Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > Hadiyth Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah - أحاديثُ عَنْ فضْل لا إلَهَ إلاَّ الله > 36-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa-Allaah: Kutamka Laa Ilaaha Illa-Allaah Wakati Wa Mafazaiko

36-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa-Allaah: Kutamka Laa Ilaaha Illa-Allaah Wakati Wa Mafazaiko

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

www.alhidaaya.com [1]

 

36-Kutamka Laa Ilaaha Illa-Allaah Wakati Wa Mafazaiko  

 

 

عَنْ زَيْنَبَ بِنْتِ جَحْشٍ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم دَخَلَ عَلَيْهَا فَزِعًا يَقُولُ: ((لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَيْلٌ لِلْعَرَبِ مِنْ شَرٍّ قَدِ اقْتَرَبَ، فُتِحَ الْيَوْمَ مِنْ رَدْمِ يَأْجُوجَ وَمَأْجُوجَ مِثْلُ هَذَا))‏ وَحَلَّقَ بِإِصْبَعِهِ وَبِالَّتِي تَلِيهَا، فَقَالَتْ زَيْنَبُ فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ أَنَهْلِكُ وَفِينَا الصَّالِحُونَ؟  قَالَ: ((نَعَمْ، إِذَا كَثُرَ الْخَبَثُ))  

 

Imepokelewa kutoka kwa Zaynba Bint Jahsh (رضي الله عنها) kwamba Nabiy alingia chumbani kwake akiwa katika hali ya kufazaika akasema:

‏ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ

 

((Laa ilaaha illa Allaah [hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah]

 

Ole kwa Waarabu kutokana na shari iliyokaribia. Leo limefunguka shimo katika boma la kizuzi cha Ya-ajuwj na Ma-ajuwj kama hivi!)) Akafanya kiduara kwa kufunga kidole chake cha gumba na cha shahada. Zaynab akasema: Kisha nikasema: Ee Rasuli wa Allaah, hivi tutaangamia na hali tumo watu wema?”. Akasema: ((Ndio pindi maovu yakizidi)) [Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (6/181) [3346], Muslim (4/2208) [2880] na Riwaayah nyengine: “Aliamka usingizini akasema….

 

 

Share [2]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/9351

Links
[1] http://www.alhidaaya.com
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9351&title=36-Fadhila%20Za%20Laa%20Ilaaha%20Illa-Allaah%3A%20Kutamka%20Laa%20Ilaaha%20Illa-Allaah%20Wakati%20Wa%20Mafazaiko%20%20