Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > Fataawaa: Kulipa Swawm Na Kafara: Hedhi, Mja Mzito, Kunyonyesha, Nifaas > 01-Imaam Ibn Baaz: Kutumia Dawa Kuzia Hedhi Katika Ramadhwaan Apate Kufunga Mwezi Mzima

01-Imaam Ibn Baaz: Kutumia Dawa Kuzia Hedhi Katika Ramadhwaan Apate Kufunga Mwezi Mzima

Kutumia Dawa Kuzia Hedhi Katika Ramadhwaan Apate Kufunga Mwezi Mzima

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [1]

 

 

SWALI:

Nini hukmu ya mwanamke kutumia dawa za uzazi ili kuzuia kufika kwa damu ya hedhi apate kumaliza swiyaam mwezi mzima? Tufaidisheni, Allaah Akufaidisheni nanyi.

 

 

JIBU:

Hakuna ubaya kufanya hivyo kwamba atumie vidonge vya kuzuia hedhi ili aweze kuswali na watu na afunge nao kwa sharti kwamba kufanya hivyo kuna usalama kwake na havitomdhuru. Na pia baada ya kupata ushauri wa daktari ili asije kujidhuru nafsi yake,  na pia apate ruhusa kutoka kwa mumewe ili asimuasi mumewe.

Itakapokuwa baada ya kushauriana na kutahadhari upande wa salama kutokana na madhara, basi hakuna ubaya.

Na hali hiyo hiyo iwe katika masiku ya Hajj.

Baaraka Allaahu Fiykum

 

 

[Al-Mawqi’ Ar-Rasmiy – Imaam Ibn Baaz] [2]

 

Share [3]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/8435

Links
[1] http://www.alhidaaya.com
[2] http://www.binbaz.org.sa/noor/9833
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8435&title=01-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20Kutumia%20Dawa%20Kuzia%20Hedhi%20Katika%20Ramadhwaan%20Apate%20Kufunga%20Mwezi%20Mzima