangulia, nikasema: Nimemtangulia, naapa kwa Al-Ka’abah. Kisha naye akavizia nafasi, akanitangulia na akasema: Nimemtangulia, wa Allaah (naapa kwa Allaah). Kisha akamtua chini ngamia wake na kuniambia: Unaona ulivyoapa kwa Al-Ka’abah! Wa Allaah, lau ningelijua kwamba umekifikiria kiapo chako hicho kabla ya kukiapa, basi ningelikuadhibu. Apa kwa Allaah upate dhambi (kwa kuvunja kiapo chako), au ukitekeleze. [Isnaad yake ni Swahiyh. Imekharijiwa na ‘Abdul Razzaaq (15927) na Al-Bayhaqiy (10/29)].
4- Toka kwa Ibn Mas-‘uwd amesema:
" لأَنْ أَحْلِفَ باللهِ كاذِبًا أَحَبُّ إِليَّ مِنْ أَنْ أَحْلِفَ بِغَيْرِهِ صَادِقًا"
“Mimi kuapa kwa Allaah nikiwa mwongo ni nafuu zaidi kwangu kuliko kuapa kwa asiye Allaah nikiwa mkweli”. [Isnaad yake ni Swahiyh. Imekharijiwa na ‘Abdul Razzaaq (15929) na wengineo. Angalia Al-Irwaa (8/192)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
015- Masuala Mawili Tata Na Majibu Yake
Alhidaaya.com [3]
Suala La Kwanza: Ni Hadiyth:
" أَفْلَحَ وَأَبِيهِ إِنْ صَدَقَ"
“Atafaulu, naapa kwa baba yake, kama atasema kweli”… na mfano wa Hadiyth hii ya kuapa kwa baba au mama.
Imeelezwa katika baadhi ya Sanad za Hadiyth ya Twalha bin ‘Ubaydul Laah (Radhwiya Allaah ‘anhu) kuhusiana na kisa cha mtu ambaye alimuuliza Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu Uislamu, Rasuli akamweleza yale aliyofaradhiwa. Sehemu ya kisa inasema:
“Akauliza tena: Je, kuna jingine zaidi ya hilo nililofaradhishiwa? Akamwambia: Hapana, isipokuwa ukijitolea la ziada mwenyewe. Akasema: Mtu yule akageuka akiondoka na kusema: Wa Allaah, sizidishi zaidi ya haya wala sipunguzi chochote. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Atafaulu, [naapa kwa baba yake], kama atasema kweli, au: Ataingia Peponi [naapa kwa baba yake] kama atasema kweli”. [Ameikhariji kwa nyongeza hii Muslim (11) na Abu Daawuwd (392). Al-Bukhaariy hakuikhariji (46)].
Kuna Hadiyth nyingine kama hii. Ni ya Abu Hurayrah aliyesema:
"جَاءَ رَجُلٌ إلى النّبِيِّ صلّى الله عَلَيْهِ وَسَلّمَ، فَقَالَ: يا رَسُوْلَ اللهِ، أَيُّ الصَّدَقَةِ أَعْظَمُ أَجْرًا ؟ فَقَالَ: أَمَا وَأَبِيكَ لَتُنَبَّأَنَّهُ"
“Mtu mmoja alikuja kwa Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kumwambia: Ee Rasuli wa Allah! Ni Swadaqah ipi yenye malipo makubwa zaidi? Akasema: “Angalia, naapa kwa baba yako, hakika hilo utaelezwa…..”. [Muslim ameikhariji ikiwa na nyongeza hii (1032). Walioikhariji bila nyongeza hii ni Al-Bukhaariy (1419), Abu Daawuwd (2865) na An-Nasaaiy (3611)].
Pia Hadiyth nyingine ya Abu Hurayrah:
“Mtu mmoja alikuja kwa Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kumuuliza: Ni mtu yupi mwenye haki zaidi ya mimi kutangamana naye vizuri? Akamwambia: “Na’am, [naapa kwa baba yako] hakika utaelezwa. Ni mama yako……”. [Imekharijiwa na Muslim (2548), Ibn Maajah (2706), na Ahmad (2/327). Katika Sanad yake yupo Shurayk bin ‘Abdallah Al-Qaadhwiy].
Baadhi ya ‘Ulamaa –akiwemo Maalik na Ash-Shaafi’iy- wametolea dalili kwa kutumia riwaayaat hizi kuwa ni makruhu na si haramu kuapa kwa asiye Allaah!!
‘Ulamaa wameliraddi hilo kwa majibu kadhaa. Kati ya majibu hayo ni:
[Fat-hul Baariy (11/534) na Twarhut Tathriyb (7/145].
1- Kutothibiti nyongeza ya "وَأَبِيْهِ". Ibn ‘Abdul Barri ameashiria kuwa nyongeza hii haikuhifadhiwa. Kadhalika, baadhi ya ‘Ulamaa wamezungumzia shaka yao kuhusu kuthibiti neno lake Rasuli "وَأَبِيكَ لَتُنَبَّأَنَّ" .
Ninasema (Abu Maalik): “Tukijaalia kwamba ziada zote hizi zipo, basi tutakuta ‘Ulamaa wana maelekezo kwa Hadiyth hizi –pamoja na unadra wake- ambayo inabidi tukomee kwenye baadhi yake kutokana na kukhalifiana kwake na Hadiyth mashuhuri zilizo wazi ambazo tumezitaja nyuma zikikataza hilo (la kuapa kwa asiye Allaah). Kati ya maelekezo hayo ni:
2- Kwamba tamko hili (la naapa kwa baba yake n.k) lilikuwa limezoeleka ulimini mwao bila kukusudia kiapo halisi. Al-Bayhaqiy ameelemea kwenye mwono huu. An-Nawawiy kasema: “Ni jibu ridhishi”.
3- Kwamba tamko lilikuwa linatokea katika maneno yao kwa picha mbili. Kwanza kwa ajili ya utukuzisho, na pili kwa ajili ya usisitizo wa neno, na katazo linahusu picha ya kwanza ya utukuzisho.
4- Kwamba hili lilikuwa linajuzu hapo nyuma kisha likafutwa. Hili linaradiwa kwa kusemwa kuwa haiwezekani kwa Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa alikuwa anaapa kwa asiye Allaah kama ambavyo hawezi pia kuapa kwa mtu kafiri. Halafu madai ya kuwa hilo lilifutwa ni dhaifu, kwa kuwa upo uwezekano wa kukusanya nususi zote, kuzioanisha na kuzifanyia kazi.
5- Kwamba katika jawabu kuna neno limeondoshwa ambalo ni ,"رَبِّ"na taqdiyr yake ni:
" أَفْلَحَ وَرَبِّ أَبِيهِ" (Amefaulu naapa kwa Mola wa baba yake).
6- Ni kwa ajili ya mshangao. Linalodulisha hilo ni kutotumiwa neno: "وأَبِي" (Naapa kwa baba yangu), bali limetumika neno la "وَأَبِيهِ" (Naapa kwa baba yake), au "وَأَبِيك" (Naapa kwa baba yako) kwa kuegemezwa kiwakilishi cha msemeshwa aliyepo (yako) au asiyepo (yake).
7- Kwamba hilo linamhusu Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) peke yake, halimhusu mwingine yeyote katika Ummah wake.
Hili linaradiwa kwa kusema: Mambo maalumu yanayomhusu Rasuli hayathibiti kwa makisio, bali kwa dalili thabiti.
Ninasema: “Linaloonekana lenye nguvu zaidi ni kuwa kuapa kwa asiye Allaah ni haramu kutokana na dalili bayana kuhusiana na hilo. Ni kama neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"مَنْ حَلَفَ بِغَيْرِ اللَّهِ فَقَدْ أَشْرَكَ"
“Mwenye kuapa kwa asiye Allaah, basi hakika amefanya shirki”.
Haiwezekani kwa tamshi hili bayana la shirki kupindishwa na kupelekwa kwenye ukaraha. Na hili ni katika vinavyowekwa nje ya qaaidah (kanuni) isemayo: الْجَمْعُ أَوْلَى مِنْ التَّرْجِيْحِ “Kukusanya (nususi na kuzifanyia kazi zote) ni bora kuliko kuteua baadhi (kwa kuzipa nguvu) na kuacha nyingine”.
Suala La Pili: Allaah Ta’aalaa Kuapa Kwa Viumbe Vyake
Kati ya mambo ambayo wanayatolea dalili wenye kusema kuwa ni karaha kuapa kwa asiye Allaah na si haramu, ni kwamba Allaah Mtukufu Ameapa kwa Viumbe Vyake Mwenyewe kwenye Kitabu Chake. Amesema:
وَالسَّمَاءِ وَالطَّارِقِ
1. Naapa kwa mbingu na kinachokuja usiku.
Na:
وَالشَّمْسِ وَضُحَاهَا
1. Naapa kwa jua na mwangaza wake.
Na:
وَالْفَجْرِ
1. Naapa kwa Alfajiri.
وَلَيَالٍ عَشْرٍ
2. Na Naapa kwa masiku kumi.
Hili linajibiwa kwa majibu mawili:
Jibu La Kwanza: Ndani ya viapo hivi kumefichwa kiapo kwa Rabbi wa Viumbe hivi. Ni kama Amesema:
"وَرَبِّ السَّمَاءِ"
“Naapa kwa Rabbi wa mbingu”. Na:
"وَرَبِّ الشَّمْسِ"
“Naapa kwa Rabbi wa jua” na kama hivi.
Pili: Kuapa Allaah kwa Viumbe Vyake ni dalili juu ya Uwezo Wake na Uadhwama Wake. Anaapa kwa Kiumbe Chake chochote Akitakacho, na hakuna njia ya ulinganishi juu ya Viapo Vyake.
Ninasema: “Imejulikana kwamba wenye kusema kwamba si haramu kuapa kwa asiye Allaah, hawana chochote tena cha kukitegemea katika yote waliyoyatolea dalili”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
016- Mwenye Kuapa Kwa Asiye Allaah, Nini Afanye?
Alhidaaya.com [3]
Toka kwa Abu Hurayrah, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
" مَنْ حَلَفَ فَقَالَ فِي حَلِفِهِ: بِاللَّاتِ وَالْعُزَّى فَلْيَقُلْ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ. وَمَنْ قَالَ لِصَاحِبِهِ: تَعَالَ أُقَامِرُكَ فَلْيَتَصَدَّقْ "
“Mwenye kuapa akasema katika kiapo chake: Naapa kwa Al-Laata na Al-‘Uzza, basi aseme: Laa ilaaha illa Allaah. Na mwenye kumwambia mwenzake: Njoo tucheze kamari, basi atoe Swadaqah”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (6650) na Muslim (1647)].
Na Sa’ad bin Abiy Waqqaasw amesema:
"حَلَفْتُ بِاللاَّتِ وَالْعُزَّى، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : " قُلْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيْكَ لَهُ ثُمَّ انْفُثْ عَنْ يَسَارِكَ ثَلاَثًا وَتَعَوَّذْ وَلاَ تَعُدْ " .
“Niliapa kwa Allaata na Al-‘Uzza. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaniambia: Sema: Laa ilaaha illa Allaah wahdahu laa shariyka lahu. Kisha pulizia pulizia mate upande wako wa kushoto mara tatu, na jilinde kwa Allaah, na usirudie tena”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Ibn Maajah (2097), Ahmad (1/183) na wengineo. Ama kwa An-Nasaaiy (7/7), kuna nyongeza ya: “Laa ilaaha illa Allaahu wahdahu laa shariyka Lahu, mara tatu”. Nayo ni Dhwa’iyf kama ilivyotajwa katika Al-Irwaa (8/192)].
Na je hili ni kwa aliyeapa kwa Al-Laata na Al-‘Uzza tu, au linamhusu kila aliyeapa kwa kinginecho badala ya Allaah? Inavyoonekana ni kwa kila aliyeapa kwa kinginecho badala ya Allaah. Na kwa ajili hiyo, Sheikh wa Uislamu amesema: [Majmuw’u Al-Fataawaa (33/122)].
“…Kuapa kwa viumbe kama kuapa kwa Al-Ka’abah, wafalme, mababu, upanga na kadhalika, viapo hivi havina dhima ndanimwe, bali pia havifungiki na wala hana kafara atakayevivunja kwa makubaliano ya Waislamu wote. Bali atakayeapa kwa vitu hivyo, anatakiwa tu aseme “Laa ilaaha illa Allaah wahdahu laa shariyka lahu” kama alivyosema Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa sallam)…”. Kisha akataja Hadiyth ya Abu Hurayrah iliyotangulia.
……………………….
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
017- Kuapa Kwa Amana
Alhidaaya.com [3]
Haifai kuapa kwa amana. Ni kwa Hadiyth ya Buraydah (Radhwiya Allaah ‘anhu), amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
" مَنْ حَلَفَ بِالأَمَانَةِ فَلَيْسَ مِنَّا "
“Mwenye kuapa kwa amana, basi si katika sisi”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3253), Ibn Hibaan (1318) na Al-Bayhaqiy (10/30)].
Kwa maana si katika wenye kufuata njia yetu, bali ni mwenye kujishabihisha na wengineo, na hii ni tabia ya Ahlul Kitaab. Huenda amekusudia kwalo makamio juu yake. [‘Awn Al-Ma’abuwd (9/79 na 80)].
Ikiwa ataongeza Jina la Allaah kwenye tamko la amana akasema: “Naapa kwa Amana ya Allaah”, baadhi ya ‘Ulamaa wamesema itazingatiwa ni kiapo chenye kuwajibisha kafara, kwa kuwa Amana ya Allaah ni Sifa kati ya Sifa Zake, hivyo inajuzu kuapa hivyo!!
Lakini hapa kuna angalizo. Tunasema hakuna dalili thibitishi kuwa Amana ni Sifa kati ya Sifa za Allaah, bali ni Amri kati ya Amri Zake, na Faradhi kati ya Faradhi Zake. Kwa ajili hiyo, wamekatazwa watu kuapia kwalo kwa sababu hilo ni kufanya sawa kati yake na kati ya Majina ya Allaah Ta’aalaa na Sifa Zake. [Ma’aalim As-Sunan cha Al-Khattwaabiy].
Isitoshe, imethibiti katazo la kuapa kwa amana. Hivyo, rai sahihi ni kuwa, haijuzu kabisa kuapa kwa neno hilo. Na hii ni kauli ya Mahanafiy. Na Ibn ‘Abdul Barri na wengineo wameinasibisha kwa Ash-Shaafi’iy. [Al-Badaai’u (3/6), Al-Mughniy (11/207) na At-Tamhiyd (14/372)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
018- Kuapa Kwa Mila Isiyo Ya Uislamu
Alhidaaya.com [3]
Rasuli amesema :
"مَنْ حَلَفَ بِمِلَّةٍ سِوَى الإِسْلاَمِ كَاذِبًا مُتَعَمِّدًا فَهُوَ كَمَا قَالَ، وَمَنْ قَتَلَ نَفْسَهُ بِشَىْءٍ عَذَّبَهُ اللَّهُ بِهِ فِي نَارِ جَهَنَّمَ "
“Mwenye kuapa kujinasibisha na dini nyingine isiyo Uislamu kwa uongo wa kusudi, basi anakuwa kama alivyojinasibishia. Na yeyote mwenye kujiua kwa kitu chochote, Allaah Atamwadhibu nacho ndani ya Moto wa Jahannam”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (1363) na Muslim (110)].
Na Hadiyth ya Buraydah, amesema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"مَنْ حَلَفَ فَقَالَ: إِنِّي َبَرِيْءٌ مِنَ الإِسْلامِ، فَإِنْ كَانَ كَاذِبًا، فَهُوَ كَمَا قَالَ، وَإِنْ كَانِ صَادِقًا، فَلَنْ يَرْجِعَ إِلَى الإِسْلامِ سَالِمًا"
“Mwenye kuapa akasema: Mimi nitaachana na Uislamu, ikiwa amesema uongo, basi anakuwa kama alivyosema. Na kama amesema kweli, basi hatorudi akiwa salama katika Uislamu”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3258), An-Nasaaiy (3772), Ibn Maajah (2100) na Ahmad (5/356)].
Kisha ‘Ulamaa wamekhitalifiana kuhusu kama kiapo hiki ni cha kishariah au la.
Maalik, Ash-Shaafi’iy, Ahmad katika moja ya riwaya mbili, Al-Layth, Abu Thawr na Ibn Al-Mundhir wamesema si kiapo, na dalili yao ni kuwa hakikuapiwa kwa Jina la Allaah wala kwa Sifa Yake. Hivyo hakiwi kiapo na hakuna kafara ndani yake.
Lakini Mahanafi, Ahmad katika -riwaayah nyingine-, Al-Hasan, Ath-Thawriy, Al-Awzaa’iy na Is-Haaq, ikiwa pia ni chaguo la Sheikh wa Uislamu wamesema ni kiapo, kwa kuwa amefungamanisha kutokufanya kitendo na ukafiri wake ambao ni kujiweka mbali na Allaah. Hivyo anakuwa ameunganisha kitendo na iymaan yake kwa Allaah. Na huu hasa ndio uhakika wa kuapa kwa Allaah. Hivyo, kuunganisha kitendo na Ahkaam za Allaah kati ya kuwajibisha au kuharamisha ni hali hafifu zaidi kuliko kukiunganisha na Allaah moja kwa moja. Na kwa muktadha huu, akivunja kiapo, ni lazima kafara.
· Hukmu Kwa Mwapaji Mwenyewe
Kama atakuwa ni mwongo (yaani hakusudii kikweli ukafiri), na kwa kiapo chake hicho alikuwa anakusudia kujiepusha mwenyewe na kitu au kujihimizia kwacho, basi anakuwa hakukufuru. Lakini pamoja na hivyo, atakuwa ameingia ndani ya wigo wa makamio makali. Na kama alikusudia kwa neno hilo kuridhia ukafiri kama atalifanya jambo, basi hapo hapo anakuwa kafiri.
Ama akiwa ni mkweli (anakusudia kweli ukafiri), basi hawi salama, kwa kuwa ndani yake kuna aina ya dharau kwa Uislamu, na atapata madhambi kwa kiapo hicho hicho. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
019- Aina Za Yamini Za Viapo: Yamini Ya Upuuzi
Alhidaaya.com [3]
Tumesema nyuma kwamba yamini za Waislamu zinakuwa ima za kiapo au za shurutisho (sharti na matokeo yake, yaani; likifanyika hili, litafanyika lile). Ama yamini za viapo, hizi ziko za aina tatu kwa upande wa kufungika kwake na kwa upande wa wajibu wa kutoa kafara mtu akivivunja. Na zifuatazo ndizo aina hizi tatu pamoja na vidokezo vya ahkaam husika kwa kila aina:
Aina Ya Kwanza: Yamini Ya Upuuzi
· Taarifu Yake:
Allaah Ta’aalaa Amesema:
لَّا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا كَسَبَتْ قُلُوبُكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ ﴿٢٢٥﴾
225. Allaah Hatokushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini Atakuchukulieni kwa yaliyochuma nyoyo zenu. Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mpole, Mvumilivu. [Al-Baqarah].
‘Ulamaa wamekhitalifiana kwa kauli kadhaa katika kufasiri maana ya “Yamini ya upuuzi”. Kauli mashuhuri zaidi ni mbili ambapo kila mojawapo inabeba maana ya neno upuuzi.
Kauli Ya Kwanza: Upuuzi ni neno linaloteleza ulimini bila kukusudia yamini kama kusema: “Laa, wa Allaah لا وَاللهِ” au “Balaa, wa Allaah بَلَى وَاللهِ ” ambapo mtu husema katika hali ya kuunga maneno yake, au katika hali ya ghadhabu, ni sawa likiwa hilo kwa wakati uliopita, au uliopo, au ujao.
Hii ni kauli ya Ash-Shaafi’iy na Hanbali ambao kigezo chao ni kauli ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa) alipoizungumzia Kauli Yake Ta’aalaa:
لَّا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ
Allaah Hatokushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi….ambapo alisema:
" أُنزِلَ فِي قَوْلِه : لا وَاللهِ، وَبَلى وَاللهِ"
“Imeteremshwa kuhusu neno la mtu kusema: Laa, wa Allaah na balaa wa Allaah”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (6663) na ‘Abdur Razzaaq (15952)].
Amesema pia ‘Aaishah:
"أيمانُ اللَّغْوِ ما كَانَ فِي الْهَزْلِ و المِراءِ وَالْخُصُوْمَةِ، وَالْحَدِيْثُ الَّذِيْ لا يُعقَدُ عَلَيْه القَلْبُ"
“Yamini za upuuzi ni zile zinazokuwa katika mzaha, mabishano na ugomvi, na maneno ambayo hayajakusudiwa na moyo.” [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na At-Twabariy (2/245) na Al-Bayhaqiy (10/49)].
