Ameamka Huku Anasinzia Akala Chakula Kisha Akatambua Kuwa Alfajiri Imeshaingia
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Niliamka asubuhi moja huku bado nusu nimelala (nasinzia) nikaenda jikoni haraka na kula chakula, lakini nilivyoanza kula, nimetazama saa nikaona kuwa ni saa 10: 45 Alfajiri Na wakati wa Alfajiri huku Tabuk (Kaskakazini Saudi Arabia) ni 10: 15 Alfajiri. Kwa hiyo nikasimama kula na kuanza kufunga, nikijua kuwa nimekula kama vijiko vitatu au vinne. Je, Sheikh inanipasa nilipe Swawm hii au hainipasi?
JIBU:
Kama hali ni kama ulivyoeleza, basi inakupasa ulipe siku hiyo kwani ulikula baada ya wakati wa Alfajiri kupita.
Allaah Atujaalie At-Tawfiyq. Swalah na Salaam ziwe juu ya Nabiy wetu Muhammad, familia yake, na Maswahaba zake.
[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah lil-Buhuwth Al-'Ilmiyyah wal-Iftaa. - Fataawaa Ramadhwaan - Mjalada 2, Uk 569, Fatwa Namba 552]
Hakujua Kama Swawm Ilikuwa Fardhi Kwake; Je, Alipe Swawm Zilizompita?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Miaka kumi nyuma, nilifikia umri wa kubaleghe baada ya kuona alama zake. Kwa hiyo mwaka wangu wa mwanzo wa ujana nimeacha Ramadhwaan imenipita na sikufunga bila ya kuwa na udhuru wowote, ila ni kwa sababu ya kutokujua kama ni fardhi wakati ule. Je, Inanipasa nilipe siku hizo na je, Inanipasa nifanye mengine juu yake kama kulipa kafara?
JIBU:
Inakupasa ulipe siku zote zilizokupita za mwezi huo ambao hukuzifunga, na kuomba maghfirah na tawbah (Kwa Allaah Ta’aalaa) kisha ulipe kafara nayo ni nusu swaa' (nusu pishi sawa na vibaba viwili, ambayo ni sawa na 1.5kg) ya chakula kinacholiwa katika nchi hiyo kama tende, au mchele au chochote chengine kama unao uwezo. Kama wewe ni maskini na huna uwezo basi inatosha kama utafunga kulipa hizo siku usizofunga.
[Imaam Ibn Baaz - Fataawaa Ramadhwaan – Mjalada 2, Uk 559, Fatwa Namba 542; Al-Fataawaa libni Baaz - Kitaab Ad-Da'wah, Mj. 2, Uk. 158]
Amefariki Wakati Bado Alikuwa Anadaiwa Swiyaam Za Ramadhwaan
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Nini hukmu ya mtu aliyefariki na huku anadaiwa Swiyaam za Ramadhwaan?
JIBU:
Ikiwa amefariki na huku anadaiwa swiyaam za Ramadhwaan, basi mmoja wa aliyekuwa na jukumu la mambo yake katika jamaa zake walio karibu naye au warithi wake wafunge kwa ajili yake. Hii imetajwa katika Hadiyth kutoka kwa ‘Aaishah (Radhiwya Allaahu ‘anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Yeyote aliyekufa wakati ana deni la (Swawm) ya Ramadhwaan, basi yule mwenye jukumu la mambo yake afunge kwa ajili yake)).
Ikiwa aliyekuwa na jukumu la mambo yake hatofunga kwa ajili yake basi amlishe masikini mmoja kwa kila siku moja aliyokuwa akidaiwa.
[Imaam Ibn ‘Uthyamiiyn Fataawas Ramadhwaan - Mjalada 2, Ukurasa 626, Fatwa Namba 626;
Fiqh Al-'Ibaadaat libni 'Uthaymiyn - Ukurasa 202-203]
Hukmu Ya Aliyeacha Swiyaam Miaka Ya Nyuma
Imaam Ibn ‘Uthyamiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Nini hukmu ya Muislamu aliyekuwa hafungi miaka ya nyuma ingawa alikuwa akitimiza fardhi nyingine, na kuacha swiyaam huko kulikuwa bila ya kizuizi au sababu yoyote? Je, Inampasa alipe swiyaam hizo hata baada ya kutubu?
JIBU:
Iliyokuwa sahihi ni kwamba haimpasi kulipa swiyaam za nyuma zilizompita alizokuwa hazifungi baada ya kutubu. Hii ni kwa sababu ‘amali zote za ‘ibaadah kwa Waumini zimewekwa katika muda wake mahsusi uliotajwa.
