Kwa Ajili Ya Allah...
Kisha Kwa Ajili Ya Historia
Kufichua Siri Na Kuwasafisha Maimamu Walio Safi
Kimeandikwa Na: As-Sayyid Husayn Al-Mussawiy (Miongoni Mwa Wanazuoni Wa Najaf)
Kimetafsiriwa Na Abu 'Ilmi
Kwa Ajili ya Allaah ... Kisha Kwa Ajili Ya Historia:
01-Utangulizi
Sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu mlezi wa viumbe na tunamtakia rehema na amani Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yeye na ahli zake na sahaba zake.
Ama baada ya salaam
Tulikua katika jumuiya ya Swalahuddiin tukizungumzia haja ya kuwa na kitabu chenye ufupi wa maelezo ya msingi wa shi’a (Ithna ashariya) kwa sharti waweze kufaidika kwa kitabu hicho watu wa kawaida na watu maalum. Pindi tulipo kuwa tunatafuta nani aandike kitabu hicho miongoni mwa wanazuoni na wenye ujuzi na waliobobea kikatufikia kitabu hiki : -
(KWA AJILI YA ALLAAH… KISHA KWA AJILI YA HISTORIA) kilicho tungwa na ASSAYED HUSSEIN AL MUSAWIY, miongoni mwa wanazuoni wa najaf na baada ya kukisoma tukaona kinakidhi lengo na ziada, ama ziada tunayoikusudia hapa ni mtungaji wa kitabu hicho kwa vile anazingatiwa ni mwanazuoni miongoni mwa wanazuoni wakubwa wa shia.na kwa sababu ya kusoma kwake na kufundisha kwake katika sehemu kuu (Vyuo vikuu) za Najaf. Na alikuwa na mahusiano makubwa na wanazuoni na Ma,aayaati wa kishia kwa mfano: Kashif Alghataa, Alkhuuiy, Al-Sadir, Al-Khamenii,na Abdul Hussein Sharafuddin, ambaye alikuwa anakuja sana katika mji wa Najaf, achilia mbali hili na lile, baba yake mtungaji pia alikuwa mwanachuoni katika wanachuoni wakishia.
Mtungaji amezungumzia katika kitabu chake maajabu aliyoyakuta na uzoefu wake katika rejea ya vitabu vya mashia kwa njia nzuri yenye kuvutia na yenye ufupi na baada ya kutaja yaliokuwa yakimtokea akiwa pamoja nao (wanachuoni wa kishia) au akiwa na mmoja wao huwarejesha wasomaji wake katika vitabu vyao mama ambavyo vinaonyesha ruhusa ya kitendo hicho kiovu.
Na yeyote atakayechukuwa kitabu hiki na kukisoma kwa utulivu basi atauona ukweli wa mtungaji. (wala hatumtakasi mtu mbele ya Allaah) na ataona tofauti ya njia alizozitumia kinyume na wenzake miongoni mwa watungaji wa kishia ambao wanaokosoa baadhi ya misingi ya dhehebu lao, Mungu amjaze kila la kheri kwa kitabu chake hiki kizuri , na amuepushie shari ya wenye chuki naTumesikia kwamba wanampangia njama Na ndio maana hakuweka jina lake kwa uwazi zaidi ili asijulikane na kamkuta ya sio mema (soma ukurasa wa 91) katika kitabu hiki.
Tuna muomba Mwenyezi Mungu ajaalie amali zetu ziwe kwa kwa ajili ya kupata radhi zake tukufu.
JUMUIYA YA SWALAHUDDIN,
14, SAFAR 1422.
Sifa njema zinamstahiki Allaah mlezi wa viumbe na rehema na amani zimshukie mjumbe wetu muaminifu na Aali zake wema watakatifu na wafuasi wao kwa mazuri mpaka siku ya kiyama.
Ama baada ya hayo, hakika muislamu anajua kuwa uhai unakwisha kwa mauti kisha inaamuliwa hatima yake ama kwenda peponi au motoni. Na bila shaka kuwa muislamu ni mwenye kupupia ili awe miongoni mwa watu wa peponi. Kwa ajili hiyo lazima afanye amali yenye kumridhisha mola wake mtukufu na ajiweke mbali na makatazo yake, mambo yanayo muingiza mtu katika ghadhabu za Allaah kisha adhabu yake. Kwa ajili hiyo tunamuona muislamu anakuwa na pupa katika kumtii mola wake, na huo ndio mwendo wa muislamu wa kawaida, seuze watu maalum (wenye elimu)?
Hakika uhai kama inavyojulikana una njia nyingi na udanganyifu mwingi,mwenye akili ni yule anayefuata njia inayomfikisha peponi hata kama ni ngumu na kuacha njia inayomfikisha motoni hatakama ni nyepesi sana.
Riwaya hii nimeiweka kwa mtindo wa utafiti (bahthi) ambayo nimeitamka kwa ulimi wangu na kuiandika kwa mkono wangu , nimekusudia kwa kazi hii kupata radhi za Allaah na kuwanufaisha ndugu zangu madamu nipo hai kabla sijavikwa sanda.
Nimezaliwa Karbala na nikaleleka katika mazingira ya kishia chini ya uangalizi wa baba yangu mfuasi mzuri wa dini. Nimesoma katika shule za mji huo(karbalaa) mpaka nimekuwa kijana baro baro na akanipeleka baba yangu kwenye vyuo vya elimu vya Najaf mama wa vyuo vya duniani ili nichote elimu kwa mabingwa wa maulamaa mashuhuri katika zama hizi kwa mfano: -
Al-imam Assayed Mohamed Al-hussein (kashif Al-ghatwaa).
Tulisoma katika madrasa za Najaf za elimu za juu ikawa matamanio yangu ifikie siku ambayo nitakuwa marejeo katika mambo ya dini siku ambayo nitakuwa kiongozi wa moja ya vyuo vikuu ili niweze kuihudumia dini yangu na umma wangu na kuwaendeleza waislamu.
Na nilikuwa nikitamani kuona waislam ni Umma mmoja, na taifa moja wakiongozwa na imam mmoja, na katika wakati huohuo nikitamani kuona mataifa ya kikafiri yakiporomoka na kuanguka mbele ya umma wa kiislam. Na kuna matarajio mengi zaidi ambayo kila kijana muislam mwenye uchungu na dini yake huyataraji. Na nilikuwa nikijiuliza ni kitu gani kilicho tupelekea katika hali hii ya udhalili tukonyuma kimaendeleo tumesambaratika tumefarikiana? Na nilikuwa nikijiuliza vitu vingine vingi vinavyopita katika fikra zangu kama inavyo pita katika fikra za kila kijana muislam, lakini sipati majibu ya maswali yangu.
Akanisahilishia mwenyezi mungu kujiunga na masomo, na kutafuta elimu, katika kipindi cha masomo zilikua zinanipitia hoja zinazo nifanya nisimame nitafakari, na mambo tofauti yanayoshughulisha moyo wangu na matukio yanayonishangaza , lakini nilikua naituhumu nafsi yangu kwa kuelewa vibaya, na uchache wa ufahamu, nikajaribu kuyaweka mambo hayo mbele ya mmoja wa viongozi na waalimu wa vitengo vya elimu ya dini; Na alikua mtu mwerevu alijua jinsi ya kuyatatua mas’ala hayo basi akataka ayazime katika uchanga wake kwa maneno mepesi akaanza kuniuliza: Unajifunza nini katika kitengo cha elimu?
Nikajibu: Madh-habu ya Ahlil- bait.
Akaniuliza, Je una mashaka na madh-habu Ahlul-bait?
Nikamjibu kwa ukakamavu, mwenyezi mungu apishie mbali.
Akasema ondoa wasiwasi huu katika nafsi yako, Hakika wewe ni mfuasi wa Ahlil-baiti wao wamepokea kwa Muhammad rehema na amani ziwe juu yake na Aali zake, na Muhammad amepokea kutoka kwa mwenyezi mungu mtukufu.
Nilinyamaza kidogo mpaka nafsi yangu ikatulia, kisha nikamwambia:- Mwenyezi mungu akubariki kwa kunitibu na wasiwasi huu, kisha nikarudi katika masomo yangu na yakanirudia Maswali yale na maulizo na kila nilipokua nikipiga hatuwa katika masomo yalikua yakiongezeka maswali, na kuongezeka kasoro ninazo zigunduwa.
La msingi ni kuwa nilimaliza masomo yangu kwa mafanikio makubwa,na nikapata shahada yangu ya kwanza ya katika daraja la “Ijtihaad” kutoka kwa mwanazuoni pekee zama hizo Mheshimiwa mkuu wa chuo Muhammad Al Hussain Al Kashif lgahtaa mkuu wa chuo,na baada ya hapo nilianza kufikiri kwa kina zaidi juu ya mas’ala haya,sisi tunasomea madhab ya Ahlulbait (AS) tunasomea masuala ya sheria ili tumuabudu mwenyezimungu kwazo,lakini ndani yake kuna vipengele vya wazi kabisa vinavyomkufuru mwenyezimungu mtukufu.
Ee mola wangu,ni mambo gani haya tunayoyasoma?! Je yanaweza yakawa haya ndio madhab ya Ahlul bait kweli?! Hakika hili humsababishia mtu ugonjwa wa nafsi katika shaksia yake,ni vipi atamuabudu mwenyezimungu hali yakuwa anamkufuru?!.
Vipi atawafuata Ahlul bait,atawapenda na atasoma madhab yao hali ya kuwa anawatukana?!
Kutokana na rehema zako mola wangu, na upole wako kwangu kama zisinge nidiriki rehema zako ningelikua miongoni mwa waliopotea , bali miongoni mwa waliopata hasara. Na ninarudi kuiuliza nafsi yangu,Ni nini msimamo wa viongozi na maimamu hawa na kila ambao walio tangulia katika mafahali wa wanazuoni. Nini msimamo wao katika jambo hili? Je hawa kuwa wameliona hili ambalo nililo lisoma?! Naam, bali miongoni mwa vitabu hivi wengi wao ndio walio vitunga, na yaliyomo ndani yake yameandikwa kwa kalamu zao basi likawa jambo hili linatonesha moyo wangu, na inauongeza uchungu na majuto.
Nilikuwa na haja ya kumpata mtu wa kumshitakia huzuni zangu, na wakumtolea masikitiko yangu,
Mwisho nikaongozwa kwenye fikra nzuri zaidi nayo ni kusoma kwa upana zaidi na kuuangalia upya mtazamo wa mada zangu za kielimu, Basi nikaanza kusoma kila kilichopo katika marejeo yenye uhakika na hata vile visivyo vya uhakika, basi nilisoma kila kitabu kilichopo mbele ya mikono yangu, ikawa zinanisimamisha baadhi ya ibara na hoja ambazo nilihisi kuna haja ya kuziwekea Taaliiq,(maelezo) basi nikawa nazinakili hoja hizo na kuzitolea maelezo kwa yanayo pita katika nafsi yangu, pindi nilipo maliza kusoma marejeo ya uhakika, Nikajikuta ndani ya rundo la vipande vya karatasi, Nikavihifadhi kwa matarajio kwamba itafika siku mwenyezimungu aktahukumu lifanyike jambo ambalo ameliandika.
Na uhusiano wangu ukabaki kuwa mzuri pamoja na kila marejeo(maulamaa) ya kidini, na wanazuoni na viongozi ambao nilikutana nao, Na nilikuwa nachanganyika nao ili niweze kufikia kwenye lengo ambalo litanisaidia pindi siku nitakayochukua uamuzi mzito, Nikasimama katika mas’ala mengi mpaka kukinai kwangu kukawa kumekamilika katika kuchukua uamuzi mzito, lakini nikawa nasubiri wakati na nafasi muafaka.
Na nikawa namuangalia rafiki yangu msomi mwanazuoni (Musa Almuusawi) Nikamuona ni mfano mzuri(wa kuigwa) wakati alipotangaza kupinga upotofu uliojitokeza katika mfumo wa kishia na kujaribu kwake kwa juhudi kwa juhudi kubwa kusahihisha mfumo huu.
Kisha kikatolewa kitabu na bwana Ahmadu Alkaatibu (maendeleo ya fikra yakishia), Na baada ya kukisoma nikaona hakika umefika wakati wangu katika kusema ukweli, Nakuwafafanulia ndugu zangu waliohadaiwa, kwa sababu sisi kama wanazuoni ni wenye kuulizwa juu yao siku ya kiyama. Basi hatuna budi (nilazima) kuwafahamishe ukweli ujapokua mchungu. Na huenda njia niliyoitumia inatofautiana na njia waliyoitumia mabwana wawili: Almusawwi na Alkaatib, katika matokeo ya utafiti wa kielimu, hii inatokana na sababu ya yale aliyoyapata kila mmoja kati yetu katika kipindi cha utafiti wake alioufanya.
Na huenda mabwana hao wawili waliotajwa hali yao inatofautiana na hali yangu, imekuwa hivyo kwani kila mmoja kati yao amehama Irak, na kuishi katika nchi miongoni mwa nchi za magharibi, na huko ndio wameanza kazi zao.
Ama mimi bado nipo ndani ya Irak , tena ndani ya Annajaf yenyewe. Na vitendea kazi nilivyo kuwa navyo haviwezi kufikia ngazi ya vitendea kazi walivyo kuwa navyo mabwana wawili hao.
Kwani mimi baada ya kufikiri sana kuhusu kubaki hapa(Irak) au kuondoka! Nikaamua kubaki na kufanya kazi hapa hapa(Anajaf) nikusubiri na kutarajia malipo kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Nami nikiwa na yakini kuwa kuna mabwana wengi wanaohisi kusononeka na kusutwa nadhamira zao kwa kunyamaza kwao na kuridhia kwao yale wanayoyaona na kuyashuhudia, na kwa yale wanayoyasoma katika vitabu vikubwa ambavyo wanavyo,basi ninamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) akijaalie kitabu changu kiwe chenye kutoa msukumo kwao katika kujirudi.Na kuacha njia ya upotevu na kufuata njia ya haki,kwani umri ni mfupi,na hoja imesimama juu yao,hawatabaki na sababu baada ya hapo.
Na kuna mabwana wengine ambao nina uhusiano nao walikubali mwito wangu (namshukuru Allaah) waliuona ukweli huu ambao niliufikia katika utafiti wangu na wao wakaanza kuwalingania watu wengine tunamuomba mwenyezi mungu atuwafikishe sisi na wao kwa kuwaonyesha watu ukweli na kuwatahadharisha kutumbukia katika batili (upotevu) hakika yeye ndie mkarimu zaidi kuliko wote wenye kuombwa.
Nami nina fahamu vyema kitabu changa hiki kitapuuzwa na nakukadhibishwa na kutupiwa tuhuma nyingi za uongo na batili, na jambo hili halitanidhuru kwani nimayaweka hayo yote katika malipo yangu. Na ninafahamu watanituhumu mimi ni kibaraka wa Israel au Amerika au watanituhumu kwamba nimeuza dini yangu na dhamira yangu kwa malipo ya Dunia, na Jambo hili halipo mbali na wala si geni,kwani alishatuhumiwa rafiki yetu mwanachuoni Musa Al-muusawi,kwa tuhuma mfano wa hizi. Ikafikia hata bwana Ally Al-gharwiyy,kusema kwamba mfalme wa Saudia Fahad bin Abdulaziz amemhadaa Dr.Al-muusawy kwa mwanamke mzuri katika ukoo wa Al-Saud, na kumfanya mzito kifedha, na kumuekea kiwango kikubwa cha fedha katika benki za Amerika. Kwa kuingia katika madh-habi ya Al waahabiya!!
Ikiwa hapa ndipo alipo fikishwa Dr. Al-muusawy kwa kusingiziwa uongo na uvumi usio kuwa na msingi wowote, je mimi nitafikishwa wapi? Na watanisingizia mabaya gani? Na huenda wao wananitafuta ili waniue, kama walivyowaua waliosema ukweli kabla yangu.Walimuua mtoto wa maulana , AAYATULLAHI AL-UDHMAA AL-IMAM ASSAYYID ABIL HASSAN AL-ASFAHANIY kiongozi mkuu wa shia katika zama za ghaibu kuu hadi sasa,(shia wanaitikadi yakuwa kuna imamu wao alie potea na atarudi siku yoyote ndio hiyo wanayoiita ghaibu kuu) na bwana mkubwa wa wanachuoni wa kishia bila kupingwa wakati alipotaka kuusahihisha mfumo wa kishia, na kuutoa uzushi ulioingizwa, jambo hilo halikuwapendezea, wakamchinja mtoto wake kama achinjwavyo kondoo ili wamzuie kiongozi huyo na mpango wake wakuusahihisha dosari na upotevu wa kishia,kama walivyo muua bwana AHMAD AL-KASRAWIY,wakati alipo tangaza kujivua katika upotevu huu,nakutaka kuusahihisha mfumo wa kishia, basi wakamkata kata kiungo kimoja kimoja.
Na kuna wengi waliofikia mwisho huu kutokana na kupinga kwao imani hiyo potofu ambayo imeingizwa katika ushia, kwa hiyo si ajabu kunitakia mimi uovo kama huo,
Haya yote hayanishughulishi,na inanitosha kusema ukweli na kuwanasihi ndugu zangu na kuwakumbusha na kuigeuza mitazamo yao waifuate haki. Na lau ningekua nataka chochote katika starehe za dunia,kwa hakika Mut’aa na khumus zingenitosha kwa kunitekelezea hilo,kama wengine wafanyavo, mpaka wakawa matajiri wa mji , na baadhi yao wanapanda magari yaliyo bora zaidi kwa kila toleo jipya,
Lakini mimi ninamshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) nimeyatupilia mbali haya yote tangu nilipo ujua ukweli,nami hivi sasa ninapata riziki yangu na familia yangu kwa kazi za biashara halali na nimegusia katika kitabu hiki muudhui maalumu ili ndugu zangu waione haki kiasi ambacho usibaki ukungu machoni mwa yeyote kati yao.
Na nina nia ya kuandika vitabu vingi vinavyohusu maudhui nyinginezo, ili waislamu wote wawe katika ubainifu,usibakie udhuru kwa mwenye kughafilika au kuwa na hoja jahili. Nami nina yakini kuwa kitabu changu hiki kita kubaliwa na wale wote wanaoutafuta ukweli na haki, nao ndio wengi zaidi,na nina mshukuru Allaah kwa hilo na ama yule atakae khiyari kubaki katika upotevu ili ukuu wao usipotee na kupoteza mut’aa na khumusi miongoni mwa wale waliovaa vilemba, na kupanda magariaina ya Mercesdes na Subaru hawa hatuna maneno nao, Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) ndie tosha yao juu ya yale waliyoyafanya na wanayoendelea kuyafanya katika siku ambayo hayatamfaa mtu mali wala watoto isipokua atakae fika kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) hali ya kuwa moyo wake umesalimika.
Na nina mshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala)ambae ametuongoza katika dini hii tusingekua tumeongoka kama Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) asingetuongoza.
Hakika inavyo julikana kwetu sisi mashia kuwa ABDULLAH IBN SABAI ni mtu wa kubuni hatambuliki kuwepo kwake, wamemtengeneza AHLUS SUNNAH, kwa ajili ya kuutia hila ushia na imani yake,wakamnasibishia (Bin Sabai ) kuanzilishi ushia ili wawazuie watu kuingia ushia, nakutofuata madhehebu ya AHLUL-BAYT. Na nilimuuliza Bwana Mohammad Ali kaashiful-ghatwaa kuhusu IBN SABAI akasema, kuwepo kwa mtu aitwae Ibni Sabai ni kitendawili kisichokuwa na ukweli wowote wamekitunga Ummawiya na Abasiyya kutokana na husda zao dhidi ya Ahlul-Bayt walio takasika,basi inatakiwa kwa mwenye akili asijishughulishe na habari za mtu huyu.
Lakini mimi nimeona katika kitabu chake maarufu kinachoitwa (ASILI YA USHIA NA MISINGI YAKE)ukurasa 40-41,maneno yanayoonyesha kuwepo kwa mtu huyu, na uhakika wake pale aliposema “Ama Abdullahi bin Sabai ambae wanamuhusisha na ushia au wanauhusisha ushia kwake, basi vitabu hivi vyote vya ushia vinatangaza kumlaani na kumkataa......” na hakuna shaka yeyote kwamba huu ni ushahidi wa kuepo kwake (Bin sabai) Na nilipomrudia kutaka ufafanuzi wa maneno haya, alisema: sisi tumesema hivi kwa njia ya Taqiyya tu (kudhihirisha kinyume cha ulicho nacho) kuhusu kitabu ulicho kitaja kimekusudiwa AHHLU SUNNA, (na wala si mashia) na kwa ajili hii nimefuatilia usemi wangu ulio tajwa kwa kusema baadala yake:(kuwa sio mbali mawazo yanayosema kuwa Abdillahi Bin sabai,na wale wanaofanana nae vyote hivyo ni vigano visivyo na uhakika wowote wameviweka wasimulizi na wakuu wa mazungumzo ya paukwa pakawa).
Na alitunga bwana Murtadha Al Asakariy kitabu chake (ABDALLAH BIN SABAI NA VITENDAWILI VINGINE) ndani yake amekanusha kuwepo kwa ibn saba, pia SHEIKH MUHAMMAD JAWAAD MUGHNIYA, kakanusha kuwepo BIN SABAI katika utangulizi wake wa kitabu cha sayyid Murtadwa kilicho tajwa.
Na Abdallah bin sabai ndie sababu mojawapo ambayo inawafanya hasa watu washia kuwa na chuki dhidi ya AHLUS SUNNAH Na bila shaka wale walio mzungumzia Ibn Sabai miongoni mwa AHLUS SUNNAH hawahesabiki , lakini mashia hawazizingatii kauli za wanachuoni wa kisunna kutokana na tofauti zilizopo kati yao, isipokuwa tunapo soma vitabu vyetu vinavyotegemewa (katika ushia) tunaona kuwa ibn sabai ni shaksiya ya uhakika wajapoipinga wanazuoni wetu au baadhi yao na huu ndio ubainifu wa hilo:
1. Imepokewa kutoka kwa Abii Jafar (a.s) kwamba Abdalllah bin saba alikuwa akijitangazia utume, na akidai kuwa kiongozi wa waislamu (Ali) ndie Mungu ametukuka Mungu kwa hilo, madai hayo yakamfikia Ali (a.s) basi akamwita na akamuuliza,akakiri na kusema :ndio wewe ndiwe hasa,kwani nimepata ufunuo katika moyo wangu kuwa wewe ni Mungu, nami ndie Nabii, hapo akasema Ali (a.s)ole wako shetani amekuhadaa,rudi kutokana na haya (yaani acha madai haya)atakukosa mama yako, na utubu,nae akakataa, akamfunga na akamtaka atubu kwa muda wa siku tatu, nae hakua atayari kufanya hivyo akamuunguza kwa moto na akasema :( hakika sheitani amemghuri,alikua akimuendea na kumuekea moyoni mwake mambo hayo).
Na anasimulia Abii Abdallah kwakusema:(Mwenyezi Mungu amlaani Abdallah bin sabai,kwani yeye alimtangazia Uungu kiongozi wa waislamu Ali (a.s), na ninaapa kwa Mwenyezi Mungu Amiril muuminin Ali (a.s) nimja wa Allah, mtiifu,ole wake yule anae tusingizia uongo,kwani baadhi ya watu wanatusemea yale ambayo hatuyasemi hata katika nafsi zetu tuna jitakasa kwa Mwenyezi Mungu na hao,tuanajitakasa na Mwenyezi Mungu na hao) (MA’RIFATU AKHBARU ARIJAL) ukurasa 70-71. na pia kuna mapokezi mengine.
2. Na amesema Almamuqani:( Abdallah bin sabai ndiye ambae amerejea kwenye ukafiri na akatangaza kuvuka mipaka) na akasema:( amelaaniwa ,amevuka mipaka, Amirii –muuminin alimteketeza kwa moto, pia alikuwa akidai kuwa Ali ni Mungu na yeye ni Nabii) TANQIYHUL- MAQAL FII ILMIL RIJAL) JUZUU 2 / 183-184.
