Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > Fataawaa: Ayyaam At-Tashriyq (Tarehe 11, 12, 13 Dhul-Hijjah)

Fataawaa: Ayyaam At-Tashriyq (Tarehe 11, 12, 13 Dhul-Hijjah)

Fataawaa Za 'Umrah Na Hajj [1]

 

 

  [2]

 

 

www.alhidaaya.com [3]

Share [4]

01-Imaam Ibn Baaz: Kufunga Swiyaam Tarehe 13 Dhul-Hijjah Kwa Niyyah Ya Swiyaam Ayyaamul-Biydwh (Masiku Meupe)

 

Hukmu Ya Kufunga Swiyaam Tarehe 13 Dhul-Hijjah

Kwa Niyyah Ya Swiyaam Ayyaamul-Biydwh (Masiku Meupe)

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [3]

 

 

SWALI:

 

Mzazi wangu alikuwa na ada ya kufunga Swiyaam kila mwezi Masiku Meupe (Ayyamul-Biydhw). Na kwa kuwa masiku haya yatawafikiana na tarehe 13 Dhul-Hijjah ambayo ni siku miongoni mwa Ayyamut-Tashriyq (Masiku ya Tashriyq), je aifunge au itamtosheleza kufunga tarehe 14 na 15 Dhul-Hijjah pekee?

 

 

JIBU:

 

Haipasi kwa mzazi wako au mwengine kufunga tarehe 13 Dhul-Hijjah kwa sababu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kufunga Ayyaamut-Tashriyq akasema kuwa hayo ni masiku ya kula na kunywa na kumdhukuru Allaah (‘Azza wa Jalla) [Ahmad katika Musnad].

Isipokuwa kwa Haji asiyepata had-yu (mnyama wa kuchinja) ikiwa ni mwenye kutekeleza Hajj Tamattu’ au Qiraan, basi hana kosa kuzifunga Swawm siku hizo kama alivyopokea Al-Bukhaariy (Rahimahu-Allaah) katika Swahiyh yake kwamba ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) na Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) wamehadithia kwamba: “Haikuruhusiwa kufunga katika Ayyaamut-Tashriyq isipokuwa kwa ambaye hakupata Al-Had-yu (mnyama wa kuchinja Hajj).

 

Hivyo anaweza (mtu) kufunga tarehe 14 na 15 na akipenda afunge tarehe 16 au siku nyingineyo katika mwezi wa Hajj hata akamilishe siku tatu (katika mwezi) na hivyo ni bora kufanya kwa sababu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameusia kundi la Maswahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum) kufunga Swiyaam siku tatu kila mwezi, ikiwa ni siku zinazoangukia Ayyamul-Biydhw au zisizoangukia.

Lakini akifunga Muislamu katika masiku meupe ni bora.

 

Na Allaah Ndiye Mwenye kuleta Tawfiyq.

 

 

[Fataawa Imaam Ibn Baaz, http://www.binbaz.org.sa/fatawa/591 [5]]

 

Share [6]

02-Imaam Ibn Baaz: Takbiyr Ayyamut-Tashriyq Na Muda Wake

Takbiyr Ayyamut-Tashriyq Na Muda Wake

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [3]

 

 

 

SWALI:

 

Je, Takbiyr (Masiku ya Tashriyq) inakusurishwa baada ya Swalaah tu au katika nyakati zote? Na kwa muda gani baada ya ‘Iyd?

 

 

JIBU:

 

Takbiyr ni Mutwlaq (nyakati zote) na Muqayyad (nyakati maalumu za kukadirika) ni muda wote na baada ya kila Swalaah. Huanzia alfajiri ya siku ya 'Arafah  hadi jua linapozama siku ya kumi na tatu. Hizo ni siku tano yaani tarehe tisa, kumi, kumi na moja, kumi na mbili na kumi na tatu mpaka jua linapozama (Magharibi) (inapaswa) Mutwlaq na Muqayyad.

 

[Majmuw’ Fataawaa Wa Maqaalaat Mutanawwi’ah Mjalada 26]

 

 

Share [7]

03-Imaam Ibn Baaz: Sifa Ya Takbiyr Ayyamut-Tashriyq Tarehe 11-13 Dhul-Hijjah

 

Sifa Ya Takbiyr Ayyamut-Tashriyq Tarehe 11-13 Dhul-Hijjah

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [3]

 

 

 

SWALI:

 

Zipi sifa za Takbiyr katika Ayyaamut-Tashriyq na je ni Muqayyad (maalumu iliyofungamanishwa) baada ya Swalaah au Mutwlaq (isiyofungamanishwa)

 

 

JIBU:

 

Takbiyr katika Ayyamut-Tashriyq (Tarehe 11-13 Dhul-Hijjah) ni Mutwlaq (wakati wote) na Muqayyid (wakati maalumu wa kukadirika) baada ya Swalaah  na nyakati zote. Akipenda mtu atamke mara mbili mbili au mara tatu tatu:

 

اللَّهُ أَكْبَرُ، اللَّهُ أَكْبَرُ،  لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، اللَّهُ أَكْبَرُ، اللَّهُ أَكْبَرُ، وَلِلَّهِ الْحَمْد

Allaahu Akbar, Allaahu Akbar, laa Ilaaha illa Allaah, Allaahu Akbar Allaahu Akbar WaliLLaahil-Hamd

 

Na azidishie kusema “Laa ilaaha illa Allaah” kwa kusema:

 

لَا إِلَهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيْكَ لَهُ، لَهُ الـمُلْكُ، ولَهُ الـحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيءٍ قَدِير

سُبْحَانَ اللَّهِ ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ ، وَلا إِلَهَ إِلا اللَّهُ ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ ، وَلا حَوْلَ وَلا قُوَّةَ إِلا بِاللَّهِ 

 

Na Riwaayah ya Ahmad (Rahimahu Allaah) na Hadiyth ya ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) “Hakuna siku adhimu mbele ya Allaah wala ‘amali Aipendayo zaidi Allaah kama masiku haya basi zidisheni humo At-Tahliyl (Laa ilaaha illa-Allaah), na At-Takbiyr (Allaahu Akbar) na At-Tahmiyd (AlhamduliLLaah).

 

Na ‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu)  alikuwa akileta takbiyr (Allaahu Akbar) katika khema lake katika masiku ya Minaa mpaka  Takbiyr zinavuma Minaa kama alivyokuwa Ibn ‘Umar na Abuu Huraryah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) wakitoka katika masikku kumi wakileta takbiyr na watu wakiwafuatilia kwa takbiyr katika masoko, wakiwafundisha watu.

 

[Majmuw’ Fataawaa Wa Maqaalaat Mutanawwi’ah]

 

 

 

Share [8]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/9331

Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/265
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/node/9331
[3] http://www.alhidaaya.com
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9331&title=Fataawaa%3A%20Ayyaam%20At-Tashriyq%20%28Tarehe%2011%2C%2012%2C%2013%20Dhul-Hijjah%29
[5] http://www.binbaz.org.sa/fatawa/591
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9332&title=01-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20Kufunga%20Swiyaam%20Tarehe%2013%20Dhul-Hijjah%20Kwa%20Niyyah%20Ya%20Swiyaam%20Ayyaamul-Biydwh%20%28Masiku%20Meupe%29
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10035&title=02-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20Takbiyr%20Ayyamut-Tashriyq%20Na%20Muda%20Wake%20
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10088&title=03-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20Sifa%20Ya%20Takbiyr%20Ayyamut-Tashriyq%20Tarehe%2011-13%20Dhul-Hijjah