Na kwa vile pia Allaah Taa’alaa Ameikabilisha yamini ya upuuzi katika Aayah Tukufu na yamini iliyochumwa na moyo (kuonyesha tofauti kati yao). Iliyochumwa na moyo ni ile iliyokusudiwa, hivyo isiyokusudiwa inaingia katika kigawanyo cha yamini za upuuzi bila kupambanua kati ya wakati wake uliopita, au wakati wake uliopo, au wakati wake ujao ili ulinganishi ufanikike.
Kauli Ya Pili: Upuuzi ni mtu kuapa juu ya kitu anachokiitakidi kwa njia ya uhakika kamili au dhana isiyo na shaka kuwa ndicho, kisha inabainika ndivyo sivyo. (Ni kama kuapa kuwa ndege yule ni kware, kumbe ni njiwa).
Ni kauli ya Hanafiy na Maalik. Kigezo chao ni yaliyothibiti toka kwa Zaraarah bin Awfaa (Radhwiya Allaah ‘anhu) aliyesema:
"هُوَ الرَّجُلُ يَحْلِفُ عَلى الْيَمِيْنِ لا يَرَى إِلَّا أَنَّهَا كَمَا حَلَفَ"
“Ni mtu anaapa yamini haoni isipokuwa kwamba yamini iko kama alivyoapa”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na At-Twabariy (2/245)].
Ninasema: “Kauli mbili zimekaribiana, na upuuzi umo ndani ya zote mbili. Kwa kuwa, katika tafsiri ya kwanza, hakukusudia kabisa kufunga yamini. Na katika ya pili, hakudhamiria kuvunja kiapo na wala hakukusudia isipokuwa kweli ambayo ana uhakika nayo. Allaah Ndiye Mjuzi wa yote”. [Al-Muhallaa (8/34), Al-Mughniy (11/181) na Adhwaaul Bayaan (2/108)].
· Hukmu Ya Kiapo Cha Upuuzi
Allaah Ta’aalaa Amesema:
"لَّا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ"
“Allaah Hatokushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi”. [Al-Baqarah (2:225)].
Aayah inadulisha kuwa Allaah Hatomwadhibu mtu kwa kiapo cha upuuzi. Hii inahusu dhambi na kafara, kwa maana, hakuna dhambi, hakuna kafara.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
020- Aina Za Yamini Za Viapo: Yamini Ya “Ghamuws”
(Ya Uongo Ili Kudhulumu Haki Ya Mtu)
Alhidaaya.com [3]
1- Taarifu Yake:
Ni mtu kuapa juu ya jambo lililokwishapita akikusudia uongo ili amege kwa kiapo hiki haki ya mtu mwingine. Kinaitwa pia “Yamiyn Az-Zuwr” na “Yamiyn Al-Faajirah”. Na katika Hadiyth kimeitwa kiapo cha “Swabr” (yaani, ambacho mtu anajifunga mwenyewe ndani yake ili ahakikishe anapata lengo lake kwa kiapo hicho).
Amesema katika An-Nihaayah: Imeitwa “ghamuws”, kwa kuwa itamtosa mwapaji wake ndani ya moto.
· Hukmu Yake:
Ni dhambi kati ya madhambi makubwa, na mwapaji wake anapata dhambi kwa itifaki ya Waislamu wote.
(a) Toka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amri kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"الكَبَائِرُ : الإشْرَاكُ بِاللهِ ، وَعُقُوْقُ الوَالِدَيْنِ ، وَقَتْلُ النَّفْسِ ، وَاليَمِيْنُ الغَمُوْسُ"
“Madhambi makubwa: Ni kumshirikisha Allaah, kutowatii na kuwaasi wazazi wawili, kuua nafsi, na yamini ya uongo wa kukusudia”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (6675), An-Nasaaiy katika Al-Kubraa (6/322) na At-Tirmidhiy (3021)].
(b) Toka kwa Abu Umaamah, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"مَنِ اقْتَطَعَ حَقَّ امْرِئٍ مُسْلِمٍ بِيَمِيْنِهِ فَقَدْ أَوْجَبَ اللهُ لَهُ النَّارَ، وَحَرَّمَ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ” فَقَالَ رَجُلٌ: وَإِنْ كَانَ شَيْئًا يَسِيْرًا يَا رَسُوْلَ اللهِ ؟ فَقَالَ: “وَإِنْ قَضِيبًا مِنْ أَرَاكٍ"
“Yeyote mwenye kumega haki ya mtu Muislamu kwa kutumia kiapo chake, basi hakika Allaah Amemwajibishia moto, na Amemharamishia Pepo. Mtu mmoja akasema: Hata japo kitu kidogo ee Rasuli wa Allaah? Akasema: Hata japo kijiti cha mti wa mswaki”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (137) na Ibn Maajah (2324)].
(c) Ibn Mas-‘uwd (Radhwiya Allaah ‘anhu) amesema, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"مَنْ حَلَفَ عَلَى يَمِينِ صَبْرٍ وَهُوَ يَقْتَطِعُ بِهَا مَالَ امْرِئٍ مُسْلِمٍ لَقِيَ اللَّهَ وَهُوَ عَلَيْهِ غَضْبَانُ"
“Mwenye kuapa yamini ya “swabr” (ya uongo) ili amege kwayo mali ya mtu Muislamu, basi atakutana na Allaah Akiwa na hasira naye”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (6676) na Muslim (38)].
(d) Abu Dharri amepokea toka kwa Nabiy (Swallah Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
"ثَلَاثَةٌ لَا يُكَلِّمُهُمُ اللَّهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ، وَلَا يَنْظُرُ إِلَيْهِمْ، وَلَا يُزَكِّيهِمْ، وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ –ثَلاثًا- قَالَ أَبُوْ ذَرٍّ: خَابُوا وَخَسِرُوا مَنْ هُمْ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ قَالَ: «الْمُسْبِلُ وَالْمَنَّانٌ وَالْمُنَفِّقُ سِلْعَتَهُ بِالْحَلِفِ الْكَاذِبِ"
“Watu watatu, Allaah Hatowasemesha Siku ya Qiyaamah, wala Hatowaangalia wala Hatowatakasa, na watakuwa na adhabu iumizayo –akasema mara tatu- Abu Dharri akasema: Wamepita utupu na wamekula hasara, ni nani hao ee Rasuli wa Allaah? Akasema: Mwenye kuteremsha nguo yake chini ya vifundo vya miguu, msimbuliaji na mchuuzi wa bidhaa zake kwa kiapo cha uongo”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (106), Abu Daawuwd (4087), An-Nasaaiy (2563), At-Tirmidhiy (1121) na Ibn Maajah (2208)].
· Je, Kiapo Cha Ghamuws Kinaruhusiwa Kwa Dharura?
Hapana shaka yoyote kwamba kiasli, kiapo cha uongo ni haramu. Lakini kinaweza kukabiliwa na mazingira halali ya kukitoa nje ya duara la uharamu na kukihalalisha. Ni kama Muislamu aliyejificha kumkimbia dhalimu, kisha mtu akaulizwa kama amemwona. Hapo ni lazima aongope ili kumficha, na hata akitakwa aape, basi ni lazima aape na atumie “tawriyah” (neno lenye kubeba maana mbili; ya juu dhahiri na ya ndani fiche) katika kiapo chake. Kama ataapa na hakutumia neno hilo, hapa pana makhitalifiano. Kuna baadhi wamesema atakuwa amevunja kiapo, na wengine wamesema atakuwa hakukivunja.
Kigezo cha ruksa ya kuapa kutokana na kulazimika, ni Kauli Yake Ta’aalaa:
مَن كَفَرَ بِاللَّـهِ مِن بَعْدِ إِيمَانِهِ إِلَّا مَنْ أُكْرِهَ وَقَلْبُهُ مُطْمَئِنٌّ بِالْإِيمَانِ وَلَـٰكِن مَّن شَرَحَ بِالْكُفْرِ صَدْرًا فَعَلَيْهِمْ غَضَبٌ مِّنَ اللَّـهِ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴿١٠٦﴾
106. Atakayemkufuru Allaah baada ya iymaan yake - isipokuwa yule aliyekirihishwa (kukanusha) na huku moyo wake umetua juu ya iymaan - lakini aliyekifungulia ukafiri kifua chake, basi hao juu yao ni ghadhabu kutoka kwa Allaah na watapata adhabu kuu. [An-Nahl].
Ikiwa kulazimishwa kunahalalisha neno la ukafiri, basi kuhalalishwa kiapo cha uongo ni ruksa zaidi.
Toka kwa Suwayd bin Handhwalah amesema:
"خَرَجْنَا نُرِيدُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ، وَمَعَنَا وَائِلُ بْنُ حُجْرٍ فَأَخَذَهُ عَدُوٌّ لَهُ فَتَحَرَّجَ الْقَوْم أَنْ يَحْلِفُوْا فَحَلَفْتُ أَنَا أَنَّهُ أَخِيْ، فَذَكَرْتُ ذلِكَ لِلنَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: "صَدَقْتَ ، الْمُسْلِمُ أَخُوْ الْمُسْلِمِ "
“Tulitoka kwenda kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) tukiwa pamoja na Waail bin Hujr. Maadui zake wakamkamata, na watu wakaona uzito kuapa. Mimi nikaapa kuwa ni ndugu yangu. Nikamweleza hilo Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) naye akasema: Umesema kweli, Muislamu ni ndugu ya Muislamu”. [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3070), Ibn Maajah (2119), Al-Haakim (4/333) na wengineo].
· Je, Kafara Ni Lazima Katika Yamini Ya Ghamuws?
‘Ulamaa wana kauli mbili kuhusu suala hili: [Angalia Fat-hul Qadiyr (4/3), As-Swaawiy (1/330), Asnal Matwaalib (4/240), Al-Mughniy (11/177), Al-Muhallaa (8/36), Majmuw’ul Fataawaa (33/128-35/324) na Fat-hul Baariy (11/557)].
Kauli Ya Kwanza: Haina kafara, bali ni lazima kutubia kwa kuapa na kuwarejeshea watu haki yao. Ni madhehebu ya Jumhuri. Dalili yao ni:
1- Hadiyth zilizotangulia zinazowakhofisha watu waepuke yamini ya ghamuws.
2- Ni Al-Ash-‘ath aliposema -kuhusu Hadiyth iliyotangulia ya Ibn Mas-‘uwd-:
"فِيَّ أُنْزِلَتْ هذِهِ الآيَاتُ وَهِيَ قَوْلُهُ تَعَالى : إِنَّ الَّذِينَ يَشْتَرُونَ بِعَهْدِ اللَّـهِ وَأَيْمَانِهِمْ ثَمَنًا قَلِيلًا أُولَـٰئِكَ لَا خَلَاقَ لَهُمْ فِي الْآخِرَةِ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ اللَّـهُ وَلَا يَنظُرُ إِلَيْهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٧﴾
“Aayaat hizi ziliteremshwa kunizungumzia mimi, nayo ni Kauli Yake Ta’aalaa:
77. Hakika wale wanaobadilisha Ahadi ya Allaah na viapo vyao kwa thamani ndogo, hao hawana sehemu yoyote katika Aakhirah, na wala Allaah Hatowasemesha, na wala Hatowatazama Siku Ya Qiyaamah, na wala Hatowatakasa, na watapata adhabu iumizayo. [Aal ‘Imraan].
Wamesema: “Matini hizi zimethibitisha kuwa hukmu ya ghamuws ni adhabu Aakhirah. Hivyo mwenye kuwajibisha kafara, basi amezidisha lisilokuwepo ndani ya matini”.
3- Hadiyth ya Abu Hurayrah toka kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"خَمْسٌ لَيْسَ فِيهِنَّ كَفَّارَةُ : الشِّرْكُ بِاللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ، وَقَتْلُ النَّفْسِ بِغَيْرِ حَقِّ، وَبُهْتُ الْمُؤمِنِ، وَالْفِرَارُ مِنَ الزَّحْفِ ، ويَمِينٌ صابِرَةً يَقْتَطِعُ بِهَا مَالَا بِغَيْرِ حَقِّ"
“Matano hayana kafara: Kumshirikisha Allaah ‘Azza wa Jalla, kuua nafsi bila haki, kumzulia Muumini, kukimbia Jihaad, na yamini ya ghamuws anamega kwayo mali pasina haki”. [Hadiyth Dhwa’iyf. Imekharijiwa na Ahmad (2/362), At-Twabaraaniy katika “Musnadu Ash-Shaamiyyiyna” (1183), Ibn Abi ‘Aaswim katika “Al-Jihaad” na katika “Ad-Diyaat” (1/16)].
4- Toka kwa Ibn Mas-‘uwd amesema:
"كُنَّا نَعُدُّ الذَّنْبَ الَّذِيْ لَا كَفَّارَةَ لَهُ الْيَمِيْنَ الْغَمُوْسَ ، فَقِيْلَ : مَا الْيَمِيْنُ الْغَمُوْسُ؟ قَالَ : اقْتِطَاعُ الرَّجُلِ مَالِ أَخِيْهِ بِالْيَمِيْنِ الْكاذِبَةِ "
“Tulikuwa tunahesabu kati ya dhambi zisizo na kafara ni yamini ya ghamuws. Pakaulizwa: Ni ipi yamini ya ghamuws? Akasema: Ni mtu kumega mali ya nduguye kwa kiapo cha uongo”. [Isnaad yake ni Hasan. Imekharijiwa na Al-Bayhaqiy (10/383)].
Wamesema: “Hakuna Swahaba yeyote tumjuaye ambaye alipingana na Ibn Mas-‘uwd, bali hata Wanazuoni kadhaa wamenukuu itifaki ya Maswahaba wote juu ya hilo”.
5- Yamini hii ni kubwa zaidi ya kutolewa kafara, na madhambi makubwa hayatolewi kafara. Ni kama kuiba, kuzini na kunywa pombe, haya hayana kafara.
Kauli Ya Pili: Yamini ina kafara. Ni madhehebu ya Ash-Shaafi’iy, riwaya toka kwa Ahmad na Ibn Hazm. Hoja yao ni:
1- Ghamuws ni yamini iliyochumwa, iliyokusudiwa, na chumo ni tendo la moyo. Na kukusudia ni kuazimia, na yeyote mwenye kuapa kwa uwongo na kwa kukusudia, basi huyo ni mtendaji kwa moyo wake kwa kupania. Huyu atawajibishwa kwa mujibu wa Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا كَسَبَتْ قُلُوبُكُمْ"
“Lakini Atakuchukulieni kwa yaliyochuma nyoyo zenu”. [Al-Baqarah (2:225)].
2- Allaah Ta’aalaa Amesema:
"لَا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا عَقَّدتُّمُ الْأَيْمَانَ ۖ فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِ مَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ أَوْ كِسْوَتُهُمْ أَوْ تَحْرِيرُ رَقَبَةٍ ۖ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ ۚ ذَٰلِكَ كَفَّارَةُ أَيْمَانِكُمْ إِذَا حَلَفْتُمْ"
89. “Allaah Hatokuchukulieni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini Atakuchukulieni kwa (kuvunja) viapo mlivyoapa kwa niyyah mlioifunga thabiti. Basi kafara yake ni kulisha maskini kumi chakula cha wastani mnachowalisha ahli zenu, au kuwavisha nguo, au kuacha huru mtumwa. Lakini asiyeweza kupata (katika hayo), basi afunge Swiyaam siku tatu. Hiyo ndio kafara ya viapo vyenu mnapoapa”. [Al-Maaidah: 5].
Hapa Aayah inaeleza kuwa inaingia kiujumla kila yamini ambayo mwapaji wake ameivunja. Na kafara haifutiki ila kwa dalili bayana.
3- Neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"فَلِيَأْتِ الَّذِيْ هُوَ خَيْرٌ وَيُكَفِّرْ عَنْ يَمِينهِ"
“…..basi na afanye lile alionalo la kheri zaidi, na atolee kafara yamini yake”. [Isnaad yake ni Hasan. Imekharijiwa na Al-Bayhaqiy (10/38)].
Wamesema: Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) akamwamuru akivunje kiapo chake na akamwajibishia kafara.
4- Yamini ya ghamuws inastahiki zaidi kutolewa kafara kuliko yamini nyinginezo zilizoazimiwa, kwa kuwa uwazi wa Aayah mbili zilizotangulia unatekelezeka juu yake bila “taqdiyr” (kuchomeka neno ili maana kusudiwa ikae sawa). Pia kiapo hiki kinakuwa batili na chenye kuvunjika tokea pale anapokikusudia mtu na kukitamka. Hivyo adhabu inakutanishwa na kiapo hiki kinyume na viapo vingine vilivyoazimiwa ambavyo havina adhabu ila tu kama vitavunjwa. Viapo hivi ili Aayah hizi mbili zitekelezeke juu yake, zinahitajia “taqdiyr” kwa kusemwa:
"وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بالحنث بِمَا كَسَبَتْ قُلُوبُكُمْ"
“Lakini Atakuchukulieni kwa kuvunja yaliyochuma nyoyo zenu”.
Na katika Kauli Yake:
"إِذَا حَلَفْتُمْ" أَيْ : حَلَفْتُمْ وَحَنَثْتُمْ
“mnapoapa na mkavunja kiapo”.
· Kauli Yenye Nguvu:
Linaloonekana ni kuwa kutowajibishwa kafara ndiko kwenye nguvu zaidi. Dalili za wenye kupinga hili zinaradiwa kwa kuambiwa kuwa yamini ya ghamuws si yamini kiuhalisia, kwa kuwa yamini ni kifungo halali cha kisheria, lakini ghamuws ni dhambi kubwa lisilo na shaka yoyote, na dhambi kubwa ni kinyume ya jambo halali la kisheria. Na yamini hii ya ghamuws imeitwa yamini kimajazi tu kwa kuwa inafanyika katika picha ya kiapo. Isitoshe, yamini inakuwa ni ghamuws kwa kuwa mtu anakusudia kusema uongo na hana niya ya kuivunja. Hivyo Hadiyth haitoshelezi kwa dalili.
Na yaliyotangulia katika mlango wa “Al-Li’aan” (mume kumtuhumu mkewe zinaa) yanatilia nguvu hili pale Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) alipowaambia wenye kulaaniana wawili:
" اللَّهُ يَعْلَمُ أَنَّ أَحَدَكُمَا كَاذِبٌ، فَهَلْ مِنْكُمَا تَائِبٌ "
“Allaah Anajua kwamba mmoja wenu ni mwongo, basi je mmoja wenu atatubu?”. [Hadiyth Swahiyh].
Lau kama kafara ingekuwa ni lazima kwa mmoja wao kwa kuwa amekusudia uongo, basi kubainisha hilo kungehitajika zaidi kuliko kubainisha suala la tawbah. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi lililo sahihi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
021- Aina Za Yamini Za Viapo: Yamini Aliyojifunga Nayo Mtu
Alhidaaya.com [3]
· Taarifu Yake:
Ni yamini kwa jambo la kulifanya mbeleni ambalo kiakili linawezekana, ni sawa ikiwa ni kwa kutolifanya au kulifanya. Ni kama kusema: “Wa Allaah, sitofanya kadhaa”. Au: “Wa Allaah, lazima nitafanya kadhaa”.
Mwapaji anakuwa ameazimia kwa moyo wake kufanya au kutofanya kisha ulimi wake unaeleza hayo kwa yamini.
Taarifu nyingine inasema kuwa ni kiapo kisicho cha ghamuws au jambo la kipuuzi.
· Masharti Yake:
Ili kiapo hiki kiwe ni cha mtu kujifunga nacho, ni lazima yawepo masharti ambayo baadhi yake yanamhusu mwapaji, mengine yanalihusu jambo linaloapiwa, na mengine yanalihusu tamshi. Haya matatu ndiyo nguzo ya yamini hii.
(a) Masharti Ya Mwapaji
Ili kiapo cha mwapaji kifungike, ni lazima awe na masharti yafuatayo:
1- Awe amebaleghe. 2- Awe na akili timamu. 3- Awe Muislamu (kwa Mahanafiy na Wamaalik).
Yamini ya kuapa kwa Allaah Ta’aalaa haifungiki kwa kafiri hata akiwa ni “dhimmiy” (kafiri aishiye chini ya himaya ya Dola ya Kiislamu). Lakini Mashaafi’iy na Mahanbali wamesema kuwa Uislamu sio sharti ya kufungika kiapo au kubakia kwake. Wanasema lau “dhimmiy” ataapa kwa Allaah kisha akavunja kiapo chake –naye ni kafiri- basi lazima atoe kafara. Na kama atashindwa kutoa kafara kwa kulisha, basi hatofanya kafara kwa kufunga mpaka atakaposilimu.
4- Kiapo kitamkwe kwa ulimi.
Haitoshi kiapo cha ndani ya nafsi. Hili ni kwa mujibu wa Jumhuwr kinyume na baadhi ya Wamaalik.
5- Kukusudia.
Kwa kuwa mtu haadhibiwi isipokuwa kwa kulikusudia jambo na kulipania. Na kwa ajili hiyo, Allaah Ta’aalaa Ameipomosha kafara ya kiapo cha upuuzi.