3. Na amesema ANNAWBAKHTY( wafuasi wa bin sabai ndio walioanza kuzungumza kuhusu uimamu wa Ali na kusema kuwa uimamu wa Ali ni faradhi kutoka kwa Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) na Bin sabai ni katika watu walio dhihirisha tuhuma kwa Abu Bakr na ‘Umar na ‘Uthmaan na maswhaba wengine na kujitenga nao na akasema kuwa Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) alimuamrisha hivyo) basi Ali (a.s) alimkamata na kumuhoji kuhusu maneno yake haya, akakiri,Ali akaamrisha auwawe, watu wakampigia kelele Ali na kumuambia ‘Ewe kiongozi wa waumuni unataka kumuua mtu anaewataka watu wakupendeni AHLUL BAYT, na kutaka uongozi wako na kujitenga na maadui zako, basi akamuhamisha katika miji mingine, wanasimulia jamaa miongoni mwa wanazuoni kuwa Abdallah bin sabai alikuwa myahudi akasilimu,na akadai kumpenda Ali (a.s) na alikuwa akisema alipokua katika uyahudi wake kuhusu Yushiu bin nuun, baada ya Musa (a.s) maneno haya na akaja kutamka baada ya kusilimu maneno hayahaya kuhusu Ali bin Abii Twalib . Nae ndie mtu wa mwanzo aliedhihirisha usemi wa kuwa uongozi wa Ali (katika uislamu) ni lazima, na kudhihirisha uadui kwa maadui zake Ali,na kwa sababu hii wanasema watu wenye kuupinga ushia asili yake ni uyahudi. kuanzia hapa anasema mwenye kwenda kinyume na shia asili yake ni uyahudi (FIRAQU ASHIAH)uk 32-44.
4. Na amesema Sa’ad bin Abdillah Al-ash’ariy Al qumiy katika mwanzo maneno yake kuhusu wafuasi wa bin sabai:( Assabaiyah ni wafuasi wa Abdillah bin sabai, nae anaitwa Abdallah bin Wahab Arraasibiyyi Al-hamdany ,na alisaidiwa katika mpango wake na Abdallah bin kharsy na bin As-wad,na watu wawili hawa ni katika wafuasi wake wakuu. Na alikuwa wa kwanza kuonesha wazi kuwatusi Abu bakar,’Umar na ‘Uthmaan na masahaba wengine na akatangaza uadui nao) (ALMAQAALAT WALFIRAQ)uk 20.
5. Amesema swaduuq: Amesema Amiril-muuminina (a.s) “Akimaliza mmoja wenu kuswali naanyanyuwe mikono yake juu na ajitahidi kumuomba mungu,basi akasema bin sabai:ewe amiril-muuminina hivi mwenyezi mungu hayupo kila mahali?akasema(Ali)kwa nini isiwe hivyo? Akasema (bin sabai)kwa nini basi mtu anyanyue mikono yake juu? Akasema (Ali) kwani wewe husomi maneno ya Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) yasemayo: " وفي السماء رزقكم وما توعدون"(na katika mbingu kuna rizqi yenu na mliyo ahidiwa) basi wapi mtu ataitafuta rizqi zaidi ya mahali pake? Na mahali pa riziqi palipo ahidiwa na Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) ni mbinguni. (MANLLAA YAHDHURUHUL-FAQIIH, 1/229).
6. Amesema bin Abil-hadyd kuwa Abdallah bin sabai alimuendea Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) huku akiwa anhutubia watu kisha akmwambia( wewe wewe naakawa anarudia rudia kusema hivyo),Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamwambia (una nini wewe? mimi nani?)akasema :wewe ni Mungu. Basi akaamrisha akamatwe yeye na watu walio pamoja nae katika mawazo yake.(SHARHU NAHJUL BALAGHA) juzuu ya 5 / uk 5.
7. Na Assayid Nematullahi Aljazaairiy, amesema:( Abdallah bin sabai aliesema kumwambia Ali (a.s) hakika wewe ndie Mungu wa kweli, Ali(a.s) akamuamisha kumpeleka Madaainu, na inasemekana kwamba alikuwa myahudi akasilimu, pia alipokua katika uyahudi alikuwa akisema khusu Yushi’u bin nun, na musa maneno kama haya aliyo yasema kwa Ali(a.s) (AL-ANUWARU ANNU’U MAANIYYA)juzuu ya 2/ uk 234, basi hizi ni dalili saba (zinazothibitisha kuwepo kwa bin sabai katika ushia) zilizopatikana kutoka kwenye vitabu vinavyotegemewa vya kishia baadhi yake vinahusu Elmul-Rijaal(elemu ya kuwatambuwa watu) na baadhi yake katika fiqhi na madhebu mbalimbali, baja na hivyo tumeacha kunukuu kutoka kwenye vitabu vingine ili tusirefushe, vitabu vyote hivyo vinathibitisha kuwepo kwa mtu aitwae Abdallah bin Sabai.basi haiwezekani kwetu sisi baada ya hoja hizi kukanusha kuwepo kwa bin sabai kwa ushahidi kwamba Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) alitoa adhabu kwa bin sabai kwa kumuita mungu kwa maana hiyo inathibitika kwamba Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikutana na bin sabai, basi hiwezekani kukanusha kuwepo bin sabai baada ya hoja hizi.
Inavyofahamika kwetu sisi mashia nikwamba tunajihusisha sana na Ahlul-Bayt, na madhehebu ya kishia yamejengeka katika misingi ya kuwapenda Ahlul-Bayt -kwa mawazo yetu-, kwa hiyo kupendana kwetu au kuchukiana na watu wengine (AHLUS SUNNAHH) ni kwa sababu ya Ahlul Bayt, na kuwachukia maswahaba hasa makhalifa watatu akiwemo Bi Aisha binti Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambae ni mke wake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na fikra za mashia wote wakubwa kwa wadogo wanawake kwa wanaume wasomi wao na wajinga wao wanaitakidi kwamba maswahaba wamewadhulumu Ahlul Bayt pia wakawauwa na wakawavunjia heshima zao .
Na fikra za mashia nikwamba Ahlus Sunnah ndio walio pandikiza fikra za uadui kwa Ahlul-Bayt kutokana na fikra hizo, hakuna anae sita katika sisi (mashia) kuwaita Ahlus Sunnah maadui, na siku zote tutaikumbuka damu ya shahidi Hussein (‘Alayhi salaam) lakini vitabu vyetu tunavyovitegemea sisi (mashia) vinatueleza ukweli wa mambo tofauti na itikadi yetu, kwani vitabu vyetu vinatufahamisha jinsi gani Ahlul-Bayt wenyewe walivyokuwa wakiwachukia wafuasi wao(mashia) vitabu hivyo pia vinatufahamisha maovu waliyo yafanya mashia waliotangulia kwa Ahlul-Bayt, pia vinatufahamisha ni kina nani walio mwaga damu za Ahlul-Bayt, na ni kina nani walio sababisha vifo vyao na nikina nani walio vunja heshima zao.
Amesema Amirul muuminina (‘Alayhi salaam) {Lau kama utawachunguza mashia (wapambe) wangu basi hutawakuta isipokuwa ni wakunisifia tu, na kama utawapa mtihani mtihani (wakupima imani zao) basi hutowakuta isipokuwa ni murtad wote (wametoka katika dini) na lau kama utawachuja hungempata hata mmoja katika elfu} (ALKAFY/ALRAUDHA 8/833).
Na akasema Amirul muuminina (‘Alayhi salaam) {Enyi wenye kufanana na wanaumme na wala si wanaume, wenye fikra za kitoto na akili za kike natamani nisingewaona wala nisingewajua, jambo ambalo limenisababishia majuto na tabu kubwa, Mwenyezimungu awalaani, hakika mmeujaza moyo wangu uchafu na kifua changu mmekijaza chuki, na mmenijengea tuhuma na mmeniharibia mawazo yangu kwa kuniasi na kunidhalilisha, mpaka maquraish wakasema kuwa mtoto wa Abii Twalib ni mtu shujaa lakini hajui vita. Lakini nitafanyaje wakati hakuna mtu anaetii amri yangu} NAHJUL BALAGHA 70-71.
Na akawaambia wao kwa kuwakemea:- nimepewa mtihani kwa ajili yenu kwa mambo matatu, na mawili: (viziwi wenye masikio, na mabubu wenye kutamka, na vipofu wenye macho, sina marafiki wa kweli wakati wa kukutana na maadui na sina ndugu wa uhakika wakati wa matatizo.mumemfedhehesha mtoto wa Abuu Twalib kama mwamke asie na nguo) NAHJUL BALAGHA 142.
Aliwaeleza hayo kwa sababu ya kumfedhehesha kwao na kumuhadaa kwao Amiril muuminina (‘Alayhi salaam) na anazo(amiril-muuminina) lawama nyingi zinazowahusu wao (mashia).
Na imam Husain (‘Alayhi salaam) amesema katika kuwaombea vibaya mashia ( wapambe) wake: { Ewe Mwenyezi Mungu ukiwastarehesha kwa muda wowote ule basi wagawe makundi, na uwafanye kuwa mapande mapande yenye kukhtalifiana nyendo zao, na wla usiridhie wao kuwa viongozi daima (milele) kwani wao walituita sisi ili watusaidie, kisha wakatufanyia uadui na wakatuua} ALIRSHADLIL MUFID uk 241.
Na aliwasemesha mara nyengine na akawaombea vibaya, katika maneno aliyo yasema: {lakini mlifanya haraka kutuunga mkono, kama ndege wanao kimbilia mzoga, kisha mkapukutika kama vile popo wanao tumbukia motoni, kisha mkaivunja ahadi yenu kwa upumbavu na kujiweka mbali na rehema na kujitumbukiza kwa matwaghuti wa umma huu, na makundi mengine maovu na walioacha kitabu cha Allah, kisha ninyi ndio mnaotudhalilisha na kutuua fahamuni yakua laana ya Mwenyezi Mungu itawashukia madhalimu} AL-IHTIJAJU 2/24
Na maelezo haya yanatuwekea wazi ni akina nani waliomuua Hussein, Nao siwengine bali ni mashia wake (wapambe) watu wa “Kuufa”, ni mababu zetu basi kwanini tunawabebesha Ahlus Sunnah majukumu ya mauaji ya Husein (‘Alayhi salaam)?
Na kwa ajili hii amesema bwana Muhsin Al Amin ( watu wa Iraq wapatao ishirini elfu walimuunga mkono Husein, kisha wakamsaliti, na wakamuasi ingawa walimuahidi kutii, na kisha wakamuua) A’YANU- SHIA 1/32.
Hasan (‘Alayhi salaam) amesema: (Naapa kwa Mwenyezi Mungu ninamuona muawiya ni m’bora kwangu kuliko hawa wanaodai kwamba wao ni kundi langu, walitaka kuniua na walichukua mali zangu, naapa kwa Mwenyezi Mungu kuchukua kutoka kwa muawiya kile ambacho kitazuia kumwagika daamu yangu na nikapata amani kwa watu wangu hilo ni bora kuliko kuniua na kuwapoteza Ahlul Bayt (jamaa zangu) naapa kwa Mwenyezi Mungu kama ningepigana na muawiya, wagenikamata na kunipeleka kwa muawiya kwa kutaka amani, naapa kwa Mwenyezi Mungu kuingia mkataba wa amani na muawiya katika hali ya heshima na utukufu ni bora kwangu kuliko kuniuwa nikiwa mateka, AL-IHTIJAJU 2/10.
Imam Zayinul- Abidin (‘Alayhi salaam) aliwaambia watu wa kuufa: {Je mnajua kwamba mlimuandikia baba yangu na kumhadaa, na mkampa ninyi wenye ahadi, kisha mkampiga vita na kumfedhehesha basi ni kwa jicho gani mtamuangalia bwana Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na watu wake? Wakati akiwaambieni mmemuua mjukuu wangu na mmeivunja heshima yangu basi ninyi si katika uma wangu} AL-IHTIJAJU2/32.
Pia aliwazungumzia akisema:(Ikiwa hawa wanatulilia sisi basi ni akinanani waliotuua wasio kuwa wao?} AL-IHTIJAJU 2/29.
Na Albaqir (‘Alayhi salaam) amesema {lau wangalikuwa watu wote kwetu sisi ni mashia ingelikua robo tatu yao ni wenye shaka na sisi na robo nyingine wangekuwa ni wapumbavu} RIJALUL KUSHY uk 79.
Na amesema Asadiq (‘Alayhi salaam){ni naapa kwa Mwenyezi Mungu lau kama ningewapata miongoni mwenu waumini watatu wanaoficha mazungumzo yangu nisingeona halali kuwaficha mazungumzo} USULUL ALKAFI 1/496.
Na amesema Fatma mdogo (‘Alayhi salaam) katika khutba aliyoitowa kwa watu wa kuufa: {Enyi watu wa (mji) wa kufa enyi watu wa hiana na vitimbi na majivuno. Hakika, Ahlul Bayt Mwenyezi Mungu ametupa mtihani kwenu, na amekupeni mtihani kwetu, lakini akaufanya mtihani wetu kuwa ni mzuri, mkatukufurisha na mkatukadhibisha na mkaona halali kutupiga vita na mkaona ni halali kuiba mali zetu, kama mlivyo muua babu yetu juzi, na panga zenu bado zinadondosha damu zetu sisi Ahlul Bayt, mmepata hasara, basi subirini laana na adhabu kama vile tayari imeshawashukia, na waonje baadhi yenu uchungu wa adhabu kwa vile mtakavyokaa milele katika adhabu yenye kuumiza siku ya kiyama kwa vile mlivyotudhulumu, basi jueni laana ya Mwenyezi Mungu huwafikia madhalimu, hakika mnastahiki hasara ni yenu enyi watu wa kuufa, nimangapi nimeyasoma kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na watu wake kabla yenu kisha mkamfanyia hadaa ya kumuua ndugu yake Ali bin Abii Talib na babu yangu na watoto wake na wajukuu wake wema.
Mmoja katika watu wa kuufa akatujibu kwa kujifakharisha akasema {sisi ndio tulie muua Ali na watoto wake, kwa panga za india na mikuki, Na tukawateka wanawake wao kama inavyo tekwa mali iliyoachwa na wenyewe, na tukawapiga pigo takatifu } AL IHTIJAJU2/28.
Na amesema Zainab mtoto wa Amirul muuminina (‘Alayhi salaam) kwa watu wa kuufa kwa kuwakemea : (baada ya hayo, (utangulizi)Enyi watu wa kuufa, enyi watu hadaa na hiana, na wasaliti Hakika ya mfano wenu ni kama mfano wa mwanamke alieukata uzi wake vipande vipande baada ya kuusokota, hamna lolote zaidi ya kujisifu kwa mambo msiyokuwa nayo na kujiona na uongo! mnamlilia ndugu yangu? Basi lieni sana na chekeni kidogo, ni hakika kuwa mmefanyiwa mtihani, kwa kumuaibisha, vipi mliona rahisi kukiua kizazi cha Mtume wa mwisho (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) AL IHTIJAJU, juzuu ya 2 ukurasa wa 29-30.
Tunafaidika kutoka na hoja hizi- na tumeziacha nyingi zisizokua hizo- faida zifuatazo:
Kwa kweli nimeyasoma maelezo haya mara nyingi na nikayafikiria sana, nani kayaandika sehemu maalum, na nikakesha masiku mengi nikiyachunguza na kuyatafakari kwa makini maelezo haya –na mengineyo ambayo ni mengi kuliko niliyo yaandika – sikuzinduka katika fikra hizo ila nilijikuta nikisema kwa sauti kubwa sana “mwenye zimungu awe pamoja nanyi Ahlul-Bayt hakika mmekutana na misukosuko mingi kutoka kwa hawa wanaodai kuwa ni wafuasi wenu (mashia)”
Sisi tunajua sote maudhi yaliyowapata manabii wa Mwenyezi Mungu na Mitume wake (‘Alayhi salaam) kutoka kwa watu wao na yale yaliyo mpata Nabii wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na watu wake, lakini nimestaajabika na mambo mawili kutoka kwa Musa (‘Alayhi salaam) na subira yake juu ya wana wa israil, kwa sababu tunaona jinsi gani qur-an ilivyo muelezea mussa kuliko mtu mwengine na ikaeleza wazi jinsi alivyo vumiliya maudhi ya wana wa israel, na hadaa zao na vitimbi vyao na uadui wao.
Pia ninawashangaa Ahlul Bayt (‘Alayhi salaam) kwa kuvumilia kwao maudhi mengi waliyo yapata kutoka kwa watu wa kufa kitovu cha mashia, waliwa fanyia hiana wakawasaliti na kuwaua na kupora mali zao hata hivyo Ahll-Bayt waliyavumilia yote hayo, pamoja na hayo yote sisi bado tunawatupia lawama Ahlul-sunnah na tunawabebesha mzigo wote!
Na tunaposoma vitabu vyetu vya kutegemewa tunapata mshangao, hawezi kuamini mmoja wetu tunaposema kuwa vitabu vyetu sisi mashia vinawakashifu Ahlul Bayt (‘Alayhi salaam) na kumkashifu Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na watu wake, kwa uthibitosha wa hayo soma maelezo yafuatayo:imepokewa kutoka kwa Amirul muuminina (‘Alayhi salaam) kwamba punda wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) aitwae Ghufayr alisema kumuambia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) : namtoa fidia baba yangu na mamam yangu kwako ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, baba yangu alinisimulia kutoka kwa baba yake na babu yake, kua baba yake : alikuwa pamoja na nuhu katika safina akasimama akapangusa katika kiuno chake kisha akasema: katika mgongo huu atatoka punda ambae atapandwa na bwana wa Mitume na wa mwisho wao, namshukuru Mwenyezi Mungu ambae amenijaalia kua mimi ndie punda huyo. USUULUL KAFI 1/237.
Riwaya hii inatufundisha haya yafuatayo:
Siku moja tulikuwa tunasoma kitabu kimoja kiitwacho Usuulul- kafi, pamoja na badhi ya wanafunzi wa chuo cha cha Annajaf kwa imam ALKHUUIY, akajibu imam ALKHUUIY kwa kusema : uangalieni muujiza huu, Nuhu(‘Alayhi salaam) anatoa khabari za Mohamad na unabii wake kabla ya kuzaliwa kwake kwa miaka mingi.
Yakabakia maneno ya imam ALKHUUIY yana gonga gonga katika masikio yangu kwa muda mrefu huku nikijisemea katika nafsi yangu: itawezekana vipi jambo hili liwe muujiza? na ndani yake kuna punda anamwambia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na watu wake, namatoa fidia kwako wewe baba yangu na mama yangu?!! Na vipi inawezekana kwa amiril-muminina (‘Alayhi salaam)(kiongozi wa waislamu) kunakili maneno kama haya? Lakini nikanyamaza kama walivyo nyamaza wasikilizaji wengine.
Na Sudduqu amenakili maelezo kutoka kwa Aridhaa(‘Alayhi salaam) katika kuyayatafsiri maneno ya Mwenyezi Mungu yasemayo
(وإذ تقول للذي أنعم الله عليه وأنعمت عليه أمسك عليك زوجك واتق الله وتخفي في نفسك ما الله مبديه)
سورة الأحزاب:37 "
{Na (wakumbeshe) ulipo mwambia yule ambae Mwenyezi Mungu amemneemesha( kwakumwaafikia uislamu) na wewe ukamneemesha kwa kuumpa ungwana, nae ni bwana Zaid bin Haritha (ulipomwambia) ‘Shikamana na mkeo na umche Mwenyezi Mungu(usimuache)’na ukaficha katika nafsi yako aliyotaka Mwenyezi Mungu kuyatoa.} ALAHZAB/37,
Amesema Arridha mfasiri wa aya hii {hakika ya Mtume (‘Alayhi salaam) na wtu wake alikwenda nyumbani kwa Zaid bin Harith kwa haja fulani, basi akamuona mke zaid ambae ni Zainab akioga akamwambia: ametakasika aliye kuumba} UYUNU AKHBARU ARRIDHA uk 113.
Je inawezekana kwa Mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kumuangalia mke wa mtu muislamu, na kumtamani na kumshangaa? kisha amwambia ametakasika aliye kuumba?! Je hivi sikumtukana Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)?!
Imepokewa kutoka kwa Amirul muuminin kuwa alimuendea Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na watu wake na akiwa pamoja na Abu bakar na Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) akasema {Nikakaa kati yake na Aisha, akasema Aisha hukuona chochote isipokua pajalangu na paja la Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)? akasema Mtume:nyamaza ewe Aisha }AL BURHAN FII TAFSIRL QUR-AN uk 4/225.
Na mara nyingine alikuja bila kupata sehemu ya kukaa, akamuashiria Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kuwa njoo hapa akimaanisha nyuma yake, wakati huo Aisha akiwa amesimama nyuma yake akiwa amejistiri:akaja Ali(‘Alayhi salaam)akakaa kati ya Mtume na Aisha, akasema Aisha kwa hasira: {hukupata sehemu ya kuweka matako yako isipokua paja langu? Akakasirika Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na akasema: Ewe kipunda usiniudhi kwa ndugu yangu) KITABU SULAIM BIN QAIS 179.
Na imepokewa na Al-majlisy kuwa Amirul muumini amesema:{nilisafiri pamoja na Mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na watu wake, akiwa hana mtumishi isipokuwa mimi na alikuwa na shuka moja hana nyengine isipokuwa hiyo na alikuwa nae Aisha katika safari hiyo, na alikuwa Mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na watu wake analala kati yangu na Aisha, hakuna mtu kati yetu aliekuwa na shuka zaidi ya shuka hiyo ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)
Basi ikawa anaposimama kwa ajili ya sala za asiku hujifunua shuka kwa mkono wake katika sehemu yake ya katikatii kati yangu na Aisha mpaka shuka hugusa shuka la tandiko ambalo liko chini yetu} BIHAARUL ANWARI 40/2.
Hivi kweli Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ataridhika ‘Ali akae katika mapaja ya bibi Aisha mkewe? Hivi Mtume hamuonei wivu mkewe itakuaje amuache kwenye godoro moja na mtoto wa Ami yake ambae hazingatiwi kuwa muharimu wake? Kisha ataridhika vipi Amiril-Muminina juu ya hayo?!
Amesema bwana ‘ALI GHURWIYU mmoja kati ya wanazuoni wakubwa wa hapa chuoni {hakika Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ni lazima utupu wake ukaingie motoni kwa sababu yeye aliwaingilia wanawake washirikina akikusudia hivyo mke wake Aisha na Hafsa, na kusema maneno haya ni kumkosea heshima Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kwasababu lau itaingia tupu ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ndani ya moto hakuna atakae ingia peponi kamwe.
Natosheka na mapokezi haya sita yaliyomuhusu Mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)na ali zake Ili niende katika maudhui nyingine.
Pia wametoa maelezo mengi yamhusuyo Amirul muuminin (‘Alayhi salaam) yafuatayo ni sehemu ndogo katika hayo:
Na sisi tuna jiuliza: Je anawezaje Amirul muuminin kuangalia mapaja ya mwanamke ajnabi (anaeweza kumuoa) Na je inaingia akilini kwa immu ASSAADIQ kunakili habari kama hii, au inawezekanaje kwa mtu anaeipenda familia ya Mtume kusema maneno kama haya?
Hivi inawezekana kwa Amirul muuminin kutamka maneno machafu
Je inawezekana kwa Amiril- muminina kumuambia mwanamke kuwa ninazifahamu habari zako vizuri?
Na je anaweza Asadiq (‘Alayhi salaam) kunukuu maneno mabaya kama haya?, Lau kama habari hizi zingekua katika vitabu vya Ahlus Sunnah dunia ingewaka moto wala isinge kalika na tungeli wafedhehesha vibaya, lakini yamo katika vitabu vyetu sisi mashia!
Nasisi tunauliza jamani hivi kweli Amirul muuminin alikuwa muoga kiasi hiki?.
Hebu angalia jinsi walivyo msifu Amirul muuminin(‘Alayhi salaam) aliposema Fatma kuhusu yeye:{Hakika wamawake wa kikuraishi walinizungumzia kuwa yeye ni mtu mwenyetumbo kubwa, mwenye mikono mirefu, mwenye miguu minene, na upara, macho makubwa, mwenye mabega mapana kama ya ngamia, meno nje, tena faqiri (masikini)} TAFSIRUL-QUMMIYU 2/336.
Imepokewa kutoka kwa Abu Is’haq kuwa alisema: Baba yangu aliniingiza msikitini siku ya ijumaa, akaninyanyua nikamuona Ali akikhutubu juu ya mimbari hali ya kuwa ni mzee, mwenye kipara, pajilauso limekunjana mwenye mabega mapana mwenye machokulegea} MUQATILU-TALIBINA.Je kweli hizi ndizo sifa alizo kuwa nazo Amirul muuminin (‘Alayhi salaam)?
