Wudhuu Kuharibika Wakati Wa Twawaaf Je Arudie Twawaaf?
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Nilipokuwa nikifanya twawaaf katika Ka'bah na nilipofika twawaaf ya tano nilihisi kama nimetokwa na pumzi. Iblisi akanitia wasiwasi lakini nikapuuza kwa sababu sikuwa na hakika na sikusikia harufu. Nikajikinga naye kwa Allaah na nikaweka imani yangu kwa Allaah nikaendelea kufanya twawaaf. Kisha nilipomaliza nikaswali Rakaa mbili. Je twawaaf yangu itakuwa ni sahihi?
JIBU:
Hukmu ya asasi ni kuwa kuwa utakuwa umebakia katika hali ya twahara, kwani kutia shaka tu kama umetokwa na pumzi hakumtoi mtu katika twahara mpaka uwe na uhakika. Hivyo twawaaf na Swalaah yako ni sahihi na salama In Shaa Allaah.
[Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah lil-Buhuwth al-'Ilmiyyah wal-Iftaa. Mjalada 11, Uk. 244, Swali Namba 4 la Fatwa Namba 11935 - Imejumuisha:
Kiongozi Mkuu: Shaykh ‘Abdul-’Aziyz bin ‘Abdillaah bin Baaz
Msaidizi Kiongozi Mkuu: Shaykh ‘Abdur-Razzaaq 'Afiyfiy
Mjumbe: Shaykh ‘Abdullaah bin Ghudayyaan
Mjumbe: Shaykh ‘Abdullaah bin Qu’uwd]
Wudhuu Katika Twawaaf Na Sa’ay
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Je, ni lazima kuwa na wudhuu ili kufanya twawaaf na sa’ay?
JIBU:
Kuwa na wudhuu ni lazima kwa ajili ya twawaaf pekee. Ama sa’ay ni bora kuwa na wudhuu. Lakini pindi ukimtoka mtu wudhuu basi sa’ay hubakia kuwa ni sahihi.
[Fataawa al-Hajj wal ‘Umrah waz-Ziyaarah]
Rai Za ‘Ulamaa Wengineo Kuhusu Kulazimika Wudhuu Katika Twawaaf:
Rai za ‘Ulamaa wengineo kama Imaam Ibn Haniyfah (Rahimahu Allaah), Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) katika Majmuw’ Al-Fataawaa (21/273), wameona kwamba wudhuu haulazimiki katika Twawaaf. Pia Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) ambaye ametoea maelezo marefu kuhusiana na swala hili katika Ash-Sharh Al-Mumti’ (7/300), kwamba hakuna ulazima wa kuwa na wudhuu katika twawaaf. Akataja pia mashaka ya kutoka nje ya twawaaf kwenda kutafuta sehemu za kutia wudhuu kwa zama hizi ambazo ni zahma kubwa mno humo Masjid Al-Haraam, khasa katika twawaaf. Hivyo akafutu kuwa mtu akitokwa na pumzi na wudhuu wake ukharibika basi aendelee tu kutekeleza twawaaf yake bila ya kwenda kutia wudhuu kwa ajili ya kuendeleza au kuanza upya, na twawaaf yake itakuwa Swahiyh In Shaa Allaah.
Wanawake Kuharakiza Mwendo Baina Ya Nguzo Za Kijani Katika Sa’y
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Katika elimu yangu ndogo niliyopata katika vitabu vya Fiqh, Milango ya Hajj na 'Umrah, sikuona kukatazwa mwanamke kuharakiza mwendo baina ya nguzo za kijani katika Sa’y. Niliwahi kumsikia Shaykh wa televisheni akisema kuwa mwanamke hakimbii eneo hilo bali ni kwa ajili ya wanaume tu. Hii ni kwa sababu ya kuhifadhika zaidi kwa wanawake kwa kutokudhihirisha yanayosababisha fitna akiwa anakimbia. Lakini hakutaja dalili yoyote katika kauli yake. Hivyo nikawaza kuwa ikiwa rai yangu ni sawa, basi kukimbia ni Sunnah aliyoianzisha Bibi Haajar (Radhwiya Allaahu 'anhaa). Hata hivyo naheshimu rai ya Shaykh, na Himdi Anastahiki Allaah kuwa Shariy’ah za Dini yetu haziundwi tu kutokana na rai (zisizostahili) kama alivyosema Amiyrul-Muuminiyn 'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu). Tafadhali naomba nasaha Allaah Akubariki, kwani mara kwa mara huenda kutekeleza 'Umrah na familia yangu, hivyo tunahitaji kujua yaliyo sahihi kuhusu mas-ala haya.