6- Kuwa na hiari.
Kama atakosea au akalazimishwa, basi kiapo hakifungiki, na hatoadhibiwa. Hii ni kauli yenye nguvu ya Jumhuwr kinyume na Mahanafiy. Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam):
"إنَّ اللَّهَ تَجَاوَزَ لِي عَنْ أُمَّتِي الْخَطَأَ وَالنِّسْيَانَ وَمَا اسْتُكْرِهُوا عَلَيْهِ" .
“Hakika Allaah Ameusamehe Umati wangu kwa ajili yangu wakikosea, wakisahau na kwa yale waliyolazimishiwa”. [Hadiyth Hasan].
(b) Masharti Ya Jambo Linaloapiwa
1- Liwe ni jambo la wakati ujao, kwa kuwa yamini juu ya jambo lililokwishapita haina kafara kwa mujibu wa kauli yenye nguvu –kama ilivyotangulia-, na kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam):
"فيُكَفِّرْ ، وَلِيَأْتِ الَّذِيْ هُوَ خَيرٌ "
“Basi atoe kafara, na afanye lile lililo la kheri zaidi”. [Hadiyth Swahiyh. Itakuja kwa ukamilifu pamoja na takhriyj yake].
2- Liwe na picha ya uhalisia wa kuwepo wakati wa kuapa (lisiwe jambo lisilowezekanika).
(c) Masharti Ya Tamko La Kiapo
1- Kiapo kisiwe kwa kiumbe. Dalili za sharti hili zimeshatajwa mwanzoni mwa mlango huu.
2- Asiachanishe kati ya mwenye kuapiwa (Allaah) na lenye kuapiwa (jambo) kwa mnyamao na mfano wake.
3- Kiapo kisiwe na tamshi la: “In Shaa Allaah”, yaani kufungamanisha na Matakwa ya Allaah na mfano wa hilo kwa namna isiyoleta picha ya kuweza kukivunja. Hili litabainishwa mbeleni In Shaa Allaah.
· Hukmu Ya Kutekeleza Na Kukivunja Kiapo Hiki
Yamini yenye kufungika inakuwa ima:
(a) Kwa kuapa kufanya jambo la waajib, au kuacha maasia. Ni kama kusema: “Wa Allaah, nitaswali Adhuhuri”, au “Wa Allaah, sitoiba usiku”. Kiapo hiki ni lazima kukitekeleza, na kukivunja ni haramu bila makhitalifiano.
(b) Au kuapa kufanya maasia au kuacha la waajib. Kiapo hiki ni haramu kukitekeleza, na ni waajib kukivunja.
Mfano wa hili ni mtu kuapa yamini kuhusu mkewe na wanawe ambapo kama hatoivunja basi watapata madhara, na kuivunja kunakuwa sio ma’aswiyah. Hapo anatakiwa avunje kiapo chake, afanye hilo jambo, na atoe kafara ya kiapo chake. Imesimuliwa na Abu Hurayrah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) amesema:
" وَاللَّهِ لأَنْ يَلِجَّ أَحَدُكُمْ بِيَمِينِهِ فِي أَهْلِهِ آثَمُ لَهُ عِنْدَ اللَّهِ مِنْ أَنْ يُعْطِيَ كَفَّارَتَهُ الَّتِي افْتَرَضَ اللَّهُ عَلَيْهِ "
“Naapa kwa Allaah, hakika mmoja wenu kushikilia atekeleze kiapo chake kwa watu wake (ambapo watadhurika) ni madhambi makubwa zaidi kwake mbele ya Allaah kuliko kutoa kafara yake ambayo Allaah Amemfaradhishia”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al Bukhaariy (6624) na Muslim (1655)].
(c) Au kuapa kufanya jambo lililosuniwa au kuacha jambo ambalo ni makruhu. Ni kama kusema: “Wa Allaah, nitaswali Sunnah ya As Subh”, au “Sitogeuka ndani ya Swalaah yangu”. Hapa kutekeleza kiapo inakuwa ni jambo linalopendeza na kukivunja ni makruhu. Na baadhi ya ‘Ulamaa wamesema: Bali ni waajib kukitekeleza na haijuzu kukivunja kutokana na Neno Lake Ta’aalaa:
"وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ"
“Na hifadhini yamini zenu.” [Al-Maaidah: 89].
(d) Au kuapa kufanya jambo la makruhu au kuacha jambo la Sunnah. Hapa itapendeza kuvunja kiapo na kutoa kafara, na itakuwa makruhu kukitekeleza. Ni kutokana na neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam):
" مَنْ حَلَفَ عَلَى يَمِينٍ فَرَأَى غَيْرَهَا خَيْرًا مِنْهَا فَلْيُكَفِّرْ عَنْ يَمِينِهِ وَلْيَفْعَلْ "
“Mwenye kuapa kiapo, kisha akaona jingine ni bora zaidi kuliko aliloliapia, basi atoe kafara kwa kiapo chake, na alifanye (hilo lililo bora zaidi). [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al Bukhaariy (1650) na At Tirmidhiy (1530)].
Na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) alimwambia ‘Abdul Rahmaan bin Samurah:
"وإذا حَلَفْتَ علَى يَمِينٍ، فَرَأَيْتَ غَيْرَها خَيْرًا مِنْها، فَكَفِّرْ عن يَمِينِكَ، وأْتِ الَّذِيْ هُوَ خَيْرٌ"
“Na kama ukila kiapo, na ukaona jingine ni bora zaidi kuliko uliloliapia, basi toa kafara kwa kiapo chako, kisha fanya hilo ambalo ni bora zaidi”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (6622) na Muslim (1652)].
Na kuhusiana na suala hili hili, Abu Bakr (Radhwiya Allaah ‘Anhu) aliapa kwamba hatompa tena pesa ya masurufu Mistwah ambaye alimzushia kwa dhulma binti yake ‘Aaishah uzushi wa kuwa amezini. Na hapo ikashuka Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَلَا يَأْتَلِ أُولُو الْفَضْلِ مِنكُمْ وَالسَّعَةِ أَن يُؤْتُوا أُولِي الْقُرْبَىٰ"
“Na wala wasiape wale wenye fadhila miongoni mwenu na wenye wasaa wa mali kuwa hawatowapa (swadaqah) jamaa wa karibu”. [An-Nuwr: 22] [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al Bukhaariy (4750) na Muslim (2770) kutoka Hadiyth ndefu ya ‘Aaishah ikizungumzia kisa cha kuzushiwa yeye zinaa].
(e) Au kuapa kufanya jambo la mubaah. Hapa kutekeleza kiapo inakuwa ni bora zaidi madhali hakuna ndani yake madhara, na hakuna kheri katika kukivunja kwa mujibu wa Hadiyth zilizotangulia.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
022- Kumwapia Kitendo Mtu Mwingine
Na Hukmu Kwa Mwenye Kuapiwa
Alhidaaya.com [3]
Mtu anaweza kuapa kufanyika au kuachwa jambo kwa kumnasibishia mtu mwingine. Anaweza kusema kwa mfano: “Wa Allaah, utafanya”, au “Wa Allaah, usifanye kadha”.
Kama amemwapia kufanya jambo la waajib au kuacha jambo la haraam, basi ni lazima kwa aliyeapiwa akitekeleze kiapo hicho. Na kama atamwapia kufanya jambo la haraam au kuacha la waajib, basi hapo haitojuzu kukitekeleza kiapo hicho. Na kama amemwapia jambo la makruhu, basi itakuwa ni makruhu kukitekeleza kiapo. Ama akimwapia kufanya jambo la Sunnah au la mubaah, au kuacha jambo la makruhu au la mubaah, basi hapo itapendeza kukitekeleza kiapo kutokana na Hadiyth ya Al-Barraa:
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) ametuamuru mambo saba: Ametuamuru kumzuru mgonjwa, kwenda kuzika, kumwombea Rahmah mpiga chafya, kutekeleza kiapo cha aliyekuapia, kumnusuru mwenye kudhulumiwa, kuitikia wito wa anayekuita na kueneza (maamkizi ya) salaam”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (6654) na Muslim (2066)].
Agizo la kutekeleza kiapo cha anayemwapia mtu atekeleze au aache jambo linaonekana kuwa ni la waajib. Lakini pamoja na hivyo, linageuzwa na kuwa mustahabbu kutokana na Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas kuhusiana na kisa cha Abu Bakr kuifasiri njozi aliyoiota mtu mmoja mbele ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) [akapatia baadhi na akakosea mengine]. Abu Bakr akasema:
"فَو اللَّهِ يَا رَسُولَ اللَّهِ لَتُحَدِّثَنِّي مَا الَّذِي أَخْطَأْتُ . فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: " لاَ تُقْسِمْ "
“Naapa kwa Allaah ee Rasuli wa Allaah. Utanieleza lile ambalo nimekosea. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) akamwambia: Usiape”. Yaani: “Usiape tena mara ya pili, kwani mimi sitokujibu”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (2293), Abu Daawuwd (3268), na Ibn Maajah (3918)].
Na huenda jibisho hili la Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) lilikuwa kwa ajili ya kubainisha kujuzu (kutotekeleza uliloapiwa kulifanya), kwani Rasuli hafanyi kinyume na jambo linalopendeza kufanywa isipokuwa kwa lengo la kubainisha kujuzu hilo. Na kama si hivyo, basi Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) alikuwa akitekeleza viapo walivyomwapia watu atekeleze jambo fulani au aache. Katika Hadiyth ya Al-Mughiyrah bin Shu-‘bah:
"...قلتُ: يا رَسُوْلَ اللَّهِ، أقسَمْتُ عَلَيْكَ إلَّا مَا أعْطَيْتَنِي ْيَدَكَ، فَنَاوَلَني يَدَهُ، فَأَدْخَلْتُهَا فِيْ كَمِّي حتَّى انتَهَيتُ بها إلى صَدرِيْ فَوَجدَهُ مَعْصُوْبًا، فَقَالَ : إنَّ لَكَ عُذرًا"
“…..nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Nimekuapia kuwa lazima utanipa mkono wako. Akanipa mkono wake, nikauingiza kwenye mpenyo wa nguo yangu nikaufikisha hadi kifuani kwangu, akakikuta kimefungwa kitambaa. Akasema: Hakika wewe una udhuru”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3826), Ahmad (4/249) na Al-Bayhaqiy (3/77)].
· Ikiwa Mwapiwa Hakutekeleza Kiapo Cha Nduguye, Je Mwapaji Ni Lazima Atoe Kafara?
1- Akimwambia nduguye: “Bil Laah (kwa Jina la Allaah), fanya kadha”, au: “Bil Laah, nakuomba, utafanya”, basi hili linakuwa ni ombi tu na si kiapo, hivyo linakuwa halina kafara ndani yake.
Hadiyth ya Rasuli inasema:
"وَمَنْ سَأَلَكُمْ بِاَللَّهِ فَأَعْطُوْهُ"
“Na atakayewaombeni kwa Jina la Allaah, basi mpeni”. [Imekharijiwa na Al-Bayhaqiy].
Na hapa hakuna kafara kwa wenye kuombwa kama hawatompa kitu.
2- Akisema: “Wa Allaah, utafanya kadha” kisha mwapiwa asitekeleze, hapa kuna kauli mbili. Kuna inayosema kuwa ni lazima mwapaji atoe kafara. Kauli hii imenukuliwa toka kwa ‘Umar, watu wa Madiynah, ‘Atwaa, Qataadah, Al-Awzaa’iy na Ash-Shaafi’iy. [Al-Mughniy (11/247). Angalia pia Al-Muhallaa (8/35)].
Kauli ya pili ya Ibn Hazm inasema kuwa hana kafara kwa kuwa hakukusudia kuvunja kiapo. Kauli hii inatiliwa nguvu na Hadiyth iliyotangulia ya Abu Bakr. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
023- Matokeo Ya Kukitekeleza Kiapo Au Kukivunja
Alhidaaya.com [3]
Ikiwa mwapaji atatekeleza jambo aliloliapia katika yamini ya kufungika, basi hana kitu juu yake na wala halazimiwi kafara. Lakini kama atakivunja kiapo chake kwa kutotekeleza jambo aliloliapia kwa kuthibiti aliloliapia kuwa halipo, au kutokuwepo lile aliloliapia kuwa lipo, basi ni lazima atoe kafara.
· Je, Kusahau, Kukosea Na Kulazimishwa Kunazuia Adhabu Ya Kuvunja Kiapo?
Mwenye kuapa kwamba hatofanya jambo fulani kisha akalifanya kwa kusahau, au kwa kukosea, au kwa kulazimishwa, basi huyo anazingatiwa kuwa hakuvunja kiapo chake kutokana na Hadiyth:
"إنَّ اللَّهَ تَجَاوَزَ لِي عَنْ أُمَّتِي الْخَطَأَ وَالنِّسْيَانَ وَمَا اسْتُكْرِهُوا عَلَيْهِ" .
“Hakika Allaah Ameusamehe Umati wangu kwa ajili yangu wakikosea, wakisahau, na kwa yale waliyolazimishwa”. [Hadiyth Hasan].
Na kwa Kauli Yake Ta’aalaa:
"رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا"
“Rabb wetu! Usituchukulie tukisahau au tukikosea”. [Al-Baqarah: 286].
Katika Hadiyth, Allaah Ta’aalaa Amesema (kuandamizia Aayah hii): “Hakika Nimefanya”. Na katika riwaayah: “Na’am”. [Hadiyth Swahiyh].
Na kwa Neno Lake Ta’aalaa:
"وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا كَسَبَتْ قُلُوبُكُمْ"
“lakini Atakuchukulieni kwa yaliyochuma nyoyo zenu.” [Al-Baqarah: 252].
Haya ni madhehebu ya Ash-Shaafi’iy na Hanbali. Ni kauli pia ya Ibn Hazm. [Al Wajiyz cha Al-Ghazaaliy (2/229), Matwaalibu Ulin Nuhaa (6/369) na Al-Muhallaa (8/35)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
024- Kusema “In Shaa Allaah” Katika Yamini
Alhidaaya.com [3]
Muradi wa neno hili “In Shaa Allaah” ni kutegemeza Matashi ya Allaah au mfano wake kwa kila tamshi ambalo haidhaniki mtu kuvunja kiapo kwalo. Ni kama kusema mwapaji baada ya kiapo chake: "إِلَّا أَنْ يَشَاءَ اللَّـهُ" ila Atakapotaka Allaah, au: "إنْ أعَانَنِي الله" kama Allaah Atanisaidia, au "إنْ يسَّرَ اللَّهُ" Allaah Akifanya wepesi, na mfano wa hivyo. [At-Tamhiyd (14/372), Al-Mughniy (11/226) na Fat-hul Baariy (11/602)].
Toka kwa Abu Hurayrah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) amesema:
" مَنْ حَلَفَ عَلَى يَمِينٍ فَقَالَ إِنْ شَاءَ اللَّهُ، لَمْ يَحْنَثْ".
“Mwenye kuapa yamini na akasema In Shaa Allaah, basi hakuvunja kiapo (asipotekeleza)”. [Isnaad yake ni Swahiyh, lakini Al-Bukhaariy ameitia dosari. Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (1532), An Nasaaiy (7/30) na Ibn Maajah (2104). Al-Bukhaariy ameikosoa akisema kuwa ‘Abdul Razzaaq ameifupisha toka kwa Hadiyth ya Ma’amar kuhusu kisa cha Nabiy Sulaymaan kinachofuatia baada yake. Nami nasema: “Inawezekana zikawa ni Hadiyth mbili tofauti. Angalia Al-Irwaa (8/197)”].
Lakini Hadiyth hii inatiliwa nguvu na Hadiyth ya Abu Hurayrah toka kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) kuhusiana na kisa cha Nabiy Sulaymaan (‘Alayhis Salaam) aliposema:
" لأَطُوفَنَّ اللَّيْلَةَ عَلَى تِسْعِينَ امْرَأَةً تَلِدُ كُلُّ امْرَأَةٍ مِنْهُنَّ غُلاَمًا يُقَاتِلُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَقَالَ لَهُ صَاحِبُهُ : قُلْ إِنْ شَاءَ اللَّهُ ، فَلَمْ يَقُلْ ، فَطَافَ بِهِنَّ فَلَمْ تَلِدْ مِنْهُنَّ إِلاَّ امْرَأَةٌ وَاحِدَةٌ نِصْفَ إِنْسَانٍ " . فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: " لَوْ قَالَ إِنْ شَاءَ اللَّهُ لَمْ يَحْنَثْ وَكَانَ دَرَكًا لِحَاجَتِهِ "
“Wa Allaah, nitawazungukia (kuwajimai) wanawake 90 leo usiku, kila mwanamke kati yao atazaa kijana atakayepigana Jihaad katika Njia ya Allaah. Sahibu yake akamwambia: Sema In Shaa Allaah, naye hakusema. Akawazungukia, na hakuzaa yeyote kati yao isipokuwa mwanamke mmoja tu aliyezaa mtu nusu (mtoto ambaye hakukamilika). Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah “alayhi wa aalihii wa sallam) akasema: Lau kama angelisema In Shaa Allaah, basi asingelivunja kiapo chake, na ingekuwa sababu ya kupata lengo lake”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al Bukhaariy (6720) na Muslim (1654)].
· Faida:
[Al Fat-h (11/605) na Subulus Salaam (4)]
Baadhi ya ‘Ulamaa wamejuzisha kusema In Shaa Allaah baada ya kumalizika kiapo kwa kitambo kidogo kutokana na Hadiyth hii. Hili limejibiwa kwa kuambiwa kuwa maneno ya yamini ya Sulaymaan yamekuwa ni marefu, hivyo inajuzu kuwa sahibu yake kumwambia sema In Shaa Allaah kulifanyika wakati huo huo. Hivyo hakuna hoja inayobakia.
La sahihi ni lile walilosema Jumhuwr ya kuwa neno In Shaa Allaah linazuia kufungika yamini kwa sharti ya yamini kuunganika moja kwa moja nalo bila kuwepo mtengano. Na lau ingejuzu kutenganika (kuwepo mnyamao) –kama walivyosema baadhi ya Salaf- basi asingeliwajibishwa yeyote kwa kuvunja kiapo na wala asingelihitajia kutoa kafara.
Na wamekhitalifiana kuhusu kitambo cha muunganiko. Jumhuwr wamesema: Ni kusema In Shaa Allaah na kuunganisha na kiapo moja kwa moja bila ya kunyamaza kati yake, na kupumua hakuharibu jambo. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
Kwa muhtasari kuhusu hili, ni kuwa mwenye kusema In Shaa Allaah katika yamini yake, basi hawajibishwi kafara asipotekeleza. Lakini pamoja na hivyo, kuna masharti katika hili:
1- Neno liungane na yamini. Lisitenganishwe na mnyamao ambao kati yake panaweza kuingia maneno mengine, na wala lisitenganishwe na maneno mengine ya kando yasiyohusika.
2- Aliseme mtu kwa ulimi wake. Haifai kulisemea moyoni.
3- Alikusudie kikweli. Si sharti alikusudie toka anapoanza kuzungumza.
4- Hakuna tofauti kati ya kulitanguliza kabla ya yamini au kulileta mwisho.
[Fiqhul Aymaan cha ‘Iswaam Jaad (uk 188-189) kwa mabadilisho madogo].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
025- Je, Yamini Ni Kwa Mujibu Wa Mwapaji Au Mwenye Kuapisha?
Alhidaaya.com [3]
[Al-Mughniy (11/242, 284), Al-Badaai’u (3/99), Ad-Dusuwqiy (2/138) na Sharhu Muslim cha An-Nawawiy].
Mchujo tunaoupata kutokana na maneno ya Wanachuoni kuhusiana na suala hili ni kuwa mwenye kuapa ana hali mbili:
Ya Kwanza:
Asiwepo kiasili mwenye kumwapisha bali aape yeye mwenyewe kwa khiyari yake mwenyewe. Marejeo ni kwa niyyah yake, kutokana na ujumuishi wa kauli yake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam):
“Hakika si vinginevyo, matendo yote yanategemea niyyah”. Hivyo basi, kama atanuwia kwa yamini yake lile ambalo yeye analikusudia, basi yamini yake itaelekea huko huko, ni sawa likiwa alilolinuwia linaafikiana na mwonekano wa maneno yake au linatofautiana.
Ya Pili:
Awe ameapishwa na hakimu au mtu mwingine kwa jambo la haki. Hapa yamini inafungika kwa mujibu wa alilolinuwia mwapishaji, na si mwapaji. Na “tawriyah” (neno lenye kubeba maana mbili; ya juu dhahiri na ya ndani fiche) haitomfaa mwapaji katika hali hii kutokana na Hadiyth ya Abu Hurayrah aliyesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) amesema:
"يَمِينُكَ عَلَى مَا يُصَدِّقُكَ عَلَيْهِ صَاحِبُكَ"
“Yamini yako ni kwa mujibu wa ambalo sahibu yako atakuamini”.