Mpaka hapa naona tutosheke na maelezo haya ili tuweze kuleta maelezo mengine yanayomhusu Fatma (‘Alayha salaam):Basi Fatma alikua ni mlevi mpaka afanye hivi?
Na wamemsifu Ali (‘Alayhi salaam) sifa nyingi wakasema: {Alikuwa mweusi wa rangi mwenye kimo cha wastani hakuwa mfupi wala mrefu, alikuwa na tumbo kubwa, vidole vyembamba, mikono iliyojaa, miundi iliyojaa, macho malegevu, ndevu nyingi, kipara, na uso uliokunjana} MAQATILU ALTALIBINA 27.
Ikiwa sifa hizi ni za Amirul muuminin kama wanavyo sema inawezekana vipi mtu kuzikubali sifa kama hizi? Basi tutosheke na maelezo haya kwa kutaka kufupisha, ingawa tulikuwa na hamu ya kunukuu maelezo yaliyo pokewa kutoka kwakila mmoja miongoni mwa viongozi wetu (wa kishia)
Lakini badala yake tukaonelea kutosheka na mapokezi matano tu yaliyo pokewa kwa kila mmoja, pia tukaonelea maelezo yatakuwa marefu sana endapo tutanukuu mapokezi aina tano yanayomhusu Mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na matano mengine yanayomhusu Amirul muuminin(‘Ali), na matano yanayomhusu Fatma tuliona maelezo hayo yatahitaji kurasa nyingi kwa hivyo tutajitahidi kupunguza zaidi tukijaribu kuweke wazi mengi yaliyo fichika.
Aliandika AL KULAINIY katika kitabu AL-USUL akinakili kutoka katika kitabu AL KAFI: maneno yasemayo: hakika Jibrilu alimteremkia Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akamwambia ewe Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria mtoto atakae zaliwa na Fatma, atauliwa na umma wako baada ya kuondoka wewe, akasema “Ewe Jibril, mpelekee mwenyezimungu salamu zangu na umuambie, sioni haja ya mtoto atakaezaliwa na Fatma kisha auliwe na umma wangu baada yangu” jibril akapanda mbinguni kisha akashuka akasema yaleyale: “Ewe Jibrilu mpelekee mola wangu salamu na umwambie sina haja na mtoto atakaeuliwa na umma wangu baada ya kuondoka kwangu, ” akaapa Jibrilu mbinguni akateremka nakusema: Ewe Muhammad mola wako amekutolea salamu na kukubashiria kua amejaalia katika kizazi cha mtoto huyo uongozi na wasia, akasema (Mtume) nimeridhika, kisha Mtume akatuma mtu kwa Fatma na kumuambia kuwa Mwenyezi Mungu amenibashiria mtoto, utakaemzaa wewe kisha atauliwa na umma wangu baada ya kuondoka (kufa) kwangu, na Fatma nae akatuma mtu kwa Mtume akimwambia sina haja na mtoto atakaeuliwa na umma wako baada ya kufa kwako, Mtume akatuma tena mtu kwa Fatma akimwambia kuwa mwenyezimungu amejaalia katika kizazi chake uongozi na wasia, Fatma nae akatuma mtu akisema nimeridhika, Fatuma akabeba mimba (ya Husain) kwa taabu, na akazaa kwa taabu, na Husain hakunyonya kwa (mama yake) Fatma (‘Alayha salaam) wala kwa mwanamke mwingine bali alikuwa akiletwa kwa Mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na kumuekea kidole chake cha gumba katika mdomo wake na kunyonya kiasi kinachomtosha kwa siku mbili au tatu.
Hapa tunjiuliza maswali je ni sahihi kuwa Mtume alikuwa anaweza kukataa jambo alilobashiriwa na mwenyezimungu? Na je Fatma nae alikuwa anaweza kukataa jambo lilopitishwa na mwenyezi Mungu na kumbashiria, kweli anaweza kufanya hivyo kwa kusema sina haja nalo?na je alibeba mimba ya Husein akiwa amemchukia, na kumzaa huku amemchukia, na je alikataa kumnyonyosha mpaka ikafikia aletwe kwa Mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na kumyonyesha kwa kidole chake cha gumba kiasi cha kumtosha siku mbili ua tatu?.
Hakika bwana wetu shahidi Husain (‘Alayhi salaam) kwa upande wake yeye haifai kusemwa maneno kama haya wala kwa upande wa mama yake kusemwa kuwa yeye alichukia kubeba mimba yake na kumzaa..kwani wanawake wote wa dunia hii wanatamani lau kila mmoja wao angezaa watoto kumi mfano wa imam Al Husein(‘Alayhi salaam), vipi itawezekana kwa Bi Fatma kuchukia kubeba mimba ya Husein na kuchukia kumzaa, na kuacha kumnyonyesha.
Katika kikao kilicho kusanya idadi kubwa ya waheshimiwa na wanafunzi wa hapa chuoni imamu ALKHUIY alizungumzia mauudhui mbalimbali kisha akamaliza maneno yake: kwa kusema Mwenyezi Mungu awalaani makafiri, tukasema ni akina nani hao? Akasema: ni wale maadui zetu (AHLUS SUNNAH), wanamtukana Husein(‘Alayhi salaam) vilevile wanawatukana Ahlu Bayt!!
Nitasema nini kumwambia imam AL KHUIY!
Alipo muozesha Amirul muuminin binti Yake Ummu Kulthum kwa ‘Umar bin Al Khatwaab, alisema Abuu Jaafar al khulainiy akimnukuu Abii Abdillah(‘Alayhi salaam) kuwa ‘Umar alisema kuhusu ndoa hiyo:{hakika huo ni utupu tulio upora!!!!} FURU’UL- KAFIY 2/141.
Hapa tumuulize msemaji wa maneno haya: je ‘Umar alimuoa Ummukulthum ndoa ya kisheria au alimchukua kwa nguvu ? Maneno aliyonasibishwa kwa Assaadiq (‘Alayhi salaam) yapo wazi je anawezaje Abuu Abdillah kusema maneno kama yakimuhusu mtoto wa ‘Ali (‘Alayhi salaam).
Lau ingekua kweli ’Umar alimpora Ummu Kulthum basi ingewezekana vipi baba yake simba wa Mwenyezi Mungu, na mwenye ukali pia ni kijana wa kiquraishi kuridhia unyonge huu?!
Basi tunaposoma kitabu kiitwacho ARRAUDHA -MINAL KAFI 8/101. katika mazungumzo ya Abii Basyr pamoja na mwanamke ambae alikuja kwa Abii Abdillah akiuliza juu ya (Abu Bakr na ‘Umar) akasema kumwabia unawapenda, akasema:nikikutana na mola wangu nimwambie kuwa wewe unaniamrisha kuwapenda (Umar na Abu Bakr)akasema ndio.
Basi mtu anaeamrisha kumpenda ‘Umar vipi atamtuhumu kuwa alimpora mwanamke katika Ahlul-Bayt?
Nilipomuuliza imam Al khuiyu kuhusu maneno ya Abii Abdillah aliyomuambia yule mwanamke kuhusu kuwapenda Abibakar na ‘Umar, akajibu kwa kusema: hakika alimuambia vile kwa Taqiya!! (kutamka au kufanya tafauti na unavyo amini kwa kuogopa)
Basi na mimi namwambia Al imam Khuiy: hakika yule mwanamke ni katika mshia wa Ahlul Bayt, na Abu Basiyr ni katika jamaa wa karibu waAssadiq (‘Alayhi salaam)(kiongozi mkubwa wa kishia) kwa hiyo hapakuwa na haja yakutumia taqiyya, kama ingekuwa sahihi kufanya hivyo, lakini maneno haya ya Abul-qassim Alkhuuiy, ni kujitetea kusiko sahihi,
Kuhusu Hassan ameeleza Al Mufidi katika kitabu kiitwacho AL- irshad akiwaelezea watu wa kuufa kuwa:{waliizingira nyumba yake na wakamkamata kwa nguvu na wakamnyang’nya mswala wake aliokua amekalia akabaki ameshika upanga wake akiwa uchi (kwa maana kua walimvuwa nguo) uk190. Je atabakije Hasan(‘Alayhi salaam) akiwa hana nguo mbele ya watu?Je kusema maneno haya ndio mapenzi kwa Hassan au kashfa?
Na aliingia Sufian bin Abii laila kwa Hasan (‘Alayhi salaam) nae akiwa ndani mwake na kumwambia imam Hasan:{Amani iwe juu yako ewe mdhalilishaji wa waumini!akasema “una ushahidi gani juu ya hilo”? akasema: umekabidhiwa jukumu la kuongoza umma ukajivuwa na kumuachia huyu muovo anawahukumu watu kwa sheria isiyo ya mwenyezi mungu!} RIJALUL KUSHIY uk 103.
Je kweli Hasan (‘Alayhi salaam)alikuwa ni mdhalilishaji wa waumini?au alikuwa ni mwenye kuwatukuza kwa kuzihifadhi damu zao, na kuwaunganisha kwa hekima zake, na kwa mtazamo wake ulio madhubuti?
Lau kama Hasan (‘Alayhi salaam) agepigana na Muawiya kwa kugombea ukhalifa(uongozi) basi Ingemwagika damu nyingi ya waislamu, na wangelikufa watu wengi isinge weza Kuijuwa idadi yao, isipokua Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala) na ungegawanyika umma makundi makundi, na usingeweza kusimamisha jambo lolote wakati huo.
Na masikitiko makubwa ni kua maneno haya yamenasibisha kwa Abii Abdillah (‘Alayhi salaam) nina apa kwa Mwenyezi Mungu kuwa yeye yuko mbali na maneno haya na mfano wake.
Ama imam Assaadiq yameshampata kutoka kwa mashia maudhui mengi na kumsingizia kila aina ya uovu, tunasoma pamoja maelezo haya yafuatayo:
Imepokewa kutoka kwa Zurara kuwa alisema:{nilimuuliza Abaa Abdillah(‘Alayhi salaam) kuhusu Tashahhud nikasema “Attahiyyaatu wa ssalawaatu” nae aksema kama nilivyo sema mimi basi nilipo toka nikamjambia kwenye ndevu zake, na kusema hatofaulu milele} RIJALUL KUSHIYI uk 142.
Ni haki yetu kumlilia kwa machozi ya damu Imam Asadiq, anawezaje mtu kutoa maneno machafu kama haya kwa kiongozi mkubwa kama imam Abii Abdillah??Je inawezekana je kwa Zurara kumjambia Abii Abdillah (‘Alayhi salaam) katika ndevu zake?! na kumwabia kuwa hatofaulu milele?
Hakika zimepita karne kumi toka kuandikwa kitabu cha ALKUSHIYI, na kimepita katika mikono ya wanazuoni wa mkundi mbalimbali ya kishia, sikuona yoyote kuyarudi maneno haya au kuyapinga Mpaka imamu Alkhuuiy wakati alipo kuwa akiandika kitabu chake kikubwa (MUUJAMU RIJALUL-HADITH) na mimi nilikua mmoja wa waliomsaiidia kuandika kitabu hiki, na katika kukusanya riwaya mbalimbali kutoka katika vitabu vikubwa, na tulipomsomea riwaya hii alinyamaza kidogo, kisha akasema:kila kizuri kina kasoro na kila mjuzi anamakosa, hakuzidisha zaidi ya maneno hayo, lakini sisi tunabaki tukijiuliza ewe imam mtukufu, hakika makosa huja kwa kughafilika, au kukosea bila kukusudia, lakini kwa sababu ya uhusiano uliopo kati yangu mimi na wewe kiasi nimekuwa kama mtoto wako na umekuwa kama baba yangu, nalazimika kuyachukua maneno yako kwa nia njema lau si hivyo nisingeridhia kunyamaza kwako juu ya udhalilishaji huu aliofanyiwa imamu Assaadiq (‘Alayhi salaam).
Na amesema sheikh AL KULAINIY (amenieleza Hisham bin hakami na Hammadu kutoka kwa Zurara kuwa alisema: Nikajisemea nafsini mwangu: sheikh hajuwi ugomvi-akimkusudia imam wake-)
Na wameandika katika sherhe ya hadith hii: Hakika sheikh huyu ni mzee asie na akili, wala hawezi kuzungumza na maadui. Basi je imam Al Sadiq(hana akili?)
Hakika moyo wangu umepata uchungu na huzuni kwa sababu ya matusi haya na shutma hizi.
Na uovu huu haustahiki kwa Ahlul Bayt, inatakiwa kuwaheshimu.
Ama Al-Abbaas na mtoto wake Abdillah, na mtoto wake mwingine Ubaidillah na Aqiil (‘Alayhi salaam) wote hawakusalimika na matusi na kubezwa na kusengenywa, soma nami maelezo haya: ameeleza AL-kushiyi kuwa aya isemayo(لبئس المولى ولبئس العشير):{Ni rafiki mbaya alioje na jamaa mbaya alioje} imeteremka kumlaumu AbasI (Radhiya Allaahu ‘anhu).( RIJALUL KUSHIYI)54, na neno lake Mwenyezi Mungu lisemalo:
(ومن كان في هذه أعمى فهو في الآخرة أعمى وأضل سبيلا)
{Na mwenyekua kipofu katika dunia hii na akhera atakua kipofu na mwenye kupotea njia}
Na neno lake Mwenyezi Mungu mtukufu lisemalo:
(ولا ينفعكم نصحي إن أردت أن أنصح لكم
){Nawala hazitowafaa nasaha zangu nitapo wanasihi}zimeteremka kwake(52-53).
Na pia amepokea Al Kushiy kwamba Amirul muuminin(‘Alayhi salaam) aliwaombea dua mbaya Abdillah bin Abbaas na ndugu yake Ubaidullah akisema: (Ewe Mwenyezi Mungu walaani watoto wawili wa Fulani akikusudia Abdullahi na Ubaydullah, na wapofoe macho yao kama ulivyo pofoa nyoyo Zao, na ujaalie kupofoka macho yao kuwa ni ushahidi wa kupofoka nyoyo zao) 52.
Na amepokea tegemeo la uislamu Abuu Jafar Al Kulainiy katika kitabu cha Alfurui kutoka Kwa imam Al- baqir kuwa aliesema kuhusu Amirul muuminin: (akabakia pamoja nae watu wawili Wanyonge madhalili wageni katika uislamu, Abasu na Aqiilu)
Hakika aya tatu ambazo Al kushiyi amedai kuwa zimeteremka kwa ajili ya Abbas maana yake Nikua anamuhukumu kua ni kafiri na atakaa milele motoni siku ya Qiyama, na
Ama kuhusu Amirulul muuminin (‘Alayhi salaam) kwamba aliwaombea vibaya watoto wawili wa Abasi-Abdillah na Ubaydullah, kwa kuwaombea laani na upofu wa macho na moyo basi hii inatosha kuwa ni kuwakufurisha pia.
Hakika ya Abdillahi bin Abbas, Ahlu-ssunna wamembandika jina la: mafasiri wa Qur-an na mwanachuoni wa ummah, iweje sisi mashia tumlaani na huku tukidai kuwapenda Ahlul –Bayt?(jamaa zake Mtume).
Na ama Aqiilu (‘Alayhi salaam) yeye ni ndugu wa amirul muuminin (‘Alayhi salaam), Je yeye ni mdhalilifu, na ni mgeni Katika uislam?
Ama kuhusu imam Ziyyinul abidina Ali bin Husein amepokea Al Kulainiyi kwamba yazidu mtoto wa muawiya alimuomba kua mtumwa wake, akaridhika (zaynul-abidin) (‘Alayhi salaam) kuwa mtumwa wa Yazidu alipomuambia (nimekubali uliyo yaomba, mimi ni mtumwa nilie lazimishwa kuwa mtumwa ukipenda nitumie au niuze) AL RAUDHA MINAL KAFI –8/235.
Angalia neno lake (zainul-abidina) na maana yake: {Nimekubali kuwa mimi ni mtumwa kwako, na mimi ni mtumwa alie lazimishwa kuwa mtumwa kwa hiyo ukipenda nibakishe niwe mtumwa wako, na ukitaka kuniuza niuze}hivi inawezekana imam zainul-abidina (‘Alayhi salaam) kuwa mtumwa wa Yazidu amuuze anavyotaka au amtumie anavyo taka?
Tukitaka kueleza maneno yote yaliyosemwa kuhusu Ahlul Bayt basi maneno yatakua marefu kwa sababu hakuna alie salimka na maneno makali na machafu au vitendo viovu wamesingiziwa vitendo vingi vichafu, na hayo yanapatikana katika vitabu vyetu vinavyo tegemewa, tutakuletea baadhi ya mneno hayo katika sehemu ijao.
Soma nami riwaya hii ifuatayo:
Imeokewa kutoka kwa Abi bdillah (‘Alayhi salaam) (Kwamba Mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alikuwa halali mpaka aubusu uso wa Fatma) BIHAARUL-ANWAR 42/44
Na imepokewa kuwa: (Alikua (Mtume) anaweka uso wake mtukufu katikati ya chuchu mbili za Fatma) BIHARUL-ANWAR 43/78.
Hakika Fatma (‘Alayha salaam) ni mwanamke aliye balehe-kufikia umri wa ukubwa- (wakati huo) basi je inaingia akilini kuweka Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) uso wake kati ya chuchu zake? Na ikiwa Mtume na mwanawe (Aaisha) wamefikiswha hapa na watu hawa (mashia) je mtu mwengine watamfikishwapi?piawamemtilia shaka imamu Mohammad Al Qaani, Je yeye ni mtoto wa imamu Ridha au ni mtoto wa (…)
Soma nami maelezo haya:
Imepokewa kutoka kwa Ali bin Jafar
{Hatujawahi kua na imamu mwenye mbadiliko ya rangi iliyochanganyika na weusi akawaambia imamu Aridhaa(‘Alayhi salaam) Je ni mtoto wangu, wakasema: hakika Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alipitisha hukumu kwa kutumia mtaalamu wa kufuatilia nyayo na koo za watu basi na sisi tumtumie mtaalamu huyo akasema imamu Ridhwaa nendeni mkamwite nyinyi lakini mimi hapana, na wala msiwafahamishe mnalo waitia na iwe mjumbani kwenu.
Walipokuja walitukalisha bustanini na wakawapanga mstari shangazi zake na ndugu zake wa kiume na wa kike, kisha wakamchukuwa Arridhwaa (‘Alayhi salaam) wakamvisha juba la sufi na kofia yake, kisha wakamuekea kwanye shingo yake futi za kupimia kisha wakamuambia ingia kwenye bustani ujifanye kama unafanya kazi, kisha wakamleta Abu jaafari (‘Alayhi salaam) wakamuambia mkutanishe huyu mtoto na baba yake, akasema hayupo hapa babayake isipokuwa huyu ni ammi wa baba yake, (ammi ni ndugu yake baba)na huyu ni ammi yake na huyu ni shangazi yake, na kama kutakuwa na baba yake hapa basi ni huyu mwenye bustani, kwa sababu miguu yao inafanana, alipo rudi ABUL-HASSAN wakasema huyu ndie baba yake. USUULUL KAF1/322.
Hii ina maana kuwa walikuwa na wasiwasi yakuwa Muhammad Al Qaaniu (AMANI YA MUNGU IMSHUKIE) alikuwa ni mtoto wa Arridhwa, wakati wa kuwa Arridhwa mwenyewe anasisitiza kuwa ni mtoto wake, lakini watu wengine wanalipinga hilo na kwa sababu hiyo walisema (hatujawahi kuwa kiongozi mwenye mchanganyiko wa rangi) bila shaka hii ni kumtukana na kumvunjia heshima Arridhwa (‘Alayhi salaam) na kumtuhumu mkewe na zinaa na kuutilia mashaka uaminifu wake kwa sababu hiyo walikwenda kumleta mtaalamu wa kufananisha na kufuatilia nyayo na kutambua koo za watu, lakini mtaalamu huyo alihukumu kuwa Muhammad Al-qaaniu ni mtoto wa Arridhwa wa kumzaa, hapo waliridhika na wakanyamaza.
Inawezekana kutuhumiwa watu wengine mfano wa tuhuma hizi na hayo wanaweza wakayaamini watu, ama kuwatuhumu Ahlul Bayt(‘Alayhi salaam), hilo ni miongoni mwa maovu makubwa, lakusikitisha ni kuwa vitabu vyetu vikubwa ambavyo tunadai kuwa vimenakili elimu ya Ahlul Bayt, vimejaa upotevu mfano wa upotevu huu, -hakuna ujanja wala nguvu isipokuwa kwa msada wa Mwenyezi mungu- tuliposoma maelezo haya wakati tukiendelea na masomo chuoni, wanazuoni wetu waliyapitia harakaharaka, bado nakumbuka sababu alizozitowa imamu Al-khuuiy pale alipo yapitia maelezo haya, alisema akimnukuu bwana Al-kaashiful-ghitwai: walifanya hivyo kwa kutaka kuubakisha ukoo wao ukiwa safi.
Pia walimtuhumu Arridhwa(‘Alayhi salaam) kua alikuwa akimpenda binti ya ammi yake maamuni nae pia alikua akimpenda.(angalia UYUNI AKHBAR ARIDHA)
Wakambandika Ja’far, nakumuita Ja’far muongo, wakamtukana na kumtusi pamoja na kuwa ni Ndugu yake Al hassanil- askariyi, amesema Al kulainiyi:(jaafari ni mwenye kudhihirisha matendo maovu, mlevi, ndie mwanamme duni kuliko wote nilio waona, ni mwenye kujivunjia heshima pia ni mtu duni sana. (USUULU LKAFI)1/504
Basi tujiulize ni kweli katika Ahlul-Bayt kuna walevi, au mafasiqi au watu waovu?
Na tunapotaka kupata ufafanuzi zaidi, ni juu yetu kusoma vitabu vinavyo tegemewa na Sisi (Mashia) ili tueze kujua nini kilicho semwa kuhusu Ahlul-Bayt wengine walio bakia amani ya mungu iwashukie, ili tujue ni vipi waliuawa watoto wao walio twaharika na wapi waliuliwa?na ni akina nani waliowaua?
Wengi wao waliuawa ndani ya miji ya Fursi kwa mikono ya watu walio katika miji hiyo lau
Na ujue kuwa walio kumbana na matusi mengi zaidi na kubezwa na kusengenywa ni maimamu wawili: Muhammadul- baagir na mtoto wake Jaafar Asadiq amani ya mungu iwashukie wao na baba zao, hakika wameegemezewa mambo mengi, kutumia taqiyyah, kufanya mut’a kuwalawiti wana wake, kuazimana wanawake, na mengi mengine. Ingawa wenyewe wako mbali na hayo yote.
Nilikuwa nataka kuweka anuani ya sehemu hii kua ni {MWANAMKE KATIKA USHIA} lakini nikaibadilisha anuani hiyo kwa sababu nimeona mapokezi yote yanayopatikana katika vitabu vyetu yananasibishwa (yanaegemezwa) kwa mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na kwa Amiril muiminina na kwa Abii abdillah (‘Alayhis Salaam) na wengineo miungoni mwawanazuoni.
Na mimi sikutaka wana zuoni hao wapatwe na lawama za aina yeyote ile kwani katika riwaya hizo kuna maneno machafu ambayo mtu yeyote hawezi kuyaridhia katika nafsi yake, vipi mtu atayaridhia maneno hayo kwa mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) au atawezaje kuyaridhia kwa Ali wa mtume au kwa maimamu watukufu (amani ya mungu iwashukie)
Hakika mut’a imetumika vibaya sana na mwanamke amedhalilishwa (kwa sababu ya dhana ya uhalali wa mut’a) udhalilishaji mbaya sana,watu wengi wakawa wanakidhi matamanio yao ya kimwili chini ya pazia ya mut’a,na kutumia jina la dini,wakilitumia neno lake Mwenyezi Mungu lisemalo:{....فما استمتعتم به منهن فآتوهن أجورهن فريضة....}
{Mtakapostarehe nao baada ya kufunga nao ndoa basi wapeni mahari
Zimepokewa riwaya nyingi kutoka kwa mashia zinahimiza mut’a mpaka wakafikia kuweka thawabu kwa mwenye kufanya mut’a na madhambi kwa mwenye kuacha mut’a,na inazingatiwa kila asiefanya si muislamu (kwa mtazamo wamashia)
Soma pamoja na mimi ushahidi huu:
Ninasema: kwa ajili ya kupata thawabu hizi (za mut’a) walimu wote wa hapa chuoni na viongozi pamoja na wanawake wazuri waliopo hapa chuoni wote wanafaya mut’a kwa wingi sana,na nakusudia kutaja miongoni mwao bwana ALSADRU- NA AL-BARO JARDY- NA ASHIRAZY- NA ALQAZ’WAYN, NA ALTABATABAI, NA ASSAYID AL MADANIY, bila kumsahau kijana anaenyanyukia, ABDUL HARITH AL-YASIRIYI, na wengineo, hakika hao (waliotajwa) wanafanya mut’a kwa wingi na kila siku kwa hamu yakupata thawabu hizo (zilizo tajwa) na kutaka kua pamoja na mtume peponi .
