Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > 006-Al-An'aam: Aayah Na Mafunzo > 098-Aayah Na Mafunzo: Nyota Zimeumbwa Kwa Ajili Ya Matatu Mapambo Ya Mbingu Kupiga Mashaytwaan Kuongoza Njia

098-Aayah Na Mafunzo: Nyota Zimeumbwa Kwa Ajili Ya Matatu Mapambo Ya Mbingu Kupiga Mashaytwaan Kuongoza Njia

Aayah Na Mafunzo

 

www.alhidaaya.com [1]

 

Al-An’aam 98

 

098-Nyota Zimeumbwa Kwa Ajili Ya Matatu

Mapambo Ya Mbingu Kupiga Mashaytwaan Kuongoza Njia

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

وَهُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ النُّجُومَ لِتَهْتَدُوا بِهَا فِي ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۗ قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٩٧﴾

 Na Yeye Ndiye Aliyekufanyieni nyota ili zikusaidieni kujua mwendako katika viza vya bara na bahari. Kwa yakini Tumezifasili waziwazi ishara na vielelezo kwa watu wanaojua. [Al-An’aam: 97]

 

 

Mafunzo:

 

Amesimulia Qataadah (رضي الله عنه): “Allaah Ameumba hizi nyota kwa malengo matatu; (i) mapambo ya mbingu (ii) vimondo vya (kuwafukuza na kuwapiga) shaytwaan, (iii) alama za kuongoza njia (wasafiri wa majangwani na baharini). Basi atakayefasiri vingine amekosea na atakuta patupu Aakhirah (atakosa thawabu) kwani atakuwa amebeba asio na elimu nayo kwa kuchupa mipaka ya ujuzi Wake.” [Al-Bukhaariy]

 

Nyota zimeumbwa kwa ajili ya mambo hayo tu. Basi Hadiyth hii inawakanusha wanajimu (watabiri wa nyota) jambo ambalo ni la kumshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى) nayo ni Shirki kubwa ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Haisamehe.

 

 

 

 

 

Share [2]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/9005

Links
[1] http://www.alhidaaya.com
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9005&title=098-Aayah%20Na%20Mafunzo%3A%20Nyota%20Zimeumbwa%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Matatu%20Mapambo%20Ya%20Mbingu%20Kupiga%20Mashaytwaan%20Kuongoza%20Njia