JIBU:
Ibn Al-Mundhir kasema:
"’Ulamaa wamekubaliana kwamba mwanamke asikimbie katika eneo la Nyumba (Ka'bah) au eneo la Sa’y (Swafaa na Marwa) baina ya nguzo za kijani. Hii ni kwa sababu kufanya hivyo ni kuonyesha ushupavu na nguvu, jambo ambalo halikukusidiwa kwa wanawake. (Mfano pia kuweka ridaa (sehemu ya juu ya nguo ya ihraam) kwapani. Mwanamke anatakiwa kujifunika asitirike, na kwa vile kukimbia kunahitaji kuweka ridaa (kuvaa rubega), itasababisha kumdhihirisha sehemu ya mwili wake."
Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah lil-Buhuwth al-'Ilmiyyah wal-Iftaa. Mjalada 11, Uk. 226, Swali Namba 5 la Fatwa Namba 8820 - Imejumuisha:
Kiongozi Mkuu: Shaykh 'Abdul 'Aziyz Ibn 'Abdillaah bin Baaz
Msaidizi Kiongozi Mkuu: Shaykh ‘Abdur-Razzaaq 'Afiyfiy
Mjumbe: Shaykh 'Abdullaah bin Ghudayyaan
Mjumbe: Shaykh 'Abdullah bin Qu'uwd]
Twawaaf Na Sa’y Wakati Swalaah Ya Fardh Inaanza
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Nini hukmu ya kutokumaliza twawaaf au Sa’y wakati Swalaah ya fardh imeanza kuswaliwa?
JIBU:
Inampasa asite, na aswali katika Jamaa, kisha aendelee twawaaf na sa’y yake pale alipofikia kabla ya kuanza Swalaah.
[Fataawa al-Hajj wal-‘Umrah waz-Ziyaarah – uk. 80]
Kumpa Mtu Zawadi Kwa Ajili Ya Kumfanyia Twawaaf
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Nini hukmu ya kumpa mtu zawadi kwa ajili ya kumfanyia mtu mwengine twawaaf. Humwendea mtu na kumwambia "Nifanyie saba" (yaani twawaaf saba) akitegemea thawabu zimfikie yeye mwenyewe. Je, inaruhusiwa?
JIBU:
Hairuhusiwi kufanya twawaaf katika Ka’bah kwa ajili ya mtu mwengine. Kwa hiyo mtu yeyote asifanye hivyo ila akiwa anamfanyia mtu fardhi ya Hajj au 'Umrah. Hivyo ni kutekeleza taratibu zote kwa niyyah ya huyo mtu.
Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Fataawa al-Lajnah ad-Daaimah lil-Buhuwth al-'Ilmiyyah wal-Iftaa. Mjalada 11, Uk. 236, Fatwa Namba 8433 - Imejumuisha:
Kiongozi Mkuu: Shaykh ‘Abdul-’Aziyz bin ‘Abdillaah bin Baaz
Msaidizi Kiongozi Mkuu: Shaykh ‘Abdur-Razzaaq 'Afiyfiy
Mjumbe: Shaykh ‘Abdullaah bin Ghudayyaan
Mjumbe: Shaykh ‘Abdullaah bin Qu’uwd]
Kulazimika Kuswali Rakaa Mbili Nyuma Ya Maqaam Ibraahiym
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Je, ni lazima kuswali Rakaa mbili baada ya kumaliza twawaaf nyuma ya Maqaam Ibraahiym? Nini hukmu ya mwenye kusahau kuziswali?