Na amepokea bwana FAT-HULLAHI ALKASHAANIY katika kitabu TAFSIR MINHAJI ALSADIQIYNA kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: “atakae fanya mut’a mara moja atapata daraja ya Husain (‘Alayhis Salaam),na atakae fanya mara mbili atapata daraja ya Hasan (‘Alayhis Salaam),na takae fanya mara tatu atapata daraja ya Alli Bin Abii Talib (‘Alayhis Salaam),na atakae fanya mara nne atapata daraja yangu”
Tuchukulie mtu mmoja mchafu ataamua kufanya mut’a mara mmoja hivi kweli ataweza kupata kama ya Husain?au akafanya mara mara mbili au tatu au nne ataweza kuwa na daraja (cheo) kama Hassan au Ali au Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)?je cheo cha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)na vyeo vya maimamu wetu ni duni kiasi hiki?
Hata kama mtu anaefanya mut’a atakuwa amefikia ngazi ya ya juu katika imani hivi kweli ana weza kufikia cheo cha Husain au Hasan au Ali au Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)?!
Hakika daraja ya Husein ni ya juu
Wameiruhusu mut’a mpaka kwa wanawake wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)
Basi ninasema kuwa jamaa zake mtume ni watukufu hawafanani kufanyiwa kitendo kama hicho (mut’a) kwa sababu wao ni kizazi cha mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)na watu wa nyumbani kwake wanawezaje kufanyiwa kitendo kama hivho, na nitawatajia sababu ya hilo inshaa Allah.
Amebainisha kulainiyi kuwa mut’a inafaa japo kwa tendo moja la ndoa , kati ya mwanaume na mwanamke, na suala hili limeelezewa katika kitabu FURUL-AL-KAFI 10/460.
Na si lazima mtu utakae fanya nae mut’a awe mkubwa bali inawezekana kufanya mut’a na mtoto wa miaka kumi, na kwa kuthibitisha hili, amepokea Al-Kulainiy katika kitabu AL-FURUI juzuu ya 5
Na hoja zote hizi zitapatiwa majibu Mwenyezi Mungu akipenda, lakini ninasema: yote yaliyo nasibishwa kwa Abii Abdillah yanaonyesha kuruhusu mut’a kwa msichana mwenye miaka kumi, lakini baadhi
Alipokuwa imama AL KHOMEINI akiishi Iraq tulikua tunaenda kwake kupata Elimu mpaka ukawa uhusiano wetu na yeye ni mkubwa sana ,na ilitokea siku moja kukubali mwito wa kuutembelea mji TAL-AFAR, (tal-afar ni mji ulio magharibi mwa mji wa AL-MUUSWAL) kiasi cha mwendo wa saa moja na nusu kwa gari, akaniomba nisafiri nae,nikasafiri nae,wakatupokea na wakatukirimu takrima iliyo kubwa kwa muda tuliokuwa kwenye familiya moja ya kishia yenye kukaa huko na walikubaliana kueneza ushia sehemu hiyo,wanaendelea kuzihifadhi picha za ukumbusho tulizo piga nao nyumbani kwao.
Na ulipomalizika muda wa safari tulirudi,na tulipokua tuna rudi tukipitia Baghdadi alitaka imamu tupumzike kutoka na na uchovu wa safari, akaamrisha tuelekee katika mji wa Al-atafiya anapokaa mtu mmoja mwenye asili ya kiirani aitwae Sayid Swahib ambae alikuwa akifahamiana sana na imama Khomeini.
Akafurahi sana Sayid Swahib kwa kuja kwetu,na tulifika kwake wakati wa Adhuhuri,akatuandalia chakula cha fakhari,akawasiliana na jama zake wakahudhuria, na wakajaa katika nyumba ile kwa kutukirimu sisi,na akatutaka Sayid Swahib usiku ule tulale kwake, na akakubali imamu khomeniy hilo, na ilipofika wakati wa isha tuliletewa chakula cha usiku,wakawa walio hudhuria wanaubusu mkono wa imamu, na kumuuliza mas-ala na akiwajibu mas-ala yao, na ulipokaribia wakati wa kulala na waliohudhuria wameshaondoka,isipokua wenye nyumba, imamu KHOMENEI alimuona binti wa umri wa miaka minne au mitano,mzuri sana imamu akamuomba baba yake mtoto (sayd swahib) amlete ili afanye nae mut’a baba yake mtoto akakubali kwa furaha kubwa, basi akalala imamu khomeni na yule msichana akiwa mapajani kwake, huku tukisikia kilio chake na kelele zake!!
Usiku ule ulipita,ilipofika wakati waasubuhi,tulikaa na kunywa chai, akaniangalia imamu khomeniy na akakuta alama ya kulipinga lile jambo waziwazi katika uso wangu,kwasababu vipi atafanya mut’a na mtoto mdogo huyu wakati katika nyumba ile kuna wasichana wakubwa wazuri anaoweza kufanya nao mut’a , kwa nini asifanye nao badala yake afanye na mtoto mdogo ?
Akaniambia: Sayid Husein umesema nini kuhusu kufanya mut’a na mtoto mdogo?nikamwabia : bwana wangu kusema ni kwako, na kitendo chako ndio sahihi , kwa sababu wewe ni imamu mwenye kujitahidi,haiwezekani kwa mtu mfano wangu mimi kuona au kusema isipokua ulivyoona wewe au ulivyosema, (nilisema hivyo kwa sababu wakati huo nisingeweza kupinga chochote)
Akasema: “Sikia Sayid Husein, hakika kufanya mut’a na mtoto mdogo inafaa lakini kwa kucheza nae na kum’busu na kumpitishia dhakari katika mapaja yake, kwa sababu tendo la ndoa haliwezi.
Na alikua Imamu Khomeini akiona inafaa kufanya mut’a mtoto hata ane nyonya, akisema: {si vibaya kustarehe na mtoto anaenyonya kwa kumkumbatia na kuichezesha dhakari kati ya mapaja yake na kum’busu} tazama kitabu chake ATAHRIRU ALWASILA 2/24/ MLANGO, NAMBA 12.
Nilikaa katika ofisi ya imamu ALKHUUIY wakaingia vijana wawili yaonekana kuwa wametufautiana katika mas-ala Fulani waka afikiana kumuuliza imamu AL KHUNIY ili awafahamishe jawabu, akauliza mmoja wao, unasemaje imamu kuhusu mut’a? je ni halali au ni haramu? Akamuangalia imamu AL KHUIY yule kijana huku akiwa amehisi jambo katika swali lake,kisha akamwambia wapi unaishi?akasema yule kijana naishi Al mauswil,lakini sasa hivi niko hapa Annajaaf inapata miezi miwili,imamu akamuuliza yule kijana : je wewe ni Ahlus Sunnah? Akasema kijana ndiyo, imamu akasema: mut’a kwetu sisi (mashia) ni halali lakini kwenu (Ahlus Sunnah) ni haramu,yule kijana akasema mimi nipo hapa yapata miezi miwili nikiwa mgeni katika mji huu,basi utaniozesha binti yako ili ni starehe nae mpaka nitapo rudi kwetu? imamu akanyamaza kidogo kisha akamwambia: mimi ni mtukufu na hili jambo ni haramu kwa watukufu,na ni halali kwa mashia wa kawaida
Kijana akamwaangalia Asayid AL KHUUIY huku akitabasamu na mtazamo wake unaonyesha kuwa kijana kafahamu kwamba imamu Al Khuuiy ametumia taqiya kisha wakasimama na kuondoka, nikamtaka rukhsa imamu Al Khuuiy ya kutoka, nikakutana na wale vijana wawili,nikaelewa kuwa mwenye kuuliza ni Ahlu sunna na mwenzake ni shia wametofautiana juu ya mut’a je ni halali au haramu? Wakaafikiana juu ya kuuliza marejeo ya dini ya Al imamu Al khuuiy,nilipo wazungumzisha vijana wawili hao, yule wa kishia alipandisha hasira na kusema: Enyi watu waovu,mnaruhusu kustarehe na wasichana wetu, na mnatueleza kua ni halali na inawakurubisha,kwa Mwenyezi Mungu na mnatuharamisha kustarehe na mabinti zenu? yule kijana akaondoka na huku akitukana na kushutumu na akiapa kuingia katika madhehebu ya Ahlus Sunnah, nikawa namtuliza yule kijana na kumuapia kwa mungu kuwa mut’a ni haramu na nikampa ushahidi wa hilo.
Hakika mut’a ilikua inafaa zama za ujinga, uislamu ulipo kuja uliibakisha mut’a kwa muda,kisha ikaharamishwa katika vita vya Khaibara, lakini lililozoeleka kwa mashia na wasomi wao ni kwamba ‘Umar bin Khatwaab ndie aliye iharamisha, na haya ndiyo yaliyoelezwa na baadhi ya wanazuoni wetu.
Na ukweli ni kwamba mut’a iliharimishwa katika vita vya khaybar.
Amesema Amirul Muuminin (‘Alayhi salaam): {aliharamisha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) siku ya khaybar kula nyama ya punda wakufugwa na ndoa ya mut’a} tazama (ATTAHDHB 2/186) (AL-ISTIBAR 3/142), (WASAILU
Na akaulizwa Abuu Abdillah (‘Alayhis salaam): {Je walikuwa waislamu katika zama za mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) wakiona bila ya kutangaza? Akasema: hapana} (tazama ATTAHDHIYB 2/189).
Amesema At Tuusiy akifafanua maneno hayo; hakika Abu Abdillahi hakukusudia kwa maneno yake hayo ndoa ya kudumu isipokuwa alikusudia mut’a ndio maana ameyaleta maelezo haya katika mlango unaohusu mut’a .
Hakuna shaka kwamba hoja mbili hizi ni zenye kuifuta mut’a na kuibatilisha. Amiril-muuminin (‘Alayhis Salaam) ameelezea kuharamishwa mut’a kutoka kwa mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na hii ina maana kuwa Amirul muuminin (‘Alayhis Salaam) amesema kwamba mut’a iliharamishwa tokea siku ya khaibara na bila shaka viongozi wengine baada yake walijua hukumu ya mut’a baada ya kuja kwao kuwa imeharamishwa . Na hapa tuko mbele ya habari aina mbili : zilizo pokewa zinazoeleza waziwazi kuhusu uharamu wa mut’a ,Na zile zinazo nasibishwa kwa maimamu zinazo himiza kufanya mut’a, Na hili ni tatizo muislamu anachanganyikiwa afanye mut’a au asifanye?
Usawa ni kuacha mut’a kwasababu ni haramu kama zilivyothibiti habari zake kutoka kwa Amirul muuminin (‘Alayhis Salaam) ama maelezo yaliyo nasibishwa kwa maimamu bila shaka si sahihi, bali ni habari za uzushi wamesingiziwa maimamu, (‘Alayhis Salaam) kwani hawawezi kwenda kinyume na jambo alilo liharamisha mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam),na Amiril-muminina akawa na msimamo huohuo baada ya mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ukizingatia wao ndio walio chukua elemu kutoka kwa mababu na mababu kwa sababu wao ni familia moja,
Alipoulizwa Abuu Abdillah (‘Alayhis Salaam): (Je walikuwa waislamu katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) wakioa bila ya kutangaza? Akasema:hapana, haikua hivyo)kama asingekua anajua kuwa mut’a ni haramu asingejibu kwa kusema hapana, hasa ukizingatia swali liliulizwa kuhusu mut’a na kwamba Abu Jaafar alieipokea habari hii ameika katika mlango wa mut’a kama tulivuo sema.
Na haikuwa inawezekana kwa Abii Abdillah (‘Alayhis Salaam) wala maimamu walikuwa kabla yake na baada yake kwenda kinyume na amri ya mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) au kuuhalalisha jambo aliloharamisha au kuzua jambo lisilo julikana katika zama zake (‘Alayhis Salaam).
Kwa hayo inakua wazi kuwa habari zilizokuja kuhimiza mut’a si maneno ya maimamu, isipokuwa nimaneno yaliyosemwa na watu kisha wakawasingizia maimamu kwa kutaka kuwatusi AHLUL-BAYT,na kuwakosea adabu , na kama si hivyo itatafsiriwaje kuhalalisha kwao kufanya mut’a na familia ya Mtume na kuwaita makafiri wasiofanya mut’a?
Pamoja na kuwa maimamu wote (‘Alayhis Salaam) haikupatikana habari sahihi kuwa mmoja wao, aliwahi kufanya mut’a wala kuihalalisha mut’a, je watakua wameishi katika dini isiyo kuwa ya kiislamu?
Likiwa wazi kwetu
Kulainy amepokea kutoka kwa Abii Abdillahi (‘Alayhis Salaam) kwamba mwanamke mmoja alikuja kwa Omar ibn Khatab akasema :hakika mimi nimezini akaamrisha kupingwa mawe,akaelezewa Amirul-muumini (‘Alayhis Salaam) akamuuliza: vipi umezini? Akasema: nilipita kijijini ikanipata kiu kali
Hakika ya mut’a kama inavyojulikana inakuwa kwa kuridhiana pande mbili na kuwa na hamu baina yao, ama katika upokezi huu mwanamke aliyetajwa alikuwa na shida, mwenye kulazimishwa,akajitolea nafsi yake ili apate kunywa maji, hii haichukuliwi ni zinaa kwa hiyo kulikuwa hakuna haja ya kutaka kutwaharishwa na ‘Umar , zaidi ya hayo -ni muhimu kuzingatia - kuwa Amirul muuminin ndie ambae amepokea uharamu wa mut’a kwa kunakili toka kwa mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) katika vita vya Khaybar,vipi atatoa fatwa hapa kuwa hii ni ndoa ya mut’a?! Na fatwa yake inaonyesha kuhalalisha kukubali na kuridhika kwa kitendo cha mme na mke?!
Hakika fatwa hii lau angalisema mmoja wa wanafunzi ingehesabiwa kwake ni kosa ambalo anstahiki lawama juu yake basi iweje kosa hili linasibishwe na Amiril-muminin (‘Alayhis Salaam)ambae anafahamika ni nani katika elimu na fatwa?
Hakika yule aliyeinasibisha fatwa hii kwa Amirul muuminina ama ni mwenye chuki anayetaka kumtukana, au ni mwenye lengo jengine kwa hiyo akazusha kisa hiki na kukinasbisha kwa Amirul-muminin ili aifanye mut’a iruhusike kisheria ili yeye na wenzake kama yeye waweze kujihalalisha zinaa kwa jina la dini, hata kwa gharama ya kuwasingizia maimamu bali hata kumsingizia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam).
Na hakika uharibifu unaopatikana katika ndoa ya mut’a ni makubwa kwa pande tofauti:
Hakika ya khumusu ni kitu kingine kilichotumika vibaya na wanazuoni na mujtahidina(wakishia),ikawa ni njia ya kuwaingizia mabwana wakubwa ikawa inawaingizia mali nyingi sana.
Ingawa maelezo ya kisheria yanaonyesha kwa mashia wa kawaida hawalazimishwi khumusu. Bali ni nkhiari yao kufanya hivyo , ispokuwa wao wanaruhusiwa kuitumia khumsi kama wanavyo tumia mali zao, Bali anazingatiwa yule anayetoa khumus kuwapa mabwana wakubwa kuwa anapata madhambi kwa anapingana na maelezo ya Amiril muuminin na viongozi wa Ahlul Bayt (Alayhim Salaam).
Na ili aufahamu vizuri msomaji uhakika wa khumus na jinsi ya kutumika kwake tutaielezea maudhui ya khumus na kushamiri kwake katika historia, na tutayatia nguvu maneno yetu hayo kwa maelezo ya kisheria na maneni ya maimamu na fat’wa za wanazuoni wanaotegemewa na kukubalika maneno yao.
[8:41](واعلموا أنما غنمتم من شيئ فإن لله خمسه وللرسول ولذي القربى) الأنفال 41
{Na jueni ya kwamba chochote mnachokiteka( mnacho kipata ngawira) , basi sehemu yake ya tano ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume na jamaa zake Mtume} (Al Anfal 41). Akasema Abuu Abdillah(Alayhis Salaam) kwa kueka mikono yake juu ya magoti yake,kisha akaashiria kwa mikono yake akasema {hivyo na apaa kwa Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) nifaida inayopatikana siku hadi siku, isipokua baba yangu amejaalia shia wake kuwahalalishia ili wajitakase}(Al Kaafi 2/499)
Basi riwaya hizi na nyinginezo nyingi ziko wazi katika kuwasamehe mashia khumus kwani wao wameruhusiwa wasitowe basi anayetaka kuitumia yeye mwenyewe,au kuila wala asiwape Ahlul Bayt chochote basi hiyo ni halali yake kufanya atakavyo na wala hakuna dhambi juu yake, bali pia haiwapaswi wao kutoa mpaka atakapo kuja mahdi anaesuniriwa, kama ilivyopokewa katika riwaya ya tatu.
Na hatakama angekuwepo Imamu (kiongozi wa kishia) asingepewa mpaka asimame kiongozi wa Ahlu Bayt, basi itawezekana vipi kupewa wanazuoni na mafaqihi?
Fatwa za mafaqih na wanazuoni wanao tegemewa katika kuwazuia mashia kutowa khumusi.
Kufuatana na hoja zilizo tangulia na nyinginezo nyingi zilizoweka wazi kusamehewa mashia kutowa kuhums zilitolewa fatwa nyingi kutoka kwa wanazuoni wakubwa na mujtahidin miongoni mwa wale wenye upeo mkubwa wa elimu na ambao wana nafasi kubwa kati ya wanazuoni wetu, zinazo halalisha khumsi kwa mashia na kutompa mtu yoyote mpaka atakapo kuja kiongozi wa Ahlul Bayt:
Ninasema: neno
(واعلموا أنما غنمتم من شيئ)
{Na jueni ya kwamba chochote mlicho kipata kitika ngawira}Al anfal:41. kisha akabainisha kuwa kuna riwaya nyingine kutoka kwa Al-Mahdiy akisema mashia tumewahalalishia khumus.
Kama hivyo tunaona ya kwamba kauli ya kuhalalisha khumus kwa mashia,na kuwasamehe wao kutowa kauli hiyo ndio inayojulikana kwa wanazuoni wote wazamani na wa sasa na ndio kauli iliyofanyiwa kazi mpaka mwanzo wa karne ya kumi na nne, achilia mbali kuwa ndiyo yenye ushahidi wa uhalali wake, ,basi itawezekana vipi na ili hali ni hii kutowa khumsi na kuwapa wanazuoni? Pamoja na kuwa maimamu (Alayhis Salaam) waliikataa khumus na wakairudisha kwa wenyewe na wakawasamehe kutowa hiyo khumusi, je inawezekana kuwa wanazuoni ni bora kuliko maimamu (Alayhis Salaam)?
Hakika fat’wa za kuhalalisha khumus kuwapa mashia haiishii kwa hawa tulio wataja peke yao miongoni mwa wanazuoni bali pia kuna zaidi ya idadi hii tulio itaja na kwa kupita karne hizi, lakini tumechagua katika kila karne moja katika mafaqihi na wanaosema kwamba si halali kuwalazimisha watu kutowa khumsi, na kauli hii ndiyo waliyo isema wanazuoni wengi kwa nyakati tofauti kwani ndio kauli inayo tegemewa katika mas’ala haya,na kwa sababu ya kukubaliana kwake na maelezo ya kisheria na vitendo vya maimamu (Alayhis Salaam).
Na tutachukua fatwa mbili za wanazuoni wawili miongoni mwa wanazuoni wa kishia nao ni: sheikh Al mufidu na sheikh Al Tuusiy,amesema sheikh Al mufid: wamekhitalifiana watu miongoni mwetu kwa hilo yaani khumus wakati wa ghaibah kila kundi na msimamo wake ( kisha anataja idadi ya kauli hizo) miongoni mwa wanazuoni kuna wano iondosha kauli ya kutowa khumsi wakati wa ghaiba na kwa sababu ya hojjah zilizo tangulia , na wengine kuna wanaolazimisha izikwe na wanaitafsiri iliyo pokewa isemayo: ( hakika ardhi itatoa hazina zake wakati atapo dhihiri Al imamu na kua yeye (Alayhis Salaam) atapo simama, Mwenyezi Mungu atamjulisha hazina zake na atazichukua kutoka kila sehemu)
Kisha akachagua kauli moja katika hizo.
Kuindosha khumus kwa mwenye mamlaka yaani Al Mahdiy, ikiwa ana wasiwasi wa kufikwa na umauti kabla ya kuja kwake atamuusia anae muamini katika akili yake na dini yake,kwa sharti hili mpaka aje amkabidhi imamu, akikuwahi kuja kwake asipowahi atamuusia mtu atakaye isimamia mwenye sifa kama zake kwa uaminifu na dini kisha wataendelea kuusiana kwa kufuata sharti hili mpaka atakapo kuja imamu, na kauli hii kwangu iko wazi zaidi kuliko zote zilizotazngulia, kwa sababu khumusi ni haki ya imamu aliyejificha na hayakutuka maelekezo yoyote kabla ya kujificha kwake ambayo yanaweza kufuatwa.
Kisha akasema na khumsi inakwenda kama vile zakka ambayo hutolewa pale anapopatikana anaye stahiki kwa hiyo haipasi kuanguka wakati huo , kisha akasema atakapo fuata mtu msimamo huo tulio utaja wa kwamba nusu ya khumsi ni fungu la imamu kisha akaifanya nusu nyingine ni kwa ajili ya familia ya Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) wasafiri wao masikini wao kama ilivyo kuja katika Qur-an.
Amesema atakaye fanya hivi hayupo mbali na kuipata haki katika
Na amesema Al sheikh Al Tuusiy aliyefariki (460H) ambae ni muasisi wa chuo cha kishia cha Al Najaf na ndiye kiongozi wake wa kwanza baada ya kutaja hukumu za khumus akasema: hii itakuwa katika muda atakao kuja imamu, kisha akasema: ama katika hali ya kutokuwepo wamewaruhusu mashia wao kufanya katika haki zao ndoa, biashara na makazi... ama isiyo kuwa hayo haifai mtu kujifanyia atakavyo kwa hali yoyote ama kile wanacho stahiki katika khumusi zilizo hifadhiwa wakati wa ghaiba, wamekhitalifiana watu wetu kwa hilo na hakuna hoja maalum isipokuwa kila mmoja kati yao mafaqihi wa shia amesema usemi wa kuondowa shaka .
Kisha Al Tuusiy akazidhibiti hoja hizi katika sehemu nne:
Na mafungu matatu mengine yatagawanywa kwa wanao stahiki miongoni mwa mayatima wa familia ya Mohammad na masikini wao na wakatikiwa na njia wao, na haya ni miongoni mwa yanayotakiwa kufanyiwa kazi, na kauli hii inalingana na fat’wa ya mufidu katika kuifananisha khumusi na zaka.
Kisha anasema (na lau wangekuwa watu ni mwenye kutumia njia ya kutoa wasiwasi kwa kuifanyia kazi njia mojawapo kati ya hizi zilizotajwa asinge pata madhambi).
Sheikh Al-Tuusiy ameyadhibiti matumizi ya khumusi katika kauli nne hizi zilizotangulia, na yeye mwenyewe amechaguwa kauli ya nne , lakini akaweka wazi kuwa mtu akichagua kauli yoyote kati ya hizi hana madhambi.
