SWALI:
Assallamu allaykum nashukuru
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako zuri kuhusu kufanya mapenzi na bila jimai.
Allaah Aliyetukuka Atuepushe na maasi ya zinaa na mengine yote.
Ama neno zinaa lina maana mbili
Ama maana ya Romance ni mapenzi ambayo mwanamme atafanya na mwanamke bila ya jimai yenyewe. Kwa mfano, kuzungumza maneno ya mapenzi, kushikana, kupigana busu na mfano wa hayo.
Kushika mimba kwa mwanamke si lazima watende tendo la jimai ikiwa ni kwa kuzini au kufanya kwa njia ya halali. Inayoleta mimba ni kuingia manii (mbegu za kiume) katika utupu wa mwanamke. Na ikiwa mwanamme atafanya romance na mwanamke na maji hayo
Mwanamke wa Kiislamu anapaswa kujiepusha na maasi hayo ambayo ni desturi za makafiri zisizopasa kuigwa. Pia maasi hayo hatimaye yatampelekea kutumbukia katika zinaa na kushika mimba, kisha matokeo yake ni hasara kwake na kwa mtoto. Juu ya hiyo atabaki kuwa katika majuto ya milele, na itamletea taathira na madhara yeye mwenyewe, mtoto, jamaa zake na jamii nzima. Vilevile maasi hayo adhabu yake ni kali mno endapo yatafanyika.
Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Awaepushe wanawake wasipate mimba nje ya ndoa wala jinsia hizo mbili zisikaribie zinaa.
Na Allaah Anajua zaidi
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/109
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F4005&title=Anaweza%20Kushika%20Mimba%20Akifanya%20Maasi%20Ya%20Zinaa%20Bila%20Ya%20Jimai%3F