SW
Ikiwa mwanamke amepewa raha zote na mahitajio yote nyumbani kwake lakini haachi kugombana na mumewe kila siku mpaka mumewe hawezi tena kukaa dakika moja nyumbani kwa sababu ya ulimi wake nipeni solution ya hili jambo.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mume kumpatia mkewe mahitaji yote. Hata hivyo, hili ni suala ambalo limeletwa na upande mmoja na kisha maneno yenyewe yana utata kwani hukuelezea raha zote ni nini? Mara nyingi huwa tunachukulia kuwa raha anayohitaji mke ni kumpa chakula na kivazi kizuri, kinywaji na samani za nyumba pamoja na vifaa vyengine. Lakini kumpatia vitu hivyo huwa bado hujamuonyesha raha kwani mara nyengine mke mwenyewe alikuwa na zaidi ya hivyo nyumbani kwao alikotoka. Mara nyingi waume husahau
Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametupatia mafundisho kuhusu maingiliano baina ya mume na mke kwa jinsi ambayo mwenye kufanya kitendo hicho kwa halali anakuwa ni
Pia akatupatia muongozo kuwa asiende mtu kwa mkewe kama anavyofanya hivyo mnyama bali kuwe na mjumbe baina
Hakika ni kuwa wapo wake majeuri kama vile walivyo wanaume wengine katika
“Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Allaah Ametia kheri nyingi ndani yake” (4: 19). Huu ndio msimamo wa Uislamu huenda mke akawa mjeuri lakini ana mazuri mengine jaribu kumrekebisha kwa njia ambayo ni nzuri. Hata hivyo, tufahamu kuwa huenda mume akawa na makosa. Na ikiwa ni hivyo inabidi pia naye ajirekebishe ili waweze kufahamiana.
Ikiwa yote umefanya na kweli makosa ana mke nawe umejaribu uwezavyo jiwekee kuanzia sasa muda kwa kufanya yafuatayo:
Allaah Aliyetukuka Anasema:
“Basi wanawake wema ni wale wenye kutii na wanaojilinda hata katika siri kwa kuwa Allaah Ameamrisha wajilinde. Na ambao mnachelea kutoka katika utiifu wanasihini, muwahame katika malazi na wapigeni. Wakikutiini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure” (4: 34).
Na Allaah Anajua Zaidi
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/60
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F3059&title=Mke%20Mjeuri%20Juu%20Ya%20Kwamba%20Anapewa%20Raha%20Na%20Mahitajio%20Yote%20Na%20Mume