Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > 06-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتابُ الْحَجّ وَالْعُمْرَة - Kitabu Cha Hajj Na 'Umrah > 22-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Hajj Na 'Umrah: Kunyoa Na Kupunguza Kwa Mwenye Kufanya Tamattu’u

22-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Hajj Na 'Umrah: Kunyoa Na Kupunguza Kwa Mwenye Kufanya Tamattu’u

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

Mlango Wa Hajj Na ‘Umrah

 

22-Kunyoa Na Kupunguza Kwa Mwenye Kufanya Tamattu’u

 

Alhidaaya.com [1]

 

 

 

Hujaji mwenye kufanya Tamattu’u akimaliza Kusai baina ya As-Swafaa na Al-Marwah, atavua Ihraam ya (atatahalluli na) ‘Umrah yake kwa kunyoa au kupunguza. Ni bora apunguze nywele kuliko kuzinyoa, kwa kuwa atakuja kuzinyoa zote Siku ya An-Nahr (tarehe 10) baada ya kumaliza ‘amali za Hajj. Katika Hadiyth ya Jaabir, Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) amesema:

 

((حلوا من إحرامكم فطوفوا بالبيت وبين الصفا والمروة، وقصروا، وأقيموا حلالا حتى إذا كان يوم التروية فأهلوا بالحج...))

 

((Vueni Ihraam zenu, mtufu Nyumba na [msai] baina ya As-Swafaa na Al-Marwah, na punguzeni nywele, na kaeni mkiwa hamna Ihraam mpaka inapofika Siku ya At-Tarwiyah, hirimieni Hajj)). [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (1568) na Muslim (1216)]

 

Akipunguza, anakuwa huru, na anaruhusiwa kufanya kila kitu hata kujimai mpaka Siku ya At-Tarwiyah.

 

 

 

 

Share [2]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/10612

Links
[1] http://www.alhidaaya.com
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10612&title=22-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Hajj%20Na%20%27Umrah%3A%20Kunyoa%20Na%20Kupunguza%20Kwa%20Mwenye%20Kufanya%20Tamattu%E2%80%99u