Pudini Ya Karameli Ya Kutengeneza Mwenyewe (Home Made) Katika Vibakuli 
   
Vipimo Vya Karameli                                                                   
Sukari - 1 ½  kikombe    
Maji - ¾  kikombe                                                               
Namna Ya Kuatayarisha Na Kupika Karameli  
- Washa oveni moto wa 150° (350°F). 
 
- Tia sukari na maji katika kisufuria, weka katika moto mdogo mdogo, koroga hadi sukari iyayuke. 
 
- Rashia (brush) pembezoni mwa sufuria kuondosha chembechembe za sukari. 
 
- Ongeza moto na acha ichemke kwa dakika 8-10 au hadi shira igeuke rangi ya ya hudhurungi iliyokoza. 
 
- Mimina kwa kugawa katika vibakuli 8 vya oveni (oven proof)  vya saizi ya ¾ (6 oz). 
 
- Weka kando dakika 5 iache karameli ipoe na itulie. 
 
Vipimo Vya Kastadi: 
Maziwa - 1 1/3  kikombe (10 fl oz) 
Malai (Cream) - 1 ½    kikombe  (6fl oz) 
Mayai -  4 
Kiiniyai (egg yolks) - 8 mayai 
Sukari -  ¾  kikombe  
Vanilla - 3 vijiko vya chai   
Namna Ya Kutayarisha Kastadi  
- Tia maziwa na malai katika sufuria, weka katika moto mdogo mdogo hadi iwe dafudafu (warm). 
 
- Tia mayai, na viini vya mayai, sukari na vanilla katika bakuli jengine na upigie kwa mchapo wa mayai (egg whipp) hadi vichanganyike. 
 
- Mimina polepole katika mchanganyiko wa maziwa huku unakoroga ili iendelee kuchanganyika. 
 
- Mimina kwa kugawa katika vibakuli 8 vilivyokuwa na karameli. 
 
- Vipange vibakuli katika treya, kisha tia maji kiasi kufikia ¾ ya usawa wa vibakuli. 
 
- Pika (Bake) katika oveni kwa muda wa dakila 35 - 40 hadi kastadi itulie na iwive. 
 
- Epua katika treya weka nje kwa muda kisha viweke katika friji zishike baridi. 
 
    
8.  Pindua katika sahani ikiwa tayari.
Kidokezo: 
Unaweza kutia flavour nyingine badala ya vanilla kama ya chungwa, au kahawa n.k.