Dalili Za Kheri Katika Mambo Yamfaayo Maiti
Mwandishi: Mahmuwd Bin Al-Jamiyl
Mfasiri: Abuu Sumayyah
Imepitiwa Na: Abu 'Abdillaah
بسم الله الرحمن الرحيم
Kutangaza kifo kwa ajili ya maslaha:
Hakika kutangaza kifo cha Muislamu ni jambo lisilohimizwa kisheria, kutangazwa kifo cha Muislamu ni kwa haja kwa wale watakaomuosha, watakaomkafini, watakaomswalia na watakaomzika. Njia zinazoruhusiwa kisheria zitatumika kwa haja bila ya kuwepo kwa Taklifu yoyote kwa mfano: watu kujulishana huo msiba, au kwa njia ya simu kama ilivyo siku hizi, vile vile inajuzu kutumia vipaza sauti (microphone) kwa haja inayolazimu kama kutumika vijijini bila ya kuzidisha zaidi ya kutaja kifo chake na wakati wa kuswaliwa na mfano wa hayo.
Katika siku ambayo Mtume aliomboleza kifo cha Najashi siku aliyokufa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) alikwenda katika mswala, akawapanga safu kisha akafanya takbir mara nne (Bukhari na Muslim)
Hali kadhalika alipoomboleza viongozi wa vita vya Mu’ta, Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) alisema, “Zaid alichukua bendera kisha akauawa baada ya hapo akachukuwa Jaafar nae akauawa kisha akachukuwa Abdullah bin Rawaaha naye akauawa…” (Bukhari)
Maombolezo yaliyoharimishwa:
Huku ni kuomboleza kijaahiliya, kama vile kutaja amali za aliyefariki kama kutaja mazuri yake, ushujaa wake na mengine aliyoyafanya, kama vile tuonavyo leo hii katika magazeti na majarida au katika matangazo mbali mbali. Haya ndiyo maombolezo ya Kijaahiliya ambayo Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) ametukataza, na jambo hili linaingia katika jumla ya maombolezo na kelele ambazo zinamdhuru maiti na watu wake wala hayawanufaishi na chochote.
Kutaja mazuri ya maiti na kuacha mabaya yake:
Ikiwa hapana budi kumzungumzia maiti ni bora wamzungumzie mazuri yake ikiwa maiti huyo ni katika jumla ya sifa aliyokuwa nayo na kuacha kuzungumzia mabaya yake ikiwa ni mtu mwenye mabaya, kwani hayo mazuri ndiyo yatakayomnufaisha yeye kwa Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) na asisingiziwe yasiyokuwa ya kwake.
Tunajifunza katika hadithi ya Bukhari na Muslim: kuwa kuna wakati lilipita jeneza na watu wakamtaja mazuri ya yule maiti, Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) akasema, “Amestahiki, amestahiki, amestahiki” jeneza lingine likapita na watu wakataja mabaya ya yule maiti wa pili, Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) akasema, ““Amestahiki, amestahiki, amestahiki” Umar akauliza, ‘Fidia iwe juu yako kwa baba yangu na mama yangu, ilipita jeneza watu wakamtaja kwa kheri ukasema, “Amestahiki, amestahiki, amestahiki” lilipopita jeneza la pili akatajwa vibaya ukasema, “Amestahiki, amestahiki, amestahiki” Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) akasema, “Mtakayemtaja kwa kheri amestahiki pepo, na mtakayemtaja kwa shari amestahiki moto, nyie ni mashahidi wa Allah katika ardhi, nyie ni mashahidi wa Allah katika ardhi.”
