Keki Za Vikombe

Vipimo 
Unga wa ngano - vikombe 2-3
Mayai - 6
Maziwa -  kikombe 1
Sukari - kikombe 1
Siagi - kikombe 1
Baking powder - vijiko vya chai 2-3 (kijiko 1 kwa kikombe cha unga 1)
Vanilla - kijiko cha chai 1
Rose essence -  kijiko cha chai robo(kiasi unavyotaka harufu ijitokeze)
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Saga siagi, sukari, mayai na essence ya vanilla na rose 
 
- Ikishasagika tia unga na maziwa koroga tena. 
 
- Mwisho tia baking powder na koroga mpaka ichanganyike. 
 
- Washa oven lako moto wa 350’F kwa dakika 2-3. 
 
- Chukua treya maalum ya kupikia cupcakes / muffins, tia karatasi za duara maalum za kupikia keki hizi kwenye kila duara la treya.(huna haja ya kupaka mafuta kwenye treya) 
 
- Kisha tumia kijiko kikubwa chota mchanganyiko huo wa keki na tia ndani ya karatasi hizo za duara kiasi cha robo tatu (3/4) yaani usijaze mpaka juu. 
 
- Ukimaliza kuvijaza vyote tia kwenye oven kwa muda wa dakika 20 – 25. 
 
- Zitoe panga kwenye sahani ziache zipoe kidogo na tayari kuliwa na chai au kuwafungia watoto shuleni kama snack.