Na katika riwaayah:
"الْيَمِينُ عَلَى نِيَّةِ الْمُسْتَحْلِفِ"
“Yamini inachukulika kwa mujibu wa niyyah ya mwapishaji”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1653), Abu Daawuwd (3255), At-Tirmidhiy (1354), Ibn Maajah (2120-2121) na wengineo].
Na kama si hivyo, basi yamini mbele ya hakimu isingelikuwa na maana yoyote, na haki za watu zingepotea.
Inavuliwa kutokana na hili kama mwapishaji atakuwa amemdhulumu mwapaji au mtu mwingine. Hapo itajuzu kwa mwapaji kutumia “tawriyah” (neno lenye kubeba maana mbili; ya juu dhahiri na ya ndani fiche) ili kulinda haki au kumnusuru mdhulumiwa. Ni kama katika Hadiyth ya Suwayd bin Handhwalah aliyesema:
"خَرَجْنَا نُرِيدُ رَسُولَ اللَّهِ وَمَعَنَا وَائِلُ بْنُ حُجْرٍ فَأَخَذَهُ عَدُوٌّ لَهُ فَتَحَرَّجَ الْقَوْمُ أَنْ يَحْلِفُوا وَحَلَفْتُ أَنَّهُ أَخِي فَخَلَّى سَبِيلَهُ فَأَتَيْنَا رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَأَخْبَرْتُهُ أَنَّ الْقَوْمَ تَحَرَّجُوا أَنْ يَحْلِفُوا وَحَلَفْتُ أَنَّهُ أَخِي قَالَ: "صَدَقْتَ الْمُسْلِمُ أَخُو الْمُسْلِمِ ".
“Tulitoka kwa niyah ya kwenda kwa Rasuli wa Allaah tukiwa pamoja na Waail bin Hujr. Adui yake akamkamata, na watu wakahisi dhiki na kuona hilo ni dhambi wakakataa kuapa. Mimi nikaapa kwamba yeye ni ndugu yangu, na adui akamwachilia. Tukafika kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) nami nikamweleza kwamba wenzangu walihisi ni kosa kuapa nami nikaapa kuwa ni ndugu yangu. Akasema: “Umesema kweli. Muislamu ni ndugu ya Muislamu”. [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh].
Na kwa sababu pia dhalimu hana haki ya kuapisha, hivyo imejuzu “tawriyah” (kuwa huyo ni ndugu yake katika Uislamu na iymaan lakini si nduguye wa damu).
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
026- Kafara Ya Yamini
Alhidaaya.com [3]
الكَفَّارَةُ “kafara” limenyambulika toka neno الْكُفْرُ “ukafiri” lenye maana ya kusitiri na kufunika. Na kafara ya yamini ni kile ambacho ni waajib kukifanya kwa kuvunja kiapo. Imeitwa hivyo kwa kuwa “inakaffir” yaani inafunika dhambi la kutotekeleza kiapo, hivyo mhusika hatoadhibiwa kwalo Siku ya Qiyaamah.
Kafara ya yamini ya kuapa kwa Jina la Allaah Ta’aalaa imethibiti katika Qur-aan, Sunnah na ‘Ijmaa.
Allaah Ta’aalaa Ameitaja katika Kitabu Chake Aliposema:
"لَا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا عَقَّدتُّمُ الْأَيْمَانَ ۖ فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِ مَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ أَوْ كِسْوَتُهُمْ أَوْ تَحْرِيرُ رَقَبَةٍ ۖ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ ۚ ذَٰلِكَ كَفَّارَةُ أَيْمَانِكُمْ إِذَا حَلَفْتُمْ ۚ وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ"
“89. Allaah Hatokuchukulieni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini Atakuchukulieni kwa (kuvunja) viapo mlivyoapa kwa niyyah mlioifunga thabiti. Basi kafara yake ni kulisha maskini kumi chakula cha wastani mnachowalisha ahli zenu, au kuwavisha nguo, au kuacha huru mtumwa. Lakini asiyeweza kupata (katika hayo), basi afunge Swiyaam siku tatu. Hiyo ndio kafara ya viapo vyenu mnapoapa. Na hifadhini yamini zenu. Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat (na Hukmu) Zake ili mpate kushukuru.” [Al-Maaidah 89].
Aayah hii Tukufu imebainisha kwamba kafara ya yamini iliyofungika ni waajib kwa kuchaguzwa mhusika kwa mujibu wa utaratibu ufuatao:
1- Kulisha. 2- Kuvisha Nguo. 3- Kuacha Huru Mtumwa.
Akishindwa haya matatu, basi ni lazima afunge siku tatu. Na haijuzu kufanya kafara hii ya kufunga ila baada ya kushindwa kuyafanya mambo matatu hayo ya kwanza. Hili ndilo lililokubaliwa kwa ‘Ijmaa ya ‘Ulamaa wote.
Hebu sasa tuyachambue mambo haya na vipengele vyake.
1- Kulisha
· Idadi Ya Masikini Wa Kulishwa
[Al-Mabsuwtw (8/50), Al-Ummu (7/91), Al-Mughniy (11/258), Al-Muhallaa (8/72) na Fiqhul Aymaan (uk 214-215)].
Katika Aayah Tukufu imeelezwa kwamba kafara inakuwa kwa kuwalisha masikini kumi. Sasa je itajuzu kumlisha masikini mmoja mara kumi, au masikini wawili mara tano kila mmoja na kama hivi?
Kuna kauli mbili za ‘Ulamaa kuhusu hili. Ya kwanza inasema kwamba inavyoonekana kiuwazi ni kuwa ni lazima kuwalisha masikini kumi kutokana na ubainisho wa Aayah. Ni madhehebu ya Ash-Shaafi’iy, Ahmad na Ibn Hazm.
Ya pili ambayo ni ya Abu Haniyfah inasema inatosha kumlisha masikini mmoja mara kadhaa kwa sharti ya kupewa chakula kwa mpigo!!
· Aina Ya Chakula Na Kipimo Chake
[Ibnu ‘Aabidiyna (3/478), Rawdhwatut Twaalibiyna (8/304), Al-Mudawwanah (2/39), Al-Muhallaa (8/72) na Majmuw’ul Fataawaa (35/349)].
Mielekeo ya ‘Ulamaa imetofautiana kuhusiana na kiasi cha chakula cha kafara. Jumhuwr –kinyume na Maalik- wanasema kafara ya chakula hukadiriwa kwa vipimo vya kisharia.
Madhehebu ya Abu Haniyfah yanasema atalisha kila masikini pishi moja ya ngano, au tende, au shayiri au unga.
Ama madhehebu ya Ash-Shaafi’iy, haya yanasema inamtosheleza kibaba, na hii pia ni kauli ya Mahanbali. Hoja yao ya kukadiria kwa kibaba ni Hadiyth ya Naafi’u aliyesema:
"كَانَ ابْنُ عُمَرَ يُعْطِي زَكَاةَ رَمَضَانَ بِمُدِّ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْمُدِّ الأَوَّلِ، وَفِي كَفَّارَةِ الْيَمِينِ بِمُدِّ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ".
“Ibn ‘Umar alikuwa akitoa Zakaah ya Ramadhwaan (fitr) kwa kipimo cha kibaba cha Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kibaba cha mwanzo. Na katika kafara ya yamini kwa kipimo cha kibaba cha Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam)”. [Hadiyth Swahiyh].
Na hoja ya waliokadiria kwa pishi ni athar ya ‘Umar bin Al-Khattwaab yeye alikuwa:
"يُطْعِمُ عَشَرَةَ مَسَاكِيْنَ –كُلَّ مِسْكِيْنِ- صَاعًا مِنْ شَعِيْرٍ أَوْ صَاعًا مِنْ تَمْرٍ أَوْ نِصْفِ صَاعٍ مِنْ قَمْحٍ".
“Analisha masikini kumi –kila masikini- pishi ya shayiri, au pishi ya tende, au nusu pishi ya ngano”. [Swahiyh. Imekharijiwa na ‘Abdul Razzaaq (10675) na At-Twabariy (5/13)].
Lakini kwa upande mwingine, Al-Imaam Maalik na Ibn Hazm –nalo pia ni chaguo la Sheikh wa Uislamu- wanaona kwamba chakula cha kuwalisha masikini kinakadiriwa kwa mujibu wa ada na mazoea ya watu, na si kwa mujibu wa kipimo cha kisharia. Hivyo watu wa kila mkoa (mji, kijiji, nchi n.k) watalisha chakula cha daraja la wastani ambacho wanawalisha watu wao kwa kiasi na kwa aina. Na hii ni kutokana na Neno Lake Ta’aalaa:
"فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِ مَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ"
“basi kafara yake ni kulisha maskini kumi chakula cha wastani mnachowalisha ahli zenu”. [Al-Maaidah: 89].
Sheikh wa Uislamu amesema (35/349): “Lililonukuliwa toka kwa Maswahaba na Taabi’iyna ni kauli hii. Na kwa ajili hiyo walikuwa wanasema: Cha wastani ni mkate na maziwa, mkate na siagi (samli), mkate na tende, na cha juu zaidi mkate na nyama. Tumezielezea kwa upana aathaar zinazowahusu mahala pengine, na tumebainisha kwamba kauli hii ndiyo sahihi ambayo imegusiwa na Qur-aan, Sunnah na kuzingatia hali halisia…”.
[Angalia aathaar hizo katika Tafsiyr At-Twabariy (5/12-13), Muswannaf ‘Abdul Razzaaq (8/507) na Sunan Al-Bayhaqiy (10/55). Ndugu yetu ‘Iswaam amezitaja baadhi ya zilizo swahiyh kwake katika kitabu cha Fiqhul Aymaan (uk. 217-219)].
Sheikh wa Uislamu ameendelea kusema (35/353): “Linalochaguliwa, ni kurejeshwa suala kwenye ada na desturi za watu. Katika mji fulani kinaweza kutosheleza alichokiwajibisha Abu Haniyfah, katika mji mwingine alichokiwajibisha Ahmad, na katika mji mwingine kati ya hiki na kile kwa mujibu wa ada za kila mji kwa mujibu wa Kauli Yake Ta’aalaa:
"مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ"
“cha wastani mnachowalisha ahli zenu”. [Al-Maaidah: 89].
Ninasema: “Na hili ndilo sahihi kutokana na yaliyotangulia. Na wala halipingani na kafara walizozitoa baadhi ya Maswahaba, kwani hilo lilikuwa linaendana na ada na desturi za miji yao. Na kwa ajili hiyo Maalik amesema: “Ama kwetu sisi hapa, basi atoe mtu kafara yake kwa kibaba cha Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika yamini. Ama watu wa miji mingine, basi hao maisha yao ni tofauti na maisha yetu. Hivyo naona watoe kafara ya chakula cha wastani kwa mujibu wa maisha yao”.
· Je, Yatosheleza Kuwalisha Tu Masikini Au Ni Lazima Kuwakabidhi Mlo?
1- Jumhuwr; Maalik, Ash-Shaafi’iy na Ahmad wanasema ni lazima kuwakabidhi masikini chakula. Na kama atawalisha mlo wa mchana au mlo wa usiku, basi haitoshelezi, kwa kuwa yaliyonukuliwa toka kwa Maswahaba ni kuwa wao walimpa kibaba kimoja kila masikini, na kwa vile pia chakula hicho ni mali ambayo imekuwa ni waajib kuwapa masikini kisharia, hivyo basi ni lazima kuwakabidhi kama Zakaah. Isitoshe, kuwakabidhi kunaingia ndani ya wigo wa kuwalisha kama ilivyo katika Hadiyth:
"أَطْعَمَ رَسُولُ اللَّهِ الجَدَّ السُدُسً"
“Rasuli wa Allaah alimpa babu sudusi”. [Hadiyth Dhwa’iyf. Angalia Al-Irwaa (6/121)].
2- Lakini Abu Haniyfah –na riwaayah toka kwa Ahmad- Ath-Thawriy, Al-Awzaa’iy, Al-Hasan na wengineo wanaona kwamba inatosheleza kuwalisha chakula cha mchana au cha usiku. Hili pia ni chaguo la Sheikh wa Uislamu, kwa kuwa makusudio hasa ni ulishaji na si umilikishaji, na hili limegusiwa na naswi, na kwa kuwa kumwezesha masikini kupata chakula ndio kumlisha kwenyewe. Allaah Ta’aalaa Amesema:
"وَيُطْعِمُونَ الطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِ مِسْكِينًا وَيَتِيمًا وَأَسِيرًا"
8. Na wanalisha chakula, juu ya kukipenda, masikini na mayatima na mateka. [Al-Insaan: 08].
Hivyo, kwa namna yoyote ile akimlisha, itaingia ndani ya maana ya Aayah. Na ndio pia katika kumkabidhi, ni sawa na kumlisha kamili. Na kwa yote mawili, wajibu unatekelezeka.
Ninasema: “Na hili ndilo sahihi zaidi. Lau atawalisha masikini kumi chakula cha mchana au cha usiku, chakula cha wastani walichozoea kukipika, basi atakuwa ametekeleza kafara yake na itakuwa imemtosheleza. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi”.
2- Kuvisha Nguo
Inamtosheleza kutoa kile ambacho kinajulikana na wote kuwa ni kivazi ambacho kikawaida huvaliwa na watu masikini. Maalik na Ahmad wamekikadiria kuwa na upana wa kusitiri uchi katika Swalaah, kwa mwanamume au mwanamke. [Al-Mudawwanah (2/44), Al-Ummu (8/92), Al-Mughniy (11/260), na Al-Muhallaa (8/75). Ndani kuna maneno yenye faida kubwa].
· Faida:
Haitoshelezi kutoa pesa badala ya chakula na nguo. Ni kauli ya Jumhuwr kinyume na Abu Haniyfah. [Al-Ummu (7/91), Al-Mudawwanah (2/40), Al-Muhallaa (8/69), Al-Mughniy (11/256) na Al-Mabsuwtw (8/154)].
3- Kuacha Huru Mtumwa
Ni kumkomboa na kumwacha huru. Jumhuwr kinyume na Abu Haniyfah wameshurutisha anayeachwa huru awe Muislamu kwa kuibebesha Aayah ya kafara ya yamini isiyo ainishi (mutwlaq) juu ya Aayah ainishi (muqayyad) ya kafara ya kuua na dhwihaar pale Aliposema Allaah:
"فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ"
“basi aachilie huru mtumwa Muumin”. [An-Nisaa: 92].
Ninasema: “Kuna mvutano wa kiuswuul katika kubebesha (Aayah) isio ainishi juu ya ainishi wakati wa kukubaliana hukmu na kutofautiana sababu. La sahihi ni kuwa haibebeshwi juu yake. Hivyo madhehebu ya Abu Haniyfah yanakuwa na nguvu zaidi, na kwa hivyo haishurutishwi anayeachwa huru katika kafara ya yamini awe Muislamu. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi”.
4- Kufunga (Kama Atashindwa Kufanya Lolote Katika Matatu Yaliyotangulia)
Akishindwa kulisha, au kuvisha, au kuacha huru, basi atafunga siku tatu.
· Je, Ni Lazima Afunge Siku Tatu Mfululizo?
Abu Haniyfah, Ath-Thawriy na Ahmad, wanasema ni waajib kuandamisha siku tatu mfululizo. Wametoa dalili ya kisomo cha Ibn Mas-‘uwd na Ubayya ambapo wawili hawa wamelisoma Neno Lake Ta’aalaa:
" فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ مُتَتَابِعَاتٍ"
“basi afunge Swiyaam siku tatu mfululizo”. Wamesema hii ni Qur-aan, kwa hiyo ni hujjah. Na kama si Qur-aan, basi ni riwaayah toka kwa Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kuwa inawezekanika kuwa wawili hao wameisikia kama tafsiyr toka kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakadhania ni Qur-aan. Na kwa makadirio yote mawili, hiyo ni hujjah!! Isitoshe, wakaongeza kusema kuwa na kwa vile hiyo ni Swiyaam ya kafara, imekuwa lazima kuandamisha siku mfano wa kafara ya kuua na ya dhwihaar!!
Lakini kwa upande wa Maalik, Ash-Shaafi’iy, Ahmad na Ibn Hazm, hawa wanasema si lazima kufululiza siku katika funga ya kafara ya yamini. Hujjah yao ni kwamba Swawm haikushurutishwa kufululiza siku zake katika Miswahafu tuliyonayo, na kisomo cha Ibn Mas-‘uwd na Ubayya ni kisomo kisichojulikana na wengi, hivyo hakuna hujjah ndani yake. Hivyo basi, mwenye kufunga siku tatu kwa picha yoyote ile, itatosha.
Na kwa vile pia hakuswihi kuibebesha ainishi juu ya isiyo ainishi pamoja na kutofautiana sababu kama lilivyogusiwa hilo nyuma.
Ninasema: “Kauli hii ya kutolazimu kufuatanisha siku ndio yenye nguvu zaidi katika funga ya kafara ya yamini”.
· Kutoa Kafara Kunatosheleza Kabla Ya Kuvunja Kiapo Na Baada Yake?
Hakuna makhitilafiano yoyote kati ya ‘Ulamaa ya kwamba kafara haimwajibikii mtu ila baada ya kuvunja kiapo chake. Kisha wakakhitilafiana kuhusu kama atatanguliza kafara kabla ya kuvunja kiapo, je itamtosheleza?
Jumhuwr wanasema itamtosheleza, ingawa ubora ni kuichelewesha hadi baada ya kuvunja kiapo. Kauli hii imenasibishwa kwa Maswahaba kumi na nne na idadi kubwa ya Taabi’iyna.
Abu Haniyfah na Maswahibu zake wanaona kwamba haitoshelezi kabla ya kuvunja kiapo.
Ash-Shaafi’iy kasema: “Haitoshelezi kwa Swawm, lakini kwa mengine inatosheleza”. [Al-Mughniy (11/222), Al-Muhallaa (8/67), Al-Mabsuwtw (8/148) na Sharhu Muslim cha An-Nawawiy].
Ninasema: “La sawa na sahihi ni kauli ya Jumhuwr. Lau kama atafanya kafara ya yamini yake kabla ya kuvunja kiapo chake au baada ya yamini, basi itamtosha. Matamshi ya Hadiyth kadhaa yanazatiti mwelekeo huu. Katika Hadiyth ya ‘Abdul Rahmaan bin Samurah, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia:
"إِذَا حَلَفْتَ عَلَى يَمِينٍ، فَرَأَيْتَ غَيْرَهَا خَيْراً مِنْهَا، فَكَفِّرْ عَنْ يَمِيْنِكَ، وَائْتِ اَلَّذِي هُوَ خَيْرٌ".
“Ukiapa yamini, kisha ukaona jambo jingine ni bora zaidi ya uliloliapia, basi fanyia kafara yamini yako, na ufanye hilo ambalo ni bora zaidi”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na An-Nasaaiy (7/10) na Abu Daawuwd (3278)].
Hadiyth hii iko wazi kabisa katika kujuzu kutanguliza kafara kabla ya kuvunja kiapo, bali pia inaonyesha wajibu wa hilo lau si ‘Ijmaa ya ‘Ulamaa iliyo kinyume chake, ingawa ubora zaidi ni kuichelewesha kafara ili kutoka nje ya duara la mvutano. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
· Je, Idadi Ya Kafara Inaongezeka Kwa Idadi Ya Viapo?
1- Hakuna makhitalifiano yoyote kuhusu mwenye kuapa yamini kisha akaivunja na akatekeleza kafara iliyomwajibikia, kwamba lau ataapa yamini nyingine na akaivunja ni lazima atoe kafara nyingine.
2- Akiapa yamini zaidi ya moja kwa mambo tofauti tofauti, la sawa ni kuwa lau atavunja kiapo kwenye jambo lolote kati ya hayo, basi ni lazima alitolee kafara. Na akivunja kwenye jingine, basi pia atalitolea kafara na hivyo hivyo. Na kafara haziingiliani, kafara ya jambo fulani haiingii kwenye jambo jingine.
3- Akiapa viapo kadhaa kwa jambo moja katika majlisi moja au majilisi tofauti, hapa Abu Haniyfah, Maalik na Ahmad wamesema itamlazimu kafara kwa kila kiapo.
Ash-Shaafi’iy kasema: “Akinuwia kwa kiapo cha pili kusisitizia kiapo cha kwanza, basi atatoa kafara ya kiapo kimoja tu”.
Ahmad amesema katika riwaayah nyingine na ambapo ni chaguo la Sheikh wa Uislamu na Ibn Hazm: “Itamwajibikia kafara moja tu kwa hali yoyote”.
Ninasema: “Hili ndilo lililo karibu zaidi. Allaah Ndiye Mjuzi zaidi”.