Nasi tunaziona kauli hizi nne, ingawa zimekhitalifiana katika baadhi ya maelezo lakini tunaziona zimekubaliana katika kitu kimoja, ambacho ndicho tunachokielezea , nacho ni kwamba
Na pamoja nakuwa kauli nne hizi zilizotangulia zimekhitalafiana katika namna ya ugawaji wa
Hakika kauli ya nne ambayo ndiyo aliyo ichagua Al shaikh al tuusiy ndiyo waliyokuwa nayo mashia wote , na Al Tuusiy. Kama inavyofahamika ndiye muasisi wa chuo cha kishia cha Annajaf nae ndie sheikh wa kikundi, je hivi unadhani sheikh huyu na mashia wote wa zama zake na wa nyuma yake walikuwa wanakosea .
Basi hii ndiyo fatwa ya kiongozi wa kwanza wa chuo cha Annajaf.
Basi sasa tuone fatwa nyingine ya kiongozi mwingine wa chuo hicho maulana al imamu aliyeaga dunia Abil- Qasim Al khuuiy ili itupambanukie tofauti iliyopo kati ya fatwa ya kiongozi wa kwanza wa chuo hiki na fat’wa ya kiongozi mwengine wa chuo hicho hicho.
Amesema al imamu al khuuiy katika kubainisha anayestahiki kupewa khumus.
Khumus katika zama zetu hugawanywa katika sehemu mbili: nusu ni kwajili ya imamu wa zama hizi Al Hujatu Al Muntadhir mwenyezimungu azifanye fidia roho zetu kwake . Na nusu ni kwa ajili ya banii Hashimu Mayatima wa na masikini wao na walio katikiwa na njia… mpaka aliposema: nusu ambayo inatolewa kwa imamu (Alayhis Salaam) inarejea katika zama za kujificha kwa naibu wake nae ni Al faqihi mwanazuoni mwenye kuaminika anae jua matumizi yake,ima kwa kumpa au kumuomba ruhusa… Angalia kitabu (Dhiyau Al Salihina Mas’ala 1259, Uk: 347) hakika fatwa ya imamu Al khuuiy ina khitalifiana na fatwa ya Al sheikh Al Tuusiy, sheikh Atuusiy hakusema khumus apewe mwanazuoni, na wamefuata maelezo ya fatwa yake mashia wote wa zama zake,ili hali tunaona fatwa ya maulana aliyefariki Al imamu Al khuuiy inatoa hoja ya kuitoa khumus au sehemu yake kupewa faqih na mujatahidin (wanazuoni).
KAULI YA KWANZA: baada ya kukatika mfululizo wa maimamu na kupotea kwa imamu mahdi ni kuwa khumus ni haki ya imamu asiye kuwepo,na wala si ya fakihi wala mtukufu yoyote na wala ya mujtahidina na kwa haya basi wengi wanadai zaidi ya watu ishirini kuwa wao ni manaibu wa imamu aliyejificha kwa ajili ya kuchukua khumus na wakasema: sisi tunakutana nae imamu aliye jificha, tunaweza kumpa khums zote za vitega uchumi ambazo zina tujia.
Na lilikua hili katika nyakati za ghaiba ndogo (kujificha kudogo) na ikaendelea baada yake muda wa karne moja au mbili kipindi chote hicho haikutolewa khumus kupewa mujtahidin au mtukufu yoyote na katika kipindi hiki vilionekana vitabu vine maarufu kwa jina la Assihahil-arbaai, na vyote hivi vimenakili kutoka kwa viongozi habari ya kuhalalisha khumus kupewa mashia na kuwaondolea mzigo wa kutowa ,,na hapa kuwepo na fatwa yeyote inayoruhusu kuwapa khumus watukufu na mujtahidina.
KAULI YA PILI: kisha likashamiri jambo la khumusi baada yakuwa mashia wameruhusiwa kutotowa khumsi wakati wa ghaiba , ikapatikana habari ya ulazima wa kutowa khumsi , ikiwa watu wenye mali wanataka kujiepusha na kauli ya kwanza , wakawa wanatakiwa kuitowa khumusi ili izikwe mpaka atakapotoka Al-mahdi.
KAULI YA TATU: kisha likaendelea jambo la khumusi wakasema ni wajibu kuiweka kwa mtu muaminifu ,na walio bora kuchaguliwa kubeba amana hii ni wanazuoni wa madhehebu ya kishia, lakini inafaa kusisitiza kuwa uchaguzi huu ni bora tu na wala si lazima , na huyo mwanazuoni akipewa khumusi si ruhusa kuitumia bali kuiweka mpaka hapo atakapoifikisha kwa imamu Al-mahdi.
Na hapa kuna dokezo muhimu nalo ni kwamba ni nani kati ya wanazuoni wetu aliyehifadhi mali zilizoletwa kwake ,kisha baada ya kufa kwake wakasema warithi wake kuna mali zilizo wekwa amana kwa baba yetu ambazo sasa hivi zinapaswa kuwekwa kwa mtu anayechukuwa nafasi yake?
Bila shaka jawabu sahihi hapa ni kuwa :hakujapatikana mtu wa aina hii , wala hatujasikia wala kusoma habari za mtu kama huyu , ambae mali za watu (khumusi) zilikuwa kwake kisha baada ya kufa kwake zikahamia kwa aliye kuja baada yake.
Na sahihi ni kwamba : kila aliyekewa amana ya mali wamekuja warithi wake nakugawana mali hiyo wakidai kua ni yao walirithi kutoka kwa baba zao ,kwahiyo khumusi ya imamu imekwenda kwa warithi wa mwanazuoni muaminifu , hali hii inajitokeza pale anapokuwa mwanazuoni huyo ni muaminifu na ile mali hakujifanya kuwa ni yake , je akiwa si muaminifu hali itakuaje?!!!
Na inafaa kukumbuka zaidi kuwa Qadhi ibn Bahraji au Baraji ndi aliyeliendeleza jambo la khumusi kutoka kwenye sunna na kufikia wajibu , kwa hiyo ndiye aliyekuwa wa kwanza kusema ni dharura kuiweka shea ya imamu kwa anayeaminika miongoni mwa mafakihi na mujtahidina ili waikabidhi kwa imamu aliejificha ikiwa watamkuta au ausiwe anaeaminika miongoni atakayekuja baada yake ili aikabidhi kwa imamu. Na hili limeelezwa katika kitabu (AL-MUHADHAB 8/80) na hatua hii ni muhimu sana.
KAULI YA NNE: kisha wakaja maulamaa wa mwishoni mwishoni, wa kayaendeleza mas-ala ya khumsi kidogo kidogo mpaka iakafikia kusema kuwa niwajibu kutolewa khumsi kupewa maulamaa wazigawanye kwa wanao stahiki miongoni mwa mayatima na masikini wa ahlulu Bait,na habari yenye nguvu ni kuwa fakihi bin Hamza ndie wa kwanza aliyevutika na kauli hii katika karne ya sita kama alivyotoa ushahidi katika kaitabu cha(Al-Wasilatu Fii Nayli Al – Fadhilat uk:182) na akaliona hil;I la kuitowa khumsi kumpa mwanazuoni ni bora kuliko kusimama mwenye khumus na kuigawa mwenyewe khasa ,ikiwa hajui kuigawa vizuri.
KAULI YA TANO: yakaendelea mageuzi kidogo kidogo katika zama hizi na imekua kabla ya karne moja mpaka ukafikia uamuzi wa mwisho,baadhi ya mafuqahi wakasema kuwa inaruhusiwa kutumia shea ya imamu katika baadhi ya mambo ambayo anayaona mwanazuoni kuwa ni muhimu kama kuwasaidia wanafunzi , na kusimamisha vituo vya dini, na mengeniyo kama alivyotoa fatwa Asayiud Muhsin Al Hakim katika Mustamsik( AL-Urwatu Al Uthqa 9/584).
Kauli hii inaambatana na kauli ya kwamba hapana haja ya kurudi kwa mwanazuoni kutaka ushauri katika kuitumia sehemu ya imamu katika khumsi
Na hii maana yake ni kuwa kule kutumia shea ya imamu katika khumusi ni jambo lililojitokeza katika zama hizi za mwishoni sana basi wao wanaiangalia hali yao ilivyo na kuona mashule yao ,na vituo vyao uchapishaji na vitu vinavyo hitajika ni katika mambo yanayo faa kutolewa khumsi kwa ajili yake.
Na vilevile wanaziangalia haja zao binafsi, basi vipi itawezekana kukidhi haja zote hizi , hasa ukizingatia kuwa mambo yote haya yanahitaji pesa nyingi .
Ukawa mtazamo wao kwa khumusi njia nzuri ya kuwaingizia kiasi kitakacho kidhi haja zao zote na itakayowahakikishia manufaa yao binafsi na kuwapa utajiri kubwa sana kama tunavyoona leo hali ya wanazuoni ilivyo.
Hakika kadhia ya khumsi imepitia duru nyingi na mabadiliko mengi mpaka mwisho ikatulia kuwa ni wajibu kuwapa khumus za vitega uchumi mafakihi na mujtahidina (wanazuoni). Na kwa haya yanatubainishia sisi kua khumus haina hoja katika kitabu(Qur-ani) wala Sunnah wala kauli ya imamu bali hiyo ni kauli iliyodhihiri katika zama za mwishoni,wameisema baadhi ya mujtahidina, nayo ni yenye kupingana na Qur-an na sunnah na viongozi wa ahlul Bait na maneno ya wanazuoni na fatwa za mafakih na mujtahidina na wenye kutegemewa.
Nami na nawaomba ndugu zangu na wanangu mashia wajizuie kutoa khumus za vitega uchumi vyao na faida zao kwa watukufu wa mujtahidina,kwa sababu hiyo ni halali yao na wala si haki ya bwana mkubwa yoyote au mwanazuoni yoyote, Na wenye kutoa khumus kwa mwanazuoni au bwanamkubwa yoyote basi ajuwe ameingia katika madhambi kwa sababu ya kupingana na maneno ya maimamu kwa sababu khumsi si wajibu kwa mashia mpaka atakaporudi imamu mahdi .
Na ninaona muhimu kautaja usemi wa Ayatulah Al Udhmaa Al Imamu A Khomeiniyu katika mas-ala haya, kwani alizungumza kuhusu khumusi katika mihadhara aliyoitowa tukimsikia sote katika chuo cha cha Najaf mwaka [1389 H]Kisha akakusanya katika kitabu Al-Hukumatul Al Islamiya au Walayatul Al Faqih: miongoni mwa aliyokuwa ameyasema: tutakuwa tuna uoni mfupi tukisema kwamba khumusi imeletwa kwa ajili kulinda maisha ya watoto wa mtume (s.a.w) peke yao.
Akendelea kusema kuwa inawatosha wao na kubaki sehemu ndogo tu ya maelfu ya mali yote ya khumusi bali wanatoshwa na khumsi ya soko moja tu kama vile soko la Iraki kwa mfano miongoni mwa masoko mengi makubwa kama vile masoko ya Irani Sirya na Islama bad na mfano wa hayo , sasa mali inayo baki itakuwaje?
Kisha akasema : hakika mimi ninaona hukumu ya kiislamu ya uadilifu, haitaki kufanyiwa takhlifi kubwa katika mambo ya upuuzi au kinyume na maslahi ya wote.
Kisha anasema: haikuwa kodi ya khumus ni kwa ajili ya kudhamini maisha ya mabwana wakubwa katika familia ya mtume (s.a.w) tu wala zaka si kwa ajili kwatenganisha mafakiri na masikini isipokuwa khumsi na zaka zinakuwa zaidi ya hajja za hao waliotajwa ,
Basi je baada ya hayo uislamu utaacha kuzuia kitendo hicho cha khumus na zaka na yanayo fanana na mtazamo wa kuizibia haja watukufu na masikini au itakuwa marejeo yao zaidi chakula cha bahari au kuzikwa chini au mfano wake?.
Walikuwa watukufu wengi miongoni mwa wanao ruhusu kupata ruzuku katika khumus siku hizo,yaani mwanzo mwanzoni mwa uislamu, hawavuki mia moja na lau tungekisia idadi yao kuwa ni nusu milioni,je ingekuwa inaingia akilini kuwa uislamu unajishughulisha kwa kufaradhisha khumsi ambayo ni mali nyingi sana na zinazidi siku hadi siku yote hayo kwa ajili ya kushibisha familia ya mtume (s.a.w).
Yote hayo angalia kitabu chake kilichotajwa,[1/39-40-42] chapa ya Al Adab Annajaf.
Hakika imamu Al Khomeniyu anaweka wazi kuwa mali ya khumus ni nyingi sana,hii ilikua wakati huo pindi alipo kuwa ni muhadhiri wa chuo cha najaf basi je ni wingi wa mali ulioje ukizingatia katika zama zetu hizi?.
Na imamau pia ameweka wazi kua sehemu moja katika maelfu ya sehemu ya mali hii kubwa inatosha kwa Ahlul, Bait wa Mtume(a.s.w) na ahli zake, basi je wataifanyeje sehemu kubwa ya mali iliyo bakia?. Imamu khomeni ana maana kwamba ni lazima kuzigawa mali hizi zinazo baki kwa mafakih na mujtahidina (wanazuoni) kutokana na ufahamu wa usemi wa imamu Al Khomeniy.
Kwa sababu hii imamu khomeni alikua na utajiri mkubwa sana alivyokuwa akiishi Iraqi na alipotaka kusafiri kwenda ufaransa kwa kuishi huko alizigeuza pesa zake kutoka dinari za Iraqi kuziweka kwenye dola za kimarekani na akazihifadhi katika mabenki ya ufaransa na kupata riba kubwa sana.
Hakika uharibifu wa mtu unakuja kwa njia mbili :- kwa njia ya kijinsia na mali na vyote hivyo vinapatikana kwa watukufu, upande wa kijinsia wanaupata kwa njia ya mut’a na isiyokuwa mut’a , mali wanazipata kwa njia ya khumusi na zile zinazotupwa makaburini , ni nani kati yao atakayeweza kupambana na vishawishi hivi , ukizingatia wengi wao wameifuata njia hii kwa ajili ya kushibisha matamanio yao ya ngono na mali ?!!
Bila shaka wislamu wote wanaamini kuwa Qur-ani ni kitabu cha mbinguni kilicho teremswa kutoka kwa Allah kuja kwa nabii wake Muhammad bin Abdillah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam).
Lakini nilipatwa na mshangao mkubwa sana baada ya kusoma kwangu na kuvipitia vitabu vyetu vya kishia ambavyo ndivyo vinavyo tegemewa kama marejeo yanayotegemewa, nilikuta majina ya vitabu vingine ambavyo vinazingatiwa kwa itikadi ya kishia kuwa navyo ni vitabu vitukufu ,na wana zuoni wetu wakubwa wa kishia wanadai kwamba vitabu hivyo pia viliteremshwa kwa mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ikiwa ni pamoja na Qur-an, na vitabu hivyo alibaki navyo Amiril-muuminina Ali bin Abi talib.
Wala hakuvibainisha kwa watu yeye Ali wala mtume na huu ni uzushi wa mashia wanaomzushia Ali.
Na vitabu vyenyewe ni hivi:
1-ALJAAMIA (Mkusanyiko wa elimu)
Imepokewa kutoka kwa Abi buswair kutoka kwa Abii Abdallah alisema: mimi na Muhammad, sisi tuna kitabu kinachoitwa Aljaamia, je, ni jambo gani litakalowafahamisha wao ni nini hiyo Aljaamia? Akasema kumuambia mtume nimejitowa muhanga kwa ajili yako , nifahamishe ni nini hiyo Aljaamia? Akasema ni sahifa kitabu chenye urefu dhiraa sabini kwa dhiraa za mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na kitabu hiki ni maneno yatokayo mdomoni mwa mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)na kuandikwa na Ali bin Abitalib kwa mkono wake, ndani ya kitabu hicho kumebainishwa halali na haramu na kila kitu wanacho kihitajia watu katika maisha yao ya kila siku, hata wadudu walio chini ya ardhi. kwa kuthibisha hayo angalia: Al-Kaafi juzuu ya kwanza uk. 239, na Bihaarul Anwaar juzuu ya 26 uk. 22.
Na kuna riwaya nyingi sana zinazoeleza habari hizi kwa uwazi zaidi na utazipata katika vitabu vifuatavyo:
1.
AL-KAAFI
2.
AL-BIHAAR
3.
BASWAIRU-ADDARAJAAT
4.
WASAAILU-SHIA
Hakika sisi tumefupisha habari hizi kwa kuwaleteeni riwaya moja kwa ajili ya kufupisha.
Mimi mpaka leo sifahamu wala sina uhakika iwapo kitabu hiki (AL-JAAMIA) kina ukweli wowote ule ama vipi jambo hilo bado limo nje ya fahamu zangu.na sijui kama ni kweli kwamba kitabu hicho kuna kila kitu ambacho wanakihitaji watu mpaka siku ya Qimaya?ikiwa ni kweli basi ni kwa mimi kimefishwa? Na tukanyimwa sisi tusikipate ni hali ya kuwa kitabu hicho kimebainisha kila jambo la halali na haramu pamoja na hukumu zote mpaka siku ya Qiyama,Je huku sikuficha elimu?hali ya kuwa kuficha elimu ni mambo yaliyo katazwa.Je kufanya hivyo sikatika kuficha elimu?jambo ambalo ni kinyume cha dini?!
2. SAHIFA YA AN-NAMUUSI.
Imepokewa kutoka kwa AL-RIDHAA (Alayhis Salaam) katika hadithi inayosimulia alama za imamu.Alisema-na Sahifa itakayo kuwa kwa imamu atakua na majina ya kishia(wafuasi) wao wote mpaka siku ya kiama.Na sahifa hiyo hiyo itakuwa imeandikwa na majina ya maadui zao wote mpaka siku ya kiyama.
Kwa ufafanuzi zaidi angalia:
1.
BIHAAR AL AN-WAAR Juzuu-25 Uk.117
2.
BIHAAR AL AN-WAAR Juzuu-26 Uk.117
Na utakuta riwaya nyingi zaidi.
Na mimi nikawa najiuliza uliza, ni kitabu cha aina gani hicho ambacho kinaweza kuandikwa majina ya mashia wote mpaka siku ya kiyama!!!!. Na lau tungeweza kuya sajili majina ya washia wa IRAQ peke yake basi ingetulazimu kuhitaji volume mia moja kwa uchache.na ingekuaje kama tungesajili majina ya mashia wa IRAN na BARA HINDI na mashia wa PAKISTAN, SYRIA na LEBANON na DOLA ZA BARA ARABU na nchi nyinginezo? Bali tungelihitaji mijalada mengi kama tungesajili majina ya watu waliokuisha kufa karne kwa karne zilizopita mpaka kudhihiri (kujitokeza) ushia mpaka zama hizi (wakati huu).
Na tungalihitaji vitabu vingapi vya kusajili majina ya mashia wetu katika karne zijazo mpaka siku ya kiyama? na tungalihitaji vitabu vingapi vya kusajili majina ya mahasimu wao kuanzia kudhihiri hiyo sahifa AN-NAMUUS hadi siku ya Qiyama. Lau hata kama bahari ingalikuwa ni wino wa kuandikia majina hayo na nyuma yake kukawa kuna bahari nyingine saba,basi wino wa bahari hizo usingeweza kutosha kuandikia majina hayo.
Na hatakama tungeweza kuzikusanya Computer zote za duniani pamoja na akili zote za ELECTRONI za kisasa vyote hivyo visingeweza kuhifadhi na kudhibiti majina hayo kutokana na wingi wake. Hata wale wajinga wasiokuwa na elimu,Akili zao haziwezi kukubali riwaya hizi (habari hizi) na mfano wake iweje watu wenye elimu na akili timamu wawe wajinga kiasi hiki?!
Hakika ni muhali mno na jambo lisilowezekana kwa maimamu watukufu kusema mfano wa maneno haya ya kipuuzi na uwenda wazimu,kwani jambo hili halikubaliki kiakili na kimantik. Na lau kama maaduii zetu wangeweza kugundua riwaya hii wangesema wanavyotaka juu ya Uislamu wangeitusi dini ya kiislamu.na wangeweza kuusingizia Uislamu wanavyopenda.
3. SAHIFA YA AL-UBAYTAN
Imepokewa kutoka kwa Amir-al muuminin (Alayhis Salaam) amesema,Ninaapa kwa jina la Allah, hakika mimi ninazo sahifa nyingi ambazo zimetoka kwa Mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam).na kuna ndani ya sahifa hizo,sahifa inayoitwa (AL-UBAYTAN) na sahifa hiyo ina habari mbaya sana zinazo husu waarabu. Na mna habari za makabila sitini ya kiarabu ambayo yameangamizwa wala hayana fungu lolote katika dini (yaani ni makafiri) Angalia BIHAAR AL ANWAR- Juzuu 26 Uk.27.
Hakika riwaya hizi hazikubaliki wala haziingii akilini, iwapo idadi yote hii ya makabila itakuwa haina chembe ya dini mbele ya Allah,kwa maana hiyo ni kwamba hakupatikana hata muislamu mmoja ambaye atakuwa ana dini mbele ya Allah. Halafu kuhusisha haya makabila kiaarabu kwa hukumu hii mbaya hapa inapatikana harufu ya ubaguzi wa kitaifa. Na ufafanuzi zaidi utakuja katika mlango unaokuja
4. SAHIFA YA DHUABA AL-SAAIF.
Imepokewa kutoka kwa Abi Buswaira kutoka kwa Abi Abdillah(Alayhis Salaam),anasema kwamba kulikuwa kwa Dhuaba SAIF RASSULI kuna sahifa ndogo ndani ya sahfa hiyo kuna herufi nyingi na kila herufi moja katika herufi hizo hufunguliwa kwa herufi elfu moja.. na amesema Abu Buswaira , alisema Abu Abdillah na hazikutoka katika herufi hizo elfu moja ila herufi mbili tu,na itabaki hivyo hadi siku ya Qiyama. Angalia BIHARU AL- ANWAR Juzuu26 Uk: 56.
Mimi ni kasema na kujiuliza, na hizo herufi nyingine zilizobaki ziko wapi? Na kwa nini zisitolewe iliwafaidi mashia wa Ahlul Bayt?,kwa herufi hizo? Au zitabaki kuendelea kufichwa mpaka hapo atakapo simama AL QAIMU (Mahd).
5. SAHIFA YA ALI NAYO NI SAHIFA NYINGINE ILIYOPATIKANA KWA DHUABA AL-SEIFU.
Imepokewa kutoka kwa Abi Abdallah alisema ilipatikana kwa Dhuaba Saifu Rasul,sahifa ambayo imeandikwa ndani yake, BISMILLAHI RAHMAN RAHIM, hakika dhalimu mkubwa mbele ya Allah siku ya kiyama ni yule aliyeuwa asiyemuua, na yule aliyempiga asiye mpiga, na yule aliyetawala asiyestahiki kutawala.basi mtu huyo atakuwa ni kafiri aliye kufuru yale yote aliyoyateremsha Allah kwa Mtume wake Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). na mwenye kuzusha uzushi katika dini na yule aliyempa makazi kila mzushi mtu huyo, Allah hatamkubali siku ya kiyama kumkombolea hata fidia yoyote. Angalia BIHARU AL ANWAAR Juzuu 27 Uk: 65-104,na Uk: 275
6. AL-JAFAR: NA AL- JAFAR NI AINA MBILI:-JAFAR NYEUPE NA JAFAR NYEKUNDU.
Imepokewa kutoka kwa Abi Alaa alisema nilisikia Aba Abdillah (Alayhis Salaam) akisema hakika mimi ninayo AL-Jafar Nyeupe, na akasema Abi Aalaa kumuuliza Abi Abdillah, kwani mna nini ndani ya AL Jafar hiyo? Akasema Abi Abdillah: mna zaburi ya nabii Dauud mna Taurat ya nabii Musa na mna injil ya nabii Issa na Suhfu ya nabii Ibrahim na mna upambanuzi kati ya mambo ya halali na haramu,na akaongeza kusema kwamba vilevile ninayo Al Jafar Nyekundu,na akaniuliza na mna nini ndani ya Jafar Nyekundu akasema na kumjibu kwamba ndani yake mna silaha,na silaha hiyo ni mtu mwenye upanga kwa ajili ya kuuwa,na akasema Abdillah Bin Abii Yaafuur kumwambia Abi Abdilah kumwambia kwa kumuombea dua;Allah akuweke katika afya njema. Je haya watakuwa wanayajua Banuu Al Hssan(kizazi cha Al Hassan) akamjibu ee!! Ndio wallahi wanayajua haya kama wanavyoujua usiku kwamba ni usiku na mchana kwamba ni mchana lakini wao wamepatwa na hasadi na kuitafuta dunia kwa kukanusha na kupinga haki, lau kama wangekua wanaitafuta haki kwa haki hilo lingekuwa bora kwao. Angaliaa USUULU AL KAAFI Juzuu 1 Uk: 24
Nilimuuliza maulana imamu Al Khui ambaye sasa ni aliyefariki, kuhusu Al jafar Nyekundu ni nani atakayeifungua? Na ni damu ya nani itakayomwagwa?.akanijibu na kusema kwamba atakayeifungua ni huyu bwana wa zama (Mwenyezi Mungu amfanyie haraka faraja yake)na watakao mwaga damu hiyo ni Ahlus Sunnah,kwa maana kwamba watakuja kuuliwa Ahlul Sunnat wote kwa pamoja na huyo bwana wa wakati huo,na ataitawanya damu yao na itakuwa nyingi sana na itakuwa inatiririka na kupita mto Dajital na Furat iliyoko IRAQ.
