Je, Swalaah Ya ‘Iyd Ina Adhana Na Iqaamah?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Swalaah ya ‘Iyd haina Adhana wala Iqaamah."
[Majmuw’ Al-Fataawaa (16/237)]
Hukmu Ya Kunadi Kwa Ajili Ya Swalaah Ya ‘Iyd
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) Na Al-Lajnah Ad-Daimah
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
"Kunadi kwa ajili ya Swalaah ya ‘Iyd ni bid’ah, haina asili."
[Majmuw’ Al-Fataawaa (13/23)]
Al-Lajnah Ad-Daimah wamesema:
"Kunadi kwa ajili ya Swalaah za ‘Iyd mbili haijuzu bali hivyo ni bid’ah."
[Al-Lajnah Ad-Daimah (8//316)]
Sifa Ya Swalaah Ya ‘Iyd
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
i-Inaletwa Takbiyrah Al-Ihraam na inafunguliwa kwa du’aa kisha zinaletwa Takbiyrah sita (jumla zitakuwa saba) kisha inasomwa Al-Faatihah na Suwrah ima (Sabbihisma) au (Qaaf) katika Raka’ah ya kwanza.
ii-Katika Raka’ah ya pili, atakaposimama kutoka katika kusujudu, atainuka huku akileta Takbiyrah kisha ataleta Takbiyrah tano baada ya kusimama kwake. Kisha atasoma Al-Faatihah na Suwrah. Ikiwa atasoma katika Rakaa ya kwanza (Sabbihismaa) basi asome katika Rakaa ya pili (Al-Ghaashiyah). Na pindi akiwa amesoma katika Rakaa ya kwanza (Qaaf), basi asome katika Rakaa ya pili (Iqtarabatis-Saa’ah .. Suwrah Al-Qamar)
[Majmuw’ Al-Fataawaa (16/223)]
Hukmu Ya Anayepunguza Takbiyrah Al-Ihraam Katika Swalaah Ya ‘Iyd
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Swalaah yake ni sahihi ikiwa atafupisha Takbiyrah Al-Ihraam kwa sababu Takbiyrah Al-Ihraam za ziada ni Sunnah."
[Majmuw’ Al-Fataawaa (16/238)]
Wakati Gani Inasomwa Du’aa Ya Kufungulia Katika Swalaah Ya ‘Iyd?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Du’aa ya kufungulia Swalaah inasomwa baada ya Takbiyrah Al-Ihraam na ni jambo lenye wasaa katika hili hata ikiwa atachelewesha kusoma du’aa ya kufungulia pale mwishoni mwa Takbiyrah hakuna ubaya."
[Majmuw’ Al-Fataawaa (16/240)]
Nini Kinasemwa Baina Ya Kila Takbiyrah Na Takbiyrah Katika Swalaah Za ‘Iyd Mbili?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) Na Al-Lajnah Ad-Daaimah
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Hakuna dhikr (utajo) maalumu bali ni kumhimidi Allaah na kumtukuza na kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa aina yoyote apendayo na ikiwa ataacha kufanya hivyo basi hakuna ubaya kwani hiyo ni mustahab."
[Majmuw’ Al-Fataawaa (16/241)]
Al-Lajnah Ad-Daimah wamesema:
Inapaswa amhimidi Allaah (AlhamduliLLaah) na amsabbih (Subhaana Allaah) na Amkabbir (Allaahu Akbar) na amswalie Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) baina ya kila Takbiyrah mbili.
[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/302)]
Nini Hukmu Ikiwa Imaam Atasahau Takbiyrah Za ‘Iyd Mpaka Atakapofikia Kisomo?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Ikiwa atasahu Takbiyrah katika Swalaah ya ‘Iyd, mpaka akafikia kusoma (Suwrah), itaanguka (itakuwa haina haja tena), kwa sababu Sunnah imepita mahali pake, kama vile atakavyosahau du’aa ya kufungulia mpaka akafikia kusoma (Suwrah) basi huanguka."
[Majmuw’ Al-Fataawaa (16/244)]
Nini Hukmu Ikiwa Imaam Amenitangulia Nikakosa Takbiyrah Za Ziada?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Ikiwa ameingia pamoja na Imaam akiwa katika Takbiyrah basi akabbir (Allaahu Akbar) kwanza, kisha amfuate Imaam katika yaliyobakia na itamuondokea kwake yaliyompita yatakuwa hayampasi tena."
[Majmuw’ Al-Fataawaa (16/245)]
Ikiwa Mtu Itampita Kitu Katika Takbiyrah Za ‘Iyd
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Yatamuondokea (hayatompasa) yale yaliyompita, na hivyo hivyo kama vile akisahau au mpaka akafikia kusoma (Suwrah) basi haleti tena (harudii tena), kwa sababu Sunnah imepita mahali pake Lakini ikiwa imempita pamoja na Imaam Rakaa kamili basi inabidi alete Takbiyrah za Rakaa hiyo iliyompita.
[Majmuw’ Al-Fataawaa (16/241)]
Ikiwa Ameingia Swalaah Ya ‘Iyd Wakati Imaam Amemaliza Rakaa Ya Kwanza; Je, Ailipe?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Ailipe anapomaliza Imaam kutoa salaam, yaani ailipe kwa kuleta Takbiyrah zake."
[Majmuw’ Al-Fataawaa (16/256)]
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/261
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8640&title=%20Fataawaa%3A%20Swalaah%20Ya%20%27Iyd%20Na%20Siku%20Ya%20%27Iyd
[4] http://www.alhidaaya.com
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8641&title=01-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Je%2C%20Swalaah%20Ya%20%E2%80%98Iyd%20Ina%20Adhana%20Na%20Iqaamah%3F
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8642&title=02-Imaam%20Ibn%20Baaz%20Na%20Al-Lajnah%20Ad-Daimah%3A%20Hukmu%20Ya%20Kunadi%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Swalaah%20Ya%20%E2%80%98Iyd
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8643&title=03-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Sifa%20Ya%20Swalaah%20Ya%20%E2%80%98Iyd
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8644&title=04-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Hukmu%20Ya%20Anayepunguza%20Takbiyrah%20Al-Ihraam%20Katika%20Swalaah%20Ya%20%E2%80%98Iyd
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8645&title=05-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Wakati%20Gani%20Inasomwa%20Du%E2%80%99aa%20Ya%20Kufungulia%20Katika%20Swalaah%20Ya%20%E2%80%98Iyd%3F
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8646&title=06-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%20Na%20Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Nini%20Kinasemwa%20Baina%20Ya%20Kila%20Takbiyrah%20Na%20Takbiyrah%20Katika%20Swalaah%20Za%20%E2%80%98Iyd%20Mbili%3F
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8647&title=07-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Nini%20Hukmu%20Ikiwa%20Imaam%20Atasahau%20Takbiyrah%20Za%20%E2%80%98Iyd%20Mpaka%20Atakapofikia%20Kisomo%3F
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8648&title=08-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Nini%20Hukmu%20Ikiwa%20Imaam%20Amenitangulia%20Nikakosa%20Takbiyrah%20Za%20Ziada%3F
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8649&title=09-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Ikiwa%20Mtu%20Itampita%20Kitu%20Katika%20Takbiyrah%20Za%20%E2%80%98Iyd
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8650&title=10-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Ikiwa%20Ameingia%20Swalaah%20Ya%20%E2%80%98Iyd%20Wakati%20Imaam%20Amemaliza%20Rakaa%20Ya%20Kwanza%3B%20Ailipe%3F