……………………………
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
027- Nadhiri
Alhidaaya.com [3]
· Taarifu Yake:
النُّذُوْرُ"“ nadhiri” ni wingi wa"نُذُرٌ" Maana yake katika lugha ni ahadi ambayo mtu anajilazimishia mwenyewe kuitekeleza kwa khiyari yake. Ama kisharia, ni mtu kujilazimishia mwenyewe kufanya jambo jema la utiifu kwa Allaah ambalo halikuwa ni waajib kwake, naye akalifanya liwe waajib kwake kwa tamshi linalohisisha hivyo.
· Hukmu Ya Kujiwekea Nadhiri:
Hadiyth Swahiyh zinazogusia suala la nadhiri zinaonyesha kuwa mtu hatakikani kuweka nadhiri, na kwamba jambo hilo limekatazwa. Na kwa ajili hiyo, Wanachuoni wengi wamesema ni makruhu, lakini kama mtu atajiwekea, basi ni lazima aitekeleze nadhiri hiyo. [Al-Muhallaa (8/2), Subulus Salaam (4/1446) na Naylul Awtwaar (8/277)].
1- Toka kwa Ibn ‘Umar, amesema:
"إنَّهُ لا يَرُدُّ شَيْئًا، وَإنَّمَا يُسْتَخْرَجُ بِهِ مِنَ اَلْبَخِيلِ".
“Hakika (nadhiri) hairudishi lolote (lililopangwa na Allaah), bali hutolewa kwayo (‘amali njema) toka kwa bakhili (wa kutenda mema)”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (6693) na Muslim (1639)].
2- Toka kwa Abu Hurayrah, amesema: Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لا تَنْذِرُوْا، فإنَّ النَّذْرَ لا يُغْنِي مِنَ القَدَرِ شيئًا، وإنَّمَا يُسْتَخْرَجُ بِهِ مِنَ البَخِيْلِ".
“Msiweke nadhiri, kwani nadhiri haisaidii lolote katika Qadar, bali hutolewa kwayo (‘amali njema) toka kwa bakhili (wa kutenda mema)”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1640), At-Tirmidhiy 1538), An-Nasaaiy (7/16) na Ahmad (2/412)].
3- Toka kwa Abu Hurayrah, amesema: Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إنَّ النَّذْرَ لا يُقَرِّبُ مِنِ ابْنِ آدَمَ شيئًا لَمْ يَكُنِ اللَّهُ قَدَّرَهُ له، وَلَكِنِ النَّذْرُ يُوَافِقُ القَدَرَ، فيُخْرَجُ بِذلكَ مِنَ البَخِيلِ ما لَمْ يَكُنِ البَخِيلُ يُرِيدُ أَنْ يُخْرِجَ".
“Hakika nadhiri haimsogezei mwanadamu lolote ambalo Allaah Hakuwa Amemkadiria, lakini nadhiri inasadifu Qadar, na hivyo kutolewa kwa hilo toka kwa bakhili jambo ambalo bakhili hakuwa anataka kulifanya”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (6694) na Muslim (1640)].
Qur-aan na Hadiyth zimedulisha ulazima wa kutekeleza nadhiri –ya jambo jema- na zimewasifu watekelezaji wake.
1- Allaah Ta’aalaa Amesema:
"ثُمَّ لْيَقْضُوا تَفَثَهُمْ وَلْيُوفُوا نُذُورَهُمْ"
29. Kisha wajisafishe taka zao na watimize nadhiri zao. [Al-Hajj: 29].
2- Toka kwa ‘Aaishah, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"مَنْ نذَرَ أنْ يُطيْعَ اللهَ فلْيُطِعْه وَمَنْ نَذَرَ أنْ يَعْصِيَ اللهَ فَلا يَعْصِهِ".
“Mwenye kuweka nadhiri kwamba atamtii Allaah, basi amtii, na mwenye kuweka nadhiri kwamba atamuasi Allaah, basi asimuasi”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (6696), Abu Daawuwd (3289), At-Tirmidhiy (1526), An-Nasaaiy (7/17) na Ibn Maajah (2126)].
3- Toka kwa ‘Imraan bin Huswayn, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"خَيْرُكُمْ قَرْنِي، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ - قالَ عِمْرانُ: لا أدْرِي: ذَكَرَ ثِنْتَيْنِ أوْ ثَلاثًا بَعْدَ قَرْنِهِ - ثُمَّ يَجِيءُ قَوْمٌ، يَنْذِرُونَ ولا يَفُونَ، ويَخُونُونَ ولا يُؤْتَمَنُونَ، ويَشْهَدُونَ ولا يُسْتَشْهَدُونَ، ويَظْهَرُ فِيهِمُ السِّمَنُ".
“Wabora wenu zaidi ni wa karne yangu, kisha wale wanaowafuatia (Taabi’iyna), kisha wale wanaowafuatia hao (Taabi’ut-taabi’iyna) –‘Imraan akasema: Sijui, ametaja karne mbili au tatu baada ya karne yake - kisha watakuja watu ambao wataweka nadhiri wala hawatozitekeleza, watafanya khiyana na watu hawatowaamini, na watatoa ushahidi bila kutakwa wautoe, na unene utaonekana kwenye miili yao”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (2651) na Muslim (2335)].
Hadiyth iko wazi kwamba wasio tekeleza nadhiri zao, wanabeba dhambi.
4- Allaah Subhaanahu Akiwasifia wenye kutekeleza nadhiri zao Anasema:
إِنَّ الْأَبْرَارَ يَشْرَبُونَ مِن كَأْسٍ كَانَ مِزَاجُهَا كَافُورًا﴿٥﴾ عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا عِبَادُ اللَّـهِ يُفَجِّرُونَهَا تَفْجِيرًا﴿٦﴾ يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيرًا﴿٧﴾
5. Hakika Waumini watendao wema kwa wingi watakunywa katika vikombe vya mvinyo, mchanganyiko wake ni Kaafuwr. 6. Nayo ni chemchemu watakayokunywa toka humo Waja wa Allaah, wataibubujua kwa wingi. 7. Wanatimiza nadhiri na wanaiogopa siku ambayo shari yake ni yenye kuenea kwa upana. [Al-Insaan: 5-7].
5- Amesema tena Ta’aalaa:
"وَمَا أَنفَقْتُم مِّن نَّفَقَةٍ أَوْ نَذَرْتُم مِّن نَّذْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُهُ"
270. Na chochote mtoacho au mkiwekacho nadhiri, basi hakika Allaah Anakijua. [Al-Baqarah: 270].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
028- Mushkil Na Ufumbuzi Wake
Alhidaaya.com [3]
[Tafsiyr At-Twabariy, Ihkaamul Ihkaam cha Ibn Daqiyq Al-‘Iyd (2/266), na Naylul Awtwaar (8/277)].
Kusema nadhiri ni jambo makruhu, na kusema nadhiri ni jambo mustahabu lipendezalo, misemo yote hii miwili ni mushkil kwa dalili za kila upande.
Jumhuwr wanaposema nadhiri ni makruhu, basi ndani ya msemo huu kuna mushkil kwa upande wa kanuni (principles). Kanuni inasema: “Njia ya twa’a ni twa’a, na njia ya ma’aswiyah ni ma’aswiyah”. Na kwa kuwa nadhiri ni njia ya kuwajibika kufanya jambo la kujikurubisha kwa Allaah, imekuwa lazima kwa hili iwe ni ukurubisho kwa Allaah. Lakini matini za mwanzo zinaonyesha kinyume chake. Basi vipi matini hizi zinakabiliwa kuweka mambo sawa?
Njia nzuri zaidi ya kuondosha mushkil huu ni kusemwa kwamba nadhiri ya kujikurubisha kwa Allaah iko aina mbili:
1- Nadhiri iliyofungamanishwa na upatikanaji wa manufaa. Ni kama mtu kusema: “Allaah Akimponya mgonjwa wangu, basi nimenadhiria kwa Allaah kufanya kadha” na mfano wa hili.
2- Nadhiri huria ambayo mweka nadhiri hakuifungamanisha na manufaa. Ni kama kujikurubisha mtu tu kwa Allaah kwa nadhiri akajisemea tu mwenyewe: “Ni juu yangu kwa Allaah kutoa swadaqah kitu kadhaa” na mfano wake.
Na itasemwa: Katazo katika Ahaadiyth linaelekea kwenye aina ya kwanza (iliyofungamanishiwa manufaa), kwa kuwa nadhiri yenyewe haikuwekwa hasa kwa ajili ya kujikurubisha kwa Allaah, bali imewekwa kwa sharti ya kupatikana manufaa kwa mweka nadhiri. Na manufaa hayo ambayo mweka nadhiri anajaribu kuyapata ndiyo hayo ambayo Ahaadiyth zimedulisha kwamba qadar humo iko juu ya nadhiri hiyo. Naye anaweka wazi kabisa kwamba kama mgonjwa wake hatopona, basi hatotoa swadaqah kwa kuwa amefungamanisha ponyo na swadaqah. Na hii ndiyo hali ya bakhili, hatoi chochote katika mali yake ila kwa mkabala wa maslaha ya haraka yanayozidi kile anachokitoa. Na maana hii ndiyo iliyoashiriwa kwenye neno lake Rasuli:
"وإنَّما يُسْتَخْرَجُ به مِنَ اَلْبَخِيلِ"
“bali kwa hakika hutolewa kwayo ('amali njema) toka kwa bakhili (wa kutenda mema”.
Na mtu asiye na ufahamu mzuri wa dini anaweza kuingizwa kwenye itikadi ya kudhani kwamba nadhiri yake ni lazima ifanikishe lengo lake, au kwamba Allaah Ta’aalaa Atafanikisha pamoja naye dhamira yake eti tu kwa sababu ya nadhiri hiyo. Hayo yote mawili yameashiriwa na Hadiyth ya Rasuli aliposema:
"إنَّهُ لا يَرُدُّ شَيْئًا".
“Hakika (nadhiri) hairudishi lolote (lililopangwa na Allaah)”.
Ninasema: “Ufafanuzi huu ni kuntu na imara kabisa. Nao umekusanya (nususi zote zinazoonekana kukinzana na kuzifanyia kazi), hivyo unatangulizwa juu ya “tarjiyh” (kuzipa nguvu baadhi ya nususi za kuziacha zingine)”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
029-Vigawanyo Vya Nadhiri Na Ahkaam Zake: Cha Kwanza
Alhidaaya.com [3]
Nadhiri ambazo Waislamu wanajiwekea zina vigawanyo viwili:
Kigawanyo Cha Kwanza
Nadhiri ya kufanya jambo jema kwa ajili ya Allaah.
Hii ni “Nadhiri ya Twa’aa”. Katika nadhiri hii, mtu hujilazimishia mwenyewe ima kufanya jambo ambalo Shariy’ah imelisunisha kufanywa kama Swalaah (za Sunnah), Swawm, Hajji (ya pili), kutoa swadaqah, kukaa ‘itikafu na mambo mengine mema yaliyosuniwa. Au ajilazimishe mwenyewe kufanya jambo la waajib kama nadhiri itafungamana na sifa mahsusi kama kuweka nadhiri ya kuswali Swalaah mwanzo wa wakati wake na mfano wa hilo.
Na ama lau ataweka nadhiri kwa jambo la waajib kama kuwa ataswali Swalaah tano za faradhi, au atafunga Swawm ya Ramadhwaan na mfano wa faradhi kama hizo, basi hakuna athari yoyote kwa nadhiri yake, kwa kuwa Allaah kuwajibisha hayo ni kukubwa zaidi ya yeye kujiwajibishia kwa nadhiri yake.
Na hapo nyuma kidogo tumeeleza kwamba nadhiri ya kujikurubisha kwa Allaah (nadhiri ya twa’a) ina picha mbili. Ya kwanza ni nadhiri isiyofungamanishwa na manufaa yoyote (nadhiri huria). Hii inafaa kisharia mtu kujiwekea na kuitekeleza. Na ya pili ni nadhiri iliyofungamanishwa na maslaha kwa mweka nadhiri. Hii inakuwa na picha ya kutaka badali na kuisimamisha ‘ibaadah juu ya sharti ya kupatikana lengo kusudiwa. Nadhiri hii imekatazwa mtu kuiweka.
· Hukmu Ya Kutekeleza “Nadhiri ya Twa’a”
Nadhiri ya twa’aa kwa aina zake mbili “Al-Mutwlaq” (isio ainishi) na “Al-Mu’allaq” (fungamanishwa), ni waajib kwa mweka nadhiri kuitekeleza kutokana na Qur-aan, Hadiyth na ‘Ijmaa. [Majmuw’u Fataawaa Shaykhil Islaam].
Baadhi ya dalili kuhusiana na hili zimetajwa nyuma. Kati yake ni:
1- Kauli Yake Ta’aalaa:
"ثُمَّ لْيَقْضُوا تَفَثَهُمْ وَلْيُوفُوا نُذُورَهُمْ"
29. Kisha wajisafishe taka zao na watimize nadhiri zao. [Al-Hajj: 29].
Na hii ni amri ya kutekeleza nadhiri, nayo inahukumia ulazima.
2- Allaah Subhaanahu wa Ta’aalaa Amewalaumu wale wanaoweka nadhiri na kisha wasizitekeleze Akisema:
وَمِنْهُم مَّنْ عَاهَدَ اللَّـهَ لَئِنْ آتَانَا مِن فَضْلِهِ لَنَصَّدَّقَنَّ وَلَنَكُونَنَّ مِنَ الصَّالِحِينَ﴿٧٥﴾ فَلَمَّا آتَاهُم مِّن فَضْلِهِ بَخِلُوا بِهِ وَتَوَلَّوا وَّهُم مُّعْرِضُونَ﴿٧٦﴾ فَأَعْقَبَهُمْ نِفَاقًا فِي قُلُوبِهِمْ إِلَىٰ يَوْمِ يَلْقَوْنَهُ بِمَا أَخْلَفُوا اللَّـهَ مَا وَعَدُوهُ وَبِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ﴿٧٧﴾
75. Na miongoni mwao wako waliomuahidi Allaah (kuwa): Akitupa katika Fadhila Zake, bila shaka tutatoa Swadaqah, na bila shaka tutakuwa miongoni mwa Swalihina. 76. Alipowapa katika Fadhila Zake; walizifanyia ubakhili, na wakakengeuka huku wakipuuza. 77. Basi Akawapatilizia unafiki katika nyoyo zao mpaka Siku watakayokutana Naye kwa sababu ya kumkhalifu kwao Allaah yale waliyomuahidi, na kwa sababu ya kukadhibisha kwao. [At-Tawbah 75-77)].
3- Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"مَنْ نذَرَ أنْ يُطِيْعَ اللهَ فَلْيُطِعْهُ"
“Mwenye kuweka nadhiri kwamba atamtii Allaah, basi amtii”. [Hadiyth Swahiyh. Imetajwa nyuma].
4- ‘Umar alimwambia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"إِنِّي نَذَرْتُ فِي الْجَاهِلِيَّةِ أَنْ أَعْتَكِفَ لَيْلَةً فِي الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ. قَالَ :" أَوْفِ بِنَذْرِكَ ".
“Mimi nilikuwa nimeweka nadhiri wakati wa ujahili ya kukaa ‘itikafu usiku mmoja ndani ya Al-Masjid Al-Haraam”. Rasuli akamwambia: Basi tekeleza nadhiri yako”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy 2042) na Muslim (1656)].
5- Imetajwa nyuma kidogo Hadiyth ya ‘Imraan bin Huswayn inayogusia lawama kwa watu watakaokuja baada ya karne bora ambao wataweka nadhiri na wasizitekeleze: "ثُمَّ يَجِيءُ قَوْمٌ، يَنْذِرُونَ ولا يَفُونَ،"
· Mtu Akiweka Nadhiri Kwa Jambo Asiloliweza, Au Akashindwa Kutekeleza Nadhiri:
Aliyeweka nadhiri ya kufanya jambo la kujikurubisha kwa Allaah, basi ni lazima aitekeleze nadhiri yake ikiwa ataweza kama ilivyotangulia. Akishindwa kuitekeleza, au aliloliwekea nadhiri kulifanya ni jambo ambalo hawezi kulifanya, basi si lazima kulitekeleza. Na hii ni kwa dalili zifuatazo:
1- Toka kwa Anas bin Maalik:
أنَّ رَسُوْلَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَأَى رَجُلاً يُهَادَى بيْنَ اثْنَيْنِ، فَقَالََ: مَا هذَا؟ قَالُوا: نَذَرَ أنْ يَمْشِيَ إِلى الْبَيْتِ، فَقَالَ: إنَّ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ لَغَنِيٌّ عَنْ تَعْذِيبِ هذا نَفْسَهُ. ثُمَّ أَمَرَهُ فَرَكِبَ".
“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwona mtu mmoja (kikongwe sana) akiegemezwa mabegani kati ya watu wawili. Akauliza: Mbona hivi? Wakasema: Ameweka nadhiri ya kutembea hadi nyumbani. Akasema: Hakika Allaah ‘Azza wa Jalla Hana haja ya mtu huyu kujitesa mwenyewe. Akamwamuru apande (mnyama), akapanda”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy 1865) na Muslim (1642)].
2- Toka kwa ‘Uqbah bin ‘Aamir (Radhwiya Allaah ‘anhu):
"أَنَّ أُخْتَهُ نَذَرَتْ أَنْ تَمْشِيَ إِلى الْبَيْتِ الْحَرَامِ حَافِيَةً غَيْرَ مُخْتَمِرَةٍ، فذَكَرَ ذَلِكَ لِرَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: "مُرْ أُخْتَك فَلْتَرْكَبْ، وَلْتَخْتَمِرْ، وَلْتَصُمْ ثَلاَثَةَ أَيَّامٍ " .
“Kwamba dada yake aliweka nadhiri ya kutembea pekupeku na kichwa wazi bila mtandio hadi Al-Baytul Haraam. Akalieleza hilo kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Rasuli akamwambia: Mwamuru dada yako apande, ajifunike kichwa, na afunge siku tatu”. [Isnaad yake ni Layyin. Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (1544), An-Nasaaiy (3815), Ibn Maajah (2134), Ad-Daaramiy (2334) na Ahmad (16668-16709-16735) kupitia kwa ‘Abdillaah bin Maalik toka kwa ‘Uqbah bin ‘Aamir. Katika Sanad yake yuko ‘Ubaydul Laah bin Zahr ambaye ni mdhaifu. Imekharijiwa pia na At-Twabaraaniy (17/324) toka kwa Abu Tamiym Al-Jayshaaniy toka kwa ‘Uqbah, na Sanad yake ni Dhwa’iyf].
Na katika riwaayah toka Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas kuhusiana na kisa hichi:
"فَمُرْها فَلْتَرْكَبْ وَلْتُكفِّرْ "
“Basi mwamuru (dada yako) apande na atoe kafara”. [Isnaad yake ni Layyin. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3295), Ahmad (2685), Ibn Khuzaymah (3046-3047) na Ibn Hibaan (4384) kupitia kwa Shurayk toka kwa Muhammad bin ‘Abdul Rahmaan toka kwa Kurayb toka kwa Ibn ‘Abbaas. Na katika baadhi ya riwaayah kuna nyongeza isemayo: (تُكَفِّرُ عَنْ يَمِيْنِهَا) “Atolee kafara yamini yake”.
Katika riwaayah nyingine pia:
"فأمرَها النَّبيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ تَرْكَبَ وَتُهْديَ هَدْيًا"
“Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwamuru apande na atoe mnyama wa kuchinjwa (Haram)”. [Isnaad yake ni Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3296 – 3303), Ad-Daaramiy (2335), Ahmad (2027 – 2032 – 2165 – 2691 – 17125), Ibn Khuzaymah (3045), Al-Bayhaqiy (10/79) na At-Twabaraaniy (11/308)].
Na nyingine:
"فَلْتَرْكَبْ وَلْتُهْدِ بَدَنَةً"
“Basi apande na atoe ngamia (wa kuchinjwa)”. [Angalia iliyotangulia].
Na katika riwaayah nyingine:
"لَمْ يَذْكُرْ هَدْيًا وَلا كَفَّارَةً"
“Hakutaja mnyama wa kuchinjwa wala kafara”. [Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3304), Al-Bayhaqiy (10/79), At-Twabaraaniy katika Al-Awsatw (9380), Ahmad (6653) na wengineo kupitia baadhi ya Sanad zilizotangulia lakini zimetiliwa nguvu].
3- Toka kwa ‘Uqbah bin ‘Aamir, kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"كَفَّارَةُ النَّذْرِ كَفَّارَةُ اليَمِينِ".
“Kafara ya nadhiri, ni kafara ya yamini”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1645), At-Tirmidhiy (1528) na An-Nasaaiy (3832)].
Kwa Hadiyth hizi na nyinginezo, ‘Ulamaa wamekhitalifiana kuhusu linalomlazimu aliyeweka nadhiri kwa jambo asiloliweza ikiwa atashindwa kulifanya. Ni kama mtu aliyeweka nadhiri ya kusafiri kwenda kuhiji kwa miguu halafu akashindwa. Wamekhitalifiana katika kauli zifuatazo:
[Fat-hul Qadiyr (3/173), Al-Majmuw’u (8/494), Al-Mughniy (10/74), Al-Inswaaaf (11/149), Al-Kaafiy cha Ibn ‘Abdil Barr (1/458), Jaami’ul ‘Uluwmi walhikami (uk. 309-310) na Majmuw’u Al-Fataawiy (35/327)].