Na vilevile atakuja kulipizia kisasi kwa masanamu wawili wa kiquraysh (anakusudia maswahaba wa Mtume ambao ni makhalifa waongofu naye ni Abu Bakr na ‘Umar pamoja na Aisha Bint Abi Bakr na Bi Hafsa Bint ‘Umar ambao ni wake zake Mtume, pamoja na ‘Uthmaan Bin ‘Affaan ambaye ni mkwe wake Mtume pamoja na Bani Umaya na Bani Abbas.na hatimaye atakwenda kuyafukua makaburi yao na kuyawacha wazi.
Nikasema hakika kauli ya Imamu Al-Khui ni chafu na inachukiza mno,kwani Ahlul Bayt ni watu watukufu na wenye heshima kwani haiwezekani kwao kwenda kufukua makaburi ya maiti waliokufa kwa karne nyingi zilizopita(kwani watapata faida gani kwa hatua kama hiyo?). hakika maimamu (Alayhis Salaam) walikuwa wakiyakabili maovu kwa kumtendea mema,muovu huyo na kumsamehe na kuyapuuza maovu yake.
Kw ahiyo haingii akilini kwa maimamu wenye sifa kama hii kuweza kuyafukua makaburi na kuwatoa hao maiti ili waweze kuwaadhibu na kulipizia kisasi na kuwasimamishia hadi (kuwahukumu)kwani maiti hawasimamishiwi hadi (kuhukumiwa hapa duniani) kwani Ahlul Bayt wote wanajulikana kwa sifa za usamehevu na kwamba ni watu wazuri wenye roho nzuri,kwani wao walikuwa ni watu wenye tabia njema walikuwa wavumilivu walibarikiwa tabia nzuri na hiyo ni nguzo madhubuti kabisa.
7. MAS-HAFU YA FAATIMAH
Kisha nikasema na kujiuliza,ikiwa hiki kitabu ni maneno yanayotoka kwa Mtume na akayaandika Ali ni kwa nini basi akifiche kitabu hicho kwa Ummati wake kwani Mwenyezi Mungu akimuamrisha Mtume wake afikishe kila kitu alichoteremshiwa na Allah kwa Ummati wake kwani amesema Mwenyezi Mungu mtukufu katika surat Al-Maaida: Aya; 67.
Vipi inawezekana kwa Mtume wa Allah kuweza kuwaficha waislamu wote Qur-an hii, na vipi inawezekana kwa Amir Al muuminina na maimamu wote waliokuja baadae kuificha Qur-an hiyo kwa mashia(wafuasi) wao.hilo ni jambo lisilowezekana hata kidogo.
8. TAURAT NA INJIL NA ZABUR
Imepokewa kutoka kwa Abi Abdillah (Alayhis Salaam) kwamba yeye alikuwa akisoma INJIL na TAURAT na ZABUR kwa lugha ya kiisoiraniah. Tazama AL HUJAJ MINAL KAAFI, Juzuu 1 Uk: 208. mlango unaoelezea kwamba maimamu wote wanavyo vitabu vilivyoteremshwa kutoka mbinguni na Allah, na hakika hao maimamu wanavijua vitabu hivyo vyote pamoja na tofauti za lugha za vitabu hivyo kwa maana kwamba maimamu wao wanazijua lugha za vitabu hivyo.
9. AL-QUR-AN
Kuthibiti kwa Qur-an kwamba ni kitabu cha Allah kisicho na shaka ndani yake hakuhitaji nasuu (ushahidi).lakini utaona vitabu wa wanavyuoni wetu na kauli za mujitahidina (wanavyuoni wakubwa)wote vinaelezea kwamba Qur-an hii imebadilishwa na sivyo ilivyo. Na hiyo Qur-an ndicho kitabu peke yake kilicho kumbwa na mabadiliko kati ya vitabu vyote vilivyoteremshwa kutoka nbinguni na Allah.
Na hakika hivyo Al-Muhadith Annuury Atwabrisiy alitunga kitabu kikubwa sana katika kuthibitisha kwamba Qur-an imebadilishwa na kitabu hicho kinaitwa Faslu Al Khitwaab Fii Ithbaat Tahriif kitab Rabi-Al-Arbaabi. Na alikusanya ndani ya kitabu hicho zaidi ya riwaya Alfu moja zinazozungumzia juu ya kubadilisha Qur-an na vilevile akakusanya kauli za mafukaa wote na maulamaa wa kishia katika kubainisha na kuweka wazi juu ya kubadilishwa Qur-an ambayo ipo kwa waislamu.
Kwani wanazouni wote wa kishia na mafukaha wao wote kuanzia waliotangulia mpaka leo hii wanaamini na kusema kwamba hakika ya Qur-an iliyopo hivi sasa kwa waislamu imebadilishwa Haifa kuwa nayo kwani siyo hawaiamini kamwe. Na huu ni uongo wa dhahiri wa kishia.
Amesema Sayid Hashimu Al Bahraaniy: mimi ninao ushahidi wa kutosha juu ya kauli ya kwamba kubadilishwa kwa Qur-an, na hayo ni baada ya kufuatilia habari hizi kwa undani kabisa,kwa kiasi ambacho inawezekana kutoa hukumu kwamba msimamo huu na itikadi hii ni katika jambo la dharura na la lazima katika madhehebu ya kishia kuamini hivyo. Na hakika hilo ndilo dhumuni kubwa la kunyang’anywa ukhalifa Ahl Bayt ; zingatia!!. Angalia: MUQADIMAT AL-BURHAN. Mlango wa tano, Uk: 49.
Na amesema Al Sayyid Niimatu Allah Al-Jazaairy, akiwajibu wale wanaosema kwamba Qur-an haikubadilishwa. Hakika kukubali ,na kuamini kwamba Qur-an, upokewaji wake,watu wake , una daraja ya Tawatur (upokeaji uliosahihi).na ni wahyi uliotoka kwa Allah na kwamba Qur-an yote aliteremka nayo Jibril kwa amri ya Allah kutoka mbinguni,basi jambo hili linapelekea kuweza kuzitupilia mbali habari ambazo zina ukweli na uhakika zaidi.pamoja na kwamba wenzetu Ahlul Sunnat wamekubaliana kwa pamoja juu ya kusihi jambo hili na kuliamini moja kwa moja.Angalia AL-ANWAR ANNUUMANIYA . (Juzuu .2- Uk: 357.)
Na kwa habari hizi amesema Abu Jaafar kama ilivyonukuliwa na Jabir, amesema hakuna mtu yoyote ambae aliyedai kwamba Qur-an ilikusanywa mtu muongo kabisa. Nahakuna yoyote aliyekusanya na kuihifadhi hiyo Qur-an kama ilivyoshushwa isipokua Ali Bin Abi Twalib na maimamu baada yake. Angalia AL HUJAJI MINA AL KAAF-(Juzuu 1 Uk: 26.)
Bila shaka hii ni uthibitisho wa wazi kabisa unaothibitisha kubadilishwa Qur-an ambayo wanyo waislamu hivi sasa. Na Qur-an ya kweli ni ile ambayo iko kwa Ali na maimamu waliomfuatia baada yake yeye mpaka ikamfikia, ikawa huyo (AL QAAIM).
Na kutokana na hali hiyo ndipo aliposema AL-Imam Al- Khaui katika wasia wake kwetu sisi wakati akiwa anakurubia kufa alisema:Shikamaneni na Qur-an hii (ambayo imebadilishwa) mpaka itakapo dhihiri Qur-an ya Fatmah. Na Qur-an ya Fatmah anayoikusudia huyu Imam, ni ule msahafu ambao alioukusanya Ali kama tulivyoeleza nyuma.
Hakika ni jambo la kushangaza na kuchukiza kwamba vitabu vyote hivyo vimeteremka kutoka kwa Allah halafu vitabu hivyo viwe vimemhusu Amirl muumini na maimamu wake baada yake.na vitabu hivyo vikasalia ni vyenye kufichwa kwa umma,na hasa kwa shia wa Ahlul Bayt isipokua Qur-an ndogo ambayo watu waliweza kuongeza wanachoongeza na kupunguza wanachopunguza. Haya ni kutokana na maneno ya wazuoni wetu wakishia.
Cha kushangaza ni kwamba iwapo vitabu hivi vyote ni kweli vimeteremka kutoka kwa Allah na Amirl muuminina kuwa amekusanya na kuhifadhi Qur-an hii,sasa ina maana gani yeye Amirl muuminin kuwafichia ummah. Na hali yakuwa huo umma unahaja sana na Qur-an hiyo ambayo imekusanya taratibu zote za maisha yao ya kila siku na mambo ya ibada zao iliwaweze kumuabudu Allah, kama inavyotakikana?!.
Na wanazuoni (mafuqahaa) wetu wengi wamelielezea jambo hili na kuliletea kwa kila hali kwa ajili ya kuwaogopea upinzani. Na ni wajibu wetu sisi kuuliza, Je inawezekana akawa amirul muuminin ambaye pia ni simba wa Banu Hashim kuwa muoga kiasi cha kushindwa kutetea jambo hili? Je anaweza kuficha habari zake na kuunyima ummah kwa ajili ya kuogopa wapinzani wake. La sivyo ninaapa kwa yule aliyeziinua mbingu pasi na nguzo. Haikuwa kwa Ibn Abi Twalib akimuogopa yoyote isipokuwa Allah peke yake. Na pindi tunapouliza atafanya nini Amirl muuminin na maimamu watakao kuja baada yake kwa Zabur na Taurat na Injil mpaka iwafikie watu wote na halafu waisome vitabu vyote hivyo kwa siri.
Na ikiwakuna nasi (hoja) zilizodai kwamba Amiril muuminin ni yeye peke yake aliyehifadhi Qur-an yote, na akavihifadhi vitabu vyote vya mbinguni na sahifu nyinginezo. Sasa kuna haja gani tena kuwa ni Zaburi, Taurat na Injil? Na hasa tunajua ya kwamba vitabu vyote hivyo vimefutwa kwa kuteremka Qur-an?
Hakika mimi ninaona kwamba kuna mikono ya watu wanaotumbukiza sumu mbaya katika Riwaya hizi,na wakawasingizia maimamu watukufu uongo huu, (na utakuja uthibitisho wa habari hizi katika mlango maalum)
Sisi sote tunajuwa ya kwamba uislamu hauna kitabu isipokuwa kimoja nacho ni Qur-an tukufu. Ama kuwa na mfano wa vitabu vingi jambo hili ni maalumu kwa mayahudi na manasara kama ilivyokuwa wazi kwenye vitabu vyao,ama kauli inayosema kwamba Amirl muuminin amevihifadhi jamii ya vitabu vyote na kwamba vitabu vyote hivyo vinatoka kwa Allah,na kwamba vitabu vyote hivyo vimekusanya mambo yote ya kishia kauli hiyo ni batil,imeingizwa kwetu na baadhi ya mayahudi ambao walijipenyeza kwenye ushia.
Wakati tunaporejea na kuvisoma vitabu vyetu vya kishia vinavyotegemewa kuwa ndivyo sahihi na rejea za msingi pamoja na kauli za wanazuoni wetu wakubwa na mujtahidina wetu,tunakuta kwamba adui peke wamashia ni Ahlus Sunnah, kushinda mayahudi na wanasara kutokana na uadui huo mashia waliwapachika Ahlus sunnah kwa kuwaita kwamba wao ni wajinga na wasiojua kitu na wakawaita pia kwamba ni wehu na madhalimu.
Na itikadi ya mashia mpaka leo hii wanamchukulia kila Ahlus Sunnah ni kama mkia ulioko nyuma [yaani ni uchafu najsi] na shia yoyote yule kama anataka kumtukana mwenzake na anapotaka kulifanya tusi hilo kuwa ni lenye kuchukiza na kutia hasira moyoni humwambia mwenzake kwa kutumia usemi huu [mwili wa sumu upo kaburini kwa baba yako] kwa sababu Sunni ni najsi kuliko nguruwe na huo ndio mtazamo wa shia wanavyowachukulia Ahlus Sunnah .
Na imefikia mashia kiwango cha kusema kwamba lau
Na ndani ya mazungumzo yetu, niligundua kwamba huyu mgeni ni msuni na anatoka sehemu inayoitwa Saamaraa na alikuja hapa Najifu kwa haja maalumu na kulipokucha tulimpeleka mgeni wetu mlo wa asubihi na akala. Hata mgeni wetu alituaga kurudi anakotoka. Na hapo mzazi wangu akampa yule mgeni kiasi Fulani cha
Yule mgeni akatoa shukrani zake kwetu kw amakaribisho mema aliyoyapata kutoka kwetu. Na baada ya yule mgeni kuondoka tu, mzazi wangu aliamuru kuchomwa kile kitanda alicholalia yule mgeni,na pia kuvitwaharisha vyombo vyote alivyotumia kula yule mgeni.kwasababu mashia wote wanaitikadi(wanaamini) kwamba wasunni wote ni najsi na hii ndiyo itikadi ya mashia wote, kwani wanazuoni wetu wote wa kishia wamemnasibisha kuwa ni kafiri na na ni sawa na nguruwe na ndipo walipomuweka kwamba yeye msuni ni miongoni mwa najsi. Na kutokana na haya:
Na imepokewa kwa Al Hussain ibn Khalid kutoka kwa Al Ridhaa kwamba alisema: mashia (wafuasi) wetu ni wale wenye kutii amri zetu, wanaozipokea kauli na kuzifanyia kazi. Na wafuasi wetu wa kweli ni wale wanaozikhalifu kauli za maaduii zetu japo kuwa ni za kweli.na yeyote katika mashia(wafuasi wetu) asiyefanya hivyo hayupo na sisi,bali na yeye ni adui wetu. [Al Fusuul Al Muhimat
Na imepokewa na Al Mufadhal ibn ‘Umar na imepokewa na Jaafar kwamba alisema ,atakuwa amesema uongo yeyote yule atakaedai kwamba yeye ni katika mashia (wafuasi) wetu na hali ya kuwa anafungana na wasiokuwa sisi (mashia). [Al fusuulu Al Muhimat
Na amesema tena: Wallahi ninaapa kwa Allah,ya kwamba Mwenyezi Mungu hakujaalia ubora kwa yeyote yule anaewafuata wasio kuwa sisi (mashia) yule anaeafikiana na sisi ni yule ambae anaewakhallifu maadui zetu, lakini yule anaewaafiki maadui zetu kwa maneno au kwa matendo basi yeye sikatika sisi wala sisi sikatika wao.
Na amesema Al Abdu Asswaleh (Alayhis Salaam) katika hadithi mbili tofauti, chukua yale yote ambayo yamewakhalifu jamaa Ahlus Sunnah na muyaache yale ambayo yaliyowaafiki jamaa. Katika kauli ya Ridhaa(Alayhis Salaam) pindi zitakapo wafikia habari mbili zenye kugongana basi zichunguzeni kwa makini mtakapo kuta moja yake ya khabari hizo zinazowakhalifu hao jamaa Ahlus Sunnah zichukueni na zile zinazowakhalifu hao Asswadiq (Alayhis Salaam) wallah hakuna haki yeyote iliyobaki kwetu isipokuwa kuelekea kibla tu. Angalia Alfusulu Al Muhimat 325-326.
Na ameandaa Fasul hii Asswadiq na akasema imepokewa na abdii Ishaaq Al Arjaaiy alisema , amesema Abu Abdiillah(Alayhis Salaam) je unajuwa ni kwanini mmeamrishwa kuyachukua(kuyafuata ) yale ambayo yako kinyume na yale wanayosema jamaa (Ahlus Sunnah) ni kasema kumwambia sijui bwana. Akasema hakika Sayidina Ali (Alayhis Salaam) hakuwa akifanya ibada yeyote ya Allah isipokua umma ulikuwa uko kinyume yake kwa ajili ya kubatilisha amri zake.
Na walipokua wakimuuliza Amirili muuminin juu ya jambo lolote wasilolijua, na pindi anapowajibu wao huenda kinyume na yeye ili kuwachanganya watu wasifuate ukweli wa mambo.
Hapa tunajiwa maswali mengi
Hapo akamjibu, Assayid Mohammad Baaqir Asswadir akasema, ndio inatupasa kulichukulia jambo
Na kwa hali
Lau tungeliwauliza mayahudi, ni nani mbora wa watu katika mila yetu (dini) Wallahi wangesema ni wale maswahaba wa Musa. Na hata tungeliwauliza maswahaba, ninani mbora wa watu katika mila yenu? Wangesema wanafunzi wa Isa.
Na lau
Hakika maswahaba wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ndio watu wa kwanza wanaokimbiwa na matusi ya mashia na kulaaniwa na kuvunjia heshima zao hasa Abu Bakr na ‘Umar na ‘Uthmaan, pamoja na wake zake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) hawa wawili Bi Aaisha bint Abi Bakr na Hafsa bint ‘Umar, kutokana na hali hii imekuja katika dua za mashia dua inayoitwa dua ya masamu mawili ya kiquraish dua yenye kusema hivi[ Ewe mola wetu wa jaalani haya masanamu mawili ya kiquraish (Abu Bakr na ‘Umar) waovu wawili hawa na matwaghuti(mashetani) mawili haya na pia uwalaani mabinti zao hawa wawili (Aaisha na Hafsa]. Na dua hiii imo kwenye vitabu vyao zinavyotegemewa. Na alikuwa Imama Khomeini akiisoma kila siku baada ya swalah ya Asubuhi.
Na imepokewa kutoka kwa Hamza bin Muhammad Atwayyaar alisema siku moja tulimtaja Muhammad bin Abi Bakr mbele ya Abii Abdillah akasema[Mungu amrehemu Muhammad bin Abi Bakr] kisha akasema siku moja Muhaamad bin Abu Bakr alisema kumwambia amirl muuminin nyoosha mkono wako ni kubaii(kukubali
Ama kuhusu ‘Umar amesema Niimatullah Al Jazairy, hakika ‘Umar bin al Khatwaab alikuwa amepatwa na maradhi katika Duburi(njia ya haja kubwa) yake na alikuwa hayatulii maumivu yake isipokuwa kwa maji ya wanaume(yaani manii) kwa maana kwamba yeye alikuwa akilawitiwa na wanaume wenzake Angalia Al Anwaar Anuumaaniyat- Juzuu 1 Uk: 63.
Ningependa ufahamu ya kwamba katika mji wa Kashan uliopo katika jimbo linaloitwa (Baghiy fiin) kuna sehemu inakaburi ambayo inadhaniwa kwamba ni ya Abii Luulula Feyruzi Al Farsiy) ambaye ndiye aliyemuuwa khalifa wa pili Bwana ‘Umar bin Al Khatwaab.
Na sehemu hiyo wakaipachikia jina na kuiita [Mapumziko ya shujaa wa diini] na jina hili walimpachikia huyu jamaa kwa sababu ya kumuuwa ‘Umar bin al khatab. Na isitoshe pia waandika katika kuta za sehemu hizo kwa lugha za kifarsy zenye maana[ Hapa ni mahala pakifo cha Abu Bakr na ‘Umar na ‘Uthmaan].
Na sehemu hizi wairan huenda wakazizuru mara kwa mara na hutoa sadaka nyingi na michango ya kila aina na sehemu hiyo nimeshaizuru mimi mwenyewe binafsi. Na nikajionea mwenyewe hali halisi ya mambo.
Na wizara ya ir-shad [uongofu] ya
Na imepokea al kulainiy kutoka kwa abi jafar. Hakika ya hawa masheikh wawili yaani [Abu Bakr na ‘Umar] walifariki dunia na wal hawakutubia kwa Allah. [ Walikufa hali yakuwa ni makafiri] na wala amirl muuminin hakuweza kuwakumbuka kwa jema lolote lile walilolifanya basi ni juu yao laana ya Mwenyezi Mungu pamoja na laana ya malaika na ya watu wote. Angalia Raudha Al Kaafiy Juzuu 7
Ama kuhusu ‘Uthmaan imepokewa kutoka kwa Ali bin Yunus Al Bayaadhiy anasema kwamba, hakika ‘Uthmaan alikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa wakichezewa [akilawitiwa] na alikuwa si mwanamume sawasawa [hafai]. Angalia Al-Swirat Al- Mustaqiim Juzuu 1
Na kuhusu Bi Aisha (Radhiya Allaahu ‘anha) amesema ibn Rajab Al Barsiy hakika Bi Aisha alikusanya dinar arubaini kutokana khiana yake. Angalia Mashaarifu Anwaar Al Yaqin
Na isitoshe ikiwa khalifa wa pili ‘Umar alikuwa na ugonjwa katika njia ya haja kubwa na ugonjwa huo hautulii isipokuwa kwa maji ya wanaume[manii] kama alivyodai Asayid Al Jazaairiy na vipi angeweza Amir Al muuminin kumuozesha binti yake Ummu Kulthum kwa mtu kama huyu mwenye sifa mbaya kama hizi?.
Je ugonjwa huu ulikuwa umejificha haukujulikana bali aliutambua huyu Al Jazaairy peke yake? Habari hizi hazihitaji jambo lolote zaidi ya kutumia akili tu si vyenginevyo. Na imepokewa na Al Kulainiy amesema hakika watu wote ni watoto wa zinaa isipokuwa mashia wetu tu. Angalia-Al Raudhat- Juzuu 7
Na imepokewa kutoka kwa Dawud bin Farqad alisema nilimuuliza Abii Abdullah unasema kuhusu kuumuuwa dhalimu [Ahlus Sunnah] akamjibu na kusema kwamba, damu yake ni halali, lakini mimi ninakuhofia wewe lakini kama utaweza kumwangushia Ahlus Sunnah ukuta ua ukamgharikisha kwenye maji ili usionekane na watu kwamba umefanya hivyo basi fanya simbaya huna dhambi. Angalia Bihaar Al Anwaar. Juzuu 27- Uk: 231.
Na maneno haya ameyatilia nguvu na kuyafafanua zaidi al Imama Khomeini kwa kusema kwamba. Na kama utaweza kuchukua
Na amesema Syyid niimat Allah al Jazairy, aliyekuwa waziri wa Al Rashid bwana Ally bin Yaqtin siku moja aliamuru vijana [wafanyakazi]wake kuvunja dari ya mahabusu [jela] yake ambaye siku hiyo ilisheheni watuhumiwa wapatao watu mia tano, wakaangukiwa na dari hiyo wote wakafariki dunia[na hao watuhumiwa walikuwa Ahlus Sunnah] Angalia Al Anwar Al Nuuman/3/308.
Na vitabu vya historia vinatusimulia kwa undani zaidi kuhusu vitendo viovu vilivyopita katika mji wa
Kutokana na mauaji hayo ya kumwaga damu tupu kutokana na wingi wa vifo vya watu ambao ndio Ahlus Sunnah damu zao zilimiminika katika mto huo na mto ukabadilika ukawa damu tupu.
Na hali hiyo haikutosha bali ukafanywa uonevu na unyama mwengine pale vilipotupwa vitabu vya Ahlus Sunnah ndani ya mto huo kiasi ambacho mto nao ukabadilika rangi yake na kuwa rangi ya bluu kutokana na wingi wa vitabu hivyo haya ni maonevu waliyotendewa Ahlus Sunnah wa mashia.