Kulipeleka upesi Jeneza:
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) amesema, “Lipelekeni upesi jeneza likiwa ni la mtu mwema basi mtakuwa mnamuwahisha kwenye kheri yenyewe na likiwa kinyume na hivyo basi mnaondosha shari kwenye mabega yenu.” (Bukhari na Muslim)
Katika hadithi nyingine amesema, “Litakapowekwa jeneza na watu wakaweka katika mabega
Muda unaokatazwa kuswalia jeneza na kuzika:
Kutoka kwa Uqbah bin ‘Amir (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema, ‘Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) ametukataza kuswalia na kuzika maiti katika nyakati tatu; pindi linapochomoza jua hadi linapotulia juu, pindi jua linapokuwa katikati hadi linapopinda, pindi jua linapoanza kuzama hadi linapokuwa limezama kabisa.’ (Muslim)
Nyakati zenyewe ni hizi: linapochomoza hadi baada yake
Kumuombea maiti baada ya kuzika:
Ilikuwa ndio ada ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) anapomaliza kuzika akisimama kaburini na husema, “Nyote muombeni Mwenyezi Mungu amsamehe ndugu yenu na amfanye thabiti kwani hivi sasa anahojiwa.” (Abu Daud na wengineo)
Je, Dua ya pamoja husihi?
Tunajifunza kulingana na hadithi iliyopita makosa mbali mbali yenye kufanywa na watu wengi wanaposimama makaburini mmoja wao anasimama na kuanza kuomba dua kwa sauti kubwa na wengine huitikia Amin, ilivyo kama tunavyojifunza katika hadithi iliyotangulia ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) aliwaamrisha masahaba zake wamtakie maghfira maiti wao kila mmoja katika nafsi yake na amuombe Mwenyezi Mungu amthibitishe pindi atakapoulizwa na malaika wawili.
Je, maiti hulakiniwa majibu ya Malaika wawili?
Imepokewa hadithi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam): Kuwa maiti anapowekwa kaburini humjia malaika wawili wakali na humweka kitako na huanza kumhoji: ni nani Mola wako? Ni ipi dini yako? Ni nani Mtume wako? Baada ya maswali hayo kila mja atajibu kulingana na maisha yake yalivyokuwa hapa duniani na Mwenyezi Mungu atawapa Ithbati wale wote waliokuwa wakimuamini yeye kwa kauli iliyo thabiti katika maisha haya ya dunia na huko akhera, na dhalimu atakuwa katika upotevu na Mwenyezi Mungu hufanya ayatakayo.
Maiti hanufaiki na Talqin ya walio hai kwake kama wanavyofanya wengine baada ya kuzika, mtu anasimama kaburini kisha anasema, ‘Ee, fulani bin fulani watakapokujia malaika wawili na wakakuuliza ni nani Mola wako, sema, Mola wangu ni Allah …’ jambo hili halikuthibiti kufanywa na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) au hata masahaba zake, lingekuwa ni jambo la kheri basi lingefanywa na hao wa mwanzo, maadamu hawakufanya basi atakayefanya atakuwa amefanya bid’a, na kila bid’a ni upotevu na kila upotevu ni katika moto. Hili si katika jambo ambalo litakalomnufaisha maiti. Hadithi iliyotangulia haina maelezo zaidi ya kumuombea na kumtaka awe thabiti katika kauli yake na sio kumlakinia kaburini.
Kutoa mkono wa pole (Taazia):
Ni vizuri kuwapa pole wafiwa ili kuwaliwaza na kuwahimiza subira na kuridhika kwa yale aliyotaka Allah (Subhaanahu wa Ta'ala), hivyo basi kuwapunguzia huzuni waliyokuwa nayo na kumbashiria malipo ya wanaosubiri. Ni vizuri zaidi kutumia matamko aliyotumia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) na aliyotufundisha katika kutoa mkono wa pole au atakachoweza mtu maadam hakuna makosa ndani yake.
Je, kunafaa kukusanyika kwa ajili ya Taazia?
Mkusanyiko wa namna hii haufai; sio makaburini au sehemu yoyote maalum kwa ajili ya tukio
Je, wafiwa huwatengenezea wahani chakula?
Haifai kwa wafiwa kutengeneza chakula kwa wahani, lakini kinyume chake ndio sahihi wao ndio wenye haja haswa ya kutengenezewa chakula kwa msiba waliokuwa nao, huzuni ambayo inawafanya kukosa hamu ya kula, hivyo basi ni katika Sunna kwa jamaa wa karibu wa maiti (wasio kuwa wafiwa wa daraja la mwanzo) pamoja na majirani zao kuwatengenezea wafiwa chakula kitakachowatosheleza.
