SWALI:
Kwa uwezo wa Allah (S.W) naomba niulize swali langu
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako
Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika jina la Allaah au Mtume, usifupishe mbele yake kwa kuweka (S.W.) au (S.A.W.)
Tukirudi kwenye swali lako Ni kitu kinachojulikana na kila mmoja katika mji/ jiji/ kijiji kuhusu hali mwanamme au mwanamke pindi anapooa au anapoolewa. Hili si jambo ambalo ni geni kwa kila mmoja kwani watu huwa wanajua kuanzia anapoposa mwanamme na kuposwa mwanamke.
Hivyo, si sawa kabisa kwa mwanamme kuanza baada ya harusi kuanza kumwambia kila mmoja au watu wake wa karibu kuwa mkewe ni bikra. Na hasa kuwa hawa ni watu wake kama ulivyosema
Ama lile jambo linalofaa ilikuwa ni kujibu kwa suali ambalo utakuwa umeulizwa na mtu ambaye labda ni mzazi wako au ndugu yako, na si kwa kila mtu kwani wengine hawahitaji kufahamu
Ifahamike hapa lengo la Mtume kumuuliza Jaabir (Radhiya Allaahu ‘anhuma) ni katika kutaka kumshauri lenye faida na manufaa naye zaidi na si kutaka tu kujua kwa ajili ya kujua tu! Na mbele ya Hadiyth hiyo ametaja sababu hiyo ya kumuuliza, ambayo ni ‘Kwa nini usioe bikra .
Na Allaah Anajua zaidi.
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/58
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F2178&title=Anatangaza%20Kuwa%20Mke%20Wake%20Ni%20Bikra