Na mauaji yote yalifanywa na mawaziri wawili katika utawala wa Al Abasiyat kwani mawaziri hawa walikuwa ni mashia nao ni annuswair Attuusiy na Muhammed Al Qami. Na vilevile walikuwa na uhusiano wa karibu na huyu Hoolakoo muuaji mkubwa.
Hawa hawa ndio waliomsaidia Hoolako kuingia Baghadad na kuuangusha utawala wa Al Abasiyat ambao wao walikuwa ni mawaziri kwenye utawala huo. Pamoja na kwamba wao walikuwa na sauti katika utawala huo lakini hakuiiridhiya hali hiyo pamoja na vyeo vyao hivyo walivyopewa kwani walikuwa na chuki za ndani kwasababu utawala wa Al Abbasiyat ulikuwa unatafuta madhhabu ya Ahlus Sunnah.
Na baada ya kuingia Hoolako Baghadad na kuuangusha utawala huo wa Al Abasiya muda mfupi tu hawa mabwana wawili wakapewa vyeo vya uwaziri tena katika utawala wa Hoolako pamoja na kwamba Hoolako mwenyewe alikuwa ni mtu wathaniy[asiyekuwa na dini] lakini bali tatizo ni kuwamaliza Ahlus Sunnah.
Pamoja na hayo yote tunamuona imam khomein anaridhisha na vitendo vya mauaji ya hawa watu Ally Yaqtin na Atuusiy na Al Qamiy na anayazingatia yale waliyoyafanya hawa mabwana ni katika moja ya hujuma kubwa
Ninahitimisha mlango huu kwa neno la mwisho ambalo ni neno la Al Sayyid Niimatu Allah Al Jazairy linalohusu hukumu ya Annawaasibu[Ahlus Sunnah] Alisema kwamba hakika ya Ahlususunnah wote ni makafiri na ni najisi kwa ijmaa[itikafi]ya wanazuoni wakishia wote,wanaitikadi kwamba mwanasuni yeyote ni kafiri na ni najisi. Na vilevile Ahlus Sunnah ni waovu kuliko mayahudi na manaswara na miongoni wa alama na dalili za watatu Abu Bakr, ‘Umar, ‘Uthmaan (Radhiya Allaahu ‘anhum) badala ya Ally (Radhiya Allaahu 'anhu) katika uimamu. Angalia- Al Anwar Annuumania Juzuu-2,
Hivyo ndivyo tunavyoona kwamba hukumu ya shia kwa Ahlus Sunnah inachambulika
Ahlus Sunnah wote ni makafiri na ni najisi kuliko nguruwe na ni watu waovu kuliko mayahudi na manaswara na ni watoto wa zinaa,na inawajibika kuwaua na inafaa kuchukua mali zao. Yaani shia kuchukua
Na wala haiwezekani kwa mashia na Ahlus Sunnah kuungana kwa jambo lolote lile, hawawezi kuungana hata wa bwana wa viumbe[Allah] yaani mashia wana Mungu wao na Ahlus Sunnah wana Mungu wao] wala haungani kwa nabii wala Imamu , yaani kila mmoja wao ana nabii wake na wala haijuzu kwa mashia kuwaafiki AhlusSunnah kwa kauli yoyote na kwa tendo lolote lile ni lazima kila mmoja awe kinyume na mwenzake.
Na vile vile ni wajibu kwa kila shia kuwalaani masuni na kuwatukana hasa wale watu waliotutangulia maswahaba ambao Allah aliwasifu katika Qur-ani tukufu,ambao walisimama bega kwa bega na mtume (Subhaanahu wa Ta’ala) katika daawa yake na jihad yake. Hapo niambie ni nani hasa ambaye alikuwa pamoja na mtume katika mapambano [vita] yake yote ambayo alipambana nayo na makafiri.
Kwahiyo kushiriki hawa mabwana watukufu katika vita vyote hivyo pamoja na mtume ni dalili ya wazi kwamba nao walikuwa na imani madhubuti na ya kweli kweli isiyo shaka kwa hiyo mtu hana haja ya kuyaangalia yale wanayosema wanazuoni wetu wa kishia kuhusu maswahaba wa Mtume.
Na ulipokwisha utawala wa al-Bah-lawiy hapo
Mimi nilikuwa na wajibu wa kupongeza zaidi kuliko yoyote yule kutokana na mafungamano yangu makubwa na imamu khomein, na niliizuru
Na moja kati ya kikao chetu maalum mimi na imam Khomein alisema kuniambia kwamba Sayyid Hussein, sasa hivi umefika ule wakati wa kutekeleza wosia wa maimamu (Subhaanahu wa Ta’ala) hivi sasa tutamwaga damu za wanaaswib [Ahlus Sunnah] na tutawauwa watoto wao na tutawaacha hai wake zao wawe vijakazi wetu.
Na wala hatutamwacha yoyote yule aweze kunusurika na mateso yetu,na mali zao zote zitakuwa ni milki ya mashia wetu, na mali zao zote zitakuwa ni milki ya mashia wa Ahlus bait, na tutafuta Makka na Madina isiwepo hapa juu ya mgongo wa ardhi yaani wataziangamiza hizi[Haram mbili] watazibomoa na kuziteketeza kabisa. Kwasababu miji miwili hii Makkah na Madina ndio kitovu cha mawahabi.
Lengo letu kuu ni kuwa kar-balaa iwe ndiyo ardhi tukufu iliyobarikiwa na iwe ndicho kibla cha watu wote wakati wa swala zao badala ya makkah.na njia hiyo tutakuwa tumezifikia fikra za maimamu wetu (Alayhis Salaam) nahapo itakuwa ile dola yetu ambayo tuliyokuwa tunaipigania kwa muda mrefu imesimama wima na kutoa kilichobakia sasa hivi isipokuwa ni kutekeleza wasia huu tu!!.
Ningependa ufahamu ewe ndugu yangu kwamba chuki za mashia kwa Ahlus Sunnah, ni chuki ambazo zisizokuwa na mfano kabisa.kutokana na chuki hizo ndiyo maana wanazuoni wetu wamejuzisha kuwasingizia uongo Ahlussunnat na kuwapandikiza kila aina ya tuhuma za uongo na kuwasingizia kwa kila ubaya na kuwapa sifa za kila machafu.
Na sasa hivi mashia wote wanawaangalia Ahlus Sunnah kwa jicho la chuki na ubaya hayo yanatokana na maelekezo aliyotolewa na baraza kuu la kishia na vilevile yametolewa maelekezo kwa watu mmoja mmoja kwa jamii yote ya kishia,kwamba ni wajibu kwa kila shia kujiingiza na kujipenyeza kuleta vurugu katika vyombo vya dola na katika taasisi zote sawa ziwe za kiserikali au za kibinafsi na hasa katika sehemu nyeti kama vile jeshini na vyombo vya usalama na ulinzi na sehemu nyingine zote hasa ukizingatia kujiingiza katika mkondo wa vyama vya kisiasa.
Na mashia wote wanasubiri wakati wa kutangazwa Jihad na kuwaangamiza Ahlus Sunnah, mashia wote wanadhania kwamba kufanya hivyo wao wanakuwa wanawahudumia na kuwatumikia AHLUL BAYT na wanasahau ya kwamba wao wanasukumwa na watu walioko nyuma ya pazia kwa maslahi yao tu. Na wao hawayatambui hayo, na tutayaonyesha haya katika fasili inayokuja.
Nilimuuliza Imamu Al Khuiy kuhusu maneno ya Amirl muuminin ya kuharamishwa mut’a siku ya khaibara na kuhusu na maneno ya Abii Abdilah ya kumjibu muulizaji wa ndoa isiyo tangazwa,je ilikuwepo katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)? Akasema: maneno ya Amirl muuminin kuhuau kuharamishwa mut’a siku ya khaibara, uharamu huo ni kuwa hiyo ya khaibar tu, baada ya hapo haikuendelea tena Uharamu huo.
Na ama usemi wa Abii abdillah akijibu swali alilo ulizwa , imamu Alkhuuiy anasema kuwa Abii abdillahi alisema hivyo kwa taqiyya (kudhihirisha kinyume na unavyo amini),na suala hili wamelikubali wamnazuoni wetu.
Mimi nasema: Kwa kweli maneno ya wanazuoni wetu hayakua sahihi, kwa sababu kuharamishwa mut’a siku ya khaibar kuliambatana na kuharamishwa punda wa kufugwa na uharamishwaji wa punda wa kufugwa,umeendelea kufanyiwa kazi toka siku hiyo ya khaibar mpaka leo hii,na itaendelea mpaka siku ya Qiyama.
Kwa hiyo madai ya kuwa mut’a iliharimshwa siku ya khaibar tu nimadai matupu yasiyo kuwa na ushahidi, hasa ukizingatia kuwa uharamu wa punda ambao ndio mwenza wa mut’a uliendelea mpaka leo hii.
Na zaidi ya hayo ingekua kuharamishwa mut’a ni kwa ajili ya sku ya khaibari tu, basi yangepatikana maelezo ya wazi kutoka kwa mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ya kufuta uharamu huo,muhimu ni kwamba tusisahau ya kua sababu ya kuhalalishw mut’a ilikua ni safari na vita , basi iweje iharamishwe katika vita hiyo na wenye kupigana wana haja zaidi na kitu hicho (mut’a) hasa ukizingatia wako mbali na wake zao na wajakazi wao,halafu tena ije ihalalishwe wakiwa nyumbani katika hali ya amani?!
Hakika maana ya Amiril-muminina (Alayhis Salaam) kwamba mut’a iliharamishwa siku ya khaibara maana yake ni kwamba mwanzo wa kuharamishwa mut’a ilikua ni siku ya khaibar, lakini maneno ya wanazuoni wetu ni kuchezea maelezo ya kisheri si vinginevyo.
Ukweli ni kwamba kuharamishwa mut’a na punda wa kufuga ni vitu vinavyokwenda pamoja iliteremka hukumu ya kuharamishwa kwake siku ya khaibar na itaendelea hivyo mpaka Qiama wala hakuna sababu ya kuleta maelezo ya mbali katika maneno ya Amiril-muminina (Alayhis Salaam)kwa sababu ya kutaka kushibisha matamanio ya nafsi na kutafuta wanawake wazuri ili kustarehe nao kwa jina la dini.
Ama maneno ya Abii Abdillah, katika kumjibu yule muulizaji kua ni taqiyya, mimi nasema kujibu hoja hiyo kwamba muulizaji alikuwa nikatika wapambe wa Abii abdillahi kwa hiyo hapakuwa na sababu ya kuleta Taqiyya kwa hiyo maneno yake hayakua ya taqiyya hasa ukizingatia maneno yenyewe yanakubaliana na maneno yaliyo nukuliwa kutoka kwa miril-muminina (Alayhis Salaam) kwamba mut’a iliharamishwa siku ya khaibar.
Hakika ya mut’a ambayo wameiruhusu wanazuoni wetu, inampa haki mwanamume kustarehe na idadi kubwa ya wanawake isiyo wezwa kudhibitiwa,hata
Watu wengi waliofanya mut’a wamesha wakusanya mtu na mama yake mtu na mtoto wake mtu na shangazi yake au na mama yake mdogo,nae hajui.
Alinijia mwanamke akinisimulia tukio lilomfikia alinieleza kuwa mmoja wa wa mabwana wakubwa ,naye ni assayed Huseini Al sadri alikua amefanya nae mut’a kabla ya miaka ishirini na kupata mimba na alipo maliza haja yake alimuacha, na baada ya muda akapata mtoto wa kike,na aliapa kua mimba hiyo ni ya huyo bwana mkubwa , kwa sababu hakufanya na mtu yoyote wakati huo isipokuwa bwana mkubwa huyo.
Baada ya kukua yule binti na kuwa msichana mzuri anae faa kuolewa, mama aligundua kuwa binti yake ana mimba,basi alipo muuliza mimba kaipata wapi , binti akamueleza mama yake kuwa ni ya yule bwana mkubwa alie tajwa alifanya nae mut’a na akapata mimba, mama akapata mshutoko na akachanganyikiwa ,na akamueleza binti yake kuwa huyo mtu (alie mpa mimba) ndie baba yake, na kumueleza kisa chote . vipi mtu anafanya mut’a na mama kisha inakuja siku nyingine anafanya mut’a na mtoto wake mwenyewe?
Kisha akanijia mwana mke huyo akinisimulia kuhusu msimamo wa bwana mkubwa huyo alietajwa kuhusiana na huyo mwanamke na binti yake.
Matukio ya aina hii ni mengi
Hakuna anayeweza kueleza matukio yote ya aina hii yaliyo tokea kwa sababu ya mut’a na sisi tumeyashudia wenyewe.
Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala) anasema:
(وليستعفف الذين لايجدون نكاحا حتى يغنيهم الله من فضله)
{Nawajizuie na machafu wale wasipate cha kuolea, mpaka Mwenyezi Mungu atakapo watajirisha kwa fadhila zake}
Aya inatufundisha kwamba asiyeweza kuoa ndoa ya sheria kwa sababu ya kutokuwa na uwezo basi ni wajbu wake kujizuia mpaka Mwenyezi Mungu atakapo mruzuku kwa fadhila zake ili aweze kuoa.
Basi ingelikuwa mut’a ni halali mtu asingeliamrishwa kujizuia na kusubiri mpaka atakapopata wepesi wa kuoa, badala yake angeelekezwa kufanya mut’a kwa ajili ya kuondoa haja yake badala ya kuumia na matamanio.
Na Mwenyezi Mungu(Subhaanahu wa Ta’ala) amesema:
(ومن لم يستطع منكم طولا أن ينكح المحصنات المؤمنات فمن ما ملكت أيمانكم من فتياتكم المؤمنات)- إلى قوله- (ذلك لمن خشي العنت منكم وأن تصبروا خير لكم والله غفور الرحيم)
{Na asie weza miongoni mwenu kupata mali ya kuolea wanawake waungwana,waislamu, na aoe katika wajakazi wenu waislamu ,na Mwenyezi Mugnu anajua sana imani zenu ninyi kwa ninyi, …endelea mpaka mwenyezimungu aliposema….
Mwenyezi mungu anawaelekeza wale ambao hawawezi kuoa kwa kutokua na uezo wawaoe wajakazi wao na mwenye kushindwa kuoa mjakazi pia basi na avumilie,
Tumeona ni lazima kunukuu hoja nyingine kutoka kwa maimamu (Alayhis Salaam) zinazo thibitisha kuharamishwa kwa mut’a!
Ni kweli kabisa kwamba Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala) amewatosheleza watu na mut’a kwa kuwaikea ndoa ya kudumu ya kisheria.
Na kwa sababu hiyo haikupokewa kuwa kuna mtu yeyote aliwahi kufanya mut’a na mwanamke katika Ahlul-Bayt (Alayhis Salaam) basi lau ingelikua ni halali wangelifanya hivyo, na hilo linatiwa nguvu na habari isemayo kwamba Abdallah bin Umair aliesema kumwambia abii Jafar (Alayhis Salaam) {inakufurahisha kuwaona wake zako na binti zako na dada na mabinti wa Maami zako wakifanya hivyo? Abuu Jafar (Alayhis Salaam) akampuuza wakati alipo taja wanawake zake na mabinti wa ammi zake (Al-Furuui 2/42, Atahdhiyb 2/186)
Na kutokana na haya inathibitika kwa kila muislamu alie na akili kuwa mut’a ni haramu,kwa kwenda kwake kinyume na Qur-an na sunna na maneno ya wanazuoni (Alayhis Salaam) .
Na atakayezitazama aya za Qur-an tukufu na hoja nyingne zilizotangulia katika kuharamisha mut’a akiwa ni mwenye kutafuta haki na kuipenda basi hatukuwa na hukumu zaidi yakuona kuwa maelezo yote yalio kuja kuthibitisha mut’a ni batili, kwa sababu ya kupingana kwake na Qur-an na sunna zilizopokelewa kutoka kwa Ahlul-Bayt (Alayhis Salaam) na kwa sababu ya uharibifu mkubwa unaopatikana katika ndoa hiyo kama tulivyo eleza hapo nyuma.
Inalojulikana Kuwa dini ya kiislamu imekuja kuhimiza maadili mema na kukataza yaliyo maovu,na imekuja kuwahakikishia mambo mazuri yatakayo wasimamishia maisha yao,na hapana shaka kua mut’a si katika mambo yaliyo na maslahi katika maisha ya watu, na tukichukulia kwamba mut’a ina maslahi basi ni maslahi ya mtu mmoja, kwa sababu inasababisha madhra mengi kama tulivyo yataja huko nyuma.
Hakika kuenea kwa mut’a imeleta tabia yakuazimana tupu (maana yake ni kumtoa mtu mkewe au mjakazi wake kumpa mwenzake afanye nae mut’a au afanye vyovyote apendavyo,mtu akita kusafiri anamuacha mke wake kwa jirani yake au rafiki yake au yeyote amtakae, anamruhusu afanye naye chochote apendacho muda wote wa safari na sababu ya kufanya hivyo inaeleweka nayo nikuwa mume anataka atulizane kwa mke wake hatozini wakati yeye hayupo!!
Pia kuna njia nyingine ya kuazimana tupu, pindi anapofika mgeni kwa watu, na wakataka kumkirimu basi mwenye nyumba atamuazima mgeni mke wake katika muda wote wa kukaa pale,
Atamuhalalishia kila kitu, la kusikitisha nikwamba wanatowa riwaya nyingi katika kuthibitisha hayo wakidai kwamba zimepokewa kutoka kwa imamu Al-ssaadiq na baba yake abii jaafar amani ya mungu iwe juu
Amepokea Al Tusiy toka kwa Mohammed Bin Abii Jafar (Alayhis Salaam) amesema, niliuliza: {Je mtu anaweza akamhalalishia nduguye kulala na mjakazi wake? Akasema ndio si vibaya ni halali kwake kile alicho halalishiwa.} (Al Istibsaar 3/136.).
Amepokea AL- KULAINIY na Al- tausiy kutoka kwa Mohammed bin Mudharib amesema aliniambia Abuu Abdillah(Alayhis Salaam):( ewe Mohamed mchukue mjakazi huyu akuhudumie na umuingilie utapoondoka turejeshee) Al Kafiy, Al Furuu 2/200, Al Istibsaar 3/136).
Nikasema: Lau wangekusanyika watu wote wakaapa kuwa maimamu wawili Al sadiq na Al Baaqir (Alayhis Salaam) kwa wamesema mneno haya nisinge kubali.
Hakika maimamu wawili hawa (Alayhis Salaam) haifanani kusema maneno maovu
Hawawezi kuruhusu kitendo kiovu kinachopingana na tabia tukufu za kiislamu , kitendo kama hiki ni udayuthi (kutokua na wivu) hapana shaka kuwa viongozi (Alayhis Salaam) wameirithi elimu hii tangu na tangu yakinasibishwa maneno haya na matendo haya kwao,ina maana kuwa yamenasibishwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na yakinasibishwa na mtume basi itakuwa ni sheria ya Allah (jambo ambalo haliwezekani)
Tulipoitembelea India na huko tukakutana na viongozi wa kishia kama bwana Al Naqwiyu na wengineo tukapita katika kundi la Mahindus na wanaoabudu N’gombe na ibada za kipuuzi na wengineo wanaofuata dini za kijahili, na tukasoma sana kuhusu dini zao lakini hatukukuta dini yoyote kati ya dini zao inayo halalisha kitendo hicho kwa wafuasi wake.
Itawezekana vipi kwa kidini ya kiislamu ihalalishe kitu kichafu
Tulitembelea chuo kimoja cha kiislamu kilichopo Iran tukawakuta mabwana wakubwa wakihalalisha kuazimana tupu , na miongoni waliotoa fatwa ya kuruhusu jambo hilo ni Asayyid Lutfillahi Asaafiy na wengineo,kwa hiyo suala la kuazimana tupu limeenea Iran yote,na likaendelea kufanyika tendo hilo mpaka baada ya kuangushwa Shaha Mohammad Ridha Bahlawiy nakuja kwa Ayatullahi Al udhma Al imam al Khomainiyu , Al muusawiy na baada ya kufa Al imam Al Khomaniyu tendo hilo liliendelea na hii ikawa moja ya sababu ambazo zilipelekea kufeli dola ya kwanza ya kishia katika zama hizi,mashia katika ulimwengu mzima walikua wakiiangalia kwa makini dola hiyo, kufeli kwa dola hiyo ni katika mambo yaliyo changia mabwana wakubwa wengi kujitenga nayo na kuuipiga vita , huyu hapa rafiki yetu mwanazuoni Assayid Musa Al muusawiy aliyaita mapinduzi ya Irani kuwa ni mapinduzi yasiyo na matumaini na akatunga vitabu na akaeneza maqala nyingi katika kuipiga vita hiyo na kubainisha makosa yake.
Anasema bwana Jawad Al muusawiy hakika mapinduzi ya kiislamu ya Ira si kwa ajili ya uislamu hata kidogo isipokua ni jina tu.
Na alikua Ayatullahi al udhma Asayid Mohamed Kadhim
Pia kuna mabwana wakubwa wengi ninao wajua mimi mwenyewe waliilaumu serekali ya imamu khomeyniy na kuiasi.
Na yanayo sikitisha sana ni kwamba mabwana wakubwa wametoa fatwa ya kuruhusu kuazimana wanawake, kuna familia nyingi kusini mwa iraki na Baghdadi pia katika maeneo ya mapinduzi zinaendelea kufanya jambo hili kwa kufuata fatwa za mabwana wakubwa wengi kama vile: Asaysatani na Asadri na Ashyrazy na Al tabatabaiy na Al burujardy na wengineo,na wengi wao wakiwa wageni sehemu kwa mtu basi wana muazima mke wake wakimuona ni mzuri ataendelea kukaa nae hivyo mpaka aondoke!!.
Hakika wajibu wetu ni kuwatahadharisha watu juu ya kitendo hiki kibaya na wala wasikubali fatwa za mabwana wanao ruhusu tendo hili baya ambalo nguvu zilizo jificha nyuma ya pzia zina mchango mkubwa
Mambo hayakuishia hapo bali wali halalisha tendo la Qaumu luti kwa wanawake na zikapokewa riwaya nyingi zilizonasibishwa kwa viongozi(Alayhis Salaam) amepokea Atuusiy kutoka kwa Abdillah bin Abii Al Ya’fur akisema: (nilimuuliza Abaa Abdillah (Alayhis Salaam)kuhusu mtu anaye muingilia mkewe nyuma, akasema: si vibaya kama ataridhika,nikasema likowapi neno la Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) lisemalo
(فأتوهن من حيث أمركم الله)
{Waendeeni katika njia aliyowamrisha Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) basi akasema hii ni kwa kutafuta mtoto,basi tafuteni watoto kwa njia aliyowaamrisha Mwenyezi Mungu, kwani Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) amesema:
(نساؤكم حرث لكم فأتوا حرثكم أنى شئتم)
{Wanawake wenu ni mashamba yenu yaendeeni mashamba yenu mpendavyo} Al-Istibsaar 3/243.
Pia Atuusiy kapokea kutoka kwa Musa bin Abdillahi kutoka kwa mtu mmoja akisema: (nilimuuliza Abal- Hassan Aridhaa (Alayhis Salaam) mtu kumuingilia mkewe nyuma, akasema: imehalalishwa na aya katika kitabu cha Mwenyezi Mungu, aliposema Lut (Alayhis Salaam)
(هـؤلاء بناتي هن أطهر لكم)
(Mabinti zangu hawa kwenu ni tahara) alijua kuwa wao hawataki njia ya kawaida ya kimaumbile, Al-Istibsaar 3/243.
Na amepokea Atuusiy kutoka kwa Ally bin Hakam amesema, nilimsikia Safwani akisema: nilimuambia Alridha(Alayhis Salaam) (hakika ya mtu mmoja wa karibu yako ameniamrisha nikuulize mas-ala anakuogopa na anakuonea haya kukuuliza,akasema ni yapi hayo? Akasema:je mtu anaruhusiwa kumuendea mkewe nyuma? Akasema: ndiyo inafaa kufanya hivyo.) Al Masdar Al Sabiq.
Hakuna shaka kuwa habari hizi zimepingwa na Qur-an kwani Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala) anasema
(يسألونك عن المحيض قل هو أذى فاعتزلوا النساء في المحيض ولاتقربوهن حتى يطهرن) البقرة :222
{Na wanakuuliza kuhusu hedhi, waambie ni uchafu basi jitengeni nao wakiwa katika hedhi na wala msiwangilie mpaka wataharike} Sura 2 Aya 222.
