Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > 003-Aal-'Imraan: Aayah Na Mafunzo > 128-Aayah Na Mafunzo: Tukio La Kuumizwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Vita Vya Uhud

128-Aayah Na Mafunzo: Tukio La Kuumizwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Vita Vya Uhud

 

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Tukio La Kuumizwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Vita Vya Uhud

Alhidaaya.com [1]

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ ﴿١٢٨﴾

Si juu yako katika jambo hili; ima Apokee tawbah yao au Awaadhibu, kwani wao ni madhalimu. [Aal-'Imraan: 128]

 

 

Mafunzo:

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

Aayah hii imeteremka kama alivyohadithia Ibn ‘Umar (رضي الله عنه) kwamba: Alimsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipoinua kichwa chake kutoka rukuu’ ya mwisho ya Swalaah ya Alfajiri baada ya kusema:

سَمِعَ اَللَّهُ لِمَنْ حَمِدَه رَبَّنَا لَكَ اَلْحَمْدُ

“Sami’a-Allaahu liman hamidah Rabbanaa Lakal-Hamd.  

Allaah Amemsikia aliyemhimidi, Ee Rabb wetu, Himdi ni Zako Wewe

 

 

 Kisha akasema:

اللَّهُمَّ الْعَنْ فُلَانًا وفُلَانًا وفُلَانًا

“Allaahumma mlaani fulani na fulani na fulani.” Ikateremka:

 

لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ ﴿١٢٨﴾

 

Jambo hili halikuhusu wewe; ima Apokee tawbah yao au Awaadhibu, kwani wao ni madhalimu. (3:128). [Al-Bukhaariy na wengineo kwa riwayaah nyenginezo]

 

 

Na Anas bin Maalik  (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Siku ya Uhud, jino la Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) lilivunjika na akachomwa mkuki begani mwake. Damu ikawa inamchirizika usoni mwake akawa anaifuta damu huku akisema: “Vipi watu watafaulu ikiwa wamerowanisha uso wa Nabiy wao kwa damu na hali yeye anawalingaia kwa Allaah?” Hapo ikateremka Aayah hii:

 

لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ ﴿١٢٨﴾

 

Jambo hili halikuhusu wewe; ima Apokee tawbah yao au Awaadhibu, kwani wao ni madhalimu” (3: 128) [At-Tirmidhiy Hadiyth Hasan Swahiyh].

 

Share [2]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/8152

Links
[1] http://www.alhidaaya.com/sw
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8152&title=128-Aayah%20Na%20Mafunzo%3A%20Tukio%20La%20Kuumizwa%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%20Katika%20Vita%20Vya%20Uhud