Kwa hiyo, ikiwa mtu atawacha kufanya ‘ibaadah hiyo au kuichelewesha na muda upite bila ya sababu yoyote, Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Hatapokea ‘amali hiyo. Na kutokana na hayo, hakuna maana kulipa yaliyompita. Lakini, inampasa atubu kikweli kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na azidishe sana ‘amali njema, na yule mwenye kuomba msamaha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), basi Allaah Atamsamehe.
[Imaam Ibn ‘Uthyamiyn - Fataawaa Ramadhwaan - Mjalada 2, Uk 556, Fatwa Namba 539;
Fataawaa Shaykh Muhammad Swaalih Al-'Uthaymiyn – Mjalada 1, Ukurasa 536]
Hakulipa Deni La Ramadhwaan Iliyopita Je, Itakuwa Ni Dhambi Na Je, Alipe Kafara?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Aliyekuwa ana deni la Ramadhwaan iliyopita hakulipa hadi imeingia Ramadhwaan nyingine. Je, Atakuwa na dhambi na Je, itabidi alipe kafara?
JIBU:
Mtu yeyote aliyekuwa na deni kutoka Ramadhwaan iliyopita, inampasa alipe kabla ya kuingia Ramadhwaan nyengine. Inaruhusiwa kuchelewesha kulipa hadi mwezi wa Sha'baan. Lakini ikiingia Ramadhwaan nyingine na yeye hakulipa Swawm zilizompita bila ya sababu yoyote, atakuwa amefanya dhambi na itabidi alipe hilo deni pamoja na kulisha maskini mmoja kwa kila siku moja ya deni. Na hivi ndivyo walivyokuwa wakifanya Maswahaba wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kama alivyowaamrisha.
Kipimo cha chakula ni nusu ya pishi (sawa na vibaba viwili au 1.5kg) ya chakula kinacholiwa sana na watu katika nchi anayoishi. Kila siku moja ya deni alishe maskini mmoja kwa kipimo hiki. Anaweza kuwapa watu mbali mbali au hata mtu mmoja.
Na kwa yule aliyekuwa anao udhuru wa kutokuweza kufunga kwa sababu ya safari au ugonjwa basi yeye inampasa swawm pekee bila ya kulisha masikini kutokana na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۗ
Na atakayekuwa mgonjwa au safarini, basi (inapaswa kulipa) idadi sawa katika masiku mengineyo. [Al-Baqarah: 185]
Na Allaah (Ta’aalaa) Ndiye Mwenye kujaalia tawfiyq.
[Imaam Ibn Baaz - Fataawa Ramadhwaan – Mjalada 2, Uk 555, Fatwa Namba 537;
Al-Fataawa libni-Baaz - Kitaab Ad-Da'wah, Mjalada 2, Uk 158-159]
Ameamka Na Huku Anasinzia Kisha Akanywa Maji Lakini Hakumbuki Wakati
Al-Lajnah Ad-Daimah
www.alhidaaya,com [11]
SWALI:
Nimeamka usiku mmoja wa Ramadhwaan nikanywa maji yaliyoko karibu na kitanda changu, kisha nikarudi kulala. Nilipoamka nimeona watu wanarudi kutoka kuswali Alfajiri na asubuhi ilishaingia nje kweupe kabisa. Kwa hali hii nikajiuliza wakati gani nilikunywa maji? Ilikuwa kabla ya Alfajiri au baada ya Alfajiri? Najua kuwa nilikuwa nimesinzia lakini nina hakika kuwa nilikunywa maji. Je, Sheikh inanipasa niilipe siku hii au hainipasi kuilipa?
JIBU:
Kama hali ilikuwa kama ulivyoelezea basi iliyo sahihi ni udhanie kuwa ilikuwa ni usiku kwa hiyo funga ilikuwa ni sawa mpaka ikuthibitikie kuwa kumbe kunywa maji huko kulikuwa baada ya kuingia Alfajiri hapo tena itakubidi uilipe siku hiyo.
Allaah Atujaalie At-Tawfiyq. Swalah na Salaam ziwe juu ya Nabiy wetu Muhammad, familia yake, na Maswahaba zake.