Lau kama kumuingilia nyuma kunaruhusiwa angaliamrisha kuacha utupu wa mbele tu. Na (angesema jitengeni na utupu wa mbele wakiwa katika hedhi).lakini kwa sababu kumuingilia mwanamke nyuma ni haramu imeamrishwa kuziepuka sehemu zote mbele na nyuma ndio maana akasema (msiwa karibie) kisha akabainisha Mwenyezi Mungu baada ya hayo sehemu ya kuingiliwa mwanamke,akasema Allah (Subhaanahu wa Ta’ala):
(فإذا تطهرن فأتوهن من حيث أمركم الله)البقرة: 222
{Wakishataharika basi waingilieni sehemu aliyo waamrisha Mwenyezi Mungu} Sura 2 Aya 222.
Na Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) ameamrisha kuwaingilia wanawake katika sehemu ya mbele aliposema:
(نساءكم حرث لكم فأتوا حرثكم أنى شئتم) البقرة:322
{Wanawake ni mashamba yenu yaingilieni mashamba yenu mpendavyo} Sura 2 Aya 223, na shamba ni sehemu ya kutafutia mtoto.
Hakika riwaya ya Abii Al Ya’fur kutoka kwa Abii Abdillah maana yake nikua kutafuta mtoto inakua katika tupu za mbele kwa maneno yake Allah (Subhaanahu wa Ta’ala)
(نساءكم حرث لكم فأتوا حرثكم أنى شئتم)
(wanawake wenu ni mashamba yenu} basi hii ni katika katafuta mtoto, maana ya riwaya hii nikuifanya tupu ya mbele ni kwajili ya kutafuta mtoto tu, ama kukidhi haja za kimwili ni kwa utupu wa nyuma na maelezo ya riwaya hii yako wazi katika kuleta ufahamu huu.
Na hili ni kosa kwa sababu utupu wa mbele siyo maalum kwa kutafutia mtoto tu bali pia kwa kukidhi haja na matamanio ya kimwili. na hiyo ndio hali halisi ya maisha ya ndowa tangu enzi za Adamu (Alayhis Salaam)mpaka qiama na Abuu Abdillah hafanani kusema maneno maovu
(فإذا تطهرن فأتوهن من حيث أمركم الله)
{Basi wakishatwaharika waingilieni sehemu aliyowamrisheni mwenyezi mungu} kwa sababu sehemu ya kumuingilia mwanamke tayari inafahamika ni mbele au nyuma na hakuna sehemu nyingine ya tatu, (hii ni kwa kuchukulia ingefaa kufanya hivyo) kama wanavyo dai.
Lakini ilipokua moja ya sehemu mbili hizi si halali haifai kuiendea na nyingine ni halali basi ulihitajika ufafanuzi ni ipi sehemu inayofaa kuiendea ikawa amri ya Allah(Subhaanahu wa Ta’ala) ni kuiendea sehemu ya kuotesha( shamba), na shamba ni ile sehemu ya kutafutia mtoto,na sehemu hii ndiyo sehemu inayoendewa kwa kutafuta mtoto na kukidhi haja za kimwili pia.
Ama riwaya iliyonasibishwa kwa Al-ridha (Alayhis Salaam) katika kuruhusu kuliwatiwa wanawake na kutoa hoja ya maneno ya nabii Luti (Alayhis Salaam).
Basi mimi ninasema :hakika tafsiri ya maneno ya Allah (Subhaanahu wa Ta’ala)
(هــؤلاء بناتي هن أطهر لكم) هود:78
{Mabinti zangu hawa kwenu ni tahara) Sura Huud Aya:78 imepatikana katika aya nyingine usemi wake Allah(Subhaanahu wa Ta’ala)(ولوطا إذ قال لقومه
إنكم لتأتون الفاحشة ما سبقكم بها من أحد من العالمين*أئنكم لتأتون الرجال وتقطعون السبيل) العنكبوت :28
{Na Lut alipowaambia watu wake kuwa ninyi mnaleta uchafu haukufanywa na yeyote katika viumbe walio kabla yenu, Ninyi mna waingilia wanaume na kukata nasab} Al Ankabuut 28-29.
Kukata njia haina maana yale yanayo fanywa na majambazi peke yao laa sihivyo ina maana pia ya kukata kizazi kwa kuingilia sehemu isiyo kua ya kutafutia mtoto,yaani sehemu ya nyuma, basi lau kama watu wangeendelea kuingilia nyuma za wanaume na wanawake na wakaacha kutafuta watoto watu wangelimalizika na kizazi kingelikoma.
Aya hii tukufu pia inatupa maana hiyo hiyo na khasa tunapoangalia kwa makini mtririko wa aya iliyo nyuma yake ,hakuna shaka kuwa haya hayakujificha kwa Imamu Al-ridha (Alayhis Salaam), hivyo inathibitika uongo wa kuinasibisha habari hii kwake.
Hakika kuingilia nyuma wanawake halikusemwa hilo na mtu yoyote isipokuwa mashia Ithna asharia.
Jua kwamba mabwana wakubwa katika chuo cha kishia cha Annajaf na vyuo vyote vya kishia na kila mahali walipo wanakifanya kitendo hicho (kuwainglia wanawake nyuma)!
Na alikua rafiki yetu Al Hujatu Asyidu Ahmad Al wailiyu akisema tangu alipo ziona riwaya hizi alianza kukifanya kitendo hicho na ni mara chache ambazo anamuingilia mwanamke katika sehemu ya mbele.
Na kila nilipokutana na mmoja kati ya hao mabwana wakubwa na katika kila sehemu ninauliza uharamu na uharamu wa mwanamke kuingiliwa nyuma basi hunijibu kuwa ni halali na kutaja riwaya mbali mbali zinazoruhusu jambo hilo nyengine ni hizi tulizo zitaja hapo nyuma.
Hawakutosheka kuruhusu kulawitiwa wanawake tu bali pia wengi kati yao wameruhusu kulawitiwa hata wanaume hasa walio karibu baleghe.
Siku moja tukiwa chuoni zilipatikana habari kuwa mtukufu Asayid Abdul Hussain Sharafu ddiyn Al Muusawiy amefika Baghdad, na atafika chuoni ili akutane na mtukufu Al Imamu Alu Kashifu Al Ghataa, na alikua Asayid Sharafu Ddiyn amepata umaarufu kwa mashia wote. Khasa baada ya kutoka vitabu vyake alivyoviandika
Alipofika Annajaf allitembelea chuoni makaribisho yake yakawa makubwa kutoka kwa wana chuo walimu na wanafunzi na katika kikao chao kilichofanyika katika ofisi ya al sayid Al Khashif Al Ghataa, kilicho kusanya idadi kubwa ya mabwana wakubwa na baadhi ya wanafunzi , nami nilikua ni mmoja ya waliohudhuria, katikati ya kikao aliingia kijana mmoja akatoa salamu kisha akasema kumwambia Asayid Al Khashif Al Ghataa: bwana nina swali,bwana Al kashiful-ghataa akamwambia: uliza swali lako kwa Asayid Sharaf Adiyn akalirusha swali kwa mgeni wake Asayid Sharaf Adiyn kwa kumtukuza na kumuheshimu.
Muulizaji akasema: bwana mkubwa, mimi ninasoma
Asayid Sharaf Adiyn, akaelewa lengo lake, na akasema kwahivyo unataka kuoa mwanamke mwingereza? Yule mtu akasema ndio, akamwambia Sharaf Adyin:
Yule mtu akasema: nimetafuta
Ama zinaa niko mbali nayo kwakua ni haramu na ndoa haiwezekani kama ulivyoona nami nakaa huko mwaka mzima au zaidi, kisha narudi likizo kwa muda wa mwezi mmoja ,na kama ujuavyo safari ni ndefu nifanyeje?
Alinyamaza Asayid Sharaf Adiyn kidogo na akasema: hakika tatizo lako hili ni zito, lakini usijali kwani niliwahi kusoma riwaya kutoka Imamu Jafar Al Sadiq (Alayhis Salaam) wakati alipojiwa na mtu anayesafiri sana na akamtolea shida na ikawa vigumu kuongozana na mke wake na ni vigumu kufanya mut’a katika mji anao safiri kiasi akawa anapata shida kama wewe, basi Abu Abdillahi akamwambia safari ikiwa ndefu kwako basi juu yako kumuoa mwanamume, hili ndilo jawabu la suala lako.
Aliondoka yule mtu akiwa na alama ya shaka kutokana na jibu hili,ama wale waliohudhuria akiwemo bwana mkubwa mkuu wa chuo hakutamka mmoja wao chochote.
Alikamatwa bwana mkubwa mmoja hapa chuoni akimlawiti mvulana mmoja mdogo katika wana funzi wa hapa chuoni, Habari zikawafikia watu wengi, siku iliyofuata alipokua bwana mkubwa huyo akitembea katika bustani ,alimkaribia bwana mkubwa mwingine miongoni mwa wanazuoni wa chuo ,na alikuwa amezipata habari , akasema kwa lugha fasaha huku akimfanyia mzaha:bwana unsema nini kuhusu kulawiti?yule mwengine akamjibu kwa mzaha zaidi akisema kumwambia na kwa ufasaha tena. Imependekezwa kuingiza kichwa cha dhakari tu,kisha wakajikohoza kwa nguvu wote wawili!!
Na yuko bwana mwingine miongoni mwa wanazuoni wa Hoza (chuo)anajulikana kw kulawiti , alimuona mtoto mdogo akitembea pamoja na bwana mkubwa wengine miongoni mwa wanazuoni wa Hoza(chuo) vilevile,akaamuuliza,ni mtoto gani huyu uliye nae? Akamjibu: huyu mtoto wangu fulani (akamtaja jina) Akamwambia: kwanini hakumleta kwetu ili tumsomeshe na kumpatia elimu ili awe mwanazuoni kama wewe? Akamjibu kwa dharau: ewe mwanachuoni muovu mpuuzi unataka nikuletee ili umfanyie (hivi na vile)?! Na tukio amenizungumzia mtu muaminifu miongoni mwa waalimu wa Hoza (chuo).
Tumeona matukio mengi kama haya, na tuliyoyasikia ni mengi zaidi mpaka imefikia rafiki yetu mpemzi bwana Abasu amekusanya matukio mengi sana, na kuyaandika kwa upana na kwa tarehe zake majina ya wahusika. Nae anakusudia kuyatoa katika kitabu anachotaka kukiita FADHAIHU AL-HOZATI AL-ILMIYAT FI AL-NAJAF (habari za kufedhehesha za chuo cha kishia cha najaf) kwa sababu ni wajibu kuuweka wazi ukweli kwa mashia wa kawaida masikini wasiojui yanayo pita nyuma ya pazia, na wala hawayajui wanayoyafanya mabwana wakubwa wa kishia , mpaka inafikia , mmoja wao anampeleka mkewe au binti yake au dada yake,kwa ajili ya ziara au kutafuta mtoto au kupeleka zawadi kwa ajili ya Hussain) basi wanampokea mabwana wakubwa hasa akiwa mzuri na kufanya nae machafu na kumfanyia kila uovu, hakuna hila wala nguvu isipokua kwa msaada wa Allah(Subhaanahu wa Ta’ala).
Kutokana na hayo yaliyo tangulia tumekwisha fahamu ya kuwa khumsi haitolewi kwa mashehe wala wanazuoni ,na limekuwa wazi jambo hili kwetu kufuatia maelezo ya maudhui hii tuliyo yatowa kwa pande zake zote ,na ni vizuri kwetu kuzindua kua mafakihi na marejeo ya kidini(wanazuoni) wanadai kuwa wao ni katika Ahlu Bayt, utamuona moja wao akikuonesha mtiririko wa nasaba yake mpaka kwa kadhim (Alayhis Salaam), jua kwamba ni jambo lisilo wezekana kwa idadi kubwa hii yote ya wanazuoni wa Iraq, Iran, Sirya, Lebanon, nchi za ghuba na Pakistan na nyenginezo kua ni katika Ahlul-Bayt , na kuhesabu wanazuoni wa Iraqi tu ataona kua ni jambo lisilo wezekana kuwa idadi yote hiyo ya wanazuoni wa Iraqi ni katika Ahlul-Bayt , vipi itawezekana tukichanganya na wanazuoni wa miji mingine?bila shaka idadi yao ni kubwa sanasana je itawezekana vipi wote hawa wawe ni katika Ahlul-Bayt ???
Na zaidi ya hayo mti wa nasabu ya mtume unauzwa na kununuliwa hapa chuoni , anaetaka kuupata utukufu wa nasabu ya Ahlul Bayt ni juu yake kuja na dada yake au mke wake kwa sharti awe mzuri kwa mtukufu mmoja wapo ili astarehe nae,au aje na kiwango cha mali na atapata utukufu kwa moja kati ya njia mbili hizi:- na hili ni jambo maarufu hapa chuoni kwetu (CHUO CHA KISHIA CH ANNAJAF).
Kwa ajili hiyo ninasema yasiwahadae yale ambayo wanayafanya baadhi ya watukufu,na waandishi wakati anapoweka mmoja wao mti wa nasaba yake katika ukurasa wa mbele wa kitabu chake ni kwa ajili ya kuwahadaa watu wepesiwepesi matajiri na masikini ,ili wampelekee khumsi za
Na mwisho wa utafiti wa khumus sitosahau kuitaja kauli ya rafiki yangu mpenzi mshairi hodari Ahmad Al Safy Al Najafiy ambae nilifahamiana nae baada yakupata shahada ya Ijtihadi tukawa marafiki wapenzi achilia mbali tofauti ya umri ilopo kati yetu , kwani alikuwa akinizidi kwa miaka takriban thelathini au zaidi ,nakumbuka alipo niambia mwanangu usiichafuwe nafsi yako kwa mali ya khumsi kwani ni mali ya haramu , na akanidadisi kuhusu khumsi mpaka akanikinaisha kua ni haramu , kisha akanitajia beti za shairi alilokuwa amelitunga kwa ajili hii, ambazo nilizihifadhi kwenye mfuko wangu wa kumbukumbu, na hapa ninazinukuu kwa kwa faida ya wasomaji watukufu
“Ninawashangaa watu, kuomba omba kwa kutumia dini
Basi ikiwa kupata elimu ndio sababu ya kuomba omba basi itakuwa ujinga ni bora kuliko elimu, na je katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kulikuwa na watu wanaoishi kutegemea
Ulianza ushindani baina ya watukufu na mujtahidina kwa ajili ya kupata khumus, na kwa ajili hii alianza kila mmoja kati yao kupunguza kiasi kinachotakiwa kuchukuliwa kutoka watu mpaka watu wawe wengi kwake kuliko mwezake, wakajiwekea njia za kishetani, mtu mmoja alikuja kwa Asayid Asaysataniy akasema kumwambia :
Hakika haki ya khumus ninayo takiwa kutowa ni milioni tano .nami nataka kutoa nusu ya kiwango hicho yani milioni mbili na nusu,akamwambia Asayid Asistaniy: lete hiyo milioni mbili na nusu, akampa Asistaniy akazipokea, kisha akamwambia : nimekupa wewe - yaani syyid Asistaniy akampa yule bwana alieleta zile hela - yule mtu akaichukua kisha, akasema Asistaniy: rejesha tena kwangu hizo hela yule mtu akampa tena, Asistaniy akamwambia sasa imekua mkusanyiko wake milioni tano dhima yako imeishaondoka katika khumsi, mabwana wakubwa wengine walipoyaona hayo wakafanya hivyo hivyo bali wakavumbua njia nyingine,ili watu waende kutowa khumsi kwao na yakawa ni mashindano kati ya mabwana wakubwa kwa ajili ya kupata khumsi , na ikawa kiwango cha khumus kinafanana na biashara ya kupunguziana ,matajiri wengi wakawa wanaitowa khumsi kwa anae chukua kiasi kidogo .
Na mkuu wa chuo cha Najaf alipoona kuwa mashindano yamekuwa makubwa na kiwango kinacho ingia kwake ni kidogo, alitowa fatwa yake inayokataza kupewa khumsi mtu yoyote kati ya watukufu, bali haitolewi isipokua kwa watu maalumu, nae anafungu kubwa au mawakala wake alio wasambaza maeneo mbalimbali.
Na baada ya kuzipokea
Amesema Amirul muuminin (Alayhis Salaam) wema ulioje kwa wenye kujitenga na dunia na wakiwa na raghba ya akhera, basi hao ndio walioifanya ardhi vitanda na mchanga wake kuwa ni godoro na maji yake kuwa ndio manukato na Qur-aan ni alama yao , na dua ndio nguo yao, kisha wakaikopa dunia kwa mfumo wa masihi……. Hakika Daudi (Alayhis Salaam) alisimama mfano wa saa hii ya usiku , na akasema hakika ya saa hiii hatoomba mja isipokua hujibiwa , isipokuwa awe Ahara u ayfa au Shartiya .[ Nahjul Balagha 4/24] hebu linganisha kati ya maneno ya Amirilul muuminin na hali za watukufu wa kishia na hukumu wewe mwenyewe , hakika maelezo haya na mengineyo ni katika maelezo matukufu ambayo hayana kasoro yoyote mbele ya mabwana wakubwa na wanazuoni wa kishia , lakini maisha ya fahari na raha na yafahari ambayo wanayaishi yamewasahaulisha juhudi ya amiril-mumini na yakawafanya vipofu wasiweze kuzingatia maneno yake na kushikamana na maana ya maneno hayo.
Hakika asshar ni yule anayechukua kodi ya sehemu ya kumi katika
Faida Tunazozipata
Kuthibiti kuwepo kwa Shakhsiya ya bin Sabai, na kuwepo kundi linalomsaidia, na kumuunga mkono katika madai yake, na kundi hili linajulikana kwa jina la Assabaiyyah.
Abdallah bin sabai huyu alikuwa myahudi akajionyesha kuwa ni muislamu,isipokuwa ukweli ni kwamba alibakia katika dini yake ya uyahudi akawa anaeneza sumu yake katika kipindi chote hicho.
Yeye ndie wa kwanza kudhihirisha matusi kwa masahaba wa mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam): Abubakar, ‘Umar,na ‘Uthmaan na masahaba wengine, Nae ndio wa kwanza aliedai ukhalifa (uongozi) kwa Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) nae (bin Sabai) ndie aliesema kwamba Ali ndie alieusiwa ukhalifa na mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na itikadi hii aliipata kutoka kwa mayahudi , na akawa (bin Sabai) anasema hakuyasema maneno haya ispokuwa kwakuwapenda familia ya mtume na kuwapigia kampeni katika ukhalifa,na kuwapiga vita maadui zao (ambao ni maswahaba na kila wenye kuwaunga mkono ) hayo ndio madai ya bin Sabai.
Ikiwa hivyo ndivyo basi kuwepo shakhsiya ya Abdallah bin saba’i ni jambo la ukweli , haiwezekani kulipuuza au kulikataa, na kwa kuthibitisha kuwepo kwake zimekuja aya mbalimbali katika vitabu vyetu vinavyo tegemewa navyo ni:
الغارات للثقفي ،رجال الطوسي ،الرجال للحلي، قاموس الرجال للتستري، دائرة المعارف المسماه بمقتبس الأثر الأعلمي الحائري، الكني والألقاب لعباس القمي، حل الإشكال لأحمد بن طاووس المتوفى سنة 673، الرجال لابن داود،التحرير للطاووسي، مجمع الرجال للقهباني، نقد الرجال للتفرشي ،جامع الرواة للمقدسي الأردبيلي مناقب آل أبي طالب لإبن شهر أشوب، مرآة الانوار لمحمد بن طاهر العاملي
.
ALGHAARAT CHA ATHAQAFIYY, RIJALU ALTWUSY, ALRIJAL CHA AL HULLY, QAMUS-ALRIJAL LITTASITIRY, DAAIRATUL-MAARIFI,AL MUSAMATU BIMUQTABIS,AL ATHAR LIL-AALAMY, ALHAAIRIYI, ALKUNI WAL-ALQABI, LIABASILALQUMIYI,HALUL-ISHKALI LIAHMAD BIN TWAUS ALMUTAWAFASANA(673),ALRIJALULIBN DAUD, ATTAHARYRU LITWAUSIYI,MAJMAUARIJALI LILQAHBAAYI, NAQDU ALRIJAL LITAFRASHYI, JAMIU AL RUWATILIL MAQDISIYI AL-ARDUBAYLIY, MANAQIBU ALUABII TWALIB LIIBN SHAHRU ADHWAB, MIR-ATUL AN WAR LI MUHHAMAD BIN TWAHIR AL-AMILIYI. Vitabu hivi tulivyo vitaja ni mifano tu, kuna zaidi ya vitabu ishirini ambavyo vinaonyesha kuwepo bin sabai , basi niajabu ilioje kwa wanavyuoni wetu mfano wa AL- MURTADHA AL- ASKARIY, NA SAYID MOHAMMAD JAWAD MUGHNIYAH, na wengineo wasiokua hao kati ya wanao pinga kuepo kwa mtu huyu , na bilashaka maneno yao haya hayana ukweli wowote .
Kuthibiti kuwepo kwa Shakhsiya ya bin Sabai, na kuwepo kundi linalomsaidia, na kumuunga mkono katika madai yake, na kundi hili linajulikana kwa jina la Assabaiyyah.
Abdallah bin sabai huyu alikuwa myahudi akajionyesha kuwa ni muislamu,isipokuwa ukweli ni kwamba alibakia katika dini yake ya uyahudi akawa anaeneza sumu yake katika kipindi chote hicho,
Yeye ndie wa kwanza kudhihirisha matusi kwa masahaba wa mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam): Abubakar, ‘Umar,na ‘Uthmaan na masahaba wengine, Nae ndio wa kwanza aliedai ukhalifa (uongozi) kwa Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) nae (bin Sabai) ndie aliesema kwamba Ali ndie alieusiwa ukhalifa na mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na itikadi hii aliipata kutoka kwa mayahudi , na akawa (bin Sabai) anasema hakuyasema maneno haya ispokuwa kwakuwapenda familia ya mtume na kuwapigia kampeni katika ukhalifa,na kuwapiga vita maadui zao (ambao ni maswahaba na kila wenye kuwaunga mkono ) hayo ndio madai ya bin Sabai.
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/53
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F477&title=Kwa%20Ajili%20Ya%20Allaah%20Kisha%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Historia
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9283&title=01-Kwa%20Ajili%20Ya%20Allaah%20Kisha%20Historia%3A%20Utangulizi
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F479&title=02-Kwa%20Ajili%20Ya%20Allaah%20Kisha%20Historia%3A%20Abdullah%20Ibn%20Saba%27i
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F480&title=03-Kwa%20Ajili%20Ya%20Allaah%20Kisha%20Historia%3A%20Uhakika%20wa%20Kujinasibisha%20Na%20Ahlul%20Bait
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F481&title=04-Kwa%20Ajili%20Ya%20Allaah%20Kisha%20Historia%3A%20Mut%27ah%20Na%20Yanayohusiana%20Nayo
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F482&title=05-Kwa%20Ajili%20Ya%20Allaah%20Kisha%20Historia%3A%20Khumus
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F483&title=06-Kwa%20Ajili%20Ya%20Allaah%20Kisha%20Historia%3A%20Ufupisho%20Wa%20Kushamiri%20Nadharia%20Ya%20Khumus
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F484&title=07-Kwa%20Ajili%20Ya%20Allaah%20Kisha%20Historia%3A%20Itikadi%20Ya%20Mashia%20Kuhusu%20Vitabu
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F485&title=08-Kwa%20Ajili%20Ya%20Allaah%20Kisha%20Historia%3A%20Mtazamo%20Wa%20Mashia%20Kwa%20Ahlus%20Sunnah
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F486&title=09-Kwa%20Ajili%20Ya%20Allaah%20Kisha%20Historia%3A%20Uzinduzi%20I
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F488&title=10-Kwa%20Ajili%20Ya%20Allaah%20Kisha%20Historia%3A%20Uzinduzi%202
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F487&title=11-Kwa%20Ajili%20Ya%20Allaah%20Kisha%20Historia%3A%20Uzinduzi%203
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9281&title=12-Kwa%20Ajili%20ya%20Allaah%20Kisha%20Historia%3A%20%20Faida%20Tunazozipata