Dua za Waislamu zinamnufaisha maiti:
Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta'ala) amesema, “Na waliokuja baada
Katika hadithi yake Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) amesema, “maombi ya Muislamu kwa nduguye ni yenye kujibiwa, katika kichwa chake kuna malaika aliyewakilishwa kila atakapomuombea nduguye kheri anasema malaika yule: Amin, nawe upate
Kumlipia maiti saumu:
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) amesema, “ Atakayekufa ilhali kaacha deni la funga basi na alipiwe na walii wake.” (Bukhari na Muslim)
Katika sahihi mbili tunasoma: kuwa mwanamke fulani alisafiri baharini akapanda chombo akanadhiria kwa Mwenyezi Mungu kuwa akimuokoa atafunga mwezi mzima, Mwenyezi Mungu akamuokoa lakini hakufunga hadi alipofariki. Wakaja jamaa zake wa karibu
Kumlipia maiti nadhiri:
Sa’ad bin ‘Ubada alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam), ‘Hakika mama yangu amefariki na alinadhiria? Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamjibu, “Mlipie nadhiri yake au tekeleza nadhiri yake.”
Kumtolea sadaka maiti:
Tunasoma katika sahihi mbili kuwa: mtu mmoja alisema, ‘Mama yangu alijisahau na lau angeliweza kusema angetoa sadaka, je, atapata ujira nikimtolea sadaka?’ Mtume akajibu, “Ndio atapata ujira na malipo kwa sadaka hiyo.” Hali kadhalika tunasoma katika sahihi ya Bukhari kuwa, “Sa’ad bin ‘Ubada alifiliwa na mama yake wakati hayupo, akasema, ‘Ee, Mtume wa Allah, mama yangu amefariki nami sipo, je, itamfaa lau nikimtolea sadaka? Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) akajibu, “Ndio (atanufaika kwa sadaka hiyo)” kisha Sa’ad akasema
Kuacha huru mtumwa, kutoa sadaka na kuhiji humnufaisha Muislamu:
Abu Daud na wengineo wamepokea kuwa, “ ‘Al-Aas bin Wail As-sahami aliusia waachwe huru watumwa mia moja, mwanawe Hisham akawaacha huru watumwa hamsini tu. Mwanawe mwingine aitwae Amruu akataka kuwaacha wale watumwa wengine hamsini waliobakia, akaenda kwanza kumuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam). alipomfikia akamuuliza, ‘Ewe Mtume wa Allah, hakika baba yangu ameusia waachwe huru watumwa mia moja, lakini ndugu yangu Hisham amewaacha watumwa hamsini tu, hivyo wamebaki hamsini. Je, niwaache huru? Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) akajibu, “lau baba yenu angelikuwa Muislamu na mkaacha huru watumwa au mkamtolea sadaka au mngelimhijia basi angenufaika na hayo na malipo yake yangemfikia.”
Kumhijia asiyehiji:
Imepokewa na Bukhari kuwa: mwanamke kutoka kabila la Juhayna alikwenda kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam), akamuuliza, ‘Mama yangu aliweka nadhiri kuwa atahiji lakini hakuhiji hadi alipofariki, je, nimuhijie? Mtume akamjibu, “Ndio, mhijie, je, huoni kuwa
Katika Sahihi Muslim inasmuliwa kuwa mwanamke kutoka kabila la Khath’am alisema, ‘Baba yangu ni mzee
Katika hadithi nyingine sahihi iliyokuwa mashuhuri, ‘kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) alimsikia mtu akisema, ‘Labaika Allahumma kwa Shubruma, Mtume akamwambia mtu yule, ‘Je, huyo Shubruma ni nani? Yule mtu akajibu, ‘Ni ndugu au jamaa yangu wa karibu.’ Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) akamuuliza, ‘Je, wewe mwenyewe umehiji.? Yule mtu akajibu, ‘hapana.’ Hapo Mtume akasema, “Jihijie mwenyewe kwanza kisha muhijie Shubrama.”