JIBU:
Sio lazima kuswali Rakaa mbili nyuma ya Maqaam Ibraahiym, bali inakuwa ni sahihi hata akiswali mtu popote kwengine katika Masjidul-Haraam. Vile vile hakuna madhara kwa anayesahau kuziswali kwani hizo ni Sunnah na sio fardhi.
Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Fataawa al-Hajj wal-'Umrah waz-Ziyaarah uk. 81]
Kukata Nywele Pembeni Tu Mwa Kichwa
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Tunaona baadhi ya watu katika Hajj wanakata nywele pembezoni tu mwa vichwa vyao wakiacha sehemu nyingine yote ya kichwa bila ya kuguswa. Tulipowafahamisha kuwa nywele zinatakiwa zikatwe sawa sawa kichwa kizima, walikanusha na kudai walivyofanya ni sawa. Je, ni sawa hivyo?
JIBU:
Wajibu ni kunyoa nywele zote, au kukata sawasawa kote kichwani, katika fardhi ya Hajj au 'Umrah. Haimpasi mtu kukata sehemu fulani tu ya kichwa. Hivyo ilivyotajwa katika Swali sio sawa kama zilivyo rai sahihi za ‘Ulamaa na wala sio Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Fataawa al-Lajnah ad-Daaimah lil-Buhuwth al-'Ilmiyyah wal-Iftaa. Mjalada 11, Uk. 217, Swali Namba 5 la Fatwa Namba 1734 - Imejumuisha:
Kiongozi Mkuu: Shaykh ‘Abdul-’Aziyz bin ‘Abdillaah bin Baaz
Msaidizi Kiongozi Mkuu: Shaykh ‘Abdur-Razzaaq 'Afiyfiy
Mjumbe: Shaykh ‘Abdullaah bin Qu’uwd]
Kuingia Hijr Ismaa'iyl Katika Kufanya Twawaaf
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Je, inaruhusiwa kuingia katika Hijr Ismaa'iyl (chumba cha Ismaa’iyl) wakati wa kufanya twawaaf?
JIBU:
Hairuhusiwi kuingia Hijr Ismaa'iyl wakati wa kufanya twawaaf katika Nyumba (Ka'abah) ikiwa ni kwa ajili ya Hajj au 'Umrah. Anayefanya hivyo hatopata thawabu kwa sababu twawaaf ni kuzunguka Ka'bah yote, na Hijr Ismaa'iyl ni sehemu ya Ka'bah. Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:
وَلْيَطَّوَّفُوا بِالْبَيْتِ الْعَتِيقِ ﴿٢٩﴾
...na watufu kwenye Nyumba ya Kale. (Al-Ka’bah). [Al-Hajj: 29]
Na kutoka kwa Mama Wa Waumini 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) ambaye amesema: "Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu Hijr akasema: ((Ni sehemu ya Nyumba [Ka'bah] [Muslim na wengineo]
Na Riwaayah nyengine amesema pia: "Niliapa kuswali ndani ya Nyumba naye (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Swali katika Hijr kwani hakika Hijr ni sehemu ya Nyumba …. ))
Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah lil-Buhuwth al-'Ilmiyyah wal-Iftaa. Mjalada 11, Uk. 233, Swali Namba 1, Fatwa Namba 1775 - Fataawa al-Hajj wal-'Umrah waz-Ziyaarah – Uk. 77
-Imejumuisha:
Kiongozi Mkuu: Shaykh 'Abdul 'Aziyz bin 'Abdillaah bin Baaz
Msaidizi Kiongozi Mkuu: Shaykh ‘Abdur-Razzaaq 'Afiyfiy
Mjumbe: Shaykh 'Abdullaah bin Ghudayyaan
Mjumbe: Shaykh 'Abdullah bin Qu'uwd]
Hakukata Au Kunyoa Nywele Baada Ya Kumaliza Sa’y
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Aliyemaliza Hajj ya Tamattu'u alifanya Sa’y kisha akabadilisha nguo zake lakini hakukata au kunyoa nywele. Kisha baada ya Hajj aliuliza akaambiwa kwamba ni makosa. Nini inampasa afanye sasa kwa vile muda wa Hajj umekwishapita?
