SWALI:
Bibi na Bwana wameelewana kutumia koil kukinga kupata mtoto kwa mda. Kisha bwana ameamua koil bibi akaitowe. Bibi akamwambia bwana haya. Ikapita mdaa. Bwana akamuuliza bibi
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), ahli zake, Swahaba zake (Radhiya Allahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho
Shukran ndugu yetu kwa swali lako
“Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Allaah Ametia kheri nyingi ndani yake” ().
Talaka amepatiwa mume kwa ajili ya utulivu wake na kuweza kusubiri na kuzingatia kabla ya kuchukua hatua yoyote
Inatakiwa kwamba mume na mke wanapopeana ahadi iwe kila mmoja afanye juhudi kutekeleza upande wake na
Uongo katika Uislamu ni mbaya na ni miongoni mwa sifa za unafiki kwa mwenye kulifanya
Katika talaka hii ambayo imetolewa na mume ni kuwa imeekewa sharti – “Bwana akamuuliza bibi
1. Ikiwa umenidanya jua nishakuacha.
Kwa muhtasari ni kuwa mke keshaachika na inabidi akae eda yake ya tohara tatu ambayo ni takriban miezi mitatu kufuata miandamo ya mwezi. Katika kipindi hiki cha eda, mume ikiwa hiyo ni talaka ya kwanza au ya pili anaweza kumrudia mkewe lakini ni nasaha yetu kuwa mtu au watu wenye uzoefu wazungumze na huyu bwana ili asiwe ni mwenye kuweka masharti kama hayo bali wawe ni wenye kushauriana na mkewe pindi anapoona kuna haja ya jambo fulani kufanyika katika njia fulani. Na pia mke anasihiwe asiwe ni mwenye kudanganya bali awe wazi kwa mumewe ili matatizo
Tunamuomba Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) Awape maelewano na masikilizano ili watu hao wawili warudi katika hayo yao ya awali kama mume na mke, na pia Awape hamu ya kushauriana katika mas-ala yote nyeti ili matatizo hayo yasiwe ni yenye kutokea tena.
Na Allaah Anajua zaidi.
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/57
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F638&title=Nimemdanganya%20Mume%20Wangu%2C%20Je%2C%20Nimeachika%3F%20Na%20Je%2C%20Inanipasa%20Nikae%20Eda%3F