Kuzuru kaburi
Ziara ya makaburi ni jambo lililoruhusiwa kisheria, ni jambo lenye faida kwa walio hai ili wawaidhike na iwakumbushe na akhera ajue mwenye kuzuru kaburi kuwa hapo alipo nduguye naye atakuwamo siku moja. Hali kadhalika faida nyingine ni kuwaombea nduguze waislamu na huyo maiti wake. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) amesema, “Nilikuwa nimewakataza kwanza kuzuru makaburi lakini kuanzia sasa yatembeleeni.” (Muslim) katika lafdhi nyingine hadithi inasema, “Kwani huko kuzuru makaburu hukukumbusheni na akhera.” (Ahmad)
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) wakati fulani alilitembelea kaburi la mama yake akalia na walio pambizoni mwa Mtume nao wakalia
Wakati tunazungumzia suala hili yapasa kuangalia sura nyingi
( وَ يَرْحَمُ اللَّهُ الْمُسْتَقْدِمِينَ مِنَّاوَالْمُسْتَأْخِرِينَ) نَسْـاَلُ اللهَ لَنَـا وَلَكُـمْ العَـافِيَةَ.
Je, Yafaa kusoma Qur’an Makaburini?
Hili ambalo halikufanywa na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam), hakuliamrisha lakini aliamrisha tu kusomwa dua na kuwaombea maghfira kwa Mwenyezi Mungu. Hakupenda watu wasome Qur’an makaburini kwa hadithi yake aliyosema, “Msizifanye nyumba zenu makaburi, kwani shetani hukimbia na huchukizwa na nyumba ambayo itasomwa
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/53
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1479&title=Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1480&title=01-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Anapougua%20Maradhi%20anayohofiwa%20kufa%20nayo
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1481&title=02-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kuridhika%20na%20kuwa%20na%20subira%20kwa%20Qadar%20ya%20Allah%20%28Subhaanahu%20wa%20Ta%27ala%29
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1482&title=03-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kumdhania%20mema%20Allah%20%28Subhaanahu%20wa%20Ta%27ala%29
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1483&title=04-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Asitamani%20Mauti
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1484&title=05-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kutekeleza%20haki%20za%20watu
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1485&title=06-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Nia%20na%20usia%20wa%20kurejesha%20haki
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1486&title=07-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kinachotakiwa%20kiwepo%20katika%20usia%3A
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1487&title=08-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Wasia%20kwa%20wasiorithi%20katika%20ndugu%20na%20jamaa%20wa%20karibu
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1488&title=09-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Hakuna%20kuusiwa%20mali%20mwenye%20kurithi
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1489&title=10-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Usia%20kwa%20theluthi%20ya%20mali%20au%20chini%20ya%20hapo
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1490&title=11-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kuacha%20kufanya%20maovu%20%28madhara%29%20katika%20kuusia
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1491&title=12-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kutokutekeleza%20Usia%20wenye%20madhara
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1492&title=13-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Baadhi%20ya%20matendo%20yenye%20kumfaa%20maiti
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1493&title=14-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kauli%20ya%20Mwisho%20ya%20Mtu%20kuwa%20ni%20Laa%20ilaha%20illa%20llahi%20
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1494&title=15-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kumuombea%20kheri%20Mwenye%20kufa
[18] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1495&title=16-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kumfunga%20macho%20na%20kumuombea%20atakapokufa
[19] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1496&title=17-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20%20Je%2C%20Surat%20Yaasin%20husomwa%20kwa%20maiti%3F
[20] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1497&title=18-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kulipa%20Deni%20kwa%20mali%20ya%20Maiti
[21] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1498&title=19-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kujitolea%20kwa%20kumlipia%20madeni%20Maiti
[22] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1499&title=20-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Walii%20kumlipia%20deni%20maiti
[23] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1500&title=21-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kuacha%20kuomboleza%20kwa%20sauti%20ni%20rehema%20kwa%20maiti
[24] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1501&title=22-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kilio%20chenye%20kukubaliwa%20kisheria
[25] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1502&title=23-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kutangaza%20kifo%20kwa%20ajili%20ya%20maslaha
[26] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1503&title=24-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kutangazwa%20kifo%20kwa%20lengo%20la%20kumuombea
[27] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1504&title=25-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Maombolezo%20yaliyoharimishwa