[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah lil-Buhuwth Al-'Ilmiyyah wal-Iftaa - Fatwa Namba 4181]
Hakuweza Swiyaam Kwa Muda Wa Miaka Minne Kwa Sababu Ya Ugonjwa
Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu-Allaah)
SWALI:
Mtu alifikwa na maradhi ya kudumu, na madaktari wakamnasihi asifunge. Akapona ugonjwa huo baada ya miaka minne. Afanye nini sasa baada ya Allaah kumponyesha. Alipe siku zilizopita?
JIBU:
Mtu yeyote aliyokuwa hakuweza Swiyaam kwa sababu ya ugonjwa, kisha akapona anatakiwa alipe Swiyaam za siku alizokuwa hakufunga kwa sababu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:
أَيَّامًا مَّعْدُودَاتٍ ۚ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۚ
184. (Swiyaam ni) Siku za kuhesabika. Lakini atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu, au yuko safarini, basi (inapaswa kulipa) idadi sawa katika masiku mengineyo
Kwa hiyo kama hakufunga Ramadhwaan nne zilizofuatana, kisha akapona, inampasa alipe siku zake kwa utaratibu maalum. Lakini anaweza kufunga siku mbali mbali (si moja kwa kwa moja) kutokana na uwezo wake hadi amalize na ajitoe katika jukumu hili. Haikuwajibika kwake kufunga zote pamoja bila ya kupumzika kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
Basi mcheni Allaah muwezavyo, [At-Taghaabun: 16]
Na hivi ndivyo ilivyo kwa vile wakati wa kulipa uko mwingi.
[Shaykh Swaalih Al-Fawzaan -
Fataawaa Ramadhwaan – Mjalada 2, Uk 592, Fatwa Namba 577;
Al-Muntaqaa min Fataawaa Ash-Shaykh Swaalih Ibn Fawzaan – Mjalada 3, Uk 139]
Mwenye Swawm Ya Kulipa Kutoka Ramadhwaan Iliyopita, Basi Ni Lazima Ailipe Kabla ya Ramadhwaan Nyingine Kuingia
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Hairuhusiwi kuahirisha ulipaji deni wa Swawm (ya Ramadhwaan iliyopita) hadi ikaingia Ramadhwaan nyingine bila udhuru (unaokubalika kishariy'ah).
Hiili ni kwa sababu ya maelezo ya mama wa Waumini 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): 'Nilikuwa na deni la Swawm ya Ramadhwaan na sikuweza kulipa ila katika Sha'baan.' [Al-Bukhaariy]
[Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 59]
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/261
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8453&title=Fataawaa%3A%20Kulipa%20Swawm%20Na%20Kafara
[4] http://www.alhidaaya.com
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8455&title=01-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Ameamka%20Huku%20Anasinzia%20Akala%20Chakula%20Kisha%20Akatambua%20Kuwa%20Alfajiri%20Imeshaingia
[6] http://alhidaaya
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8456&title=02-Imaam%20Ibn%20Baaz%20%3A%20Hakujua%20Kama%20Swawm%20Ilikuwa%20Fardhi%20Kwake%3B%20Je%2C%20Alipe%20Swawm%20Zilizompita%3F
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8457&title=03-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Amefariki%20Wakati%20Bado%20Alikuwa%20Anadaiwa%20Swiyaam%20Za%20Ramadhwaan
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8458&title=04-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthyamiyn%3A%20Hukmu%20Ya%20Aliyeacha%20Swiyaam%20Miaka%20Ya%20Nyuma
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8462&title=05-Imaam%20Ibn%20Baaz%20%3A%20Hakulipa%20Deni%20La%20Ramadhwaan%20Iliyopita%20Je%2C%20Itakuwa%20Ni%20Dhambi%20Na%20Je%2C%20Alipe%20Kafara%3F
[11] http://www,alhidaaya,com
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8461&title=06-Al-Lajnah%20Ad-Daimah%3A%20Ameamka%20Na%20Huku%20Anasinzia%20Kisha%20Akanywa%20Maji%20Lakini%20Hakumbuki%20Wakati
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8463&title=07-Shaykh%20Swaalih%20Al-Fawzaan%3A%20Hakuweza%20Swiyaam%20Kwa%20Muda%20Wa%20Miaka%20Minne%20Kwa%20Sababu%20Ya%20Ugonjwa
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8571&title=08-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Mwenye%20Swawm%20Ya%20Kulipa%20Kutoka%20Ramadhwaan%20Iliyopita%2C%20Basi%20Ni%20Lazima%20Ailipe%20Kabla%20ya%20Ramadhwaan%20Nyingine%20Kuingia