Kauli Ya Kwanza: Halazimiwi Chochote
Ni kwa ubayana wa Kauli Yake Ta’aalaa:
"لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا"
286. Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake. [Al-Baqarah: 02].
Na Kauli Yake Subhaanah:
"فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ"
16. Basi mcheni Allaah muwezavyo. [At-Taghaabun: 064].
Na Kauli Yake ‘Azza wa Jalla:
"رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِ"
286. Rabb wetu! Usitutwike tusiyoyaweza. [Al-Baqarah: 02].
Na kauli yake (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"فإذَا أَمَرْتُُكُمْ بِشَيْءٍ فأْتُوا مِنْهُ مَا اسْتَطَعْتُمْ"
“Na nikiwaamuruni kitu chochote, basi fanyeni kwa kadiri mnavyoweza”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (7288) na Muslim (1337)].
Hii ni kauli ya Ash-Shaafi’iy, na riwaayah toka kwa Ahmad na Al-Awzaa’iy.
Kauli Ya Pili: Ni Lazima Afanye Kafara Ya Yamini
Ni kwa Hadiyth ya ‘Uqbah bin ‘Aamir iliyotajwa nyuma. Na kwa neno la Rasuli kwa ‘Uqbah kuhusiana na dada yake:
"فَمُرْها فَلْتَرْكَبْ وَلْتُكفِّرْ "
“Basi mwamuru (dada yako) apande (kipando) na atoe kafara”.
Haya ni madhehebu ya Ahmad na Ath-Thawriy. Ni chaguo pia la Sheikh wa Uislamu.
Kauli Ya Tatu: Ni Lazima Afunge Siku Tatu
Ni riwaayah toka kwa Ahmad.
Kauli Ya Nne: Ni Lazima Atoe Ngamia (au Ng’ombe)
Ni kauli ya Mashaafi’iy.
Kauli Ya Tano: Atoe Mnyama Wa Kuchinjwa (Haram)
Ni kauli sahihi zaidi kwa Mashaafi’y, ni riwaayah toka kwa Ahmad, na ni kauli ya Mahanafiy na Al-Layth.
Wanenaji wa kauli tatu za mwisho, wote wametegemea riwaayah kati ya riwaayah za kisa kilichotangulia cha dada wa ‘Uqbah bin ‘Aamir.
Kauli Ya Sita: Haimtoshelezi Kupanda, Bali Atahiji Mwaka Ufuatao, Ambapo Atatembea Mwendo Aliopanda, Na Atapanda Mwendo Aliotembea, Na Ni Lazima Atoe Ngamia (au Ng’ombe) Wa Kuchinjwa.
Ni kauli ya Maalik.
· Kauli Yenye Nguvu:
Ninaloliona mimi baada ya kuzitafiti Asaaniyd za Hadiyth hii ni kuwa riwaayah yenye nguvu zaidi kwa upande wa Sanad, ni riwaayah ya kutoa kafara kwa mnyama wa kuchinjwa (au ngamia, ng’ombe). Kisha inafuatiwa na riwaayah ya (Kufunga siku tatu).
Halafu ikanidhihirikia kuwa lenye nguvu zaidi kwa upande wa “Diraayah” (uhakika wa riwaayah na wapokezi wake) ni kuwa atalazimika kafara ya yamini. Na hii ni kwa haya yafuatayo:
1- Ni kwamba riwaayah ya kutoa ngamia au mnyama wa kuchinjwa (Haram) ambayo ndiyo imara zaidi kwa upande wa Sanad, inaweza kutiwa dosari kutokana na aliyoyaeleza Al-Haafidh katika Al Fat-h (11/589) ya kwamba At-Tirmidhiy amenukuu toka kwa Al-Bukhaariy kuwa kasema “Haiswihi kutaja mnyama wa kuchinjwa katika Hadiyth ya ‘Uqbah bin ‘Aamir”. Al-Bayhaqiy (10/80) amenukuu vile vile.
2- Ni kwamba riwaayah ya kufunga haikinzani na riwaayah isemayo: “Na atoe kafara”, na “Na atoe kafara ya yamini yake”, kwani kufunga siku tatu ni moja kati ya vipengele vya kafara ya yamini kama ilivyotangulia.
3- Ni kwamba hili ndilo lenye kuafikiana na Hadiyth ya ‘Uqbah bin ‘Aamir mwenyewe –naye ndiye aliyemuulizia dada yake-, ni kuwa Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"كَفَّارَةُ النَّذْرِ كَفَّارَةُ اليَمِينِ".
“Kafara ya nadhiri, ni kafara ya yamini”.
Huenda yeye ameifupisha toka fatwa ya Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika hali ya dada yake.
4- Ni kwamba Ihraam haimwajibishii mtu kutembea, hivyo si waajib kuchinja mtu akiacha kutembea.
5- Ni kwamba kusema kuwa inamwajibikia kafara ya yamini, usemi huu utafaa ikiwa nadhiri haihusiani na Hijjah kutokana na Hadiyth iliyotangulia. Na haiingii akilini kusemwa kuwa kila aliyeweka nadhiri kisha asiweze kuitekeleza atoe ngamia wa kuchinjwa! Allaah Ndiye Mjuzi zaidi.
Kiufupi Kwa Muhtasari: Mwenye kuweka nadhiri ya kufanya jambo jema la utiifu kwa Allaah kisha akashindwa kulitekeleza, basi halazimikiwi kulifanya bali ni lazima afanye kafara ya yamini.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
030-Hakuna Nadhiri Ya Kujikurubisha Kwa Allaah
Kwa Asichokimiliki Mtu
Alhidaaya.com [3]
Katika Hadiyth ya ‘Imraan bin Huswayn (Radhwiya Allaah ‘anhu) kuhusiana na kisa cha mwanamke wa Kianswaar ambaye alitekwa:
"وَنَذَرَتْ لِلَّهِ إنْ نَجَّاهَا اللَّهُ عَلَيْهَا لَتَنْحَرَنَّهَا [أي: العَضْبَاءُ]، فَلَمَّا قَدِمَتِ المَدِينَةَ رَآهَا النَّاسُ، فَقَالُوْا: العَضْبَاءُ نَاقَةُ رَسولِ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَتْ: إنَّهَا نَذَرَتْ إنْ نَجَّاهَا اللَّهُ عَلَيْهَا لَتَنْحَرَنَّهَا، فأتَوْا رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ، فَذَكَرُوا ذلكَ لَهُ، فَقَالَ: سُبْحَانَ اللهِ، بِئْسَمَا جَزَتْهَا، نَذَرَتْ لِلَّهِ إنْ نَجَّاهَا اللَّهُ عَلَيْهَا لَتَنْحَرَنَّهَا، لا وَفَاءَ لِنَذْرٍ في مَعْصِيَةٍ، وَلَا فِيما لا يَمْلِكُ العَبْدُ".
“Na akaweka nadhiri kwa Allaah kwamba Allaah Akimwokoa akiwa juu ya mgongo wake, yaani “Al-‘Adhbaa” (akiwakimbia maadui), basi atamchinja. Alipofika Madiynah, watu walimwona, wakasema: Al-‘Adhbaa, ngamia jike wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Akasema kuwa yeye ameweka nadhiri kuwa Allaah akimwokoa akiwa juu ya mgongo wake, basi atamchinja. Wakaenda kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam wakamweleza hilo. Rasuli akasema: Subhaana Allaah! Amefanya kosa baya kumtoa kafara! Ameweka nadhiri kwa Allaah kuwa Allaah Akimwokoa akiwa juu ya mgongo wake atamchinja! Hakuna nadhiri katika jambo la maasia, wala katika ambacho mja hakimiliki”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1641), Abu Daawuwd (3316), An-Nasaaiy (7/19), Ibn Maajah (2124) na wengineo].
Na toka kwa ‘Amri bin Shu’ayb toka kwa baba yake toka kwa babu yake amesema: “Amesema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"لَا نَذْرَ لِابْنِ آدَمَ فِيمَا لَا يَمْلِكُ"
“Hakuna nadhiri kwa mwanadamu kwa kisicho mali yake”. [Hadiyth Hasan. Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (1181), Abu Daawuwd (2190), Ibn Maajah (2047) na wengineo].
· Na Je Atalazimiwa Kafara Akiweka Nadhiri Kwa Kisicho Chake?
Kuna kauli mbili. Yenye nguvu zaidi ni ile isemayo kuwa halazimiwi. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
· Mwenye Kuweka Nadhiri Ya Kutoa Swadaqah Mali Yake Yote
Mwenye kuiwekea nadhiri mali yake yote kwa ajili ya Allaah ili itumiwe katika mambo ya kheri, ‘Ulamaa katika hili wana madhehebu kumi ambapo mengi yake hayana mwega wa dalili. Na yale yenye mwega wa dalili kati yake yana kauli tatu: [Al-Mughniy (10/72) na Kash-Shaaful Qinaa (6/279)].
Kauli Ya Kwanza: Ni Lazima Atoe Swadaqah Mali Yake Yote. Hili limesimuliwa toka kwa Ash-Shaafi’iy na An-Nakh’iy pamoja na Abu Haniyfah (ikiwa ni mali ya Zakaah). Hujjah ya kauli hii ni dalili zilizotangulia juu ya uwajibu wa kutekeleza nadhiri ya twa’a au utiifu kama neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"مَنْ نذَرَ أَنْ يُطيْعَ اللهَ فلْيُطِعْهُ".
“Mwenye kuweka nadhiri kwamba atamtii Allaah, basi amtii”. [Hadiyth Swahiyh. Imetajwa nyuma].
Na kwa yaliyothibiti kwamba Abu Bakr (Radhwiya Allaah ‘anhu) alitoa swadaqah mali yake yote, na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamkubalia. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (1678), At-Tirmidhiy (3675) na Ad-Daaramiy (1660)].
Kauli Ya Pili: Yamtosheleza Kutoa Theluthi Ya Mali Yake. Ni madhehebu ya Maalik, Ahmad (katika riwayah mashuhuri), Al-Layth na Az Zuhriy. Hujjah yao ni:
Hadiyth ya Ka-‘ab bin Maalik (Radhwiya Allaah ‘anhu) kuhusiana na Tawbah ya Allaah kuwasamehe watatu ambao walibaki nyuma wasende vitani (Vita vya Tabuk). Mwisho wa maneno yake alisema:
"يَا رَسُولَ اللَّه إنَّ مِن تَوْبَتي أنِّي أنْخَلِعُ مِن مَالِي صَدَقَةً إِلى اللَّهِ وَرَسُولِهِ، فَقَالَ النبيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أمْسِكْ عَلَيْكَ بَعْضَ مَالِكَ، فَهُوَ خَيْرٌ لَكَ".
“Ee Rasuli wa Allaah! Hakika sehemu ya tubio langu ni kwamba mimi najiondoa na kujivua na mali yangu iwe swadaqah kwa Allaah na Rasuli Wake. Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: Bakisha sehemu ya mali yako kwa ajili yako, hilo ni bora zaidi kwako”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (2758) na Muslim (2769)].
Na katika riwaayah nyingine:
"إنَّ مِنْ تَوْبتي إِلَى اللَّهِ أَنْ أُخْرِجَ مِنْ مَاليْ كُلِّهِ إِلَى اللَّهِ وَرَسُولِهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ صَدَقةً. قَالَ: لا، قُلْتُ: فَنِصْفَهُ، قَالَ: لا، قُلْتُ: فَثُلُثَهُ؟ قَالَ: نَعَمْ، قُلْتُ: فَإِنِّيْ أُمْسِكُ سَهْمِيْ مِنْ خَيْبَرَ".
“Hakika sehemu ya tubio langu kwa Allaah ni kuwa mimi ninaitoa mali yangu yote kwa Allaah na Rasuli Wake (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) iwe swadaqah. Akasema: Hapana. Nikasema: Basi nusu yake. Akasema: Hapana. Nikasema: Basi theluthi yake. Akasema: Na’am. Nikasema: Basi mimi nabakisha fungu langu (la ngawira) lililoko Khaybar”. [Isnaad yake ni Hasan. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3331)].
Wenye kauli hii wamesema: “Mwonekano wa Hadiyth ni kwamba Ka’ab alikuja kwa niya ya kutaka kutoa mali yake yote kama nadhiri na toba, hakuja kutaka ushauri, na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwamuru abakishe sehemu ya mali na kumweleza wazi kuwa hilo ni bora zaidi”.
Utoaji huu wa dalili umepingwa kwa kusemwa kwamba tamshi alilokuja nalo Ka’ab bin Maalik si la kutoa swadaqah mali yake mpaka liingie ndani ya duara la mvutano, bali ni tamshi linaloelezea niya ya kukusudia kufanya jambo ambalo bado hajalifanya. Na Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwashiria asifanye hilo, bali abakishe sehemu ya mali yake, na hiyo ni kabla hajafanya aliloliazimia. Hivi ndivyo tamshi linavyoonekana, au linavyochukulika.
Hoja hii imejibiwa kwa kusemwa kwamba inavyoonekana ni kuwa yeye hakuja kwa ushauri, bali alishaazimia kwa kukata, kwa sababu tamshi lake limeanzwa kwa sentensi taarifu iliyotiliwa usisitizo na herufi ya usisitizo ambayo ni "إِنَّ" katika neno lake: "إنَّ مِنْ تَوْبَتِي" . Na tamshi ambalo liko katika muundo huu haiwezekani kulipa maana ya kusita na kutaka ushauri.
Wamesema: Hili linatiliwa nguvu na kwamba wakati Allaah Ta’aalaa Alipomkubalia Abu Lubaabah tawbah yake alisema:
" يَا رَسُولَ اللَّه، إِنَّ مِنْ تَوْبَتِي أَنْ أَهْجُرَ دَارَ قَوْمِي وَأُسَاكِنُكَ وَأَنْ أَنْخَلِعَ مِنْ مَالِي كُلِّهِ صَدَقَةً لله عَزَّ وَجَلَّ وَلِرَسُوْلِهِ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "يُجْزِئُ عَنْكَ الثُّلُثُ"
“Ee Rasuli wa Allaah! Hakika sehemu ya tubio langu, ni kuwa mimi naihama nyumba ya watu wangu (ambayo nilifanyia makosa ndani yake) na badala yake nakuja kukaa karibu nawe, na ninajivua na mali yangu yote iwe swadaqah kwa Allaah ‘Azza wa Jalla na Rasuli Wake. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: Hapana, inakutosheleza theluthi”. [Kuna mvutano kuhusu Sanad yake. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3319), Ahmad (3/452-502) na Maalik (1039)].
Kauli Ya Tatu: Halazimiwi Chochote. Ni riwaayah toka kwa Abu Haniyfah (isiyohusiana na mali ya Zakaah). Na haya ni madhehebu ya Abu Muhammad bin Hazm ambaye anategemeza hujjah yake kuwa kutoa swadaqah mali yote si jambo halali akitolea dalili kwa haya yafuatayo:
1- Neno Lake Ta’aalaa:
"وَآتِ ذَا الْقُرْبَىٰ حَقَّهُ وَالْمِسْكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ وَلَا تُبَذِّرْ تَبْذِيرًا"
26. Na mpe jamaa wa karibu haki yake, na masikini, na msafiri (aliyeharibikiwa); na wala usifanye ubadhirifu wa ufujaji mkubwa. [Al-Israa: 017].
2- Neno Lake Ta’aalaa:
" وَآتُوا حَقَّهُ يَوْمَ حَصَادِهِ ۖ وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ"
“Na toeni haki yake (Zakaah) siku ya kuvunwa kwake; na wala msifanye israfu. Hakika Yeye Hapendi wafanyao israfu. [Al-An’aam: 006].
Amesema: “Hapa Allaah Amelaumu na Ameeleza wazi kuwa Hampendi mtu mwenye kutoa swadaqah mali yake yote anayoimiliki”.
3- Hadiyth ya Jaabir bin ‘Abdillaah, amesema:
"كُنَّا عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذْ جَاءَهُ رَجُلٌ بِمِثْلِ بَيْضَةٍ مِنْ ذَهَبٍ فَقَالَ يَا رَسُولَ اللَّهِ : أَصَبْتُ هَذِهِ مِنْ مَعْدِنٍ فَخُذْهَا فَهِيَ صَدَقَةٌ مَا أَمْلِكُ غَيْرَهَا . فَأَعْرَضَ عَنْهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِرَارًا، وَهُوَ يُرَدِّدُ كَلاَمَهُ هذَا، ثُمَّ أَخَذَهَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَحَذَفَهُ بِهَا، فَلَوْ أَنَّهَا أَصَابَتْهُ لأَوْجَعَتْهُ أَوْ لَعَقَرَتْهُ، وَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: " يَأْتِيْ أَحَدُكُمْ بِمَا يَمْلِكُ فَيَقُولُ هَذِهِ صَدَقَةٌ ثُمَّ يَقْعُدُ فَيَتَكَفَّفُ النَّاسَ، خَيْرُ الصَّدَقَةِ مَا كَانَ عَنْ ظَهْرِ غِنًى".
“Tulikuwa kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomjia mtu mmoja na dhahabu ya uzito wa yai. Akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Nimeipata hii kwenye mgodi, basi ichukue ni swadaqah, sina ninachokimiliki zaidi yake. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakumjibu kitu mara kadhaa huku mtu akikariri maneno yake hayo hayo. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaichukua akamrushia nayo. Lau ingelimpata ingemtia maumivu au kumuumiza vibaya. Na Rasuli wa Allaah akasema: Analeta mmoja wenu kile anachomiliki na kusema hiki ni swadaqah, kisha anakaa na kuanza kuomba omba watu. Bora ya swadaqah ni kile atoacho mtu huku yeye amejitosheleza”. [Isnaad yake ni Layyin. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (1673), Ad-Daaramiy (1659), Bin Humayd (1121), Abu Ya’alaa (2084) na Ibn Hibaan (3372). Kuna upokezi wa Ibn Ishaaq ambaye ni mdanganyifu].
Amesema: Na kama watatoa hoja kwa kutumia Kauli Yake Ta’aalaa:
وَيُؤْثِرُونَ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ
“na wanawapendelea kuliko nafsi zao japokuwa wao wenyewe wanahitaji”. [Al-Hashr: (59:09)], basi wataambiwa kwamba Aayah hii haimaanishi kwamba hawakujibakishia wenyewe cha kuwaendeshea maisha yao, bali walikuwa wakitoa kidogo na kujibakishia baadhi ya chakula.
Kauli Yenye Nguvu:
Linalonibainikia mimi ni kuwa kusema kuwa halazimiwi na chochote ikawa ndio basi katika kauli ya mwisho (ya tatu), usemi huu ni dhaifu. Mtu kutoa swadaqah mali yake yote ni jambo linaloruhusiwa, kwani imethibiti kwamba Abu Bakr (Radhwiya Allaah ‘anhu) alileta mali yake yote akaikabidhi kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na Rasuli akamkubalia hilo na akamsifia kwa kheri kwa hilo. Aidha, ‘Umar alitoa swadaqah nusu ya mali yake –ambayo ni zaidi ya theluthi- na Rasuli akamkubalia. Hivyo inaonekana kuwa mwenye kuweka nadhiri kwa mali yake yote –bila kuweko madhara kwake na kwa wanaomtegemea kwa hilo- basi ni lazima atoe swadaqah mali yake yote.
Lakini kama yatakuwepo madhara kwake na kwa wanaomtegemea, hapo ni lazima atoe swadaqah kwa kiasi ambacho hakitomletea madhara, ni sawa ikiwa theluthi, au chini yake, au zaidi. Na hii ni kwa Neno Lake Ta’aalaa:
" وَيَسْأَلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَ قُلِ الْعَفْوَ"
“Na wanakuuliza nini watoe. Sema: Yaliyokuzidieni”. [Al-Baqarah: (02:219)].
Na neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa sallam):
" لاَ ضَرَرَ وَلاَ ضِرَارَ "
“Usidhuru mtu (kwa kukusudia) wala msidhuriane (kwa kukusudia). [Hadiyth Swahiyh. Angalia Al-Irwaa (896)].
· Mwenye Kuweka Nadhiri Ya Kuswali Baytul Maqdis Itamtosheleza Kuswali Al-Masjidul Haraam
Toka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah:
"أنَّ رَجُلاً قَامَ يَوْمَ الْفَتْحِ فَقَالَ : يَا رَسُولَ اللهِ، إِنِّيْ نَذَرْتُ لِلهِ إِنْ فَتَحَ اللهُ عَلَيْكَ مَكَّةَ أَنْ أُصلِّيَ فِيْ بَيْتِ الْمَقْدِسِ رَكْعَتَيْنِ . فَقَالَ لَهُ النَّبيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: صَلِّ هَاهُنَا . ثُمَّ أَعَادَ عَلَيْهِ، فَقَالَ : صَلِّ هَاهُنَا . ثُمَّ أَعَادَ عَلَيْهِ فَقَالَ : شَأنُكَ إذًا".
