أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com [1]
Al-Anfaal: 1
01- Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu ngawira. Sema: Ngawira ni ya Allaah na Rasuli.
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَنفَالِ ۖ قُلِ الْأَنفَالُ لِلَّـهِ وَالرَّسُولِ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَصْلِحُوا ذَاتَ بَيْنِكُمْ ۖ وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿١﴾
Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu ngawira. Sema: Ngawira ni ya Allaah na Rasuli. Basi mcheni Allaah na suluhisheni yaliyo baina yenu. Na mtiini Allaah na Rasuli Wake mkiwa ni Waumini. [Al-Anfaal: 1]
Sababun-Nuzuwl:
Aayah hii imeteremka kama alivyohadithia Musw’ab bin Sa’d (رضي الله عنه) kutoka kwa baba yake kwamba: “Aayah nne za Qur-aan zimeteremshwa kuhusu mimi. Niliukuta upanga (katika ngawira za vita). Ukaletwa kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Baba yangu akasema: Ee Rasuli wa Allaah, nipatie mimi. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Uweke hapa! Kisha (baba yangu) akasimama na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: “Uweke ulipoukuta.” Kisha akasimama akasema: Ee Rasuli wa Allaah, nipatie mimi. Akamwambia: “Uweke!” Akasimama akasema tena: Ee Rasuli wa Allaah nipatie. Je, nitafanywa kama ambaye hana sehemu (ya ngawira)? Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: “Uweke ulipoukuta.” Hapo ikataremshwa:
يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَنفَالِ ۖ قُلِ الْأَنفَالُ لِلَّـهِ وَالرَّسُولِ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَصْلِحُوا ذَاتَ بَيْنِكُمْ ۖ وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿١﴾
Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu ngawira. Sema: Ngawira ni ya Allaah na Rasuli.
[Muslim Kitaab Al-Jihaad was-Siyar, Baab Al-Anfaal]
Pia Musw-‘ab bin Sa’d amehadithia kutoka kwa baba yake (Sa’d bin Abiy Waqqaasw): “Nilikuja kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) siku ya Badr nikiwa na upanga nikasema: Ee Rasuli wa Allaah, hakika Allaah Amenipa shifaa ya kifua changu kutokana na adui leo, basi nipe upanga.” Akasema: “Upanga si wangu wala si wako.” Nikaondoka huku nikisema: “Leo atapewa huo (upanga) mtu ambaye hakutiwa mtihanini kama mimi.” Mara akaja mjumbe akaniambia: “Itikia.” Nikadhani kwamba imeteremshwa Wahy kuhusu mimi kutokana na kauli yangu. Nikaenda kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ulinitaka nikupe upanga huu lakini huu haukuwa wangu wala wako. Lakini sasa Allaah Amenipa mimi kwa hiyo sasa ni wako.” Kisha akasoma:
يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَنفَالِ ۖ قُلِ الْأَنفَالُ لِلَّـهِ وَالرَّسُولِ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَصْلِحُوا ذَاتَ بَيْنِكُمْ ۖ وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿١﴾
Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu ngawira. Sema: Ngawira ni ya Allaah na Rasuli.
[Abuu Daawuwd, Kitaab Al-Jihaad]
Links
[1] http://alhidaaya.com
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9035&title=001-Asbaabun-Nuzuwl%3A%20Al-Anfaal%20Aayah%20001%3A%20%D9%8A%D9%8E%D8%B3%D9%92%D8%A3%D9%8E%D9%84%D9%8F%D9%88%D9%86%D9%8E%D9%83%D9%8E%20%D8%B9%D9%8E%D9%86%D9%90%20%D8%A7%D9%84%D9%92%D8%A3%D9%8E%D9%86%D9%81%D9%8E%D8%A7%D9%84%D9%90%20%DB%96%20%D9%82%D9%8F%D9%84%D9%90%20%D8%A7%D9%84%D9%92%D8%A3%D9%8E%D9%86%D9%81%D9%8E%D8%A7%D9%84%D9%8F%20%D9%84%D9%90%D9%84%D9%91%D9%8E%D9%80%D9%87%D9%90%20%D9%88%D9%8E%D8%A7%D9%84%D8%B1%D9%91%D9%8E%D8%B3%D9%8F%D9%88%D9%84%D9%90%20