Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > Fataawaa: Kulipa Swawm Na Kafara: Hedhi, Mja Mzito, Kunyonyesha, Nifaas > 06-Imaam Ibn Baaz: Imemjia Hedhi Dakika Tano Kabla Ya Magharibi Akidhi Swalaah Ya Magharibi?

06-Imaam Ibn Baaz: Imemjia Hedhi Dakika Tano Kabla Ya Magharibi Akidhi Swalaah Ya Magharibi?

Imemjia Hedhi Dakika Tano Kabla Ya Magharibi

 

Akidhi Swalaah Ya Magharibi Baada Ya Kutoharika?

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [1]

 

 

SWALI:

Nimefunga siku moja katika Ramadhwaan na haikubaki kitu siku hiyo isipokuwa dakika tano tu kufikia wakati wa kufuturu ikanijia hedhi ya mwezi. Je, ninawajibika kuswali Swalaah ya Magharibi kama kukidhi baada ya kutwaharika au la?

 

 

JIBU: 

 

Ikiwa hedhi imemjia kabla ya Magharibi kuingia basi haimuwajibikii kuswali Swalaah ya Magharibi wala Swalaah nyinginezo.

 

Na Swawm pia siku hiyo haitosihi, siku ambao imemjia hedhi kabla ya kuzama jua kwani swawm imebatilika na imemuwajibikia kulipa siku hiyo, ikiwa anajua kuwa imemjia hedhi kabla ya  Magharibi kuingia.

 

 

[Al-Mawqi’ Ar-Rasmiy - Imaam Ibn Baaz] [2]

 

 

Share [3]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/8438

Links
[1] http://www.alhidaaya.com
[2] http://www.binbaz.org.sa/noor/4580
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8438&title=06-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20Imemjia%20Hedhi%20Dakika%20Tano%20Kabla%20Ya%20Magharibi%20Akidhi%20Swalaah%20Ya%20Magharibi%3F%20%20%20%20%20%20%20%20%20%20%20%20%20%20%20%20%20%20%20%20%20%20