“Kwamba mtu mmoja alisimama Siku ya ukombozi (wa Makkah) akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Hakika mimi niliweka nadhiri kwa Allaah kwamba Allaah Akikufungulia Makkah, basi nitaswali rakaa mbili huko Baytul Maqdis (Al-Masjidul Aqswaa). Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: Swali hapa hapa. Mtu yule akarudia maneno hayo hayo. Rasuli akamwambia: Swali hapa hapa. Akarudia tena maneno hayo hayo. Rasuli akamwambia: Basi fanya uonavyo mwenyewe (nenda ukaswali huko)”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3305), Ahmad (3/363), Ad-Daaramiy (2339) na wengineo].
· Tanbihi:
Lau ataweka nadhiri ya kufunga safari kwenda kuswali Msikiti mwingine na si Al-Masjidul Haraam, au Al-Masjidun Nabawiy, au Al-Masjidul Aqswaa, basi haijuzu kuitekeleza, kwa sababu ni nadhiri ya ma’aswiyah, lakini ni lazima atoe kafara ya yamini. Kwani Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
" لَا تُشَدُّ الرِّحَالُ إِلَّا إِلَى ثَلَاثَةِ مَسَاجِدَ: مَسْجِدِ الْحَرَامِ وَالْمَسْجِدِ الْأَقْصَى وَمَسْجِدِي هَذَا. "
“Safari ndefu hazifungwi isipokuwa kwenda Misikiti Mitatu: Masjidul Haraam, Al-Masjidul Aqswaa na Msikiti wangu huu”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (1189) na Muslim (1397)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
031- Nadhiri Ya “Al-Lijaaj” (Nadhiri Itokanayo Na Hasira)
Alhidaaya.com [3]
Hii ni nadhiri ambayo mtu anakusudia kwayo kujizuia na jambo au kuhimizia alifanye (wakati yuko katika hali ya hasira au hamaki), na si kwa ajili ya kujikurubisha kwa Allaah. Ni kama kusema: “Nikifanya kadhaa mimi, basi ni juu yangu kwa Allaah nihiji, au nitoe swadaqah au nifunge”, na mfano wa hivyo. Kauli hii inatokea pale pale inapotokea yamini, kwa kuwa mweka nadhiri hapa hakukusudia kujikurubisha kwa Allaah, na maneno yanazingatiwa kwa maana yake na si kwa matamshi yake. Na haya ndio hasa makusudio yake ya kufanya au kutokufanya. Na juu ya msingi huu, si lazima ayatekeleze maneno yake, bali atalazimika kutoa kafara ya kiapo kama atavunja nadhiri yake.
Haya ni madhehebu ya Ahmad na Ash-Shaafi’iy. Nayo ni madhehebu ambayo Abu Haniyfah aliyarejelea. Ni kauli pia ya Ishaaq, Abu ‘Ubayd, Abu Thawr na Ibn Al-Mundhir. Vile vile, ni chaguo la Sheikh wa Uislamu. Kadhalika, ni kauli ya Ibn ‘Umar, Ibn ‘Abbaas, ‘Aaishah na Maswahaba wengine. [Fat-hul Qadiyr (5/93), Al-Majmuw’u (8/459), Al-Mughniy (11/194) na Majmuw’ul Fataawaa (35/253)].
Imesimuliwa toka kwa ‘Imraan bin Huswayn ikiwa marfuw’u:
"لاَ نَذْرَ فِي غَضَبٍ وَكَفَّارَتُهُ كَفَّارَةُ الْيَمِينِ".
“Nadhiri haizingatiwi katika hali ya hasira, na kafara yake ni kafara ya yamini”.
Lakini Hadiyth hii ni Dhwa’iyf, haizingatiwi. [Imekharijiwa na Ahmad (4/433) na wengineo. Angalia Al-Irwaa (2587)].
Na Ibn ‘Abbaas aliulizwa:
"مَا تَقُوْلُ فِي امْرَأةٍ جَعَلَتْ بُرْدَهَا عَلَيْهَا هَدْيًا إِنْ لَبِسَتْهُ؟ فَقَالَ: ابْنُ عَبَّاسٍ: فِيْ غَضَبٍ أَمْ فِيْ رِضا؟ قَالُوْا: فِيْ غَضَبٍ، قَالَ: إِنَّ الله تَعَالى لا يُتَقَرَّبُ إِلَيْهِ بِالْغَضَبِ، لِتُكَفِّرَ عَنْ يَمِيْنِهَا".
“Unasemaje kuhusu mwanamke aliyesema atachinja kama atajifunika burda lake? Ibn ‘Abbaas akauliza: Katika hali ya ghadhabu au ya kawaida? Wakasema: Katika hali ya ghadhabu. Akasema: Hakika Allaah Ta’aalaa hakurubiwi kwa ghadhabu. Basi akitolee kafara kiapo chake”. [Isnaad yake ni Layyin. Sheikh wa Uislamu (35/256) ameinasibisha kwa Al-Athram].
Maalik na Abu Haniyfah –katika kauli yake ya zamani- wamesema ni lazima atekeleze nadhiri.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
032- Kafiri Akinadhiria Jambo Jema Kisha Akasilimu
Alhidaaya.com [3]
“Ulamaa wamekhitalifiana kuhusu wajibu wa kutekeleza nadhiri yake baada ya kusilimu katika kauli mbili: [Al-Muhallaa (8/25) na Naylul Awtwaar (8/286)].
Kauli Ya Kwanza:
Ni lazima atekeleze nadhiri yake akisilimu. Ni madhehebu ya Ash-Shaafi’iy, Daawuwd Adh-Dhwaahiriy na Ibn Hazm. Dalili yao ni:
1- Hadiyth ya Ibn ‘Umar kwamba ‘Umar alisema:
"يَا رَسُوْلَ اللهِ، إنِّي نَذَرْتُ أَنْ أَعْتَكِفَ لَيْلَةً فِي الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ فِي الْجَاهِلِيَّةِ. قَالَ: "أَوْفِ بِنَذْرِكَ ".
“Mimi niliweka nadhiri wakati wa ujahili ya kukaa ‘itikafu usiku mmoja ndani ya Al-Masjid Al-Haraam”. Rasuli akamwambia: Tekeleza nadhiri yako”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (2032) na Muslim (1656)].
2- Hadiyth ya ‘Amri bin Shu’ayb toka kwa baba yake toka kwa babu yake kwamba mwanamke mmoja alikuja kwa Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:
"يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنِّي نَذَرْتُ أَنْ أَضْرِبَ عَلَى رَأْسِكَ بِالدُّفِّ . قَالَ : " أَوْفِي بِنَذْرِكِ " . قَالَتْ : إِنِّي نَذَرْتُ أَنْ أَذْبَحَ بِمَكَانِ كَذَا وَكَذَا، مَكَانٌ كَانَ يَذْبَحُ فِيهِ أَهْلُ الْجَاهِلِيَّةِ . قَالَ : " لِصَنَمٍ " . قَالَتْ : لاَ . قَالَ : " لِوَثَنٍ " . قَالَتْ : لاَ . قَالَ : " أَوْفِي بِنَذْرِكِ".
“Ee Rasuli wa Allaah! Mimi niliweka nadhiri nikupigie dufu mbele yako. Akamwambia: Tekeleza nadhiri yako. Akasema: Niliweka nadhiri ya kuchinja mahala fulani na fulani; mahala ambapo watu wa ujahili walikuwa wakichinjia. Akamuuliza: Kwa ajili ya sanamu (lenye sura)? Akasema: Hapana. Akamuuliza: Kwa ajili ya “wathan” (kiabudiwa kisicho na sura)? Akasema: Hapana. Akamwambia: Tekeleza nadhiri yako”. [Sanad yake ni Hasan. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3312). Angalia Al-Irwaa].
Kauli Ya Pili:
Nadhiri ya kafiri haizingatiwi, na halazimishwi kuitekeleza akisilimu. Ni madhehebu ya Jumhuwr. Wametoa dalili kwa:
1- Kauli Yake Ta’aalaa:
"لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ"
“Ukifanya shirki bila shaka zitaporomoka ‘amali zako”. [Az Zumar: (39: 65)].
2- Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَقَدِمْنَا إِلَىٰ مَا عَمِلُوا مِنْ عَمَلٍ فَجَعَلْنَاهُ هَبَاءً مَّنثُورًا"
23. Na Tutayaendea yale waliyoyatenda ya ‘amali yoyote ile, Tutayafanya chembechembe za vumbi zinazoelea hewani zikitawanyika. [Al-Furqaan: 25].
Ibn Hazm amejibu kuhusu hili akisema kwamba hakuna hujjah yoyote ndani yake, kwa kuwa haya yote yameteremka kumzungumzia mtu ambaye amekufa hali ya kuwa ni kafiri kwa matini ya kila Aayah kati ya Aayah hizi mbili. Na Allaah Ta’aalaa Amesema:
"وَمَن يَرْتَدِدْ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَيَمُتْ وَهُوَ كَافِرٌ فَأُولَـٰئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ"
“Na atakayeritadi miongoni mwenu kutoka Dini yake, akafariki hali ya kuwa ni kafiri, basi hao zimeporomoka ‘amali zao”. [Al-Baqarah: 217].
Kisha wao baada ya haya, wanajuzisha mauzo ya kafiri, ndoa yake, akitoacho bure, swadaqah yake na kuacha kwake huru!!
Na katika Hadiyth ya Abu Hurayrah –kuhusu kisa cha kusilimu Thumaamah bin Uthaal (Radhwiya Allaah ‘anhu) kwamba alimwambia Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"وَإِنَّ خَيْلَكَ أَخَذَتْنِي وَأَنَا أُرِيدُ الْعُمْرَةَ فَمَاذَا تَرَى، فَبَشَّرَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَأَمَرَهُ أَنْ يَعْتَمِرَ".
“Na askari wako wa farasi waliniteka, na hali mimi nataka kufanya ‘Umrah. Je, waonaje? Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akampa khabari njema, na akamwamuru afanye ‘Umrah”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (4372) na Muslim (1764)].
Na huyu ni kafiri, alitoka hali ya kuwa anataka kufanya ‘Umrah, akasilimu, na Rasuli akamwamuru akamilishe niyyah yake.
Ninasema: “Lenye nguvu ni kwamba inamlazimu atekeleze nadhiri ya twa’a aliyoiweka wakati wa ukafiri wake anaposilimu. Na Allaah Ndiye Ajuaye zaidi”.
· Kumlipia Maiti Nadhiri Yake Ya Twa’a
Mwanadamu akiweka nadhiri ya twa’a katika ambalo inamlazimu kulitekeleza kisha akafariki kabla ya kulitekeleza, basi walii wake atamlipia nadhiri yake. Ikiwa nadhiri ni mali, basi atatoa katika mali ya maiti kabla ya kutoa madeni ya watu kutokana na Kauli Yake Ta’aalaa:
"مِن بَعْدِ وَصِيَّةٍ يُوصِي بِهَا أَوْ دَيْنٍ"
“baada ya kutoa wasia aliousia (maiti) au kulipa deni”. [An-Nisaa: (11)].
Hapa Allaah Ta’aalaa Amelitaja deni kiujumla, yaani deni lolote lile; la mali au la ‘ibaadah. Na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"فَدَيْنُ اللَّهِ أَحَقُّ أَنْ يُقْضَى ".
“Basi Deni la Allaah lina haki zaidi kulipwa”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (1953) na Muslim (1148)].
Na kama nadhiri ni ‘ibaadah kama Hijjah, swawm, ‘itikafu na mfano wa hayo, basi walii wake atamfanyia kwa dalili zifuatazo:
1- Toka kwa Ibn ‘Abbaas:
" أَنَّ سَعْدَ بن عبَادَة رَضِي اللهُ عَنْهُم اسْتَفْتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي نَذْرٍ كَانَ عَلَى أُمِّهِ فَتُوُفِّيَتْ قَبْلَ أَنْ تَقْضِيَهُ فَأَفْتَاهُ أَنْ يَقْضِيَهُ عَنْهَا".
“Kwamba Sa’ad bin ‘Ubaadah (Radhwiya Allaah ‘anhu) alimuuliza Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu nadhiri ambayo mama yake aliiweka na akafariki kabla hajaitekeleza. Akamjibu kuwa amlipie mama yake”. Hadiyth Swahiyh. [Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (2761) na Muslim (1638)].
Na katika tamshi jingine alimwambia:
"اقْضِهِ عَنْهَا"
“Mlipie”.
2- Toka kwa Ibn ‘Abbaas kwamba:
جَاءَتِ امْرَأَةٌ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَتْ : يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّ أُمِّي مَاتَتْ وَعَلَيْهَا صَوْمُ مِنْ نَذْرٍ، أَفَأَصُومُ عَنْهَا؟ فقَالَ لَهَا النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: " أَرَأَيْتِ لَوْ كَانَ عَلَى أُمِّكِ دَيْنٌ فَقَضَيْتِيهِ أَكَانَ يُؤَدِّي ذَلِكِ عَنْهَا؟ " . قَالَتْ نَعَمْ . قَالَ " فَصُومِي عَنْ أُمِّكِ "
“Mwanamke mmoja alikuja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Hakika mama yangu amekufa naye anadaiwa swawm ya nadhiri. Je, naweza kumfungia? Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) akamwambia: Hebu angalia, je kama mama yako alikuwa na deni halafu wewe ukalilipa, je hilo litakuwa limemlipia deni lake? Akasema: Na’am. Akamwambia: Basi mfungie mama yako”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (953) na Muslim (1148) na tamshi ni lake].
3- Imeripotiwa toka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa):
"أَنَّهَا اعْتَكَفَتْ عَنْ أَخِيْهَا بَعْدَ مَا مَاتَ".
“Kwamba alimkalia ‘itikafu kaka yake baada ya kufariki”. [Isnaad yake ni Dhwa’iyf. [Imekharijiwa na Sa’iyd bin Mansour (424) na Ibn Abiy Shaybah (2/339)].
· Je, Maiti Hulipiwa Swalaah Aliyoiwekea Nadhiri?
Mwelekeo wa Jumhuwr ya ‘Ulamaa ni kuwa mtu hamswalii mwingine, bali Ibn Battwaal amehadithia kufikiwa ‘Ijmaa juu ya hilo!! Lakini hili linatenguliwa na:
"أَنَّ ابْنَ عُمَرَ أَمَرَ امْرَأَةً جَعَلَتْ أُمَّهَا عَلَى نَفْسِهَا صَلاَةً بِقُبَاءَ فَقَالَ: صَلِّيْ عَنْهَا"
“Kwamba Ibn ‘Umar alimwamuru mwanamke mmoja ambaye mama yake alijiwekea nadhiri ya kuswali Qubaa kwa kumwambia: “Swali kwa niaba yake”. [Al-Bukhaariy amesema ni Mu’allaq (11/584) kwa tamko la “Jazm”, na Al-Haafidh hakuifanya Mawsuul katika At-Taghliyq (5/203)].
Daawuwd na Ibn Hazm wamewajibisha kulipwa Swalaah iliyowekewa nadhiri na maiti. [Al-Muhallaa].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
033- Vigawanyo Vya Nadhiri Na Ahkaam Zake: Kigawanyo Cha Pili
Alhidaaya.com [3]
Ni nadhiri isiyo na utiifu kwa Allaah Ta’aalaa ndani yake. Nadhiri hii iko aina mbili:
Aina Ya Kwanza:
Isiyo na ma’aswiyah ndani yake kwa dhati yake yenyewe (yaani jambo la mubaah).
Akiweka nadhiri mtu kwa jambo lisilo ma’aswiyah na halina sifa ya utiifu wa kujikurubisha kwa Allaah, basi si wajibu kwake kulitekeleza. Jumhuwr wanasema kwamba jambo kama hilo ni mubaah na haliingii kwenye duara la nadhiri. Na hii ni kutokana na Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas aliyesema:
"بَيْنَمَا النَّبيُّ صلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسلَّم يخطُبُ إذا هُوَ بِرَجُلٍ قَائمٍ فِي الشَّمْسِ، فَسَأََلَ عَنْهُ، قَالُوْا: هذَا أَبُوْ إِسْرَائِيْلَ نَذَرَ أَنْ يَقُوْمَ وَلا يَقْعُدَ وَلا يَسْتَظِلَّ وَلا يَتَكلَّمَ وَيَصُوْمَ، قال: مُرُوهُ فَلِيَتَكَلَّمْ وليَِسْتَظِلَّ ولِيَقْعُدْ وليُتِمَّ صَوْمَهُ".
“Wakati Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa anakhutubu, mara akamwona mtu amesimama juani. Akauliza nani huyo? Wakamwambia: Huyu ni Abu Israaiyl, ameweka nadhiri kwamba atasimama tu na hatokaa, wala hatosimama kivulini, wala hatozungumza na amefunga. Akasema: Mwamuruni azungumze, akae kivulini, aketi na aikamilishe Swawm yake”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (6704), Abu Daawuwd (3300), Ibn Maajah (2136) na wengineo].
Hadiyth inatubainishia kwamba lile aliloliwekea nadhiri ambalo ni kiini cha twa’a kama Swawm, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwamrisha alitimize kwa ajili ya kutekeleza nadhiri yake. Ama yale ambayo ni mubaah yasiyo na twa’a ndani yake kama kuacha kuzungumza, au kutoketi chini, au kusimama kivulini, hayo aliamuru aachane nayo na asiyatekeleze.
Lakini Ahmad anasema nadhiri ya jambo la mubaah inafungika, lakini mweka nadhiri huchaguzwa baina ya kuitekeleza au kutoitekeleza, na wakati huo ni lazima atoe kafara.
Mhakiki Swiddiyq Khan amekhitari kuwa nadhiri ya jambo mubaah hubeba kwa njia rasmi jina la nadhiri, na hivyo huingia chini ya ujumuishi ubebao amri ya kuitekeleza. Amesema: “Linalotilia nguvu hilo ni lile alilolikhariji Abu Daawuwd:
"أَنَّ امْرأةً قَالَتْ: يا رَسُوْلَ اللهِ، إنِّي نَذَرْتُ إِذَا انْصَرَفْتُ مِنْ غَزْوَتِكَ سَالِمًا أَنْ أَضْرِبَ عَلى رَأْسِكَ بِالدُّفِّ. فَقَالَ لَهَا: أَوْفِيْ بِنَذْرِكِ".
“Kwamba mwanamke mmoja alisema: “Ee Rasuli wa Allaah! Mimi niliweka nadhiri nikupigie dufu mbele yako ukirudi salama toka vitani. Rasuli akamwambia: Tekeleza nadhiri yako”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (3690), Abu Daawuwd (3316), Ahmad (5/356) na Ibn Hibaan (4386)].
Na ikiwa kupiga dufu si jambo la mubaah, basi itakuwa ima ni makruhu au baya zaidi kuliko makruhu, na wala haliwi kamwe ni jambo la kujikurubisha kwa Allaah. Na kama ni mubaah, basi hiyo ni dalili juu ya wajibu wa kutekeleza nadhiri ya jambo mubaah. Na kama ni makruhu, basi kuruhusu kulitekeleza kunaonyesha kwamba kutekeleza jambo la mubaah ni bora zaidi. Vile vile, kuwajibisha kafara kwa aliyeweka nadhiri ambayo hakuitaja, kunaonyesha juu ya wajibu wa kafara kwa jambo la mubaah kwa ubora zaidi.
Hivyo kwa ufupi, tunaweza kusema kuwa nadhiri ya jambo la mubaah, haitoki nje ya moja ya vigawanyo viwili: Ima itekelezwe kama ni waajib, au kafara iwe waajib kama haikutekelezwa..”. [Ar-Rawdhwatun Naddiyyah (uk. 177-178)].
Al-Bayhaqiy (Rahimahul Laah amesema (10/77): “Inafanana kama vile Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimruhusu kupiga dufu kwa kuwa hilo ni jambo mubaah, na ndani yake kuna kuonyesha furaha ya kuonekana Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kurejea kwake salama, na si kwamba nadhiri ni wajibu kwa hilo. Na Allaah Ndiye Ajuaye zaidi”.
Ninasema: “Lakini mushkil kidogo upo kwa aliyoyaeleza Al-Bayhaqiy (Rahimahul Laah). Ni kwamba Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia (mwanamke huyo):
"إِنْ نَذَرْتِ فَافْعَلِيْ، وَإلَّا فَلاَ".
“Kama uliweka nadhiri, basi fanya, na kama sivyo, basi usifanye”.