[28] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1505&title=26-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kutaja%20mazuri%20ya%20maiti%20na%20kuacha%20mabaya%20yake
[29] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1506&title=27-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kuoshwa%20maiti%20upesi
[30] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1507&title=28-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kinachomlazimu%20mwenye%20kukosha
[31] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1508&title=29-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kumkafini%20na%20kumpamba%20maiti
[32] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1509&title=30-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Je%2C%20maiti%20itahamishwa%20kutoka%20katika%20nchi%20aliyofia%20na%20kupelekwa%20nchini%20kwake%3F
[33] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1510&title=31-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kulisindikiza%20Jeneza
[34] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1511&title=32-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Swala%20ya%20Jeneza
[35] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1512&title=33-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Sifa%20ya%20swala%20ya%20Jeneza
[36] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1513&title=34-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Dua%20zilizopokelewa%20katika%20dua%20za%20Jeneza
[37] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1514&title=35-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kulipeleka%20upesi%20Jeneza
[38] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1515&title=36-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Muda%20unaokatazwa%20kuswalia%20jeneza%20na%20kuzika
[39] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1516&title=37-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kumuombea%20maiti%20baada%20ya%20kuzika
[40] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1517&title=38-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Je%2C%20Dua%20ya%20pamoja%20husihi%3F
[41] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1518&title=39-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Je%2C%20maiti%20hulakiniwa%20majibu%20ya%20Malaika%20wawili%3F
[42] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1521&title=42-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kutoa%20mkono%20wa%20pole%20%28Taazia%29
[43] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1522&title=43-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Je%2C%20kunafaa%20kukusanyika%20kwa%20ajili%20ya%20Taazia%3F
[44] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1523&title=44-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Je%2C%20wafiwa%20huwatengenezea%20wahani%20chakula%3F
[45] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1524&title=45-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Matamko%20ya%20taazia%20ni%20haya%20yafuatayo
[46] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1525&title=46-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Matamko%20yaliyokatazwa
[47] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1526&title=47-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Dua%20za%20Waislamu%20zinamnufaisha%20maiti
[48] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1527&title=48-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kumlipia%20maiti%20saumu
[49] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1528&title=49-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kumlipia%20maiti%20nadhiri
[50] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1529&title=50-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kumtolea%20sadaka%20maiti
[51] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1530&title=51-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kutoa%20sadaka%20mali%20ambayo%20haikuusiwa
[52] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1531&title=52-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kuacha%20huru%20mtumwa%2C%20kutoa%20sadaka%20na%20kuhiji%20humnufaisha%20Muislamu
[53] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1532&title=53-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kumhijia%20asiyehiji
[54] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1533&title=54-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Au%20kijana%20mwema%20atakayemuombea%20dua
[55] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1534&title=55-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Je%2C%20husomewa%20Qur%E2%80%99an%20na%20Al-Faatiha%3F
[56] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1535&title=56-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Je%2C%20huswali%20swala%20yake%20na%20ya%20babake%20au%20hufunga%20kwa%20funga%20yao%3F
[57] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1536&title=57-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kuzuru%20kaburi%20lake%20na%20kumuombea
[58] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1537&title=58-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Je%2C%20ni%20ruhusa%20kwa%20wanawake%20kutembelea%20makaburi%3F
[59] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1538&title=59-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Matamko%20yanayotumika%20katika%20kuwaombea%20wafu%20makaburini
[60] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1539&title=60-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Je%2C%20Yafaa%20kusoma%20Qur%E2%80%99an%20Makaburini%3F
[61] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F1540&title=61-Dalili%20Za%20Kheri%20Katika%20Mambo%20Yamfaayo%20Maiti%3A%20Kuzuru%20makaburi%20wakati%20wa%20matukio%20maalum