Kibainisho Muhimu

Ukumbusho Wa Swiyyaam (Funga) Za Ayyaamul-Biydhw Mwezi Wa Shawwaal 1441H

Swiyaam (Funga) Za Siku Tatu Kila Mwezi Thawabu Zake

Ni Sawa Na Thawabu Za Swiyaam Za Milele!

 

 

Swiyaam (funga) za Ayyaamul-Biydhw (masiku meupe) ni tarehe 13, 14, 15 katika kila mwezi wa Kiislamu (Hijriyyah). Masiku hayo mwezi huu wa Shawwaal 1441H  yataangukia  tarehe 4, 5, 6, June 2020M (Alkhamiys, Ijumaa, Jumamosi).

 

Tanbihi: Isipowezekana kuzifunga siku hizo za Biydhw, basi inajuzu kufunga siku tatu zozote nyengine katika mwezi ili kupata fadhila hiyo.

 

عَنْ أَبي ذَرٍّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيهِ وَسَلَّمَ:((مَنْ صَامَ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ ثَلاثَةَ أَيَّامٍ فَذَلِكَ صِيَامُ الدَّهْرِ)) فَأَنْزَلَ اللهُ تُصْدِيقَ ذَلِكَ في كِتَابِهِ الْكَرِيمِ: ((مَنْ جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا))، الْيَوْمُ بِعَشَرَةِ أَيّامٍ. أخرجه أحمد والترمذي وقال حديث حسن ، والنسائي وابن ماجه وابن خزيمة

Imepokelew a kutoka kwa Abuu Dharr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Yeyote atakayefunga (Swawm) kila mwezi siku tatu, ni sawa na Swawm ya milele)) Kisha Allaah Akateremsha Aayah ithibitishayo hayo: “Atakayekuja kwa 'amali nzuri basi atapata (thawabu) kumi mfano wa hiyo.” Siku moja kwa malipo ya siku kumi. [Imepokewa na At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan, An Nasaaiy na Ibn Maajah, Ibn Khuzaymah na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Al-Irwaa (4/102)]. Aayah: Suwrat Al-An’aam (160)]

 

Bonyeza Upate fadhila za Ayyaamul-Biydhw, fadhila za Swawm ya Jumatatu na Alkhamiys na fadhila za Swawm kwa ujumla.

 

 

Share

Kipengele Maalumu

Nasiha Za Minasaba

Nini Baada Ya Ramadhwaan?

Nini Baada Ya Ramadhwaan?

Alhidaaya.com

 

Tumeuaga mwezi wa Ramadhwaan, mwezi wenye Baraka na Rahmah. Tumeaga mchana wake tulipokuwa katika subira ya Swawm, na usiku wake tulipoonja ladha ya Qiyaamul-Layl (kusimama usiku kuswali). Tumeuaga mwezi wa Qur-aan, mwezi wa taqwa, mwezi wa jihaad, mwezi wa maghfirah, mwezi wa kuomba du'aa kwa wingi, mwezi wa kuepushwa na Moto. Amefaulu aliyetimiza Swiyaam ilivyopaswa akachuma thawabu nyingi na akajitahidi kuzidisha ‘ibaadah. Lakini amekula hasara aliyepuuza Swiyaam na hukmu zake na kutokujitahidi katika ‘ibaadah.    

 

Kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) katika Aayah zilizofaridhishwa kufunga Swiyaam katika Ramadhwaan kuwa lengo la Swiyaam ni taqwa.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٨٣﴾

Enyi walioamini! Mmefaridhishwa Swiyaam kama ilivyoandikwa kwa wale ambao wa kabla yenu mpate kuwa na taqwa [Al-Baqarah: 183]

 

Kila Muislamu aliyeingia katika mwezi wa Ramadhwaan atakuwa ameingia na ametoka katika madrasa ya taqwa. Na mtu anapoingia katika madrasa yoyote ile, hutoka humo akiwa amepata manufaa au shahada ya lile somo alilolisoma, na baada ya hapo...

 

Bonyeza Endelea...

 

 

Share

Tarjama Ya Maana Ya Qur-aan (Translation Of The Meaning Of Al-Qur-aan)

Bonyeza Hapa Kwa Faida Ziada