JIBU:
Atahesabika kuwa ameacha kitendo cha waajib katika vitendo vya fardhi vya 'Umrah, nacho ni kukata au kunyoa nywele. Kutokana na rai za ‘Ulamaa, inampasa atoe kafara nayo ni kuchinja na kugawa nyama kwa masikini na wahitaji wa Makkah na Hijja yake haitoharibika.
[Fataawa al-Hajj wal-'Umrah waz-Ziyaarah – Uk. 93]
Amefanya Twawaaful-Widaa'i Kisha Hakuweza Kuondoka Makkah Wakati Huo
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Mtu amefanya Hajj, alipomaliza kafanya twawaaful-widaa'i usiku lakini akashindwa kuondoka Makkah baada ya twawaaf, hivyo akabakia Makkah hadi asubuhi kisha akasafiri. Nini hukmu ya yake?
JIBU:
Shariy’ah inavyopasa ni kuwa twawaaful-widaa'i iwe pindi mtu anapokuwa tayari kuondoka Makkah pale pale kutokana na Hadiyth kutoka kwa Ibn 'Abbaas: "Watu waliamrishwa kuwa kitendo chao cha mwisho (kabla ya kuondoka Makkah) kiwe ni twawaaf katika Ka'abah, isipokuwa kwa wanawake wenye hedhi". [Al-Bukhaariy na Muslim].
Hivyo ikiwa alifanya twawaaf kwa niyyah ya kuondoka usiku kisha akazuilika hadi asubuhi, basi hakuna ubaya In Shaa Allaah. Akiweza kurudia twawaaful-widaa'i kabla ya kuondoka ni bora zaidi.
Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Fataawa al-Hajj wal-'Umrah waz-Ziyaarah – Uk.84]
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/265
[2] http://www.alhidaaya.com
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9238&title=Fataawaa%3A%20Twawaaf%20Na%20Sa%27y
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9239&title=01-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Wudhuu%20Kuharibika%20Wakati%20Wa%20Twawaaf%20Je%20Arudie%20Twawaaf%3F
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9240&title=02-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20Wudhuu%20Katika%20Twawaaf%20Na%20Sa%E2%80%99ay
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9241&title=03-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Wanawake%20Kuharakiza%20Mwendo%20Baina%20Ya%20Nguzo%20Za%20Kijani%20Katika%20Sa%E2%80%99y
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9242&title=04-Imaam%20Ibn%20Baaz%3ATwawaaf%20Na%20Sa%E2%80%99y%20Wakati%20Swalaah%20Ya%20Fardh%20Inaanza
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9245&title=05-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Kumpa%20Mtu%20Zawadi%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Kumfanyia%20Twawaaf
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9246&title=06-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20Kulazimika%20Kuswali%20Rakaa%20Mbili%20Nyuma%20Ya%20Maqaam%20Ibraahiym%20%20
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9247&title=07-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Kukata%20Nywele%20Pembeni%20Tu%20Mwa%20Kichwa
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9248&title=08-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Kuingia%20Hijr%20Ismaa%27iyl%20Katika%20Kufanya%20Twawaaf%20%20
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9249&title=09-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Hakukata%20Au%20Kunyoa%20Nywele%20Baada%20Ya%20Kumaliza%20Sa%E2%80%99y
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9250&title=10-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Amefanya%20Twawaaful-Widaa%27i%20Kisha%20Hakuweza%20Kuondoka%20Makkah%20Wakati%20Huo%20