Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > Fataawaa: Ihraam Na Talbiyah > 01-Imaam Ibn Baaz: Akiwa Ndani Ya Ihraam Amechezea Nywele Kisha Zimeng'oka

01-Imaam Ibn Baaz: Akiwa Ndani Ya Ihraam Amechezea Nywele Kisha Zimeng'oka

 

 

Akiwa Ndani Ya Ihraam Amechezea Nywele Kisha Zimeng'oka

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [1]

 

 

SWALI:

 

Nina tabia ya kuchezea nywele ninapoikuwa na fikra. Nilipokwishaingia katika ihraam, bila ya kujitambua, nilifanya hivyo na baadhi ya nywele ziling'oka na kuanguka. Je, napaswa kulipa kafara?

 

JIBU:

 

Hakuna haja kufanya hivyo (kulipa kafara) kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ametaja kuhusu Waumini kwamba wamesema:  

رَبَّنَا لاَ تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا

“Rabb wetu Usituchukulie tukisahau au tukikosea. [Al-Baqarah:286]

 

Kisha Allaah Akawajibu du'aa yao hii kama ilivyotajwa katika Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  Aliitikia kwa kusema:

((قَدْ فَعَلْت))  

(Nimeiitikia [du'aa]) [Muslim katika Swahiyh yake]

 

[Fataawa Al-Hajj Wal 'Umrah waz-Ziyaarah Uk. 58]

 

 

 

Share [2]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/9225

Links
[1] http://www.alhidaaya.com
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9225&title=01-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20Akiwa%20Ndani%20Ya%20Ihraam%20Amechezea%20Nywele%20Kisha%20Zimeng%27oka