Na hii inaonyesha kwamba alimwamuru kufanya hilo ili atekeleze nadhiri yake. Lakini inabakia kwamba mwanamke kupiga dufu mbele ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na hadhira ya Maswahaba wanaume si jambo linaloruhusiwa. Na kwa muktadha huo, inaonyesha kwamba Hadiyth hii ni tukio maalum linalomhusu mtu mmoja tu bila kuwahusu wengineo, na haitakikani kulitolea dalili. Na asili ni kwamba nadhiri inakuwa kwa jambo ambalo ndani yake kuna twa’a ya kujikurubisha kwa Allaah, nayo ni ‘ibaadah. Hivyo haiwi isipokuwa kwa lile ambalo Allaah Ta’aalaa Ameliamuru.
Linaloonekana ni kwamba mubaah huangaliwa: Ikiwa ni njia kwa jambo la waajib au la Sunnah, basi nadhiri hufungika nalo, na kama si hivyo, basi lililo sahihi ni kuwa nadhiri haifungiki nalo kama walivyosema Jumhuwr. Allaah Ndiye Mjuzi zaidi”.
Aina Ya Pili:
Lililowekewa nadhiri liwe ni ma’aswiyah kwa dhati yake lenyewe (nadhiri ya ma’aswiyah).
Mtu akiweka nadhiri kwa jambo la ma’aswiyah kama kunywa pombe, au kuua nafsi iliyoharamishwa, au kuchinja juu ya kaburi, au kufunga safari kwenda kwa isiyo Misikiti Mitatu, au kutofanya usawa baina ya watoto wake, au kuwatukuza zaidi baadhi yao, au kuwanyima mirathi na mfano wa ma’aswiyah kama hayo, basi haya si waajib kwake kuyatekeleza, bali pia ni haramu.
1- Toka kwa ‘Aaishah, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"مَنْ نَذَرَ أَنْ يُطِيْعَ اللهَ فَلْيُطِعْهُ وَمَنْ نَذَرَ أَنْ يَعْصِيَ اللهَ فَلا يَعْصِهِ".
“Mwenye kuweka nadhiri kwamba atamtii Allaah, basi amtii, na mwenye kuweka nadhiri kwamba atamuasi Allaah, basi asimuasi”. [Hadiyth Swahiyh].
2- Toka kwa ‘Imraan bin Huswayn kwamba Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لا وَفَاءَ لِنَذْرٍ فيْ مَعْصِيَةٍ، وَلَا وَفَاءَ لِنَذَرٍ فِيْمَا لا يَمْلِكُ العَبْدُ، أَوْ: ابْنُ آدَمَ".
“Hakuna kutekeleza nadhiri katika jambo la maasia, na wala hakuna kutekeleza nadhiri katika ambacho mja hakimiliki, au: mwanadamu”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1641), Abu Daawuwd (3316), An-Nasaaiy (7/19) na Ibn Maajah (2124)].
3- Toka kwa Thaabit bin Adh-Dhwahhaak (Radhwiya Allaah ‘anhu), amesema:
" نَذَرَ رَجُلٌ عَلَى عَهْدِ رَسُوْلِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ يَنْحَرَ إِبِلًا بِبُوَانَةَ، فَأَتَى النَّبيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: إِنِّي نَذَرْتُ أَنْ أَنْحَرَ إِبِلًا بِبُوَانَةَ: فَقَالَ النَّبيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: هَلْ كَانَ فِيهَا وَثَنٌ مِنْ أَوْثَانِ الْجَاهِلِيَّةِ يُعْبَدُ؟ قَالَ: لَا، قَالَ: هَلْ كَانَ فِيهِ عِيدٌ مِنْ أَعْيَادِهِمْ؟ قَالَ: لَا، قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أوْفِ بِنَذْرِك فَإِنَّهُ لَا وَفَاءَ لِنَذْرٍ فِي مَعْصِيَةِ اللَّهِ وَلَا فِيمَا لَا يَمْلِكُ ابْنُ آدَمَ".
“Mtu mmoja wakati wa enzi ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliweka nadhiri ya kuchinja ngamia (eneo la) Buwaanah. Akamjia Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: Mimi niliweka nadhiri ya kuchinja ngamia Buwaanah. Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamuuliza: Je, kulikuweko huko kiabudiwa chochote kati ya viabudiwa vya enzi ya ujahili kinaabudiwa? Akasema: Hapana. Akamuuliza: Je, kulikuwa kunafanyika sherehe yoyote kati ya sherehe zao? Akasema: Hapana. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: Tekeleza nadhiri yako, kwani hakuna kutekeleza nadhiri katika kumwasi Allaah wala katika ambacho mwanadamu hakimiliki”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3313)].
Hapa kuna dalili wazi kwamba kuchinja katika mahala ambapo kulikuweko kiabudiwa kinachoabudiwa au mahala popote ambapo ilikuwa ikifanyika sherehe yoyote katika sherehe za kijahili (enzi kabla ya Uislamu) ni ma’aswiya kwa Allaah Ta’aalaa, na kwamba kwa hayo, haijuzu kuitekeleza nadhiri. Kuna Hadiyth nyingi tu zinazogusia hili.
· Je, Ni Lazima Kafara Kwa Nadhiri Ya Ma’aswiyah?
‘Ulamaa wana kauli mbili kuhusu hili:
Kauli Ya Kwanza:
Hana kafara mwenye kuweka nadhiri ya ma’aswiyah. Ni madhehebu ya Maalik, Ash-Shaafi’iy na riwaayah toka kwa Ahmad. Dalili zao ni:
1- Neno lake (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"لا نَذرَ فِيْ مَعْصِيَةِ اللَّهِ".
“Hakuna nadhiri katika kumwasi Allaah”. [Hadiyth Swahiyh].
Hivyo nadhiri haifungiki kwa ma’aswiyah.
2- Neno lake Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"وَمَنْ نَذَرَ أَنْ يَعْصِيَهُ فَلاَ يَعْصِهِ".
“Na aliyeweka nadhiri ya kumwasi (Allaah), basi asimwasi”. [Hadiyth Swahiyh].
Na wala hakuamuru kafara.
3- Hadiyth zilizotangulia: Kuhusu mwanamke aliyeweka nadhiri ya kumchinja Al-‘Adhwbaa (ngamia wa Rasuli), na mwanaume aliyeweka nadhiri ya kutosimama kivulini au kutozungumza na mfano wa hayo. Katika Hadiyth hizi, Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaamuru kutotekeleza nadhiri zao, na hakuna kiashirio chochote ndani yake kuwa aliwalazimisha kutoa kafara.
Kauli Ya Pili:
Ni lazima atoe kafara. Ni madhehebu ya Abu Haniyfah, Ath-Thawriy na riwaayah nyingine toka kwa Ahmad. Ni kauli iliyosimuliwa toka kwa Ibn Mas-‘uwd, Ibn ‘Abbaas, Jaabir, ‘Imraan bin Huswayn na Samurah bin Jundub (Radhwiya Allaah ‘anhum). Dalili za wenye kauli hii:
1- Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhu), Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"النَّذْرُ نَذْرَانِ، فَمَا كَانَ لِلهِ كَفَّارتُهُ الْوَفاءُ، وَمَا كَانَ لِلشَّيْطَانِ فَلا وَفَاءَ فِيْهِ، وَعَلَيْهِ كَفَّارَةُ يَمِيْن".
“Nadhiri ni nadhiri mbili. Inayokuwa kwa ajili ya Allaah, kafara yake ni kuitekeleza. Na inayokuwa kwa ajili ya shaytwaan basi haitekelezwi, na ni juu yake kafara ya yamini”. [Hadiyth Hasan. Imekharijiwa na Ibn Al-Jaaruwd (935), na kupitia Sanad yake Al-Bayhaqiy (1072). Abu Daawuwd amekhariji mfano wake (3322) kupitia Sanad nyingine toka kwa Ibn ‘Abbaas. Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh katika As-Swahiyhah (479)].
2- Hadiyth ya ‘Aaishah, Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لاَ نَذْرَ فِيْ مَعْصِيَةِ اللهِ، وَكَفَّارَتُهَ كَفَّارةُ يمينٍ".
“Hakuna nadhiri katika kumwasi Allaah, na kafara yake ni kafara ya yamini”. [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3290), At-Tirmidhiy (1524), An-Nasaaiy (2/145) na Ibn Maajah. Angalia Al-Irwaa (2590)].
Lenye Nguvu:
Hakuna shaka kwamba dalili za Hadiyth hizi mbili zina nguvu zaidi kuliko dalili za Hadiyth zilizotolewa na kundi la kwanza, kwani kafara kwenye Hadiyth hizo imenyamaziwa bila kutajwa. Hivyo Hadiyth za kundi la pili zinatangulizwa kwa kuwa zimethibitisha kafara. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
· Akiweka Nadhiri Ambayo Hakuitaja
Mtu akiweka nadhiri ambayo hakuiainisha au hakuitaja kama kusema: “Nimejiwekea nadhiri kwa Allaah”, basi ni lazima atoe kafara ya yamini. Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa sallam) toka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhu):
"مَنْ نَذَرَ نَذْراً لَمْ يُسَمِّهِ، فَكَفَّارَتُهُ كَفَّارَةُ يَمِينٍ، وَمَنْ نَذَرَ نَذْراً فِي مَعْصِيَةٍ، فَكَفَّارَتُهُ كَفَّارَةُ يَمِينٍ، وَمَنْ نَذَرَ نَذْراً لَا يُطِيقُهُ، فَكَفَّارَتُهُ كَفَّارَةُ يَمِين" .
“Mwenye kuweka nadhiri ambayo hakuitaja, basi kafara yake ni kafara ya yamini. Na mwenye kuweka nadhiri katika ma’aswiyah, basi kafara yake ni kafara ya yamini. Na mwenye kuweka nadhiri asiyoiweza, basi kafara yake ni kafara ya yamini”. [Imekharijiwa na Ibn Abiy Shaybah (4/173) ikiwa mawquwf. Pia imekharijiwa na Abu Daawuwd (3322)].
Imehadithiwa mfano wake ikiwa marfuw’u katika Hadiyth ya ‘Uqbah bin ‘Aamir kwa tamko lisemalo:
"كَفَّارَةُ اَلنَّذْرِ [إِذَا لَمْ يُسَمِّ ] كَفَّارَةُ يَمِينٍ" .
“Kafara ya nadhiri (kama haikutajwa) ni kafara ya yamini”. Lakini Hadiyth hii ni Dhwa’iyf. [Ni Dhwa’iyf kwa nyongeza hii (kama haikutajwa). Imekharijiwa na Abu Daawuwd (2324), At-Tirmidhiy (1528), na An-Nasaaiy (7/26). Angalia Al-Irwaa (2586)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ
Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri
034- Nadhiri Kwa Asiye Allaah Ni Shirki
Alhidaaya.com [3]
Nadhiri ni ‘ibaadah. Haijuzu kuielekeza kwa asiye Allaah Ta’aalaa. Yeyote atakayeielekeza kwa asiye Allaah, akaielekeza kwa Malaika mwenye hadhi kubwa kwa Allaah, au kwa Nabiy Mursal, au kwa walii katika mawalii akiwa hai au maiti, au kwa jua, au kwa mwezi na mfano wa hayo katika mambo wanayoyafanya waabudiaji masanamu, au waabudiaji makaburi na mfano wao, wakiamini kwamba hao au hivyo vitawadhuru au kuwanufaisha, au kuwakidhia haja zao, au kuwaondoshea matatizo yao, basi mtu huyu atakuwa amefanya dhambi kubwa kuliko yote, nalo ni kumshirikisha Allaah Ta’aalaa. Haya ni sawa na yale Aliyoyaelezea Ta’aalaa katika Neno Lake:
"وَجَعَلُوا لِلَّـهِ مِمَّا ذَرَأَ مِنَ الْحَرْثِ وَالْأَنْعَامِ نَصِيبًا فَقَالُوا هَـٰذَا لِلَّـهِ بِزَعْمِهِمْ وَهَـٰذَا لِشُرَكَائِنَا ۖ فَمَا كَانَ لِشُرَكَائِهِمْ فَلَا يَصِلُ إِلَى اللَّـهِ ۖ وَمَا كَانَ لِلَّـهِ فَهُوَ يَصِلُ إِلَىٰ شُرَكَائِهِمْ ۗ سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ".
136. Na wamemfanyia Allaah fungu katika mimea na wanyama Aliyoumba. Wakasema: Hili ni la Allaah kwa madai yao, na hili ni kwa ajili ya washirika wetu. Basi yaliyokuwa kwa ajili ya washirika wao hayamfikii Allaah. Na yaliyokuwa kwa ajili ya Allaah hufika kwa washirika wao. Uovu ulioje wanayoyahukumu! [Al-An’aam: 06].
Sheikh wa Uislamu amesema: “ ‘Ulamaa wamekubaliana kwa sauti moja kwamba haijuzu kwa yeyote kuweka nadhiri kwa asiye Allaah, si kwa Nabiy wala kwa asiye Nabii, na kwamba hilo ni shirki isiyopasa kutekelezwa”. [Majmuw’ul Fataawaa (1/286)].
Na amesema (Rahimahul Laah): “Ama nadhiri yake (yaani mja) kwa asiye Allaah kama kuweka nadhiri kwa masanamu, jua, mwezi, makaburi na mfano wa hayo, basi hilo ni sawa na kuapa kwa asiye Allaah katika viumbe”.
Al-Amiyr As-Swan-’aaniy (Rahimahul Laah) amesema: “Ama nadhiri tuzijuazo katika wakati wetu wa sasa wanazoziweka watu kwa makaburi na wafu, hili halina makhitilafiano kabisa katika uharamu wake, kwa kuwa mweka nadhiri anaitakidi kwamba maiti aliyemo ndani yake ana uwezo wa kunufaisha na kudhuru, au kuleta kheri na kuondosha shari, au kumfariji mwenye maumivu na kumponya mgonjwa. Na haya ndiyo hasa waliyokuwa wakiyafanya waabudiao miungu, nayo ni haramu kama ilivyo haramu kuyawekea nadhiri.
Ni haramu pia kuyapa nafasi na uwanja mambo haya, kwani kufanya hivyo ni kuikubali shirki. Aidha, ni lazima kuyakemea na kubainisha kwamba hayo ni katika maharamisho makubwa ambayo waabudiao masanamu na miungu walikuwa wakiyafanya zamani, na muda ukarefuka mpaka mema yakageuka munkari, na munkari yakawa mema. Na hata kumekuwa kunafanywa minasaba kwa wapokeaji nadhiri za wafu, na wale wajao pale alipo maiti huandaliwa makaramu na kuchinjwa wanyama kwenye mlango wake. Na haya ndiyo hasa waliyokuwa wakiyafanya waabudiji masanamu. Innaa lil Laahi Wa Innaa Ilayhi Raaji’uwn. Na watu wetu wamesoma mengi muhimu kuhusiana na haya katika tasnifu yenye anwani isemayo: “Kuitwaharisha aqiydah kutokana na uchafu wa kumkana Allaah”. [Subulus Salaam].
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/284
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11147&title=07-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20%D9%83%D9%90%D8%AA%D8%A7%D8%A8%D9%8F%20%D8%A7%D9%84%D8%A3%D9%8A%D9%85%D8%A7%D9%86%20%D9%88%D9%8E%D8%A7%D9%84%D9%86%D9%91%D9%8F%D8%B0%D9%88%D8%B1%20-%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%20%20
[3] http://www.alhidaaya.com/sw/
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11257&title=001-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Taarifu%20Ya%20Viapo
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11258&title=002-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Usharia%20Wa%20Kiapo
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11259&title=003-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Viapo%20Vya%20Waislamu
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11260&title=004-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Haifai%20Kuapa%20Kila%20Wakati%20
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11261&title=005-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3AKiapo%20Hakiapiwi%20Ila%20Kwa%20Allaah%20Tu
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11262&title=006-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Kuapa%20Kwa%20Majina%20Na%20Sifa%20Za%20Allaah
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11263&title=007-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Kuapa%20Kwa%20Sifa%20Za%20Allaah%20Ta%E2%80%99aalaa
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11264&title=008-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Kuapa%20Kwa%20Qur-aan
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11265&title=009-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Mwenye%20Kuapa%20Kwa%20Kusema%3A%20%D9%84%D9%8E%D8%B9%D9%8E%D9%85%D9%92%D8%B1%D9%8F%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%E2%80%9CNaapa%20kwa%20Uhai%20wa%20Allaah%E2%80%9D
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11266&title=010-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Mwenye%20Kusema%3A%20%D9%88%D9%8E%D8%B9%D9%8E%D9%87%D9%92%D8%AF%D9%90%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%91%D9%8E%D9%80%D9%87%D9%90%20%E2%80%9CNaapa%20kwa%20Ahadi%20ya%20Allaah%E2%80%9D
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11267&title=011-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Mwenye%20Kusema%3A%20%D8%A3%D9%8E%D9%82%D9%92%D8%B3%D9%8E%D9%85%D9%92%D8%AA%D9%8F%20%E2%80%9CNimeapa%E2%80%9D%20au%20%D8%A3%D9%8F%D9%82%D9%92%D8%B3%D9%90%D9%85%D9%8F%20%E2%80%9CNinaapa%E2%80%9D
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11268&title=012-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Mwenye%20Kusema%3A%20%D8%A3%D9%8E%D8%B4%D9%92%D9%87%D9%8E%D8%AF%D9%8F%20%D8%A8%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%91%D9%8E%D9%80%D9%87%D9%90%20%E2%80%9CNinashuhudia%20kwa%20Allaah%E2%80%9D%20au%20%D8%A3%D9%8E%D8%B4%D9%92%D9%87%D9%8E%D8%AF%D9%8F%20%E2%80%9CNinashuhudia%E2%80%9D
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11269&title=013-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Mwenye%20Kusema%3A%20%D9%88%D9%8E%D8%A7%D9%8A%D9%92%D9%85%D9%8F%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%91%D9%8E%D9%87%D9%90%20%E2%80%9CWaiymul%20Laah%E2%80%9D
[17] http://www.hadithportal.com/show.php?show=show_tragem&id=5913
[18] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11270&title=014-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Kuapa%20Kwa%20Asiye%20Allaah%20Ni%20Shirki
[19] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11271&title=015-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Masuala%20Mawili%20Tata%20Na%20Majibu%20Yake
[20] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11272&title=016-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Mwenye%20Kuapa%20Kwa%20Asiye%20Allaah%2C%20Nini%20Afanye%3F
[21] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11273&title=017-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Kuapa%20Kwa%20Amana
[22] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11274&title=018-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Kuapa%20Kwa%20Mila%20Isiyo%20Ya%20Uislamu
[23] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11275&title=019-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Aina%20Za%20Yamini%20Za%20Viapo%3A%20Yamini%20Ya%20Upuuzi
[24] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11276&title=020-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3AAina%20Za%20Yamini%20Za%20Viapo%3A%20Yamini%20Ya%20%E2%80%9CGhamuws%E2%80%9D%20%20%28Ya%20Uongo%20Ili%20Kudhulumu%20Haki%20Ya%20Mtu%29
[25] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11277&title=021-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3AAina%20Za%20Yamini%20Za%20Viapo%3A%20Yamini%20Aliyojifunga%20Nayo%20Mtu
[26] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11278&title=022-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Kumwapia%20Kitendo%20Mtu%20Mwingine%20%20Na%20Hukmu%20Kwa%20Mwenye%20Kuapiwa
[27] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11279&title=023-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Matokeo%20Ya%20Kukitekeleza%20Kiapo%20Au%20Kukivunja
[28] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11280&title=024-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Kusema%20%E2%80%9CIn%20Shaa%20Allaah%E2%80%9D%20Katika%20Yamini
[29] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11281&title=025-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3AJe%2C%20Yamini%20Ni%20Kwa%20Mujibu%20Wa%20Mwapaji%20Au%20Mwenye%20Kuapisha%3F
[30] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11282&title=026-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Kafara%20Ya%20Yamini
[31] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11283&title=027-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Nadhiri%20
[32] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11284&title=028-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3AMushkil%20Na%20Ufumbuzi%20Wake
[33] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11285&title=029-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Vigawanyo%20Vya%20Nadhiri%20Na%20Ahkaam%20Zake%3A%20Cha%20Kwanza
[34] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11286&title=030-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Hakuna%20Nadhiri%20Ya%20Kujikurubisha%20Kwa%20Allaah%20Kwa%20Asichokimiliki%20Mtu
[35] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11287&title=031-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3ANadhiri%20Ya%20%E2%80%9CAl-Lijaaj%E2%80%9D%20%28Nadhiri%20Itokanayo%20Na%20Hasira%29
[36] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11288&title=032-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Kafiri%20Akinadhiria%20Jambo%20Jema%20Kisha%20Akasilimu
[37] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11289&title=033-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Vigawanyo%20Vya%20Nadhiri%20Na%20Ahkaam%20Zake%3A%20Kigawanyo%20Cha%20Pili
[38] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11290&title=034-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Nadhiri%20Kwa%20Asiye%20Allaah%20Ni%20Shirki